Simulizi : Hili Ni Jiji La New York
Sehemu Ya Pili (2)
Bado mpelelezi Sam alikuwa akishangaa kuhusiana na mahali pale alipokuwa. Watu bado walikuwa wakiendelea kucheza ngoma mbalimbali ambazo zilimuonyesha kama walikuwa wakiushangilia uwepo wake mahali pale. Eneo zima lilionekana kutisha kupita kawaida, ushirikina ambao ulikuwa ukionekana mahali pale ulikuwa ukimpa hofu kubwa moyoni.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ngoma ambazo zilikuwa zikipigwa zikasimamishwa na kisha mwanaume mmoja ambaye alikuwa uchi wa mnyama kuanza kumsogelea Sam mahali pale alipokuwa amesimama akishangaa. Uso wa mwanaume yule ulionekana kuwa wa ajabu, vitu fulani ambavyo vilikuwa vikionekana kama funza vilikuwa vikitoka mdomoni mwake.
Macho yake yalikuwa makubwa, mboni ambayo ilitakiwa kuwa nyeusi haikuwa hivyo, ilikuwa nyekundu kabisa jambo ambao ilionyesha kwamba hakuwa mwanadamu wa kawaida. Ingawa alipokuwa mbali alikuwa akionekana kuwa binadamu wa kawaida lakini kadri alivyokuwa akizidi kupiga hatua kumsogelea na ndivyo ambavyo alikuwa akizidi kubadilika na kutisha zaidi.
Alipomfikia, tayari miguu yake ilikuwa imekwishabadilika, ilikuwa ni kwato za ng’ombe ambaye alikuwa amekomaa. Sam akaazidi kutetemeka kupita kawaida jambo ambalo alitamani kuona kwamba ile ilikuwa ndoto ambayo baada ya muda angeshtuliwa na kujikuta yupo nyumbani kwake jijini New York.
Mwanaume yule akazidi kumwangalia Sam, ghafla akaanza kubadilika na kuurudia ubinadamu wa kawaida. Alipofikia Sam, tayari kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka. Mwanaume yule akampulizi vitu fulani usoni mwake, Sam akaanza kuona mambo ya ajabu hata zaidi ya yale ambayo alikuwa akiyaona mahali pale.
Akaanza kuona pango kubwa mbele yake, na wale wanaume ambao alikuwa akiwaona na kugundua kwamba walikuwa wale watu walioingia msituni na kutorudi tena kuanza kuingia ndani ya pango lile. Giza kubwa lilikuwa likionekana ndani ya pango lile huku sauti za kutisha zikiwa zinasikika ndani ya pango lile.
Sam akajikuta akianza kuvutwa kuelekea pangoni mule pasipo kumuona mtu ambaye alikuwa akimvuta. Akaingizwa ndani ya lile pango, giza ambalo lilikuwepo ndani ya pango lile likamfanya kutokuona kitu chochote kile.
Moyo wake ukaanza kujuta, aliujutia uamuzi wake aliouweka wa kuamua kuingia ndani ya msitu ule na wakati alikuwa amekwishaonywa kabla, ubishi wake ukaanza kumletea majuto moyoni. Tayari akaonekana kukata tamaa ya kutoka nje ya msitu ule huku akiwa salama kabisa na kurudi nchini Marekani.
Ndani ya pango lile kulikuwa na harufu kali ya damu, harufu ambayo hakuwahi kukutana nayo kabla. Muda mwingi alikuwa akiziba pua yake lakini wala haikuonekana kumsaidia hata kidogo. Akafika katika sehemu ambayo ilikuwa na uwanja mkubwa na wote kuamuliwa kukaa mahali hapo.
Wakaachwa wazungu peke yao katika eneo lile, Sam akashindwa kuvumilia, akaanza kupiga hatua na kumfuata mzee mmoja ambaye mwili wake ulikuwa ukionekana kuchoka kupita kawaida na kisha kuanza kuongea nae.
“Kwa nini tupo hapa?” Sam alimuuliza.
“Sifahamu hata kidogo. Nimekaa katika sehemu hii kwa miaka zaidi ya ishirini, hii ni sehemu iliyokuwa na mateso sana, unapoingia hapa kamwe hauwezi kutoka” Mzee yule alimwambia Sam maneno ambayo yalionekana kumkatisha tamaa.
“Kwa nini hauwezi kutoka?”
“Ulinzi. Yaani kila sehemu kuna majini yao. Kama unataka kutoroka basi ni lazima ujue masharti ya kuondoka mahali hapa” Mzee yule alimwambia.
“Kwani kuna masharti gani?”
“Hayo ndio ambayo hatuyajui kabisa”
Sam akatulia kwa muda, tayari moyo wake ukaonekana kukata tamaa, ni kweli alikuwa na hamu ya kuondoka mahali hapo na kisha kurudi nchini Marekani lakini akaonekana kuanza kuuona ugumu wa yeye kuondoka mahali hapo. Kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuondoka tu, hakutaka kujali kuhusu kuendelea kuitafuta ndege mahali hapo, kutoroka ndio ulikuwa mpango ambao ulimjia kichwani.
Akajiona kuwa mfu, aliona ilikuwa ni bora kujaribu kutoroka kuliko kuendelea kubaki mahali hapo. Alijua fika kwamba kama angeendelea kubaki mahali hapo basi ilikuwa ni lazima kufa. Aliona ni bora ajaribu kutoroka tu kwani hata akifa itakuwa ni sawa na kukaa ndani ya sehemu hiyo.
Namna ya kutoroka ndani ya pango lile kukaanza kuonekana kuwa jukumu kubwa kwake, hakujua ni kwa namna gani angetoroka mahali pale. Mawazo mbalimbali yalikuwa yakimjia kichwani mwake lakini mawazo hayo yote aliyaona kutokustahili.
Kwanza aliona kulikuwa na uhitaji mkubwa wa kufahamu masharti ambayo alikuwa ameambiwa hata kabla ya kuweka mipango yake ya kuondoka mahali pale. Hakujua ni mahali gani ambapo angeweza kuyatambua masharti yale. Kitu alichoamua kukifanya ni kuanza kuzungazunguka ndani ya pango lile huku idadi zaidi ya watu themanini na tano ikiwa ndani ya lile pango.
Watu wote hao wala hawakujishughulisha na kitu chochote kile, ilionyesha kwamba walikuwa wamejaribu kwa njia mbalimbali kuweza kutoroka ndani ya sehemu ile lakini walishidwa kabisa. Sam alitembea zaidi na zaidi, giza ambalo lilikuwa ndani ya pango lile likaonekana kuanza kupungua kwani tayari macho yake yalikuwa yamekishalizoea giza lile.
Pango lilikuwa limezunguka sehemu yote, Sam akaanza kuangalia sehemu moja ambayo ilikuwa na kitundu kimoja kidogo, akajaribu kuchungulia lakini kulikuwa na giza upande wa pili. Alipoonekana kuridhika akaanza kupiga hatua kuwafuata wenzake.
“Tutatoroka mahali hapa” Sam aliwaambia.
“Unasemaje?”
“Tutatoroka kwa kupitia pale. Ila kuna kazi moja kubwa ambayo tunatakiwa kuifanya” Aliwaambia.
“Kazi gani?”
“Tutatoboa pale na kisha tutajua tutatokea wapi” Aliwaambia.
“Sawa. Ila unawafahamu hawa watu?”
“Hapana. Ila inaonekana kuwa ni wachawi” Sam alijibu.
“Sasa tufanye nini? Nadhani wataweza kujua kwamba tunatoroka kwa sababu wana nguvu za giza” Mzee yule alimwambia Sam ambaye alikuwa makini kumsikiliza huku akionekana kufikiria kitu.
“Nakumbuka kabla sijaingia huku kuna kitu niliulizwa”
“Kitu gani?”
“Kama nilikuwa na rozali”
“Sasa ulikuwa nayo?”
“Hapana. Hii inaonyesha kwamba unapokuwa na rozali inaweza kusaidia”
“Sasa rozali tutapata wapi?”
“Tatizo sio rozali. Kitu ambacho kinaonekana kuwaogopesha ni alama ya msalaba” Sam aliwaambia huku wote wakiwa makini kusikiliza.
“Kwa hiyo tufanye nini?”
“Ngojeni” Sam aliwaambia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo hapo akaanza kuzunguka zunguka ndani ya pango lile huku akionekana kutafuta kitu fulani. Alizunguka kwa muda wa dakika kadhaa, akaanza kuwafuata watu wale huku akiwa na miti miwili ambayo ilikuwa na urefu wa mkono wake.
“Inatubidi tutengeneze misalaba haraka iwezekanavyo mara baada ya kumaliza kuvunja mahali hapa. Miti hii tutaifanya kuwa misalaba, mimi nitakuwa mbele yenu katika kipindi cha kutoroka huku nikiwa nimeushika msalaba na kuunyosha mbele. Mwingine atakuwa nyuma huku nae akiwa ameshika msalaba mmoja. Mmenielewa?” Sam aliwauliza.
“Tumekuelewa. Ila itaweza kufanya kazi hii?”
“Asilimia mia moja. Umekwishawahi kukisoma kitabu cha ‘WITCHES IN 1678’” Sam aliwauliza.
“Hapana”
“Kama haujakisoma basi acha tufanye hivi. Hii itasaidia sana. Hakuna atakayejua. Alama za misalaba zitawafanya kutokuona wala kuhisi chochote. Cha msingi tuanzeni kuvunja mahali hapa” Sam aliwaambia.
“Sasa tukianza kuvunja hawatojua?”
“Inawzekana wakajua. Nimepata wazo. Wakati tunavunja, inabidi mtu mmoja asimame mlangoni huku akiwa ameishika miti hii na kuweka alama ya msalaba” Sam aliwaambia.
“Sawa”
Hiyo ndio ikaonekana kuwa njia rahisi kwa wao kuanza kuifanya kazi ile. Hawakutakiwa kuchelewa kwani walijiona kuna uwzekano wa kuamishwa pango lile. Kwa sababu kulikuwa na majiwe tofauti ndani ya pango lile, wakaanza kuyatumia kuvunja sehemu ambayo waliambiwa kuivunja huku mwanamke mmoja akiwa mlangoni huku akiwa ameishika miti kama alama ya msalaba.
Uvunjani ukaendelea zaidi na zaidi, hawakutakiwa kupumzika hata kidogo, kila mmoja alikuwa na hamu ya kuondoka mahali hapo na kuelekea katika ulimwengu wa kawaida, ulimwengu ambao kwao haukuonekana kuwa na mateso yoyote yale.
Tayari Sam akaonekana kuwa mkombozi wao, wakaendelea kuvunja zaidi na zaidi, sehemu ile ikaanza kuachia, hawakutaka kuacha, waliendelea zaidi na zaidi mpaka tundu kubwa lilipopatikana. Sam akaanza kumfuata mwanamke yule aliyeishika miti ile na kisha kuishika yeye huku akimwambia mzee yule aliyekuwa nae karibu kuichukua miti mingine kutengeneza alama ya msalaba.
Miti mingine ikatengenezwa kama alama ya msalaba na kisha kwenda kusimama pale mlangoni huku Sam akianza kuwaambia watu kuondoka mahali pale kupitia katika tundu lile kubwa huku yeye akiwa mbele yao na miti ile iliyokuwa na alama ya msalaba akiwa ameishikia juu.
“Yesu tusaidie” Mwanamke mmoja alisikika akisema huku safari ikianza rasmi.
****
Maisha yao hayakuonekana kuwa ya amani kabisa katika kijiji kile japokuwa walikuwa wamekaribishwa na kujisikia huru kabisa. Bado walijiona kuwa na haja ya kuondoka mahali hapo kutokana na wale waasi kutokuwa mbali kabisa na kijiji kile.
Siku iliyofuata, hawakutaka kutulia, saa kumi na moja alifajiri walikuwa wamekwishaamka na tayari kuanza safari yao ya kuelekea mbele zaidi. Mwenyekiti wa kijiji kile aliwasihi sana kwamba waendelee kubaki kijijini pale kwa kuwa tu kulikuwa sehemu ya amani kwao lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikubaliana nae.
Asubuhi hiyo hiyo wakapanga safari ila kabla ya kuondoka mahali hapo Williams akaanza kukifuata kitanda na kisha kuiweka mito kama mtu ambaye alikuwa amelala na kisha kuifunika na shuka huku akimtaka mwenyekiti kutokuigusa mito ile.
Wakaanza safari ya kuelekea katika barabara ambayo ilikuwa ikipitiwa na magari mengi ambayo yalikuwa yakielekea mjini na hata yale ambayo yalikuwa yakitoka mjini. Hapo, wakapanda basi moja na safari ya kuelekea mjini kuanza huku wakiwa na kofia vichwani mwao ambazo zilikuwa zimewaficha nyuso zao.
Safari ilikuwa ikiendelea huku kila mmoja akijiona kuwa huru. Lengo lao katika vichwa vyao kwa wakati huo ilikuwa ni kusafiri mpaka mjini ambako huko wangefanya kila liwezekanalo kuwasiliana na watu wa karibu nchini Marekani na kisha kuwaambia kile ambacho kilikuwa kinaendelea.
Safari ilikuwa ndefu, walichukua zaidi ya masaa manne, wakaanza kukaribia mjini katika jiji la Bangkok. Kila mmoja akaonekana kutabasamu, kitendo chao cha kukaribia mjini kiliwafanya kujiona kama walikuwa wakikaribia jijini New York.
Zilikuwa zimebakia kilometa kumi hata kabla ya kufika mjini. Wakaanza kuangalia nyuma, umbali mkubwa kulionekana kukiwa na gari ambalo lilikuwa likisogea kule walipokuwa hali ambayo iliwafanya kuwa na wasiwasi kupita kawaida.
Williams akaanza kuwaambia kuhusu gari lile ambalo alionekana kulitilia wasiwasi lakini Phillip akaanza kumuondoa wasiwasi kwamba hakutakiwa kutilia shaka kila kitu ambacho alikuwa akikiona.
Williams hakuwa na amani kabisa, alikuwa akizidi kuliangalia gari lile ambalo lilikuwa mbali sana kutoka pale walipokuwa. Kitu alichokuwa akitaka ni kumwambia dereva asimamishe basi na kisha wao kuteremka lakini kila alipokuwa akimwambia Phillip kuhusu wazo lake hilo, Phillip alikuwa akipinga kupita kawaida, kwake aliona kila kitu kuwa shwari.
****
Hata kabla hawajakifikia kitanda kile, wakaanza kumimina risasi mfululizo katika kitanda kile na kisha kukisogelea na kufunua shuka, hakukuwa na mtu yeyote zaidi ya mito tu jambo ambalo lilionekana kuwatia hasira kupita kawaida.
Kwa hasira walizokuwa nazo wakatoka chumbani pale na kumfuata Mwenyekiti wa kijiji kile na kisha kumtaka awaambie mahali walipokuwa watu wao ambao walikuwa wakiwatafuta kwa udi na uvumba. Mwenyekiti muda wote alikuwa akionyesha wasiwasi mkubwa, midomo ya bunduki ile ilionekana kumtisha kupita kawaida.
“Waliondoka” Aliwaambia.
“Kwenda wapi?”
“Mjini”
“Muda gani?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Saa kumi na moja” Mwenyekiti alisema huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.
Hakukuwa na sababu ya kuendelea kubaki mahali pale, waliona kwamba kama wangewahi basi wangeweza kuwakuta njiani kutokana na muda huo kuwa saa kumi na mbili kasoro. Walichokifanya ni kulifuata gari la mwenyekiti ambalo lilikuwa karibu na nyumba ile na kisha kuingia.
Hakukuwa na ufunguo jambo ambalo wakamtaka mwenyekiti kuwapatia ufunguo wa gari lile aina ya Defender iliyochakaa. Bwana Robinson akaliwasha na kisha kuondoka mahali hapo kwa mwendo wa kasi.
Kila mmoja alionekana kuwa na hasira, kitendo cha kuwakosa watu wale ambao walikuwa wamewakusudia kilionekana kuwakasirisha kupita kawaida. Bwana Robinson ndiye ambaye alionekana kuwa na hasira zaidi, alitamani awakamate haraka na kisha kuwaua kwa mikono yake mwenyewe.
Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikiifikiria Marekani. Alijua fika kwamba kama asingefanikiwa kuwaua basi ni lazima watu hao wangweza kwenda nchini Marekani na kuuelezea uovu wake ambao alikuwa ameufanya wa kuwaua wachezaji mpira wa timu ya kikapu ya Bucketts.
Aliendesha gari kwa kasi kama mtu ambaye alikuwa akichelewa ndege. Kasi ile ilionekana kuwatia wasiwasi watu wote lakini wala hakuonekana kujali, bado alikuwa akiedesha kwa mwendo wa kasi mpaka pale ambapo kwa mbali sana wakaanza kuliona basi la abiria. Tayari walikuwa na uhakika kwamba basi lile ndilo ambalo lilikuwa limewabeba watu wale ambao walikuwa wakiwatafuta.
“Lile pale” Bwana Robinson alisema huku akiongeza kasi zaidi.
Basi lilikuwa mbali sana, walizidi kulisogelea, mpaka kulifikia walitumia muda wa dakika kumi, wakawa wamebakisha umbali wa robo kilometa na hivyo kuanza kupiga risasi hewani kumtaka dereva kulisimamisha basi lile.
Kila abiria alionekana kuogopa, milio ya bunduki ambayo walikuwa wameisikia ikaonekana kuwatia wasiwasi kupita kawaida, kama ambavyo alivyotakiwa na ndivyo ambavyo alivyofanya, dereva akasimamisha basi lile.
Vijana watano pamoja na Bwana Robinson wakateremka na kuanza kulisogelea basi lile huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Wakaufungua mlango na kuingia, kila abiria alionekana kuwa na wasiwasi, wote walikuwa kimya.
“Hili ni basi la ngapi kwenda mjini siku ya leo?” Mekong alimuuliza dereva.
“La kwanza” Dereva alijibu huku akionekana kuwa na wasiwasi.
Hapo ndipo Bwana Robinson na wenzake wakaanza kuwatafuta watu wao ndani ya basi lile. Kila abiria alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi, uwepo wa bunduki zile ulionekana kuwaogopesha kupita kawaida.
“Watakuwa humu tu” Bwana Robinson alijisemea huku akianza kwenda nyuma ya basi lile katika siti ya mwisho ambako vijana watatu walikuwa wameinamisha vichwa vyao chini katika staili ya kuficha nyuso zao.
Williams aliendelea kuwa na wasiwasi juu ya gari lile ambalo alikuwa akiliona kwa mbali likija, moyoni hakuwa na amani kabisa, kila alipokuwa akimwambia Phillip kuhusiana na gari lile, Phillip alionekana kubisha kabisa kwa kumwambia kwamba hakutakiwa kuwa na wasiwasi kwa sababu tayari walikuwa wamekwishanusurika kifo na kwa kipindi hicho walikuwa wakielekea katika jiji la Bangkok na kisha kuwasiliana na Marekani kuwaeleza kilichotokea.
Maneno ya Phillip hayakumridhisha kabisa Williams, wasiwasi wake ulikuwa ukiongezeka kdri muda ulivyokuwa ukisonga mbele. Baada ya kuona kwamba Phillip anakataa kumuelewa, moja kwa moja Williams akasimama na kisha kuanza kumfuata dereva wa basi lile na kisha kumuamuru kusimamisha gari.
Kila abiria akaonekana kumshangaa Williams ambaye alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa. Williams akazidi kung’ang’ania basi lisimamishwe. Dereva hakuwa na jinsi, Williams alionekana kubadilika kupita kawaida, alichokifanya dereva ni kulisimamisha basi lile.
Williams akaanza kumfuata Philip na kisha kumwambia kuteremka mahali hapo kwani amani yake ilizidi kupotea kadri alivyokuwa akiliangalia gari lile ambalo lilikuwa mbali sana kuwafikia. Phillip hakuonekana kumuelewa, aliendelea kugoma kwamba kwa wakati huo ilikuwa ni lazima wafike Bangkok.
“I cant go anywhere Williams (Siwezi kwenda popote Williams)” Phillip alimwambia Williams.
“Please Phillip, we have to get out of here (Tafadhali Phillip, tuondoke mahali hapa)” Williams alimwambia Phillip.
Bado malumbano ya muda yalikuwa yakiendelea, Williams alikuwa aking’ang’ania wateremke ndani ya gari lile na kisha kuingia porini lakini kwa Phillip alionekana kutokukubaliana nae. Abiria wote wakaonekana kukasirika, Williams na Phillip wakaonekana kuwachelewesha.
“They are coming to kill us, please lets go (Wanakuja kutuua, tafadhali tuondoke)” Williams alimwambia Phillip kwa sauti ya chini.
“Ok! Ok! Ok!” Phillip alisema huku akionekana kutokuridhika japokuwa alikuwa amekubaliana nae.
Phillip na Gong wakasimama na kisha kuanza kumfuata Williams ambaye alikuwa akielekea nje ya basi lile. Wakateremka na kisha kuanza kuelekea porini huku wakiliacha basi lile likiondoka mahali pale. Phillip alionekana kutokuridhika kabisa japokuwa walikuwa wameteremka ndani ya basi lile. Walichokifanya kwa wakati huo ni kutaka kuwa na uhakika kama gari lile ambalo lilikuwa likija lilikuwa la wale waasi au watu wengine, walichokifanya, wakajificha porini huku wakiangalia barabarani.
Baada ya dakika mbili, gari lile likapita. Kila mmoja alionekana kushtuka, gari lile lilikuwa na watu wasiopungua kumi ambao walikuwa wameshika bunduki huku likiwa linaendeshwa kwa mwendo wa kasi. Williams akayageuza macho yake na kumwangalia Phillip ambaye alionekana kuwa na hofu kubwa.
“Oh my God! How did you know? (Mungu wangu! Uliajuaje?)” Phillip alimuuliza Williams huku akionekana kuwa na wasiwasi zaidi.
“God told me (Mungu aliniambia)” Williams alijibu.
Hawakutaka kuendelea kubaki mahali pale, walichokifanya ni kuanza kuondoka kwa kupitia maporini, katika kipindi hicho, Gong ambaye kwa kiasi fulani alikuwa akizifahamu njia ndiye ambaye alikuwa akiwaongoza. Safari yao iliendelea zaidi mpaka kufika katika sehemu ambayo ilionekana kuwa mji mdogo, mji ambao ulikuwa ukiongoza kuwa na tembo wengi kuliko mji wowote ule pale Thailand, mji ulioitwa Phittich.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mji ulionekana kuwa mzuri japokuwa haukuwa mkubwa sana, wote wakaanza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka japokuwa Phillip alikuwa akitetemeka. Kitu cha kwanza ambacho walikuwa wakikihitaji mahali hapo ni kupiga simu nchini Marekani na kisha kuwaambia kile ambacho kilikuwa kimeendelea kule walipokuwa wametekwa.
Kazi ya kutafuta simu ikaanza. Watu wengi ambao walikuwa wakiishi katika mji huo walikuwa wakiwashangaa, kwao, walionekana kuwa kama watalii ambao walikuwa wametoka katika nchi za Kiafrika kwa ajili ya kuangalia baadhi ya mambo ambayo yalikuwa yakipatikana mahali hapo hasa hasa tembo ambao walikuwa wakionekana kuwa tofauti na tembo wa nchi nyingine, tembo ambao walikuwa ni wakubwa huku wakiwa na manyoya mengi.
Hawakuonekana kujali kabisa, katika kipindi hicho kiu ambacho walikuwa wakikihitaji ni simu tu. Gong akajaribu kuuliza katika kila kona kama kulikuwa na uwezekano wa kupata simu lakini hakukuonekana kuwa na uwezekano wowote wa kupata simu.
Tayari mambo yakaonekana kuwa magumu kwao. Walichokifanya ni kuanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na majengo kadhaa ya shule ya sekondari huku lengo lao likiwa ni kuongea na mmoja wa walimu ambao walikuwa wakipatikana mahali hapo kwa kuamini kwamba wangeweza kuwasiliana nao kwa lugha ya Kingereza.
Walipofika shuleni pale, moja kwa moja wakaanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na ofisi na kisha kuanza kuongea na waimu huku wakiwauliza baadhi ya maswali.
“Mmmh! Long distance (Mmmh! Umbali mrefu)” Phillip alimwambia Phillip mara baada ya kuambiwa kwamba kulikuwa na umbali wa kilometa kumi mpaka kufika mjini, Bangkok.
“Can you help us to get there? (Mnaweza kutusaidia kufika huko?)” Williams aliwauliza.
“No. We cant (Hapana. Hatuwezi)” Mwalimu mmoja alijibu.
Kila mmoja alionekana kuchoka, jibu ambalo alilitoa mwalimu huyo lilionekana kuwachosha kupita kawaida. Usafiri ambao ulikuwa ukipatikana katika shule hiyo lilikuwa ni basi moja tu ambalo lilikuwa likiwabeba wanafunzi na kuwapeleka majumbani kwao hasa wale ambao walikuwa wakikaa Bangkok.
Basi hilo lilikuwa likitumika kwa wanafunzi tu na si watu wengine kama ambavyo serikali ya nchi hiyo ilivyokuwa imeagiza mara baada ya kutoa msaada wa mabasi katika shule mbalimbali nchini hapo. Alichokifanya Williams ni kumba zaidi na zaidi ili waweze kusaidi kutokana na hali mbaya ambayo walikuwa nayo, mwalimu yule pamoja na walimu wenzake waliendelea kukataa zaidi na zaidi.
Gong alikuwa kimya lakini alivyoona kwamba walimu walikuwa wamekataa kila kitu, hapo ndipo alipochukua nafasi ya kuanza kuwaelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea na hadi kuwa na umuhimu mkubwa wa kufika Bangkok haraka iwezekanavyo.
Kila mwalimu ambaye alisikia habari hiyo alionekana kushtuka, hawakuamini kama wale wamarekani ambao walikuwa wametekwa nyara ndio walikuwa hao, tena wakiwa wawili huku wengine wakiwa wameuawa njiani. Walichokifanya ni kuwachukua na kisha kuwapeleka katika ofisi ya mwalimu mkuu na kisha kuanza kuwaelezea juu ya watu wale ambao walikuwa wamefika mahali pale.
“I know you. I like the way you play. Can we have a snapshot together? (Nawafahamu. Ninawapenda kwa jinsi mnavyocheza. Tunaweza kupiga picha pamoja pamoja)” Mwalimu mkuu wa shule ile aliwaambia huku akionekana kufurahia kuwa na watu wale mahali pale.
Kwa haraka haraka kamera ikaletwa na kisha kupiga picha pamoja na Williams na Phillip. Ile ikaonekana kuwa kama ndoto kwa mwalimu mkuu yule, hakuamini kama siku hiyo angeweza kupiga picha na wachezaji wa mpira wa kikapu ambao alikuwa akiwapenda sana. Mara baada ya upigaji picha kukamilika, mwalimu mkuu akaruhusu basi la wanafunzi kutumiwa kwa ajili ya kuwapeleka mjini, Bangkok.
******
Wote walikuwa wameshika bunduki zao kwa ajili ya kuwamiminia wale watu watatu ambao walikuwa katika viti vya nyuma kabisa ndani ya basi lile. Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba watu wale watatu ambao walikuwa wameviinamisha vichwa vyao chini walikuwa watu wale ambao walikuwa wakiwatafuta.
Walipowafikia, Bwana Robinson akawainua vichwa vyao, hawakuwa watu ambao walikuwa wakiwatafuta. Kila mmoja alikuwa amechanganyikiwa, hawakuamini kama kwa mara nyingine tena walikuwa wamewakosa wale watu ambao walikuwa wamewatafuta. Kwa hasira alizokuwa nazo, Bwana Robinson akaanza kupiga hatua kumfuata dereva na kumshika shati kwa hasira.
“Where are they? (Wapo wapi?)” Bwana Robinson aliuliza huku akionekana kuwa na hasira. Dereva hakujibu chochote kile, swali ambalo alikuwa ameulizwa hakuwa amelielewa, lugha ya Kingereza hakuwa akiifahamu.
Mekong akamfuata Bwana Robinson na kisha kuanza kumtuliza. Abiria wote ambao walikuwa ndani ya basi ile walikuwa wakitetemeka kupita kawaida, uwepo wa bunduki mbele ya macho yao ulionekana kuwatisha kupita kawaida. Watu ambao walikuwa wakionekana mbele ya macho yao walionekana kuwa watu hatari sana ambao wala hawakuhitaji kuletewa mzaha hata mara moja.
Hapo ndipo Mekong akaanza kuongea na dereva yule ambaye alimtolea ufafanuzi juu ya mahali ambapo watu waliokuwa wakiwatafuta walikuwa wameshukia. Hawakutaka kuchelewa, walichokifanya ni kuanza kutoka ndani ya basi lile, wakaingia ndani ya gari lao na kisha kuanza kuelekea katika sehemu hiyo ambayo kulikuwa na njia ya kuelekea katika mji wa Phittich, kila mmoja alionekana kuwa na uhakika wa watu hao kuwa ndani ya mji huo.
Safari ya kuondoka ndani ya pango lile ikawa imeanza mahali hapo, kila mtu alionekana kutetemeka huku wakionekana kutokuamini kama kweli siku ile ndio ilikuwa siku ya mwisho kuihsi ndani ya pango lile ambalo lilikuwa likitisha, pango ambalo halikuwa na chakula chochote kitamu zaidi ya kile chakula ambacho walikuwa wakiletewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mpelelezi Sam, kwao akaonekana kuwa mkombozi mkubwa na kila mmoja aliona kwamba mtu huyo alikuwa ameletwa mahali pale kwa sababu ya kuwakomboa tu na si kingine. Miti ile ambayo waliishika iliyokuwa na alama ya msalaba ikaonekana kuwalinda, katika kipindi cha nyuma haikuwezekana kabisa kutoroka ndani ya pango lile, kwani kila ulipokuwa ukitaka kufanya hivyo, ulikuwa ukigundulika.
Leo hali ilionekana kuwa tofauti kabisa, walikuwa wakitoroka huku wakiwa hawagunduliki hali iliyowafanya kugundua kwamba alama ya msalama ilikuwa ikiwasaidia sana. Waliendelea kutembea mpaka walipoingia kabisa msituni, wakaanza kutembea kwa mwendo wa kasi kuelekea upande wa kaskazini mwa msitu ule.
Msitu ulikuwa mkubwa tena wenye kutisha kupita kawaida. Watu wengine walikuwa wakiogopa lakini Sam alikuwa akiwaondoa hofu mara kwa mara huku akiwataka kutokupiga kelele zozote zile mpaka pale ambapo wangetoka ndani ya msitu ule.
Safari yao ya kuelelea wasipopafahamu bado ilikuwa ikiendelea. Kwa wakati mwingine, Sam alikuwa akipanda juu ya mti mrefu na kisha kuanza kuangalia kama kulikuwa na uwazi wowote sehemu yoyote ile lakini hakuona kitu. Msitu bado ulionekana kuwa mkubwa kupita kawaida.
Waliendelea na safari zaidi na zaidi, baada ya kutembea kwa masaa matatu, wote wakaonekana kuchoka na hiivyo kuhitaji muda wa mapumziko. Wakatafuta sehemu ambayo ilikuwa na kivuli kikubwa na kisha kukaa chini huku wanaume wakiwa wamechoka miti ilikuwa na ncha kali na kuwa kama silaha endapo wanyama wakali wangetokea mahali pale.
“Najua Mungu atatulinda tu” Mwanaume mmoja alimwambia Sam.
“Huko kote tulipotoka alitulinda, basi naamini hata hapa tulipobabakisha atatulinda pia” Sam alimwambia.
Idadi yao yote ilikuwa ni themanini na tano na wote walitakiwa kuondoka katika msitu huo na kuelekea katika nchi zao. Watu wote ambao walikuwa mahali hapo walikuwa ni watu wa kutoka katika mataifa mbalimbali duniani, hasa mataifa ya Ulaya ambayo walikuwa wakipenda sana kufanya utalii katika nchi mbalimbali.
Walichukua muda wa saa moja kupumzika mahali pale, na sasa walitakiwa tena kuendelea na safari yao ya kuelekea nje ya msitu ule. Hapo ndipo ambapo Sam akaamua kupanda juu ya mti ili kuangalia kama angeweza kuona sehemu yoyote ambayo ilikuwa wazi kwa kuona kwamba sehemu hiyo ingekuwa makazi ya watu.
Sam akaupanda mti mmoja mrefu na kisha kuanza kuangalia kila upande. Mbele ya macho yake akaiona sehemu moja kubwa ambayo wala haikuwa na miti, Sam akaonekana kuwa na furaha kwa kuona kwamba hatimae walikuwa wamefika katika sehemu ambayo ilikuwa na makazi ya watu, alichokifanya ni kuteremka na kisha kuanza kuwaeleza wenzake kuhusiana na seheumu hiyo.
“Kwa hiyo kuna kijiji hapo mbele?” Mwanaume mmoja alimuuliza.
“Ninafikiri itakuwa hivyo, sehemu hiyo iliyo wazi ambayo haina miti ni kubwa sana. Inukeni tuanze kuelekea huko” Sam aliwaambia.
“Ni mbali sana kutoka hapa?” Mwanamke mmoja aliuliza huku akionekana bado amechoka.
“Sio mbali sana” Sam alimwambia.
Hapo hapo wote wakasimama na kisha kuanza kuondoka mahali hapo kusonga mbele kuelekea katika sehemu hiyo ambayo kila mmoja aliamini kwamba kulikuwa na makazi ya watu. Umbali haukuwa mdogo, walitembea kwa muda wa dakika thelathini na ndipo wakafika katika sehemu hiyo.
Macho yao yakatua katika barabara moja kuwa ya lami ambayo ilionekana kuwa kuu kuu, ila pamoja na lami hiyo, pia macho yao yakatua katika ndege moja ambayo ilikuwa mahali hapo, kila mmoja akagundua kwamba ule ulikuwa ni uwanja wa ndege ambao haukuwa ukitumika katika kipindi hicho.
Kila mmoja alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kuiona ndege mahali pale kilionekana kuwafurahisha kupita kawaida, wakaanza kupiga hatua kuifuata ndege ile ambayo ilikuwa ikionekana kuwa na milango ambayo wala haikuwa imefungwa.
Kwa Sam, akaonekana kuwa na furaha zaidi, akajua fika kwamba ndege ile ndio ambayo ilikuwa imetumika kuwabeba wachezaji wa mpira wa kikapu wa New Bucketts. Walipokuwa wakiisogelea, Sam akaanza kuangalia aina ya ndege ile, ndege ilikuwa ile ile.
Sam akawaambia wote wbaki pale nje na kisha yeye mwenyewe kuingia ndani. Sam akaingia ndani ya ndege ile. Hapo ndipo alikuwa na uhakika zaidi, mipira mbalimbali ya mchezo wa kikapu ilikuwa ikionekana katika viti mbalimbali ndani ya ndege ile huku katika kiti kimoja kukiwa na kombe moja kubwa.
“Ndio yenyewe” Sam alisema.
Kwa haraka haraka akaanza kupekua hapa na pale huku lengo lake likiwa ni kutafuta simu. Wala hakupata tabu, katika kila kiti kulikuwa simu ambapo akachukua simu moja na kisha kupiga katika kitengo cha upelelezi nchini Marekani na kuanza kuwaeleza kile ambacho alikuwa amekutana nacho.
“Lakini mbona ulikaa kimya kwa kipindi kirefu sana?” Sauti ya mtu wa upande wa pili iliuliza.
“Nilipata matatizo makubwa” Sam alijibu.
“Matatizo gani?”
“Nitakuja kuwaambia nikifika huko. Ila kwanza jueni kwamba ndege imepatikana” Sam alisema na kisha kuanza kuwaelekeza mahali pale na namna ya kufika. Akaanza kuelekea katika viti vya marubani mbele kabisa na kisha kutafuta kifaa cha GPS na kisha kukiwasha ili kule makao makuu ya ndege ile wafahamu mahali ndege ile ilipokuwa katika kipindi kile.
Sam alipoona kila kitu kipo tayari, akaanza kurudi katika viti vya watu wengine na macho yake kutua katika sehemu ambayo kulikuwa na mizigo mingi hasa ya vyakula ambavyo vilikuwa vimenunuliwa pamoja na vinywaji. Sam akaanza kuifuata mizigo ile na kisha kuifungua, vyakula vilikuwa mahali pale pamoja na vinywaji.
Akachukua kinywaji cha Red Bull na kisha kuanza kunywa. Akaanza kutoka katika sehemu ile ili aende nje na kuwaaambia watu wale waliokuwa nje waingie ndani ili waweze kunywa na kula huku wakisubiri msaada kutoka katika makao makuu ya kipelelezi ya FBI ambapo aliamini kwamba ndege pamoja na marubani walikuwa wakifika mahali pale kwa ajili ya kuichukua ndege ile na kuondoka nayo.
Alipofika mlangoni na kuangalia pale nje, hakukuwa na mtu yeyote yule. Sam akaonekana kushtuka, hakujua sababu ambayo iliwafanya watu wale ambao alikuwa amewaacha pale nje kutoonekana mbele ya macho yake. Tayari akaanza kufikiria kwamba kuna watu wenye silaha ambao walifika mahali pale na kisha kuwachukua watu wale au wale watu ambao walikuwa wakifanya ibada za kishirikina.
Alipoangalia chini vizuri, ile miti ambayo ilikuwa imejengwa na kuwa na alama ya misalaba ilikuwa mahali pale. Sam akaonekana kuchanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kukifanya kama ni kuwatafuta watu wale au aendelee na safari yake. Huku akiwa anafikiri ni nini cha kufanya, ghafla akaona kitu ambacho alikuwa na uhakika ndicho kilichokuwa kimewafanya watu wale kutoonekana mahali pale, Sam akabaki akitetemeka kupita kawaida, alichokifanya ni kujifucha huku akimuomba Mungu amnusuru kutoka katika hatari ile ambayo ilikuwa inamkabili kwa kipindi hicho.
“Mungu nisaidie” Sam alisema huku akiwa amejificha ndani ya ndege ile huku akichungulia nje kupitia kidirisha kimoja cha ndege ile.
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Robinson na wenzake walionekana kuwa na hasira kupita kawaida, hakuamini kama katika kipindi hicho bado watu wale ambao walikuwa wakiwatafuta walikuwa wakiendelea kuwasumbua namna ile, hasira za kutaka kuwaua ziliogezeka zaidi na zaidi.
Kila wakati Bwana Robinson alikuwa akipiga usukani kwa hasira sana. Hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa amewakosa watu wale ambao kwake walionekana kuwa wa hatari sana kama angewaruhusu kuingia nchini Marekani au hata kupata mawasiliano na watu wa Marekani.
Alijiona kuwa na kila sababu za kuwatafuta watu hao na kisha kuwaua kwa mkono wake mwenyewe. Japokuwa alikuwa akiendesha gari kwa kasi kubwa sana mpaka alamu ya hatari kuanza kulia lakini kwake kasi ile ilionekana kuwa ndogo sana jambo ambalo alitamani gari lile kuwa na kasi zaidi.
Walipofika katika barabara ambayo ilikuwa ikikata kuingia katika mji wa Phittich, Bwana Robinson akapunguza mwendo na kisha kukata kona na safari kuendelea zaidi. Katika kipindi hicho mawazo ya Bwana Robinso hayakuwa yametulia kabisa, kitu ambacho alikuwa akikitamani ni kuwaua watu hao na kisha kuendelea na maisha yake.
Gari lilitembea kwa muda mrefu na ndipo wakaanza kuingia katika mji huo, wakati wanaingia ndani ya mji huo, napo gari la kubebea wanafunzi la shule ile likawa linatoka. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kulitilia mashaka gari lile, walichokifanya ni kuteremka na kisha kuanza kuangalia huku na kule.
Silaha ambazo walikuwa wamezishika zilionekana kuwaogopesha sana watu kiasi ambacho hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuwa na amani katika kipidi hicho. Walizunguka katika kila mahali sehemu hiyo huku wakiwaulizia watu mbalimbali juu ya watu ambao walikuwa wakiwatafuta.
“Mmmh! Wawili au watatu?” Kijana mmoja aliuliza.
“Watatu” Mekong alijibu.
“Watu hao niliwaona. Wawili walikuwa weusi na mmoja alikuwa mweupe tena wa nchi hii hii” Kijana yule alisema.
“Uliwaona wapi?”
“Hapa hapa Phittich”
“Wapo wapi sasa?”
“Walielekea pale shuleni. Walikuwa wakitafuta simu” Kijana yule alisema.
Mekong akamwambia Bwana Robinson kile ambacho alikuwa ameambiwa na kijana yule, Bwana Robinson akaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, maneno aliyoambiwa kwamba watu wale walionekana mahali hapo tena wakiwa wanatafuta simu yalionekana kumshtua kupita kawaida.
Kwa haraka haraka bila kupoteza muda wakaanza kuelekea katika shule ile. Kila mwalimu alionekana kushtuka, uwepo wa risasi katika mikono ya watu wale ulionekana kuwatisha kupita kawaida. Walipowafikia walimu wale, walichokifanya kwanza ni kupiga risasi hewani, hiyo ilikuwa ni kama tukio moja wapo ambalo lingeonekana kuwatisha walimu wale na hatimae kueleza ukweli.
Watu wote ambao waliusikia mlio ule wa risasi wakaanza kukimbia huku wanafunzi darasani wakilala chini kama walivyokuwa wamefundishwa na walimu wao. Wakawasogelea zaidi walimu wale na kisha Mekong kuanza kuwauliza kuhusiana na watu wale ambao walikuwa wakiwatafuta.
“Walikwenda kwa mwalimu mkuu” Mwalimu mmoja alijibu huku akitetemeka.
Hawakutaka kupoteza muda, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika ofisi ya mwalimu mkuu. Walipoufikia mlango, Mekong akaupiga teke na kisha wote kuingia ndani. Mwalimu mkuu akabaki akitetemeka, macho yake yalipokuwa yakitazama matundu ya bunduki zile yalionekana kumtisha.
“Watu wetu wapo wapi?” Mekong aliuliza huku akiikoki bunduki yake.
“Wameondoka” Mwalimu alijibu huku akitetemeka.
“Kuelekea wapi?”
“Mjini”
“Muda gani?”
“Dakika chache zilizopita, walipelekwa na basi la shule” Mwalimu alijibu.
“Kwa nini uliwaruhusu kuchukua basi la shule?”
“Nao walikuja na bunduki kama ninyi, nikaogopa” Mwalimu alidanganya.
Hawakutaka kubaki ndani ya chumba kile, walichokifanya ni kuanza kuondoka. Basi lile la shule ambalo walikuwa wamepishana nalo katika kipindi kilichopita kumbe ndilo ambalo lilikuwa limewabeba watu wao bila kujua. Bwana Robinson kama kawaida yake akaushikilia usukani na kisha kuliondoka gari lile kwa kasi ya ajabu ili kuliwahi basi lile la shule ambalo liliwabeba Williams na wenzake.
Njiani hakukuwa na stori, kila mmoja katika kipindi hicho alikuwa akifikiria lake tu. Bwana Robinson aliendesha gari kwa kasi ya ajabu huku lengo lake likiwa ni kuliwahi lile basi njiani ambapo wangewaua watu wao na kisha kurudi porini na kesho yake kuondoka kuelekea nchini Marekani.
“Ni lazima niwaue” Bwana Robinson aliseme huku kwa mbali sana akiwa analiona basi lile, tena ikiwa ni kilometa tatu kabla ya kuingia katika jiji la Bangkok.
Usiku ulionekana kuwa mrefu kwao, muda wote walionekana kutokuwa na furaha kabisa, taarifa ya kutekwa kwa mtoto wao bado ilionekana kuwasumbua vichwa kupita kawaida. Mara kwa mara walikuwa wakiangalia taarifa za habari katika televisheni kuona ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea.
Nchini China, taarifa ya kutekwa kwa ndege waliokuwa wachezaji wale ndio ilikuwa taarifa ambayo ilikuwa ikisikika sana kwa kipindi hicho, kitendo kile bado kilionekana kuwa kitendawili hasa katika kumjua mtu ambaye alikuwa amehusika katika utekaji ule.
Usiku hawakulala kama ambavyo walikuwa wakilala siku yingine, walikuwa wakiongea mambo mengi ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yao. Kitendo cha mtoto wao, Williams kuwa mmoja wa mateka wale waliokuwa wametekwa kikaonekana kuanza kuwaunganisha kwa mara nyingine tena.
Walikaa wakiongea mambo mengi, kwa mara ya kwanza toka watengane, siku hiyo wakijikuta wakianza kupigana mabusu na hatimae kujikuta wakiwa watupu huku wakifanya mapenzi kama wapenzi wengi wafanyavyo mara wanapokuwa chumbani peke yao.
Asubuhi ilipofika, hapo wakaanza kuelekea katika uwanja wa ndege wa Shanghai na kisha kuulizia ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea mahali pale na kuona kama kulikuwa na mafanikio yoyote ambayo yaliwafanya kujua mahali ambapo ndege ile ilipokuwa imepelekwa katika kipindi hicho.
Majibu ambayo waliyopewa kwamba hakukuwa na dalili zozote yalionekana kuwashtua na kuwaongezea majonzi ndani ya miono yao. Bi Latifa hakuweza kuvumiia, akajikuta akianza kulia mahali hapo. Moyo wake uliumia kupita kawaida, kuona kwamba hakukuwa na dalili za ndege ile kuonekana kulimuumiza kupita kawaida.
Siku hiyo na siku zilizoendelea ndaniya wiki hiyo ikaonekana kuwa siku ya majonzi, hakula chakula kabisa, moyo wake ulikuwa ukimfikiria mtoto wake tu, Williams ambaye alikuwa ametekwa pamoja na wachezaji wenzake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Waliendelea kukaa nchini China kwa wiki nzima na ndipo waliporudi kurudi nchini Marekani huku wakiwa hawana hata mafanikio juu ya kile ambacho kilikuwa kimewapeleka nchini China katika kipindi hicho. Kuanzia hapo, maisha ya Bi Latifa yalikuwa ni ya majonzi, mtu ambaye alikuwa akimpenda na kumthamini, katika kipindi hicho hakuwepo tena karibu nae.
Kama kulia, Bi Latifa alikuwa amelia sana, kama ni kuwa na majonzi, Bi Latifa alikuwa amekubwa na majonzi mengi hasa juu ya kumfikiria mtoto wake, Williams. Mpenzi wake, Bwana Kurt ndiye ambaye alikuwa mfariji wake mkubwa kwa wakati huo, alikuwa akimfariji katika kila hatua ambayo walikuwa wakipitia katika kipindi hicho.
Maisha yaliendelea kuwa hivyo hivyo mpaka pale ambapo taarifa zilipoanza kusikika kwamba ndege ile ilikuwa imeonekana katika msitu mkubwa uliokuwa nchini Thailand. Taarifa hiyo hiyo ilionekana kuwa taarifa nzuri sana katika masikio ya kila Mmarekani ila taarfa hiyo nzuri ilikuwa imekuja na taarifa mbaya kwamba hakukuwa na mchezaji yeyote ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo, ndege ilikuwa yenyewe.
******
Bwana Robinson alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi kupita kawaida, muonekano wa basi lile la shule ambalo lilikuwa likionekana mbali kwa mbele lilikuwa likimpa nguvu kwamba wangeweza kulifikia na hatimae kuwaua watu wale ambao walikuwa wakiwatafuta.
Kila mmoja alikuwa ameishikilia vizuri bunduki yake tayari kwa kuwamiminia risasi Williams na Phillip ambao walikuwa wakizidi kuwatafuta zaidi. Bwana Robinson hakuonekana kujali kama wangeweza kupata ajali endapo gari lile lingekanyaga jiwe au kitu kingine, kitu ambacho alikuwa akikijali kwa wakati huo ni kulifikia basi lile na kisha kutekeleza kile ambacho walikuwa wamekipanga.
Kadri walivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo walionekana kulifikia basi lile mpaka pale ambapo walifikisha umbali wa nusu kilometa. Kila mmoja akatabasamu, tayari waliona kwamba walikuwa wamelifikia basi lile ambalo liliwabeba watu wao waliokuwa wakiwahitaji kwa kipindi hicho.
Ndani ya dakika chache wakawa wamelifikia basi lile na kisha kwenda nalo sawa ubavuni huku wakichungulia chungulia katika madirisha. Kila mmoja alikuwa akishangaa, ndani ya basi lile alikuwepo dereva tu ambaye alionekana kuwa bize kuendesha basi lile.
Alichokifanya Bwana Robinson ni kumtaka dereva yule asimamishe basi lakini hali ikaonekana kuwa ngumu kwa dereva yule kutekeleza jambo hilo. Bwana Robinson akaonekana kukasirika zaidi, alichokifanya ni kupunguza mwendo na kisha kumpisha Mekong kitini na yeye kushikilia bunduki na kumwangalia dereva yule.
“Stop the bus (Simamisha basi)” Bwana Robinson alimwambia dereva yule ambaye alijifanya kama kutokusikia.
Bwana Robinson alisema zaidi na zaidi huku wakiendelea kuwa ubavuni mwa basi lile. Dereva hakuonekana kuwasikia japokuwa alijua fika kwamba kulikuwa na gari ubavuni mwa basi lile. Alichokiamuru Bwana Robinson baada ya kuona kwamba dereva wa basi lile hasikii chochote kile, akamtaka Mekong kuligoga ubavuni basi lile na ndipo dereva yule akayaguza macho yake na kuwaangalia.
“Stop the bus (Simamisha basi)” Bwana Robinson alimwambia dereva kwa sauti kubwa.
Hata kabla dereva hajafanya kile ambacho alikuwa ameambiwa, macho yake yakatua kwa mapolisi ambao walikuwa mbele kama hatua mia moja kutoka pale ambapo walikuwepo. Waasi wote ambao ndio walikuwa ndani ya gari lile wakazificha silaha zao, tayari hali ikaonekana kutoweka, hakukuonekana kama kungekuwa na uwezekano wa kutumia bunduki zile ambazo walikuwa nazo.
Ndani ya dakika moja, basi lile likaanza kuingia ndani ya jiji lile la Bangkok ambalo lilikuwa na watu wengi sana. Tayari wakaonekana kushindwa katika mpango waowote ambao walikuwa wakitaka kuufanya, Bwana Robinson akabaki akimwangalia dereva yule kwa macho yaliyojaa hasira.
Katika hali ambayo hakuitegemea, Williams na Phillip wakajitokeza dirishani na kisha kuwaangalia na kuwanyooshea vidole vya kati kitendo ambacho kilionekana kuwakasirisha watekaji wote. Katika kipindi hicho, Williams na Phillip hawakuonekana kuwa na wasiwasi kabisa, waliona kuwa na uhakika kwamba wasingeweza kuuawa kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu.
Basi lile likaeendeshwa mpaka katika sehemu ambayo ilikuwa wazi zaidi na kisha Williams na Phillip kuteremka. Mekong nae akaliendesha gari lile mpaka pembeni na kisha kuteremka. Hakukuwa na mtu ambaye aliteremka na bunduki, wote wakaziacha ndani ya gari lile na kisha kuanza kulifuata basi lile na kuufungua mlango.
Williams na Phillip pamoja na Gong hawakuonekana, walikuwa wamekwishateremka. Walichokifanya ni kumuuliza dereva mahali ambapo walipoelekea na dereva kuwaonyesha. Hawakutaka kupoteza muda mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuelekea kule.
Waliamini kwamba kwa sababu walikuwa wengi basi ingekuwa rahisi kwao kukamilisha kile ambacho walikuwa wakikitaka, kwanza kuwakamata na kisha kuwapeleka katika sehemu ambayo ilikuwa na gari lao.
Waliingia ndani zaidi na zaidi na hatimae kuwaona wakiwa wanakimbia kusonga mbele. Hapo hapo wakaanza kuwakimbiza, kutokana na Phillip kuendelea kuwa na maumivu mguuni mwake kutokana na ule mtego wa wanyama ambao ulikuwa umembana porini, alijikuta akikimbia taratibu tena kwa mwendo wa kuchechemea.
Williams hakutaka kumuacha Phillip, alichokifanya ni kumshika ubavuni na kisha kujitahidi kukimbia nae. Hawakufika mbali sana, kasi ya watu ambao walikuwa wakiwaimbiza ilikuwa kubwa, wakawafikia na kisha kuwakamata. Kwa kuwa Gong hawakuwa na haja nae katika kipindi hicho, wakamwambia aondoke zake ila walichokifanya ni kuondoka na Wiliams na mwenzake, Phillip kuelekea katika sehemu walipoliacha gari lao na kisha kuanza kuelekea porini ambapo huko wangeweza kuwaua na kuwa mwisho wa kila kitu.
“You will never run from me (Kamwe hamuwezi kunikimbia)” Bwana Robinson aliwaambia huku akionekana kukasirika na huku vijana wake wakiwa wamewashika Williams na Phillip ambao walikuwa wakioba msamaha japokuwa walijiona kutokuwa na kosa lolote.
“I will kill you like I the way I killed you team mates (Nitawaua kama nilivyowaua wachezaji wenzenu)” Bwana Robinson aliwaambia huku hasira zake zikiwa zinazidi kuongezeka kadri sekunde zilivyozidi kwenda mbele.
Simu ambayo aliipokea mkuu wa kitengo cha upelelezi cha FBI, Bwana Mikey Swan ilionekana kmshtusha kupita kawaida, hakuamini kama katika kipindi hicho mpelelezi Sam alikuwa amefanikiwa kuiona ndege ambayo iliwabeba wachezaji wa mpira wa kikapu wa klabu ya New Bucketts na kutekwa.
Kwa haraka haraka pasipo kupoteza muda wowote ule akapiga simu katika vitengo vingine na kutoa amri kwamba ilikuwa ni lazima ndege ya kivita ya Pantion Air 52 ambayo ilikuwa ikitumika sana kubeba mabomu makubwa ya kivita kama B52 ielekee nchini Thailand na kisha kutua katika uwanja huo ambao ulikuwa hapo msituni huku ikiwa imebeba marubani kadhaa pamoja na mafundi kwa ajili ya kuangalia kama ndege ile ilikuwa na matatizo yoyote yale.
Kila kitu ambacho kilitakiwa kufanyika katika kipindi hicho kilifanyika kwa haraka haraka sana, ndege hiyo ikaandaliwa, ndege ambayo wala haikuhitaji kutembea umbali fulani ndio ipae au itue huku ikiwa imetembea hatua fulani, ndege hiyo kubwa ya kivita ilikuwa na uwezo mkubwa wa kusimama sehemu moja kama helkopta katika kipindi ambacho inatua na kupaa.
Wanajeshi kumi ambao walikuwa na bunduki kali kama zile ambazo zilitumika katika vita vya Wamarekani na Wairaq mwaka 1992 wakaingia ndani ya ndege hiyo huku wakiwa na marubani wa kijeshi pamoja na mafundi wanne ambao walibeba vifaa vyote ambavyo vingeweza kuhitajika mahali kule walipokuwa wakielekea katika kipindi hicho.
Kasi ya ndege ile ilikuwa kubwa sana, ilikuwa ni zaidi ya ndege ya rais wa Marekani, Air force One Ndege ile ilichukua dakika arobaini na tano kutoka nchini Marekani mpaka kuingia ndani ya nchi ya Thailand na kisha kuanza kuelekea katika msitu huo mkubwa wa Chian Rai.
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Watu themanini na nne walikuwa wakimsubiria Sam ambaye alikuwa ameingia ndani ya ndege ile kwa ajili ya kuangalia kama kulikuwa salama. Kila mmoja mahali pale alionekana kuwa na furaha, hawakuamini kama katika kipindi hicho walikuwa wamefanikiwa kuiona ndege ambayo wala hawakuwa wakifahamu ni nani ambaye alikuwa amekuja nayo mahali pale.
Kila mmoja alikuwa na kimuemue cha kutaka kuingia ndani ya ndege ile, kwa asilimia kubwa mioyoni mwao, waliona kwamba katika kipindi hicho walikuwa wamekwishafanikiwa kuingia katika nchi yao. Matatizo makubwa ambayo walikuwa wamepitia katika maisha yao ya nyuma, katika kipindi hicho waliona kuwa walitakiwa kuyasahau kwani maisha ya raha yalikuwa yakianza tena maishani mwao.
Maisha ya ndani ya pango lile yalionekana kuwa kama historia ambayo ingeendelea kubaki katika maisha yao yote. Hakukuwa na mtu ambaye alitamani kubaki ndani ya msitu ule, wengine walikuwa hawakwenda nyumbani kwao kwa zaidi ya miaka kumi, katika kipindi hicho walikuwa wakihitaji kuelekea nyumbani kwao kuonana na ndugu zao.
Sam alionekana akichelewa kutoka ndani ya ndege ile jambo lililowafanya watu wale kuanza kufikiria mambo mengine. Huku kila mmoja akiwa kimya kumsikilizia Sam, mara sauti za mbwa zikaanza kusikika kutoka katika miti ile mikubwa hali ambayo ikawafanya watu wale kuanza kutetemeka kwa hofu.
Kadri sekunde zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo mbwa wale walivyozidi kusikika zaidi na zaidi tena wakisikika kwamba walikuwa wakija katika sehemu ambayo walikuwa wamesimama. Japokuwa mbwa wale hawakuwa wakionekana machoni mwao kutokana na kuendelea kusogea kutoka kule kwenye miti, lakini tayari walikwishajua kwamba mbwa wale walikuwa wakija kule walipokuwa.
Walichokifanya ni kuanza kukimbia, hakukuwa na mtu ambaye alidiriki kumsubiria Sam ambaye alikuwa ndani ya ndege ile. Mbio zao zikaishika katikati ya miti na kisha kuanza kuchungulia kuona ni wakina nani ambao walikuwa wakija mahali pale.
Wanaume zaidi ya ishirini ambao walikuwa na mbwa walioonekana kuwa wakali wakaanza kuonekana machoni mwao. Kila mmoja akabaki akitetemeka, watu wale walionekana kuwa makatili kutokana na jinsi walivyovaa pamoja na bunduki ambazo walikuwa wamezishika.
Mbwa wale walikuwa wakizidi kupiga kelele, tayari walionekana kujua kwamba kulikuwa na uwepo wa watu kutoka umbali fulani pale walipokuwa. Kila mmoja akaonekana kuwa na wasiwasi, tayari ubwekaji wa mbwa wale ulionekana kuanza kuwatia wasiwasi kupita kawaida.
Walipoiona ndege ile wakaanza kuifuata. Ubwekaji wa mbwa wale ndio ambao uliwafanya kuanza kuzikoki bunduki zao tayari kwa kumfyatulia risasi mtu yeyote ambaye angeonekana mbele ya macho yao. Walizidi kuisogelea ndege ile zaidi na zaidi, mpaka walipofika hatua ushirini kabla ya kuifikia, mara mlio mkubwa wa ndege ya kijeshi ukaanza kusikika angani.
Kila mmoja akayapeleka macho yake angani, ndege kubwa ya Pantion Air 52 ilikuwa ikionekana angani. Hata kabla hawajaulizana nini cha kufanya, wakaanza kuipiga risasi ndege ile ambayo wala haikuwa juu sana. Risasi zao zilionekana kuwa si kitu, rubani wa ndege ile alipoziruhusu risasi zitoke, ndani ya sekunde kumi zilikuwa zimewaingia watu wote pamoja na mbwa wao.
Ndege ile ikaanza kutua chini huku wanajeshi wakiruka na kisha kuangalia huku na kule. Tayari kila mmoja alionekana kugundua kwamba sehemu ile ilikuwa ni ya hatari sana, hivyo walihitajika kuangalia katika kila upande kwa makini zaidi. Wanajeshi wale walipohakikisha kwamba kila kitu mahali pale kilikuwa salama, hapo ndipo marubani wale pamoja na mafundi wa ndege wakateremka na kuanza kuisogelea.
“Who are you? (Wewe nani?)” Mwanajeshi mmoja alimuuliza Sam katika kipindi alichoingia ndani ya ndege ile na kumkuta akiwa amekaa kitini amejiinamia. Sam alipoinua macho yake, wakaonekana kumfahamu mtu wao.
Walichokifanya marubani wale ni kuelekea katika sehemu ya marubani na kisha kuiwasha ndege ile. Marubani wakaangalia kila kitu, ndege haikuonekana kuwa na tatizo lolote lile hali iliyowafanya mafundi kutofanya kazi yoyote ambayo walitarajia kuifanya mara waifikiapo ndege ile.
“We have to go back home (Inabidi turudi nyumbani)” Mwanajeshi mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi alimwambia Sam.
“No! I have to stay here (Hapana. Itanibidi nibaki hapa)” Sam alijibu.
“Why(Kwa nini?)”
“I have not complited my work that brought me here (Sijaimaliza kazi iliyonileta hapa)” Sam alimwambia.
“Didnt you see them? (Haukuwaona?)”
“Yeah!”
Msimamo ambao alikuwa ameuweka Sam ndio ambao alikuwa ameuweka mahali hapo na ndio ambao alitakiwa kuusimamia. Hakutaka kuondoka kuelekea nyumbani, alihitaji kubaki msituni pale mpaka katika kipindi ambacho angekamilisha kazi ile ambayo ilikuwa imemfanya kuwa mahali pale.
Kila mmoja alionekana kumuelewa, walichokifanya ni kujiandaa na kurudi nchini Marekani kuendelea na mambo mengine huku wakiwa wamekwishatoa taarifa kwamba ndege ilipatikana ikiwa katika hali nzuri bila matatizo yoyote yale. Amri ambayo ilitolewa na Bwana Swan ni kwamba hata wanajeshi wale walitakiwa kubaki kulekule msituni kwa kuwatafuta wachezaji ambao walikuwa wametekwa kwani kwa hali ambayo ilionekana, mateka hawakuwa mbali kutoka hapo.
“Kuna tu niliwaokoa huku msituni ila sifahamu wapo wapi” Sam alimwambia mwanajeshi yule.
“Watu gani?”
“Subiri”
Sam akatoka ndani ya ndege ile na kisha kuanza kuita, aliita kwa muda wa zaidi ya dakika mbili, mara watu wale ambao walikuwa wamejificha wakatokea jambo ambalo muonekano wao ulionekana kuwashangaza wanajeshi na marubani wote.
“Wakina nani hawa?”
“Mtawafahamu baadae. Ila kwanza watu hawa wangekwenda nyumbani kwa kutumia ndege hii. Sisi tuingieni zaidi msitunikuwatafuta mateka” Sam aliwaambia huku akichukua bunduki moja na kuikoki.
“Basi hwa itabidi waende nchini Marekani pamoja na ndege hii ya wachezaji na kisha sisi kuingia zaidi ndani ya msiti huu” Mwanajeshi yule alisema.
“Hiyo ndio maana yangu”
Hakukuwa na kitu cha kuchelewesha, moja kwa moja watu wale themanini na nne wakaingia katika ndege ile na kisha kuwashwa na kupaa kuelekea nchini Marekani huku wanajeshi wakibaki mahali pale pamoja na ndege ile ya kijeshi ya Pantion Air 52.
“Tuingieni msituni, watu kumi na moja tunatosha kabisa” Sam aliwaambia.
Wanajeshi wale wakajikoki zaidi na kisha kuingia zaidi msituni huku kila mmoja akiwa na lengo moja, kuwakuokoa wachezaji ambao walikuwa wamechukuliwa mateka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mishemishe za watu waliokuwa jijini Baghkok bado zilikuwa zikiendelea kama kawaida. Watu walionekana kutembea kwa mwendo wa haraka haraka huku wakionekana kuwahi nyumbani kwao. Wakinamama ambao walikuwa wakiuza vitu mbalimbali kama mboga za majani bado walikuwa wakiendelea na biashara yao katika masoko mbalimbali ambayo yalikuwa yakipatikana katika sehemu maalumu ndani ya jiji hilo.
Kwa wale watu ambao walikuwa wakitoka nje ya jiji hilo, usafiri wa tembo ndio ambao ulikuwa ukitumika mara kwa mara. Mapolisi ambao walikuwa na bunduki nao hawakuwa mbali, walikuwa wakilandalanda huku na kule kana kwamba walikuwa wakimtafuta mtu fulani, kwa kifupi, katika kipindi hicho kila mtu alikuwa akionekana kuwa bize kupita kawaida.
Sehemu za kupaki magari zilikuwa chache sana tena zikiwa sehemu ambazo zilikuwa zimetengwa katika maeneo ambayo yalionekana kutokuwa salama kabisa. Kutokana na watu wengi waliokuwa na magari nchini Thailand kuvunja sana sheria za barabarani hasa katika kupaki magari yao, hapo ndipo ilipoanzishwa sheria maalumu ya kuegesha magari ambayo ilionekana kuwapa tabu sana madereva huku mtu ambaye alikuwa akivunja sheria hiyo akiwa anapigwa faini kiasi kikubwa sana.
Madereva walionekana kuogopa, kuanzia hapo wakawa na nidhamu ya kupaki magari yao katika maeneo ambayo yalikuwa yametengwa maalumu kwa ajili ya kupaki magari yale. Mara kwa mara mapolisi ambao walionekana kuwa na hamu ya kuwakamata madereva ambao walikuwa wakipaki magari katika sehemu zisizoruhusiwa walikuwa wakizunguka zunguka sana hapo mjini lakini hawakuwa wakimuona mtu yeyote ambaye alikuwa akivunja sheria hiyo.
Siku hii ambayo mawingu yalikuwa yametanda angani ndio ilikuwa siku ambayo mapolisi walionekana kufurahi sana hasa mara baada ya macho yao kutua katika gari ambalo lilikuwa limepakiwa katika sehemu ambayo wala haikuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya kupakia magari. Mapolisi watano ambao walikuwa wameshika bunduki zao mikononi mwao wakaanza kulisogelea gari lile aina ya Pick Up ambayo ilionekana kuchoka sana.
Katika kila hatua ambayo walikuwa wakiipiga kulisogelea gari lile, nyuso zao zilikuwa zikionyesha tabasamu pana jambo ambalo lilioonyesha kwamba walikuwa wakienda kuchukua japo kiasi kidogo kwa dereva ambaye alikuwa amevunja sheria ile ya kuliegesha gari lile.
Mara baada ya mapolisi kulifikia gari lile, wakaanza kuangalia ndani ya lile gari kule nyuma, macho yao yakatua katika bunduki kadhaa ambazo zilikuwa zimewekwa katika gari lile. Mapolisi wote wakaonekana kushtuka, uwepo wa bunduki zile uliwafanya kuanza kuhisi mambo fulani fulani vichwani mwao.
Walichokifanya ni kuanza kuangalia huku na kule, tayari wakaonekana kuwa na wasiwasi, hata kabla hawajaamua ni kipi ambacho walitakiwa kukifanya kwa wakati huo, mara macho yao yakatua kwa vijana kadhaa ambao walikuwa wamewashikilia vijana wawili ambao walikuwa wakiongea maneno mengi.
Macho ya mapolisi wale yalipogongana na macho ya watekaji wale ambao walikuwa wakiongozwa na Bwana Robinson, wote wakaonekana kushtuka. Kwa presha ambayo walikuwa nayo katika kipindi hicho huku wakijua dhahiri kwamba mapolisi wale walikuwa wameziona bunduki zile, watekaji wale wakawaachia Williams na Phillip na kisha kuanza kukimbia.
Mapolisi wale wakaanza kupiga filimbi kama tukio la kuwaita mapolisi wenzao ambao walikuwa wakiendelea kuzurura hapa na pale maeneo yale ya mjini. Hakukuwa na cha kusubiria, kwa haraka sana na bila kujiuliza chochote kile, mapolisi wale wakaanza kuwakimbiza vijana wale huku kukiwa hakujabakia hata polisi mmoja katika gari lile.
Milio ya risasi ikaanza kusikika ikilia hewani kuashiria kwamba mapolisi wale walikuwa wamedhamiria kutumia risasi katika kipindi kile. Williams, Phillip na Bwana walikuwa wamesimama pale pale walipokuwa, kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, walionekana kutokuwa na tatizo lolote lile.
“Tukimbie” Phillip alimwambia Williams huku wakimwangalia Bwana Robinson ambaye alionekana kuwa na hasira.
“Kwa nini tukimbie? Wewe tutembee tu. Hana risasi huyu. Huu ndio mwisho wa kila kitu. Tuanze safari ya kuelekea nyumbani” Williams alimwambia Phillip.
Wote wakaanza kutembea, Bwana Robinson alibaki mahali pale huku akiwaangalia kwa hasira. Moyoni mwake alitamani kama angekuwa na bunduki na kuweza kuwamiminia risasi wote ili kila kitu kiwe mwisho kabisa. Kwa kuondoka vile kulimaanisha kwamba wangeanza safari ya kuelekea nchini Marekani ambako huko kila kitu kingeelezwa na hivyo kufungwa jela maisha au kuhukumiwa kunyongwa.
Bwana Robinson alibaki mahali pale akiwa amesimama huku akionekana kama amemwagiwa maji ya baridi katika kipindi cha baridi kali, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya mahali pale. Huku akiwa katika hali ile, mara ghafla wazo la kufanya jambo fulani likawa limemjia kichwani, kwa wakati huu aliona bora kama angefanya kitu chochote ili awauwe Williams na Phillip na kisha kuendelea na maisha yake, alichokuwa akikiamini kwa wakati huo, asingeweza kupata tatizo kabisa, angetumia fedha kwa polisi yeyote ambaye angeonekana kumsumbua hapo Thaila.
“Nawaua” Bwana Robinson alijisemea.
Hapo hapo na kwa haraka haraka akaanza kulisogelea gari lile ambalo walikuja nalo na kisha kuufungua mlango wa mbele na kuichukua bunduki yake ndogo ambayo alikuwa ameiacha kwenye kiti. Tayari katika kipindi hicho Bwana Robinson alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, alijiona kuwa radhi kufanya kitu chochote kile.
Mara baada ya Williams na Phillip kuona hivyo, wakaanza kukimbia. Bwana Robinso hakutaka kuchelewa, alichokifanya mahali hapo ni kuanza kupiga risasi. Milio ya risasi ile ikaonekana kuwashtua wananchi kupita kawaida, wakaanza kukimbia huku na kule huku wengine wakipiga kelele kupita kawaida.
Siku hiyo ikaonekana kuwa kama vita ndani ya jiji la Bangkok, milio ya risasi ilikuwa ikionekana kutawala kila sehemu mahali hapo. Watu walikuwa wakiendelea kukimbia ovyo huku Bwana Robinson akizidi kuwakimbiza Williams na Phillip ambao walijiona dhahiri kuwa katika siku za mwisho za uhai wao. Hawakukata tamaa, kifo kilionekana kuwa karibu yao, walikuwa wakiendelea kukimbia zaidi na zaidi huku Bwana Robinson akiendelea kuwakimbiza zaidi na zaidi huku akiwamiminia risasi.
Walikimbia kwa kasi mpaka kutoka mjini na kuanza kuingia mitaani. Kila milio ya risasi iliposikika, watu walikuwa wakikimbia huku na kule huku kila mmoja akionekana kutaka kuyaokoa maisha yake katika kipindi hicho. Williams na Phillip walikimbia mpaka kufika katika sehemu ambayo walionekana kutokuwa na jinsi ya kujinusuru, mbele yao kulionekana kuwa na ukuta mkubwa, kwa Williams ilikuwa ni rahisi kuupanda ukuta ule na hatimae kurukia upande wa pili, ila kwa Phillip ambaye alikuwa akiendelea kuchechemea, alionekana kutokuweza.
“Tufanye nini sasa?” Williams alimuuliza Phillip huku wote wakihema sana.
“Ruka uondoke”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Niruke niondoke! Na wewe je?” Williams alimuuliza.
“Acha nife hapa” Phillip alisema huku akionekana kutoweza kupandisha ukuta ule.
Hata kabla hawajaamua nini cha kufanya, mara Bwana Robinson akatokea mahali hapo huku akiwa na bunduki yake mkononi na huku akihema kupita kawaida. Alipowaona mbele yake, akaachia tabasamu kubwa lilionekana kuwa na mafanikio makubwa.
“Hatimae nimewakamata. Niliwaambia hamtofika nchini Marekani, Huu ndio mwisho wenu” Bwana Robinson aliwaambia huku akiwa amewanyooshea bunduki ile.
Je nini kitaendelea?
Je Huo ndio mwisho wa kila kitu?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment