Simulizi : Mikono Michafu
Sehemu Ya Tano (5)
KWA haraka ya ajabu nikapata taarifa zote nilizokuwa nazihitaji juu ya Boimanda, hii inatokana na mahojiano waliyoyafanya watu wangu na wale walionivamia. Boimanda alikuwa mtumishi mwadilifu wa serikali katika wizara kadhaa na kumalizia utumishi wake ofisi ya rais ambako alikuja kustaafu. Hakuwa na utajiri kutokana na usimamizi mzuri wa sera ya ujamaa na kujitegemea, pamoja na kupitia kwenye nafasi hizo pia Boimanda alikuwa usalama wa Taifa aliyestaafu akiwa kwenye ngazi za juu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati akiwa usalama wa Taifa aliwaingiza vijana wake wengi sana, na mmojawapo alikuwa Kazikanda Moluwi ambaye sasa ndiyo Mkuu mpya. Kwa mara ya kwanza nikawa namtazama Boimanda kwa mtazamo mwingine, na nikaona bayana kilichokuwa kikimpa jeuri yule bwege aliyekuja kunihoji nyumbani kwangu.
Kwa kuanzia, ilibidi niwachukulie watu wote walioingizwa kazini na Boimanda pamoja na KM kuwa ni maadui zangu. Haikuwa rahisi kuwajua wote lakini kimsingi nikajua kuwa ndani ya taasisi yetu nyeti tayari tuna mitazamo tofauti kuusiana na mustakabali wa nchi yetu. Kwa kuogopa mtandao wetu kuvuja, tukapanga na Omari kuwaelezea vijana wetu kila kitu kuhusu mtazamo wetu na kuwa maadui zetu ni nani.
Kwanza nilikuwa nayafanya yote kwa mapenzi tu kwa nchi yangu lakini kwa sasa nafanya kwa kulipiza damu ya Mkuu na hasa damu ya Mwajuma, mrembo aliyetolewa uhai wake kwa vile tu alikuwa tu na dhamira ya kunisaidia. Kwa kweli nilikuwa naumia sana moyoni na nilijiona nina jukumu zito ila kazi ilikuwa ngumu kwa kuwa jamaa hawa ni kama wako juu ya sharia kutokana na mtandao wao ulivyo na nguvu.
Baada ya siku tatu niliitwa tena kwa Kazikanda Moluwi, ni tofauti na maneno yake ya awali kwamba nisubiri kupewa maagizo. Siku hiyo yalizuka mabishano makali sana kati yangu na KM baada ya kuniambia kuwa kashfa ya Mwajuma ndiyo itumike kama sababu ya kufukuzwa kazi ili kusiwe na mtu wa kuhoji uamuzi huo.
Maneno hayo yalikuwa ni kama uthibitisho rasmi kuwa KM, Boimanda na wenzao ndiyo walihusika na kumuua Mwajuma na uvamizi uliotokea nyumbani kwangu. Nilimwambia KM kuwa kama wanadhani nimehusika kwa namna moja au nyingine kwenye kifo cha Mwajuma wasiishie kufanya ni sababu ya mimi kufukuzwa kazi, wanifikishe moja kwa moja mahakamani.
“Unajiamini nini?” aliniuliza KM
“Sio suala la kujiamini, ni kufanya tu haki itendeke kwa kuwa inaelekea mnalijua sana jambo hilo sasa ni kwanini marehemu asipewe haki zake kwa kumkamata muuaji” nilimjibu kwa kujiamini.
“Hapa suala ni sababu ya wewe kufukuzwa kazi, usilete habari zako ningine” KM alijaribu kunitoa kwenye hoja.
“Kama uamuzi wa mimi kuingia kwenye siasa umetoka kwa mheshimiwa rais, kwanini zitafutwe sababu za kunifukuza kazi kwa kuogopa watu watahoji? Ni nani mwenye mamlaka ya kumhoji mheshimiwa rais? Labda ingekuwa nafanya kazi moja kwa moja na jamii mnesingizia kuwa wananchi watahoji.
Siwalazimishi kufuata ninavyotaka mimi ila kama mtataka kunikandamiza nitatutumia nguvu zangu zote kupata haki yangu.” Nilimwambia kwa kujiamini nikimtazama machoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
KM alinitaka niondoke ili atafakari uamuzi wa kuchukua lakini kwangu maneno yake yalikuwa yakimaanisha kuwa anaenda kuwaeleza waliomtuma ili wachukue uamuzi kutokana na hoja nilizozitoa.
Haikuchukua muda kupata uamuzi wa waliomtuma KM, maana nilipofika tu nyumbani nikapigiwa simu kuelezwa walichoamua. Nadhani alipopeleka hoja hiyo, waliomtuma wakajua waking’ang’ania hoja yao nitawashtukia. Ikakubalika kuwa niandike barua ya kuacha kazi. Nikafanya taratibu zote.
Siku ambayo nilimalizana na taasisi hii nyeti, tayari nilikuwa nishaandaa mpango wa namna ntakavyotekeleza majukumu niliyojipangia nikiwa nje ya ajira. Pia nilipangisha nyumba yangu niliyokuwa naishi pamoja na kutengeneza utambulisho mpya kabisa kwa ajili ya matumizi ya simu, mitandao na huduma za kibenki. Kifupi hadi wakati huo kulikuwa na watu wawili tofauti nje yangu.
Kitu ambacho viongozi hawakuwa wanakijua ni kwamba, badala ya kuwa kazi imeisha kwangu ndiyo ilikuwa imeanza rasmi.
Baada ya siku kadhaa nilikuwa nikiishi sehemu tulivu nikiwa na mpenzi wangu Tausi, sehemu ambayo ilikuwa na mtandao wa ulinzi mkali kuliko nilipokuwa nakaa zamani kwa kuwa mtandao wetu ulijua kuwa nakabiliwa na hatari kubwa zaidi kuliko mwanzoni. Lakini kwa macho ya kawaida usingehisi kama sehemu hiyo ilikuwa na ulinzi wowote.
Nilitambulishwa kwa viongozi wa siasa ambao ni mamluki wenzangu kwenye chama hicho nilichoagizwa nijiunge nacho. Nilishangaa sana kuona kuwa ni wale walio mstari wa mbele kupiga kelele kwenye vyombo vya habari kila kukicha.
Inamaanisha kuwa na mimi natakiwa kuwa kimbelembele? Nilijiuliza kwa haraka haraka kabla sijapewa majukumu tofauti na ‘kutokelezea’ mbele ya waandishi wa habari kila mara, nikashusha pumzi.
Nilipewa kazi ya kuwasafisha viongozi wa chama tawala na chama kile cha upinzani waliokuwa na dhamira ya dhati katika kupigia kelele wizi unaofanywa na baadhi ya viongozi walio madarakani na wengine walio nje ya madaraka wanaotaka kurudi katika hatamu za kuishika nchi. Siku hiyo sikulala usiku kucha, pamoja na ushujaa wangu nilijihisi kupwaya katika jukumu hilo.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu toka nimfahamu Tausi, siku hiyo nilimpa mgongo nikijikunyata kwenye kona ya kitanda mithili ya watoto wa mitaani wanavyolala vibarazani wanavyokuwa wamejikunyata kwabaridi. Sikuwa nimemhadithia Tausi kilichojiri ila aligundua kuwa nina jambo zito kichwani, akanifunika shuka akalala pembeni yangu kwa utulivu.
Kikubwa nilichotakiwa kukijua kwanza, ni kiongozi mkuu wa harakati hizi. Kutokana na ukubwa wa mtandao, njia rahisi niliyoiona na kuiamnini ni ya kuling’oa shina na kuacha matawi yasambaratike yenyewe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kazi ya kwanza ndiyo ilinishangaza zaidi. Nilipigiwa simu na kutaarifiwa kuwa nikachukue maagizo ya kazi ya kwanza kwenye sanduku langu la barua, nilicheka na kujiamini zaidi baada ya kupokea maagizo hayo kwa kuwa ilinipa picha kuwa wakina KM hawanijui vizuri. Sanduku langu la barua huwa liko pale kuzuga tu.
Jambo nililokuja kuligundua baadaye ni kuwawastaafu wa serikalini, waliaminishwa kuwa nchi ni yao na wakafanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kuishia kwa na kipato duni. Sasa wanavyoona watumishi wa siku hizi wakitajirika kwa haraka kwa kutumia mbinu chafu, mioyo inawauma sana hivyo wanataka hatua kali zichukuliwe kwa haraka jambo ambalo halifanyiki kutokana na kinachoitwa ‘utawala wa sheria’.
Wenye uroho wa madaraka wakaligundua hilo na kuwaaminisha wastaafu hao kuwa wao wana uwezo wa kuisafisha hali iliyopo ili wapate sapoti kutoka kwao itakayowapeleka madarakani. Wakitumia hata njia chafu kupata utajiri huku wakiwadanganya wastaafu hao kuwa ni namna ya kujijengea uwezo ili waweze kuingia madarakani na kuisafisha nchi.
Walikuwa kwenye nafasi nzuri kweli kweli kwa sababu, serikalini walikuwa wakiaminika hata kwa mheshimiwa Rais mwenyewe, nje walikuwa wakiaminiwa na wastaafu na wao ndiyo watafuna nchi kwa kushirikiana na ‘mchwa’ wenzao wanaojinadi kuwa wanataka kuingia kuwashughulikia. Kazi ilikuwa ngumu sana.
Nikaanza kuumiza kichwa ni kwa namna gani nitaweza kusambaratisha mtandao huo ili nisilazimike kuua watu wasio na hatia ambao wanatetea maslahi ya nchi yetu. Kikubwa nilichotakiwa kukijua kwanza, ni kiongozi mkuu wa harakati hizi.
Kutokana na ukubwa wa mtandao, njia rahisi niliyoiona na kuiamnini ni ya kuling’oa shina na kuacha matawi yasambaratike yenyewe.
Kazi ya kwanza ndiyo ilinishangaza zaidi. Nilipigiwa simu na kutaarifiwa kuwa nikachukue maagizo ya kazi ya kwanza kwenye sanduku langu la barua, nilicheka na kujiamini zaidi baada ya kupokea maagizo hayo kwa kuwa ilinipa picha kuwa wakina KM hawanijui vizuri. Sanduku langu la barua huwa liko pale kuzuga tu.
Barua na vifurushi vyote vinavyoelekezwa kuingia kwenye namba ya sanduku langu huletwa moja kwa moja mahali nitakapoagiza na kwa wakati ninaotaka. Kwa hiyo simu yao ilikuwa ni kama kuniambia tu kuwa kati ya vifurishi nilivyopokea muda mfupi uliyopita kuna kimojawapo kina kazi yao.
Nikavifungua kwa haraka haraka na kuikuta kazi yenyewe iliyonishangaza. Aliyetakiwa kuondolewa duniani hakuwa kiongozi wa upinzani bali alikuwa ni waziri wa serikali ambaye siku za karibuni alikuwa amevunja mtandao mmoja mkubwa sana uliokuwa ukiwaingizia watu wachache mabilioni ya hela kila mwezi.
“Hawa ni watetea maslahi ya taifa kweli?” nilijikuta najiuliza kwa sauti. Bahati nzuri hakukuwa na mtu karibu yangu. Tausi alikuwa jikoni akipika. Katika vitu ambavyo nilishindwa kumshawishi Tausi ni suala la kutafuta msichana kwa ajili ya kumsaidia kazi. Mara zote alikuwa akinijibu “nahitaji kumhudumia mume wangu mimi mwenyewe”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo ndipo anapowapiga bao wasichana wengine wasomi na waliotoka kwenye familia ya kitajiri kama yeye. Nadhani ni kwa ajili ya kumcha Mwenyezi Mungu.
Kichwa kilianza kuniuma kuhusiana na hiyo kazi. Nilipewa ratiba yake yote ikielekea kuwa mmojawapo wa wasaidizi wake wa karibu alikuwa anahusika na mpango huo. Wakati mzuri zaidi ilikuwa ni mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya wizara yake katika kukabiliana na uhujumu wa uchumi. Kibaya zaidi mimi nilitakiwa kupanga tu mpango, watekelezaji walikuwa ni vijana wao na wakubwa hao walinisisitiza kuwa wanataka kazi safi.
Ilinibidi nipange mpango ambao haukuwatia mashaka yeyote, ilikuwa tutumie sumu ya kunusa ambayo ingewekwa kwenye kinasa sauti chake na walipangwa vijana wa kumuuliza maswali ya kukera ili aweze kuivuta nyingi iwezekanavyo. Pia nilipanga kuwa akizidiwa apelekwe hospitali ambayo ina daktari wao ili atoe taarifa za uongo kuhusiana na kifo chake. Kila kitu kiliandaliwa kama kilivyopangwa.
Hadi muda ambao ofisi zinafungwa, siku moja kabla ya mkutano huo ambao ulipangwa kufanyika kwenye chumba cha mikutano cha wizara yake kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa umahiri mkubwa. Hadi wakati huo nilikuwa sijajua ni hatua zipi za ziada nizichukue. Ilipotimia saa 3 usiku likanijia wazo ghafla ambalo nililifanyia kazi kwa ukamilifu.
Siku ya tukio, waandishi walikusanyika tayari kumsubiri waziri huyo. Waziri akaeleza kwa kina alichowaitia waandishi wa habari kabla ya waandishi kuanza kuuliza maswali. Wakati anajibu swali la tatu waziri akaanguka na kuzua pilika pilika za hapana pale kabla hajachukuliwa na wana usalama kupelekwa kwenye hospitali mojawapo kati ya zinazohudumia viongozi na ndiyo aliyopangwa daktari wa ‘watetea maslahi ya taifa’.
Wazo nililolipata saa 3 usiku wa siku ya kuamkia mkutano wa waziri na waandishi wa habari lilinifanya nitoke usiku huo nikiwa tayari kwa lolote nikaenda moja kwa moja hadi kwenye jengo la wizara.
Nje niliwakuta askari wanne wakiwa na silaha, nikazunguka kwa nyuma ambako kuna jengo jingine. Nikafanikiwa kuwapenya walinzi wa jengo ambalo limepeana mgongo na jengo la wizara, nikapanda juu kabisa ya jengo hilo na kurukia juu ya jengo la wizara. Nikateremka pole pole hadi kwenye ghorofa ilipo ofisi ya wizara na chumba cha mikutano, nikakifungua chumba cha mikutano kwa namna ninayoijua mimi.
Moja wa moja nikatoa kinasa sauti chenye sumu, nikaweka nilichoenda nacho ambacho kinafanana na kile kwa kila kitu kabla ya kuenda kwenye kona moja ya dirisha na kutoa kifaa maalumu cha kurekodia picha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kama nilivyokuhadithia awali kuwa nilikuwa nawaza hatua za ziada za kuchukua, ni za ziada kwakuwa za awali tayari zilikuwa zimefanyika kwa kutumia watu wa mtandao wangu tulifunga kifaa hicho kwa ajili ushahidi wa siri ambao tulidhani ungetusaidia katika mipango yangu ya kuwamaliza wenye uchu wa mali na madaraka.
Nikatoka moja kwa moja hadi ilipo nyumba ya waziri ambayo iliimarishwa ulinzi na mheshimiwa rais kutokana na maamuzi makubwa aliyoyafanya waziri huyo. Nikatumia mbinu za kijasusi kuingia humo ndani, na baada ya kukagua vyumba kadhaa nikakigundua chumba cha waziri na kumkuta akiwa amelala na mkewe.
Nikawasha taa, wakakurupuka toka usingizini na kubaki wamehamaki wakiangaza huku na kule. Nikawahi kuwanyamazisha kwa kuwaonyeshea bastola na kuwaamuru wakae kitandani wakiwa kimya. Wakawa wanalalamika tu kuwa wako tayari kunipa chochote ili nisiwaue.
Nikawaamuru wainuke taratibu na wasogee mbali kidogo na kilipo kitanda, wakafanya hivyo huku mheshimiwa waziri akionekana kama anayepanga na kupangua mambo kichwani.
“Mimi nakulinda mheshimiwa waziri, unatakiwa kuuawa kesho.
Kuna watu ambao wana nguvu sana katika nchi hii wanaotaka ufe, kwa hiyo ukionyesha ushirikiano utaendelea kuwepo na nitaendelea kukulinda wewe na wenzio mnaolitakia mema taifa hili. Lakini ukijifanya mjanja kukwepa ninayokwambia ndiyo utakuwa unakimbilia kifo chako mwenyewe” nilimueleza kwa ufasaha nikimwangalia usoni.
Nilimweleza kwa kirefu na kumuonyeza picha za namna walivyofunga kinasa sauti chenye sumu na kumuelekeza cha kufanya na ndivyo alivyofanya na kudondoka. Pia nilimsisitiza mke wa waziri kuwa akifanya upumbavu wowote maisha ya mumewe yatakuwa hatarini na yeye ataisaidia polisi kwa kuwa ni yeye tu anayejua ninachowaambia pale. Japo walisisitiza kutaka kunijua na kujua nimetumwa na nani, hawakuweza kupata jibu lolote kisha nikaondoka kama ambavyo niliingia.
Baada tu ya waziri kufikishwa hospitali, lilikuja gari la Ikulu kumuondoa na kumpeleka kwenye chumba maalumu cha hopitali ya jeshi huku uvumi ukiwa umeshazagaa kuwa waziri huyo amefariki dunia. Ikaja kutangazwa kuwa yuko mahututi na mipango inafanyika kumpeleka nje ya nchi.
Kwa msaada mkubwa kutoka kwa mhehimiwa rais, maagizo yote ya waziri huyo yaliendelea kutekelezwa huku ikielezwa kuwa hali ya waziri huyo ni mbaya mno. Mambo yote alikuwa yakiratibiwa na maofisa ambao walionekana kuwa wasafi kutokana na taarifa za mtandao wetu wa siri. Lakini ukweli ni kuwa waziri huyo alikuwa ni mzima wa afya.
Upande wa wale wapuuzi wanaojiita watetea maslahi ya taifa waliamini kuwa nimefanya kazi vile ilivyotakiwa ila matatizo yalikuwa upande wao kwa kushindwa kumshikilia mgonjwa katika mikono yao ila hawakuwa na wasiwasi na mimi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kilichonifurahisha zaidi ni uamuzi wao kuwa wasimamishe kwa muda opereseni yao ya kuwasafisha vimbelembele hadi hali itakapotulia, nikawa likizo isiyo rasmi. Likizo hiyo nikaitumia kuchunguza vyanzo vyao vyote vya mapato visivyo halali vya watu hawa kwa kushirikiana na mtandao wangu wa siri. Na kikubwa ni kumjua kiongozi wao, au ‘Rais mtarajiwa’.
Ndipo nikamgundua Mheshimiwa Dickson Malyato Ndagila, waziri wa za mani wa fedha aliyefukuzwa kazi serikalini kutokana na wizi mkubwa uliyotokea Benki Kuu na kumhusisha yeye kwa namna moja au nyingine japo hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja.
Huyo ndiye ‘Rais wao mtarajiwa’.
*****MWISHO*****MWISHO***MWISHO***
NB: SEMA LOLOTE KUHUSU SIMULIZI HII.
0 comments:
Post a Comment