Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

HILI NI JIJI LA NEW YORK - 3

 





    Simulizi : Hili Ni Jiji La New York

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Kila mmoja alibaki kama amechanganyikiwa, mauti ndicho kitu ambacho kilikuwa kikionekana mbele ya macho yao, mioyo yao kwa wakati huo ilikuwa ikisali sala ya mwisho ya kutaka kujikomboa kutoka katika mikono ya Bwana Robinson ambaye alionekana kuwa na hasira kupita kawaida. Alikuwa tayari kufanya kila kitu kwa wakati huo, tena kuwaua tu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Machale yakaonekana kumcheza Bwana Robinson, alichokifanya ni kuziangalia risasi ambazo zilikuwa zimebakia ndani ya bunduki yake, ilikuwa imebaki risasi moja tu. Hiyo ikaonekana kuwa si hali nzuri, ilimaanisha kwamba kama angeweza kumpiga risasi mtu mmoja, mwingine angebaki hai na hivyo kutokutimiza kile ambacho alikuwa amekipanga.

    Akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikifanya kazi kwa haraka sana kuliko siku nyingine, wazo ambalo lilimjia kichwani mwake ndilo ambalo lilikuwa linaonekana kufaa kufanyika mahali hapo. Alichokifanya ni kuimalizia ile risasi moja kwa kupiga hewani, watu ambao walikuwa wamejificha waliendelea kujificha zaidi, baada ya kuipiga risasi hiyo, akaanza kuifuta futa kisiri na kisha kumgawia Williams ambaye alikuwa hajui kama risasi zilikuwa zimekwisha ndani ya bunduki ile.

    “Just kill me now. I have done worst thing in my life (Niue sasa. Nimefanya mambo mabaya maishani mwangu)” Bwana Robinson alimwambia Williams huku akiwa anamkabidhi bunduki ile, tena akiwa ameishika kwa kutumia koti lake alilokuwa amelivua.

    Williams na Phillip wakaonekana kushangaa, hawakujua Bwana Robinson alimaanisha nini mpaka kuamua kuwapa bunduki huku akitaka auawe yeye. Hakukuwa na cha kujiuliza tena, alichokifanya Williams ni kuichukua bunduki ile na kisha kumnyooshea Bwana Robinson maeneo ya kichwani. Picha za matukio ya nyuma ya kuuawa kwa marafiki zake msituni zikaanza kumjia kichwani, kadri alivyokuwa akifikiria zaidi na ndivyo ambavyo hasira zilivyokuwa zikizidi kumjia moyoni zaidi na zaidi.

    Kwa yale ambayo Bwana Robinson alikuwa ameyafanya katika kipindi cha nyuma yalitosa kabisa kummiminia risasi mfululizo na kisa kumuua, hakuonekana kama alistahili kupona mahali hapo. Williams akaanza kutokwa na machozi, hasira ambazo alikuwa nazo juu ya mzee yule zilionekana kumshinda na hatimae kumliza.

    “Taa taa taa” Bunduki ililia mara baada ya kubonyeza kitufe, mlio ambao ulimaanisha kwamba hakukuwa na risasi.

    “Bullshit....!” Williams aijisemea huku akiendelea kung’ang’ania bunduki itoe risasi.

    Bwana Robinson alibaki kimya pale chini alipokuwa amepiga magoti, kwa kila kilichokuwa kikiendelea mahali pale kilionekana kumfurahisha. Mara milio ya risasi ikaanza kusikika kwa mbali, alichokifanya Williams pamoja na Phillip ni kuanza kukimbia mahali hapo huku akiwa ameiacha bunduki ile chini.

    Ni ndani ya dakika kadhaa, mapolisi wakafika mahali hapo na kushangazwa na hali ambayo walimkuta nayo Bwana Robinson huku mbele yake kukiwa na bunduki. Wakaanza kumfuata mzee huyo na kisha kumuinamia huku polisi mwingine akiifuata bunduki ile.

    “Don’t touch it (Usiiguse)” Bwana Robinson alimwambia polisi yule ambaye alionekana kushtuka.

    “This is my evidence (Huu ni ushahidi wangu)” Bwana Robinson aliwaambia huku akiichukua bunduki ile kwa kutumi kitambaa chake cha mkononi tena akiwa ameishika kwa umakini.

    Mapolisi hawakutaka kumuacha mahali pale, walichokifanya ni kumchukua na kuanza kuelekea nae katika kituo cha polisi ambapo huko akaanza kujitambulisha kwamba alikuwa ametokea nchini Marekani, maelezo yake ya dakika tano yakawafanya mapolisi wote kumgundua.

    “We know you (Tunakufahamu)” Mkuu wa kituo kile cha polisi alimwambia.

    Bwana Robinso hakutaka kuongea kitu chochote cha ukweli mahali hapo, kila kitu ambacho alikuwa akikielezea kilikuwa ni uongo kabisa. Maneno ambayo aliyaongea kwamba Williams alitaka kumuua yalionekana kumshtua kila mtu mahali pale huku akidai kwamba Williams ndiye ambaye alikuwa amehusika na mauaji yote ambayo yalikuwa yamefanyika msituni, mauaji ya wachezaji mpira wa kikapu.

    Maneno yale yaliwashtua zaidi, kilichofanyika kwa wakati huo ni kuchukulia kwa ile bunduki na kisha kuweka kwenye kifuko kidogo cha nailoni na kisha kuituma Marekani huku Bwana Robinson nae akielekea huko na ushahidi wake wa kuieleza Marekani kwama Williams ndiye ambaye alikuwa akihusika kwa kila kitu huku hata akitaka kumuua yeye mwenyewe.

    Maneno yale yaliposikika katika masikio ya mapolisi nchini Marekani yakaonekana kutokuaminika lakini mara baada ya bunduki ile kuchukuliwa na kuanza kupimwa, alama za vidole zilikuwa ni za Williams jambo ambalo lilionekana kumshtua kila mtu mahali hapo.

    “Baada ya kila kitu, akakimbilia Bangkok, alipiga risasi nyingi sana kwa kuamini kwamba hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akimuona, mwisho wa siku aliponiona, alitaka kunipiga risasi lakini akajikuta akiwa amemaliza risasi zote” Bwana Robinson alisema huku akionekana kuwa na huruma.

    “Kwa muonekano wake ulikuwa vipi wakati huo?” Mkuu wa polisi wa jiji la New York alimuuliza.

    “Alikuwa na shati lililokuwa na damu mwili mzima, Williams alikuwa amebadilika, kwa mtazamo alionekana kuwa kama simba mwenye hasira kali. Damu ambazo alikuwa amezimwaga msituni zilikuwa zimemchanganya sana” Bwana Robinson alimwambia.

    “Sasa ilikuwaje wewe kwenda Bangkok?”

    “Nilikwenda nchini Thailand kwa sababu kuna nyumba ya kifahari nilikuwa nakwenda kuinunua kule katika ufukwe wa Panchok. Nilipofika kule, kuna tetesi ambazo nilizisikia kwamba kuna ndege imetua katika msitu wa Chein Rai, nilichokifanya ni kwenda huko kwani nilijua fika kwamba kuna habari kwamba ndege ya wachezaji ilikuwa imetekwa. Nilipofika kule, nikatekwa na watu ambao walikuwa wamekula njama na Williams, kwa hiyo wakataka kuniuaila kwa bahati nzuri nikaokolewa na wakulima waliokuwa na mashamba msituni humo” Bwana Robinson alisema.

    “Sasa ilikuwa vipi ukawa Bangkok?”

    “William hakuonekana kukubali alijua fika kwamba ningekuja huku na kisha kuusema uovu wake, hivyo alichokitaka kukifanya ni kuniua tu. Aliwatuma watu wake wanitafute, na kweli alipokuja Bangkok, akanikuta huku vijana wake wakiwa wamekimbizwa na mapolisi hasa mara baada ya kulikuta gari ambalo alikuwa akilitumia pamoja na vijana wake likiwa na bunduki. Mapolisi waliwakimbiza, ila yeye hakutiliwa mashaka hata kidogo. Baada ya muda, akanikuta nikiwa nakimbia, akaniweka chini ya ulinzi. Alipoona kwamba mahali pale kulikuwa na watu, akaanza kupiga risasi juu na hivyo watu kukimbia. Akanitaka nisali sala ya mwisho, nikasali, alipotaka kunipiga risasi, Mungu alikuwa upande wangu, risasi zilikuwa zimekwisha ndani ya bunduki ile, kwa kuchanganyikiwa zaidi, akaitupa bunduki ile chini na kuanza kukimbia kwani mapolisi walikuwa wakipiga risasi sana na hivyo kumchanganya. INATIA HURUMA SANA” Bwana Robinson aliwaeleza.

    Maneno mengi ambayo yalikuwa yameongelewa kinywani mwake yakaanza kueleweka huku ushahidi wa alama za vidole ambazo zilikuwa zimekutwa zikiwa ushahidi tosha kwamba Williams alikuwa amehusika katika mauaji yote ambayo yalikuwa yametokea msituni nchini Thailand.

    Taarifa ile ile ilipotangazwa rasmi, kila mtu akaonekana kushtuka, hakukuwa na mtu ambaye aliamini kwamba Williams alikuwa amehusika katika mauaji yale. Taarifa za kupimwa kwa alama za vidole vyake zilipotangazwa, kila mtu akapigwa na bumbuwazi. Waliotaka kulia wakaanza kulia, waliotaka kukemea vitendo vya mauaji ambavyo vilikuwa vimefanyika wakaanza kulaani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mashabiki wote wa mchezo wa mpira wa kikapu ambao walikuwa na picha za Williams pamoja na jezi za Williams wakaanza kuzichoma moto, mapenzi yao yakaonekana kutoweka kama upepo kabisa mioyoni mwao juu ya Williams ambaye kwao alionekana kuwa kama gaidi namba moja. Kitita cha dola milioni mia mbili kikatangazwa kwa mtu ambaye angeweza kufanikisha kukamatwa kwa Williams ambaye mpaka katika kipindi hicho alikuwa nchini Thailand.

    “MOST WANTED” Yalikuwa maneno ambayo yalikuwa yakisomeka katika kila picha ambayo ilikuwa ikibandikwa mitaani au kuonekana katika televisheni mbalimbali. Wapelelezi wa shirika la F.B.Ipamoja na C.I.A wakaingia kazini, wakamiminika nchini Thailand kwa ajili ya kufanikishwa kukamatwa kwa mtu mmoja ambaye alikuwa ameua watu wengi, tena watu ambao walikuwa wameliletea sifa taifa la Marekani katika masuala ya michezo.

    “NI LAZIMA AKAMATWE” Kila mmoja alisema kwa hasira.





    Hakukuwa na kitu cha kuchelewa mahali hapo, walichokifanya wanajeshi wale ni kuanza kuingia msituni huku mikononi mwao wakiwa na bunduki tayari kwa kushambulia kila hatari ambayo wangeweza kukutana mbele yao. Walikuwa wakitembea kwa mwendo wa tahadhali kabisa, macho yao yalikuwa makini kuangalia katika kila kona msituni mule.

    Msitu bado ulikuwa ukionekana kutisha kupita kawaida, mioyo yao ilikuwa ikihofia lakini wakati mwingine walikuwa wakijipa moyo kutokana na silaha ambazo walikuwa nazo katika kipindi hicho. Walizidi kusonga mbele zaidi na zaidi huku macho yao yakiwa makini kabisa. Msitu huo haukuonekana kuwa msitu wa kawaida, utisho ulikuwa mkubwa sana mbele yao.

    Miti minene ambayo ilikuwa imechanua sana juu na kuufanya mwanga kutokuingia vizuri msituni mule ulilifanya hata giza kutawala msituni mule. Nyasi zilikuwa kubwa kupita kawaida kiasi ambacho zilikuwa zikiwafikia viunoni mwao. Hatari ndicho kitu ambacho kilikuwa kikionekana mbele yao kwa wakati huo, ila pamoja na hayo yote, wala hawakutaka kurudi nyuma, waliendelea kusonga mbele zaidi na zaidi.

    Uwepo wa ndege ile mahali pale walipoikuta walikuwa na uhakika kwa asilimia mia moja kwamba hata wachezaji wale ambao walikuwa wametekwa hawakuwa mbali kutoka mahali pale walipokuwa. Kila mmoja alikuwa akijipa uhakika, umakini wao ulikuwa mkubwa sana, walikuwa wakiona kila dalili ya kufanikiwa kile ambacho kilikuwa kimeendelea pamoja na kuwaokoa wachezaji hao kutoka katika mikono ya watekaji.

    Waliendelea mbele zaidi, hali ya hewa ikaanza kubadilika, kivuli kikubwa ambacho kilisababisha kigiza fulani kikaanza kuongezeka msituni mule hali iliyoonyesha kwamba mawingu yalikuwa yamejikusanya kama dalili za mvua kubwa kutaka kunyesha mahali hapo. Hakukuwa na mtu ambaye alisimama, bado walikuwa wakiendelea kusonga mbele zaidi, kitu ambacho walikuwa wakikitaka mahali hapo ni kuwaokoa wachezaji mpira wa kikapu wa timu ya New Bucketts na kisha kurudi nao nchini Marekani.

    Walitembea kwa masaa zaidi ya matatu na ndipo kwa mbali mbele yao wakaanza kuona nyuma moja kubwa kidogo ambayo ilionekana kuwa kama gofu. Walichokifanya kwanza, wote wakajificha kwa kuchuchumaa. Mwanajeshi mmoja akachukua darubini yake na kisha kuanza kuangalia kule. Hakukuonekana kuwa na mtu yeyote yule, katika kila sehemu ambayo alikuwa akiiangalia kwa wakati huo, hakukuonekana kuwa na mtu hata mmoja.

    Alichokifanya ni kuwapa wenzake ishara ya kusonga mbele huku wakiwa wanatambaa kama nyoka. Akili zao kwa wakati huo ziliwaambia kwamba pale ndipo ambapo wachezaji wale walipokuwa wametekwa na kupelekwa, hivyo walitakiwa kwenda kwa uangarifu mkubwa kutokana na uwezekano wa watekaji kuwepo mahali pale.

    Kuni ambazo zilionekana kuteketezwa na moto usiku uliopita zilikuwa zikionekana kimafungua katika maeneo mengi mahali pale. Hawakuonekana kujali sana, katika kila sehemu ambayo walikuwa wakiifikia, walikuwa makini kupita kawaida huku bunduki zao zikiwa tayari kwa chochote mahali hapo. Walitambaa mpaka kulifikia gofu lile na kisha mpelelezi Sam pamoja na mwanajeshi mmoja kuingia ndani huku wenzao wakiwa nje wakiwasubiria, tena huku wakiwa wamejificha.

    Ndani ya gofu ile walijaribu kuangalia katika kila chumba, hakukuwa na dalili za kuwepo mtu yeyote yule. Walipoona hakukuwa na mtu yeyote yule, wakatoka ndani ya chumba kile na kuanza kutembea tembea ndani ya eneo lile. Hapo ndipo ambapo walipokutana na sehemu ambayo ilikuwa na shimo lililokuwa limefukiwa, kwa haraka hara Sam akapiga magoti chini na kuanza kufukua.

    Wanajeshi wengine walipoona hivyo, nao wakapiga magoti chini na kisha kuanza kumsaida kufukua. Walikuwa wakifukua kwa haraka sana, tayari walikuwa wamekwishahisi kwamba mahli hapo kulikuwa kumefukiwa kitu ambacho wakajikuta kuwa na hamu ya kutaka kufahamu ni kitu gani. Walitumia muda wa dakika mbili, nguo zikaanza kuonekana.

    Kila mmoja akashtuka kupita kawaida, wakafukua zaidi na kuutoa mwili ule, baada ya kuuangalia usoni, ulikuwa ni mwili wa Simpson. Kila mmoja akaanza kupata uhakika kwamba ile ndio ilikuwa sehemu ambayo wachezaji wale walipokuwa wamehifadhiwa baada ya kutekwa. Wanajeshi wale walichokifanya pamoja na Sam ni kuanza kuangalia zaidi katika eneo lile kama wangeweza kuona kama kulikuwa na miili mingine.

    Kitu kingine ambacho walikiona ni maganda ya risasi ambayo yalikuwa mengi sana, hapo wakaona kwamba kulikuwa na risasi kadhaa ambazo zilikuwa zimepigwa, walichokifanya ni kuanza kwenda mbele kuona ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea.

    “Kutakuwa na kitu zaidi hapa” Mwanajeshi mmoja, Kielon alimwambia Sam.

    “Hata mimi ninaona hivyo hivyo” Sam alimwambia huku wakianzakusonga mbele.

    Hawakutembea umbali mrefu sana na ndipo macho yao yakatua katika miili kadhaa ya wachezaji ambao walikuwa wamepigwa risasi na kufa. Kila mmoja akaonekana kushtuka, kadri walicyokuwa wakipiga hatua mbele zaidi na ndivyo ambavyo miili ile ilivyozidi kuonekana zaidi na zaidi machoni mwao. Hali ambayoilionekana ilikuwa imewatisha na kuwahuzunisha kupita kawaida, vijana wadogo ambao walikuwa wakitafuta mafanikio walikuwa wamepigwa risasi na kuuawa.

    Hasira zikaongezeka zaidi, kuuawa kwa wachezaji wale kulionekana kuwatia hasira kupita kawaida. Kilichoendelea mahali hapo ni kuchukua simu zao na kisha kupiga nchini Marekani na kuwaeleza kile ambacho kilikuwa kimeendelea msituni mule. Walichokuwa wakikihitaji ni kuletewa magari msituni mule kwa kutumia ndege kubwa za kivita na kisha kuipakiza miili ile tayari kwa kurudi nayo nchini Marekani.

    Mpaka katika kipindi hicho, tayari walikuwa wameiona miili ishirini huku mingine ikiwa haijaonekana jambo ambalo liliwafanya kuendelea kuitafuta zaidi na zaidi mpaka kuipata yote isipokuwa miili mitatu tu, Williams, Phillip na Bruce ambaye aliuawa pembezoni mwa mto.

    Ni ndani ya masaa matatu ndege kubwa ya kijeshi ambayo ilikuwa na magari mawili ikatua katika uwanja wa ndege msituni pale na kisha magari yale kuanza kuelekea kule kulipokuwa na miili ile. Mawasiliano ya simu ambayo yalikuwa yakiendelea kufanyika yaliwawezesha kufika sehemu husika na kisha kuipakiza miili ile.

    “Na vipi kuhusu miili hiyo mitatu iliyobakia?” Sam aliuliza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hatujajua itakuwaje. Cha msingi twendeni tu tutajua cha kufanya”

    Hakukuwa na kingine cha kufanya, jitihada kubwa za kuitafuta miili ile zilikuwa zimefanyika lakini wala hawakuambulia chochote kile kiasi ambacho kiliwafanya kukata tamaa na kisha kupanga ni kitu gani ambacho kilitakiwa kufanyika mahali hapo. Wakaingia ndani ya magari yale na kisha kuelekea kule kulipokuwa na uwanja ule na kisha kuingia ndani ya ndege na safari ya kuelekea nchini Marekani kuanza.

    *****

    Magazeti pamoja na vyombo mbalimbali vya habari bado vilikuwa vikiendelea kutangaza kwamba Williams ndiye alikuwa mhusika mkubwa wa kutekwa kwa ndege ya wachezaji wa mpira wa kikapu ya New Bucketts na hatimae kuwaua wachezaji wenzake wote na yeye kukimbia huku akiwa ameshindwa kumuua bosi wa timu ya kikapu ya Boston Five hasa mara baada ya risasi kumuishia katika bunduki yake.

    Wamarekani pamoja na watu wote duniani walikuwa wamesikitishwa sana na taarifa ile, macho ya chuki ndio ambayo yalikuwa yakitumiwa kumwangalia Williams ambaye kwao tayari alionekana kuwa kama mnyama mkali ambaye wala hakuwa na huruma hata kidogo. Mapenzi ya watu juu ya Williams yakapotea kabisa mioyoni mwao, walimchukia Williams kupita kawaida.

    Vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa vikiendelea kutangaza juu ya kutafutwa kwa udi na uvumba kwa Williams ambaye mpaka katika kipindi hicho alikuwa akijulikana kuwa nchini Thailand. Williams akaonekana kuichoma mioyo ya watu kupita kawaida, aliigawia mamivu makali ambayo wala hayakuwa na dalili ya kupona mpaka pale ambapo angekamatwa na kuhukumiwa kifo kwa kunyongwa tena mbele ya macho ya watu.

    Kila mtu alikuwa akilaani vitendo vitendo vile vya mauaji ambavyo vilikuwa vimetokea msituni nchini Thailand. Unyama ambao ulikuwa umefanyika ndani ya msitu ule ulionekana kuwa mkubwa zaidi kutokea nchini Thailand, tena kufaywa na Mmarekani ambaye alikuwa akipendwa sana na Wamarekani kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao wa kucheza mpira wa kikapu.

    Wazazi wake, Bwana Kurt na Bi Latifa walionekana kuchanganyikiwa, hawakuamini kama kijana wao, Williams angekuwa na uwezo wa kufanya mauaji yale ambayo alitangazwa kuwa aliyafanya. Kila siku mioyo yao ilionekana kupinga, walimfahamu vilivyo Williams, walifahamu ni kwa jinsi gani kijana wao alikuwa mtu mpole na mtaratibu sana, hawakuwa na uhakika kama Williams alikuwa na roho mbaya ya kinyama ambayo ilimpeleka kufanya tukio kubwa kama lile.

    Kila siku walipokuwa wakihojiwa katika vyombo vya habari, wazazi hao walionekana kupinga kwa nguvu zote kwamba Williams hakuwa amehusika katika mauaji hayo japokuwa alama za vidole vyake zilikuwa zikionekana katika bunduki ambayo alikuwa ameishika huku akiwa anataka kumuua Bwana Robinson. Pamoja na hayo yote kuelezwa lakini bado wazazi hao walionekana kubisha, Williams alionekana kuwa mtu wa tofauti na namna ambavyo watu walivyokuwa wakimsema katika kipindi hicho.

    Kila siku Celine alikuwa mtu wa kujifungia chumbani na kulia tu, kila kitu ambacho kilikuwa kikisemwa juu ya mpenzi wake kilionekana kumuumiza kupita kawaida. Alimfahamu vilivyo mpenzi wake, alikuwa mtu mcheshi na mkimya ambaye wala hakutaka kufuatilia mambo ya watu kabisa. Katika kila wakati kipindi hicho, Celine alikuwa akijiuliza maswali mbalimbali juu ya mpenzi wake kubadilika ghafla na kuwa na roho ya kinyama namna ile lakini hakupata jibu lolote lile.

    Viongozi wa chama cha mpira wa kikapu nchini Marekani, NBA wakakutana na kisha kuweka kikao kizito cha siri. Kikao hicho kilifanyika kwa zaidi ya masaa mawili na maamuzi kutolewa kwamba Williams kufutwa kabisa kuwa kama mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani. Bado watu waliendelea kuumia, kufutwa kwake hakukuonekana kuwaridhisha, kitu ambacho walikuwa wakikitaka ni kumuona akikamatwa na kisha kufikishwa katika vyombo vya sheria ambapo huko angehukumiwa kifo.

    *****

    Ndege ambayo ilikuwa imebeba miili ya wachezaji ikaanza kuingia nchini Marekani, waandishi wengi wa habari walikuwa wamejikusanya katika uwanja wa ndege wa kijeshi kwa ajili ya kupiga picha kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali pale. Vilio vya wakinamama ambao walikuwa wakiangalia matangazo hayo moja kwa moja wakabaki wakilia tu, kile ambacho walikuwa wakikiona kilionekana kuwaumiza kupita kawaida.

    Williams akaonekana kuwawekea vidnda vikubwa mioyoni mwao, vidonda ambavyo havikuwa na dalili ya kupona kabisa. Watu wengine hasa ndugu, jamaa na marafiki wakabaki wakilia mpaka kuzimia, kila kilichokuwa kikionekana kilionekana kuwa kama ndoto ambapo baada ya muda fulani wangejikuta wakiamka na kujikuta wapo vitandani mwao.

    Kia kilichokuwa kikiendelea mahali pale kilikuwa ni kitu halisi, haikuwa ndoto kama watu walivyokuwa wakitaka iwe. Timu nzima ya New Bucketts ilikuwa imeteketezwa kwa risasi, si makocha wala benchi zima la ufundi, wote walikuwa wameuawa jambo ambalo lilioekana kuwahuzunisha zaidi Wamarekani na watu wengine duniani.

    Ibada za kuiaga miiili ikafanyika siku iliyofuata katika kabisa kubwa la St’ Joseph, kanisa ambalo lilikuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya watu elfu tano. Ibada ya kuaga miili ya marehemu wale ilikuwa ni ibada ya kihistoria ambayo iliwahi kutokea nchini Marekani, kila aliyehudhuria alikuwa katika hali ya majonzi isipokuwa mtu mmoja tu, Bwana Robinson.

    Moyo wa Bwana Robinson haukuumia hata kidogo, kila alipokuwa akiiangalia miili ile alionekana kufurahisa sana japokuwa uso wake ulikuwa ukionyesha huzuni la bandia. Moyo wake haukuwa umeridhika kabisa, katika kipindi hicho alijiona kuwa na uhitaji wa kufanya jambo moja tu, kumtafuta Williams na Phillip na kisha kuwaua.

    Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kanisani pale kilionekana kumpotezea muda wake, alihitaji kutoka katika kanisa lile na kisha kuwafuata vijana wake ambao angewaagiza kuelekea nchini Thailand na kumtafuta Williams pamoja na Phillip na kisha kuwaua tu. Bado moyo wake haukuwa na amani kabisa, japokuwa kila mtu duniani alijua fika kwamba ni Williams ndiye ambaye alikuwa amehusika na mauaji yale lakini alijiona kuwa na uhitaji wa kumuua na kisha kuifuata historia yake katika uso wa dunia.

    Ibada ile ilichukua muda wa saa moja na ndipo watu wakaondoka kanisani hapo. Alichokifanya Bwana Robinson ni kuwasiliana na vijana wake na kisha kutaka kumfuata nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa na kazi kubwa ambayo alitaka ifanyike tena kwa haraka sana hata kabla mambo hayajawa makubwa na kujulikana kwa kile ambacho kilikuwa kimefanyika nchini Thaila.

    Ndani ya nusu saa vijana hao wanne waliokuwa na miili mikubwa wakafika katika nyumba ya Bwana Robinson na kisha kuanza kuongea nae. Bwana Robinson hakutaka vijana wale wafahamu kwamba alikuwa akitaka kumuua Williams na Phillip kwa sababu walikuwa wakiujua ukweli wenyewe, ila alichokifanya ni kubadilisha maneno.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ninataka wauawe” Bwana Robinson aliwaambia.

    “Kwani wapo wangapi?” Kijana mmoja. Filbert aliuliza

    “Wapo wawili. Williams na Phillip” Bwana Robinson aliwaambia.

    “Hilo si tatizo. Unavyoona tuanzie wapi mkuu?” Gotz, kijana mwenye asili ya Ujerumani aliuliza.

    “Nchini Thailand. Natumaini watakuwa hawajatoka huko. Ila kuweni makini kwani hata F.B.I wapo huko” Bwana Robinson aliwaambia.

    “Usijali” Filbert alijibu.

    Huo ndio mpango ambao ulikuwa umepangwa na Bwana Robinson wa kutaka Williams na Phillip wauawa tu. Hakutaka kabisa watu hao wabaki hai, uwepo wao ndani ya dunia hii ungemfanya kuwa katika wakati mbaya sana. Hakutaka kuwaona watu hao wakiendelea kuvuta pumzi ya dunia hii, kwake walionekana kuwa watu hatari sana kiasi ambacho kama angewapa nafasi zaidi ya kuishi, basi wangeweza kumpa siku chache za kuishi na kuyafurahia maisha yake ya kitajiri ambayo alikuwa akiishi.







    Mara baada ya kufukuzwa na Bwana Robinson kwa kuambiwa kwamba hakuwa akihitajika, Gong akaondoka mahali hapo na kuelekea Bangkwan, sehemu ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya watu katika sehemu yote ya Bangkok. Huko, Gong akaanza kuwatafuta marafiki zake ambao kila siku katika kipindi cha nyuma alikuwa akisaidiana nao kufanya biashara mbalimbali katika mitaa ya Bangkok.

    Kwa sababu alikuwa akizijua sana maskani zao, Gong wala hakupata tabu sana, ni ndani ya dakika kumi akaweza kuwapata marafiki zake watatu ambao akawaweka chini. Lengo lake kubwa la kuwatafuta marafiki zake lilikuwa ni kwenda msituni ambapo aliamini kwamba Williams na Phillip walikuwa wakipelekwa katika kipindi hicho, alionekana kuhitaji msaada wa watu hao huku akiahidi kuwalipa kiasi fulani cha fedha.

    Vijana wale hawakuwa na pingamizi lolote lile, wakakubaliana nao na hivyo kujiandaa kwenda huko msituni kwa ajili ya kufanya uvamizi huku wakiwa na mapanga tu, lengo lilikuwa ni kuwaokoa Williams na Phillip ambao walikuwa wamekamatwa. Huku wakiendelea kupanga kila kitu ikiwa namna ya kuanza kufanya uvamizi katika msitu huo, mara milio ya risasi ikaanza kusikika kutoka mjini, sehemu ambayo haikuwa mbali kabisa kutoka hapo walipokuwa.

    Milio ile ikaonekana kumshtua Gong kwa kuona kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilitokea. Kichwa chake kikakataa katakata kuona kwamba hao walikuwa mapolisi, moja kwa moja akajua kwamba hao walikuwa vijana wa Bwana Robinson ambao walikuwa wamewakamata Williams na Phillip. Gong hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, kwa kasi ya ajabu tena ya kushtukiza, akachomoka mahali hapo huku akiwaacha wenzake wakiwa na mshangao.

    Gong akaanza kukimbia kuelekea mjini, njiani alionekana kuwa tofauti na watu wengine, wakati watu wengine wakikimbia kutoka mjini yeye alikuwa akikimbilia kule kule kulipokuwa kukisikika milio ya risasi. Hakuchukua dakika nyingi, akafika mjini na moja kwa moja kuelekea kule ambapo alikuwa ameambiwa ageuze, hakukuwa na mtu yeyote, sehemu yote ilionekana kutokuwa na watu kutokana na watu kukimbia.

    Gari lile ambalo walikuwa wakilitumia Bwana Robinson na vijana wake liliendelea kuwa mahali pale pale, Robinson hakutaka kulisogelea, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo huku akijua dhahiri kwamba watu ambao walikuwa wamewakamata Williams na Phillip wakiwa katika eneo jingine tofauti na eneo lile.

    Kwa mwendo wa haraka haraka akaanza kuelekea katika upande wa Magharibi ambapo milio ya risasi ilikuwa ikiendelea kusikika, alipofika huko, hakuwakuta Williams na Phillip zaidi ya mapolisi ambao walikuwa wamewaua vijana watekaji watatu huku wengine wakiwa wamekimbia. Gong hakuishia hapo, tayari alijua kwamba mapolisi wale walikuwa wameharibu kila kitu na hivyo kuwa na uwezekano kwamba Williams na Phillip kuwa hai sehemu fulani.

    Gong aliendelea kuwatafuta katika kila kona na ndipo masikio yake yakaanza kusikia tena milio ya risasi. Alichokifanya Gong kwa wakati huo ni kuanza kuifuatilia milio ile ya risasi. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo milio ile ilivyozidi kusikika zaidi na zaidi mpaka pale ambapo alifika sehemu ambayo ilikuwa na makutano ya barabara mbili, moja iliyokuwa ikitoka mjini na nyingine iliyokuwa ikitoka Runghut, sehemu iliyokuwa ikisifika na kuwa na watu wataratibu kuliko sehemu zote Bangkok.

    Gong akaanza kuifuata ile barabara iliyokuwa ikielekea Rughut, sehemu ambayo milio ya risasi ilipokuwa ikizidi kusikika zaidi na zaidi. Katika kipindi chote hicho, Gong alikuwa akizidi kukimbia, akili yake ilikuwa ikizidi kumwambia kwamba watu ambao alikuwa akiwatafuta katika kipindi hicho walikuwa kule ambapo milio ile ya risasi ilipokuwa ikisikika zaidi na zaidi.

    Kila mtu ambaye alikuwa akisikia milio ile ya risasi alikuwa akikimbia kuelekea popote ambapo alikuwa akipaona kuwa na usalama katika maisha yake. Gong hakukata tamaa, jasho lilikuwa likimtoka kupita kawaida lakini hakutaka kusimama, kitu ambacho alikuwa akitaka kukiona ni kuwaona Williams na Phillip wakiwa wazima kabisa.

    Baada ya sekunde kadhaa, akafika katika eneo ambalo kulikuwa na njia tatu, Gong akaonekana kuchanganyikiwa zaidi, hakujua ni njia gani ambayo alitakiwa kwenda katika kipindi hicho, alichoamua ni kwenda katika njia ya Kaskazini ambayo alikuwa akiijua sana. Hata kabla hajapiga hatua tano, mara milio ya risasi ikaanza kusikika katika njia ya upande wa Kusini, hapo hapo akageuka na kisha kuanza kuifuata njia ile.

    Aliendelea kukimbia mpaka pale alipofika na kumuona Bwana Robinson akiwa amepiga magoti chini huku Williams akiwa amemnyooshea bunduki na kuitupa chini kisha kukimbia. Gong hakuonekana kuelewa kitu chochote kile kilichokuwa kikiendelea mahali pale, hakuelewa kama Williams na Phillip ndio ambao walikuwa wakipiga risasi zile au la, hakujua sababu ambayo ilimfanya Williams kumuacha hai Bwana Robinson katika kipindi ambacho alikuwa ameshika bunduki.

    Alichokifanya Gong ni kuanza kukimbia kuelekea kule ambapo Williams na Phillip walipokuwa wamekimbilia kwani kwa mbali nyuma milio ya risasi tayari ilikwishaanza kusikika. Gong aliendelea kuwakimbilia huku akijitahidi kuita mpaka pale ambapo Williams na Phillip walipogeuka nyuma na kukutanisha macho.

    Gong akawapa ishara kwamba walitakiwa kumfuata, hakukuwa na mtu aliyebisha mahali hapo, wakaanza kumfuata Gong ambaye alianza kuelekea katika njia ambayo ilikuwa ikitokea Khathog, mtaa ambao ulikuwa ukikaliwa na masikini wakubwa, masikini ambao walikuwa wakipata mlo mmoja kwa siku, masikini ambao walikuwa wakishinda Bangkok mjini na kuuza biashara ndogo ndogo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gong akaanza kwendda nao huku Williams akiendelea kuchechemea kutokana na mguu wake kuendelea kuuma huku ukiwa umeanza kutoa kidonda kikubwa. Watu ambao walikuwa njiani walikuwa wakiwashangaa kupita kawaida, hawakuonekana kuelewa kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika kipindi hicho. Kutokana na watu wengi wa Thailand kutokufuatilia sana mpira wa kikapu nchini Marekani, hakukuwa na mtu ambaye aliwaangalia na kugundua kwamba wale walikuwa Williams na Phillip.

    Safari yao ikaishia katika nyumba moja kuu kuu ambao ilikuwa imeezekwa kwa mabati yaliyokuwa na kutu kubwa na kisha Gong kuanza kugonga mlango ule. Mwanamke mmoja mzee akafika mahali pale na kisha kuufungua mlango ule. Macho yake yalipotua kwa Gong, akaonyesha tabasamu pana ila alipoyapeleka macho nyusoni mwa Williams na Phillip, tabasamu lile likapotea na hali ya mshangao kumjia.

    Mwanamke yule akaanza kuuliza maswali mfululizo huku Gong akyajibu maswali yote tena kwa ufasaha mkubwa na ndipo mwanamke yule alipoamua kuwakaribisha ndani. Wote wakaingia ndani na kisha kutulia sebuleni, sebule ambayo ilionekana kuwa ovyo ovyo huku ikiwa imekusanya vitu vingi katika sehemu moja, kama jiko hapo hapo, sehemu ya kulia chakula hapo hapo na vitu vingine.

    Gong akaanza kumuelezea mwanamke yule kuwa wale walikuwa marafiki zake ambao walikuwa wamepata ajali ya kudondoka na pikipiki katika kipindi ambacho walikuwa wakielekea mjini maneno ambayo yaliweza kuamini katika moyo wa mwanamke yule ambaye alikuwa shangazi yake.

    Chakula kikaandaliwa, ingawa chakula kilikuwa tofauti na kile ambacho walikuwa wamezoea kukila lakini kutokana na njaa kubwa ambayo walikuwa nayo, walikila hivyo hivyo japokuwa hakikuwa na ladha yoyote midomoni mwao. Baada ya kumaliza kula chakula kle, mwanamke yule akaelekea nje ambapo akachuma majani fulani ambayo yalikuwa katika mti mdogo ambao ulikuwa nyuma ya nyuma ile na kuja ndani na kuanza kuyachemsha na baade kuyakamua na maji yake kuyapaka katika kidonda kile alichokuwa nacho Phllip.

    Siku hiyo walipanga kulala hapo hapo hata kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Marekani. Williams na Phillip katika kipindi hicho walikuwa wakihitaji simu ili waweze kuwasiliana na ndugu zao ambao walikuwa nchini Marekani na kisha kuwaambia kile ambacho kilikuwa kimeendelea nchini Thailand, toka ndege ile ilipotekwa.

    Ingawa kupatikana kwa simu lilionekana kuwa jambo kubwa sana lakini ndani ya dakika arobaini na tano tu, Gong akafanikiwa kupata simu na kisha kumpelekea Williams ambaye akaanza kupiga nyumbani kwao nchini Marekani. Simu ikaanza kuita, iliita kwa zaidi ya sekunde kumi, ikapokelewa na sauti ya Bwana Kurt kusikika.

    “Mungu wangu! Kumbe upo hai? Upo wapi?” Bwana Kurt alimuuliza.

    “Tupo Thailand. Ndege yetu ilitekwa na kisha kupelekwa porini. Kila mchezaji ameuawa porini, ni mimi na Phillip ndio tupo hai” Williams alisema.

    “Kuna nini kinaendelea huko?”

    “Tuliweza kuwatoroka watekaji. Walikuwa wakitaka kutuua. Siku yoyote kuanzia sasa tutakuwa nchini Marekani” Williams alijibu.

    “Asante Yesu! Nani alikuwa amehusika kwa kutekwa kwenu, au bado hamjajua?” Bwana Kurt aliuliza.

    “Tumeshamjua”

    “Nani?”

    “Bwana R........” Simu ikaisha chaji na kujizima.

    “Hallooow....hallloow....” Williams aliita.

    Akaanza kuiangalia simu ile, simu ilikuwa imezima jambo ambalo likaonekana kumkasirisha kupita kawaida. Akaanza kuyapepesa macho yake huku na kule kutafuta kama kulikuwa na soketi ya umeme ndani ya nyumba ile, hakukuwa na soketi yoyote ile kutokana na nyumba yenyewe kutokuwa na umeme jambo ambalo likaonekana kumchanganya.

    Gong akaichukua simu ile na kisha kumpelekea mtu ambaye alikuwa amemuazima. Mwenye simu hakutaka tena kuitoa simu yake kutokana na muda huo kutaka kuondoka. Gong akajitahidi kutafuta simu sehemu nyingine lakini hakufanikiwa kupata simu jambo ambalo likamfanya kurudi nyumbani.

    Siku hiyo walishinda ndani huku kila mmoja akiwa na mawazo tele. Walilala pale pale sebuleni mpaka asubuhi ambapo mipango ya chai ikaanza kufanyika. Gong akachukua kiasi cha fedha cha kununulia vitafunwa na kisha kwenda dukani kununua vitafunwa hivyo. Akiwa dukani, macho yake yakatua katika televisheni ambayo ilikuwa ikionyesha moja kwa moja kutoka katika kituo cha televisheni ya Taifa ya Thailand kwamba Williams alikuwa akitafutwa kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili za kufanya mauaji ya wachezaji wa mpira wa kikapu.

    Gong akaonekana kushtuka, alichokifanya ni kutulia huku akijaribu kuifuatilia habari ile. Picha ya Bwana Robinson ikaonekana huku ikielezwa kwamba Williams alikuwa ameshindwa kumuua Bwana Robinson kwa kuwa tu risasi zilikuwa zimemuishia katika bunduki yake. Taarifa ile ilionekana kumchanganya Gong, alijua fika kwamba taarifa ile ilikuwa ni ya uongo kabisa ila suala la kutaka kumuua Bwana Robinson aliliona kuwa sahihi kutokana na kile kipindi alipomuona Williams na Phillip, Bwana Robinson alikuwa amepiga magoti chini.

    Gong hakutaka kuendelea kubaki mahali pale, alichokifanya ni kuondoka na kuelekea nyumbani kwao. Uso wake ukaonekana kuwa tofauti sana, tayari alionekana kuwa na kitu moyoni. Kila walipojaribu kumuuliza, Gong hakuwa akiwaelewa. Kwa bahati nzuri, Shangazi yake, Bi Thum alikuwa akielewa lugha ile kutokana na kipindi cha nyuma kufanya kazi za ndani katika nyumba ya mzungu mmoja nchini hapo kabla ya kurudi kwao nchini Uingereza.

    Gong akaanza kumwambia Bi Thum kile ambacho alikuwa amekiona katika televisheni na kisha Bi Thum kuwaambia Williams na Phillip. Kila mmoja akaonekana kushtuka, hapo ndipo Williams alipopata majibu juu ya sababu ambayo ilimfanya Bwana Robinson kumgawia bunduki ili amfyatulie.

    “Kwa nini ulinidanganya?” Bi Thum alimuuliza Gong.

    “Niliogopa”

    “Uliogopa nini?”

    “Kwamba usingewaruhusu kuingia”

    Gong aliendelea kujitetea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo alikuja kueleweka. Baada ya hapo, zikapita dakika hamsini, mara mlango ukaanza kugongwa. Kila mmoja akaonekana kuwa na wasiwasi, hakukuwa namtu ambaye alionekana kuwa amani isipokuwa Bi Thum ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule. Bi Thum akainuka na kisha kuufuata mlango ule, kila mmoja akatega macho yake kuona mgongaji alikuwa nani, hata kabla ya kufungua mlango, Bi Thum akachungulia, alikuwa jirani yake, akaufungua mlango.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea na jirani yake huyo kwa dakika kadhaa na kisha kurudi ndani, wala hakukaa sana, mara mlango ukasikika ukigongwa tena. Bi Thum akaonekana kukereka, umri wake ulikuwa mkubwa, mwili wake haukuwa ukihitaji usumbufu kwa wakati huo. Huku akiwa amekasirika na kuonekana kuchoka, Bi Thum akasimama na kisha kuufuata mlango. Kama kawaida yake, kabla ya kuufungua akaanza kuchungulia. Kwa wakati huu, mgongaji alikuwa mtu wa tofauti. Walikuwa wazungu watatu ambao walikuwa wamevaa suti nyeusi, F.B.I.





    Kila mtu kutoka katika kitengo cha upelelezi cha FBI alikuwa bize kwa wakati huu huku wakitaka kukamilisha kazi ya kumkamata Williams na kisha kumfikisha katika vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo. Walijua fika kwamba kwa wakati huo Williams alikuwa nchini Thailand, moja ya nchi kubwa barani Asia ambayo ilikuwa na watu wengi.

    Walichokifanya kwa wakati huo ni kutegesha mitambo yao yote. Kitu cha kwanza ni kuchukua namba za wazazi wake kwa kujua kwa ilikuwa ni lazima Williams angeweza kuwasiliana na wazazi wake na kisha kuwaambia kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea katika maisha yake huko alipokuwa kwa wakati huo. Wataalamu wa mambo ya kompyuta wakawekwa tayari katika chumba kimoja kikubwa ambacho kilikuwa kimejaza kompyuta nyingi huku hata kioo cha kompyta moja ikiwa ukutani.

    Kila mmoja alikuwa makini kwa wakati huo, kitu ambacho walikuwa wakikisikilizia kwa wakati huo ni simu kutoka kwa Williams ambayo ingeingia ndani ya moja kati ya simu za wazazi wake. Siku ya kwanza walikaa wakisikilizia lakini wala hakukuwa na simu yoyote ambayo iliingia kutoka kwa Williams jambo ambalo lilionekana kuwa si rahisi kutokea.

    Waliendelea kusubiri zaidi na zaidi na hatimae ilipofika saa tatu asubuhi, simu kutoka nchini Thailand ikaanza kuingia ndani ya simu ya Bwana Kurt. Kwa haraka haraka wakaanza kuifuatilia simu ile. Kila kitu ambacho kilikuwa kikifanyika mahali hapo kilikuwa kikifanyika kwa haraka haraka sana. Wakaanza kuangalia kwa kutumia ile kompyuta kubwa iliyokuwa ukutani.

    Ramani ya dunia ikajitokeza, kompyuta yenyewe ikaanza kutafuta huku mshale mwekundu ukionekana katika kompyuta ile. Dunia ikaanza kujizungusha huku msahle ule ukianza kutafuta sehemu ya kutua. Dunia ilipojizungusha na kufikia katika usawa wa nchi ya Thailand, ukaanza kushuka chini. Mshale ulikuwa ukishuka chini kwa kasi kubwa, ukaanza kwenda mpaka katika jiji la Bangkok na kuanza kuzunguka huku na kule huku ukiendelea kutafuta mahali ambapo simu ile ilipokuwa imetoka.

    Mshale ule ukasimama katika mtaa wa Khathog, kila mmoja ndani ya chumba kile alikuwa makini akiauangalia mshale ule ambao ulikuwa ukiendelea kuchunguza zaidi na zaidi. Baada ya hapo, mshale ule ukaanza kutafuta nyumba ambayo simu ile ilikuwa ikipigwa. Mshale ukafika katika sehemu ambayo ilikuwa na nyumba tano na ghafla mawasiliano kukatika, ulikuwa ni muda ambao simu ile ilikuwa imeishiwa chaji.

    “Dammn....!” Mkubwa wa kituo cha upelelezi cha FBI alisema huku akionekana kukasirika.

    Kupotea kwa mawasiliano yale kulionekana kuwakasirisha kupita kawaida, kila kitu ambacho walikuwa wakikifuatilia kilikuwa kimepotea kwa wakati huo. Hawakujua ni kitu gai cha kufanya, walibaki kimya huku kila mmoja akionekana kuchanganyikiwa. Huku kila mmoja akiwa kimya, wazo likatolewa kwamba iliwabidi kufanya kitu kimoja, wawatume wapelelezi ambao walikuwa wamekwishafika Thailand na kisha waanze kuelekea huko katika mtaa wa Khathog.

    Hakukuwa na cha kusubiri kwa wakati huo, kwa haraka haraka mawasiliano yakafanyika na hivyo wapelelezi hao kutakiwa kuelekea katika mtaa huo kwa ajili ya kuangalia mahali ambapo wangeweza kumkuta Williams. Wapelelezi watatu huku wakiwa na bunduki zilizokua viunoni mwao wakaanza kuelekea katika mtaa huo kwa kutumia gari lao ambalo lilikuwa na vioo ambavyo havikumuwezesha mtu wa nje kuona ndani.

    Ndani ya gari lile, walikuwa na kompyuta ambayo walikuwa wametumia picha yote ambayo ilirekodiwa kutoka kwenye mtambo ambao ulikuwa ukionyesha jinsi mshale ule ulivyokuwa ukitafuta sehemu ambayo simu ile ya Williams ilipokuwa imetoka. Kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea katika kompyuta ile nchini Marekani katika jengo la makao makuu kilikuwa ndani ya kompyuta ndogo waliyokuwa nayo pamoja na simu zao zilizoonekana kuwa na uwezo mkubwa.

    Mara baada ya kufika ndani ya mtaa ule, wote wakateremka na kisha kuanza kuzitafuta nyumba zile kwa kutumia simu zao. Kazi wala haikuwa kubwa, simu zile zilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutafuta kile ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo. Wakafika katika eneo ambalo lilikuwa na zile nyumba tano na kisha kuanza kwenda katika nyumba ya kwanza.

    Wakaanza kupiga hodi, wakazi wa mtaa ule walikuwa wakiwashangaa tu, kwao, wazungu kutoka nchini Marekani walionekana kuwa watu wa ajabu sana kwao, ugeni ule ukaanza kuwajaza maswali mfuluizo ndani ya vichwa vyao. Mara baada ya kugonga hodi katika nyumba hiyo, mlango ukafunguliwa na mzee mmoja.

    Mpelelezi mmoja ambaye alikuwa akifahamu sana lugha ya Thailand akaanza kuongea na mzee huyo na kumuomba nafasi ya kuingia ndani. Wakaingia ndani, wala hawakufanya upekuzi wowote ule, walichokufanya ni kutoa simu moja na kisha kuifungua na alama za vidole vya Williams kutokea katika kioo cha simu ile na kisha kuanza kumulika mulika ndani ya nyumba ile, simu haikutoa mlio wowote ule jambo lililowafanya kuondoka na kuelekea katika nyumba ya pili.

    Kazi yao ilikuwa ni ile ile, kumulika mulika hapa na pale na kama kulikuwa na kitu chochote ambacho kilishikwa kwa mkono wa Williams basi simu ile ingeweza kutoa mlio mmoja ambao wala haukuwa wa kawaida. Wakaingia katika nyumba ya pili, hawakufanikiwa, wakaingia katika nyumba ya tatu, hawakufanikiwa, wakaingia katika nyumba ya tano napo hali ilikuwa ile ile.

    Hapo ndipo ambapo wakaamua kwenda kwenye nyumba ya tano na ya mwisho ambayo ilikuwa ni nyumba aliyokuwa akiishi Bi Thum. Walipoufikia mlango, wakaanza kugonga. Tofauti na nyumba nyingine, mlango wa nyumba ule ulichelewa kufunguliwa jambo ambalo lilionekana kuwatia wasiwasi, walichokifanya ni kuanza kutoa bunduki zao.

    Mara Bi Thum akaufungua mlango ule, uso wake ulionekana kama mtu ambaye alikuwa ametoka kulala, mtu ambaye alikuwa na uchovu mwingi wa asubuhi. Mara baada ya kuufungua mlango ule, wapelelezi wakaomba kuingia ndani, hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuwazuia, akawakaribisha kuingia ndani ya nyumba yake.

    Mara baada ya kuingia ndani, wakatulia vitini. Bi Thum akajifanya kutokuwa na wasiwasi wowote ule, alikuwa akijipa uhuru kama hakukuwa na kitu chochote kibaya ambacho kilitokea au kutokuwa na mtu ambaye alikuwa akitafutwa na watu wale ambao walikuwa wameingia ndani ya nyumba yake kwa wakati huo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mpelelezi mmoja, Adrian akatoa simu yake na kisha kuanza kufanya kama kile ambacho alikuwa akikifanya katika nyumba zile nne zilizopita. Ile kumulika mulika ndani ya sebule ile, simu ikaanza kutoa mlio huku alama zikionekana katika kila kitu ambacho Williams alikuwa ameshika. Alama za mikono yake zilikuwa zikionekana katika kikombe, mlangoni, kwenye kiti pamoja na sehemu nyingine.

    “Where is this guy? (Mtu huyu yupo wapi?)” Adrian alimuuliza Bi Thum.

    “Who?(Nani?)” Bi Thum aliuliza huku akijifanya kushtuka.

    “Williams)

    “What are talking about? (Mnaongea kuhusu nini?)” Bi Thum aliuliza swali ambalo liliwafanya wapelelezi wale kupandwa na hasira kwani tayari waliona kwamba walikuwa wakifanyiwa masihala.

    Alichokifanya Adrian ni kutoa picha ya Williams na kisha kumuonyeshea Bi Thum. Kitu alichokifanya Bi Thum ni kuonyesha mshangao kana kwamba alikwishawahi kumuona mtu huyo mahali fulani japokuwa hakuwa akikumbuka. Adrian alipoona kwamba Bi Thum haridhiki, akampa kabisa ile picha na kuanza kuiangalia vizuri.

    “Where is he? (Yupo wapi?)” Adrian aliuliza.

    “He left (Aliondoka)” Bi Thum alijibu huku kwa mbali akionekana kuanza kutetemeka, kitendo cha kuiona bastora iliyokuwa kiunoni mwa Adrian kilimuogopesha.

    “Was he alone? (Alikuwa peke yake?)”

    “No)

    “With who was he? (Alikuwa na nani)”

    “His friend (Rafiki yake)” Bi Thum alijibu.

    Bila kuchelewesha muda wowote ule, Adrian akatoa picha ya Bruce na Phillip na kisha kumuonyesha. Bi Thum akazichukua picha zile na kisha kuanza kuziangalia. Wala hakuangalia zaidi ya sekunde tano, akawaonyeshea mtu ambaye alikuwa akiongozana nae, alikuwa Phillip. Wapelelezi wakaonekana kuridhika, walichokifanya ni kumuomba Bi Thum awaonyeshe mahali ambapo alipoelekea pamoja na huyo rafiki yake, akawaonyeshea na kisha kuondoka mahali hapo huku wakiwa na uhakika kwamba ni LAZIMA Williams akamatwe na kisha kupelekwa katika vyombo vya sheria.





    Kila kitu kilikuwa kimewekwa tayari na kwa kipindi hicho ni safari ya kuelekea nchini Thailand ndio ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hali na mali. Bwana Robinson akawa amekwishawagawia kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya matumizi yao ambayo wangeweza kuyafanya katika kipindi ambacho wangekuwa nchini humo.

    Filbert, Gotz, Silva na Kelvin wakaanza safari ya kuelekea nchini Thailand huku kila mmoja kichwani mwake akiwa na lengo moja tu, kumuua Williams na Phillip ambao walikuwa nchini Thailand. Hawakuwa na bunduki zozote zile, kitu walichokuwa nacho katika kipindi hicho ni fedha tu za kununulia bunduki katika kipindi ambacho wangefika nchini humo.

    Kila mmoja alitakiwa kuwa makini katika kipindi hicho, hwakutakiwa kuleta mchezo wowote ule, walitakiwa kufanya kila kitu katika muda muafaka huku wakihakikisha kwamba wanakamilisha kila kitu na ndipo waanze kurudi nchini Marekani. Mara baada ya kufika nchini Thailand, wakachukua vyumba katika hoteli ya kifahari na kisha kuanza kupanga mipango yao kabambe ya kukamilisha kila kitu walichokuwa wamekifuata nchini hapo.

    Filbert ambaye ndiye alikuwa kiongozi wao akafungua kompyuta yake ya mapajani na kisha kuanza kufungua Google Map. Katika kipindi hicho alikuwa akitaka kufahamu kitu kimoja tu, sehemu ambayo awalielekezwa na Bwana Robinson kwamba kulikuwa na uwezekano wa William na Phillip kuwepo. Kutokana na bwana Robinson kuwalekeza kwa umakini sana sehemu ambayo alikuwa ameachana na Williams na Phillip, wakaanzia na huko kwani walikuwa na uhakika kwamba watu hao ambao walikuwa wakiwatafuta kuwepo mahali hapo.

    Waliiangalia ramani ile kwa kipindi kirefu sana na ndipo ambapo wakaamua kutoka ndani ya chumba kimoja walichokuwa wamekutania na kisha kutoka nje. Ingawa kulikuwa na usafiri wa bajaji, wakaamua kuchukua taksi ya hotelini hapo na kisha kutaka kuwapeleka katika mtaa mwingine wa kimasikini wa Tuktug ambao ulikuwa ukipakana na mtaa mwingine wa kimasikini wa Khathog.

    Pale Tuktug ndipo ambapo walipoanza kutafuta msaada wa mtu yeyote ambaye alikuwa akifahamu lugha ya Kingereza na kisha kuanza kuongea nae. Kitu cha kwanza walichokifanya ni kumuonyeshea picha ya Phillip huku wakimuuliza maswali mbalimbali ambayo mtu yule aliyajibu kwa ufasaha mkubwa sana.

    Kijana yule ambaye alikuwa akiwasikiliza alionekana kumuona mtu ambaye alikuwa ameonyeshewa katika picha ile, alikuwa amemuona tena akiwa na mwezake, William pamoja na kijana mwingine wa Kithailand, Gong. Ujanja ambao aliufanya Filbert mahali hapo ni kumuonyeshea picha ya Phillip ambayo aliamini kwamba haikuwa imeonekana katika vyombo mbalimbali vya habari kwa wakati huo.

    Kitu alichokifanya kijana yule ni kuwaita wenzake ambao akaanza kuongea nae na kisha kuwauliza zaidi kuhusiana na watu wale ambao aliwaona siku iliyopita na vijana wale kuwaelekeza kwamba walikuwa wameelekea katika mtaa wa Khathog. Filbert alichokitaka ni kuelekezwa katika mtaa huo, wakaanza kuelekea huko.

    Kutokana na mitaa hiyo miwili kupakana, wala hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika katika mtaa huo na kisha kuanza kuwauliza vijana wengine kuhusiana na Phillip na Williams. Kwa sababu vijana wale walikuwa wamewaona mpaka katika nyumba ambayo walikuwa wameingia, wakawaonyeshea nyumba ya Bi Thum.

    Filbert na wenzake hawakuwa na silaha yoyote katika kipindi hicho na ilikuwa ngumu sana kuvamia, walichokifanya wao ni kuondoka huku kila mmoja akiwa na uhakika kwamba watu ambao walikuwa wakiwatafuta walikuwa ndani ya nyumba ile. Kitu cha kwanza wakaanza kuelekea mjini huku lengo lao kubwa likiwa ni kupata bunduki za kuweza kuwaua Williams na Phillip.

    Kazi ya kupata silaha haikuwa rahisi hata kidogo, kwa sababu walikuwa wageni walipata tabu sana kuuliza kitu ambacho kiliwafanya kuanza kutafuta makundi mbalimbali ya kihuni hapo Bangkok. Kutokana na msaada ambao walikuwa wamepewa na vijana wa mjini, wakafanikiwa kulipata kundi moja ambalo lilikuwa likijiita KINGS OF THAILAND na kisha kununua silaha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kiasi cha fedha ambacho walikuwa wamekitoa kilikuwa kikubwa sana, wakauziwa bunduki nne na kisha kuondoka mahali hapo huku ikiwa imetimia saa sita usiku. Walipofika hotelini, wakapanga mikakati ya mwisho mwisho kabla ya kwenda katika nyumba ile ambapo hapo wangeanza kazi ya kuwaua. Kwao, tayari kazi ilionekana kuwa rahisi sana tofauti na jinsi ambavyo walivyokuwa wakifikiria kabla.

    Ilipofika asubuhi, wakajiandaa na saa nne kamili asubuhi kuanza safari ya kuelekea katika mtaa ule ambapo baada ya kufika wakaanza kuelekea katika nyumba ambayo walikuwa wameelekezwa. Mara baada ya kuufikia mlango, Filbert akaanza kuugonga na baada ya sekunde kadhaa Bi Thum kuufungua mlango.

    “You came back (Mmerudi tena)” Bi Thum alisema huku akionekana kukasirika.

    Alichokifanya Filbert ni kutoa bunduki yake na kisha kumwamuru Bi Thum kurudi ndani. Mara baada ya kuiona bunduki ile, Bi Thum akaanza kutetemeka, akaonekana kuogopa kupita kawaida. Akaanza kurudi ndani huku mikono akiwa ameiweka kichwani kama kusalimu amri, akaamrishwa kukaa kitini na kisha Filbert na wenzake kuanza kuangalia huku na kule.

    “Where are they? (Wapo wapi?)” Filbert aliuliza huku akionekana kukasirika.

    Woga ulionekana kimshika Bi Thum kiasi ambacho midomo yake ilikuwa ikicheza cheza tu. Tayari mbele yake alikiona kifo, alijiona kumfuata mume wake katika kipindi chochote kuania hapo. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku haja ndogo ikianza kumbana. Alishindwa kujua kama watu wale ambao walikuwa wamekuja ndani kwake walikuwa ni wale ambao aliagana nao katika kipindi kilichopita au wengine, na kama walikuwa ni wale wale, kwa nini walikuja na bunduki? Kila alichokuwa akijiuliza mahali hapo, alikosa jibu.

    “Where are they? (Wapo wapi)” Filbert alilirudia swali lake kwa sauti kubwa zaidi ambayo ilimuogopesha zaidi Bi Thum.

    “They left as I told you (Wameondoka kama nilivyowaambia)” Bi Thum alijibu.

    “What? Did we meet before? (Nini? Tulionana kabla?): Filbert aliuliza huku kila mmoja akionekana kushangaa.

    “Yes”

    “No. Who came and ask for them? (Hapana. Nani alikuja kuwaulizia?)” Filbert aliuliza.

    “You (Ninyi)

    “F.B.I” Silva alisema.

    Kila mmoja akapata uhakika kwamba watu kutoka katika kitengo cha upelelezi nchini Marekani cha FBI ndio ambao walikuwa wamefika mahali hapo, wote wakaonekana kuwa na wasiwasi kwamba hawakuwa peke yao, tayari F.B.I walikuwa wamefanya kama ambavyo walitakiwa kufanya katika suala hilo. Walichokiona katika kipindi hicho ilikuwa ni lazima kuwatafuta Williams na Phillip na kisha kuwaua.

    Walijua fika kwamba kama wasingefanikiwa kuwakamata na kuwaua basi FBI wangeweza kuwakamata na kisha kumfikisha Williams katika mikono ya sheria jambo ambalo wala hawakutaka litokee kabisa katika kipindi hicho. Walichokifanya kwa wakati huo ni kumlazimisha Bi Thum awaonyeshe mahali ambapo vijana wale walipoelekea.

    Bi Thum akasimama na kisha kuelekea pembeni kidogo mwa chumba kile, kulikuwa na mlango wa kutokea katika upande wa pili na kisha kuufungua. Kila mmoja akafahamu kwamba Williams na Phillip walikuwa wamekimbia kupitia mlango ule, walichokifanya, ni kutoka kupitia mlango ule na kusonga mbele. Mwendo wao ulikuwa ni wa haraka haraka sana, walijiona kuwa nyuma ya muda kupita kawaida.

    Kila kitu ambacho walikuwa wakiendelea kukifanya walikuwa wakikifanya kwa haraka sana, walikuwa na hamu ya kukutana na watu hao na kisha kuwamaliza ili kuifanya midomo yao iwe kimya milele. Walikuwa wakitembea kwa haraka haraka mpaka kufika sehemu ambayo ilikuwa na soko kubwa na kisha kuanza kuingia ndani ya soko lile.

    Watu ambao walikuwa ndani ya soko lile wakabaki wakiwaangalia tu, walionekana kuwashangaa lakini nyuso zao zilionekana kuwa katika mtazamo fulani ambao kwa mtu ambaye alikuwa akiwaangali vizuri, alifahamu uangaliaji ule ulikuwa unamaanisha nini.

    “Mmegundua nini?” Filbert aliwauliza wenzake.

    “Kuhusu nini?” Kelvin aliuliza.

    “Mitazamo yao”

    “Sijakuelewa”

    “Kwa jinsi wanavyotuangalia”

    “Mmmh! Sijui” Kelvin alijibu.

    “Hamuoni kama mitazamo yao inaonyesha dhahiri kwamba kuna watu kama sisi walipita hapa?” Filbert aliuliza.

    “Mmmh! Hapo ndio nimegundua hilo. Sawa sawa. Kuna kitu kama hicho” Kelvin alisema.

    Walikuwa wakipishana na watu mbalimbali ndani ya soko lile. Walikuwa wakiendelea mbele mpaka kulivuka soko lile na kukutana na wazungu wengine watatu ambao kwa kuwaangalia japokuwa walikuwa mbali, waligundua kwamba watu wale walikuwa ndio FBI ambao walikuwa wamekuja kwa ajili ya kumtafuta Williams.

    Wote wakaanza kuangaliana kwa macho ya kushtukiana, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akimuongelesha mwenzake, wote walikuwa wakibaki kuangaliana tu huku wakiendelea na safari yao. Ingawa walionekana kuwa karibu karibu kana kwamba walikuwa safari moja, lakini katika kipindi hicho kila mmoja alionekana kuwa bize na lake.

    Walipita katika njia moja, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alimuongelesha mwenzake jambo lolote lile. Wakafika katika sehemu ambao ilikuwa imekusanyika watu wengi waliokuwa wamesimama nje ya nyumba fulani huku minong’ono ikisikika mahali pale. Alichokifanya mpelelezi Adrian ni kuwasogelea watu wale na kisha kuanza kuongea na mtu mmoja kwa kutumia lugha ya Kithailand.

    “Kuna mtu ameingia humu halafu ni mhalifu” Kijana yule alisema Kithailand.

    “Mtu gani?” Adrian aliuliza.

    “Huyu hapa” Kijana yule alijibu huku akitoa karatasi ambayo ilikuwa na picha ya Williams. Adrian akaonekana kushtuka, tayari akaona kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtafuta alikuwa ndani ya nyumba ile, alichiokifanya akawapa wenzake ishara ya kumfuata na kisha kuwaomba watu wawapishe kwa ajili ya kuingia ndani jambo ambalo watu wale walionekana kutii.

    Filbert na wenzake wakabaki nje, tayari kwa muonekano ambao ulionekana ulionyesha dhahiri kwamba watu ambao walikuwa wakiwatafuta kwa lengo moja la kuwaua walikuwa ndani ya nyumba ile. Walijua fika kwamba kama wangejifanya kuingia moja kwa moja ndani, wasingeweza kufanikiwa kutokana na wapelelezi wale kuingia ndani ya nyumba ile, walichokiamua ni kusubiri pale nje ili hata kama wapelelezi wale wangetoka na watu wao, wangewaua wote bila kujali chochote kile na kisha kurudi nchini Marekani.

    “Wakitoka nao tu, tunawashambulia. Mmesikia?” Filbert aliwaambia wenzake.

    “Tumesikia” Silva, Gotz na Kelvin walijibu huku wakiwa tayari wamejiandaa kwa kuchukua bunduki zao zilizokuwa viunoni.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila mmoja alikuwa akimwangalia Bi Thum ambaye alikuwa amefika mlangoni na kuonyesha mshtuko hasa mara baada ya kuchungulia mlangoni kuona ni nani ambaye alikuwa akigonga mlango katika kipindi hicho. Bi Thum akageuka nyumba na kisha kuanza kuwaangali, kwa jinsi mtazamo wake alioutumia kuwaangali, ilionekana dhahiri kwamba mgongaji hakuwa mtu wa kawaida.

    Hapo hapo akachomoka kutoka pale mlangoni na moja kwa moja kuwafuata na kuwaambia kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kwani wagongaji waliokuwa wakiugonga mlango walionekana kumtia wasiwasi. Bahati ikaonekana kuwa upande wao hasa mara baada ya kuuona mlango wa upande wa pili ukiwa umefungwa. Kwa taratibu sana, Bi Thum akaanza kuufungua mlango ule na kisha kuwaambia waondoke katika nyumba hiyo huku yeye akijifanya kwenda kuufungua mlango na kujifanya kwamba ametoka kulala.

    Wote walikuwa wakikimbia kuelekea mbele, katika kipindi hicho angalau phillip alikuwa na uwezo wa kukimbia kwani ile dawa ambayo alikuwa amepakwa jana na Bi Thum ilionekana kumsaidia na kuufanya mguu wake kuwa katika hali ya kawaida.

    Bado walikuwa wakikimbia mbele pamoja na Gong, hawakutaka kusimama, tayari walikwishaona kwamba walikuwa katika hatari ya kukamatwa mahali hapo kwa hiyo walichokuwa wakikifanya katika kipindi hicho ni kujinusuru kutoka katika kila mkono wa mtu ambaye alionekana kuwa hatari kwao. Hawakutaka kumuamini mtu yeyote yule, vichwa vyao vikajua kwamba Bwana Robinson angeweza kutuma watu kwa ajili ya kuwatafuta na kuwauwa kama kuficha siri juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea.

    Waliendelea kukimbia zaidi mpaka kufika katika sehemu ambayo ilikuwa na soko kubwa, wakaingia ndani ya soko huku wakiendelea kukimbia. Waliendelea kusonga mbele mpaka pale ambapo wakafanikiwa kutoka nje ya soko na kuendelea mbele zaidi.

    Watu ambao walikuwepo sokoni pale wakaanza kuwaangalia kwa jinsi ambavyo walivyokuwa wakikimbia, tayari wasiwasi ukaanza kuwaingia kwamba mmoja wa watu wale ndiye alikuwa akitafutwa sana na Marekani katika kipindi hicho. Watu hawakutaka kutulia, wanaume nane ambao walionekana kuwa na miili ambayo ilikuwa imejazia, wakaanza kuwakimbiza.

    Williams, Phillip na Gong wakaonekana kushtuka kupita kawaida, kitendo cha kuwaona watu wakiwakimbiza kilionekana kuwashtua kwa kuona kwamba tayari watu wale walikuwa wamekwishawagundua wao walikuwa wakina nani. Kilichotokea mahali hapo, nao wakaanza kukimbia.

    Picha iliyoonekana mahali hapo ilionekana kuwa kama filamu fulani hasa kama zile za kina Rambo za kukimbizana mitaani. Watu wale walikuwa wakipiga kelele sana ili watu wengine ambao walikuwa wakipishana nao basi watoe msaada wa kuwakamata lakini hakukuwa na mtu ambaye alidiriki kufanya hivyo.

    “Tuingie humu” Williams alisema katika kipindi ambacho waliiona nyumba moja ikiwa mlango wazi, wakaingia ndani na Gong kuufunga mlango kwa kutumia makomeo.

    “Mmmh! Kweli hii ndio salama yetu?” Phillip aliuliza.

    “Hatujui. Ila hatutakiwi kutoka mpaka usiku”

    “Na vipi wenye nyumba wakija?”

    “Tutajua tutaongea nao vipi” Williams alijibu.

    Mara milango ya chumbani mule ikafunguliwa na wenye nyumba ambao walikuwa chumbani kutoka nje. Kila mmoja alionekana kushtuka, hawakuwafahamu watu ambao katika kipindi hicho walikuwa wameingia ndani ya nyumba yao. Kwa sababu wenye nyumba hao walikuwa ni wanawake, wote wakajikuta wakianza kutetemeka kwa woga.

    Gong akaanza kupiga hatua kuwafuata na kisha kuanza kuongea nao na kuwaeleza hali ambayo ilikuwa ikiendelea nje. Wanawake wale wakazidi kuogopa, walikuwa wakiwafahamu sana watu wa mtaa ule kwa jinsi walivyokuwa na hasira katika kipindi ambacho ulikuwa ukimficha mtu ambaye walikukuwa wakimhitaji.

    Watu wale ambao walikuwa wakiwakimbiza mara baada ya kufika nje ya nyumba ile wakaanza kugonga mlango kifujo fujo huku wakitaka wafunguliwe mlango na kisha kuingia ndani. Kila mmoja katika kipindi hicho alikuwa na hamu ya kumkamata Williams na kisha kumpeleka yeye mwenyewe katika kituo cha polisi kwa ajili ya kupata kiasi kile cha fedha cha dola milioni mbili ambacho kilikuwa kimeandaliwa na serikali ya Marekani.

    Ugongaji ule wa fujo wa mlango ndio ambao ukawafanya watu pale nje kukusanyika. Mara ya kwanza walipoulizwa kwamba kitu gani kilikuwa kikiendelea watu wale wala hawakutaka kujibu chochote kile ila baada ya kuona watu wakiongozeka na kuhofia kuhisiwa vibaya, wakaamua kuwaambia kwamba yule mtu ambaye alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani alikuwa ndani ya nyumba ile.

    Kila mtu ambaye alisikia hivyo, hakutaka kuondoka mahali hapo kitu ambacho kiliwafanya watu kujazana mahali hapo. Kila mtu ambaye alikuwa akipita njia aliposikia kwamba William alikuwa ndani ya nyumba hiyo, alisimama, nae alikuwa akitaka kumuona kwa macho yake mtu huyo.

    Ndani ya nyumba, kila mmoja alionekana kuwa na wasiwasi, hawakujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya ili kuondoka ndani ya nyumba hiyo bila kujulikana. Walijaribu kwenda nyuma ya nyumba, ni kweli kulikuwa na mlango ila hakukuwa na njia ya kutokea nje ya nyumba ile, sehemu moja ambayo ilikuwa ikitumika kutokea na kuingilia ni mlango wa mbele tuy, upande ambao watu walikuwa wamejikusanya kutaka kuwaona watu hao.

    “Tufanye nini?” Williams alimuuliza Phillip.

    “Sijui. Naona tunakamatwa hapa” Phillip alijibu.

    Gong alikuwa kimya kwa muda, katika kipindi hicho akili yake ilikuwa ikifikiria vitu vingi kwa wakati mmoja. Kichwa chake kikaanza kufikiria mitaa mbalimbali ndani ya jiji hilo la Bangkok huku, hakuwa radhi kuona kwamba wakati huo ndio ulikuwa mwisho wa kila kitu. Kama Williams na Phillip wangekamatwa, hiyo ilikuwa na maana kwamba huo ndio ungekuwa mwisho wake kuonana na watu hao na hata ndoto yake la kwenda nchini Marekani ingekuwa imefutika kabisa katika maisha yake.

    “Ni lazima nifanye kitu” Gong alijisemea na kisha kutoka nje ya nyumba ile na kuelekea nyuma ya nyumba ile. Kila mtu alikuwa akimwangalia Gong ambaye alionekana kuwa mtu wa haraka sana, alipofika nyuma ya nyumba ile, akaanza kuangalia huku na kule kama mtu ambaye alikuwa akitafuta vitu fulani.

    Kichwa chake katika kipindi hicho kilikuwa kikifikiria jambo moja tu, kuondoka ndani ya nyumba ile bila kuonekana na mtu yeyote. Macho yake yakatua katika ngazi ambayo ilikuwa pembeni ya ukuta wa nyumba ile, akaifuata ngazi ile na kisha kuisimamisha vizuri.

    Akawafuata Williams na Phillip na kisha kuwaonyeshea kitendo kwamba walitakiwa kumfuata na hivyo kufanya hivyo. Alichowataka kukifanya kwa wakati huo ni kuwaambia wapande juu ya ngazi na kisha kuelekea kwenye bati la nyumba hiyo na kisha kuanza kutembea tembea kwa kukanyaga kanyaga misumali na kisha kurukia upande wa pili.

    Wazo lake lilionekana kuwa bora kabisa, walichokifanya ni kufanya kama ambavyo aliwataka kufanya na kutokea juu ya bati. Wakaanza kutembea tembea juu ya bati kwa nia ya kutokea upande wa pili. Kwao, waliona njia ile kuwa njia nzuri ya kuweza kutoroka mahali hapo. Walipoona kwamba wamefanikiwa kutokea upande wa pili, wakarukia chini.

    “Hapa ni kukimbia tu” Williams aliwaambia na kisha kujiandaa kukimbia.

    Ila kabla hawajafanya hivyo, wakajikuta wakiwekwa chini na vijana wa bwana Robinson ambao walikuwa na bunduki katika mikono yao.

    “You are under arrest (Mko chini ya ulinzi)” Filbert alisema huku akionyesha tabasamu, kwao, kazi ambayo walikuwa wametumwa kuifanya nchini Thailand ikaonekana kukamilika kwa asilimia tisini na tano.

    “Oooh! My God! (Oooh! Mungu wangu!): Phillip alijikuta akisema kwa mshtuko huku midomo ya bunduki ikiwa imewaelekezea, ni kitu kimoja tu ndicho ambacho kilikuwa kimebaki, kuwafyatulia risasi na kisha kuondoka mahali hapo.

    ****

    Vijana wa Bwana Robinson walikuwa wametulia huku wakiwaangali wapelelezi ambao waliingia ndani ya ile nyumba huku lengo lao katika kipindi hicho likiwa moja tu, kuwamiminia risasi wote katika kipindi ambacho wangetoka ndani ya nyumba ile. Waliendelea kusimama mahali pale huku wakifuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kikiendelea. Ghafla, kwa mbali macho yao yakafanikiwa kuwaona watu ambao walikuwa juu ya bati, japokuwa hawakuwa wakiwaona vizuri, walikuwa na uhakika kwamba watu wale walikuwa Williams na Phillip.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa haraka sana bila kupotyeza muda wakachomoka mahali pale. Tayari walijua kwamba watu wale ambao walikuwa wakiwatafuta walikuwa wametoka ndani ya nyumba ile na kwa kipindi hicho walikuwa wakijitahidi kutoroka kusonga mbele, walijua kwamba kama wasingeamua kuwafuata basi wangeweza kuwatoroka.

    Wakakimbia mpaka kufika nyuma ya nyuma ile na kisha kujificha katika ukuta huku kwa mbali wakisikia mlio wa kukanyagwa kwa bati. Wakaziandaa bunduki zao vilivyo, Williams, Phillip na Gong waliporukia chini, wakawafuata na kuwaweka chini ya ulinzi.

    Kila mmoja alikuwa na hamu ya kuwapiga risasi haraka haraka na kisha kupotea mahali hapo,. Huku kila mmoja akiwa amejiandaa kuwafyatulia risasi, zaidi ya watu ishirini wakatokea mahali hapo, kitu ambacho kiliwafanya kuziweka bunduki zao viunoni na kisha kujifanya kuwaweka chini ya ulinzi kwa kuwaambia wasonge mbele huku nao wakiwa nyuma wakiwafuatilia kwa ukaribu.

    Vichwa vya Williams na Phillip kwa wakati huo vilikuwa vikifikira mambo mengi mfululizo namna ambayo wangefanya kuwatoroka watu hao ambao walikuwa wakiwafuatilia nyuma yao huku watu wengine wakiwa wanafuatilia kila kilichokuwa kikiendelea. Walijua fika kwamba kama wangetamua kukimbia basi watu wale wangeweza kuwamiminia risasi na huo ndio kuwa mwisho wao.

    Walipofika katika usawa wa mbele ya nyumba ile, watu wakaanza kupiga kelele, tayari waliona kwamba watu wale ambao walikuwa wamekimbilia ndani ya nyumba ile walikuwa wamekwishawekwa chini ya ulinzi na wazungu ambao hawakuonekana kuwafahamu zaidi ya kuhisi kwamba watu wale walikuwa mapolisi kutoka nchini Marekani.

    *****

    Mpelelezi Adrian pamoja na wenzake wakaingia ndani ya nyumba ile na kisha kuanza kuwatafuta Williams na Phillip lakini hawakufanikiwa kuona kitu. Walipojaribu kuwauliza watu wale juu ya watu ambao walikuwa wakiwatafuta katika kipindi hicho, mwanamke mmoja akawaonyeshea ishara kwamba watu hao walikuwa wamekimbilia nyuma ya nyumba huku wakiwa na lengo la kutoroka.

    Kwa haraka haraka wakaelekea huko nyuma ya nyuma, wakakuta ngazi ikiwa imesimamishwa ukutani jambo ambalo liliwafanya kujua kwamba watu hao walikuwa wamekimbia kwa kutumia ngazi ile, wakajiona wakiwa wameshindwa unjanja kwa mara nyingine tena. Huku kila mmoja akiwa ameikodolea macho ngazi ile, mara kelele zikaanza kusikika kutoka nje, mbele ya nyumba ile hali ambayo iliwafanya kuelekea kule.

    Walipofika nje ya nyumba ile, macho yao yakatua kwa watu ambao walikuwa wakiwatafuta, Williams na Phillip huku nyuma yao wakiwa wanafuatwa kwa ukaribu na watu ambao wala hawakuwa wakiwaelewa ni wakina nani. Wote saba walipokutanisha macho, wakaonekana kushtuka. Kila mmoja kwa wakati huo alionekana kutokumuelewa wenzao, makundi mawili yakawa yamekutana huku kila mmoja akiwa anawataka watu ambao tayari walikuwa chini ya ulinzi.

    Watu wengi ambao walikuwa wakifuatilia mchezo ule walishindwa kuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea mahali pale, tayari nao wakaanza kuhisi kitu kwamba yale yalikuwa makundi mawili ambayo yalikuwa tofauti huku wote kwa pamoja wakiwataka watu wale ambao walikuwa wamewaweka chini ya ulinzi katika kipindi hicho.

    Williams na Phillip walikuwa wamesimama wakiwaangalia watu hao ambao walikuwa wakiangaliana kwa wasiwasi mkubwa sana, tayari nao wakajua kwamba yale yalikuwa makundi mawili tofauti, na walijua kabisa kwamba kundi moja lilikuwa limetumwa na Bwana Robinson huku kundi jingine likiwa ni la wapelelezi wa FBI.

    Kila mmoja kwa wakati huo akaanza kujishika kiunoni kuonyesha kwamba kilichofuatia kwa wakati huo ni kurushiana risasi tu na kuuawana huku kundi ambalo lingekuwa mshindi basi lingeondoka na Williams pamoja na Phillip. Kila mtu alikuwa makini kufuatilia kila kichokuwa kikiendelea, ghafla, kila mmoja akatoa bunduki yake kiunoni na milio ya risasi kusikka mahali hapo jambo ambalo lilimfanya kila mtu kukimbia huku akipiga kelele.



    Je ni nini kitaendelea mahali hapo?

    Hii ni hadithi iliyokaa mtindo wa muvi.



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog