Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

DOMO LA MAMBA - 5

 





    Simulizi : Domo La Mamba

    Sehemu Ya Tano (5)







    Sajini Kitowela alikata simu na kujipapasa mfuko. Akatoa pochi yake na kuifungua kisha akatoa noti zilizokuwemo na kuzihesabu. Zilikuwa ni shilingi 12,000. “Zinatosha,” alinong’ona huku akiirudisha pochi hiyo mfukoni. Alikuwa na maana ya kuzikagua fedha hizo. Ni kwamba, tayari ameshakabidhiwa majukumu mazito. Na amekabidhiwa huku akiwa mbali na ofisi na akiwa hana usafiri, hivyo, pesa hizo zilikuwa ni nyenzo kama kutatokea suala lolote la dharura litakalohitaji gharama.

    Akaendelea na zoezi lake la kumchunguza mtu wake. Mara akamwona akikimbilia teksi ambayo mara tu alipoingia iliondoka. Kitowela hakumwachia, alianza kutekeleza moja ya maagizo ya mkuu wake; naye akaivaa teksi nyingine na kumwamuru dereva kuifuata teksi iliyotangulia.

    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Teksi aliyokuwemo Kessy ilikwenda umbali wa mita kama mia moja hivi na Kessy akapata sababu ya kuteremka. Upande wa kulia aliliona jengo kubwa lililoezekwa paa la makuti. Kwenye ukuta wa jengo hilo kulikuwa na maandishi makubwa: STEREO CLUB.

    “Paki hapo,” alimwamuru dereva. Kisha akachomoa noti moja ya shilingi 10,000 na kumpatia.

    “Nikusubiri, bosi?” dereva alimuuliza.

    “Biashara imekwisha,” Kessy alijibu huku akitoka.

    Akiwa hataki dereva huyo ajue chochote ambacho kitaendelea, na hasa kujua kuwa sasa yeye, Kessy, ataelekea wapi, alitulia kwanza akiiangalia teksi hiyo ikiondoka, kisha akaanza kuvuta hatua akirudi usawa wa Kongo Guest House. Alipofika mkabala na lango kuu akatupa macho kwenye eneo la ndani la gesti hiyo. Akawaona wanawake wawili, watatu wakiongea kwa sauti kubwa huku wakinyoosheana vidole. Hakuwajali. Akaendelea kutembea, safari hii macho yakiwa upande wa kulia ambako kulikuwa na baa.

    Nafsi ikamtuma aingie ndani ya baa hiyo. Na akaridhika baada ya kupata sehemu ambayo angeweza kuona kwa usahihi eneo lote la nje hadi kule Kongo Guest House.

    “Karibu, kaka,” mhudumu alisimama mbele yake.

    Kessy alimtazama kidogo kisha akamuuliza, “Kuna vinywaji gani?”

    “Soda aina zote, bia aina zote na maji kila aina. Pia kama unavyoona pale mbele, kitimoto ni ya kumwaga.”

    “Lete Sprite.”

    Mhudumu alipoondoka, Kessy aliyarejesha macho kule nje. Akili yake haikutulia, na isingeweza kutulia hadi akutane na yule mwanamke aliyemfuata. Aliichukulia nafasi hii kama ya kipekee, ambayo kama ataipoteza basi mchezo utakuwa umekwisha vibaya. Dakika kumi baadaye, akiwa anaendelea kunywa soda yake taratibu, macho yake yakiwa hayabanduki kule kwenye gesti, mara akamwona mmoja wa wale wanawake waliokuwa wakizungumza kwa shari akitoka na kukifuata kibanda cha chipsi.

    Kessy alivutiwa na mwanamke huyo, na akajiwa na wazo la kumtumia katika kufanikisha kuwa karibu na Fatma. Akamwita mhudumu na kumuuliza, “Unamfahamu yule dada?”

    Mhudumu aligeuka na kutazama kwenye kibanda cha chipsi. “Yupi, yule aliyevaa suruali nyeusi?”

    “Huyohuyo.”

    “Kwa kweli namfahamu kijuu-juu tu,” mhudumu huyo alijibu “Huwa namwona mara moja-moja akija hapa kunywa bia au kula kitimoto.”

    “Atakuwa anaishi pale gesti?” Kessy aliendelea kudadisi.

    Mhudumu akanyanyua mabega na kuyashusha. “S’jui. Hapa kila mtu anaishi kivyake-vyake, hakuna kuchunguzana. Vipi, nikuitie?”

    “Ni kama umeusoma moyo wangu,” Kessy alimdaka. “Kama unajua siyo mapepe, kamwite. Zawadi yako, bia moja.”

    “Us’konde.”

    Mhudumu alisogea hatua mbili, tatu na kupaza sauti, “Sauda!”

    Yule mwanamke aligeuka na kumtazama kidogo mhudumu kisha akaropoka kwa sauti yenye mkwaruzo wa kilevi, “Unasemaje wewe mjinga?”

    “Hebu njoo, acha kulemaa! Kuna mgeni wako!”

    Wito kutoka kwa mhudumu huyo, mara nyingi ulimnufaisha Sauda. Mara kwa mara wanaume wakware walimtumia mhudumu huyo kumpata Sauda. Hivyo, hata asubuhi hii Sauda alijua kuwa tayari kuna tenda. Hakuchelewa, akavuta hatua akimfuata mhudumu huyo huku akitembea kwa madaha, miondoko ambayo mara nyingi ilikuwa ikiwafanya wakware washindwe kuyabandua macho yao kwenye robota la kiuno chake.

    “Unamwona kaka yule?” mhudumu yule aliyeitwa Siamini alimuuliza.

    “Yupi?”

    “Yule aliyevaa shati la dukani, kofia la pama na miwani ya giza.”

    Sauda alimtazama Kessy kwa makini na kwa chati, kisha akashusha pumzi ndefu na kusema, “Ndiyo. Kwani inakuwaje?”

    “Hilo siyo swali, kwani kazi yako ni nini? Ni kipi kinachokupeleka barabarani kila siku usiku?”

    Sauda akaachia cheko la kimbea. “Mambo si hayo? Kwa hiyo nikamfuate?”

    “Nd’o maana’ake. Kazi kwako mwanamke; kiuno ni chako na pesa ni zako. Lakini usikose kuniachia hata bia mbili.”

    “Aah, mimi na wewe!” Sauda alisema huku akiondoka. “Wewe siwezi kukuangusha.”

    “Poa.”

    Sauda alimfuata Kessy kwa hatua fupifupi na alipomfikia alivuta kiti na kuketi.

    Wakatazamana kidogo. Sauda akajitia kutazama kando haraka kwa aibu ya kulazimisha. Aibu! Yeye ni mtu wa kuona aibu?

    Kwa Kessy, ilimchukua dakika moja tu kumtambua Sauda baada ya kumchunguza usoni. Alikuwa ni mwanamke mwenye macho yaliyodhihirisha wazi kuwa yuko tayari kwa lolote na kwa mwanamume yeyote mradi tu pesa zitue katika himaya yake.

    “Mambo?” Kessy alimwingia kwa mfumo huo.

    “Shwari tu.”

    “Si ndiye Sauda, eti?”

    “Ndiye mwenyewe. Nimeambiwa unaniita.”

    Kessy alimtazama tena kwa makini. “Ndiyo. Najisikia upweke kukaa peke yangu. Nahitaji kupata kampani toka kwa demu wa nguvu kama wewe.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sauda aliguna na kumtazama Kessy kwa macho malegevu. “Kwa hiyo inakuwaje? Funguka mwanaume!” hatimaye aliuliza huku akikisogeza kiti chake jirani zaidi na Kessy.

    “Unatumia kinywaji gani?”

    “Soda.”

    Kessy alishangazwa na kauli hiyo ya Sauda. Alizijua tabia na hulka za akinadada wengi wanaotumia miili yao kama vitegauchumi vya kuwastarehesha wanaume wakware. Wengi wao huwa ni waroho wa bia. Hupenda kuanza kumkamua mapema mkware aliyejilengesha, ndipo zoezi jingine litafuata. Mwanamke atataka bia bila kukosa kutafuna kuku au hata hiyo ‘kitimoto’ ili alishindilie kabisa tumbo na kuokoa bajeti ya pato atakalolipwa baada ya kumstarehesha mwanamume aliyemfuata.

    Lakini huyu Sauda hakuonyesha kuwa ana pupa ya kunywa bia. Kessy alimshangaa. Akamuuliza, “Kwa nini unywe soda? Hutumii bia?”

    “Asante. Bia, baadaye. Si bado tupo?”

    Dakika tano baadaye walikuwa wamezoeana. Na walikuwa wameshafikia makubaliano ya kuimaliza siku hiyo wakiwa pamoja.

    “Nakwambia utafurahi mwenyewe,” Sauda alimwambia.

    “Una hakika?” Kessy alimuuliza huku akiutazama ujazo wa matiti yake kifuani.

    “Mi’ si mchezo,” Sauda alijibu kwa madaha huku akinyanyuka. “Nakwambia utanikumbuka. Na lazima utanitafuta tena.”

    “Sawa, ya nini kuandikia mate?”

    Sauda alibibitua midomo na kujitingisha makusudi huku akimpa mgongo Kessy, labda akitaka ashuhudie ziada ya vituko vyake. Kisha akamgeukia na kusema, “Hapo umesema. Hakuna haja ya kuandikia mate huku wino upo.”

    Wakatazamana. Sauda alicheka huku akiangaza macho ukumbini humo, na alipogundua kuwa hakuna aliyewafuatilia alimwinamia Kessy na kuikita mikono mapajani kwake. Kisha aliupenyeza mkono kwa chati na kuutua katikati ya miguu ya Kessy ambako uliminya kwa namna iliyomfanya Kessy atoe mguno hafifu na kusisimkwa mwili.

    “Mmh, mwanaume umejaaliwa,” Sauda alinong’ona huku akirudia kumminya kwa namna ileile, safari hii akifanya hivyo mara kadhaa hadi Kessy alipomzuia kwa kuutoa mkono huo kistaarabu.

    “Subiri, hapa s’o mahala pake,” alimwambia.

    Sauda alitii na kunyanyuka akielekea msalani. Kessy akamtazama jinsi alivyotembea kwa namna ya uchokozi wa dhahiri kwa wanaume wasio wavumilivu. Aliporejea tu, Kessy alimwanza, “Hivi, Sauda unaishi hapo gesti?”

    “Ndiyo, kwani vipi?”

    “Una muda mrefu tangu uanze kuishi hapo?”

    Sauda alicheka. “Hapo nd'o maskani. Nipo zaidi ya mwaka sasa.”

    “I see.”

    “Kwa nini unauliza?”

    Kessy akajifanya kama hakulisikia swali hilo. Badala yake akarusha swali jingine: “Kuna mwanamke mmoja mrefu hivi, ameingia hapo muda mfupi uliopita.Unamfahamu?”

    “Yupi, yule aliyevaa jeans na miwani myeusi?”

    “Nadhani ni huyo…”

    “Si anatembea kwa kujisikia-sikia hivi?”

    Kessy akaachia tabasamu la mbali.

    “Kajazia-jazia mihipsi,” Sauda akaendelea. “Kwa kifupi anaonekana ananata. Siye huyo unayemsema?”

    “Ni mwenyewe,” Kessy alijibu.

    “Enhe, wa nini? Au unamtaka?”

    “Siyo kwamba namtaka…”

    “Sasa unamuulizia wa nini?” Sauda alijitia ukali. “Kwa taarifa yako yule usimchukulie ka’ mimi. Yuko pale kivyake-vyake.”

    “Najua. Lakini ninataka kujua, ni mpangaji wa hapo?”

    “Ndiyo. Lakini hana siku nyingi.”

    “Ok, sasa sikia,” Kessy aliishusha sauti. Akamtazama Sauda kwa makini na kwa macho makali.

    Sauda naye alikunja uso kidogo akionyesha kushtushwa na kauli ya Kessy. “Kwani vipi?” akauliza kwa sauti yenye dalili za woga.

    “Mimi nataka chumba hapo kwenye gesti yenu,” Kessy alisema. “Lakini sitaki huyo mwanamke ajue kuwa niko hapo.”

    “Kwa nini? Ni mkeo au hawara yako?”

    “Aliwahi kuwa hawara yangu, na anamfahamu mke wangu. Mtu wa aina hiyo siyo wa kumwamini, anaweza kwenda kunichomea kwa waifu.”

    Ukimya mfupi ukatawala. Sauda hakuwa na hoja yoyote, alikuwa hapo kufuatia wito aliopata. Hivyo akasubiri kauli ya Kessy, kufuatia maelezo yake kuhusu hofu juu ya huyo mwanamke aliyekuwa akimzungumzia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa ni hivi,” Kessy alisema, “ kahakikishe kama vyumba vipo vya kutosha halafu uje un’ambie.”

    Sauda aliguna. “Mbona vyumba vipo!” alisema kwa mshangao. “Gesti hiyo huwa haijai. We twende ukachague chumba utakachoona kinafaa, tukajichimbie zetu, tule raha zetu.”

    Kessy alirekebisha miwani yake na kunyanyuka. Alishaamua kwenda katika gesti hiyo na aliamini kuwa hakuna mtu yeyote mwingine ambaye angemtambua. Lakini wakati huo akawaza juu ya huyu Sauda. Kwa ujumla hakumhitaji rasmi kwa minajili ya kustarehe naye kimwili. La hasha. Alihitaji msaada wake tu, msaada ambao tayari anaona kuwa huu aliokwishaupata unatosha. Pia hakuwa mtu wa kuingia naye chumbani na kumwachia uhuru wa kukitawala chumba. Hapana, kufanya hivyo kunaweza kumgharimu. Huenda Sauda akagundua kuwa ana bastola; ni hilo ambalo hakutaka litokee.

    Mfukoni alikuwa na pesa kidogo tu kiasi cha shilingi 30,000 hivi. Kwa mtu wa aina ya Sauda shilingi 5,000 ni nyingi sana kwake na hasa kwa kuzingatia kuwa hizo pesa kazipata bila ya kuzitolea jasho na soda juu! Hivyo alichomoa noti moja ya kiasi hicho na kumpatia huku akisema, “Tuonane jioni. Kwa sasa ngoja nichukue chumba nipumzike.”

    “Jioni ya saa ngapi?”

    “Tufanye saa tatu hadi tatu na nusu. Tukutane hapahapa. Sawa?”

    “Poa tu.”

    Kessy alinyanyuka na kuelekea katika gesti ile, macho yake yakiwa makini katika kuwachunguza wakazi wa hapo. Hatimaye alifika mapokezi ambako alikaribishwa na binti mwingine mwenye mvuto mkali.

    “Karibu , kaka,” alikaribishwa.

    “Asante. Nitapata chumba?”

    “Vyumba vipo. Double au single?”

    “Single,” Kessy alijibu huku akiachia tabasamu la mbali. “ Si unaniona niko single? We mrembo vipi?”

    Yule mhudumu naye akajibu tabasamu la Kessy kwa tabasamu lake hafifu. Kisha akasema, “Ok, ni shilingi alfu kumi na tano tu, kaka.”

    Dakika iliyofuata alikuwa akionyeshwa chumba alicholipia. Alipobaki peke yake akajilaza kitandani na kuwaza nini afanye katika kutekeleza azma ya safari yake iliyomfikisha hapo. Aliamua kuwa hii iwe ndiyo siku ya kuhitimisha kazi. Na, ni lazima akutane na Fatma, iwe, isiwe. Kitakachofuata baada ya kuonana kitajulikana wakati huohuo. Lakini dhamira yake ni kupewa fungu la fedha zilizopatikana kwenye tukio lililomtoa roho Beka Bagambi, nje ya Benki ya CRDB Mtaa wa Azikiwe kiasi cha mwezi mmoja uliopita.

    Aliwaza, kwa nini Fatma aje kupanga gesti ilhali ana pesa lukuki alizotokomea nazo? Na kwa nini aichague gesti hii ambayo ina sifa ya kupata wapangaji machangudoa? Kwa jinsi Fatma anavyojiweza kipesa, angeweza kwenda kukaa katika hoteli yoyote ya hadhi ya juu kwenye maeneo yenye hadhi ya wenyenazo! Siyo huku Kinondoni Moscow, uswahilini kulikofurika vibaka na machangudoa wa sirini na hadharani.

    Atakuwa anajificha kukamatwa, Kessy aliwaza. Kisha akacheka kidogo, kicheko cha dhihaka. Ndiyo, kwa kuwa tayari anamiliki zaidi ya milioni hamsini hakuwa na sababu ya kumfanya aje kukodi chumba katika gesti hii ya uswahilini, gesti ambayo hata milango yake haina vitasa vya kisasa, vyumba havina viyoyozi na mambo mengine mengi yaliyotosha kuiweka katika daraja la chini zaidi.

    Akilini mwa Kessy aliona kuwa kama angekuwa ni yeye, akiwa anamiliki pesa lukuki vile, takriban shilingi milioni 100, asingeendekeza kuendelea kuishi Tanzania. Ya nini kuendelea kuishi Tanzania ambako kila kukicha kila rasilimali inauzwa kwa kampuni za kigeni? Je, haitatokea hatimaye hata Watanzania wenyewe wakauzwa? Kama angekuwa yeye, angepaa hadi Ulaya au Amerika na kuyamalizia maisha hukohuko!

    Alimwona Fatma kuwa kwa kiasi fulani ni mjinga kwa kuendelea kuishi Tanzania, na pia kwa kiasi fulani siyo mjinga kwani kitendo cha kulemaa ndani ya nchi hii inayonuka ufisadi, kumemsaidia yeye, Kessy, kuweza kumpata.

    Akiba aliyokuwa nayo kilikuwa kichocheo kingine cha kulazimisha upatikanaji wa pesa kutoka kwa Fatma siku hiyo. Alisaliwa na shilingi 10,000 tu! Hazikuwa ni pesa ambazo kwake, yeye ambaye pindi anapobakiwa na akiba ya shilingi 100,000 hujiona hana kitu. Akakunja uso na kupiga ngumi kiganjani, kisha akaapa kwa mnong’ono, “Liwalo na liwe…ama pesa ama roho yake!”







    Kessy hakuweza kujibu. Sauti ilikwama. Swali hili la Sauda halikutoka hivihivi, tayari mkono wake mmoja ulishapotea njia na kutua kifuani mwa Kessy ambako ulipapasa kwa muda mfupi na kushuka chini zaidi hadi katikati ya miguu ambako ulitulia na kufanya kile kilichomkausha sauti mwanamume wa watu. Kessy akashindwa kustahimili. Naye akajikuta akimpapasa Sauda hapa na pale, akimminya na kumtomasa huku na kule hadi wakajikuta wakianguka kitandani ambako Sauda aliendelea kuwa mtundu maradufu, akiutumia ulimi wake kutalii kila sehemu ya mwili wa Kessy kwa namna ya kipekee. Ni pale tu Kessy alipoonekana kuhitaji zaidi ya hapo walipofikia, ndipo Sauda alipojing’atua na kuketi pembeni.

    “Baadaye,” Sauda alisema huku mkono bado ukitalii kwenye maungio ya miguu ya Kessy. Akaongeza, “Saa hizi noma, si tulikubaliana iwe jioni?”

    Kessy akaitika kwa kutikisa kichwa.

    “Basi poa,” Sauda alisema. “Mwenyewe utafurahi. Lakini lazima unipe bia mbili kwanza ili akili ikae sawa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****



    “Endelea kuifuata,” Kitowela alimwambia dereva teksi wakati walipofika eneo la Mwembejini na kuiona teksi iliyokuwa mbele ikikata kushoto kuifuata Barabara ya Wakulima.

    Safari yao ilikoma baada ya kuiona teksi hiyo ikiegeshwa kando ya ukumbi wa STEREO CLUB. Kitowela alimwamuru dereva apaki kando ya ukumbi huo kama magari mengine mawili waliyoyakuta hapo. Alipoteremka na kuiruhusu teksi kuondoka, akamwona Kessy akishika njia walikotokea hadi kwenye baa.

    Dakika chache baadaye Kitowela naye alikuwa ndani ya baa hiyo. Akawa akiendelea kufuatilia kwa makini nyendo za Kessy huku sasa badala ya kuwasiliana na Mbunda moja kwa moja, aliamua kutumia ujumbe wa maandishi. Ni pale Kessy alipoondoka na kuingia ndani ya gesti ile ndipo Kitowela alipoamua kumpigia Mbunda.“Kaingia gesti…!” alimwambia.



    “Bana hapo hapo!” Mbunda aliwaka. “Kwa vyovyote atakuwa makini, akijua kuwa anatafutwa. Na lazima atakuwa na silaha. Tutakuja baadaye tukiwa kamili!”



    Halikuwa ni zoezi la kumshinda mtu kama Kitowela. Alichofanya ni kuagiza bia na kuketi kwa namna ambayo angeweza kuyaona kwa usahihi yote ambayo yangetokea pale kwenye ile gesti. Kuanzia pale Kessy alipofika na kisha akawa akizungumza na Sauda, yeye aliendelea kutulia na bia yake. Na hata Kessy alipoondoka na kuelekea ndani ya gesti, Kitowela alishuhudia. Hakuwa na haraka. Alikuwa makini kwa muda wote akihakikisha kuwa Kessy hampotei.

    Muda ulizidi kwenda huku Mbunda hatokei. Hatimaye alimpigia simu na kupewa jibu lililomshangaza.

    “Unasikia Kito, nimeona huyo mtu tumkamate wakati kijigiza kimeshaanza kuingia,” ndivyo Mbunda alivyomwambia.

    “Lakini anaweza kuondoka, afande!”

    “Akiondoka, ondoka naye! Cha muhimu ni kutompoteza. Hata kama atakwenda mbinguni tutamfuata na kumkamatia hukohuko!”

    Saa kumi ilifika.

    Kumi na moja!

    Kumi na mbili!

    Kitowela alikuwa na bia tatu na nyama-choma tumboni. Jua lilianza kutokomea na watu walizidi kuongezeka katika baa hiyo. Mara akaitazama tena saa na kuguna. Lakini papohapo simu ikaita. Akatoka na kusogea eneo la vyoo ambako hakukuwa na watu.

    “Nimefika Stereo Club. Bado uko hapo baa?” alikuwa ni Mbunda.

    “Ndio, afande.”

    “Ok, nakuja.”

    Dakika chache baadaye walikuwa pamoja.

    “Enhe, inakuwaje?” Mbunda alimhoji.

    “Nina uhakika hajatoka,” Kitowela alijibu. “Tangu alipoingia sijabandua macho pale getini.”

    “Kwani hawezi kutumia mlango wa uwani? Gesti nyingi za huku uswazi huwa zina milango ya nyuma-nyuma.”

    “Siyo gesti hii.”

    “Una hakika?”

    “N’na hakika.”

    Ukimya wa muda mfupi ukatawala, kisha Mbunda akasema, “Niko kamili hapa nilipo. Sidhani kama tuna haja ya kuchelewa zaidi. Kuna kikosi cha askari kumi kimepaki pale Stereo. Tutakitumia itakapotulazimu. Twende.”

    Baada ya kuiacha hiyo baa tu, Mbunda akaingiza mkono mfukoni na kutoa bastola moja. Akampatia Kitowela, akimwambia, “Iko full. Akileta kujua ni kumlipua tu. Kifo cha jambazi mmoja ni nafuu kwa mamilioni ya Watanzania.”

    ****

    TANGU Fatma aliporudi kutoka benki, hakutoka chumbani mwake kwa kwenda umbali zaidi ya msalani. Alipohitaji maakuli ya mchana alimwagiza mhudumu. Hakupenda kutoka siyo tu kwa kuhofia kukamatwa na askari, bali ni kwa kuwa hakuwa na mazoea ya kutembeatembea.

    Magazeti mawili ya udaku aliyoyanunua mjini ndiyo yalikuwa mwenzi wake kwa mchana kutwa. Zaidi, fikra zake zilikuwa kwa yule kijana, dalali wa nyumba ambaye alimwahidi kuja saa 2 usiku kuzungumzia suala hilo na kupata mwafaka. Hatimaye aliamua kwenda bafuni kuoga kabla hajaagiza viazi mbatata kwa ajili ya mlo wa usiku. Akatwaa taulo lake na kutoka. Kama kawaida, umakini ulikuwa mkubwa; alifunga mlango kwa funguo kisha akaingia bafuni.

    *****

    Kukifahamu chumba cha mbaya wake, ilikuwa ni hatua kubwa sana kwa Kessy Mnyamani. Alijisikia kufarijika kwa kiasi kikubwa na kujipa matumaini ya kufanikisha malengo yake. Ni kwa matumaini hayo yaliyomjaa moyoni, hata hakuihisi njaa ingawa zaidi ya supu nzito aliyopata asubuhi, hakuwa ametia chochote tena tumboni hadi alasiri hii.

    Alichofanya baada ya Sauda kuondoka ni kupanga namna ya kumvaa Fatma huko chumbani. Alijenga imani moyoni kuwa Fatma lazima atakuwa na silaha, na kama watakutana ana kwa ana huko chumbani haitakuwa vigumu kwa Fatma kuitumia dhidi yake.

    Alipaswa kuwa makini. Akawa habanduki dirishani ambako aliweza kukiona chumba cha Fatma kwa usahihi. Zoezi hilo nalo lilikuwa gumu kiasi lakini alivumilia. Aliona amekwishamla ng’ombe mzima, vipi ashindwe kumalizia mkia?

    Ni katika zoezi lake hilo ndipo alipomwona Fatma akitoka chumbani, taulo mkononi akielekea maliwatoni. Dakika chache baadaye akamwona tena akirudi. Sasa akaamua kukamilisha azma ya safari yake hii.

    Bila ya kuzichomoa bastola zake ndani ya mifuko mipana ya suruali yake, alitoka chumbani mwake taratibu na kukifuata chumba cha Fatma. Hisia kuwa huenda Fatma akawa amejifungia kwa funguo zikamjia akilini lakini papohapo akajifariji kwa mbinu ambayo angeitumia katika kuingia chumbani humo; njia nyepesi tu. Angegonga mlango kama mhudumu anavyoweza kumgongea mpangaji yeyote wa gesti hiyo.

    “Nani?” huenda Fatma angehoji. Ni kawaida kwa mtu yeyote anapobishiwa hodi huuliza hivyo. Anauliza bila ya kuwa na uamuzi kama utambulisho wa huyo agongaye ndiyo utakaomfanya afungue mlango au asifungue. Mara nyingi imetokea kuwa agongaye akitaja jina lake, bila hata ya mwenyeji kumjua, atafungua mlango. Hivyo, kuuliza nani? umekuwa utamaduni uliokwishageuka sheria badala ya kawaida kwa baadhi ya watu.

    Bisha hodi kwenye nyumba ya kawaida, kwenye makazi ya kawaida kama hapo Kinondoni Moscow. Ukiulizwa hivyo wewe jibu kwa jina lolote la kubuni, mathalani Hamisi, ilhali jina lako halisi ni Zuberi. Cha kushangaza, badala ya aliye ndani kuhoji kwa kuhitaji ufafanuzi zaidi wa utambulisho wako, yeye atakimbilia kufungua mlango! Atakapofungua ndipo atakapokumbana na sura asiyoijua! Na si kwamba kulikuwa na mtu aitwaye Hamisi ambaye alikuwa akimfahamu, hapana, ni mazoea tu!CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kessy aliamini kuwa hata Fatma ataingia mkenge kwa mbinu hiyo. Kwa vyovyote lazima Fatma angelaghaika na kufungua. Kazi ambayo ingefuata ingekuwa nyepesi kuliko ilivyotarajiwa.

    Muda mfupi baadaye alikuwa akiutazama mlango wa chumba hicho. Kisha akashika kitasa na kukizungusha taratibu. Kitasa kikatii. Na kama alivyoufungua mlango huo taratibu, ndivyo pia alivyousukuma na kuingia kwa hatua za kunyata, mkono mmoja ukiwa mfukoni umeikamata bastola tayari kwa matumizi kama italazimu. Hatua zake hazikutofautiana na paka anayemnyatia panya. Akafanikiwa kupenya ndani na kuurudisha mlango taratibu bila ya mwenyeji wake kubaini.

    Akatulia tuli akimtazama Fatma aliyekuwa akijifuta maji kwa taulo huku akiwa mtupu, kama alivyozaliwa, kaelekea ukutani. Fatma hakujua kuwa kuna ugeni wa ghafla uliomfikia. Aliendelea kujifuta maji taratibu hadi aliporidhika na zoezi hilo. Hatua ya pili ilikuwa ni kutwaa mafuta ya kulainisha ngozi ambayo nayo alipaswa kujipaka mwili mzima. Hapo ndipo alipogeuka akitaka kulifuata begi alikohifadhi vifaa vyake vyote.

    Hakuyaamini macho yake! Moyo ukapiga paa! Taulo alilokuwa amelishika mkononi likadondoka sakafuni. Akakodoa macho kwa mchanganyiko wa mshangao mkali na woga wa wastani. Akatamani kupiga kelele lakini sauti ikamgomea. Koo likamkauka ghafla. Kisha, woga na mshangao vikayeyuka na badala yake hasira zikachukua nafasi hiyo. Zikaja kwa kiwango cha juu kiasi cha kumfanya atetemeke mwili mzima. Mbele yake alitazamana na mtu ambaye hakutarajia kumwona tena maishani mwake!

    Alihisi yu ndotoni!

    “Kessy!” alibwata huku akihema kwa nguvu.

    Ndiyo, alikuwa ni Kessy Mnyamani aliyekuwa mbele yake. Kessy ambaye sasa alisimama, mikono mifukoni akilitazama umbo zuri la msichana huyo, umbo lililozidi kuudhihirisha ubora wake kwa kipindi hicho alichokuwa mtupu kama alivyozaliwa. Alikiri kuwa katika usiku huo mchanga, zikiwa ni siku zaidi ya thelathini tangu walipoonana kwa mara ya mwisho, Fatma alikuwa amependeza maradufu. Alinenepa, alinawiri, akanang’anika, akiwa ni tofauti kabisa na wakati walipokuwa wakigaragazana chumbani enzi za uhusiano wao. Hata hivyo, cha ajabu hakuridhishwa wala kutamanishwa na mwili huo kwa wakati huo. Aliliona umbo hili zuri la Fatma likiwa halitofautiani na umbo la nyoka, tena yule nyoka mwenye sumu kali ya kuua kwa sekunde.

    “Kessy! Kessy!” kwa mara nyingine Fatma alibwata. “Kessy! Hujafa!? Yaani hujafa! Hapana. Wewe ni Kessy au mzimu wa Kessy?”







    Tabasamu la mbali lilichanua usoni pa Kessy, tabasamu lililomtoka huku nyuma yake kukiwa na kilo nyingi za hasira na chuki dhidi ya mrembo huyo. “Huu sio mzimu wa Kessy wala msukule wake,” hatimaye alisema, sauti yake nzito, yenye mkwaruzo wa mbali akihakikisha haiyafikii masikio yasiyohusika. “Hapana. Ni yuleyule Kessy unayemjua, Kessy uliyewahi kumvulia nguo mara kibaao! Sijafa! Mungu alitaka kuhakikisha ananikutanisha tena na wewe ili mkakati wetu ukamilike.”

    “Toka!” Fatma Mansour alifoka. “Kessy, nasema toka! Toka!”

    Tabasamu la Kessy lilizidi kuchanua, na wala hakuonyesha hata dalili ya kutishika kwa maneno ya Fatma. Aliendelea kusimama vilevile, tabasamu usoni, mikono mifukoni.



    “Kessy,” Fatma aliendelea kuwaka. “Nasema kwa mara ya mwisho, toka! Toka au n’takutoa roho!”

    Katika kudhihirisha kuwa asemayo siyo masikhara, papohapo alilifuata begi lake. Ndiyo, alikuwa mwepesi , lakini kama alikuwa akitarajia kutoa chochote katika begi hilo, haikuwa kama alivyotaka. Kwa wepesi usio wa kawaida, maradufu ya ule wepesi wa Fatma, Kessy alimwahi na kumminya mkono huo kabla haujatoka ndani ya begi hilo. Akaongeza nguvu ya uminyaji kwa dhamira ya kumtia maumivu.

    “N’achie! N’achie nakwambia!” Fatma alilalama kwa sauti kali. Alipotaka kufungua tena mdomo, Kessy hakumruhusu. Kono lake la kushoto lilimziba huku kono la kulia likitumika kumvuta hadi kitandani ambako alilazimika kuketi puu!

    “Sikia Fatma,” Kessy alinong’ona. “Sipendi kukuua. Na wala sikuja hapa kwa lengo hilo. Hapana. Mwenyewe unakijua kilichonileta. Ni pesa tu. Tena siyo pesa za kukuomba; ni ule mgawo wangu halali. Ni hilo tu!”

    Fatma alikuwa akihema kwa nguvu. Ule ujasiri wake sasa ulianza kumomonyoka taratibu. Hakuiamini kabisa hii kauli ya Kessy. Atamwamini vipi jambazi? Atamwamini vipi wakati anatambua fika kuwa aliyageuka makubaliano yao ghafla na kutoweka na fedha taslimu, shilingi milioni mia moja? Na hata kama angempatia huo mgawo wake, ni kipi kingemzuia Kessy asimshindilie risasi ya kichwa na kutokomea?

    “Umenielewa?” Kessy alimshtua. “Sina jingine lililonileta hapa! Ni pesa tu! Na wala siyo kwamba nataka ziada. Hapana. Nipe mgawo wangu na wa wenzangu. Milioni ishirini na tano tu. Siyo zaidi ya hizo.”

    Kwa kipindi kifupi ukimya ulitawala chumbani humo. Wakati huo Fatma alikuwa amepiga moyo konde na kuamua kupigania maslahi yake hadi dakika ya mwisho, ikibidi kufa, afe. Hivyo akawa akibuni mbinu ya kumzidi maarifa Kessy. Alitambua kuwa ujeuri wa aina yoyote hautamsaidia. Mbele yake alisimama mwanamume, pandikizi la mtu, ambaye kutoa roho ya mtu kwake ni aina fulani ya burudani. Utanashati wa mtu huyu ulificha kila ubaya alionao; ubakaji, uuaji, uporaji na kadhalika.

    Huenda katika mmoja wa mifuko iliyotapakaa katika mavazi yake kuna bastola, aliwaza. Ni kipi kingemzuia asimtie risasi kisha akapekua ndani ya begi lake na kujitwalia pesa? Hakutaka kujidanganya eti Kessy anaweza kuwa na moyo wa huruma ilhali amesota muda mrefu akijifichaficha, tena bila ya kuwa na pesa. Ana hasira, na hasira alizonazo hazitofautiani na za nyati aliyejeruhiwa. Yuko tayari kwa lolote!

    Tayari kuua.

    Tayari kufa.

    Kwa hali hiyo, Fatma aliamini kuwa busara inahitajika katika kuinusuru roho yake. Na alikuwa na mbinu moja tu iliyomjia kichwani wakati huo, mbinu ambayo aliamini kuwa ingekuwa ngao madhubuti na silaha bora zaidi. Moja tu!

    Mwili wake!

    Ndiyo, aliamini kuwa mwili wake ni ulimbo pekee uwezao kuwanasa ndege wajanja. Wakati huo bado alikuwa mtupu, hana hata kijipande cha nguo mwilini mwake, na alihitaji kuutumia mwonekano huo kama nyenzo madhubuti ya kumwokoa.

    “Sikia, Kessy,” alisema kwa upole. “Hakuna haja ya kugombana. Tusahau yaliyopita. Yaliyotokea, yameshatokea. Yamepita. Najua nilikukosea, tena nilikukosea sana. Lakini wewe ni mwanamume. Unapaswa kuwa na subira na kutafuta mwafaka au ufumbuzi wa tatizo lolote kwa umakini, bila kuchukua uamuzi kutokana na hasira.

    “Hapa ulipo una haki na kila sababu ya kuniua au kunifanya vyovyote upendavyo. Lakini sidhani kama utakuwa umechukua uamuzi wa busara kuniua. Nasema hivyo kwa sababu pesa zako ninazo. Siyo kwamba ni za kufuata benki, hapana. Ziko hapahapa. Nadhani utakuwa mstaarabu sana kama utachukua pesa zako na kuniachia roho yangu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ziko hapa?” Kessy alimuuliza huku kamkunjia uso.

    “Ndiyo. Zipo.”

    “Kiasi gani?”

    “Kwani tulikubaliana wewe na wenzako mchukue kiasi gani?”

    “Milioni ishirini na tano.”

    “Kwa hiyo ulitaka zaidi ya hizo?”

    Lilikuwa ni swali lenye kilo mia moja za dharau akilini mwa Kessy. Kwa kawaida yake, katika ukongwe wa kazi za ushenzi na ukatili usiomithilika dhidi ya mtu yeyote, hakuwa na muda wa kumsikiliza zaidi msichana huyu mdogo aliyeketi kitandani, mbele yake, akiwa mtupu kama alivyozaliwa. Angembaka kiroho mbaya, kisha akamzamishia risasi mbili usoni na nyingine mbili katika sehemu za siri.

    Asingetosheka, angetumia nyembe mpya kumchanjachanja mapaja yake manono, akamtia visu kadhaa kwenye matiti yake mazuri na kumalizia kwa kuutoa utumbo nje. Kingebaki kiwiliwili chenye sura ya kusikitisha mioyo ya majasiri na kutisha macho ya waoga.

    Ndiyo, angeweza kutenda ukatili huo wa aina yake, lakini, usiku huu, na siku hii, hakupenda kufanya hivyo. Kwa ujumla hakutaka kuwa na papara. Hatua aliyofikia ilikuwa ni muhimu sana, hivyo umakini ulipaswa kupewa kipaumbele sanjari na kuyatafakari matokeo ya lolote lile alilotarajia kulitekeleza.

    Ingawa swali hili la Fatma lilimkera sana, hata hivyo alijitahidi kwa nguvu zote kuidhibiti hasira iliyomnyemelea kwa kasi, na kwa unafiki akaachia tabasamu dhaifu kisha akasema, “Sizihitaji zaidi ya hizo. Ni hizo tu. Lakini,” kufikia hapo akasita. Sura yake ikabadilika tena. Mikunjo ikajiunda pajini. Akamtazama Fatma kwa macho makali zaidi. Kisha akaendelea, “Nataka kuziona, tena haraka sana. Nipe changu kwanza ndio mengine yatafuata.”

    “Kwani huniamini?”

    “Nipe!” Kessy aliwaka. “Sikuja hapa kuyaangalia mapaja yako wala…” akasita tena. “Ni kweli, kwa siku hizi chache umezidi kupendeza mpaka unanitamanisha. Lakini hilo sio lililonileta hapa. Ni la ziada tu. Elewa kuwa nimepata shida sana hadi kukupata. Nimetumia pesa nyingi huku nikilazimika kujifichaficha kwa wanoko wa ‘Mwema.’ Ulipomuua Matiko na ukaona mie na Morris tumepata ajali pale Faya, basi ukajua mzigo wote umebaki kwako. Utakula kiulainii kwa sababu hata bwanako tu’shamlipua. Nani wa kukughasi?

    “Hilo ndilo kosa ulilofanya,” aliendelea. “Nimepona. Nimepona Fatma. Sikufa, na wala usidhani kuwa unaongea na mzimu wangu. Ni mimi. Ni yuleyule Kessy uliyeongea naye kule Ada Estate kwa siku mbili ukipanga naye mkakati wa kumwibia bwana’ko mamilioni ya pesa, halafu siku ya siku, ile siku isiyosahaulika ukawazidi ujanja yeye na wenzake, ukatoweka na mamilioni yote ya pesa! Milioni mia moja, Fatma!

    “Ok, sitaki kupoteza muda. Nipe pesa zangu. Vinginevyo n’taondoka nikiacha roho yako pia imeondoka. Kwa hilo sina mzaha; nadhani unazielewa vizuri sera zangu. Bado sijabadilika.”

    Fatma aliutazama uso wa Kessy ulivyobadilika. Alitisha! Aliashiria kuua sekunde au dakika chache tu zijazo. Mwonekano huo ulimfanya Fatma ajenge hisia kuwa dakika zake za kuishi ziko ukingoni. Akaunda uso wa unyonge, macho yake yakabembeleza kabla mdomo haujatamka: “Tafadhali, Kessy, naomba uniamini. Pesa zako ninazo humuhumu ndani…”

    “Nazitaka!”

    Kimya cha sekunde chache kikatawala. Wakatazamana katika hali hiyo ya ukimya wa kuogofya. Fatma akajawa na ujasiri. Akahisi sauti ikimwambia, usihofu kitu. Uwe mjanja. Hatachukua pesa. Kishalegea, tumia ujanja ukiwa ni mwanamke mjanja. Si unamjua jinsi alivyo mgonjwa wa mapaja ya wanawake?Cheza naye.

    Ujasiri ukazidi kumjaa. Akasimama na kulitwaa begi lake lililohifadhi pesa, nguo pamoja na vikorokoro vingine. Ndani ya begi hilo kulikuwa na mkoba mweusi uliokuwa na zile pesa alizochukua benki asubuhi. Akautoa mkoba huo na kumkabidhi Kessy huku akisema, “Shika. Pesa zako ziko humo.”

    Mkono wa kulia wa Kessy ulikuwa mwepesi. Aliuchukua mkoba huo na kurudi nyuma hatua moja. Wakati huo alikuwa makini zaidi. Akawa akitupa macho katika begi sekunde ya kwanza na sekunde ya pili kwa Fatma. Kisha akatulia na kumkazia macho Fatma. Akampa onyo: “Nakuomba utulie hivyohivyo ulivyo. Ukijitia ujanja wowote, nakutoa roho. Itakuwa vizuri kama utanielewa.”

    Kufikia hapo akaichomoa bastola moja, akairusharusha kwa kono la kulia na kutia mkwara, “Unaiona hii? Ziko full ndani yake.”

    Fatma alibaki ametulia. Hakuihofia bastola hiyo kwani hata yeye alikuwanayo, ndani ya begi. Alichohitaji ni muda tu, muda wa kuzirejesha pesa hizo katika himaya yake.

    Kessy aliufungua mkoba ule na macho yakashuhudia mrundikano wa noti za Tanzania zikiwa zimefungwa na mipira maalumu. Hakutarajia kukumbana na hali hiyo! Kwa ujumla hakuwa akiyaamini maneno ya Fatma. Machoni mwake zilikuwa ni pesa nyingi, na hata kama hazikutimu shilingi milioni 25, hilo kwake halikuwa tatizo. Na hakuwa na nafasi ya kuzihesabu.

    Akacheka kidogo, hiki kikiwa ni kicheko halisi kutoka moyoni, akifurahia kufanikisha malengo yake. Sasa akajisikia kuwa na utulivu moyoni. Akairejesha bastola mfukoni na kuutua mkoba sakafuni. Akamrudia Fatma.

    “Ok, sasa nimekuelewa,” alisema huku akimsogelea. “Lakini bado. Bado kidogo. Ni muhimu kuagana. Tuagane vizuri, kistaarabu, tukikumbushia.” Akaachia tabasamu kubwa, macho yake ya kikatili yakitalii katika umbo tupu la Fatma, uchu wa ngono ukijidhihirisha katika mboni za macho hayo.

    Kama kuna kauli ambayo Fatma aliihitaji na kuisubiri kwa hamu kubwa, basi ni hii aliyoambiwa punde. …Tuagane vizuri, kistaarabu, tukikumbushia ni maneno yaliyojirudia kichwani mwake mara mia kwa sekunde zisizozidi tano. Yalikuwa ni maneno yenye uzito wa kilo nyingi na thamani kubwa, zaidi ya pesa zilizokuwa mkobani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akamshukuru Mungu kimoyomoyo bila ya kujua shukrani hizo amezilenga juu ya nini. Kisha kwa sauti akasema, “Sina tatizo lolote, Kessy. Mimi na wewe hakuna aliye mgeni kwa mwenzake. Lakini, tafadhali tu uniachie roho yangu.”

    “Sasa kila kitu ni shwari, bibie,” Kessy alisema huku akianza kuchojoa nguo zake. Akaongeza, “ Kwa kweli umezidi kupendeza, Fatma. Yaani kwa leo hata mtu akinipa Benz ili nikuue, nitamwua yeye kwanza kisha Benz lake nakuletea.”

    Fatma hakusema kitu bali aliachia tabasamu la mbali huku akipandisha miguu kitandani, macho yake yaliyolegea kisanii yakimtazama sawia Kessy kiasi cha kumwongezea papara ya kuzichojoa nguo zake.



    Muda mfupi baadaye, nguo za Kessy zikiwa sakafuni, viumbe hao wawili walikuwa katika zoezi jingine, mwanamume akiwa katika sterehe halisi ilhali mwanamke akiigiza kustarehe ilhali moyoni hakuwa hata na chembe ya burudani. Lakini Fatma akitambua fika kuwa kwake, hii ndiyo ilikuwa karata ya mwisho, hakutaka kufanya kosa. Aliupa unafiki kipaumbele, akijituma vilivyo katika shughuli hiyo na kufanya ziada ya yale aliyoyajua katika nyanja hiyo. Na hakuwa na soni ya kutoa pendekezo:

    “Tufanye hivi…”

    “Sasa tubadili…”

    “Fanya hivi…







    Kachero Mbunda na Sajini Kitowela walifikia kwenye ofisi ya mapokezi ambako walimkuta msichana mmoja mrembo akijitazama kwenye kioo kidogo huku akitabasamu peke yake. “Kama ni uzuri, tayari unao,” Mbunda alimwambia huku akimgusa begani.

    Binti yule alishtuka, akanyanyua uso na kuachia tabasamu dhaifu. “Karibuni,” hatimaye aliwaambia huku akiwageukia na kuwatazama kwa zamu. Huenda alitegemea kuwa kapata wateja.

    “Asante, mrembo,” Mbunda aliitika. “Samahani, tumekuja kumwona jamaa yetu.”

    “Jina lake?”

    Mbunda alifikiri kidogo kisha akajibu, “Khalfan. Khalfan Suleiman.”

    “Khalfan,” mhudumu yule alilitamka jina hilo kwa sauti ya chini zaidi huku akionekana kufikiri. Kisha akamtazama tena Mbunda na kuuliza, “Ni mpangaji hapa?”

    “Yeah. Ni mpangaji.”

    “Tangu lini?”

    Lilikuwa ni swali gumu kwa Mbunda na mwenzake, Kitowela. Kwanza jina wamelibuni, na bado wanapachikwa swali jingine. Askari hao wakatazamana kwa sekunde chache kisha Kitowela akatoa kitambulisho na kumwonyesha mhudumu huyo.“Tuko kazini,” alimwambia. “Kuanzia sasa unatakiwa kufanya kila tutakalokuamuru.”

    Msichana yule aligwaya. Akawatazama askari hao huku akihemea juu-juu.

    “Ok, tupe leja ya wageni wako,” Mbunda alimwamuru.

    Msichana huyo alifanya alivyoamuriwa. Wakati Mbunda akifunua ukurasa wa kwanza wa leja hiyo, mara Kitowela akamwuliza msichana huyo, “Kwa rekodi zako za haraka haraka zilizoko kichwani, una mpangaji yeyote ambaye yuko hapa kwa zaidi ya mwezi mmoja au chini kidogo ya hapo?”

    Msichana alifikiri kidogo kisha akajibu, “Hapana. Wapangaji wetu hawachukui zaidi ya siku mbili, tatu. Sana, mpangaji akiingia leo, kesho asubuhi anatoka.”

    “Kwa siku huwa unapokea wapangaji wangapi kwa wastani?” Mbunda naye alirusha swali.

    “Hata kumi.”

    Mbunda na Kitowela walitazamana. “Nadhani tuwaite,” Mbunda alimwambia Kitowela akimaanisha kukiita kikosi cha askari kilichokuwa kimebaki kando ya jengo la Stereo Club.

    Akaitwaa simu yake na kuwasiliana na mmoja wa askari hao. Na haikutimu hata dakika moja askari hao waliovaa sare walikuwa nje ya gesti hiyo. “Kuna operesheni ya chumba hadi chumba,” aliwaambia. “Hakikisheni hakuna anayeingia wala kutoka. Mimi na Kitowela tutazunguka vyumbani.”

    Mara akamgeukia yule mhudumu na kumwambia, “Utatusamehe, bibie. Tutatembelea vyumba, kimoja baada ya kingine. Wewe utakuwa pamoja nasi.”

    Zoezi hilo lilianza wakati huohuo. Gesti hiyo ilikuwa na vyumba kumi na vitano lakini vingi havikuwa na watu. Chumba kimoja walimkuta mwanamke mmoja aliyekuwa kalewa chakari, na hawakupata shida kutambua kuwa ni fuska wa kutupwa kwani mara tu alipowaona alianza kubwata, “Njooni. Nawaweza nyote wawili… tutakeshaa… pesa yenu tu…na leo natoa punguzo la teni pasenti… vyovyote mnavyotaka nitawaridhisha… hapa mmefika… mi’ nd’o Salma-kiuno, mkisikia mwingine basi ni fotokopi…” Wakati akijinadi hivyo tayari alishaitupa kanga pembeni na kubaki mtupu kama alivyozaliwa. Mbunda alimtazama Kitowela.

    Wakacheka.

    “Ama kweli Kinondoni inatisha!” Kitowela alisema huku wakimwacha mwanamke huyo na kukifuata chumba kingine.

    Vyumba vingine vitatu walivyovipitia ama walikuta wapangaji wametoka ama havijapangishwa. Ni wakati wamekifikia chumba fulani, walishtuka na kutulia. Ndani ya chumba hicho kulisikika maongezi yasiyokuwa hata na chembe ya amani. Isitoshe, jina moja lilitajwa kwa sauti ya juu na mmoja wa hao waliokuwa ndani kiasi cha kuyafikia masikio ya askari hawa sawia. Kutajwa kwa jina hilo kuliwafanya wajikute wakitazamana huku mikono yao ikiwa imekwishazama kwenye mifuko ya suruali zao na kuzishika bastola tayari kwa matumizi.



    *****



    Fatma aliamua kumwadhibu Kessy kwa namna ya kipekee. Alimdhihirishia kuwa yeye ni mwanamke aliyefundwa, akafundika. Ni mwanamke anayeweza kumfanya mwanamume mwenye ndoa amtaliki mkewe. Na, ni mwanamke aliyepanda chati kivitendo katika nyanja ya ngono tofauti na enzi zile kabla hawajaachana na kuchukuliwa na Beka Bagambi.

    Ilikuwa ni patashika tupu chumbani humo. Kessy ‘aliwehuka’, akili yote ikahamia kwenye starehe hiyo. Kwa ujumla alimwona Fatma kama mwanamke mpya, mwenye shahada ya juu katika nyanja ya mapenzi kivitendo.

    Ndiyo, Kessy ambaye baada ya kuoneshwa lile bulungutu la pesa sasa alikuwa timamu kisaikolojia, alitaka Fatma aendelee kufanya kila anachomfanyia mwilini mwake, na kutia ziada ya hayo anayoendelea kumtendea.

    Hilo halikuwa jambo zito kwa mwanamke aina ya Fatma, mwanamke ambaye hakumbuki idadi ya wanaume waliokwishapenya katikati ya miguu yake wakati alipokuwa akijinadi barabarani na kwenye klabu za usiku. Alishafanya mengi, na alifanya na wengi, baadhi ya hayo yakiwa ni yale yanayodaiwa kuwa hufanywa na magwiji wa starehe ya ngono pekee.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa, usiku huu anamfanyia huyu mpenzie wa zamani kiasi cha kuiparaganyisha akili yake kwa kiwango kisichokadirika. Hakushangaa pale alipomsikia Kessy akibwabwaja mithili ya mlokole aliyejazwa roho mtakatifu na kuanza ‘kunena kwa lugha.’ Ndiyo, hakushangaa, alijua kuwa hayo yalikuwa ni matokeo ya kiuno chake; mwanamume rijali anapomwaga chozi kifuani pake!

    Katikati ya starehe hiyo ndipo Fatma alipoona kuwa muda aliokuwa akiuhitaji uliwadia. Ilitokea kama aina fulani ya tamthilia ya kusisimua. Kwa nguvu za ajabu alimsukuma kando Kessy na papohapo akajitoa kitandani haraka na kulivaa begi lake ambalo kwa kuwa halikuwa limefungwa, hakupata shida kuupenyeza mkono na kuichomoa bastola yake.

    Sasa hakuwa yule Fatma Mansour aliyekuwa akinong’ona kimahaba huku akivishughulisha viungo vyake kwa namna ya kunogewa na starehe ya ngono muda mfupi uliopita. La. Huyu alikuwa Fatma mwingine, Fatma mwenye sura iliyojaa ukatili na aliyeonyesha bayana kutokuwa hata na chembe ya mzaha wala urafiki tena na Kessy. Alisimama kando ya kitanda, uchi vilevile kama alivyozaliwa, akiwa ameishikilia bastola kwa mkono wa kulia na kumwelekezea Kessy, ambaye kwa kipindi hicho alilichukulia tukio hilo mithili ya ruya ipaayo hewani usiku.

    “Nakusikitikia sana Kessy,” ilikuwa ni sauti ileile nyororo, ya kimahaba, lakini safari hii ikitofautiana kabisa na uso wake uliotisha na kuashiria kuua dakika yoyote. Akaendelea, “Unapaswa kujilaumu kwa kunifuata mpaka huku. Nakupa pole kwa usumbufu ulioupata kwa kunisaka, na, nadhani kila ulichokitaka mwilini mwangu leo nimekupatia. Lakini hizo pesa ulizotaka kuchukua ni kidogo sana. Zitakwisha mapema na utakamatwa na polisi ambao kwa vyovyote watakuwa wanakusaka hadi leo hii.

    “Kwa hiyo Kessy ili usipate taabu, hutaondoka humu na roho yako. Kwa hilo sina mzaha. Beka wangu ameshakufa, sitaona ajabu kuitoa roho ya kinyangarika kama wewe! Ukithubutu kuleta ujanja wa aina yoyote unaotumia kwa ujambazi wako, kwangu umeumia. Sikufichi, utaharakisha kifo chako!”

    Kessy alilala chali pale kitandani akionyesha kuishiwa nguvu kimwili na kiakili. Jasho lilimtoka chepechepe, akamtazama Fatma bila ya kupepesa!

    Fatma hakutaka kuchelewa, alishaona mdudu mbaya kaingia. Akavaa nguo zake harakaharaka na kujiweka tayari kwa kuondoka. Na katika kuyaweka mambo sawa, alidhamiria kumzamishia risasi Kessy ili asipate tena bughudha maishani mwake. Kama Matiko Kidilu alishatangulia, hali kadhalika Morris Maguru, huyu Kessy atakapowafuata huko kuzimu, ni nani tena atakayeleta usumbufu? Jibu lilikuwa ni moja tu; hakuna.

    Ambako angekwenda baada ya kumuua Kessy hilo lilikuwa ni jambo jingine. Kwanza ni kutoka hapo Kongo Guest House ambako hakupatofautisha na makazi ya wafu kwa siku hii. Kitendo cha Kessy kumfuma hapo ndicho kilichomfanya apachukulie hivyo.



    Wakati alipounyoosha mkono akimlenga kifuani Kessy kwa bastola yake, hakubaini kuwa mlango wa chumba chake ulikuwa ukifunguka taratibu na mkono mwingine wenye bastola ulikipenyeza kisha risasi kufyatuka na kuzua kishindo kikubwa chumbani humo.



    *****

    Yowe kubwa lilimtoka Fatma Mansour. Maumivu makali yakampata katika kiganja cha mkono wa kulia kilichoanza kububujikwa damu. Bastola yake ilianguka sakafuni. Alipotupa macho mlangoni, akakutana na bastola mbili zilizoshikwa na Kitowela pamoja na Mbunda ambao walikivamia chumba hicho ghafla wakifuatiwa na askari wengine wawili.

    “Watie pingu!” Mbunda alimwamuru mmoja wa askari wale.

    Watu wakaanza kukusanyika ndani na nje ya gesti hiyo. Wafanyakazi wa gesti nao walifuatilia kwa ukaribu zaidi.

    “Hivi kumbe huyu anti ni jambazi!” mmoja wao alisema kwa mshangao.

    “Ni wabwia unga,” mwingine aliropoka.

    “Wewe! Siku hizi kuna majambazi hata wa kike!” wa tatu alibwata.

    Mara Land Rover iliwasili na kuegeshwa nje ya gesti hiyo. Mrembo Fatma Mansour na jambazi hatari, Kessy Mnyamani walishurutishwa kupanda ndani ya gari hilo huku wakiwa chini ya ulinzi mkali. Safari ya kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi ilipoanza, Kessy Mnyamani na Fatma Mansour walitazamana, ndoto za neema maishani zikiota mbawa nafsini mwao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog