Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

CHAGUO LANGU NI WEWE - 4

 





    Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bi.Ramla pamoja na wageni wake walikuwa wakiongea maneno ya chini kwa chini, Shamsa alipitiliza mpaka mlangoni na kumuaga mama yake anakwenda Saluni kutengeneza nywele zake kutokana na ugeni huo Mama yake akamwambia kuwa akirudi atamkuta anamsubili kwa hamu kubwa sana kwani ana mazungumzo ya maana juu yak. Shamsa alimwambia Mama yake atochelewa kurudi kwani anakwenda kuosha tu nywele na sio kusuka kama ilivyo siku nyingine. Kipindi chote hicho ambaye ni Aisha na Abdul pamoja na Bi.Ramla walikuwa kwenye maongezi ambapo Mama Shamsa alimtaka yule Abdul afanye awezalo aweze kumuoa mwanae kwani amemchagua yeye awe mume wa mwanae.Abdul alimwambia Bi.Ramla kuwa asiwe na mashaka kwa hilo atalitimiza kwa muda mfupi tu ujao.

    “Shaka ondoa nitahakikisha kila kitu kinakwenda sawa na Shamsa atakuwa mke wangu”Abdul alisema huku akijiamini

    “Nimefurahi sana kusikia hivyo mwanangu nitakuwa nawe kwa kila jambo”

    “Usijali Bi.Ramla Shamsa atafurahi mwenyewe maana kila kitu kitakwenda sawa nitajitahidi Ili kumpa furaha mtoto wako na si vinginevyo”Abdul aliongeza

    “Itapendeza maana hata yeye atafurahi mwanangu kupata mume kama wewe ili kuondokana na mawazo ya huyo kipofu wake”

    “Ndio maana nimekwambia tulia tu niachie mwenyewe mambo haya yatakwenda sawa”



    “Hakika nakuamini Abdul wewe upo makini sana kwa jambo hili”

    “Usijali mama pia waweza kuniambia kama mwahitaji kitu chochote nimfanyie huyo kijana?”

    “Hapana mwanangu kwa wakati huu naomba umchote kwanza Shamsa hapo baadae tutaona kama akikataa basi tutajua jinsi ya kumfanya Jongo”

    “Sawa ila uwe makini sana kile ambacho unahitaji kukifanya, kumpatia pesa mtu na kufanya ukatili wa namna hii inatakiwa akili ya nyongeza”

    “Najua ninachokifanya ni kumlinda binti yangu juu ya kijana huyo kipofu, sijui kitu gani alichokipenda juu ya kipofu huyu, sijui nifanye nini ili aweze kuachana na mwanangu”Bi.Ramla alilalama

    “Lakini yawezekana Shamsa atakuwa na upendo kupita maelezo juu ya kijana huyo ujue moyo ukipenda vingine uwezi kuelewa”

    “Hata kama amempenda lakini mimi mama yake sijampenda kijana huyo awe na mwanangu,pia nakupa pesa yangu ili uweze kufanya kile nilichokwambia”

    “Sawa Bi.mkubwa nimekuelewa sana nitafanya kile nilichokuahidi kwamba nitakuwa naye siku zote za maisha yangu pesa yako tu mama”Abdul alisema huku akiwa mtu mwenye hali ya ulevi

    Baada ya masaa machache Bi.Ramla akiwa na wageni wake ambao Shamsa hakuwa akiwafahamu kwa wakati huo.Waliongea mambo mengi ambayo Shamsa hakujua kile kinachozungumzwa na kuja nyumbani hapo kwa wageni hao wakiwa na mama yake.Baada ya muda kwenda Shamsa akarudi na kuwakuta Mama yake na wageni hao wapo vile vile kama alivyowaacha Shamsa alipitiliza na kuingia chumbani kwake huku akiwa na mawazo tele kichwani,hakujua hatma yake juu ya kumpata Jongo alimtafuta kila sehemu lakini ilishindikana alijaribu kutembea morogoro nzima kumtafuta Jongo pia hakufanikiwa kumpata hivyo ndivyo ilivyokuwa na mawazo tele kichwani yamemuandama.Shamsa akiwa juu ya kitanda chake chumbani amejipumzisha muda huo alitega masikio yake aliposikia sauti za wageni hao wakiagana na mama yake kisha wakaondoka.Siku hiyo Shamsa aliboleka sana pale alipomuwaza mama yake kusudio lake nini hasa kuja na wageni nyumbani kwake kisha kumtambulisha kwa majina yao tu na sio kama kufahamishwa kiundani kama ndugu au majirani. Shamsa alipohakikisha wabeni hao wameonda kwa kuchungulia dirisha kwake na kuangalia getini aliwaona wageni hao wakitokomea nje na mama yake alifunga geti na kurudi tena ndani. Shamsa naye alituka mpaka sebuleni na kumkuta mama yake akiwa amekaa macho yangali kwenye runinga alimwangalia mama yake kwa mashaka makubwa hakujua kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka akaongozana na watu kama hao.Siku hiyo mama Shamsa alikuwa kwenye mawazo sana juu ya kumuondoa Jongo mikononi mwa mtoto wake, alijiapia lazima atamtafuta Jongo kwa udi na uvumba ili kumuangamiza kibasa hasikuwepo machoni mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama, kitu gani ambacho kinakutatiza naona kama una wawazo sana? Shamsa alimuuliza mama yake baada ya kukaa kitini

    “Hapana binti yangu, nipo kawaida sana mwanangu”Bi.Ramla alimjibu

    “Nilitaka kukujuza ya kwamba Naomba uniambie kile ulichotaka kuniambia, maana ulisema una mazungumzo nami”Shamsa alimwambia

    “Sawa, nilichotaka kukuambia ya kwamba Baba yako ameamua ya kwamba tuondoke hapa nyumbani kwako na kurudi katika nyumba yetu kutokana na Shangazi yako kuondoka nyumbani hapo na kuamia katika nyumba yake hivyo nasi tunatakiwa kuilinda nyumba yetu mwanangu”

    “Sawa mama haina tatizo kama mmeamua hivyo basi sina pingamizi kwenu”Shamsa alimjibu mama yake

    “Kuanzia sasa hatuonekana hapa isipokuwa siku moja moja tutakuja kukusalimu mwanangu wala usijali” Bi.Ramla alimpoza mwanae

    “Lakini mama sijajua kuhusu wito wa wageni uliokuja nao ndio kina nani?”

    “Shamsa mwanangu si nimekutambisha kwao mara hiyo umesahau mama?”Bi.Ramla nae alimtupia swali mwanae

    “Sio kwamba nimewasahau la hasha sijawai kuwaona wala kuwasikia hapo kabla”

    “Sawa yule msichana anayeitwa Aisha ni mwalimu mwenzangu yule ni mgeni shuleni hivyo amekuja kuniulizia kuhusu ratiba ya kesho kazini”Bi.Ramla alijitetea

    “Okay sawa je, yule mwanaume?”Shamsa alimtupia swali lingine mamaye

    “Yule mwanaume ni rafiki wa yule mwalimu niliyekueleza mwanangu usiwe na mashaka sana juu ya ugeni huo wana nia nzuri nawe, amekuulizia sana maana wanapenda kuwa rafiki yao”

    “Hee! Mama Urafiki wa aina gani huo?”Shamsa alihamaki

    “Urafiki wa kawaida tu mwanangu wala sio kwa nia mbaya”Mama yake alimjibu

    “Sawa, tuachane na hayo nakupa funguo ya akiba mama kama siku nyingine unakuja upite tu ndani moja kwa moja maana mara nyingi naweza kuwa sipo nyumbani” Mama yake alifurahi na kumshuku mwanae.



    Siku moja Shamsa alijipangia ratiba ya kurudi mapema kazini ili apate muda wa kwenda kutembea kwa marafiki zake pamoja na kuonganisha nyumbani kwao Ilala kwani ndipo yalipokuwa makazi mapya kwa Jongo. Lakini jambo hilo hakulifahamu kumtafuta hata siku hiyo alikuwa kama alivyokuwa kawaida yake alipotoka alielekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa baba yake lakini Ilala nzima alizunguka hakumuona japo alisikia kuna mtu akiitwa sana kwa jina hilo ila hakuwa na uhakika kama anayeongelewa alikuwa Jongo yule anayemtafuta.Shamsa alikuwa kawaweka watu wa kumsaidia kumtafuta Jongo pia alipojaribu kufanya mawasiliano nao hakupata jibu la kulizisha kwani Jongo hakuonekana sehemu popote pale.

    Je, alikuwa wapi, kama ndani ya chuo jina lake lilikuwepo ndani ya orodha ya wahitimu wa chuo hicho sasa amekwenda wapi na Je, shule ipi aliyopangiwa kufundisha baada ya kumaliza elimu yake? .........



    Mawazo yote yalikuwa yamemzunguka Shamsa juu ya mtu ampendaye Jongo alikuwa amemuacha kwenye wakati mgumu kwanini hakumwambia mapema kile ambacho kilikuwa kikimtatiza.Siku hiyo baada ya Shamsa kumkosa Jongo alirudi nyumbani akiwa amechoka sana kutokana na kazi ndefu.Alipofika mlangoni Laah! Alishangaa na kukuta mlango upo wazi hakushituka alijua ni mama yake hata alipoingia sebuleni alikuta mkoba kwenye meza iliyopo sebuleni hapo, ulimfanya aondoe shaka kabisa Shamsa alijitupa sofani ili kujipumzisha kwenye kochi.Ghafla akiwa hana hili wala lile macho yakiwa juu ya dali alisikia sauti ya kiume ikimsalimia alistuka na kunyanyuka sofani haraka na kusimama wima na kugeuka mzima mzima hakutaka kuitikia wala kusema neno.Alikuwa mwanamume wa mashaka machoni mwake alijionyesha alimkumbuka fika yule mwanaume ndiye yule aliyewakuta nyumbani hapo akiwa na mama yake pamoja na yule msichana.Abdul alipomwambia kuwa yeye ametumwa na mama yake kuja kumliwaza, Shamsa alimwangalia kwa jicho kali na kushangaa ndipo alipohoji.



    “Umefikaje ndani ya nyumba yangu wewe?”

    “Mama yako ndio aliyenikabizi funguo ili nije kukusaidia kazi za hapa nyumbani pamoja na kuwa na wewe siku ya leo”

    “Hee! wewe una maana gani sasa mpaka unadhubutu kuingia ndani kwangu?’Shamsa alimuuliza kwa hasira

    “Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu yako nakupenda ndio maana nimekuja kuwa nawe siku ya leo”Abdul alionge kwa kujiamini

    “Yaani wewe heti uwe nami inawezekana kweli?” Shamsa alimjibu kwa dharau

    “Inawezekana Shamsa niamini nakupenda na nina uwezo wa kukutimidhia kwa kila kitu”

    “Hapana sihitaji mwanaume wa aina yoyote”

    “Nakuomba sana Shamsa wewe ndio chaguo langu.....Nakupenda mama”Abudul alilalama

    “Hee! we vipi utanipendaje wakati hatujuani hata”Shamsa alisema

    “Nipo chini ya miguu yako Shamsa”

    “Nimesema sitaki naomba utoke ndani ya nyumba yangu”Shamsa alisema kwa ukali

    “Kwa hilo Shamsa umefika mbali”

    “Iwe mbali au karibu nishasema ondoka ndani ya nyumba hii”Shamsa aliongeza kwa ukali

    “Sawa kuondoka nitaondoka lakini sio kwa kunifukuza kama hivyo”Abdul alilalamika

    “Utaondoka muda gani sasa?”Shamsa aliuliza kwa mashaka

    “Muda si mrefu nitatoka ila nataka nikwambie kiu”

    “Sema nakusikiliza”

    “Si nimekwambia nakupenda”



    Muda wote Shamsa aliona vituko kutoka kwa kijana huyo hakutaka kuongea zaidi alimwambia anaenda chumbani kwake kupumzika muda mfupi ujao anataka kutoka kwenda kwenye biashara zake binafsi.Abdul alikubali huku akimwangalia Shamsa kwa jicho la tamanio na kumuambia ya kwamba anampenda na kumdhamini sana yupo tayari kwa kila jambo ili kuhakikisha anakuwa mikononi mwake.Kisha Jongo alimwambia ameshamchagulia nguo za kuvaa ambazo alimnunulia kama zawadi kwa upendo wake zipo ndani ya mfuko,Abdul alipomaliza kusema maneno hayo alichukua mfuko uliokuwepo hapo mezani na kumkabidhi. Shamsa aliupokea kwa mashaka makubwa akaufungua palepale na kuangalia kilicho ndani ya mfuko huo kama kweli ni nguo.Shamsa alitabasamu na kumwangali Abdul ambaye alikuwa na sura yenye bashasha, akaondoka na kuingia chumbani kwake.Alipoingia tu chumbani aliziangalia na kujalibu nguo hizo, alipoona zimemkaa sawa na kumpendeza aliziweka vizuri kitandani kisha alienda kuoga na baada ya muda alirudi. Hata pale alipotaka kuvaa nguo nyingine alishindwa moyo ulimsuta alijiona mkosaji kuupokea mzigo huo na kuuweka tu ndani ,akaamua kuvaa alizonunuliwa na Abdul ili kumfurahisha , baada ya kuvaa alitoka hadi sebuleni ili kumuonyesha Abdul zawadi aliyomnunulia ilikuwa imempendeza kweli Abdul alishangaa alipomuona Shamsa akiwa amebadilika na kuwa msichana mrembo wa huba.Shamsa alimshukuru Abdul kwa zawadi hiyo kisha aliongoza njia maana hakutaka kuzungumza sana na kijana huyo alimuaga kuwa anatoka kwa safari zake akimtaka naye atoke ili aweze kufunga mlango wa nyumba yake.Abdul hakutaka kutoka,badala yake aliendelea kukaa mahali hapo na kumwambia kabisa Shamsa kile alichokusudia kuwepo hapo nyumbani kwa siku hiyo, Shamsa hakuwa tayari alitoka na kumwacha Abdul ambaye mama yake alimtambulisha kama Rafiki wa mwalimu mwenzake Laah! Shamsa haikumuingia akilini kabisa, akawaza Abdul mwenyewe alisema ni mfanya kazi ambaye atamsaidia kazi za pale nyumbani.Kumbe hakuwa ni mwalimu bali ni kijana wa mitaani hakaona ni majanga sasa yamemkumba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda wa saa moja jioni Shamsa akiwa anarejea nyumbani kwake alikuta mlango upo wazi safari hii wala hakushituka kama mara ya kwana alishajua ya kwamba kijana huyo alikuwapo na wala hakuwa na dalili ya kuondoka siku hiyo.Wakati Shamsa akiingia ndani huku akitafakari juu ya kijana huyo kuvamia nyumba yake yote sababu ya mama yake Bi.Ramla,hakuwa na namna.Baada ya Shamsa kuketi sofani huku mawazo tele kichwani yametawala,Alikuja kustuliwa na Abdul akimwambia ya kwamba yeye alikuwa ameshapika na sasa chakula kipo mezani tayari ameivisha.Laah! salale Shamsa alishangaa akasimama wima na kumkatalia,Abdul akukubali kushindwa mwanaume kama yeye kubembeleza na kushawishi aliweza na ndivyo alivyofanya alimsogelea Shamsa pale aliposimama na kumwambia “Unajua jinsi gani nilivyoumia kutoka nje na kutafuta masoko ili nikuandalie chakula mpenzi wangu lakini mwenzangu utaki kula,sasa wataka nani ale mpenzi,nakuomba ule ata vijiko viwili tu vinatosha mpenzi nami nitapata furaha na buraha ndani ya moyo wangu”.Shamsa alimsikiliza kwa makini sana alimshangaa pale alipoingiwa na moyo wa huruma na kumuangalia Abdul kwa anavyolalamika akiwa chini ya miguu yake,Shamsa akaamua kula chakula hicho kilichopikwa na mkono wa mwanaume hasiyemjua.



    Shamsa alikula chakula kwa mbwembwe huku aibu ikiwa imemkaba moyoni mwake. Na alipomaliza kula chakula hicho akamsifia Abdul kwa uwezo wake wa kupika chakula kitamu kama kile,alimshukuru kwa chakula kizuri Abdul alifurahi na kumtaka asiwe na shaka kwa hilo.

    Muda wote Shamsa na Abdul walikuwa kwenye maongezi ya hapa na pale huku wawili hao wakionekana kuwa na furaha ndani ya mioyo yao.Waliongea mpaka saa tatu ya usiku ndipo kijana Abdul alipoaga na kuondoka huku akimtaka Shamsa hasiwe na wasiwasi juu ya kile anachokifanya. Shamsa hakuwa na papala alimwangalia tu Abdul akimuaga kwa ukalimu wa hali ya juu.Walipoachana kwa Abdul kuondoka Shamsa alikuwa na maswali mengi yasiokuwa na majibu kuhusu mwanaume huyo ambaye alikuwa mgeni machoni mwake.Shamsa ni kama kawaida yake mawazo yake yalihama mara moja na kumfikiria kijana Jongo kile ambacho alikihisi moyoni mwake kumpenda sana kijana huyo kuliko kitu chochote.Asubuhi kulipokucha aliingia kwenye vituo vya watu wenye ulemavu ili kuweza kuhoji kama kuna uwezekano wa mtu kumfahamu Kijana Jongo au kubahatika kumuona, siku hiyo ilikuwa haina matumaini tena kwa Shamsa kwa jinsi alivyompenda Jongo kwani alirudi nyumbani bila mafanikio.



    Siku zilizidi kwenda wiki siku zikapita bila Jongo kuonekana wala Abdul kuonekana akija nyumbani kwake,Shamsa mawazo yalimuendea kombo alijihisi kuumwa kila wakati lakini wala hakukubaliana na hali hiyo ya kushidwa.Alikaa chini na kujiuliza kile kinachomsumbua na hakujua hatma ya kijana ampendaye Jongo wala hakujua atampata wapi Jongo.Siku hiyo Shamsa alirudi mapema nyumbani alipofika alikuta tena mlango wa nyumba yake upo wazi, Shamsa alishtuka aliingia mpaka ndani na kuelekea hadi jikoni hakumuona mtu.Alitafuta huku na kule kila chumba akimwita mama yake lakini hakuna aliyemuhitikia basi aliingia chumbani kwake na kujitupa kitandani.Shamsa alikuwa ametingwa na mawazo mengi sana juu ya hali aliyokuwa nayo,alisikitika na kujutia huku akimlaumu mama yake juu ya hali aliyomuachia juu ya mwanaume anayemsumbua nyumbani kwake.Alijifikilia jinsi gani atamdhibiti Abdul ili asiweze kuinga tena nyumbani kwake bila ruhusa sababu ya funguo aliyokuwa nayo.Shamsa alikusanya mawazo yake na kupata jibu ya kwamba lazima abadili funguo ili aweze kumdhibiti kujana huyo hasiyemfahamu zaidi ya kuletwa na mama yake.....



    Muda mfupi baadae Shamsa akiwa amejilaza kitandani ndani ya chumba chake alisikia Sauti ya mtu akikohoa katika bafu analolitumia ndani ya chumba hicho kwake.Alistuka na kukaa kitandani huku macho yake yakiwa kwenye mlango wa choo kilichomo ndani ya chumba hicho. Moyo ulimuenda mbio Shamsa sasa akiwa hajui hafanye nini kwa wakati huo, mawazo yakamjia akaamua kusubili ili kumuona mtu atakayetoka ndani ya choo hicho.Hakiwa hajui nani atakayetoka, alikaa ndani ya chumba chake huku akitetemeka hasira zimemkaba akitamani kuvamia chooni na kumtoa mtu huyo.Muda huo huo bila kupepesa Shamsa macho yamemtoka pima kuyaelekeza mlangoni mwa choo hicho, pale alipoona mlango wa msalani ukifunguliwa.Laaah! mdomo alihacha wazi, hakuamini macho yake pale alipomuona Abdul akitoka maliwatoni akiwa amevalia bukta tu, ulikuwa mtihani mkubwa sana kwa Shamsa, kwani Abdul alikuwa hedsome boy hasa, alivyoumbika kwa umbo lake matata lililojengeka kwa mazoezi Shamsa alijikuta akikaa chini macho ymeganda maungoni mwa Abdul. Alijikuta akimtamani sana na kile kifua chate kipana ilikuwa mtihani kwa Shamsa, mwanamke yoyote angetokea kumkuta kwenye hali kama hiyo basi lazima angeshawishika kwa uzuri wa Abdul.Muda huo huo Abdul nae alifahamu hali aliyokuwa nayo Yaani wewe umeamua kunifanyia Shamsa, hivyo alitumia nafasi hiyo kumsogelea mahali alipokuwepo Shamsa.Alipoona hivyo Shamsa aliamua kuangalia na kusogea upande mwingine huku akimtaka Abdu asimsogelee badala yake avae nguo zake.



    “Yaani wewe umeamua kunifanyia kitendo kama hicho?”Shamsa alimuuliza angali macho pembeni

    “Ndio Shamsa sababu nakupenda sana nipo kwa ajili yako”Abdul alijibu kwa kujiamini

    “Hapana wewe utawezaje kunisaidia Mimi…sihitaji msaada wa aina yoyote”

    “Hapana sina msaada wowote kwako zaidi ya mapenzi nakupenda sana” Abdul alilalamika

    “Ndio nimekwambia sihitaji msaada wa aina yoyote kutoka kwako naomba uondoke nyumbani kwangu”Shamsa alisema kwa hisia

    “Sawa nitaondoka lakini sidhani kama kuna mtu akayetokea kukupenda kama mimi”Abdul alilalamika

    “Kama hayupo basi yupo njia anakuja wala sitakubali kuwa nawe”

    “Please Shamsa niangalie mara mbilimbili unifikilie maana nakupenda sana sipo tayari kukukosa”



    Shamsa alinyanyuka na kutaka kuondoka ,kabla hata hajapiga hatua mbili mbele Abdul alimuwai na kumshika mkono,Shamsa aliruka kutaka kujiondoa mikononi mwa afla wakajikuta Abdul lakini ilishindikana kwani alikuwa ameshikilia vilivyo na kumdhibiti maungoni mwake.Kukulu kakala zilianza Shamsa akimtaka Abdul amuachie lakini Abdul aliendelea kumshikilia kinguvu.Ghafla wanajikuta wakidondoka kitandani kwa pamoja wakagalagala na kulifanya shuka kujikunja, Shamsa aliogopa sasa akakusanya nguvu zake zote kutaka kujiondoka kitandani hapo alishindwa kumbe Abdul alikuwa amemshika vizuri kiunoni looh! Shamsa aligwayana hakuweza kutoka hakatulia.Abdul akaona nafasi ndio hiyo kutaka kufanya kile alichodhamilia kukifanya, taratibu Shamsa akaanza kuingiwa na joto la huba baada ya kumgusa Abdul kifuani mwake kumbuka alikuwa na bukta tu wala hakuwa na nguo nyingine.Shamsa aliweweseka kutaka kutoka maungoni mwa Abdul lakini mwenzake alimng’ang’ania kisawa sawa wala hakuona haja ya kumuachia.

    “Lakini kitu gani inanifanyia wewe mwanaume”Shamsa alibwata huku akijaribu kujiondoa mikononi mwa Abdu

    “Unajifanya uelewi kinachotokea basi utaelewa tu”Abdul alisema huku pumzi zikimuishia

    “Nakuomba uniache tu ukijalibu kunibaka utanikosea sana “

    “Hapana Shamsa ataka uwe na amani sababu nakupenda wewe”Abdul alimjibu

    “Niachie basi tuzungumeze, sasa unavyonibana hivi unafikiri nitawezaje kuongea”

    “Sawa basi kaa nakuacha mpenzi wangu”Abdul akamuachia Shamsa



    Shamsa haraka alinyanyuka toka kitandani na kujiweka vizuri kisha alisimama wima kando ya kitanda hicho,hakika alimuhacha njia ya panda Abdul hakutegemea kama Shamsa ataweza kumchomoka kiaina namna hiyo.Sasa aliwezaje kumkosa tena mwanamke kama huyo,Abdul hakuwa na jinsi alimwangalia kwa jicho la matamanio makubwa,alimpenda na kumtamani sana ila hakuwa na jinsi tena kwani mali alihiacha mwenyewe.Shamsa alipitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni na kukaa sofani huku akitetemeka.Muda huo huo Abdul nae alivaa nguo zake na kumfuata Shamsa sebuleni.Abdul alifika sebule akiwa na aibu moyoni mwake uso kaukinja huku akitazama chini wala hakuwa na haja ya kuangali kile kilichopo sebuleni hapo zaidi ya sakafuni. Shamsa alipomuona Abdul akikaa naye sofani Shamsa hakusema neno zaidi alimtakaAbdul aondeke na hakuwa tayari kumuona akiendelea kuwepo nyumbani hapo.Abdul hakuongea neno zaidi alivaa viatu vyake kisha akaondoka, baada ya Abdul kutoka muda huo huo Shamsa aliuwai mlango na kuufunga kwa ndani akarudi sofani huku akitweta.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku inayofuata hakutoka kabisa nyumbani kwake hata Abdul alipofika, alimkuta Shamsa yupo sebuleni aligonga mlango na alipofunguliwa Abdul aliingia moja kwa moja mpaka sebuleni.Baada ya kusalimiana Shamsa alimwangali kijana huyo huku akiwa na mashaka alimuuliza kile alichomleta tena ndani ya nyumba hiyo,Abdul alimjibu ya kwamba ametumwa na mama yake kuja kusuluisha kwa yale yaliyotokeaa.Shamsa akuendelea kuongea zaidi alijiuliza kama mama yake aliyajua vipi yale yaliyotokea jana,alishikwa na mshangao zaidi pale alipomuona mama yake akija nyumbani kwake bila ya taarifa ina maana walikuwa msafara mmoja Abdul na mama yake. Shamsa alijiuliza bila kupata jibu mwishowe alisikia mlango ukigongwa na mama yake akaingia ndani huku akiwa na tabasamu mdomoni mwake.Shamsa alinyanyuka na kumkaribisha mama yake kisha wakakumbatiana, Abdul aliwaangalia mama na mwana walivyokuwa wakikumbatiana kwa huba. Bi.Ramla alikaa sofani huku akiwa na mashaka kuhusu kile alichoambiwa na Abdul, hakujua kama Shamsa alikuwa ampendi Abdul zaidi moyoni mwake alimpenda kijana Jongo.

    “ Habari za huku mama “Shamsa alimsalimia mama yake

    “Salama tu mwangu niambie maendeleo yake”Bi.Ramla alimjibbu

    “Salama tu,naona leo umewai maana nilikuwa na safari ya huko huko”Shamsa alimjuza mama yake

    “Hivyo ulikuwa unataka kuja nyumbani, mbona ujaniambia”

    “Ndio maana nikakuambia umeniwai, hata hivyo karibu…Vipi Baba nae anaendeleaje?”

    “Baba yako ajambo mwanangu anakusalimia”Bi.Ramla alimjibu

    “Nashukuru….lakini mama bora umekuja nataka kujua huyu kijana ni nani?”

    “Si nilikuambia Rafiki wa yule mwalimu mwenzangu….vipi kwani kunanini?

    “Sio kweli mama naomba uniambie ukweli mama”

    “Hahaha….Shamsa bwana matendo yote anayokufanyia bado hujajua huyu ni nani?

    “Matendo yake ni dhahiri kwamba mwanaume huyu umenitafutia wewe ili aje kunioa mimi kwangu haiwezekani mama”Shamsa alisema

    “Ha! Shamsa binti yangu mpe nafasi mwenzako”

    “Hee! Mama jamani unannikuwadia kwa huyu mtu nisiyemjua”

    “Hapana mwanangu, naona siku zote hupo ndani ya nyumba hii peke yako ndio nikaamua nikutafutie mwenzi wa maisha mwanagu “Bi.Ramla alisema bila woga

    “Hapana mama mimi ndio mwenye maamuzi siwezi kukubaliana na hilo mama”Shamsa alimwambia mama yake huku machozi yanamtoka.



    Shamsa kwa hasira alitoka sebuleni na kuingia chumbani kwake huku akimuacha mama yake akiwa pamoja na yule kijana Abdul.Baada ya muda Shamsa alitoka chumbani kwake, uwii! Alishangaa akajishika kiuno looh! Alichokiona kilimuwaza mdomo wazi,alistuka alipomkuta mama yake akiwa amejiacha kihasara kwenye sofa moja alilokuwa amekaa pamoja na yule kijana anayedai kuwa ni rafiki wa mfanyakazi mwenzake.Shamsa alishikilia mdomo wake kwa kitendo alichokiona kwa mama yake mzazi akiwa anadendeka na Abdul,haijamuingia akilini hata lakini mama yake na kijana huyo walishtuka haraka na kukaa vizuri walijua hakuwaona kumbe mwenzao tayari alishayaona waliyokuwa wakifanya.Shamsa aliduwaa kwa sekunde kadhaa bila kusema neno Shamsaalipitiliza mpaka mlango na kuwaaga kuwa natoka kuelekea kwa rafiki yake aliyepo Tandika, mama yake alimuitikia kisha akatoka. Matembezi yake Shamsa alikuwa mwenye mawazo kila hatua anayopiga ndivyo alivyokuwa akizidi kuwaza na kuwazua mpaka akahisi kichwa kikimuuma na kamasi zikimtoka.Alikwenda moja kwa moja mpaka standi kisha akapanda gari la tandika na kufika nyumbani kwa rafiki yake anayeitwa Rose......



    Siku hiyo Shamsa alikuwa hana furaha kutokana na hali hiyo hata rafiki yake Rose alitambua tofauti aliyokuwa nayo Shoga ake,Akaamua kumuuliza kilichomsibu lakini Shamsa wala hakuwa na namna ya kumjibu shaga yake huyo kwa kile alichikioni kule nyumbani kwake alipomua mama yake na yule kijana Abdul wakifanya yao.Alimezea moyo wakazungua kile kilichomleta ya kwamba Shamsa alimuulizia rafiki yake Rose amefikia wapi juu ya kumuona kijana Jongo,Rose hakuwa na namna alijibu rafikiye pale alipokuwa amefikiajuu ya kumpata Jongo.Alimwambia kwamba alimwambia kwamba alimfuatilia Jongo baada ya kusiikia ndani ya chuo cha Uwalimu West Ilala.Alipoenda kule aliambiwa jinsi anapoishi jinsi alivyofika jijini Dar na kwa kipindi hicho Jongo alikuwa ameshaajiliwa jijini kwenye shule moja ya watoto walemavu inayoiwa Uhuru mchanganyiko iliyopo Buguruni.Shamsa alivyosikia hivyo alishangaa moyoni alijawa na furaha japo hakumuona hila kufahamu kwake alipo ndio faraja pekee aliyokuwa nayo.Baada ya maongezi hayo Shamsa na rafikiye walishinda pamoja huku wakiongea maongezi ya hapa na pale kisha ilipohitimu saa kumi ya jioni Shamsa alimuaga Rose kisha safari ya kurejea nyumbani ilipoanza.



    Ilikuwa jioni kwenye foleni kubwa Shamsa alimuona kijana mmoja Kipofu na fimbo yake mkononi, anatoka kwenye Super Market moja maeneo ya Buguruni Malapa huku akitembea kuelekea pembeni mwa barabara. Shamsa alipata mshituka bahada ya kuhisi kitu kati ya yule kipofu aliyemuona nje ya gari alilokuwepo, akiwa anaendelea kumwangalia yule kijana aliyekuwa akipiga hatua huku akifuatisha fimbo aliyokuwa mkononi mwake.Shamsaalianza kuvuta hisia akamtazama viruri yule kaka pale nnje, kama anamfananisha na mtu aliyewahi kumuon. Kabla Shamsa hajafaya lolote, alianza kufungua dirisha ili amwangalie vizuri ghafla ikaja Bajaji mpaka aliposimama yule kipofu, wakati kijana huyo akipanda Bajaji kuna mdada alitoka dukani anakimbilia sehemu iliposimama Bajaji huku akiita Kaka Jongo” yule kijana kipofu aliitikia na dada huyo alipofika pale alimpa mfuko alioshika. Shamsa aliona yote hayo akiwa ndani ya gari ila alishtuka, alipomuona live yule kijana aliyepewa mfuko Haa! Alishangaa mdomo ukiwa wazi alipomuona Kipofu huyo akipanda Bajaji kisha dereva aliondoa kwa mwendo wa kawaida. Shamsa haraka alimuomba konda kumpisha mlangoni, konda akagoma kwa vile alikuwa katikati ya barabara tena kwenye foleni hivyo asubiri kituoni,lakini Shamsa aligoma alimbembeleza vya kutoka huku akimuomba dereva kumruhusu konda wake kwani kuna jambo la muhimu ameliona lakini watu wote walikuwa kimya wengine wenye busara zao wakimtaka asubili kituo kipo jirani atatushwa Shamsa aligwaya na kutulia kusubili foleni.Akiwa amesimama mlangoni macho yake yaliiona ile bajaji iliyompakia Jongo ikaondoka.



    Baada ya kukataliwa kushushwa hapo dari ilifanikiwa kusogea konda akamshusha Shamsa kituoni kisha aliongoza moja kwa moja kwenda kule ilipoelekea hile Bajaji.Shamsa alipata kiwewe alipomuona Jongo ameshapita akiwa ndani ya Bajaji hiyo. Shamsa alivuruga akili yake hakujua la kufanya kwani alikuwa tayari ameshamkosa Jongo, wala hakukata tamaa haraka mawazo yalimjia alimfuata yule mdada aliyetoka dukani na kumletea mfuko kijana yule kipofu.Alipoingia tu ndani kumuuliza yule dada kama kijana aliyetoka mle kununua vitu na kumkimbilia kumpelekea mfuko wake jina lake anaitwa Jongo? Alipojibiwa ndiyo hakuridhika na kuamua kuuliza tena kwa mara ya pili jibu lilikuwa lilelile kwamba ndiyo huyo anayeitwa Jongo. Shamsa alirudi mpaka pale stand ya daladala aliona achukue pikipiki ili kuifuatilia ile Bajaji iliyombeba Jongo, alipofika hapo alielekea zinapopaki pikipiki na kuongea dereva kisha kuanza kuifuata Bajaji ilipoelekea kwa mwendo kasi.Alifuata kwa kuhisia barabara lakini hakufanikiwa kuiona, muda wote huo dereva bodaboda alimshangaa, hata alipomuliza kitu gani kimetokea lakini Shamsa alikuwa anahema wala hakuwa na muda wa kujibu .Hivyo dereva huyo alibaki na maswali kibao maana hakujibiwa kitu, baada ya kufuatilia na kuikosa bajaji huyo aliamua kumuomba dereva ampeleke nyumbani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku hiyo Shamsa alirudi nyumbani akiwa amechoka sana, alipofika aligonga mlango maana alijua ya kwamba amewaacha Bi.Ramla na Abdul, kweli mlango ulifunguliwa alitoka mama yake akiwa amevaa kanga moja akiwa amejifunga juu ya kifua chake na nyingine ameizungushia kiunoni.Shamsa alishangaa zaidi kumuona mama yake akiwa katika vazi hilo alihamaki hakujua kwa nini siku hiyo mama yake alikuwa kwenye hali hiyo hakuelewa.Kitu alichokifanya Shamsa baada ya kuingia ndani alijitupa sofani macho yake yakiwa juu ya kufua cha mama yake kuanzia juu mpaka chini,Bi.Ramla wala hakujali alipitiliza moja kwa moja mpaka ndani ya chumba alichokuwa akilala na mume wake kabla ajaondoka nyumbani kwa mwanae.Shamsa alikuwa na mashaka makubwa hakujua mama yake siku hiyo alipatwa na nini mpaka kuwa katika hali hiyo alimwangalia jinsi alivyokuwa akitembea kwani aligundua kitu kisicho cha kawaida pale alipomuona mama yakke nywele zikiwa zigizaga huku makalio yake yakitikisika na kuonyesha kama ndani ya makalio hayo kukuwa na nguo ya ndani aliyovaa zaidi ya kujitupia kanga hizo.Shamsa alizidi kumakinika pale sebuleni alipoviona viatu vya Abdul vikiwa pembeni vimeifadhiwa, nguvu zilimuishia hakujua kama mwanamume huyo alikuwa sehemu gani,haraka alijipa nguvu alinyanyuka na kuelekea jikoni alimtafuta lakini hakumkuta, alirudi tena chumba kingine mpaka msalani kote alimtafuta lakini hakukuwa na uwepo wa kijana huyo.



    Sio kama Shamsa hakuwa akimpenda Abdul la hasha alipata mashaka juu ya uwepo wa Mama yake na kijana huyo ndani ya chumba alichoingia mama yake.Ni chumba ambacho kilikuwa ndicho alizokuwa akiweka ubavu wake na mumewe mahali hapo, sasa Shamsa akakihesabia chumba hicho ni cha heshima kwa baba na mama yake.Alifikiri kwamba baba yake amekuja na labda yupo ndani na mama yake lakini mawazo hayo Shamsa aliyapinga wala hakuona kama yalikuwa sahihi kuwa akilini mwake.Alifikiria kwa jinsi gani mama yake amebadilika kiasi hicho,hakutaka kupoteza muda aliongoza chumbani kwake huku akiwa na mawazo juu ya mahali alipo kijana Abdul.Shamsa akiwa nyumbani kwake alikuwa mtu mwenye mawaza ghafla akiwa chumbani mwake alisikia sauti ya ajabu ikitokea ndani ya nyumba yake,alistuka alitoka kitandani na kutoka mpaka sebuleni akasikiliza vizuri na kughundua kwa sauti hiyo inapotokea.Shamsa moyo ulianza kumuendea mbio baada ya kukifikia chumba walichokuwa wanalala wazazi wake hapo kabla hawajaondoka.Akasikia sauti na biguno ya mahaba , shamsa alizidi kuchanganyikiwa hakuamini kile alichokua anakisikia alisogelea karibu kabisa na mlango wa chumba hicho kisha ajivutz mpaka ukutani na kushikilia mlango huo akachungulia ndani kuptia tundu la funguo. Looh! Shamsa alipagawa hakuamini kama funguo ilikuwa imeziba kuona cha ndani kinachoendelea, hakukubali hali hiyo alichungulia tena na tena akagongana na kutu cha kushangaza hakuamini macho yake aliona kila kitu kilichokuwa kimetokea ndani ya chumba hicho. Zaidi alishangaaakaona kizunguzungu kwa jambo lile aliloliona kupitia utundu wa funguo pembeni yake, maana funguo ilikuwa ikining’inia kwa ndani.Mda huo alisikia mama yake akibishana na Abdul chumbani wakiwa peke yao Shamsa hakuamini,aliona kama yupo ndokani lakini kiukweli ndio ilikuwa kweli pale alipojichunguza kuwa hakuwa akiota bali ilikuwa kweli.Shamsa hakutaka kuangalia kinacoendelea maana alikuwa ameshawaona wakivyokuwa wakibishana namna ya kutoka ndani ya chumba hicho kama kufanya walikuwa wameshayafanya tayari sasa walisubili kutoka naye Shamsa ndio akarudi....



    Wakati wote huo Bi.Ramla akibishana na Abdul jinsi ya kutoka ndani ya chumba walichokuwepo, Shamsa yeye alikuwepo tu sebuleni amejituliza macho yake yakiwa ameyaelekeza kuangalia chumba walichokuwa. Hakika ilikuwa fedhaha kubwa Shamsa kumuona mama yake kulala chumba kimoja na kijana huyo, moja kwa moja mawazo yalimjia juu ya usariti uliotawala yaani hakuelewa kwa jinsi gani alikuwa kwenye hali hiyo.Mama yake alimueleza juu ya kijana huyo juu ya kuwa ni rafiki ya maana kwamba mpenzi wa yule mama mwenzake lakini leo hii anakuja kila kukicha nyumbani kwake na kujifanya anampenda. Ametumwa na Bi.Ramla kumsaidia kazi kumbe ni muongo kabisa akamtongoza lakini Shamsa alimkatalia ndipo leo anakuja kuwafuma wakiwa chumbani na mama yake Loo! Laana iliyoje kwa mama mtu mzima kutembea na kijana mdogo Shamsa alichoka.



    Wa kwanza kutoka alikuwa alikuwa Abdul kisha nyuma yake alitokea Bi.Ramla wote wakiwa wamevaa nguo zao kama ya kwamba walikuwa tu wametulia ndani ya chumba hicho kumbe Shamsa alikuwa ameshajua kinachoendelea kati yao.Cha kushangaza Abdul alipitiliza mpaka mlangoni kisha alivaa viatu vyake na kutoka bila kuaga,Bi.Ramla alijipindapinda na kukaa sofani huku macho yake yakimwangalia kwa kuibia mwanae.Shamsa hakutaka kuzungumza kitu alimwangalia mama yake anaye naye alikuwa akimwangalia wakajikuta wakigonganisha macho yao na Bi.Ramla akatazama pembeni kwa aibu.Shamsa alipoona hivyo hakutaka kumuuliza kitu mama yake badala yake alinyanyuka na kuingia chumbani kwake,lakini Bi.Ramla alijisikia vibaya kwa aibu aliyokuwa nayo alimuita mwanae lakini Shamsa hakuwa na muda naye alipitiliza na kuzama chumbani kwake.



    Siku iliyofuata Shamsa alienda kazini alifanya kazi zake kama kawaida lakini hakukaa sana na kuamua kuomba ruhusa kwa madai ya kwamba anajisikia kuumwa kichwa hivyo aliomba kwenda hospitali.Shamsa alipotoka hakwenda hspitali kama alivyodai badala yake alikwenda kwenye ile supermarket ya jana yake alipomuona kijana aliyemfananisha kama ndio Jongo. Alipofika aliingia ndani na kumkuta yule dada wa jana aliyekuwa akimuhita, Shamsa alipofika ndani ya duka hilo kwa bahati nzuri alimkuta dada huyo mrefu mwembamba kwa adabu akamsalimia. Shamsa hakutaka kupoteza muda akaanza kujieleza na kumtaka dada huyo ambaye alikuja kujitambulisha kuwa anaitwa Mwanahamisi, Shamsa alimtaka amsaidie jinsi ya kumpata Jongo. Haikuwa kazi ngumu kwa Mwanahamisi kumjibu Shamsa kile anachokijua juu ya kijana huyo mwenye ulemavu wa macho.Mwanahamisi alimueleza Shamsa ya kwamba kuna msichana mmoja anayeitwa Zainabu ambaye yeye ni rafiki yake mkubwa hivyo kupitia rafiki yake huyo ambaye ni dada wa Jongo atafanikiwa kuonana naye. Mwanahamisi aliendelea kumjuza ya kwamba mara nyingi Jongo upendelea kufika hapo akiwa pamoja na dada yake ambaye ni Zainabu. Jongo pamoja na dada yake huyo wanaishi pamoja maeneo ya Tabata ila yeye hakupajua tabata sehemu gani hivyo alimtaka amsubiri kwani Zainabu anaweza kufika siku hiyo. Shamsa alimshukuru Mwanhamisi kisha walipeana namba za simu kisha Shamsa hakutaka kuondoka alikuwa tayari kukaa hapo hili kumsubili muda huo ambao Zainabu alitarajiwa kufika.



    Jioni ilipofika Shamsa akiwa hapo hapo amejiinamia akiangalia saa yake kama imefika muda ambao alitakiwa kuonana na dada wa Jongo. Alikaa macho yake yakiwa kwenye saa kubwa iliyopo ndani ya duka hilo jicho la pili lilikuwa likiangaza kwenye llango kuu la kuingilia ndani ya duka hilo.Kila mteja aliyekuwa akiingia Shamsa alimtupia jicho akijua ya kwamba ndio mtu aliyekusudia kuonana nae lakini haikuwa hivyo, alikaa na kusubili mpaka akachoka na kukata tamaa.Shamsa akiwa mtu mwenye mawazo sana juu ya kijana Jongo mara ghafla alistushwa na Mwanahamisi akimwita jina lake, Shamsa alimshangaa pale dada huyo aliponyoosha kidole kikimuelekezea msichana mmoja akitembea kule walipoketi.Moja kwa moja Shamsa amawazo yalamtoka sasa alimwangalia kwa makini msichana huyo mrembo, ilikuwa kama saa kumi na moja jioni Dada huyo aliingi huku Mwanahamisi akimkaribisha kwa bashasha tele usoni mwake, huku akimwita jina la Zainabu.Yule msichana mrembo Zainabu alifika na kuanza kusalimiana na Mwanahamisi kisha akamsalimi Shamsa bila kuchelewa Zainabu akaanza kutafuta vitu anavyovitaka kutoka ndani ya duka hilo.

    “Samahani anti?” Shamsa alimwambia baada ya kumfuata Zainabu kule alipokuwa

    “Bila samahani dada!”Zainabu alimjibu

    “Naomba unisaidie kitu kimoja dada”

    “Nimabie dada kama kikiwa ndani ya uwezo wangu nitakusaidia”Zainabu alimjibu

    “Nadhani unaitwa Zainabu wewe ni dada ake na Jongo?” Shamsa aliuliza

    “Yes! Jongo ni mdogo wangu”

    “Sawa naomba unisaidie nionane naye tafadhali”Shamsa aliomba

    “Unataka kuonana na Jongo kuna tatizo?” Zainabu aliuliza

    “Hapana…mimi ni rafiki yake ninayeitwa Shamsa, tulisoma wote jiji Mwanza”Shamsa alijibu“Oooh! Wewe ndiye msichana Shamsa?” Zainabu aliuliza kwa wahika huku akiwa mwenye tabasamu usoni mwake

    “Ndio mimi dada, naomba kuonana na Jongo namtafuta sana”Shamsa alisema

    “Hata Jongo pia anakutafuta sana mdogo wangu, kila siku simulizi yake Shamsa naona leo akikuona itakuwa furaha sana kwake”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hanishindi mimi hapa nilipo natamani angekuwa mbele ya macho yangu, nampenda sana Jongo” Shamsa alitoa hisia zake

    “Usijali tutayazungumza cha zaidi Jongo yupo salama tunaishi pamoja nyumbani hivyo nisubili nikimaliza tu kukusanya vitu basi tutakwenda pamoja”Zainabu alimwambia

    Maneno ya Zainabu yalikuwa yenye barafu ndani ya moyo wa Shamsa, alijawa na furaha kusikia habari za Jongo alitamani dada huyo amalize upesi ili kuwai kumuona Jongo.Shamsa alijipa moyo na kumsubili Zainabu mpaka pale alipomaliza, wakaanga na dada mwenye duka hilo na safari ya kuelekea nyumbani kwa kina Jongo ilianza.Njia nzima Shamsa alikuwa mtu mwenye mawazo, hakuamini kama kweli siku hiyo ndiyo siku ambayo anakwenda kukutana kwa mara nyingine na Jongo. Hawakukawia kufika tabata kutokaa na siku hiyo kutokuwa na foleni, mtu wa kwanza kuingia ndani alikuwa Zainabu, Shamsa alifuatia nyuma huku akiwa na mashaka kukutana Jongo siku hiyo kulipa kiwewe..



    Zainabu alipofungua mlango tu, Shamsa hakuamini macho yake yalikutana na Jongo aliyeketi kwenye kochi lililokuwa sebuleni, Shamsa alishindwa kujizuia alikimbia moja kwa moja na hadi karibu alipoketi Jongo na hapo hapo akajikuta machozi yakimtoka. Kwa bashasha aliyokuwa nayo akamuhita kwa hamaki “Jongo!” alishtuka kwa vile hakujua kama dada yake amekuja na mgeni, Jongo kwa mshangao akakulupuka na kuuliza “nani tena wewe?, kabla Shamsa hajajibu Mama Jongo alitokea naye kwa mshangao akalopoka na kumuhita “Shamsa!” wakati wote huo Zainabu alikuwa anawaangalia hasijue la kufanya, akamuona Shamsa akinyanyuka na kwenda alipokuwa Mama Jongo amesimama kwa hamaki. Shamsa kama swala alimrukia Mama Jongo kwa pamoja wakakumbatiana.Kila mmoja alionekana kuwa na furaha huku Jongo akiwa kwenye mshangao hakuamini wala hakutarajia kama Shamsa angekuja kukutana nae tena. Alijiuliza kichwa mwake iweje Shamsa apajue pale nyumbani? Na kama ameulizia je, amejuaje kama yupo jijini dar, alikumbuka siku moja miaka miwili iliyopita akiwa chuoni alisikia sauti ya Shamsa lakini hakubahatika kumuona. Jongo alinyanyuka na kusimama akionekana mtu mwenye mawazo na kumuuliza mama yake.

    “Mama huyu ndie Shamsa ninayemfahamu mimi?”

    “Ndiyo Jongo mwanangu huyu unayemsikia ndio Shamsa uliyekuwa ukimuulizia kila siku”



    “Hapana mama mbona kama unanidanganya, naomba Shamsa usogee karibu yangu”



    Shamsa alisogea karibu na Jongo huku machozi yakimtoka, alipofika karibu na Jongo alimshika mkono na Jongo naye akafanya hivyo na kuanza kumpapasa Shamsa Pajini mwa uso wake Shamsa yalizidi kumtoka pale Jongo alipomshika juu ya jicho lake na kukutana na kipele kikubwa cheusi kinachojulikana kama kidoti. Hapo ndipo Jongo alipolidhika kama kweli aliyekuwa mbele ya macho yake alikuwa Shamsa. Bila kutarajia Jongo machozi yalimtoka, si kwa hudhuni yalikuwa machozi ya furaha, Shamsa japo alikuwa akilia pia ila hakutaka kumuona Jongo akitokwa na machozi alichukua kitambaa chake na kuanza kumfuta machozi. Jongo alimwambia Shamsa ya kwamba “nimekutafuta kwa muda mrefu bila ya mafanikio mpaka nikakata tamaa ya kukutana tena nawe” Shamsa kusikia maneno hayo alisikitika na kumkumbatia tena Jongo. Muda wote walikuwa wamekaa chini wametulia wawili hao na kuanza kuongea, ambapo kila mmoja alimwambia mwenzie jitihada alizozifanya kumtafuta mwenzie.Siku hiyo ilikuwa ya furaha kwao kwani kutokana na mambo yote yaliyokuwa yakifanyika nyumbani kwake wala hakuwa na haja ya kurudi mapema, Shamsa alichelewa kutoka nyumbani kwa kina Jongo.Aliondoka usiku sana na aliporudi nyumbani alimkuta Mama yake anapika, Shamsa hakuhoji kitu badala yake alimsalimia mama yake na kuingia chumbani. kwa shingo upande Bi.Ramla alimwita mwanae ili wazungumeze,Shamsa hakusita alimkubalia mama yake na kueleke sebuleni.

    “Shamsa binti yangu naomba usinifikirie vibaya mama” Bi.Ramla alisema baada ya kuketi sofani

    “Sawa mama lakini naomba uiambie ukweli kuhusu huyo Abdul ni nani?”

    “Abdul ni kijana wangu uwa ananisaidia mambo mengi sana hivyo naomba usinifikirie vibaya mwanangu” Bi.Ramla alijitetea



    “Lakini mama si ulinitambulisha ya kwamba Abdul ni rafiki wa yule dada, kumbe ulikuwa unanidanganya”Shamsa alisema

    “Hapana Shamsa siwezi kukudanganya” Bi. Ramla alisema kwa hofu

    “Nimeshajua kama Abdul ni Baba yangu mdogo hee! Wala sio kama ulivyokuwa ukidai”

    “Sio kweli kama natembea na huyo mvulana ni mdogo kwangu angalia, niwezaje kutembea nae wakati baba yako yupo jamani”Bi.Ramla alijitetea

    “Unayosema wewe ndio unadanganya mama nimeyaona kwa macho yangu unayoyafanya mama”

    “Haa! We mtoto umeyaona wapi kutuona tukitoka chumbani ndio tushafanya, hapana usifike huko binti yangu”



    “Hapana sitaweza kunyamaza lazima nimwambie baba”

    “Shamsa huyu Abdul anakupenda wewe anataka akuoe mwangu”

    “Hati anioe wakati ameshalala na wewe mama lakini mbona sikuelewi kabisa jamani”Shamsa alimwambia mama yake yale aliyoyaona wakiyafanya na hivyo kupelekea Mama huyo kujisikia vibaya kupita maelezo. Yote hayo Shamsa hakujali hivyo alimtaka mama yake kuwa na amani lakini si kuendelea tena kuwa na Abdul ahachane naye kabisa la sivyo atamueleza baba yake yake.Bi.Ramla alimsihi mwanae asifanye hivyo ili kuondokana na matatizo yatakayoweza kutokea.Shamsa alimkubalia mama yake kisha alimwambia habari juu ya kumuona Jongo, b. Ramla alijifanya kufurahi lakini kumbu moyoni alikuwa na kinyongo na Jongo hakumpenda mwanae kuwa na mwanaume huyo kipofu.



    Siku hiyo muda wa kulala Shamsa alikuwa mwepesi sana tofauti na siku zote,alichukua simu yake na kumpigia Jongo.Haraka Jongo alipokea simu hiyo na kuiweka masikioni mwake kisha wakaanza kuzungumza mambo mbalimbali,Jongo alifurahi sana kumsikia Shamsa akizungumza ahadi walizokuwa nazo juu ya mahusiano yao. Walimaliza kuzungumza kisha kila mmoja akimtakia mwenzake awe na usiku mwema na Shamsa akahaidi siku inayofuata atakwenda tena nyumbani kwa mama Jongo. Asubihi kulipokucha kama kawaida Shamsa alijiandaa kisha alitoka mpaka sebuleni ili kumsalimu mama yake, alipofika sebuleni alikuwa tayari ameshajiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda kwa Jongo.Shamsa hakutaka kumuaga mama yake kama anakwenda kwa Jongo badala yake alimuaga anakwenda Kazini, Shamsa alianzaf safari hadi Tabata nyumbani anapoishi Jongo.Alipofika aliwasalimia kisha hakukaa sana alimuomba mama Jongo amchukue Jongo ili waende kutembea, Mama Jongo hakuwa na pingamizi alikubali Shamsa na Jongo waende wanapotaka kwenda.



    Siku hiyo Shamsa alikuwa na furaha sana walitoka huku Shamsa akiwa na Bajaji iliowapeleka mpaka Msasani Beach Club. Walikunywa wakala na kusaza huku wakiongea mambo mengi juu ya maisha yake Jongo baada ya kuachana nae jijini mwanza, kisha Jongo naye alimueleza ya kwamba alipoamishwa shule ya sekonda alikaa sana nyumbani ndipo baadae walitokea wasamalia kumsaidia kumleta jijini Dar. Jongo aliendelea kumueleza baada ya kusaidiwa akajiunga na chuo cha uwalimu pale Ilala walimlipia ada pamoja na mambo mengine kisha kufanikiwa kuhitimu ndani ya miaka mitatu akawa mwalimu kamili aliyetunukiwa Diploma.Sasa ameajiliwa kufundisha shule ya msingi uhuru mchanganyiko, Jongo alisimulia zaidi ya kwamba pale anapoishi ni kwa dada yake Zainabu alimuomba waishi pamoja mpaka pale atakapomaliza kuijenda nyumba yake huko mpiji magoe......CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Shamsa alimpa hongera yake na kufikia hapo alipofikia ni juhudi za muumba wa mbingu na ardhi kwa uwezo wake, kwani ndio aliyefanikisha kukutana kwao, Shamsa na Jongo walishinda pamoja mpaka jioni. Shamsa alipoona muda umekwenda na walitakiwa kurejea nyumbani walitoka na kutaka kupanda bajaji yao waliokuwa wamekodi kwenda na kurudi. Ilikuwa majira ya saa kumi na mbili kuelekea saa moja jioni kiza nacho kikianza kuingia, Jongo alimuomba Shamsa akubali ili amvalishe pete ya uchumba ili aweze kutambulishana kwa wazazi. Shamsa hakuamini alimuuliza Jongo alipoipata Pete hiyo, Jongo alimuomba kwamba Shamsa akubali kuvalishwa Shamsa alikubali kisha aliomba aelezwe aliinunua wapi na kwa muda gani maana usiku wa jana walikuwa wote na asubuhi pia alifika nyumbani kumchukua sasa kama kwenda alikwenda saa ngapi kuinunua? Jongo alimueleza ya kwamba Pete hiyo alimuagiza dada yake siku nyingi sana kabla hawajaonana kwani alimueleza dada yake juu ya msichana Shamsa ndipo alipokubali kuinunua pete hivo na kuiweka ndani mpaka pale watakapokutana na kumvisha na kweli yametokea sasa pete ilitakiwa ivishwe sehemu yake.Hakika ilikuwa furaha sana kwao, kiukweli Shamsa alimpenda sana Jongo kwani yeye ndio alikuwa chaguo la moyo wake.



    Muda wote huo Jongo akiongea Shamsa alikuwa akilia kwa furaha, taratibu alinyoosha mkono wake na kuachia kiganja chake, Jongo naye alishika pete hiyo na kuivisha kidoleni mwa Shamsa kisha wote kwa pamoja wakakumbatiana kwa furaha.Wala hawakutaka tena kuendelea kukaa mahali hapo walipanda bajaji iliyokuwa ikiwasubili muda wote wakaongoza njia kurudi nyumbani kwa mama Jongo Tabata.Walifika nyumbani kwa Mama Jongo, walimkuta mama huyo akiwasubili kwa hamu kubwa, baada ya kufika na kuketi sofani Jongo alimueleza Mama yake kuhusu mahamuzi yaliyofikia. Mama Jongo hakuwa na pingamizi lolote juu ya maamuzi yao kwani Mama huyo anajua walipotoka mpaka walipofikia pia alifurahi mno mwanae kumuoa mtu ampendaye.Siku hiyo Shamsa na Jongo walipanga siku ya kwenda nyumbani kwa wazazi wake Shamsa, hawakutaka kuchelewa, walipanga siku inayofuata ndio watafanya taratibu za kufika nyumbani hapo kujitambulisha.Siku hiyo Shmsa aliongea mambo mengi sana huku wakiwa na furaha ya hali ya juu kwa kila mmoja wapo, alimueleza Jongo na mama yake kuwa kesho yake ndio walitakiwa kwenda kujitambulisha nyumbani kwao. Jongo na mama yake walikubali japo waliona harakalakini hawakuwa namna.Shamsa aliongea kwa muda kisha akaaga na kuondoka nyumbani kwake huku akiwa mtu mwenye mawazo, alimuwaza sana Jongo kila wakati alijiangalia kidoleni na kuishikashika pete yaani akionekana ahamini kile kilichotokea. Haikuchukua muda Shamsa alifika nyumbani kwake huku akiwa mtu mwenye furaha alitamani Jongo awepo jirani yake wayafurahie maisha. Baada ya kufika nyumbani hapo alipitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni, aliangaza huku na kule lakini nyumba ilikuwa kimya kabisa, hata alipokwenda chumbani mwa mama yake pia hakukuwa na mtu moja kwa moja akajua ya kwamba mama yake tayari alikuwa ameshaondoka.



    Kutokana na furaha aliyokuwa nayo siku hiyo Shamsa hakutaka kusubili alichukua simu na kuwasiliana na wazazi wake, wazo la kwanza alimpigia mama yake na kumuuliza kama ameondoka nyumbani hapo. Bi.Ramla alimuitikia mwanae kwa sasa yupo nyumbani kwake akiwa na mume wake Samir, Shamsa alimueleza mama yake kuwa siku inayofuata atamleta mchumba atakayemuoa, wazazi waliitikia kwa furaha ila ilikuwa furaha zaidi kwa mama mtu akijua ataletewa amtakaye yeye yaani Abdul.

    Kesho yake muda aliowaambia wazazi wake kama atafika Shamsa uliwadia mama na baba yake walisubili kwa hamu ili wamuone mkwe wao, Mara walisikia mlango ukigongwa na walimtaka anayegonga apite. Kama mawazo yao yalivyokuwa walimuona Shamsa akiingia huku akimsaidia Jongo kuingia sebuleni na kuketi nae kwenye kochi, wakati wao wanaingia ndani ulikuwa na mshangao kwa wazazi kwani hawakujua yule ndiye mkwe wao mtarajiwa mwenyewe? Bi.Ramla hakuwa na namna alisubili utambulisho kutoka kwa mtoto wake.

    Kisha wazazi waliwakalibisha na kuwasalimia pia walimchangamkia mtoto wao na wageni aliokuja nao kisha ukimya ulitawala mpaka Shamsa alipoamua kumtambulisha Jongo kwa wazazi kama Mume mtarajiwa. Mama yake Shamsa alishtuka akamuliza mwanae “huyu ndiye mwanaume unayetaka akuoe?” mama Shamsa akiwa katika mshangao Shamsa alijibu na akiwaeleza kuwa alimchagua muda mrefu, ndiye mwanaume atakayemfaa na pia wanapendana sana. Baba yake Shamsa Bwana Samir aliingilia kati na kumpongeza binti yake“Hongera sana Mwanangu usiwe na wasiwasi najua kwa kiasi gani umeteseka juu ya kijana huyu” kwa kumpoza mwanae kwa sababu anajua vizuri mkewe kuwa hakulizika na yule mwanamume mlemavu wa macho.



    Bwana Samir alimfuata Jongo na kumkalibisha kwa mikono miwili na kumtaka ajisikie yupo nyumbani, Kwa kitendo cha bwana Samir kumpa faraja Shamsa ilikuwa furaha kwa Jongo kwani alijua jinsi alivyo mlemavu, ingekuwa vigumu kukubalika na wazazi wa Shamsa kwa sababu ya ulemavu wake. Shamsa na Jongo walifarijika na kuongea kwa muda mrefu huku wakionesha furaha waliyokuwa nayo juu ya mapenzi yao.Bwana Samir alifurahi ila Bi.Ramla alionyesha chuki ya wazi kwa mwanamume huyo Kipofu, Jongo alifahamu ilo kwa hisia kuhisi mama huyo kukaa kimya.Hata alipojalibu kuhoji kilichotokea mpaka mama kukaa kimya Shamsa hakuwa na muda wa kumjibu alimtaka Jongo kuwa na hamani, kwani asingejisikia vizuri kwa tabia aliyoinesha mama yake.Baada ya maongezi ya hapa na pale Bwana Samir alimuuliza Shamsa wangependa harusi ifanyike lini, Shamsa alitaka ifanyike mwezi unaofuata haraka iwezekanavyo. Mama na baba yake walishtuka kusikia kauli ya mtoto wao kuona akitaka harusi ifanyike haraka namna hiyo, Shamsa hakuwa na jibu la maana alichoamua yeye ndio ifanyike mwezi ujao. Shamsa aling’ang’ania ndivyo alivyoamua mwenyewe shughuli ifanyike kama kawaida, walipomaliza mazungumzo yao Shamsa na Jongo waliaga na kutaka kuondoka, Jongo anyanyuka na kumfuata Baba Shamsa vizuri alipewa mkono na kuagana kisha alimfuata Bi.Ramla kutaka kumuaga Mama huyo hakuitikia kitu wala mkono hakuupokea. Jongo hakujali hivyo aligeuka na kuanza kutoka nje ya nyumba huyo na kuondoka.



    Shamsa na Jongo walipokuwa wanatoka na kuondoka Bi. Ramla aliachia sonyao kali lililomfanya mumewe Samir kumwangalia jicho kali kwa fedheha.Jongo alikosa kuelewa kwa nini Mama Shamsa hakuwa na furaha na hivyo hakujua kama harusi itafanyika hama haitofanyika ila hakuonyesha dalili ya kushtuka au kushangaa kwa jambo hilo.Waliondoka wakiwa ndani ya Bajaji waliyoikodi, wakati wakiwa njiani wakirejea nyumbani Jongo alimuambia Shamsa kuwa harusi haitaki kufanyika haraka inahitaji subira.Shamsa alishtuka kusikia vile kutoka kinywani kwa Jongo Shamsa alimuuliza “kwani wewe mwenzangu utaki kunioa mimi” Jongo alimjibu “sina maana hiyo ila tunahitaji muda hili mambo yaende sawa” Shamsa alishindwa kuelewa na kutaka kuelezwa kwa kirefu alikuwa na maana gani. Sauti ya Shamsa ilimfanya Jongo kujua kam amekasilika kusikia vile maana ni kweli Shamsa amekasilika kwani ni muda mrefu alikuwa anasubiri jambo hilo litokee kwa wawili hao.Ilibidi Jongo amueleze alivyokuwa akihisi na kuwa na mashaka juu ya mama yake Shamsa.

    “Shamsa naona mama yako ajalizika na mimi kukuoa wewe kwa hiyo tunahitaji muda wa kumshawishi mama yako ili akubaliane nasi na kutupa Baraka”



    “Hapana Jongo wewe ndio changuo langu kumbuka niliyekupenda ni mimi” Shamsa alijibu maneno hayo kwani yalikuwa yamemuingia akilini mwake na kumfanya apunguze makali, sababu yeye alijionea mwenyewe jinsi mama yake alivyomchukia Jongo ikabidi Shamsa amuulize,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa unafikiri tutafanyaje kama tusipochukua maamuzi mapema”

    “Sijui cha kufanya kwa sasa maana naona mama yako hayupo tayari kutuona pamoja”“Hapana haiwezekani kututenganisha tena, basi naomba kuanzia sasa tuishi pamoja nyumbani kwangu” Shamsa alisema kwa kujiamini



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog