Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

JINI MWEUSI - 1

 







    IMEANDIKWA NA :Eric Shigongo



    *********************************************************************************





    Simulizi : Jini Mweusi

    Sehemu Ya Kwanza  (1)




    Sauti kubwa ya muziki ilikuwa ikisikika, huku watu wengi wakionekana kurandaranda huku na kule katika eneo maarufu la Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam. Japokuwa ilikuwa ni usiku wa manane, mandhari ya mahali hapo ilikuwa imechangamka mno utafikiri mchana.

    Taa za rangi mbalimbali zilikuwa zikimulika huku na kule, sauti kubwa ya muziki ikazidi kupachangamsha mahali hapo ambapo kulikuwa na baa kadhaa zilizojipanga ambazo zote zilikuwa zikikesha mpaka asubuhi.

    Idadi ya wanawake waliokuwa eneo hilo, ilikuwa kubwa ukilinganisha na wanaume. Wanawake wa kila rika, wasichana wadogo, wa makamo na wanawake watu wazima, walikuwa wakizungukazunguka huku na kule, tena wakiwa wamevalia mavazi ambayo yaliacha wazi sehemu kubwa za miili yao.

    Kama ndiyo mara yako ya kwanza kufika eneo hilo, ungeweza kudhani zile zama za Sodoma na Gomora zimerejea tena kwani uchafu mkubwa ulikuwa ukifanyika hadharani, huku kukiwa hakuna mtu anayejali, kila mmoja akiendelea na shughuli zake.

    “Psii! Psiii! Njoo basi anko, si unaniona nilivyo bomba?” nichukue mimi ukafurahi, hata ukitaka usiku kucha ni wewe tu na roho yako,” msichana mmoja alisikika akiongea kwa sauti ya kilevi, huku akipandisha juu kisketi kifupi alichokuwa amevaa, wakati akizungumza na mwanaume aliyekuwa ndani ya gari dogo, akitafuta sehemu ya kuegesha gari hilo.

    Mwanaume huyo aliposimamisha gari lake, wanawake wengine wengi walilizunguka gari lake na kila mmoja akawa anatangaza ‘biashara’ yake. Baada ya majadiliano yaliyochukua dakika chache, mlango ulifunguliwa, mmoja kati ya wale wanawake akaingia kwenye gari kisha likaondoka kwa kasi eneo hilo.

    Hali ilikuwa hivyohivyo, magari mengi ya kila aina yakawa yanakuja eneo hilo na kuondoka yakiwa na wanawake hao ambao bila hata kuuliza, ungeweza kugundua kwa urahisi kwamba walikuwa wakifanya biashara haramu ya ngono iliyokuwa inasifika mno katika eneo hilo.

    Wale ambao hawakuwa na magari, nao hawakuwa nyuma, walikuwa wakifika eneo hilo kwa teksi za kukodi, Bajaj au bodaboda huku wengine wakitembea kwa miguu. Baada ya makubaliano, kila mtu alikuwa akiondoka na wake. Kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo watu walivyokuwa wanazidi kuongezeka eneo hilo huku pilikapilika zikizidi kupamba moto.

    Saa tisa na dakika kadhaa za usiku, gari jipya la kisasa aina ya Volkswagen lenye rangi nyeusi liliwasili eneo hilo, kama kawaida akina dada hao walilikimbilia na muda mfupi baadaye, changudoa maarufu wa eneo hilo, Aisha au Ndembendembe kama wengi walivyokuwa wanamfahamu, alipanda kisha gari hilo likaondoka kwa kasi.

    Pilikapilika ziliendelea mpaka kulipoanza kupambazuka ambapo watu walianza kupungua na ilipofika majira ya saa kumi na mbili za asubuhi, eneo lote lilikuwa kimya kabisa baada ya watu wote kuondoka.

    Kulipopambazuka kabisa, watu mbalimbali waliendelea na shughuli za kawaida eneo hilo kiasi kwamba kama ulikuwa mgeni, usingeweza kujua chochote kinachoendelea mahali hapo giza likiingia.

    Saa ziliyoyoma na hatimaye giza likaanza kuingia tena. Kama kawaida, watu kutoka sehemu mbalimbali wakaanza kumwagika kwa wingi eneo hilo, wanawake wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao nao wakaingia kazini kama kawaida. Mambo yalianza taratibu lakini kadiri muda ulivyokuwa unakwenda mbele ndivyo eneo hilo lilivyozidi kuchangamka.

    “Jamani leo Aisha Ndembendembe mbona hajafika mpaka saa hizi wakati yeye ndiye anayesifika kwa kuwahi?” changudoa mmoja alimuuliza mwenzake lakini hakuna aliyekuwa na jibu. Wakajua huenda kuna sehemu alikuwa amepitia, kila mmoja akaendelea na kazi ya kuwinda wateja mpaka usiku wa manane.

    Magari yaliendelea kumiminika kwa wingi kama kawaida na kila lililokuwa linafika eneo hilo, lilikuwa likiondoka na changudoa. Saa tisa juu ya alama, lile gari lililofika eneo hilo siku moja iliyopita, Volkswagen la kisasa kabisa, lenye rangi nyeusi na vioo vyenye ‘tinted’, liliwasili na kuegesha pembeni.

    Kama kawaida, wanawake wa kila aina wasiopungua kumi walilizunguka na kuanza kujinadi kwa dereva ambaye alikuwa ameshusha kioo kidogo, mahali palipomtosha kuzungumza na watu wa nje tu ila siyo yeye kuonekana. Baada ya kuridhika na changudoa mmoja, Sikitu ambaye alikuwa akisifika kwa kupenda kupigana na machangudoa wenzake kugombea wanaume, aliingia na kukaa siti ya nyuma. Gari likaondoka kwa kasi na kutokomea kusikojulikana.

    Kama ilivyokuwa kwa Aisha Ndembendembe, Sikitu naye hakurejea tena tangu alipochukuliwa usiku huo. Hata hivyo, hakuna aliyetilia maanani sana, wenzao wakawa wanahisi wamepata fedha nyingi hivyo wanaendelea kuzitumia mpaka ziishe kama ilivyokuwa kawaida yake.

    Siku ya tatu iliwadia, kama kawaida ya eneo la Sinza Afrikasana, pilikapilika zilianza pale tu giza lilipoingia. Biashara ya ukahaba ikaendelea kufanyika waziwazi usiku kucha. Kama ilivyokuwa kwa siku mbili zilizopita, ilipofika majira ya saa tisa za usiku, Volkswagen nyeusi yenye vioo vya tinted iliwasili eneo hilo na kupaki pembeni.

    “Anko leo nichukue mimi, kila siku unanikataa unawachukua wenzangu, kwani mimi siyo mzuri? Cheki nilivyojazia,” alisema changudoa mmoja machachari ambaye wenzake walimbatiza jina la utani la Lily Mcharuko, akaendelea kumfanyia vituko dereva huyo mpaka alipomuoneshea ishara kwamba aingie ndani ya gari.

    Akaondoka naye na kutokomea kusikojulikana. Siku iliyofuatia, Lily hakuonekana kabisa wala lile gari halikuonekana kufika eneo hilo. Siku kadhaa baadaye, liliendelea kuja na kuchukua machangudoa wengine ambao baada ya kuchukuliwa, hawakuonekana tena eneo hilo, jambo lililoanza kuzusha hofu kwa wenzao.

    “Jamani mbona wenzetu wanapotea kimaajabu na hakuna mwenye taarifa zozote?” aliongea changudoa mmoja katika mkutano ambao haukuwa rasmi usiku mmoja, wakaanza kujadiliana kwani ilionesha dhahiri kuna jambo halikuwa sawa.

    “Lile gari jeusi lina nini? Mbona kila anayelipanda harudi tena hapa wala simu yake haipatikani tena?”

    “Jamani ee, wasiwasi wa nini? Huenda yule bosi anatoa fedha nyingi mpaka kila anayetoka naye anaamua kuacha kazi ya uchangudoa,” alisema changudoa mmoja na kushambuliwa vikali na wenzake ambao walimtaka kutoleta masihara wakati wenzao walikuwa wakizidi kupukutika.

    Mjadala mkali uliendelea na muafaka waliofikia, ilikuwa ni kwenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwani walishindwa kupeleka malalamiko hayo polisi kwani kazi yao haikuwa halali kisheria na mara kwa mara walikuwa wakisumbuana na polisi waliokuwa wanawavamia eneo hilo na kuwakamata. Kutokana na mtandao mpana waliokuwa nao machangudoa hao, habari zilisambaa kwa kasi kubwa.

    “Mpaka sasa wenzenu wangapi wamepotea?”

    “Wenzetu kumi na moja hawafahamiki walipo, kwa kweli hali ni mbaya sana, tunawaomba nyie waandishi wa habari mtusaidie kufikisha taarifa sehemu husika, tunakwisha jamani,” changudoa mmoja ambaye hakutaka jina lake wala sura vionekane, alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambao walifika eneo hilo baada ya habari kuanza kusambaa.

    Habari zilisambaa kama moto wa nyikani kuhusu kupotea kimaajabu kwa machangudoa hao ambao walikuwa wakichukuliwa na mtu aliyekuwa anaendesha gari jeusi aina ya Volkswagen.

    Ndugu wa waliopotea walianza kujitokeza ambapo familia mbili kutoka Tandale Kwa Mtogole zilidai kupotelewa na mabinti zao wawili kwa siku mbili tofauti. Familia hizo zilipotoa picha ya watoto wao, machangudoa wenzao waliwatambua kuwa ni wenzao.

    “Mungu wangu, kumbe mwanangu alikuwa anafanya uchangudoa?” mwanamke mmoja aliangua kilio kwa nguvu kwenye eneo hilo baada ya machangudoa kadhaa kukiri kumfahamu binti yake na kueleza kuwa alikuwa mwenzao.

    “Alikuwa ananiaga anasema anafanya kazi kiwanda cha soda na kila siku anapangiwa shifti za usiku,” aliendelea kueleza mwanamke huyo huku akilia kwa uchungu mno. Mambo mengi yalizidi kufichuka ambapo ndugu wengine waliendelea kujitokeza na kueleza kupotelewa na ndugu zao.

    Hata hivyo, kati ya waliopotea, ni ndugu wa wasichana wanne tu ndiyo waliojitokeza na kukiri hadharani kupotelewa na ndugu zao.

    Utambulisho wa wasichana wengine waliopotea ulikuwa mgumu kwani hakukuwa na taarifa zozote za kina lakini kutokana na habari hiyo kuanza kutawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ukweli ulizidi kufichuka kila kukicha na kuzidi kuwashangaza wengi kuhusu wanawake waliokuwa wakijihusisha na biashara ya uchangudoa na kilichokuwa kinawapata.







    Wasichana wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao au maarufu kwa jina la machangudoa katika eneo la Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam, wanajikuta katika wakati mgumu baada ya wenzao kuanza kupotea mmoja baada ya mwingine katika mazingira ya kutatanisha.

    Kinachozidi kuzua utata, kila anayepotea, inaonesha kwamba mara ya mwisho alichukuliwa na mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, ambaye alikuwa akienda eneo hilo usiku wa manane.

    Awali walidhani mwanaume huyo huwapa fedha nyingi machangudoa anaotoka nao kiasi cha kuwafanya waachane na biashara hiyo lakini kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele ndivyo hofu ilivyoanza kuwaingia ndani ya mioyo yao. Tayari machangudoa kumi na moja wamepotea katika mazingira ya kutatanisha baaada ya kuchukuliwa na mwanaume huyo aliyekuwa anakuja na gari jeusi lenye vioo vyenye tinted.

    Taarifa za kupotea kwa machangudoa hao zimeanza kuripotiwa na vyombo vya habari ambapo polisi wanalazimika kuingilia kati na kuanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya wasichana hao waliopotea na mtu aliyekuwa anawachukua. Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

    Miongoni mwa wasichana waliopotea, ni wanne tu ndiyo ambao ndugu zao walijitokeza na kutoa vithibitisho vyote vilivyoonesha kwamba wao ni ndugu zao, huku wote wakikiri kwamba hawakuwa wakijua mabinti hao walikuwa wanafanya kazi ya ukahaba. Uchunguzi wa kina uliendelea kufanyika kupata utambulisho wa wasichana wengine ambao bado walikuwa hawafahamiki walipo.

    Maafisa wa polisi hususan kutoka kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai walikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha wanapata taarifa zote kuhusu wasichana hao na mtu aliyekuwa anatajwa kuhusika na kutoweka kwao.

    Mitego iliwekwa kila sehemu, kuanzia kwenye barabara zote zilizokuwa zinaingia na kutoka eneo la Sinza Afrikasana, kwenye gesti bubu zilizokuwa zimetapakaa eneo hilo na kwenye maeneo yote ambayo biashara ya uchangudoa ilikuwa ikifanyika.

    Maafisa usalama wa kike waliokuwa wamepikwa vizuri kimafunzo, walipandikizwa katika kundi la machangudoa kwa lengo la kufuatilia kwa karibu kila kilichokuwa kinaendelea ili kuujua ukweli uliokuwa umefichika nyuma ya pazia.

    ***

    “Jamani kwani Nancy yuko wapi? Siku ya pili hahudhurii kwenye group discussion (majadiliano ya vikundi).” “Labda tuwaulize wenzake wanaokaa pamoja hosteli, eti Neema, shosti wako yuko wapi?” “Mh! Kwa kweli sijui alipo, mara ya mwisho aliondoka karibu siku nne zilizopita akasema anaenda kumtembelea shangazi yake Mabibo na atalala hukohuko, hajarudi mpaka leo.”

    “Kwani namba yake ya simu si unayo?” “Ninayo ndiyo lakini hapatikani, kila mara najaribu kumpigia lakini hapatikani.” “Mh! Sasa itakuwaje?” “Kwani umeshaenda kutoa taarifa kwa Dean of Students (Mlezi wa wanachuo)?” “Hapana, labda tukitoka hapa ndiyo niende.”

    “Fanya hivyo, inawezekana amepata matatizo dada wa watu hakuna anayejua,” wanachuo wa Chuo Kikuu cha Ustawi wa Jinsia, walikuwa wakijadiliana jioni moja wakiwa kwenye ukumbi maalum wa majadiliano, baada ya kutomuona mwanachuo mmoja, Nancy Emanuel kwa siku kadhaa, jambo ambalo halikuwa kawaida yake. Baada ya majadiliano hayo ya vikundi kumalizika, rafiki mkubwa wa msichana huyo, Neema Timbuka, alifanya kama alivyoshauriwa na wenzake, akaenda kutoa taarifa kwa Dean of Student wa chuo hicho, Profesa Sijaona Matiko.

    “Umesema mara ya mwisho aliondoka lini?” “Aliondoka Jumamosi usiku, muda wa kama saa mbili hivi usiku.” “Alisema anakwenda wapi?” “Alisema anaenda kumsalimia shangazi yake Mabibo na kwamba angelala hukohuko. “Alikuwa amevaaje?”

    “Alivaa gauni la zambarau lakini kwenye mkoba wake alikuwa na nguo nyingine,” alisema mwanachuo huyo, Profesa Sijaona akawa anaandika maelezo yote kwenye kitabu maalum kwa ajili ya kuanza ufuatiliaji. Baada ya kuchukua taarifa zote muhimu, Profesa Sijaona aliamuahidi kuwa kwa sababu muda ulikuwa umeenda, kesho yake asubuhi ataanza kulishughulikia suala la mwanachuo huyo.

    Neema akaondoka na kurudi hosteli. Muda mfupi baada ya mwanachuo huyo kuondoka, wanachuo wengine wawili nao walienda kwa mlezi huyo wa wanachuo, nao wakiwa na taarifa za kutoonekana kwa mwenzao, Sarafina Mshana kwa zaidi ya siku tano huku namba ya simu ikiwa haipatikani wala kukiwa hakuna taarifa zozote juu ya mahali alipo.

    “Alipoondoka alisema anakwenda wapi?” “Alisema anaenda klabu kucheza muziki na kuanzia hapo hakurudi tena wala simu yake haipatikani hewani,” alisema mmoja kati ya wanachuo hao, jambo lililomshangaza sana Profesa Sijaona. Akahisi lazima kuna jambo lilikuwa linaendelea nyuma ya pazia, ikabidi aanze kushughulikia suala hilo jioni hiyohiyo kwani aliona kesho yake atakuwa amechelewa. Harakaharaka akatoka na kuwasha gari lake, breki ya kwanza ilikuwa ni kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama kilichokuwa jirani na chuo hicho, akateremka kwenye gari na kwenda moja kwa moja mpaka ndani ya kituo hicho.

    Kwa kuwa alikuwa akifahamiana vyema na mkuu wa kituo hicho, aliingia moja kwa moja mpaka ofisini kwake. “Vipi mzee mwenzangu, mbona mbiombio muda huu?” “Nina tatizo afande, wanachuo wangu wawili hawafahamiki walipo, nahitaji msaada wako,” alisema Profesa Sijaona akiwa bado hajakaa, mkuu huyo wa kituo akamtaka kukaa kwanza ili wazungumze vizuri.

    Akaanza kumhoji mazingira ya wasichana hao walivyopotea ambapo profesa huyo alimueleza kila kitu kama alivyokuwa amechukua maelezo kutoka kwa marafiki wa wanachuo hao waliokuwa wamepotea. “Unajua hivi sasa kuna wimbi la kupotea kwa wanawake katika mazingira ya kutatanisha lakini taarifa tulizonazo ni kwamba ni machangudoa ndiyo waliopotea, tena wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao kwenye Kituo cha Sinza Afrikasana,” alisema mkuu wa kituo, Profesa Sijaona akashtushwa na taarifa hizo.

    Mkuu wa kituo akaendelea kumueleza jinsi walivyokuwa wakihangaika kumtafuta mwanaume ambaye inadaiwa ndiye aliyekuwa akiwanunua machangudoa hao na kutokomea nao kusikojulikana. Waliendelea kujadiliana, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa cha Profesa Sijaona na kuhisi kuwa huenda wanachuo wake nao walikuwa wakijihusisha kwenye biashara ya uchangudoa, jambo ambalo alikuwa akisikia minong’ono kwa muda mrefu ingawa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja.

    “Kalete picha zao ili machangudoa wanaoisaidia polisi waweze kuwatambua kama ni miongoni mwao au la,” alisema mkuu wa kituo na bila kupoteza muda, Profesa Sijaona alitoka na kuwasha gari lake, akarudi chuoni haraka ambapo alichukua picha mbili kama alivyoelekezwa na kurudi kituoni hapo. Akazikabidhi na kupewa maelezo kwamba afike asubuhi kwa ajili ya kupata majibu ya kilichoendelea.

    Kesho yake asubuhi, Profesa Sijaona aliwahi kuripoti kazini kisha muda mfupi baadaye, akaondoka kuelekea Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ambapo alikutana na mkuu wa kituo ambaye alimpa maelezo yaliyomshangaza na kumshutua mno.

    “Tumefanya uchunguzi na machangudoa wamewatambua wote wawili kuwa ni wenzao na wamekuwa wakifanya biashara haramu ya kuuza miili yao kwa kipindi kirefu ingawa nao walikuwa hawajui kwamba ni wanachuo,” alisema mkuu wa kituo, Profesa Sijaona akasimama na kumsogelea mkuu wa kituo, macho yakiwa yamemtoka pima.





    Tayari machangudoa kumi na moja wamepotea katika mazingira ya kutatanisha baaada ya kuchukuliwa na mwanaume huyo aliyekuwa anakuja na gari jeusi lenye vioo vyenye tinted . Taarifa za kupotea kwa machangudoa hao zimeanza kuripotiwa na vyombo vya habari ambapo polisi wanalazimika kuingilia kati na kuanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya wasichana hao waliopotea na mtu aliyekuwa anawachukua. Hata hivyo , wakati uchunguzi wa kina ukiendelea kufanyika , taarifa za kupotea kwa baadhi ya wanachuo wa kike zinaanza kusikika na kuongeza hofu kwenye jamii . Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO Baada ya kupokea taarifa za kupotea kwa wanachuo wawili wa Chuo Kikuu cha Ustawi wa Jinsia, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama alishirikiana na maafisa upelelezi wa kituo hicho kujaribu kukusanya taarifa zinazoweza kuwasaidia kujua mahali walipo wasichana hao. Kwa kutumia picha za wanachuo hao, waliwahoji baadhi ya wanawake waliokuwa wanafanya biashara ya kuuza miili yao ambapo katika hali ya kushangaza, walionesha kuwatambua na kueleza kuwa walikuwa ni wenzao katika biashara ya ukahaba. Wanachuo wangu hawafanyi biashara ya ukahaba afande, utakuwa umechanganya ,” alisema Profesa Sijaona lakini mkuu huyo wa kituo akaendelea kumsisitiza kwamba hakuwa na sababu yoyote ya kuwatetea kwani wanachuo wengi siku hizi wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo . “ Huwa tukiendesha msako wa machangudoa usiku , tunawanasa wengi ambao ni wanachuo, ukiwauliza wanasingizia kwamba fedha za mikopo zimechelewa kutoka , ” mkuu wa kituo alimtolea ufafanuzi, Profesa Sijaona akajikuta akiishiwa kabisa nguvu . Kwake aliiona hiyo kuwa skendo kubwa kwake hasa kutokana na ukweli kwamba yeye ndiye aliyekuwa mlezi na mshauri wa karibu wa wanachuo. Akajihisi aibu kubwa ndani ya moyo wake huku akili yake ikikataa kuukubali ukweli . Muda mfupi baadaye, taarifa zilifika kwenye vyombo vya habari na kuendelea kusambaa kwa kasi ya moto wa nyika , kila aliyekuwa akisikia habari hizo alishindwa kuamini kwamba wasichana waliokuwa wanasoma vyuo vikuu wanaweza kuwa wanajihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao . “ Ama kweli Mungu akiamua kukuumbua hakuna cha kumzuia , sasa kama hao wazazi wao wanajua wapo chuoni kusoma kumbe kazi yao ni kujiuza ?” wanawake wawili walikuwa wakijadiliana baada ya kumaliza kuangalia taarifa ya habari iliyokuwa inaeleza kuhusu wanachuo wawili waliotoweka baada ya kuchukuliwa na mtu asiyejulikana wakati wakifanya biashara ya kujiuza . Taarifa hizo ziliendelea kuwa gumzo kila sehemu na kabla hazijatulia, ziliibuka taarifa nyingine zilizozidi kuwashangaza wengi . Wanachuo wengine watatu wa Chuo Kikuu cha Mlimani nao waliripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, kila mtu akazidi kupigwa na butwaa. Kabla habari hizo nazo hazijatulia, zilikuja taarifa nyingine ambazo zilieleza kuwa kati ya machangudoa kumi na moja waliopotea , wawili ambao bado walikuwa hawajatambuliwa , walikuwa ni wanachuo wa Chuo Kikuu cha Uhasibu ambao nao walipotea katika mazingira yaleyale kama wenzao . “ Jamani hawa wanachuo wa siku hizi wamekumbwa na nini? Badala ya kuhangaikia elimu ili wapate digrii za maana wao wanajishughulisha na uchangudoa , tunajenga taifa gani ?”“ Wewe umechelewa kujua tu , unafikiri wameanza leo biashara ya uchangudoa? Mbona tangu kipindi kirefu tu wanachuo wa kike walikuwa wakijiuza, hasa ‘ bumu ’ zikichelewa kutoka ndiyo mchezo wao, ” watu waliokuwa wamekusanyika pembeni ya kituo cha polisi cha Kijitonyama walikuwa wakijadiliana kwani hali ilionekana kuwa tete. Vyombo vya habari navyo vikatawaliwa na habari hizo za wanachuo wa kike kufanya biashara haramu ya kuuza miili yao badala ya kusoma kama walivyotumwa na wazazi wao. Magazeti pendwa nayo hayakuwa nyuma , kurasa za mbele zikawa zinapambwa na picha za wanachuo hao waliopotea na habari zao kwa undani. Habari ilibadilika kabisa kutoka kupotea kwa machangudoa mpaka wanachuo kufanya ukahaba. Kila mtu alikuwa akizungumza lake, wapo waliokuwa wakiwalaumu wazazi kwa kushindwa kuwalea watoto wao kwenye maadili mazuri mpaka kufikia hatua ya kujiuza na wengine walikuwa wakiwalalamikia viongozi wa vyuo vikuu kwa kuwaachia uhuru wanachuo mpaka kufikia hatua ya kwenda kujiuza usiku bila mtu yeyote kujua . Upelelezi wa kina uliendelea kila mahali kuhakikisha mwanaume aliyekuwa akihusishwa na kupotea kwa machangudoa hao anapatikana na kuwekwa chini ya ulinzi . Hata hivyo , kazi haikuwa nyepesi kama polisi walivyodhani kwani kuanzia siku ya kwanza walipowapandikiza polisi wa kike ambao walikuwa wakivaa kama machangudoa, lile gari jeusi lililokuwa linatumiwa na mwanaume huyo halikuonekana tena eneo hilo. Hata kwenye maeneo mengine ambayo machangudoa walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu , halikuonekana gari jeusi wala mwanaume huyo, hali iliyosababisha ugumu mkubwa wa kuupata ukweli wa kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia. “ Kama angekuwa anawaua si lazima maiti zao zingeonekana?” “ Ni kweli kabisa lakini hakuna taarifa zozote za kuonekana maiti wala wanawake hao waliopotea . ” “ Inabidi upelelezi uongezwe, haiwezekani mtu mmoja atusumbue kichwa kiasi hiki , ” maafisa wa ngazi za juu wa polisi walikuwa wakijadiliana ndani ya ofisi ya mkuu wa polisi kuhusu kilichotokea. Upelelezi uliongezwa maradufu , mashushushu wengi wakamwagwa kwenye kumbi za starehe na kwenye madanguro yote yaliyokuwa yanafahamika na yale yasiyofahamika ili kuhakikisha mhusika anapatikana. “ Haloo ! Haloo ! Koplo Jenifa hapa , ova . ” “ Tunakupata Koplo Jenifa, ova . ” “ Nipo hapa Afrika Sana, kuna gari jeusi linakuja mbele yangu , linafanana na maelezo ya gari la mtuhumiwa namba moja, ova !”Askari walikuwa wakiwasiliana moja kwa moja na mwenzao aliyekuwa amepandikizwa kuwa kama changudoa kwenye eneo la Sinza Afrika Sana ili kurahishisha kazi ya kumnasa mtuhumiwa. Baada ya taarifa hizo , polisi waliokuwa doria kwenye maeneo mbalimbali, walipeana taarifa haraka kwa kutumia simu za upepo na ndani ya muda mfupi, wote wakawa wanaelekea eneo hilo, huku kila mmoja akiwa makini kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa usiku huohuo . Gari jeusi la kisasa lilisimama eneo la Sinza Afrika Sana, ikiwa ni saa nane za usiku . Machangudoa waliokuwa wakiendelea na biashara yao kama kawaida, walipoliona tu gari hilo, walianza kutimua mbio huku wakipiga kelele kwamba muuaji amewasili tena . Hakuna aliyekuwa tayari kuchukuliwa na mtu huyo, ndani ya dakika chache, machangudoa wote wakawa wamejikusanya upande wa pili wa barabara huku wakisikika wakipiga kelele za kumlaani mwenye gari hilo ambaye mpaka muda huo hakuwa ameteremka garini wala kushusha vioo . Waliobaki eneo hilo walikuwa ni mashushushu pekee ambao kwa kuwatazama , ungeweza kudhani ni machangudoa. Muda mfupi tu baadaye, magari manne ya polisi yakiwa na askari wenye silaha, yalivamia eneo hilo kutoka kila upande na kulizingira gari hilo, wale machangudoa wakawa makini kutaka kuona kitakachotokea . Polisi wakashuka kwenye magari yao na kulizunguka gari hilo, kila mmoja akiwa ameiweka bunduki yake tayari kwa chochote.





    Kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa wanawake waliokuwa wakifanya biashara haramu ya kuuza miili yao , maarufu kama machangudoa , kunalitingisha Jiji la Dar es Salaam hasa maeneo ya Sinza Afrika Sana , biashara hiyo ilipokuwa ikifanyikia . Kinachozidi kuzua utata , kila anayepotea, inaonesha kwamba mara ya mwisho alichukuliwa na mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, ambaye alikuwa akienda eneo hilo usiku wa manane . Awali walidhani mwanaume huyo huwapa fedha nyingi machangudoa anaotoka nao kiasi cha kuwafanya waachane na biashara hiyo lakini kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele ndivyo hofu ilivyoanza kuwaingia ndani ya mioyo yao . Tayari machangudoa kumi na moja wamepotea katika mazingira ya kutatanisha baaada ya kuchukuliwa na mwanaume huyo aliyekuwa anakuja na gari jeusi lenye vioo vyenye tinted . Taarifa za kupotea kwa machangudoa hao zimeanza kuripotiwa na vyombo vya habari ambapo polisi wanalazimika kuingilia kati na kuanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya wasichana hao waliopotea na mtu aliyekuwa anawachukua. Hata hivyo , wakati uchunguzi wa kina ukiendelea kufanyika , inakuja kubainika kuwa wengi kati ya machangudoa waliopotea , walikuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu , jambo linalowashangaza wengi na kuzua gumzo kubwa. Mipango ya kumnasa mhusika bado inaendelea lakini kazi haiwi nyepesi kama watu walivyodhani . Upande wa pili , historia ya kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu inaelezewa . Wanafunzi wenzake wanamtania na kumuita Zinja kwani alikuwa akifanana na binadamu wa kale. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Kwa kuwa sasa Dickson Maduhu alikuwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi katika Shule ya Tosamaganga aliyokuwa akisoma , alipunguza matukio ya kuwajeruhi wenzake waliokuwa wakimtania na kumuita jina la Zinja . Taratibu akaanza kulizoea jina hilo ambalo liliendelea kuwa maarufu mno miongoni mwa wanafunzi wenzake na walimu. Kiumri, Dickson alizidi kuwa mkubwa na kupevuka, sasa hisia za ujana zikawa zinamsumbua. Mara kwa mara alikuwa akiota ndoto nyevu usiku akiwa amelala, jambo ambalo ni kawaida kumtokea mvulana yeyote anayevuka kutoka hatua ya utoto kuingia utu uzima . Siku zilizidi kusonga mbele , kama ilivyokuwa kawaida ya shule hiyo ambayo ilikuwa ni ya wavulana tu, kila mwisho wa muhula, kulikuwa kukifanyika disko ambapo wanafunzi wa kike wa shule jirani ya Iringa Girls Secondary School walikuwa wakija kuwatembelea shuleni hapo na kucheza muziki pamoja. Japokuwa tangu ajiunge na kidato cha tano shuleni hapo kulifanyika disko zaidi ya mara nne, Dickson hakuwahi kushiriki hata mara moja. Hakuwa akipenda kuchanganyikana na wasichana na aliona kama hakukuwa na umuhimu wowote wa kucheza disko . Hata hivyo , baada ya mwili wake kupevuka, alianza kujiapiza kuwa disko ambalo lilikuwa likifuatia, lazima na yeye akacheze muziki na mmoja kati ya wasichana wengi wazuri waliokuwa wakija kutoka Shule ya Sekondari ya Iringa Girls. Tarehe ya disko hiyo ilipotangazwa tu , wanafunzi wengi walianza kujiandaa kwa kwenda kununua nguo za kuchezea muziki na wale ambao hawakuwa na uwezo, walikuwa wakianza kuazima kwa wenzao tangu mapema. Siku zilizidi kusonga mbele huku matangazo mengi yakibandikwa kwenye kuta za matangazo shuleni hapo . Wanafunzi wengi wakawa wanaisubiri kwa hamu siku hiyo . Dickson naye hakuwa nyuma, aliazima nguo nzuri kwa rafiki yake kipenzi , Lupakisyo Mwanyumba waliyekuwa wakilala chumba kimoja . Kwa kuwa hakuwa akijua kucheza muziki , mara kwa mara alikuwa akisubiri wenzake wote watoke chumbani humo na kuanza kufanya mazoezi ya kucheza huku akijiapiza kuwa siku hiyo lazima na yeye atafute msichana wa kucheza naye. “ Wenzangu wote wana wapenzi kutoka Iringa Girls, na mimi safari hii lazima nitafute mpenzi. Nitacheza naye muziki taratibu , nitamkumbatia na kusogea naye kwenye kona , kama hakuna mtu atakayekuwa anatuangalia , nitaanza kumtongoza, nimechoka maisha ya upweke , ” Dickson alikuwa akiwaza akiwa amelala kwenye kitanda chake cha juu ( double decker ) huku tabasamu pana likianza kuchanua kwenye uso wake . “ Vipi Zinja mbona unafurahi peke yako ?” “ Nafikiria jinsi nitakavyoopoa mkosho siku ya disko ,” alisema Dickson kwa lugha iliyokuwa imezoeleka shuleni hapo akimaanisha kuwa anasubiri kwa hamu jinsi atakavyopata msichana wa kumtongoza siku hiyo . Siku zilizidi kusonga mbele , hatimaye siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa iliwadia. Ilikuwa ni Jumamosi nzuri ambapo sauti kubwa ya muziki ilianza kusikika kuanzia mapema kutoka ndani ya ukumbi wa kulia chakula au maarufu zaidi kwa jina la DH (Dining Hall ), wanafunzi wa kiume wakawa wanapishana kwenda mabafuni. Hata wale ambao hawakuwa na utaratibu wa kuoga mara kwa mara kwa kisingizio cha baridi kali ya Iringa, siku hiyo walioga . Kila mtu akawa bize kujiandaa kwa kuvaa nguo nzuri na kujipulizia marashi , tayari kwa kupokea ugeni wa wanafunzi wa kike kutosha shule hiyo ya jirani. Majira ya saa saba za mchana , magari mawili yaliwasili shuleni hapo yakiwa yamejaa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iringa Girls au Zoo kama walivyokuwa wakijulikana zaidi . Wanafunzi wa kiume wa Tosamaganga waliokuwa wakiendelea kujiandaa, walianza kushangilia kwa nguvu, kila mtu akaacha kila alichokuwa akifanya na kukimbilia kwenye eneo magari hayo yalipokuwa yamepaki. Wasichana hao wakawa anateremka kwenye magari huku wakipokelewa kwa furaha na wenzao . Wale waliokuwa na marafiki zao wa kudumu , walichukuana na kutafuta sehemu tulivu huku wale ambao hawakuwa na marafiki kama Dickson, wakihangaika huku na kule kutafuta marafiki wa kucheza nao muziki kama fisi wanaotafuta mifupa. Dickson naye hakuwa nyuma, akiwa amevalia tisheti nzuri , pensi ya kisasa na raba nyeupe alivyoazimwa na Lupakisyo, alikuwa akizunguka huku na kule akijitahidi kutafuta msichana wa kucheza naye muziki . Hata hivyo , tofauti na wenzake ambao kila mtu alikuwa akipata rafiki , kila msichana ambaye Dickson alimsogelea, alikuwa akipiga kelele na kukimbia . “ Mbona wananikimbia ? Au kwa sababu nimenuna sana ?” alijiuliza Dickson na kuanza kulazimisha tabasamu kwenye uso wake lakini ilikuwa sawa na kazi bure . Mpaka muda wa kuingia disko unafika , Dickson bado hakuwa amefanikiwa kupata msichana wa kucheza naye. Hata hivyo , hakukata tamaa , naye aliingia kwenye ukumbi wa disko kwenda kujaribu kujaribu bahati yake kwani hisia zake zilikuwa hazijatulia kabisa, alichokuwa akikitaka ilikuwa ni kupata msichana wa kucheza naye, amkumbatie na kufurahi naye ili angalau roho yake itulie . Hata alipoingia kwenye ukumbi huo , haikuwa rahisi kupata msichana wa kucheza naye. Pensi aliyokuwa amevaa ilifanya vinyweleo vya miguuni vionekane vizuri na kumfanya azidi kutisha . Tisheti ya mikono mifupi nayo ilifanya vinyweleo vingi vilivyokuwa kwenye mikono yake vionekane, ukichanganya na jinsi sura yake ilivyokuwa, kila msichana alikuwa akimkimbia. Alilazimika kucheza peke yake muda wote huku roho ikimuuma sana , akafikia hatua ya kuwa anamkufuru Mungu wake kwa kumuumba akiwa tofauti na wenzake. Baadaye alipoona jitihada zake zote zimeshindikana, alitoka kabla hata muziki haujaisha na kwenda kujifungia bwenini ambapo alikuwa akiangulia kilio kwa uchungu, akiiona dunia yote mbaya . Mpaka muda wa disko kuisha , yeye bado alikuwa chumbani kwake , akiwa amejifunika blanketi mwili mzima ili wenzake wakirudi wasimuone kwamba alikuwa analia. Wakati wenzake wanatoka na kuhadithiana jinsi walivyofaidi kucheza muziki na wasichana, yeye alikuwa akiendelea kulia . Siku hiyo ilipita , akawa anaendelea kumkufuru Mungu mara kwa mara kwani hisia za kutamani kuwa na rafiki wa kike ziliendelea kumsumbua lakini hakuwa na uwezo wa kumpata. Siku zilizidi kusonga mbele , ikawa kila wasichana hao wakija kucheza disko , Dickson anaambulia patupu





    Jiji la Dar es Salaam linatingishika kutokana na wimbi la kupotea kwa wanawake waliokuwa wanafanya biashara haramu ya kuuza miili yao , maarufu kama machangudoa . Awali ilianza kama masihara lakini kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, machangudoa walizidi kupotea hadi idadi yao ikafikia kumi na moja . Kinachozidi kuzua utata , kila anayepotea, inaonesha kwamba mara ya mwisho alichukuliwa na mwanaume mmoja asiyejulikana. Mwanaume huyo aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, alikuwa akienda eneo la Sinza Afrikasana usiku wa manane na kununua machangudoa ambao hawakurudi tena baada ya kuondoka naye. Awali machangudoa wengine walidhani mwanaume huyo huwapa fedha nyingi machangudoa anaotoka nao kiasi cha kuwafanya waachane na biashara hiyo lakini kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele ndivyo hofu ilivyoanza kuwaingia ndani ya mioyo yao . Baada ya taarifa za kupotea kwa machangudoa hao kuanza kuripotiwa na vyombo vya habari , polisi wanalazimika kuingilia kati na kuanza kufanya uchunguzi wa kina juu ya wasichana hao waliopotea na mtu aliyekuwa anawachukua . Hata hivyo , wakati uchunguzi wa kina ukiendelea kufanyika , inakuja kubainika kuwa wengi kati ya machangudoa waliopotea , walikuwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu , jambo linalowashangaza wengi na kuzua gumzo kubwa. Mipango ya kumnasa mhusika bado inaendelea lakini kazi haiwi nyepesi kama watu walivyodhani . Upande wa pili , historia ya kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu inaelezewa . Kutokana na mwonekano wake wa kutisha, wasichana wanamuogopa na kumkimbia kila anapojaribu kuwasogelea. Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Kitendo cha wanafunzi wa kike waliokuwa wanasoma shule ya jirani na aliyokuwa anasoma , Iringa Girls kumkataa na kumkimbia kila alipokuwa akijaribu kutafuta wa kucheza naye muziki kipindi walipokuwa wakitembelea shule yao , kilimuathiri sana kisaikolojia . Akawa anajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu huku wakati mwingine akifikia hatua ya kumkufuru Mungu wake kwa jinsi alivyomuumba tofauti na binadamu wengine. Kwa kuwa hisia za kimapenzi nazo zilizidi kumtesa , mara kwa mara akiota ndoto nyevu , aliendelea kuteseka huku akijaribu kuwashawishi hata wasichana waliokuwa wakifanya biashara ndogondogo shuleni hapo wakubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi. Kila alipokuwa akijaribu kutongoza, alikuwa akigonga mwamba kutokana na mwonekano wake uliokuwa ukimfanya aonekane kama mnyama wa porini . Hisia za kutamani kukutana kimwili na mwanamke zilipomzidi , alijikuta akianza kujihusisha na mchezo wa kujichua. Kila alipokuwa akienda bafuni kuoga , alikuwa akitumia muda mrefu akiwa amejifungia ambapo alikuwa akifanya mchezo huo mara kwa mara na kumaliza matamanio yake. Kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele , Dickson alionekana kuendelea kuufurahia mchezo huo , kiasi cha kufikia hatua ya kuwa anakwenda kuoga mara mbili hadi tatu kwa siku moja , bila kujali baridi kali ya eneo hilo. Siku zilizidi kusonga mbele , hatimaye wanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo wakaanza kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya sekondari . Kama ilivyokuwa kawaida , kabla ya kuingia kwenye kipindi cha mitihani, wanafunzi hao wa kidato cha sita walifanyiwa mahafali ya kuwaaga. Wanafunzi wa kike kutoka shule jirani ya Iringa Girls wakaalikwa kuja kujumuika na wenzao kufurahi pamoja, kucheza muziki na kutakiana heri kwenye mitihani yao . Safari hii Dickson hakutaka kabisa kuihangaisha nafsi yake kwa kujaribu kutafuta msichana wa kucheza naye muziki au wa kuanzisha naye uhusiano wa kimapenzi. Alishapata mbinu ambayo aliamini inamsaidia kutuliza hisia zake bila usumbufu . Mahafali yakafanyika na wakati wenzake wakiendelea kucheza muziki na wasichana hao, yeye alielekea bafuni kuoga . Baada ya hapo, alivaa vizuri na kutafuta sehemu tulivu, akaenda kukaa peke yake kwani hakupata ugeni wowote kutoka nyumbani kwao kama ilivyokuwa kwa wenzake ambao walitembelewa na wazazi , ndugu , jamaa na marafiki kwenye siku hiyo muhimu. Uduni wa maisha ya familia aliyotokea, ulikuwa kikwazo kingine kwenye maisha yake. Siku hiyo ilipita , maandalizi ya mitihani yakazidi kupamba moto na hatimaye , waliianza mitihani. Kutokana na uchungu aliokuwa nao ndani ya moyo wake, uliosababishwa na hali ngumu ya maisha ya nyumbani kwao na jinsi alivyokuwa anatengwa na kutaniwa na wenzake, Dickson au Zinja kama wenzake alivyozoea kumuita , aliamini kitu pekee kinachoweza kumkomboa na kuyabadili maisha yake ni elimu. Akatulia na kufanya mitihani yake yote kwa umakini mkubwa huku akimuomba Mungu wake amsimamie . Hatimaye alimaliza elimu ya sekondari na kurudi kijijini kwao , Ichenjezya mkoani Mbeya walikokuwa wakiishi wazazi wake. Alikaa nyumbani kwao kwa muda usiozidi miezi mitatu ambapo kila siku alikuwa akiendelea na mchezo wake wa kujichua kwani hata wasichana wa kijijini kwao nao hawakuwa wakimkubali kutokana na mwonekano wake na umaskini wa familia yao . Hatimaye matokeo ya kidato cha sita yalitoka na miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wamefaulu kwa kiwango cha juu, Dickson au Zinja naye alikuwemo . Alifurahishwa sana na matokeo hayo , wazazi wake nao wakafurahi sana kwani sasa walikuwa na uhakika kwamba mtoto wao huyo atawakomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini . Dickson alianza kufanya taratibu za kujiunga na chuo kikuu , japokuwa wazazi wake hawakuwa na uwezo kiuchumi, alibahatika kupata nafasi ya kipekee ya kusomeshwa na serikali kutokana na jinsi alivyokuwa amefaulu vizuri. “ Naenda kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,” alisema Dickson wakati akiwaonesha wazazi wake fomu alizotoka kuzifuatilia serikalini. Kila mmoja alifurahishwa mno na mafanikio aliyoyapata mtoto wao. Siku zilizidi kuyoyoma hatimaye siku ya kwenda kuripoti chuo kikuu ikawadia, wazazi wake wakamsindikiza mpaka kwenye Stendi ya Mabasi ya Vwawa ambapo alipanda basi la kuelekea jijini Dar es Salaam. Japokuwa hakuwa amewahi kufika jijini Dar es Salaam hata siku moja, aliamini atafika salama chuoni kwao . Saa kumi na mbili asubuhi , basi alilopanda liliianza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam. Baada ya safari iliyochukua saa nyingi , hatimaye aliwasili kwenye Stendi ya Mabasi ya Ubungo majira ya saa kumi na moja jioni . Akateremka kwenye basi pamoja na mizigo yake michache , akajaribu kuulizia njia ya kuelekea chuo kikuu ambapo alielekezwa na vijana ambao nao walikuwa wakimshangaa kwa jinsi alivyokuwa na mwonekano wa tofauti na watu wengine. Mwenyewe hakujali, akatoka mpaka nje ambapo alipanda daladala kama alivyoelekezwa na hatimaye akawasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alienda moja kwa moja kwenye ofisi za utawala ambapo alijiandikisha sambamba na wanachuo wenzake wa mwaka wa kwanza waliokuwa wamewasili siku hiyo . Kila mtu alikuwa akimshangaa kutokana na jinsi alivyokuwa anafanana na binadamu wa kale, mwili wake ukiwa na vinyweleo vingi vilivyomfanya atofautiane kabisa na binadamu wa kawaida. Hata hivyo , kwa kuwa alishataniwa sana na wenzake tangu akiwa sekondari , wala hakujali watu waliokuwa wanamshangaa . Baada ya kumaliza kujiandikisha , alipangiwa hosteli ambayo angekuwa anaishi kwa kipindi chote ambacho angeishi chuoni hapo. Wanachuo wenzake waliopangwa naye chumba kimoja , awali walikuwa wakiogopa kulala naye wakidhani angeweza kuwadhuru hasa nyakati za usiku lakini kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele , taratibu walianza kumzoea . Siku zikawa zinazidi kusonga mbele , Dickson akaanza kuwa maarufu kwa sababu ya mwonekano wake ambapo kama ilivyokuwa wakati akisoma sekondari , alipachikwa tena jina la Zinjathropus au kwa kifupi Zinja , likimaanisha binadamu wa kale. Mwenyewe hakujali sana , akawa anajitahidi kuikubali hali hiyo na kuiona kama ya kawaida . Mwili wake nao ulizidi kutanuka na kuwa mkubwa, hisia za mapenzi zikawa zinazidi kumtesa na licha ya kujitahidi kuendelea kujichua mara kwa mara , bado hamu yake ya kukutana kimwili na mwanamke, ilikuwa ikizidi kuongezeka kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele . Ikafika mahali , akawa hawezi tena kutulia , nafsi yake ilikuwa ikihitaji jambo moja tu, mwanamke wa kufanya naye ngono .



    Mipango ya kumnasa mhusika bado inaendelea lakini kazi haiwi nyepesi kama watu walivyodhani . Upande wa pili , kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu amehitimu kidato cha sita na kupata nafasi ya kuendelea na masomo ya chuo kikuu . Tayari ameshafika jijini Dar es Salaam alikojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam . Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Siku za mwanzo zilikuwa ngumu sana kwa Dickson chuoni hapo kwani kama ilivyokuwa kila mahali alipowahi kuishi, watu walikuwa wakimshangaa sana na kuanza kumtania kutokana na mwonekano wake uliokuwa tofauti kabisa na binadamu wa kawaida. Kama ilivyokuwa wakati akisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Tosamaganga , baadhi ya wanachuo wenzake walianza kumtania na kumuita jina la Zinjathropus au kwa kifupi Zinja , wakimaanisha binadamu wa kale . Hata hivyo , kwa kuwa sasa alikuwa na uzoefu wa kutaniwa na kuitwa majina mabaya, haikumuumiza sana , wanachuo wenzake wakawa wanaendelea kumshangaa na baadaye wakamzoea, maisha yakazidi kusonga mbele . Hata hivyo , bado hisia za mapenzi zilizidi kumsumbua Dickson, kila kukicha alikuwa akitamani sana kumpata rafiki wa kike ambaye angekuwa akikidhi haja zake za kimwili lakini haikuwa rahisi. Kila msichana aliyejaribu kumtongoza chuoni hapo, alikuwa akimkataa huku wengine wakimtolea kashfa waziwazi kwamba hawawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na sokwe - mtu , jambo ambalo lilimuumiza sana moyo wake. “ Kuanzia leo sitatongoza tena mwanamke hapa chuoni, nimechoshwa na matusi haya , ni bora niendelee kuteseka , ” alijisemea Dickson huku akijifuta machozi yaliyokuwa yanaulowanisha uso wake baada ya kutukanwa na msichana machachari lakini mrembo , Euclesia alipojaribu kumtongoza. Njia pekee aliyoona inamfaa , ilikuwa ni kuendelea kujichua ingawa alikuwa akiufanya mchezo huo kwa siri kubwa akihofia wenzake wasijue. Siku zilizidi kusonga mbele , jioni moja akiwa kwenye chumba alichokuwa akiishi na wenzake, mwanachuo mmoja , Hans aliyekuwa na kawaida ya kwenda kunywa pombe mitaani na kurudi usiku wa manane , alikuwa akiwapigia stori wenzake. “ Jana bwana nimeenda kuopoa changu pale mitaa ya kati , jirani na Meeda Bar . Nikaenda naye gesti palepale jirani. Hata sijui ishu gani ilitokea kwani baada ya kwenda kujimwagia maji ili nije kujilia vitu vyangu , alinipa juisi na nilipokunywa tu , nilianza kusikia kizunguzungu kikali . ” “ Ebwana eeeh ! Duh, ikawaje?” “ Mara kidume nikaangusha gari , kuja kushtuka tayari kumekucha , demu kanikomba mazagazaga yote , kaniacha mweupee, kanilostisha kichizi yule demu!” “ Ayaaa! Kakuibia ? Na wewe umezidi kuopoa machangu, acha yakukute fala wewe. Lazima alikuwekea madawa ya kulevya huyo, ” alisema Maten , mwanachuo mwingine , wenzake wakacheka sana . Stori hiyo aliyowasimulia Hans , iliwafurahisha wote waliokuwa ndani ya chumba hicho, akiwemo Dickson ambaye muda wote alikuwa ametega masikio kwa makini akiwa na shauku kubwa ya kujua kilichotokea. Badala ya kumpa pole , wenzake wote waliendelea kumcheka Hans kutokana na kilichomtokea. Dickson ambaye hakuwa na kawaida ya kupiga stori na wenzake , akamuuliza Hans swali lililowashangaza wenzake. “ Kwani huko Meeda ndiyo wapi?” “ Ni hapo jirani tu , ukifika Mlimani City , unavuka ng’ ambo ya barabara, upande wa pili kwenye kituo cha daladala kuna barabara ya lami inaingia kule ndanindani, ukimuuliza mtu yeyote atakuelekeza. ” “ Ebwana vipi Zinja na wewe unataka ukaopoe nini? Angalia watakuibia mpaka nguo ya ndani urudi mtupu hapa , ” alisema mwanachuo mwingine na kuwafanya wazidi kuangua vicheko. Kwa Dickson, huo ulikuwa ni msaada mkubwa sana kwake, moyoni akajiapiza kuwa lazima akipata fedha kidogo, na yeye aende kujaribu kununua changudoa mmoja ili auonje ulimwengu wa kikubwa ambao mpaka wakati huo, hakuwa akiujua. Ili asisahau , aliandika kwenye kitabu chake kidogo namna ya kufika eneo hilo. Siku zilizidi kusonga mbele na hatimaye , fedha kutoka kwenye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu au maarufu kama ‘ bumu ’ , iliingizwa kwenye akaunti ya kila mwanachuo aliyekuwa akisoma kwa mkopo . Dickson alikuwa miongoni mwa wanachuo walioingiziwa fedha hizo . Akaongozana na wenzake mpaka kwenye tawi la benki lililokuwa jirani na chuo hicho ambapo alitoa fedha kiasi kwa ajili ya matumizi madogomadogo. “ Leo lazima na mimi niende kununua changudoa, nimechoshwa na maisha ya kujichua kila siku , ” alisema wakati akijiandaa jioni moja . Hakumuaga mtu yeyote , akatoka na kujifanya haendi mbali, akapita njia za vichochoroni mpaka alipotokezea kwenye barabara ya lami . Akakodi bodaboda na kumuelekeza dereva kumpeleka mitaa ya Meeda Bar . Muda mfupi baadaye, tayari alikuwa amefika eneo hilo, akamlipa dereva wa bodaboda fedha zake kisha akashuka na kuanza kuangaza macho huku na kule . Kwa kuwa hakutaka mtu yeyote amtambue , alisimama kwenye duka moja kubwa na kununua kofia ambayo aliivaa na kuuficha uso wake, akawa anazungukazunguka mitaa hiyo , akiwa makini kutafuta wanawake waliokuwa wakifanya biashara ya kujiuza . Kwa kuwa bado ilikuwa ni mapema, hakuweza kuwaona kwa urahisi, ikabidi atafute sehemu ya kutulia kusubiri giza liingie kwani alishawahi kusikia kwamba machangudoa wengi hufanya biashara hiyo nyakati za usiku . Sauti kubwa ya muziki iliyokuwa ikisikika kutoka jirani na mahali alipokuwa amekaa akisubiri giza liingie , ilimvutia kuinuka na kuanza kuifuata . Muda mfupi baadaye, alifika kwenye baa kubwa ya kisasa , iliyokuwa imechangamka sana. Aliangaza macho huku na kule , akaamua kuingia ndani kwani kama ni fedha , siku hiyo alikuwa nazo za kumtosha kufanya chochote. Aliingia ndani na kuanza kushangaa mandhari ya baa hiyo , taa za rangirangi zilizokuwa zikiwaka na kumulika huku na kule , zilizidi kupafanya mahali hapo pazidi kuchangamka . Alienda kukaa kwenye kona moja na kuagiza kinywaji, kwa kuwa hakuwa mnywaji wa pombe, aliagiza juisi ya kwenye boksi na kutulia , macho yake yakiwa makini kuangalia huku na kule . Muziki ulizidi kupigwa na kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele , ndivyo watu walivyozidi kuongezeka ndani ya baa hiyo . Miongoni mwa watu hao, wengi walikuwa ni wanawake waliokuwa wamevalia nusu utupu ambao bila hata kuuliza , alijua ndiyo machangudoa wenyewe kwani wengine walikuwa wakivuta sigara , wengine kunywa pombe na wengine kucheza muziki kwa kujiachia . Kila alipofikiria kumuita mmoja kati yao , mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio mno , akaamua kupiga moyo konde na kujikakamua kiume . “ Pssssiiii!” Dickson aliita, wanawake zaidi ya watano wakamgeukia huku kila mmoja akimuuliza kwa ishara kama yeye ndiye aliyekuwa akiitwa . Harakaharaka alimchagua mmoja kati yao aliyekuwa jirani , akamuoneshea ishara ambapo bila kujivunga , alimfuata mpaka pale alipokuwa amekaa.



    Mipango ya kumnasa mhusika bado inaendelea lakini kazi haiwi nyepesi kama watu walivyodhani . Upande wa pili , kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam . Hata hivyo , hisia kali za mapenzi zinaendelea kumsumbua na kusababisha aende kwenye eneo maarufu lililokuwa na machangudoa waliokuwa wakiuza miili yao , jirani na Baa ya Meeda, Sinza. Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … “ Pssssiiii!” Dickson aliita, wanawake zaidi ya watano waliokuwa eneo hilo walimgeukia huku kila mmoja akimuuliza kwa ishara kama yeye ndiye aliyekuwa akiitwa . Harakaharaka alimchagua mmoja kati yao aliyekuwa jirani, akamuoneshea ishara ambapo bila kujivunga , alimfuata mpaka pale alipokuwa amekaa. “ Mambo!” alisema Dickson huku akishusha kofia yake kuziba uso wake kwani alijua kuwa huenda mwanamke huyo akiiona sura yake, atafanya kama ambavyo wanawake wengi wamekuwa wakifanya . “ Poa, mambo bebi , ” alisema msichana huyo huku akiwa ameshajisogeza mwilini mwa Dickson, mapigo ya moyo ya kijana huyo yakawa yanamuenda mbio kuliko kawaida kwani katika maisha yake, hakuwahi kusogelewa jirani na mwanamke kiasi hicho. Kilichozidi kumchanganya akili zake ni kwamba mwanamke huyo alikuwa amevaa nguo fupi iliyoyaacha mapaja yake yote wazi . Juu alikuwa amevaa kiblauzi chepesi kilichomuonesha mwili wake waziwazi, macho ya Dickson yakatua juu ya kifua cha mwanamke huyo, akazidi kuishiwa nguvu. “ Aah! Ee … unajua nakufana … nisha ka …” Dickson alibabaika , maneno yakawa yanatoka nusunusu, msichana huyo akamkata kauli. “ Jamani we kaka, mbona unaniogopa kiasi hicho? We sema tu una shilingi ngapi twende nikakupe raha ,” alisema msichana huyo, safari hii akimkumbatia Dickson na kumwangushia mvua ya mabusu. “ Shi… li . . ngi nga… pi nikupe ?” alihoji Dickson huku kijasho chembamba kikianza kumtoka japokuwa ilikuwa ni jioni . Msichana huyo akamtajia bei pamoja na gharama za chumba cha gesti . Harakaharaka Dickson alikubaliana naye, wakainuka na kutoka mpaka nje ya baa hiyo , msichana huyo akamuongoza mpaka mtaa wa pili kulikokuwa na nyumba ya kulala wageni ambayo machangudoa wengi wa eneo hilo walikuwa wakiwapeleka wateja wao. “ Kinga unayo ?” “ Hapana. ” “ Nenda kanunue , ” alisema changudoa huyo lakini kwa kuwa tayari hisia za mapenzi zilikuwa zimekolea kwenye kichwa cha Dickson, hakukubali kutoka nje ya chumba hicho na kumuacha msichana huyo. “ Ukitaka bila kinga inabidi uongeze fedha , ” alisema msichana huyo , Dickson akakubali harakaharaka, akampa mwanamke huyo kiwango cha fedha alichokuwa anakitaka kisha akaenda kuzima taa kisha akavua kofia yake. Hakupoteza muda , akavua nguo zake zote na kuzitupa pembeni, akapanda kitandani huku akiwa haamini kwamba hatimaye kitu alichokuwa akitamani kitokee kwa siku nyingi kilikuwa kikielekea kutimia. Muda mfupi baadaye, kijana huyo alikuwa akielea kwenye bahari ya huba, ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza kushiriki mchezo wa kikubwa tangu alipopata akili . Hakujali usalama wake wala matatizo anayoweza kuyapata kwa kufanya ngono na changudoa, tena bila kinga . Aliendelea kuogelea kwenye bahari ya huba mpaka alipokidhi haja zake. Kwa kuwa alishasimuliwa kwamba machangudoa wana kawaida ya kuwaibia wateja wao, alikuwa makini kuhakikisha na yeye hayamkuti kama yaliyomkuta mwenzake. Harakaharaka alienda kuchukua nguo zake, akavaa . Alipomaliza alivaa na kofia yake kisha akawasha taa . Yule mwanamke hakutaka kupoteza muda , aliingia bafuni kuoga kisha akatoka na kurudi kwenye eneo lake kuendelea kuwinda wateja wengine. Kwa kuwa Dickson alikuwa ameshapata alichokitaka , hakutaka kuendelea kukaa eneo hilo, alikodi bodaboda iliyomrudisha mpaka chuoni kwao . Njia nzima alikuwa akijipongeza kwa kufanikisha jambo lililokuwa likimtesa kwa kipindi kirefu. “ Kumbe nilikuwa nazikosa raha za dunia kiasi hiki ? Nitakuwa nakuja mara kwa mara , sina haja ya kuhangaika kutongoza tena ,” alijisemea moyoni kijana huyo wakati bodaboda ikikata mitaa kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikokuwa anasoma . Alipofika jirani na eneo la chuo, alimlipa dereva wa bodaboda kisha akapita njia za mkato na kuingia eneo la chuo. Harakaharaka akatembea mpaka kwenye hosteli aliyokuwa anaishi. Alipitiliza bafuni ambako alioga kisha akarudi kitandani kwake na kujibwaga , tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake. “ Vipi Zinja mbona leo una furaha sana ?” mwanachuo mwenzake waliyekuwa wakiishi chumba kimoja alimuuliza baada ya kumuona muda wote akiwa na tabasamu pana , jambo ambalo halikuwa kawaida yake. “ Kuna kitu kimenifurahisha sana leo , ” alisema Dickson au Zinja kama wanachuo wenzake walivyokuwa wakimuita, akageukia upande wa pili wa kitanda na kuendelea kutabasamu kwa furaha. Kwa jinsi alivyokuwa amechoka, usingizi ulimpitia akiwa hapohapo kitandani . Alikuja kuzinduka kesho yake alfajiri . Akaamka na kuanza kujiandaa kama kawaida kwa ajili ya kuingia darasani . Siku hiyo pia alikuwa na furaha sana tofauti na siku zote tangu aanze kusoma chuoni hapo. Kila aliyekuwa anamjua , alikuwa akimshangaa kwani haikuwa kawaida yake kutabasamu , watu wakawa wanajiuliza maswali yaliyokosa majibu. Ratiba ziliendelea kama kawaida, jioni baada ya masomo , Dickson alijiandaa tena kwa kuvaa nguo nzuri , akaomba pafyumu kwa mwenzake waliyekuwa wakikaa naye chumba kimoja na kujipulizia. Akavaa na kofia yake iliyouziba kabisa uso wake na kumfanya kuwa na mwonekano tofauti kabisa, akatoka na kupita njia alizopita jana yake, akafanikiwa kutoka nje ya eneo la chuo na kuelekea moja kwa moja mpaka barabarani alikosimamisha bodaboda . “ Nipeleke ule mtaa ilipo Baa ya Meeda, ” alisema Dickson wakati akikaa kwenye siti ya bodaboda, safari ikaanza . Muda mfupi baadaye, tayari walikuwa wamewasili eneo hilo, akashuka na kumlipa fedha zake kisha akanyoosha moja kwa moja kwenye ile baa aliyokaa jana yake. Akaenda kwenye kona ileile na kuagiza kinywaji, akawa anakunywa taratibu huku akipepesa macho huku na kule kuangalia mwanamke wa kumuita. Kwa kuwa hicho kilikuwa kituo maarufu cha machangudoa, giza lilipoanza kuingia tu, wanawake wa kila aina walianza kumwagika kwa wingi , wengi wakiwa wamevaa nusu utupu . Dickson aliachia tabasamu pana , mate ya uchu yakawa yanamtoka kama fisi aliyeona mfupa. Kwa kuwa jana yake alitoka na mwanamke mwembamba , safari hii aliamua kujaribu kitu tofauti. Alitaka mwanamke mnene na kwa kuwa walikuwepo wengi eneo hilo, alipotoa ishara tu , mwanamke mmoja mnene, alitembea harakaharaka kuelekea pale alipokuwa amekaa.



    Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Mara ya kwanza anafanikiwa kuopoa changudoa na kushiriki naye tendo la ndoa kwa mara ya kwanza . Anaonekana kunogewa na mchezo huo. Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya kufanikiwa kwa mara ya kwanza kukutana kimwili na mwanamke aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza mwili wake , Dickson au Zinja kama wengi walivyokuwa wanapenda kumuita , alikuwa ni kama ameonja asali na sasa alitaka kuchonga mzinga. Kesho yake alijiandaa tena na kuelekea eneo lilelile , akakaa kwenye kona ileile na kutulia kusubiri muda usonge mbele ili aopoe changudoa mwingine na kwenda kuvunja naye amri ya sita . Muda mfupi baadaye, wanawake wengi waliokuwa wakifanya biashara hiyo haramu , walianza kumiminika kwa wingi kwenye baa ambayo kijana huyo alikuwa amekaa ndani yake. Dickson aliachia tabasamu pana , mate ya uchu yakawa yanamtoka kama fisi aliyeona mfupa. Kwa kuwa jana yake alitoka na mwanamke mwembamba , safari hii aliamua kujaribu kitu tofauti. Alitaka mwanamke mnene na kwa kuwa walikuwepo wengi eneo hilo, alipotoa ishara tu , mwanamke mmoja mnene, alitembea harakaharaka kuelekea pale alipokuwa amekaa. “ Mambo bebi !” alisalimia mwanamke huyo ambaye hata kabla hajatongozwa, alimkumbatia Dickson na kumbusu shavuni . Naye hakutaka kulaza damu , akamkumbatia kiunoni na kumbusu. Akazungumza naye maneno machache ambapo walikubaliana bei . Muda mfupi baadaye, wawili hao walitoka wakiwa wamekumbatiana mithili ya wapenzi ambao wapo pamoja kwa kipindi kirefu na kuelekea moja kwa moja mpaka mtaa wa pili , kwenye gesti ileile ambayo siku moja iliyopita Dickson aliingia na mwanamke mwingine. Kwa muda wote huo, Dickson alikuwa amevaa kofia na kuishusha usoni kiasi cha kufanya isiwe rahisi kwa msichana huyo kuiona sura yake halisi. Walipoingia chumbani , Dickson alimlipa msichana huyo fedha zake. Msichana huyo alianza kuvua nguo zake mwenyewe, Dickson akazima kwanza taa kisha na yeye akaanza kuvua zake. Muda mfupi baadaye, miguno ya kimahaba ilikuwa ikisikika ndani ya chumba hicho, Dickson akiendelea kujisifu ndani ya moyo wake kwa kuanza kuzipata raha ambazo kwa kipindi kirefu alikuwa akizikosa. Baada ya kukidhi haja zake, Dickson aliwahi kuamka na kuvaa nguo zake, akatoka chumbani humo haraka ili msichana huyo asipate nafasi ya kuiona sura yake. Kwa kuwa tayari alishakuwa amekidhi haja zake, hakutaka kusubiri chochote, alitoka na safari ya kurudi chuoni kwao ikaanza . Kama kawaida, alikodi pikipiki iliyompeleka mpaka jirani na chuo chao ambapo alimlipa dereva fedha zake kisha akashuka na kujipenyeza kwa kupitia njia za vichochoroni mpaka kwenye hosteli aliyokuwa anaishi. Moja kwa moja alipitiliza bafuni ambako alijimwagia maji kisha akarudi kitandani kupumzika , tabasamu pana likiwa limeupamba uso wake . Alijiona mshindi kwa kufanikiwa kukidhi haja za mwili wake kwa urahisi kuliko alivyokuwa akitegemea. Aliendelea kujiapiza kuwa kamwe hatapata shida ya kutongoza mwanamke yeyote chuoni hapo na kuishia kuambulia matusi na kejeli kama ilivyokuwa siku za nyuma. “ Nikihitaji mwanamke wa kujirusha naye tu, naelekea eneo la tukio kisha nachagua ninayempenda , hayo ndiyo yatakuwa maisha yangu , ” aliwaza Dickson huku akijigeuzageuza kitandani , tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake . Siku hiyo hakwenda hata kujisomea masomo ya usiku kama ilivyokuwa kawaida yake, alipitiwa na usingizi mzito mpaka kesho yake asubuhi . Kulipopambazuka, aliwahi kuamka na kuelekea bafuni kwa ajili ya kujiandaa na siku mpya ya masomo . “ He ! Mbona nasikia maumivu makali kiasi hiki ,” Dickson alijiuliza wakati akijisaidia haja ndogo . Awali alihisi ni maumivu ya kawaida lakini kadiri alivyokuwa anajikamua ili kutoa haja ndogo , ndivyo maumivu kwenye sehemu zake za siri yalivyozidi na kujikuta akipiga kelele . Kwa kuwa wanachuo wengi walikuwa bado hawajaamka, hakuna aliyemsikia . Akaendelea kujikamua na katika hali ambayo ilimshtua kuliko kawaida, alishangaa kuona akitokwa na usaha baada ya haja ndogo kuisha. “ Mungu wangu, nimeambukizwa gonjwa la zinaa, ” alisema Dickson huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio kuliko kawaida . Hakuna kitu alichokuwa anakiogopa maishani mwake kama kupata magonjwa ya zinaa, akawa anatetemeka huku akiwa hajui nini hatima yake. Kwa kuwa alikuwa na uelewa wa kutosha wa somo la Biolojia, moja kwa moja aligundua kuwa kilichosababisha akapata gonjwa hilo ni kitendo cha kufanya mapenzi na machangudoa wawili bila kutumia kinga . Hakujua ni yupi kati ya wawili hao ndiye aliyemuambukiza gonjwa hilo kwani wote alikutana nao kimwili bila kutumia kinga . Majuto makubwa yakaanza kuizonga nafsi yake. Alimalizia kuoga na kurudi chumbani kwake, hakuweza kuendelea kujiandaa kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayahisi . “ Watu wakijua kwamba naumwa ugonjwa wa zinaa si itakuwa aibu sana ? Hapana, sitakubali mtu yeyote ajue , ” alisema Dickson huku akijikongoja na kuamka kitandani , akavaa nguo zake na kutoka bila kumwambia mtu yeyote mahali alikokuwa anaenda . Akasubiri wakati wenzake wameenda kwenye vipindi vya asubuhi ambapo yeye aliondoka na kuelekea nje kabisa ya chuo hicho. Akapanda daladala iliyompeleka mpaka Mwenge kwenye duka kubwa la dawa la Makete Pharmacy alikonunua dawa za kuzuia uambukizo wa bakteria ( antibiotics ) kwa ajili ya kujitibu gonjwa alilolikwaa . “ Kwani unaumwa nini kaka?” “ Siyo mimi , kuna rafiki yangu ana matatizo ya mkojo mchafu. ” “ Cheti cha daktari kiko wapi?” alihoji mhudumu wa duka hilo la madawa, ikabidi Dickson apenyeze rupia kwani alishahisi kuna uzia mbele yake. Akampa mhudumu huyo shilingi elfu tano nje ya malipo ya kawaida ya dawa na kumwambia kuwa atakunywa soda , anachotaka yeye ni dawa tu. Mhudumu huyo alifanya kama alivyoambiwa, akampa dawa aina ya Ampicillin na kumuelekeza namna ya kutumia. Alimshukuru na kuondoka , mbele kidogo alinunua maji ya kunywa na kumeza dawa alizoandikiwa . Alirudi chuoni kwao ambapo aliendelea kuficha kilichokuwa kinamsumbua huku akiendelea kutumia dawa hizo kimyakimya. Hata hivyo , licha ya kutumia dawa hizo na kuzimaliza , bado hakuwa na dalili zozote za kupona, usaha ulizidi kumtoka kwa wingi na safari hii ulianza kutoa harufu kali .



    Mipango ya kumnasa mhusika bado inaendelea lakini kazi haiwi nyepesi kama watu walivyodhani . Upande wa pili , kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam . Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa . Anafanikiwa kuopoa machangudoa mara mbili lakini baada ya hapo, anajikuta akianza kuumwa ugonjwa wa ajabu na kuanza kutokwa usaha sehemu za siri. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Baada ya kufanikiwa kwenda kununua dawa mitaani, Dickson au Zinja kama wenzake walivyozoea kumuita kutokana na mwonekano wa sura yake, alirudi chuoni kwao ambapo aliendelea kuficha kilichokuwa kinamsumbua huku akiendelea kutumia dawa hizo kimyakimya. Hata hivyo , licha ya kutumia dawa hizo na kuzimaliza , bado hakuwa na dalili zozote za kupona, usaha ulizidi kumtoka kwa wingi na safari hii ulianza kutoa harufu kali. “ Ebwana unasumbuliwa na nini mshikaji wangu? Mficha maradhi kifo humuumbua, ” Jaicko, rafiki yake waliyekuwa wanaishi chumba kimoja , alimuuliza Dickson baada ya kuona wiki nzima imekatika bila rafiki yake huyo kwenda darasani huku muda wote akilalamikia maumivu makali . Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya , ilibidi Dickson awe mkweli na kumweleza rafiki yake huyo aliyeonesha nia ya kumsaidia lakini akamuomba sana suala hilo liwe siri yao wawili tu . “ Usiwe na wasiwasi, nakuahidi kwamba itakuwa siri yetu mimi na wewe tu ,” alisema Jaicko na kumsogelea Dickson ambaye alimueleza ukweli kwamba alifanya ngono na machangudoa wawili bila kutumia kinga na baada ya hapo ndipo alipoanza kusikia maumivu makali kwenye sehemu zake za siri hasa wakati wa kujisaidia haja ndogo . “ Utakuwa umeambukizwa ugonjwa wa zinaa lakini utapona wala usiwe na wasiwasi, nenda kaoge kisha ujiandae twende hospitalini ,” alisema rafiki yake huyo na kuamua kukatisha ratiba yake ya kwenda darasani kwa ajili ya kumsindikiza rafiki yake huyo hospitalini . Kwa kuwa bado Dickson alikuwa na fedha , walikubaliana kwenda Hospitali ya Marie Stopes, Sinza. Baada ya kijana huyo kumaliza kujiandaa, aliongozana na Jaicko bila mtu yeyote kujua walikokuwa wanaelekea . Kwa kuwa tayari ugonjwa huo ulishamshambulia sana Dickson, alikuwa akishindwa hata kutembea vizuri, akawa anaitanua miguu yake na kuchechemea huku akiinama kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayahisi . Ilibidi wakodi teksi kwani kwa hali aliyokuwa nayo Dickson , isingekuwa rahisi kutembea mwenyewe mpaka nje ya chuo hicho. Wakamuelekeza dereva sehemu ya kuwapeleka ambapo baada ya takribani dakika ishirini, walikuwa tayari wamewasili kwenye hospitali hiyo . Wakaingia ndani na kufuata taratibu za kawaida na hatimaye zamu yao ya kuingia kumuona daktari ikafika . Walipoingia kwenye chumba cha daktari, walikutana na mwanaume wa makamo, aliyekuwa amevalia koti la kidaktari na miwani aliyoishusha chini kidogo ya macho yake, akawapokea kwa uchangamfu. “ Nani anayeumwa kati yenu ?” “ Ni mimi dokta, ” Dickson alijibu harakaharaka huku akionesha kuugulia maumivu makali , daktari huyo akamuomba Jaicko atoke nje na kuwapisha ili Dickson apate uhuru wa kuzungumza kilichokuwa kinamsumbua, kama maadili ya kidaktari yalivyokuwa yanaelekeza . Baada ya Jaicko kutoka , Dickson alikaa vizuri kwenye kiti chake ambapo daktari alianza kumhoji na kumtaka awe huru kueleza kilichokuwa kinamsumbua . Japokuwa alikuwa akijihisi aibu kubwa ndani ya moyo wake kutokana na aina ya ugonjwa aliokuwa akiumwa , Dickson hakuwa na ujanja zaidi ya kueleza ukweli . Hata alipotakiwa kuvua suruali yake na kumuonesha daktari jinsi ugonjwa huo ulivyokuwa umemuathiri, Dickson hakuwa na cha kufanya. Baada ya kumchunguza kwa kina, daktari huyo alimuandikia vipimo ambapo alitoka na kuelekea maabara. Baada ya kuchukuliwa vipimo vyote alivyoandikiwa , Dickson alitoka na kwenda kukaa na rafiki yake Jaicko kwenye sehemu maalum ya kusubiria majibu. Baada ya takribani dakika ishirini, majibu yalikuwa tayari yameshatoka. Akarudi tena kwa daktari ambaye baada ya kuyasoma vizuri majibu hayo , alivua miwani yake na kuifuta vumbi kwa kitambaa laini kisha akaivaa tena na kuishusha chini ya macho, akawa anamtazama Dickson akiwa ni kama haamini alichokibaini kwenye majibu ya vipimo vyake . “ Kijana , una mpenzi?” “ Hapana dokta, wasichana wote ninaowatongoza wananikataa . ” “ Mara ya mwisho ulifanya ngono lini ?” “ Wiki moja iliyopita dokta. ” “ Ulitumia kinga ?” “ Hapana. ” “ Sasa majibu yanaonesha kwamba umeambukizwa ugonjwa wa kaswende lakini kwa mujibu wa sheria za kidaktari , sitaweza kukutibu peke yako mpaka ukamlete mwanamke uliyekutana naye kimwili ili mje kutibiwa wote ,” alisema daktari huyo huku akiendelea kumtazama Dickson usoni. Kijana huyo alijiinamia chini kwani huo ulikuwa ni mtihani mwingine kwake. Hakuwahi kukutana kimwili na mwanamke yeyote mpaka siku chache zilizopita ambapo alifanya mapenzi na machangudoa wawili tofauti ndani ya siku mbili, tena bila kinga . Hakujua ni yupi kati ya machangudoa hao ndiye aliyemuambikiza ugonjwa huo, hata kama angemjua bado isingekuwa rahisi kumpata na kukubali kuongozana naye kwenda hospitalini , akajikuta akikosa majibu. Alishusha pumzi ndefu na kuinua sura yake, akamtazama daktari kwa macho yake ya kutisha . “ Mbona hujibu chochote?” daktari huyo alimuuliza, akashusha pumzi ndefu kwa mara nyingine kisha ikabidi ajikaze kisabuni na kuamua kumwambia ukweli kwamba gonjwa hilo alikuwa ameambukizwa na machangudoa. “ Aisee una hatari sana kijana . Lazima ujihurumie nafsi yako vinginevyo ndoto zako zote zitaishia kaburini. Unawezaje kufanya ngono na changudoa, tena bila kinga ?” alisema daktari huyo na kuanza kumpa nasaha Dickson juu ya kuepukana na magonjwa ya zinaa na Ukimwi. “ Usikubali kufanya ngono na mtu yeyote bila kutumia kinga , siku hizi maradhi yamekuwa mengi mno na ukifanya mchezo , utakufa huku unajiona , ” alisema daktari huyo na kuendelea kumpa nasaha . Baadaye alimuandikia sindano na kumpa dawa nyingine za kumeza na kumtaka kuzingatia alichomwambia. Dickson alimshukuru sana na kutoka mpaka nje alikomuacha rafiki yake akimsubiri. Walienda kulipia huduma na dawa kisha wakaondoka kurudi chuoni kwao huku Dickson akijiapiza kuwa makini siku nyingine ili asije akaambukizwa tena magonjwa ya zinaa au Ukimwi. Baada ya wiki moja tu tangu aanze kutumia dawa , tayari alikuwa na maendeleo mazuri lakini kama kawaida yake, alianza kujisikia hamu ya kukutana tena kimwili na mwanamke.



    Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Anafanikiwa kuopoa machangudoa mara mbili lakini baada ya hapo, anajikuta akianza kuumwa ugonjwa wa ajabu na kuanza kutokwa usaha sehemu za siri. Inabainika kwamba ameambukizwa ugonjwa wa zinaa ambapo anatibiwa lakini hakomi. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Kama wahenga walivyosema kwamba mwonja asali haonji mara moja, licha ya kuambukizwa gonjwa la zinaa na machangudoa , bado Dickson au Zinja hakutaka kukoma . Hata kabla hajamaliza dozi aliyopewa hospitalini , alianza tena kujisikia hamu ya kukutana kimwili na mwanamke. Kwa kuwa bado fedha za mkopo wa chuo au ‘ boom ’ kama wengi wanavyopenda kuita zilikuwa hazijaisha , Dickson aliamua kutoka na kwenda eneo lake la kuwindia machangudoa lakini safari hii akijiapiza kuwa makini ili yasije kumtokea kama yaliyomtokea mara ya kwanza. Alisubiri wenzake wote wameenda kujisomea na kumuacha peke yake chumbani , akaenda kuoga na kujiandaa ambapo harakaharaka alitoka na kupita njia za vichochoroni mpaka alipotokea kwenye barabara ya lami , nje kabisa ya chuo. Akasubiri kwa dakika chache na kusimamisha bodaboda, akamuelekeza dereva kumpeleka jirani na Baa ya Meeda, mahali alikokuwa akijipatia machangudoa kwa urahisi. Alipofika , kama kawaida yake aliingia mpaka ndani ya baa moja iliyokuwa ikipiga muziki kwa sauti kubwa na kwenda mpaka kwenye kona moja alikoenda kujibanza huku akiwa ameishusha kofia yake kiasi cha kuuziba uso wake. Akaagiza kinywaji na kuanza kuangaza macho huku na kule , huku akiendelea kuburudishwa na sauti kubwa ya muziki uliokuwa ukipigwa ndani ya baa hiyo . Kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo jinsi baa hiyo ilivyokuwa inazidi kuchangamka . Wanawake nao walizidi kuongezeka kwa wingi, huku wengine wakicheza muziki uliokuwa ukipigwa bila aibu yoyote . Kama kawaida, karibu wote walikuwa wamevalia nguo zilizoyaacha wazi maungo yao nyeti na kuzidi kumuweka Dickson katika wakati mgumu. Kigiza kikiwa kimeshaanza kuingia , Dickson aliamua kumuita changudoa mmoja aliyekuwa akicheza muziki kwa mbwembwe nyingi huku akijitingisha sana sehemu za nyuma ya mwili wake. Harakaharaka msichana huyo ambaye kiumri alionekana kuwa mtu mzima, alimfuata Dickson na kumkumbatia . “ Nambie mpenzi wangu, ” alisema huku akimbusu na kuendelea kumkumbatia Dickson , wakazungumza biashara na baada ya kukubaliana, walitoka wakiwa wamekumbatiana utafikiri walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu. Badala ya kuelekea moja kwa moja gesti kama alivyokuwa akifanya , Dickson alimtaka mwanamke huyo wapitie kwanza kwenye duka lililokuwa jirani ambapo alinunua kondom na safari ikaendelea . Wakaenda kwenye gesti ileile ambayo Dickson alishaitumia mara mbili za awali. Wakalipa mapokezi na kuingia mpaka ndani ambapo hakukuwa na cha kusubiri . Dickson alizima taa kisha akaanza kuvua nguo zake huku yule changudoa naye akifanya hivyohivyo. Muda mfupi baadaye, hakukuwa na kilichokuwa kinasikika ndani ya chumba hicho cha gesti zaidi ya kelele za kitanda na miguno ya kimahaba . Dakika kadhaa baadaye, taa iliwashwa Dickson akiwa ameshavaa nguo zake, akatoka huku mkononi akiwa ameshika ‘ zana zilizotumika ’ alizoenda kuzitupa nje . Dickson hakutaka kuendelea kukaa eneo hilo baada ya kukidhi haja zake, alienda kukodi bodaboda iliyomrudisha chuoni kwao ambapo kwa kuwa hakuna aliyejua kwamba kuna muda alitoka, aliingia kimyakimya na kwenda kuoga kisha akarudi kitandani na kujipumzisha . “ Ebwana vipi unaendeleaje ? Dawa zinakusaidia?” Jaicko, mwanachuo mwenzake na rafiki yake kipenzi ambaye ndiye pekee aliyekuwa anajua kinachomsumbua Dickson, alimuuliza baada ya kumkuta akiwa amejilaza kitandani kwake, akionesha kuchoka sana . “ Zinanisaidia sana , naelekea kupona ila namalizia dozi tu ,” Dickson alimjibu huku akijaribu kuvaa sura ya ugonjwa, hali iliyomfanya rafiki yake huyo asigundue kwamba muda mfupi tu uliopita, alikuwa ametoka kufanya ngono na changudoa mwingine. Siku hiyo ilipita , maisha yakaendelea kama kawaida ambapo Dickson aliendelea na dozi yake mpaka alipomaliza, akawa ameshapona kabisa lakini bado mchezo wake wa kwenda kununua machangudoa haukukoma . Kilichobadilika ni kwamba baada ya kupata gonjwa la zinaa, hakuthubutu tena kufanya ngono bila kinga , siku zikawa zinasonga mbele huku tabia hiyo ya Dickson ikizidi kuota mizizi. “ Hivi Zinja starehe yako kubwa huwa ni nini? Hunywi pombe , huvuti sigara , hupendi michezo , huendi disko wala sijawahi kukuona na demu . ” “ Mi starehe yangu ni kusoma tu, nataka kuja kuwa mwanasheria mkubwa nchini , ” alisema Dickson jioni moja wakati mwanachuo mwenzake mmoja alipomuuliza kwa masihara. “ Watu kama hawa ambao hata pombe hawanywi wanakuwaga na mambo yao ya chini kwa chini , hakuna mtu ambaye hana starehe anayoipenda, huyu Zinja anatuzuga tu hapa , ” alisema mwanachuo huyo na kusababisha wenzake wote wacheke kwa nguvu. Hatimaye mwaka wa kwanza wa masomo uliisha, Zinja na wanachuo wengine wakarudi makwao ambapo baada ya mapumziko , walirejea tena chuoni kuuanza mwaka wa pili . Kadiri Dickson alivyokuwa akizidi kuwa mkubwa, ndivyo hamu ya kukutana kimwili na wanawake ilivyokuwa inazidi kuongezeka. Ikafika kipindi akawa hawezi kuvusha zaidi ya siku tatu bila kwenda kununua changudoa na kufanya naye ngono . Hata fedha za mkopo alizokuwa anazipata kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu, zilionekana kutotosha kwani hakuwa akifanyia kitu kingine chochote zaidi ya kununua machangudoa . Hata vitabu na vifaa vingine kwa ajili ya masomo yake, alikuwa akilazimika kuazima kwa wenzake kwani yeye hakuwa na uwezo wa kununua kutokana na kuendekeza ngono . Kilichomsaidia ni kwamba Mungu alikuwa amemjalia uwezo mkubwa wa kiakili hivyo hakuwa na haja ya kusoma sana ili aelewe. Mwaka wa pili nao uliyoyoma mpaka ulipofika mwisho, tabia ya Dickson ya kwenda kununua machangudoa na kufanya nao ngono ikawa imeshakuwa sugu. Ilikuwa ni bora akose chakula anaweza kuvumilia lakini asikose changudoa wa kufanya naye ngono . Alipokosa fedha , alikuwa akitamani hata kuiba au kuuza vitu vyake . Hata hivyo , kutokana na umakini aliokuwa akiutumia , haikuwa rahisi kwa wanachuo wenzake kumgundua kuwa alikuwa na tabia hiyo chafu . Alipoona baadhi ya watu wameanza kumzoea au kumhojihoji maswali kutokana na kumuona mara kwa mara Meeda, aliamua kubadilisha kiwanja na kuelekea Sinza Afrika Sana.



    Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa . Anafanikiwa kuopoa machangudoa mara mbili lakini baada ya hapo, anajikuta akianza kuumwa ugonjwa wa ajabu na kuanza kutokwa usaha sehemu za siri. Inabainika kwamba ameambukizwa ugonjwa wa zinaa ambapo anatibiwa lakini hakomi . Tabia hiyo inashamiri na kuwa sugu. Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Mwaka wa pili nao uliyoyoma kwa kasi , tabia ya Dickson ya kwenda kununua machangudoa na kufanya nao ngono ikawa imeshakuwa sugu. Ilikuwa ni bora akose chakula anaweza kuvumilia lakini asikose changudoa wa kufanya naye ngono . Alipokosa fedha , alikuwa akitamani hata kuiba au kuuza vitu vyake . Hata hivyo , kutokana na umakini aliokuwa akiutumia , haikuwa rahisi kwa wanachuo wenzake kumgundua kuwa alikuwa na tabia hiyo chafu . Alipoona baadhi ya watu wameanza kumzoea au kumhojihoji maswali kutokana na kumuona mara kwa mara mitaa ya Baa ya Meeda , aliamua kubadilisha kiwanja na kuelekea Sinza Afrika Sana. Aliamua kuhamishia makazi yake Sinza- Afrika Sana ambako aliendelea kununua machangudoa kwa kipindi kirefu. Hata hivyo , baada ya kuanza kuwaona wanachuo wa kike nao wakiwa wanajiuza eneo hilo, hasa kipindi ambacho mikopo waliyokuwa wanapewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuisha , aliona inaweza kuwa rahisi kwa siri yake kuvuja . Akaamua kuhamishia makazi yake Manzese na Mabibo ambako aliendelea na tabia yake hiyo kwa kipindi kirefu mpaka mwaka wa pili nao ulipoisha . Mwaka wa tatu wa masomo ulipoanza, baada ya likizo ndefu, wanachuo wengi walirejea chuoni , akiwemo Zinja ambaye huo ulikuwa ndiyo mwaka wake wa mwisho chuoni hapo alipokuwa akisomea Shahada ya Kwanza ya Sheria au kwa kifupi LLB (Legum Baccalaureus) . Bado aliendelea na tabia yake ileile, siku alipokosa fedha za kwenda kununua machangudoa, alikuwa akifanya kila liwezekanalo na pale aliposhindwa kabisa, alikuwa akirudia mchezo wake wa kujichua bafuni mpaka anapokidhi haja zake. Hisia za mapenzi zilimfanya awe kama mtumwa, hakuwa na tofauti na mraibu wa madawa ya kulevya ambaye bila kupata kete kadhaa, hawezi kujisikia vizuri zaidi ya kuteseka na arosto . Licha ya ubize wa wanachuo wa mwaka wa tatu, hasa waliokuwa wanasomea sheria , bado Dickson au Zinja kama wengi walivyokuwa wakimuita, hakuacha tabia yake. Alishaathirika kiakili na kitu pekee kilichokuwa kinamtuliza , kilikuwa ni ngono . “ Jamani we kaka unatisha !” msichana mmoja mdogo aliyekuwa amejiunga na chuo hicho kwa mwaka wa kwanza , akisomea shahada ya kwanza ya elimu ya watu wazima , Neema alimwambia Dickson, jioni moja baada ya kukutana naye wakati wakielekea kantini kupata chakula cha jioni . Dickson hakumjibu kitu zaidi ya kuendelea na safari yake ya kuelekea kantini , hata hivyo msichana huyo aliendelea kumfuata nyumanyuma huku akimsemesha, jambo ambalo halikuwa kawaida ya Dickson chuoni hapo. Hakuna msichana ambaye alikuwa anaweza kuzungumza naye zaidi ya mara moja. Mwenyewe alishajua kuwa hayo yote yanasababishwa na mwonekano wa sura yake ndiyo maana hakuwa akijishughulisha kabisa na wasichana wa chuoni hapo, zaidi ya machangudoa ambao nao alipokuwa akienda kuwawinda, ilikuwa ni lazima avae kofia ya kuziba sura yake na wakati wa kuvua nguo, ilikuwa ni lazima azime kwanza taa . Msichana huyo aliendelea kumsemesha huku akimfuata nyumanyuma, ikabidi asimame na kumgeukia , macho yao yakakutana . Licha ya sura iliyokuwa ikifanana na binadamu wa kale, akiwa na nywele nyingi zilizokaribia kukutana na nyusi na macho mekundu , bado msichana huyo hakukwepesha macho yake, wakatazamana kwa sekunde kadhaa. “ Kaka kwani wewe unaitwa nani ?” alisema Neema huku akiendelea kumtazama Dickson usoni. Katika maisha yake, hakuwahi kutazamana na msichana kama ilivyotokea kwa binti huyo mdogo , akahisi kitu tofauti ndani ya moyo wake . Hata pale alipotegemea kwamba msichana huyo ataonesha hofu, wala hakufanya hivyo zaidi ya kuachia tabasamu kwa mbali. “ Naitwa Dickson . ” “ Naomba uwe rafiki yangu na kaka yangu ,” alisema msichana huyo na kuzidi kumshangaza Dickson. Hakuwahi kuambiwa kauli kama hiyo na mwanamke yeyote tangu alipopata akili zake timamu , akajikuta naye akitabasamu. “ We huniogopi ?” aliuliza huku akianza kupiga hatua za taratibu kuelekea kantini , msichana huyo akawa anamfuata huku akimjibu kwamba hawezi kumuogopa kwani na yeye ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Walienda pamoja mpaka kantini ambapo Dickson alienda kuagiza chakula kisha akarudi na kutafuta meza ya peke yake na kukaa kama kawaida yake. Muda mfupi baadaye, msichana huyo mdogo naye alikuja akiwa na sahani yake na kukaa pembeni yake, wakatazamana tena kisha wakaendelea kula taratibu huku kila mmoja akiwa kimya . “ Hujanijibu ombi langu,” alisema Neema na kuuvunja ukimya . “ Ombi gani ?” “ La kutaka uwe rafiki yangu , ” alisema msichana huyo huku akiwa anamtazama Dickson usoni. “ Tumeshakuwa marafiki ndiyo maana tumekaa meza moja tunakula pamoja, ” alijibu Dickson, msichana huyo akacheka kwa furaha kisha wakaendelea kula . Stori za kawaida za hapa na pale ziliendelea ambapo msichana huyo alijitambulisha kwamba ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro . “ Nimefurahi sana kukufahamu . ” “ Mimi pia nimefurahi kukufahamu , ” alijibu Dickson wakati wakiinuka baada ya kumaliza kula chakula cha jioni , wakawa wanatembea taratibu kurudi hosteli huku mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea . “ Kwani wewe unakaa hosteli gani ?” Neema alimuuliza Dickson, akamuelekeza ambapo msichana huyo aliahidi kwenda kumtembelea . Wakaagana na kila mmoja kushika njia yake. Hatua kadhaa mbele , Dickson aligeuka na kumtazama msichana huyo. Alilitathmini umbo lake la kuvutia na kujikuta akitabasamu mwenyewe, muda mfupi baadaye, Neema naye aligeuka na kumkuta Dickson akiwa ameganda kama sanamu , akimkodolea macho, akampungia mkono kisha kila mmoja akaendelea na safari yake. “ Mbona mzuri sana halafu haoneshi kuniogopa kama wasichana wengine?” Dickson alijiuliza wakati taswira ya msichana huyo ikipita kwenye kichwa chake. Licha ya umri wake mdogo , msichana huyo alikuwa na umbile lililojengeka vizuri sana . Alikuwa na kiuno chembamba kilichogawanyika vizuri, eneo la chini kidogo likiwa limetanuka na kujaa kwa nyuma. Rangi ya weusi wa asili aliyokuwa nayo , uso mzuri na meno meupe yaliyojipanga vizuri, zilikuwa ni baadhi ya sifa za msichana huyo zilizomfanya Dickson azidi kuchanganyikiwa . Siku hiyo ilikuwa ya kipekee sana kwa Dickson , muda wote akawa amejawa na tabasamu huku akiendelea kumfikiria msichana huyo



    Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono . Fedha zake zote zinaishia kwa machangudoa na anaendelea na tabia hiyo mpaka anapoingia mwaka wa tatu chuoni hapo. Msichana mdogo aliyekuwa akisoma mwaka wa kwanza chuoni hapo, anaanza kujenga mazoea na Dickson, jambo ambalo halijawahi kumtokea kwani wasichana wengi walikuwa wakimuogopa kutokana na jinsi sura yake ilivyokuwa ya ajabu . Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya kuachana na msichana huyo, Dickson aliendelea kumfikiria huku muda mwingi tabasamu likichanua kwenye uso wake, hasa alipokuwa akivuta taswira ya jinsi msichana huyo mdogo alivyokuwa na mvuto wa kipekee . Kiuno chake chembamba kilichogawanyika na kumfanya kuwa na umbo linalokaribia kufanana na namba nane , macho yake meupe, ambayo muda wote alikuwa akiyarembua utafikiri anasikia usingizi , miguu yake iliyojaa vizuri na kufanana na chupa ya shampeni zilikuwa ni baadhi ya sifa zilizomfanya Dickson ajikute akipagawa mno kila alipomfikiria msichana huyo. Ukiachana na sifa hizo , pia msichana huyo alikuwa na kifua kibichi , kilichojaa vizuri na kuchomoza mithili ya michongoma na meno meupe ambayo alipokuwa akicheka yalikuwa yakizidi kumuongezea mvuto , sifa ambazo kwa pamoja zilimfanya Dickson aendelee kuchekacheka mwenyewe kama mwendawazimu. Japokuwa katika kuhangaika kwake na machangudoa, alishafanya mapenzi na wanawake wa kila aina , hakuwahi hata mara moja kukutana na msichana mrembo kama Neema, akawa anajiapiza kuwa endapo msichana huyo atamuonesha mapenzi ya dhati, yupo tayari kufanya chochote ilimradi awe mkewe wa ndoa . Usiku huo ulikuwa mrefu sana kwake, taswira ya msichana huyo iliendelea kukisumbua kichwa chake mpaka alipopitiwa na usingizi. Alipokuja kuzinduka , tayari kulikuwa kumeshapambazuka, akaamka na kuelekea bafuni kisha alirudi chumbani na kujiandaa kwa ajili ya kuelekea darasani kwani siku hiyo alikuwa na kipindi cha asubuhi . Wakati akielekea darasani , alishtuka baada ya kusikia sauti laini ya kike ikimuita , akageuka na kuangalia ni nani aliyekuwa anamuita kwani haikuwa kawaida yake kuitwaitwa na wasichana. “ Whaooo!” alijikuta akijisemea baada ya kugeuka na kugundua kuwa ni yule msichana waliyekuwa naye jana yake, Neema ndiye aliyekuwa akimuita . Kwa jinsi alivyokuwa amependeza, ungeweza kudhani siyo yule waliyekutana naye jana yake chuoni hapo. Japokuwa kiumri alikuwa mdogo , alivaa na kupendeza mithili ya mwanamke anayejiheshimu, anayefanya kazi kwenye ofisi au taasisi kubwa nchini . Sketi iliyoishia chini kidogo ya mapaja aliyokuwa ameivaa, iliifanya miguu yake iliyonawiri vizuri ionekane sawia , ukichanganya na viatu vyenye visigino virefu alivyokuwa amevaa, hakuna ambaye hakugeuka kumtazama kila alipopita . Juu alivaa blauzi laini iliyokifanya kifua chake kionekane vizuri, kichwani akiwa ametengeneza nywele na kuzibana katika mtindo wa kisasa kabisa na kumfanya apendeze mno . “ Habari za asubuhi Dickson, ” alisema msichana huyo huku akinyoosha mkono wake na kumpa Dickson, tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake . Alikuwa ananukia manukato mazuri yaliyomfanya Dickson ajihisi kama yupo kwenye dunia ya tofauti. Alishindwa kujibu kwa wakati , akabaki amemtumbulia macho msichana huyo huku tabasamu hafifu likianza kuchanua kwenye uso wake. Alimshika mkono kwa sekunde kadhaa akiwa bado amezubaa vilevile mpaka msichana huyo alipovunja ukimya kwa kumsalimia tena . “ Ooh! Samahani, akili zilikuwa mbali kidogo, umependeza sana , utafikiri malaika, ” alisema Dickson na kusababisha msichana huyo aangue kicheko kwa nguvu , meno yake meupe yaliyopangika vizuri yakaonekana na kumfanya Dickson azidi kuwa kwenye wakati mgumu kihisia. “ Nilitaka nikusalimie tu, basi tutaonana baadaye,” alisema msichana huyo na kubeba vizuri vitabu vyake , akageuka na kuanza kutembea harakaharaka kuelekea darasani sambamba na wanachuo wenzake wa mwaka wa kwanza . Dickson alibaki ameduwaa kwa sekunde kadhaa, akitazama sehemu za nyuma za msichana huyo ambazo zilikuwa zikitingishika kwa utaratibu maalum kufuata hatua alizokuwa anazipiga. Akamsindikiza kwa macho mpaka alipopotelea kwenye kundi la wanachuo wenzake, akatingisha kichwa huku akitabasamu na kuendelea na safari yake. Hata utulivu darasani siku hiyo ulipungua sana, wakati wenzake wakiwa makini kufuatilia walichokuwa wanafundishwa na mhadhiri aliyekuwa mbele kabisa ya ukumbi huo mkubwa, Dickson alikuwa akimuwaza Neema kiasi cha kumfanya asielewe chochote kilichokuwa kinaendelea . “ Ananipenda kweli au ananitania ? Halafu kitu gani kimemvutia kwangu? Mbona sina sifa yoyote ya kupendwa na msichana mrembo kama yeye? Isitoshe anaonekana kutokea kwenye familia inayojiweza sana kiuchumi, kanipendea nini?” Dickson aliendelea kuwaza kwa muda mrefu . Mpaka kipindi kinaisha, hakuwa ameambulia chochote kilichofundishwa siku hiyo . Mhadhiri wao alipotoka tu, Dickson alikuwa wa kwanza kutoka , akawa anatembea harakaharaka kuelekea kwenye majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza kusomea . Hata hivyo , alikuwa amechelewa kwani wanachuo wote wa mwaka wa kwanza walikuwa wameshamaliza vipindi vya asubuhi na kutawanyika kusubiri awamu ya pili ya kuingia tena darasani . Dickson hakukata tamaa , akawa anazunguka huku na kule kujaribu kumtafuta Neema bila mafanikio. Kila alikokuwa anapita , wanachuo wa mwaka wa kwanza ambao wengi walikuwa hawamjui, walikuwa wakimshangaa , huku wengine wakimkimbia , hasa wasichana . Hali hiyo iliitibua kabisa furaha aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake . Alipoona wanachuo hao wanazidi kumshangaa , aliamua kuacha kazi ya kumtafuta Neema , akarudi kwenye hosteli aliyokuwa anaishi huku akionesha kuwa na huzuni kutokana na jinsi wale wanachuo wengine walivyokuwa wanamshangaa . Hakutaka kuzungumza na mtu , akaenda kujilaza kitandani kwake huku akiendelea kutafakari hili na lile kuhusu maisha yake. Akiwa amelala juu ya kitanda chake, alisikia akiitwa na mwenzake waliyekuwa wakikaa naye chumba kimoja . “ Kuna mgeni wako anakutafuta huku, ” alisema mwenzake aliyekuwa akifua nguo nje ya hosteli hiyo . “ Mgeni gani bwana, tangu lini mimi nikatembelewa na wageni ?” alisema Dickson huku akijigeuza pale kitandani . “ Ni mimi Dickson !” sauti laini ya kike ilisikika kutoka nje , harakaharaka akakurupuka pale alipokuwa amelala, akiwa ni kama haamini alichokisikia. Akatoka lakini kabla hajafika nje , alikutana na Neema koridoni akiingia huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.



    Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono . Fedha zake zote zinaishia kwa machangudoa na anaendelea na tabia hiyo mpaka anapoingia mwaka wa tatu chuoni hapo. Msichana mdogo aliyekuwa akisoma mwaka wa kwanza chuoni hapo, anatokea kumpenda Dickson, jambo ambalo halijawahi kumtokea . Ukaribu kati yao unazidi kuongezeka. Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya kugonga ukuta kwa jitihada za nguvu za Dickson kujaribu kumtafuta Neema muda mfupi baada ya kumaliza kipindi kutokana na jinsi wanachuo wa mwaka wa kwanza walivyokuwa wakimshangaa , aliamua kwenda kwenye hosteli aliyokuwa akiishi na kujibwaga kitandani huku mawazo mengi yakiendelea kuzunguka ndani ya kichwa chake. Akiwa kwenye hali hiyo , mwanachuo mwenzake waliyekuwa wakiishi pamoja kwenye hosteli hiyo , alimuita na kumwambia kuwa kulikuwa na mgeni wake nje lakini mwenyewe akapuuza. Muda mfupi baadaye akamsikia msichana huyo akiingia, moyo wake ukashtuka na mapigo kuanza kumuenda kasi. Hakuweza kuamini kwamba msichana huyo anaweza kuwa na kichwa chepesi kiasi chaa kukariri chumba anachoishi kwa kumtajia mara moja tu . “ Karibu,” alisema Dickson huku akitabasamu, uso wake ukiwa umejawa na haya kwani hakutegemea ugeni kwa muda huo. “ Ahsante, ” alisema msichana huyo na kupeana mkono na Dickson, wakaingia mpaka ndani huku bado Dickson akiendelea kujishtukia. Wakaanza kupiga stori za hapa na pale , msichana huyo akionesha kuwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake kufahamu chumba anachoishi Dickson. Mazungumzo ya kawaida yaliendelea kwa muda mrefu huku wakicheka na kufurahi pamoja. Kadiri walivyokuwa wakizidi kupiga stori za hapa na pale, ndivyo hofu ilivyokuwa inapungua ndani ya moyo wa Dickson kwani kiuhalisia hakuwa na mazoea ya kuzungumza ana kwa ana na msichana , tena mrembo kama Neema. Kwa upande wa Neema, naye moyo wake ulitokea kumpenda tu Dickson kwani licha ya ubaya wa sura yake, macho yake mekundu yanayotisha na vinyweleo vingi vilivyotapaa sehemu kubwa ya mwili wa kijana huyo, alijikuta akivutiwa naye na kutamani kuendelea kukaa karibu yake. Hata muda wa kuingia kwenye vipindi vya masomo ya mchana ulipofika, Si Dickson wala Neema aliyekuwa na habari , walipokuja kushtuka baadaye, hosteli zote zilikuwa kimya kabisa kuashiria kwamba wenzao walikuwa wameshaingia madarasani . Dickson akainuka pale kwenye kitanda alipokuwa amekaa na msichana huyo mrembo na kwenda mpaka kwenye mlango wa chumba hicho, akachungulia huku na kule , alipoona hakuna mtu , aliufunga kwa ndani na kurudi pale alipokuwa amemuacha msichana huyo. Akakaa pembeni yake, safari hii akiwa amemsogelea zaidi kiasi cha kila mmoja kuanza kuyasikia mapigo ya moyo ya mwenzake. Ni kama msichana huyo naye alikuwa anaisubiri nafasi hiyo kwani alijilegeza mwili wake kama mtoto mchanga anayetaka kulala, akaegamia kifua cha Dickson huku naye pumzi zake zikimuenda mbio . “ Nee… ma, ” aliita Dickson kwa sauti nzito ya kukwaruzakwaruza , msichana huyo akaitikia kama hataki , kwa sauti iliyokuwa imejaa huba ndani yake. “ Na … ku . . penda sa … , ” alisema Dickson lakini kabla hajamalizia kauli yake, msichana huyo alimvutia kwake na kumkumbatia kwa nguvu kisha wakagusanisha ndimi zao . Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Dickson kufanyiwa kitendo hicho, akawa hata hajui na yeye afanye nini. Licha ya kuwa na orodha ndefu ya machangudoa ambao alikuwa amevunja nao amri ya sita ndani ya kipindi kifupi tu tangu ajiunge na chuo hicho, Dickson hakuwahi kukutana na mwanamke aliyekuwa akimfanyia uchokozi wa kimahaba kama ilivyokuwa kwa msichana huyo mdogo . Alishazoea kwamba akiopoa changudoa, wanaingia gesti na kuzima taa kisha kazi inafanyika chapchapu na kila mmoja kuendelea na hamsini zake kama wafanyavyo machangudoa wengi na wateja wao. Hali ilikuwa tofauti mno siku hiyo , Dickson akajikuta akianza kutokwa na kijasho chembamba wakati msichana huyo akiendelea kumfanyia visa vya hapa na pale , akawa anamwagia mvua ya mabusu shingoni huku akiwa amemkumbatia kwa nguvu, mikono yake ikivinjari sehemu mbalimbali za mwili wake . Hisia za mapenzi zilizidi kuwa kali zaidi kwa Dickson, akawa anaendelea kugugumia huku akitoa sauti za miguno ambazo kama wanachuo wengine wa vyumba jirani wangekuwepo, wangeweza kuzisikia kila kipingamizi chochote. Baada ya kuona uzalendo unamshinda, ilibidi Dickson amuombe msichana huyo wavunje amri ya sita lakini tofauti na alivyotegemea , Neema alikataa na kueleza kuwa hawezi kufanya hivyo mpaka atakapokuja kufunga ndoa halali . “ Si unajua kwamba ni dhambi ? Isitoshe mi bado mdogo nikipata mimba huoni itakuwa hatari kwangu, ” alijitetea Neema huku akijitoa kwenye mwili wa Dickson ambaye alishachanganyikiwa kabisa. Akili yake ilikuwa inahitaji jambo moja tu ; ngono . Dickson aliendelea kubembeleza lakini msichana huyo naye aliendelea kushikilia msimamo wake mpaka muda wa wanachuo wengine kutoka darasani ulipowadia . Dickson hakuwa na ujanja , akakubali yaishe lakini akiwa amebaki na maumivu makubwa ndani ya moyo wake . Kwa kuwa hakutaka wanachuo wengine wamkute chumbani akiwa na Dickson, Neema aliaga harakaharaka na kuvaa nguo zake vizuri, akatoka na kumuacha Dickson akiwa amelala palepale kitandani , akiwa hajiwezi kutokana na kuzidiwa na hisia za mapenzi . Alijikaza na kuinuka , akaelekea bafuni ambako kwa hasira aliamua kutumia muda mrefu akijichua mpaka alipokidhi haja zake. Akarudi kitandani ambapo tayari wenzake walikuwa wamesharejea. Akasingizia kwamba hakuingia darasani kwa sababu hakuwa akijisikia vizuri. Aliendelea kujilaza pale kitandani kwa muda mrefu huku bado akiwa anaendelea kuteseka na hisia kali za mapenzi . Baadaye alipoona hali yake inazidi kuwa mbaya , ilibidi aelekee tena bafuni na aliporudi , alianza kujiandaa. “ Vipi huingii vipindi vya jioni ?” mwanachuo mwenzake mmoja alimuuliza baada ya kumuona akijiandaa kama mtu aliyekuwa na safari ya nje ya chuo. “ Nafuata dawa mara moja nikiwahi nitaingia , ” alidanganya Dickson . Japokuwa bado ilikuwa mapema, akili zake zilimtuma kwenda kutafuta changudoa yeyote ili akidhi haja zake kwani ni kama Neema alikuwa ameyaamsha mashetani yaliyokuwa yamelala kwenye kichwa chake. Alitoka akiwa na imani hakuna anayemuona , akapita njia yake ileile na kutoka mpaka nje ya chuo. Neema ambaye naye alikuwa akimfuata tena Dickson ili wakae tena pamoja, alimuona kwa mbali akiondoka, ikabidi aanze kumkimbilia kimyakimya bila kumuita. Akashangaa kumuona anapita njia za vichochoroni na hatimaye akatokezea barabarani. Na yeye akapita njia ileile bila Dickson kujua kwamba kuna mtu alikuwa akimfuatilia kwa nyuma.Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa

    mtumwa wa ngono .



    Fedha zake zote zinaishia kwa machangudoa na anaendelea na tabia hiyo mpaka anapoingia mwaka wa tatu chuoni hapo. Msichana mdogo aliyekuwa akisoma mwaka wa kwanza chuoni hapo, anatokea kumpenda Dickson , jambo ambalo halijawahi kumtokea . Hata hivyo , msichana huyo hayupo tayari kuanza kufanya mapenzi na Dickson mpaka watakapokuja kufunga ndoa, jambo ambalo kijana huyo haliafiki na kuamua kwenda tena kutafuta machangudoa . Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya Neema kukataa katakata kufanya mapenzi na Dickson, alimuacha kwenye hali mbaya sana kihisia. Akajaribu kutumia mbinu ya kwenda kujichua bafuni kama alivyokuwa akifanya kwa muda mrefu lakini haikusaidia chochote. Uamuzi wa mwisho aliofikia ulikuwa ni kwenda kutafuta changudoa wa kukidhi haja zake. Hakuwa na habari kwamba wakati akitoka kupitia njia za vichochoroni, Neema naye alikuwa akimfuatilia kwa nyumanyuma akitaka kujua alikuwa akielekea wapi muda huo. Baada ya kufika barabarani , kama kawaida, Dickson alisimamisha bodaboda na kumuelekeza dereva kumpeleka Sinza Afrika Sana . Akapanda na safari ikaanza , huku kama kawaida akiwa amevaa kofia kichwani iliyoziba sehemu kubwa ya uso wake . “ Anaenda wapi? Mbona simuelewi ?” Neema alisema huku naye akiipungia mkono bodaboda iliyokuwa inakuja upande wake, ikasimama ambapo bila kupoteza muda , alipanda na kumuelekeza dereva kuifuatilia bodaboda aliyopanda Dickson ambayo tayari ilishafika mbali. Wakaondoka kwa kasi huku dereva akitii alichoambiwa . Dakika chache baadaye, walikuwa kwenye mzunguko wa Mlimani City , dereva akakunja upande wa kushoto na kushika Barabara ya San Nujoma kumfuata dereva yule wa bodaboda aliyembeba Dickson . “ Usiwapite, endelea kuwafuata nyumanyuma mpaka wanakoelekea , ” alisema Neema baada ya kuona wamewakaribia akina Dickson eneo la vinyago , Mwenge. Walipokata kona upande wa kulia nao waliwafuata na kuingia barabara ya TRA ambapo walinyoosha mpaka Afrika Sana. Wote wakashuhudia bodaboda iliyombeba Dickson ikisimama jirani na kituo cha mafuta eneo la Sinza Afrika Sana. Harakaharaka Neema naye alishuka na kumlipa dereva huyo . Kwa kuwa alishukia mbali haikuwa rahisi kwa kijana huyo kumuona. Akasimama pembeni ya magari yaliyokuwa yamepaki na kuendelea kumtazama Dickson . Alipomuona amevuka barabara na kuhamia upande wa pili , naye alitoka pale alipokuwa amejificha na kutembea harakaharaka mpaka kwenye barabara ya lami ya Shekilango, naye akavuka kuelekea upande ule alioelekea Dickson. Alimfuatilia kwa makini mpaka alipoenda kukaa kwenye viti vingi vilivyokuwa vimepangwa mita chache kutoka barabarani. Akamshuhudia akiagiza soda na kuanza kunywa taratibu . Kwa tahadhari kubwa, Neema naye alitafuta sehemu na kukaa , harakaharaka wahudumu wakamfuata kumhudumia . Naye aliagiza soda tu kama Dickson , akawa anaendelea kumfuatilia Dickson kwa makini kwani alionekana kuwa kwenye harakati za kufanya jambo fulani ambalo msichana huyo hakuwa akijua ni jambo gani . Akiwa bado amekaa eneo hilo, Neema alishtushwa na wingi wa wasichana waliokuwa wakirandaranda huku na kule , wengi wakiwa wamevaa nusu utupu japokuwa bado giza lilikuwa halijaingia kabisa. Bila hata kuuliza, alitambua kwamba hao ni machangudoa kutokana na mavazi ya ajabu waliyokuwa wamevaa, yaliyoacha sehemu kubwa za miili yao wazi na jinsi walivyokuwa wakigombea wanaume . “ Psiii ! Psiii !” ilisikika sauti kutoka kwa mmoja kati ya watu waliokuwa wamekaa upande aliokuwepo Dickson . Neema ambaye alikuwa ameinyanyua chupa ya soda ili anywe , alishtuka kuona wanawake zaidi ya wanne waliokuwa wamevaa nusu utupu wakipigana vikumbo kuelekea pale Dickson alipokuwa amekaa. Baada ya sekunde chache, wale wengine waliondoka na kubakia mmoja ambaye alikuwa na umbo kubwa lililogawanyika vizuri na kubinuka sehemu ya nyuma. Neema akiwa bado amepigwa na butwaa , alimuona Dickson akiinuka na yule mwanamke, wakatoka eneo hilo na kuelekea upande wa nyuma. “ Dickson ananunua machangudoa? Mungu wangu, ” alisema msichana huyo huku akiinuka kwa tahadhari na kuanza kuwafuatilia kwa nyuma ili kuhakikisha kama kile alichokuwa anakihisi ndicho walichokuwa wanaenda kukifanya . Kwa macho yake, aliwashuhudia wawili hao wakiingia kwenye nyumba iliyokuwa upande wa nyuma wa baa hiyo , iliyokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka ‘ Catalonia Guest House ’ . Neema alijikuta akitetemeka kama aliyemwagiwa maji ya baridi, hakutaka kabisa kuamini kwamba mwanaume ambaye saa kadhaa zilizopita walikuwa pamoja chumbani, wakifanyia michezo ya kimahaba iliyozihamisha hisia za kila mmoja , sasa hivi alikuwa akienda kufanya ngono na changudoa, tena aliyemzidi umri na umbo . Ndani ya nafsi yake alijikuta akijilaumu kutokana na hatua yake ya kuamua kumfuatilia Dickson kwani maumivu aliyokuwa anayahisi ndani ya moyo wake yalikuwa sawa na mtu aliyechomwa na mkuki mkali moyoni. Kwa upande mwingine , alimshukuru Mungu wake kumuonesha suala lile kwani kama asingegundua mapema, angeendelea kumpenda mtu ambaye kumbe ana tabia hatarishi kama hiyo , ambazo zingeweza kusababisha aambukizwe magonjwa hatari ukiwemo Ukimwi. Licha ya kujifariji lakini bado moyo wake uliendelea kumuuma sana hasa kutokana na jinsi alivyokuwa akimpenda kijana huyo licha ya kasoro zote alizokuwa nazo . Uchungu mkali aliokuwa nao ndani ya nafsi yake ulisababisha ashindwe kuyazuia machozi yasiulowanishe uso wake . Akawa anatembea taratibu kurudi pale alipokuwa amekaa awali huku akiendelea kulia kwa uchungu mithili ya mtu aliyepokea taarifa za msiba . Hakuweza kukaa tena pale alipokuwa amekaa awali wala hakuweza kumalizia hata soda yake. Aliamua kuondoka , akawa anatembea taratibu kuelekea kwenye barabara ya lami kwa lengo la kuvuka hadi upande wa pili ili akapande bodaboda ya kumrudisha chuoni. Bado alikuwa akiendelea kulia kwa uchungu kwani hakutegemea kama Dickson anaweza kuwa anajihusisha na mchezo hatari kama huo . Baada ya Dickson kukidhi haja zake, alitoka harakaharaka kwenye chumba cha gesti alichokuwa ameingia na yule changudoa na kumuacha akiendelea kuvaa nguo zake. Kwa kuwa kilichompeleka tayari alishakipata , hakutaka kuendelea kukaa eneo hilo. Akawa anaelekea barabarani kwa lengo la kuvuka kwenda kutafuta usafiri wa kumrudisha chuoni lakini akiwa amekaribia kuvuka barabara, alishtushwa na kelele za watu waliokuwa wanakimbilia barabarani . “ Amegonga mtu ! Daah , sijui kama atapona yule dada , ” alisema mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo. Dickson akawa miongoni mwa watu waliokuwa wanakimbilia eneo huku akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichotokea.



    Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono , anaendelea na mchezo huo mpaka anapoingia mwaka wa tatu chuoni hapo. Msichana mdogo aliyekuwa akisoma mwaka wa kwanza chuoni hapo, Neema, anatokea kumpenda Dickson, jambo ambalo halijawahi kumtokea . Hata hivyo , msichana huyo hayupo tayari kuanza kufanya mapenzi na Dickson , jambo linalosababisha kijana huyo aende tena kununua machangudoa bila kujua kuwa Neema alikuwa akimfuatilia kwa nyuma . Kwa macho yake anamshuhudia Dickson akinunua changudoa, jambo linalomuumiza sana . Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya Neema kumshuhudia kwa macho yake mwenyewe, Dickson akinunua changudoa na kuelekea naye gesti , alijisikia maumivu makali mno ndani ya moyo wake. Licha ya kujipa moyo kwamba afadhali ameujua ukweli mapema, bado maumivu makali yaliendelea kumtesa kiasi cha kuamua kuondoka kabisa eneo hilo, huku machozi yakimtoka. Akaelekea barabarani kwa lengo la kuvuka Barabara ya Shekilango ili atafute usafiri wa kumrudisha chuoni, huku mawazo mengi yakizidi kukitesa kichwa chake, akawa anahisi kama amebeba jiko la mkaa kichwani mwake . Machozi yakawa yanaendelea kumtoka na kuulowanisha uso wake mzuri . Hata alipokuwa anavuka barabara , hakukumbuka kuangalia magari huku na kule kabla ya kuvuka, akajikuta ameingia barabarani huku akiendelea kulia kwa uchungu. Penzi la Dickson lilimtesa mno , upande mwingine akawa anajilaumu kwamba kama mchana wa siku hiyo angekubali kufanya mapenzi na Dickson, huenda hayo yote yasingetokea . “ Lakini mimi sijawahi kufanya mapenzi na nimejiwekea nadhiri kwamba sitampa ruhusa mwanaume yeyote auguse mwili wangu mpaka nitakapo …” Neema aliendelea kuwaza lakini kabla hajamalizia , alishtukia honi kali zikipigwa upande wake wa kushoto, alipogeuka, gari dogo la kifahari , Toyota Mark X tayari lilishamfikia mwilini. Licha ya dereva kujitahidi kufunga breki kali, gari hilo lilimgonga Neema na kumrusha mita kadhaa juu , akadondoka katikati ya lami na kusababisha taharuki kubwa eneo hilo. *** Baada ya kukidhi haja zake, Dickson alitoka harakaharaka kwenye chumba cha gesti alichoingia na changudoa yule kama ilivyokuwa kawaida yake. Kwa kuwa kazi iliyomleta alishaimaliza, hakutaka kuendelea kukaa eneo hilo. Akawa anaondoka kwa lengo la kuvuka barabara na kuchukua usafiri wa kumrudisha chuoni lakini ghafla alipoikaribia barabara , alishtushwa na umati wa watu uliokuwa umekusanyika barabarani huku watu wengine wengi wakikimbilia eneo hilo. “ Kuna nini kimetokea pale ?” Dickson alimuuliza mmoja kati ya watu wengi waliokuwa wanakimbilia eneo hilo. “ Amegonga mtu ! Daah , sijui kama atapona yule dada , ” alisema mtu huyo huku akizidisha mwendo , Dickson naye akaongeza mwendo mpaka mahali mtu aliyegongwa alipokuwa ameangukia. “ Ooh my God! Neema , what happened to you?” (Mungu wangu ! Neema, nini kimekutokea?) “ Mnafahamiana?” Patrick Buzohela, mwandishi mahiri kutoka Kituo cha Runinga cha Global TV , alimhoji Dickson huku akimsogezea ‘ maikrofoni ’ mdomoni, mwandishi mwingine akiwa makini kuchukua picha za video kwa ajili ya kurusha kwenye runinga hiyo . “ Ni mwanachuo mwenzangu , tunasoma naye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ” alisema Dickson kwa sauti ya juu huku akiwasukuma watu wote na kwenda mpaka pale chini msichana huyo alipokuwa ameangukia, damu nyingi zikimtoka puani, mdomoni na kwenye majeraha mengi aliyoyapata . Patrick na mwenzake waliendelea kuchukua picha za tukio hilo kwa umakini mkubwa, wakawa wanarekodi kila kitu kilichokuwa kinaendelea pamoja na kuwahoji baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo . Bila kujali chochote, Dickson alimuinua na kuanza kuomba msaada kwa mtu yeyote mwenye usafiri ili wamkimbize hospitali . Bahati nzuri , gari lililomgonga halikuwa limeharibika sana , dereva akashuka huku akitetemeka na kukubali kumkimbiza hospitalini . Kwa kuwa askari wa usalama barabarani hawakuwa mbali na eneo hilo, walifika na kuchukua taarifa zote muhimu kisha wakaruhusu mgonjwa akimbizwe hospitalini . Dickson akiwa kwenye siti ya nyuma ya gari hilo, alimpakata Neema ambaye damu nyingi zilikuwa zikiendelea kumvuja na kumlowanisha kijana huyo mwilini lakini mwenyewe hakujali. Muda mfupi baadaye, tayari walikuwa wamewasili kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo waliteremka na kupokelewa na wahudumu waliomlaza msichana huyo kwenye kitanda cha magurudumu na kumkimbiza wodini. Tayari giza lilishaanza kuingia . Dickson akawasaidia mpaka walipofika kwenye mlango wa wodi ya wagonjwa mahututi ambapo hakuruhusiwa kuingia . Msichana huyo ambaye alishapoteza fahamu kuanzia muda uleule aliogongwa na gari , aliingizwa wodini ambapo madaktari walianza kuhangaika kuokoa maisha yake. “ Mgonjwa ni nani yako?” “ Ni mwanachuo mwenzangu . ” “ Mnasoma wapi?” “ Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ” alisema Dickson wakati akitoa maelekezo kwa mtu aliyekuwepo mapokezi , kwa ajili ya kuandaa faili la mgonjwa . Baada ya kumaliza kutoa maelezo hayo , Dickson ambaye damu nyingi zilizokuwa zimemvujia kwenye nguo zake zilikuwa zimeanza kukauka, alienda kukaa kwenye benchi lililokuwa jirani na wodi ya wagonjwa mahututi . Tayari Kituo cha Runinga cha Global TV kilikuwa kikiirusha habari ya mwanachuo huyo kugongwa na gari na kueleza kila kitu kilichokuwa kinaendelea mpaka muda huo . Watu wengi, wakiwemo wanachuo wenzake wakasikia taarifa hiyo na kuanza kukusanyana kuelekea hospitalini . Maswali mengi yaliyokosa majibu yaliendelea kupita kwenye kichwa cha Dickson, akiwa haelewi ilikuwaje mpaka Neema akafika eneo hilo na kupata ajali mbaya kiasi hicho. Aliendelea kujiuliza maswali mengi ambayo hakuna hata moja alilopata jibu lake. “ Au alikuwa ananifuatilia nini? Lakini haiwezekani , alijuaje kwamba nimekuja huku?” alijiuliza lakini akajipa moyo mwenyewe. Aliendelea kukaa kwenye benchi hilo kwa muda mrefu mpaka baadaye aliposhtukia viongozi wa serikali ya wanachuo na baadhi ya wahadhiri wakija kwa wingi hospitalini hapo. “ Kumetokea nini Zinja ?” “ Neema kapata ajali mbaya , amegongwa na gari. ” “ Neema yupi ? Yule mwanachuo wa mwaka wa kwanza mliyekuwa mmekaa naye jana wakati wa chakula cha jioni ?” “ Ndiyo huyohuyo ,” alijibu Dickson na kuinamisha kichwa chake chini . Maswali aliyokuwa anaulizwa na wanachuo wenzake yalizidi kumtia uchungu na kusababisha machozi yaanze kumlengalenga . Muda mfupi baadaye, mlango wa wodi ya wagonjwa mahututi ulifunguliwa, watu wote wakasimama wakiwa na shauku kubwa ya kusikia chochote juu ya hali ya mwanachuo mwenzao.



    Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono , anaendelea na mchezo huo mpaka anapoingia mwaka wa tatu chuoni hapo. Msichana mdogo aliyekuwa akisoma mwaka wa kwanza chuoni hapo, Neema, anatokea kumpenda Dickson, jambo ambalo halijawahi kumtokea . Hata hivyo , msichana huyo hayupo tayari kuanza kufanya mapenzi na Dickson , jambo linalosababisha kijana huyo aende tena kununua machangudoa bila kujua kuwa Neema alikuwa akimfuatilia kwa nyuma . Kwa macho yake anamshuhudia Dickson akinunua changudoa, jambo linalomuumiza sana . Anapoteza umakini na kujiingiza barabarani bila kuangalia magari, jambo linalosababisha agongwe vibaya. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Baada ya Neema kumshuhudia kwa macho yake mwenyewe, Dickson akinunua changudoa na kuelekea naye gesti , alijisikia maumivu makali mno ndani ya moyo wake. Licha ya kujipa moyo kwamba afadhali ameujua ukweli mapema, bado maumivu makali yaliendelea kumtesa kiasi cha kuamua kuondoka kabisa eneo hilo, huku machozi yakimtoka. Akaelekea barabarani kwa lengo la kuvuka Barabara ya Shekilango ili atafute usafiri wa kumrudisha chuoni, huku mawazo mengi yakizidi kukitesa kichwa chake, akawa anahisi kama amebeba jiko la mkaa kichwani mwake . Machozi yakawa yanaendelea kumtoka na kuulowanisha uso wake mzuri . Wanachuo wengi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani ) waliendelea kufurika kwenye Hospitali ya Mwananyamala baada ya kuona taarifa ya habari ya dharura ( breaking news ) kupitia Kituo cha Runinga cha Global TV . Wakiwa nje ya wodi ya wagonjwa mahututi aliyolazwa msichana huyo aliyepata ajali mbaya ya kugongwa na gari , mara mlango ulifunguliwa, madaktari wawili wakatoka wakionekana kuwa na haraka sana . Wanachuo wote wakasimama , wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua hali ya mwenzao. “ Bado hali siyo nzuri , tunafikiria kumkimbiza Muhimbili, ” alisema daktari aliyekuwa amevalia koti jeupe , shingoni akiwa na kifaa cha kupimia mapigo ya moyo au kwa kitaalamu Stethoscope. Kauli hiyo ilimnyong’ onyeza kila mmoja kwani ilivyoonekana hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya sana. Muda mfupi baadaye, gari la kubebea wagonjwa ( ambulance ) liliwasili eneo hilo na kupelekwa mpaka jirani kabisa na mlango mkubwa wa kuingilia kwenye wodi hiyo . Manesi kwa kushirikiana na madaktari, wakasaidiana kumtoa msichana huyo kutoka kwenye wodi ya wagonjwa mahututi na kumpakiza kwenye gari la kubebea wagonjwa. Gari hilo likaondoka kwa kasi huku likiwa limewashaa taa zote na lilipotoka eneo la hospitali hiyo , lilianza kupiga ving ’ ora . Ilibidi viongozi wa serikali ya wanachuo waitane na kuwakusanya wanachuo wote waliokuwa wamefurika hospitalini hapo , wakawasihi kwamba ni vyema wakarejea chuoni na wachache kati yao wataenda kuwawakilisha kufuatilia hali ya mgonjwa . “ Muda umeshaenda sana na giza linazidi kutanda kila mahali , nashauri nyote mrejee chuoni halafu sisi viongozi wenu na baadhi ya rafiki zake wa karibu tutaelekea Muhimbili kufuatilia kinachoendelea . Nawaomba wote muwe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu ,” rais wa serikali ya wanachuo, aliwaambia wenzake. Japokuwa kila mmoja alikuwa na shauku ya kutaka kwenda Muhimbili , maelezo hayo ya kiongozi wao yaliwafanya wanachuo kukubaliana na kilichosemwa. Safari ya kurejea chuoni ikaanza huku kila mmoja akizungumza lake, wengi wakimuonea huruma msichana huyo kwa kilichotokea. Wengine walikuwa wakihoji alikuwa akitokea wapi mpaka apate ajali hiyo kwani kulikuwa na umbali mrefu kutoka chuoni mpaka eneo kulipotokea ajali, Sinza Afrika Sana. “ Halafu ilikuwaje mpaka Zinja naye afike eneo la tukio haraka kwenda kutoa msaada ? Au walikuwa pamoja?” mwanachuo mmoja alihoji wakati wakirejea chuoni. Hakuna aliyekuwa na majibu ya kilichotokea. Viongozi wa serikali ya wanachuo na watu wengine wachache, akiwemo Dickson walielekea Muhimbili ambapo mpaka wanawasili, tayari mgonjwa alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu kwenye wodi ya wagonjwa mahututi . “ Amepata madhara makubwa kwenye uti wa mgongo na fuvu la kichwa , tunaendelea kuchunguza kwa kina ukubwa wa madhara hayo na kutafuta njia ya kumsaidia lakini kazi haitakuwa nyepesi, ” alisema Dokta Innocent Nzunda wakati akizungumza na Dickson pamoja na wenzake walioongozana nao kutoka Hospitali ya Mwananyamala. “ Msaidieni dokta apone , niko chini ya miguu yenu , ” alisema Dickson huku akilia kama mtoto mdogo , wenzake wakawa na kazi ya kumbembeleza. Hakuna kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea kama Neema kupoteza maisha . Alitamani na yeye angekuwa daktari ili aingie mwenyewe wodini kwani alihisi madaktari hao hawajitumi ipasavyo kumsaidia mpenzi wake huyo. Bado alikuwa akiendelea kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu kuhusu mazingira ya ajali yenyewe. Hakujua Neema alikuwa akitoka wapi mpaka akapata ajali hiyo mbaya , bado akili nyingine zilikuwa zikimtuma kuamini kwamba huenda msichana huyo alikuwa akimfuatilia nyumanyuma na alishuhudia wakati Dickson akimnunua changudoa na kuingia naye gesti na huenda ndiyo sababu iliyomfanya Neema akose umakini na kujikuta akigongwa na gari. “ Hapana! Haiwezi kuwa hivyo , haiwezekani , ” Dickson alizungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya wenzake waliokuwa pembeni yake wamshangae . “ Nini hakiwezekani Dickson?” mmoja wao alimuuliza , ikabidi avunge kwamba alikuwa akimaanisha haiwezekani Neema apoteze maisha . “ Usiwe na wasiwasi sana , yupo kwenye mikono salama, si unaona jinsi madaktari wanavyopishana kuingia na kutoka kwenye wodi aliyolazwa ? Cha msingi ni kuendelea kumuombea kwa Mungu , ” alisema kiongozi wao lakini bado Dickson alionekana kuendelea kuwaza kwa uchungu , machozi yakimtoka na kuulowanisha uso wake . Dakika kadhaa baadaye, Dokta Nzunda alitoka wodini na kuwasogelea akina Dickson, nao wakainuka pale walipokuwa wamekaa kila mmoja akionekana kuwa na shauku kubwa ndani ya moyo wake kutaka kusikia daktari huyo atasema nini. “ Jamani hali siyo nzuri sana, mwenzenu amevunjika uti wa mgongo na pia damu imevujia ndani ya fuvu la kichwa chake, tunamuandaa kwa ajili ya upasuaji mkubwa utakaofanyika usiku huuhuu , mzidi kumuombea kwa Mungu wakati na sisi tukitimiza majukumu yetu , ” alisema Dokta Nzunda . Kauli hiyo ilikuwa sawa na mkuki ndani ya moyo wa Dickson, japokuwa hakuwa akijua chochote kuhusu mambo ya kitabibu lakini maelezo ya daktari huyo yalitosha kumfanya ajue kwamba kazi ya kuokoa maisha ya msichana huyo haikuwa nyepesi.



    kununua machangudoa bila kujua kuwa Neema alikuwa akimfuatilia kwa nyuma . Kwa macho yake anamshuhudia Dickson akinunua changudoa, jambo linalomuumiza sana . Anapoteza umakini na kusababisha agongwe na gari na kupoteza fahamu. Anapelekwa hospitali hali yake ikiwa mbaya sana .Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … “ Jamani hali siyo nzuri sana, mwenzenu amevunjika uti wa mgongo na pia damu imevujia ndani ya fuvu la kichwa chake, tunamuandaa kwa ajili ya upasuaji mkubwa utakaofanyika usiku huuhuu , mzidi kumuombea kwa Mungu wakati na sisi tukitimiza majukumu yetu , ” alisema Dokta Nzunda aliyekuwa akisimamia matibabu ya msichana huyo. Kauli hiyo ilikuwa sawa na mkuki ndani ya moyo wa Dickson, japokuwa hakuwa akijua chochote kuhusu mambo ya kitabibu lakini maelezo ya daktari huyo yalitosha kumfanya ajue kwamba kazi ya kuokoa maisha ya msichana huyo haikuwa nyepesi. Palepale Dickson alipiga magoti na kuinua mikono juu kama ishara ya mtu anayeomba , akafumba macho yake na kuanza kusali kimyakimya, akimuomba Mungu aoneshe miujiza yake kwa kumnusuru Neema na kifo kwani hali yake ilishakuwa tete. Japokuwa watu walianza kumshangaa , huku wengine wakihisi anaelekea kuchanganyikiwa , mwenyewe hakujali, aliendelea kusali huku machozi yakimtoka kwa wingi. “ Dickson, unahitaji kwenda kupumzika kidogo. ” “ Siwezi kupumzika wakati Neema yupo mahututi , nitakaa hapahapa mpaka nione mwisho wake . ” “ Tazama nguo ulizovaa zimekaukia damu kibao , kwa nini usiende mara moja chuoni japo ukaoge na kubadilisha nguo ? Atakuwa sawa si unaona madaktari wanavyomhangaikia?” kiongozi wa serikali ya wanachuo alikuwa akijaribu kumtuliza Dickson au Zinja kama wengi walivyozoea kumuita lakini ilikuwa ni sawa na kazi bure . Muda mfupi baadaye, mlango wa wodi ya wagonjwa mahututi ulifunguliwa, manesi kadhaa wakatoka wakiwa wanasukuma kitanda chenye magurudumu huku Neema akiwa juu yake, majeraha makubwa aliyoyapata yakiwa yamefungwa na bandeji . Bado hakuwa na fahamu hata kidogo . Dickson ambaye bado alikuwa amepiga magoti , harakaharaka aliinuka na kukimbilia kule manesi walikokuwa wanaelekea huku akiendelea kulia kwa uchungu . “ Usiondoke Neema , unaniacha na nani jamani ?” Dickson alisema huku akilia , machozi na kamasi vikimtoka mfululizo. “ Kaka tafadhali tunaomba utupe nafasi tufanye kazi yetu , kulia hakusaidii chochote kwa sasa, ” alisema nesi mmoja huku walinzi waliokuwa pembeni nao wakianza kumsogelea Dickson. Alitii alichoambiwa , kitanda cha magurudumu kikaendelea kusukumwa mpaka kwenye wodi iliyokuwa na maneno makubwa mlangoni yaliyosomeka THEATRE yakimaanisha chumba cha upasuaji . Milango ikafunguliwa, wakaingia kisha ikafungwa . Muda mfupi baadaye, madaktari kadhaa walionekana wakitembea harakaharaka kuelekea kwenye chumba cha upasuaji huku manesi wengine wakiwa wamebeba vifaa mbalimbali kwa ajili ya upasuaji. Kila mmoja alikuwa katika pilikapilika za kuhakikisha msichana huyo anapatiwa matibabu ya uhakika haraka iwezekanavyo ili kunusuru maisha yake. Tangu madaktari hao na manesi waingie kwenye chumba cha upasuaji, muda uliendelea kuyoyoma kwa kasi bila mlango kufunguliwa wala mtu yeyote kutoka au kuingia ndani ya chumba hicho cha upasuaji . Kwa muda wote huo, Dickson alikuwa amekaa nje , mita chache kutoka kwenye mlango wa kuingilia ndani ya wodi hiyo , akiendelea kusali na kumuomba Mungu wake aoneshe miujiza . Japokuwa kwa kipindi kirefu alikuwa amempa kisogo Mungu wake , akiwa ameshasahau hata mara ya mwisho kwenda kanisani ilikuwa ni lini , kipindi kigumu alichokuwa anapitia kilimfanya akumbuke kuwa kumbe Mungu yupo na ana uwezo wa kufanya hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu hayawezekani . Baada ya takribani saa sita kupita , ndipo kwa mara ya kwanza mlango wa wodi hiyo ulipofunguliwa, kitanda cha magurudumu kikatolewa huku manesi kadhaa wakikisukuma, wakionesha kuchoka mno . “ Anaendeleaje? Amezinduka? Nesi… amepona?” maneno mfululizo yalikuwa yakimtoka Dickson, akihangaika kama kuku anayetaka kutaga . Nesi mmoja alimjibu kwamba asiwe na wasiwasi kwani kazi imekamilika lakini bado mgonjwa hakuwa amerejewa na fahamu zake. Kidogo moyo wa Dickson ulitulia , akawa anawasindikiza kwa macho manesi hao wakati wakiendelea kukisukuma kitanda ambacho Neema alikuwa amelazwa juu yake, akiwa ameunganishwa na mashine ya kupumulia na kutundikiwa dripu iliyokuwa ikiendelea kushuka mishipani mwake kwa kasi. Alirudishwa mpaka kwenye wodi ya wagonjwa mahututi ambako aliendelea kutibiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari. Hata hivyo , licha ya madaktari kufanya kila kilichowezekana siku hiyo , bado msichana huyo hakuweza kurejewa na fahamu. Siku ya kwanza ikapita, Neema akiwa bado anapumulia mashine ndani ya wodi ya wagonjwa mahututi , siku ya pili nayo ikapita hali ikiwa bado vilevile . Mwisho Dickson akawa hana ujanja zaidi ya kukubali kurudi chuoni kupumzika kwani kwa zaidi ya saa 48, hakupata muda wa kupumzika hata kidogo. Akaondoka kwa shingo upande huku bado akiendelea kumuomba Mungu wake aoneshe miujiza kwa kumzindua msichana huyo kutoka kwenye usingizi wa mauti . Hakukaa sana chuoni, akarejea tena hospitalini ambako bado hali ilikuwa ileile, Neema alikuwa amelala tu kitandani , akiwa hajui chochote kilichokuwa kinaendelea kwenye ulimwengu wa kawaida.





    Jioni moja msichana huyo anaamua kumfuatilia Dickson na kwa macho yake anamshuhudia akinunua changudoa. Mshtuko anaoupata , unasababisha apoteze umakini na kujikuta akigongwa na gari linalomjeruhi vibaya na kukimbizwa hospitalini , hali yake ikiwa mbaya mno . Madaktari wanajaribu kumsaidia lakini kazi haiwi nyepesi. Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Siku ya kwanza ilipita , hali ya Neema ikiwa bado ni tete, akiendelea kupumulia mashine ndani ya wodi ya wagonjwa mahututi kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili . Hata siku ya pili ilipowadia , bado hali ya msichana huyo haikuwa ya kuridhisha. Mwisho Dickson akawa hana ujanja zaidi ya kukubali kurudi chuoni kupumzika na kwenda kubadilisha nguo kwani kwa zaidi ya saa 48, hakupata muda wa kupumzika hata kidogo. Akaondoka kurudi chuoni kwa shingo upande huku bado akiendelea kumuomba Mungu wake aoneshe miujiza kwa kumzindua msichana huyo kutoka kwenye usingizi wa mauti . Hakukaa sana chuoni, akarejea tena hospitalini ambako bado hali ilikuwa ileile, Neema alikuwa amelala tu kitandani , akiwa hajui chochote kilichokuwa kinaendelea kwenye ulimwengu wa kawaida. Wazazi wa msichana huyo walikuwa kwenye wakati mgumu zaidi kwani hakuna aliyekuwa tayari kuona mtoto wao huyo wa kipekee anapoteza maisha . Kwa kuwa kiuchumi walikuwa na uwezo mkubwa, walianza kujadiliana na baadhi ya ndugu wa karibu juu ya kufanya taratibu za kumsafirisha msichana huyo kwenda nchini India kwani kwa hali ilivyokuwa, isingekuwa rahisi kutibiwa na kupona nchini Tanzania . “ Kijana kwani wewe una uhusiano gani na mwenetu ? Unaonekana kuguswa sana na tangu mimi nije nakuona upo tu hapa hospitalini , ” mwanaume mmoja aliyekuwa na sura inayofanana na Neema, alimuuliza Dickson baada ya kumkuta amekaa kwenye benchi lililokuwa nje ya wodi aliyokuwa amelazwa msichana huyo. Dickson alibabaika kidogo kwani alijua kuwa lazima huyo anayezungumza naye ni baba wa msichana huyo au ndugu yake wa karibu kwa jinsi walivyokuwa wakifanana sura. “ Mimi ni rafiki yake wa karibu, naitwa Dickson. ”“ Oooh! Wewe ndiye Dickson uliyekuwa wa kwanza kumtambua baada ya kupata ajali?” “ Ndiyo mimi mzee . ” “ Sisi kama familia tunakushukuru sana kwa wema wako uliouonesha . Muda mrefu nilikuwa namtafuta mtu aliyemsaidia mwanangu , wala sikujua kama ni wewe. Mimi ndiye baba mzazi wa Neema , ” alisema mzee huyo na kushikana mikono na Dickson . Akaendelea kumshukuru na kumueleza kuwa sura yake haikuwa ikifanana na moyo wa kipekee aliokuwa nao. Mwisho akamueleza kuhusu uamuzi ambao wao kama wanafamilia walikuwa wameufikia , wa kumsafirisha msichana huyo mpaka nchini India kwa matibabu zaidi kwani vipimo vilionesha alikuwa na matatizo makubwa kwenye uti wake wa mgongo na kichwani . “ Tupo kwenye maandalizi ya mwisho ya kumpeleka India , endeleeni kutuombea , ” alisema mzee huyo na kabla hajahitimisha mazungumzo yake na Dickson , alikuja kuitwa na daktari mmoja waliyeongozana naye mpaka ofisini kwake. Japokuwa Dickson alikuwa anaomba usiku na mchana msichana huyo apone , alitamani aendelee kutibiwa hapohapo ili iwe rahisi kwake kuendelea kumuona lakini hakuwa na ujanja, akajiinamia huku machozi yakiendelea kumtoka. Maandalizi ya kumsafirisha Neema kwenda nchini India kwa matibabu yalizidi kupamba moto , Dickson akawa anafuatilia kila hatua, ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa wanachuo wenzake ili wapate nafasi ya mwisho ya kumuona msichana huyo kabla hajasafirishwa. Baada ya taarifa kuwafikia wanachuo wenzake, kwamba msichana huyo alikuwa mbioni kusafirishwa kwenda nchini India , walienda kwa wingi hospitalini hapo kumuangalia . Bado Neema hakuwa amerejewa na fahamu, hakuwa akimtambua mtu yeyote aliyekuwa akiingia wala kutoka kwenye wodi aliyokuwa amelazwa. Hali aliyokuwa nayo iliwaliza wanachuo wenzake wengi ambao baadhi walikuwa wakishindwa kuyazuia machozi yasizilowanishe nyuso zao . Wanachuo waliendelea kumiminika kwa wingi chuoni hapo mpaka ikabidi uongozi wa hospitali uingilie kati na kuwataka kuanza kuingia kwa awamu ili kuruhusu shughuli nyingine kuendelea hospitalini hapo. Wazazi wake nao waliendelea kuhangaika na baada ya muda mfupi , tayari maandalizi yalikuwa yameshakamilika , ikiwa ni pamoja na kupata nafasi kwenye ndege maalum iliyokuwa na chumba maalum cha kuhudumia wagonjwa kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini India . Hakukuwa na cha kusubiri tena , gari la kubebea wagonjwa liliandaliwa, Neema akatolewa wodini chini ya uangalizi wa madaktari na manesi wengi na kuingizwa ndani ya gari hilo la kubebea wagonjwa. Daktari mmoja aliyechaguliwa kusafiri pamoja na mgonjwa ili kuendelea kumhudumia wakati ndege ikiwa angani , naye tayari alishakuwa amejiandaa, wakaingia pamoja na wazazi wa msichana huyo kwenye gari hilo. Gari likawashwa na kuanza kuondoka hospitalini hapo kuelekea uwanja wa ndege huku wanachuo wengi waliokuwa wakisoma pamoja na msichana huyo wakiwa wanashuhudia kila kilichokuwa kinaendelea , wengine wakitokwa na machozi ya uchungu . Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Dickson ambaye muda wote alikuwa akilia kama mtoto mdogo na kusababisha macho yake yabadilike rangi na kuwa mekundu huku yakiwa yamevimba . “ Jikaze Dickson, ukilia sana utakuwa unamkufuru Mungu wako , piga moyo konde na tuendelee kumuombea kwa Mungu atapona tu, ” mwanachuo mmoja aliyekuwa akikaa chumba kimoja na Dickson alimfariji kijana huyo ambaye alionekana kuumia sana ndani ya moyo wake . Baada ya kutoka kwenye eneo la hospitali , gari lililokuwa limembeba Dickson lilianza kupiga ving ’ ora kwa nguvu na kusababisha magari mengine yapishe njia . Likazidi kuchanja mbuga kuwahi uwanja wa ndege . Baada ya dakika kadhaa, tayari gari hilo lilikuwa limeshawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo gari lilisogea mpaka kwenye mlango maalum wa kuingilia uwanjani hapo . Kwa kuwa tayari wahudumu wa uwanja huo walikuwa na taarifa juu ya mgonjwa huyo, walisaidiana kumteremsha kwenye gari, baba yake akaenda kukamilisha taratibu zote za kiusalama kisha akapelekwa moja kwa moja kwenye ndege kubwa ya Indian Airways. Akaingizwa mpaka kwenye chumba maalum na kulazwa huku yule daktari akiendelea kumhudumia .



    Jioni moja , msichana huyo anamfuma Dickson kwa macho yake akinunua changudoa na kuingia naye gesti. Mshtuko anaoupata, unasababisha apoteze umakini na kujikuta akigongwa na gari linalomjeruhi vibaya. Anakimbizwa hospitalini lakini hali inazidi kuwa mbaya . Wazazi wa msichana huyo wanaamua kumsafirisha kwenda nchini India. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Gari la kubebea wagonjwa lilikuwa likipiga ving ’ ora kwa nguvu huku taa zote zikiwa zimewashwa , likawa linachanja mbuga kwa kasi kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Muda mfupi baadaye, tayari lilikuwa limewasili kwenye uwanja huo ambapo lilisogea mpaka kwenye mlango maalum wa kuingilia uwanjani hapo . Kwa kuwa tayari wahudumu wa uwanja huo walikuwa na taarifa juu ya mgonjwa huyo, walisaidiana kumteremsha kwenye gari, baba yake akaenda kukamilisha taratibu zote za kiusalama ambapo baada ya tiketi na hati za kusafiria za wote waliokuwa wakisafiri kukaguliwa, msichana huyo alipelekwa moja kwa moja kwenye ndege kubwa ya Indian Airways. Akaingizwa mpaka kwenye chumba maalum na kulazwa huku yule daktari akiendelea kumhudumia . Muda mfupi baadaye, ndege hiyo ilianza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia, ikazidi kuongeza kasi huku injini zake kubwa zikitoa muungurumo mkubwa, baadaye ikapaa na kuiacha ardhi ya Tanzania. Ikawa inapasua mawingu kuelekea nchini India huku msichana Neema bado akiwa kwenye hali yake ya kutojitambua. * * * “ Jikaze Dickson, ukilia sana utakuwa unamkufuru Mungu wako , atakuwa sawa tu , madaktari wa India wanasifika kwa ufanisi na hakuna kinachoweza kuwashinda , tuendelee kumuombea kwa Mungu , ” rafiki yake Dickson waliyekuwa wakikaa naye chumba kimoja , alimbembeleza mwenzake baada ya kumuona akiwa kwenye hali mbaya sana kihisia. Muda wote alikuwa akilia tu, hata chakula hakutaka kula wala hakutaka kwenda darasani kujisomea, ungeweza kudhani amepokea habari za msiba wa mama au baba yake kwa jinsi alivyokuwa na huzuni. Licha ya jitihada kubwa za kumbembeleza kufanyika , bado Dickson au Zinja aliendelea kulia muda wote, macho yake ya kutisha yakazidi kuwa mekundu na kuzidi kumfanya awe na mwonekano wa ajabu . Kama ndiyo ungemuona kwa mara ya kwanza , ungeweza kudhani ni mnyama mkali wa mwituni anayekaribia kusababisha madhara makubwa kwa binadamu. * * * Ndege kubwa ya Indian Airways iliendelea kupasua mawingu kwa kasi kubwa, ikikatiza juu ya Bahari ya Hindi kuelekea nchini India ambako msichana Neema alipangwa kupelekwa kwenye Hospitali ya Apollo jijini Mumbai kwa matibabu . “ Mabibi na mabwana, ahsanteni kwa kuchagua kusafiri na ndege ya Shirika la Indian Airways , muda mfupi baadaye, tutakuwa tukitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chatrapati Shivaji jijini Mumbai , India , tafadhali abiria wote mnaombwa kufunga mikanda wakati ndege ikijiandaa kutua, ahsanteni sana , ” sauti nyororo ya mhudumu wa kike wa ndege ilisikika ikiwataarifu abiria wote kilichokuwa kinaendelea . Abiria wakaanza kufunga mikanda kama walivyoelekezwa, msichana Neema ambaye alikuwa kwenye chumba maalum akiendelea kupewa uangalizi wa karibu na daktari aliyesafiri naye kutoka jijini Dar es Salaam, naye alifungwa mikanda maalum iliyokuwa kwenye kitanda chake. Muda mfupi baadaye, ndege ilianza kuinama upande wa mbele na kuanza kushuka chini kwa kasi, ikaendelea kufanya hivyo kisha ikatingishika kidogo na kurudi kwenye usawa wake kuashiria kwamba tayari ilishatua kwenye ardhi ya Jiji la Mumbai . Ilikimbia kwa kasi na baadaye ikaanza kupunguza mwendo kabla ya kusimama kabisa mbele ya jengo kubwa lililokuwa na maandishi yaliyosomeka Chatrapati Shivaji International Airport, Mumbai . Baada ya kusimama kabisa, milango ilifunguliwa ambapo magari yenye ngazi yalisogezwa kisha abiria wakaanza kuteremka. Wahudumu wa ndege pamoja na wale wa uwanja huo , walisaidiana kuteremsha kitanda cha matairi ambacho juu yake alikuwa amelazwa msichana Neema akiwa hajitambui kabisa. Baada tu ya kuteremshwa, wahudumu hao walianza kukisukuma kitanda hicho kwa kasi kuelekea kwenye mlango maalum wa kutokea kwani tayari taarifa zake zilishakuwepo uwanjani hapo . Wazazi wake pamoja na daktari aliyekuwa akimhudumia, wao wakawa wanakimbia kuelekea kwenye mlango wa kawaida wa kuingilia sehemu ya ukaguzi . Wakawa abiria wa kwanza kukaguliwa ambapo baada ya taratibu zote za kiusalama kukamilika , walitoka mpaka nje ambapo waliwakuta madaktari wengine wawili namanesi wawili waliokuwa wamevalia sare za Hospitali ya Apollo , wakiwa kwenye harakati za kumpakiza mgonjwa kwenye ambulance iliyokuwa na maandishi makubwa ubavuni yaliyosomeka Apollo Hospital , Mumbai. Muda mfupi baadaye, ambulance hiyo iliondoka kwa kasi uwanjani hapo, huku taa zote zikiwa zimewashwa na ving ’ ora vikipiga kelele kwa nguvu, magari mengine yakawa yanaipisha kama sheria za usalama barabarani zinavyosema . Watu wengine waliosalia pale uwanjani , walipanda kwenye gari jingine ambalo nalo lilikuwa na maandishi ubavuni yaliyosomeka Apollo Hospital , Mumbai na kuondoka kwa kasi kuelekea kule ambulance ile ilikoelekea. Kila mmoja alikuwa kimya kabisa ndani ya gari, wazazi wake wakawa wamejiinamia chini huku kila mmoja akiendelea kumsalia kimyakimya binti yao huyo ili aamke kutoka kwenye usingizi wa mauti aliokuwa amelala . Dakika kadhaa baadaye, tayari walikuwa wamewasili kwenye Hospitali ya Apollo , Mumbai ambapo gari la wagonjwa alilokuwa amepakizwa Neema , lilipitiliza moja kwa moja mpaka sehemu iliyokuwa na maandishi makubwa ukutani yaliyosomeka ‘ Emergency Patients’ yakimaanisha sehemu ya kupokelea wagonjwa wa dharura. Taratibu za kumpokea msichana huyo zikaanza kufanyika ambapo muda mfupi baadaye, tayari alikuwa ameingizwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi , madaktari bingwa zaidi ya wanne wakaanza kazi ya kumfanyia upya vipimo kubaini alikuwa na tatizo gani .



    Jioni moja , msichana huyo anamfuma Dickson akinunua changudoa, mshtuko anaoupata unasababisha muda mfupi baadaye agongwe na gari . Matibabu yake hayawi mepesi , hali inayolazimu asafirishwe kwenda India. Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya ndege kubwa ya Indian Airways kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chatrapati Shivaji jijini Mumbai, India , msafara kutoka nchini Tanzania uliokuwa umemsafirisha msichana Neema kwa matibabu, ulipokelewa na timu ya madaktari na wauguzi kutoka Hospitali ya Apollo . Harakaharaka akapakizwa kwenye gari la kubebea wagonjwa na safari ya kuelekea kwenye hospitali hiyo ikaanza . Dakika kadhaa baadaye, tayari walikuwa wamewasili kwenye Hospitali ya Apollo , Mumbai , Neema akapokelewa na kulazwa kwenye kitanda cha magurudumu na kukimbizwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi . Madaktari bingwa zaidi ya wanne wakaanza kazi ya kumfanyia upya vipimo kubaini alikuwa na tatizo gani . Akafanyiwa vipimo vyote kuanzia X - Ray, MRI (Magnetic Resonance Imaging), CT Scan (Computerized Tomography Scan) na vingine vingi ambavyo madaktari waliona vinafaa kutoa majibu ya uhakika ya kilichokuwa kinamsumbua . Kutokana na ubora wa vifaa vyote vya kupimia wagonjwa vilivyokuwepo hospitalini hapo, muda mfupi tu baadaye, tayari majibu yote yalikuwa yametoka . Jopo la madaktari waliopewa jukumu la kumtibu likakutana kuyajadili majibu ya vipimo vyote alivyochukuliwa . “ She got severe injuries in her spinal cord , vertebrae and the skull. ” (Amepata majeraha makubwa kwenye uti wake wa mgongo, pingili na fuvu la kichwa) “ What? Ooh my God. ” (Niniii ? Mungu wangu ) mmoja kati ya madaktari waliokuwa wakijadiliana kuhusu matokeo ya msichana huyo, alijikuta akishindwa kuzizuia hisia zake. Alielewa vizuri athari za madhara aliyokuwa ameyapata. Daktari wa awali aliyekuwa akiwasomea wenzake matokeo hayo , Siddharth Shivam , aliendelea kutoa ufafanuzi wa kitaalamu kwa wenzake. “ The bundle of nerves that extend downward from the spinal cord which is called Cauda Equina are injured too ,” (Neva zake za fahamu zinazopita kwenye uti wa mgongo kutokea kichwani kuelekea kiunoni ziitwazo Cauda Equina nazo zimejeruhiwa pia ) alisema daktari huyo, kila mmoja akashusha pumzi ndefu kwani kazi iliyokuwa mbele yao haikuwa nyepesi. Kwa maelezo hayo , jambo ambalo lilikuwa ni lazima limtokee msichana huyo ilikuwa ni kuendelea kupoteza fahamu kwa kipindi kirefu, mwili kupooza na kupoteza uwezo wa kuinuka kitandani , kuhisi , kuona , kukumbuka wala kuzungumza chochote. Kila mmoja alionekana kumsikitikia msichana huyo kwani alikuwa bado mdogo kustahili mateso makubwa kiasi hicho. “ Administer her with analgesics , Acetaminophen 3cc syringe thrice a day and connect her to effective Oxygen pumping machine while we prepare ourselves for surgery as soon as possible . ” (Mchomeni sindano ya kupunguza maumivu , Acetaminophen sentimita tatu za ujazo , mara tatu kwa siku na muunganisheni na mashine ya Oxygen yenye nguvu wakati tukijiandaa kumfanyia upasuaji haraka iwezekanavyo ) alisema Dokta Shivam, harakaharaka manesi wakatii walichoambiwa huku wakizingatia maelekezo aliyowapa kwamba msichana huyo hakutakiwa kutingishwa au kugeuzwa kwa namna yoyote ili kuzuia uti wake wa mgongo usizidi kupata madhara zaidi . Neema ambaye hakuwa na fahamu hata kidogo, alichomwa sindano ya kuzuia maumivu kisha akabadilishiwa mashine ya Oxygen na kuwekewa nyingine yenye nguvu zaidi. Jopo la madaktari waliopaswa kumshughulikia mgonjwa huyo, wakaingia kwenye chumba maalum kuelekezana nini cha kufanya kwani hali ya mgonjwa wao ilikuwa ikihitaji umakini wa hali ya juu, vinginevyo maisha ya msichana huyo yalikuwa hatarini. Baada ya kuelekezana kwa zaidi ya saa tatu kwa nadharia, huku wakitumia vipimo vya msichana huyo kuoneshana nini cha kufanya na kugawana majukumu ya kila mmoja pindi watakapoingia kwenye chumba cha upasuaji , hatimaye madaktari hao wakiongozwa na daktari bingwa wa mifumo ya fahamu (neurosurgeon ), Dk . Shivam walitoka na kuelekea kwenye vyumba vya maandalizi . Manesi nao wakamtoa Neema kwa tahadhari kubwa kutoka kwenye wodi ya wagonjwa mahututi na kupelekwa kwenye wodi ya kisasa ya upasuaji. Muda mfupi baadaye, madaktari wote walikuwa tayari wameshaingia kwenye wodi hiyo , manesi nao wakawa wanapigana vikumbo huku na kule kuhakikisha vifaa vyote muhimu vilivyokuwa vinahitajika , vipo sehemu yake. Kwa muda wote huo, wazazi wa Neema walikuwa nje wakiendelea kumuomba Mungu wao atende miujiza . Licha ya uwezo mkubwa wa kifedha waliokuwa nao, Neema ndiye aliyekuwa mtoto wao wa kipekee na hakuna aliyekuwa tayari kuona anapoteza maisha wakati uwezo wa kumsaidia walikuwa nao. “ Wakishindwa hapa India ni bora hata tusafiri naye kuelekea Uingereza , lazima mwanangu apone , ” alisema baba mzazi wa msichana huyo huku akimbembeleza mkewe ambaye muda wote alikuwa akisali huku akilia kwa uchungu. Muda mfupi baadaye, madaktari waliianza kazi ngumu na ya hatari ya kumfanyia upasuaji msichana huyo, kuanzia kwenye fuvu la kichwa mpaka kwenye uti wa mgongo ambao vipimo vilionesha kwamba umeathirika zaidi kuliko sehemu nyingine . * * * Wakati hayo yakiendelea nchini India , Tanzania hali ilikuwa mbaya sana kwa Dickson. Hakutaka kula wala kuingia darasani , bado moyo wake ulikuwa na majonzi makubwa kuhusu kilichomtokea Neema, msichana pekee aliyetokea kumpenda na kumuonesha mapenzi ya dhati licha ya sura na mwonekano wake wa kutisha uliosababisha wengi wamuogope . Juhudi za wanachuo wenzake pamoja na uongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alichokuwa akisomea kujitahidi kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida, zilionekana kugonga mwamba , mwisho kila mmoja akaamua kumuachia mwenyewe.



    akinunua changudoa, mshtuko anaoupata unasababisha muda mfupi baadaye agongwe na gari . Matibabu yake hayawi mepesi , hali inayolazimu asafirishwe kwenda India ambako jopo la madaktari linaingia kazini kuokoa maisha ya msichana huyo. Upande wa pili , Dickson anaonesha kuchanganywa mno na kilichotokea , kiasi cha kupoteza hamu ya kufanya jambo lolote. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Siku zilizidi kusonga mbele huku Dickson au Zinja akiendelea kuteseka ndani ya moyo wake kutokana na hali aliyomuona nayo mara ya mwisho Neema . Hata hivyo , kama wahenga wasemavyo kwamba hakuna daktari mzuri kama muda , kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele ndivyo majeraha aliyokuwa nayo Dickson ndani ya moyo wake yalivyozidi kupungua. Akaanza kuona kama kila kilichotokea kilikuwa ni kitu cha kawaida na kilitokea kwa sababu maalum. Ule uchangamfu wake ukaanza kurudi taratibu , akaanza upya kuhudhuria darasani na kushirikiana na wenzake kwenye mambo mbalimbali kama ilivyokuwa kawaida yake kabla Neema hajapatwa na ajali mbaya ya kugongwa na gari. Mara chache alizokuwa anamkumbuka Neema , alikuwa akijisikia vibaya ingawa hali haikuwa mbaya kama ilivyokuwa mara ya kwanza. Kwa kipindi kirefu, alikuwa akiendelea kupiga namba ya simu ya baba yake Neema aliyopewa siku walipokutana Hospitali ya Muhimbili kabla Neema hajasafirishwa kwenda India lakini mara zote , namba hiyo haikuwa ikipatikana hewani . * * * Jopo la madaktari kadhaa , wakiongozwa na daktari bingwa wa mifumo ya fahamu (neurosurgeon ), Dk . Siddharth Shivam waliendelea na kazi ngumu ya kumfanyia upasuaji msichana mdogo , Neema , ndani ya Hospitali ya Apollo , Mumbai nchini India . Kazi haikuwa nyepesi kwani maeneo aliyokuwa ameathirika , hasa kwenye uti wa mgongo, kulikuwa na mishipa mingi ya fahamu ambayo ilihitaji umakini wa hali ya juu katika kuishughulikia kwani hitilafu yoyote ambayo ingetokea wakati wa upasuaji huo ingeweza kuhatarisha maisha ya msichana huyo mdogo , jambo ambalo hakuna aliyekuwa tayari kuona linatokea. Baada ya takribani saa nane , hatimaye msichana huyo alitolewa kwenye chumba hicho cha upasuaji , akiwa amepandikizwa vyuma maalum kwenye uti wake wa mgongo kwa ajili ya kushikilia pingili za mifupa mpaka zitakapojiunga na kuwa kama awali . Kutokana na aina ya upasuaji wenyewe , manesi walipewa angalizo la kuhakikisha kuwa msichana huyo hatingishiki hata kidogo , akafungwa kwa mikanda maalum kwenye kitanda hicho na kusukumwa taratibu kuelekea kwenye wodi ya wagonjwa mahututi ambako alilazwa . Siku zilizidi kusonga mbele huku Neema akiwa bado hajarejewa na fahamu zake. Hakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote, kila kitu alisaidiwa na mashine maalum alizokuwa ameunganishwa nazo pale kitandani kwake, kuanzia kula , kupumua mpaka kutoa haja ndogo na kubwa. Alikuwa kwenye usingizi mzito wa kifo , akiwa haelewi chochote kilichokuwa kikiendelea katika ulimwengu wa kawaida. Wazazi wake kamwe hawakumkatia tamaa , kila siku wakawa wanamuombea kwa Mungu huku wakihakikisha anapatiwa kila kitu kilichokuwa kinahitajika kwenye matibabu yake. Baada ya kulala kitandani akiwa hana fahamu kwa zaidi ya miezi miwili, huku kila siku madaktari wakiendelea kumfanyia uchunguzi wa karibu kuonesha maendeleo ya afya yake, hatimaye jioni moja msichana huyo alifumbua macho, jambo lililoamsha shangwe kubwa kwa wazazi wake . “ Siamini macho yangu , siamini mume wangu, ” alisema mama mzazi wa msichana huyo huku akimkumbatia mumewe kwa nguvu , akitokwa na machozi mengi. Kuzinduka kwa Neema kulikuwa ni zaidi ya miujiza . Madaktari ambao nao walikuwa wakihangaika usiku na mchana bila kupata hata muda wa kupumzika , walipongezana sana kwa kitendo cha msichana huyo kurejewa na fahamu zake. Wakawa wanaendelea kumfanyia vipimo mbalimbali lakini baadaye wakagundua kitu ambacho hakikuwafurahisha sana . Licha ya msichana huyo kuzinduka lakini vipimo vilionesha kwamba itamchukua muda mrefu kurudi kwenye hali yake ya kawaida kwani uti wake wa mgongo ulikuwa ukipona kwa kasi ndogo sana . Jambo hilo lilimaanisha kwamba angechelewa sana kurejewa na fahamu zake, kuwa na uwezo wa kuinuka mwenyewe kitandani na uwezo wa kuzungumza kama ilivyokuwa mwanzo kabla hajapata ajali hiyo . Baada ya majadiliano ya muda mrefu na wazazi wa msichana huyo, walikubaliana kwamba kwa sababu itamchukua muda mrefu msichana huyo kupona, ni bora warudi naye nyumbani ambako daktari maalum atakuwa akifuatilia maendeleo yake na kuwasiliana na madaktari hao moja kwa moja nchini India . Lengo la kufanya hivyo ilikuwa ni kupunguza gharama na kumuepusha msichana huyo asije akapata magonjwa mengine kwa kuendelea kukaa zaidi hospitalini hapo. Wazazi wake walikubaliana na ushauri huo wa kitaalamu na kwa sababu tayari walikuwa na daktari wao waliyesafiri naye kutoka nchini Tanzania ambaye aliondoka mara tu baada ya upasuaji wa msichana huyo kukamilika , waliwasiliana naye wakiwa hukohuko nchini India . Daktari huyo akapewa maelekezo na wenzake waliokuwa nchini India juu ya namna ya kumshughulikia mgonjwa huyo. Baada ya makubaliano kufikiwa, taratibu za kurejea nchini Tanzania zilianza kufanywa, huku hospitali hiyo ikigharamia mambo mengi , ikiwemo usafiri wa kumpeleka mpaka uwanja wa ndege na gharama za kitabibu kwa muda wote wa safari mpaka msichana huyo atakapowasili nchini Tanzania . Safari ilianza kutoka hospitalini hapo ambapo kutokana na wazazi wa msichana huyo kukaa muda mrefu wakimuuguza mtoto wao, walishazoeana na madaktari na manesi , watu wengi walishikwa na huzuni kutokana na kuondoka kwao , wakawasindikiza na kuwatakia kila la heri katika maendeleo ya mtoto wao. Neema akapakizwa kwenye ‘ ambulance ’ na kupelekwa mpaka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chhatrapati Shivaji jijini Mumbai. Kwa kuwa tayari tiketi za ndege na taratibu zote za usafiri zilishakamilika, hawakukaa sana uwanjani hapo , Neema akapitishwa kwenye lango maalum akiwa kwenye kitanda cha magurudumu huku akiwa amefungwa mikanda maalum ya kumzuia asitingishike . Akapelekwa moja kwa moja mpaka kwenye ndege ambako alipelekwa kwenye chumba maalum na kuwekwa chini ya uangalizi maalum. Abiria wengine nao wakapanda , wakiwemo wazazi wake na muda mfupi baadaye, ndege kubwa ya Shirika la Indian Airways ikapaa kuelekea nchini Tanzania .



    Upasuaji mkubwa unafanyika lakini bado hali ya msichana huyo inaonesha kulegalega . Baadaye madaktari wanashauriana na wazazi wake kumrudisha nyumbani Tanzania kuendelea na matibabu akiwa nyumbani . Je , nini kitafuatia? SONGA NAYO … Baada ya taratibu zote kukamilika , Neema alipelekwa moja kwa moja mpaka kwenye ndege ambako aliingizwa kwenye chumba maalum na kuwekwa chini ya uangalizi maalum wa daktari. Abiria wengine nao wakapanda, wakiwemo wazazi wake na muda mfupi baadaye, ndege kubwa ya Shirika la Indian Airways ikapaa kuelekea nchini Tanzania. “ Sitaki mtu yeyote ajue kinachoendelea kuhusu mtoto wetu, si unajua tena mambo ya Kiswahili , wanaweza kummalizia bure !” mama mzazi wa Neema alimwambia mumewe wakiwa angani , wakati ndege waliyopanda ikiendelea kupasua mawingu kuelekea nchini Tanzania. Kwa jinsi alivyokuwa anampenda mkewe , alikubaliana naye na kwa pamoja wakafikia muafaka kwamba watakapofika nchini Tanzania, kila kitu kitafanyika kwa usiri mkubwa. Baada ya kusafiri saa nyingi angani , hatimaye waliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo Neema alipokelewa na daktari wake ambaye alikuja na gari maalum la kubebea wagonjwa uwanjani hapo akiwa sambamba na dereva . Msichana huyo akashushwa kwenye ndege kwa tahadhari ya hali ya juu, akiwa amefungwa kwa mikanda maalum kwenye kitanda alichokuwa amelala juu yake, akatolewa taratibu mpaka nje na kupakizwa kwenye gari la kubebea wagonjwa lililokuwa limeandaliwa kwa ajili yake. Akasafirishwa kwa umakini mkubwa mpaka Masaki , yalipokuwa makazi ya familia yake. Kwa kuwa tayari baba yake alishafanya mawasiliano na wafanyakazi wake waliokuwa nchini Tanzania tangu akiwa India , kila kitu kilikuwa kimeshaandaliwa . Akaingizwa mpaka kwenye chumba maalum kilichokuwa kimetengenezwa maalum kwa ajili ya kumhudumia Neema , kikiwa na vifaa vyote muhimu kama chumba cha wagonjwa mahututi hospitalini . Kwa jinsi mpango wa kumsafirisha ulivyofanywa kwa siri kubwa, ni watu wachache sana waliokuwa na taarifa kwamba msichana huyo tayari amesharejea nyumbani kwao . Kila kitu kiliendelea kufanyika kwa usiri mkubwa huku akiendelea kupatiwa matibabu na daktari wake ndani ya chumba hicho. *** Siku zilizidi kusonga mbele huku Dickson au ZInja akiendelea na masomo yake. Zile hisia chungu kuhusu Neema zilizidi kupungua kadiri siku zilivyokuwa zinayoyoma na sasa alikuwa na uwezo wa kusoma vizuri kama zamani . Mara chache alizokuwa akimkumbuka Neema , alikuwa akijaribu kupiga namba za simu za baba yake lakini hazikuwa zikipatikana , akawa na imani kubwa kwamba bado wapo kwenye matibabu nchini India . Siku moja jioni , alijaribu tena kupiga namba ya simu ya baba yake Neema ambapo katika hali ambayo hakuitegemea, simu hiyo ilianza kuita . Mapigo ya moyo wake yakawa yanamuenda mbio huku akiwa na shauku kubwa ya kusikia taarifa juu ya maendeleo ya Neema. “ Haloo !” sauti nzito ya mwanaume ilisikika baada ya simu kupokelewa. Huku akitetemeka, Dickson alimwamkia mwanaume huyo ambaye bila hata kuuliza alijua ni baba yake Neema . Jambo la kwanza baada ya salamu , ilikuwa ni kumuuliza kuhusu maendeleo ya Neema . Hata hivyo , tofauti na alivyotegemea , mzazi huyo wa Neema alimjibu kwa kifupi kwamba yeye hajui chochote kwa sababu amerejea Tanzania na Neema bado anaendelea kutibiwa nchini India . Akamwambia kwa muda huo alikuwa na kazi nyingi hivyo aulizwe siku nyingine . Kwa kuwa tayari Dickson alishakuwa na akili za kiutu uzima , alielewa tafsiri ya majibu ya mzee huyo kwamba hakuwa akipenda kuulizwa habari kuhusu mwanaye . Alijisikia vibaya sana ndani ya moyo wake lakini hakuwa na cha kufanya , akaamua kupiga moyo konde na kuendelea na masomo . Siku zilizidi kuyoyoma , Dickson au Zinja kama wanachuo wenzake walivyokuwa wamezoea kumuita, akawa anaendelea na masomo na hatimaye , alihitimu Shahada ya Kwanza ya Sheria . Kwa kuwa ndoto zake za siku nyingi zilikuwa ni kuingia jeshini , aliamua kutimiza ndoto zake ambapo alirudi nyumbani kwao wakati akiendelea kufanya maandalizi ya kujiunga na mafunzo ya jeshi la polisi . Miezi michache baadaye, Dickson alipata nafasi ya kujiunga na Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi (CCP ). Baada ya maandalizi yote kukamilika , alisafiri mpaka mkoani Kilimanjaro kilipokuwa chuo hicho na kwenda kuripoti . Akaungana na wanachuo wengine wengi kuyaanza mafunzo ya kijeshi. Awali alipata shida sana kwani tayari alishazoea kukutana kimwili na machangudoa mara kwa mara lakini sheria za jeshini zilikuwa kali mno kiasi kwamba hakupata hata upenyo wa kufanya mchezo huo aliouzoea. Njia pekee aliyokuwa anaitumia kukidhi haja zake, ikawa ni kujichua kama alivyokuwa akifanya kipindi alichokuwa anasoma sekondari . Hata hivyo , hata nafasi ya kufanya mchezo huo pia ilikuwa ikipatikana kwa mbinde sana kwani muda mwingi alikuwa akibanwa na ratiba ya jeshini ambapo kila siku walikuwa wakiamshwa alfajiri na mapema na kuanza kucheza kwata kwa saa nyingi mfululizo. Baada ya hapo, walikuwa wakipata kifungua kinywa kisha kuendelea na mazoezi mengine ikiwemo kupanda Mlima Kilimanjaro huku mgongoni kila mtu akiwa na begi lenye mawe mazito, mazoezi ambayo ama kwa hakika yalikuwa yakimchosha sana. Muda pekee waliokuwa wakipumzika ilikuwa ni kuanzia saa nne za usiku ambapo siku nyingine alikuwa akishindwa kufanya mchezo huo kutokana na jinsi alivyokuwa anachoka kwa msoto wa kutwa nzima jeshini . Siku zilizidi kusonga mbele , hatimaye mwezi wa kwanza ukaisha, Dickson akiwa bado anaendelea na mafunzo ya kijeshi. Hata hivyo , hamu ya kukutana kimwili na mwanamke iliendelea kumsumbua , ikafika kipindi akawa anafanya makosa ya kizembe kwa sababu ya akili yake kufikiria jambo hilo kupitakiasi . “ Lazima leo nitoroke niende uraiani kutafuta mwanamke wa kuipooza nafsi yangu , siwezi kuishi maisha haya , nimechoka kuvumilia , ” aliwaza Dickson jioni moja wakiwa kwenye mazoezi ya kulenga shabaha .





    Upasuaji mkubwa unafanyika lakini bado hali ya msichana huyo inaonesha kulegalega . Baadaye madaktari wanashauriana na wazazi wake kumrudisha nyumbani Tanzania kuendelea na matibabu akiwa nyumbani.

    Upande wa pili, hatimaye Dickson au Zinja anafanikiwa kuhitimu chuo na baada ya hapo anaenda kujiunga na Chuo cha Polisi mjini Moshi, Kilimanjaro lakini usiku mmoja, uzalendo unamshinda na kuamua kutoroka chuoni kwenda mitaani kutafuta machangudoa. Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO …

    Muda mfupi baadaye , Dickson alikuwa kama alivyotoka kwenye tumbo la mama yake , ndani ya chumba cha gesti akiwa na changudoa , akamsogelea mwanamke huyo ambaye naye alimalizia kutoa nguo yake ya mwisho , wakakumbatiana lakini kabla hawajafanya chochote, wote wawili walishtuka baada ya kusikia mlango wa chumba walichokuwemo ukigongwa kwa nguvu.

    “ Nani!”

    “ Fungua, ” sauti ya zaidi ya wanaume sita ilisikika kutokea nje ya chumba cha gesti ambacho Dickson au Zinja alikuwa ndani na mwanamke huyo anayefanya biashara haramu ya kujiuza , aliyemnunua muda mfupi uliopita kwenye mtaa maarufu kwa biashara hiyo , Majengo, Moshi mkoani Kilimanjaro.

    “ Mungu wangu , ” alisema Dickson baada ya kufunua pazia kidogo na kuchungulia nje ambapo alishuhudia kundi la wanaume , wengine wakiwa na silaha za jadi, wakiwa wameuzingira mlango wa chumba alichokuwa amejifungia na mwanamke huyo .“ Kwani kuna nini?” mwanamke huyo aliuliza huku naye akisogelea dirishani hapo, wote wakiwa kama walivyotoka kwenye matumbo ya mama zao.

    “ Yeleuwiiii, mume wangu! Mume wangu ametufumania, ” alisema mwanamke huyo kwa lafudhi ya wenyeji wa mkoa huo .“ Mume wako ? Kwani wewe umeolewa ?”

    “ Ndiyo nimeolewa lakini mume wangu huwa anasafiri halafu haniachii pesa za matumizi ndiyo maana huwa nakuja kujiuza , ” alisema mwanamke huyo huku akionesha dhahiri hofu kubwa aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake .

    Kwa kasi ya ajabu, Dickson alikimbilia nguo zake, akazivaa huku mlango ukiendelea kugongwa kwa nguvu .

    “ Tunahesabu mpaka tatu , usipofungua tunavunja mlango, ” sauti ya mwanaume mmoja aliyeonekana kuwa na mamlaka kuliko wenzake ilisikika, wakati Dickson akimalizia kuvaa nguo zake.

    Kufumba na kufumbua, mlango wa chumba hicho cha gesti ulivunjwa, wanaume wenye hasira wakavamia huku kila mmoja akipiga kelele za ‘mgoni !’ Mgoni ! Mwizi wa wake za watu leo amepatikana !’

    “ Jamani mimi sikujua ka …” Dickson alijaribu kujitetea lakini ilikuwa sawa na kazi bure, ngumi nzito ilitua kwenye uso wake, sauti yake ikamezwa na watu hao ambao tayari walishamtia mikononi na kuanza kumshushia kipigo kwa kumgombania kama mpira wa kona .

    Yule mwanamke alipata upenyo na kutoroka , akamuacha Dickson peke yake akiendelea kuchezea kichapo kutoka kwa wanaume hao walioonesha kumpania kwelikweli . Japokuwa alikuwa ameiva kwa mafunzo ya kijeshi , hakutaka kuyatumia kumjeruhi yeyote kwani alikuwa anajua fika kwamba ni kosa kisheria .

    Hata hivyo , alipoona hali inaanza kuwa mbaya kwake , hakuwa na namna zaidi ya kujitetea. Kwa kasi ya ajabu akafungua mkanda wa kijeshi aliokuwa ameuvaa kiunoni na kuanza kuwatawanya watu hao ambao walishaonesha nia ya kumdhuru kutokana na jinsi walivyokuwa wanampiga kwa hasira kama mwizi.

    “ Ana mkanda wa jeshi, jamani klumbe ni mwanajeshi…” alisema mwanaume mmoja baada ya kukoswakoswa na mkanda huo lakini alikuwa ameshachelewa kwani Dickson alishapandisha hasira zake , ndani ya sekunde chache tu , tayari alikuwa amefanikiwa kuwaangusha watu wote waliokuwa ndani ya chumba hicho, huku kila mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya.

    Wakati anataka kukimbia, mmoja kati ya wale wanaume aliyefanikiwa kutoka nje ya chumba cha gesti , alimnyooshea upinde uliokuwa na mshale wenye sumu , akamtaka kusalimu amri vinginevyo atamjeruhi vibaya.

    Kwa kasi ya ajabu, Dickson aliurusha ule mkanda wake na kumpiga nao mwanaume huyo kichwani, akadondoka chini na kupiga kelele zilizowakusanya watu wengi. Dickson hakuwa na ujanja zaidi ya kuanza kutimua mbio, akakimbia na mita chache mbele, alipotelea kwenye mashamba ya migomba na kuendelea kutimua mbio kuelekea kambini.

    Dakika kadhaa baadaye, tayari alishawasili kambini, akapitia kwenye njia ileile aliyoitumia kutorokea na kutambaa mpaka ndani ya eneo la jeshi, huku mwili mzima akiwa amechafuka vibaya kutokana na kuanguka mara kadhaa wakati akikimbia kwenye mashamba ya migomba.

    Ebwana vipi mbona umechafuka kiasi hicho?” askari mmoja ambaye naye alikuwa mafunzoni kama Dickson , alimuuliza swali ambalo hakulitegemea baada ya kumkuta amejibanza kwenye korido ya mabweni yao , akitafuta njia ya kuingia bila kugundulika na wakufunzi wao .

    “ Nilikuwa shambani, ” Dickson alidanganya huku akijitahidi mwenzake huyo asimuone usoni. Hatimaye akafanikiwa kuingia mpaka ndani ambapo alienda kubadilisha nguo, akaenda kuoga kisha akaenda kuziloweka nguo hizo bafuni na kuzifua usiku huohuo ili kupoteza ushahidi.

    Kesho yake asubuhi , wananchi kadhaa waliwasili kwenye kambi hiyo ya jeshi , huku wengi wakionesha kuwa na majeraha makubwa miilini mwao . Wakaomba kukutana na mkuu wa chuo hicho aliyekuwa akisifika kwa ukali kiasi cha wanachuo kumtungia jina la Pilipili Kichaa.

    Baada ya kuwasilikiza malalamiko yao pamoja na kupokea kidhibiti kilichoachwa eneo la tukio na mhusika, cha mkanda wa jeshi uliokuwa umetapakaa damu , mkuu huyo wa chuo aliomba kwanza apewe muda wa kutafakari.

    Akakaa ndani ya ofisi yake na kutulia kwa dakika kadhaa. Kawaida yake, alikuwa akikasirika sana anacheka mwenyewe kabla ya kuanza kuchukua hatua kali.

    Alipoinuka, aliamuru wanajeshi wote waliokuwa mafunzoni ambao asubuhi hiyo walikuwa wakiendelea na mazoezi, kuacha kila kitu walichokuwa wanakifanya na kuelekea ‘Assembly Square’ , eneo maarufu lililokuwa likitumika kwa mikusanyiko ya kusikiliza matangazo . Kutokana na jinsi alivyokuwa amekunja sura, kila mtu akajua kazi ipo siku hiyo.

    Je , nini kitafuatia



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog