Simulizi : High School
Sehemu Ya Pili (2)
“Cathe hakuwa na tabia hizo ni mambo tu ya ujanani muwaonye waendelee na masomo yao wamalize wafaulu kwa maana hiyo ndio lengo la kuwaleta watoto wetu shuleni na ni lengo lenu sio muwafukuze mtaua ndoto zao muwaache wasome wamalize mimi kama mzazi mzazi wake naomba hivyo” aliongea kwa utulivu, nilibaki nimeshangaa sikutaka kuamini kama huyu ni baba yangu mzee Kindamba
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mkuu wa shule aliongea na baba na kumwambia kuwa nimekuelewa na tumewasamehe watoto hawa na hatuta wafukuza shule tutawapa adhabu na kisha waendelee na masomo yao.
Nilivuta pumzi ya shukurani kwa sababu jinsi navyomjua baba ageweza kuwaambia walimu wanifukuze shule nirudi nikakae nyumbani hakupenda nifanye ujinga wowote.
Ilijadiliwa kuwa Martin aondolewe cheo kama raisi wa shule baadhi ya walimu walipinga kwasababu utendaji kazi wake ulikuwa uko juu na pia shule ingeendeshwa bila kuwa na kiongozi mkuu wa serikali ya wanafunzi hivyo ingeleta katika uwasilishwaji wa matatizo ya wanafunzi katika uongozi wa shule hivyo alionywa endapo tatizo hili likijirudia tena hatua za kinidhmu zitachukuliwa dhidi yake.
Martin alisimama bila kuongea chochote akiwa amenishikilia na sura yake aliyokosa matumaini akiwa ameielekeza kwa chini. Nililaumu nafsi yangu kuwa chanzo cha matatizo ya Martin.
Tulitolewa ofisin hadi katika eneo la mkutano wa asubuhi, katika eneo la mkutaniko. Kengele iligongwa wanafunzi wote walisogea pale. Mkuu wa shule alisimama na kisha kuongea kwa sauti kali.
“Mmekuja hapa shuleni kwa ajili ya kusoma mnapaswa mfuate kilichowaleta hapa sisi tupo hapa kuwasaidia kutimiza ndoto zenu kila kitu kina wakati wake, mambo
mengine yote mtayakuta. Fanyeni kilichowaleta hapa na mwachane na mambo mengine yote” kisha mkuu wa shule aliondoka akiwa amejawa hasira sana.
Mwalimu wa nidhamu alijongea mbele na kisha kuueleza umma wa wanafunzi makosa yetu mimi na Martin, makosa yasiyo na ukweli wowote.
Wapo walionicheka wapo walionikebei na wapo wachache waliohuzunika kwa ajili yetu.
“Adhabu yao tutawachapa mbele yenu ili iwe fundisho kwenu na kisha watapewa wiki mbili za kufyeka manyasi yaliyopo nyuma ya shule na baada ya hapo watakuwa mawesamehewa. Na nilazima kwa wao kuingia darasani kuingia darasani vipindi vyote bila kukosa na ndani ya wiki mbili lazima wawe wamemaliza kufanya kazi waliyopewa”
aliongea mwalimu wa nidhamu na kisha kuanza kutuchapa mimi na Martin.
Lilikuwa ni tukio la aibu sana kuwahi kutokea katika maisha yangu kuadhibiwa mbele ya wanafunzi wenzangu kwa kosa kama hilo, niliumia sana moyoni. Tulichapwa fimbo nyingi tu mimi na Martin na kisha wanafunzi wakaruhusiwa kurejea darasani huku wakiongea mambo mbalimbali kuhusiana na tukio hilo.
Nilianza adhabu yangu ingawa kiunyonge zaidi kila mara nilipokuwa eneo la adhabu nilikuwa nikilia sana, sikutamani kukutana tena na martiniingawa sikuwa na jinsi kuonana nae wakati wa vipindi darsani, mara zote sikupenda kumwangalia.
Siku ya tatu ya adhabu yangu niliitwa na mwalimu ofisini ofisini kwake alikuwa ni mwalimu wa michezo, sir Benson, nilipofika aliniambia kuna simu kutoka kwa mama yangu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimpigia simu mama na kisha nikaongea nae,
“mwanangu Cathe uhali gani” aliongea mama kwa sauti ya upole
“mama mimi mzima shikamoo mama” nilimwamkia,
“marhaba mwanangu nimekukumbuka sana”
“mimi pia mama nilimjibu”
“cathe nataka nikwambie kitu mwanangu”
“ndio mama nasikia” nilisema.
“natamani sana utimize ndoto zako ufike pale ulipokuwa unatamani kufika mwanangu, usiwe na haraka na haya mambo usikimbilie kula pilau kabla haijaiva unakosa utamu wake ni vibaya” aliongea kwa huzuni,
“naelewa mama ni makosa tu mi binadamu nakuahidi kwamba hayatatokea tena” nilisema.
“Usijali mwanagu yote ya dunia siku moja utafika unakotaka kufika, hiyo itakuwa furaha yako alisema kwa upole na kutakia kila la kheri mwanangu tutaonana mungu akipenda” alisema na kukata simu.
Nilijawa na furaha yenye uchungu nilifurahi sana kuongea na mama yangu lakini nilisikitika kwa maneno aliyoniambia na kwa upole aliouonesha niliondoka ofisini nikiwa na mawazo mengi, mama yangu na baba yangu siku hizi wamebadilika sana natamani kuwaona tena nilirejea bwenini.
Zilipita siku kama tano nilipoitwa tena ofisini kwa mwalimu mwalimu alinitazama kwa jicho la uchungu sana.
“Cathe” mwisho aliamua kuniita,
“abee mwalimu”
“yote ni mambo ya dunia kuna siku utayavuka na kuwa na furaha tena” aliniambia,
“najua mwalimu”
nilijua alikuwa akihudhunika sana kutokana na matatizo yaliyokuwa yakinikumba hapo shuleni,
“kuna simu yako” aliongea huku akishusha pumzi.
Nilipokea,
“mwanagu cathe” aliongea baba kwa sauti ya upole kuliko ilivyokawaida
“bee baba shikamoo”
“marhaba ujambo”
“sijambo” sauti yake ilizidi kufifia kila alipokuwa akiongea,
“unaendeleaje mwanangu”
“naendelea vizuri” nilisema,
“Mwanangu Cathe” aliiniita,
“abee baba” alinyamaza kimya nilishindwa kuelewa mapigo yangu ya moyo yalianza kwenda kasi, nilishindwa kujua tatizo ni nini.
“Baba” niliiita,
“Eee mwanangu” aliongea kwa sauti ya kilio
“Kuna nini?” nlimuuliza.
“Mwanangu” aliniita.
“Mama yako mpenzi amefariki dunia” aliongea baba kwa sauti iliyochanganyika na kilio,
“Say whaaat?” niliongea kwa mshituko sana.
“Ni hivyo mwanangu, kazi ya mola haina makosa” Machozi yalinichuruzika mfululizo huku mdomo ukitetemeka nilishindwa kuongea neno lolote.
“Cathe” baba aliinita kwa utulivu,
Nilishindwa kuendelea
Aliongea,
“pamoja na hayo yote nasikitika kukwambia kwamba hutoweza kuhudhuria mazishi yake kwa maana anazikwa leo.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maneno hayo yalinishingaza nilipata ujasiri wa kuongea,
“baba kwanini sipaswi kuudhuria mazishi ya mama yangu, ina maanisha mama amefariki na siwezi kuona sura yake ya mwisho kwanini sikupewa taarifa mapema baba kwanini lakini?”
Niliongea kwa sauti kubwa ya kilio,
“Hapana mwanangu hatuna jinsi mama yako hawezi kuendelea kukaa tena naomba unielewe endelea kusoma utakuja wakati wa arobaini yake” aliongea baba,
Niliangua kilio kikubwa hatukuweza kusikilizana tena, baba alikata simu.
Nililia, niliona duniani niko peke yangu nilihisi nimetengwa mbali na dunia sikuwa sawa na viumbe wengine roho iliniuma kuliko kawaida sikuwahi kuhisi maumivu makali moyoni kama nilivyoyahisi kwa wakati huo, nililia sana sikuwa na nguvu ya kunyanyuka. Mwalimu alinionea huruma alininyanyua akanikokota kuelekea bwenini wakati tuko njiani tulipishana na Martin , Martin alikuwa amekonda sana nilimtazama huku nikilia kwa sauti mwalimu aliniongoza mpaka bwenini akaanza kunifariji kwa maneno mazuri, hii ni njia ya kila mmoja wetu kila mtu atapita kila nafsi itaonja mauti jipe moyo Cathe. Nililia sikuwa namsikiliza alikuwa anaongea nini wala sikutamani kusikia alichokuwa akiongea, kwanini baba asinipe taarifa na kuhudhuria msiba mapema kwanini? Nililia huku nikiwaza hayo yote, nilishindwa kupata majibu.
Nililia hadi nilipopitiwa na usingizi nilikuja kushituka ilikuwa ni asubuhi siku ya pili roho iliniuma sana, sikuweza kunyanyuka kuelekea darasani nilibaki nimejilaza tu chumbani.
Nikiwa nimezama kwenye fikra huku nikidondokwa na machozi nilihisi mlango wa chumba chetu umefunguliwa nilijuwa ni Candy, cha kushangaza alikuwa ni Martin, nilipomuona machozi mfululizo yalianza kunidondoka, Martin alijongea kitandani nilipokuwa nimelala akanikumbatia ,
“Cathe pole”, alioongea kwa upole.
Nilishindwa kuongea
“pole sana yote ni mambo ya kidunia usijali mungu yupo pamoja nawe” aliendelea kunifariji na kunitia moyo, nilijitahidi kurudia katika hali yangu ya kawaida ingawa kwa kiasi fulani nilishindwa baada ya muda alitoka kwa sababu aliingia kwa makosa.
Dunia sasa imeniacha peke yangu mama ambaye nilikuwa nikimtegemea na nikimpenda kuliko watu wote ndio huyo ameniacha nililia sana kwa kweli. Baada ya muda kupita nilirejea katika hali yangu ya kawaida lakini haikuwa kawaida
kama kawaida nilikonda nilipungua mara zote nilikuwa mwenye huzuni machozi yakinidodoka, sikupennda kujiunga na watu katika makundi nilipenda kukaa peke yangu. Sikupenda kula chakula nilikula pale tu niliposikia njaa. Usiku iliniwia vigumu sana kupata usingizi kila nilipolala sura ya mama yangu ilinijia, sikuwa na wakati hata wa wakusoma kila niliposoma machozi yalinibubujika nilipenda kusoma ili nitimize ndoto zangu.
Kutimia kwa ndoto zangu ilikuwa ni furaha ya mama yangu, sasa mama yangu hayupo ninasoma kwa ajili ya nani?
Nilikata tamaa ya kusoma nilikata tamaa ya kuishi.
Walimu walijitahidi sana kunifariji, na kunipa nasaha mbalimbali. Haikusaidia kitu.
Martin naye hakuacha kunihusia kwamba hayo yote ni mambo ya dunia yapasa kujipa moyo.
Ilikuwa ni siku ya jumanne asubuhi, tukiwa kwenye mkusanyiko jina langu liliitwa mbele kiukweli saikolojia yangu haikuwa vizuri kabisa nilijuwa tu tayari nina kesi nyingine hapo shuleni nilikuwa tayari kwa kila kitu, hata kama nikiambiwa kwamba leo nimefukuzwa shule ningepokea kwa kawaida kabisa, nilishachoshwa na mambo yaliyokuwa yakinikuta, nilijongea mbele kiunyonge zaidi. Shule nzima walinyamaza kimya, wakitegemea kusikia ni tukio gani tena nimelifanya. Maana nilishazoelekea kuwa mtu wa matukio hapo shuleni. Nilipanda mpaka mbele. Mwalimu alichomoa barua na kunikabidhi nilibaki nimeshangaa imetoaka wapi, nilijiuliza.
Nilirudi huku nikiwa na mshawasha wa kuifungua barua ili nione ni nini kilichoandikwa ndani yake nilifika darasani hata sikukaa sana nilinyenyuka na kuelekea bwenini nikaifungua barua hiyo na kuanza kuisoma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilichokutana nacho kilichoandikwa kwenye hiyo arua kilinifanya nilie upya.
Kiliibua huzuni na simanzi ndani ya moyo wangu.
Kiliuua kabisa tumaini langu na furaha yangu.
Matumaini yangu ya kuwa na furaha yalikatizwa na barua ile, ilikuwa ni barua kutoka kwa mama yangu,
“Kwako mwanagu mpendwa na wa pekee naandika barua hii kwa huzuni nyingi nikijua kuwa sitaweza kukuona tena wewe ni kipenzi cha moyo wangu Cathe mama yako anakupenda sana na siku zote nilitamani ufike pale ambapo ulitaka kufikia, najua unajua tumaini langu kwako kuwa natamani utimize ndoto zako lakini, moyo wangu unaumia sana kujuwa kwamba utatimiza ndoto zako ingawa sitoshuhudia naomba ujipe moyo mama yako natangulia na wewe utafata, mpendwa wangu ujaposoma barua hii sitaki ujenge chuki yoyote na mtu yoyote bali uzidishe upendo, mwanangu kilichokupeleka shuleni ndicho unachotakiwa kukizingatia usiangaike na vitu ambavyo siyo lengo lako wala la kwetu sisi kama wazazi wako kukufikisha shuleni, soma sana mwanangu. Wala usisahau kumkumbuka mungu wako kwa maana ndiye atakuwa kiongozi wa maisha yako mwanangu napenda ujue hiki kitu nitakuwa na furaha sana endapo barua hii itakufikia na kuifungua na kuisoma.
Mwanangu Cathe, nilipokuzaa wewe ukiwa na miezi minne tu nilikuwa na ujauzito mwingine baba yako alinishawishi kuutoa ingawa nilikataa aliniambia kwamba sitakupa muda wa wewe kukua vizuri kama nitakuwa na ujauzito mwingine baaada ya ushawishi wa muda mrefu nilikubali kuitoa hiyo mimba ambayo ilikuwa ni ya mdogo wako, nilifanikiwa kuitoa lakini ilitoka vibaya, iliharabu mfuko wangu wa uzazi.
Baada ya muda, nilianza kusikia maumivu ya tumbo yasiyoisha nilipoenda hospitali niliambiwa mfuko wangu wa uzazi umeharibika haufai tena. Hivyo napaswa kutolewa. Hapo ndipo nilopohakikishiwa kuwa mgumba maisha yangu yote, baba yako alibadilika sana kila mara tulikuwa tukizozana kwasababu alikuwa anataka kupata mtoto mwingine aliniambia endapo sitaweza kumpatia mtoto mwingine basi ataenda kuzaa nje ya ndoa, niliumia sana kwa maana sio mimi niliyetaka kutoa ujauzito bali ni yeye aliyeniamasisha sikuwa na jinsi nilivumilia hayo yote huku nikiweka juhudi kuomba mwanangu.
Cathe tukio lililotokea shuleni kwako ingawa sina imani kama ni kweli umefanya hivyo lilimkasirisha sana baba yako, mara zote alijuwa kwamba mimi ni mtu wako wa karibu sana kuliko yeye, kwa maana hiyo kosa lolote wewe ambalo ukifanya
lawama zote nilibeba mimi, nashukuru katika kipindi chote katika uhai wangu nilibeba majukumu yangu sawasawa na hata sasa naelekea mwisho wa maisha yangu nimekupigania wewe kama mtoto wangu na naamini utafika sehemu ambayo unatamani kufika baba yako alinipiga sana kwa kosa lako ulilolifanya shuleni.
Na baada ya hapo aliondoka hadi ninapoandika waraka huu sijui yuko wapi, nahisi maumivu makali mwilini na hakuna mtu wa kunisaidia. Sitamani tena kuendelea kuishi katika mateso kiasi hiki acha tu nife mwanangu. Nilimwomba tu kijana wa hapo jirani anisaidie kukutumia hii barua ili mwanangu ujue baba yako ni mtu wa aina gani. Sio kwamba umchukie bali umpende na kuishi naye vizuri katika tabia aliyokuwa nayo baba yako ni mkatili sana, mwanangu naona nafsi yangu haina mda mrefu sana nitakufa wakati wowote ule.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kutimiza ndoto zako usiache kusomea kile unachokipenda mkumbuke sana mungu usiache kusali kila unapoingiakatika tatizo lolote, mimi ni mama yako mpendwa nakutakia maisha mema binti yangu”.
Nilijikuta nimekaa sakafuni bila kujua.
Nilikosa nguvu ya kufanya kitu chochote nilianza kulia upya niliumia sana na kitu alichokifanya baba yangu, furaha yangu ilikuwa imetoweka kabisa kiukweli nilimchukia sana baba yangu, alikuwa ni zaidi ya shetani kwangu, kwa upande mwingine niliilaumu nafsi yangu kwa kusababisha kifo cha mama yangu nilijiona sina thamani tena nililia na nafsi yangu.
“Nisamehe mama nisamehe kwa kusababisha kifo chako popote ulipo mama naomba unisikie naomba unisamehe mama yangu”, nililia sana.
Maisha yaliendelea ingawa kiakili nilikuwa siko sawa, taaluma yangu ilishuka sana wala sikujali katika hilo niliishi tu ili mradi siku zisogee mbele.
Maisha yangu yalibadilika kwa kiasi kikubwa nilikuwa nina hasira muda wote hata hivyo sikupenda tena kuonewa nilipanga mtu yoyote atakaye nifanyia kitu chochote nitalipiza kisasi kisasi kilitawala ndani ya moyo, wangu mtu wa kwanza niliye muwazia alikuwa ni baba,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“lazima nitakaporudi nyumbani nilipizie kwa kifo cha mama” nilisema,
Niliwaza kumlipizia Candy endapo angenifanyia tukio lolote lile.
Sikumhofia tena Maloya, sikuhofia kupigwa kwasababu nilishakuwa sugu nilipigwa sana, sikuogopa kufanya tukio lolote lile kwa kuhofia adhabu au kutangazwa mbele za watu, nilijikuta nimekuwa sugu sikuogopa chochote adhabu kwa upande wangu zilizidi mara nyingi. Maloya alikuwa alinisingizia mambo mbalimbali, nilikuwa nikipokea adhabu mara kwa mara kutoka kwa Maloya kwa makosa ya kusingiziwa nilifanya tu sikuwa nahisi chochote katika moyo wangu
Candy alizidi kunionea kutokana na kwamba yeye alikuwa ni kiongozi mara kwa mara alikuwa akinisingizia makosa na kupewa adhabu, niliona kawaida tu na mara nyingi nilimdharau sikusita kumwonesha dharau kila tulipokutana naye sikulihofia tena kundi lake, chuki zao na dharau zao kwangu zilikuwa ni kawaida sana maisha yangu yaliendelea vizuri na hata ufaulu wangu ulianza kuongezeka
Mawasiliano na baba yalipungua, mara kwa mara alikuwa anajaribu kunitafuta lakini sikuweza kuitikia simu zake alipokuwa akipiga simu ofisini nilipoitwa kwa ajili ya kuongea naye nilikataa,
Martin alikuwa akinionea huruma sana kutokana na adhabu nilizokuwa nikipata pale shule,
siku yake alinitafta
“Cathe sijakuona mda mrefu sana”
Nilitabasamu nikamwambia “niko busy sana”
“Busy busy na nini aliuliza?”
“Jamani kwani hapa shuleni tunafanya nini, niko busy na kusoma” alicheka kisha akaniangalia kwa muda nilijisikia aibu.
“Aaaah yaah niko busy na kusoma sasa hivi sitaki kukutwa na matukio yoyote yale ya ajabu”,
“uamuzi mzuri sana kwa maana ufaulu ulikuwa umeshuka sana” alisema.
“Cathe najisikia vibaya sana kwa ajili yako mara nyingi nakuona katika adhabu inaniumiza sana”, nilitoa tabasamu jepesi kisha nikamwangalia usoni
“Marti usijali kuhusu yote haya ninachoangalia sasa ni kufanya kile kitu ambacho kimenileta hapa shuleni kwa sababu hilo ndio lililokuwa tamani la mama yangu na ameondoka kabla sijalitimiza ni lazima nilitimize ili hata uko alipo apumzike kwa amani”, aliniangalia sana kana kwamba sio mimi niliyekuwa nikiongea hivyo,
“Cathe umeongea kitu kizuri sana lakini hujui kuwa hizo adhabu zinaweza zikakuathiri kisaikolojia na kimasomo pia?”
“Martin siwezi kuruhusu kitu chochote kikaniharibu tena najua kwamba nikiwa mpole nikiwa mkali haya matukio kwangu ndiyo yameshakuwa yangu na hayawezi kuondoka vyovyote vile niwavyo lazima yatanijia siwezi kuyakimbia siwezi kumkimbia Candy siwezi kumkimbia Maloya siwezi kuikimbia shule nitaendelea kupambana hivyo hivyo” niliongea.
Alifurahi sana alinivuta na kunikumbatia nililihisi joto lake tulibaki tumekumbatiana kama dakika mbili hivi ilikuwa ni wakati mzuri sana kwangu ambao sikuwahi kuwa nao katika maisha yangu yaliyopita, tuliachiana huku tukitweta, aliachia tabasamu na mimi pia,
“uwe na wakati mwema Cathe” alisema na kuondoka.
Tukio hilo liligoma kufutika katika akili yangu kabisa kila mara nilikuwa nikifikiria liwazo kutoka kwa Martin, nilihisi nampenda sana Martin.
Huyu mkaka niliwaza na kisha nikatabasamu na kuondoka eneo hilo na kuelekea bwenini.
Nilipofika bwenini nilipanda kitandani kwangu nikiwa na tabasamu hatimaye katika maisha yangu nimepata liwazo mtu ambaye anaweza akarejesha furaha yangu katika mazingira magumu kama haya, nilifikiria.
Niamua kwenda kumwambia wakati tutakapokutana tena baada ya kufikia uamuzi huo nilikuwa nikitabasamu kila wakati, ulipofika wakati wa kuhudhuria kipindi cha dini alikuwepo pia, aliimba vizuri sana moyo wangu ulijawa na furaha na amani tele kila mara nilikuwa nikimwangalia.
Tulipotoka kwenye kipindi nilienda nilimshika mkono tukaongozana darasani alikuwa na furaha sana.
Tulipofika darasani nilimwambia “Martin baada ya hapa nilikuwa nahitaji kuongea na wewe”, aliachia tabasamu.
“usijali bibie” aliongea kwa sauti yake tamu,
kisha akaendelea kusoma na mimi nikachukua madaftari yangu na kuanza kusoma.
Baada ya muda wa prepare kuisha wanafunzi walianza kutoka madarasani na kuondoka, aliniangalia kisha akanibinyia jicho nikaachia tabasamu tu.
Mara baada ya watu wote kutoka alinigeukia na kunitazama
“haya niambie bibie”, alisema nilitabasamu alitabasamu pia
“Martin” niliita kwa sauti nzuri ya kike,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naam”
“unajisikiaje tunavyoonewa kwa kosa lisilo la kwetu?”
“Hamuna mtu ambaye angeweza kujisikia vizuri Cathe kila mtu lazima angeumia na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu” aliniambia.
“Pole” nilisema.
“Na naomba nisamehe kwa kuwa chanzo cha mambo haya yote kutokea kwa upande wako.”
“Usijali Cathe hata mimi pia napaswa kusema sorry kwako kwasababu hata mimi ni chanzo cha haya yote kutokea kwako.”
“Aaah kwahiyo kila mtu amwombe msamaha mwenzie si ndiyo?” nilisema.
“Mmmh” alicheka
“Ndio nisamehe pia na mimi”,
Tulicheka wote kwa pamoja.
Cathe” aliniita.
Nilimwangalia, nilishindwa kumtizama moja kwa moja machoni,
“Uliniambia kuna kitu unataka kuniambia nakusikia na utakapomaliza kuniambia unachotaka kuniambia na mimi kuna kitu nataka nikwambie.”
“Asa kwanini hukuniambia toka saa zile?” nilimuuliza
“Kimenijia ghafla” alisema na kisha akacheka.
Na mi nikacheka pia
“Ok Martin mara zote huwa najisikia vibaya sana kusemwa au kuhukumiwa kwa kosa ambalo kweli sijalifanya na najua kabisa kwamba sijafanya”
“Ni kweli inaumiza” alisema Martin kwa utulivu,
“Martin sorry kama nitakukwaza kwa nitakacho kwambia” nilimwambia.
“Lakini nimeona kwamba tusiache ibaki midomoni kwa watu nataka iwe kweli kwasababu wewe ni mzuri kwangu”
aliniangalia sana,
“Cathe are you serious?”
“Nataka kuwa na uhusiano na wewe.”
“Ngoja na mimi nikwambie ambacho ninatakanikwambie” alisema Martin.
Niliishiwa nguvu mwili mzima ulikuwa ukitetemeka nikiwaza Martin anataka kuniambia nini? Akili yangu hakutulia niliwaza sana nimewezaje leo kumwambia mwanaume kuwa nakupenda kitu ambacho sikuwahi kufikiria katika maisha yangu. Akili yangu haikuwa sawa kabisa,
“Cathe” sauti yake ilinitoa kwenye wimbi la mawazo,
niliongea kwa kitetemeshi, “nakusikia martin”.
“Mawazo yetu yanafanana”, nilibaki namshangaa nisijue akimaanisha nini
“una maana gani Martin?” nilimuuliza.
Alivuta pumzi ndefu na kisha kuishusha
“ulichokuwa unakiwaza ndicho kilichokuwa akilini mwangu” alisema.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sentensi yake fupi ilitosha kuufanya moyo wangu ujae na furaha sana niliruka kwa furaha na kumkumbatia. Kila mtu akiwa na furaha moyoni mwake na huo ndio mwanzo wa mahusiano kati yangu na Martin, tulipendana sana huku tukishirikiana katika mambo mbalimbali pale shuleni, alikuwa mshauri wangu mkubwa na pia tulishirikiana kimasomo ili kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri katika mitihani yetu. Ukizingatia wakati huo tulikuwa tumebakiza wiki chache tu kufanya mitihani yetu ya muhula wa pili.
Candy mahusiano yetu yalimuumiza sana, Candy na kundi lake, alizidi kunipa adhabu mbalimbali lakini sikujali kwakuwa kwa wakati huo hakuwa akinionea tena.
Mahusiano yetu yalizidi kustawi ingawa ndani ya nafsi yangu sikuwa na amani, kisasi juu ya baba kilinisumbua sana mara zote nilitamani kumlipizia kisasi. Niliwaza sana nitakapoporudi nyumbani lazima nilipize kisasi kwa baba haiwezekani kuniulia mama yangu,
“haiwezekani baba lazima ulipe damu ya mama yangu”, niliwaza.
Martin alikuwa akinishauri sana kuhusu swala la kulipiza kisasi,
“achana nayo yamesha pita hata ukilipiza kisasi mama yako hatoweza kurudi mwache msamehe baba” alikuwa akinishauri.
Nilifanya kama namwelewa ingawa nafsi yangu ilikataa kabisa kuendana na mawazo yake lazima nikalipize kisasi nilisema.
Tulifanikiwa kufanya mitihani yetu ya mwisho na kufaulu kwa ufaulu mzuri kabisa.
Tulirudi nyumbani mimi na Martin tulikuwa tukitokea Dar es salaam. Candy alikuwa akitokea Arusha hivyo naye alielekea kwao ingawa kwa masikitiko sana alikuwa akiumia sana kumpoteza Martin.
Wakati wa likizo tulitumia muda mwingi sana kuwa pamoja mara nyingi tuliongozana sehemu mbalimbali za burudani. Nilipata amani na furaha sana moyoni mwangu kuwa pembeni ya Martin wazo langu la kulipiza kisasi bado nilikuwa nalo.
Mara nyingi baba hakuwepo nyumbani nilikuwa nabaki peke yangu, toka nimerudi likizo baba alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani na akiwahi sana kuondoka alikuwa marachche sana nilikutana na baba yangu na hakuwa katika hali ya kawaida.
Kila mara nilikuwa nikimshangaa jinsi alivyo baba alivyobadilika sana. Nilipanga lazima tu nilipize kisasi kwa namna yoyote ile ingawa hadi wakati huo sikuwa naijua ni kwa namna gani nitalipiza kisasi siwezi kumuua baba yangu nilisema.
Muda mwingi niliutumia kuwa na Martin na wakati huo niliweza kupoteza usichana wangu. Martin aliniingiza katika dunia ya mapenzi sikujali kuhusu hilo ingawa mama yangu alikuwa akinihusia sana kuhusu kujitunza sikuona umuhimu wowote kwasababu mama yangu mwenyewe hakuwepo duniani niliona ni kawaida.
Mapenzi kati yetu yalizidi kuongezeka hata hivyo akili yangu ilikuwa ikifikiria vitu vingine kabisa. Muda ulienda na wakati wa kurudi shuleni ulikaribia.
Nilichelea kuona kwamba sijafanya kisasi kwa baba yangu niliamua kwa muda huo mchache lazima niwe nimefanya kitu, kama kawaida yake baba alichelewa sana kurudi nyumbani na aliwahi kuondoka asubuhi.
Alipotoka tu nilinyatia hadi chumbani kwake, nilipoingia nilishangaa kukuta baba hafungi chumba chake siku hizi. Nilikuwa naogopa sana kuingia chumbani kwa baba yangu enzi za uwepo wa mama. Mara zote sikuruhusiwa kuingia bila ruhusa maalumu niliingia mara chache sana. Nilikuwa nikitetemeka mno kuingia chumbani kwa baba. Mazingira niliyokutana nayo pale chumbani yalinishtua sana, palikuwa ni pachafu kana kwamba haishi mtu.
“Nahisi toka mama amefariki hiki chumba hakijawahi kufanyiwa usafi”, niliwaza.
Nilipofika katikati ya chumba nikasimama,
“nafanya nini humu sasa?” Nikajiuliza,
“humu ndio nimekuja kulipiza kisasi kwa baba yangu?” Nilibaki nimesimama nisijue nini cha kufanya. Ghafla nikaijiwa na wazo la ghafla nikaenda kwenye droo ya baba yangu na kuanza kufungua fungua droo moja baada ya nyingine.
Nilikuwa nafungua tu nisijue nini natafuta. Katika kupekua pekua nilikutana na vyeti vya hospitali vingi, moyo wangu ulinishawishi kuviangalia,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“aaaah! mimi si nimekuja kwaajili ya kulipiza kisasi? Hivi vyeti vya nini? Mimi naachana navyo bwana” nilijiwazia, upande wa pili nafsi yangu iliniambia nivifuatilie. Nikaviweka kitandani kisha nikaanza kukagua kimoja baada ya kingine. Moyo wangu ulizimia cheti cha kwanza kukiona kilikuwa ni cha marehemu mama yangu. Ilikuwa ni ripoti ya daktari kuhusiana na kifo chake ambayo sikuwa na shaka kuwa haikusomwa siku ya msiba wake. Mama yangu alikufa kwa stroke (kiharusi). Na hii imetokana na kupasuka kwa mirija yake ya damu kutokana na kipigo kikali alichokipokea kutoka kwa baba. Hadi kufikia mwisho ripoti ya daktari machozi yalikuwa yakinitoka huku mwili mzima ukitetemeka. Nilijawa na hasira mara mbili yake nilitamani baba awepo karibu yangu nichukue hata kisu nimchome aondoke mbele ya macho yangu sikumpenda kabisa. Nikasimama ili niondoke nikagundua kuna vyeti vingine ambavyo vimebakia hapo chini nilivichukua huku mikono ikitetemeka na kuanza kuvisoma,
“mungu wangu!” Nilisema.
Vilikuwa ni vyeti vya baba yangu kutoka katika hospital maarufu sana hapa mjini. Vilikuwa vikionesha kwamba baba yangu yupo katika hatua za mwanzo za kansa ya ini na hii imetokana na ukweli kwamba baba yangu alikuwa mlevi kupindukia hasa mara baada ya kifo cha mama.
Nililia sana ni sawa nilikuwa nikimchukia baba yangu lakini kujua kwamba baba yangu ana kansa ya ini na asingekuwa na maisha marefu iliniuma sana wazo la kisasi lilipotea kabisa katika moyo wangu
“kwanini mimi? Kwa nini matatizo hayaniishi?” nililia mno.
“Baba ukiondoka nitabaki na nani sasa?”
Nilitoka chumbani kwa baba nikawa nimenyong’eya nilijutia kiherehere change kutaka kulipiza kisasi bora nisingejua nililia siku nzima sikutaka hata kuongea na Martin na mtu mwingine yoyote nilijifungia chumbani siku nzima.
Nilikuja kusituka ni asubuhi yake Martin alikuwa amekuja nyumbani alikuta mlango uko wazi akaingia moja kwa moja hadi chumbani kwangu,
“Cathe kwanini hupokei simu yangu wala hujibu meseji zangu?” Aliniuliza,
“Hapana hamna kitu” nilisema
“Kuna tatizo? kama lipo naomba niambie” aliniuliza.
“Hapana hakuna tatizo lolote”
Sikupenda ajue.
Tulishinda wote hadi ilipofika jioni. Jioni baba aliporejea alitukuta na Martin mara nyingi alizoea kutukuta na Martin nyumbani, alisalimia pasipo uchangamfu na kupitiliza chumbani kwake. Sikuweza kupata muda wa kuongea na baba muda mwingi alikuwa akinikwepa.
Wakati wa kurudi shuleni ulipofika nilirudi shuleni kinyonge sana Marti alikuwa akiniuliza mara kwa mara kwa nini umepoteza uchangamfu wako Cathe aliniuliza.
“Hapana usijali” ilisema
Ingawa hata ndani ya nafsi sikuona kama nipi kawaida nilihisi nina kitu ndani yangu sikujua ni kitu gani.
Nilirudi shuleni nikiwa na unyonge sana
Safari hii Candy alikuwa amenipania sana sikuogopa kitu.
Martin alizidi kunipenda na tulizidi kudhijirisha uhusiano wetu haikuwa siri tene pale shuleni.
Tatizo na lenye kuumiza kuliko yote lilijitokeza.
Chuki ya Candy ilizidi juu yangu pamoja na faraja niliyokuwa naipata kutoka kwa wanafunzi na kwa baadhi ya marafiki zangu, Martin akiwa mmoja wapo haikutosha kunifanya nisiogope, niliingiwa na woga sana kwa sababu alikuwa akinitisha mara kwa mara nilipokea meseji za vitisho kutoka kwake mara nyingi akiniambia kwamba atanifanyia kitu kibaya, nilianza kuogopa sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Martin aliweza kunitia moyo na mara nyingi alikuwa akinisisitizia kuwa makini, nilijaribu kujiweka busy na masomo na kumtoa Candy katika akili yangu, sikutaka
kurudia makosa niliyoyafanya hapo kabla, nilitamani kufanya vizuri katika mitihani yangu ya mwisho hivyo sikupaswa kurudi nyuma tena.
Siku moja niliitwa ofisini kwa mwalimu Maloya niliogopa sana kwenda ingawa sikuwa na jinsi kila nilipokuwa nikipiga hatua moyo wangu ulikuwa mzito nafsi ilinishauri sana nisiende ingawa upande mwingine uliniambie niende laiti ningejua nisingeusikiliza upande huu.
Nilipiga hatua zangu za kinyonge hadi ofisini kwa Maloya nilipoingia hakunikaribisha kama ilivyokuwa siku zote, niliingia na kubaki nimesimama,
“shikamoo mwalimu” nilimsalimia hakunijibu
“nimeitikia wito” nilimwambia bila kujali jinsi ambavyo alikuwa amechukia, alisimama
“karibu binti mrembo, mrembo ambaye unajisikia unajiona mzuri kuliko wote hapa shuleni” aliongea kwa dharau,
Unamaanisha nini mwalimu
“Hivi we unafikiri ni mzuri sana kiasi cha kinikatalia mimi?, wasichana wenzio wazuri wazuri kabisa kama wakina Candy hawaringi kama unavyoringa wewe, wewe ni nani hasa?”
Nilishindwa kumwelewa.
Akili ilianza kuniambia kuwa tukio baya litatokea, miguu iliniwia mizito sana kuondoka , nilitamani kukimbia lakini nguvu zilinishia.
“Wewe ni mtoto mdogo sana huwezi kunishinda mimi alaaa!”
Alisema na kusogea pale nilipokuwa, nilisimama kujizatiti kwa ajili ya kile kilichokuwa mbele yangu. Alikuja hadi mbele yangu akasonya kisha akinipita alielekea mlangoni nilijua alikuwa akienda kuchukua fimbo kwa ajili ya kuniadhibu .
Adhabu nilishazizoea nilikuw tayari aniadhibu, maloya alifika mlangoni na kujifanya kama anachukua fimbo akafunga mlango na kisha akanigeukia
“Leo utaongea na mimi” akanisogelea,
“Unanikubali hunikubali? aliongea kwa ghadhabu,
“Hapana mwalimu siko tayari” Niliongea kwa sauti ya chini sana.
“Utanipa hunipi nilishituka”
“Hapana mwalimu siwezi kukupa”
“Siwezi kukupa unachotaka naomba niruhusu niondoke”
“Huendi popote leo Cathe ama zako ama zangu”
Alinishika kwa nguvu na kufanya kile ambacho alitarajia kufanya.
Nilihisi maumivu makali sana ndani ya moyo wangu.
Sikutegemea mtu ambaye nilikuwa nikumheshimu kama mwalimu na mlezi wangu katika mazingira kama haya angenitendea kitendo hicho.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maloya alinibaka bila huruma nililia sana, alinizidi nguvu nilishindwa kujiokoa nilijaribu kupiga kelele aliniziba mdomo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment