Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

HIGH SCHOOL - 1

 





    IMEANDIKWA NA : JENIPHER ALPHONCE



    *********************************************************************************



    Simulizi : High School

    Sehemu Ya Kwanza (1)







    Jina langu ninaitwa Catherine Kindamba,



    Ilikua ni siku ya jumanne nilipowasili shuleni Hans pope Academy mkoani Mwanza kutoka Dar es salaam. Nilimaliza kidato cha nne katika shule ya secondary Canossa na kupata division one na kisha kuchaguliwa kujiunga katika shule ya secondary Kibasila kwa mchepuo wa ECA, yani Economics, commerce na Accountancy.



    Baba yangu hakuyapenda kabisa mazingira ya pale Kibasila, hivyo aliamua kuniamishia Hans pope Academy Mwanza. Ni kiasi kama mwenzi wa pili niliamia shuleni hapo. Mimi ni msichana mpole na mwenye ushirikiano na wenzangu. Ninapenda dini na kulelewa kimaadili. Marafiki wawili tu Winnie na Angel walitosha kuifanya jamii yangu ndogo. Daima sikupenda company ya wavulana kwakuwa sikupenda vile baba alivyokuwa akimfanyia mama, hali iliyopelekea kuwepo kwa migogoro isiyoisha pale nyumbani. Pamoja na hayo yote baba yangu ambaye alikuwa mhasibu wa pale bandarini pamoja na mama yangu ambaye alikuwa mwalimu wa shule ya msingi ya Academy International school niliyosoma hapo awali walinipenda sana nikiwa kama mzaliwa wa pekee.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mazingira ya shule mpya ya Hans pope Academy yalikuwa mazuri niliyapenda. Ilifika jioni saa moja nikaingia chumba nilichopangiwa katika jengo lililoitwa white house nikalala fofofo. Saa kumi na mbili kamili ya alfajiri nilishtushwa na mlio wa kengele, nilishuka dekani kwangu na hapo ndipo niligundua kuwa sikuwa peke yangu. Kilikuwa ni chumba kidogo kizuri kilichopangiliwa vizuri, cha watu wawili. Kulikuwa na makabati mawili makubwa yaliyojigawa ukutani, meza ya kusomea na madirisha mapana ambayo yaliweza kuingiza mwanga na hewa safi.



    Katika kitanda cha chini alikuwepo msichana ambaye pamoja na kuwa alikuwa bado usingizini haikuniwia vigumu kujuwa kuwa huyu kiumbe aliyeko mbele



    yangu ni mzuri na mrembo wa kutosha kutwaa taji la miss Dunia. Ninajiamini kuwa mimi ni mzuri huyu msichana hakika alikuwa shani mbele ya macho yangu. Nilimsanifu kuanzia sura yake zuri, lips zake ambazo kwa juu zilichora kama umbo la kopa, rangi yake nyeupe ya kung’aa, ngozi yake laini, shape yake, hakika huyu msichana alikuwa ni mzuri sana. Nilimuangalia hadi macho yangu yalipotosheka kisha nikasimama tu nisijue nini cha kufanya nikageuka kwenda sehemu ambayo niliweka mabegi yangu.



    “wewe ni nani” sauti tamu ilipenya katika masikio yangu.



    Niligeuka kwa mshituko na kutazama pale sauti ilipotokea. Yule mrembo wa dunia alikuwa bado amelaa alikuwa akiniangalia macho yake makubwa na matamu yalitosha kunihakikishia kuwa huyu msichana aliumbwa kwa utulivu zaidi.



    “aaaaah aaaaa mimii” nilishikwa na kigugumizi sikujua nimjibu nini kile kitu kilinichanganya.



    “naitwa Catherine Catherine Kindamba” hatimaye niliweza kuongea na kujitambulisha.



    “Catherine unafanya nini hapa” aliongea huku akinyanyuka kutoka kitandani.



    “mimi ni mgeni nimefika hapa jana usiku, nimehamia” niliongea



    “mmmh” alinitazama kwa Dharau huku akibetua midomo yake.



    “Catherine karibu”



    “Ahsante” nilijibu



    “Sasa umeamka saizi unaenda wapi” aliniuliza.



    “aaaaah nimesikia kengele nataka nijue ni nini kinaendelea”



    “oooh sasa hivi ni mda wa jogging kama unapenda nenda ila sio lazima sana unaweza kubaki hapo ukijiandaa kwa ajili ya kuingia darasani, mi pia nipo siendi jogging.”



    “Aaaaah sawa hata mimi pia sipendelei jogging acha nipange vitu vyangu” niliongea.



    “ooooh unsoma Combination gani?” aliniuliza



    “niko ECA” nilijibu



    “ooooh”



    “wewe je unaitwa nani” nilimuuliza



    “naitwa Candy, niko HGE na ukipenda unaweza kuniita Queen Candy” alisema.



    Hakika nilijua kwamba huyu msichana aliyekuwa mbele yangu ni mtu mwenye Dharau sana hata hivyo sikuwa na papara dharau zake hazikuwa kitu kwangu lakini katika siku hizo za mwanzo ilikuwa ni hali ya kawaida tu kwakuwa nilihitaji kuijua shule vizuri sikumtilia maanani sana.



    Nilifanikiwa kupanga vitu vyangu katika mpangilio uliopendeza mbele za macho yangu baada ya hapo nilijiandaa kwa ajili ya ratiba za siku hiyo. Uniform mpya zilinipendeza hakika, sketi yangu fupi nyeusi iliyochanua vyema, shati langu jeupe la mikono mirefu, tai ya pundamilia, soksi ndefu zilizonifika magotini na viatu nilipendeza sana.



    Muda ulipokaribia mimi na Candy tuliongozana hadi mstarini na baada ya matangazo machache tuliruhusiwa kuingia madarasani. Candy aliniongoza mpaka kwenye darasa letu.



    Ili ndilo darasa lako aliongea kwa dharau na kisha akaondoka kwa hatua za mikogo, nilibaki nikimtazama mpaka alipopotelea. Hakika Candy ni msichana mzuri niliwaza.



    Dakika moja ya kumshangaa Candy ilipoisha niliamua kuingia darasani na wakati huo wakati naingia darasani nilijigonga kwenye paji la uso mlangoni. Nilihisi maumivu makali.



    Madaftari mawili ambayo hayakutosha kwenye kibegi changu cha mgongoni yalidondoka. Nilichutama ili kuyaokota na hapo nilijigonga tena na safari hii sio kwenye mlango tena bali ni mtu alikuwa amenigonga, nilikasirika sana. Nikageuka kwa ghadhabu ili nimuone ni nani ambaye amenigonga nilikutana na sura nzuri ya kiume iliyopambwa na tabasamu laini, hakika sikuwahi kukutana nalo katika maisha yangu yaliyopita.



    “Sorry” alisema kwa sauti tamu.



    “Aaaanh usijali nilikua nakusaidia kuokota madaftari yako lakini kwa bahati mbaya nikakugonga samahani kwa hilo.”



    “usijali na asante sana” nilisema.



    Aliniokotea madaftari yangu na kisha akanikabidhi, “wewe ni mgeni mahali hapa sijawahi kukuona.”



    “Ndio nimehamia jana”



    “Karibu sana”



    “Asante” nilisema.



    “Unasoma combination gani?”



    “Niko ECA”



    “Wooow karibu kwenye darasa letu”



    “Asante”



    “Naitwa Martin, sijui wewe unaitwa nani?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naitwa Catherine.”



    “Catherine karibu sana.”



    “Asante.”



    Alinishika mkono na kuniongoza darasani, alisimama mbele ya darasa na kuongea kwa sauti nzuri ya kiume.



    “Hello class huyu ni mwanafunzi mpya atajitambulisha anahitaji ushirikiano wenu.” Akaniachia nafasi nijitambulishe mbele ya darasa.



    Nikasema kwa uwoga hali nimeshikwa na aibu za kike.



    “Hello class naitwa Catherine nimetokea Kibasila” nilishindwa kuendelea, watu walicheka na kisha wakanikaribisha. Nilioneshwa sehemu ya kukaa pembeni



    yangu aliketi msichana mzuri alinisalimia “hello naitwa Martha karibu sana.” Nilitabasamu na kisha nikamwambia asante.



    Ghafla mwalimu aliingia akiwa mwenye ghadhabu, tulisimama kumsalimia.



    Hakujibu salamu yetu alianza kufoka “kama hujafanya assignment simama hivyohivyo na kama umefanya kaa chini.”



    Nilijikuta nimesimama peke yangu.



    “All eyes on me.” Nilihisi nimejisemea mwenyewe lakini kumbe niliongea kwa sauti darasa zima wakacheka, nikatoa macho hali nimeachia mdomo.



    Mwalimu aliniuliza “je wewe ndio ambaye ujafanya kazi yangu ni kitu gani kimekufanya usifanye assignment?”



    Nilishikwa na kigugumizi, “Eeeeh aaanh mimi ni mgeni”



    “ahaaa” alisema mwalimu yule ambaye baadae nilikuja kumtambua kama Mr.



    Maloya.



    “Kaa chini” nikakaa.



    Alianza kufundisha huku akitumia muda wake mwingi kunitazama, sikujua kwa sababu ya ugeni wangu au vipi.



    Tuliendelea na vipindi mpaka wakati wa mapumziko ulipofika. Darasa zima waliondoka.



    Nilibaki peke yangu nisijue wapi pa kuelekea. Na wakati nimeinama nikifuta viatu vyangu nilisikia nimeguswa begani kwangu.



    Kwa kuwa sikuwa nimemzoea mtu yeyote nilijua lazima ni Candy ambaye amenipitia kwa ajili ya mapumziko.



    “Candy” niliita huku nikigeuka, hakuwa Candy nilikutana na sura nzuri ya kiume.



    “Martin hapa”



    niliachia tabasamu.



    “oooh Martin” nilishindwa kuendelea.



    “Mbona uko hapa peke yako?” aliuliza.



    “Sijui nielekee wapi” nikasema.



    “Aaanh ngoja twende restaurant” nikanyanyuka tukaongozana.



    Tulipofika niliagiza maziwa na slace tatu za mkate.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unayaonaje mazingira ya shule yetu” aliuliza.



    Kabla sijamjibu msichana ambaye alikuwa mmoja kati ya wanafunzi alifika mezani kwetu.



    “Wewe ndio Catherine si ndio?” aliuliza.



    “Ndio” nilimjibu



    “Academic master kasema upeleke barua zako za uhamisho ofisin kwake sasa hivi.” Alisema.



    “Asante kwa taarifa” nilijibu.



    Nilinyanyuka haraka bila kuaga na kuelekea yalipo mabweni yetu. Nilipofungua nilishangaa kumkuta Candy amelala usingizi, nikashangaa wakati wa mapumziko Candy amelala kwa uchovu gani?



    Sikumtilia sana maanani kwa vile nilikuwa mgeni, nikachukua barua zangu na kuzipeleka panapohusika na kisha kurejea darasani. Masomo ya siku hiyo yaliendelea kama kawaida. Muda wa vipindi ulipoisha nilirejea bwenini na wakati huo Candy ndio alikuwa akiamka, tulipata chakula cha mchana na kisha kwenda kwenye michezo. Wakati wa jioni ulipofika tuliingia kwenye kusali. Nilikaribishwa vizuri sana nilijihisi ni mmoja kati yao. Nilipata faraja mno kwa vile nilikuwa nikikubalika kila sehemu. Maisha ya shule yaliendelea vizuri.



    Niliyazoea mazingira ya shule mpya, ilikuwa ni shule ya kifahari ambayo haikuwa rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kumsomesha mtoto wake. Ufaulu wangu pia ulikuwa juu. Mwalimu Maloya ambaye alikuwa ni mwalimu wa mazingira alikuwa akifatilia maendeleo yangu kwa ukaribu zaidi, mara zote nilipokosea aliniita ofisini kwake na kunionya. Na wakati nilipofanya vizuri hakusita kunisifia mbele ya watu, nilimpenda kwakuwa alijali maendeleo yangu.



    Candy aliendelea na tabia yake ya kulala kila mara, mara nyingi nilimkuta amelala wakati wa vipindi, nilijua ndio aina yake ya maisha aliyokuwa akiishi tangu alipofika shuleni kwani pamoja na tabia yake ya kulala kupitiliza Candy alikuwa vizuri kimasomo, kitaaluma alikuwa juu na alikuwa akiwaongoza wenzie darasani. Dharau za Candy zilizidi maradufu sikujali kabisa.



    Urafiki wangu na Martin ulizidi kadri siku zilivyozidi kwenda, alikuwa ni mvulana mwenye kujali, mpole na mwenye haiba nzuri. Mwanzoni sikupenda kampani ya wavulana, lakini kutokana na haiba yake niliweza kumzoea na tulishirikiana kwenye masomo na kuweka ushindani baina yetu. Nilikuja kugundua martin ni raisi (kiranja mkuu wa shule) na pia alikuwa ni kiongozi wa kwaya kwenye jumuiya yetu kanisani. Alipenda kuimba na alikuwa na sauti nzuri sana.



    Pia nilikuja kujua kuwa Candy alikuwa ni kiongozi wa mazingira. Candy alianza tabia ya kujiandaa alfajiri mapema kabla sijaamka kila nilipoamka nilikuta tayari ameshamaliza na wakati mwingine alishaondoka. Hakuwa na nafasi katika akili yangu hivyo nilimpotezea.



    Ilikuwa ni siku ya ijumaa siku niliyowahi kuamka tofauti na kawaida nilimshuhudia candy akivaa mkanda wa kupunguza tumbo nilijiuliza maswali bila majibu mkanda wa nini na hakuwa na tumbo. Huku nikijifanya nimelala niliendelea kumtazama wakati akivaa.



    “Ili tumbo mwishowe litaniumbua, looh!” alijiongelesha mwenyewe.



    “Leo lazima huyu kidudu mtu anipe mustakabali wangu kabla mambo hayajawa mabaya”, aliongea.



    Nilichelewa kugundua kuwa candy ni mjamzito. aliendelea kujiandaa na kisha alijongea kabatini kwake. Alipofika kwenye meza ya kujisomea mahali nilipoweka daftari zangu na vitu vyangu alisita, alichomoa kitambaa ambacho hata kwangu kilionekana kipya sikuwa nimewahi kuwa na kitambaa cha namna hiyo nilijiuliza kimetoka wapi na cha nani na kimefikaje kwangu, bila majibu. Candy alikitazama, akasonya na kisha akakirudisha kilipokuwa na kisha akaliendea kabati lake.



    “Candy” sauti ilipenya kwenye masikio yangu, alikuwa ni msichana mwingine ambaye nilizoea kumwona pale shuleni ambaye alikuwa akiitwa Naima alipenda kujiita Nana.



    “Niambie best yangu” Candy alijibu,



    “meseji yako nimeiona leo asubuhi nikaona nije sasa hivi kabla ya kuingia darasani” alisema Naima.



    “Ndio hivyo shoga yangu” Candy alijibu.



    “sasa itakuwaje?” Naima aliuliza,



    “Nataka nimfate maloya anipeleke nikaitoe kwa maana imeshafikisha miezi miwili, mwisho wake tumbo litakuwa kubwa itajulikana hali itakuwa mbaya zaidi.”



    Kijasho chembamba kilinitiririka kumbe Candy ana uhusiano na Maloya uhusiano uliozaa mimba na sasa wanampango wa kuitoa hiyo mimba, duuh! Nilichoka.



    Waliendele na maongezi yao hadi walipofikia muafaka kuwa candy aende kwa Maloya ampeleke kuitoa hiyo mimba.



    “Huyu kiazi ajasikia kweli?” aliongea Naima kwa dharau



    “mmmh, linalala kama ling’ombe” Candy alijibu kwa nyodo wakacheka na kisha wakatoka.



    Niliendelea kuwaza pale kitandani candy kwanini umefanya hivyo jamani we ni msichana mzuri kwanini unajiaribia uzuri wako niliwaza. Ni kweli Maloya alikuwa kijana tena mzuri alikuwa ni mwalimu mzuri sana na zaidi ya yote alikuwa na haiba nzuri, lakini Candy ni kwanini ukaingilia mambo haya wakati sio wako. Ona sasa umepata ujauzito na sasa unataka kuhatarisha maisha yako kwa kutoa huo ujauzito. Niliendelea kuwaza pasipokuwa na majibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuja kushituka wakati umeshaenda na nilikuwa nimeshachelewa sana niliamka na kujiandaa kwa haraka na kukimbilia darasani muda wote nilionekana mtu mwenye mawazo sana, Martha aliligundua hilo na Martin pia, kila mmoja aliniuliza kwa wakati wake. Nilimjibu Martha sina tatizo.



    “Martin ninaomba mda niongee na wewe” nilimwambia Martin



    “aaanh sawa tutaongea wakati wa mapumziko” alinijibu kwa sauti yake nzuri.



    Kiukweli nilishindwa kuvumilia kuyabeba mambo ambayo niliyasikia asubuhi ya siku hiyo niliona ni vema kumshirikisha Martin kwa sababu nilikuwa nikimuamini na alikuwa rafiki yangu wa karibu sana. Wakati wa mapumziko hatukwenda kula tulibakia darasani.



    “Martin”



    “nakusikiliza bibie” Martin alijibu.



    “Unafahamu kwamba naishi na Candy chumba kimoja?”



    “ndiyo najua” alisema.



    “Kiukweli nimejua kitu ambacho binafsi kimenichanganya sana na nimeshindwa kuvumilia kukaa nacho nimeona bora nikushirikishe”



    “niambie kitu gani hiko?” alisema Martin.



    “Candy ni mjamzito” Martin alishituka isivyo kawaida tofauti na nilivyo tegemea.



    “Say whaaat!?” alisema kwa ghadhabu



    “Martin candy ni mjamzito.”



    “Huweza kuwa serious Catherine, kwanini unaongea utani?” aliniuliza.



    “Hapana sio utani nina uhakika na hilo.”



    Alishindwa kuendelea alibakia akitweta huku jasho jembamba likimtiririka.



    “Na ana mpango wa kuitoa” niliendelea,



    hakujibu aliendelea kujiinamia pale chini.



    “Kibaya zaidi” niliendelea,



    “ujauzito huo ni wa mwalimu maloya.”



    Martin aligeuka na kunitazama kwa jicho kali “unaongea nini wewe?”



    “Martin huamini ninachokuambia?” niliongeza.



    “Katika siku ambayo umewahi kunichanganya leo ni siku ya kwanza sitaki kukwamini Catherine sitaki kabisa” alisema Martin kwa sauti ya kukata tamaa.



    “Martin nina uhakika na ninacho kiongea.”



    “Kumbe ndo mana candy amebadilika sana siku hizi aonekani darasani hataki tena kuja kuniona naa…..”



    Ni kama alishitushwa na akaishia hapo, “ok sawa nitalifanyia kazi kwaheri Catherine.”



    Aliondoka Martin mbele yangu, nilitamani kumwita lakini nilishindwa nilijua kutokana na yeye kuwa ni raisi wa shule lazima ingemchanganya lakini sio kwa kiwango kama hicho.



    Ana nini huyu Candy anamhusu vipi? Nilijiuliza maswali bila majibu.



    Mwisho wa yote niliendelea kukaa darasani kwa ajili ya vipindi Martin hakurudi tena, vipindi vilipoisha nilirejea bwenini kwetu. Nilipoingia chumbani kwangu nilimkuta Naima na Candy wamesimama kana kwamba wanamsubiri mtu kisharishari nilisita nikaingia na kisha nikawasalimia mambo zenu, hawakunijibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilishangaa kwani kuna tatizo lolote niliuliza hawakunijibu baada ya kukosa majibu niliamua kuendelea na mambo yangu, nikasogea mezani kwangu kwa ajili ya kuweka madaftari yangu, candy alinisukuma.



    “Wewe ndiyo unaejifanya mzuuuuri kuliko wote hapa shuleni kiasi cha kuchukua wanaume za watu unajiamini nini na kwa uzuri gani unanitafta nini wewe kidudu mtu, eeenh” aliongea Candy kwa hasira zenye mchanganyiko wa jazba, nilishindwa kumwelewa nilibaki nimetoa macho huku nimeachama mdomo.



    “Candy sielewi unaongea nini?” nilisema.



    “Uelewi naongea nini?” Candy aliongea huku amenibania pua.



    “Mpumbavu sana we msichana umefika hapa shuleni unaanza kujiona wewe ni mzuri umeshazoea shule kiasi unaingia anga za watu nataka nikwambia kwamba hapa umekalia kuti kavu.”



    “Candy unanichanganya sijui unaongea kuhusu nini mbona sikuelewi kwani nimekufanya nini mimi?”



    “hujui ee hujui unajifanya hujui” alidakia Naima.



    “Usione tumekunyamazia kimya tunakuogopa tunakuchora tu maana umekuja hapa unataka kujifanya wewe staaa eee” walizidi kunichanganya nilishindwa kuwaelewa.



    “Candy kama hutaki kunielezea ni nini kimetokea mimi sikuelewi na siwezi kuendelea kukusikiliza nina mambo mengi ya kufaya nielezee tatizo ni lipi ili mi nijue tatizo likowapo sasa unaniambia tu unaniongeleshaongelesha mi vitu sivielewi nashindwa kukuelewa” niliongea kwa kupaniki,



    “unashindwa kunielewa?”



    Alichukua leso ambayo ilikuwa katika madaftari yangu pale juu.



    “hii leso umeipata wapi unajua imetoka wapi hii wewe eee?”



    haaa! Nilishangaa.



    “Hiyo leso hata sijui kwangu imefikaje” niliongea huku nikionesha kutojiamini



    “hiyo leso hata sijui kwangu imefikaje” Aliongea huku amebana pua zake, nilibaki tu nimeshangaa.



    “sikia nikwambie kaa mbali na wanaume za watu”



    nilijiuliza maswali yaliyokosa majibu, maloya ameweka wapi leso yake kwenye madaftari yangu na ni lini?, nikabaki najiuliza.



    Waliendelea kunipasha na kunipashua. Sikutamani kuendelea kuwasikiliza, nilijawa na mawazo mengi sana, waliongea, walinisema na matusi makali ya nguoni walinitukana waliporidhika walicheka kwa dharau na kisha wakatoka.



    Nilipanda kitandani kwangu nikiwa mnyonge na mwenye mawazo mengi, nililia sana, nililia mno nimekosa nini mimi, toka nimefika hapa shuleni sina hata miezi miwili tayari nimeshaanza kukutana na mambo ya ajabu kama haya nitaweza kweli, Maloya kwanini umenisababishia matatizo hivi uliweka vipi leso yako



    katika madaftari yangu ona sasa jinsi nilivyotukanwa, mungu nisaidie, nililia kwa uchungu.



    Nililia hadi nilipopitiwa na usingizi nilikuja kuamka tayari ilishakuwa jioni, nilihisi njaa lakini sikuwa na hamu ya kula kabisa. Nilioga na kisha nikatoka kwenda darasani sikutamani hata kuhudhuria kwenye kipindi cha dini cha siku hiyo nilikuwa na mawazo mengi sana, nilipoingia darasani nilishindwa kujisomea, nilikuwa mnyonge sana niliendelea kuwaza na kuwazua pasipo majibu.



    “Cathe” Martin aliniita niligeuka na kunitazama kisha nikaendelea nikarudisha macho yangu chini alivuta kiti na kukaa pembeni yangu,



    “Cathe unaonekana mnyonge sana leo, unaumwa?” aliniuliza kwa upole



    “hapana siumwi niko salama” niliongea kana kwamba nimelazimishwa,



    “unaonekana hauko sawa any way kama huoni umuhimu wa kuniambia sawa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliinama pasipo kumjibu lolote



    “Cathe nataka nikwambie kitu” aliongea.



    “Nilipofika hapa shuleni nilikuwa nikisumbuliwa sana na wasichana, wengi walikuwa wakinitaka kimapenzi lakini nilikataa kwa vile sikutaka kuwa nao yote kwa yote nilishindwa kwa mtu mmoja tu sio kwa sababu ya kwamba yeye ni mzuri au kwa sababu alikuwa na kila kitu ambacho nilikuwa na kihitaji au kwasababu alikuwa na pesa ila kwasababu alitumia nguvu kuniforce. Muda mchache wa mapenzi yetu nilijikuta nampenda sana aliongea kwa hisia kali zenye kugusa moyo niligeuza macho yangu na kumtazama



    “eeeehe” nilimwambia huku nikionesha utayari wa kuendelea kumsikiliza.



    “Alitumia nguvu sana kuniforce sikuwa na jinsi kwa maana alitumia hadi vitisho kwa vile mimi nayeye hatutokei mkoa mmoja niliona atakuwa akinisumbua sijui ni nini kilinifanya najikuta nampenda hivi, vituko vyake vilinichosha. Maisha yaliendelea lakini alikuwa akionekana akibadilika sana kitabia nilichoka kumvumilia,, nikampa uhuru afanye kile anachokitaka, niliendelea na maisha yangu. Siku akinimisi alikuwa akija kwa mbwembwe nyingi, vizawadi na ahadi kemukemu, alikuwa anajishaua mbele yangu, nilikuwa nikimwonesha ushirikiano



    kwasababu yeye ni mtoto wa kigogo mkubwa sana baba yake ndiye anamiliki hii shule alikuwa akinitishia kunifukuzisha shule mara kwa mara wazazi wangu walikuwa wakinihusia sana kuhusu kusoma, kwasababu wanatoa hela nyingi sana kunilipia ada hapa shuleni hivyo walikuwa hawapendi nifanye ujinga hapa shuleni nilitii amri, kiukweli taarifa yako imeniumiza sana sitaki kuamini kwamba candy wangu alikuwa anatembea na maloya kiasi cha kubeba mimba”



    Nilishituka, nikajikuta nimetoa macho, nilishtuka pasipo na kifani. Nilishituka pasipo kawaida pasipo na kifani,



    “Martin unaongea nini?” nilimuliza kwa sauti darasa zima waligeuka na kutuangalia



    “aaanh sorry class mnaweza mkaendelea kusoma” niliongea kwa woga



    Martin alitikisa kichwa pasi na hakuniangalia



    “ndivyo ilivyokuwa Cathe” nilishusha pumzi za uwoga,



    “inamaana wewe ndiyo uliweka leso yako kwenye madaftari yangu”



    aligeuka kwa haraka na kuniangalia



    “sijaiyona leso yangu leo nina siku ya pili, ni leso ambayo alinipatia candy”



    “ooh my god kumbe” nilionge



    “nimetukanwa sana na Candy kisa hiyo leso nilijua ni leso toka kwa Maloya sikujua kama una mahusiano na Candy samahani kwa kukuletea taarifa mbaya” niliongea nilinyanyuka na kusimama, alinivuta mkono,



    “martin sikuwahi kujua kama uhusiano wangu na wewe utaleta shida nimekuja hapa kwa ajili ya kusoma sio vitu vingine tazama nimeanza kugombana na watu kisa ni wewe endelea na candy wako na mimi niache nisome” nilisema kwa hasira lakini kwa upole wa ajabu chozi likinitoka.



    “Candy yupi sasa?” ailiniuliza kwa kutojiamini,



    “Candy mwenye ujauzito wa mwalimu na bado unasema Candy wangu” nilishindwa kuongea nilimwonea huruma sana



    “pole kwa kilichokukuta Cathe”



    “asante” nilisema kwa upole



    “yaliyotokea yamesha tokea la muhimu ni kujua nini kinachofuata nashukuru mungu sihusiki na ujauzito wa Candy” aliongea lakini kwa sauti iliyoonesha kukata tamaa,



    “martin kuna tatizo zaidi ya hili?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ndio tatizo lipo….., nilijua ni kwa nini Candy alinitakaa mimi na hakupenda



    uhusiano wetu uwe wazi”



    “kwa nini?” niliuliza



    “anataka kunitumia mimi kama chambo endapo tatizo litakuwa kubwa” “unamaanisha nini?”



    “ninamaanisha huo ujauzito utakapogundulika Candy atanitaja mimi na sio Maloya”



    “huuu” nilishusha pumzi ndefu



    “pole Martin”



    “sijapoa na sitapoa mbele yangu naona giza kubwa sana.”



    Nilijutia kiherehere changu cha kwenda kumwambia Martin kuhusu Candy. nilishindwa nimwambie nini mtoto wa watu aliyekuwa mbele yangu amekata tamaa.



    “Martin nitakuwa bega kwa bega na wewe nitahakikisha kwamba hakuna kitu kibaya kinatokea kwako, nitakupigania kadri ya uwezo wangu naomba usikate tamaa wala usijifikirie vibaya kuhusu Candy nitasimama upande wako” niliongea kwa kujiamini zaidi, aliniangalia, akaachia tabasamu la uchungu



    “aaahh sawa” alisema.



    “ok”



    “tuendelee kusoma” nilisema.



    “sina mood wa kusoma kabisa” alisema,



    “mimi pia”



    “basi tupige story nyingine.”



    Tuliendelea kupiga story nyingine mpaka mda wa prepo ulipoisha aliomba kwenda kupumzika na mimi nilielekea chumbani kwajili ya kupumzika.



    Kila siku ugumu ulizidi, nilikuwa nikitukanwa kila sehemi niliyokuwa napita na marafiki zake Candy nilichekwa bila sababu, huku nikiendelea kupata adhabu.



    Siku moja niliitwa na mwalimu Maloya ofisini kwake niliogopa hata kwenda ingawa na jinsi, nilipofika alinikaribisha kwa tabasamu pana lililofanya uzuri wake uzidi kuonekana zaidi.



    “karibu Cathe, karibu ukae.” Nilikaa kwenye kiti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Cathe unajua wewe ni msichana mzuri sana sijaona msichana mzuri kama wewe hapa shuleni, naomba unisaidie kitu kimoja” aliongea, nilishikwa na bumbuwazi lisilo na kifani.



    “nikusaidie nini tena mwalimu, mimi nina uwezo wa kukusaidia kitu gani?”



    “aaaaa usiwe na haraka Cathe nisikilize kwa umakini” aliongea.



    Alisimama kutoka kwenye kiti chake akazunguka meza iliyokuwa katikati yetu hadi alipofikia kwenye kiti ambacho nilikuwa nimeketi akanishika begani,



    “Cathe nakuhitaji” alisema



    “aaaaaa hapana mwalimu” niliongea nikiutoa mkono wake.



    “sitaki”,



    “Cathe embu nionee huruma mwenzio nakuhitaji sana”



    Alinichefua nilitamani kumwambia kuhusu yeye na Candy lakini nilisita nikaamua kunyamaza kimya.



    “hapana mwalimu ninakuheshimu sana naomba heshima hii iendelee kati yangu mimi na wewe, siwezi naomba uniache ” niliongea kwa kujiamni na kisha kutoka nje.



    Nikarejea bwenini, sikuweza kuendelea na vipindi vya siku hiyo, nikajifungia mlango nikaanza kulia.



    Nikajuta kujua kwangu mahusiano kati ya Candy na Martin na kati Candy na Maloya.



    Nilijiona nimejisababishia matatizo makubwa sana kitu ambacho sikujua ni kwamba kuna matatizo makubwa mbele yangu zaidi ya hayo yaliyokuwa yakinikabili, katika maisha yangu yote niliilaumu high school imenibadilisha maisha yangu sana na kunifanya kuwa kiumbe mwenye roho ya utofauti.



    Nilianza kukosa raha, maisha ya shule yakawa magumu sana kila nilipopita Candy na kundi lake walikuwa wakinisimanga, matusi, dharau, kusemwa vibaya ikawa kawaida kwangu. Nilibadili ratiba ili kumkwepa Candy nilichelewa sana kulala na kuwahi sana kuamka, siku nzima ningeweza kukaa darasani.



    Maloya pia alinisumbua mara kwa mara alinipa vitisho nilishindwa kumkubali ilionekana kama ni tabia yake kutembea na wasichana wa pale shuleni na kuwapa mimba na kisha kuwatoa alinifanya nizidi kumchukia sana.



    Martin naye alikuwa akinipa wakati mgumu sana kadri siku zilivyozidi kuendelea alizidi kukosa amani na furaha hakua Martin niliye mzoea, alikonda sana, kiwango chake cha kusoma kilipungua, alikuwa aonekani darasani mara kwa mara ilibidi walimu waanze kufatilia maendeleo yake.



    Kwa upande wangu ufaulu wangu ulishuka pia mwalimu mkuu aliingiwa na wasi wasi alimwagiza matron afatalie kwa ukaribu sana maendeleo yangu ili kujua ni nini tatizo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku moja niliitwa ofisini kwa walimu, jopo zima la walimu lilikuwa mbele yangu walinitazama kwa dharau sana sikuwa najua tatizo ni nini walikuwa kimya tu huku wakinong’ona nong’ona, mwalimu Maloya alikuwa akionekana akiwa na ghadhabu kuzidi ya walimu wenzie wote. Nilisimama mbele yao walikuwa wakinitazama bila kusema lolote nilikuwa nimesimama mithili ya mnazi kando ya



    bahari, nikisukwa na upepo wa kifikra zisizoleta majibu yoyote. Mara martin aliingia akiwa na sura ya kukosa tumaini nilijua mambo yameharibika lakini niishindwa kuelewa ni nini vikao vyote vya kinidhamu lazima Martin awepo kama raisi, moja kwa moja nilijua maloya amenizushia jambo, niliishiwa nguvu nilibaki nikitetemeka na ningeweza kuanguka wakati wowote, Martin alielezwa asimame pembeni yangu nilishindwa kuelewa maana yake nini kama nimefanya kosa hili peke yangu Martini alitakiwa akae pamoja na walimu kwa nini asimame na mimi hapa, sikunyanyua macho yangu kumtazama Martin nilibaki nimejiinamia mithiri ya mtuhumiwa akisubiri akisubiri hukumu yake baada ya kuthibitishwa kuwa ametenda kosa.



    Wapendanao hao sauti kali ya mkuu wa shule mwalimu Maige ilitasua ngoma ya masikio yangu niliishiwa nguvu nikataka kuporomoka Martin alinidaka akabaki amenishikilia sikuwa na nguvu ya kuweza kuendelea kusimama nguvu zilikuwa zikiniisha kwa kasi nilipumua kwa shida sana, kitendo cha Martin kunidaka na kunishikilia vile kama amenikumbatia kiupande mkono mmoja ameuweka kiunoni na mwingine amenishikilia bega la kulia kutoka kushoto kwangu alipokuwa amesimama kilitosha kuwafanya walimu wathibitishe uhusiano wetu usiokuwepo.



    Machozi ya kukata tamaa yalinitoka



    “ni nini hii lakini?” nilijiuliza tu



    “uchunguzi uliofanywa na baadhi ya walimu juu ya sababu ya kushuka kwa kiwango cha ufaulu wetu mimi na Martin ulileta majibu kuwa tuna uhusiano wa kimapenzi, jambo lisilokuwa na ukweli wowote.



    “Sasa cha ajabu nini kinachokushangaza wewe ni nini au kujua kwamba tumeufahamu uhusiano wenu ndio kinachokushangaza zimia kabisa alafu tuone kama kuna kinachobadilika mtoto Malaya sana wewe umekuja juzi tu umeshaanza mambo ya ajabu ona sasa unavyomshusha mwenzako kimaendeleo martin hakuwa wa akifeli hivi.”



    Kauli za kejeli ziliwatoka mfululizo walimu hasa wa kike nilisemwa kwa maneno yote mabaya yanayopatikana katika dunia.



    Maloya alikuwa na ghadhabu sana hakika alinisema sana. Nilibaki nikibubujikwa na machozi sielewi hatima yangu walisema sana.



    Martin alibaki amenishikilia. Mwishowe waliamuliwa apigiwe simu baba yangu na kuelezwa, baba alipigiwa simu akaelezwa mbele yangu huku simu ikiwa imewekewa mfumo wa sauti mvumo. Nilishangaa utulivu wa baba na aliongea kiupole sana haikuwa kawaida nilimjua baba yangu vizuri.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Cathe hakuwa na tabia hizo ni mambo tu ya ujanani muwaonye waendelee na masomo yao wamalize wafaulu kwa maana hiyo ndio lengo la kuwaleta watoto wetu shuleni na ni lengo lenu sio muwafukuze mtaua ndoto zao muwaache wasome wamalize mimi kama mzazi mzazi wake naomba hivyo” aliongea kwa utulivu, nilibaki nimeshangaa sikutaka kuamini kama huyu ni baba yangu mzee Kindamba.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog