Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

CHAGUO LANGU NI WEWE - 5

 





    Simulizi : Chaguo Langu Ni Wewe

    Sehemu Ya Tano (5)



    Halikuwa wazo baya wala gumu kwa Jongo kwani alikubali mara moja, Shamsa hakuwa na kinyongo alimpeleka Jongo nyumbani kwao kisha wakaagana watakutana siku inayofuata na yeye kurudi nyumbani kwake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shamsa alipofika nyumbani kwake alimkuta Abdul, Shamsa alishangaa sana hakujua afanye nini kwa wakati huo hata alipomsalimia, hakuitika badala yake alipokea lawama kutoka kwa Abdul. Shamsa alimshangaa Abdul akiwa ana hasira akidai amemsaliti kwa kutembea na mwanaume kipofu wakati wameshakubaliana waanze kuwa marafiki kisha ndio uchumba utafuata.Shamsa alimsikiliza kisha akamwambia pole yake kwa kupoteza muda kwani kipindi chote alikuwa na mpenzi aliyekuwa akimtafuta kwa muda mrefu sasa amempata.Abdul alikuja juu ghafla na kupinga maamuzi ya Shamsa, Shamsa alipomuona Abdul yupo kwenye hali hiyo nae hasira zikamjaa akamtaka ampe funguo yake ya nyumba, kwani mwenyewe ameshampata mchumba wake wa siku nyingi na kesho anakuja kuhamia nyumbani hapo kuishi pamoja. Abdul hakuwa na namna alitoa funguo kwenye mfuko wake wa shati lake na kumtupia Shamsa bila kuonyesha dalili yeyote kama alikuwa nazo zaidi ya moja kisha aliondoka kwa hasira. Shamsa alimsindikiza kwa macho hadi mlangoni na kupotelea gizani.....



    Siku iliyofuata asubuhi na mapema Shamsa alienda kumchukua Jongo nyumbani kwao alipofika alikaa mpaka mchana wakiongea mambo mabalimbali na mama Jongo. Ilipohitimu saa kumi za jioni Shamsa na Jongo waliagana na Mama Jongo kisha kuanza safari ya kurudi Nyumbani kwa Shamsa. Siku hiyo Jongo na Shamsa walikua ndani ya nyumba ya Shamsa, walikuwa watu wenye furaha hata walipotembelewa na ndugu na jamaa waliona sahihi kuwa wawili hao waliishi na furaha kupita kiasi ni mama yake Shamsa tu ndiye aliyekuwa hana furaha na mahusiano ya mwanae hata siku moja hakumpenda Jongo.



    Siku moja Bi.Ramla na kijana Abdul aliyekataliwa na Shamsa walipanga kuonana sehemu ili wayajenge juu ya harusi inayotaka kufanyika kati ya Shamsa na Jongo. Walipokutana Mama Shamsa hakuwa na amani hata kidogo alianza kumwambia kile kilichokuwa kinamtatiza



    “Tufanye nini kwani sipo tayari kuona mwanangu akiolewa na yule kipofu”? Bi.Ramla aliongea



    “Hata mimi mama sipo tayari kumkosa na kumpoteza Shamsa kirahisi namna hii, nampenda sana binti yako ila ujui tu”



    “Sawa ndio maana nimekuhita hapa ili tujue cha kufanya” alisema Bi.Ramla



    “Ikiwezekana kumuua Jongo basi itakuwa vizuri” Abdul alitoa wazo



    “Hapo sasa umenena kijana wangu ndio maana napenda vijana wakakamavu kama wewe, ila tu kama huyu kijago akishauawa najua Shamsa hatokubali kuolewa na wewe kwa sababu ameshajua mahusiano kati yangu na wewe” Bi.Ramla alimwambia



    “Hee! Unasemaje? Shamsa amejuaje, umemwambia au?” Abdul aliuliza maswali mfululizo



    “Sikumwambia ila ametuona tulichokuwa tunafanya tukiwa chumbani”



    “Mmmh! Lakini aitakuwa tatizo nitafanya kila njia niwe nae” Abdul alisema kwa kujiamini

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa tuzungumze kilichotuleta ni kwamba Shamsa atasafiri hivi karibuni kikazi hivyo itakuwa nafuu kumteka Jongo au nitampigia simu usiku kumwambia kwamba naumwa lazima atatoka na kumuacha Jongo peke yake hapo itakuwa vizuri zaidi” Bi.Ramla alisema walikubaliana na kuagana na kupanga kuonana siku nyingine.

    Siku ya jumamosi majira ya saa saba usiku Shamsa na Jongo wakiwa wamelala hawana hili wala lile, ghafla simu ya Shamsa ikaita walistuka haraka Shamsa aliichukua na kuangalia mpigaji alikuwa mama yake akapokea na kuiweka sikioni. Simu upande wa pili ilisikika mama yake akidai na kulalamika kwamba amezidiwa ghafla na anataka msaada wa kupelekwa hospitali, Shamsa alitoka usiku hakuona haja ya kumsumbua. Hakutaka kumuamsha Jongo sababu alilala fofofo pia Mama yake alimsihi asisumbuke kumwamsha Jongo sababu ya hali yake ya kutokuona wasije kumsumbua.Shamsa alimwacha Jongo akiwa kwenye usingizi, Shamsa alipotoka nje na kuingia kwenye gari ambalo lilikuwa linamsubili baada ya kumpigia dereva amfuate na kuondoka, huku nyuma Abdul aliingia ndani na kufungua mlango mdogo wa geti ambao alikuwa ameuchongesha. Abdu alikuwa na msichana yule ambaye Bi. Ramla alimtambulisha mwanae kuwa ni mwalimu mwenzake.

    Waliingia mpaka sebuleni na kusimama nje ya mlango wa chumba cha kulala cha Shamsa kisha na kuanza kushauriana jinsi ya kumbeba Jongo wakamuue na wamtupe polini, wakakubaliana, waliingia ndani. Abdul alichukua kichpa kidogo kisha akamimina dawa kwenye kitambaa kilichokuwa mikononi mwake kisha akamfunika nacho juu ya pua ya Jongo kisha akambeba Jongo mpaka nje kisha walikuta gari ikiwasubili wakampakia Jongo na wapo wakaingia kisha wakaondoka mpaka polini walianza kumpiga na kumwagia maji. Jongo alishtuka fahamu zikamrudia na kujikuta yupo sehemu tofauti na alipokuwa mara kwanza kitandani sasa alipapasa chini akahisi majani na watu wawili wamemzunguka wakiwa wameshikilia mapanga na visu wakivinoa. Jongo alihisi kitu cha ajabu kikimgusa mgongoni mwake moja kwa moja alifahamu lilikuwa panga limemgusa mgongoni mwake, alijalibu kupiga kelele lakini Abdul alimzuia na kumwambia akijalibu kufanya hivyo basi mara moja atakitoa kichwa chake. Aisee Jongo alichoka akanyama huku machale yakimcheza kuhusu watu hao, waliendelea kumuuliza maswali ambapo Jongo hakuweza kuwajibu zaidi alisisitiza kuhachiwa, lakini wao waliendelea kumpiga mpaka Jongo akapoteza fahamu na kuanguka chini kama mzigo.Hawakutaka kupoteza muda Abdul na yule msichana walimchukua na kumtupa kichakani ndani ya poli hilo, kisha walikimbia kwa woga wakijua kuwa Jongo tayari ameshakufa.

    Akiwa ndani ya tax Shamsa alikuwa mtu mwenye mashaka usiku huo, hakujua mama yake amepatwa na tatizo gani, alijiuliza mara mbilimbili ila hakupata jibu. Shamsa aliwasili nyumbani kwa mama yake, alimuomba dereva wa tax amsubili ili akamuangalie mama yake yupo kwenye hali gani kama ikiwezekana wampeleke hozpitali, dereva alikubali na Shamsa mara moja akagonga geti kubwa na mlinzi alimfungulia. Shamsa hakumsalimia mlinzi wala kumuuliza kitu akazama ndani, mlinzi alimshangaa kitu gani kilichokuwa kimetokea kwa usiku huo, alitoka akiwa na mashaka makubwa na kuifuata ile gari iliyopaki nje. Huku Shamsa aliingia mpaka ndani akakuta taa imezimwa akaiwasha kisha akapitiliza mpaka chumbani mwa mama yake huku akiita Mama….Mamaaa, Maama…Shamsa aliita bila kuitikiwa alifufungua mlango wa chumba cha mama yake na kuingia ndani na kuwasha taa, alipoingia tu macho yake yalitua juu ya kitanda alicholala mama yake. Shamsa alimsogerea mpaka karibu kabisa na kitanda hicho kisha akaanza kumuamsha mama yake laikini kila akimuamsha Bi.Ramla alikuwa kimya, alimtingisha tena lakini wapi Bi.Ramla alikuwa kimya kitandani hakukohoa wala kutikisika alilala chali huku povu likimtoka mdomoni.

    Shamsa alichanganyikiwa kumuona mama yake akiwa kwenye hali hiyo alitoka mpaka nje na kumkuta mlinzi hayopo alihita kwa sauti kubwa akiomba msaada.Mlinzi pamoja na yule dereva wa tax aliyokuja nayo pale nje waligutushwa na sauti hiyo, kwa pamoja walikimbilia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Shamsa akiangaiki huku na kule kumwamsha mama yake. Mlinzi alipoona hivyo walisaidiana na dereva na kumnyanyua Bi.Ramla na kumtoa nje na kumpeleka mpaka kwenye gari wakamuingiza ndani.Shamsa akaingia siti ya nyuma akiwa amemkumbatia mama yake, huku dereva haraka alipanda ndani ya gari na safari ya kuelekea hospitali ilipoanza.Muda wote Shamsa alikuwa akimlilia mama yake huku kijasho chembamba kikimtoka hakutaka kumuona mama yake akipoteza maisha kwa wakati huo, njia nzima alimuomba mama yake jinsi gani awasaidie ili wafike hospitali salama na mama yake atibiwe na kupata nafuu.



    Gari ilikuwa mwendo kasi ilipita mitaa na maeneo mbalimbali na hatimaye waliwasili hospitali ya Amana, Dereva alipiga honi geti likafunguliwa na Gari ikapita mpaka ndani na kuegeshwa Bi.Ramla akafumbua macho yake na kumtazama mwanae ambaye alikuwa akilia hasijue la kufanya. Ghafla Shamsa alishtuka alipomuona mama yake akinyanyuka na kukaa kitako, Dereva nae sasa alikuwa wima akiwa tayari kumnyanyua mgonjwa kumuingiza mapokezi ile anafungua mlango tu aliachia mdomo wazi akimshangaa Bi.Ramla alivyokuwa kama mzimu nywele zote timtimu. Looh! Shamsa hakutaka kuamini mara wahudumu nao walikuwa wanafikika kuwasaidia kumbemba mgonjwa.

    “Habari, mgonjwa mwenyewe yuko wapi tafafali” mhudumu mmoja alisema kati ya wezake watatu

    “Huyu hapa…” Shamsa alisema bila kupepesa na kumnyooshea kidole mama yake

    “Oooh! Kumbe anaweza kutembea haina haja ya kitanda, basi njoo mama tukusaidie twende kwa daktari” Muuguzi huyo alisema

    “Njoo nikushike mkono twende Bi.Mkubwa” Mwingine nae aliongeza

    Bi.Ramla alitoka mwenywe ndani ya gari na kuongozana huku wauguzi wawili wakiwa wamemshika huku na huku na kumsaidia kumpeleka mpaka kwa daktari. Daktari alipomuona alishangaa alijua labda mama huyo hana akili timamu maana Bi.Ramla alikuwa akicheka tu hovyo, Shamsa alijieleza jinsi ilivyokuwa maana Bi.Ramla kila alipouliza kitu gani kinachomsibu yeye alijibu wala hakuwa mgonjwa hivyo aliomba tu wamrudishe nyumba lakini Shamsa alisisitiza mama yake kuwa mgonjwa alitakiwa kupata matibabu.Daktari na manesi walishauriana jinsi ya kufanya maana Bi.Ramla aligoma kupatiwa kipimo chochote na kusisitiza hakuwa mgonjwa kama alivyokuwa bali usingizi tu ulimchukua na kumfanya kuwa vile alivyokuwa, Shamsa hakuwa na namna alikubali mama yake apewe dawa na kurejea naye nyumbani na ndivyo ilikuwa Bi.Ramla aliandikiwa dawa za marelia wakidhamilia ya kwamba itakuwa imempanda kichwa hivyo walimuandikia kuanza dozi.Shamsa na Dereva wa tax aliyokuja nayo walikuwa wamechoka haswa, Bi.Ramla alikuwa amewachanganya yaani ametoka nyumbani mgonjwa kufika hospitali mgonjwa anasema kwamba haumwi kumbe ilikuwaje, alidanganya au alifanya kusudi ?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya nusu saa Jongo alilejewa na fahamu zake ndipo taratibu kumbukumbu zilianza kumrudia mpaka akawa sawa, alikumbuka kuwa alikuwa ametekwa na watu asio wafahamu. Hapo hapo akaanza kuogopa akijua kuwa wale watu bado wapo mahali hapo, Jongo akaanza kusema “jamani nioneeni huruma mimi sina kosa lolote lile mnaniua bure” aliongea maneno mengi huku akibwabwaja lakini hakuna aliyemjibu.Alipoona kimya hakuna dalili ya kuwa na mtu maeneo hayo alianza kuinuka na kukimbia hovyo huku mikono yake ameielekeza mbele kumsaidia kujikinga na kitu kibaya.Jongo hakujua sehemu aendako alifuata tu kijia cha nyasi na hatimaye baada ya hatua mbili tatu alikutana na barabara kubwa ya waendao kwa miguu, kwa hatua za haraka aliifuata barabara hiyo kubwa. Jongo alikuwa akitembea kwa pupa kama mtu aliyekimbizwa hofu ilimjaa tele moyoni mwake aliwaza na kumuomba mungu wake amsitiri na kumfikisha salama nyumbani.Jongo alitembea kwa kila hatua na kipande chake cha mtu kilichokuwa mkononi mwake akikitanguliza mbele, akafikia kwenye nyumba mmoja ya nyasi ndefu aliichunguza kwa pale nje ile nyumba kisha akaketi akimuomba mungu wake atende miujinza kama kuna mtu ndani ya nyumba atokee kumsaidia.



    Ghafla Jongo akiwa nje ya nyumba hiyo alitokea Mzee mmoja mwenye ndevu nyingi, Mzee huyo akashangaa kumuona mtu nje ya nyumba yake, alisogea hili kumuangalia vizuri mtu huyo. Alishangaa alipomuona kijana kipofu akiwa amegeemea kiwambaza cha nje ya nyumba yake, Mzee huyo aliyeitwa Kilapo alijongea mkapa mlangoni mwa nyumba yake na kumsalimia Jongo. Jongo alishituka kusikia sauti ya mtu akimsabahi haraka aliitikia kwa mashaka na hofu moyoni mwake akahamkia, Mzee Kilapo aliitikia na kumkaribisha huku akimuangalia na kuingia ndani kwake kisha akatoka. Mzee Kilapo alimwangalia Jongo kwa mara nyingine tena kisha akamuuliza alipotokea.



    “Kijana naona sura yako ngeni kwangu, sijawai kukuona hapa kijijini unatokea wapi?”



    “Yaani historia ndefu sana mzee wangu nakuomba unisaidie maji ya kunywa kwanza”Jongo alisema



    “Sawa wala usijali kijana wangu” Mzee Kilapo alisema na kuingia ndani kisha akatoka na maji kumpati Jongo akapokea



    “Kijana wangu naona kama una majeraha sijui umepatwa na maswahibu gani, niambie kilichokusibu” Mzee Kilapo alisema baada ya kumchunguza Jongo



    “Mzee nilikuwa nimetekwa na vijana nisiowafahamu, walikuja nyumbani usiku wakanichukua bila kujijua, nilipokuja kuzinduka nikajikuta polini nimezungukwa na jamaa mmoja akiwa na mwanamke. Walinipiga na kunitesa mpaka nikapoteza tena fahamu, baadae nilipokuja kuzinduka sikusikia sauti zao wala sikujua walipokuwa ndio nikajikuta Napata nguvu na kutembea mpaka nikafikia hapa”Jongo alimwambia



    “Aisee! pole Sana kijana nikupatie huduma kwanza kisha mengine yatafuata”



    “Hapana mzee wala nisikupe taabu nahitaji mawasiliano kama inawezekana nifike kwanza nyumba au nimjulishe mama naona atakuwa ananitafuta muda huu”



    “Kwa hilo usijali nitakupeleka mjini kwa baiskeli yangu kisha utapiga simu na kupanda gari kurejea nyumbani lakini kwanza subili utapate hata kifungua kinywa”



    “Sawa Babu nashukuru sana kwa msaada wako”



    Mzee Kilapo aliingia ndani kisha akachemsha maji, yalipopata moyo aliyatoa na kuanza kumkanda Jongo sehemu alizoumia, baadae alibadika chai na ilipoiva walikunywa pamoja na Jongo.Mzee huyo alimkilimu Jongo alimpa kila aina ya huduma kisha na dawa akampatia na kumataka apumzike ili yeye aende kuijaza upepo baiskeli yake kwa jirani.Baada ya nusu saa Mzee huyo alirejea na kumtaka Jongo ajiandae kwa ajili ya safari ya kumuongoza mjini, walianza safari kwa amani, Mzee Kilapo aliwa dereva na Jongo akikaa nyumba kwenye kiti cha abilia akisikilizia baiskeli ikiyoyoma. Walipanda mabonde na kuyashusha milima, hatimaye wakawasili mjini wakiwa na amani, Mzee Kilapo alimuongoza Jongo kwenye kibanda cha kupigia simu, kisha Jongo alitaja namba za mama yake na simu upande wa pili ikahita.Jongo alimueleza mama yake jinsi ilivyokuwa na jinsi pale alipofika alimuomba mama yake ajiandae kumlipia nauli kwani yeye anapanda tax itakayomfikasha nyumbani.Mama yake alikmkubalia mwanae huku akiwa na mashaka makubwa juu ya hali aliyokuwa nayo mtoto wake. Baada ya kumaliza kuongea simuni Jongo alimgeukia Mzee Kilapo na kumwambia ampeleke zilipo tax, Mzee huyo alishangaa atawezaje kupanda tax kwa umbali uliokuwepo kuanzia Kibaha mpaka dar ni nauli nyingi lakini Jongo hakujali wala hakutaka kupanda gari ya kawaida kwa kuofia usalama wake hivyo mzee Kilapo alimuelewa akampeleka zilipo tax.

    Jongo waliongea na dereva wa tax walielewana atampeleka kutoka kibaha mpaka Dar kwa shilingi 30,000. Jongo alikubali kisha aliagana na Mzee Kilapo kisha safari ya kurejea jijini ilipoanza.Walitumia masaa mawili kufika jijini Dar,Jongo alimueleza kabisa mahali anapoishi mama yake dereva akamfikisha mpaka Ilala Boma kisha dereva alisimamisha gari mbele ya nyumba yao.



    Baada ya gari kusimama alionekana Mama Jongo na dada yake Zinabu walikuja mpaka nje ya tax hiyo na kumtoa Jongo ndani ya gari kisha mama Jongo alimlipa Dereva pesa yake.Jongo alijitaidi kujikokota huku Zainabu akimsaidia mpaka chumbani na hata mama Jongo alipomalizana na dereva aliingia ndani na kumkuta mwanae analia sana huku kainamisha kichwa chini Zainabu akimbembeleza.Mama Jongo alimbembeleza na kumuliza kilichotokea Jongo alimwadithia kama ilivyotokea na Mama yake aliamini sababu mwanae kupendwa na Shamsa ndio sababu ya kutekwa na watu hasiowafahamu je, muda huo Shamsa alikuwa hayupo na kama hakuwepo alikwenda wapi na wakati walilala wote usiku huo?.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mama yake alimshauri wasubili kama Shamsa akimtaka basi atakuja kumtafuta au atapiga simu lakini Jongo aling’ang’ania kumpigia simu Shamsa muda huo. Shamsa hakupiga simu wala kwenda nyumbani kwa mama Jongo, alikuwa tu kwa mama yake akimuuza na kumsaidia kazi. Shamsa wala kazi hakwenda. Siku hiyo alishinda tu nyumbani lakini moyo wake ulikuwa mzito kila lipokuwa akiwaza juu ya jongo kutompigia hata simu naye alipatwa na mashaka, hakujua kama Jongo amepatwa na maswahibu gani. Siku hiyo jioni Shamsa aliamua kumpigia simu Jongo, Jongo aliipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwake na simu upande wa pili ikasikika.



    “Hallow Jongo” Shamsa alitamka



    “Hallow Shamsa kwema mke wangu?”



    “Kwema kiasi Jongo..Mbona kimya sana upo wapi?”



    “Nipo kwa mama nilipata matatizo makubwa sana” Jongo alisema



    “Najua ukufahamu nilipotekwa na kupelekwa msituni kuteswa” Jongo alimwambia



    “Umetekwa na nani Jongo mbona unanichanganya mpenzi?” Shamsa alilalama



    Shamsa hakutaka kusubili haalijilaumu kukaa kimya muda wote bila kujua kama Jongo anaendeleaje nyumbani alipomuacha peke yake, alijilaumu kwanini alimuacha Jongo peke yake, alipata wapi ujasili wa kutoka huku akimuacha Jongo amelala hakujua kama mtu aliyemuacha alihitaji msaada kwa namna gani. Yote hayo alijiwazia huku akiwa makini kumuangalia mama yake, Bi.Ramla alikuwa tuli ametulia kwani aliyasikia maongezi yote yaliyokuwa yakisimuliwa kati ya mwanae na Jongo, hivyo yeye akuongea kitu alichukizwa na kitendo cha Jongo kuwa hai tena, hili akulionyesha usoni mwake bali lilikuwa likimtibua ndani ya moyo wake aliwalaumu sana Abdul na mwenzake kumuacha kijana huyo kipofu akiwa mzima.Haraka Shamsa alinyanyuka kwa hasira na kutoka mpaka nje kisha akaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Jongo.......



    Baada ya mwendo wa boda boda Shamsa aliwasili nyumbani kwa Mama Jongo akiwa na mashaka makubwa, alipoingia tu ndani alimkuta Jongo na mama yake sebuleni, Shamsa alishangazwa na hali aliyomkuta nayo Jongo.Mama Jongo alipomuona Shamsa alihamaki na kumkalibisha kwa shingo upande, baada ya Shamsa kuwasalimia na kutaka kujua kitu gani kilikuwa kimemtokea mpenzi wake huyo, Mama Jongo alimwangalia kwa jicho kali kama kwamba Shamsa alijua kila kitu kilichomsibu kumbe hakuwa akijua chochote kinachoendelea.



    “Mama Mbona Jongo yupo hivi…. sana kwema mama?” Shamsa aliuliza kwa mshangao



    “Unauliza nini wewe…..ulichofanya unadhani kizuri kwa mwanangu?” Mama Jongo alijibu kwa dharau



    “Hapana Mama ulikuwa ni usiku sana na niliona nikimuamsha nitamsumbua Jongo kwani nilitoka kumpeleka mama yangu hospitali, maana alinipigia simu usiku wa manane kichwa kikimsumbua nikaamua kuondoka na kumuacha Jongo chumbani” Shamsa alimjibu



    “Unamwona mwanangu mlemavu si ndio, unamfanyia vitu vya makusudi utamuachaje peke yake nyumbani, alafu unanidanganya eti umempeleka mama yako hospitali wakati ulikwenda kwa wanaume wako” Mama Jongo alibwata



    “Hapana Mama nakuambia ukweli muulize hata Bi.Ramla atakuambia kilichomsibu” Shamsa alishtuka kuona mama mkwe wake yupo kwenye khari hile



    “Wewe na mama yako lenu moja ulimtaka mwanangu ili kumtesa kisha umuue”Mama Jongo alisema



    “Jongo sielewi kwa nini wewe na mama mnanishutumu kwani nimefanya kosa kutoka bila kukuaga, sikutaka kukusumbua mpenzi” Shamsa alimlalamikia Jongo



    “Bora ungekaa huko huko bila mimi kujua lakini ndani ya nyumba yako wanakuja watu kunichukua wanipeleke kuniua nimekukosea nini Shamsa” Jongo alilalama



    “Sijakuelewa una maana gani Jongo kusema hivyo?” Shamsa alimtupia swali



    “Sababu ya mapungufu yangu sioni hili wala lile, dhamani kwako imeshuka ndio uniingizie watu ndani sababu ni nyumbani kwako Shamsa, waje kuniua bora usingenipeleka nyumbani kwako, Ndio Kama tabia zako za ushenzi namna mimi nawe basi tena tuachane sitaki kuteska” Jongo alisema huku akilia



    Maneno ya Jongo yalimshtua Shamsa kwa kweli akilini mwake akujua nini kimetokea, alijitahidi kumweleza kuwa alienda kumpeleka mama yake hospitali, hivyo hakuwepo ndani usiku huo yeye akitekwa lakini Jongo hakumwelewa.Jongo alinyanyuka ghafla na kutaka kuingia chumbani lakini mama yake alimuwai na kumzuia, akamshika mkono akimtaka arudi kitini wayamalize. Badala ya Jongo kukubali lakini alikataa alijivuta ili kuunasua mkono wake toka mikononi mwa mama yake lakini ilishindikana Jongo alijikuta akiponyoka mikononi mwa mama yake na kuteleza akadondoka chini kama mzigo na kuzimia.Shamsa alipata kiwewe kumuona Jongo pale chini ametulia na mama Jongo nae liweweseka hasijue la kufanya, kwa pamoja walishauriana kumbeba Jongo na kumpeleka hospitali.Baada ya kufika hospitali Jongo alipatiwa matibabu haraka na hatimaye kuamka, dokta alimwita Shamsa na mama Jongo kuwataalifu ya kwamba Jongo alipata mshtuko pia kwa vipimo zaidi inaonyesha ana presha na ndio imesababisha yeye kuanguka na kuzimia kwa mshtuko aliopata.Ilikuwa taarifa njema kwa Shamsa na mama Jongo kwani kila mmoja alinyoosha mikono juu na kumshukuru mungu baada ya kumnusulu na matatizo mengine Jongo. Baada ya kutoka chumbani kwa dokta Shamsa alimtaka mama yake Jongo waongee pembeni na Shamsa akatoka na kuwaacha wawili hao wakizungumza.



    Baada ya muda mama Jongo alitoka, Shamsa alimuliza mama Jongo alichoambiwa na Daktari kisha nae akamwelezea jinsi Jongo alivyopata mshtuko na sasa ameandikiwa dawa za kutumia akiwa nyumbani. Shamsa alifurahi na kumkumbatia mama Jongo huku akimuomba msamaha na kumueleza hatoweza tena kwenda sehemu bila kumuaga Selemani wala baya kama lile kujitokeza tena.

    Jongo akiwa kwenye chumba cha kulazwa mgonjwa mama yake aliingia akiwa na Shamsa pembeni, Jongo alipogundua mama yake ndiye aliyeingia alifurahi Sana na kuonyesha furaha wazi wazi wala hakuja kama Shamsa alikuwepo pia. Alishambiwa na dokta kama hakuna tatizo na tayari alihusiwa kurea nyumbani. Wakati Wakiwa kwenye maongezi ya furaha mama yake aliingizia swala la Shamsa pale pale kuhusu kuuguliwa na mama yake Jongo hakuelewa mama yake kwa nini alianzisha mazungumzo hayo Jongo alibadilika mara moja na kuacha kumuangalia mama yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mwanangu najua unampenda Shamsa au naongopa?” Mama Jongo alianzisha mazungumzo kisha akaedelea



    “Mwanangu mahusiano si kitu cha kuchezewa ni lazima upitie mambo mengi na usimlaumu Shamsa kwa mambo yaliyotokea, inawezekana yeye hakufahamu kitendo ulichofanyiwa kwani huna ushaidi kamili mwanangu?”



    “Mama inauma mi sijui nani aliyenifanyia kitindo hiki jamani au mama wewe unajua?”



    “Hapana mwanangu hamna mzazi anayemtakia mabaya mwanae, unatakiwa kukumbuka wapi ulipotoka na Shamsa pia ufikilie jitihada za Shamsa kahakikisha upo kwenye furaha na la mwisho ufikilie sasa upo kwenye wakati gani na unamuhitaji Shamsa ili kuishi pamoja kama mke na mume” Mama yake alisema......



    Maneno ya mama yake yalianza kumuingia akilini Jongo pia aliona anahitaji kuwa karibu na Shamsa kwani ndio mapenzi yake yalipo na ndiye chaguo la moyo wake. Jongo alikuwa mtu mwenye mawazo alifikilia jinsi gani alipopata shida kumtafuta Shamsa, akajikuta kweli toka moyoni akimpenda Shamsa pia hakutaka kumuumiza. Alijisemea moyoni inanibidi nisamehe tu kwa yaliyotokea Jongo na mama yake walikumbatiana kwa furaha tena, Mama Jongo alimtaka Shamsa asogee karibu yao ili azungumze na mwenzake. Jongo alishangaa kumbe wakati akiongea na mama yake kila kitu Shamsa alikisikia ina maana alikaa kimya huku mama yake alijua kama Shamsa alikuwepo chumbani humo ila hakumwambia. Shamsa alikuwa na woga kwani hakujua ahanzie wapi kuhusu kosa linalomkabili, Shamsa alianza kwa kumsalimia Jongo na Jongo alitikia kwa furaha na buraha kama kawaida kisha Shamsa aliendelea kumuuliza hali yake Jongo kisha akamuomba msamaha kwa kile kilichomtokea kwani yeye hakuwepo ndio maana yote hayo yakatokea.Jongo akafurahi kusikia Shamsa akitubu na kuomba msamaha naye kwa moyo mkunjufu akamsamehe.Shamsa alifurahi kuona ya kwamba Jongo amekubali kumsamehe na kuelewa kile kilichotokea kama Shamsa hakuwepo wakati akitekwa. Kwa furaha na upendo Shamsa na Jongo wakakumbatiana huku Shamsa na kumuahidi haitokuja kutokea tena akatekwa au kufanyiwa kitu kibaya.



    *******

    Wakati Shamsa akiondoka bila kumwambia mama yake alijua kila kitu alichokuwa akiongea na simu juu ya hali aliyokuwa nayo kijana Jongo.Bi.Ramla hakutaka kusubili maana rohoni alijutia kwanini alimkabidhi Jongo mikononi mwa Abdul aliyekuwa akimuamini kumbe ilikuwa kazi bule wala hakukikamilisha kile kilichokuwa kinahitajika kufanyika.Bi.Ramla alinyanyuka na kuingia ndani akachukua simu yake na kumpigia Abdul na kumueleza kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa Shamsa. Abdul hakuamini aliamua kumupigia mwenzake na kumueleza kile alichoambiwa naye alishangaa kwani wao walijua tayari Jongo ameshakufa, walilaumiana kwanini hawakuwa tayari kumpima Jongo kwa kile kilichokuwa wamekifanya kilikuwa kitu cha uzembe wa hali ya juu.Wakapanga kukutana ili wajue kwa namna gani watamtafuta tena Jongo ili kufanikisha kile walichodhamilia.



    Baada ya Bi.Ramla kuzungumza na Abdul na kupanga kwa namna gani watakuwa pamoja kufanya mahamuzi, Bi. Ramla alishangaa akawaza na kuwazua kwa jinsi gani atamdhibiti Jongo kuwa na mwanae. Kiukweli akupenda kumuona Shamsa akiwa pamoja na Jongo hivi alihakikisha atafanya kila njia ili kumualibia Jongo kuwa pamoja na Shamsa.Siku hiyo ilikuwa mbaya kwake japo alijifanay mgonjwa kumbe hakuwa mgonjwa ila yote sababu ya kutaka kumuua na kumpoteza Jongo.Lakini hata hivyo Bi.Ramla anatembea na Abdul je atafanikisha vipi kwa kijana huyo Abdul kuwa na mapenzi kwa mwanae wakati yeye pia anatembea nae, hivyo itakuwaje sasa haya tungoje tuone itakavyokuwa mimi na wewe tunasubili.



    *******

    Siku moja Shamsa alikuwa nyumbani kwake baada ya wao kumalizana na Jongo kuruhusiwa hospitali, siku hiyo Shamsa hakwenda kazini alikuwa mapumziko ametulia sebuleni akiongea na Jongo story za hapa na pale. Shamsa alikuwa mwingi wa furaha mara wakiwa wanaendelea na maongezi yao simu ya Shamsha akaiangalia simu hiyo kwa makini maana hakujua namba ya mpiga ilitokea tu bila jina hivyo alipatwa na mashaka juu ya hali hiyo. Alipiga moyo konde na kuipokea simu hiyo, wala hakuamini masikio yake kile alichokisikia kuwa kwa siku hiyo ya mapumziko akihitajika kazini, kila alipojalibu kumuuliza mpigaji wa simu hiyo ni nani lakini mtu huyo wala hakumjibu badala yake simu ikakatwa na kutokuwa hewani tena. Shamsa hakutaka kuchelewa wala kuipuuza simu hiyo Shamsa alimwambia Jongo kuwa anatoka mara moja na kwenda ofisini. Kwa vile Jongo alikuwa ameyasikia maongezi ya Shamsa kweny simu akammpa ruhusa Shamsa ya kwenda, kabla ya kwenda Shamsa alimpigia simu Zainabu dada yake Jongo aje nyumbani kwake ili kukaa na Jongo.Zainabu alikubali na kudai kwamba atachelewa kidogo kufika Shamsa alimuelewa, alipokata simu ya Zainabu simu ya Bi.Ramla ikaingia Shamsa alipokea na simu upande wa pili ikasikika.



    “Vipi Mwanangu upo nyumbani, maana mimi nipo njiani nakuja kwako”



    “Hapana mama muda huu najiandaa nataka kutoka ila ni vizuri kama ukija utamkuta Jongo” Shamsa alisema



    “Kwani wewe unakwenda wapi muda huu”Bi.Ramla alijifanya kuuliza kimtego



    “Nakwenda ofisini muda huu mama maana nimepigiwa simu muda si mrefu hapa kuna dharura mama”



    “Sawa mwanangu hakuna tatizo mwanangu itakuwa vizuri mimi nitafika hapo muda si mrefu”



    Wakati Shamsa akiongea na mama yake Jongo alikuwa makini akimsikiliza mpenzi wake anachozungumza na mama yake, hata pale alipoambiwa juu ya Bi.Ramla kuja nyumbani hapo Jongo hakusishtuka wala kuteteleka juu ya mama huyo.



    *******

    Mama Shamsa alipomaliza kuongea na mwanae huku moyoni akiwa na furaha ya kweli kabisa kwa kile alichopanga kummaliza kijana huyo kipofu. Akatafuta sehemu yenye majina na kumpigia simu Abdul kumueleza kwa kile kilichofanyika ya kwamba Jongo atakuwa peke yake nyumbani kwani ndio nafasi pekee waitumie kumuua kabis.Abdul alimueleza kila kitu na kuelezana jinsi walivyopanga na kukubalia nafasi hiyo waitumie vizuri bila kugundulika kwa mtu yoyote. Baada ya muda Bi.Ramla alikuwa mbele ya duka la dawa na kununua sumu aina ya dawa za unga utumika kuuwa wadudu kama panya mende na kunguni, akuna aliyegundua dawa hizo amezinunua kwa madhumuni gani hivyo wala hakuonyesha dalili yoyote maana hakuwa na muda na mtu. Alipotoka dukani akachukua tax na kuelekea nyumbani kwa Shamsa, alipofika alikuta Shamsa ndio anatoka akiwa kwenye bajaji, akamuambia dereva tax asimamishe gari pembeni kidogo na nyumba hiyo bila kuuliza kitu, wakiwa kando kando ya barabara Bi.Ramla na dereva walimuona Shamsa akiwa ndani ya bajaji na dereva wa bajaji hiyo alikata kona na kuifuata barabara kuu kuelekea mjini....

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bi.Ramla hakutaka kusubili hivyo yeye alishuka na kuingia ndani, alipofika sebuleni alimkuta Jongo amekaa kitini peke yake, Jongo alihisi kuna mtu akiingia alipohita jina la ndugu yake hakuitikia badala yake alisikia sauti ya mama yake Shamsa, akidai kuwa yeye ndiye aliyeingia pia alipigiwa simu na Shamsa kuwa aje amuangalie mpaka pale dada yake Zainabu atakapofika.Bi.Ramla alipotaja jina la Zainabu basi Jongo aliondoa wasi wasi moyo wake ukapoa na kuamini kile alichokisikia, akamsalimi Bi.Ramla kisha alitulia lakini Bi.Ramla alimuhitikia kwa kejeli bila Jongo kuona mama huyo alivyommwangalia kwa dharau.Wakati Bi.Ramla akiendelea kuzungumza na kumzugazuga Jongo mlango ulifunguliwa na Abdul akaingia ndani huku akiwa mwenye mashaka, macho juu ameyatoka akimtazama Bi.Ramla kwa tahadhari.Bi.Ramla akaamua kuvunja ukimya akamtambulisha Abdul kwa Jongo lakini Jongo machale yakamcheza akashtukia kitu lakini hakutaka kujionyesha akatulia.



    “Ungependa nikuandalie nini”? Bi.Ramla akavunja ukimya



    “Ah asante mi nishatosheka tayari” Jongo alijibu kwa hamaki



    “Jamani nimekuja kukuona nisikufanyie chochote kwa nini lakini baba, hata juice?” Bi.Ramla alisema



    “Asante ila usijisikie vibaya sana mama ningehitaji Juice ya maembe ipo kwenye friji” Jongo alisema huku akitabasamu



    “Ah usijali subiri nikakuchukulie, nakuletea sasa hivi usijali”Bi.Ramla alisema huku akinyanyuka sofani



    Bi.Ramla alikwenda kuchua juice aliyoambiwa na Jongo, alifungua friji kisha akatoa jagi lenye juice ya embe iliyosangwa na kuimimina kwenye glasi moja wapo iliyokuwa juu ya meza kubwa sebuleni hapo. Alipomaliza kuimimina juice hiyo aliweka ile sumu kwenye juice hiyo iliyokuwa kwenye glasi kisha akairudisha ya kwenye jagi frijini na kumpelekeaJongo.Jongo aliipokea glasi hiyo na kuanza kuifakamia juice yote bila kubakisha, Bi.Ramla alifurahi sana kumuona Jongo ameinywa Juice hiyo bia kugundua. Muda si mrefu wakiwa sebuleni hapo ilisikika sauti kutoka kwa Jongo akilalamika tumbo likimuuma, hapo Bi.Ramla na Abdul walikuwa kimya wakimuangalia Jongo alivyoshikilia tumbo lake, wao walishaona sumu tayari ishaanza kufanya kazi yake. Abdul alinyanyuka na kuanza kuondoka Bi.Ramla naye taratibu alinyanyuka na kuondoka wakamuacha Jongo peke yake akilia kwa uchungu, Jongo alipiga kelele akitaka msaada. Kwa vile alijua kuwa ndani ya nyumba hiyo walikuwa wawili yaani yeye na Bi. Ramla aliona amuombe mkwewe huyo amsaidie akaanza kumuhita Bi.Ramla aliyekuwepo, kwa muda huo wala hakuitikiwa, Jongo alirudia kuhita tena na tena lakini sauti yake haikuwa na mafanikio kwake.



    Bi.Ramla na Abdul waliongozana huku wakikazana kuwai kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini mungu si adhumani wakati wanatoka walikutana nje na dada yake Jongo ambaye ni Zainabu aliyekuwa amepigiwa simu na kudai atachelewa kufika na kweli amechelewa.Japo Abdul na Bi.Ramla walimuona dada huyo hawakumtilia maanani na kumdharau hatoweza kuwatambua, Zainabu aliwaangalia kwa makini kwani alipatwa na mashaka juu ya watu hao ndani ya nyumba hiyo, hivyo alihisi kitu kutokea haraka akaingia ndani bila kuwaangalia watu hao walipoelekea. Alipofungua tu mlango alisikia makelele kutoka kwa mtu akiugulia maumivu, alipoisikiliza vizuri sauti hiyo mara moja akaitambua kuwa ya ndugu yake Jongo.



    Haraka alikimbilia sebuleni ndipo aliposhtuka zaidi alipomuona Jogo akiwa peke yake sakafuni akigalagala huku mapovu yakimtoka mdomoni naye mikono akishikilia tumbo lake. Zainabu alichanganyikiwa alienda karibu na pale alipolala Jongo na kuanza kumnyanyua huku akimuliza nini kilichokuwa kinamsumbua. Jongo alimwambia Zainabu huku kama alikunywa juice anayohisi kuwa na sumu huku akilalamika kwa maumivu, kusikia hivyo Zaina haraka alifungua friji na kwa bahati nzuri aliyakuta maziwa haraka alirudi bila kulifunga friji na kuanza kunywesha Jongo maziwa hayo. Jongo alikunywa kwa pupa ili kuokoa maisha yake baada ya dakika mbili Jongo alianza kutapika pale sebuleni, Zaainabu kuona hivyo haraka alichukua simu na kumpigia Shamsa. Kwa muda huo Shamsa alikuwa hapatikani hivyo dada hiyo alibonyeza namba kadhaa na siku ya upande wa pili ikasikika kutoka kwa mama yake Jongo. Baada ya kama dakika tano Jongo akiwa hana hili wala lile amelegea na kuishiwa nduvu pale sakafuni, Zainabu alisikia mlio wa gari nje ya nyumba hiyo mara moja akajua ya kwamba Mama yao alikuwa amefika kuwasaidia.



    Punde mama Jongo na kijana wa makamu wakaingia ndani ya nyumba hiyo na kumkuta Zainabu akimlilia kaka yake kwa uchungu, wao walimchukua Jongo na kumpeleka hospitali, huku nyumbani walimuacha Zainabu peke yake ikiwa Mama Jongo na kijana huyo msamalia mwwema wakimpeleka Jongo hospitali. Ndipo Zainabu alipoamua kumpigia simu Shamsa ambaye sasa simu ilikuwa inapatikana, baada ya Shamsa kusikia kile alichoambiwa na Zainabu haraka hakutaka kubaki kazini aliacha kazi ofisini na kukimbilia hospitali Amana alipoelezwa........



    Njia nzima alikuwa mwenye mawazo hakuelewa kitu gani kimempa mpenzi wake, Shamsa alimuomba dereva wa bajaji kuongeza mwendo ili kuwai.Baada ya nusu saa waliwasili hospitalini hapo, Shamsa alishuka na kuingia mapokezi kisha kuulizia hali ya mpenzi wake muuguzi wa zamu alimuelekeza kwa madaktari kabla hajafika chumba cha daktari alimuona Zaina akiwa na mama yake wameketi wakisubili kuingia chumba cha daktari. Shamsa hakutaka kusubili aliwafuata na kuwamuliza nini hasa kilichokuwa kimemtokea mpenzi wake, Zainabu alimwambia jinsi alivyomkuta Jongo na kuomba msaada kisha wasamalia wema walimsaidia kumpeleka hospitali. “Kwani madaktari wamewaambiaje, nini kimedhuru mwilini mwake? Shamsa aliuliza maswali mfululizo, Zainabu alimwangalia kwa udhuni kisha akamwambia kuwa Jongo amekunywa sumu na hawakujua sumu hiyo amepewa na mtu hama amekunywa mwenyewe.



    Zainabu alimueleza Shamsa jinsi alipokutana watu hao ambao walikuwa wametokea nyumbani kwake akiwa mwanamke mtu mzima na kijana wa kiume, Shamsa alishangaa aliposikia maneno hayo, aliwaza na kuwazua juu ya watu hao maana Zainabu hakuwajuwa watu hao kina nani hata Bi.Ramla hakuwai kumuona zaidi ya siku hiyo na hakujua kama ndio mama yake Shamsa. Kinachomumiza Shamsa kichwa kuwa Jongo kapata wapi sumu wakati nyumbani kwake hawana sumu ya aina yoyote ile, Shamsa kichwa kilimgonga sana alifikilia na kukumbuka tukio lililotokea na lile lililowai kumtokea mpenzi wake huyo, akapata jibu kama kuna mtu atakuwa anamfuatilia na kutaka kumuua mpenzi wake Jongo hivyo akaona kabisa watu hao walioingia ndani ya nyumba yake ndio waliompa Jongo sumu hiyo.



    Shamsa alikuwa amefura kwa hasira hasijue la kufanya kwa wakati huo alimgeukia Zainabu na kumtaka amjulishe jinsi watu hao walivyo na huyo Mvulana aliyeingia alikuwaje. Zainabu alimfafanulia jinsi watu hao walivyo na mama huyo mtu mzima jinsi muonekano wake ulivyo, Kwa umakini mkubwa alivuta kumbukumbu na kuona taswira ya mama yake ikimjia kichwani mwake.Shamsa jinsi alivyoelezwa hakupata shida kumtambua Bi.Ramla na Abdul, alichokifanya Shamsa baada ya kuujua ukweli wenye ushahidi tosha aliondoka bila kuaga na kuelekea kituo cha polisi buguruni na kuandikisha jalada kwa maelezo yote aliyoyatoa kama alivyoambiwa na Zainabu pamoja na kuonganisha yale ya utekaji.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Shamsa kujieleza na kufunga mashtaka aliongozana na Askari watatu wakiwa ndani ya difenda na safari ya kuelekea nyumbani kwa mama yake ilipoanza.Shamsa hakuwa na huruma hata kidogo kwani kwa kitendo alichomfanyia mpenzi wake kilionyesha Mama yake kuwa na dharau kwake kumpenda kijana huyo kipofu. Baada ya mwendo wa robo saa kutoka kituoni Buguruni mpaka Ilala boma hawakuchukua muda sana walifika nyumbani hapo na kuwakuta Bi.Ramla na Abdul wakiwa sebuleni wanakunywa na kufurahi huku wamefungulia muziki kwa sauti ya juu sana. Shamsa alikuwa wa kwanza kuingia ndani huku maaskari wawili wakimfuata kwa nyuma, Bi.Ramla alipomuona mwanae alimkaribisha kwa furaha, Shamsa alimuangalia kwa dharau kisha akamuuliza mama yake “mama anafanya nini, mbona umebadilika sana mama yangu mpaka unafikia kutaka kumuua Jongo kijana wa watu” Bi.Ramla hakujibu badala yake alimuona Abdul akinyanyuka na kuanza kumfuata, kabla ajamfikia mlango ulifunguliwa na Askari wawili waliingia ndani. Kwa uwoga aliokuwa nao kwa polisi hao wenye siraha mikononi mwao Abdul alirudi nyuma na kuanza kukimbia kipitia mlango wa uwani, Lakini hakufanikiwa kufika mbali kwani tayari Askari hao walikuwa wamejipanga na kitakachotokea hivyo walimkamata Abdul pamoja na Bi.Ramla na kuwafunga pingu huku wakianza kumpa kipigo Abdul......



    Walipakiwa ndani ya difenda na safari ya kuelekea kituoni ilipoanza, njia nzima Bi.Ramla alikuwa akilia tu na kumtaka mwanae amsamehe, lakini Shamsa hakutaka kuzungumza kitu kwani alijisikia kumchukia mama yake kwa kitendo alichomfanyia Jongo alistahiri adhabu. Hata walipofika kituoni kipigo sasa kikaanza upya wakiwataka waseme ukweli nani aliyekuwa amehusika na tukio hilo la kumpa sumu kijana Jongo.Abdul alipoona maumivu yanamzidi kuongezeka kutokana na kipigo hicho aliamua kujisalimisha na kuamua kusema vitendo vyote kwa mabaya waliyomtendea Jongo yeye pamoja na Bi.Ramla. Shamsa alishangaa kuona mama yake ndio mhusika mkuu wa maovu yale, hakuwa na la kusema aliwaacha polisi wafanye kazi yao kisha aliwasiliana na baba yake juu ya jambo hilo na kumueleza kila kitu kuhusu mama yake na Abdul.Bwana Samir kipindi chote hicho alikuwa mjini Mwanza akifanya kazi kwa muda, hivyo hakuwa akifahamu kitu gani kilichokuwa kinaendelea juu ya mama yake na Shamsa, ndio maana alivyoelezwa alishangaa kusikia mkewe yupo kituo cha polisi kwa kosa la kukusudia kuua .Bwana Samir alimtaka mtoto wake kuwa mvumilivu ili siku inayofuata atafika dar kulishughulikia jambo hilo.



    Shamsa alirejea hospitali na kumkuta mama yake Jongo pamoja na Zainabu wakiwa wamekaa kwenye mabenchi ya hospitalini hapo, Shamsa aliwasogelea na kuwauliza habari za muda huo, wakamjibu ya kuwa ni nzuri kwani wamefanikiwa kumuona Jongo akiwa anaendelea vizuri ingawa fahamu bado hazijarejea sawasawa. Mama Jongo alimuangalia Shamsa kwa umakini kisha akamuuliza nini kimetokea huku alikotoka, Shamsa alikosa la kujibu maana donge lilikuwa limemkaba kooni alipotaka kuzungumza alishindwa na kuanza kulia, Zainabu alianza kumbeleza Shamsa na baadae aliponyamaza aliwaeleza ukweli kile kilichotoka.



    Wakati wakiwa kwenye maongezi walimuona daktari akija maeneo yale waliokuwa wamekaa, alipofika hapo alimtaka Shamsa kwenda wodini kwani mgonjwa anamuhitaji kuzungumza nae kabla ya mtu mwingine kuingia. Shamsa aliposikia anaitwa aliacha mdomo wazi na kumkimbilia daktari na kumuliza nini kimetokea, Daktari alimwondoa wasi wasi Shamsa kwa kumwambia kuwa mpenzi wake Jongo anaendelea vizuri, hivyo alimtaka amfuate ofisini kwa maelezo zaidi ili aweze kwenda kumuona Jongo wodini. Shamsa aliongozana na Mama Jongo mpaka kwa daktari, walipoketi vitini Daktari aliwaeleza ya kwamba wamefanya kila liwezekanalo kuokoa maisha ya Jongo, lakini wamekumbana na changamoto nyingi mpaka kupelekea kukata tamaa kutokana na mgonjwa kuchelewa kurejewa na fahamu zake. Hivyo mungu amewapigania hatimaye wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuokoa maisha ya kijana huyo.Shamsa na Mama Jongo walikumbatiana kwa furaha walimgeukia Daktari na kumshukuru sana, Shamsa alimuhaidi kumpatia zawadi Daktari huyo lakini daktari alimwambia ni wajibu wao kufanya kazi kama inavyotakiwa ila cha msingi amshukuru mungu tu.



    Shamsa na Mama Jongo walitoka mpakaa nje na kumkuta Zainabu akiwasubili, waliongozana mpaka wodiani alipolazwa Jongo, walipoingia tu wakasikia Jongo akihita jina la Shamsa. Haraka Shamsa alihitika na kukimbilia kitandani pale lipokuwepo kijana huyo amelala huku dripu ya maji ikiingia mwilini mwake.Shamsa alimbusu shavuni Jongo na kumpa pole mpenzi wake kisha Jongo akamueleza kuwa mama yake Bi.Ramla alivyokuwa mbaya kwa kwenda nyumbani kisha kumpatia Juice aliyokuwa ameweka sumu ili kuua.Shamsa macho yalimtoka na kumtaka Jongo amsamehe kwa kumuamini mama yake kumbe hakuwa mtu mzuri kwake, Jongo alimsamehe na kumwambia kuwa kosa ni la mama yake hivyo kama msamaha angetakiwa kuomba mama yake na sio yeye hivyo anyamaze kulia.Shamsa alinyaza kulia huku akijiapiza ya kwamba atoweza kuja kumsamehe mama yake kwa kitendo alichokifanya.



    Siku iliyofuata Shamsa akiwa nyumbani alisikia mlango ukigongwa, alipokwenda kufungua alikutana na Baba yake Bwana Samir akiwasili kutoka Mwanza, Shamsa alifurahi kumuona baba yake alimpokea mizigo yake na kumkaribisha. Shamsa alipoingiza mizigo ya baba yake ndani kisha akarejea na kuchukua maji kisha kumpatia baba yake kama alivyohitaji.Bwana Samir alipokea kisha alipiga funda moja kinywa kisha akaishusha na kuiweka glas mezani. Muda wote Shamsa alikuwa akimwangalia baba yake asijue la kufanya kwani aliona itakuwa aibu kama akimueleza uchafu aliokuwa akiufanya mke wake.



    “Haya niambie binti yangu kitu gani hasa kilichomfanya mama yako kuwekwa ndani” Bwana Samir alimuuliza mtoto wake baada ya kusalimiana



    “Yaani baba we acha tu…Mama Amebadilika sana siku hizi” Shamsa alisema huku akikaa vizuri sofani



    “Amebadilika kivipi, ameiba au?” Bwana Samir aliuliza kwa mshangao



    “Sio hivyo ni hivi unakumbuka siku ile nilipokuja hapa kumtambulisha Jongo?”



    “Yes, nakumbuka sana jinsi alivyokuwa akionyesha kuchukizwa na uwamuzi wako”



    “Ni kweli mama alichukia na mpaka nisemavyo nahisi bado anachukia na ndio sababu kuu iliyompeleka polisi”



    “Sasa Baba niambie maana sijui kisa kamili zaidi ya kuonganisha”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Bi.Ramla alikuwa na kijana anayeitwa Abdul sijui kama unamfahau, huyo kijana ndiye aliyekuwa akimpa jeuri ya kujifanya anajua kila kitu”



    “Abdul ndio nani huyo kijana, anatokea wapi?



    “Simjui anapotokea wapi ila alikuwa mtu wake mama kwa muda mrefu tu”



    “Alikuwa mtu wake kivipi yaani mbona unanichanganya” Bwana Samir aliuliza kwa hamaniko



    “Siku moja niliwakuta wamelala chumbani humu kwenye chumba chenu kile hivyo sikuwa na namna kukueleza baba yangu juu ya hali iliyotokea, cha kushangaza huyo kijana anataka anioe mimi nilipokataa kuachana na Jongo ndipo visa na matukio kila kukicha wakimfanyia kijana wa watu”



    “Hee! ina maana mama yako alikuwa ananisaliti si ndio, alafu wewe unajua umeshindwa kuniambia kwa kipindi chote hicho?” Bwana Samir alifura kwa hasira



    “Hapana mzee wangu nilikuwa sina uhakika na jambo hilo hivyo nilikuwa nachunguza ndipo nilipobahini kuwa ni kweli” Shamsa alijitetea



    “Sasa wapo kituo gani?” Bwana Samir aliuliza kwa hasira



    “Wapo kituo cha polisi Buguruni” Shamsa alisema



    Kutokana na hasira za kitendo hicho alichofanya Bi.Ramla Bwana Samir alikuwa hashikiki mpaka Shamsa akaanza kumuogopa baba yake kwa siku mzee huyo hakuwa na masihara, hivyo Shamsa alimuacha kama alivyokuwa ila moyoni alijirahumu kwa kumuambia jambo hilo sasa hajui kitakachotokea katika familia yao. Shamsaalimnyenyekea baba yake na kumfuata kisha kumpigia magoti mbele ya miguu yake na kumtaka amsamehe Mama yake kwa kitendo alichokifanya kwani anaamini atajirekebisha.Bwana Samir akamuambia mtoto wake yeye hayupo tayari kumsamehe mwanamke huyo mwenye roho mbaya kiasi hicho, kwani alifanya unyama na ukatili kwa Jongo hivyo wamuache kwanza apate adabu kula adhabu kwa hiyo wawaachie polisi ili wakubaliane na Serikali watachoamua na sheria ifuate mkondo wake. Shamsa alimkubalia baba yake ila waliagana siku inayofuata asubuhi na mapema kwenda polisi kufuatilia inavyoendelea.....



    Baada ya siku mbili kupita Jongo aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani kwa mama yake, Shamsa akawa kila siku uenda kushinda nyumbani kwa mama Jongo ili kuwa karibu na mpenzi wake huyo mpaka pale hali yake itakapotengemaa. Siku moja wakati Shamsa akiwepo, pia Jongo na Zainabu wamekaa nyumbani hapo, walikuwa wakiongea maongezi ya hapa na pale, Ghafla bila kutarajia Jongo akimtaka Shamsa aifuatilie kesi kuhusu mama mkwe yaani Bi.Ramla. Shamsa alihachia tabasamu pana usoni mwake kisha akamwambia Jongo ya kuwa Baba Bwana Samir ndiye anayeifuatilia kesi hiyo hivyo yeye haijui kinachoendelea, Jongo alifika mbali zaidi akisema kwamba Kesi ya Bi.Ramla angependa ifutwe kwa sababu alishamsamehe siku nyingi sana. Yalikuwa maongezi ambayo yaliwaacha watu wote mdomo wazi, baada ya muda mfupi baadae walikuja wageni akiwepo Bwana Samir na rafiki yake kumwangalia Jongo.Hapo sebuleni sasa watu waliongezeka walikuwepo baba yake Shamsa, rafiki yake Mzee Mashaka, Mama yake Jongo na dada yake Jongo Zainabu, wakati wanasalimiana Jongo alionekana kuwa mnyonge alimtaka Bwana Samir amueleze jinsi gani kesi ya mkewe inavyoendelea. Bwana Samir alimueleza ya kwamba sababu ya kukosa ushahidi wa kutosha hivyo kila siku Kesi inasimamishwa sababu haijakamilika, hivyo alingoja ushahidi ili wasomewe mashtaka na kuukumiwa. Jongo hakulidhika na majibu hayo hata walipotaka ahachane na jambo hilo lakini Jongo aling’ang’ania wafanye iwezekanavyo, ili Bi.Ramla atoke.



    Shamsa na baba yake walifuatilia jambo hilo kwa kiasi kikubwa huku Jongo akimtumia mjomba wake wasaidiane kufanikisha kumtoa na kuifuta kabisa kesi hiyo inayomkabili mama Shamsa. Baaba ya wiki moja mbele walifanikiwa baada ya kulipia na kumtolea dhamana ya shilingi milioni kumi na mbili, na baada ya siku kadhaa Mama Shamsa alitoka mahabusu na kurejea nyumbani. Tofauti na siku zote Bi.Ramla muda mwingi alikuwa mtu mwenye mawazo hakujua kama kijana yule Abdul atawezaje kutoka maana kumuacha kwake mahabusu ilionekana kwamba kesi zote za mama Shamsa alizibeba kijana huyo na ndio ilikuwa mwisho wake lazima haukumiwe kwa kosa kama hilo. Baada ya siku ya pili kupita tangia atoke mahabusu Bi.Ramla aliomba apelekwe nyumbani anapoishi Jongo ili aende kumuomba msamaha mkwe wakemtarajiwa, Shamsa na Baba yake walikubali na siku iliyofuata wakampeleka Bi.Ramla nyumbani kwa mama Jongo.Mama Shamsa alipofika nyumbani kwa Mama Jongo alimkuta Jongo na mama yake wameketi sebuleni, Mama Shamsa aliwasalimia kisha alimfata Jongo na kumpigia magoti kisha kuanza kuomba msamaha.



    Jongo kwa huruma na unyenyekevu alimshika mkono mama Shamsa na kumnyanyua na kumuambia “nilishakusamehe tangia zamani mama, kuwa na amani kabisa” Bi.Ramla alishindwa kujizuia machozi yakamtoka kujutia kitendo alichokifanya kwa pamoja walisimama kisha wakakumbatatiana kwa furaha na Shamsa kumkumbatia mama yake na kumuambia“Kwa pamoja tumekusamehe Mama sahau yaliyopita tugange yajayo” Kwa hudhuni Bi.Ramla alilia machozi ya furaha akamfuata mumewe Samir naye akanyanyuka sofani wakakumbatiana na Shamsa naye akamfuata Jongo akamkumbatia kwa nguvu huku akimbusu sehemu kadhaa katika paji lake la uso huku akimuambia Jongo “ Chaguo langu ni wewe!” Wote wakafurahai na makofi yakasikika wote wakiwaangalia Jongo na Shamsa walivyogandana. Hapo ndio ukawa mwanzo wa maisha ya furaha na amani kwa Shamsa na Jongo kwani baada ya miezi miwili harusi ikafanyika kwa furaha na kwa muda mchache Shamsa alipata ujauzito na kujifungua watoto mapacha wawili wa kike na kiume aliwapa majina ya Amina na Amani wote wakiwa wazima wenye afya bora na hapo ndio ukawa mwisho wa ubaya wa mama Shamsa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog