Sehemu Ya Pili
(2)
Upande wa pili, hatimaye Dickson au Zinja anafanikiwa kuhitimu chuo na baada ya hapo anaenda kujiunga na Chuo cha Polisi mjini Moshi, Kilimanjaro lakini usiku mmoja, uzalendo unamshinda na kuamua kutoroka chuoni kwenda mitaani kutafuta machangudoa ambapo anasababisha mtafaruku mkubwa .
Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO…
Baada ya kupata malalamiko hayo , mkuu wa chuo cha polisi alipandwa na hasira kali, akainuka na kuamuru askari wote waliokuwa mafunzoni ambao asubuhi hiyo walikuwa wakiendelea na mazoezi, kuacha kila kitu walichokuwa wanakifanya na kuelekea ‘Assembly Square’ , eneo maarufu lililokuwa likitumika kwa mikusanyiko na kusikiliza matangazo . Kutokana na jinsi alivyokuwa amekunja sura, kila mtu akajua kazi ipo siku hiyo.
Mkuu huyo wa chuo cha mafunzo ya polisi alianza kwa kuwataka watu wote kukaa kwenye mistari kwa ajili ya gwaride la utambuzi . Bila kueleza chochote , alitoa ishara ambapo wanaume zaidi ya wanne , wote wakiwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao, walitoka kwenye ofisi kuu na kuelekea mpaka pale ‘ Assembly ground’ .
Akaanza kuwapitisha kwenye mistari waliyokuwa wamejipanga askari hao waliopo mafunzoni huku akiwahimiza kumtazama kila mmoja kwa umakini ili kumbaini aliyefanya tukio lililochafua mno taswira ya chuo hicho .
Dickson aliyekuwa miongoni mwa askari waliokuwa wamepanga mstari kwa ajili ya gwaride hilo la utambuzi , alikuwa akitetemeka kwa hofu kubwa kwani ni yeye peke yake ndiye aliyekuwa akijua kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
“ Eeh Mungu wangu, onesha miujiza yako , ” Dickson alisema huku akiendelea kutetemeka . Japokuwa hakuwa mhudhuriaji mzuri wa nyumba za ibada, siku hiyo alitamani Mungu amfanyie muujiza wowote kwani kwa jinsi alivyokuwa akimfahamu mkuu wao wa chuo , alijua moto utawaka.
Kila alipokumbuka kwamba katika purukushani hiyo kofia yake ilianguka na kusababisha watu wote waione sura yake halisi , alizidi kuishiwa nguvu, akajua lazima atanaswa .Ukaguzi mkali uliendelea huku askari wengi wakongwe wakirandaranda huku na kule kuhakikisha hakuna anayetoroka eneo hilo la ukaguzi .
“ Huyu hapa, ni yeye kabisa. ”
“ Ndiyo mwenyewe , sura yake ni hiihii , anafanana na binadamu wa kale, ” wanaume wawili kati ya wale wanne walisema kwa sauti ya juu na kuungwa mkono na wenzao , askari wengi wakamzunguka Dickson huku mkuu wa chuo hicho, akimtazama akiwa ni kama haamini.
Siku zote alikuwa akimchukulia Dickson kama kijana mpole , asiyependa kujichanganya na wenzake na mwenye staha kubwa lakini kumbe haikuwa hivyo , akabaki anamtazama huku jazba zake zikionekana waziwazi .
“ Siyo mimi, wananisingizi …” alisema Dickson lakini kabla hajamalizia kauli yake hiyo , alipigwa mtama na mmoja wa askari aliyekuwa na mwili mkubwa , akadondoka chini kama mzigo, puuuh!
“ Mkanda wako wa kijeshi uko wapi ?” alisema mkuu wa chuo hicho huku akimkagua vizuri Dickson.
“ Nimeibiwa, ” alisema Dickson , kauli iliyozidi kumpandisha hasira mkuu huyo wa chuo . Siku zote hakuna kitu alichokuwa anakichukia kama mtu kushindwa kukiri kosa. Hata hivyo , Dickson hakuwa mwepesi kukiri kosa kwa sababu kwa askari kukubali kirahisi namna hiyo , ulikuwa ni udhaifu mkubwa kutokana na mafunzo waliyokuwa wanapewa .
“ Unaujua huu mkanda?” kiongozi huyo alisema huku akimuonesha Dickson mkanda ulioletwa na wananchi hao kama ushahidi , ukiwa na damu zilizokaukia. Dickson aliutazama ule mkanda kisha akainama chini .
“ Mpelekeni Guantanamo, ” alisema mkuu huyo wa chuo hicho akimaanisha Dickson apelekwe kwenye gereza maalum la jeshi lililokuwa likisifika kwa kutoa adhabu kali na mateso ya hali ya juu kwa wote wanaobainika kuvunja sheria za chuo hicho.
Kitendo hicho kilionesha kumkasirisha mno mkuu huyo wa chuo , mikunjo ikazidi kuongezeka kwenye uso wake . Akawapeleka wale walalamikaji mpaka ofisini kisha akarudi na kuanza kuzungumza na wanachuo wa chuo hicho cha kijeshi .
Akawaeleza jinsi tukio zima lilivyokuwa na akaahidi kumchukulia hatua kali Dickson kwa alichokifanya kwani mbali na kuwasababishia maumivu makubwa raia wasio na hatia, pia alikuwa amechafua sifa ya chuo hicho mbele ya jamii kwa kuonesha kwamba askari wanaofundishwa hapo, hawana maadili ndiyo maana wanafikia hatua ya kwenda kufanya mapenzi na wake za watu mitaani.
Baada ya kumaliza kuzungumza kwa ukali , mkuu huyo wa chuo aliondoka akiwa na askari wengine kadhaa na kuelekea mpaka kwenye gereza la jeshi lililopewa jina la Guantanamo kwa ajili ya kwenda kumshughulikia Dickson .
Huku nyuma , askari wengine waliruhusiwa kuendelea na majukumu yao ambapo kila mmoja alianza kucheka kutokana na tukio lililofanywa na Dickson . Wengi walimuonea huruma kwani walijua mateso atakayoenda kukutana nayo Guantanamo, hayaelezeki .
Baada ya kufikishwa Guantanamo , Dickson alianza kuteswa vikali kwa kuchapwa mijeledi akilazimishwa aeleze ukweli wa kilichotokea. Haikuwa kazi nyepesi lakini kwa kuwa kulikuwa na watalaamu waliobobea katika kazi ya kuwatesa binadamu wenzao , hatimaye Dickson alikiri baada ya kuwa ameteswa sana .
Baada ya kukiri, alitolewa Guantanamo mwili wote ukiwa umechakaa kwa mateso, akapelekwa mpaka ofisi kuu, damu nyingi zikimvuja kila sehemu ambapo alilazimishwa kukiri mbele ya waathirika juu ya makosa aliyoyafanya .
Huku akiugulia maumivu makali , Dickson aliwaomba radhi wote aliowajeruhi na kueleza kwamba wakati anakutana na mwanamke huyo , hakujua kama ni mke wa mtu bali alidhani ni changudoa. Watu hao walikubali kumsamehe lakini wakataka kila mmoja alipwe fedha za matibabu ambapo Dickson hakuwa na ujanja zaidi ya kukubali.
“ Chuo kitakusaidia kuwalipa lakini itabidi hizo fedha zikatwe kwenye ada yako , ” alisema mkuu wa mafunzo ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya ofisi hiyo wakisikiliza mashtaka.Baada ya makubalianao hayo , watu wote wanne walilipwa fedha za matibabu kisha wakaondoka wakiwa wameridhika, kazi ikabakia kwa Dickson ambapo alikuwa na kesi ya pili ya kujibu .
“ Kwa nini ulitoroka chuoni na kwenda kufanya ufuska uraiani?” aliuliza mkuu wa chuo , Dickson akawa hana majibu zaidi ya kugugumia kwa maumivu makali, akaamrisha arudishwe tena Guantanamo na kufungiwa kwa siku saba kisha baada ya hapo, atalazimika kufanya kazi ngumu atakazopangiwa na viongozi wake na atakuwa chini ya uangalizi maalum kwa kipindi chote atakachokuwepo chuoni hapo.
Japokuwa Dickson alikuwa na roho ngumu, alishindwa kuyazuia machozi yasiulowanishe uso wake wakati akikokotwa na askari kurudishwa Guantanamo huku viungo vyote vya mwili wake vikimuuma sana kutokana na mateso makali . Akaingizwa kwenye gereza hilo la jeshi na kufungiwa, mateso yakaendelea
Upande wa pili, hatimaye Dickson au Zinja anafanikiwa kuhitimu chuo na baada ya hapo anaenda kujiunga na Chuo cha Polisi mjini Moshi, Kilimanjaro lakini usiku mmoja, uzalendo unamshinda na kuamua kutoroka chuoni kwenda mitaani kutafuta machangudoa, jambo linalomgharimu sana kwani anapewa adhabu kali sana inayomfanya ajute.
Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO…
Siku saba zilikatika Dickson au Zinja kama wengi walivyokuwa wanamuita kutokana na sura yake kufanana na binadamu wa kale (Zinjathropus ) , akiendelea kuteseka ndani ya gereza la chuo cha polisi almaarufu Guantanamo kutokana na makosa makubwa aliyokuwa ameyafanya ya kutoroka chuoni na kwenda kununua changudoa mitaani na kujikuta akisababisha vurugu kubwa baada ya kufumaniwa .
Maumivu aliyokuwa anayasikia mwili mzima yalimfanya ajiapize kuwa kamwe hatarudia tena kufanya upuuzi kama alioufanya kwani ilikuwa ni lazima kila asubuhi aje kuamshwa kwa mijeledi kisha kufanyishwa kazi ngumu ndani ya gereza hilo, hali iliyomfanya aijutie sana nafsi yake.
“ We kenge amka , vaa nguo zako adhabu yako ya kukaa humu imeisha , ” askari mmoja aliyekuwa amevalia magwanda , alimwambia Dickson huku akimtupia magwanda waliyokuwa wanavaa chuoni hapo , Dickson akajikongoja na kusimama, akavaa nguo hizo na kutoka mpaka nje.
Kutokana na kukaa kwenye giza kwa siku zote hizo, macho yake yalikuwa ni kama yamepigwa na upofu kwenye mwanga wa jua , ikamlazimu kukaa kwa zaidi ya dakika kadhaa ndipo alipoanza kuona vizuri, akaongozwa na yule mwanajeshi mpaka kwenye ofisi ya mkuu wa chuo ambapo alitakiwa kuandika barua maalum ya kukiri makosa yake yote kwa maandishi na kueleza kwamba hatarudia tena .
“ Hiki ulichokiandika hapa ndicho kitakachotumika kukuhukumu endapo utarudia tena makosa yako , baada ya kumaliza kifungo chako adhabu inayofuata ni kazi ngumu, utapasua kuni kwa ajili ya kupikia chakula cha wanachuo wote kwa muda wa wiki nzima.
“ Pia utapalilia ekari tatu za shamba la migomba la chuo na utapasua mawe ili kupata vifusi vitatu vikubwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya , ” alisema mkuu huyo wa chuo huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Baada ya kumaliza kumsomea adhabu anazotakiwa kuzifanya , mkuu huyo wa chuo alimuonesha Dickson sehemu maalum ya kusaini kuonesha kwamba amekubali adhabu hizo.
Aliposaini, Dickson aliruhusiwa kwenda bwenini kuoga na kujiweka kwenye hali ya usafi , tayari kwa kuendelea na shughuli nyingine za chuoni hapo ikiwa ni pamoja na kutekeleza adhabu alizopangiwa.Kwa wiki kadhaa mfululizo , Dickson aliendelea kupata msoto wa nguvu wakati akitekeleza adhabu alizopangiwa. Hata ile hamu ya kukutana kimwili na wanawake iliyokuwa inamsumbua , ilimuisha kabisa kwani kila siku alikuwa akilala hoi bin taaban na kuamshwa alfajiri na mapema kama ilivyokuwa kawaida ya chuoni hapo.
Mpaka alipomaliza adhabu alizopangiwa, mwili wake ulikuwa umepungua uzito kwa kiasi kikubwa , akawa ameshika adabu na kujiapiza kuwa ni bora aendelee kuteseka na hisia za kimapenzi kuliko kufanya upuuzi wa kutoroka tena kwenda mitaani.
Mafunzo yakaendelea huku Dickson akiwa amenyooka kitabia . Kila alipokuwa akizidiwa na hamu ya kukutana kimwili na mwanamke, alikuwa akienda kumaliza haja zake kwenye mabafu ya chuo hicho kwa kujichua mpaka alipokidhi haja zake.
“ Nikirudi uraiani watanikoma , nitalipiza hizi taabu ninazonipata , ” alijisemea Dickson wakati akijichua bafuni . Kutokana na mazoea yake ya kujichua mara kwa mara , huku wakati mwingine akipiga kelele bafuni , wenzake waliokuwa wakisoma naye walikuwa wakimcheka sana na kumtania mara kwa mara.
Kwa kuwa alishazoea kutaniwa tangu akiwa mdogo, hakujali kitu , akaendelea na tabia yake hiyo ya ajabu mpaka alipohitimu mafunzo ya upolisi. Wakafanyiwa sherehe kubwa chuoni hapo na kutunukiwa vyeti na nishani zao , tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania .
Hatimaye wakatunukiwa vyeti na nishani mbalimbali, huku wanachuo waliong ’ara katika kada mbalimbali , nao wakitunukiwa tunu mbalimbali. Kutokana na tukio alilolifanya Dickson miezi kadhaa nyuma , hakupata tuzo yoyote zaidi ya cheti na nishani .
Kwa kuwa kulikuwa na uhaba wa maafisa wa jeshi la polisi , Dickson na wenzake wengi walipata ajira ya moja kwa moja katika Jeshi la Polisi. Dickson akapangiwa kwenye mji mdogo wa Tunduma, kwenye mpaka kati ya Tanzania na Zambia. Siku kadhaa baadaye, askari wote walikuwa tayari wamesharipoti kwenye vituo vyao vya kazi, Dickson na wenzake kadhaa wakaripoti Tunduma ambapo walipokelewa kijeshi kwa kupigiwa saluti kisha wakapangiwa majukumu ya kila mmoja.
Siku hiyohiyo aliyoripoti kazini, Dickson hakulaza damu , baada ya kupanga vitu vyake kwenye nyumba aliyopewa, alivaa nguo za kiraia na kuingia barabarani, akatafuta mwenyeji mmoja na kumuuliza mahali anakoweza kupata machangudoa.
“ Ukivuka mpaka na kwenda upande wa kule Zambia, Nakonde kuna wanawake wazuri sana wanajiuza , kama utanilipia na mimi twende nikupeleke, ” alisema kijana mdogo aliyekuwa akifanya biashara ya kuuza maji barabarani , Dickson akamwambia yupo tayari kumlipa .
Kwa kuwa hakukuwa na umbali mrefu kutoka hapo walipokuwa kuelekea Nakonde, Zambia , walitembea kwa miguu na kuvuka mpaka unaozitenganisha nchi hizo mbili kwenye sehemu maarufu ya Custom na kuingia upande wa pili, wakatembea kwa miguu na dakika kadhaa baadaye, tayari walikuwa wamewasili Nakonde.
Kijana huyo akampeleka moja kwa moja mpaka eneo maarufu liitwalo Zesco ambapo walikatiza mitaa na kutokea kwenye nyumba moja kubwa ya kifahari, iliyokuwa na wanawake wengi wazuri waliokuwa wamekaa kibarazani.
Wanawake hao waliokuwa wamevalia kihasarahasara, walipowaona tu Dickson na mwenzake, waliwachangamkia na kuanza kuwazungumzisha Kiwemba , lugha kubwa inayozungumzwa nchini Zambia .
“ Watshani boizi , kulichi kung ’anda, ” ( mambo zenu kina kaka, habari za nyumbani) walisema wanawake hao huku wengine wakiinuka haraka kuwafuata Dickson na mwenzake .
“ Bwino , kung ’anda kulichete! Tulefwaya sevisi, ” ( Nzuri , za nyumbani salama, tunataka huduma) alijibu kijana huyo aliyeonekana kuielewa vyema lugha hiyo , wanawake hao wakawazunguka, wengine wakawa wanawamwagia mvua ya mabusu huku wengine wakiwavuta kuelekea ndani, Dickson akawa anameza mafunda ya mate mfululizo , kama fisi aliyeona lundo la mifupa
Anaendelea na masomo chini ya uangalizi mkali na hatimaye anahitimu na kupangiwa kituo cha kazi katika mji mdogo wa Tunduma, uliopo kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
aada ya kusafiri kwa muda mrefu, hatimaye Dickson au Zinja na wenzake waliokuwa wamepangiwa kwenda kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Tunduma, waliwasili kwenye mji huo mdogo na kupokelewa vizuri na wenyeji wao kisha kila mmoja akapangiwa majukumu pamoja na kuoneshwa nyumba ya kuishi.
Siku hiyohiyo, Dickson hakutaka kulaza damu, kwa jinsi alivyokuwa akijisikia hamu ya kukutana kimwili na mwanamke, aliona kama hawezi kufika kesho yake, akaingia mitaani na kukutana na kijana mmoja aliyekubaliana naye ampeleke kwenye sehemu anazoweza kupata machangudoa.
Wakavuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Zambia, kwenye Mji wa Nakonde alikoelekezwa kwamba ndiyo kuna machangudoa wazuri, akaongozana na kijana huyo mpaka kwenye mtaa maarufu wa Zesco na hatimaye wakatokezea kwenye nyumba nzuri iliyokuwa na wanawake wengi waliovalia kihasarahasara.
Kwa kuwa mwenzake alikuwa akiielewa Lugha ya Kiwemba ambayo ndiyo iliyokuwa inatumika sana nchini humo, alifanikiwa kuzungumza na wanawake hao na kuwaeleza shida yao, wakawagombania kama mpira wa kona na kuingizwa ndani.
Muda mfupi baadaye, Dickson na mwenzake walikuwa wakielea kwenye ulimwengu tofauti kabisa, huku Dickson akionesha kufurahia sana alichokuwa anakifanya, hasa ukizingatia jinsi alivyokuwa anabanwa kwa sheria kali kipindi alipokuwa jeshini.
Baada ya kukidhi haja zao na kulipa gharama walizotajiwa, waliaga na kuondoka huku Dickson akionesha kunogewa mno na mchezo huo. Njiani akawa na kazi ya ziada ya kukariri mitaa na njia ili siku nyingine awe anaenda peke yake.
Mpaka Dickson anarejea kwenye nyumba yake mpya, tayari ilishatimia saa moja za usiku, akaenda kuoga na kupumzika kwani tangu afike hakupata hata muda wa kupumzika. Akawa ameyaanza maisha mapya huku akionesha kuufurahia sana mji wa Tunduma.
Kesho yake asubuhi, alienda kuripoti kazini kwa mara ya kwanza, akapangiwa kukaa kaunta na askari wenzake wakati akielekezwa kazi mbalimbali anazotakiwa kuwa anazifanya kila siku kituoni hapo.Mchana, alichukuliwa na askari wenzake na kuingia kwenye difenda, wakawa wanazunguka na askari wenzake sehemu mbalimbali za mji huo mdogo lakini uliochangamka sana kibiashara.
Alitembezwa mitaa yote, kuanzia Maporomoko, Mwaka, Black Market, Tukuyu, Majengo mpaka Majengo Mapya kisha wakarejea kituoni, ikiwa tayari imeshatimia saa kumi na moja jioni, akakamilisha taratibu za kawaida na kuruhusiwa kwenda kwenye nyumba yake, iliyokuwa jirani na kituo hicho kwa ajili ya mapumziko.
Japokuwa hakuna aliyeweza kumuonesha dhahiri, askari wenzake na watu wote waliokuwa wakikutana na Dickson, walikuwa wakionesha mshangao kwa jinsi sura yake ilivyokuwa mbaya.Alipofika nyumbani kwake, alibadilisha nguo na kuvaa za kiraia, akavaa kofia yake kubwa iliyokuwa inaziba sehemu kubwa ya uso wake na kutoka, akaianza safari ya kuelekea Nakonde huku akiwa makini kuhakikisha hapotei.
Akafanikiwa kuvuka mpaka na kuingia Nakonde bila tatizo, akachanja mitaa na hatimaye akatokea Zesco na kunyoosha moja kwa moja mpaka kwenye nyumba ya wale machangudoa ambapo walipomuona tu, walimchangamkia kwani walikuwa wanamkumbuka.
Tatizo likawa namna ya kuelewana naye kwani hakuwa akijua Kiwemba, akalazimika kutumia Kiingereza, kwa bahati nzuri wengi walionekana kumuelewa alichokuwa anakisema, akamchagua mmoja aliyekuwa anamtaka na kuingia naye mpaka kwenye vyumba vya ndani, wakamalizana kisha Zinja akalipa fedha na kuondoka zake.
Huo ndiyo ukawa mchezo wake, ikawa kila siku jioni ni lazima avuke mpaka na kuelekea Nakonde kutafuta machangudoa ambao kila siku alikuwa akiwabadilisha kama nguo, leo akitoka na mnene, kesho anamtaka mwembamba, keshokutwa akitoka na mfupi siku inayofuatia anatoka na mrefu!
Siku alizokuwa anaingia shifti za usiku, alikuwa anapata sana shida ambapo asubuhi na mapema baada ya kutoka kazini, ilikuwa ni lazime avuke mpaka. Hayo ndiyo yakawa maisha yake.Hata hivyo, kipato alichokuwa anakipata kutokana na kazi yake ya upolisi, hakikuwa kinamtosha kwa matumizi ya aina hiyo kwani ukiachilia mbali kwenda kununua machangudoa, ilikuwa ni lazima pia ale na kufanya mambo mengine mengi ambayo yote yalihitaji fedha.
Upande wa kazi, japokuwa alikuwa mgeni, alianza kupata umaarufu mkubwa kutokana na jinsi alivyokuwa mahiri wa kupambana na matukio ya uvunjifu wa amani, huku alama yake kubwa ikiwa ni sura yake mbaya ambayo hata akicheka alikuwa akionekana kama analia.
Vijana wakorofi wa Tunduma, waliokuwa wakisifika kwa matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani, wakambatiza kwa jina la Afande Sura Mbaya, huku wengi wakionekana kumchukia kutokana na umakini wake awapo kazini.
Hata hivyo, kutokana na uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya kwenda kununua machangudoa, Dickson alijikuta akianza kutoka nje ya mstari, akaanza tabia ya kupokea rushwa ndogondogo kutoka kwa wahalifu aliokuwa anawakamata, lengo lake likiwa ni kuhakikisha kila siku hakosi kwenda kuopoa changudoa.
Siku moja, akiwa amepangwa zamu ya usiku, wakiwa mitaani ndani ya gari la polisi, walishtushwa na milio mfululizo ya risasi zilizokuwa zinamiminwa kuelekea kwenye gari walilokuwemo, vioo vyote vikapasuliwa pamoja na matairi huku risasi zikiendelea kurindima, ikabidi askari wote watumie mafunzo yao kunusuru maisha yao yaliyokuwa hatarini.
Wakajirusha kwa ufundi mkubwa mpaka nje ya gari lakini haikusaidia kitu, risasi ziliendelea kufyatuliwa kwa kasi ya ajabu.
Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono . Baadaye Dickson au Zinja anahitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwenda kujiunga na Chuo cha Polisi mjini Moshi, Kilimanjaro. Anapohitimu anapangiwa kwenda kufanya kazi katika mji mdogo wa Tunduma, uliopo kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia. Baada ya mafanikio makubwa, anahamishwa kikazi na kuelekea Dar es Salaam, huko, kama alivyofanya sehemu nyingine, napo anaendelea na mchezo wake kama kawaida . Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO…
Ilisikika milio mingi ya risasi kutoka katika Benki ya Dar es Salaam iliyokuwa maeneo ya Ubungo . Watu wengi waliokuwa karibu na eneo hilo wakaanza kukimbia kuyaokoa maisha yao , wanawake walikuwa wakipiga kelele huku wengine wakilala chini ili wasiweze kupigwa na risasi hizo .
Hakukuwa na utulivu hata mara moja, milio ile ya risasi ambayo ilisikika kutoka ndani ya benki ile ikawapelekea polisi waliokuwa karibu na benki hiyo kufika eneo la tukio huku wakiwa na bunduki zao mikononi .Benki ya Dar es Salaam ilikuwa imevamiwa na majambazi watano waliokuwa na bunduki zenye nguvu mikononi mwao. Kila mtu aliyekuwa ndani ya benki ile aliamriwa kulala chini na kutoangalia kitu kilichokuwa kikiendelea .
“ Weka fedha haraka dada, usiniangalie usoni, mimi siyo mjomba wako , ” alisema jambazi mmoja kwa sauti yenye utetemeshi mkubwa iliyomtisha dada huyo na kufanya kama alivyoagizwa.
Ndani ya dakika kadhaa, polisi waliendelea kuongezeka karibu na eneo hilo. Kila aliyejaribu kuingia ndani, alipigwa risasi, damu zikatapaa katika eneo la nje ya benki hiyo .
Hakukuwa na polisi aliyetaka kuingia ndani, kila mmoja aliona hatari iliyokuwa mbele yake, waliyapenda maisha yao, hivyo hawakuwa radhi kuona wakipigwa risasi na kufariki dunia na wakati walikuwa na familia zao. Wala hazikupita dakika nyingi , Inspekta wa polisi , Dickson akafika eneo la tukio huku akiwa ametangulizana na baadhi ya polisi . Alichokifanya ni kuteremka ndani ya gari na kuanza kuwafuata polisi wenzake ambao walimwambia kile kilichokuwa kikiendelea .
Hiyo, kwake ilionekana kuwa kazi ndogo , alichokifanya, akachukua bastola ndogo, akaiweka kiunoni mwake na kisha kuanza kuufuata mlango wa benki ile . Kila polisi akaogoppa, alimshangaa Dickson kwani hakukuwa na mtu aliyekuwa radhi kuusogelea mlango ule ambapo ndani yake, risasi ziliendelea kurushwa kila wakati .
Alipoona ameukaribia mlango ule, akajibanza pembeni ukutani na kisha kuitoa bunduki yake na kuishikilia. Polisi wote waliokuwa wakimwangalia , walishangaa , hawakujua Inspekta wao alipata wapi ujasiri kiasi kile , alichokifanya ni kuanza kuupiga risasi mlango ule wa vioo mpaka kioo chote kilipovunjika .
“ Pigeni risasi mfululizo , ” aliwaambia polisi wake.
Risasi zilipigwa mfululizo kuelekea ndani ya benki ile , zaidi ya risasi hamsini zikapigwa hali iliyowafanya majambazi wale kujificha. Hiyo ilikuwa nafasi pekee kwa Inspekta Dickson , kama ninja mwenye mafunzo makubwa , akarukia ndani ya benki ile ambapo majambazi walikuwa wamejificha na bunduki zao .
Alipotua ndani tu , kwa kasi ya ajabu, akaanza kuwamiminia risasi majambazi wale ambao kwa ghafla sana walimuona kama mzimu kutokana na uharaka wake wa kuingia ndani ya benki ile .
Kazi ilikuwa kubwa lakini ndani ya dakika moja tu , majambazi wote watano walikuwa chini , damu zilikuwa zikiwatoka hali iliyomaanisha kwamba jengo lilikuwa salama.
Hilo likawa tukio jingine kubwa ambalo alikuwa amelifanya Inspekta Dickson. Taarifa juu ya umahiri wake zikatangazwa , serikali ikajivunia kuwa na polisi kama yeye hivyo kupandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishina wa Polisi ( DCP) kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
* * *
Pamoja na umahiri wake wa kupambana na majambazi lakini bado Dickson hakuachana na tabia yake ya kuendekeza kununua machangudoa mitaani na kwenda nao hotelini kufanya nao ngono . Aliyazoea maisha hayo tangu Tunduma hivyo kuachana nayo ilikuwa kazi ngumu mno.
Siku zikaendelea kukatika, kama kawaida yake , kila siku usiku alikuwa akienda sehemu wanawake walipokuwa wakijiuza na kumchukua mwanamke mmoja kisiri na kuondoka naye .
Hakutaka kujulikana kutokana na umaarufu wake. Kila kitu alichokuwa akiendelea kukifanya, alikifanya kisiri mno.
“ Mpaka asubuhi nitakufanyia elfu hamsini , ” alisema changudoa mmoja, alikuwa akizungumza na mteja wake aliyevalia kofia ambaye hakutaka kuteremka garini, DCP Dickson.
“ Ingia twende , ” alisema Dickson na msichana yule kuingia .
Safari yao ikaishia ndani ya hoteli moja ya kifahari ambapo akaingia ndani na msichana yule. Kitu cha kwanza kabisa kukifanya , alifanya kila liwezekanalo kuhakikisha taa haiwashwi , hilo halikuwa na tatizo kwani alichokihitaji changudoa yule ni hela yake tu .
Walifanya mapenzi kwa zaidi ya masaa matatu, walipomaliza, msichana yule akasimama na kuifuata swichi ya taa ya chumba kile . Alitaka kuuona uso wa mwanaume huyo aliyempa haki yake mpaka kuridhika , akawasha taa na DCP Dickson kushtuka kutokana na mwanga mkali.
“ Aaah! Dickson. ..!!” msichana yule alijikuta akisema huku akiwa na mshtuko mkubwa, Dickson akamwangalia mwanamke yule , naye akahofia kwa kuona aligundulika . Akabaki akiwa ameduwaa tu
Kwa upande wa kazi , Dickson anaendelea kujituma kadiri ya uwezo wake , jaribio la kutaka kumuua linashindikana na muda mfupi baadaye, anafanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi kwenye benki , hali inayosababisha apandishwe tena cheo na kufikia ngazi ya DCP. Hata hivyo , michezo yake ya kununua machangudoa anaendelea nayo .
Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO…
Baada ya kukidhi haja za mwili wake , DCP Dickson au Zinja kama alivyokuwa akifahamika tangu akiwa chuoni, alijitupa kitandani huku akionesha kuchoka sana kutokana na kazi nzito aliyotoka kuifanya .
Ghafla akashtuka taa ya chumba cha gesti aliyokuwa amelala na mwanamke huyo ikiwashwa, jambo ambalo lilimfanya ashtuke mno, akajua siri yake imefichuka. Mshtuko alioupata ulisababisha mwanamke yule ambaye bado alikuwa amesimama pembeni ya swichi kushtuka, akamtaza vizuri Dickson na kujikuta akipigwa na butwaa.
“ Haaa ! Dickson ?” alisema mwanamke huyo kwa mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa mwanaume aliyekuwa amelala naye , alikuwa kiongozi mkubwa kwenye jeshi la polisi .Kutokana na jinsi mwanamke huyo alivyoshtuka, almanusra atoke nje bila nguo lakini Dickson alimuwahi na kuchomoa funguo na kuificha .
“ Nisamehe, nisamehe , ” alisema mwanamke huyo kwa hofu huku akihisi kwamba huenda kiongozi huyo wa jeshi la polisi alikuwa anataka kumkamata na kumfungulia mashtaka kwa kujihusisha na biashara ya uchangudoa.
Kwake aliamini haiwezekani kabisa Dickson akawa ni mteja wa kawaida kwani kwa hadhi aliyokuwa nayo , aliamini lazima ana familia yake.
“ Wala sina nia mbaya na wewe , tafadhali usiogope, ” alisema Dickson kwa sauti ya chini kwani kwa jinsi mwanamke huyo alivyoonesha kushtuka, angeweza hata kupiga kelele za kuomba msaada , Dickson akawa anaendelea kumbembeleza na kumtoa wasiwasi .
Ilimchukua muda mrefu sana mwanamke huyo kutulia, japokuwa hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuonana uso kwa uso na Dickson, kila kukicha alikuwa akimuona kwenye runinga na kwenye magazeti au wakati mwingine kusikia habari zake kwenye redio jinsi alivyokuwa shujaa wa kupambana na ujambazi na vitendo vingine vya uvunjifu wa amani .
Akawa anamtazama kwa hofu huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio kwani ukiachilia mbali vyeo alivyokuwa navyo Dickson, sura yake pia ilikuwa inatisha sana . Dickson akaendelea kumbembeleza kwa muda mrefu mpaka akatulia.
“ Unaniahidi hutamwambia mtu yeyote kwamba usiku wa leo umelala na mimi?” Dickson alimuuliza mwanamke huyo ambaye harakaharaka alitingisha kichwa kukubali.
Japokuwa aliahidi kuitunza siri hiyo , ndani ya moyo wake alikuwa na hofu kubwa kwamba siri ile itavuja na kumsababishia fedheha kubwa na pengine kusababisha afukuzwe kazi kabisa.
Japokuwa makubaliano yao ilikuwa ni kulala mpaka alfajiri na mapema , Dickson aliamua kubadilisha mawazo , akainuka na kuanza kuvaa nguo zake , akamwamuru mwanamke huyo naye kuvaa nguo zake .
“ Tunaenda wapi ?”
“ Nataka tuhame gesti , sidhani kama hapa panatufaa, ” alisema Dickson huku akilazimisha tabasamu kwenye uso wake . Akamuahidi mwanamke huyo kumuongeza fedha kutoka shilingi elfu hamsini walizokuwa wamekubaliana awali mpaka shilingi laki moja, jambo lililomfanya mwanamke huyo kukubali kirahisi .
Wakaongozana mpaka nje ya gesti waliyoingia huku Dickson akiwa ameshusha kofia na kuziba sura yake ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kumtambua, wakatoka mpaka kwenye gari lake ambapo Dickson alimfungulia mwanamke huyo mlango wa gari , naye akaingia upande wa pili na kuondoa gari taratibu mpaka alipoingia kwenye barabara ya lami .
“ Tunaelekea wapi ?”
“ Kuna hoteli moja nzuri sana ipo Mbezi Beach inaitwa Ichenjezya Resort, nadhani itatufaa sana , ” alisema Dickson huku akibadilisha gia kwenye gari lake na kuzidi kuchanja mbuga.Walipofika Mwenge, Dickson alisimamisha gari pembeni kidogo ya stendi ya kuelekea Tegeta , akamwambiamwanamke huyo amsubiri kidogo anaenda kununua vinywaji. Ili kuhakikisha kwamba hamkimbii, Dickson alipoteremka garini alibonyeza rimoti ya gari na ‘kuiloki’ milango yote .
Dakika chache baadaye, alirejea akiwa na vinywaji viwili mkononi , kimoja kikiwa kimeshafunguliwa . Akamkabidhi mwanamke huyo kile kinywaji kilichokuwa kimefunguliwa kisha na yeye akafungua cha kwake huku akiwasha gari . Muda mfupi baadaye, tayari walikuwa kwenye barabara ya lami , wakichanja mbuga kuelekea Mbezi.
Tofauti na awali , safari hii Dickson alionesha kuchangamka sana , akawa anamsemesha mwanamke huyo mambo mbalimbali huku akimsisitiza kunywa kinywaji chake mpaka amalize . Baada ya kunywa mafunda kadhaa, mwanamke huyo alianza kulalamika kwamba anasikia usingizi mzito.
Dickson akamtegulia siti na kumwambia apumzike, wakifika atamuamsha . Dakika chache baadaye , alikuwa hajitambui kwa usingizi, Dickson akaachia tabasamu pana na kuzidi kukanyaga mafuta , gari likawa linakimbia kwa spidi 120 huku akiwa makini kuhakikisha hakuna mtu anayemfuatilia.
Saa nane za usiku juu ya alama , Dickson alikuwa akichepuka kutoka kwenye barabara kuu, eneo la Madale na kuifuata barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea kwenye Msitu wa Pande , nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa muda wote huo, mwanamke huyo alikuwa akiendelea kukoroma, akiwa haelewi kabisa kilichokuwa kinaendelea.
Anapohitimu anapangiwa kwenda kufanya kazi katika mji mdogo wa Tunduma, uliopo kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia . Baada ya mafanikio makubwa, anahamishwa kikazi na kuelekea Dar es Salaam , huko , kama alivyofanya sehemu nyingine, napo anaendelea na mchezo wake kama kawaida .
Kwa upande wa kazi , Dickson anaendelea kujituma kadiri ya uwezo wake , jaribio la kutaka kumuua linashindikana na muda mfupi baadaye, anafanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi kwenye benki , hali inayosababisha apandishwe tena cheo na kufikia ngazi ya DCP. Hata hivyo , michezo yake ya kununua machangudoa anaendelea nayo huko.
Je , nini kitafuatia ? SONGA NAYO…
Tabasamu pana lilikuwa usoni mwa Dickson, aliendelea kuendesha gari lile kwa kasi kuelekea msituni. Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi, alijua kwamba alikuwa akienda kufanya kitu kibaya kwa mtu asiyekuwa na hatia yoyote ile lakini hakuwa na jinsi.
Hakutaka suala lake la kununua machangudoa lijulikane, alitaka liendelee kuwa siri katika maisha yake yote. Alizidi kuliendesha gari lile kwa dakika kadhaa na ndipo alipofika sehemu ambayo aliiona kuwa nzuri kufanya kile alichotaka kukifanya .
Akasimamisha gari na kuteremka, akaelekea nyuma ya gari ambapo akafungua buti na kisha kutoa koleo kisha kuelekea sehemu iliyokuwa na udongo laini na kuanza kuchimba . Haikuwa kazi nyepesi lakini alitakiwa kumalizana nayo haraka sana . Aliendelea kuchimba shimo kubwa ambapo alitumia zaidi ya dakika arobaini , lilipokamilika akalifuata gari lake na kumchukua mwanamke yule ambaye bado alikuwa akikoroma.
“ Ni lazima nimuue, haina jinsi , ” alijisemea , akambeba mwanamke yule na kuelekea naye kule kulipokuwa na shimo kubwa. Alipomfikisha , akamtumbukiza shimoni na yeye mwenyewe kuingia . Moyo wake ulikwishabadilika, hakuwa katika hali ya ubinadamu , alikuwa mnyama wa kutisha asiyekuwa na masihara hata mara moja.
Alichokifanya mara baada ya kuingia shimoni ni kuanza kumpiga mwanamke kichwani kwa kutumia koleo lake. Alimpiga na kumsababishia jeraha kubwa, damu ikaanza kuvilia ndani ya ubongo wake na haikuchukua muda mrefu , mapigo ya moyo ya mwanamke yule yakasimama, akawa amefariki dunia palepale shimoni.
Dickson akatoka na kuangalia huku na kule kuona kama kulikuwa na mtu aliyekuwa akimuona kwani kwa mbali tayari mwanga ulianza kuonekana, alfajiri ilianza kuingia . Hakutaka kupoteza muda , alitaka kufanya kila kitu haraka hivyo akaanza kuufukia mwili ule.
“ Saa kumi na moja hii , ngoja nifanye haraka, ” alisema huku akiiangalia saa yake .
Hakuchukua muda mrefu , akamaliza. Alichokifanya ni kushindilia sehemu ile huku akichukua baadhi ya majani na kuyaweka juu ya shimo lile , alipoona kila kitu kipo vizuri, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo huku akiwa na amani moyoni mwake .
* * *
Japokuwa Dickson aliamini kwamba alikuwa peke yake na hakukuwa na mtu yeyote yule aliyekuwa akimuona, lakini ukweli ni kwamba kulikuwa na mzee mmoja, mwindaji ambaye alikuwa amejificha katikati ya miti akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea .
Mzee huyu aliyeitwa Gombana alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiingia katika Msitu wa Pande kila siku alfajiri kwa ajili ya uwindaji wa wanyama wadogo. Siku hiyo ambayo aliamini kwamba angeweza kupata chochote kile , aliingia lakini kitu cha ajabu ni kwamba akakuta kitu cha tofauti kabisa .
Mbele yake , umbali kama wa hatua hamsini aliliona gari limesimama , kwanza akashtuka, haikuwa kawaida kabisa kulikuta gari ndani ya msitu huo . Akaogopa sana , akatamani kukimbia kwani moyo wake ulijua kwamba inawezekana gari lile lilikuwa la majambazi hivyo kumfanyia kitu kibaya , ila kila alivyotaka kufanya hivyo , moyo wake ulisita.
Alichokifanya mara baada ya kufikisha hatua ishirini kabla ya kulifikia gari lile ni kujificha, akamuona mwanaume mmoja akiubeba mwili wa mwanamke na kuutumbukiza shimoni kisha kuanza kuufukia. Mzee Gombana hakuamini alichokuwa akikiona, alitamani kupiga simu polisi ili aweze kuwafahamisha juu ya kile kilichokuwa kikiendelea lakini hakuwa na simu .
Alibaki akimwangalia mtu yule aliyekuwa bize na kazi yake . Kwa kuwa hakujua ni kwa namna gani angeweza kufikisha taarifa zile kwa polisi , alichokifanya ni kukariri namba za gari lile tu ambazo aliamini kwamba zingekuwa msaada mkubwa kwake katika kutoa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea .
Mpaka gari linaondoka mahali hapo, alikuwa na uhakika kwamba taarifa ambayo angeitoa polisi ingekuwa ya uhakika iliyokuwa na ushahidi wa kutosha.
Mzee Gombana hakutaka kumwambia mtu yeyote yule juu ya kile kilichokuwa kimetokea , alikifanya kuwa siri mpaka asubuhi iliyofuata akajiandaa kwenda katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya kile alichokuwa amekiona .
“ Vipi mume wangu ?” aliuliza mkewe .
“ Safi tu .”
“ Mbona upo hivyo ?”
“ Nipo vipi ?”
“ Hujiaminiamini .”
“ Nipo kawaida tu , usihofu, ” alimwambia mke wake.
Hakutaka kitu hicho kijulikane kwa mtu yeyote yule, alikifanya kuwa siri kubwa mpaka ilipofika saa tatu asubuhi, muda ambao alianza kuelekea katika kituo hicho kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea .
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha . Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea. Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata , wote wanapotea katika mazingira yanayofanana . Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen , aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea. Upande wa pili , kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono. Baadaye Dickson au Zinja anahitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwenda kujiunga na Chuo cha Polisi mjini Moshi , Kilimanjaro. Anapohitimu anapangiwa kwenda kufanya kazi katika mji mdogo wa Tunduma, uliopo kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia. Baada ya mafanikio makubwa, anahamishwa kikazi na kuelekea Dar es Salaam, huko, kama alivyofanya sehemu nyingine , napo anaendelea na mchezo wake kama kawaida . Kwa upande wa kazi, Dickson anaendelea kujituma kadiri ya uwezo wake , jaribio la kutaka kumuua linashindikana na muda mfupi baadaye , anafanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi kwenye benki, hali inayosababisha apandishwe tena cheo na kufikia ngazi ya DCP. Hata hivyo, michezo yake ya kununua machangudoa anaendelea nayo huko. Je, nini kitafuatia ? SONGA NAYO … Tabasamu pana lilikuwa usoni mwa Dickson, aliendelea kuendesha gari lile kwa kasi kuelekea msituni. Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi , alijua kwamba alikuwa akienda kufanya kitu kibaya kwa mtu asiyekuwa na hatia yoyote ile lakini hakuwa na jinsi. Hakutaka suala lake la kununua machangudoa lijulikane , alitaka liendelee kuwa siri katika maisha yake yote. Alizidi kuliendesha gari lile kwa dakika kadhaa na ndipo alipofika sehemu ambayo aliiona kuwa nzuri kufanya kile alichotaka kukifanya. Akasimamisha gari na kuteremka, akaelekea nyuma ya gari ambapo akafungua buti na kisha kutoa koleo kisha kuelekea sehemu iliyokuwa na udongo laini na kuanza kuchimba . Haikuwa kazi nyepesi lakini alitakiwa kumalizana nayo haraka sana . Aliendelea kuchimba shimo kubwa ambapo alitumia zaidi ya dakika arobaini, lilipokamilika akalifuata gari lake na kumchukua mwanamke yule ambaye bado alikuwa akikoroma . “Ni lazima nimuue, haina jinsi, ” alijisemea , akambeba mwanamke yule na kuelekea naye kule kulipokuwa na shimo kubwa . Alipomfikisha , akamtumbukiza shimoni na yeye mwenyewe kuingia. Moyo wake ulikwishabadilika, hakuwa katika hali ya ubinadamu , alikuwa mnyama wa kutisha asiyekuwa na masihara hata mara moja . Alichokifanya mara baada ya kuingia shimoni ni kuanza kumpiga mwanamke kichwani kwa kutumia koleo lake . Alimpiga na kumsababishia jeraha kubwa , damu ikaanza kuvilia ndani ya ubongo wake na haikuchukua muda mrefu , mapigo ya moyo ya mwanamke yule yakasimama , akawa amefariki dunia palepale shimoni. Dickson akatoka na kuangalia huku na kule kuona kama kulikuwa na mtu aliyekuwa akimuona kwani kwa mbali tayari mwanga ulianza kuonekana, alfajiri ilianza kuingia. Hakutaka kupoteza muda , alitaka kufanya kila kitu haraka hivyo akaanza kuufukia mwili ule . “Saa kumi na moja hii , ngoja nifanye haraka,” alisema huku akiiangalia saa yake . Hakuchukua muda mrefu, akamaliza. Alichokifanya ni kushindilia sehemu ile huku akichukua baadhi ya majani na kuyaweka juu ya shimo lile , alipoona kila kitu kipo vizuri, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo huku akiwa na amani moyoni mwake. * * * Japokuwa Dickson aliamini kwamba alikuwa peke yake na hakukuwa na mtu yeyote yule aliyekuwa akimuona , lakini ukweli ni kwamba kulikuwa na mzee mmoja, mwindaji ambaye alikuwa amejificha katikati ya miti akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Mzee huyu aliyeitwa Gombana alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiingia katika Msitu wa Pande kila siku alfajiri kwa ajili ya uwindaji wa wanyama wadogo. Siku hiyo ambayo aliamini kwamba angeweza kupata chochote kile, aliingia lakini kitu cha ajabu ni kwamba akakuta kitu cha tofauti kabisa . Mbele yake , umbali kama wa hatua hamsini aliliona gari limesimama, kwanza akashtuka, haikuwa kawaida kabisa kulikuta gari ndani ya msitu huo. Akaogopa sana , akatamani kukimbia kwani moyo wake ulijua kwamba inawezekana gari lile lilikuwa la majambazi hivyo kumfanyia kitu kibaya , ila kila alivyotaka kufanya hivyo , moyo wake ulisita. Alichokifanya mara baada ya kufikisha hatua ishirini kabla ya kulifikia gari lile ni kujificha , akamuona mwanaume mmoja akiubeba mwili wa mwanamke na kuutumbukiza shimoni kisha kuanza kuufukia . Mzee Gombana hakuamini alichokuwa akikiona , alitamani kupiga simu polisi ili aweze kuwafahamisha juu ya kile kilichokuwa kikiendelea lakini hakuwa na simu . Alibaki akimwangalia mtu yule aliyekuwa bize na kazi yake . Kwa kuwa hakujua ni kwa namna gani angeweza kufikisha taarifa zile kwa polisi, alichokifanya ni kukariri namba za gari lile tu ambazo aliamini kwamba zingekuwa msaada mkubwa kwake katika kutoa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea . Mpaka gari linaondoka mahali hapo , alikuwa na uhakika kwamba taarifa ambayo angeitoa polisi ingekuwa ya uhakika iliyokuwa na ushahidi wa kutosha . Mzee Gombana hakutaka kumwambia mtu yeyote yule juu ya kile kilichokuwa kimetokea , alikifanya kuwa siri mpaka asubuhi iliyofuata akajiandaa kwenda katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya kile alichokuwa amekiona. “Vipi mume wangu ?” aliuliza mkewe . “Safi tu.” “Mbona upo hivyo?” “Nipo vipi?” “Hujiaminiamini .” “Nipo kawaida tu, usihofu ,” alimwambia mke wake . Hakutaka kitu hicho kijulikane kwa mtu yeyote yule , alikifanya kuwa siri kubwa mpaka ilipofika saa tatu asubuhi , muda ambao alianza kuelekea katika kituo hicho kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya kile kilichokuwa kimetokea . Je, nini kitafuatia ?
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote waliopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa.
Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono. Baadaye Dickson au Zinja anahitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwenda kujiunga na chuo cha polisi mjini Moshi, Kilimanjaro.
Anapohitimu anapangiwa kwenda kufanya kazi katika mji mdogo wa Tunduma, uliopo kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia. Baada ya mafanikio makubwa, anahamishwa kikazi na kuelekea Dar es Salaam, huko, kama alivyofanya sehemu nyingine, napo anaendelea na mchezo wake kama kawaida.
Kwa upande wa kazi, Dickson anaendelea kujituma kadiri ya uwezo wake, jaribio la kutaka kumuua linashindikana na muda mfupi baadaye, anafanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi kwenye benki, hali inayosababisha apandishwe tena cheo na kufikia ngazi ya DCP.
Hata hivyo, michezo yake ya kununua machangudoa anaendelea nayo.
Anapoona amemnunua changudoa na kugunduliwa, anamuua na kumzika msituni.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Alitembea kwa harakaharaka, moyoni alikuwa na kimuemue cha kusema kile kilichokuwa kimetokea msituni ambacho hakutaka mtu yeyote yule afahamu zaidi ya polisi wao na kisha kuwaambia juu ya lile gari aliloliona msituni kwani namba zake alikuwa nazo kichwani.
Alichukua zaidi ya dakika kumi ndipo alipofika kituoni huku akiwa anahema kwa nguvu na kijasho chembamba kikimtiririka. Jambo lililowashangaza polisi wale.
“Karibu. Unataka nini?” aliuliza polisi aliyekuwa kaunta mara baada ya salamu.
“Nimekuja kutoa taarifa.”
“Taarifa gani?”
“Ya mauaji,” alijibu mzee Gombana.
“Hebu njoo huku,” alisema polisi yule huku akimvuta ndani ya chumba kidogo kwa ajili ya mahojiano marefu kwani taarifa ya mauaji haikuwa ndogo. Polisi waliokuwa wamemsikia ambao walikuwa karibu na kaunta ile, nao wakaelekea ndani. Hawakujua kama taarifa aliyoileta mzee huyo ilikuwa ni ya mauaji yaliyofanywa na kamanda wao.
“Umesema umeleta taarifa ya mauaji, si ndiyo?” aliuliza mkuu wa kituo hicho.
“Ndiyo!”
“Wapi?”
“Kule msituni.”
Alichokifanya mzee Gombana ni kuanza kuhadithia kilichokuwa kimetokea kule porini, aliwaambia kwamba alimuona mtu akiwa amefika msituni akiwa na gari, baada ya kusimama aliitoa maiti moja na kuizika katika shimo kubwa alilokuwa amelichimba.
Kila polisi aliyesikia taarifa ile alishtuka, walijaribu kumuuliza mzee huyo mara mbilimbili kama alikuwa na uhakika na kile alichokuwa amekisema, akawaambia kwamba alikuwa na uhakika na wangefika mpaka katika eneo hilo.
Hawakutaka kuendelea na mahojiano ndani ya chumba kile, walichokifanya ni kutoka, wakachukua gari lao, difenda, polisi wanne waliokuwa na bunduki wakaingia garini na safari ya kuelekea huko msituni kuanza.
Walichukua dakika arobaini mpaka kufika katika msitu huo ambapo wakaanza kuingia ndani zaidi. Dereva hakuendesha gari kwa mwendo wa kasi kutokana na miti mingi iliyokuwepo hali iliyosababisha ukosefu wa barabara ya magari.
“Wapi?” aliuliza polisi mmoja.
“Kule mbele mkuu! Nyie twendeni tu,” alisema mzee Gombana na hivyo dereva kuliendesha gari kuelekekea mbele zaidi.
Waliendelea kwenda mbele mpaka walipofika sehemu moja iliyoonekana kuwa na uwazi mkubwa, hapo ndipo mzee Gombana alipotaka gari lisimamishwe na kuegeshwa pembeni kwani hiyo ndiyo ilikuwa sehemu alipomuona Dickson akimzika mwanamke na kuondoka zake.
Kwa jinsi eneo lile lilivyokuwa, hawakuwa na shaka kwamba muda mchache uliopita sehemu hiyo ilichimbwa na kufukiwa, walichokifanya polisi wale ni kuchukua makoleo yaliyokuwa garini na kuanza kufukua lile shimo.
“Bila shaka huyu mzee yupo sahihi kabisa, humu kutakuwa na maiti, si unaona udongo unavyoonesha?” alisema polisi mmoja huku wengine wakiendelea kufukua lile shimo.
Kazi haikuwa ndogo, japokuwa walikuwa wengi lakini walipata kazi kubwa kulifukua lile shimo. Mzee Gombana alisimama pembeni, alikuwa akifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo huku moyoni akimuomba Mungu mwili wa mtu huyo ukutwe ili aweze kuaminika kwa taarifa aliyoitoa.
Baada ya dakika kadhaa, makoleo yao yakaanza kudunda mwilini mwa maiti na kugundua kwamba tayari walikuwa wameifikia, hivyo wakayatupa makoleo yao pembeni na kuanza kutoa mchanga kwa kutumia mikono.
“Ni msichana!” alisema polisi mmoja na hivyo kusaidiana kuutoa mwili ule.
Kila mmoja akapigwa na mshtuko, alionekana kuwa msichana mrembo wa sura na umbo, kila mtu aliyemwangalia alishindwa kuelewa kipi kilichotokea katika maisha yake mpaka huyo mtu aliyemuua na kumzika aliamua kufanya hivyo.
Walichokifanya ni kuubeba mwili ule na kuondoka nao kwa ajili ya uchunguzi wa kujua ni kitu gani kilisababisha kifo chake hata kabla ya kuzikwa. Hawakutaka kumuacha mzee Gombana, bado alihitajika kwa ajili ya kuisaidia polisi juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Kuna chochote unachokikumbuka kuhusu muuaji?” aliuliza mkuu wa polisi.
“Ndiyo! Nililiona gari lake!”
“Aina gani? Unazijua namba zake?”
“Ndiyo! Nakumbuka kila kitu.”
“Safi sana, ngoja tufike kituoni kwanza,” alisema polisi yule.
Hawakutaka kuendelea kubaki pale, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika kituo chao kwa ajili ya mahojiano zaidi na mzee Gombana ambaye alitakiwa kutaja kila kitu alichokuwa amekiona, likiwemo suala la namba za gari ambalo kwao lilionekana kuwa muhimu.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba ni yeye, anaamua kumuua na mwili kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika, kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kilichoendelea.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Dickson alikuwa na furaha tele kwani alijua huo ndiyo ungekuwa mwanzo wa kuficha siri juu ya kile kilichokuwa kimetokea msituni. Hakutaka ajulikane na mtu yeyote kama yeye ndiye aliyehusika na mauaji ya msichana yule kisha kumzika msituni.
Mzee Gombana alikuwa na furaha tele, kwake kuwa mikononi mwa Dickson kulimpa faraja na kuona alikuwa kwenye mikono iliyo salama. Garini, mzungumzaji mkubwa alikuwa yeye, alimhadithia namna alivyomuona mwanaume huyo akiutoa mwili kutoka garini kisha kuuzika katika shimo alilokuwa amelichimba.
“Kuna watu katili sana aiseee, nilishuhudia kila kitu mkuu, yaani mpaka nikatetemeka,” alisema mzee Gombana
“Ni lazima tuhakikishe anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Dickson huku akiendesha gari.
Bado furaha ilikuwa moyoni mwake, hakuamini kama kazi ingekuwa nyepesi namna ile, alichokuwa akikifikiria kichwani mwake kwa wakati huo ni kumuua mzee Gombana tu ili ile siri iendelee kuwa siri.
Alimshukuru Mungu kwani kile ambacho mzee Gombana alikiona kule msituni, hakutoa ushahidi wa kutosha kuhusiana na lile gari hivyo kuona kwamba hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya kumnyamazisha milele.
Hakutaka kuwa na presha, kwa kuwa tayari alikuwa ameaminika vya kutosha, alichokifanya ni kuelekea ofisini kwake ili huko ndiyo uwe mwanzo wa kufanya kile alichotaka kukifanya. Wakati wakiwa wamefika Manzese Tip Top, Dickson akalipaki gari lake pembeni kisha kuteremka.
Akaanza kuelekea katika duka la dawa ambapo akanunua dawa za mafua, piriton. Akazichukua na kuondoka dukani hapo kurudi garini pasipo kuzungumza chochote, mzee Gombana hakusema kitu, alinyamaza huku kwa kumwangalia alionekana kuwa mtu mwenye furaha tele.
“Samahani! Mafua yananisumbua mno,” alisema Dickson na kuingia garini.
“Pole sana mkuu.”
“Asante.”
Akaingia ndani ya gari na safari kuendelea. Hawakuchukua dakika nyingi wakaingia katika jengo la makao makuu ya polisi ambapo wakateremka na kuanza kuelekea ndani huku kila polisi aliyekutana naye, alipiga saluti kama kumpa heshima.
Walipofika ofisini, akamwambia mzee Gombana akae kitini kwa lengo la kuzungumza naye. Ila kabla ya mazungumzo hayo kuanza, akainuka, akaelekea nje ya ofisi ile ambapo alichukua zile dawa za priton, akazisagasaga kisha kuchukua sumu aina ya phenomenon yenye makali ya kuua hapohapo na kuiweka kwenye kikombe ambacho alitaka kumuwekea kahawa mzee Gombana.
Kwa sababu phenomenon ilikuwa miongoni mwa sumu zilizoua kwa haraka sana mara ziingiapo mwilini mwa binadamu, alichokifanya ni kupunguza makali yake na dawa ya piriton ambayo nayo aliisaga na kuiweka ndani ya kile kikombe kisha kurudi ofisini.
Aliporudi ofisini, akachukua chupa ya kahawa na kuimimina katika vikombe viwili na kumgawia mzee yule kikombe kilichokuwa na kahawa yenye sumu na kuanza kunywa. Dickson akafurahi, kitendo cha mzee yule kunywa kahawa ile kikamuoneshea kwamba alikuwa mshindi juu ya kilichokuwa kimetokea, hivyo alijiona kushinda vita kubwa na nzito iliyokuwa mbele yake.
“Kwenye maisha nimejifunza mengi mno,” alisema Dickson.
“Umejifunza nini mkuu?”
“Unapokuwa kiongozi ni lazima uwe mnyenyekevu pia. Siku kama ya leo huwa sipendi niandaliwe kahawa, ninapenda kuandaa mwenyewe, ninapenda kuwaoneshea watu wengine jinsi kiongozi unavyotakiwa kuwa,” alisema Dickson huku akitoa tabasamu.
“Wewe ni kiongozi bora, jinsi ulivyo, ukarimu wako na matendo yako ni vitu viwili tofauti. Wengine wanakuona una roho mbaya sana, ila tangu nimekutana nawe, hakika umekuwa tofauti na nilivyokuwa nikifikiria,” alisema mzee Gombana.
“Ninapokuwa kazini huwa ninauvaa mwili wa kazini, huwezi kwenda kupambana na majambazi huku uso wako ukiwa na tabasamu pana, unatakiwa kubadilika, uso uwe kwenye muonekano wa kikazi. Ninapofanya vitu kwa ujasiri na kuingia kazini huku nikionekana mwenye hasira, wengi wanafikiri nipo hivyo, ila nipo tofauti,” alisema Dickson huku tabasamu pana likiwepo usoni mwake.
Hawakuzungumza mengi kwani tayari alijua kwamba ile sumu iliyoingia mwilini mwa mzee Gombana ingeweza kufanya kazi muda wowote ule. Alichokifanya ni kumshukuru mzee huyo kwa ushirikiano wake huku akimtaka kwenda na yeye kuendelea na kazi.
Mzee Gombana akasimama kisha kuondoka ofisini hapo huku akiwa ameiacha ile namba ya gari aliloliona msituni ambalo ndilo lilikuwa gari la Dickson aliyekuwa Mkuu wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam. Kwa Dickson, ilikuwa ni furaha tele.
*****
“Vipi tena mbona unaonekana hivyo?” aliuliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mbezi.
“Kuna taarifa mbaya mkuu!” alijibu polisi mmoja.
“Mbona unanitisha! Taarifa ipi?”
“Yule mzee kafariki jana usiku.”
“Mzee yupi?”
“Yule aliyeleta taarifa juu ya lile gari porini. Amekufa baada ya kulalamika maumivu makali ya tumbo.”
“Unasemaje?”
”Ndiyo hivyo mkuu!”
Mkuu wa kituo cha polisi akachanganyikiwa.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba ni yeye, anaamua kumuua na mwili wake kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika, kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kilichoendelea.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Taarifa iliyofika kituoni ilimshtua kila polisi aliyeisikia kwamba shahidi waliyekuwa wakimtegemea kuwaambia juu ya gari lile lililokuwa msituni kufariki dunia ghafla nyumbani kwake.
Mkuu wa kituo hicho hakutaka kubaki ofisini, haikuwa taarifa nzuri hata kidogo kwani viongozi wake walitaka kufahamu kila kitu akiwemo Dickson ambaye alihusika katika kifo cha shahidi huyo, mzee Gombana.
Ofisini hakukukalika tena, alichokifanya ni kuondoka ofisini hapo kuelekea nyumbani kwa marehemu. Hakwenda peke yake, alikuwa na polisi kadhaa ambao wote kwa pamoja walichanganyikiwa kwa kilichokuwa kimetokea.
“Haiwezekani, hapa kuna kitu,” alisema mkuu wa kituo.
“Kweli mtu anaweza kufariki ghafla? Tena kwenye kipindi tunachomuhitaji sana?” aliuliza polisi mmoja huku akimwangalia mkuu wake usoni.
“Haiwezekani, hapa kuna kitu, subiri tufike.”
Japokuwa barabara ilikuwa mbaya lakini dereva hakujali, aliendesha kwa mwendo wa kasi huku wakitaka kufika msibani hapo haraka iwezekanavyo. Kitu cha kwanza walichokuwa wakihitaji ni kuuchunguza mwili wake kwani waliamini hakikuwa kifo cha kawaida, kulikuwa na mtu aliyekuwa amemuua mzee Gombana kwa kutaka kuficha siri juu ya kile kilichokuwa kimetokea kule msituni.
Bado muuaji wa msichana yule na mzee Gombana aliwachanganya, hawakujua ni nani aliyekuwa nyuma ya mauaji yale, walichokuwa wakikifanya ni kuhakikisha muuaji anapatikana haraka iwezekanavyo hata kabla wakuu wao hawajachukua uamuzi mbaya.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika msibani hapo, hata kabla gari halijasimamishwa, kama makomandoo, polisi wale wakaruka, watu wote waliokuwa msibani wakashangaa, hawakujua sababu iliyowafanya polisi hao wafike msibani hapo huku wakiwa na bunduki mikononi, amani iliyokuwepo ikaanza kupotea.
Hawakuzungumza na mtu yeyote yule, walichokifanya ni kuingia ndani na kuonana na wafiwa ambapo wakazungumza nao na kuwaambia kwamba kabla ya mwili kuzikwa ilikuwa ni lazima ufanyiwe uchunguzi ili kuona kama ulijeruhiwa sehemu yoyote au kulikuwa na kitu kingine kilichosababisha kifo chake.
Hawakuwa na jinsi, japokuwa walipanga kufanya mazishi yake siku hiyo ikabidi waahirishe ili polisi wafanye kazi yao. Mpaka siku iliyofuatia, majibu ya uchunguzi yakatolewa na kuonesha kwamba mzee Gombana alikufa baada ya kunywa sumu iitwayo Phenomenon iliyokuwa na nguvu ya kummaliza mtu kwa haraka mno.
“Nani alimnywesha?”
“Hatujui, labda tumuulize mkewe,” alisema polisi mmoja.
Hawakutaka kuchelewa, bado akili zao hazikuwa sawa mpaka pale ambapo wangehakikisha kwamba kila kitu kinajulikana siku hiyo, walichokifanya ni kurudi tena nyumbani ambapo huko wakakutana na mke wa marehemeu na kuanza kuzungumza naye.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kumnunua changudoa wa kwanza na kumgundua, Dickson akamuua na kumzika msituni. Baadaye, kuna mzee alimuona lakini kabla hajatoa ushahidi, akaamua kumuua. Siri imebaki kuwa siri. Baada ya wiki moja na nusu kupita tangu amuue changudoa yule, Dickson amerudi tena kununua mwanamke kwa ajili ya kulala naye usiku kucha.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Dickson alibaki akimwangalia changudoa yule kimahaba, tayari uchu wa kufanya naye mapenzi ulikwishampanda. Vazi alilovaa, sketi fupi ambayo iliishia mapajani mwake ilimuacha hoi, kila alipokuwa akiyaangalia mapaja yake, akili yake ilichanganyikiwa mno.
Kilipita kipindi cha wiki moja na nusu tangu mara ya mwisho kumnunua changudoa ambaye mwisho wa siku aliamua kumuua kutokana na kumuona usoni na kugundua kwamba alikuwa yeye, tangu siku hiyo mpaka siku aliyosimama na msichana huyo, hakuwa amelala na msichana yeyote yule.
“Ingia basi twende,” alisema Dickson.
“Twende wapi?”
“Hotelini.”
“Mimi nataka tutumie hoteli ile pale,” alisema msichana yule huku akiinyooshea kidole Hoteli ya Maradava iliyokuwa pembeni ya eneo hilo.
“Jamaniiiii...”
“Ndiyo! Tena ile ni bei chee”
“Za bei rahisi si nzuri, mimi nataka ile iliyokuwa ya gharama, si unaona hata gari langu linaongea mimi ni mtu wa aina gani,” alisema Dickson huku akijisifia.
Msichana yule alibaki njia panda, ni kweli alikuwa na shida ya kuhitaji hela lakini kwenda mbali na mwanaume kwake lilionekana kuwa tatizo kubwa. Kwa kipindi cha wiki nzima stori za rafiki yao ambaye alikutwa amefukiwa porini ziliwatisha, wasichana wengi waliogopa kutoka na mwanaume yeyote yule kwenda naye hotelini, kwa jinsi alivyokuwa Dickson, msichana yule alijawa na hofu.
“Unajua kuna kitu kilitokea wiki moja na nusu iliyopita ndiyo maana hatutaki kwenda mbali na sehemu hii,” alisema msichana yule huku akionekana kuwa na hofu.
“Kama unaogopa, basi sawa haina noma,” alisema Dickson, akapandisha kioo cha gari, akaliwasha kwa lengo la kuondoka.
Biashara haikuwa ya uhakika sana, mara baada ya mwanamke yule kuona kwamba mteja wake alikuwa siriazi kuondoka mahali hapo, akakipigapiga kioo kisha Dickson kukiteremsha na kuanza kumsikiliza.
Kipindi chote hicho changudoa yule hakujua kama mtu aliyekuwa akizungumza naye alikuwa Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam kutokana na giza lililokuwemo ndani ya gari ambalo halikuruhusu uso wake kuonekana kwa urahisi.
“Subiri kwanza!”
“Nisubiri nini na wakati unaniletea pozi?”
“Naomba unisikilize kwanza!”
“Wewe sema!”
“Niongezee hamsini! Tutalala mpaka asubuhi!”
“Daah! Sawa! Haina noma! Ingia twende!”
Changudoa yule akazunguka upande wa pili. Alipopita mbele ya gari lile na taa kummulika, umbo lake lilionekana vizuri machoni mwa Dickson, alikuwa msichana mrembo aliyeumbika, msichana aliyekuwa na nyonga zilizoweza kumtia matatani mwanaume yeyote yule.
Dickson akameza mate kwa uchu, kila alipomwangalia, jinsi alivyotembea na umbo lake kutingishika vilivyo, alijikuta akipagawa mno. Alipoufikia mlango, akaufungua na kuingia ndani. Dickson akashusha pumzi ndefu.
“Kumbe huwa kunakuwa na wasichana warembo hivi!” alisema Dickson huku akiachia tabasamu.
“Kwani hujawahi kuchukua msichana huku?”
“Ndiyo! Hii ni mara ya kwanza.”
“Wazuri tupo, kama vipi tutabadilishane namba za simu ili tuwe tunashtuana,” alisema msichana yule.
“Hakuna tatizo!”
Dickson hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kutekenya ufunguo kisha kuliondoka gari. Kadiri walivyokuwa wakiendelea kusonga mbele ndivyo uchu wa kufanya mapenzi ulivyozidi kumshika.
Ndani ya gari kulikuwa na mwanga hafifu ambao haukumfanya changudoa yule kumuona Dickson usoni, gari lilizidi kwenda na wala hakuwa na shida ya kumuona kwani kitu alichokuwa akikitaka ni fedha tu na si kitu kingine.
Njiani, Dickson alijipa uchangamfu mkubwa, alitawala mazungumzo kwa kipindi kirefu mno, alihitaji changudoa huyo amzoee ili hata watakapofika chumbani kusiwe na tatizo lolote lile. Hiyo wala haikuwa shida, walizungumza mno kiasi kwamba ilionesha kama walikwishakutana tangu miaka mitatu iliyopita.
Baada ya dakika kumi, gari likaanza kuingia katika nyumba ya wageni ya Chenchebe iliyokuwa Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Alijua kwamba alikuwa na fedha nyingi lakini kwa kuwa alikuwa kamanda wa jeshi la polisi na kujulikana mno, kwenda hotelini aliona ni lazima angejulikana kutokana na umakini uliokuwepo kwenye hoteli nyingi, hivyo alichoamua ni kutumia gesti bubu.
Huko hakukuwa na uchunguzi, pamoja na kofia yake kubwa aliyoivaa, akalipia kisha kuelekea chumbani huku akiwa amekishikilia kiuno cha changudoa huyo. Walipoufikia mlango wa chumba hicho, wakaingia ndani, kama kawaida hakutaka taa iwashwe, mwanga hafifu uliokuwa ukitoka kwenye taa ya nje, uliwatosha mno.
“Huwa sipendi taa kabisa,” alisema Dickson.
“Kumbe wewe kama mimi, sipendi pia,” alijishaua msichana yule maneno yaliyoonekana kuwa uongo ila alitaka kuwa naye pasipo kujua sababu ya mwenzake kutopenda mwanga wa taa. Hapohapo akamshika kiuno na kumvutia kitandani.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea na tabia yake ya kununua machangudoa pasipo watu kufahamu kwamba yeye ndiye aliyekuwa amefanya mauaji ya msichana aliyeuawa siku kadhaa zilizopita.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Mzuka wa kufanya mapenzi ulikwishampanda Dickson, alimchukua changudoa yule na kumvuta kitandani pale, akili yake ilichanganyikiwa, umbo zuri na ngozi nyororo aliyokuwa nayo msichana yule ilizidi kumhamasisha kufanya naye mapenzi mle chumbani.
“Subiri kwanza,” alisema msichana yule.
“Kuna nini?”
“Mbona una haraka?”
“Sasa si tumelipia short time, tufanye fasta,” alisema Dickson, hata sauti aliyoitoa chumbani hapo ilionesha ni jinsi gani alikuwa kwenye mhemko mkubwa wa kufanya mapenzi.
Dickson hakutaka kusikia kitu chochote kile, alichokuwa akikitaka ni kufanya mapenzi tu. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi, damu ilizunguka kwa kasi mno, kilipita kipindi kirefu kufanya mapenzi kabla ya siku hiyo, ule mzuka wa wiki mbili zote alikuwa nao ulimzidi nguvu.
Alimchojoa changudoa nguo zake katika haraka ambayo hata yeye mwenyewe aliishangaa, alipomaliza, akamlaza kitandani. Katika kila kitu alichokuwa akikifanya mahali hapo hakutaka kugundulika kama alikuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kila alipomgeuza huku na kule, alihakikisha kwamba mwanga wa taa iliyokuwa nje haimpigi usoni mwake.
Walitumia muda huo vilivyo, baada ya saa mbili baadaye, kila mmoja alikuwa hoi, Dickson alibaki akimwangalia changudoa yule huku hata hamu ya kuendelea hakuwa nayo kabisa.
“Kiasi gani?”
“Unataka unilipe ipi? Ya mpaka asubuhi au short time?” aliuliza changudoa yule.
“Mpaka asubuhi japokuwa nataka kuondoka.”
“Laki moja na nusu.”
“Hakuna tatizo.”
Dickson akaivuta suruali yake na kutoa pochi yake ambapo akaifungua na kuanza kuhesabu fedha zake. Hakukuwa na hela ndogo, noti zote zilizokuwa ndani ya pochi ile zilikuwa ni elfu kumi tu, hivyo akazihesabu mpaka zilipofika kiasi hicho akamgawia msichana yule.
“Laki moja na nusu hii?” aliuliza msichana yule.
“Ndiyo!”
“Mmmh! Usije ukawa umenipiga changa la macho, ngoja niwashe taa nizihakikishe,” alisema msichana yule huku akisimama kitandani pale. Dickson akamshika mkono.
“Baby...”
“Abee kipenzi!”
“Huniamini?”
“Kwenye suala la fedha, hautakiwi kumuamini mtu, hata shemasi tu anaiba sadaka kanisani” alijibu msichana yule.
“Siwezi kukufanyia mchezo huo, niamini kipenzi. Kwanza hebu andika namba yako hapa,” alisema Dickson, aliamua kuliingizia suala la namba kwani hakutaka changudoa yule aendelee kuweka msisitizo wake juu ya kuwasha taa ile.
Dickson akafanikiwa kumlaghai msichana yule na mwisho wa siku hakuweza kabisa kuwasha taa ile kitu kilichomfurahisha sana Dickson. Mpaka alipoamua kuondoka na kumuachia changudoa yule fedha za kutosha zaidi, wakaahidiana kwamba kuanzia siku hiyo angekuwa mteja wake, yaani kuhusu suala la fedha hakutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.
Kila siku usiku Dickson alipokuwa akifika Sinza Mori, hakutaka kumchukua msichana mwingine zaidi ya huyohuyo aliyejitambulisha kwa jina la Magreth, ila awapo kazini alipenda sana kuitwa Mage.
Uwepo wa Dickson ukawa gumzo mahali hapo, machangudoa wengi wakamfahamu kama mwanaume aliyekuwa akija na gari jeusi, kila walipoliona usiku mahali hapo, walijua fika kwamba alifika mahali hapo kwa ajili ya kumchukua Magreth, hivyo hawakutaka kumuingilia.
Katika kipindi cha wiki mbili, Magreth hakuweza kugundua kwamba yule mtu aliyekuwa akimchukua kila usiku alikuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Siku zikaendelea kukatika, kutokana na fedha alizokuwa akizipata Magreth, akawa changudoa aliyekuwa na maendeleo kuliko yeyote mahali hapo.
“Niitie Magreth...” alisema Dickson, kama kawaida alikuwa amefika Sinza Mori kwa ajili ya kumchukua Magreth na kuondoka naye kama kawaida yake.
“Hajafika!” alijibu msichana mmoja aliyevalia kimini.
“Amekwenda wapi?”
“Hajafika. Anaumwa tumbo!”
“Sawa! Asante.”
“Hutaki huduma?”
“Nataka, ila kama ye....”
“Hata mimi naweza kukupa huduma, tena zaidi ya huyo Mage,” alisema msichana huyo.
“Kweli?”
“Kweli kabisa.”
“Basi ingia twende nikaone,” alisema Dickson.
Kutokuwepo kwa Magreth hakukuwa na tatizo lolote lile, alichokuwa akikitaka mahali hapo ni kufanya mapenzi tu, hakujali chochote kile, akamchukua msichana yule na kuanza kuondoka naye mpaka kwenye gesti bubu ya Chenchebe iliyokuwa maeneo ya Mwananyamala. Walipofika, wakateremka na kuingia ndani pasipo dada wa mapokezi kuhoji sana kwani alikuwa mteja wake ambaye hakuwahi hatakumuona uso, alimzoea mno na hata wakati mwingine aliachiwa kiasi fulani cha fedha.
“Nataka unionyeshee ulichonacho sasa,” alisema Dickson.
“Usijali,” alisema msichana yule, akakifuata kitanda na kuanza kujinyonganyonga maungo yake, alipomaliza akazivua nguo zake na Dickson kumfuata pale kitandani.
“Anza na kifua changu kwanza,” alisema msichana yule, kwa haraka pasipo kuuliza chochote Dickson akafanya kama alivyoambiwa pasipo kujua kwamba huo ulikuwa mtego mkubwa, msichana yule alitaka kumlevya na madawa ya usingizi aliyoyapaka kifuani.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Huko, tabia yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja anapokwend hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni Kamanda Dickson.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Usiku ulikuwa mkubwa, milio ya risasi ilisikika kila sehemu, watu waliokuwa ndani ya nyumba zao, wakafunga milango na madirisha ili kuyaokoa maisha yao. Wale waliokuwa wakipita njia kuelekea kule kulipokuwa na kituo kikubwa cha polisi ambapo milio kadhaa ya risasi ilisikika, wakasimama na kurudi walipotoka, tena wakikimbia kwa mwendo wa kasi.
Polisi walikuwa wakishambuliana na watu waliokisiwa kuwa majambazi. Walifika kituoni hapo kwa malengo mawili tu, kuwaua polisi kisha kuiba silaha kama walivyofanya katika vituo vingine vilivyokuwa katika mikoa mingine.
Polisi hawakukubali, kwa kuwa nao walikuwa na silaha nzito, wakaanza kushambuliana na majambazi hao walioonekana moto wa kuotea mbali katika kutumia silaha hizo na hata ukwepaji wao.
Polisi walidondoka chini, damu ziliwatoka, risasi zilipenya miilini mwao, hakukuwa na aliyemuokoa mwenzake wakati huo, kila mmoja alikuwa bize kutetea nafsi yake, majambazi wale waliendelea kuwamiminia risasi mfululizo.
“Wanakuja…” alisema polisi mmoja, alionekana kuchanganyikiwa mno.
“Wapigie simu makao makuu uwaambie tunahitaji msaada,” alisema polisi mwingine.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, hapohapo akapiga simu, jina la mtu lililomjia kichwani mwake ni Kamanda Dickson, hapohapo akampigia simu, simu ikaanza kuita. Majambazi wale waliokuwa wamevaa kininja waliendelea kuwasogelea polisi wale, eneo zima la kituo hicho likabadilika na kuwa uwanja wa vita. Ni polisi watano ndiyo waliobakia kati ya polisi kumi waliokuwepo kituoni hapo.
* * *
Dickson alikuwa na mhemko mkubwa, alipoambiwa kwamba kifua cha changudoa yule kiliachwa kwa ajili yake, akaanza kukisogelea pasipo kujua kwamba kilikuwa kimepakwa dawa ya usingizi, ili alewe na kukombwa kila kitu.
Wakati akiwa tayari amekikaribia, mara akaanza kusikia simu yake ikiita. Haikuwa kawaida kupigiwa simu usiku, hakuwa na familia, hakuwa na marafiki wa karibu kutokana na ukali wake na hata polisi wake alikwishawaambia kwamba hataki kupigiwa simu usiku mpaka kuwe na kazi kubwa hasa majambazi.
Alihitaji muda wa kupumzika kutokana na kazi ngumu alizokuwa akizifanya kila siku. Kitendo cha kusikia simu yake ikiita, alijua kwamba kulikuwa na tatizo sehemu, hakutaka kuendelea, aliheshimu sana kazi kuliko mapenzi, alichokifanya, huku akionekana kama mtu aliyeshtuka, akaifuata suruali yake na kuichukua simu.
“Nani wewe?” aliuliza kibabe.
“Mkuu! Tumevamiwa hapa Kituo cha Polisi cha Jangwani, tunaomba utusaidie…” ilisikika sauti ya polisi mmoja simuni huku milio ya risasi ikiendelea kusikika mahali hapo.
Hakutaka kuuliza kitu chochote kile, tayari akajua kwamba kulikuwa na majambazi yaliyokuwa yamevamia kituo hicho. Hiyo ndiyo hali iliyokuwa ikiendelea nchini Tanzania, vituo mbalimbali vilivamiwa na polisi kuuawa kisha bunduki kuibwa, alichokifanya ni kuanza kuvaa harakaharaka.
“Nini tena mpenzi?” aliuliza changudoa yule, wakati huo alikuwa akimalizia kuvaa shati lake.
“Chukua hiyo,” alimwambia changudoa yule huku akimtupia noti za shilingi elfu kumi kitandani, ilikuwa elfu sabini.
Hakutaka kuchelewa, akatoka mle chumbani huku akikimbia kiasi kwamba hata dada wa mapokezi alimshangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea chumbani mpaka Dickson kukimbia, alipojaribu kumuita, Dickson hakugeuka, akalifuata gari lake, kitu cha kwanza kabisa akaangalia kama bastola yake ilikuwepo pale alipokuwa akiiweka, akaiona, akawasha gari na kuanza kuelekea huko.
Kutoka Mwananyamala mpaka Jangwani hakukuwa mbali, tena kwa sababu alitumia gari binafsi huku ikiwa ni usiku sana ambapo hakukuwa na magari mengi barabarani, aliendesha kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba baadhi ya watu waliokuwa barabarani walimshangaa.
Alipofika Magomeni, kitu cha kwanza akazima taa za gari lake na kuendelea kusogea kule kulipokuwa na kituo kile. Bado milio ya risasi iliendelea kusikika mahali hapo, alipokaribia zaidi, akasimamisha gari lake kisha kuteremka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kunyata tena kwa kuinamainama huku akisogea kule kulipokuwa na kituo.
Mbele kabisa, aliwaona wanaume watano wakitembea kuelekea kituoni huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Hakutaka kujiuliza mara mbilimbili, akajua wale ndiyo walikuwa majambazi na walikuwa wakikisogelea kituo huku wakipiga risasi, hakukuwa na majibu kutoka kwa polisi hali iliyoonesha walikuwa wameishiwa risasi.
“Paaa…paaa…paaa…” ilisikika milio mingine ya risasi mahali hapo, alifyatua risasi tatu mfululizo, kutokana na shabaha aliyokuwa nayo, hapohapo majambazi watatu wakaanguka chini, damu zikaanza kuwatoka shingoni na vichwani mwao.
Wale wengine wawili wakaonekana kuchanganyikiwa, wenzao walikuwa chini, hawakujua risasi zilitoka upande gani, walichokifanya ni kuanza kurudi nyuma.
Mpaka kufikia hapo, Dickson akaona hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee, alichokifanya ni kuwasogelea kwa mwendo wa kuinama tena kwa kasi. Majambazi wale waliokuwa wamepaki pikipiki zao pembeni, wakazichukua na kuziwasha kwa lengo la kukimbia.
“Paaa…” ulisikika mlio mmoja wa risasi, jambazi mmoja akadondoka chini.
Dickson hakutaka kuchelewa, kwa mwendo wa kasi akamfuata jambazi aliyetaka kutimua mbio na pikipiki, alipomkaribia, kama ndege, akamrukia kwa nyuma, wote wakadondoka chini.
Jambazi akachukua bunduki yake ili amfyatulie risasi Dickson, bunduki haikuwa na risasi, Dickson alipoichukua bunduki yake na kujaribu kumfyatulia risasi jambazi yule, nayo haikuwa na risasi. Wakabaki wakiangaliana, kilichobakia ni kuoneshana kazi kama wanaume, kila mmoja akakunja ngumi. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya kila mmoja kuiokoa nafsi yake.
“Fight like a man,” (Pigana kama mwanaume) Dickson alimwambia jambazi yule.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Huko, tabia yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja alipokwenda hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni Kamanda Dickson. Hata kabla hajafanya mapenzi na changudoa huyo, anapigiwa simu na kuambiwa kituo kimoja cha polisi kimevamiwa.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Walibaki wakiangaliana tu, hali ya ukimya ilikuwa imetawala mahali hapo mara baada ya milio ya risasi kutawala sekunde chache zilizopita. Dickson akabaki akimwangalia jambazi yule kwa umakini mkubwa huku akionekana kuwa na hasira mno.
Tayari alikunja ngumi, kilichofuata ni kumsogelea na kuanza kupigana. Mpaka kufikia hatua ya kuwa DCP wa Kanda ya Dar es Salaam, alifanikiwa kupitia mafunzo mengi, kupambana kwa kutumia risasi au kwa kutumia mikono na miguu.
Hakutaka kuchelewa, mara baada ya kumsogelea jambazi yule ambaye alionekana kutokuwa na mafunzo yoyote ya mapigano, akampiga teke moja zito la mbavu ambalo lilimfanya kupepesuka huku kabla hajaamua nini cha kufanya akapigwa ngumi moja ya shavu ambayo ilimpeleka chini moja kwa moja na kuanza kugaragara kwa maumivu makali.
Haikuwa kazi kubwa, ni ndani ya sekunde thelathini, kila kitu kilikuwa tayari alichokifanya ni kulichukua jambazi lile na kulipeleka kituoni ambapo askari wenzake bado walikuwa wamejificha wakiogopa kupigwa risasi.
“Kamanda..” aliita polisi mmoja aliyekuwa amejificha nyuma ya meza kubwa ya kaunta, alikuwa na wenzake wawili, wakasimama na kuanza kupiga saluti.
“Hebu liwekeni ndani kwanza,” alisema Dickson.
Mara baada ya ukimya mkubwa kutawala hapo ndipo watu waliokuwa ndani ya nyumba zao wakafungua milango na kutoka ndani kuona ni kitu gani kilichokuwa kimetokea. Macho yao yakatua katika miili ya majambazi na polisi iliyokuwa chini huku damu zikionekana kukauka.
Polisi waliokuwa mahali hapo wakaanza kuwazuia raia wasisogee kule ilipokuwa miili ile. Ni ndani ya dakika kadhaa, tayari polisi wengine wakafika kituoni hapo wakaichukua miili ya majambazi wengine na kuondoka nayo.
“Nani kafanya haya yote?” aliuliza raia mmoja, alionekana kutokuamini kilichotokea.
“Nilisikia polisi mmoja akisema ni kamanda Dickson,” alijibu raia mwingine.
“Kamanda Dickson?”
“Ndiyo! Kama kweli ni yeye, huyu mtu kweli hatari, tukipata makamanda watano tu kama yeye, mbona amani itakuwepo,” alidakia raia mwingine.
Siku iliyofuata, vyombo mbalimbali vya habari vikaanza kutangaza kilichotokea katika Kituo cha Polisi cha Jangwani, kila aliyesikia hakuamini, kitendo cha kishujaa alichokifanya kamanda Dickson kiliendelea kuwaonesha watu ni jinsi gani alikuwa shupafu.
Sifa zake ziliendelea kutapakaa kila kona, kila alipoitwa alipongezwa kwa kazi kubwa aliyokuwa ameifanya ambayo kwa namna moja au nyingine ilionesha namna alivyo hatarisha maisha yake kwa ajili ya kuleta heshima katika kazi ngumu ya kipolisi.
Japokuwa alionekana kuwa mwanaume shupavu, mwenye umakini mkubwa awapo kazini lakini bado tatizo lake lilikuwa palepale kwamba alikuwa mtu wa kupenda kununua mno machangudoa barabarani pasipo kujulikana.
Sura yake ikamfanya kukosa mke, hakupendwa na wanawake wengi kwani pamoja na sura yake mbaya bado wengine walimuogopa kutokana na matukio aliyokuwa akiyafanya kila majambazi walipokuwa wakifanya uhalifu sehemu fulani.
* * *
Alikuwa miongoni mwa wanawake wazuri, waliojaliwa kuwa na umbo zuri ambalo watu wanaojua jinsi mwanamke alivyo, wangeliita umbo namba nane. Uzuri wake ulimvutia kila mtu aliyekuwa akimwangalia, alikuwa na sura nyembamba, lipsi nene huku macho yake muda wote yakionekana kuwa mazito kama mtu aliyekuwa na usingizi mzito.
Kwa jina aliitwa Pamela Samsoni, msichana mwenye kimo cha wastani, mweupe na mwenye mwendo wa maringo mithili ya twiga. Katika Mtaa wa Sakina jijini Arusha alipokuwa akiishi, Pamela alikuwa gumzo kila kona, alipendwa na wanaume wengi, kila alipopita, alipokuwa akipigiwa miluzi, kwa kasi ya ajabu kama feni izungukayo, aligeuka na kuangalia mluzi ulipotoka.
Japokuwa alikuwa mzuri mno aliyewatetemesha wanaume wengi lakini hakuuthamini uzuri wake, alikuwa radhi kulala na mwanaume kwa kuwa tu alichokiangalia ni pesa. Alipendwa na watu wenye fedha, hakutaka kujua mwanaume alikuwa mzuri kiasi gani, kitu cha kwanza alichokuwa akitaka kuona ni mifuko na pochi, zilikuwa zimetuna au zilidhoofika.
“Umeumbika vizuri, una sura nzuri, kwa nini usiolewe?” aliuliza mwanaume mmoja, alikuwa akimwangalia Pamela kwa macho ya matamanio.
“Una sura nzuri, kifua kipana, kwa nini usioe?” naye alimrudishia swali mwanaume huyo.
“Mmh! Aya nimeelewa unamaanisha nini.”
Alikubalika mitaani, alipendwa kila kona, si kwa wanaume tu bali hata wanawake waliokuwa wakimwangalia Pamela walisema wazi kwamba alikuwa miongoni mwa wasichana wazuri mno. Mbali na uzuri aliokuwa nao, tabia ya kujiuza kwa wanaume mbalimbali, Pamela alikuwa na udhaifu mmoja tu.
Alipokuwa akimpenda mwanaume, alimpenda haswa, katika mapenzi, alikuwa na hasira za karibu, kumshambulia mtu kwa ajili ya mapenzi ilikuwa moja ya sehemu ya maisha yake. Wanawake wengi walilifahamu hilo, kila mwanaume aliyekuwa akimpata, hakukuwa na mtu aliyemuingilia kwani waliujua fika ukorofi wake, walijua namna ambavyo binti huyo alikuwa radhi kukurushia chupa ilimradi mwisho wa siku ujutie kitendo cha kumchukulia mwanaume wake.
Siku zikaendelea kukatika huku Pamela akiendelea kujiuza kwa mteja mmojammoja lakini baada ya kipindi cha miezi sita, hapo ndipo alipoanza kujiuza karibu na Hoteli ya Chibuchibu iliyokuwa jijini Arusha ambapo hapo alipata wateja wengi.
“Twende Mererani,” alisema rafiki yake mmoja.
“Kufanya nini?”
“Sasa swali gani hilo Pamela? Kwani unaweza kuchimba madini?” aliuliza rafiki yake huyo.
“Kuchimba madini?”
“Sasa umeniuliza kufanya nini kwani hujui kazi yako inayokuweka mjini?’ aliuliza rafiki yake huyo kwa sauti ya chini.
Siku iliyofuata wakaanza safari ya kuelekea Mererani, bado maisha ya kujiuza yalimsumbua, alikuwa radhi kuzunguka sehemu yoyote ile lakini mwisho wa siku aweze kuingiza kiasi kikubwa cha fedha.
Huko alipokuwa akienda na rafiki yake huyo, walikuwa na kazi moja tu, kujiuza kwa wanaume waliokuwa na fedha nyingi baada ya kuuza madini yao. Kwake, hivyo ndivyo maisha yalivyokwenda.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Huko, tabia yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja anapokwenda hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni Kamanda Dickson.
Je, nini kitafuatia?
SONGA NAYO…
Hata kabla Pamela na rafiki yake hawajafika Mererani, tayari watu wenye fedha zao wakapata taarifa juu ya ujio wao, stori iliyokuwa ikienea tena kwa kasi kubwa ni kwamba msichana mrembo, mwenye umbo matata aliyekuwa akikaa katika Mtaa wa Sakina, leo hii alikuwa akiingia Mererani kwa ajili ya kuwasalimia wanaume wa sehemu hiyo.
Waliokuwa na fedha zao, wakaziweka tayari, walikuwa tayari kwa kila kitu, hawakutaka kuona msichana huyo akifika na kuondoka huku wakiwa hawajafanya kitu chochote kile, hivyo wakamsubiria kwa hamu kubwa kama walivyomsubiria mbunge wao.
Ilipofika majira ya saa nane mchana, Pamela akafika hapo Mererani, wanaume walipomuona tu, wakakiri kwamba kweli msichana huyo alikuwa mrembo mno na alistahili kulitingisha Jiji la Arusha.
Watu wenye pesa zao, waliopata mzigo wa maana wakaanza kuwekeana madau wao wenyewe, kwa Pamela, ilikuwa furaha yake, alichokifuata Mererani hakikuwa kitu kingine zaidi ya pesa tu. Alizaliwa akiwa maskini, aliwalaumu sana wazazi wake na hivyo kupambana huku akijiahidi kwamba siku atakapokufa, awe ameweka kiasi kikubwa sana cha fedha katika akaunti yake.
Wanaume wakapangwa kwa zamu, leo Pamela alikuwa akilala na huyu kesho na yule. Hayo yalikuwa maisha yake ya kila siku, hayakuanzia hapo Mererani bali tangu alipokuwa Arusha Mjini alilala na wanaume mbalimbali.
Baada ya kukaa kipindi cha mwezi tena huku akiwa amepata kiasi kikubwa cha fedha, hapo ndipo alipopanga kwenda jijini Dar es Salaam. Hakuwahi kufika katika jiji hilo, alisikia sifa nyingi kwamba lilikuwa jiji zuri, lenye starehe za kila aina, hivyo naye alitaka kwenda huko.
“Ninataka kwenda Dar,” alisema Pamela.
“Kufanya nini?” aliuliza rafiki yake.
“Kufanya hiki ninachokifanya hapa,” alijibu Pamela.
“Mmmh! Shosti, yaani pamoja na kupata fedha hapa bado unataka kwenda Dar?” aliuliza rafiki yake huku akishangaa.
“Ndiyo! Sifuati fedha, ninataka kwenda kupaona, natamani niishi sehemu Ikulu ilipo,” alisema Pamela huku akiachia tabasamu pana.
“Sawa! Utafikia wapi?”
“Hilo nalo ni swali jamani?”
“Ndiyo! Una ndugu?”
“Sina ndugu ila nina pesa,” alijibu Pamela.
Hakutaka kubadilisha mawazo yake, alichokuwa amekifikiria mahali hapo ilikuwa ni lazima kwenda jijini Dar es Salaam, alitaka kufanya matanuzi, alitaka kuwa katika jiji lililosifika kwa starehe na kuwa na wanaume wengi waliojua kuhonga.
Katika wiki ya mwisho kukaa Mererani, aliamua kukusanya fedha nyingi mno, kila mwanaume aliyelala naye katika siku hizo, alimlipa kiasi kikubwa cha fedha na baada ya siku kadhaa, alikuwa ndani ya ndege akielekea jijini Dar.
Hakuwahi kufika huko, hakuijua mitaa ya huko zaidi ya kuisikia tu. Hakuwa na presha, aliamini katika pesa kwamba unapokuwa nazo kila kitu kitakwenda sawa. Baada ya saa kadhaa, ndege hiyo ikaanza kushuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akateremka, hakuamini kama mwisho wa siku miguu yake ingekanyaga ardhi ya Jiji la Dar, akaanza kupiga hatua na abiria wengine kuelekea katika jengo la uwanja huo kwa ajili ya kuchukua mabegi yake, kila alipokuwa akitembea, hakuamini kama alikuwa jijini Dar.
*****
Kama kawaida yake, Dickson alikuwa amesimamisha gari lake pembezoni mwa baa maarufu ya Caspinho iliyokuwa Sinza Mori jijini Dar. Macho yake hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule, alionekana kuwa bize kumtafuta msichana fulani.
Wanawake wengi walijipanga barabarani, kila mwanaume aliyekuwa akipita karibu na eneo walilosimama, walimfuata na kumwambia kiasi walichokuwa wakijiuza, ili kama mnunuzi asimame na kununua na kama si mnunuzi basi aendelee na safari yake.
Machangudoa wengi walioliona gari la Dickson, hawakutaka kulisogelea, walizoea kuliona mahali hapo, mara kwa mara alikuwa akifika na kumchukua changudoa mmoja ambaye kwa siku mbili tatu hakuwepo, changudoa huyo alikuwa Magreth.
Aliendelea kuangalia huku na kule, mara kwa mbali akamuona msichana mmoja akimfuata, akamwangalia vizuri, hakuwa mgeni, alikuwa Magreth ambaye alikuwa akitembea kwa kasi kumfuata kule aliposimamisha gari lake, alipofika, akaufungua mlango na kuingia ndani.
“Nimekumisi mpenzi,” alisema Magreth kwa sauti ndogo, garini kulikuwa na mwanga hafifu mno, hakuweza kumuona vizuri Dickson.
“Nimekumisi pia, upo tayari?” aliuliza Dickson.
“Ndiyo! Ushindwe wewe tu,” alisema Magreth, hapohapo akawasha gari na kuondoka.
Njiani walizungumza mengi, walizoeana na kuwa marafiki wa damu, Dickson alikuwa na maswali mengi mno, yote hayo alitaka kufahamu mahali alipokuwa Magreth kipindi cha nyuma kwani alifika mahali hapo mara ka mara lakini hakuwa akimkuta.
“Niliumwa sana, ila kwa sasa nipo fiti,” alisema Magreth.
“Hahaha! Usije ukanifia kitandani.”
“Usijali kipenzi,” alisema Magreth, muda wote huo alikuwa akiongea kwa sauti ya kimahaba.
Walipofika katika gesti ya Chenchebe iliyokuwa Mwananyamala A, wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Dickson akalipia na kuingia ndani huku akiwa amemshikilia kiuno Magreth, tena kofia ikiwa kichwani mwake.
Walipoingia chumbani, hata kabla ya kufanya kitu chochote, Dickson akachukua taulo na kuelekea bafuni kuoga. Alitaka kujiandaa hata kabla ya kufanya kile kilichompeleka ndani ya gesti ile.
Wakati anatoka, huku akiwa amejisahau, tena taa ikiwaka, macho yake yakatua usoni mwa mhudumu wa kike wa gesti ile aliyekuwa akielekea chooni. Macho ya mhudumu yule yalipotua usoni mwa Dickson, akaonesha mshtuko mkubwa, akakumbuka kwamba hata kofia yake aliisahau bafuni.
“Mungu wangu! Kamanda Dickson..!!” alisema mhudumu yule huku akionesha mshtuko wa waziwazi. Dickson akachanganyikiwa, akajikuta akirudi bafuni haraka kuchukua kofia yake na kuanza kumtafuta yule mhudumu.
Licha ya kumtafuta mapokezi na nje ya gesti hiyo, hakuweza kumuona yule mhudumu, akaanza kuiona aibu ikianza kumsogelea. Akapagawa!!
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea na tabia yake ya kununua machangudoa na kwenda nao gesti. Siku moja akiwa huko na changudoa aliyeitwa Magreth, ghafla mhudumu wa gesti hiyo anamuona na kugundua kwamba alikuwa DCP Dickson, anashtuka mno na kuanza kukimbia.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
“Samahani kaka!”
“Bila samahani!”
“Nataka nifike kwenye hoteli moja ya kawaida.”
“Poa! Panda twende! Unataka ya chumba kiasi gani kwa siku?”
“Hata elfu thelathini!”
“Umefika! Ingia!”
“Ipo wapi?”
“Kinondoni, kuna hoteli nzuri tu, usijali.”
Pamela alikuwa akizungumza na dereva ambaye alikuwa nje ya teksi yake iliyokuwa imepaki nje ya jengo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Macho yake yaliangalia huku na kule, hakuamini kama pale alipokuwa kwa kipindi hicho alikuwa jijini Dar es Salaam.
Alilisikia tu jiji hilo alipokuwa Arusha, aliambiwa kwamba lilikuwa jiji la raha lenye wanaume wengi waliojua kuhonga huku kukiwa na starehe za kila aina na ndiyo maana katika kipindi hicho aliamua kufika jijini humo ili kushuhudia kile alichokuwa amekisikia.
Gari likaanza safari, katika njia nzima, Pamela alikuwa akiangalia huku na kule, kulikuwa na idadi kubwa ya watu. Alihitaji kulizoea jiji kwani aliamini kwamba humo ndimo yangekuwa maisha yake yote katika miaka yote.
Walichukua dakika arobaini na tano ndipo wakaingia katika Hoteli ya Swing iliyokuwa Kinondoni B. Mlango ukafunguliwa na Pamela kuteremka, akamlipa dereva kiasi cha fedha alichokuwa akikihitaji kisha kuelekea mapokezi.
Hakuwa mshamba wa hoteli, aliwahi kukaa katika hoteli nyingi, zenye gharama kubwa na kulala chumba chochote alichokihitaji, kuwa ndani ya hoteli hiyo kwake lilionekana kuwa suala la kawaida. Macho yake hayakutulia, bado alikuwa akiangalia huku na kule, alitamani kuyazoea mazingira kwa haraka sana ili pale atakapoanza kufanya kazi basi asiweze kupata shida yoyote ile.
Alipopewa chumba na kuelekea chumbani, akalala kitandani, mawazo yakamsonga, akili ikachemka. Alikuwa ndani ya jiji jingine, alikuwa mgeni, hakumfahamu mtu yeyote yule, kwake, kila kitu kilikuwa kigeni. Hakujua ni wapi angeanzia kufanya biashara yake ya kuuza mwili, hakujua viwanja, kiwanja pekee alichokuwa amekisikia ni kile kilichoitwa Kinondoni Makaburini ambacho hakujua kilikuwa mahali gani.
Usiku hakutaka kukaa ndani, akatoka nje ili kuona ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea. Nje ya hoteli ile aliwaona wasichana wengi wakiwa wamesimama pembezoni, walivalia nguo fupi na kuyaacha mapaja yao wazi kabisa huku wengine wakiwa wameshika sigara.
Hakutaka kujiuliza hao walikuwa akina nani, kitu kilichomjia kichwani ni kwamba wanawake wale aliokuwa amewaona walikuwa machangudoa kama alivyokuwa.
“Kumbe hapa napo kuna biashara, nitaanza kufanya,” alisema Pamela.
Kitu alichokifanya hata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo ni kumtafuta msichana ambaye aliamini kwamba kupitia yeye angeweza kumwambia mambo mengi ili hata siku atakapoanza kufanya biashara hiyo asiweze kupata usumbufu wowote.
“Wapi kupo poa tu, kodi yako ndiyo inahitajika,” alisema msichana huyo.
“Hiyo kodi inalipwa wapi?”
“Paleee…kwenye ile kaunta. Kama mnunuaji atakuwa bahili, utawaambia wenye Bajaj, wote watu wetu, unaweza kumalizia shida zako humo,” alisema changudoa huyo, maneno hayo yakamwingia akilini Pamela.
*****
Hakukuwa na siku ambayo Dickson alichanganyikiwa kama siku hiyo, msichana wa mapokezi ambaye alimuona uso wake na kumgundua hakuwepo, alikimbia na kwenda kusipojulikana. Dickson akarudi chumbani kwake, alionekana kuwa na haraka mno, kijasho chembamba kikaanza kumtoka japokuwa alitoka kuoga.
“Vipi tena?”
“Unasemaje?” aliuliza, hata hakumsikia vizuri Magreth, tayari alianza kuvaa nguo zake haraka.
“Mbona unavaa nguo?”
“Nimepigiwa simu nimefiwa!”
“Umefiwa? Hiyo simu umepigiwa wapi na wakati ilikuwa kwenye nguo yako?” aliuliza Magreth.
“Subiri kwanza. Ni lazima niondoke.”
Uondoke tena?”
“Ndiyo!”
Hakutaka kuzungumza sana, kichwa chake kilichanganyikiwa, kitendo cha msichana yule wa mapokezi kuondoka na kuelekea asipopafahamu kilionekana kuwa tatizo kubwa kwa upande wake, hakutaka kubaki ndani ya chumba kile.
Alichokifanya ni kumpatia Magreth kiasi cha shili laki moja kisha kutoka mle chumbani kwa kasi.
Alipofika mapokezi, msichana yule hakuwepo, alichanganyikiwa zaidi, hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kuelekea nje. Alijua kwamba msichana yule hakuwa mtu wa kukaa mbali na gesti ile, alikuwa na uhakika alikuwa akiishi karibu na maeneo hayo.
Huku akiwa na kofia yake kichwani, akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika upande waliokuwepo wanaume fulani waliokuwa wamekaa wakipiga stori kwenye banda la muuza chipsi. Alipowafikia, akawasalimia na kuanza kuzungumza nao.
“Kuna dada namuulizia,” alisema Dickson huku akiwaangalia wanaume hao, hawakuwa wakimtambua kutokana na giza pamoja na ile kofia kubwa aliyokuwa ameivaa.
“Dada yupi?”
“Yule anayehudumia kwenye ile gesti! Mnamfahamu?”
“Nani? Fatuma?”
“Sijui, ni mweupe, mrefu kidogo ana kidoti hapa karibu na pua.”
“Ni Fatuma huyo! Anaishi nyumba ile pale.”
“Ipi?”
“Ile inayowaka taa nyekundu yenye bustani ya maua kwa nje,” alisema kijana mmoja.
“Asante sana.”
“Kwani kuna nini braza? Tumemuona ametoka huku akikimbia!”
“Hakuna kitu, asanteni,” alisema Dickson na kuanza kupiga hatua kuelekea kule ilipokuwa nyumba ile. Hakuonekana kuwa na masihara, alichokuwa amekipanga, ilikuwa ni lazima Fatuma afe.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa na kuwa DCP Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Dickson anaendelea na utaratibu wake wa kununua machangudoa mitaani. Akiwa kwenye harakati hizo anakutana na changudoa mmoja aitwaye Magreth, wanakuwa marafiki na kila anapofika pa kununulia machangudoa, anamtafuta Magreth kwani ndiye aliyemzoea.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Dickson aliendelea kuisogelea nyumba ile, alichokuwa akikitaka ni kumuona Fatuma tu, yule msichana wa mapokezi kwani alihisi kama angemuacha ilikuwa ni lazima kutoa siri kwamba alikwenda katika gesti ile usiku akiwa na mwanamke kitu ambacho kwake alikiona kuwa aibu kubwa.
Mishipa ya shingo ilimsimama, mzunguko wake wa damu ukazidi kuongezeka mwilini mwake, alikuwa na hasira iliyochanganyikana na hofu kubwa kwa kuhisi kwamba ilikuwa ni lazima kwa mtu kama Fatuma kuwaambia watu kile alichokiona mle ndani.
Alipoifikia nyumba ile, hakutaka kupiga hodi, kwanza akatulia na kusikiliza ndani kama kulikuwa na sauti za watu waliokuwa wakiongea, aliposikiliza kwa kutegesha sikio lake, ukimya mkubwa ulitawala.Alichokifanya ni kuanza kuusogelea mlango wa kuingilia ndani, alitaka kuufungua na kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba vingi vya kupanga. Alijaribu kuusukuma mlango, haukufunguka.
“Ngoja...” alijisemea, alichokifanya baada ya hapo ni kuanza kupiga hodi. Alitaka kufunguliwa mlango, aingie ndani kisha kutekeleza kile alichotaka kukifanya mahali hapo. Haukuchukua muda mrefu, mlango ukafunguliwa, mwanaume mwenye kipensi akatoka ndani.
“Karibu,” alisema kijana yule huku macho yake yakiwa mazito kwa usingizi.
“Fatuma yupo?” aliuliza Dickson hata kabla ya salamu.“Fatuma! Sasa hivi? Mmmh! Sidhani! Hebu subiri,” alisema kijana yule, akarudi ndani.
Dickson hakutaka kubaki pale mlangoni, akaanza kumfuata kijana yule kwani alijua dhahiri kwamba endapo msichana huyo angejua kwamba kulikuwa na mtu aliyekuja kumuulizia, ni lazima angesema hayupo, ili kumkamata kirahisi, naye akaanza kumfuata kijana yule ambaye aliishia katika mlango wa chumba kimoja na kuanza kuugonga huku akiliita jina la Fatuma.
“Hayupo kaka! Kwanza huwa harudi muda huu,” alisema kijana yule.
“Huwa anarudi muda gani?”
“Mpaka asubuhi! Analala hukohuko kazini kwake.”
“Ila kuna vijana wameniambia amekuja huku!”
“Mmhh! Sidhani! Au amekwenda kwa bwana wake, kwa sababu huko ndipo huwa anakwenda,” alisema kijana yule.
“Anaishi wapi?”
“Nani? Huyo bwana wake?”
“Ndiyo!”
“Hapo mbele, kuna nyumba fulani hivi kalikali, ila kuwa makini, kuna wavuta bangi wengi wasije wakakutoa roho,” alisema kijana yule kama kumtahadharisha.
“Usijali.”
Kila kitu alikifanya harakaharaka, hakutaka kupoteza muda, kwa kuwa alikwishaambiwa juu ya nyumba ambayo ilisemekana kuwepo kwa Fatuma, akaanza kwenda huko.Hakutaka kusikia kitu chochote kile, kile alichokitaka ni kumuua msichana huyo tu. Aliifikiria nchi ya Tanzania, akawafikiria watu wake, akaifikiria heshima aliyojijengea na kukumbuka siku alizokuwa akiongea kwa msisitizo kwamba machangudoa wote wakamatwe kwani hakupendezwa na uwepo wao, kweli walikamatwa, sasa leo hii, yeye mwenyewe alionwa gesti akiwa na changudoa, alijaribu kuiifikiria aibu yake, ilikuwa kubwa mno.
Nyumba ile haikuwa mbali sana na alipotoka, baada ya dakika mbili, akafika na kulifuata geti. Pua yake ikaanza kunusa harufu kali ya bangi iliyotoka ndani ya nyumba hiyo, hapo akajua kwamba hiyo ndiyo nyumba aliyokuwemo msichana Fatuma hivyo hakutakiwa kugonga, alitaka kuingia moja kwa moja ndani.
Ndivyo alivyofanya, geti lilifungwa ila kwake haikuonekana kuwa tatizo, akauparamia ukuta na kurukia ndani, akaanza kupiga hatua kuelekea kulipokuwa na chumba ambacho kwa nje kilikuwa na viatu vingi. Hata kabla hajaingia, akaanza kusikiliza ndani kulikuwa na watu wangapi, alizisikia sauti ambazo zilimpa uhakika kwamba watu waliokuwamo mle ndani hawakuzidi watatu.
Akakishika kitasa, akajaribu kuufungua mlango, ukafunguka, hapohapo akaanza kuingia ndani kwa mwendo wa kunyata. Taa ilikuwa inawaka, alipoingia tu, macho yake yakatua kwa vijana watatu waliokuwa wamekaa kitandani, walikuwa wakivuta bangi huku pembeni yao kukiwa na karatasi iliyokuwa na madawa ya kulevya.
“Oyaa! Mbona unaingia bila hodi mwana?’ aliuliza jamaa mmoja, kila mmoja alikuwa amelewa kutokana na kubwia madawa yale na kuvuta bangi kwa kiasi kikubwa.
“Fatuma yupo wapi?”
“Nani? Fatuma! Wewe nani mpaka umuulizie demu wangu?” aliuliza kijana mmoja kwa sauti yake ya kilevi.
Hakuwa na muda wa kupoteza mahali hapo, kuulizwa maswali yasiyokuwa na msingi, maswali aliyojua kabisa kwamba yaliulizwa na mtu aliyefahamu fika alizungumzia nini, akajikuta zile hasira alizokuwa nazo zikiongezeka zaidi.
Akakunja ngumi na kuwasogelea vijana wale kitandani pale kisha kuanza kuwapiga ngumi mfululizo. Alikuwa na nguvu, alipitia mafunzo makali hivyo kuwapiga vijana hao watatu halikuwa tatizo kabisa, aliwashushia ngumi mfululizo.
“Fatuma yupo wapi?’ aliuliza huku akiwa amekasirika mno.
“Yupo bafuni anaoga,” alijibu kijana mmoja, uso wake ulikuwa umejaa damu.
Alichokifanya Dickson ni kuchukua ufunguo wa chumba hicho, akatoka ndani kisha kuufunguka mlango kwa nje na kuelekea bafuni. Akaanza kupiga hatua kulifuata bafu ambapo kulisikika sauti ya maji yaliyokuwa yakimwagika,
kaufuata mlango, hakutaka kupiga hodi, akaupiga teke, ukavunjika, naye akaingia ndani. Macho yake yakagongana na macho ya Fatuma aliyekuwa akioga.
“Naomba unisamehe...sitomwambia mtu,” alisema Fatuma mara baada ya kugundua kwamba yule aliyeingia bafuni alikuwa kamanda Dickson.
“Hakuna siri ya watu wawili, ili siri itunzwe, lazima mmoja afe,” alisema Dickson, hapohapo akamsogelea Fatuma na kuanza kumkaba. Japokuwa msichana huyo alianza kukukuruka lakini Dickson hakuitoa mikono yake shingoni mwa Fatuma, alimkaba vilivyo, alitaka kumuua tu.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinunua machangudoa kwa kuwa tu hakuwa na sura nzuri ya kumpata mwanamke. Kila anapokwenda kuwanunua, kofia kubwa inakuwa kichwani mwake huku akimzuia msichana yeyote kumfahamu alikuwa nani na kila aliyebahatika kumuona na kumgundua, ilikuwa ni lazima auwawe.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Pamela hakuishi sana hotelini akafanikiwa kupata chumba katika nyumba moja ambayo haikuwa mbali na eneo la Makaburini hapohapo Kinondoni. Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na wanawake wanne ambao wote hao walikuwa na kazi ya kuuza miili yao nyakati za usiku katika eneo la Majaburini.
Wakajikuta wakianza kuwa karibu naye, Pamela alionekana kuwa msichana mrembo, mwenye sura nzuri na umbo matata ambalo hata machangudoa hao walipomwangalia, walibaki wakimsifia tu.
Kuishi ndani ya nyumba moja, wakajikuta wakianza kuwa marafiki, uchangamfu wa Pamela ulimvutia kila mmoja, wakajikuta wakimuuliza maswali mengi mpaka pale walipogundua kwamba mawazo yao yalikuwa sahihi kwamba msichana huyo alitaka kuwa changudoa na kufanya kazi pamoja nao.
“Kwa hiyo umekuja kwa ajili ya kazi hii?” aliuliza msichana mmoja, aliitwa Juliana.
“Ndiyo! Ila kule hotelini wameniambia nilipie,” alijibu Pamela.“Achana nao, wamekaa kitamaa na hakuna wateja wengi, kama vipi njoo kambini kwetu,” alisema Juliana.
“Wapi?”
“Makaburini.”
“Hakuna tatizo, ninashukuru, kesho tutakuwa pamoja.”
Alifika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kazi hiyo tu, alitaka kuwa na fedha nyingi, alitaka kuwa tajiri, ajijengee heshima kubwa nchini Tanzania. Hakukuwa na kitu alichokitegemea kwa wakati huo zaidi ya kujiuza tu.
Siku ya kwanza kufika katika eneo la Makaburini, Pamela alikuwa gumzo, kila changudoa aliyemuona alishtuka, umbo lake liliwaacha midomo wazi, miguu minene, ngozi yake yenye kung’ara na sura ya kitoto iliwafanya machangudoa wote kumkubali na kumuonea wivu.
Kuanzia siku hiyo, hapo ndiyo ilikuwa ofisi yake, kila siku usiku alifika hapo na kujiuza kama walivyofanya wengine. Wale wateja wazoefu waliojiwekea mazoea ya kufika makaburini hapo kununua machangudoa walipomuona Pamela walichanganyikiwa, hawakuamini kama katika eneo hilo kungekuwa na msichana mrembo kama Pamela, umbo na mvuto wake walizoea kuwaona wasichana wa namna hiyo katika klabu kubwa jijini Dar au hata kwenye makasino mbalimbali.
“Mmmh! Wewe ni mgeni?” aliuliza mwanaume mmoja, alikuwa mtu wa miraba minne, kichwani alinyoa upara, pembeni alipaki gari lake la kifahari, kwa kumwangalia, alionekana kuyazoea mazingira ya eneo hilo.
“Siyo sana, wiki yangu ya pili hii.”
“Ooh! Kumbe, basi nilikuwa napitwa sana. Mbona sikuwa nikikuona?”
“Mara nyingi huwa natoka na wateja.”
“Sawa, hakuna tatizo. Gharama yako iko vipi?”
“Showtime au kuamsha popo?”
“Kuamsha popo, mpaka asubuhi.”
“Elfu hamsini.”
“Hakuna tatizo.”
Mara baada ya kukubaliana, wakalifuata gari na kuingia ndani kisha kuondoka. Machangudoa wengine walionekana kumchukia Pamela, tangu kufika kwake ndani ya eneo hilo, biashara ikawa ngumu, wateja wengi waliofika mahali hapo, mtu waliyekuwa wakimtaka alikuwa Pamela tu.
Safari iliendelea mpaka walipofika Upanga ambapo gari hilo likasimama nje ya nyumba moja ya kifahari iliyozungushiwa ukuta. Mzee yule akapiga honi, hapohapo mlinzi akafungua geti na kuanza kuliingiza gari ndani. Pamela akabaki akiishangaa nyumba hiyo, ilikuwa ni ya kifahari sana, ilionesha ni jinsi gani mzee huyo alivyokuwa na fedha.
* * * * *
Hakukuwa na kitu kingine alichokuwa akikitaka zaidi ya kumuua Fatuma. Hakutaka kuamini kama kulikuwa na siri ya watu wawili duniani, alikuwa na uwezo wa kumuacha Fatuma lakini kwa jinsi alivyomuona msichana huyo, hakuwa na moyo wa kutunza siri ile.
Hakutaka kujulikana, hakutaka kupata aibu baada ya kugundulika kwamba hata yeye ambaye kila siku alikuwa mkemeaji mzuri wa uwepo wa machangudoa naye alikuwa mmoja wa wanunuzi waliofika katika viwanja vya machangudoa.
Alimkaba vilivyo, Fatuma alikukuruka huku na kule lakini mkono wa Dickson haukutoka shingoni mwake, aliendelea kumkaba vilivyo. Wala hazikuchukua dakika nyingi, Pamela akaanza kulegea, mapovu yaliyochanganyikana na damu yakaanza kutoka mdomoni mwake, mishipa ikamtoka na hapohapo pumzi ikakata na kufariki dunia.
Alichokifanya Dickson ni kuanza kuufuta mwili ule kwa taulo la Fatuma kwa ajili kuficha alama za vidole vyake, alipomaliza akatoka mle bafuni na kuondoka zake huku akiwa na uhakika kwamba kile kilichokuwa kimetokea kingeendelea kuwa siri milele.
*****
“Mnasemaje?”
“Kuna mwanaume aliingia ndani jana usiku.”
“Mwanaume gani?”
“Mfupi kiasi fulani, alikuwa na mwili uliojazia.”
“Unaweza kumfahamu hata ukimuona?”
“Hapana! Alivalia kofia kubwa ya Marlboro, sikuweza kumuona vizuri.”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu tena.”
“Na kwa nini alimuua Pamela?”
“Sijui mkuu.”
“Sawa. Mpelekeni sero, tutamhitaji tena. Mleteni mwingine.”
Vijana wale waliokuwa wakivuta bangi na madawa ya kulevya katika nyumba aliyouawa Fatuma walifikishwa kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa ushahidi juu ya mauaji yaliyokuwa yametokea usiku waliokuwa ndani ya nyumba ile.
Kila aliyeulizwa, majibu yake yalikuwa yaleyale kwamba hawakuweza kumfahamu muuaji kwa sababu kichwani alikuwa na kofia kubwa hivyo uso wake kutokuonekana vizuri. Polisi wakachanganyikiwa, mauaji yale yaliwachanganya mno.
Mwili ulipelekwa katika chumba cha uchunguzi hospitalini kwa ajili ya kumbaini muuaji kwa njia ya kuangalia alama za vidole mwilini mwake lakini majibu yaliyotoka yalionesha mwili ulioshwa na kufutwa, hivyo alama za vidole hazikuonekana kitu kilichowafanya polisi kugundua kwamba mtu aliyefanya mauaji alifahamu mengi, hasa yote walivyokuwa wakifanya wapelelezi. Kukaonekana kuwa na ugumu wa kumpata muuaji huyo. Hawakujua kama kiongozi wao ndiye aliyehusika kwa kila kitu.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea kununua machangudoa sehemu mbalimbali na kila changudoa anayegundua kwamba ni yeye, anamuua. Sasa hivi amekutana na changudoa aitwaye Magreth, wametokea kuzoeana mno. Mbali na Dickson, upande wa pili kuna changudoa aliyetoka Arusha, anaitwa Pamela, anasafiri kwenda Dar kwa ajili ya kufanya biashara zake.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
“Unasemaje?” aliuliza kamanda Dickson huku akijifanya kushtuka.
“Kuna mwanamke aliuawa jana, taarifa hizo zililetwa saa kumi na mbili asubuhi,” alisema polisi aliyepeleka taarifa.
“Wapi?”
“Mwanayamala.”
“Na muuaji mmemkamata?”
“Hapana. Ila anaonekana kufahamu mambo mengi hasa yanayohusu uchunguzi katika mwili wa marehemu. Tulijaribu kuchunguza ili tupate hata alama za vidole, hatukuambulia kitu,” alisema polisi huyo.
“Kwa hiyo baada ya hapo mkaamua tu mrudi ofisini, mkalie viti, mkunje nne na mgongesheane glasi?” aliuliza Dickson.
“Hapana mkuu.”
“Kumbe?”
“Bado tunalishughulia suala hilo, nakuahidi baada ya wiki moja tutakuwa na majibu,” alisema polisi huyo.
“Sawa. Nenda.”
Polisi yule alipotoka ndani ya ofisi yake, Dickson akashusha pumzi ndefu, akakenua meno kwa furaha. Moyo wake ukafarijika baada ya kuona kwamba alifanya mauaji na mpaka kipindi hicho polisi bado waliendelea kumtafuta muuaji.
Hakuacha kwenda kununua machangudoa usiku, kila baada ya siku tatu ilikuwa ni lazima kwenda huko na mtu ambaye alimchukua alikuwa Magreth. Kwake alikuwa msichana mrembo lakini kitendo cha kumchukua mara kwa mara kikamchosha, akahitaji kuwa na wanawake wengine.
Kumwambia Magreth lilikuwa jambo gumu, alimzoea na hakujua ni kwa namna gani angeweza kumwambia ili amchukue changudoa mwingine. Baada ya kuona ameshindwa kabisa, hapo ndipo alipoamua kufanya maamuzi yaliyoonekana kuwa magumu kwake.
Siku hiyo alipofika katika eneo la kununua machangudoa, kama kawaida yake alilisimamisha gari lake mbali kabisa, akashusha kioo cha dirisha kisha kuchungulia nje. Machangudoa walipoliona gari hilo, wakaanza kujipitisha mbele yake huku wakiinadi miili yao, wengine walivaa suruali za jeans na wengine sketi fupi. Dickson akatoa ishara ya kumuita changudoa mmoja, mwenye umbo namba nane huku akiwa amezibana nywele zake kwa nyuma.
“Niambie baby,” alisema msichana yule mara baada ya kulifikia gari lile.
“Umependeza sana, nahisi nitakuwa mtu mwenye bahati sana kama nitapata huduma yako leo,” alisema Dickson, kama kawaida kofia ya Marlboro ilikuwa kichwani mwake, mwanga hafifu uliokuwa ndani ya gari ulimfanya kutokuonekana vizuri.
“Hakuna tatizo. Laki mbili mpaka asubuhi.”
“Mmmh!”
“Nini tena?”
“Mbona gharama?”
“Wewe unanionaje? Unalionaje hili umbo? Hili ni umbo la kulipia vijisenti hivyo kweli baby wa mie?” aliuliza changudoa yule, ikambidi Dickson amwangalie vizuri, alikuwa msichana mwenye umbo la kuvutia mno.
“Ingia twende,” alisema Dickson, msichana yule akaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea katika nyumba ya wageni ikaanza.
* * *
Gari likaingizwa ndani, Pamela akabaki akiliangalia jumba lile la kifahari, hakuamini kwamba kungekuwa na mtu ambaye alimiliki jumba kubwa kama hilo tena ndani ya nchi kama Tanzania, nchi iliyokuwa na wananchi wengi maskini.
Wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Muda wote mzee yule aliyemnunua alionekana na furaha tele, kila alipokuwa akimwangalia Pamela, alijiona kuwa miongoni mwa watu ambao wangefaidi usiku wa siku hiyo.
“Twende tukaoge kwanza,” alisema mzee huyo, hivyo wakavua nguo zao na kuingia bafuni.
Muda wote huo mzee yule alibaki akimwangalia Pamela kwa macho ya matamanio, hakuamini kama kweli amekutana na mwanamke aliyekuwa na umbo zuri kama alivyokuwa Pamela. Wasichana wa aina hiyo hawakuwa wakipatikana kirahisi katika eneo kama Kinondoni Makaburini, wengi wao walipatikana katika makasino makubwa, tena wakilipwa kwa dola kuanzia mia moja kwenda juu.
Walipomaliza, wakatoka bafuni na kuelekea chumbani, huko, mzee yule aliyeonekana kuwa na uchu mkubwa alibaki akimwangalia Pamela, hakutaka kusikia kitu chochote kile, aliituliza akili yake ipasavyo na hata simu yake aliizima, hakutaka kupata usumbufu wowote.
Baada ya kuvua nguo zote, wakapanda kitandani, Pamela aligundua kwamba mzee yule alikuwa tajiri hivyo alipania kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha anamteka kimapenzi. Alijiandaa vilivyo mahali hapo lakini hata kabla hajafanya lolote lile, mzee yule akaanza kujishika koo yake na kuanza kukukuruka kitandani pale kama mtu aliyehitaji msaada hali iliyomfanya Pamela kushtuka.
“Nini tena?” aliuliza Pamela, mzee yule alibaki akijikunjakunja huku mikono yake ikiwa mdomoni.
“Give me Fluticasone,” (Nipe Fluticasane)
“What is that?” (Ni nini hicho?)
“I am dying, give me Fluticasone,” (Ninakufa, nipe Fluticasane) alisema mzee yule huku akionesha kidole chake katika droo ndogo iliyokuwa pembeni mwa kitanda.
Mpaka kufikia hatua hiyo Pamela alikuwa amechanganyikiwa, hakujua mzee huyo alikuwa akiumwa ugonjwa gani na hiyo Fluticasane kilikuwa kitu gani. Kwa kuwa yule mzee alionesha kidole katika droo ile ndogo, akaifungua na kuanza kuangalia ndani.
Alikutana na vitu vingi, kulikuwa na dola zaidi ya elfu tano, kamera, bastola, picha na vitu vingine vingi. Hakujua atoe kipi na aache kipi, alibaki akishangaa tu.
“Fluticasone ndiyo nini?” aliuliza Pamela lakini hata kabla hajajua nini cha kuchukua ndani ya droo ile, mzee yule akatulia kitandani, pumzi ikakata, akafariki dunia, Pamela akapata mshtuko.
Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akapandishwa vyeo na mwisho wa siku akajikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.
Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.
Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.
Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.
SONGA NAYO.
Pamela aliogopa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya mahali pale, dawa ya Fluticasone aliyoambiwa aichukue hakuwa akiiona katika droo ile ya kitanda, alihisi kuchanganyikiwa mno. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hakujua ni kitu gani cha ziada alichotakiwa kufanya.
Sekunde zilisonga mbele, alibaki akiendelea kupekuapekua ndani ya droo ile mpaka alipofanikiwa kukiona kikopo kimoja kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na dawa, kikopo kile kiliandikwa Fluticasone, kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika kikopo kile, ndipo alipogundua kwamba hiyo ilikuwa ni dawa ya pumu.
Wakati anamwangalia yule mzee kitandani, ndiyo alikuwa katika hatua ya mwisho kuvuta pumzi, dawa aliipata, hakujua namna ya kufungua kikopo kile, akabaki akihangaika kufanya hili na lile lakini kikopo hakikufunguka.
“Kinafunguliwa vipi kutoa dawa?” alijiuliza lakini hakupata jibu.
Wakati akijiuliza hayo, hali ya yule mzee iliendelea kuwa mbaya zaidi, hakuchukua muda mrefu, akatulia pale kitandani, pumzi ikakata na kufariki dunia. Wakati mzee huyo anakufa, Pamela hakuligundua hilo, aliendelea kuangalia namna ya kufungua kile kikopo, baadaye ndipo kumbukumbu ikamjia kwamba inawezekana zile dawa walizokuwa wakizitumia Wazungu kujipulizia mdomoni ndiyo ilikuwa kama ile.
Alipoangalia pembeni na kubonyeza kwa juu, akaona dawa ikitoka, hakutaka kuchelewa, hapohapo akamsogelea yule mzee kisha kumuweka tundu la lile kopo mdomoni mwake kisha kubonyeza kwa juu, dawa ikatoka lakini alikuwa amekwishachelewa kwani tayari alifariki dunia.
Hakuwa akimfahamu, siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuona lakini kifo chake kilimuhuzunisha mno. Alibaki akimuita pale kitandani lakini yule mzee hakuweza kuamka. Pamela akaogopa, hakutaka kubaki mahali hapo, kitu alichokifikiria muda huo ni kukimbia tu.
“Siwezi kubaki,” alijisemea, hapohapo akavaa nguo zake harakaharaka na kuondoka mle chumbani, tena huku akikimbia, akafungua geti na kutokomea gizani, hata viatu alisahau kuvaa, alivishikilia mkononi.
* * * *
Kichwa cha Dickson kiliwaza mapenzi tu, hakufikiria kitu kingine mahali hapo, kwa kumwangalia msichana yule, alimtamani sana, hakuona kama kulikuwa na sababu ambazo zingemfanya kumuacha hivihivi.
Pepo la ngono alilokuwa nalo lilimuweka kwenye wakati mgumu, hakufikiria kitu kingine chochote kile zaidi ya kulala na mwanamke huyo tu. Njiani, humo ndani ya gari alikuwa akizungumza naye, alitaka kuona akizoeana kabla ya kuingia ndani.
Walichukua muda wa dakika ishirini ndipo walipofika nje ya nyumba moja ya wageni, wote wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Muda wote huo Dickson alikuwa na kofia yake kichwani mwake, hakutaka kugundulika, hakukuwa na kitu alichokuwa akikihofia kama kugundulika kwani aliona kama hilo lingetokea ilikuwa ni lazima ashtakiwe hata kama alikuwa kiongozi mkubwa wa jeshi la polisi.
Wakaingia ndani, akalipia kisha kuelekea chumbani. Walipofika humo, akamlaza kitandani msichana yule na kuanza kumwangalia kwa matamanio. Hakutaka taa iwake, aliogopa kugundulika, alichokifanya ni kuifuata swichi na kuizima.
“Mbona unazima taa?” aliuliza mwanamke yule huku akionekana kuhamaki.
“Sasa si ninataka tuanze kufanya kilichotuleta humu ndani,” alijibu Dickson.
“Yaani tufanyie gizani?”
“Ndiyo! Kwani kuna ubaya?”
“Hapana! Kufanyia gizani siwezi,” alisema mwanamke yule huku akiinuka kitandani.
“Kwani kuna tatizo gani kufanyia gizani?”
“Raha ya chumbani tuonane, sasa giza la nini?” alisema mwanamke yule.
“Sasa kama mimi mteja nahitaji giza!”
“Hapana! Kwa giza siwezi kabisa.”
Wakati akiyasema maneno hayo, tayari yule mwanamke alikwishaifikia swichi iliyokuwa mle chumbani na kuiwasha. Dickson akashtuka, mwanga mkali ukampiga usoni mwake, kofia haikuwepo kichwani mwake, alikuwa amekwishaiweka pembeni tayari kwa kulala na mwanamke yule.
Alipoiwasha taa ile akarudi kitandani pasipo kumwangalia mteja wake, alipolala tu kitandani na kumwangalia mteja wake usoni, mwanamke yule akashtuka sana, mtu aliyesimama mbele yake alimfahamu vilivyo, alikuwa yuleyule mwanaume ambaye mara kwa mara alizungumza mbele ya waandishi wa habari akipinga sana wanawake kujiuza, yuleyule ambaye aliagiza machangudoa wote wakamatwe na wapigwe faini, alikuwa kamanda Dickson.
“Aaah! Kamanda Dick,” alisema mwanamke yule kwa kuhamaki.
Dickson akashtuka, hakuamini kama mwanamke yule alikuwa akimwangalia usoni, hakuwa na kofia wala miwani, alionekana kuchanganyikiwa mno.
Yule mwanamke akasimama kitandani kwa lengo la kuondoka, alipoanza kupiga hatua, Dickson akamshika mkono.
“Niachie niondoke,” alisema yule mwanamke.
“Kwenda wapi?”
Kumuacha hivihivi halikuwa jambo rahisi, hata kabla yule mwanamke hajafanya chochote akashtukia akipigwa kofi moja usoni, kofi lililompepesua na kujikuta akiangukia kitandani. Alichokifanya Dickson ni kumfumba mdomo wake kwa kutumia taulo lililokuwa kitandani na kuiziba pua yake.
Yule changudoa alibaki akikukuruka lakini Dickson hakumuacha, aliendelea kumziba mdomo na pua yake kwa lengo la kumuua tu. Hakukuwa na kingine alichotakiwa kufanya, kugundulika na yule mwanamke aliamini kwamba kungemletea matatizo makubwa hivyo ili kuficha kila kitu kilichokuwa kimetokea ilikuwa ni lazima amuue.
“Siku zote hakuna siri ya watu wawili, ni lazima ufe kama wenzako,” alisema Dickson.
Mwanamke yule akatulia kitandani, shuka lilikunjikakunjika, mwili wake ulivimba, Dickson akaelekea bafuni, akalilowesha maji lile taulo kisha kuurudia mwili wa yule mwanamke na kuanza kufuta sehemu zote ambazo vidole vyake vilitumika kumgusa. Alipomaliza, akatoka nje.
“Hapo nje si kuna chipsi?” alimuuliza dada wa mapokezi.
“Ndiyo!”
“Oke! Ngoja nikanunue kwanza, nakuja,” alisema Dickson, dada yule akakubaliana naye, akatoka nje na kulifuata gari lake, kilichosikika baada ya hapo ni muungurumo wa gari lililoanza kuondoka mahali hapo.
Je, nini kitafuatia?
Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akajikuta akipandishwa vyeo na mwisho wa siku akijikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.
Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.
Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.
Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.
SONGA NAYO...
Taarifa zikaanza kusambaa Upanga kwamba kulikuwa na mwanaume aliyekuwa amekufa chumbani kwake. Kila mtu aliyezisikia taarifa hizo alishtuka, walimfahamu mzee huyo, alikuwa mzee mpole, aliyeheshimika ambaye alisumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu.
Watu walihuzunika mno, wengi walisema kwamba pumu ndiyo iliyokuwa imemuua mzee huyo lakini baadhi ya watu wakaibuka na kusema kwamba mzee huyo alikuwa ameuawa. Hakukuwa na aliyejua ukweli halisi wa kifo chake.
Polisi walipoingia ndani ya chumba chake waliukuta mwili wake ukiwa kitandani, alikuwa ameishika shingo yake na pembeni kulikuwa na dawa yake iliyokuwa kwenye kichupa, dawa iitwayo Fluticasone ambayo ilikuwa maalum kwa wagonjwa wa pumu.
Pamoja na kukuta hali halisi ndani ya chumba hicho, hali iliyoonesha kwamba mzee huyo alikuwa amekufa lakini bado baadhi ya watu waliendelea kung’ang’ania kwamba mzee huyo alikuwa ameuawa jambo lililowafanya polisi kuanza kuhoji.
“Mnasema ameuawa?” aliuliza polisi mmoja, alikuwa mbele ya vijana wanne.
“Siyo sisi, ni walinzi wa maeneo haya,” alijibu kijana mmoja huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Walinzi gani?”
“Wa nyumba zile kule,” alijibu kijana mwingine huku akizinyooshea kidole nyumba mbili.
Polisi huyo hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuelekea kule kijana yule aliponyoosha kidole, alipoifikia nyumba moja miongoni mwa nyumba zile mbili, akapiga hodi ambapo mlinzi akaufungua mlango na macho yake kukutana na macho ya polisi.
“Kwa nini unasema kwamba mzee Ibrahim ameuawa?” aliuliza polisi yule mara baada ya salamu.
“Jana alikuja usiku kama saa nane hivi mzee Ibrahim alifika nyumbani kwake hapa na kuliingiza gari lake ndani ya ngome ya nyumba yake. Sikujua alikuwa na nani kwa sababu gari lake lilikuwa na vioo vyeusi,” alijibu mlinzi huyo kwa kirefu.
“Ikawaje?”
“Baada kama ya saa moja hivi, nikamuona msichana mmoja akitoka huku akikimbia, kilichotokea ndani, sikukijua na hata wenzangu hawakujua pia,” alisema mlinzi yule.
Maelezo ya mlinzi yalikuwa muhimu kwani yule polisi aliamini kwamba yangeweza kufanikisha kukamatwa kwa muuaji huyo, alichokifanya ni kumchukua na kutangulizana naye kituoni kwa sababu ya kutoa maelezo zaidi.
* * *
Ukiachana na taarifa za kufariki kwa tajiri aliyekuwa akiishi Upaga, pia kukawa na taarifa zingine za mwanamke aliyeuawa ndani ya nyumba moja ya wageni iliyokuwa Mwananyamala. Polisi waliosikia tetesi hizo hawakubaki kituoni, wakaelekea mpaka katika nyumba hiyo ya wageni kwa ajili ya kushuhudia kilichokuwa kimetokea.
Umati wa watu uliokuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni uliwapa uhakika kwamba kile walichokuwa wamekisikia kilikuwa kweli kabisa, wakateremka kutoka garini na kuelekea ndani huku wakiwa na bunduki zao mikononi.
Msichana mrembo wa sura, aliyekuwa na umbo la kuvutia alikuwa kimya kitandani. Mapovu yalikuwa yamemtoka mdomoni, shuka lilikuwa limechafuliwa kwa haja kubwa iliyokuwa imemtoka mara baada ya kunyongwa na muuaji.
Kila polisi aliyemwangalia msichana yule, alimkumbuka yule msichana Fatuma aliyenyongwa bafuni alipokuwa akioga. Watu wa kwanza waliotiwa hatihani walikuwa vijana waliokuwa chumbani wakivuta bangi, walichokisema ni kwamba aliyemuua Fatuma alikuwa mwanaume aliyevalia kofia kubwa kichwani.
Haikuwa hiyo tu, hata alipouawa msichana mmoja porini na mzee aliyeshuhudia tukio lile kusema kwamba mtu aliyefanya mauaji alikuwa amevalia kofia kubwa kichwani, iliwapa uhakika kwamba mtu huyo ndiye aliyehusika katika mauaji ya watu hao wawili.
Leo hii kulikuwa na mtu mwingine aliyeuawa, alikuwa msichana mrembo ambapo kwa maelezo ya dada wa mapokezi alisema kwamba msichana huyo alikuwa akijiuza na alikuja katika nyumba hiyo ya wageni na mteja wake, kilichotokea, baadaye yule mwanaume akatoweka, hata sura hakuwa ameiona.
“Kwa nini? Kwa sababu ya giza?”
“Hapana! Alikuwa amevaa kofia,” alijibu msichana huyo.
Polisi wakachanganyikiwa, mtu mmoja mwenye utambulisho wa kuvaa kofia alikuwa amefanya mauaji ya watu watatu kwa nyakati tofauti, polisi wakaanza kujiuliza juu ya mtu huyo kufanya mauaji hayo lakini hakukuwa na yeyote aliyefahamu.
Wapo waliohisi kwamba muuaji alitumwa na mganga kuua ili kupata utajiri lakini kitu kilichowafanya kuyapuuzia mawazo hayo ni kwamba miili ya watu hao ilikutwa na viungo vyote, hakukuwa na kiungo kilichonyofolewa.
Taarifa zikapelekwa kwa DCP Dickson, alichokifanya ni kuwaita polisi wawili waliokuwa katika kitengo cha upelelezi na kuanza kuwauliza juu ya kile kilichotokea katika upelelezi wao.
“Kuna mtu anavaa kofia, huyo ndiye anayeua,” alisema polisi mmoja.
“Yaani ishu ya kuvaa kofia mmeiona kuwa sababu kubwa? Wangapi wanavaa kofia? Yaani badala ya kuja na kuniambia kwamba muuaji ni fulani, mnakuja hapa na kuniambia muuaji anavaa kofia, kweli mnaweza kuniletea taarifa ya kijinga namna hii?” aliuliza Dickson huku akijifanya kuwa na hasira.
“Tutafanya kazi kwa juhudi mkuu! Mpaka atakapopatikana,” alisema polisi mmoja.
“Acheni uvivu, fanyeni kazi kama watu wanaotaka kufanya kazi, siyo mnakuja hapa na kuniambia mambo ya kofia,” alisema Dickson.
“Sawa mkuu! Tutafanya hivyo,” alisema polisi mmoja kisha wote kwa pamoja kupiga saluti kama heshima, baada ya hapo wakaondoka.
Dickson akarudi ofisini na kutulia kitini, uso wake ulijawa na tabasamu pana lakini kwa mbali alionekana kuwa na hofu mno. Alihisi kama angeweza kukamatwa kwani staili ya kofia aliyokuwa akiivaa ingemponza.
“Ni lazima nitoke kivingine, siwezi kukamatwa kirahisi,” alisema Dickson huku akijipanga usiku wa siku hiyo atoke na kwenda kuonana na msichana mwingine maeneo ya Kinondoni Makaburini. Alitaka soko lake lihamie huko, hivyo akajipanga.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba ni yeye, anaamua kumuua na mwili kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika, kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kinachoendelea.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Uzuri wake uliendelea kuwa gumzo, machangudoa wengine waliogopa kwa kuwa kila alipokuwa, hakukuwa na biashara nzuri kwa upande wao. Kila mteja ambaye alifika mahali hapo na kumuona Pamela, hakutaka kumuacha, alimfuata na kumnunua kisha kuondoka naye au wakati mwingine kumaliza shida zake katikati ya makaburi.
Machangudoa wengi walimuonea wivu na wengine kumkasirikia, ili biashara zao ziende kama inavyotakiwa ilikuwa ni lazima Pamela aondoke mahali hapo kwani uwepo wake uliwaletea shida sana.
Baadhi ya machangudoa wakakutana na kuanza kumjadili kwamba ilikuwa ni vizuri kumfukuza au wamuache. Katika kushauriana huko, wengine wakaona ilikuwa ni lazima aendelee kubaki kwani kwa wakati huo Pamela alikuwa kivutio, wanaume wengi walifika na walipomkosa, waliwachukua machangudoa wengine.
Maisha yaliendelea kila siku, thamani yake ikaanza kupanda, akawa msichana mwenye bahati, alitengeneza kiasi kikubwa cha fedha mpaka pale alipokuja kukutana na mwanaume aliyemfuata huku akiwa na kofia kubwa kichwani, mteja aliyekuwa na muonekano wenye fedha ambaye kwake alijitambulisha kama muuzaji wa nafaka kutoka vijijini aliyejiita kwa jina la Mandingo.
“Mandingo!” alisema kwa mshangao.
“Ndiyo! Mimi ni Mkurya, huwa nasafirisha nafaka kutoka huko vijijini kuja huku mjini,” alisema mwanaume huyo.
“Aisee! Kumbe nipo na bosi!”
“Yeah! Nipo hapa kwa ajili ya kutumbua hela, zinaniwasha sana. Kwanza gharama yako inakwendaje?” aliuliza mwanaume huyo.
“Kwa sababu wewe ni mfanyabiashara mkubwa, mwenye fedha, nitakufanyia laki mbili kwa usiku mmoja,” alisema Pamela.
“Mmmh! Hakuna tatizo, kwa ajili yako, kwa jinsi ulivyo, nipo tayari,” alisema mwanaume huyo.
Huyo hakuwa mfanyabiashara kama alivyojitambulisha, alikuwa Dickson ambaye aliamua kubadilisha kiwanja cha kuchukua machangudoa na kuhamia Kinondoni Makaburini. Alipomuona Pamela kwa mara ya kwanza, moyo wake ukafarijika, alifurahia moyoni mwake kwani kwa kipindi kirefu alichokitumia kununua machangudoa, hakuwahi kukutana na changudoa aliyekuwa na umbo zuri, sura nzuri kama alivyokuwa Pamela.
Staili yake ilikuwa ileile, hakutaka kujulikana, kichwani alikuwa na kofia kubwa ya Marlboro huku kukiwa na mwanga hafifu ambao hata ulipompiga usoni, hakuonekana vizuri.
“Unaishi wapi?’ aliuliza Pamela.
“Naishi Msasani, ila hatutoweza kwenda nyumbani,” alijibu Dickson.
“Kwa hiyo tutafanyia wapi? Garini?”
“Hapana. Tutakwenda kuchukua chumba katika gesti moja uswahilini.”
“Mmmh!”
“Nini sasa?”
“Umejisifia mfanyabiashara mkubwa, halafu tuchukue gesti! Kweli jamani baby? Kwa nini tusichukue hoteli kabisa?” aliuliza Pamela huku akionekana kushtuka kwa mbali.
“Hahaha! Si unajua sisi wengine watu maarufu Tanzania, tukionekana, siyo poa kabisa,” alijitetea Dickson.
“Basi sawa. Cha msingi hela tu,” alisema Pamela.
Hakukuwa na muda wa kupoteza tena mahali hapo, alichokifanya Dickson ni kuliondoa gari mahali hapo na kuelekea katika gesti moja iliyokuwa Manzese Midizini. Hakutaka kwenda katika hoteli kubwa kwa kuwa alijua fika kwamba kugundulika ilikuwa rahisi sana tofauti na gesti bubu za mitaani.
Huko, aliamini kwamba hakukuwa na ulinzi wa kutosha, wahudumu hawakuwa na umakini wowote ule kwa wageni waliokuwa wakiingia, zaidi, wao waliangalia fedha tu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kutokugundulika katika kila gesti aliyokwenda kule Mwananyamala.
Garini alikuwa mzungumzaji mkubwa, alitaka kuzoeleka kwa msichana huyo ili hata watakapofika chumbani kusiwe na maswali mengi. Hapohapo garini ndipo Dickson alipomwambia Pamela kwamba hakukuwa na kitu alichokichukia kama kufanya mapenzi katika chumba kilichokuwa na mwanga mkali wa taa.
“Kwa nini?”
“Basi tu, unajua sisi wengine tunakuwa na aibu kubwa sana.”
“MmmH! Kweli makubwa, halafu si kwako tu, mpo wengi wa namna hiyo, sijui huwa mnaogopa nini,” alisema Pamela.
Maneno hayo yakawa ahueni kwa Dickson, alijiona kuwa mshindi, kitendo cha Pamela kumwambia kwamba yeye hakuwa mmoja wake akawa na uhakika kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuzima taa ya chumbani na hatimaye kufanya mapenzi kama alivyokuwa amepanga.
Hakuwa na hofu tena, alijua jinsi ya kucheza na wanawake hao, kuua, wala hakuogopa, alitaka kuona mambo yake yote yanakwenda sawa kama inavyotakiwa hivyo kunapotokea kizuizi chochote cha kuitunza siri ile, hakuhofia kuua hata kidogo.
Waliendelea na safari mpaka walipofika katika gesti hiyo iliyokuwa Manzese Midizini, tena kwa kuingia ndani kabisa. Walipofika, akasimamisha gari na kisha kuteremka. Katika kipindi chote hicho alihakikisha kofia yake haitoki kichwani mwake.
Vijana waliokuwa wamekaa pembeni mwa gesti hiyo walibaki wakimwangalia Pamela ambaye alikuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo na Dickson ambaye hawakuwa wamemtambua kabisa.
Umbo lake liliwaacha midomo wazi, hawakuamini kama kulikuwa na mwanamke aliyekamilika kama alivyokuwa Pamela. Sura nzuri na yenye mvuto, umbo namba nane, hipsi kubwa ambazo vijana wa mitaani walipenda kuziita kwa jina la pisto.
“Nahitaji chumba.”
“Vipo. Show time au mpaka asubuhi?” aliuliza dada wa mapokezi.
“Mpaka asubuhi.”
“Elfu sita.”
“Hakuna tatizo,” aliitikia Dickson, akalipia, wakapewa ufunguo na kuelekea huko chumbani. Wakati Pamela akifikiria fedha, hakujua kama alikuwa katika mikono ya mtu muuaji. Endapo angejua, asingekubali kuelekea gesti na mwanaume huyo.
Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea. Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea. Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam. Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinogewa na penzi la changudoa mmoja aitwaye Pamela, umbo lake, ngozi vinamchanganya na kujikuta akianza kumganda pasipo kujua kwamba ukaribu wake na msichana huyo ungeweza kubadilisha kila kitu.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO… Huo ulikuwa mwanzo wa ukaribu baina ya Dickson na changudoa Pamela. Msichana huyo mrembo ambaye alivutia kila alipomwangalia aliliteka penzi la Dickson kiasi kwamba hata alipokuwa ofisini, hakuwa akifikiria kitu chochote kile zaidi ya penzi la msichana huyo mwenye umbo lenye mvuto. Siku zikaendelea kukatika, hakukuwa na muda wa kutulia, saa mbili ofisini pasipo Pamela zilionekana kuwa nyingi, wakati mwingine alihakikisha anafanya kazi zake haraka iwezekanavyo kisha kurudi nyumbani ambapo alimpigia simu Pamela na kuja nyumbani kwake. Wivu ukamjaa moyoni, wakati mwingine alimlazimisha msichana huyo alale nyumbani kwake kwani kila alipokuwa naye mbali, alihisi msichana huyo kulala na wanaume wengine kitu kilichouumiza mno moyo wake, kwa jinsi alivyokuwa na mapenzi mazito kwa Pamela, kuna kipindi alisahau kabisa kwamba msichana huyo alikuwa changudoa tu ambaye alilala na mwanaume yeyote aliyekuwa na pesa. “Vipi tena?” aliuliza Pamela, ilikuwa mchana wa saa saba, alipigiwa simu na Dickson, haikuwa kawaida kitu hicho kutokea. “Upo wapi?” “Nipo nyumbani, kuna nini mpenzi?” aliuliza Pamela. “Unaweza kuja mara moja?” “Wapi?” “Nyumbani kwangu.” “Kwani haupo kazini?” “Haujanijibu swali langu, unaweza kuja?” “Naweza. Ila kuna nini?” “Wewe njoo, wala usiogope,” alisema Dickson na simu kukatwa. Kichwa chake kilichanganyikiwa mno, alichokitaka mahali hapo ni kumuona msichana huyo tu kwani hakukuwa na kitu alichokuwa akipenda kama kuwa karibu na Pamela. Hakutaka kuendelea kukaa ofisini, alichokifanya ni kuondoka na kurudi nyumbani haraka ambapo wala hazikupita dakika nyingi, Pamela akafika, moja kwa moja akampeleka chumbani na kulala naye, hata kazi aliamua kuachana nayo kwa siku hiyo kwani penzi la Pamela lilimchanganya. **** Magreth alibadilisha ratiba yake, kila siku akawa mtu wa kutembea katika viwanja mbalimbali vya machangudoa huku lengo lake likiwa ni kuona kama angefanikiwa kumpata mteja wake aliyemkimbia katika kipindi alichomhitaji sana. Alizunguka na kuzunguka, tena wiki nzima mpaka alipofanikiwa kupata taarifa ambazo aliamini kwamba mtu aliyekuwa akizungumziwa alikuwa huyohuyo aliyekuwa akimhitaji. “Umesema ana BMW nyeusi?” aliuliza changudoa mmoja. “Ndiyo! Unamfahamu?” “Kwa kweli sijawahi kumuona, ila huyo mteja anafika sana hapa kiwanjani,” alijibu changudoa huyo. “Nitampata vipi?” “Kwani ni nani kwako? Mumeo?” “Hapana! Ila ninataka kuonana naye,” alisema changudoa huyo. Jibu pekee alilopewa ni kwamba isingewezekana kuonana na mteja huyo kwani siku hizo hakuwa akifika sana kutokana na kulipata penzi la kudumu kutoka kwa msichana mrembo aliyetokea Arusha, Pamela. Kitu alichokitaka Magreth ni kuonana na huyo Pamela kwa kuamini kwamba angepata taarifa nyingi juu ya mwanaume huyo na hata ikiwezekana kupafahamu kwake kwani hakukuwa na mteja ambaye alimpa fedha nyingi kama mwanaume huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua alikuwa na sura gani. Alipofanikiwa kuonana na Pamela, akajaribu kutengeneza urafiki naye, akaanza kumzoea, kila siku mchana akawa mtu wa kwenda kumtembelea, kwa kuwa Pamela hakuwa na marafiki wengi na pia hakuwa amelizoea sana jiji, akaupokea urafiki wa Magreth pasipo kujua msichana huyo alihitaji nini. Mpaka siku ambayo Dickson alimpigia Pamela simu na kumuita nyumbani, Magreth alikuwa pamoja naye chumbani, alichokifanya ni kumuaga kwa lengo la kwenda huko. “Ndiyo unakwenda kuonana naye?” aliuliza Magreth. “Ndiyo! Unataka twende wote?” aliuliza Pamela huku akionekana dhahiri kwamba alikuwa akitania. “Hahah! Kama inawezekana! Kwani hawezi kulala na wanawake wawili?” aliuliza Magreth, naye mwenyewe alionesha kutania. Pamela hakujibu swali hilo zaidi ya kucheka kisha kuondoka nyumbani hapo. Kwa Magreth alionekana kuwa na uhakika kwamba mwanaume huyo ambaye Pamela alikwenda kuonana naye ndiye yule ambaye alifika sana katika kiwanja chake, Sinza Mori na kumnunua, lakini ghafla akapotea na hakurudi tena. “Atakuwa ndiye yeye tu, ni lazima nimtafute, nipajue kwake na kumrudisha mikononi mwangu,” alisema Magreth pasipo kujua mtu huyo alikuwa nani. Je, nini kitafuatia?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment