IMEANDIKWA NA : STALLONE JOYFULLY
*********************************************************************************
Simulizi : Changudoa
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya kitongoji cha Mazizini, ilikuwa ni ya simanzi kubwa huko katika visiwa vya zanzibar. Wageni walikuwa wengi kutoka katika visiwa hivyo na wengine waliotoka bara kwa ajili ya tukio hilo lililoleta simanzi ndani ya nyumba ya Mansoor. Hakika wema wake ukajidhihirisha kwa wingi wa watu waliokuja katika sherehe yake ya mwisho. Sherehe ya kwanza ikiwa ni kuzaliwa, akaoa hiyo ikawa sherehe ya pili na kupata watoto watatu, wawili wakiwa wa mke mdogo aliyeishi Koani na sherehe ya tatu ndiyo hiyo ya kumsindikiza katika maisha yake ya umilele.
Wakina mama, watoto pamoja na baadhi ya wazee wasiojiweza kutoka Tunguu, Fuoni na chukwani walikuwa wakilia huku wakipiga piga vifua vyao kwa uchungu
Kifo hicho kilikuwa na utata mkubwa, mbali na ripoti iliyotolewa na mganga wake maalumu. Mganga wa familia bwana Ramadhani Nasoro.
"Amekufa kutokana na mshituko wa kuona kitu kilichomsababishia mshituko wa moyo na kupelekea kifo chake" Suleya bi mkubwa, Mama yake Nadia, aliyekuwa akiishi naye ndani ya nyumba hiyo, akaibishia kabisa ripoti hiyo.
"Mume wangu hakuwa na magonjwa hayo jamani, hizi ni hila" alilia kwa kwikwi na kikohozi
"njama hizi alishazijua muda mrefu mume wangu"
Ukweli wa kifo cha Mansoor ukabaki kifuani mwa mmoja wa wanaume waliohudhuria katika msiba huo. Mwanaume huyo aliivaa pama kubwa ya ngozi nyeusi na miwani iliyoficha macho yake. Alikuwa ni mrefu mwenye umbo la kati lakini mwenye kifua kipana. Alionekana mwenye simanzi lakini hakujichanganya na watu msibani hapo, hakuna aliyeweza kumgundua. Masaa kadhaa akatoweka.
Msiba ukahudhuriwa na watu wa kila aina na nyadhifa mbalimbali. Ukawa msiba uliogusa wengi kama ulivyogusa vyombo mbali mbali vya habari. Baada ya wote kufika msibani, siku moja baadaye akazikwa Mwembe kiwete, alipozaliwa Mansoor miaka arobaini na tano iliyopita.
Simanzi na lawama, hazikuisha mdomoni mwa Suleya.
"Nadia mwanangu baba yako ameuwawa" alikuwa akimwambia Nadia aliyejikunyata kwa simanzi "sijuhi kwa nini hawa watu hawana huruma?"
"Mama acha kukufuru mama. Vitabu vya dini vinasema kila nafsi itaonja umauti. Acha mama" Huenda Nadia alikwishachoshwa na lawama za mama yake. Akajisimamia na kuelekea mbali na kinywa cha mama yake. Kinywa kilichomtonesha maumivu ya siku chache zilizopita. Mansoor hakuwa baba tu pekee bali ni kama rafiki kwake.
nadia aliumizwa na kumbukumbu hizo.
Hali hiyo akawa ameizoea, mpaka ilipofika tena ile siku mbaya. Siku ambayo Nadia akiwa ametoka nje kukwepa mdomo wa mama yake, aliyekuwa akilalama juu ya kifo cha mumewe kilichotokea siku arobaini zilizopita. Alirudi ndani na kumkuta mama yake ameudondosha ulimi upande wa kulia wa mdomo wake, macho yamemtoka pima, pumzi zimekata.
Balaa!!
"Mama, mama!!"
Aliita bila mafanikio lakini kwa hofu, akaogopa kukiri kuwa mama yake amefariki.
"Amenyongwa"
Majibu ya daktari yakasema hivyo. Jibu ambalo lilimshangaza sana Nadia.
"Amenyongwa?" Alimaka kwa hofu, macho yalimtoka pima "Hapana haiwezekani"
Utata ukazuka ndani ya kichwa chake.
'Wamemuua mume wangu' aliikumbuka kauli ya mama yake aliyekuwa akiirudia mara kwa mara.
"Sasa mama yangu amenyongwa. Ni nani aliyemnyonga? Nani aliyemuua baba yangu?"
Akaliwazwa kwa machozi yaliyomdondoka na kulimeza funda zito la mate.
Siku chache baadaye akamzika mama yake. Ni hapo ulipopita mwezi mmoja akiwa na miaka kumi na tisa alipoanza kushuhudia mambo ya kushangaza. Mambo ya ajabu kutoka kwa upande wa familia ya mke mdogo wa baba yake. Familia ambayo ilikuwa ikiishi huko Koani.
Faudhia, mke mdogo wa Mansoor kutoka koani, alifunga safari mpaka Mazizini mara baada ya kifo cha Suleya na kuzikwa kwake. Faudhia alikuwa mshari, aliyepoteza staha na utu. Alikuwa mwanamke mwenye mdomo ulioghabidhika na mchafu mbele ya watu wa heshima.
Nadia alimfahamu vizuri.
Faudhia alikuwa mke mwenye watoto wawili wa kiume. Watoto ambao yeye alidhani ilikuwa ni bahati na heshima kwa mumewe lakini haikuwa hivyo. Mansoor akampenda zaidi Suleya kuliko yeye. Kila kitu Mansoor alipitisha kwanza kwa suleya kabla hajapeleka kwa Faudhia. Faudhia hakuiona thamani yake kwa mumewe akajenga chuki.
"Baada ya kumuua mume wangu wewe na mama yako, umeona haitoshi ukamnyonga na mama yako?" Alijifunga kibwebwe kiunoni tayari kwa shari.
Nadia hakujibu chochote.
"Sasa kwa taarifa yako nyumba ya koani ya Salim na nyumba hii ya Mazizini ni ya Rashid nakupa siku chache ujipange ukatafute pa kujihifadhi bibi wewe"
Mungu wangu!!
Ndivyo ilivyokuwa, kabla Faudhia hajaondoka kwa tambo akijitupa huku na kule kisha alisonya na kuubamiza mlango.
Nadia akabaki katika mawazo mazito hata njaa iliyomtafuna tangu asubuhi, hakuisikia kabisa. Alianza kulia upya. Maisha yake yakawa ni kulia hata asijue nini kinaendelea katika vifo hivyo viwili vilivyotokea kwa mpigo na katika hali ya kutatanisha.
Simu yake ikaita.
"Halo ka' Rashid" alikuwa kaka yake kutoka kwa Faudhia.
"Asalam aleykum Nadia" akamsalimu
"Walek muislam kaka, hali si nzuri kaka" akaanza kulia kwa deko.
"Vipi tena mdogo wangu?"
"Bi Faudhia kaka" akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa uchungu zaidi.
"Mama?" Rashud akamaka kwa wahka "amekufanyaje tena, Nadia?"
Nadia hakujibu. Rashid akapokea sauti ya kilio kilichomkaba Nadia na kamasi alizozivuta kwa uchungu.
"Basi Nadia usilie naja hapo sasa hivi"
Kisha Rashid akakata simu.
Laiti kama Nadia angemfahamu vizuri kaka yake, basi asingemuamini kiasi hicho. Mbali ya kuzaliwa na mama tofauti, Rashid ndiye mtu pekee aliyeonekana kuwa upande wa Nadia mara baada ya madhira yote yaliyomkuta. Alionekana akimfariji na kumtetea mara kwa mara pale ambapo kulikuwa na ukungu mzito machoni mwa Nadia. Yeye pekee ndiye akawa liwazo pekee la Nadia lililobakia. Lakini moyoni mwake akawa na zaidi ya undugu uliowaunganisha kuwa hivyo pamoja. Rashid tangu siku ambayo alifanikiwa kutambulishwa kuwa huyo ni ndugu yake, akamtamani. Chuchu zake zilizomsimama Nadia na midomo yake haikumfanya muda wote kumtazama. Aliwahi kumkonyeza lakini sidhani kama Nadia atakumbuka. Alikuwa mdogo kiasi, huenda hata hakujua kama alikuwa akikonyezwa.
Rashid akabisha hodi alipokuwa akiishi Nadia.
"Oh kaka"
Wakakumbatiana pale na machozi yakamtoka Nadia.
"Usilie Nadia" Rashid akawa anamfuta machozi huku mkono wake mwingine kaupitisha juu ya bega akizichezea chuchu za Nadia. Nadia hakujisikia vizuri, Hivyo akauputa mkono ule. Wakakaa sofani na Nadia akaanza kumuelezea kwa kina kila kilichotokea punde.
"Pole sana Nadia. Lakini nafahamu huna tabu kwa kuwa unamfahamu mama vizuri" akamtazama kwa muda Nadia, kisha akaendelea kusema "sasa mimi ninachokuomba usilie kama unaeomboleza"
Rashid akanyanyuka pale akipokaa na kuimfuata Nadia katika kochi alilokaa.
"Pia nina ombi naomba unisaidie"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nadia alimtazama kwa hofu kiasi huku akijitahidi kuukwepa mkono wa Rashid uliokuwa ukitalii kwenye mapaja yake.
"Una shida gani ka' Rashid?"
"Nahitaji uwe mpenzi wangu" bila aibu wala kushitushwa na alichoongea Rashid akatoa tabasamu akitoa maana ya alichoongea alimaanisha kweli.
"Pumbavuu"
Nadia akaropoka na sonyo zito likamtoka. Aliponyanyuka na kutaka kuondoka, Rashid alimkamata mkono. Rashid alikuwa ni mwenye nguvu. Hivyo alimkamata Nadia mikono yote miwili na kumtupa juu ya zuria zito la manyoya. Nadia akapiga yowe hafifu kabla hajazibwa kwa mikono ya Rashid ambaye muda wote alikuwa akicheka. Mikono ya Nadia iliyokuwa ikitupwa hewani huku na kule, haikuweza kumzuia Rashid kutimiza azma yake. Nadia alikuwa amevaa khanga nyepesi iliyomsaidia Rashid kuendeleza alichodhamiria. Kiulaini Nadia akabakwa na Rashid aliyeingoja siku hii kwa muda mrefu. Nadia alilia sana kwa uchungu huku Rashid akifunga mkanda wa suruali yake na kumuinamia Nadia na kumbusu kila sehemu ya uso wake. Nadia alinyanyuka kwa ghadhau na kumnasa Rashid kibao kikali.
"Mwanaharamu wewe"
"Ahsante Nadia lakini nipo ayari kukusaidia lakini ukikaidi" Rashid akabinua midomo yake na kuitupa mikono yake hewani "sina jinsi akili kichwani mwako"
Akanyanyuka na kutaka kuondoka, akamgeukia Nadia pale sakafuni alipolala
"Na nisisahau kukusifia kuwa wewe ni mtamu haswa. Ahsante"
Akamkonyeza kisha akatoka nje huku akimuacha Nadia amelowa machozi khanga yake pembeni na titi moja likichungulia nje ya blazia aliyojisitiri nayo.
Akamkonyeza kisha akatoka nje huku akimuacha Nadia amelowa machozi khanga yake pembeni na titi moja likichungulia nje ya blazia aliyojisitiri nayo. Yalikuwa ni maumivu yasiyozoeleka na kumuumiza Nadia, ndani ya kifua chake. Hakuwa amezoea hali ya upweke baada ya kufiwa na wazazi wake, lakini Rashid na Bi Faudhia hawakulijali hilo. Faudhia akatamani mali zilizoachwa na Mansoor, huku Rashid akiendelea kuwaka tamaa ya kimapenzi kwa Nadia. Nadia akaona kulia hakukuwa na maana, alijinyanyua kivivu na kujisitiri maungo yake. Akaingia chumbani kwake na kukaa juu ya kitanda kilichobeba godoro pana Akabaki akiwaza.
Aliwaza kwenda kutoa malalamiko yake kituo cha polisi. Aibu. Aibu ikawa kikwazo katika wazo lake. Aibu ya kubakwa na kaka yake? wengi wangemcheka.
"Mungu wangu!"
Mikono ikiwa imepakata mashavu yake huku viwiko vyake vimejiegemeza juu ya mapaja.
"Nitafanya nini yatima mie?"
Machozi yakamtiririka kwa uchungu.
Jioni ikapitiliza, usiku ukagonga hodi bila kutia chochote mdomoni.
Akalala hivyo hivyo. Majogoo yaliyowika kwa fujo na mafagio yaliyopitishwa katika viwanja vya majirani zake ikamfanya amke sanjari na mwanga mkali wa jua uliojipenyeza katika chumba chake. Alinyanyuka na kukaa kitandani mwake. Alikuwa amevaa vile vile alivyovaa jana.
Alijishangaa.
Hakuwa ameoga wala kubadilisha nguo zake. Aliingia bafuni kupata maji, baada ya kupiga mswaki. Akiwa huko bafuni, alisikia sauti ya mlango ukigongwa hodi. Hodi zile hazikuwa za wema. Hodi zilizogongwa kwa fujo zikamtisha kiasi. Nadia akatoka bafuni akijitupia upande wa kanga kutokea kifuani na kuishia chini kidogo ya magoti yake.
Ndani hakuvaa chochote.
Alipoufikia mlango na ile alipotaka kuufungua akakumbana na kikumbo cha Bi Faudhia.
Salimu na Rashidi wakamfuata nyuma. Bi faudhia akasonya na kumuwasha Nadia kibao kikali kilicho acha alama za vidole kwenye shavu lake.
Hakuelewa kinachoendelea
"Mtoto kibri sana wewe" Bi Faudhia alimaka kwa wahka huku mate yakimtoka mfululizo "Tunagonga! Unatujia na upande wa kanga"
Rashid na Salim walikuwa wameshaingia vyumbani na kupekua vitu ambavyo Nadia hakuelewa. Nadia bado alikuwa amezubaa akitazama kila kilichokuwa kinaendelea.
"Hazipo yaani hazipo kote kabisa mama"
Rashidi akaongea kwa mara ya kwanza. Faudhia akamsogelea Nadia kwa hasira za mbogo na kumtingisha tingisha mabegani. "Ziko wapi"
"Nini jamani?"
Nadia huku akitokwa machozi akashikilia upande wake wa kanga usimponyoke.
"Nakuuliza we malaya"
Macho yakamtoka pima Nadia. Sawa Rashid hakuwa mwanaume wa kwanza kumjua mwili wake lakini alikuwa mwaminifu sana kwa Mbarouk aliyeujua usichana wake.
'Kweli ninaitwa malaya?' Kibao kingine kizito kikamzindua kutoka katika mawazo ya uchungu kwa kuitwa Malaya
"Unalia nini mshenzi wewe?" Ilikuwa sauti ya Salimu, kijana mnene mwenye asili ya kiarabu "utajibu au utaendelea kukubali kupokea mkong'oto mpaka utakapoamua kutuambia wapi zipo hati za nyumba mbili za baba?"
Hati? Neno hilo ndio likamshitua zaidi Nadia. Hakujua kuwa muda wote alikuwa akipigwa na kusukwa sukwa hivyo kutokana na kitu asichokijua kilipo.
Baba na mama yake, walikufa vifo vya ghafla ambavyo hawakuvitarajia. Hivyo hawakujiandaa katika kumkabidhi chochote Nadia kama msaada kwake katika mambo ya mirathi.
Nimepatikana!!
Nadia akajaribu kujitetea huku Rashidi akiendelea kupekua huku na kule
"Sifahamu chochote mimi jamani" kilio kikambana akakohoa kidogo na kuendelea "sielewi zilipo hizo hati mnanionea"
Salimu akamnyanyua kwa fujo na kumkata mtama. Nadia akaisalimia sakafu kwa kuibusu na uji mzito wa chumvi chumvi ukamchuruzika kutoka puani ukaweka makazi kwenye papi za juu ya midomo yake.
Maumivu ya kupasuka sehemu ya mishipa ya pua zake haikumfanya kusahau kuwa yu uchi wa kuzaliwa. Alikuwa amemwaga radhi mbele ya kaka yake huyo wa kambo pamoja na mama yake mwenye gubu. Hakika Nadia alihisi kuonewa sana. Akaizoa kanga yake na kujisitiri upya. Akaipangusa damu iliyokuwa ikimtoka puani kwa ngumi ndipo hapo akaisikia tena sauti ya yule kaka yake aliyedhani yu upande wake.
"Hizi hapa" uso wa Rashidi ukang'aa kwa furaha "Nimezipata zote na za shamba la chukwani"
Wote kwa pamoja wakafurahi huku kicheko kikali cha Bi faudhia kikizidi kuongeza uchungu ndani ya moyo wa Nadia. Salimu akampiga Nadia teke la makalio huku Faudhia akimringishia makaratasi ambayo ni hati za mali ya baba yake na Rashidi akiwa nyuma na kujitia kusikitika kwa kejeli.
Wakatokomea bila kujua kuwa imekula kwao.
...
Baada ya wiki chache kinatokea kitu ambacho Nadia alikitarajia. Alikuwa akifukuzwa nyumbani. Bi faudhia akiwa na askari wawili waliovalia sare zao pamoja na mwanasheria ambaye Nadia hakumtambua, walimjia wakati ambao yeye alikuwa jikoni akijipikia.
"Msichana mwenyewe ni huyu" Faudhia aliongea kwa jazba sana "Ana dharau sana huyu mtoto"
Wale askari nao wakijitia kusikitika na kusonya huku yule mwanasheria aliyeshikilia makaratasi kadhaa akimkazia macho Nadia. Nadia hakutambua kinachoendelea akawasalimia kila mmoja. Mwarabu mwenye adabu ya kisukuma akawasalimia wageni wake kwa goti mpaka chini. Faudhia akasonya na kubetua midomo yake huku akitingisha mguu wake wa kulia na mikono yake ikiwa imeshika kiuno chake chembamba.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hatuna haja ya salamu yako" Askari mmoja akadakia. Kisha akaendelea "kitu ambacho tumekuja hapa hatujafuata salamu yako binti. Hauhitajika kukaa ndani ya nyumba hii kwanzia dakika hii"
Mungu wangu!!
Macho yakamtoka pima Nadia na kuhisi kuchanganyikiwa. Hakujua kama ingekua ni mapenma sana kutokea hayo anayoyasikia, akahisi kizunguzungu.
"Nini!?"
Akauliza kwa sauti iliyokuwa ikitetemeka. Mwanasheria yule ambaye alikuwa akitazama kwa dharau muda wote, akafungua karablasha zake na kupunga hewani. Alimuonesha Nadia baadhi ya karatasi zenye sahihi ya baba yake. Hakuna ambacho Nadia alielewa.
"Sielewi chochote jamani" machozi yakaanza kumbubujika "Mama!" Akamgeukia bi Faudhia aliyekuwa akimtazama kwa nyodo. "Nionee huruma mama yangu"
"Mimi sio mama yako eboo" akamsukumiza Nadia huko "Muuwaji mkubwa wewe"
Muuaji! Nadia alishangazwa. Mwanasheria yule mwenye uso uliotangaza roho mbaya akaongea.
"Tunachoomba binti uchukue nguo na viatu vyako tu kutoka ndani ya hii nyumba na kisha utokomee mbali na jicho la sheria" akamtazama Nadia jinsi alivyohamanika kisha akaendelea kuzungumza "usisahau kuwa una kesi ya kumuua mama yako! Hivyo salama yako utokomee mbali kabisa"
Wakamtisha Nadia. Nadia alijaribu kuwasihi wamuonee huruma lakini walivaa roho ya kishetani. Hakuna aliyeyaonea huruma machozi ya yatima yule aliyelazimika kuiacha shule akiwa bado siku chache afanye mtihani wake wa mwisho wa kidato cha sita. Tatizo likawa ada. Nadia akafukuzwa kama mbwa ndani ya nyumba aliyoijenga baba yake. Akatupiwa nguo zake nje huku machozi yakimbubujika.
Sheria ikapindishwa.
Nadia hakuwa na pa kwenda zaidi ya kukimbilia kwa Mbarouk. Wapi angeenda kama kila aliyemtegemea alimgeuka? Tegemeo lake la mwisho likabaki kwa Mbarouk. Mwanaume aliyemjua kwa kipindi kirefu na kumuamini sana.
Akaelekea huko jioni ya siku ile baada ya kufukuzwa. Huko akakuta mlango wa chumba cha Mbarouk upo wazi lakini ulifungwa kwa ndani. Akabisha hodi haikuitikiwa lakini alisikia vishindo vya mtu aliyekuwa akitembea kwa ndani. Akaita jina la Mbarouk
"Muba" alipenda kumuita kwa ufupisho. Lakini ukimya ukamzomea. Alipokaa kwa muda zaidi akasikia mabishano ndani ya chumba hicho. Ghafla mlango ukafunguliwa.
Lahaula!!
Mbele ya macho yake Nadia, alisimama msichana mrembo aliyevimba kwa hasira. Nyuma yake akafuatiwa na Mbarouk aliyeghafirika na uso uliojaa wasiwasi mkubwa
Nini hiki!!
Nadia alibaki ameduwaa akimtazama Mbarouk na msichana yule kwa zamu.
Akiwa katika kushangaa, Nadia akapigwa kikumbo kizito na msichana yule kilichomfanya apepesuke na kupoteza muhimili sahihi.
Aliposimama sawia na mfuko wake aliobebea nguo, akamfuata Mbarouk kwa hali ya hudhuni. Ukweli ni kwamba alifahamu fika kuwa Mbarouk alitoka kumsaliti lakini hakuitaji kuwa mkali hata pale alipoona kuwa angepata msaada.
"Mpenzi nimefukuzwa"
Aliongea kwa hudhuni nusu kulia.
"Ati nini!?" Mbarouk alimaka kwa wahka. Hiyo ikamtia hofu sana Nadia. Akapoteza tumaini la kupata msaada. Nadia hakutaka kuondoka mpaka kushuhudia mwisho wa kuhamanika huko kwa Mbarouk. Mbarouk hakuishia kuuliza tu, akasimama kwa ghadhabu akihema kwa fujo macho yamemtoka pima.
"Sikuelewi Nadia"
Alikuwa akizungumza kama mwenye hasira za mume aliyefumania mkewe. Alikuwa hana tofauti na mbogo. Hali hiyo ikamtisha Nadia aliyekaa pembeni ya mbao za kitanda mara baada ya kuingia mpaka ndani. Chumba cha Mbarouk kikasadifu zinaa lakini Nadia hakuonesha kujali. Si kwamba hakuwa na wivu lakini alizihifadhi hasira zake ndani ya moyo wake wenye nyama na kusukuma damu.
"Huwezi kunieleza kuwa ndio unataka kuhamia" Mbarouk alikaa akimtazama Nadia.
"Ndio muba mpenzi" Nadia alizungumza kwa uoga "Sina pa kwenda na wewe ndio kimbilio langu la mwisho Muba tafadhali nionee huruma"
"Hapana Nadia sitaweza" macho yakamtoka pima Nadia baada ya kauli hiyo ya Mbarouk "Unajua vie naganga njaa nikijitahidi angalau nipate japo mlo mmoja kwa siku na wewe unataka kuja kuniongezea mzigo? Hapana Nadia. Nenda kwa ndugu zako na vile vile nilikuwa njiani kusafiri naelekea Mafia na pia hii si nyumba ya wasio na makazi uende zako bibi wee!!"
Akapenyeza mkono wake katika mfuko wa nyuma na kutoa noti za shilingi elfu kumi kumi mbili.
"Hizi zitakusaidia katika safari yako na kula njiani tafadhali nenda Nadia"
Nadia alihisi dunia imegeuka juu chini chini kukawa juu. Aliomtazama mara ya pili Mbarouk hakuamini kama huyu ndiye yule kijana waliyeanza mahusiano wakiwa shule. Mapenzi yao yalianza katika shule ya sekondari Michungwani. Nadia hakuwa akijua chochote kuhusu mwanaume. Kipindi hicho alikuwa ameimeza miaka kumi na miwili pekee, hivyo ndio kwanza alikuwa akipevuka. Hakuwa mweupe lakini nywele zake alizifuga na kudondokea juu ya mgongo uliobeba kiuno chembamba na kuunganisha makalio yaliyojijengea kichuguu cha peke yake na kutamanisha macho yoyote ambayo yangemtazama na kisha kichuguu hiko kikabebwa na mapaja manene yaliyojivimbia pembeni na kujenga umbo la chungu cha mfinyanzi pale alipovaa nguo za kubana. Ni mwanaume yupi rijali asingeacha kuutamani urembo wa mwanamke huyu mbichi kabisa ambaye hata matiti yake hayakudondoka kama lapa la choo cha nje bali dodo mbivu zilizosimama juu ya kifua chake kichanga huku tabasamu lake la kitoto likizidi kuchanua mdomoni mwake? Kiukweli sura yake ikasadifu kuwa mbali na kuwa kidato cha kwanza lakini hakuwa akimjua mwanaume yeyote. Mbali na hadithi mbalimbali zilizozagaa kuwa waarabu huwa wanafanya mchezo mbaya kwa kujamiiana kinyume na maumbile ili kulinda bikra zao basi huyu hata busu hakulifahamu. Katikati ya wanaume wengi waliodiriki kumfuatilia na kumsumbua kwa neno moja "Nakupenda"
Alikuwako Mbarouk aliyefanikiwa kuuteka moyo wa Nadia. Mbarouk alimfahamu kwa kuwa walikuwa wakisoma darasa moja. Mbarouk hakuwa akitokea katika maisha yenye uhafadhali lakini kichwani zimo. Nadia nyumbani kulikuwa na pesa za kutosha na hakusumbuka na chochote juu ya swala lililohitaji pesa lakini darasani yeye alikuwa wa wastani. Hivyo akamtegemea Mbarouk kumtoa ukungu pale ambapo hakuwa akielewa jambo walilofundishwa. Kikaja kipindi kigumu katika mahusiano yao pale Mbarouk alipofiwa ghafla na wazazi wake. Umasikini ukashamiri na ilibaki ncha ya uzi aikache shule. Nadia akatambua umuhimu wa shule katika maisha ya Mbarouk. Akadiriki kuiba pesa nyumbani ili akidhi matakwa ya Mbarouk. Mbarouk akaendelea na shule huku kila kitu akimtegemea Nadia. Kipindi chote wakawa bado watoto walioishia kupigana mabusu ya shavuni. Walipofika kidato cha tatu, Mbarouk akafukuzwa katika nyumba nzima kwa kukosa kodi, Nadia akamlipia chumba kimoja maeneo ya chukwani. Ndio chumba hiki ambacho leo Mbarouk anamfukuza. Kwa fedha zake za pedi alizozificha na yeye kuamua kutumia kanga kwa kuhifadhi uchafu huku akimpelekea ela ya kodi Mbarouk bado leo Mbarouk hakumbuki kule walipotoka. Hakuonekana msibani kwa baba yake wala hakuja kwenye msiba wa mama.
Nadia bado hakuamini kama Mbarouk angekuwa hivyo. Akalia hata pale alipohisi labda Mbarouk angebadilisha mawazo yake lakini Mbarouk akatumia nguvu kumtoa nje. Nadia akakosa nguvu za kustahimili kujikwaa akaisalimia ardhi. Alimuona kuwa Mbarouk anaongea huku akitupa mikono hewani lakini hakuelewa alichozungumza.
Uchungu
Uchungu ulimfanya asisikie. Akajinyanyua akajikung'uta vumbi lake mfuko wake ukatupwa miguuni mwake. Mbarouk akaongea
"Nenda Nadia mimi na wewe basi umeshachoka"
He! Kwa kisa gani? Alihisi kizunguzungu kikitaka kumpiga mtama lakini akastahimili uchungu uliokamata koo yake. Machozi yaliyolowesha mashavu yake akayapangusa kwa ngumi upande wa juu ya kiganja chake.
"Kwa heri Mbarouk"
Aliongea kwa dhati kutoka moyoni mwake. Aliongea akitambua Mbarouk hakuwa akimpenda kwa dhati kama kinywa chake kilivyokuwa kikimlaghai siku zote. Hakupenda kutumia neno
"Utanikumbuka"
Kwa kuwa alitambua fika kwa hali aliyofikia Mbarouk asingeweza kumkumbuka. Kama kulala ameshalala naye, kutumia pesa zake amekwishazitumia. Mbarouk akamuumiza sana Nadia kuliko alivyoumizwa na Rashid aliyembaka. Kaka yake ambaye aliamini ndiye mtu wa pekee anayemjali na kumthamini. Akaondoka kwa unyonge huku akili yake ikimpa kuhama kisiwa hicho na kwenda bara. Mfukoni alikuwa na shilingi elfu hamsini huku mkononi alipewa shilingi elfu ishirini na Mbarouk jumla akawa na shilingi elfu sabini. Elfu ishirini zilitosha kumvusha maji mpaka bara elfu tatu akatafuta chakula kwenye mgahawa wa mamantilie aliyekuwa akiwahudumia wajenzi wa ghorofa moja pale stesheni.
Ukweli ni kwamba Bi Faudhia alifurahi sana kuzipata hati zile. Alitamani kuisimamisha dunia na kuitangazia ni kiasi gani alikuwa na furaha siku hiyo. Akamtazama Rashid kisha akamgeukia Salim kwa tabasamu pana zaidi.
"Vijana wangu" akazungumza "leo sina cha kuwaeleza kiasi gani ninafuraha"
Rashid na Salim waliotundika miguu yao juu huku wakitazama runinga ya chogo, nao wakatabasamu kama mama yao.
"Tumeuaga umasikini kiulaini" Salim akaongea huku akibadilisha chaneli kwa rimoti.
"Lakini mimi n'na wazo" Rashid akaushusha mguu wake na akaiweka chini, akamtazama mama yake na Salim kwa zamu na kuendelea "Mnaonaje tuiuze ile nyumba ya mazizini tubaki nayo ya koani kisha pesa tufanyie jambo la msingi?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapo umenena" Faudhia akaafiki lakini Salim akapinga
"Jamani enhe!" Salim huyo "Mimi naonelea tuipangishe tupate pesa kila mwisho wa mwezi"
"Hapana tuiuze jamani" Rashid akakazia. Bi Faudhia akakubaliana na Rashid akapuuza shauri la Salim.
Wakaanza kutafuta mteja.
Wiki chache baadaye mteja akapatikana. Mteja huyo alikuwa ni mwanamke lakini mwenye uhafadhali katika maisha. Mteja ambaye hakutaka longolongo katika ununuzi wa nyumba au mali yenye uhitaji wa fedha nyingi. Nyumba aliyooneshwa na Rashid akaipenda bei wakaafikiana shilingi milioni hamsini. Pesa haikuwa tatizo kwa Bi Fatma.
"Naomba mwanasheria wangu awepo na ahakiki hati zenu"
Kwa kuwa Rashid na Bi Faudhia walikuwa wakijiamini, hawakuwa na tatizo. Bei hiyo ikamchanganya sana Bi Fatma. Nyumba yenye hadhi kama hiyo haikuthubutu kuuzwa walau kwa milioni themanini, ndio iwe hamsini?
Kuna tatizo.
Mwanasheria alipohakiki hati sehemu husika, majibu yakatoka tofauti na vile Bi Faudhia na vijana wake walivyotegemea.
"Hati hizi ni za kugushi sio halali"
Macho yakawatoka pima huku bi fatma akiwacheka kwa kung'amua kuwa walikuwa na nia ya kutaka kumuibia. Vichwa vikawachemka juu ya kuzipata hati halali za mali zote walizozimiliki.
….
Faudhia na watoto wake walijawa na jazba. Hasira zikajikita katika nyuso zao. Matuta kadhaa yakajikita juu ya paji za nyuso zao huku michirizi ya jasho ikimtoka Faudhia.
"Haiwezekani" Faudhia akafoka "kuna mchezo hapa"
"Mchezo upi mama?" Rashid akauliza.
"Huyu mtoto katuchezea jambo" alisema Faudhia huku sura ya wasiwasi wa tafakuri ukiwa wazi "Inawezekana huyu mtoto ndiye amecheza mchezo huu"
Rashid akapinga tena "Anha mama sidhani kama ni yeye kwa hilo napinga mama" Mjadala ukafa baada ya muda kwenda kasi.
Asubuhi yenye pambazuko lenye mwanga hafifu wa jua la udhurungi ukamuamsha Bi Faudhia sambamba na Hodi zilikuwa zikibishwa kwenye mlango wa mbele ya nyumba yao. Alijinyanyua na kwenda kufungua
La haula!!
Mbele yake wakasimama askari wawili waliovalia sare zao na Bi Fatma aliyepambwa na tabasamu pana. "Vipi bi Fatma!?" Faudhia akauliza kwa hofu.
"Naomba mnipishe kwenye nyumba yangu" Fatma akazungumza kwa dharau huku akibetua betua midomo yake. He!! Faudhia alipigwa mshangao kama aliyepigwa na ngumi nzito ya uso. Akacheka asielewe kama Fatma alikuwa akiongea kwa kumaanisha au alitania. Akaunda kitu kama tabasamu lakini halikuwa halisi. Tabasamu ambalo lilijaribu kuonesha kitu kama dharau lakini haikuwa dharau iliyofua dafu mbele ya Fatma. Huyo ndiye mwanamama mwenye jeuri ya pesa. Dharau kwake ikawa makazi. Kwa sauti iliyokera huku akijitia kujipepea Fatma akasema tena.
"Fau nadhani wewe sio kiziwi"
"Lakini sikuelewi?" Faudhia alikatishwa na kikumbo alichopigwa na askari wale njaa waliopewa kiasi kidogo cha pesa kuja kifanya ubabe nyumbani kwa Faudhia.
"Jamani hii si sheria" Faudhia akalalama. Hakuna aliyemsikiliza huku Fatma akipunga karatasi za hati ya nyumba hiyo hewani.
"Hii ndio hati halisi na nimeinunua nyumba hii na ya mazizini kwa bei halisi. Isitoshe na mashamba ya chukwani na huku koani yote ni yangu"
Weweee!! Likawa jipya kwa Bi Faudhia. Macho yakamtoka pima alipokuwa akikodolea karatasi ile ya hati. Sahihi ya Mansoor ilikuwa tofauti lakini ilikuwa ile halisi.
"Nini hiki?"
"Hati hiyo Faudhia" Fatma akamjibu kwa kejeli na dharau ya hali ya juu.
"Pumbavu tokeni nyumbani kwangu kabla sijawaitia polisi"
Fatma alicheka kwa nyodo na kuzirushia nywele zake changa lakini laini nyuma ya shingo yake na kumuuliza kwa mshangao usio wa kweli. "Polisi? Polisi gani Faudhia zaidi ya hawa unaowaona mbele yako?"
"Hawa si polisi ni vibaraka wako Fatma"
Mmoja wa polisi wale akamzaba kibao Faudhia aliyesimama huku akijitingisha tingisha kwa nyodo mbele ya macho yake. Yule polisi akakipunga kitambulisho chake hewani. Alikuwa ni koplo.
"Hii hapa ni barua ya mahakamani unahitajika kesho saa nne ili unikabidhi haki yangu kihaki kama nilivyofanya mimi"
Mama wee!! Barua ilisahihiwa na hakimu mkuu wa mahakama ya madai na kugongwa muhuri mzito. Mambo yameiva.
"Lakini Fatma mbona unanichanganya? Sielewi wewe umepata wapi hati za mali ya mume wangu"
Fatma kwa tabasamu laini akapunga mkono wake aliipekecha pekecha vidole vyake kwa ishara ya kuonesha pesa. "Pesa Faudhia" Kisha akapiga hatua za kuondoka. Ni wakati huo alipotokea Rashid pamoja na Salim katika moja ya vyumba ndani ya nyumba hiyo. Fatma alipowaona, akasimama na kuwatazama kwa dharau akabetua midomo yake na kusonya. Lakini alipotazamana na Rashid, Fatma akaachia tabasamu ambalo hakuonesha wazi meno yake. "Tuondokeni" Faudhia akaachwa akiwa ameduwaa huku akili yake ikiwa haifanyi kazi sawia. "Mama kuna nini?" Salim akauliza huku akiwa na kijibukta kifua wazi. Faudhia hakuwa na nguvu ya kujibu. "Mama" Rashid akaita, Faudhia akajibweteka kochini kivivu na kuendelea kuwatazama watoto wake bila kuwajibu chochote.
"Tumepatikana wanangu"
Ni kweli Faudhia alikuwa amehamanika. Hakujua cha kufanya zaidi akili yake ikiwaza juu ya Nadia. "Nadia katufanyia ushenzi"
"Kivipi?" Salim ndiye alikuwa ana hamu ya kujua sana. Faudhia hakuwajibu. Akanyanyuka na kuingia zake ndani. Mchezo wa akili ukawa umechezwa na mtu wao wa karibu.
...
MWEZI MMOJA ULIOPITA
Katika msiba wa baba yake, Rashid alikuwa akimtazama mshirika wake muda wote. Yule aliyevaa pama ya ngozi na kuyaficha macho yake kwenye miwani mipana ya rangi nyeusi. Huyu alikuwa mtu wa karibu sana kwa Mansoor. Mtu ambaye iliaminika ndiye mtu wa mwisho kuwa na Mansoor kabla ya kifo chake. Huyu ndiye alifahamu siri ya kifo cha Mansoor. Alilipwa ahadi ya pesa nyingi kwa kuwa alikuwa na hakika nazo.
Mchezo ulipangwa na Rashid baada ya kufahamu sehemu ya siri zilipofichwa hati na amana kubwa ya fedha kwa baba yake. Rashid hakuona mtu mwingine wa kumshirikisha zaidi ya Majid, mdogo wa baba yake yaani babamdogo.
"Wewe ndiye upo naye pale ofisini. Hivyo naomba ufanye kila mbinu ya kuweka hiyo sumu kwenye kahawa yake au hata sigara akikutuma, weka huo unga mbele kisha akivuta tu inaingia taratibu kwenye moyo lakini matokeo yake yatachukua muda kiasi" Majid akatekeleza kama alivyoambiwa. Baada ya habari za kifo cha Mansoor kumfikia Majid, Rashid akamshauri akimbie mji. Majid akakubali kwa Rashid lakini moyoni mwake akafikiria ujira wake.
"Siendi popote shenzi" Akafoka kwa hasira. Rashid alipomuona baba yake mdogo msibani hapo, damu yake ikamsisimka. Si kwamba alikuwa na nia ya kweli ya kumdhulumu pesa zake walizopanga, lakini kuonekana kwake mara ya mwisho na marehemu ingebidi aisaidie polisi kueleze hali ambayo alimuona nayo mara ya mwisho kaka yake.
Akapanga kumuua.
Baada ya kutoka msibani, Rashid akelekea moja kwa moja Pongwe alipokuwa akiishi Majid. Palikuwa mbali kiasi lakini hakutaka kumuacha Majid. Alimfuatilia kisiri siri bila Majid kufahamu kuwa alikuwa akifuatiliwa.
Saa Tano ya usiku kwa gari la kahawa Majid akafika pongwe kwa nauli ya shilingi elfu tatu kama lift. Rashid alikuwa nyuma na gari binafsi aliyokodi pale Mazizini sokoni na kuifuatilia gari ile kimya kimya. Majid hakuwa na mke wala mtoto. Lakini alikuwa mtu wa vimada. Leo akawa peke yake huku ikiwa afadhali kwa Rashid.
Majid alipoingia ndani akawasha taa na kujitupa sofani kinywaji kikali alichokitoa kwenye friji kilipita mdomoni kikaiburudisha na koo yake. Rashid akaufungua mlango taratibu akapokelewa na sauti za runinga iliyokuwa ikionesha taarifa ya habari. Akamnyatia Majid mpaka pale alipokuwa amekaa.
Majid alikuwa amelala.
Ikawa kazi rahisi kwa Rashid. Akakichomoa kisu chake alichokuja nacho kutoka kiunoni na kukichomoka kwenye mbavu za Majid. Majid akapiga yowe hafifu huku Rashid akichomoa tena na kukichomeka sehemu nyingine ya tumboni. Yowe la pili akatapika na damu. Rashid akachukua simu ya Majid na kutokomea nayo. Aliporudi tena Koani, Faudhia akamueleza kuwa Suleya alikuwa akilalama mumewe ameuwawa na sio ugonjwa ambao daktari amethibitisha kuwa ni kusimama kwa ufanyaji kazi wa moyo kusukuma damu. Rashid akaipuuza taarifa hiyo huku akiwa na lake moyoni. Alipanga pia kumuua mama yake mkubwa(mke mkubwa wa baba yake) Siku aliyopanga kwenda kumuangamiza ndiyo siku ile ambayo Nadia alitoka na kwenda nje. Hakwenda nje ya karibu bali mbali kiasi huko kwa rafiki yake Sara.
Ikawa rahisi kwa Rashid tena kama kumsukuma mlevi.
Akakuta mlango wa nyumbani kwa Suleya ukiwa wazi. Suleya alikuwa sebuleni akizungumza peke yake. Mkononi alishika karatasi kadhaa. "Oh mwanangu Rashid karibu" Suleya alikuwa na roho nzuri na ya upendo kwa upande wa mke mdogo. Na ndiye yeye aliyemshauri mumewe aowe mke mwingine ili ampatie watoto. Hiyo ilikuwa baada ya Suleya kuchelewa kunasa mimba. Hivyo Suleya akampenda sana mke mwenzie.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa tabasamu lisilo halisi Rashid akamuitikia mama yake mdogo. Alipoingia mpaka sebuleni ikiwa Suleya amesimama akimpokea karatasi zile, Rashid akafanya kile alichopanga. Mikono yake ikapishana pale alipoipindua shingo ya Suleya mpaka ilipolia kama ujita mkavu uliovunjika. Suleya akakamaa na kudondoka chini kwa kishindo. Rashid akabadilisha hati alizokuwa nazo mkononi mwake na zile halali, akatokomea nazo kupitia mlango wa uani.
Baada ya mazishi na siku ile walipokuja kufanya fujo nyumbani walipomkuta Nadia mpaka walipompata bi Fatma na kutaka kumuuzia nyumba kwa hati feki, yeye akamfuata binafsi kwa usiri mkubwa na kumuuzia mali zote kwa kiasi kikubwa cha fedha. Hiyo ikawa siri kati ya rashid na Fatma.
…
ENDELEA KUANZIA HAPA Nadia alishuka kutoka katika boti ya Flying horse akitokea zanzibar majira ya saa mbili usiku. Ni kweli alikuwa akilia muda wote na kuna ambao waliomuona, lakini alipofuatwa na kijana Emmanuel na kuulizwa kwanini analia, akakataa "Mimi?" Huku akijufuta futa kwa upande wake wa khanga "Silii bwana" Kisha akaachia tabasamu hafifu lililolegea na hivyo kutoonesha dalili yeyote ya furaha.
Emmanuel na Nadia wakawa marafiki mara baada ya chombo kufika robo ya safari kuja dar kutokea zanzibar. Emmanuel alikuwa mkazi wa kibaha eneo la Kumba. Alishughulika na biashara za kuuza vifaa vya umeme vya mtumba alivyovinunua kutoka zanzibar. "Unaenda Dar kwa nani sasa?"
Nadia alikwisha mueleza kwa ufupi juu ya kuwapoteza wazazi wake kwa kipindi kifupi. Nadia akajiuma uma bila kuwa na jibu sahihi. Mwisho akaamua kumueleza ukweli. "Mimi sina ninapopajua Dar naenda kutafuta maisha" Emmanuel akamjibu kwa utani "Unatafuta maisha yamekosa nini?" Nadia hakuelewa, Emmanuel kwa tabasamu laini la kumlegeza Nadia akamuuliza tena kwa utani "Sasa hayo maisha unayajua yalipojificha hadi unaenda kuyatafutia huko unapoenda?" Kama ambavyo Emmanuel alitaraji, akaliona tabasamu hakika kwenye uso wa Nadia. Ile hali ya huzuni ikapotea furaha ikawa katikati ya mazungumzo yao. Hiyo ikawa furaha kwa Emmanuel.
Wakashuka pamoja posta na Emmanuel aliahidi kumsaidia sehemu ya kufikia. Mzigo pekee alio nao Nadia mkononi mwake, ni mfuko mkubwa wa nailoni aliohifadhia nguo zake. Chini alikuwa na ndala. Emmanuel akaita Taksi aliyopakia mizigo yake mingi iliyowekwa kwenye boksi mbili kubwa.
"Tupeleke ubungo" alimwambia dereva alipomuinamia kwa kuweka kiwiko cha mkono wake juu ya paa la gari hiyo huku uso wake ukichungulia kupitia dirishani.
"Elfu kumi kaka" Emmanuel akaguna baada ya kusikia bei ya kuumiza aliyomtajia dereva huyo. Nadia alikuwa pembeni akiangaza huku na kule huku nywele zake ndefu kiasi zikipeperushwa kwa upepo mwanana wa bahari ya hindi.
"Nina Elfu saba"
"Ongeza japo buku kaka" dereva akaongea kwa sauti iliyopwaya. Emmanuel akaafiki akaingiza mizigo kwenye buti ya gari baada ya kufunguliwa, kisha safari ikaanza baada ya Nadia kuingia ndani ya gari. Ubungo walipofika ilikuwa ishatimu saa mbili usiku. Nadia na Emmanuel wakapanda gari ya mlandizi kuelekea Kumba.
Emmanuel alikuwa kijana mwenye umri wa kati ya miaka 20 na 23. Uso wake ukasadifu dhiki iliyokuwa ikimtafuna huku aijaribu kupambana nayo. Alikuwa akiishi peke yake ndani ya chumba kimoja kichafu kama uwajuavyo vijana wengi ambao bado hawajaoa. Chumba chake kilibeba kitanda kipana chenye urefu na upana wa sawa sita kwa sita. Kochi moja kuwa litakaloweza kubeba watu watatu lililotengenezwa kwa aina fulani ya asili. Runinga pana lakini yenye muundo wa chogo ilibebwa kwenye stuli iliyohifadhi vumbi jingi. Jiko la mchina na sufuria iliyojaa masizi meusi ya moshi mbaya uliotoka kwenye jiko hilo likiwa limejikita kwenye kona moja ya chumba hicho.
Emmanuel akamkaribisha Nadia ndani ya chumba chake.
"Haya wee"
"Vipi tena Kaka Ima?" Nadia akauliza kwa uoga kiasi. "Dah umeme umekatika hii ni luku halafu nimesahau kununua bwana"
"Usijali Ima kwani hakuna hata kibatari?"
"Ngoja kuna mshumaa" akaingiza mizigo ndani na kuweka kwenye kona moja pembeni ya kochi lile upande wa magharibi ya chumba chake. "Nitawasha mshumaa upo humu chini ya hiki kiti" akabinua juu kiti kile alichokisogelea pasipo Nadia kumuona kutokana na giza mara mwale wa kiberiti ukaleta mwanga.
Nadia akakaa juu ya kitanda akamsikiliza Emmanuel. "Sasa kaoge basi nikuletee chakula" Akamtoa nje ya chumba na kumpitisha kwenye korido la vyumba vya wapangaji wenzake Emmanuel. Wakatokea katika mabanda ya uani kilipo choo ambacho pia huwa wanatumia kwa kuogea. Nadia aliingia kuoga na Emmanuel akaenda kununua chakula katika mitaa ya jirani. Kulala ikawa mtihani mwingine.
Kutokana na ugeni kwa Nadia, Emmanuel akaficha makucha yake ya kutamani wasichana kila kukicha na kuamua kulala chini huku akimuachia Nadia kitanda. Chumba kilikua kikubwa kiasi hivyo palimtosha Emmanuel kulala hapo. Asubuhi kulipokucha, mlango ukawa unatoa mlio wa hodi iliyokuwa ikigongwa kwa fujo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment