Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

HILI NI JIJI LA NEW YORK - 4

 





    Simulizi : Hili Ni Jiji La New York

    Sehemu Ya Nne (4)



    Wapelelezi walinekana kuwa na mafunzo makubwa sana ya kupigana na maadui, kitendo cha vijana wale kutoa bunduki zao viunoni, kwa kasi ya ajabu wapelelezi wale wakabinuka sarakasi za kiupande upande huku wakiiacha mikono yao ikiwa imeshika bunduki huku zikiwa zimewaelekezea vijana wale. Risasi za vijana wale hazikumpata mtu, zilikuwa zimekwenda patupu ila risasi za wapelelezi wale zilikuwa zimewalenga vijana wale.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Milio ile ya risasi ambayo ilikuwa imesikika mahali hapo ikawafanya watu wote kukimbia hovyo, hakukuwa na mtu ambaye alikumbuka kama katika sehemu ile ambayo walikuwa wamekusanyika ndio sehemu ambayo alikuwepo Williams, mtu ambaye alikuwa akitafutwa sana huku kwa mtu ambaye angeweza kufanikisha kukamatwa kwake basi angekuwa akiuaga umasikini, katika kipindi hicho, kila mtu alikuwa akijaribu kuiokoa nafsi yake.

    Kitendo kile cha watu kukimbia ovyo kikaonekana kuwa kama mwanya kwa Williams na Phillip, nao wakaanza kukimbia pamoja na watu hao huku wakiwaacha wapelelezi na vijana wale wakiendelea kurushiana risasi. Gong ambaye alikuwa mbali kabisa alikuwa akifuatilia kila kitu kwa ukaribu, mara baada ya kusikia milio ya risasi, macho yake alikuwa ameyaelekeza kwa Williams na Phillip tu.

    Katika maisha yake, milio ya risasi wala haikuonekana kumtisha, kwake, milio ile ilizoeleka na kuwa kama mdundo wa muziki masikioni mwake kutokana na kutumia bunduki kwa kipindi kirefu sana walipokuwa msituni pamoja na waasi wenzake ambao walikuwa na tabia ya kuwateka watoto wa viongozi na matajiri mbalimbali.

    Kwa kasi kubwa Gong akaanza kukimbia kuelekea kule ambapo Williams na Phillip walipokuwa wakikimbilia, katika kipindi hicho hakutaka kabisa kuwapoteza, alijua fika kwamba kwa jinsi ambavyo angekuwa akijaribu kuwa nao karibu na ndivyo ambavyo angeweza kupata kile ambacho alikuwa akikitarajia kukipata katika maisha yake, kuishi nchini Marekani tu.

    Mara baada ya kuwafikia, akaanza kukimbia nao kusonga mbele zaidi. Watu bado walikuwa wakikimbia ovyo, milio ile ya risasi iliwafanya kujiona kama kuwa kwenye uwanja mkubwa na wa hatari wa vita, kila mtu alikuwa akijaribu kuokoa maisha yake.

    “Are you okey? (Upo sawa)” Williams alimuuliza Phillip huku wakikimbia.

    “I am okey (Nipo sawa)” Phillip alijibu.

    Bado walikuwa wakiendelea kusonga mbele kama kawaida yao, hakukuwa na haja ya kusimama sehemu yoyote ile, kila mmoja alikuwa akitaka kuiokoa nafsi yake. Tayari katika kipindi hicho walikwishajua kwamba walikuwa wanatafutwa na makundi mawili, kundi moja lilikuwa likimtaka Williams kwa udi na uvumba huku kundi jiingine likiwa linawataka wote wawili.

    Gong akawachukua na kuwapeleka katika sehemu ambayo ilikuwa na uwanja mkubwa na kisha kutafuta mti na kisha kup[umzika. Walikaa katika eneo hilo chini ya mti huku wakianza kuongea mambo mengi ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yao, hawakuamini kama Mungu alikuwa amewalinda na kila njia ambayo walikuwa wakipita katika maisha yao kwa kipindi hicho. Bwana Robinson ndiye ambaye alionekana kuyatawala mazungumzo yao, mtu huyo alionekana kuwa mtu katili sana ambaye kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima afikishwe katika vyombo vya sheria kwa makosa ya mauaji.

    Katika kipindi chote hicho, Gong alikuwa kimya huku akiwa hayatulizi macho yake sehemu moja, yeye ndiye alikuwa mlinzi wa watu hao katika kipindi hicho, alijiona kuwa na uhitaji wa kuendelea kuwalinda watu hao, alijiona kuwa radhi kufa lakini si kuona watu hao wakiuawa mbele ya macho yake, alikuwa tayari kupigana kufa na kupona kwa ajili ya kuwalinda watu hao.

    “What should we do? (Tufanye nini?)” Phillip aliuliza.

    “We have to run (Itatubidi kukimbia)”

    “To run? All the time? No Williams. We have to do something else (Kumbia? Muda wote? Hapana Williams. Inatakiwa tufanye kitu kingine)” Phillip alimwambia Williams.

    “What should we do? (Tufanye nini?)

    “Lets get back to America (Turudi Marekani)” Phillip alishauri.

    “Immpossible (Haiwezekani)” Williams alijibu.

    “We are going back and explain what the hell went on here (Tunarudi na kuwaambia kile kilichoendelea hapa)” Phillips alimwambia Williams.

    “Listen to me Phillip, we aint’t go back. We have to run, we have to hide. If we go back there, Robinson will kill us (Nisikilize Phillp, haturdi. Inatupasa tukimbie, inatupasa tujifiche. Kama tutarudi, Robinson atatuua)” Williams alimwambia Phillip huku akiwa amesimama.

    Malumbano yakawa yameanza mahali hapo, Phillip bado alikuwa aking’ang’ania waondoke hapo nchini Thailand na kisha kurudi nchini Marekani lakini kwa Williams jambo hilo likaonekana kuwa gumu kwake. Mtu ambaye alikuwa akimfikiria mahali hapo alikuwa ni Bwana Robinson. Alijua fika kwamba endapo wangerudi nchini Marekani, mzee huyo angeweza kuwaua hata kabla hawajatoka nje ya uwanja wa ndege wa John F Kennedy kutokana na kuwa na watu wengi kila kona ambao walikuwa wakimfanyia kazi.

    Bwana robinson alionekana kuwa mtu hatari sana kwao, mtu ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kutumia kiasi chochote kikubwa cha fedha ili mladi kukamilisha kitu ambacho alikuwa akitaka kukikamilisha. Williams alikuwa akiopgopa kupita kiasi kuelekea nchini Marekani, alijua fika kwamba kama wangekwenda huko kulikuwa na uwezo wa kuuawa hata kabla ya kutoa siri juu ya kilichokuwa kimeendelea.

    Hwakukaa sana mahali hapo, wakainuka na kisha kuendelea na safari yao. Katika kipindi hicho walijiona kuwa na kila sababu ya kuondoka ndani ya nchi hiyo kuelekea katika nchi nyingine tena kwa kutumia meli yoyote ya mizigo. Kila kitu ambacho walikuwa wakikifikiria vichwani mwao waliviona kustahili kufanyiika. Katika kipindi hicho, Williams alitaka waelekee sehemu moja tu, Ghana, nchi aliyokuwa akiishi mama yakje,

    “Tutapata vipi fedha za kusafiria?” Phillip aliuliza.

    “Hilo si tatizo kubwa”

    “Hapana. Usitake kuona kila kitu kuwa si tatizo Williams, Ni lazima tujue namna ya kupata fedha” Phillip alimwambia Williams.

    “Tumtumie huyu kijana” Williams alimwambia Phillip.

    “Tumtumie vipi?”

    “Kutupatia fedha”

    “Unanichanganya. Tutamtumia vipi hapo?” Phillip aliuliza.

    “Unaonaje kama akienda kufungua akaunti benki na kisha kumwambia baba antume hata dola milioni mbili kupitia katika akaunti ambayo ataifungua?” Williams alimwambia Phillip na kisha kumuuliza.

    “Wazo zuri ila....”

    “Ila nini?”

    “Limejaa hatari”

    “Hatari gani?”

    “Atawezaje kutoa kiasi kikubwa cha fedha namna hiyo huko benki?” Phillip aliuliza.

    “Hilo usilitilie shaka. Niamini kwamba kila kitu kitafanikiwa. Ila kuna tatizo moja limejitokeza” Williams alimwambia Phillip.

    “Tatizo gani?”

    “Nani atakayemwambia mpango huu na wakati lugha yake hatuifahamu?”

    “Mmmh! Sasa tufanye nini?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ngoja. Kuna wazo nimelipata”

    “Wazo gani?”

    “Nenda nae mpaka benki na kisha fungua nae akaunti” Williams alimwambia Phillip.

    “Mmmh! Nikikamatwa?”

    “Na nani?”

    “Wanaotutafuta. Au hata wananchi”

    “Wananchi hawakujui. Wananijua mimi. Wewe hautafutwi. Natafutwa mimi tu” Williams alimwambia Phillip.

    “Mmmh! Mbona naona moyo hautaki kabisa” Phillip alisema huku akimwangalia Williams usoni.

    “Jikaze. Saa sita sasa hivi. Ikiwezekana nendeni hata sasa hivi mkafungue hiyo akaunti benki. Ila cha msingi nendeni kwenye benki ambayo haina gharama yoyote katika kufungua akaunti, si unajua hatuna fedha hata kidogo” Williams alimwambia Phillip.

    “Sawa. Usijali” Phillip alimwambia Williams.

    “Nyie nendeni. Mtanikuta hapa hapa” Williams alimwambia.

    “Ila usiondoke mahali hapa”

    “Usijali”

    Hakukuwa na cha kupoteza mahali hapo, alichokifanya Phillip ni kumchukua Gong na kisha kuanza kuondoka nae. Gong hakuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea, lugha ya Kingereza ambayo ilikuwa imeongelewa mahali pale haikuwa imeeleweka kabisa kwake. Alichokifanya Phillip ni kuongea neno moja tu, Benki, neno ambalo aliona kwamba lilikuwa likieleweka na watu wengi katika mataifa mbalimbali.

    Alichokifanya Gong ni kuanza kuelekea katika njia ambayo ilikuwa ikielekea katika benki ya People ambayo wala haikuwa mbali kutoka mahali hapo walipokuwa. Wala hawakuchukua muda mrefu, wakawa wamekwishafika katika benki hiyo na kuingia ndani. Kwa haraka haraka Phillip akaanza kupiga hatua kumfuata mfanyakazi mmoja wa benki na kuanza kuongea nae kuhusiana na kitu kilichowaleta mahali pale.

    “Hakuna gharama kufungua akaunti. Ila tungehitaji akapigwe picha upande wa pili wa benki hii” Msichana huyo, mfanyakazi wa benki alimwambia Phillip.

    “Kuna gharama zozote katika upigaji picha?”

    “Ndio. Paundi moja”

    “Fedha nyingi sana”

    “Mmmh! Fedha nyingi?”

    “Ndio. Hapa hatuna kitu mifukoni. Hatuwezi kusaidiwa halafu fedha zenu tutawalipa?” Phillip aliuliza.

    “Hilo suala ni la kuongea na mpiga picha”

    “Sawa. Ila yeye hatujui. Hauwezi kutusaidia?”

    “Itakuwa ngumu sana. Mimi mwenyewe siwajui”

    “Tafadhali. Naomba utusaidie. Naomba utusaidie” Phillip alimwambia msichana yule.

    Macho ya Phillip yalionyesha dhahiri kuhitaji msaada kwa wakati huo, msichana yule akajiona akianza kuingiwa na huruma moyoni mwake, kadri alivyokuwa akiyaangalia macho ya Phillip ndivyo ambavyo alikuwa akijiona kuwa na mzigo wa kuwasaidia. Alichokifanya mahali hapo ni kuelekea huko kwa mpiga picha na kisha kumwambia ampige Gong na kisha kuanza kurudi benki na kuanza harakati za kufungua akaunti.

    Walichukua dakika thelathini na ndipo kila kitu kikakamilika na kisha kuanza kuelekea kule ambapo walikuwa wamemuacha Williams. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha kwani kila kitu kilikuwa kimekwenda kama kilivyotakiwa kiwe. Ni upigaji wa simu ndio ambao ulikuwa ukihitajika kufanyika na kisha Williams kuongea na Bwana Kurt na kumuomba amtumie fedha katika akaunti ile.

    Kitu cha kushangaza ambacho walikutana nacho, walipofika mahali pale, Williams hakuwepo jambo ambalo likaonekana kuwashtua kupita kawaida. Phillip akaanza kuota mahali hapo lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliitikia. Kila mmoja alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, halikuwa jambo jepesi kumuacha mtu sehemu halafu usimkute, moja kwa moja vichwa vyao vikaanza kujua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kimetokea mahali hapo.

    Phillip akaanza kukimbia huku na kule akijaribu kuliita jina la Williams lakini wala hakuweza kumuona jambo ambalo lilionekana kumuongezea wasiwasi kupita kawaida. Waliendelea kumuita na kumtafuta zaidi na zaidi lakini bado majibu yalikuwa ni yale yale, Williams hakuoneklana hali ambayo ilionekana kuwachanganya wote wawili.









    Hali bado ilikuwa ikichanganya kichwani mwa mkuu wa kitengo cha upelelezi cha FBI nchini Marekani, Bwana Mikey Swan. Kila wakati alikuwa akipiga meza yake kwa hasira, alikuwa akishangaa sana sababu ambayo ilikuwa ikimfanya Williams kutokupatikana mpaka muda huo na wakati mtu huyo wala hakuwa amesomea ujasusi hata mara moja.

    Ripoti ya mwisho ambayo alikuwa amepewa ni kwamba wapelelezi ambao walikuwa wametumwa nchini Thailand walikuwa wamekutana na kizuizi kikubwa, mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Williams alikuwa amewekwa chini ya ulinzi na watu wengine wanne ambao wala hakuwa akiwafahamu wale walikuwa wakina nani.

    Jambo jingine ambalo lilikuwa limemshtua zaidi ni baada ya kuambiwa kwamba Williams alikuwa pamoja na Phillip, mchezaji mwingine wa kikapu ambaye alikuwa katika timu hiyo. Bwana Swan alichanganyikiwa kupita kawaida, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea. Kila swali ambalo alikuwa akijiuliza kuhusiana na watu hao, hakuwa akipata jibu.

    Hapo ndipo ambapo alikuja kupata kitu fulani kwa kuona kwamba watu ambao walikuwa wakimtafuta Williams hawakuwa FBI tu bali walikuwa hata watu wengine ambao wala hawakuwa wakijulikana. Tayari hapo alikuwa na uhakika kwamba kama wasingefanya jambo la ziada basi Williams angeweza kuuawa hata kabla hawajamtia mikononi mwao kwani hadi katika kipindi hicho watu wale hakuwa akiwaelewa kabisa.

    Hapo ndipo likamjia wazo jingine, wazo ambalo aliliona kama angelifanya basi lingekuwa bora zaidi. Kichwa chake kikaanza kumfikiria Sam, mpelelezi bora ambaye alikuwa amefanikiwa kujua ndege ilipo pamoja na kuileta miili ya wachezaji nchini Marekani, aliona kuwa na kila sababu za kutaka kumrudisha mtu huyo kazini kwani kazi nyingine kubwa tayari ilikuwa imejitokeza, kazi ya kumkamata Williams.

    Alichokifanya ni kunyanyua mkonga wa simu na kisha kupiga namba fulani na baada ya muda fulani akawa anaongea na mtu simuni. Aliongea kwa sekunde kadhaa na kisha kukata simu ile. Bwana Swan akaanza tena kuwa katika hali ya mawazo, kelele za Wamarekani ambao walikuwa wakitaka Williams akamatwe haraka sana bado zilikuwa zikisikika masikioni mwake, tena kwa ndani kabisa.

    Bwana Swan alikaa katika hali hiyo kwa dakika kadhaa, mara mlango wake ukaanza kugongwa, alipomkaribisha mgongaji, alikuwa mpelelezi Sam. Bwana Swan akatoa tabasamu pana, kitendo cha kumuona Sam ndani ya ofisi yake tayari alijiona kukamilisha kile ambacho alitaka kikamilishwe kwa wakati huo. Akamkaribisha kitini na kisha kuanza mazungumzo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kuna kazi nataka uifanye” Bwana Swan alimwambia Sam.

    “Ndio mkuu” Sam aliitikia.

    “Nadhani unajua ni kwa jinsi gani tunamhitaji Williams. Tunamtaka mikononi mwetu ili dunia itulie na isitupigie kelele tena” Bwana Swan alimwambia sam.

    “Hao waliokwenda huko wamesemaje?”

    “Nani? Adrian na wenzake?”

    “Ndio”

    “Walimuona. Ila walimuona na watu ambao walimuweka chini ya ulinzi. Tena nahisi kutoka nchini Marekani” Bwana Swan alimwambia Sam.

    “Watu kutoka nchini Marekani?” Sam aliuliza kwa mshtuko.

    “Ndio”

    “Kuna mambo mengi sana nimeanza kuhisi. Hasa hapa uliposema kwamba watu kutoka nchini Marekani. Kuna jambo nimelihisi” Sam alimwambia Bwana Swan.

    “Jambo gani?”

    “Utaweza kuniamini kama nikikwambia?” Sam aliuliza.

    “Ninakuamini. Kila siku nimekuwa nikikwambia kwamba nakuamini sana” Bwana Swan alimwambia Sam.

    “Utaniamini kama nikikwambia kwamba inawezekana Williams hakufanya mauaji hayo wala kuiteka ndege?” Sam alimwambia Bwana Swan ambaye akaonekana kushtuka.

    “Unasemaje?”

    “Nahisi kwamba Williams hakufanya mauaji. Hiyo ni kwa sababu ya upelelezi ambao niliufanya kwa siku kadhaa” Sam alimwambia Swan.

    “Siwezi kuamini hilo”

    “Ngoja kwanza” Sam alisema na kisha kuichukua brifukesi ambayo alikuwa ameingia nayo ndani ya ofisi ile.

    Bwana Swan akabaki kimya, akili yake ikaonekana kuchanganyikiwa zaidi, maneno ambayo alikuwa ameongea Sam yalionekana kumchanganya kwa wakati huo. Hakuamini kama Williams hakuwa amefanya mauaji hayo na wakati kila kitu kilikuwa kikijulikana na hata alama zake za vidole zilikuwa zimekutwa katika bunduki ambayo alikuwa nayo na kutaka kumuua Bwana Robinson. Sam akaifungua brifukesi ile na kisha kutoa makaratasi fulani.

    “Ngoja nikwambie kitu kimoja” Sam alimwambia bwana Swan na kuanza kuelezea.

    “Bwana Robinson alituambia kwamba Williams ndiye ambaye alikuwa amewaua wachezaji wengine na hata kufanya mchakato wa kuiteka ndege. Unakubaliana nae?” Sam alisema na kuuliza.

    “Asilimia mia moja” Bwana Swan alijibu.

    “Sawa. Huyo huyo Bwana Robinson alisema kwamba alitaka kuuawa na Williams. Ila kumbuka kwamba Williams yupo pamoja na Phillip. Kwa nini hakumtaja Phillip?” Sam aliuliza.

    “Mmmh! Sijui”

    “Sawa. Inawezekana hilo hujui. Ila kwa nini Bwana Robinson alikwenda nchini Thailand?” Sam aliuliza.

    “Kutokana na maelezo yake, alisema kwamba alikwenda kule kwa ajili ya kununua nyumba ya kifahari” Bwana Swan alijibu.

    “Sawa. Ila kwa nini iwe Thailand? Unakumbuka kwamba Serikali ya Thailand imekataza wageni kununua nyumba, mashamba pamoja na viwanda katika nchi yao? Unakumbuka kwamba katiba yao inapinga sana jambo hilo kutokea?” Sam alimuuliza.

    “Ndio nakumbuka”

    “Sasa kwa nini Bwana Robinson amesema kwamba alikwenda huko kununua nyumba na wakati anajua dhahiri katiba ya nchi hiyo hairuhusu?” Sam aliuliza.

    “Oooooppppsss” Bwana Swan alitoa pumzi ndefu.

    “Sawa. Tujifanye tupo upande wake. Ila nadhani unajua kwamba matajiri wengi wanapenda kutembea na walinzi hasa wanapokuwa katika nchi ngeni kwa ajili ya usalama wao. Sasa inakuwaje yeye kuwa peke yake? Ok! Tufanye kwamba alikuwa na mlinzi, ila alikuwa wapi katika kipindi ambacho alikuwa akitaka kuuawa na Williams?” Sam bado alikuwa akiendelea kuuliza maswali mfululizo.

    “Mmmh! Maswali magumu sana kujiuliza hayo”

    “Sawa. Tufanye walikuwa wote. Ila kumbuka kwamba matajiri wote wanaotembea na walinzi wao, walinzi wanakuwana bunduki. Si ndio hivyo?” Sam aliuliza.

    “Ndio”

    “Sasa kama mlinzi alikuwepo hapo na baada ya kuona kwamba bunduki aliyoishika Williams ilikuwa haina risasi, kwa nini asingetumia bunduki yake kumfyatulia?” Sam aliuliza.

    “Mmmh! Maneno yako yanazidi kunichanganya”

    “Hayo hayawezi kukuchanganya. Ili linalofuatia ndio litakuchanganya zaidi” Sam alimwambia Bwana Swan.

    “Lipi?”

    “Bunduki iliyotumika kushikwa na Williams, ni moja ya bunduki chache sana ambazo zinapatikana nchini Marekani tu. Sasa swali linakuja. Kama hii ilikuwa ni bunduki ya Williams, aliweza vipi kusafiri nayo kuanzia hapa, Marekani mpaka China, na kutoka China mpaka Thailand bila kuonekana katika viwanja vya ndege?” Sam aliendelea kuuliza.

    “Mmmh!”

    “Mara nyingi watu wanaokwenda kununua nyumba hasa matajiri huenda na mawakili wao, sasa kwa nini yeye hakwenda na wakili wake kama kawaida? Je ni kweli alikuwa akienda kununua nyumba au kuna jingine?” Sam aliuliza.

    “Mmmh!”

    “Nilijiuliza sana maswali haya. Mwisho wa siku nikaguna kama ulivyoguna” Sam alimwambia Swan.

    “Hapa umenichanganya”

    “Najua. Sikuishia hapo, nikaendelea zaidi kufanya uchunguzi wangu. Nikaanza kuangalia ushindani wa timu za mpira wa kikapu. Timu ya New Bucketts inaongoza huku ikifuatiwa na timu ya Boston Five kwa kipindi cha miaka miwili sasa” Sam alisema.

    “Hilo linafahamika”

    “Nashukuru kulifahamu hilo. Ila unajua ni nani mmiliki wa timu ya Boston Five?” Sam aliuliza.

    “Mungu wangu! Robinson!” Bwana Swan alisema kwa mshtuko.

    “Ok! Nimefurahi kwa sababu umelijua hilo”

    “Kuna ukweli hapo..... Ila sasa muuaji ni nani?”

    “Ni afadhali usiweze kusoma lakini picha unaiona”

    “Unamaanisha nini?”

    “Utakuwa ukimjua muuaji ni nani” Sam alimwambia Bwana Swan.

    “Robinson”

    “Nashukuru kwa usikivu wako mkuu. Ngoja niende nikajiandae na safari. Nitakapompata Williams, ataniambia ukweli. Nakutakia kazi njema” Sam alimwambia Bwana Swan na kuondoka ndani ya ofisi ile.

    “Genius” Bwana Swan alijikuta akisema huku akimwangalia Sam ambaye alikuwa akiondoka ndani ya ofisi yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****

    Damu zilikuwa zimetapakaa mahali hapo, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akionekana katika eneo hilo zaidi ywa wapelelezi wale pamoja na wale vijana ambao walikuwa wametumwa na Bwana Robinson, tena huku wakiwa chini na damu zikiwatoka. Adrian pamoja na wapelelezi wenzake wakaanza kuwasogelea vijana wale na kisha kuanza kuwaangalia, walikuwa wamekufa.

    Hapo hapo ndipo kumbukumbu zikawajia kwamba lengo lao la kuwa mahali pale lilikuwa ni kumchukua Williams ambaye alikuwa katika eneo hilo katika kipindi kichache kilichopita tena huku akiwa pamoja na Phillip. Wakaanza kuangalia mahali hapo, hakukuwa na mtu yeyote jambo ambalo likawafanya kuanza kuondoka mahali hapo huku wakikimbia, tayari walijiona kumpoteza mtu ambaye walikuwa wakimtafuta kwa wakati huo.

    Adrian na wenzake waliendelea kukimbia zaidi na zaidi, kila mmoja alikuwa makini kuangalia huku na kule kwa kuamini kwamba wangeweza kumuona Williams au Phillip ambao walikuwa na uhakika kwamba kama walikuwa wamekimbia basi wangekuwa hawajafika mbali kutoka hapo ambapo walipokuwa.

    “Twende upande upi?” Mpelelezi mmoja alimuuliza Adrian.

    “Kushoto” Adrian alijibu na kisha wote kuanza kuelekea upande wa kushoto.

    Waliendelea kwenda mbele zaidi lakini bado hali ilionekana kuwa vile vile, si William wala Phillip ambaye alikuwa akionekana mbele ya macho yao. Kila mmoja alionekana kukata tamaa, hawakuami kama kweli mtu ambaye alikuwa wakimtaka mahali hapo walikuwa wamemkosa, walijiona kufanya kosa moja kubwa sana kumuacha Williams akimbie katika kipindi kile ambacho walikuwa wakirushiana risasi na vijana wale.

    “Tufanye nini sasa?” Brian, mmoja wa wapelelezi aliuliza.

    “Tumtafuteni zaidi” Adrian alijibu.

    “Ila tutaendelea kumtafuta tu huku hatuopni hata dalili yake?”

    “Subiri” Adrian alisema na kisha kuchuchumaa chini.

    Adrian akainama chini na kisha kuliweka jicho lake karibu na ardhi na kisha kuanza kuangalia kwa makini. Adriaan aligeuka katika kila upande, mafunzo fulani ambayo alipewa katika kipindi alichokuwa akianza upelelezi yalimfanya kuwa na hisia kali hasa kugundua mambo mengi katika kipindi ambacho angetakiwa kwenda sehemu gani. Machale yakaonekana kumcheza, akasimama na kisha kuwaambia wenzake kumfuata.

    “Twendeni upande huu” Adrian aliwaambia.

    Wote wakaanza kumfuata mpaka pale ambapo wakatokea katika uwanja mkubwa. Wakaanza kuyapitisha macho yao katika uwanja ule mkubwa ambao kwa mbali kulionekana kuwa na mti mdogo. Adrian akaanza kuuangalia mti ule, kadri ambavyo alivyozidi kuuangalia mti ule na ndivyo ambavyo machale yakaanza kumcheza zaidi jambo ambalo likamfanya kuwaggeukia wenzake.

    “Jua kali sana. Nahisi tunahitaji kupumzika. Au nyie mnaonaje?” Adrian aliwaambia.

    “Sawa sawa”

    “Mngependa twende tukapumzikie wapi kwenye kivuli?” Adrian aliuliza.

    “Nadhani kwenye ule mti”

    “Hivyo ndivyo walivyokuwa wameamua” Adrian aliwaambia.

    “Wakina nani?”

    “Williams na Phillip. Inaonekana walikimbia sana, jua likaanza kuwachoma na kisha kuhitaji kupumzika kwa muda. Unafikiri kama walifika katika sehemu hii wangehitaji sehemu gani kupumzika?” Adrian aliuliza.

    “Nadhani kwenye ule mti”

    “Safi sana. Twendeni pale, baada ya hapo nitawaambia wapi pa kwenda” Adrian aliwaambia na kisha wote kuanza kuelekea katika mti ule.

    Adrian alijua fika kwamba kwa wakati huo walikuwa wamekwishashindwa kumpata Williams kitu ambacho kilimfanya kuanza kutumia ujuzi wa nyongeza aliokuwa amefundishwa pamoja na akili ya kuzaliwa tu. Walizidi kupiga hatua mpaka kwenye mti ule na kisha kupumzika. Adrian hakutaka kupumzika, kitui alichokuwa akikifanya ni kuanza kuuzunguka zunguka mti ule huku akiangalia chini.

    Tayari hisia zake zilikuwa kali sana katika kipindi hicho, alionekana kugundua kitu kwa wakati huo. Alama za miguu ya watu zilikuwa zikionekana ardhini jambo ambalo likampa uhakika kwamba alikuwa akienda sawa na hisia zake ambazo zilikuwa zikimjia kichwani mwake. Hapo hapo akawaambia wenzake wainuka na kisha kuanza kuzifuata alama za miguu ambazo zilikuwa zikielekea katika upande wa Kaskazini.

    Waliendelea kuzifuata alama zile za miguu mpaka pale ambapo walifika katika eneo ambalo halikuwa na alama za miguu ile. Wote wakaanza kuangalia angalia, mara kwa mbali, wakafanikiwa kumuona mtu akiwa amesimama pembeni ya jengo moja ambalo lilionekana kuendelea na ujenzi. Kwa kumwangalia tu, walikuwa na uhakika kwamba mtu yule alikuwa Williams kwa jinsi ambavyo mavazi yake aliyokuwa ameyavaa kuwa yale yale.

    Kwa mwendo wa machale tena wa kujificha ficha wakaanza kusogea kule alipokuwa amesimama. Williams alipoyainua macho yake juu, akapatwa na mshtuko mkubwa mara baada ya kuona midomo ya bunduki nne ilikuwa ikimwangalia. Williams akaanza kutetemeka, mpaka katika kipindi hicho alionekana kutokuwa na ujanja wowote ule.

    “Huu ndio mwisho wa kila kitu. Huu ndio mwisho wa kutukimbia” Adrian alimwambia Williams na kisha kumchukua huku akiwa chini ya ulinzi wao.

    Kwa haraka haraka mawasiliano yakaanza kufanyika nchini Marekani kwamba Williams, mtu ambaye alikuwa akitafutwa alikuwa amepatikana nchini Thailand. Simu ile ikaonekana kuwa ya furaha katika jengo zima la upelelezi la FBI, watu wakshindwa kujizuia kabisa, kutokana na furaha kubwa ambazo walikuwa nazo, wakajikuta wakianza kuwaambia waandishi wa habari ambao wakaanza kuja katika jengo hilo.

    “Huwezi kucheza na Marekani. Hili taifa kubwa. Hata ukijiua na kujizika, tutakukamata tu endapo tukiamua kukutafuta” Watu mbalimbali walisikika wakitamba kwa waandishi wa habari bila kujua kwamba kazi ilikuwa kubwa sana mbele yao. Kufanikiwa kumkamata Williams sio kufanikiwa kumpeleka nchini marekani salama.







    Fujo zilikuwa zimekaribia kufanyika nchi nzima ya Thailand kutokana na serikali kuamua kuwauza baadhi ya tembo mia tatu katika nchi ya Marekani. Japokuwa katika kipindi hicho bado tembo hao hawakuwa wameuzwa lakini wananchi walionekana kuwa na hasira sana, kamwe hawakutaka tembo wao wauzwe katika nchi yoyote ile.

    Tembo ndio ambao walikuwa wanyama waliokuwa wakitumika sana katika nchi ya Thailand, idadi ya tembo katika nchi hiyo ilikuwa kubwa sana. Kila siku walikuwa wakijivunia tembo wao ambao walikuwa wakizidi kuongezeka zaidi na zaidi. Tembo ndio ambao walikuwa wakitumika sana nchini Thailand. Kama wakulima nchini Tanzania walikuwa wakitumia kile kilimo cha kutumia ng’ombe kusukuma mashine, basi kwa Thailand walikuwa wakitumia tembo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Idadi ya tembo nchi ya Thailand ilikuwa kubwa sana, kila mtu alikuwa kwenye mapenzi mazito na tembo, tembo walikuwa wakipendwa sana kuliko wanyama wengine. Kitendo cha serikali kuamua kutaka kuuza tembo mia tatu kuelekea nchini Marekani kilionekana kuwakasirisha Wathailand kupita kawaida, hapo ndipo maandamano yalipokuwa yakianza kufanyika katika sehemu mbalimbali hasa Bangkok.

    Maandamano yalikuwa yakifanyika kila siku jijini Bangkok. Watu walikuwa wakibeba mabango na kisha kuingia mitaani. Kipindi cha nyuma waandamanaji walikuwa wachache sana, ila kadri siku zilivyozidi kuongezeka na ndivyo ambavyo waandamanaji hao walivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi mpaka kufikia watu elfu tatu ambao walikuwa wakitembea barabarani kuelekea katika ofisi za serikali.

    Waandamaji hao hawakuwa mikono mitupu, walikuwa na mabango mbalimbali ambayo yalikuwa yakieleza hasira zao ambazo zilikuwa mioyoni mwao. Si wanaume, wanawake, watoto kwa wakubwa, wote walikuwa mitaani wakiandamana tu. Jambo hilo likaonekana kuanza kuchochea mapigano, wananchi wakaonekana kuanza kuuchukia uongozi wa rais huyo, Bwana Zukeng.

    Asubuhi watu walikuwa wakielekea kazini au katika mihangaiko yao kama kawaida ila walipokuwa wakirudi nyumbani na kupumzika, jioni wakawa wakijikusanya na kisha kuanza kuelekea katika maandamano. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya tatu tangu maandamano hayo yaanze nchini Thailand. Mapolisi walipoona kwamba maandamano hayakuwa ya amani, wakaanza kutapakaa mitaani huku wakiwa na mapolisi maalumu wa kuzuia fujo.

    Hali tayari ikaonekana kuanza kuchafuka, amani ambayo ilikuwa imetawala kwa kipindi kirefu ikaonekana kuanza kuondoka mioyoni mwa Wathailand, kisa kikubwa, kilikuwa tembo. Watu walionekana kuwa tayari kupigwa na kujeruiwa vibaya, watu walijiona kuwa tayari kuuawa lakini mwisho wa siku wapate kile ambacho walikuwa wamekikusudia kukipata, tembo waachwe nchini Thailand kwa manufaa ya wananchi tu.

    Katika siku hizo mbili zilizopita, polisi wa kuzuia fujo walijitahidi sana kutuliza ghasia lakini hali haikuonekana kubadilika, hapo ndipo ambapo wakaamua kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji yaliyokuwa yakiwasha kama upupu. Waandamaji hawakuonekana kukoma, kila walipoona kwamba polisi walikuwa wakitumia mabomu ya machozi, kila mmoja alikuwa na chupa ya maji mkononi huku kila walipoona kwamba siku hiyo yangekuwa yakitumika maji ya kuwasha, walikuwa wakivaa majaketi mazito ya mvua.

    Thailand ikaonekana kubadilika kwa wakati huo, kwa asubuhi na mchana amani ilikuwa kubwa ila ilipokuwa ikifika alasili, maandamano yalikuwa yakianza mitaani. Hofu ikawa imewakumba watu, wanasiasa wengi pamoja na watu wenye elimu kubwa na ya juu wakamtaka rais kusitisha mpango wake wa kutaka kuuza tembo katika nchi ya Marekani, alishauriwa kuacha kila kitu kama kilivyokuwa kwa wakati huo.

    “Ni bora tufe lakini tembo wasiende sehemu yoyote ile” Mwananchi mmoja alisikika.

    “Hawa dawa yao mpaka hao Waingereza wao tuwaue” Mwananchi mwingine alisikika akisema.

    Kila mtu kwa wakati huo alikuwa akiongea lake, hasira kali ambazo walikuwa nazo katika kipindi hicho ziliwapelekea mpaka kuwachukia Wamarekani ambao kazi yao ilikuwa ni kumshawishi rais wa nchi hiyo, Bwana Zukeng kufanya biashara hiyo ya tembo mia tatu kwa ajili ya kuiingizia nchi kiasi kikubwa cha fedha.

    Maandamano bado yalikuwa yakiendelea zaidi na zaidi, katika kipindi hiki, zaidi ya waandamanaji elfu tatu walikuwa wakielekea mahali ambapo kulikuwa na ubalozi wa Marekani. Njiani, waandamaji walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuwapa nguvu katika kila kitu ambacho walikuwa wakienda kukifanya.

    Polisi wa kuzia ghasia walizidi kuongezeka kwa ajili ya kuwazuia waandamanaji hao ambao mpaka katika kipindi hicho walionekana kuchoka na mambio ambayo yalikuwa yakiendelea katika serikali ya nchi hiyo. Magari manne yaliyokuwa na maji ya kuwahsa yakawa yamejikusanya sehemu moja, polisi wa kuzuia ghasia ambao walikuwa na bunduki za mabomu ya machozi nao walikuwa wamejiweka tayari kwa ajili ya kuzuia ghasia hizo.

    Waandamaji hao hawakuwa na silaha yoyote ile mikononi mwao, walichokuwa nacho ni makopo ya maji pamoja na milli yao kuvaa makoti mazito ya mvua, walionekana kujiandaa kwa kila kitu ambacho kingeendelea mahali hapo. Tangazo likaanza kutolewa kwamba wananchi walitakiwa kuacha kuandamana kwa sababi maandamano yao hayakuwa na kibali chochote kile, walitakiwa kurudi nyumbani kwao lakini hakukuwa na mtu ambaye alielewa japokuwa walikuwa wakilisikia vizuri tangazo ambalo lilikuwa likitolewa kwa vitisho vikubwa.

    “Moja...rudini nyumbani kwenu” Mkuu wa polisi wale wa kuzuia ghasia alitangaza lakini hakukuwa na mtu aliyerudi nyuma.

    “Mbili natangaza, rudini nyumbani. Kama mmekataa, sasa tunawafuata” Mkuu wa polisi wale alisema na hapo hapo kupiga bomu la machozi, kilichotokea ni watu kuanza kukimbia ovyo huku wakipiga kelele na polisi kuanza kuwafuata na kuanza kuwakamata wengine.

    ****

    Adrian pamoja na wapelelezi wenzake walikuwa wakiendelea na safari yao kama kawaida huku wakiwa na Williams ambaye alikuwa akitafutwa sana kwa wakati huo. Hawakuwa na pingi yoyote katika kipindi hicho, japokuwa mawazo yao yalijua fika kwamba Williams alikuwa mtu hatari sana, hivyo walimwacha awe hatua mbili mbel huku wao wakiwa nyumba na bunduki ambazo walikuwa wamemuelekezea.

    Alichokifanya Adrian kwa wakati huo ni kuchukua simu yake na kisha kupiga makao makuu nchini Marekani na kuwaambia ushindi mkubwa ambao walikuwa wameupata. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuamini kile ambacho kilikuwa kikisikika kutoka kwa Adrian, kitendo cha kumkamata Williams kilionekana kuwa kitendo kimoja kikubwa na cha historia kwa muuaji wa watu wengi kukamatwa kwa kipindi kichache sana, hapo ndipo walipojigundua kwamba Taifa lao lilikuwa kubwa sana ambalo hakukuwa na mtu ambaye alitakiwa kucheza nalo.

    Katika kipindi hicho, wapelelezi hawakuhitaji msaada wa mtu yeyote yule, hawakuwaamini polisi wa nchi hiyo wala wananchi kwa kuona kwamba ingewezekana hata mpango wa Williams kuiteka ndege ile ulikuwa umehusisha baadhi ya mapolisi, hivyo walitaka kufanya kila kitu peke yao. Waliendelea zaidi na zaidi na safari yao, kwa wakati huo walikuwa wakitaka kuelekea katika ubalozi wa nchi yao, Marekani na kisha kuanza mipango ya kumsafirisha mtu huyo hadi nchini Marekani.

    Kila mmoja alionekana kuwa na furaha, wakajiona kuwa washindi hata zaidi ya washindi, kwa wananchi ambao walikuwa wakipishana nao njiani, walionekana kushtuka mara baada ya kumuona Williams akiwa amewekwa chini ya ulinzi. Ingawa wapeleezi walijua fika kwamba kumsafirisha kwa miguu Williams lilikuwa kosa kubwa lakini hawakutaka kuchukua usafiri wowote ule kutokana na mafunzo ambayo walipewa kwamba mpelelezi kama mpelelezi hakutakiwa kumuamini mtu yeyote yule.

    :”Tungekazana kidogo ili tuwahi kufika na huyu mpumbavu kufikishwa haraka” Brian aliwaambia.

    “Twendeni hivi hivi, hatujui huyu mtu ni hatari kiasi gani” Adrian alisema huku akiangalia huku na huko huku akionekana kuwa na machale.

    “Na kwa nini tusipige simu ili magari ya ubalozini yaje kutuchukua?” Thomas alishauri.

    “Kutoka hapa na ubalozini si mbali sana. Twendeni kwa miguu tu” Adrian alisema huku bado akiwa hayatulizi macho yake, yalikuwa kodokodo yakiangalia katika kila upande.

    Waliendelea kwenda mbele mpaka pale ambapo walikata kona na kuishika njia ya kwenda katika ubalozi wa Marekani. Hatua hamsini mbele yao wakakutana na umati mkubwa wa watu wasiopungua elfu mbili ambao walikuwa katika maandamano na ambao walionekana kuanza kuelekea katika ubalozi wa Marekani.

    “Mmmh! Tupiteni njia nyingine” Brian alishauri.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna njia nyingine zaidi ya hii. Hatutakiwi kuwa na wasiwasi, tunapita hapa hapa” Adrian aliwaambia.

    Akili ya Williams kwa wakati huo ilikuwa ikifikiria mambo mengi, idadi ya watu wengi waliokuwa katika maandamano ambao walikuwa mbele yao huku wakiwa wamewapa mgongo ilionekana kumfurahisha kupita kawaida, akili yake ikafikiria kuhusu kuwatoroka tu.

    Huku kila mmoja akiwa anasonga mbele, mara mlio kama wa risasi ukasikika, watu wakaanza kupiga kelele na kuanza kurudi walipotoka huku wakiyatupa mabango yale. Moshi ukaanza kuonekana huku macho yakianza kuwasha. Kutokana na waandamanaji wale kuanza kukimbia kwa kasi, wakajikuta wakiwakumba Williams na Adrina pamoja na wapelelezi wengine na kuanguka chini.

    Bunduki ambazo walikuwa wamezishika kisiri, zikaanguka chini. Waandamaji ambao walikuwa wakikimbia hawakuonekana kujali, wengine wakaanza kuwakanyaga, kila mtu alikuwa akikimbia ovyo kwa wakati huo. Moshi wa mabomu kadhaa ya machozi ulivyokuwa mkubwa, eneo zima likatawaliwa na moshi, macho ya wapelelezi yakaanza kuwasha, tena yaliwasha kupita kawaida.

    Mpaka sekunde thelathini zinatimia huku watu wakiwa wameanza kusambaa mahali hapo na wengine kukamatwa na polisi, Williams hakuwa akionekana mbele yao, nae alikuwa amekimbia na wale waandamanaji ambao walikuwa wakikimbia ovyo. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuamini kile ambacho alikuwa amekiona, kutokuonekana kwa Williams eneo hilo kulionekana kuwachanganya kupita kawaida.

    “Yupo wapi?”

    “Mungu wangu! Ametukimbia” Adrian alisema huku akiyafikicha macho yake ambayo yalikuwa yakiwasha kutokana na moshio wa mambo ya machozi.







    Williams alibaki akiwa ameduwaa katika kipindi ambacho waandamaji walikuwa wakija kwa kasi kule ambapo alipokuwepo pamoja na wapelelezi wale. Kila mtu akaanza kuhofia, kazi ambayo walikuwa wakija nao waandamaji zaidi ya elfu tatu ilionekana kuwatogopesha kupita kawaida. Tayari mabomu ya machozi yalikuwa yamekwishaanza kupigwa na hivyo moshi kuanza kutawala hewani.

    Waandamaji wale walikuwa wakikimbia kule walipokuwa kwa kasi ya ajabu kiasi ambacho hata kabla hawajajua ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya, waandamaji wale walikuwa wamekwishawafikia na kuwakumba kitendo ambacho kiliwafanya wote kuanguka chini. Williams alionekana kuwa makini kwa wakati huo, alipoona ameanguka chini, akajitahidi kujiinua japokuwa alikuwa akikumbwa na watu hao mara kwa mara. Alipoweza kusimama imara, akaanza kukimbia pamoja nao.

    Muda wote Williams alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kuweza kuwatoroka wapelelezi wale kilionekana kuwa kitendo kikubwa na kilichompa furaha kubwa kwa kuona kwamba huo haukuwa muda wake sahihi wa kukamatwa na kurudishwa nchini marekani. Williams alikuwa akizidi kukimbia, hakujua ni sehemu gani ambapo alikuwa akielekea katika kipindi hicho, alichokuwa akikijua yeye ni kuwatoroka wapelelezi wale ambao walionekana kuwa na haja nae.

    Williams alikimbia pamoja na wale watu mpaka kufika Chunk Chunk, sehemu ambayo ilikuwa na bahari pamoja na bandari kubwa ya nchi hiyo. Williams akaenda pembeni ya ukuta mmoja wa nyumba kubwa na kisha kujificha. Watu wale walipokuwa wamepita na kumalizika, akatoka katika ule ukuta na kisha kuanza kulifuata geti la bandari ile.

    Kwa macho yake aliweza kuwaona watu ambao walikuwa wakiingia ndani ya bandari ile wakionyesha vitambulisho pale getini na kuruhusiwa kuingia. Kwa kitendo kile, kwa Williams ilionekana kuwa ngumu kufanikiwa kupita katika geti lilekwa hali ya usalama. Alichokifanya ni kuondoka mahali hapo na kuelekea baharini. Kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kupata meli ya kumpeleka katika nchi ya mama yake, Ghana na kisha huko kuanza maisha kivyake vyake.

    Ufukweni pale akaanza kuangalia angalia huku na kule. Hakukuwa na watu wengi sana, kulikuwa na vijana kama saba hivi ambao walikuwa wakiogelea na wengine kuwa mchangani huku wakiendelea kuyafurahia maisha kama kawaida. Alichokifanya Williams ni kuanza kupiga hatua kuwafuata vijana watatu ambao walikuwa wamekaa mchangani na kisha kuanza kuongea nao huku wakionekana kuifahamu lugha yake.

    “Nataka kuondoka hapa kuelekea Afrika” Williams aliwaambia vijana wale ambao walionekana kushtuka.

    “Maisha ya hapa magumu nini ndio maana unataka kurudi nyumbani?” Kijana mmoja alimuuliza Williams.

    “Ndio. Nimepakumbuka nyumbani” Williams aliwaambia vijana wale.

    “Kwa nini usiungane pamoja nasi kuelekea Ulaya au hata Marekani? Tunazamia kwenye meli halafu tukija kutoka, tupo Ulaya au Marekani, maisha yanaendelea” kijana mmoja alimwambia Williams.

    “Sipendi kwenda Ulaya au Marekani. Ninataka kwenda nyumbani” Williams aliwaambia.

    “Unatokea Afrika nchi gani?”

    “Ghana”

    “Meli za kwenda Afrika wala sio ngumu kupatikana. Kwanza wala hauzamii. Toka lini mtu akazamia kwenda Afrika? Kama unataka nikufanyie mipango, uingie kwenye meli kama mfanyakazi uweze kurudi kwenu” Kijana mmoja alimwambia Williams huku wote wakionekana kutokumjua kutokana na kutopenda kuangalia mcheza wa kikapu wa nchini Marekani.

    “Itakuwa vizuri sana. Naomba unisaidie”

    “Una kiasi gani?”

    “Msaada mpaka fedha?”

    “Yeah! Maisha magumu sana hapa Bangkok, bila fedha, maisha hayaendi” Kijana yule alimwambia Williams.

    “Naomba mnisaidie. Nimepoteza kila kitu. Sina kitu chochote kile, natamani niende nyumbani nikaanza maisha upya, nikijipanga niane safari ya kwenda Ulaya” Williams aliwaambia.

    Vijana wale wakabaki kimya, wakaanza kumwangalia Williams kwa makini, kwao walionekana kumshangaa kupita kawaida. Hawakuwahi kukutana na mtu kama yeye, mtu ambaye alikuwa ameishi nchini Thailand na mwisho wa siku kutaka kurudi nyumbani kwao kwa kuona kwamba maisha yalikuwa yamemshinda nchini Thailand.

    “Tumsaidieni tu” Kijana mwingine aliingilia.

    “Tutamsaidia vipi?”

    “Ngoja niongee na Tong. Alikuwa akitafuta vijana wa kufanya kazi katika meli yake ambayo ilikuwa inaelekea Nigeria kesho” Kijana huyo alimwambia wenzake.

    “Sawa. Jaribu kuwaisliana nae. Naona bahati imemuangukia”

    Moja kwa moja mawasiliano kati ya kijana huyo na Tong yakaanza kufanyika mara moja. Mpaka kijana yule alipokata simu, Tong alikuwa akihitaji kukutana na kijana huyo ambaye alikuwa akitaka kufanya kazi katika meli yake. Alichokifanya kijana yule ambaye alijitambulisha kwa jina la Wong ni kumchukua Williams na kisha kuanza kuelekea katika sehemu ambayo meli hiyo ilipokuwa imepaki.

    “Mbona haujiamini. Unaonekana kuangalia kila upande huku ukiwa na wasiwasi?” Wong alimuuliza Williams.

    “Hapana. Unajua sisi wengine tumekuja huku bila pasipoti wala viza. Najaribu kuangalia kama polisi wanaweza kuwa karibu” Williams alidanganya.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari kutoka hapo mpaka katika meli ile wala haikuchukua muda mrefu, wakafika katika sehemu hiyo na kisha Wong kuanza kumtafuta Tong na kuonana. Tong akaanza kumwangalia Williams, kwake alionekana kuwa kijana mkakamavu sana ambaye alikuwa nguvu za kubeba mizigo ndani ya meli ile pamoja na kufanya kazi nyingine za ndani ya meli ile ya mizigo.

    “Huwa tunalipa kwa dola elfu moja. Upo tayari?” Tong alimuuliza Williams.

    “Nipo tayari” Williams alijibu.

    Tong akaonekana kutokuamini kama mtu ambaye alikuwa ameletwa mbele yake alikuwa amekubali kulipwa dola elfu moja tu kwani malipo yale yalikuwa ni ya chini sana. Alichokifanya Tong ni kuondoka mahali hapo huku akionekana kuwa na furaha, safari yake iliishia kwa mkuu wa meli ile ambaye alikuwa amemwambia kwamba alipata kijana ambaye alijitolea kufanya kazi katika meli ile kwa malipo ya dola elfu tatu, huku dola elfu mbili akichukua yeye.

    “Hebu kamuite” Mkuu wa meli ile, kapteni Cheng alimwambia Tong.

    Huku nyuma, Wong alikuwa akimwangalia Williams kwa macho ya mshangao, hakuamini kama kweli alikuwa amekubali malipo yale madogo kwa kazi kubwa ambazo angezifanya ndani ya meli ile. Alichokifanya ni kumvuta Williams pembeni na kisha kuanza kuongea nae huku akionyesha mshangao wake usoni.

    “Mbona umehitaji kiasi kidogo sana” Wong alimuuliza Williams.

    “Si ninakwenda nyumbani na sitorudi”

    “Hata kama. Malipo ya humu ndani huwa ni dola elfu tatu. Sasa unasema vipi ulipwe dola elfu moja?” Wong aliuliza huku akionekana kushangaa.

    “Ni kwa sababu nakwenda nyumbani” Williams alijibu.

    “Sawa. Ila kumbuka kwamba meli hii inaishia Nigeria. Ukifika Nigeria, shuka na uendelee na safari yako. Sikutaka kumwambia kwamba unakwenda kwenu, yeye anakuchukulia kama mfanyakazi” Wong alimwambia Williams.

    “Nashukuru sana” Williams alimwambia Wong.

    “Usijali. Ila na mimi kuna kitu nataka unisaidie kama nilivyokusaidia” Wong alimwambia Williams.

    “Kitu gani?”

    “Ukifika Nigeria, naomba unifanyie mipango ili na mimi nije huko” Wong alimwambia Williams.

    “Sawa. Ila nitawasiliana nawe vipi?” Williams alimuuliza.

    Hapo hapo bila kuchelewa, Wong akatoa karatasi na kuchukua kalamu na kisha kuanza kuandika namba zake tatu za simu. Aliandika kwa makini sana na wala hakutaka kukosea namba hata moja. Mara baada ya kumaliza kuandika, akampa Williams karatasi ile.

    “Sasa mbona na wewe unataka kuja Afrika?”

    “Kwa sababu watu wa huko huwa mnazamia kirahisi sana Ulaya na Marekani. Naamini kama nikipata watu wa huko, nami nitakwenda kirahisi Ulaya au Marekani” Wong alimwambia Williams.

    “Kwa hiyo lengo lako ni kwenda Ulaya au Marekani?” Williams alimuuliza.

    “Yeah! Nikifika huko, nitajua nitapigana vipi na maisha. Yaani lengo ni kufika Ulaya tu”

    “Sawa. Nitahakikisha nakusaidia”

    “Nitashukuru sana. Kumbuka wema ambao nimekufanyia. Usisahau kitu chochote uko uendako. Nakutegemea mshikaji wangu” Wong alimwambia Williams huku akimpa tano.

    “Poa” Williams aliitikia na hapo hapo Tong kurudi na kisha kumchukua Williams kwa ajili ya kwenda kumtambulisha kwa Bwana Cheng.

    Moja kwa moja wote wawili wakaanza kwenda katika ofisi ya Bwana Cheng kwa ajili ya utambulishoo wa Williams kama mfanyakazi mpya ndani ya meli ile. Kutokana na kuwa na kazi nyingi ndani ya meli ile, Bwana Cheng akawa amekwishaondoka ndani ya ofisi yake na kwenda katika sehemu nyingine kuangalia jinsi kazi zilivyokuwa zikifanyika, Tong hakuonekana kujali, alichokifanya ni kuanza kumuonyesha Williams mazingira ya meli ile na kisha kazi kuanza huku akiwa amepewa chumba kimoja kama wafanyakazi wengine.

    Muda mwingi Williams alikuwa akiwafikiria marafiki zake ambao aliwaacha wakiwa wamekwenda benki, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea mara baada ya kurudi kutoka benki. Alijiona kufanya makosa sana kutorudi na kuangalia kama walikuwa wamerudi au la, ila kwa wakati mwingine alikuwa akijiona kuchukua uamuzi sahihi kwa kuona kwamba kama angerudi, angeweza kukamatwa tena na wapelelezi wale ambao walikuwa wakimtafuta sana.

    Maisha ya ndani ya meli ile yakawa yameanza huku Williams pamoja na wafanyakazi wengine wakiwa wanapandisha mizigo kadhaa ndani ya meli ile, Kazi haikuwa rahisi hata mara moja, walikuwa wakibeba mizigo mingi mikubwa na mizito kuipakiza ndani ya meli ile. Ubebaji wa mizigo ulichukua zaidi ya masaa manne na ndipo mizigo yote ilipokamilika.

    Wafanyakazi wote wakatakiwa kuelekea katika vyumba vyao ambapo huko walitakiwa kupumzika kabla ya meli kung’oa nanga siku ijayo. Ilipofika usiku, muda wote Williams alikuwa akifikiria kuhusiana na marafiki zake, hakujua mahali ambapo walipokuwa, hakujua kama walikuwa wamefanikiwa kufungua akaunti hiyo au la. Safari ya kuelekea nchini Ghana wala haikuwa na raha kabisa, mawazo yalikuwa yamemjaa.

    Siku iliyofuata saa kumi na mbili alfajiri, meli ikatoa nanga na kuanza safari ya kuelekea katika nchi za Afrika ikiwepo Nigeria. Muda mwingi Williams alikuwa ndani ya chumba kile huku akionekana kutokuwa na furaha kabisa. Katika muda ambao mizigo ilikuwa ikihitajika kupangwa vizuri, Williams alikuwa akifuatwa na kuchukuliwa katika kupanga mizgo hiyo pamoja na wafanyakzi wasiopungua hamsini ndani ya meli ile.

    “Ukitokea ukafanikiwa kuupata huu utajiri, utakula maisha yako yote na hata wajuu zako nao watakuja kula fedha zako” Bwana Cheng aliwaambia makapteni wenzake huku akiwa ameishika picha ya Williams ambaye alikuwa akitafutwa huku kitita cha dola milioni mbili kikiwa kimetajwa.

    “Utajiri gani?”

    “Wa kumkamata mtu huyu. Ila sisi hatuwezi, si unajua tupo melini masaa ishirini na nne” Bwana Cheng aliwaambia huku akiwaonyesha picha ya Williams.

    Makapteni wale wakaanza kuiangalia ile picha bila kujali. Maongezi bado yalikuwa yakiendelea kama kawaida mpaka pale ambapo Tong alipoingia ndani ya chumba kile na kuitwa na bwana Cheng ambaye alikuwa amekaa pembeni kabisa ya chumba kile, kwenye kochi.

    “Mbona haukumleta mfanyakazi mpya nimuone?” Bwana Cheng alimuuliza Tong.

    “Nilimleta ila haukuwepo”

    “Sawa. Umemwandikisha jina lake?”

    “Ndio”

    “Anaitwa nani”

    “Antony Bumura”

    “Sawa. Ni muafrika?”

    “Ndio”

    “Safi sana. Hao watu ndio tunaotaka kufanya nao kazi. Huwa wanajituma sana. Chukua hii picha kaniwekee chumbani kwangu kisha uniletee maji” Bwana Cheng alimwambia Tong ambaye akaichukua ile picha, akaanza kuiangalia hata kabla hajaondoka mahali pale.

    Tong akaonekana kushtuka, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona mahali katika karatasi ile. Mshtuko ule ndio ukamfanya bwana Cheng kumwangalia Tong huku akionekana kumshangaa. Alichokifanya Bwana Cheng ni kuichukua ile picha.

    “Vipi tena? Mbona umeshtuka” Bwan cheng aliuliza.

    “Huyo mtu”

    “Amefanya nini?”

    “Ndiye aliyekuja kuomba kazi. Na ndiye mfanyakazi mpya niliyekwambia” Tong alimwambia Bwana Cheng ambaye alionekana kushtuka.

    Alichokifanya Bwana Cheng ni kuangalia kama manahodha wengine kama walikuwa wamesikia alivyoongea Tong, alipoona kwamba hawakuwa wamesikia, akamvuta Tong pembeni kabisa na kisha kuanza kuongea nae.

    “Umesemaje?”

    “Huyu mtu yupo ndani ya meli hii. Amejitambulisha kama Antony”

    “Una uhakika na unachokisema?”

    “Nina uhakika. Yupo chumbani”

    “Kweli?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Asilimia mia tatu”

    “Hebu twende” Bwana Cvheng alimwambia Tong na kisha kuanza kuelekea huko alipokuwa Williams ambaye alijitambulisha kama Anton Bumura.

    Hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika katika mlango wa chumba kile na kisha kuanza kugonga. Mlango uligongwa kwa sekunde kadhaa na kisha Williams kuufungua mlango. Bwana Cheng hakuonekana kuamini kama kweli mtu ambaye alikuwa akitafutwa na serikali ya Marekani alikuwa ndani ya meli yake katika kipindi hicho. Uso wake ukajawa na tabasamu pana, utajiri ambao alikuwa akiuzungumzia, tayari ukaonekana kumjia mikononi bila kuuangaikia.

    “Williams Kurt, mcheza mpira wa kikapu” Bwana Cheng alisema huku akicheka kwa furaha. Tayari alijiona kuwa tajiri.









    Viongozi mbalimbali wa shirika la kipelelezi la F.B.I bado walikuwa wakiendelea kutamba muda wote. Walijiona kufanikisha kile ambacho walikuwa wamekisumbukia kwa muda mrefu, kwa wakati huo, walikuwa wakisubiri Williams asafirishwe na kupelekwa Marekani tu. Waandishi wa habari wakaanza kutangaza kuhusiana na kukamatwa kwa Williams, waliona kila kitu kuwa sawa katika kipindi hicho.

    Wamarekani wakajiona wao ndio wao, hawakutaka hata siku moja Serikali yao ichezewe na watu ovyo na ndio maana kama ulikuwa umefanya jambo fulani na kuahidi kukutafuta, ni lazima wangekupata hata kama ulikuwa umejificha sehemu gani. Watu wakaona kwamba shirika la kipelelezi la F.B.I lilikuwa noma kwani hazikuwa zimepita siku nyingi tangu mauaji yatokee, tayari Williams alikuwa amekamatwa na hivyo alikuwa akitakiwa kusafirishwa na kupelekwa nchini Marekani.

    Bwana Swan alikuwa kwenye lindi la mawazo, katika kipindi hicho hakuwa akielewa ni kitu gani hasa ambacho kilikuwa kinaendelea, alijua fika kwamba alimwamini sana mpelelezi Sam lakini maneno ambayo alikuwa ameongea nae siku hiyo yalionekana kumchanganya kupita kawaida. Moyo wake ulikuwa umekwishapata uhakika kwamba Bwana Robinson ndiye alikuwa nyuma ya mipango yote, lakini kabla hajafanya kitu chochote kile ilikuwa ni lazima upatikane ushahidi, na ushahidi wenyewe ulikuwa ni Williams na Phillip tu, hakukuwa na mwingine.

    Katika kipindi hicho ambacho alitaarifiwa kwamba Williams alikuwa amekamatwa na hivyo wapelelezi walikuwa wakielekea ubalozi wa Marekani nchini thailand kwa ajili ya kumsafirisha, alionekana kufurahi sana kwani alikuwa na uhakika kwamba kwa wakati huo ushahidi wa kumuingiza Bwana Robinson matatni ulikuwa umekamilika, hivyo alitakiwa kupanga kila kitu ili hata Williams atakapofika, kusiwe na tatizo lolote lile.

    “Ametukimbia” Ilisikika sauti ya mpelelezi Adrian ambayo ilisikika kutoka simuni.

    “Unasemaje?” bwana Swan aliuliza huku akionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amekisikia.

    “Ametukimbia kwa kujumuika pamoja na watu ambao walikuwa kwenye maandamano kuelekea katika ubalozi wa marekani” Adrian alimwambia bwana Swan ambaye alionekana kuchanganyikiwa.

    “Kwa hiyo hampo nae?”

    “Ndio mkuu. Labda tuendelee kumtafuta” Adrian alimwambia Bwana Swan ambaye alichanganyikiwa zaidi.

    Bwana Swan hakutaka kuongea na simu zaidi, alichokifanya ni kukata simu hiyo. Bwana Swan akaonekana kuchanganyikiwa, maneno ambayo alikuwa ameambiwa yalionekana kutokueleweka kichwani mwake. Ilikuwaje Williams akamatwe na baada ya muda fulani awatoroke Wapelelezi kirahisi sana bila hata kutumia nguvu. Sababu ya kuchanganyikana na watu waliokuwa kwenye maandamano ilionekana kutokutosha kabisa kumshawishi mpaka kukubaliana nao.

    Hapo hapo bwana Swan akawaita wafanyakazi wenzake na kisha kuwaambia kile ambacho kilikuwa kimetokea nchini Thailand. Kila mtu akaonekana kushtuka, hawakuamini kama Williams alikuwa amewatoroka kirahisi namna ile. Kwa haraka haraka mawasiliano yakafanyika mpaka kwa waandishi wa habari na kuwaleleza kwamba Williams alikuwa amewatoroka wapelelezi, hivyo wananchi walitakiwa kutangaziwa huku wakitakiwa kufuta uhakika wa Williams kuletwa ndani ya nchi hiyo huku akiwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahakamani.

    Taarifa hiyo ikaonekana kuwa kama mwiba kwa wananchi, hawakuamini kama Williams alikuwa na ujanja wa kuweza kuwatoroka wapelelezi kirahisi namna ile na wakati wala hakuwa jasusi au kupokea mafunzo yoyote yale ya kijasusi. Japokuwahakukuwa na mtu ambaye aliamini hilo lakini kikafikia kipindi ambacho kila mmoja alitakiwa kuamini kwamba mtu ambaye alikuwa akihitajika sana nchini Marekani na kupelekwa mahakamani, Williams alikuwa amewatorola wapelelezi.

    “Kama mchezo wa kitoto vile” mwananchi mmoja aliyeoinekana kuwa na hasira alimwambia mwenzake.

    “Huu ni mchezo wa kitoto. Kwanza toka lini mnamkamata mtu halafu mnatembea nae kwa miguu. Huu ni uzembe, na hii ni kwa sababu hawa wapelelezi hawana ndugu ambaye aliuawa kule porini” Jamaa mwingine alimwambia.

    “Huu utakuwa ni mchezo uliopangwa”

    “Inawezekana vipi kupangwa na wakati majaa ni wapelelezi?”

    “Huwezi jua. Katika dunia ya sasa hivi, hata wazazi wako hautakiwi kuwaamini, muda wowote ule wanakugeukia”

    Kila mtu kwa wakati huo alikuwa akiongea lake, kwa wale ambao walitaka kuwalaumu wapelelezi, walitoa lawama zao. Wapelelezi wakaonekana kuzembea katika kuifanya kazi yao ambayo walikuwa wamepewa ya kumleta Williams katika nchi ya Marekani. Televisheni mbalimbali zikaanza kuzungumzia suala hilo ambalo lilionekana kuwa la ajabu ambalo halikuwahi kutokea katika shirika hilo la kipelelezi la F.B.I.

    ****

    Adrian na wenzake wakaonekana kuchanganyikiwa, mara baada ya kuona kwamba Williams alikuwa amewatoroka, hapo hapo wakaanza kuelekea kule ambapo walikuwa wamemkamata. Kila mmoja njiani alionekana kuchanganyikiwa, hawakuamini kama Williams alikuwa amewatoroka kirahisi namna ile. Kila mmoja alikuwa akiangalia huku na kule huku akionekana kuchanganyaikiwa, mpaka katika kipindi hicho, waliona wakikaribiwa na lawama kubwa kutoka kwa wananchi wa Marekani.

    Walikuwa wakitembea kwa haraka hara sana kupita kawaida huku wakijaribu kuangalia katika kila kona, kitu ambacho walikuwa wakikifahamu kwa wakati huo ni kwamba kulikuwa na uwezekano wa Williams kukimbilia kule ambapo walikuwa wamemkamata, sehemu ambayo alikuwa akionekana kumsubiria mtu fulani mahali hapo.

    Mara baada ya kufika katika eneo lile, wakaanza kuangalia huku na kule, hakukuonekana mtu yeyote jambo ambalo lilikuwa limewachanganya kupita kawaida. Huku kila mmoja akitaka kuondoka katika eneo hilo, kwa mbali wakawaona watu wawili wakiwa wanaongea, walikuwa na uhakika kwamba yule alikuwa Williams au Phillip. Hawakutaka kuzembea, walichokifanya ni kuanza kuwafuata kwa kasi huku wakiwa wameshika bunduki zao mikononi.

    “Mko chini ya ulinzi” Sauti ya Adrian ilisikika.

    Wapelelezi wakawafuata watu wale, alikuwa Phillip na Gong ambao walikuwa mahali hapo wakijadili ni kitu gani ambacho kilitakiwa kufanyika kwa wakati huo. Kila mpelelezi akaonekana kufurahi, kitendo cha kumpata Phillip katika kipindi hicho kidogo ikaonekana kwamba walikuwa wamefanikiwa kwa asilimia chache kwani waliamini kwa kupitioa Phillip, wangeweza kujua mahali alipokuwa Williams.

    Walichokifanya kwa wakati huo, wakamchukua Phillip pamoja na Gong na kisha kuondoka nao. Walichokitaka kwa wakati huo ni kufika ubalozini ambapo wangewaweka chini na kisha kuwauliza kuhusiana na sehemu alipokuwa Williams kwa kipindi hicho. Kwa sasa walikuwa makini, hawakutaka kumpoteza Phillip kama ambavyo walimpoteza Williams katika kipindi kichache kilichopita, walikuwa nae bega kwa bega mpaka wanaingia ubalozi wa marekani.

    “Williams yupo wapi?” Lilikuwa swali la kwanza lililotoka kwa mpelelezi Adrian.

    “Sijui” Phillip alijibu huku akionekana kweli hajui.

    “Mmehusika wote kwenye mauaji?”

    “Mauaji gani?”

    “Ya wachezaji wa mpira wa kikapu”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana. Nitalizungumzia hilo nikifika nchini Marekani” Phillip alimwambia.

    Alichokifanya Adrian ni kupiga simu mpaka nchini Marekani na kisha kuwaambia kwamba walikuwa wamefanikiwa kumpata Phillip. Hiyo ikaonekana kuwa habari bora kwa Bwana Swan kwani alijua kwa namna moja au nyingine, Phillip alikuwa akifahamu kila kitu ambacho kilitokea porini kutokana na yeye kuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wametekwa nyara.

    “Vizuri. Msafirisheni. Atakuwa anaujua ukweli” Bwana Swan alisema.

    “Sawa”

    ****

    Bwana Cheng alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida, muda wote alikuwa akimwangalia Williams kwa furaha kubwa kwa kuona kwamba alikuwa akikaribia kuupata utajiri ambao ulikuwa umeahidiwa na serikali ya marekani kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwa Williams. Katika kipindi hicho, alibaki akimwangalia Williams mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini kama kweli alikuwa amempata Williams ambaye alikuwa akitafutwa sana na Wamarekani.

    “Wewe ndio utajiri wangu kwa sasa. Ni lazima tukufikishe katika miko ya sheria. Umeushikilia utajiri wangu wa kutumia mimi, watoto wangu na hata wajukuu wangu” Bwana Cheng alimwambia Williams.

    “Itatubidi tuzungumze kwa muda kati yangu mimi na wewe” Williams alimwambia Bwana Cheng.

    “Kuongea na mimi?”

    “Ndio”

    “Wawili?”

    “Ndio”

    “Sawa. Ila si kusema kwamba nikuache. Ninachojua nimekwishakuwa tajiri kupitia wewe” Bwana Cheng alimwambia Williams.

    “Usijali. Naomba tuongee kwanza” Williams alimwambia Bwana Cheng na hivyo Tong kuambiwa kutoka nje huku akionywa kutokuzungumza chochote kama Williams alikuwa ndani ya meli hiyo.

    Bwana Cheng akakaa kitini na kuanza kumwangalia Williams huku uso wake ukiwa na tabasamu. Kadri alivyokuwa akimwangalia Williams na ndivyo ambavyo alivyokuwa akiuona utajiri mbele ya macho yake. Hakuamini kama Mungu alikuwa amemuwezesha kuupata utajiri kirahisi namna ile.

    “Unataka kuongea nini Bingo?” Bwana Cheng alimuuliza Williams huku hata jina akiwa amembadilisha.

    “Nataka tufanye dili”

    “Dili gani?”

    “Hivi unajua kama ukiwaambia mapolisi juu ya uwepo wangu humu ndani hata wewe unakwenda jela kama mimi?” Williams alimwambia Bwana Cheng.

    “Nakwenda jela? Kivipi?”

    Williams akasimama na kuanza kumwangalia Bwana Cheng, kwa sasa hivi hali ikaanza kubadilika, Williams akawa ndiye mtu wa kutabasamu huku Bwana Cheng akiwa mtu mwenye wasiwasi mwingi. Williams akafungua kabati la nguo lililokuwepo ndani ya chumba kile na kisha kulifunga tena, Bwana Cheng akashtuka zaidi.

    “Tupange dili. Nifikishe nchini Nigeria, niache niende zangu hapo ndipo nawe utasalimika. Upo tayari?” Williams alimuuliza bwana Cheng ambaye alionekana kubadilika na kuwa mpole.

    “Nipo tayari mkuu. Nitakufikisha na kukupa mahitaji yote utakayo” Bwana Cheng alimwambia Williams.

    “Safi sana. Kama ni hivyo, dili litafanyika” Williams alimwambia Bwana Cheng.

    “Sawa. Nitafanya kama dili lisemavyo”

    “Hakuna tatizo. Nasikia njaa. Naomba niletewe chakula kizuri” Williams alimwambia Bwana Cheng.

    “Usijali. Kinaletwa” Bwana Cheng alisema na kisha kutoka ndani ya chumba kile akiwa mpole kama kamwagiwa maji ya baridi tena katika kipindi cha baridi.









    Williams alikuwa ndani ya kile chumba akiwa ametulia, mwili wake ulikuwa umechoka kupita kawaida kutokana na kazi ya kubeba mizigo ambayo alikuwa ameifanya ndani ya meli ile. Njaa ilikuwa imemtawala kupita kawaida, muda wowote alikuwa akimsikiliza Tong afike ndani ya chumba kile na kisha kumueleza hali ambayo alikuwa nayo mahali hapo.

    Williams aliendelea kukaa ndani ya chumba kile huku akimsikilizia Tong lakini mtu huyo wala hakuweza kutokea katika kipindi hicho. Williams hakutulia, muda mwingi alikuwa akismama kutoka pale kitandani na kisha kuzungazunguka ndani ya chumba kile. Tumbo lake likaonekana kutokuwa na chakula chochote kile jambo ambao lilisababisha hata mwili kuuhisi ukianza kuishiwa nguvu.

    Williams hakutulia, akaanza kuangalia huku na kule ndani ya chumba kile huku akiona kama angeweza kupata chakula chochote ndani ya chumba kile lakini hakufanikiwa kupata chakula chochote kile. Williams akaendelea kutafuta jambo ambalo likamfanya kulifuata kabati lililokuwa ndani ya chumba kile na kisha kulifungua. Ndani ya kabati, nguo nyingi zilikuwa zimerundikwa sehemu moja jambo ambalo likamfanya kulifunga kabati lile.

    Williams akakaa kitandani na kisha kuanza kujifikiria ni kitu gani ambacho alitakiwa kufanya kwa wakati huo. Kitu ambacho kilimjia kichwani ni kwamba atoke ndani ya chumba kilena kisha kumtafuta Tong na kisha kumueleza hali ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho. Huku akiwa amekwishakubaliana na moyo wake kile ambacho alikuwa ameamua kukifanya mahali hapo, akaanza kujisikia uzito katika kulifanya jambo hilo.

    Mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda kasi kana kwamba kulikuwa na jambo la hatari ambalo lilikuwa likitaka kutokea mahali hapo. Williams akasimama na kisha kuanza kuzunguka tena ndani ya chumba kile. Katika kila kipindi ambacho alikuwa akiliangalia kabati lile, amani ikamtoka moyoni mwake, hakuwa akijisikia vizuri jambo ambalo akalifuata kabati lile na kisha kuanza kulifungua tena.

    Alichokifanya katika kipindi hiki ni kuanza kuzitoa zile nguo ambazo zilikuwa zimerundikwa ndani ya kabati lile. Alipozitoa nguo zile, macho yake yakatua katika mfuko mmoja mkubwa, mfuko ambao ndani ulionekana kuwa na kitu kama unga wa sembe, unga wa ngano au maziwa. Williams akatoa tabasamu, katika kipindi hicho, akili yake ikamwambia kwamba kitu kile ambacho alikuwa amekishika kilichokuwa ndani ya mfuko ule yalikuwa ni maziwa.

    Kwa haraka haraka akaanza kuufungua mfuko ule, alichokutana nacho, zilikuwa ni pakti za madawa ya kulevya ambayo yalikuwa yamefungwa katika mifuko midogo tofauti tofauti. Williams akahtuka sana, akagundua kwamba tofauti na kusafirisha mizigo kupeleka barani Afrika, pia meli hiyo ilikuwa ikisafirsha madawa ya kulevya, biashara ambayo ilikuwa haramu sana na iliyokuwa ikipigwa vita sana duniani.

    Williams akauhisi mwili wake ukisisimka kupita kiasi, ni kweli alikuwa akisikia mengi sana kuhusiana na madawa ya kulevya pamoja na kuyaona katika televisheni hasa alipokuwa akiangalia taarifa ya habari au hata muvi za mapigano lakini katika maisha yake hakuwahi kuyaona kwa macho yake hata siku moja. Hiyo ndio ilikuwa siku yake ya kwanza kuyaona madawa hayo ambayo kwa kuyaangalia tu, yalikuwa ykifanana sana na maziwa ya unga.

    “Mmmmh!” Williams akaguna huku akianza kuufunga mfuko ule kama ambavyo aliukuta.

    Mara baada ya kuhakikisha kila kitu amekirudisha kama kilivyokuwa, akakifuata kitanda na kisha kutulia. Bado kichwa chake kilikuwa kikifikiria mengi, uwepo wa madawa yale ndani ya meli ile ulionekana kumtisha kupita kawaida. Williams akakosa amani mpaka pale ambapo bwana Cheng alipoingia ndani ya chumba kile huku akionekana kuwa mwenye furaha na kuondoka huku akiwa mpole zaidi ya mtu aliyemwagiwa maji katika kipindi cha baridi.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bwana Robinson alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Kitendo cha vijana wake watatu ambao alikuwa amewatuma kupigwa na risasi na wapelelezi mpaka kufa kilionekana kumhuzunisha kupita kwaida. Kwa jinsi hali ilivyokuwa ikionekana, alijua fika kwamba ilikuwa ni lazima Williams afanikiwe kuja nchini Marekani na hivyo kumsababishia matatizo makubwa katika maisha yake.

    Kitu alichokifanya ni kuwaita watu wengine ambao pia alitaka kazi ifanyike kwa haraka sana, katika kipindi hicho, kitu ambacho alikuwa akikihitaji ni kumuona Williams akifa, basi. Hakuwa na wasiwasi na Phillip, kutokana na upole ambao alikuwa nao Phillip, alijua kwamba angeweza kumtuliza olakini isingewezekana kwa Williams ambaye alionekana kuwa machachari kupita kawaida.

    Baada ya dakika thelathini, vijana wawili ambao walikuwa ni hatari hata zaidi ya wale wa kwanza walikuwa ndani ya nyumba yake na kisha kuwaambia kile ambacho alikuwa akitaka kuwaambia katika siku hiyo. Hata taarifa ilipotoka kwamba Williams alikuwa amewakimbia wapelelezi wale, hiyo ikaonekana kuwa taarifa nzuri kwake, hivyo akawagawia kiasi kikubwa cha fedha vijana wale, mfaransa, Thuram pamoja na mfaransa mwenye asili ya Afrika, Kaposhoo.

    Vijana hawa wawili walikuwa wmetoka nchini ufaransa, katika kipindi cha nyuma, walikuwa wamechukua mafunzo katika nchi ya Marekani, mafunzo ya ujasusi ambayo yalikuwa makali kuliko hata yale ambayo walikuja kupewa wengine katika miaka ya mbele. Vijana hawa walikuwa wakiaminika sana na taifa la marekani lakini pale ambapo nchi ya Ufaransa ilipowataka vijana wao, hawakuwa na jinsi, wakawaruhusu kurudi nchini kwao na hiyo ndio kuwa sababu ya Marekani kutotaka kuwapa mafunzo ya kijasusi kwa watu ambao walikuwa wakitoka katika nchi nyingine kwani kwa kitendo kile, waliona kama wamesalitiwa.

    Katika kipindi hicho, vijana wale walikuwa likizo na ndio ilikuwa sababu ya Bwana Robinson kuwapata na kuwaahidi kiasi kikubwa cha fedha hata zaidi ya kile ambacho aliwapata wale vijana wa kwanza. Kaposhoo na Thuram hawakuonekana kuwa na wasiwasi, walikuwa wakijiamini sana kupita kawaida, walichokifanya katika kipindi hicho ni kuelekea katika hoteli ambayo walikuwa wamepanga na kisha kuchukua vifaa vyao.

    Thuram na Kaposhoo walionekana kuwa juu sana hata zaidi ya F.B.I wa kipindi hicho. Walijua kwamba data zote za Williams zilikuwa katika ofisi ya F.B.I, walichokifanya ni kuchukua kompyuta yao na kisha kuanza kutafuta mawasiliano na idara ya uhamiaji. Wala hawakupata shida, kwa sababu walikuwa wakijua kucheza na sode za kompyuta, wakafanikiwa kuzipata alama za vidole za Williams na hivyo kuendelea na mambo mengine.

    “Hii kazi itafanyika kiutaalamu zaidi. Hatutokosea hata sehemu moja. Upo tayari tusafiri mpaka Thailand?” Thuram alimuuliza Kaposhoo.

    “Usijali. Tunaweza kusafiri. Tutasafiri mpaka katika ubalozi wa Marekani, si unajuwa wapelelezi walikuwa safarini kuelekea huko pamoja na Williams?”

    “Ndio”

    “Basi itabidi tuanze na huko. Hii kazi hatutochukua muda mrefu itakuwa imekamilika” Thuram alimwambia Kaposhoo.

    Hao ndio vijana ambao walikuwa wametumwa na Bwana Robinson kuifanya kazi hiyo, hao ndio vijana ambao walikuwa na hisia kubwa katika kuifanya kazi yao, mafunzo ya kijasusi ambayo walikuwa wamepewa kipindi cha zamani yalikuwa makali kupita kawaida. Vijana hao ndio walikuwa wakiifahamu kazi yao ambyo walikuwa wametumwa kuifanya. Kwa jinsi walivyokuwa wakijua, mpelelezi Sam hakunusa hata nusu yao. Hao ndio Wafaransa ambao walikuwa wakijua kuifanya kazi yao kiufasaha zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Je nini kitaendele?

    Je Thuram na Kaposhoo watafanikiwa kumpata Williams?



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog