Simulizi : High School
Sehemu Ya Tatu (3)
Alinishika kwa nguvu na kufanya kile ambacho alitarajia kufanya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilihisi maumivu makali sana ndani ya moyo wangu.
Sikutegemea mtu ambaye nilikuwa nikumheshimu kama mwalimu na mlezi wangu katika mazingira kama haya angenitendea kitendo hicho.
Maloya alinibaka bila huruma nililia sana, alinizidi nguvu nilishindwa kujiokoa nilijaribu kupiga kelele aliniziba mdomo.
Baada ya kutekeleza unyama huo alivaa nguo zake
“Vaa uende bwana, unaringa nilijua unajitunza kumbe na wewe hamna kitu ondoka” aliniongea kwa dharau,
Moyoni mwangu niliumia sana,
“Unajifanya mlokole kumbe huna lolote wajanja washa kuchezea wewe toka bwana” aliongea.
Nilivaa nguo zangu kiunyonge sana na kupiga hatua za kinyonge kuelekea mlangoni
“Cathe” aliniita,
“Ole wako unyanyue mdomo kumwambia mtu yoyote nitakuua” alisema.
Niliondoka kinyonge kuelekea bwenini nilifunga mlango na kuanza kulia
Nililia sana “kwanini matukio haya yote yananitokea mimi tu ina maana hamna mtu mwingine wa kushea na mimi shida hizi kwa nini mimi peke yangu”
Nililia sana
“kwanini haya yote” nililia,
Nililia mpaka nilipopitiwa na usingizi nilikuja kushtuka ilikuwa jioni sana.
Sikusikia hamu ya kula wala kutoka kwenda sehemu yoyote .
Nilibaki hapo kitandani hadi siku ya pili yake. Sikujisikia kuingia darasani, nilobaki tu nimelala sikuwa na hamu ya kula nilikula tu pale nilipohisi njaa, hali hiyo iliendelea kwa wiki nzima.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Martin alikuwa akinitafta kila kona huku walimu wakiulizia ni wapi nilipo.
Nikiwa bwenini niliwaza haya yote yatakwisha lini ndani ya nafsi yangu niligundua
Ni lazima niyachukulie kama sehemu ya maisha yangu. Lazima niwe na amani sasa.
Kujua kwamba nimezaliwa ili niteseke, nilizaliwa ili nipate uchungu, kamwe haikuniumiza katika maisha yangu.
Nilijitia moyo sana kwamba hayo yote ni maisha yangu ambayo nimeletwa nije niishi.
Hakika nilipata faraja kubwa sana na kwa wakati huo niliapa sitolia tena, kwa sababu hayo ni maisha yangu Mungu amenileta ili niyaishi.
Nilitoka bwenini na kisha kuelekea nyuma ya shule Martin aliniona na kunifuata, alikuja
Cathe kwanini huingii darasani wiki nzima , una nini? Una unaumwa? Kwanini uko hivyo Cathe kwanini lakini? Aliuliza maswali mfululizo ambayo nilishindwa kujibu.
“Aaah Martin uwe na amani niko sawa kabisa”
“Nakujua vizuri kama una tatizo ni bora uniambie ili nijue ni nini naweza kukusaidia.”
Sikutaka kumwambia sikutaka ajue, ningewezaje kwanza kumwambia.
Hapana hakuna kitu nilihisi machozi yanaanza kunitoka nilinyanyuka pole pole na kumwacha Martin peke yake pale. Niliondoka na kuelekea bwenini jioni ya siku hiyo niliamua kuingia darasani.
Nikiwa na furaha kwa kujua kwamba matatizo ni sehemu ya maisha yangu nilingia darasani kwa bashasha zote. Nilikutana na Martin tukasalimiana kwa uchangamfu tukaketi,
“Nilikumis sana Cathe, ingawa hutaki kuniambia tatizo lilikuwa ni nini” nilicheka,
“Martin sina tatizo lolote uwezi kuniamini mimi mpenzi wako” alitabasamu.
“Nakuamini mke wangu wangu mtarajiwa” alisema, nilicheka, tukacheka kwa pamoja kisha tukaendelea kusoma
Siku hiyo ilipita kana kwamba hakuna kilichotokea, maisha yaliendelea.
Watu walihisi uhusiano wangu mimi na Maloya na hiyo ikawa habari mpya shuleni, kwakuwa Maloya alikuwa akihofu kitendo chake alikuwa akiniuliza mara kwa mara nimwambie kuhusu mahali nilipo na maendeleo yangu.
Candy alichukia sana hivyo nilipokea ujumbe wa vitisho nilipoamka kitandani kwangu
“We Malaya naona sasa unataka kuniingilia katika anga zisizofaa, nakuhakikishia ama zangu ama zako hii wiki haitopita lazima nikufanyie kitu cha kihistoria.”
Yalikuwa ni maneno mafupi na mazito, niliogopa sana “huyu anataka kunifanyia nini?” Niliishi kwa uwoga mno nilipoteza furaha tangu asubuhi ya siku hiyo, ilikuwa ni jumatatu, niliingia darasani kiunyonge, Martin aliweza kugundua kuwa sipo sawa
“Cathe uniamini, umuamini mme wako mtarajiwa?” Aliniambia
“namuamini sana” niliongea ingawa sio kiuchangamfu.
“Kwanini hutaki kuniambia tatizo linalokusibu?”
Nilijitahidi kuonesha kwamba niko kawaida ingawa najuwa kuwa nilishindwa
“Martin niko kawaida” niliongea huku nikitazama pembeni,
“Hauko kawaida”
Niliamua kunyanyuka na kuondoka ili kumkwepa
“Unaenda wapi?”
“Aaah” nilishikwa na kigugumizi.
“Naenda toilet mara moja”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliachia tabasamu na kisha akaniambia nenda.
Niliondoka na kuelekea chooni, vyoo vilivyokuwa bwenini kwetu, niliingia kule nikabaki nimesimama sikuwa najua ni nini nifanye.
“Nimwabie nini Marti ili aelewe sitaki kukosana naye wala sitaki kumkosesha amani” niliwaza.
“Nilikwambia leo ni ama zangu ama zako” sauti ya candy ilipenya kwenye masikio yangu.
Ilikuwa ni sauti ya Candy, niligeuka kwa mshituko na kumtizama alikuwa amjishika kiuno na yuko peke yake.
Una nini wewe unakitu gani hasa ina maana shuleni umetafuta watu wote wa kuwachokonoa ukaniona mimi, mimi sio saizi yako Cathe huoni nimekuzidi vingapi na mpaka leo bado unazidi kunifatilia kwani hakuna watu wengine, bora hata ungemchukua huyo Martin kwasababu ni wa kawaida. Lakini sio Maloya wewe hujui mimi na Maloya tumetoka wapi ni kitu gani kinakufanya uingilie eee
“Mi sitoki na Maloya” niliongea kwa dharau,
“Siwezi kudate na Maloya wakati najua fika kabisa ni baba wa mtoto wako” niliongea makusudi kumkasirisha.
“Nakuonea huruma Candy nakuonea bila kosa”
“Unajitia jeuri si ndio ee?”
“Nataka nikuangalie tu ongea ukishamaliza nataka nikutie adabu. Sitaki uendelee kunifatafata”
“Siwezi kudate na Maloya sio saizi yangu”
“Ila Martin ndio saizi yako si ndio ee?” aliniuliza,
“Ndio” Nilisema.
“Tunaendana sana na ndio maana mpaka saivi tupo pamoja hakuna mtu anaweza kutuingilia wala kufanya tuachane na mimi” niliongea kwa dharau.
“Kwanini unaniongelesha kwa dharau?”
“Naongea na mtu ambaye mwanafunzi mwenzangu, ni msichana mwenzangu tuko sawa na hatujapishana chochote” niliongea kumshushua,
alishikwa na ghadhabu.
“Nikwambie Candy mimi hunitishi kwa lolote na wala siogopi chochote unanikosesha amani kwani wewe ni nani? Tumekutana hapahapa shuleni na tutaachana hapahapa shuleni, mimi sikuogopi kama unafikiri unaweza kufanya kitu chochote nataka nikwambie na mimi naweza kuwa vilevile kwa sababu mimi na wewe wote tuko sawa. Unanitishatisha unaniambia kwamba eti ama zangu ama zako, na mimi nakwambia ama zangu ama zako kama wewe ni mwanamke aliyekamilika. Unachokifanya ndio mwezako atakifanya fanya chochote niko tayari” niliongea kwa kujiamini.
Candy hakutegemea kitu kama hicho mara zote alikuwa akinionea na kuniburuza leo ilikuwa ni tofauti.
“Unanijibu nini wewe hivi unafikiri mimi utanitisha kwa hivyo vineno vyako siogopi mwanaharamu wewe”
“Nitakufanyia kitu kibaya leo hutoamini”, alinisogelea nilishikwa na uwoga ingawa sikuweza kumwonesha kama nimeogopa alinisogelea alipofika karibu alinikunja shati langu na alinibabatiza ukutani niliogopa sana lakini sikutaka kuonesha nimeshindwa, nikamshika nayeye nikamtizama kwa dharau na kumsonya, alishikwa na hasira alinyanyua mkono wake ili kunipiga niliudaka na kisha nikamsonya”
Tulibaki tukitweta huku tukitazamana hakuna aliyethubutu kumsogelea mwenzie wala kuongea neno lolote.
“Candy sikuogopi” nilisema,
“Cathe nitakuumiza” aliongea kwa hasira na ghadhabu.
Na hapo ndipo nilimshuhudia nafsi nyingine ya Candy pamoja na uzuri aliokuwa nao Candy alikuwa ni mafia. Ni kama alikuwa amedhamiria kuniua hiyo siku niliogopa sana katika mazingira hayo ambayo tulikuwa wawili hata ningepiga kelele vipi zisingeweza kusikika kwa wakati huo.
Ni kweli sikuwahi kupigana na sikuwa na tabia ya ugovi ilikuwa ni mara yangu ya kwanza hakika niliogopa sana
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Candy alizidi kunisogelea nilizidi kurudi nyuma hadi nilipogota ukutani.
Nikawa najaribu kuondoka eneo hilo nikawa natafuta sehemu ya kutokea.
Lazima nikufundishe adabu alinisogelea na kunikwida shati na kisha akaanza kunivutavuta kila upande,
“Niache Candy” niliongea
“Sikuachi” alisema
Nilipatwa ujasiri wa ajabu na nguvu ambazo sikujua zimetokea wapi, nilimsukuma Candy akajigonga ukutani na kisha kudondoka chini na kisha akatulia.
Nilimwangalia bila kuelewa chochote,
“nilisha kwambia sikuogopi tena naomba kaa mbali na mimi kaa mbali, usifikiria kwamba mi nitahofia kitu chochote, kwasababu huna chochote unachoweza kujisifu, Sawa yule ni mumeo”, Candy alitulia vilevile pale chini, nilishangaa ana nini huyu.
“We Candy” nilimwita.
Hakuitika wala hakutikisika.
“Mungu wangu”
“Candy umepatwa na nini?” nilimsogelea na kumshika.
Hapo ndipo nilipogundua kuwa Candy alikuwa akivuja damu kutoka sehemu ya nyuma ya kichwa chake, nilitoa macho nikiogopa na kisha kumwachia Candy
“Nimeua”
Nilipiga hatua kurudi nyuma nikibaki nimekodolea macho maiti ya Candy
“Mungu wangu mungu wangu”
Nikibaki najishangaa nisijue nini cha kufanya
“Nikikutwa hapa si nitaishia gerezani”
“Mungu wangu nisaidie mimi nisaidie, nililia na kuwaza, nikaona kulia kwangu hakutosaidia chochote nilifuta machozi na kukimbia kuelekea darasani huku nikitweta na machozi yakinichuruzika, mdomo ukinitetemeka na mwili wote umeniisha nguvu huku nikipumua harakaharaka. Niliingia darasani na kusimama mlangoni kila mtu alinitazama, Martin alinyanyuka akanishika mkono na kisha kunikalisha kwenye kiti.
“una nini Cathe? alafu siku hizi sikuelewi, una tabia za ajabu sasa ni nini kinachokushangaza hivyo?”
nilishindwa kumjibu nilibaki nikimwangalia tu huku machozi yakinitoka,
“kwani unatatizo gani alafu Candy anakutafta” aliongea
“Candy ananitafta?”
Alinishitua sana
“Candy ananitafta?!” niliongea kwa mshituko.
“Kaja hapa kukuulizia nikamwambia umeenda chooni nafikiri alikuwa amekufata huko hujakutana naye.”
“Mungu wangu mungu wangu” niliwaza.
“Eee mungu niepushe na kitendo hiki”
“Aaah” nilishikwa na kigugumizi sikuweza kuonge chochote.
“Aaah aaaah hapana, yah yah ndio nilikutana nae lakini aaah” nilishindwa kuendele kuongea nilihisi naweza kuharibu kila kitu,
“nifanye nini?” Niliwaza.
Martin alikuwa akiniangalia jinsi ambavyo nilikuwa nimehamanika, alibakia kunishangaa
“ana nini huyu” aliwaza.
“nifanye nini sasa?” nilijiuliza
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Napaswa kujitoa kabisa kwenye hii kesi ngoja niende ofisini nikaripoti” nilimweleza bila kusema chochote nikatoka mbio darasa zima walishangaa na mwisho wakamalizia na kicheko,
“mmmh huyu mtoto akiendelea kusoma lazima achanganyikiwe, hapa tupo sekondari ameshakuwa hivi kama mvuta bangi, je tukifika chuo?” aliongea msichana mmoja darasani kwetu na kisha darasa zima wakacheka.
Martin alisonya na kukaa chini alibaki ameshangaa bila kuelewa kitu
Martha alimfata Martin “kwani Cathe ana nini?”
“Mi mwenyewe sijui Nashindwa kumwelewa kabisa, Labda kuna tatizo”
“Inawezekana nitatafta muda mzuri niongee naye” aliongea Martin kwa kuonesha kuwa haitaji kuendelea na maongezi hayo.
nilikimbia hadi ofisini kwa mwalimu mkuu. Nilimkuta mwalimu yupo na Mr. Maloya wanaongea nilipoingia mwalimu alinitazama na kisha kugundua kuna kitu hakipo sawa.
“Cathe una nini?” aliongea mwalimu.
nilibaki nikitetemeka nikishindwa kuongea mwalimu Maloya alihisi moja kwa moja nimekuja kumshitakia.
“Hawa wadada wanamatatizo gani sijui hasa huyu Cathe sijui ana nini embu mtoe ofisini”,
mwalimu mkuu aliniangalia na kisha kumwambia “Maloya naomba unipe dakika chache kuongea na Cathe.”
Maloya aliniangalia kwa jicho kali sana na kisha kutoka nje kwa ghadhabu
Alivyotoka nilienda kumshika mkono mwalimu mkuu
“Twende ukaone” niliongea
“Kuna nini wewe hebu niache mkono wangu binti” aliongea
“Twende” niliendelea kumvuta
“Twende”, alisita lakini alipatwa na hamu ya kujua ni nini kimetokea
Tuliongozana hadi chooni mwalimu alipigwa na bumbuwazi kubwa sana alitoa simu yake na kupiga sikuwa najua alikuwa akimpigia nani nilichanganyikiwa
“Eee njoo huku kwenye maeneo ya mabweni ya wasichana kwenye upande wa vyooni jengo la Queen Elizabeth sasa hivi” aliongea na kukata simu.
Mungu wangu nimezidi kujiharibia niliwaza.
Dakika chache baadae jopo la walimu liliingia, kila mtu alionekana akiwa na mshituko sana, nilizidi kutetemeka.
Jasho lilinichuruzika kwa wingi nilishindwa kusema chochote, walimu waliingiwa na mshangao baadhi ya walimu wa kike walishindwa kujizuia na kuangua kilio, eneo zima ilishikwa na taharuki. Wanafunzi madarasani hawakuelewa nini kinaendelea ingawa walihisi kuna kitu hakipo sawa pilikapilika zilizidi.
Mwalimu mkuu mr. Maige alikuwa akipiga simu kila wakati. Dakika chache baadaye polisi waliwasili eneo la shule, ving’ora vyao vikali vilinishitua nilijua kabisa mwisho wangu umekaribia, waliingia wakiwa wameongozana na madaktari pamoja na wandishi wa habari. Nilijua tukio lililokuwa mbele yangu sio dogo.
“Nini kimetokea?” polisi walianza kumhoji mkuu wa shule.
Mkuu wa shule alinyoosha kidole kwangu nilishituka sana,
Nilijua angeweza kujielezea yeye mwenyewe, Mungu wangu nitawambia nini mimi hawa Mungu nisaidie mimi niondoe katika mzigo huu, nilisali kimoyo moyo.
Polisi walinikata jicho na kisha wakanisogelea, wakanishika kama mtuhumiwa rasmi na kisha kunikokota nje kwa nguvu,
mkuu wa operesheni ile aliamrisha “piga picha za tukio na rekodi hali nzima ya tukio mimi nampeleka huyu polisi kuhojiwa na baada ya hapo mwili huo upelekwe hospitali kwaajili ya uchunguzi” aliongea na kuondoka.
Nilikokotwa na kupitishwa katika korido za madarasa watu wote walinishangaa Martin alishindwa kujizuia na kuuliza nini kinaendelea, polisi walimsukuma pembeni na kupita hakuna aliyejali, Martin alilia sana nilimtizama Martin huku machozi yakinitiririka.
Nilimwonesha kwa ishara kuwa kila kitu kipo sawa awe na amani.
Niliondoka na polisi hadi kituo cha polisi cha kati mkoni mwanza, niliogopa sana ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika polisi hakika nilitetemeka ee mungu wangu,
eee yesu wa majeshi uliyewavusha wana wa Israeli katika bahari ya shamu naomba unitetee ukinitoa katika kifungo hiki jehova nitakutumika wewe siku zote,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
siku hiyo nilikumbuka kusali tena kusali kwa kumaanisha huku nikibeba vifungu vya biblia ambavyo hata sikujua vinatoka sehemu gani.
Na wala sikuwa nafahamu mara ya mwisho nilivisoma lini.
Kweli shida hutufanya tumkumbuke Mungu.
Niliingizwa katika chumba ambacho nilihisi moja kwa moja ni chuma cha mahojiano.
Hakika kilinitisha sana,
Walinikagua hawakunikuta na kitu chochote kile.
“Mwanafunzi” sauti kali ya polisi wa kike iliinita,
niligeuka huku nikitetemeka jasho na machozi vikinitoka kwa pamoja.
Mkuu wa upelelezi alikaa mbele yangu alikuwa ni mbaba mtu mzima mwenye umri kati ya miaka 42-43 alikuwa na sura ya upole wala hakuendana na cheo alichokuwa nacho alinitazama.
“Jina lako ni nani?”
Polisi wa kike alikuwa pembeni yangu aliniuliza, mwanadada huyu alionekana kuwa katili sana na mwenye dharau tena alikuwa jeuri.
Alikuwa akiongea na mimi kama mtuhumiwa ambaye alikuwa akitafutwa muda mrefu sana na hatimaye siku hiyo alinasa katika mtego
“Jina lako ni nani wewe kahaba” aliniuliza kwa dharau na kwa kejeri,
Nilishindwa kuongea midomo ilinitetemeka.
Hatimaye mkuu wa upelelzi ambaye nilikuja kujua kwamba alikuwa akiitwa afande Lodrick aliniuliza alimwambia askari yule wa kike samahani naomba utupishe ingawa hakuridhia na uamuzi huo yule askari hakuwa na jinsi ni amri kutoka kwa bosi wake alipiga saluti na kuondoka tulibaki wawili tu.
Kwa kiasi fulani nilipatwa na ujasiri wa kuongea nilimwamini huyu mbaba kuliko yule mwanamke.
“Unaitwa nani?” aliniuliza,
“Naitwa Catherine kindamba”
“Catherine unaweza kutuambia ni nini kimetoke hata tukamkuta msichana yule akiwa katika hali ile?”
Nilisita nimwambie ukweli , nikimwambia ukweli nimejimaliza, kanisani tumefundishwa kuongea ukweli na sio uongo sijawahi kudanganya.
Upande mwingine uliniambia Cathe bado una nafasi ya kuishi kama utatumia ulimi wako vizuri na ukijiamini.
Ni kweli nimefundishwa kutodanganya lakini siku moja tu haitokuwa vibaya kumbuka unatetea nafsi yako.
Nilishikwa na ujasiri wa ajabu.
“Nilikuwa nimeenda chooni kwa ajili ya kujisaidia nilimkuta Candy amedodoka na anavuja damu.”
“Ina maana hujui nini kimemtokea Candy?”
“Hapana sijui”
“Unaweza kuzungumzia mazingira halisi”
“Niliingia darasani nikaambiwa kwamba natafutwa na Candy na ameelekea chooni nilikokuwa”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ikabidi nitoke nimfate Candy huko chooni nikamkuta hivyo.” “Inamaanisha Candy alikuwa anakutafta kabla hajadondoka”
“Ndio sijui ni nini kimemtokea hata akadondoka niliongea kwa upole.” “Sawa binti tunashukuru kwa ushirikiano wako tukikuhitaji tutakuita tena.” Nilitolewa nje nikapandishwa kwenye gari nikarudishwa shuleni.
Kurejea kwangu kuliamsha kelele zisizo na mpangilio kila mtu alitamani kujua ni nini kimetokea, nilikuja kujua kwamba wanafunzi walipewa taarifa juu ya tukio lilitokea na kuhusu kukamatwa kwangu.
Niliporejea niliitwa moja kwa moja kwa mwalimu. “Cathe ni nini kimetokea?” mwalimu maige aliuliza. “Mwalimu nimemkuta Candy akiwa ameanguka kule chooni” “Mungu wangu amepatwa na nini huyu binti?”
“Sijui mwalimu ni tukio la kuogofya sana nimelishuhudia” “Sijawahi kuona tukio la hivi niliongea nikiwa nalia”
“Pole Cathe ni sehemu ya maisha jipe moyo Candy atapona na atarejea” “Usijali hiyo ni mipango ya Mungu Candy atapona na atarudi” nilishikwa na mshangao.
Inamaana Candy hajafa, nilijiuliza, mungu wangu kupona kwa Candy ni kifo changu Mungu wangu nifanye nini mimi nilibaki nimeduwaa,
sauti ya maige ilinishitua
“Nenda bwenini ukapumzike”
Niliamka kiunyonge nikitetemeka nilishindwa kutembea nilijikuta nimedondoka ghafla nikaona giza mbele yangu sikujua nini kimeendelea tena.
Nilishituka na kujikuta nimelala katika zahanati ya shule, dripu zikichuruzisha maji mwilini mwangu, nilihisi maumivu makali sana ya kichwa na macho pia yaliniwia mazito, uchovu ulinitawala, na mwili mzima ulikuwa ukiuma, sikufahamu ni kitu gani kimetokea hata nikafika hapo.
Kumbukumbu zangu ziliniwia vigumu sana kunirejea nilibaki nikiwa nimelala hapo kitandani sikuweza kujiinua, nilipogeuka upande wa pili nilikutana na nesi akiwa anaongea na wanafunzi wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.
Nilipata shida sana kuwatambua kuwa alikuwa ni Martin na Martha.
Baada ya maongezi mafupi Martin aliyekuwa amebeba hotpot na Martha waliongozana kuja kitandani kwangu walipofika walinipa pole na kisha kukaa kwenye kitanda cha pembeni.
Martin alinishika kichwani akiushusha mkono wake usoni mwangu kisha akaniambia “pole Cathe” aliongea kwa sauti yake nzuri ya kiume.
“Asante Martin”
“Nesi amesema unaendelea vizuri unaweza kuruhusiwa kuanzia leo”
“kwani nimelazwa hapa tokea lini?” niliuliza.
“Tokea juzi huko hapa”
“Ninaumwa nini?!” Niliuliza kwa mshangao,
“Ulipatwa tu na mshituko kidogo baada ya kutoka polisi”
Alipotaja polisi kumbukumu zilianza kunirejea,
“Mungu wangu”
“Candy anaendeleaje?” Niliuliza kwa kiherehere ,
“Candy anaendelea vizuri hali yake imetengemaa sasa”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha”
Niliwaza “Candy akipona nimekufa, Candy akipona tu ndio mwisho wa maisha yangu”
“Mbona umeshituka sana?”
“Hapana” niliongea kwa kigugumizi,
“Namwombea Candy apone” nilisema,
“Kila mtu anamwombea kwa kweli hatujui amepatwa na nini, kupona kwake ndipo kutakapojibu maswali yetu yote”, akili ilizidi kwenda kasi,
“nifanye nini mimi?”, nilijiuliza.
“Ndio”
Mwishowe nilijibu, huku nikionesha kunyong’onyea.
Martin alifungua hptpot na kuanza kunilisha chakula, kilikuwa ni chakula kizuri sana tofauti na ambacho tunakula hapo shuleni.
Martha aliniangalia kwa huruma sana,
“pole wifi” alisema.
Niligeuka na kumwangalia Martha,
“Asante” nilijibu.
“Cathe” Martin aliniita,
“Bee” niliitika.
“Sikuwahi kukwambia kwamba Martha ni mdogo wangu” aliniuliza,
“Whaat?”
“Ndio, Martha ni mtoto wa baba yangu mkubwa”
“Tangu nilipopoteza ufahamu ni kitu cha kwanza kilichonipa faraja,
“Nafurahi sana kukufahamu Martha”
“Usijali”
Nilikula nikiwa katikati ya watu hao walionionesha upendo, nilijisikia amani sana kuwa katikati yao.
Baada ya muda alikuja nesi,
“Martha inabidi ukakae na Cathe ili umwangalie, tunamruhusu leo kwa sababu hali yake inaendelea vizuri, tutakupa dawa za kutumia ukisikia maumivu yoyote urudi hapa, Sawa Cathe” nesi alisema kwa sauti yake ya upole.
“sawa asante” nilishukuru kwa sababu sikupenda kuendelea kuwepo hapo.
Walinisaidia kukusanya vitu vyangu na kisha nikarejea bwenini.
Martin alinibusu mdomoni kisha akaniacha nikiwa na Martha.
“Martha, naomba uniangalizie mke wangu” alisema Martin.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliachia tabasamu, nilipenda alivyoniita.
“Mchumba tutaonana baadae” alisema kisha akatoka.
Nilitamani aendelee kuwepo karibu yangu ingawa ilikuwa kinyume cha sheria za shule kuwepo katika mabweni ya wasichana.
Aliniacha na Martha
Martha alikuwa akinitunza vizuri sana hakika nilifurahi.
Baada ya muda kupita hali yangu iliweza kutengemaa kabisa na nikaweza kuingia darasani, nilijitahidi kujiamini mbele ya kila mtu ili nisihisiwe kwa tukio lolote. Nilijitahidi sana kuomba mungu aniepushe na tatizo hili
“ee mungu ingawa sio vizuri lakini naomba uichukue roho ya Candy, kumwacha Candy hai ni kuniingiza mimi mkwenye matatizo, mbona umesha nitesa sana hebu saa hizi tu basi unionee huruma na mimi, na mimi niishi kwa amani, Mungu naomba usikie maombi yangu”
Niliomba maombi hayo huku nikiwa sina imani ya kujibiwa.
Nilikata tamaa kabisa.
“Candy usipokufa nitakufa mimi kwa namna yoyote ile”, nilisema.
Niliendelea kusoma kwa bidii huku nikisali.
Kila siku mwalimu alipoingia darasani hasa mwalimu Maloya alitusisitiza tuendelee kumwombea Candy kwasababu hali yake ilikuwa ikitengemaa.
Maneno hayo yalizidi kunikera, kila mara alipotangaza kuhusu hali ya Candy moyo wangu ulikosa amani kabisa.
Ilikuwa ni alfajiri siku ya jumamosi, ni siku ambayo huwa hatuamshwi mapema tunaamka pale utakapojisikia wewe kwa maana shuleni kwetu tulikuwa hatufanyi usafi hiyo siku nilitaka kulala sana.
Ilipofika saa moja kasoro kengele iligongwa, nilikerekwa sana kuamshwa asubuhi siku hiyo nilitamani kuendelea kulala, wakati kengele ikizidi kugongwa nilivuta shuka na kujifunika.
“Hawa vipi bwana ahaaa, fyuuu”, nikasonya
Martha aliniamsha “Cathe amka ni kengele ya tahadhari huwezi kujua pengine kuna tukio baya amka usikute mabweni yanaungua amka haraka”,
nilishuka haraka na kutoka nje huku nikiwa nimevaa night dress.
Martha alicheka “wewe hebu rudi uvae nguo wewe vipi?”, aliongea kwa utani.
Moyo wangu ulikuwa hauna amani kabisa,
niliwaza “sijui polisi wamekuja kunifata tena, mungu wangu kama hali ya Candy ikitengemaa inamaanisha anaweza kuongea na angewasimulia polisi kila kitu, kwa maana mara zote walikuwa wakimsubiria apate unafuu ili aelezee tukio zima, ameelezea na sasa hivi nakuja kufatwa na polisi, ee mungu wa majeshi sijui nikimbie” niliwaza.
“Mi siendi” nilimwambia Martha,
“amna usiogope hamna tukio la ajabu”
“Hapana moyo wangu unasita kabisa kwenda”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Twende tu Cathe hakuna jinsi”
“Mi nabaki naomba uende utaniambia”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment