Simulizi : Changudoa
Sehemu Ya Pili (2)
"Ima, we Ima" ilikuwa sauti ya Mama Sikitu. Mama mwenye nyumba katika chumba anachoishi Emmanuel. Emmanuel akajinyanyua kwa uchovu huku akijipangusa tongotongo kwenye ncha ya macho yake.
"Shikamoo mama"
"Kuwa na wewe upate yako" mama alikuwa na gubu iliyopitiliza "Nipe pesa ya umeme" Emmanuel aliyevaa kipensi kifupi kifua kikiwa wazi akarudi tena ndani kwenye suruali aliyoivaa jana na kuipekua pekua kisha akatoa shilingi elfu tano ya umeme. "Hii hapa mama" Mama Sikitu akaikwapua kwa hasira na kusonya baada ya kumpandisha Emmanuel juu mpaka chini na kutokomea chumbani kwake.
Maisha yakaendelea huku Nadia akiona hali isiyo ya kawaida kwa mtazamo wa majirani aliokutana nao hapo kwa Emmanuel. Kuna wakati alihisi aibu lakini alipiga moyo konde na kuendelea na maisha. Kuna wakati alipomueleza Emmanuel, Emmanuel akampooza. "Achana nao ndivyo walivyo"
Ndipo jirani mmoja akamfuata na kumuuliza Nadia swali ambalo likampa mwanga. "Samahani dada yangu!" Alikuwa ni msichana mwenye umri sawa na Nadia. "Mimi jina langu naitwa Mwajuma, wewe ni mgeni hapa Kumba?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio ila nina mwezi kiasi" Nadia akamjibu kwa hofu kiasi. Yule msichana akamuinamia kama anayetaka kumnong'oneza Nadia.
"Sikia nikuambie dada yangu huyu kaka unayeishi naye ameathirika na anagawa kama njugu umeshatembea naye?" Macho yakamtoka pima Nadia lakini ukweli ni kwamba hakuwahi kutembea na Emmanuel ila Emmanuel alishamsumbua mara kadhaa kuwa anamuhitaji kimapenzi na ahadi nyingi za kumuoa. Nadia akakataa kwa kutingisha kichwa kisha Mwajuma akatoa tabasamu la furaha.
...
VISIWANI ZANZIBAR
Rashid baada ya kufanikiwa kuupata utajiri wa pesa nyingi kutoka kwa Fatma kazi na tabu ikabaki kwa Faudhia. Asubuhi aliyohitajika, akawahi mahakamani. Fatma alikwisha fika na wapambe wake, Faudhia yeye akaongozana na Rashid pembeni akiwa Salim aliyevimba akimtazama Fatma kwa hasira na chuki.
Waliyoyakuta huko, yakawa yale yale. Yale yale kuwa hawakuwa wamiliki halali wa mali zile. Hata walipozitoa hati zao jibu likawa vile vile
"Hizi ni feki"
Fatma akatabasamu huku akijipepea kwa nyodo midomo kaibetua. Rashid alikuwa akimtazama mama yake kwa huzuni lakini hakuwa tayari kuharibu njama zake za kumiliki pesa nyingi kama alizokuwa nazo kwa kipindi hicho. Milioni 240, si ndogo.
Bi Faudhia alilia kama mtoto mpaka kamasi likamvuja. Salim akambembeleza mama yake huku Rashid akimbembeleza kwa kutoa ushahidi.
Hakimu yule akazungumza "Hili jambo si lazima tulipeleke mahakamani moja kwa moja" akarekebisha miwani yake kisha akaendelea "Mathalani wanasheria wenu wote wapo hapa ninaomba nitoe muda wa familia yako bi Faudhia munaruhusa ya kukaa katika nyumba ile ya Koani kwa muda wa siku tano tu ili muweze kutafuta huifadhi sehemu nyingine" Ni kweli yote yaliyotokea, ilimbidi Faudhia kukubaliana na hali hiyo. Akatoka kinyonge yeye na watoto wake. Kilichomchanganya zaidi hawakuwa na pa kwenda. Lakini akajipa moyo na kutokomea zake na familia yake.
….
Nadia hakufikiria kutoa penzi kwa mwanaume yeyote na haswa, mtu kama Emmanuel. Alimuheshimu na kumpa nafasi ya ukaka katika maisha yake. Msaada ambao Emmanuel alimpa ulikuwa ni mkubwa sana kwake. Alikuja bara bila kujua angefikia wapi lakini Emmanuel amejitolea kummsaidia bila hata kumjua. "Hapana, Ima ni kaka yangu" Akajiambia kwa sauti ya ndani. Si kwamba alimuhesabu Emmanuel kama kaka yake lakini hakuwa na uoga, alimtazama kwa hofu mara kadha kila walipokutanisha macho yao. "Vipi Nadia?" Nadia akakwepesha macho yake kwa haya na kutazama chini.
Hali hiyo ikaibua wazo lililofichwa ndani ya moyo wa Emmanuel. wazo ambalo alitamani kumueleza tangu walipokutana lakini hakuona kama ulikuwa ni muda muafaka. "Nadia" Emmanuel akamuita kwa sauti ya kunong'ona, Nadia akainua uso na kuurudisha chini haraka. Emmanuel akaendelea "najua itakuwa ngumu kukueleza hili ukanielewa lakini kuna jambo linalosumbua nafsi yangu" Akaweka kituo mara baada ya kuitupa karata yake. Akasikilizia pumzi ndefu zilizoshushwa na Nadia, akatoa tabasamu laini baada ya Nadia kuibuka na kugonganisha nyuso zao. "Nadia" akaita tena huku mkono mmoja kauweka katika bega la kushoto la msichana huyo mrembo "Nakupenda, nakupenda sana" Nadia akaendelea kushusha pumzi nzito kutokana na uzito wa jambo lenyewe.
Ni mwezi mmoja uliopita alitoka Zanzibar na kuja Bara kutafuta maisha. Nani basi amsaidie bila kumtaka kimapenzi? Nadia wa watu akashindwa kujibu. "Nadia" Emmanuel akendelea kuita kwa sauti yake ya kishababi "Mbona kimya?"
"Kaka Ima!" Nadia akaita kwa sauti iliyopwaya. Emmanuel akaonesha uso wa kuwa anamsikiliza. Nadia akaendelea. "Mimi ninakuheshimu kama kaka yangu kwa kuwa umejitolea kunisaidia kama mdogo wako. Sipo tayari kulipa fadhila zangu kwako kwa penzi hiyo ni sawa na rushwa ya ngono. Naomba tuendelee kuheshimiana kama awali tafadhali Ima"
Nadia akaongea jambo lililomgusa Emmanuel, lakini haikusaidia jambo. Emmanuel hakuwa na historia ya kukataliwa na mwanamke. Wenzake ndio walimpa nguvu ya kumfuata Nadia na kumueleza kuwa anampenda. "Wewe unaleaje mtoto mzuri kama yule kama Khanisi vile?" Hivyo vilikuwa vijembe vya rafiki zake alivyoviona kama dharau kwake.
Akapanga nao jambo.
Jioni ya siku hiyo kabla hajarudi nyumbani Emmanuel alikuwa na rafiki zake kijiweni wakipiga soga za hapa na pale. Ndipo akaona apasue jipu lake ili dharau zisiendelee.
"Hoya wana" Wenzake wakamtazama bila kusema chochote. "Sasa mimi nataka leo mje kupiga chabo wakati namtafuna mtoto"
Wakacheka huku wengine wakishika mbavu zao "Wewe Ima pale huwezi sijuhi unataka kumuoa yule mtoto"
"Mi sitaki kubishana na nyinyi leo time ya saa mbili fulani njoeni magetoni halafu mi ntaacha pazia wazi" Ndivyo ilivyokuwa. Sasa kukataa kwa Nadia, kukaendelea kukuza ile dhana ya joka la kibisa aliyoonekana nayo Emmanuel kwa rafiki zake. Hakutaka iendelee hali hiyo.
"Nadia wewe sio ndugu yangu" Akaongea kwa jazba huku akimsogelea, Nadia naye akisogea pembeni zaidi. "Wala hatujazaliwa tumbo moja. Sasa basi, utake utanipa, usitake nitachukua kwa nguvu" Macho yakamtoka pima Nadia.
"Uchukue kwa nguvu? Kitu gani Ima"
"Ndio utaelewa" Emmanuel hakuwa yule Emmanuel mwenye uso wa upole tena na mwenye roho ya malaika. Roho mbaya iliyomvaa hata uso wake ukabadilika. Sura ikamvimba, ndita zikatuna na kuliharibu paji lake la uso.
Huyo ndiye Emmanuel kweli si yule aliyekuwa akiigiza kwa Nadia. Ndiye yule aliyeapa kuwa atawaangamiza wasichana wote watakaojaribu kudondoka naye kitandani kimapenzi. Kwa eneo hilo la Kibaha alifanikiwa kuwapata wengi kwa tamaa zao za pesa. Ndio hapo jina lake likaanza kuchafuka mara baada ya kila aliyekuwa akitembea naye alidondoka kama jani la mpapai ama kuti la mnazi.
"Ameathirika" Wengi wakaanza kumtambua Emmanuel huku fununu zikizidi kusambaa eneo lote la kumba. Lakini alikwisha wapa zawadi hiyo ya tamaa zao zaidi ya wanawake kumi wa eneo hilo tu. Yeye alijifahamu kama ameathirika na alikuwa na kila sababu ya kufanya hivyo. Alipomtazama Nadia akahisi kama anamwona Jenifa mbele ya uso wake. Jenifa mwanamke aliyejitia mwema lakini mwenye lake moyoni. Ni kipiondi hicho ambacho Emmanuel alitoka zake Mwanjelwa mbeya na kuingia Dar es salaam akakutana na Jenifa kwa mara ya kwanza. Jenifa msichana aliyekuwa akifanya kazi za ndani na kubakwa kisha akaambukizwa ukimwi. Yeye akapania kuambukiza wanaume zaidi ya elfu moja na mia tano kati kati yao ndipo alikuwako Emmanuel. Emmanuel akijiona mwenye bahati kwa kupendwa na msichana mrembo aina ya Jenifa. Baada ya miezi nane ya kukaa na Jenifa huku safari za uongo kusingizia nje ya nchi hazimuishi Jenifa, Emmanuel akaumwa magonjwa asiyoyaelewa. Akaelekea hospitali na kuambiwa kile ambacho hakukitegemea. "Umeathirika Emmanuel" Macho yakamtoka pima Emmanuel hakuamini alichokisikia. "Nini dokta"
"Ndiyo tena vipimo vinaonesha una virusi vya ukimwi pamoja na kaswenda ambayo bado haijaanza kukuathiri sana na nitakupatia dawa yake lakini huu ukimwi inabidi uje kuhudhuria clinic ya mafunzo kujua jinsi ya kuishi kwa matumaini"
Emmanuel akamwaga machozi mbele ya dokta na kuondoka kinyonge. Aliporudi nyumbani mambo ya ajabu yakazidi kumfunikia. Hiyo ilikuwa ni baada ya kuzungumza na Jenifa na kufahamu kuwa Jenifa alikuwa akifahamu yote na alimuambukiza kwa makusudi.
"Hicho chumba pia ndio ofisi yetu naomba urudishe ufunguo kwa Madam kwa kuwa mimi pia nilipata wazo la kuhama hapo muda mrefu" Danguro!? Emmanuel hakuamini jinsi alivyomuamini Jenifa. Madam ambaye alidhani ndiye mama mwenye nyumba kumbe ndiye mama anayewauza wanawake zaidi ya kumi waliopo katika vyumba vilivyopangana kwenye nyumba hiyo.
Emmanuel naye akaapa kufa na wake.
Mmoja kati ya hao akaingia Nadia. Kuonesha urijali wake kwa wenzake ambao aliamini walikuwa dirishani wakimtazama, akamkaba Nadia asilete upinzani wowote. Emmanuel akaingiwa na jinamizi la kutaka kumbaka Nadia. Nadia alijitahidi kujinasua lakini ama hakika Emmanuel alishiba misuli na nguvu zilizomnyong'onyeza Nadia. Wazo la mwisho la kujiokoa ili atokomee likampitia Nadia. Emmanuel akiwa amehakikisha amemdhibiti akaanza kufungua zipu yake ya suruali. Nadia akatumia mwanya huo wa kufyatua mguu wake wa kulia na kwa goti alilolikunja sawia, akampiga pale pale katikati ya miguu ya Emmanuel. Emmanuel akatoa yowe hafifu la kugugumia maumivu na akasikia vicheko vya wenzake waliosimama dirishani. Nadia akafungua mlango mbio na kutokomea gizani.
Emmanuel akiwa anagugumia pale kitandani akasikia sauti za wenzake wale watatu wakishauriana "Twenzetuni tumfuate yule demu" Vishindo vya mbio za wenzake zikamthibitishia Nadia alikuwa hana ujanja Tena.
...CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha aliyoishi na watoto wake, yalitosha kuwa fundisho kwa Faudhia. Nyodo zake zote zikamuisha akahifadhiwa na mdogo wake huko Mazizini. Hawakuwa na chochote. Moyoni mwa Faudhia alikuwa na chuki za dhati kwa Nadia. Aliamini kuwa Nadia ndiye anahusika na upotevu wa hati hizo halali. Rashidi akapanga mengi juu ya pesa alizo nazo. Pesa zilikuwa nyingi zikamuwasha. Rashid akafikiria kuwa Mazizini zanzibar hakukuwa sehemu sahihi ya kufanya biashara kwa pesa zake. Angeulizwa alipozipata asingekuwa na jibu.
kuelekea Dar es salaam sehemu ambayo alipata taarifa ilikuwa ni sehemu nzuri na mji mkubwa kwa ajili ya biashara. Usiku wa saa mbili akakwea boti bila kutoa taarifa kwa yeyote. Jiji la Dar likampokea Rashidi katika maeneo ya Magomeni mapipa alipojitwalia chumba chake katika moja ya lodge zenye hadhi nzuri. Mawazo yakasafiri ndani ya biashara gani afanye ili aweze kuizungusha pesa aliyo nayo isipotee kwa kuifuja. 'Ninunue gari? Nifungue duka? Hapana nadhani heri ninunue nyumba ya biashara. Nyumba hiyo nitafungua guest kubwa nitakayojipatia kutoka kwa wazinzi wa huku dar' Akatabasamu kisha akafunga macho akapotelea usingizini.
Bi Faudhia alichanganyikiwa sana kuondoka kwa Rashidi. Yeye ndiye mtoto aliyeona angalau kwa kiasi fulani alikuwa na msaada kwake. Yeye Rashid alionekana kama mwenye akili timamu zaidi ya Salim aliyeanza kujivutia mibangi na kunywa pombe eti kwa kudai anapoteza mawazo. Faudhia naye mawazo yakamtafuna nyama akabaki mifupa mitupu.
"Nataka niende Dar es salaam mdogo wangu"
“Kuna nini huko dada Fau?"
"Naamini Nadia atakuwa huko nataka nimkomeshe amenifadhahisha sana"
Mdogo wake hakujisikia vizuri kumruhusu Faudhia kuondoka lakini Faudhia akawa kero na safari ya Dar es salaam. Siku chache baadaye Faudhia akawa kwenye boti kuelekea Dar es salaam. Jazba ikamfanya atoe pumzi za hasira kila alipokaribia kuingia Dar es salaam.
Faudhia akapokelewa kwenye jiji alilotamani kulifika kwa muda mrefu. Saa 2 usiku jiji hilo likapendeza macho, likapendeza kila kitu kilichosogea na kisicho na uhai. Alikuwa na kiasi cha pesa ambacho kilimtosha kwenda kupanga nyumba ya kulala wageni huko Buguruni. Ni daladala ya konda aliyekuwa akipiga mbinja za uhakika na kukera baadhi ya abiria ila zilimvutia Faudhia kulipanda gari hilo hilo.
Lilikuwa linaelekea Buguruni.
Faudhia alikuwa na ndugu zake huko Kipawa, hakupenda kuwasumbua usiku huo wote akaamua kujihifadhi ndani ya guest hiyo aliyoitwaa kwa usiku huo pekee. Asubuhi ilikuwa ndefu kuifikia kutokana na usingizi kumpaa Faudhia. Aliwaza kuhusu Nadia alihisi maumivu makubwa moyoni mwake. Maumivu yaliyompata kila alipofikiria kutokana na umasikini uliomkumba gafla kwa kushindwa kumiliki mali za mumewe.
"Nikimuona sijuhi nitamfanya nini!?"
Alijinong'oneza kwa hasira huku akiuma midomo yake.
Akapitiwa na usingizi.
...
Rashid aliamka na kwenda bafuni baada ya jua kuchomoza. Akaswaki na kuoga huko huko. Aliweza kujiona kuanzia juu mpaka chini kupitia kioo chenye urefu sawa na yeye. Akarudi tena chumbani kwake akiwa anajifuta maji kwa taulo zito jeupe la lodge hiyo.
Alipomaliza alizitwaa nguo zake nadhifu zilizokolea pasi hakika. Akazivaa na kutoka nje ya chumba. Alikuwa amependeza sana. Ana damu ya kiarabu, lakini haikuwa rahisi kumtambua kutokana na damu ya mama yake Faudhia, kuwa na damu kali zaidi.Hivyo asili ya kiswahili ikamtawala.
Alielekea moja kwa moja katika mgahawa kupata kifungua kinywa. Akaagiza supu na chapati. Akanywa na kula haraka haraka kisha akaondoka. Alipoenda hakupajua lakini alikuwa na hakika asingekosa alichokuwa akikitafuta.
Akafika kituoni, Magomeni hospitali. Akakwea gari ambalo konda wake alikuwa akipiga nduru za bakhresa, kariakoo mia tatu. Rashid akalipanda hilo hilo.
Msongamano wa watu ukawa mkubwa eneo hilo la kariakoo hivyo akajichomoa katikati ya kundi hilo na kuibukia mtaa wa kongo katika kituo cha daladala, akapanda gari la kwenda Buguruni. Alishukia kituo cha bungoni na hapo akakiona alichokuwa akikitafuta. Alikiona kibao cha madalali wa nyumba viwanja na mashamba. Kulikuwako na namba za simu pale kibaoni, kikwazo kikawa ni simu. Hakuwa na simu tangu alipoingia Dar es salaam. Akainunua pale katika maduka ya rozana alipoenda haraka haraka na taksi aliyoichukua bungoni.
Nusu saa baadaye alikuwa kwenye taksi na dalali wa nyumba, viwanja na mashamba wakielekea maeneo ya keko. Nyumba ilikuwa kama ile aliyoitaka hakuchelewa kuichukua, akalipa haraka haraka. Akafanikiwa kupata nyumba maeneo ya keko machungwa.
...
Wale vijana wanne waliomkimbilia Nadia, walifanikiwa kumpata karibu na mwarobaini. Nadia alikuwa anatweta kwa kilio huku akijaribu kuwasihi wasimfanye jambo, haikusaidia. Mmoja wao ndiye alimkamata na kumnyanyua juu juu kisha mwingine akampiga mtama. Bado Nadia alikuwa akilia huku watatu wao wakicheka mmoja akiwa hajisikii raha kwa jambo lile. Walikuwa wameanza kutaka kufanya kile walichopanga na Emmanuel tangu mwanzo.
Kumuingilia kwa zamu.
Kwa kuwa Emmanuel alishindwa kuanza, wao wamemkamata. Lakini bado yule mmoja kati yao hakutaka hilo litokee. Lakini mwanzo ni yeye aliyetamani sana jambo hilo. Ni yeye ndiye aliyetilia mkazo wa kumwingilia Nadia kwa zamu. Lakini si huyu wa sasa aliyekaa pembeni akiwa anaumwa na roho kwa jambo wanalotaka kufanya wenzake.
Wawili waliotaka kuanza baada ya kumlaza chini Nadia, wakapigwa kikumbo na yule mwenzao. Walishangazwa sana.
"Hoya we Tony vipi!?"
"Sikia Haruni" akamnyooshea kidole yule aliyezungumza kwa wahka "Huyu ni kama dada yako, hii si busara hata kidogo acheni huu ushenzi"
Wenzake wote walistaajabu. Nadia pia alishangazwa kwa kuwa alijua hakuwa na msaada mwingine. Machozi yakaacha kumtoka akimuangalia yule aliyekuwa akibishana na rafikize.
"We boya nini au unataka kwenda naye wewe? Hapa hupati kitu fala wewe" Yule aliyeonekana kama kiongozi wa kundi hilo akataka kupigana na Tony ambaye alionekana akimtetea Nadia. Wakazikunja ngumi. Ngumi zilitifuka huku wakiwa wamemsahau kabisa Nadia aliyeanza kunyanyuka, naye akishangaa jambo lile la ajabu.
Haruni alipigika. Damu zilimvuja kutoka puani, mdomoni; akapoteza ujasiri wake wa kuendelea kupigana. Wale wengine walivyoona yule waliyedhani ana nguvu amepigwa, wao hawakubaki. Wakakimbia mpaka wakajikwaa, wakanyanyuka na kukimbia tena.
Tony akamshika mkono Nadia na kuondoka naye nyumbani kwao. Huko alikuwako baba yake mwenye kituo cha kulea watoto yatima na wale wa mtaani. Yeye ndiye mwenye kituo maarufu kule Dar es salaam kilichoitwa Mtaa umezaa.
"Mnh Tony mwanangu umetuletea mkwe sio?" Ilikuwa sauti ya mama yake aliyeongea naye kwa utani. Tony akatoa kicheko dhaifu na kumkaribisha Nadia ndani. Ndani akamkuta baba yake kitini amejipumzisha gazeti lake mkononi.
"Baba!" Baada ya kumsalimia baba yake akamuita kama mwenye jambo la kuzungumza. Hata hivyo baba yake alilitupa gazeti pembeni akisuburi maelekezo kuhusu binti mbichi aliyesimama mbele yake, Nadia.
"Huyu ni rafiki yangu ana matatizo makubwa sana baba"
"Yapi?"
Baba yake akauliza kwa hali ya mamlaka. Tony akamueleza kifupi kama alivyoelezwa na Nadia wakati wapo njiani kuja hapa nyumbani. Baba yake akaonesha masikitiko kwa madhira yaliyomkuta Nadia. Akaahidi kumsaidia.
"Nitampeleka kwenye ile kambi yangu, nitamsaidia Tony usijali"
Nadia alijisikia ahueni kuwa katika mikono salama. Akashusha pumzi ndefu akidhani ndio ameutua mzigo. Bila kujua kuwa ndio hali ngumu na mbaya katika maisha kwake ndio ilikuwa imeanza.
Mzee Kumbo, Baba yake Tony, ndiye aliwaamsha kuiwahi gari ya kwanza kuelekea Dar es salaam.
"We Tony!" Akawa amesimama mbele ya mlango wa chumba cha Tony huku anagonga gonga "Tony, Tony wee"Tony aliitika kwa sauti ya kujivuta na kuonesha bado usingizi umemteka.
Mzee Kumbo akafoka"Amka bwana utamchelewesha mwenzio"
Akatoka na kwenda chumba ambacho Nadia amelala. "Nadia" alipoita mara moja ya pili akaitikiwa na sauti nyororo ya Nadia.
"Bee baba"
"Oh! Umeshaamka mwanangu?" Huku akijichekelesha.
"Na nimeshajiandaa baba"
Kumbe Nadia alikuwa akitembea, mara mlango ukafunguliwa. Ilimbidi Mzee Kumbo asimame kwa kuwa yeye pia alikuwa ameanza kupiga hatua kuondoka. Alipogeuka akakutana uso kwa uso na Nadia.
"Oh! Mama huyo! Umependeza sana"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa akimtazama Nadia kuanzia chini mpaka juu. Hakika Nadia alivutia.
Nguo yake japo ilichora na kuutangaza ufukara ikachora umbo lake zuri kwa uzuri zaidi. Nadia kwa aibu akarudia kujitazama tena na alipoibuka na kumtazama Mzee Kumbo, akaachia tabasamu fulani. Tabasamu lililobadilisha mpangilio wa mapigo ya moyo ya Mzee Kumbo. Mzee Kumbo kuna kitu alitamani kuzungumza, lakini koo likajifunga.
"Mh! Asante baba" akadakia Nadia, "Lakini sikujua kama Tony ni mlalaji wa hivi"
"Anha we Nadia, kausha bwana" sauti ikatoka nyuma ya mgongo wa Mzee Kumbo, alikuwa Tony "Sasa ndio nini kunisemea kwa dingi"
Hakuwa amezungumza kwa ukali, hivyo wote wakacheka.
"Jiandae bwana twen'zetu"
Kila mmoja akajitawanya kujiandaa kwa ajili ya safari. Nadia, Mzee Kumbo na Tony walishuka huko Magomeni mapipa. Mzee Kumbo alionekana akisalimiana haswa na vijana. Hiyo haikumshangaza Nadia lakini hata majina pia hayakumshangaza.
"Fataki, we Mzee Fataki"
Hizo zilikuwa kelele za kijana mmoja aliyekaa juu ya ukuta wa nyumba mbovu, zilizozimwa na ukimya wa mzee kumbo.
"Nadia karibu mwanangu" alimsaidia mfuko alioubeba Nadia, alipofungua mlango wakaingia "Hii ndio nyumba yangu ya mjini"
Nadia alikuwa akishangaa kila kitu alichokuwa akikiona ndani ya nyumba hiyo. Runinga iliyopachikwa ukutani ukubwa wake ukamchanganya, sofa pana za ngozi zikamvutia hakuacha pia kutazama mapazia mapana yaliyoning'inia dirishani.
"Anh!" Aliguna huku uso wake ukitalii juu ya dari "Nyumba yako nzuri sana baba"
Aliporudisha uwepo wake mahali hapo, akashangaa wao wakimshangaa.
"He vipi jamani?"
Akajitia kucheka.
"Si ukae" Tony akawa amegandwa na tabasamu usoni mwake. Mzee Kumbo alikuwa ni mzee wa totozi ndio maana hakupenda kuleta wake zake wawili dar. Mmoja alimuacha Tanga huyo aliitwa Tunu, mwingine ni yule aliyeishi naye kibaha yeye aliitwa Salama. Siku anayokuja Nadia mpaka wanaondoka yeye Salama alikuwa kijiji cha jirani Msongola kwa baba yake yaani mkwe wa Mzee Kumbo.
Giza likawa jirani kuiathiri siku na jua likaangukia magharibi. Hiyo ilikuwa ni baada ya Nadia, Tony na mzee Kumbo kushinda siku nzima nyumbani hapo. Nadia alielekezwa kilipo chumba chake naye akaelekea huko. Nyumba ilikuwa kubwa na hata vyumba vilikuwa vikubwa.
"Hiki ni chumba alichokuwa akilala binti yangu Faidha, sasa yupo masomoni Mtwara"
Nadia alipoachwa peke yake, akaendelea kushangaa kila alichokiona. Godoro pana na kubwa
likamvuta katikati ya usingizi, naye akapotelea huko. Nadia akawa ameingia nyumbani kwa Mzee Kumbo
...
Tony baada ya kuingia chumbani kwake, akatafakari jinsi alivyomsaidia Nadia.
"Lazima atalipa Fadhila siku moja"
Akaachia kitu kilichofanana na tabasamu. Akalikumbuka umbo zuri la Nadia. Kifua kilichobeba embe mbichi bivu zilitoa rangi nyekundu zikamfanya katikati ya miguu yake kutune na kitu kama ujiti kimsimame. Akakumbuka kile kimpacho raha siku zote. Hakuwa na mwanamke muda mrefu wa maana akajiridhisha kama siku zote. Aliishusha bukta yake na kufanya kile kilichomrahisishia kujiona kama vile yupo na Nadia. Akawa anajaribu kukumbuka ile siku aliyoyaona mapaja ya Nadia kama sehemu ya kuvuta hisia zake; akamaliza na kuridhika.
Akalala.
Kesho akapanga njama za kumwambia Nadia kuwa anampenda. Alitaka awe nae kihalali na sio kwenye hisia za kimfikisha katika kilele cha mapenzi. Tony hakujua anajaribu kujiingiza katika vita vya mapenzi na baba yake. Tony hakujua kuwa hata baba yake alikwishavutiwa na Nadia. Baada ya siku kadhaa kupita, walikuwa mezani wakinywa chai, Mzee Kumbo alikuwa akimshuhudia Tony alipokuwa akimchokoza Nadia huku Nadia naye akijibu uchokozi wa Tony kwa aibu ya kujichekelesha kwa aibu.
Akanyanyuka kwa hasira na kuondoka. Kunyanyuka kwa Mzee Kumbo, pia kulimshitua Nadia.
Angenyanyuka kimya kimya, isingedhuru jambo. Kusonya! Na kile kite cha hasira alichopigiza meza? Hapana!
Hata angalia yake, macho yake yakamtisha Nadia. Tony hakuelewa chochote ndio maana akaendelea kumtekenya Nadia kwa unyayo wake akiupitisha juu ya mguu wa Nadia.
Nadia akaona kero mchezo ambao Tony alikuwa akiundeleza. Naye akakiacha chakula, akatoka mezani.
"Vipi tena?"
Tony akauliza huku akipunga mikono yake hewani domo kaliachia likitepweta.
"Mnh! Mhhh!! Hamna kitu" Nadia akajibu huku akiendelea kutafuna mnofu wa sato.
Jioni ya siku hiyo, Nadia alirudi chumbani kwake akitafakari kitendo cha Mzee Kumbo. Si mara ya kwanza kwa kuonesha kitendo cha hasira. Mara ya kwanza ilikuwa siku ambayo Tony alimpangusa nywele zake fupi zilizoangukiwa na vumbi la utovu wa mpapai. Nadia akacheka.
"Ina maana gani huyu mzee alichokifanya?" Akajinong'oneza.
Akakumbuka mara ya pili ni siku ambayo wanaingia humo ndani, Tony alitaka kumpokea mzigo Nadia, Mzee Kumbo akamtupia jicho la chuki Tony mara ghafla kwa kitendo cha kushitukiza, Mzee Kumbo akampora Nadia ule mfuko. Tony hakuelewa chochote muda huo. Na mara ya tatu ni leo, pale mezani. Nadia alikuwa akimtazama kwa ncha ya kope yake na kumuona vile ambavyo Mzee Kumbo amehamanika kwa hasira. Dakika chache ndipo Mzee Kumbo akafanya jambo lisilopendeza. Jambo lililomkinaisha Nadia naye akaamua kuacha chakula.
Akiwa katika kuwaza huko, akapitiwa na usingizi.
Mlango ukafunguliwa taratibu kwa dhumuni la kutomuamsha Nadia endapo amelala. Kitasa kilinyongwa kiustadi baada ya kushushwa, mlango ukanyanyuliwa kwa juu ili mradi usipige kelele. Mlango nao katii. Kivuli kikajitoma ndani taratibu huku kikinyata. Mwanga wa mbalamwezi ulisaidia kuonyesha japo kiwiliwili cha mtu huyo. Alivaa msuli wa kijivu na singlend pana yenye makwapa marefu. Kabla hajamfikia Nadia, Nadia akawa ameamka na kumuona.
"Tony" macho yakamtoka pima kwa mshangao Nadia. "Unataka nini chumbani kwangu Tony"
"Shiiip!!"
Tony akamnyamazisha. Hakuwa akinyata tena. Akapiga hatua chache na kumfikia Nadia alipo.
"Nataka kuongea na wewe"
"Ndio uje chumbani usiku Tony!?"
Akawa anaongea kwa mshangao huku akipandisha brazia yake akifunika mabega yake.
"Usiogope Nadia nataka kukuambia" Akasita kuzungumza alipohisi kuna mtu mlangoni.
'Nani huyu?' Alijiuliza huku akinyanyuka kutoka kitandani. Nadia naye aliona kivuli kile kilichokuwa kimesimama pale mlangoni.
Mara kitasa kikanyongwa.
....
Mzee Kumbo ni mpenzi sana wa tumbaku. Yeye ni mzee wa mjini lakini anapohisi kupata ghafiriko la moyo hutumia tumbaku kama sehemu ya kupunguza hasira alizo nazo.
"Shit"
Alikuwa chumbani kwake akipiga mikupuo kadhaa ya tumbaku aliyoifinyangia kwenye kiko chake.
"Haiwezekani!!"
Akapuliza mkupuo mwingine na kuona ametosheka. Yeye akatumia muda mwingi kuwaza juu ya kumpata Nadia. Nadia alikuwa msichana mzuri sana. Nadia alionekana ni msichana ambaye ana misimamo na mambo yake. Hizo zikawa ni fikra zilizotembea kwenye ubongo wa mzee Kumbo.
"Nifanyaje sasa?"
Hakutaka kabisa kumpoteza Nadia. Akasimama baada ya kuona kana kwamba kukaa hakukumletea majibu aliyoyataka. Akakuna kichwa kama vile alikuwa akijaribu kuzivuta karibu fikra zake. Yote hayakumpa majibu.
Mara akashituka kama ametoka usingizini. Akajibwaga kitandani huku miguu kaining'iniza chini japo haikufika chini moja kwa moja. Akawa analitazama dari la nyumba yake.
"Najua Nadia ana shida" akawaza "Sasa nikitumia mbinu ya mamlaka ya nyumbani wangu yaani nikimwambia kama hunitaki nenda unapopajua sidhani kama anaweza kunikataa kamwe"
Akacheka kwa furaha mpaka akakohoa. "Haya inabidi nimwambie saa ngapi?" Akajiuliza aliponyanyuka na kutaka kutoka nje. Akarudi tena ndani na kujiuliza "Nimfuate usiku huu ili kesho atoe jibu au nimwambie kesho hiyo hiyo?" Akatoka bila kuwaza chochote. Moja kwa moja mpaka mbele ya mlango wa Nadia. Akasimama kwa sekunde kadhaa mahali hapo, akanyonga kitasa kilipofika chini ili ausukume mlango ufunguke? Akapatwa na wazo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Subiri mpaka kesho Kumbo"
Kama vile kuna sauti ilikuwa ikizungumza naye. Akakiacha lakini hakuondoka. Hakuona sababu ya kuingia chumbani kwa Nadia tena. Hakuona sababu ya kumghasi kama ikiwa bado anao muda wa kutosha wa kumuweka Nadia katika himaya yake. Alitoka sehemu hiyo na kuelekea sebuleni mpaka kwenye jokofu. Alitoa dumu lenye maji na kujimiminia kwenye glasi na kuigida funda moja, yote ikawa nyeupe.
Akarudi chumbani kwake kulala.
...
Baada ya Tony kutazama chini pale penye uwazi, alikiona kivuli cha mzee Kumbo kikitembea. Aliendelea kuganda pale kwa muda baada ya kumtazama Nadia na kumuona akiwa ametoa macho pima. Aliweka sikio lake kwenye mlango kusikilizia vishindo vya miguu vya baba yake. Nadia akawa ananong'ona.
"Kuna nini!?"
"Shiiiip!!"
Tony akamnyamazisha. Mara Tony akarudi kwenye kitanda alichokikalia Nadia. Kila mmoja alikuwa akipumua kwa kasi sana huku mapigo ya moyo yakiwaenda kasi sana. Nadia alikuwa akitumbua macho huku Tony akibaki amebung'aa zaidi.
Mara kivuli kikarudi tena.
...
Tony hakuweza kufanya chochote tena na Nadia kwa uoga wa kivuli cha baba yake Mzee Kumba. Akatoka na kurudi chumbani kwake Siku iliyofuata. Nadia alikumbuka kuwa yeye hakupaswa kukaa katika nyumba hiyo. Kumbukumbu zake zilimjia baada ya mambo yaliyokuwa yakitokea kwa kipindi hicho.
Hakupenda kutembea na Tony wala Mzee Kumba.
Alitoka chumbani kwake na kwenda mpaka sebuleni alipotegemea labda angekutana na mzee Kumba, hakumkuta.
"Yuko wapi sasa huyu mzee!?"
Akajiuliza taratibu akifungua mlango wa kutoka nje. Huko alimkuta. "Shikamoo mzee"
Mzee Kumba alikunja sura kwa hasira kisha akaiacha tumbaku yake pembeni ikizidi kuteketea na kumwambia. "Nadia jamani mimi n'na uzee gani?" Alijitazama kila upande na kujiking'uta kung'uta "Enhe! Mama? Au unataka kuninyima nini?" Nadia akacheka upuuzi wa Mzee Kumba na kuendelea na lililomleta. "Mzee" akarudia neno lililomkera Mzee Kumba, yeye hakujali makunyanzi yaliyotokea juu ya uso wa Mzee Kumba "Ningependa kufahamu juu ya ile safari ya kwenda kukaa katika nyumba ya kulea watoto yatima?"
Ni hapo mzee Kumba aliposhituka kuwa kumbe hata Nadia alikuwa akikukumbuka jambo hilo. Akakenua meno yake machafu na kuliachia tabasamu baya la kizee.
"Nakumbuka Nadia, ni vyema umezungumza kunikumbusha kukueleza kuwa ujiandae siku ya kesho nikupeleke"
Nadia alifurahi kusikia hivyo. Tofauti na Mzee kumba alivyotaraji labda Nadia angejihisi vibaya Mzee Kumba kumpeleka katika kituo cha kulea watoto yatima ikiwa yeye ana uwezo wa kumlea.
Nadia akaondoka huku akiiumiza nafsi ya mzee kumba aliyegeuka kumtazama. Milima miwili nyuma ya sketi yake Nadia laini, ilikuwa ikigombana na kufanya fujo ya kupandiana pandiana kiasi cha kutokeza mtikisiko fulani wa ajabu na kuupeleka puta moyo wa Mzee Kumba.
Akaapa kumpata. Kisha akacheka mwenyewe.
……
Ni muda mrefu tangu Rashid aingie Dar es salaam. Ni nani angemshika kwa pesa? Yeye ndiye tajiri aliyemiliki pesa nyingi kwa ujanja wa watoto wa mjini. Alishajulikana kila kona kwa msaada wa rafiki yake aliyemfundisha ujanja. Huyo alianza kumuita baba lakini yeye rafiki yake, alikataa.
"Usiniite baba bwana" alizungumza rafiki yake Rashid "Una nia gani ya kuniita ita baba Rashid?"
Ni yeye ndiye alimpa wazo la kutumia kituo cha kulea watoto yatima kuuza madawa ya kulevya. Na ni yeye ndiye alimfundisha utukutu Rashid na ni yeye ndiye ambaye alikuwa mtu wa karibu sana kwa Rashid hivyo hata kila jambo lililokuwa likimtokea mmoja wao walikuwa wakipeana taarifa.
"Kuna msichana nataka kumleta kituoni" Alisema
"Mzee Kumbo!" Rashid aliongea "kwanini wewe unaleta wasichana tu!?"
Rashid alishangazwa na rafiki yake huyo mzee kijana. Si kwamba hakujua tabia zake za kuchukua wasichana wadogo. Rashid akamuuliza mara alipomuona Mzee kumbo akiwa anapata shida kujibu.
"Ana umri gani?"
"Anha!" Kama anayekumbuka, mara akajibu "kama miaka 19 hivi"
"Lakini mzee si unajua pale kituoni mwisho miaka 16?"
"Nimeshakukataza kuniita mzee Rashid" akikuna kuna ndevu zake chafu "Mimi ni kijana kwa kuwa sijapoteza nguvu bado. Huyo msichana ni mrembo na anaonekana mdogo sana"
"Mimi sina la kuzungumza naomba nikuachie hilo kwenye mikono yako. Naomba nikuambie kuwa naelekea south afrika kesho kufuatilia mzigo"
Japo kituo kile kilianzishwa na Mzee Kumbo na kilisajiliwa naye, lakini Rashid ndiye alikuwa na sauti ya mamlaka kutokana na pesa zake. Mzee Kumbo akatoa macho ya mshangao.
"Mbona imekuwa ghafla hivyo?" Rashid akanyanyuka.
"Mambo ya biashara zetu si unayajua? Huna haja ya kuniuliza kama hujui"
Alinyanyuka na kutokomea zake kuelekea ofisi ya juu ya jengo hilo la kuhifadhi watoto wenye uhitaji.
Alikuwa amepata mwili aliyependeza na kunawiri. Mzee kumbo akamfikiria Nadia na kuona hapo ndipo kulikuwa sehemu sahihi pa kumtenganisha Nadia na Tony na kumuweka karibu pamoja naye.
….
Maisha ya Bi faudhia yalikuwa ya mawazo na fikra zisizoisha na kumtoa machozi. Hakika alijuta kwa mabaya yote aliyowahi kumfanyia Nadia. Alidhani huenda asingewahi kumtesa na kumnyanyasa Nadia, asingemdhurumu hati. Faudhia akilini mwake alihesabu kama kubadilishwa kwa hati feki na halali ulikuwa ni mchezo wa Nadia.
"Ndio maana hakubisha hata tulipomfukuza" Alijinong'oneza.
Alikuwa ndani ya mtumbwi kurudi Mazizini, zanzibar kwa mdogo wake. "Maisha ya mjini siyawezi"
Alijifuta chozi kwa upande wake wa khanga. Alitia huruma na kila aliyemtazama alimsikitikia kabla hajasikia masahibu yaliyomkuta. Si kwamba amefika Dar es salaam miaka mingi iliyopita. Si kwamba alizaliwa na kukuwa katika maisha ya kifukara, yote ni yeye aliyatafuta. Alikuwa akiwahadithia wale abiria wenzake waliokuwa wakisafiri pamoja wakivuka bahari ya hindi usiku wa manane.
"Baada ya kutoka katika ile guest, nikaenda kwa rafiki yangu anayeishi huko kipawa" Faudhia alikuwa analia "Najuta kuja Dar es salaam. Siamini jamani siamini"
Akashindwa kuendelea baada ya kilio kumkaba zaidi.
"Nyamaza kulia dada, tueleze nini kimekukuta"
Dada mmoja alisema huku mwingine akidakia "Ndiyo tueleze mama" huyu alikuwa kijana aliyeonekana kama nahodha wa chombo walichopanda.
"Nilipofika pale, nilimkuta shemeji yangu mume wa rafiki yangu huyo Mwamtumu. Mwam hakuwepo. Baada ya salamu shemeji akanieleza kuwa Mwamtumu ametoka, lakini akanikaribisha. Kwa kuwa sikuwa na pa kwenda, sikukataa na nilishukuru sana. Mwamtumu alikuwa akifanya kazi za kutoa mbao iringa na kuja kuuza Mjini, siku hiyo ilikuwa tofauti"
Faudhia akaanza kulia tena, kisha akaendelea "kawaida ya kufuatilia mbao ilimbidi asafiri usiku wa manane na alikuwa akitumia siku hata tatu nje ya mji mpaka atakaporudi lakini safari hiyo ilikuwa ya kushangaza. Nikiwa chumbani nikimtoa mumewe Mwamtumu kifuani kwangu kwa kumkataza kitendo alichotaka kukifanya kwangu, mara mlango ukafunguliwa. Wote tulishituka"
Hata wale wasafiri wa majini walishituka sanjari na ukimya uliotawala "Lakini mimi nilikwisha vuliwa nguo zangu na kubaki ya ndani pekee. Wakati ambao nahangaika kuziba matiti yangu, ni wakati ambao nilimuona Mwamtumu amesimama katikati ya chumba amefura kwa hasira.
'Mwanahizaya mkubwa malaya wewe' Mwamtumu huyo alimrukia mume wake. Mimi niliogopa sana nikata kukimbia, Mwamtumu akaniwahi. Alinivuta shati yangu nikapiga mweleka nikadondokea kisogo. Baada ya hapo alitoka na kuingia jikoni. Mwamtumu.. Mwamtumu mimi!? Mwamtumu akanim.. Akanimwagi.. Akanimwagia maji ya moto katika kila sehemu ya mwili wangu. Siwezi kusema ni kiasi gani niliumia lakini ni maji yaliyotokota kama yanayonyonyoa kuku"
Faudhia hakuweza tena, akaendelea kulia na kulia zaidi. Ngalawa yao ikazidi kupeperushwa huku na huko.
"Na kule kazimzumbwi kisarawe umefikaje?"
Msichana yule wa mwanzo akamuuliza. "Maisha mdogo wangu" huku akivuta kamasi akazidi kueleza "Niliokolewa pale na majirani. Nikakimbizwa hospital na kupatiwa matibabu. Sikupona kuondoa makovu lakini nilipona maumivu" Akafunua khanga na kwa msaada wa mwanga wa kandili, akawaonesha makovu makubwa yaliyoharibu uso wake. Japo alikuwa ameubishia hodi uzee.
"Nikawa sina pa kulala, kula wala kuishi. Nikaingia mtaani kutafuta maisha. Nikawa naingia kwenye kila nyumba kuomba kazi za ndani sikupata. Nikajaribu kwa mamantilie mpaka leo nikaishia kuosha vyombo na kuwahudumia wateja kwa malipo ya shilingi elfu tatu kwa mwezi" sauti ya Faudhia ikakwama "Inauma sana. Nikaendelea kutafuta kazi ndipo nikafika Kazimzumbwi"
Wakati anaendelea kuzungumza, Faudhia, ngalawa ikaanza kusukwa sukwa. Ilimbidi Faudhia anyamaze.
"Maji yameanza kuingia" Kwa wahka nahodha akafoka. Kila mmoja akaingiwa na hofu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
...
Rashid aliziandaa maiti zake mbili na wanafamilia aliowapanga kwa ajili ya msiba wa kupanga. Hakuwa na tatizo juu ya hati za kusafiria, alikwisharatibu mipango yote. Hati kumi na moja yake na wanafamilia hao, zilikuwa zikionesha kuwa wao ni wazuru. Alicheka alipotafakari ushauri wa Mzee Kumba. Kujiunga naye katika Kituo cha kulea watoto yatima kisha watasaidia katika biashara zao za kupitisha madawa ya kulevya.
Alitazama maiti zile ndani ya sanduku zilibeba madawa ya kulevya yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni tatu za kitanzania. Haikuwa pesa ndogo. Alitumia pesa kidogo kusafirisha mzigo mkubwa. Hivyo hakuona sababu ya kutumia ndege za kawaida, akakodisha yake na wenzake aliowalipa kabisa pesa nyingi ambazo kwake hazikuwa nyingi. Uwanja wa ndege wa mwalimu julius nyerere alikuwa na wenzake, mzigo wake haukuweza kukaguliwa ipasavyo akapitishwa kiujanja.
Ndege aliyopanga kusafiri nayo, ikapaa. Aliamua kushukia Cape town. Hapo hakuna aliyemjua hivyo ilibidi asimamishwe afanyiwe ukaguzi.
...
Kizaazaa kilichoibuka katika bahari, kilikuwa ni kikubwa sana. Ilikuwa mita chache kufika Zanzibar, mawimbi makubwa yakaivaa ngalawa yao. Kila mmoja alihamanika.
Ngalawa ilipeperushwa huku na huko kelele za hofu zikitawala. Manahodha walijitahidi kutoa maji ndani ya ngalawa hiyo, lakini ilionekana kana kwamba ngalawa ilizidiwa. Ilikuwa inaelekea kuzama.
"Tunakufa"
Nahodha mwenye moyo mdogo akamwambia mwenzake wa upande wa nyuma. Walikuwa wawili tu wanaoendesha chombo. Bi Faudhia aliyatoa macho pima akikiona kifo karibu yake. Ngalawa haikuwa na boya la msaada kwa tahadhari mara chombo kinapotaka kuzama wala kifaa chochote.
"Subhanaallah"
Bi Faudhia akaropoka mara wimbi zito lilipopiga chombo na kupepesua huku na huko kisha maji yakajaa ndani ya chombo. Wote wakawa wamelowa na pazia likachanika. Hakuna aliyekumbuka kumsikitikia Bi Faudhia na hadithi yake ya Dar es salaam kule kipawa. Walikuwa wanahangaika kuokoa nafsi zao.
"Mungu tusaidie" Kila mmoja akamtaja Mungu.
Wimbi lingine zito la pili, likapindua ngalawa na kuwabwaga wote majini. Chombo kikapinduka chini juu, juu chini. Ikawa dhahama ndani ya bahari karibu na eneo lijulikanalo kama Kiongwa. Wasiojua kuogelea, walipotupwa tu majini walikunywa vikombe kadhaa. Hata wanaojua pia hawakuwa na uwezo wa kuogelea mpaka nchi kavu, wanawake walianza kuzama. Bi Faudhia alijitahidi kuyapiga maji huku akiendelea kunywa vikombe kwa uwezo wake wote bila kupenda. Wanawake wakaisha wanaume wanne na mwanamke mmoja tu, Bi Faudhia wakaendelea kuyapiga maji huku kina kikionekana kuwa kirefu zaidi na maji yakiwavuta kwenda chini.
"Nakufaa!!!"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment