Simulizi : High School
Sehemu Ya Nne (4)
niliwaza “sijui polisi wamekuja kunifata tena, mungu wangu kama hali ya Candy ikitengemaa inamaanisha anaweza kuongea na angewasimulia polisi kila kitu, kwa maana mara zote walikuwa wakimsubiria apate unafuu ili aelezee tukio zima, ameelezea na sasa hivi nakuja kufatwa na polisi, ee mungu wa majeshi sijui nikimbie” niliwaza.
“Mi siendi” nilimwambia Martha,
“amna usiogope hamna tukio la ajabu”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana moyo wangu unasita kabisa kwenda”
“Twende tu Cathe hakuna jinsi”
“Mi nabaki naomba uende utaniambia”
“Unaogopa nini?” Aliingiwa na ghadhabu,
niliogopa anaweza kunishitukia huyu,
“Sawa twende, Ila nilikuwa na woga kweli kwenda huko”
“Hamna usiogope wifi yangu we twende tu”
Tuliongozana hadi kufika mstarini, tulikuwa watu wa mwisho mwisho kufika kwa maana watu wengi walikuwa washafika.”
Walimu wote walikuwa katika eneo hilo, niliingiwa na uwoga sikuwa najiamini hata kidogo mwili mzima ulikuwa ukitetemeka,
“unatetemeka nini Cathe” sauti ya Martha ilinishitua.
“Hapana, ila nahisi kuna kitu hakipo sawa, sijui ni nini” niliongea.
“usijali kila kitu kitakuwa sawa”
Tulijongea mstarini.
Walimu walisubiri hadi kelele zote ziishe, baada ya wanafunzi kunyamaza kimya na kuonyesha kuwa tayari kwa kusikiliza tulichoitiwa mapema asubuhi hiyo, mwalimu mkuu Mr. Maige alisogea mbele kututangazia kitu ambacho walikusudia kwa asubuhi hiyo.
Shule nzima ilikuwa kimya kusikiliza ni kitu gani ambacho tungetangaziwa. Baada ya ukimya wa mda mfupi Mr. Maige alisimama mbele ya wanafunzi wote, alikohoa kidogo kurekebisha koo lake na kisha kuanza kusema kwa sauti iliyonyong’onyea,
“Hamjambo wanafunzi”
“Hatujambo” tuliitikia na kisha ukimya mzito ukafatia.
“Poleni kwa masomo natumaini mko salama wote, lakini kuna jambo moja ningependa kuwaambia wanafunzi, shule imepata msiba mzito,tumempoteza mwanafunzi mwenzetu Candy Carry”
Vilio vilianza watu walilia, sio wanafunzi peke yake hata walimu pia.
Nilishusha pumzi nzito kisha machozi yalianza kunitoka, ingawa mara zote nimekuwa katika maombi nikiomba mungu amuondoe Candy duniani, lakini kifo cha Candy kiliniuma sana.
“Uwepo wangu hapa shuleni umesababisha kifo cha Candy, nisamehe Candy, Mungu naomba unisamehe pia”,
Mwalimu Maloya alilia sana, Nikama vile hakuwa akijua chochote hadi wakati huo tulipotangaziwa.
Alionekana akiwa na huzuni wakati wote, baadhi ya walimu walimfariji Maloya alikuwa akilia kuliko kawaida, wanafunzi wengi walikuwa wakinitupia macho kujua ningezipokeaje taarifa hizo sikupenda jinsi walivyokuwa wakinitazama.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikajifanya nimezimia.
Nilibebwa na kupelekwa hospitalini, nikawekewa drip za maji ingawa kiukweli sikuwa nimezimia sikutaka kuamka wakati huo, nilitaka kufikiria upya kuhusu hilo swala na jinsi maisha ambavyo yangeenda.
Nililala hapo siku nzima, huku taratibu za kuuaga mwili wa Candy hapo shuleni zikiendelea kufanyika.
Vipindi vilihairishwa kila mtu alikuwa na huzuni sana kuhusu kifo cha Candy.
Ulipofika wakati wa jioni hali bado nikiwa nimefumba macho yangu nilihisi mtu akiingia.
Nilifumbua jicho kwa mbali ili kuweza kutazama ni nani kwa maana huo haukuwa wakati wa kuona wagonjwa, nilitamani awe Martin ili kunifariji kwa wakati huo.
Hakuwa Marti alikuwa Maloya, alipofika nesi aliingia,
“bado hajarudiwa na fahamu, anahitaji muda mwingi wa kupumzika akili yake haiko sawa.”
“Sawa” Maloya alijibu,
“nimekuja tu kumwangalia, nitaondoka muda si mrefu hauna haja ya kuhofu nesi.”
“Sawa” nesi aliitikia na kuondoka. Alituacha mimi na Maloya.
“Wewe mshenzi ninajua kuwa unahusika na kifo cha Candy, utakapoamka hapo utanieleza. Nitapambana na wewe na kuhakikisha kwamba unapata adhabu stahiki, lazima uhukumiwe kwa kosa la kumuondoa kipenzi changu. Unajua mimi na Candy tumetoka wapi? Wewe kidudu mtu ama zako ama zangu” aliongea kwa hasira kwa sauti ya chini huku machozi yakimtoka.
Alinisonya na kisha kuondoka kwa ghadhabu. Nilipata kujua kwamba Maloya amefahamu kila kitu kilichotokea.
Moyo uliniuma sana nilijua nimeimaliza kesi kumbe ndio nimeianza.
Jela ilikuwa ikiniita.
Nilikata tamaa ya kuendelea kuishi.
Kitu pekee cha kufanya ni kuondoka tu hapa.
“Sijui nitoroke sasa hivi, nikitoroka saa hizi itajulikana kwamba ninahusika kwa namna Fulani, kwanini niondoke.”
Mwili wa Candy uliagwa nikiwa hospitali na ulisafirishwa kuelekea Arusha kwa maziko, kila mtu alikuwa na huzuni sana, Maloya akiambatana na wanafunzi wawili akiwemo Naima waliondoka na mwili wa Candy kuelekea Arusha.
Ilichukua muda watu kurejea katika hali ya kawaida kisha maisha yaliendelea.
Maisha ya shida yalianza hapo shuleni nilikuwa nikipokea vipigo mara kwa mara kutoka kwa Maloya, nilikuwa nikipigwa sana,adhabu za mara kwa mara hazikuniisha.
Martin alikuwa akinionea huruma sana, wakati mwingine alikuwa akijitahidi kunisaidia baadhi adhabu nyingine nilizokuwa nikipewa.
“Cathe una una nini na maloya? siku moja aliniuliza nilishindwa cha kumjibu,
“kwanini akutese hivi umemfanyia nini yeye? Mimi siwezi kuendelea kuvumilia nitamfata”
Nilimshika mkono na kumzuia,
“Unaenda wapi” niliongea kwa upole.
“Namfata Maloya kwanini anakupiga na anakupa adhabu kila siku nimechoka hata mimi siwezi kuendelea kuvumilia namfata.”
“Hapana subiri” niliongea.
“Siwezi kuendelea kusubiri” nilimzuia.
“Martin sitaki kukwambia siri ya Maloya kunichukia, utaumia sana.”
Kwa muda mchache aliweza kutuliza hasira aliyokuwa nayo.
“Naomba uniambia, sitachukia”
“Najua”
“hujui kitu Martin” nilimwambia.
“Hapana Cathe niambie”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nitakwambia, ngoja nipate wakati mzuri nitakwambia kila kitu” nilimwambia.
Alitulia na kisha kuendelea na mambo yake.
Baba Candy, Mr. Carry alikuwa mbogo hakutaka kuamini kwamba Candy alikufa kwa kudondoka mwenyewe bafuni, alitaka uchunguzi ufanyike ili kujua chanzo cha kifo cha Candy.
“Lazima nimjue mtu aliye husika na kifo cha mwanangu na nitampoteza” alisema.
Mara moja uchunguzi ulianza kufanyika, nijikuta naishiwa nguvu.
Kilichoniogopesha zaidi ni kugundua kuwa……………
Niliogopa sana kujua kuwa nilikuwa nina ujauzito, sikuwa najua kama ujauzito ni wa Maloya au wa Martin.
Nililia sana, nafsi iliniuma mno, kila ninapojitahidi kutoka kwenye tatizo moja linakuja jingine,
“ eee Mungu wangu kwanini umeniacha mimi? Nimezaliwa kwa ajili ya kuteseka tu, ee Mungu wangu, bora basi ungeichukua roho yangu na mimi nipumzike” nilijikuta nikimkufuru Mungu.
Nilishindwa kufanya kitu chochote kile nilishindwa kula vizuri nilishindwa kusoma hata usingizi uliniwia shida sana kupata. Nilianza kukonda tena.
Ujauzito wangu ulikuwa ukinilazimisha kulala usingizi kila wakati, nilikuwa nasinzia sana, nilihisi unaweza ukawa mkubwa kwasababu hata sikuwa najua una miezi mingapi.
Nafsi iliniuma kuona kwamba sitaweza kuendelea na shule. Tumbo langu lilianza kuonekana, nilijitahidi sana kujizuia lisionekane. Nilimkumbuka sana Candy,
“nilikuwa namsema Candy sasa ni zamu yangu” nilijiwazia,
“nitamwambia nini baba yangu siku akigundua kuwa nina ujauzito?” niliwaza.
“Eee Mungu wangu najikabidhi mikononi mwako”, nilimalizia maombi yangu.
Hesabu zangu ziliniambia kuwa ujauzito huo ni wa Maloya, kwasababu yeye ndio aliyekuwa mtu wa mwisho kukutana na mimi kimwili. Hivyo basi ujauzito huu ulikuwa na takribani miezi minne, kwa hesabu zangu ningeweza kujifungua wakati uliokaribia sana na mtihani, aidha mwezi wa nne ambapo tulitegemea kuanza mitihani mwezi wa tano mwanzoni, mitihani ya kumaliza shule. Hivyo basi endapo nisingeitoa hiyo mimba nisingeweza kufanya mtihani.
“Niitoe” niliwaza
“hapana siwezi kuitoa hii mimba, nimuue kiumbe asiye na hatia siwezi kujua mungu amempangia nini kiumbe wake, siwezi kuitoa hii mimba” nilisita sita sita katika mawazo mawili. Nafsi nyingine ikiniambia unahitaji kusoma, zaidi ya sana unamuhitaji Martin endapo Martin akigundua kwamba una ujauzito wa Maloya mapenzi yenu yatakuwa yameishia hapo, potelea mbali lolote na liwe.
Uchunguzi kuhusu kifo cha Candy ulianza mara moja, Mzee Carry baba yake Candy hakutaka masihara katika hilo, alitoka Arusha na kuja Mwanza kusimamia kesi hiyo, alitaka kuona kwamba aliyehusika na kifo cha mwanae anakamatwa na kuhukumiwa.
Kwa kuanzia mwalimu mkuu aliitwa polisi kutoa maelezo, alieleza kila kitu ambacho alikijua kuhusiana na tukio hilo.
Alirejea shuleni kwa upole sana, kisha akagonga kengele na kutuita wanafunzi wote mstarini, tulienda, alituambia mambo yote ambayo yalitokea hako polisi, maneno yake yalinitikisa sana,
“Cathe” alisema, nilitetemeka
“polisi wamesema endapo watakuhitaji watakuita tena ila kwa sasa hawakuhitaji kwasababu ulishatoa maelezo mara ya kwanza” alisema,
“ee mungu wangu naomba unifanyie miujiza” nilisali kimoyomoyo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya hapo wanafunzi wengi walisogea kunipa pole akiwemo Martin.
Nafsi yangu ilikosa amani kabisa Martin aliligundua hili ingawa akuniuliza.
Mtu wa pili kuitwa kwaajili ya kutoa maelezo ni Maloya. Nafikiri polisi waligundua uhusiano wa karibu kati ya Maloya na marehemu Candy, aliitwa kutoa maelezo, nilijua mwisho wangu umekaribia .
Maloya alianza kujieleza “mimi ni mtu wa karibu sana na Candy na pia ni mwalimu wake”
“ukaribu wenu uko vipi?” aliulizwa,
Maloya alishindwa kutoa maelezo mazuri, mara nyingi alikuwa akijing’atang’ata, nafikiri alikuwa akihofia kuweka wazi uhusiano wake na Candy ukizingatia baba yake na Candy alikuwepo hapo na hakuwa akipenda utani kabisa.
Siku Candy anafariki Maloya alikuwepo, polisi walitaka kumuhoji kwasababu alikuwa akiendelea vizuri. Walipoingia walikutana na Maloya akiwa ameketi kitandani pembeni ya Candy tunataka kumhoji Candy
“sawa na mimi naomba niwepo”
“we kama nani?” polisi waliuliza,
“mimi ni mpenzi wake” alijibu.
“Sawa”
Candy alianza kujieleza, aliongea kwa shida sana kutokana na hali yake ilivyokuwa, alikuwa akijitahidi sana kuongea ingawa alionekana kushindwa, askari aliyekuja kumhoji, alishindwa kuelewa nini cha kufanya aidha ahairishe mahojiano hayo au aendelee kumtia moyo Candy aongee mara simu yake iliita, alinyanyuka na kuelekea nje Candy aliweza kuongea neno moja, alitaja jina langu na kisha kukata roho.
Na hii ndio sababu aliyofanya Maloya ahisi na ajue kwamba ninahusika kwa namna moja au nyingine na kifo cha Candy.
Pamoja na hayo yote maloya alishindwa kujieleza. Baba yake na Candy alikasirika sana,
“wewe ni mwalimu una taaluma ya ualimu nimemleta mwanangu kumfundisha unamfanya mkeo, nitadili na wewe kwanza, aliongea mzee Carry,
“huyu afunguliwe mashitaka ya kutembea na mwanafunzi”, alisema.
Maloya alilia sana alishindwa kujitetea, aliwekwa mahabusu kusubiria kesi yake ianze.
Ripoti ya daktari ilisaidia kummaliza Maloya, Candy alikufa baada ya kugongwa na kitu kizito kichwani, hivyo damu kuvijia katika ubongo, lakini pia alikuwa na ujauzito mkubwa.
Mzee Carry alikasirika sana alisahau kabisa kuhusu swala kifo cha binti yake aliamua moja kwa moja kuhusika na Maloya ambaye moja kwa moja alionekana kuwa ndiye aliyekuwa akihusika na mimba ya Candy, ilikuwa ni afuheni kwangu.
Nilikuwa na tabia ya kurekodi matukio yote yaliyokuwa yakinitokea kwenye kitabu change cha kumbukumbu, mimba yangu ilizidi kuwa kubwa hata hivyo nilishindwa kumueleza Martin, sikuwa najua wapi nianzie.
Nilipanga kutoroka ili nisije kushitukiwa kwa ujauzito niliokuwa nao, lakini nisingeweza kuondoka bila kumwaga Martin, niliwaza nitamwambiaje?
Nilivuta pumzi ya nguvu na kisha kuishusha,
“nitafute uongo gani? Nitamwambia Martin kuwa hii mimba ni yakwake na hivyo napenda yeye aendelee kusoma hivyo basi naondoka ili asije akatafutwa kwa kosa
la kunipa mimba, tutaonana uraiani” nilipanga kumwambia hivyo, hali nikijua kabisa ujauzito huo sio wa kwake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilimwita Martin, baada ya kutoka prepo usiku,
“Martin nataka nikwambie kitu”
“nakusikiliza mke wangu mtarajiwa” niliachia tabasamu hafifu, ingawa niliumizwa na maneno yake nilijua kwamba hakuna ndoa kati yangu mimi na yeye hasa akijua kwamba nina ujauzito ambao sio wa kwake.
“Martin napenda sana tutimize ndoto zetu ingawa kwa upande wangu naona ni vigumu sana kutimiza” niliongea.
“Unamaanisha nini Cathe”
“nakupenda sana Martin, sana zaidi ya unavyofikiria napenda usome, utimize zile ndoto ambazo hata baba yako pia anapenda kukuona siku moja unafikia, upate shahada yako, upate kazi nzuri, uitunze familia yako ya sasa hivi na baadae”, niliongea kwa uchungu sana.
“Naelewa, naelewa baba yangu anatamani sana nifike sehemu ambayo natamani kufika na ndio maana kila mara nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii”
Maneno yake yalinichoma sana.
“Martin nina ujauzito” sikutaka kusema ni wa nani.
Nafsi yangu iliniwia vigumu sana kumdanganya, hakika alishituka,
“Cathe una uhakika?” aliniuliza kwa sauti ya utulivu na upole,
“ndio” nilisema, alinitazama kisha akashusha sura yake kwa huzuni, alibaki amejiinamia tu pale.
“Nimeamua kuacha shule ili nikupe nafasi wewe uendelee kusoma”, nilisema
Alinyanyua uso wake na kunitazama, tayari uso wake ulishakuwa umelowa machozi, moyo uliumia sana, alishindwa kuongea neno lolote.
“Martin usijali kuhusu mimi, nakupa nafasi hii ya kusoma, usome kwa ajili yako na usome kwa ajili yangu, naenda kuanza kumtunza mtoto” niliongea.
Alinivutia kifuani kwake akanikumbatia,
“nitakapo ondoka naomba usome kwa bidii zote sahau kama nilishawahi kuwepo hapa, Soma sana, Sali sana, kula sana, uwe na nidhamu, tunza mapenzi yangu moyoni mwako” niliongea kwa huzuni huku machozi yakinitiririka.
“Ombi langu la mwisho kwako Martin, naomba unisaidie kuondoka hapa shuleni”, alishindwa kuongea lolote alinikumbatia kwa nguvu huku akilia, nilishukuru Mungu tu kwa hilo sikuwa na jinsi.
Alfajiri na mapema ya siku iliyofuata tulikutana na Martin darasani, alikuwa ameniletea begi lake la madaftari, weka humu nguo zako na kila kitu ambacho unahitaji kuondoka nacho nitatangulia kwenda mjini tutakutana huko.
Tukutane stendi usiondoke na begi lako la nguo ilkiwezekana nikabidhi, nilifanya kama alivyosema, nilimkabidhi begi langu kubwa la nguo nilibeba vitu vyangu vichache nilivyovihifadhi katika begi lake la madaftari, niliomba ruhusa shuleni, kana kwamba naelekea mjini, nikiwa na yunifomu zangu.
Nilipotoka nilienda moja kwa moja dukani kununua nguo ambazo ningezitumia kwa ajili ya kusafiria nilipofika stendi nilikutana na Martin, alikuwa akinisubiria hapo, alionekana mwenye huzuni kuliko siku zote. Alishanikatia tiketi alinikabidhi tiketi yangu muda ulipofika nilipanda kwenye gari kwa ajili ya kurejea nyumbani Dar.
Ulikuwa ni wakati wa huzuni kuliko wote kupata kutokea katika maisha yangu niliachana na Martin siku hiyo, njia nzima nilikuwa nikilia tu.
Nilifika Dar usiku sana, sikuweza kuelekea nyumbani wakati huo hivyo nililala hotelini.
Asubuhi ya siku iliyofuata nilibeba begi langu kuelekea nyumbani, nilitembea kiunyonge sana nilipokaribia kufika nyumbani. Niliwaza naenda kumwambia nini baba na nimerudi kabla shule haijafungwa.
Niliingia nyumbani kwetu, hali niliyoikuta ilinipa afuheni kidogo nyumba haikuwa chafu ilikuwa imetunzwa vizuri. Niliingia ndani nikitetemeka sana. Nilimkuta baba akiwa amekaa sebuleni alishangaa sana kuniona,
“Cathe umerudi mama”,
“ndio”
“karibu tena nyumbani” alisema
“Asante baba”
Nilishangazwa baba hakuwa na maneno mengi.
Nilielekea chumbani kwangu kisha nikalala usingizi mzito. Na kuamka jioni ya siku hiyo nikiwa nimechoka sana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baba yangu alikuwa amedhoofu sana, lakini hakuwa tena akinywa pombe wala akivuta sigara, muda mwingi alikuwa akiutumia kuwepo nyumbani akifanya mazoezi, akijitahidi kula vizuri, afya yake haikuwa kama mwanzo.
Nilifurahi kujua kwamba baba sasa amejitambua na ameelewa umuhimu wa afya yake.
Niliendelea kukaa na baba, hakuniuliza hata siku moja kuhusu kurejea kwangu kabla ya muda sikuwa najua baba amepanga nini kuhusu hilo na mimi niliendelea kunyamaza kimya.
Takribani mwezi ulipita.
Asubuhi ya siku hiyo baba alijiandaa mapema sana.
Kisha alikuja chumbani kwangu na akanigongea mlango niliamka na kutoka nje nikiwa na uchovu sana.
“Cathe mimi naelekea kliniki, hatuwezi kwenda wote?” alisema
“Aaah, Baba unaenda kiliniki ya nini?”
“Aaah, Mwanangu nahudhuria kliniki ya kansa kwa ajili ya matatizo ya ini langu” alisema
“Aaah, Ngoja nijiandae basi tuongozane”
“Sawa maana nimeona ujauzito wako unazidi kukua na hujawahi kuhudhuria kliniki hata siku moja.”
Moyo ulinipasuka paaaa…….!!!!!
Sikutegemea kujua kwamba baba anafahamu kuhusu ujauzito niliokuwa nao, uso ulinishuka kwa ashuo, niliinama kwa aibu huku nikiwa nimepwaya, nilishindwa kuongea chochote wala kumtazama baba alikuwa amesimama mbele yangu
“Catherine” baba aliniita.
“Bee” niliitika bila kunyanyua uso wangu.
“Tutakaporudi kutoka hospitali tutaongea, jiandae kwa ajili ya kuelekea hospitali”
Aliongea baba na kisha kuondoka, sikupata hata nafasi ya kumjibu.
Niliingia chumbani kwangu na kuketi kitandani,
“Mungu wangu baba akiniuliza kuhusu ujauzito nimtaje nani?”
“Nitamwambia nini mimi?”
Nilishusha pumzi ndefu.
“Eee Mungu naomba uniongoze katika hili” niliendelea kusema.
Nilijiandaa kwa unyonge nilivaa gauni pana pana ambalo lilificha tumbo langu na kisha tukatoka na baba kwa ajili ya kwenda hospitalini.
Niliingia kwenye gari nikiwa na uoga sana niliketi siti ya nyuma wakati baba akiwa dereva.
Tuliongozana mpaka hospitalini muhimbili, tulianza kwa baba ambapo alihudhuria katika kitengo chake alichotakiwa kwenda na baada ya hapo alinipeleka kliniki.
“Baba wa huyo mtoto wako mtarajiwa yuko wapi?” swali la kwanza kwa nesi.
“Na kwanini umechelewa kuhudhuria?”
Baba alimtazama nesi,
“Amekuja na mimi hapa baba yake” aliongea, nilijisikia aibu sana nilishindwa hata kumtazama nesi usoni, nesi aliishiwa pozi wala neno la kuongea alinihudumia,
“umechelewa sana kuanza kliniki mimba kubwa ya miezi mitano” alisema.
Sikujali.
Nilihudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na maendelea ya mtoto wangu yalikuwa mazuri nilirejea nyumbani.
Tulipofika nyumbani nilipitiliza moja kwa moja chumbani kwangu, wakati nafungua mlango kuingia chumbani kwangu baba aliniita,
“Catherine njoo tuongee”
mwili mzima ulikuwa ukitetemeka nilishindwa cha kufanya, nilirudi sebuleni kiunyonge nikakaa.
“Mwanangu naomba unisamehe kwa yote yaliyotokea katika maisha yako, najua kama sio sisi wazazi wako yote yasingekupata.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilishindwa kuelewa namaanisha nini hata hivyo niliogopa kuuliza kwa sababu hapo mimi ndiye niliokuwa na makosa.
“Mwanangu, laiti kama nisingesababisha kifo cha mama yako, mama ako angekuwa anakuhudumia na akikufundisha. Mimi na mama yako tulikuwa na migogoro mingi hapa nyumbani na nafikiri ilikuathiri kwa kiwango kikubwa, kama mtoto wetu ulipaswa upate malezi bora, tukutunze, tukujenge katika hali ya kujiamini ambayo ingekuwezesha wewe kupambana na kila aina ya matukio unayokutana nayo katika maisha yako lakini hatukuweza kuyafanya hayo yote na ndio mana hata sasa uko hapa. Sikushituka sana siku ya kwanza tu uliporudi niligundua kuna tatizo haliko sawa, sikutaka kukuliza kwa sababu najua mimi ndio chanzo cha haya yote, nilikuja kugundua kuwa una ujauzito hata hivyo nilishachelewa nisingeweza kukufanya jambo lolote ningeweza kukupiga, sio kwamba sikukasirika, nilikuwa na hasira sana lakini isingesaidia kitu chochote, ila ukae ulee ujauzito, ujifungue, utapata second chance sawa mwanangu uwe tu na amani.”
Nililia sana.
Baba aliongea maneno mazito kiasi yaliniumiza moyo wangu pia ilikuwa ni ukweli mtupu, nilishusha pumzi ya faraja maisha yaliendelea.
Huko Mwanza kesi dhidi ya Maloya ilizidi kuendeshwa, alikutwa na hatia kutembea na mwanafunzi na kumpa mimba na kisha akahukumiwa jela miaka thelathini.
Kwa upande wangu sikutaka kuendelea kuwasiliana na Martin tena nilijua kufanya hivyo ni kujiumiza tu, ipo siku angegundua huu ujauzito sio wa kwake na angeniacha, nilikuwa sitaki kuachwa ni bora nimwache mwenyewe.
Niliamua kubadilisha laini, niliitupa laini niliyokuwa naitumia ambayo Martin alikuwa akiifahamu niliivunja na kuitupa mbali na kisha nikasajili laini mpya, na huo ulikuwa mwisho wa mawasiliano kati yangu na Martin.
Baada ya baba yake na Candy kuridhika na hukumu ambayo Maloya alipewa sasa aligeukia kuhusu kesi ya kifo cha mwanaye.
Taarifa mbalimbali zilianza kukusanywa ili kumbaini mtu ambaye alihusika na kifo hiko.
Nilifatwa shuleni kwa ajili ya kutoa ushahidi na ikagundulika kuwa sipo.
Mwalimu alishikwa na fadhaa sana kupata taarifa kwamba nimeondoka shuleni, alishindwa kuelewa ni kwasababu gani, inawezekana huyu mtoto anahusika na kifo cha Candy kwanini atoroke.
Martin alitamani kunitetea lakini alishindwa angesema mimi nina ujauzito si angehusishwa na huo ujauzito wangu kwa maana hakuna mtu ambaye hafahamu mahusiano yetu pale shuleni.
Alijaribu kunitafuta kwa kutumia simu hakunipata tena, alikuwa amenipoteza milele.
Niliendelea kuutunza ujauzito wangu chini ya uangalizi wa baba na baadhi ya ndugu wachache ambao waliguswa na matatizo ya familia yetu.
Shangazi yangu alihamia pale nyumbani kwa ajili ya kutuhudumia mimi na baba ukizingatia hali zetu hazikuwa nzuri
Nashukuru mungu kila kitu kilienda sawa, mimba yangu ilikuwa vizuri na wala sikupatwa na matatizo yoyote.
Nilifanya mazoezi, nilikula vizurui na kuhudhuria kliniki kila mara.
Asubuhi moja nikiwa bado nina usingizi mzito nilisikia hodi ikibishwa nyumbani kwetu, sikutaka kuamka hata hivyo sikuona kama huyo mtu ana dalili ya kuacha kugonga mlango, hodi zilipozidi niliona zinanisumbua nikatoka kiuchovu na kiunyonge huku nikiwa na hasira sana,
“kwanini shangazi hajaamka kwenda kufungua mlango mtu anagongaa.” Nilijiongelesha mwenyewe.
Nilitembea mpaka getini moyo ulinisita,
“au nirudi tu nikalale utakuta jimtu la ajabu ajabu sijui nini nini, aaaah nishafika getini ngoja tu nifungue”
nilifungua geti,
“Mungu wangu nimekwisha” nilisema.
Walikuwa ni askari wawili ambao sura zao zilionekana hazitaki masihara,
“samahani” waliongea kabla sijawasalimia,
“bila samahani”, niliongea huku nikitetemeka,
“hatuna shaka kuwa wewe ni Catherine Kindamba” alisoma kwenye karatasi lake na kisha kuniambia.
Nilijua mwisho wangu umefika, nilijibu kwa kitetemeshi,
“ndio, ndio mimi.”
Walitikisa vichwa wakaangaliana na kisha kunigeukia,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“uko chini ya ulinzi kwa kuhusika na mauaji ya Candy Carry jijini Mwanza.”
Waliongea.
Nilishusha pumzi nzito, nilishindwa la kuongea, waliichukua mikono yangu kisha kuifunga pingu.
“Naombeni basi nimuage baba yangu” nilisema huku nikitetemeka kwa woga huku machozi yakianza yakinitiririka,
“apewe taarifa kuhusu kukamatwa kwangu.”
Walinisukumiza ndani, na kisha kugonga mlango wa ndani, shangazi alifungua alishangaa kunikuta na pingu mkononi.
“Kakaaa!!” aliita kwa woga.
“Njoo uone!!”
Baba alitoka kwa uchovu.
“Hatuna shaka wewe ndiyo mzee Kindamba”
“Ndiyo, ndiyo mimi”
“Mwanao Catherine anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya mwanafunzi mwenzie katika shule ambayo alikuwa akisoma Hanspop Academy Mwanza, hivyo tunamweka chini ya ulinzi na mara moja tutamsafirisha kuelekea mwanza kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo.”
Baba aliishiwa nguvu alidondoka na kuzimia papo hapo, bila kujali polisi wale walinitoa nje na kunipandisha kuelekea katika difenda lao na safari ya kuelekea kituo cha polisi cha kati ilianza.
Nilikuwa nikilia njia nzima mungu wangu naomba uniokoe katika shimo la simba hawa.
Nilifikishwa pale kituo cha kati cha polisi, nikaandika baadhi ya maelezo kuhusu mimi na baada ya hapo nilianza safari ya kuelekea mwanza mji ambao sikutamani tena kurudi.
Machozi yakinibubujika njia nzima nilibaki nimetulia tu nikitafakari jinsi ninavyoenda kufia gerezani, niliwaza mtoto wangu aliyeko tumboni moyo uliniuma sana.
Tulifika mwanza usiku wa siku hiyo ulikuwa ni usiku sana nilipelekwa moja kwa moja kituo cha polisi na kisha kufungiwa kwenye chumba kilichokuwa na giza. Nilianza kulia upya nililia sana.
“Mtoto mdogo muuaji.”
Polisi mmoja wa kike alisema kwa dharau.
“hebu acha kelele huko unasumbua masikio yetu”, alisema.
“Eee Mungu naomba uniokoe”
Nilipiga magoti na kuanza kusali.
“Mungu naomba unisaidie, wewe unajua sikuhusika na kifo cha Candy naomba niokoe” nilisali sana.
Baada ya hapo kesi yangu ilipelekwa mahakamani.
Nilisimama mahakamani siku ya kwanza na sikutakiwa kujibu chochote hadi nitakapopata wakili wangu.
Nilimaliza kusema hayo huku nikilia, wakili alikuwa mbele yangu ambaye nilikuwa namuhadithia mkasa mzima wa maisha yangu, alikuwa akilia pia. Mwanamama huyo mrefu mweusi hakusita kuonesha huruma aliyokuwa nayo kwangu,
“pole sana binti yangu.”
“Asante”
“Umekaa hapa mahabusu kwa muda gani?”
“Nina miezi miwili”
“Pole sana”
“Asante”
“Ujauzito wako unaweza ukawa una miezi mingapi?”
“Mara ya mwisho kuhudhuria hospitali ulikuwa na miezi mitano, unaweza ukawa na miezi saba kwa sasa.”
“Pole sana”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nashukuru”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment