Simulizi : Hili Ni Jiji La New York
Sehemu Ya Tano (5)
Thuram na Kaposhoo wakaingia katika jiji la Bangkok na kisha kuchukua chumba katika hoteli ya Peacock ambayo ilikuwa katikati ya jiji hilo. Katika vichwa vyao kwa wakati huo walikuwa wakifikira namna ya kujua mahali Williams alipokuwa ili waweze kukamilisha kile ambacho walitakiwa kukamilisha katika kipindi hicho, kuumua Williams.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya hotel ya Peacock hawakutulia, muda mwingi walikuwa wakicheza na kompyuta zao huku wakicheza na code tu. Kitu ambacho walikuwa wakikitaka kwa wakati huo ni kufahamu mahali ambapo Williams alipokuwa tu. Kitu cha kwanza walichokifanya huku wakiwa ndani ya chumba kile ni kuingiza code zote ambazo zilikuwa zinazifanya mafaili kadhaa ya ubalozi wa marekani nchini thailand kujihifadhi katika kompyuta hiyo.
Jambo hilo wala halikuwa gumu kwao, kitendo cha kufahamu code mbalimbali kiliwafanya kupata urahisi wa kufanya kazi zao kwa wakati huo. Waliangalia kila kitu ambacho walikuwa wakitaka kuangalia katika kipindi hicho na kisha kuifunika kompyuta yao na kuanza kuangalia. Kwa wakati huo kila mmoja alikuwa na uhakika wa kukamilisha kile ambacho walikuwa wakitakiwa kukikamilisha ndani ya nchi hiyo, hawakuonekana kuwa radhi kuondoka mahali hapo bila kukamilisha kile ambacho kilikuwa kimewaleta ndani ya nchi hiyo.
“Unakumbuka walisema kuhusu kutoroka kwa Williams?” Kaposhoo alimuuliza Thuram.
“Walisema kwamba aliwatoroka katika kipindi ambacho waandamanaji walikuwa wakiwakimbia polisi wa kutuliza ghasia” Thuram alijibu.
“Sawa. Kwanza twende huko halafu nitakwambia nini cha kufanya” Kaposhoo alimwambia Thuram.
Kila kitu ambacho kilitakiwa kufanyika mahali hapo kilitakiwa kufanyika kwa ufasaha mkubwa sana kiasi ambacho hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeonekana kufahamu kitu chochote kile. Walichokifanya mahali hapo ni kuondoka na kisha kuelekea katika ubaloozi wa marekani kwa kuamini kwamba kila kitu wangeweza kukifahamu mara baada ya kufika huko.
Walichukua teksi ambayo iliwapeleka mpaka karibu na ubalozi ule, kwa kuulizia, wakapata kujua sehemu ambayo waandamanaji walipokuwa wamekusanyika na hivyo mapolisi kuanza kuwakimbiza. Wakabaki wakiiangalia sehemu ile na kisha kupiga hatua hamsini nyuma na kisha kusimama. Kufika hapo, wote wakaangaliana na kisha kuanza kutabasamu, walionekana kuanza kufanikiwa kile ambacho kilikuwa kimewaleta mahali hapo.
“Maneno yao yalisema kwamba waandamanjai waliwavamia na kisha kuwasukuma na kuanguka kama hivi” Kaposhoo alimwambia Thuram huku nae akianguka.
“Kwa hiyo kama Williams alikimbia, basi alikimbia huku nyuma. Asingeweza kukimbia kuelekea mbele kwa sababu kulikuwa na polisi. Unakubaliana nami?” Kaposhoo alimwambia Thuram na kumuuliza.
“Nakubaliana nawe”
“Kama unakubaliana nami, twende mbele” Kaposhoo alimwambia Thuram.
Hapo hapo wakaanza kazi ya kuondoka mahali hapo na kuelekea kule ambapo waliamini kwamba Williams alikuwa amekimbilia. Kwa wakati huo, kazi ile ilionekana kuwa rahisi sana na si kama kazi ambazo walikuwa wamezifanya katika kipindi cha nyuma kama nchini Urusi na nchi nyingine, kwa wakati huo walikuwa na uhakika kwamba wangefanikiwa kupafahamu sehemu ambapo Williams alipokuwa.
“Kuna njia mbili hapa” Kaposhoo alimwambia Thuram huku wakisimama katika njia panda”
“Unafikiri alielekea wapi?” Thuram alimuuliza Kaposhoo.
“Kwa jinsi kunavyoonekana, ukiende huku upande wa kulia unatokea katika soko kuu la hapa Bangkok na kama ukielekea kushoto unatokea bandarini. Hivi ingekuwa wewe ungekimbilia wapi?” Kaposhoo alimuuliza Thuram.
“Huku kwenye soko kuu”
“Ila kumbuka kwamba unatafutwa na picha zako zimesambazwa na kuonekana kwenye televisheni” Kaposhoo alimwambia Thuram.
“Kama ni hivyo, ningekwenda bandarini” Thuram alimwambia Kaposhoo.
“Kwa nini ukimbilie bandarini?”
“Kwa sababu hakuna watu wengi”
“Safi sana. Twende huko. Nimekwishakwambia toka mwanzo kwamba kazi hii ni rahisi hata zaidi ya zile tulizozifanya nchini Urusi” Kaposhoo alimwambia Thuram na kisha kuanza kuelekea kule kulipokuwa na bandari.
Walitembea zaidi na zaidi huku wakiendelea kuongea mambo yao, tayari kwa kipindi hicho waliamini kwamba kila kitu kilikuwa kinakwenda kama ambavyo kilipangwa na wala hawakuwa na uhakika kama awangeweza kuharibu kitu chochote kile. Masomo ya hisia za binadamu ambaye alikuwa akitafutwa walikuwa wakiyakumbuka vizuri sana, upelelezi wao pamoja na ujasusi wao ulikuwa mkubwa kupita kawaida. Walietembea mpaka walipofika karibu na geti la kuingilia bandarini, hawakutaka kwenda katika geti lile, wakasimama na kuanza kuangaliana.
“Twende huku ufukweni” Kaposhoo alimwambia Thuram.
“Kwa nini tusiende kule kwenye geti kuu?”
“Williams si mfanyakazi wa bandari. Hawezi kuingia pale bila kitambulisho. Atakuwa amekwenda njia hii. Niamini” Kaposhoo alimwambia Thuram.
Wote wakaanza kuelekea katika njia ile ambayo ilikuwa ikielekea ufukweni huku wakiangalia katika kila kona mahali hapo. Walikuwa na uakika kwambaWilliams alikuwa mahali hapo na kama hakuwa mahali hapo, kuna sehemu alikuwa amekwenda ila kupitia mahali hapo. Mbele ya macho yao kulikuwa na vijana wengi ambao walikuwa wakiogelea kitu ambacho kiliwafanya kumuangalia mtu mmoja baada ya mwingine.
“Akili yangu imefikia mwisho” Kaposhoo alimwambia Thuram.
“Umefanya kazi kubwa sana. Akili yangu ndio imeamka sasa hivi” Thuram alimwambia Kaposhoo na kuendelea.
“Unazikumbuka sehemu nne kuu ambazo mtu anayetafutwa huwa anapenda kujificha?” Thuram alimuuliza Kaposhoo.
“Nazikumbuka sana. Huwa ni msituni, kwenye mahandaki, mapango. Sehemu moja nimeisahau” Kaposhoo alimwambia Thuram.
“Ngoja nikukumbushe. Unaukumbuka ule upelelezi ambao tuliufanya Afrika Kusini mwaka juzi pale ambapo Bheki alipokuwa akitafutwa na serikali ya Afrika Kusini?” Thuram alimuuliza kaposhoo.
“nakumbuka”
“Kama unakumbuka alijifichia wapi mpaka tukampata?”
“Kwenye meli ya Wagiriki. Nimekumbuka sehemu ya nne. Huwa wanapenda kujifichia kwenye meli, hasa zinazokwenda sehemu fulani” Kaposhoo alimwambia Thuram.
“Safi sana. Unahisi nini?”
“Mungu wangu! Twende bandarini” Kaposhoo alimwambia Thuram.
Hawakutaka kubaki mahali hapo, tayari wakaona kwamba kulikuwa na uwezekano wa mtu ambaye walikuwa wakimtafuta, Williams alikuwa amekwenda katika moja ya meli ambazo zilikuwa zinaanza safari ya kuondoka mahali hapo. Walikuwa wakikimbia kwa mwendo wa kasi, kwa wakati huo walikuwa wakitaka kufika sehemu ile haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuangalia kama wangeweza kumuona William kule ambapo walikuwa wakimtafuta.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kufika katika geti la kuingilia ndani ya bandari ile, wakaonyesha vitambulisho vyao na kisha kuruhusiwa. Wakaanza kuangalia huku na kule kama kumtafuta Williams, walipoona kwamba hwakufanikiwa kumpata, hapo ndipo ambapo walianza kuuklizia kama njia moja wapo ya kujua mahali ambapo mtu huyo alipokuwa amekimbilia.
“Samahani” Thuram alimwambia jamaa ammoja ambaye alikuwa akipita karibu yao.
“Bila samahni”
“Kuna meli yoyote iliyoondoka hivi karibuni? Namaanisha kuanzia juzi?” Thuram aliuliza.
“Ndio. Kuna moja iliondoka juzi, mbili zimeondoka jana na tatu zimeondoka leo asubuhi” Jamaa huyo alijibu.
“Sawa. Zimekwenda wapi?”
“Hiyo ya juzi imekwenda Afrika nchini Nigeria, mbili za jana zimeondoka kuelekea Uingereza na tatu za leo zimeondoka kuelekea Marekani” Jamaa yule alijibu.
“Tunashukuru” Thuram alimwambia jamaa yule na kisha kumgeukia Kaposhoo.
“Meli ya juzi. Siku ya tukio la kuwatoroka wapelelezi” Thuram alimwambia kaposhoo.
“Umefikiria nini? Kwa nini usiseme ya jana au leo?”
“Williams ni Mwafrika. Atakuwa amekimbilia kwao. Unafahamu kwamba mama yake ni Mwafrika kutoka Ghana?” Thuram alimuuliza Kaposhoo.
“Nakumbuka”
“Basi jua kwamba Williams atakuwa amepanda meli hiyo kuelekea Nigeria kabla ya kuingia Ghana. Inatupasa kufuatilia kwa ukaribu” Thuram alimwambia Kaposhoo.
“Sasa tutafuatiliaje?”
“Kwa helkopta”
“Tutaitoa wapi?”
“Usijali” Thuram alimwambia kaposhoo.
Hawakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, walichokifanya mahali hapo ni kuondoka kuelekea katika kambi ya kijeshi ya Thailand na kisha kuwaelezea kila kitu kilichokuwa kikiendelea na huku wakiwaonyeshea vitambulisho vile vya F.B.I na kujua kwamba watu hao walikuwa wametoka nchini Marekani na hivyo walikuwa wakihitaji msaada mkubwa wa helkopta kwa ajili ya kumfuata mtu ambaye alikuwa akitafutwa na dunia nzima.
Japokuwa jambo hilo lilionekana kuwachanganya wanajeshi lakini kutokana na maneno matamu ambayo walikuwa wakiongea Kaposhoo na Thuram, wakajiona wakianza kuwaamini kwamba watu hao walikuwa wametoka katika serikali ya Marekani tena kubwa zaidi kutoka katika shirika la upelelezi la F.B.I. Hakukuwa na maswali mengi ambayo waliulizwa, kitu kilichofanyika mahali hapo ni kuruhusiwa kuchukua helkopta huku wakisindikizwa na wanajeshi wawili ambao walionekana kuwa msaada kwao endapo wangepata matatizo makubwa kwani mpaka katika kipindi hicho, Williams alikuwa akionekana kuwa mtu hatari ambaye alikuwa amechukua mafunzo ya kijeshi.
Mara baada ya kusaini baadhi ya karatasi, moja kwa moja Kaposhoo, Thuram na wanajeshi wawili na dereva wakaingia katika helkopta ya kijeshi na kisha kuanza kuelekea baharini kwa ajili ya kuiwahi meli hiyo ya mizigo ambayo ilikuwa ikielekea Afrika katika nchi ya Nigeria. Mawasiliano kutoka kwa rubani na nahodha wa meli ile yakaanza kufanyika na kuambiwa kila kitu kuhusiana na helkopta ile jambo ambalo wafanyakazi pamoja na nahodha hawakutakiwa kuhofia kitu chochote kile.
Helkopta ilichukua saa moja na nusu na ndipo kwa mbali walipoiona meli ile ikiendelea na safari kama kawaida. Mpaka kuifikia meli ile tangu waione ilichukua dakika ishirini na ndipo helkopta ile ikaanza kutua katika meli ile ya mizigo ambayo kama kawaida ilikuwa ikiendelea na safari kama kawaida. Wanajeshi wale pamoja na kaposhoo na Thuram wakateremka na kisha kuanza kuongea na Bwana Cheng juu ya kile ambacho kilikuwa kimewaleta ndani ya meli ile.
Bwana Cheng alionekana kukataa kata kata kwamba hakumbeba mtu huyo. Wafanyakazi wote wa meli ile wakatakiwa kukaa sehemu moja ili wapelelezi wale waanze kufanya kazi yao kama kawaida. Kutokana na kuwa na nyaraka zote za serikali kuhusiana na upekuzi, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa amepinga, wakawaruhusu kuifanya kazi ile. Hapo ndipo ambapo Kaposhoo alipotoa chombo kidogo ambacho kilikuwa na alama za vidole vya Kaposhoo na kisha kuanza kuchunguza.
Mara kwa mara kifaa kile kilikuwa kikipiga kelele mara baada ya kuona kwamba kulikuwa na alama katika sehemu ambazo zilikuwa zimeshikwa na mikono ya Williams. Mpaka kufikia hapo, wote wawili walikuwa na uhakika kwamba Williams alikuwa ndani ya meli ile na hivyo ilikuwa ni lazima wamkamate. Waliendelea kuchunguza meli nzima lakini hawakuonekana kuambulia kitu chochote mpaka pale ambapo walifika katika mlango wa chumba kimoja ambao ulikuwa umefungwa kwa ndani.
“Mikono yake iliweza kushika hata hiki kitasa. Unaona?” Kaposhoo alimwambia Thuram huku akimuonyeshea alama za vidole vile kwenye kifaa kile.
“Ina maana aliwahi kuingia hata ndani ya chumba hiki?”
“Ndio maana yake. Hebu fungua” Kaposhoo alimwambia Thuram ambaye akaanza kuufungua mlango ule lakini akashindwa.
“Kuna nini humu. Unaweza kuufungua mlango huu?” Thuram alimwambia bwana Cheng ambaye alikuwa akitetemeka kwa kumfikiria Williams pamoja na madawa ya kulevya ambayo yalikuwa ndani ya chumba kile.
“Hakuna kitu humo. Chumba hiki hakitumiki” bwana Cheng aliwaambia.
“Tunajua. Tunaomba ukifungue”
“Haiwezek.......” Bwana Chebg alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, Kaposhoo akatoa bunduki na kumnyooshea.
Bwana Cheng akachukua ufunguo wake na kisha kuanza kuufungua mlango ule. Mlango ulipofunguka, chumba kikaonekana kuwa kitupu. Hapo ndipo walipoanza kuangalia kila kona. Katika kipindi chote hicho Bwana Cheng alikuwa akitetemeka tu, kwa hali jinsi alivyokuwa akiiona aliona kwamba kila kitu kilikuwa kinakwenda kujulikana.
“Huyu huku” Kaposhoo alimwambia Thuram mara baada ya kuangalia nyuma ya kabati. Williams alikuwa amejificha huko, walichokifanya ni kumuweka chini ya ulinzi na kisha kumfunga pingu.
“Unamficha mharifu halafu unasafirisha madawa. Hatuna haja na madawa yako. Sisi tulikuwa tunamtaka huyu tu” Thuram alimwambia Bwana Cheng huku wakiwa wanatoka ndani ya chumba kile.
“Nilikwambia kwamba kazi hii ilikuwa rahisi sana na si kama zile za Urusi” Thuram alimwambia Kaposhoo huku wakiwa wamemuweka Williams chini ya ulinzi na kisha kupana ndani ya helkopta ile na kuondoka mahali hapo kuelekea Bangkok.
“Kazi itafanyika mara baada ya kuwakabidhi helkopta yao. Tutaondoka na kumuua” Thuram alimwambia Kaposhoo kwa lugha ya Kifaransa ambayo haikueleweka na mtu yeyote yule mahali pale. Katika kipindi chote hicho, Williams alikuwa kimya huku akiwa amejiinamia, alionekana kuishiwa nguvu kwani aliona kwamba alikuwa amekwishakamatika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Phillip alitakiwa kusafirishwa kwa haraka sana kuelekea nchini Marekani, mambo yakaonekana kuanza kubadilika kwa wakati huo. Kelele za Wamarekani zikaonekana kuongezeka zaidi na zaidi kiasi ambacho kikawafanya wafanyakazi wa shirika la kipelelezi la F.B.I kukosa amani kabisa. Kila siku watu walikuwa wakiongea yao huku hata mambo mengine mengi yakiwa yanaongezeka tu japokuwa hayakuwa na ukweli wowote ule.
Phillip alitulia katika ubalozi wa Marekani pamoja na Gong huku wakionekana kuwa na wasiwasi mwingi, katika kipindi chote cha maisha yake katika nchi ya Thailand, Phillip hakutaka kumuamini mtu yeyote yule. Kila siku maisha yake aliyaona yapo hatalrini, kitendo cha Bwana Robinson kutaka kuwaua kilikuwa kimemuondolea uaminifu na kuwaona watu wote kuwa ni wabaya sana.
Walikaa katika ubalozi ule kwa masaa mawili na ndipo Phillip akatakiwa kusafirshwa kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kimefanyika nchini Thailand hasa kule msituni. Suala hilo lilikuwa likifanyika kimya kimya sana pasipo Wamarekani kupewa taarifa kwamba Phillip alikuwa amepatikana na hivyo alikuwa akitarajiwa kuingia nchini Marekani katika kipindi cha masaa kadhaa yajayo.
Kwa Phillip kuondoka nchini Thailand bila Gong likaonekana kuwa suala gumu sana, hakutaka kuondoka na kumuacha Gong nchini Thailand na wakati mtu huyo alikuwa amewasaidia sana huku jambo jingine kubwa yeye mwenyewe akiwa shahidi mkubwa kwa kile ambacho kilikuwa kinakwenda kuongelewa mahakamani. Japokuwa balozi pamoja na wapelelezi kumazimisha sana kuondoka peke yake lakini bado Phillip aliendelea kung’ang’ania kwamba ilikuwa ni lazima kwenda pamoja na Gong japo hakuwaambia sababu.
Kilichofanyika mahali hapo ni simu kupigwa nchini Marekani na kisha kuwaeleza kile ambacho Phillip alikuwa akiking’ang’ania kwa wakati huo. Hakukuwa na jinsi zaidi ya kumruhusu Gong kuelekea nchini Marekani pamoja nae huku shughuli zote za vibali vikitarajiwa kufanyika ndani ya siku mbili. Gong hakuonekana kuamini mara baada ya kugundua kwamba nae alikuwa akitakiwa kuelekea nchini Marekani pamoja na Phillip.
Hiyo, kwake ikaonekana kuwa kama ndoto, hakuamini kama siku hiyo alikuwa akitakiwa kuelekea nchini Marekani, nchi ambayo alikuwa akitamani sana kufika, si yeye tu, bali asilimia tisini na nane ya vijana wa Thailand walikuwa wakitamani sana kuingia katika nchi ya Thailand. Siku hiyo Gong alionekana kuwa mwenye furaha tele, mara kwa mara alikuwa akimshukuru Phillip kwa kile ambacho alikuwa amemfanyia cha yeye kutakiwa kuelekea nchini Marekani pamoja nae.
Mawazo ya Phillip katika kipindi hicho ndipo yakaanza kumfikiria rafiki yake mkubwa, Williams ambaye tangu waliporudi kutoka benki hawakumuona pale walipokuwa wamemuacha. Katika kipindi hicho, Phillip hakujua mahali alipokuwa Williams kiasi ambacho wakati mwingine alikuwa akifikiria kwamba Williams alikuwa ametekwa na vijana wa Bwana Robinson na kisha kuuawa kama njia mojawapo ya kutunza siri ile.
Muda ambao walitakiwa kusafiri ukawa umefika na hivyo wote walitakiwa kutoka nje ya ubalozi ule na kisha kuingia ndani ya gari pamoja na wapelelezi wale na kisha safari ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bangkok kuanza. Ndani ya gari, Gong hakuweza kuificha furaha yake, alikuwa akifurahia kupita kawaida kwani katika kipindi hicho alikuwa akielekea katika nchi ambayo mara kwa mara alikuwa akiiota ndotoni mwake.
Mara baada ya gari kufika uwanja wa ndege, moja kwa moja wakateremka na kisha kuanza kuelekea katika ndege maalumu ambayo ilikuwa imesimama pembeni ya uwanja ule. Gong hakuonekana kuamini kama kweli katika wakati huo alikuwa akipiga hatua kuifuata ndege ile ndogo, katika kila kitu ambacho kilikuwa kikitokea mahali pale, kwake kilionekana kuwa kama ndoto fulani nzuri ambapo baada ya muda angeshtuka na kujikuta yupo msituni akiwa mmoja wa walinzi ambao walikuwa wakiwalinda wachezaji wa mpira wa kikapu ambao walikuwa wamewateka.
Mpaka pale alipokuwa akikanyaga ngazi na kisha kuanza kuzipanda, hakuwa akiamini kabisa, bado kila kilichoendelea kwake kilionekana kuwa kama ndoto fulani. Mara baada ya kuingia ndani ya ndege, wakakaa na baada ya muda ndege kuanza kupaa. Kwa sababu mpelelezi Adrian ndiye alikuwa akifahamu lugha ya Thailand na Kingereza, kazi yake kubwa mahali hapo ilikuwa ni kuwaonganisha wote wawili kwenye maongezi ambayo yalikuwa yakizidi kuchangamka kdri muda ulivyozidi kwenda mbele.
Ndege ile ilichukua masaa saba na ndipo ilipoanza kutua katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy ndani ya jiji la New York na kisha kuanza kuteremka huku gari moja lililokuwa limeletwa maalumu kwa ajili yao likiwa limepakiwa katika eneo la uwanja ule. Moja kwa moja wakaingia ndani ya gari lile na kisha safari ya kuelekea makao makuu ya jengo la shirika la F.B.I kuanza.
Hawakuwa na uwezo wa kuona nje, gari lile lilionekana kujitosheleza kwa kila kitu. Vioo vilikuwa havimruhusu mtu wa nje kuona ndani na wala wa ndani kuona nje. Kila mmoja ndani ya gari lile akaonekana kuwa na furaha, kwa wakati huo kila kitu kikaonekana kukamilika kwani walijua kwamba kila kitu ambacho walikuwa wamekiangaikia kwa wakati huo kilikuwa kinaelekea mwisho.
Gari lile likaendeshwa mpaka kufikia sehemu fulani na kisha gari kusimamishwa. Kwa sababu hawakuwa wakiona nje, sehemu ile ya nyuma kuwa kama imetengwa na kutokumuona dereva, kila mmoja akafikiria kwamba walikuwa wamekwishafika katika sehemu ambayo walikuwa wakitakiwa kuwepo kwa wakati huo. Mpelelezi Adrian akaufungua mlango kwa nia ya kutoka nje huku akitarajia kupokelewa kwa shangwe kwa kile ambacho walikuwa wamekifanya, mlango ukaonekana kupigwa loki.
Adrian hakutaka kuishia hapo, aliendelea zaidi na zaidi kuufuangua mlango ule lakini bado hali ilikuwa ile ile jambo ambalo likamfanya hata mpelelezi Brian nae kutaka kuufungua mlango lakini nao mlango wa upande ule ukaonekana kupigwa loki. Mara ghafla sauti ya muungurumo wa treni ukaanza kusikika kwa mbali, honi kadhaa zilikuwa zikisikika zikipigwa na baada ya sekunde chache, gari lile likagongwa na treni na kisha kuanza kubimbirika bimbirika relini kwa umbali wa hatua thekathini na kisha kutolewa nje ya reli ile.
Ile ikaonekana kuwa ajali kubwa ambayo haikuwa ikitegemewa kutokea mahali pale. Mara watu wawili ambao walikuwa wamevaa vinyago wakaanza kulifuata gari lile kwa mwendo wa haraka haraka huku mikono wakiwa wameishika bunduki, walipolifikia, mpelelezi Adrian alikuwa ameufungua mlango kwa ajili ya kutoka garini huku akiwa ametapakaa damu, hata kabla hajatoka vizuri, akapigwa risasi kadhaa kifuani na kufa pale pale.
Kijana yule mwingine akaanza kuelekea katika upande wa pili ambapo akamkuta Brioan akiwa ameufungua mlango huku akionekana kuwa kwenye maumivu makali na mwili wake kujaa damu, nae akapigwa risasi mfululizo. Walichokuwa wamekipanga mahali hapo ni kuwapiga risasi na kuwaua watu wote ambao walikuwa ndani ya gari lile lakini hata kabla hawajafanya kitu hicho, mara wakata miti kwa ajili ya mbao zaidi ya kumi wakaanza kuonekana wakielekea kule ambapo gari lile lilipokuwa, vijana wale walipowaona, wakaanza kukimbia huku wakiwa hawajakamilisha kile ambacho walikuwa wamekipnaga.
Gari lilikuwa limebondeka kupita kawaida, kiwa jinsi lilivyokuwa likionekana ilikuwa ngumu sana kujua kama kulikuwa na mtu yeyote ambaye alisalimika ndani ya gari lile. Mara baada ya kulifikia gari lile, wakata miti wakaanza kuitoa miili ile na kisha kuangalia kama kulikuwa na watu wengine ambao walikuwa salama. Ni watu watatu tu, Phillip, Gong na mpelelezi Ben ndio ambao walikuwa wakipumua japo kwa mbali sana huku miili yao ikiwa imetapaa damu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakawatoa watu wale na kisha kuwapakiza ndani ya gari na kisha kuanza kuelekea katika hospitali ndogo ya Manhhatan ambayo ilikuwa hapo hapo New York. Gari lilikuwa likiendeshwa kwa kasi, wote watatu walikuwa wakilia kwa maumivu makali, damu bado zilikuwa zikiwatoka kupita kawaida, kwa jinsi hali ilivyokuwa ikiendelea kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali zao ziliendelea kuwa mbaya zaidi.
Huku wakiwa wamebakisha umbali wa kilometa mbili mpaka kufika hospitalini, akaanza mpelelezi Ben kuwa kimya, tayari alikuwa amekwishakata roho jambo ambalo likaanza kuwatia hofu watu wote ambao walikuwa ndani ya gari lile kwa kuona kwamba kama wasingefanya haraka bbasio hata watu wawili ambao walikuwa wamebakia nao wangeweza kukata roho mule mule ndani ya gari.
Mara baada ya kufikishwa hospitalini, kwa haraka sana machela zikaletwa na kisha Phillip na Gong kupakizwa katika machela hizo. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akimtambua Phillip, katika kipindi kile, damu zilikuwa zimetapaa usoni mwake na watu walikuwa bize katika kipindi hicho kuokoa maisha yake pamoja na Gong ambao wote walionekana kuwa katika hali mbaya sana.
Huku machela ile ikizidi kusukumwa kuelekea ndani, mara mkono wa Phillip ukalegea na kisha kujiachia hewani huku mwili wake akiwa ameulaza katika machela ile. Manesi ambao walikuwa wakiwasukuma kuelekea katika chumba kimoja kwa ajili ya matatibabu wakaonekana kuwa na wasiwasi, mashine ya oksijeni ambayo walikuwa wamemuwekea puani mwake ilikuwa imetapakaa damu kutokana na kila alipokuwa akipumua, damu zilikuwa zikitoka mdomoni na puani.
Hali ile ikaonekana kuwatia wasiwasi manesi wale kwa kuona kwamba kulikuwa na uwezekano wa kumpoteza mtu yule. Wakazidi kutembea haraka zaidi na zaidi mpaka kuzifikisha machela zile ndani ya chumba kile. Katika hali ambayo ilionekana kumshtua kila mmoja, mwili wa Phillip ulikuwa wa baridi kabisa, alikuwa amekwishakufa katika kipindi ambacho walikuwa wakimleta ndani ya chumba kile mara baada ya kichwa chake kupata jeraha kubwa ambalo lilisababishwa na kichwa chake kugongwa katika vyuma ndani ya gari lile hali iliyopeleka fuvu lake kuvunjika sehemu tatu.
“Amekufa” Nesi mmoja alisema kwa sauti ya chini. Hata kabla majonzi hayajawaisha, Gong akaanza kurusha miguu na mikono yake huku na huku jambo ambalo likawafanya manesi wote kuwa kuwa na wasiwasi mahali hapo kwa kuonamkwamba hata mtu huyo nae alikuwa njiani kufa kama ambavyo alivyokufa Phillip.
Siku iliyofuata ndio ilikuwa siku ambayo mpelelezi Sam alipoanza safari yake ya kuelekea nchini Thailand kwa mara ya pili. Kwa wakati huu alikuwa akielekea huko kwa ajili ya kumtafuta Williams na kisha kumpeleka nchini Marekani ambapo huko mahojiano yangeanza rasmi juu ya nani ambaye alikuwa amehusika katika mauaji ya wachezaji wale kule msituni.
Bado moyo wake ulikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba Bwana Robinson ndiye ambaye alikuwa amehusika na mauaji hayo ila alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni kumpata Williams ambaye alikuwa akiufahamu ukweli wote. Safari ile ilichukua masaa kadhaa akawa amekwishaingia ndani ya nchi ya Thailand ambapo moja kwa moja akaelekea katika hoteli na kutulia.
Hakujua ni wapi ambapo alitakiwa kuanza kazi hiyo, hakujua mahali ambapo Williams alipokuwa katika kipindi hicho. Kazi hiyo ambayo ilikuwa mbele yake ilikuwa kubwa sana ambayo ilikuwa ikimpa wakati mgumu wa juu ya nini cha kufanya. Alikaa katika chumba kile kwa muda wa masaa mawili na ndipo simu yake ilipoanza kuita, alipoipokea, alikuwa Bwana Swan.
“Kuna nini mkuu?” Sam aliuliza.
“Nimepokea simu kutoka katika kituo cha jeshi huko nchini Thailand” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Hiyo simu inasemaje?”
“Kwamba kuna watu wamefika hapo jeshini na kutaka helkopta”
“Helkopta ya nini?”
“Wanataka kumfuatilia Williams ambaye anakisiwa yupo kwenye boti akielekea barani Afrika” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Hao watu ni wakina nani?”
“Hata siwajui japokuwa walijitambulisha kama wapelelezi kutoka F.B.I na hata vitambulisho waliwaonyeshea wanajeshi wa hapo kambini” Bwana Swan alimwambia Sam ambaye akaonekana kuanza kuhisi kitu.
“Kwa hiyo waliwapa hiyo helkopta?”
“Ndio. Niliwaambia wawape kwani hao ni ndugu zetu japokuwa sijawatuma” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Kwa nini sasa uliruhusu?”
“Kwa sababu ninajua kwamba wewe upo huko. Cha msingi ondoka hapo na kuelekea kambini. Ninachotaka ni kuwaweka watu hao chini ya ulinzi na kisha kumchukua Williams endapo wakiwa nae” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Hakuna tatizo mkuu.
Sam hakutaka kuendelea kukaa ndani ya chumba kile hotelini, alichokifanya ni kuchomoka na kisha kutoka nje ya hoteli ile. Akakodi taksi ambayo ikaanza kumpeleka mahali ambapo kulikuwa na kambi ya jeshi. Walichukua muda wa dakika thelathini, wakafika katika geti la kuingilia ndani ya kambi hiyo ambayo teksi ile ikageuka na yeye kumlipa dereva kiasi cha fedha ambacho kilikuwa kikihitajika.
Sam alipofika getini, akawaonyeshea kitambulisho na kisha kuruhusiwa kuingia ndani ya kambi ya jeshi hilo. Alichokifanya ni kufika katika ofisi ya mkuu wa jeshi wa kambi ile na kisha kumwambia kile ambacho kilikuwa kimetokea, mkuu wa jeshi akaonekana kushtuka. Kilichofanyika ni kuwaambia wanajeshi wote wajiandae kwani watu wale ambao walikuwa wamekuja kuchukua helkopta hawakuwa wapelelezi wa kitengo cha F.B.I kama walivyojitambulisha.
Wanajeshi walijiandaa na bunduki zao huku wakitakiwa kutokuonyesha ishara yoyote mbaya kwa watu wale katika kipindi ambacho wangekuja na helkopta pamoja na mtu huyo ambaye walikwenda kumchukua, Williams. Ndani ya dakika arobaini, helkopta ile ikaanza kutua ndani ya uwanja wa kambi ile ambapo Kaposhoo, Thuram na wanajeshi wengine wakateremka huku wakiwa na Williams ambaye bado alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa.
Walichokifanya Kaposhoo na Thuram ni kwenda kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa jeshi katika kambi ile. Katika kipindi hicho, wote wawili walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, tayari walikuwa na uhakika kwamba kazi kubwa ambayo walikuwa wameifuata kule Thailand ilikuwa imekwishakamilika na hivyo kilikuwa ni kipindi cha kuondoka na Williams mabahli hapo na kwenda sehemu yoyote iliyojificha na kisha kumuua.
Mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ile wakaelezea kila kilichotokea na kutoa shukrani kwa niaba ya F.B.I nchini Marekani kwa msaada wa helkopta ambayo walikuwa wameirudisha huku wakiwa na mtu wao ambaye walikuwa wamemfuata. Mara baada ya kumaliza kila kitu, wakatoka ndani ya ofisi ile kwa lengo la kuondoka mahali hapo ila kilichowashtua ni baada ya kutoka ndani ya ofisi ile na kukuta zaidi ya wanajeshi mia moja walikuwa wamewanyooshea bunduki.
“Kuna nini tena?” Kaposhoo aliuliza kwa sauti.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo wakatakiwa kuziweka chini bunduki zao na kufanya hivyo. Wote walikuwa wamepigwa na mshangao, hawakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea. Hapo hapo Sam akatokea mahali hapo na kisha kuanza kupiga hatua kuwafuata na kuanza kuwasachi mifukoni mwao na kuchukua vitambulisho vyao.
“Mimi ni F.B.I. Ninyi ni nani?” Sam aliwauliza swali ambalo likawafanya kuwa kimya.
Sam hakutaka kuongea nao sana, alichokifanya ni kutaka watu wale wawekwe ndani kwa muda mpaka hapo ambapo watakuja kuchukuliwa na kupelekwa nchini Marekani na kuipewa mashitaka juu ya kile ambacho walikuwa wamekwenda kukifanya nchini Thailand kwa kumkamata Williams huku wakijifanya wao ni wapelelezi.
“Kuwa huru Williams. Unahitajika sana nchini Marekani” Sam alimwambia Williams.
“Sijaua. Wananisingizia tu. Sijaua” Williams alimwambia Sam huku akianza kutokwa na machozi.
“Nafahamu. Nitataka kuongea na wewe kwa muda wa dakika kumi. Nielezee kila kilichotokea. Umesikia?” Sam alimwambia na kumuuliza Williams.
“Sawa. Ila sijaua”
“Nafahamu kwamba wewe si muuaji. Muuaji ni Bwana Robinson. Si ndio hivyo?”
“Ndio. Ni yeye ndiye aliyekuwa nyuma ya kila kilichotokea” Williams alimwambia Sam.
Alichokifanya Sam ni kutoa shukrani zake mahali pale na kisha kutaka gari ambalo likawapeleka mpaka katika ubalozi wa Marekani nchini hapo na kisha kusubiri safari ya kuondoka na kuelekea nchini Marekani. Hapo ndipo Sam alipopata nafasi ya kuongea na Williams na kutaka kuelezewa kila kilichotokea tangu pale ambapo ndege ilipotekwa.
Williams akaanza kuelezea kila kitu. Kila kilichoelezewa kutoka kinywani mwa Williams ndicho ambacho kilikuwa kikihisiwa kichwani mwa Sam. Williams alizungumza mambo mengi ambayo mengine Sam hakuwa akiyafahamu kabisa kama yalikuwa yametokea. Mara baada ya kuelezea kila kitu, akakaa kimya huku akimsikilizia Sam.
“Safi sana. Kila kitu kitakuwa salama, usijali” Sam alimwambia Williams.
“Ila marafiki zangu wapo wapi?” Williams aliuliza.
“Nani?”
“Phillip na yule kijana wa kithailand”
“Wameelekea nchini Marekani. Nadhani nao watasaidia kutoa ushahidi”
“Sawa”
Walikaa katika ubalozi huo kwa muda wa masaa mawili na ndipo ambapo wakaanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege ambapo wakachukua ndege ya kijeshi ambayo ilikuwa imeletwa kwa ajili ya kumchukua Williams na kisha kuanza safari ya kuelekea nchini Marekani. Ndani ya moyo wa Williams alikuwa na wasiwasi mwingi, mpaka katika kipindi hicho alikuwa haamini kama Wamarekani wangeweza kuamini kile ambacho kilikuwa kimetokea.
Alichokifanya Sam ni kuanza kuwasiliana na Bwana Sam kupitia simu maalumu ndani ya ndege ile. Alichokifanya Bwana Sam ni kuonganisha simu ile na hivyo wakubwa wote wa shirika lile la kipelelezi kusikiliza kile ambacho alikuwa akikiongea Sam.
“Kwa hiyo upo nae?”
“Ndio. Nipo nae. Kila kitu nilichokueleza kina ukweli. Yeye mwenyewe atakuja kueleza kila kitu” Sam aliwaambia hali iliyowafanya watu wote ndani ya kile chumba kidogo kuanza kupiga makofi.
“Na vipi kuhusiana na Phillip?”
“Mpaka sasa hivi mambo mabaya sana”
“Kwa nini?”
“Amekufa. Gari ambalo lilikwenda kuwachukua lilikuwa likiendeshwa na watu ambao si tuliowatuma” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Kivipi tena?”
“Wale ambao tulikuwa tumewatuma waende kuwapokea uwanja wa ndege walikutwa wakiwa wameuawa na miili yao kutupwa. Kwa maana hiyo wale ambao waliwapokea hawakuwa watu wetu, walikuwa watu wengine ambao wakawachukua na gari lao kulipaki katikati ya reli ya zile treni zipsafirishazo mizigo, tena porini kabisa” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Ikawaje baada ya hapo?”
“Phillip amekufa akiwa hospitalini baada ya fuvu lake kuvunjika mara tatu. Ni mtu mmoja tu ndiye aliyenusurika na hali yake ipo kwenye wakati mgumu” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Huyo mtu ni mtu wa Thailand?”
“Ndio”
“Sikiliza. Huyo mtu ni muhimu sana, waambie madaktari wafanye kila kinachowezekana kuhakikisha anapata nafuu. Huyo mtu akipona ndipo kila kitu kitakuwa sawa. Fanyeni hivyo. Huyo ni shahidi namba mbili ambaye ni muhimu sana” Sam alimwambia Bwana Swan.
“Sawa. Ngoja tuwapelekee taarifa madaktari”
“Sawa. Ikiwezekana hata ulinzi uwekwe katika hospitali hiyo na asiingie mtu yeyote ndani ya chumba hicho” Sam alimwambia bwana Swan.
“Sawa”
Sam akakata simu ile, kichwa chake katika kipindi hicho hakikuwa sawa kabisa. Alijiona kama kuanza kuchanganyikiwa. Mambo ambayo yalikuwa yameendelea yalikuwa makubwa kupita kawaida. Alikaa katika hali ya ukimya kwa muda fulani na ndipo akashtuliwa na na Williams ambaye alikuwa akitaka kujua alikuwa ameongea kuhusu nini.
“Nani amekufa?” Williams aliuliza.
“Phillip. Gari lao liligongwa na treni” Sam alitoa jibu ambalo likamfanya Williams kuanza kutiririka machozi mashavuni mwake.
“Usilie Williams. Kila kitu kitakuwa sawa” Sam alimwambia Williams.
Baada ya masaa kadhaa ndege ikaingia nchini Marekani ambapo magari matatu yalikuwa yamefika mahali hapo kwa ajili ya kuwapokea. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiamini kama kweli Williams alikuwa amekamatwa na katika kipindi hicho alikuwa akipelekwa katika jengo la shirika la upelelezi la F.B.I hata kabla ya kumfikisha polii.
Alipofikishwa huko, Williams akaingizwa ndani ya chumba ambacho kilikuwa na vioo vitupu na kisha kuwekwa kitini huku Bwana Swan pamoja na Sam wakiwa pembeni yake. Hapo ndipo ambapo Williams akaanza kuelezea kila kitu huku sauti yake ikiwa inarekodiwa. Kila mtu ambaye alikuwa akiangalia na kusikiliza alikuwa akilengwa na machozi, mambo ambayo Williams alikuwa akiyaelezea yalikuwa yamewagusa kupita kawaida, yalikuwa ni mambo makubwa ambayo yalikuwa yakichoma kupita kawaida.
“Wakili wetu ndiye atakuwa pamoja na Williams” Bwana Swan alimwambia Sam.
“Hata mimi ninlikuwa nikifikiria hivyo. Cha msingi Bwana Robinson akamatwe na kisha kufikishwa mbele ya sheria na kushitakiwa” Sam alimwambia Bwana Swan.
“Sawa. Ngoja tuwasiliane na polisi ambao wataongozana na vijana wetu kukamilisha kazi hiyo”
”Sawa”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Manesi bado walikuwa wakiangaika na hali ambayo alikuwa nayo Gong hospitalini pale, muda wote alikuwa akirusha miguu na mikono yake kama mtu ambaye alikuwa katika hatua za mwisho katika uzima wake. Walichokifanya manesi ni kubadilisha mashine ya hewa safi na kumwekea nyingine lakini hali bado haikuweza kubadilika jambo ambalo likaonekana kuwa geni machoni mwao. Kwa haraka haraka nesi mmoja akondoka mahali hapo na kwenda kumuita dokta Lawrance ambaye akafika hapo huku akionekana kukimbia kufika mahali hapo.
Kitu cha kwanza akayapeleka macho yake usoni mwa Gong, alikuwa ametulia kitandani pale kama mtu ambaye tayari alikuwa amekufa. Alichokifanya dokta Lawrence ni kuchukua mashine ya kushtulia mapigo ya moyo ambayo yalionekana kuanza kushuka sana na kisha kuanza kuushtua moyo wake. Katika kila hatua ambayo alikuwa akigusishwa mashine zile kifuani mwake, Gong alikuwa akiinua kifua chake juu na kukipeleka chini.
Dokta Lawrence hakutaka kuacha, alikuwa amekwishagundua kwamba Gong hakuwa amekufa bali mapigo yake ya moyo yalikuwa yameshuka kwa kiasi kikubwa sana na hivyo alikuwa katika jitihada za kuyarudisha katika hali ya kawaida. Zoezi lile lilichukua dakika moja, mapigo ya moyo yakaanza kurudi katika hali yake ya kawaida jambo ambalo likaonekana kuwafurahisha wote mahali pale. Kilichofanyika baada ya hapo ni kumbadilishia mashine nyingine ya hewa safi na kisha kumuwekea dripu ya maji ambayo yaliwekwa dawa ya Methropholies, dawa ambayo ilikuwa na kazi kubwa ya kuyarudisha mapigo ya moyo katika hali ya kawaida na kuishtua mishipa ya damu katika mwili wa binadamu.
Manesi pamoja na dokta Lawrence wakaonekana kupumua, kazi ya dakika moja ambayo walikuwa wameifanya ilikuwa kubwa sana katika macho yao. Baada ya kuona kwamba kila kitu kilikuwa kikienda sawa, hapo ndipo walipotoka nje ya chumba kile. Hawakukaa sana mahali hapo, mapolisi huku wakiongozana na F.B.I wakafika mahali hapo na kuhitaji kumuona Gong, kwa sababu walikuwa wameonyesha vitambulisho pamoja na kuwa na mapolisi, wakaruhusiwa kuingia ndani ya chumba kile.
Gong alikuwa ametulia kitandani huku mashine ya hewa safi ikiendelea kuwa mdomoni mwake. Mapolisi pamoja na wale F.B.I wakabaki wakimwangalia, walipoonekana kuridhika, wakaanza kuelekea katika ofisi ya dokta Lawrence huku mapolisi wale wakibaki nje ya chumba kile kwa ajili ya kuimalisha ulinzi. Huko ndipo ambapo wakaanza kuambiwa na dokta Lawrence juu ya hali ilivyokuwa mpaka Phillip kukutwa na mauti.
“Ulisema kwamba waliletwa hapa hospitali?” Bwana Mickey aliuliza.
“Ndio”
“Waliletwa na nani?”
“Kuna watu wapo hapo nje”
“Sawa. Tunataka kuwaona” Bwana Mickey alisema na hapo hapo kuanza kuelekea nje.
Katika kipindi hicho walikuwa wakitaka kuongea na watu ambao walikuwa wamewaleta Gong na marehemu Phillip hospitalini hapo, walijiona kuwa na maswali mengi ya kuuliza ambayo walihitaji majibu yake kwa haraka sana ili kuangalia ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea. Mara baada ya kufika nje, moja kwa moja wakaanza kuwafuata watu hao ambao walikuwa wamekaa pembeni ya mlango wa kutokea huku wakionekana kulizungumzia tukio lile.
“Ofisa anataka kuongea nanyi” Dokta Lawrence aliwaambia watu wale ambao wakaanza kuhojiwa maswali na F.B.I wale ambao walikuwa makini kuwasikiliza.
“Kwa hiyo hamkuweza kuwagundua watu hao?”
“Hapana. Walikimbia”
“Hamkuwakimbiza?”
“Hapana. Walikuwa na bunduki kwa hiyo tuliogopa” Mzee mmoja alijibu.
“Sawa. Gari lenyewe lipo wapi?”
“Nje ya mji wa Manhhatan. Kule karibu na pori la Bronswille” Mzee yule alisema.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, walichokifanya mahali hapo ni kuondoka na kuanza safari ya kuelekea katika msitu wa Bronswille ambao ulikuwa pembezoni mwa mji wa Manhhatan. Gari lilikuwa likiendeshwa kwa kasi, kwa wakati huo walikuwa wakitaka kufika sehemu hiyo kwa haraka zaidi kwa ajili ya kufanya kile ambacho walikuwa wakitaka kukifanya kwa wakati huo. Walichukua dakika thelathini wakafika katika sehemu hiyo ambapo moja kwa moja wakateremka na kisha kuanza kulifuata gari lile huku kukiwa na gari la polisi pamoja na baadhi ya mapolisi ambao walikuwa wakiendelea na vipimo.
Maiti zote zilikuwa zimetolewa mara baada ya vipimo kufanyika mahali hapo. Bwana Mickey alipofika na wenzake mahali pale wakaanza kuuliza maswali kadhaa na kupewa ufafanuzi kwamba wale ambao walikuwa wameuawa walikuwa F.B.I. Kila kitu ambacho walikuwa wakitaka kukisikia mahali hapo walikisikia kutoka kwa polisi wale huku wakiangalia kwa namna ambavyo vipimo vile vilivyokuwa vimeandikwa.
Hawakutaka kukaa sana mahali hapo, mara baada ya kuangalia kila kilichokuwa kikiendelea mahali hapo, wakaanza kuondoka kurudi ofisini huku wakiwa wamekwishachukua vitu ambavyo walikuwa wakivitaka kwa wakati huo.
****
Bwana hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo, kitendo cha kila aliyemtuma kutokamilisha kazi yake ilionekana kumuumiza kupita kawaida. Akili yake kwa wakati huo ilikuwa imechanganyikiwa kupita kawaida, hakujua afanye nini, hakujua ni kitu gani hasa alitakiwa kukifanya mpaka kumpata Williams ambaye alionekana kuwa kama mwiba wa moto katika maisha yake. Alichokifanya kwa wakati huo akachukua simu yake na kisha kuanza kupiga namba fulani na baada ya muda sauti ya mtu upande wa pili ikaanza kusikika.
Bwana Robinson aliongea kwa muda wa dakika kadhaa na kisha kuikata simu ile. Mipango yake ilikuwa ikiendelea kama kawaida, alikuwa akijitahidi kufanya kila njia na hata kutumia gharama zake zote ili mladi mwisho wa siku aweze kumpata Williams ambaye mpaka katika kipindi hakujua mtu huyo alikuwa mahali gani.
“Kila mtu anashindwa. Kwa nini? Kwa nini wanashindwa kumkamata na kumuua?” Bwana Robinson alijiuliza huku akionekana kuwa na hasira.
Maisha yake katika kipindi hicho yakaonekana kuwa katika wakati mgumu, hakutaka kukaa kwa raha na wakati Williams hakuwa amepatikana. Kuna kipindi kikafika, kipindi ambacho akaanza kujutia uamuzi ambao aliuchukua wa kuiteka ndege ile na kisha kuchelewa kuwaua watu wale. Kila wakati alikuwa akiuma meno yake kwa hasira, hakuonekana kuwa na furaha kabisa mpaka pale ambapo angehakikisha Williams anakamatwa na kuuawa tu.
Masaa yaliendelea kusogea mpaka pale ambapo akaonekana kuwa na presha mara baada ya kupigiwa simu kutoka getini kwamba alikuwa akiuliziwa na mapolisi ambao walikuwa wamefika mahali hapo. Bwana Robinson hakutaka kuamini kama polisi walikuwa wamefika mahali hapo, alichokifanya ni kuelekea katika chumba kilichokuwa na kompyuta ambazo zilionganishwa na kamera zote ambazo zilikuwa ndani ya nyumba ile na kisha kuanza kuangalia kamera ile ya mlangoni, polisi walikuwa wakimsubiri.
Bwana Robinson alikuwa akitetemeka kwa woga, tayari alijua fika kwamba watu walikuwa wamekwishajua kwamba yeye ndiye ambaye alikuwa nyuma ya kila kilichotokea. Kichwa chake kikaanza kufikiria ni mtu gani ambaye alikuwa amewaambia ukweli na wakati Wamarekani wote walikuwa wakijua fika kwamba Williams ndiye ambaye alikuwa akihusika katika kila kitu kuhusiana na mauaji yale.
Bwana Robinson akajitoa wasiwasi na kisha kuruhusu polisi wale kuingia ndani ya eneo la nyumba yake na kisha kutoka na kuanza kuongea nao. Katika kipindi hicho, polisi hawakutaka kusikia kitu chochote kile, walichokuwa wakikitaka ni kuondoka na Bwana Robinson kituoni tu. Bwana Robinson hakutaka kuuliza sababu yoyote ambayo ilimfanya kuchukuliwa na kupelekwa katika kituo cha polisi.
“Mnaweza kuniruhusu kuwasiliana na Mwanasheria wangu?” Bwana Robinson aliwauliza.
“Hakuna tatizo”
Bwana Robinson akachukua simu yake na kisha kuanza kumpigia mwanasheria wake, Freddy ambaye alikuwa akimtaka kufika katika kituo kikuu cha polisi hapo New York. Ingawa usoni alikuwa akionekana kutokuwa na wasiwasi lakini moyo wake ulikuwa katika hali tofauti kabisa, hakuwa na furaha, alikuwa na wasiwasi kupita kawaida huku akijifikiria ni mtu gani ambaye alikuwa amewaambia polisi kuhusiana na kile alichokifanya.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna mtu. Au Hughes alinisaliti? Hapana kwani kama mimi nipo matatizoni basio hata nae atakuwa kwenye matatizo. Au labda Simmon, lakini napo haiwezekani, wote wapo kwenye mchongo huu. Sasa atakuwa nani? Au Malik? Mmmh! Au Gilbert? Hapana. Au labda Sinclair” Bwana Robinson alijiuliza huku akiyataja majina ya watu waliokuwa na fedha nyingi pamoja na viongozi wa serikalini nchini Marekani hali ambayo ilionyesha kwamba ukiachilia yeye, kulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wamehusika katika mchongo huo.
Kifo cha Phillip kikaonekana kuwashtua Wamarekani hasa mara baada ya kugundua kwamba F.B.I walikuwa wamemleta Phillip, mtu ambaye alionekana kunusurika katika mauaji yale ya porini ambayo waliamini kwamba yalikuwa yamepangwa na Williams. Kila mtu ambaye alizipata taarifa za kifo juu ya Phillip alionekana kushttuka.
Kila mtu katika kipindi hicho alikuwa akitaka kusikia mengi ambayo yalikuwa yamejiri kule msituni lakini kutokana na kifo cha Phillip, tayari wakaona kwamba kulikuwa na kitu juu ya tukio hilo. Mazingira ya ile ajali yalivyokuwa yameelezwa, FBI wakapewa lawama zote ambazo zilistahili kutolewa kutoka kwa wananchi hao ambao walionekana kuwa na hasira kali.
Maswali yakaanza kumiminika vichwani mwa watu kwamba ni kwa namna gani Phillip alikuwa amenusurika kuuawa na watekaji wale ambao walikuwa wamewateka katika ndege ile. Katika kila swali ambalo walikuwa wakijiuliza mahal;i hapo, walikosa jibu kabisa kwani waliamini kupata kila kitu kutoka kwa Phillip ambaye kwa kipindi hicho alikuwa amekwishakufa.
Fujo zikaonekana kuanza kutokea katika kipindi ambacho watu walipofahamu kwamba mtu ambaye alikuwa akihitajik sana katika kipindi hicho, Williams alikuwa ameletwa nchini Marekani kinyemela bila mtu yeyote kufahamu sababu zilizopelekea jambo kama lile kutokea. Taarifa hizo ndizo ambazo zikawafanya watua kuanza kuandamana zaidi.
Watu walitaka Williams auawe, hakukuwa na sababu ya mtu huyo kufichwa na kuendelea kuvuta pumzi ya dunia hii na wakati katika kipindi hicho walikuwa wameipoteza timu yao ambayo walikuwa wakiipenda sana. Kadri muda ulivyozidi kuongezeka na ndivyo ambavyo watu walivyokuwa wakizidi kuongezeka zaidi na zaidi mitaani huku wakiwa na mabango ambayo yalikuwa yakimtaka Williams ahukumiwe kifo.
Walichokifanya waandishi wa habari ni kuanza kuelekea katika nyumba ambayo walikuwa wakiishi Bwana Kurt na mpenzi wake, Latifa ambao walikuwa wazazi wa Williams ili kutaka kujua ukweli wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika kipindi hicho. Waandishi wa habari zaidi ya nane walikuwa wamekusanyika katika uwanja wa nyumba ile ambapo Bwana Kurt akatoka huku akiwa pamoja na mpenzi wake, Latifa na mpenzi wa Williams, Latifa.
“Unajua chochote kuhusu uwepo wa mtoto wako nchini hapa?” Mwandishi mmoja wa habari alimuuliza.
“Hapana. Hiyo taaruifa niliipata kwenye vyombo vya habari kama mlivyoandika” bwana Kurt alisema.
“Kwa hiyo hauna uhakika kama yupo kweli nchini hapa?”
“Hatujui chochote kile. Tungependa sana kumuona mtoto wetu na kuongea nae” Bwana Kurt alisema huku akionekana kuwa mwingi wa huzuni.
Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kwa wakati huo kilikuwa kikifanyika chini ya FBI hata kabla ya kukabidhi mafaili yao yote kwa polisi ambao wangetakiwa kushughulikia kesi hiyo. Baada ya siku moja kupita, Bwana Kurt, Bi Latifa na Celine wakaitwa kwa ajili ya kuongea na Williams kama kumsalimia na si kumuuliza chochote kuhusiana na kila kilichotokea.
“Kumbukeni. Hatutaki aulizwe chochote kile kuhusiana na kilichotokea Thailand” Mkuu wa polisi aliwaambia.
“Hakuna tatizo”
“Kuna vipaza sauti vyetu ambavyo tumeviweka, hivyo vitatufanya kusikia maongezi yenu yote. Msiongee chochote kuhusiana na Thailanda. Mna dakika kumi tu” Mkuu yule aliwaambia huku FBI wakiwa pembeni yao.
Bwana Kurt, mpenzi wake pamoja na Celina wakaingia ndani ya chumba kile kidogo ambacho kilikuwa na vioo sehemu zote. Kitu cha kwanza walichokifanya ni kukumbatiana kwa furaha, hawakuamini kama siku hiyo wangeweza kumuona Williams kwa mara nyingine tena.
Wakakaa na kuanza kuongea, Bwana Kurt alimwambia wazi Williams kwamba hawakutakiwa kuongea kitu chochote kile ambacho kilitokea nchini Thailand kule msituni. Walichukua muda wa dakika tano kuongea na kisha Williams kuwaaga wazazi wake huku akitaka kutumia dakika tano zilizobakia kuongea na mpenzi wake, Celina.
Muda mwingi, wote wawili walikuwa wakilia huku wakiwa wameshikana mikono yao huku kila mmoja akitokwa na machozi. Katika kipindi hicho, kila mmoja alikuwa kimya, hakukuwa na mtu ambaye alizungumza chochote zaidi ya kukaa kimya tu na kuangaliana zaidi. Dakika ziliendelea kwenda mbele lakini hakukuwa na aliyeongea chochote kile, muda wote walikuwa wakiangaliana tu.
“Nakupenda” Hatimae Williams akaamua kuvunja ukimya.
“Nakupenda pia” Celina alijibu na kisha kutakiwa kuondoka mahali hapo na polisi.
Siku ziliendelea kukatika mpaka siku ambayo mazishi ya Phillip kufanyika katika makaburi ya Melphine Land ambayo yalikuwa pembeni kidogo ya jiji la New York, makaburi ambayo walikuwa wakizikwa watu maarufu na watu waliokuwa na fedha za kutosha. Kila mtu ambaye alikuwa akiyaangtalia mazishi yake yalikuwa yakimfanya kulia na kuongeza chuki kwa Williams.
Mpenzi wake Phillip, Rebecca, muda wote alikuwa akilia, moyo wake uliumia kupita kawaida. Moyoni hakuamini, hakuamini kabisa kama Williams yule ambaye alikuwa akimfahamu sana kama rafiki mkubwa wa mpenzi wake ndiye ambaye alikuwa amefanya mambo yale yote. Chuki kubwa moyoni mwake juu ya Williams ilikuwa imeukumba moyo wake.
Siku zikaendelea kukatika mpaka siku ambayo ikapangwa kwamba ilikuwa siku ya kesi kusikilizwa. Kila mtu alikuwa makini kwa wakati huo, kila mtu alikuwa akitaka kuiona kesi hiyo ambayo ilikuwa ikisikika sana kutawala vichwa vya habari katika magazeti mengi duniani. Watu wakaonekana kushtuka sana hasa mara baada ya kugundua kwamba mwanasheria wa FBI, Frankie ndiye ambaye alikuwa akimsimamia Williams.
Hali ile ikawafanya watu kutokuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea, tayari FBI wakaonekana kuwa upande wa Williams ambaye alikuwa akihitajika kuhukumiwa kifo muda wowote ule hasa mara baada ya kesi kusikilizwa. . Watu wakaanza kutembea na mabango ambayo yalikuwa yakielezea hasira zao ambazo walikuwa nazo juu Williams.
Siku ambayo kesi hiyo ilitakiwa kuanza ikasikilizwa huku polisi wakimtaka kilazima Bwana Robinson kuhudhuria mahakamani pale. Kitu ambacho watu walikielewa ni kwamba Bwana Robinson alitakiwa kuwa shahidi mkuu mahali pale kwani alionekana kufahamu mengi kuhusiana na mauaji yale ambayo yalikuwa yamefanyika msituni nchini Thailand.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesi ilipomaliza kusikilizwa, watu wakaruhusiwa kuondoka mahali hapo na Williams kupakizwa katika basi kubwa la wafungwa. Waandishi wa habari bado walikuwa wakiendelea kupiga picha kwa kila kilichoendelea kufanyika mahali hapo. Watu bado waliendelea kuchanganyikiwa, hawakujua ni sababu gani Bwana Robinson hakuwa miongoni mwa mashahidi na badala yake alikuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi katika kipindi chote.
“Mbona na yule mzee wamemkamata tena?” Mwanaume mmoja aliuliza.
“Sijui kwa nini. Hii kesi hadi sasa hivi inanichanganya sana. Wakili anayemsimamia Williams ni Frankie, wakili kutoka FBI. Mbaya zaidi, inasemekana Williams ana mashahidi wawili. Mmoja ni Mthailand ambaye yupo hospitali. Sasa huyo mwingine nikikwambia...utashtuka” Jamaa mwingine alimwambia mwenzake.
“Nani?”
“Mpelelezi Sam” Jamaa alitoa jibu lililomfanya mwenzake kushtuka
Watu walionekana kuchanganyikiwa, walikuwa na maswali mengi ndani ya vichwa vyao ambayo hayakuwa na majibu yoyote yale. Kwa mambo ambayo yalikuwa yakiendelea ndio ambayo yalikuwa yakiwachanganya zaidi. Kila mmoja alikuwa na hamu ya kuona Williams akihukumiwa kifo, lakini sasa kulikuwa na sababu gani ya FBI kumchukua wakili wao, Frankie na kutaka kumsimamia Williams huku mpelelezi ambaye alikuwa akiaminika, Sam akiwa mmoja wa mashahidi ambao walikuwa wakijipanga kumtetea Williams?
Maswali hayo yalikuwa yakiwachanganya sana, ukiachilia maswali hayo, pia kulikuwa na swali moja ambalo liliwafanya kujiuliza mengi sana, kukamatwa kwa Bwana Robinson napo kukaonekana kuwachanganya kupita kawaida. Kila mmoja alikuwa akijiuliza sababu ambazo ziliwafanya mapolisi kumakata Bwana Robinson lakini hawakupata jibu. Ilikuwa ni kwa nini bwana Robinson akamatwe na wakati yeye ndiye ambaye alitoa taarifa juu ya unyama ambao alikuwa ameufanya Williams msituni nchini Thailand? Kila swali ambalo walikuwa wakijiuliza vichwani mwao, wakakosa jibu.
Vyombo vya habari bado vilikuwa vikiendelea kuandika kuhusiana na kesi hiyo ambayo kwa wakati huo ilikuwa imeshika vyombo vingi vya habari duniani. Kwa siku ile ambayo kesi ilikuwa ikisikilizwa tu, iliahirishwa kwa siku kumi na nne na ndipo ilipotakiwa kuendelea kwa Williams kuongea yake na kisha mambo mengine kuendelea. Kila mtu kwa wakati huo alikuwa akiongea lake, lakini pamoja na kila mtu kusema yake, hakukuwa na mtu ambaye alihisi kwamba Williams hakuwa muuaji, wote walimuona kuwa mshtakiwa namba moja.
Mpelelezi Sam na Bwana Swan ndio ambao walikuwa wakipewa ruhusa ya kuongea na Williams huku wakimtaka kutokuwa na wasiwasi juu ya kesi ambayo ilikuwa ikiendelea mahali pale, alitakiwa kuamini kwamba alikuwa akienda kushinda kwa ushindi mkubwa, ila kitu ambacho alikuwa akitakiwa ni kuongea ukweli wote.
Pamoja na kuzungumza na Williams pia FBI walikuwa wakiendelea kufuatilia maendeleo ya Gong kule hospitalini. Hali yake kwa sasa haikuwa mbaya sana, alikuwa akizungumza japokuwa kwa tabu sana. Miguu yake miwili ilikuwa imevunjika na hivyo kuwekewa PoP ambayo ilikuwa na kazi ya kuonganisha mifupa yake ambayo ilikuwa imeachiana kwa kuvunjika.
Baada ya siku kumi na nne kufika, kesi ikatakiwa kuendelea tena na hivyo Williams pamoja na Bwana Robinson ambaye alionekana kutokuwa na kosa lolote kupelekwa mahakamani kwa mara nyingine. Siku hiyo watu wakaonekana kuwa na hasira kupita siku nyingine, ingawa siku hiyo walitakiwa kusikiliza maneno kutoka kwa mshatakiwa na hukumu kutolewa siku nyingine lakini watu walitaka kila kitu kimalizwe siku hiyo hiyo, kwao, Williams alionekana kuwa mtuhumiwa hata kama hawakusikiliza kitu chochote kutoka kwake.
Siku hiyo, watu wote ambao walikuwa na mabango ambayo yalikuwa yakimtaka Williams kuhukumiwa kifungo walikuwa wamesisitiziwa kutokuingia ndani ya mahakama hiyo, kwa wale ambao walichelewa kufika mahakamani na kutokuingia kutokana na umati mkubwa wa watu kuwa mahakamani, wakaomba kuwekewa televisheni nje kwa ajili ya kufuatilia kila kilichoendelea ndani ya mahakama ile na hivyo kuwekewa.
Saa 2:10 Williams alikuwa akiingizwa ndani ya mahakama ile huku akifuatiwa na Bwana Robinson ambaye muda mwingi alikuwa akionekana kuwa na mawazo kupita kawaida. Mara baada ya kufikishwa sehemu ambayo walitakiwa kukaa, hakimu wa mahakama hiyo, Bi Scolastica akaanza kuingia ndani ya mahakama hiyo huku watu wote mahakamani wakiwa wamesimama kama kuonyesha heshima kwake.
Mara baada ya hakimu kukaa kitini, watu wote wakatakiwa kukaa. Siku hiyo, minong’ono ya hapa na pale ilikuwa ikiendelea kusikika mpaka pale ambapo Williams akahitajika kuelekea kizimbani. Minong’ono ile ikasikika zaidi na zaidi, watu wakakunja nyuso zao huku watu ambao walikuwa wakifuatilia nje kupitia televisheni wakipiga kelele kwamba ahukumiwe. Baada ya muda wa sekunde kadhaa, hakimu akamtaka Williams kuelezea kilichotokea hata kabla hukumu haijasomwa.
Williams akakaa kimya kwa muda, akainamisha kichwa chake chini, alipokiinua, alikuwa akitokwa na machozi. Matukio ya nyuma ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yake yakaanza kujirudia kichwani kama mkanda wa filamu. Kila alipokuwa akimwangalia Bwana Robinson, Williams alikuwa akizidi kutokwa na machozi. Hapo ndipo ambapo Williams alipoanza kuhadithia kila kitu ambacho kilitokea mara baada ya kuondoka nchini Marekani na kuelekea nchini China.
Williams alielezea kwa uchungu kila kitu ambacho kilitokea huku machozi yakiendelea kumtoka kumaanisha kwamba alikuwa ameumizwa sana kwa kile ambacho kilikuwa kimetokea kule msituni. Williams alitumia dakika ishirini kuelezea matukio yote, alipomaliza, nusu na robo ya watu waliokuwa mahakamani walikuwa wakitokwa na machozi.
“Hicho ndicho kilichotokea. Nilitaka kumuua Bwana Robinson kwa sababu bunduki ile alikuwa amenipa yeye mwenyewe, na ninadhani alijua fika kwamba ilikuwa na risasi moja kwa hivyo hata kama angeniua mimi, Phillip angebaki hai na kama angemuua Phillip basi mimi ningebaki hai na hivyo kumfanya kuwa katika hali mbaya” Williams aliiambia mahakama.
Watu wote ambao walikuwa nje ya mahakama ile ambao walikuwa wakifuatilia katika televisheni za pale nje wakaanza kuyachana mabango yao, tayari mioyo yao ikaanza kubadilika, ukweli ambao alikuwa ameuongea Williams ulionekana kuwaumiza kupita kawaida, ukweli ukajulikana kwamba Bwana Robinson ndiye ambaye alikuwa amehusika na kila kitu kilichotokea nchini Thailand.
Mawakili hawakuwa na maswali yoyote yale ya kuuliza, wao wenyewe walionekana kuumizwa na kiile ambacho kilikuwa kimetokea, Williams akaruhusiwa kushuka kizimbani huku akilia kama mtoto jambo ambalo likaanza kuibua vilio pale mahakamani. Mara baada ya hakimu kufuta miwani yake, kwa kuwa Bwana Robinson nae alikuwepo mahali hapo, akaitwa kuja kuelezea kile kilichotokea.
“Kila alichoongea Williams ni uongo, tena uongo mkubwa. Hivi nitaweza vipi kuua?” Bwana Robinson aliuliza huku akiangalia kila kona mahakamani.
“Naomba nikuulize kitu Bwana Robinson” Wakili Frankie alisema.
“Uliza”
“Unauamini ulinzi wa Marekani?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndio nauamini”
“Unaamini kwamba mtu yeyote hawezi kupita kupita sehemu za kukagulia wasafiri bila ya kuwa na bunduki?”
“Ndio naamini”
“Sasa kama Williams alitumia bunduki hiyo, alipita nayo vipi katika sehemu hiyo?” Frankie aliuliza.
“Hata sijui alipita nayo vipi”
“Sawa. Kutokana na maelezo yako yanasema kwamba bunduki ile ni ya Williams, si ndio hivyo?” Frankie aliuliza.
“Ndio”
“Unakumbuka kwamba katika kipindi chako cha maisha yote umekwishawahi kuomba bunduki zaidi ya kumi na nne na kupewa kwa kisingizio cha moja moja kupotea?”
“Ndio. Nakumbuka”
“Unaikumbuka vizuri bunduki yako ya pili kuomba miaka kumi na sita iliyopita ambayo ulisema kwamba nayo ilipotea?”
“Hapana”
“Ngoja nikukumbushe. Mwaka 1996 saa 4:13 asubuhi ulikwenda kuchukua bunduki katika kituo cha polisi cha Bloocklyne kwa madai kwamba bunduki yako ya kwanza ilipotea. Siku hiyo ulivaa shati jeupe, tai ya blue pamoja na suti nyeusi. Usoni mwako ulikuwa umevaa miwani ya macho, mkononi ulikuwa na saa iliyoandikwa Vesco ambayo ilikuwa na gharama ya dola laki nane. Siku hiyo ulifika mahali hapo ukiwa na gari aina ya Ferarri ambalo lina gharama ya dola milioni tano, mpenzi wako, Jesca alikuwa ndani ya gari hilo. Bunduki ambayo uliinunua ilikuwa na namba 23YU. Ulipata kiburi cha kutumia bunduki hiyo kwa sababu ilitangazwa kwamba mafaili ya watu waliokuwa wamechukua bunduki kuanzia mwaka 1991 mpaka mwaka 2000 yalikuwa yamepotea kutokana na virusi viitwavyo Y2K kuzishambulia kompyuta pamoja na satelite. Kumbuka kwamba habari ile ilikuwa ni ya uongo, mafaili yote yalikuwepo na tulikuwa tunataka kujua ni wangapi ambao wangeweza kuzitumia bunduki zao vibaya. Wewe umekuwa ni mmoja wapo. Nimekukumbusha sana, bado na mimi pamoja na maelezo yangu tumedanganya?” Frankie aliuliza. Swali ambalo likamfanya kuwa kimya.
“Kuna ukweli wowote hapo?” Hakimu alimuuliza lakini Bwana Robinson alikaa kimya huku akiangalia chini.
“Kutokana na mpelelezi wetu, Sam, tumeweza kugundua kwamba haukuwa peke yako katika suala zima. Jambo hili haukulifanya peke yako bali ulilifanya pamoja na watu wengine kwa kushirikiana na kutengeneza mtandao wenu wa siri ulioitwa ‘HILI NI JIJI LA NEW YORK’ mkiwa na maana kwamba kila kitu ambacho kilitakiwa kutokea jijini New York basi kilikuwa ni lazima kipitie kwenu. Sam alipeleleza kwa makini sana na kupata makala zenu mbalimbali ambazo mlikuwa mmeziandika kwa kirefu sana juu ya mchakato mzima. Katika makala zenu hizo, kulikuwa na mipango yenu yote, kuiteketeza timu hii ilikuwa moja ya mipango yenu. Katika kundi lenu hilo kulikuwa na mtu kama Hughes, tajiri ambaye anamiliki viwanda kadhaa hapa Marekani, Simmon, mtu ambaye ni tajiri nae anamiliki timu ya kikapu ya Bolivian 67, pia kulikuwa na mtu kama Malik, tajiri wa kiarabu ambaye anamiliki vituo vya mafuta vya Getroleum, kuna mtu kama Gilbert ambaye ni gavana wetu wa jiji hili la New York. Mara baada ya kuona kwamba haitoshi, mkamchukua mmoja wa wafanyakazi wa FBI ambaye alikuwa akisaidia kwa nguvu zote, huyu aliitwa Sinclair. Hatujui ni kiasi gani mlikuwa mkimlipa, ila yeye ndiye aliwaambia kwamba Phillip alikuwa amekamatwa na hivyo kujipanga kwa ajili ya kummaliza, huku FBI wakijifanya hawajui kitu, wakawatuma watu wao kwenda kuwapokea uwanja wa ndege. Kwa mchezo alioucheza Sinclair, akawaongoza juu ya barabara ambayo gari lilikuwa likitumia, mkafanikiwa kuwatuma watu wenu na kuwauawa wote waliokuwa mule garini na vijana wenu kuchukua gari lile na kwenda kuwapokea na kisha kuelekea Manhattan kwa ajili ya kuwaua. Kuna uongo wowote hapo ambao nimeuongezea?” Frankie alisema na kuuliza lakini Bwana Robinson alikaa kimya.
“Niliposoma shule kipindi cha nyuma, mwalimu alipokuwa akiniuliza swali hasa kama nimefanya kitu fulani au sijafanya, nilipokuwa nikikaa kimya, aliniambia kwamba nilikuwa nakubaliana na alichokuwa amekisema. Wewe na wenzako mmefanya mambo hayo yote niliyosema na bila Sam kupeleleza kwa makini tungeweza kukwama kuwakamata. Mpango wote mlioufanya umejulikana na ningependa kukwambia kwamba watu wote ambao ulishirikiana nao katika mipango yenu wamekamatwa” Frankie alimwambia Bwana Robinson na kisha kumgeukia hakimu.
“Nadhani kila kitu kimekwenda sawa mheshimiwa, sidhani kama kutakuwa na umuhimu wa mashahidi. Kila nilichoelezea kimekuwa kinajitosheleza” Frankie alimwambia hakimu na kisha kurudi kitini.
Mahakama nzima ilikuwa kimya ikimwangalia Bwana Robinson kwa chuki kubwa, hawakuamini kwamba mzee yule ndiye ambaye alikuwa amefanya mambo yale yote na hatimae kumsingizia Williams ambaye alionekana kutokuwa na kosa lolote mahali hapo. Kila mtu akawa amegeuka kwa kipindi hicho, mambo ambayo alikuwa ameyafanya yalionekana kuwa makubwa na mabaya ambayo yaliwahi kutokea nchini Marekani.
Watu hawakuamini kama hata gavana wa jiji hilo nae alikuwa amehusika katika kutekeleza mpango wote ambao walikuwa wameufanya pamoja na matajiri wengine ambao walionekana kuwa vipenzi vya watu kutokana na misaada mbalimbali ambayo walikuwa wakiitoa kwa jamii. Sifa nyingi zikaenda kwa mpelelezi Sam ambaye alionekana kufanya kazi kubwa sana katika kipindi kichache.
Hakimu Scolastica akaifuata miwani yake na kisha kuiangalia mahakama na kuvuta kitabu kikubwa na kuanza kukisoma, alikisoma kwa muda wa dakika moja tena kifungu mpaka kifungu na kutoa hukumu nzito kwa wote ambao walikuwa wameufanya mpango mzima wa kuiteka ndege ile na kisha kuwaua wachezaji wale. Kwa Bwana Robinson pamoja na wenzake ambao walikuwa wakifuatilia huku wakiwa wamekamatwa ikaonekana kuwa adhabu kubwa lakini kwa wananchi inakonekana kustahili kabisa kwa vile ambavyo walikuwa wamevifanya.
“Kwa Williams, hakuonekana kuwa na kosa lolote lile, kila kitu kimewekwa wazi na mahakama ilisikia kila kilichoongelewa. Kesi kama hii ingeweza kuahirishwa na hukumu kutolewa siku nyingine lakini kutokana na kila kitu kuwa wazi na kutokuwa na umuhimu wa ushahidi, huku nitaitoa leo hii. Williams atakuwa huru kuanzia muda huu ila kwa Robinson na wenzake watachomwa na sindano za sumu mpaka kifo kitakapowakuta” Hakimu alisema na kisha kufunga kesi.
Mahakama nzima ikaanza kupiga kelele za shangwe, watu wengi wakaanza kumfuata Sam na kisha kuanza kumpongeza kwa kazi kubwa ambayo alikuwa ameifanya katika kipindi chote hicho. Kwa Williams, muda wote alikuwa amekumbatiana na Celine huku wote wakiwa wanalia kwa furaha, kipindi kile, hawakuamini kama kweli walikuwa pamoja kwa mara nyingine.
Familia ya wachezaji ambao walikuwa wameuawa wakaanza kumsogelea Williams na kisha kumkumbatia na kumpongeza kwa utu ambao alikuwa ameufanya wa kuwasaidia wachezaji wengine kama Bruce na Phillip ambao walikuwa wameuawa.
Mara baada ya kumaliza kila kitu, Williams na Celine pamoja a Bwana Sam wakaanza kuelekea hospitalini kwa ajili ya kumwangalia Gong ambaye katika kipindi hicho alikuwa akiendelea vizuri mpaka pale ambapo aliruhusiwa na kuanza kuishi pamoja na Williams ambaye akaanza kuichezea timu ya La Lakers huku akisaidiana na mmiliki wa klabu ya New Buckets kuifufufa upya kwa kuwafundisha vijana mbalimbali ambao walikuwa na hamu ya kuwa wachezaji wakubwa wa mchezo wa kikapu baadae.
Kila kitu ambacho alikuwa amekitaka Gong aliweza kukipata kwa wakati huo. Hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa nchini Marekani, nchi ambayo alikuwa akitamani sana siku aingie japo akae kwa siku moja na kuangalia mazingira. Williams hakutaka kumsahau mtu yeyote ambaye alionyesha ushirikiano wake katika kipindi cha nyuma. Alichokifanya ni kusafairi pamoja na Celine na Gong mpaka nchini Thailand na kisha kuonana na Wong, kijana ambaye alimsaidia kumpeleka kwenye meli iliyokuwa ikielekea Afrika japokuwa hakuwa amefika huko.
“Mbona umerudi tena? Afrika mambo magumu nini?” Wong alimuuliza Williams ambaye alikuwa akicheka tu.
“Unakumbuka uliniambiaje?” Williams alimuuliza.
“Nakumbuka nilikwambia ukipata nafasi na mimi nije Afrika ili niweze kuondoka na kwenda Ulaya au Marekani” Wong alimwambia Williams.
“Sawa. Nimekufuata ili tuondoke” Williams alimwambia Wong huku akiendelea kucheka.
“Kwenda wapi? Afrika? Meli bado hazijaja. Au unataka tutumie basi hapa mpaka Misri na kisha tuuvuke mfereji wa Suezi?” Wong alimuuliza Williams.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana. Nimekuja kukuchukua na kuelekea na wewe nchini Marekani” Williams alimwambia Wong.
“Acha utani bwana”
“Ndio hivyo. Jiandae, kila kitu kitakamilika baada ya siku kadhaa. Nimekwishaandaa kadi ya mwaliko kwa ajili yako. Utakuja kule na kukaa kwa miezi sita. Baada ya hapo, nitakuongezea zaidi na kukaa kwa mwaka mwingine huku ukifanya kazi sehemu mbalimbali ambazo nitakuwa nimekutafutia kwa ajili ya maisha yako. Usijali. Kipindi cha kwanza utakaa kwangu na kuendelea na maisha mpaka pale ambapo utaweza kuishi katika chumba chako mwenyewe. Huo ndio msaada pekee ambao nimeona nikusaidie kama nilivyokwambia” Williams alimwambia Wong ambaye hakuonekana kuamini.
“Inawezekana vipi na wakati wewe ni mwafrika?”
“Mimi ni mtu mweusi japokuwa nimezaliwa Marekani. Baba yangu ni Mmarekani. Unafuatilia mchezo wa mpira wa kikapu?” Williams aliuliza.
“Sio sana”
“Ulishawahi kumsikia Michael Jordan?”
“Yeah! Nimekwishawahi kumsikia na kuziona picha zake”
“Na umekwishawahi kumsikia Williams Kurt?”
“Yeah! Namsikia sana huyo jamaa japokuwa sijawahi kumuona”
“Huyo Williams Kurt ndiye mimi”
“Unasemaje?”
“Najua umenisikia. Jiandae na baada ya wiki moja tutaondoka kuelekea nchini Marekani” Williams alimwambia Wong ambaye alionekana kutokuamini.
Williams hakutaka kumuacha Wong hivyo hivyo, akamuachia kiasi cha dola elfu ishirini na kisha kuondoka na Celina kuelekea hotelini. Walichokifanya baada ya hapo ni kwenda nyumbani kwa Bi Thum ambaye alikuwa na maisha ya kimasikini na kisha kumshukuru kwa kila kitu ambacho alikuwa amewafanyia katika kipindi ambacho walikuwa mahali hapo.
“Unasema alikufa?” Bi Thum aliuliza kuhusu Phillip.
“Ndio. Alikufa kwenye ajali ya gari nchini Marekani” Gong alijibu na kisha kuelezea kilichotokea.
Siku hiyo wakakaa na kuyafurahia maisha mahali hapo kwa kula na kunywa huku Williams akiahidi kumtengenezea nyumba kubwa Bi Thum kama zawadi ya shukrani kwa kile ambacho alikuwa amewafanyia huku akimuachia kiasi cha dola elfu hamsini kama kumsaidia katika maisha yake huku akiahidi kumsaidi kila mwezi kwa kumtumia kiasi fulani cha fedha.
Kama ilivyopangwa na ndivyo ilivyotokea, baada ya wiki moja, wote wanne wakaanza safari ya kuelekea nchini Marekani huku Wong akionekana kutokuamini kama nae mzamiaji alikuwa akielekea nchini Marekani kwa njia ya halali.
Hiyo ndivyo ilivyokuwa. Mambo yote ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yao ya nyuma yakaonekana kuwa kama historia ambayo iliendelea kubaki katika kumbukumbu za maisha yao ya nyuma. Kila kitu kwa wakati huo kilikuwa kimebadilika, hawakutaka kufikiria kitu chochote kile katika maisha yao.
Ikaonekana kuwa furaha zaidi kwa Williams mara baada ya wazazi wake kuamua kwa moyo mmoja kwamba walitaka kuaoana na kuishi pamoja. Williams hakuamini, alichokifanya ni kutaka kufunga ndoa na Celine katika siku moja ndani ya kanisa moja pamoja na wazazi wake. Baada ya mwezi mmoja, harusi mbili za familia moja zikafanyika katika kanisa la St’Luke lililokuwa jijini New York na kisha fungate kwenda kula katika visiwa vya Hawaii hapo hapo nchini Marekani.
**********************************MWISHO***********************
0 comments:
Post a Comment