Sehemu Ya Tatu
(3)
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote waliopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa.
Ananogewa na mchezo huo kiasi cha kuwa mtumwa wa ngono.
Baadaye Dickson au Zinja anahitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwenda
kujiunga na chuo cha polisi mjini Moshi, Kilimanjaro.
Anapohitimu
anapangiwa kwenda kufanya kazi katika mji mdogo wa Tunduma, uliopo kwenye mpaka
wa Tanzania na Zambia. Baada ya mafanikio makubwa, anahamishwa kikazi na
kuelekea Dar es Salaam, huko, kama alivyofanya sehemu nyingine, napo anaendelea
na mchezo wake kama kawaida.
Kwa upande wa kazi, Dickson anaendelea
kujituma kadiri ya uwezo wake, jaribio la kutaka kumuua linashindikana na muda
mfupi baadaye, anafanikiwa kuzima jaribio kubwa la ujambazi kwenye benki, hali
inayosababisha apandishwe tena cheo na kufikia ngazi ya DCP.
Hata
hivyo, michezo yake ya kununua machangudoa anaendelea nayo.
Anapoona
amemnunua changudoa na kugunduliwa, anamuua na kumzika msituni.
Je,
nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Alitembea kwa harakaharaka, moyoni
alikuwa na kimuemue cha kusema kile kilichokuwa kimetokea msituni ambacho
hakutaka mtu yeyote yule afahamu zaidi ya polisi wao na kisha kuwaambia juu ya
lile gari aliloliona msituni kwani namba zake alikuwa nazo
kichwani.
Alichukua zaidi ya dakika kumi ndipo alipofika kituoni huku
akiwa anahema kwa nguvu na kijasho chembamba kikimtiririka. Jambo
lililowashangaza polisi wale.
“Karibu. Unataka nini?” aliuliza polisi
aliyekuwa kaunta mara baada ya salamu.
“Nimekuja kutoa
taarifa.”
“Taarifa gani?”
“Ya mauaji,” alijibu mzee
Gombana.
“Hebu njoo huku,” alisema polisi yule huku akimvuta ndani ya
chumba kidogo kwa ajili ya mahojiano marefu kwani taarifa ya mauaji haikuwa
ndogo. Polisi waliokuwa wamemsikia ambao walikuwa karibu na kaunta ile, nao
wakaelekea ndani. Hawakujua kama taarifa aliyoileta mzee huyo ilikuwa ni ya
mauaji yaliyofanywa na kamanda wao.
“Umesema umeleta taarifa ya
mauaji, si ndiyo?” aliuliza mkuu wa kituo
hicho.
“Ndiyo!”
“Wapi?”
“Kule
msituni.”
Alichokifanya mzee Gombana ni kuanza kuhadithia kilichokuwa
kimetokea kule porini, aliwaambia kwamba alimuona mtu akiwa amefika msituni
akiwa na gari, baada ya kusimama aliitoa maiti moja na kuizika katika shimo
kubwa alilokuwa amelichimba.
Kila polisi aliyesikia taarifa ile
alishtuka, walijaribu kumuuliza mzee huyo mara mbilimbili kama alikuwa na
uhakika na kile alichokuwa amekisema, akawaambia kwamba alikuwa na uhakika na
wangefika mpaka katika eneo hilo.
Hawakutaka kuendelea na mahojiano
ndani ya chumba kile, walichokifanya ni kutoka, wakachukua gari lao, difenda,
polisi wanne waliokuwa na bunduki wakaingia garini na safari ya kuelekea huko
msituni kuanza.
Walichukua dakika arobaini mpaka kufika katika msitu
huo ambapo wakaanza kuingia ndani zaidi. Dereva hakuendesha gari kwa mwendo wa
kasi kutokana na miti mingi iliyokuwepo hali iliyosababisha ukosefu wa barabara
ya magari.
“Wapi?” aliuliza polisi mmoja.
“Kule mbele mkuu!
Nyie twendeni tu,” alisema mzee Gombana na hivyo dereva kuliendesha gari
kuelekekea mbele zaidi.
Waliendelea kwenda mbele mpaka walipofika
sehemu moja iliyoonekana kuwa na uwazi mkubwa, hapo ndipo mzee Gombana alipotaka
gari lisimamishwe na kuegeshwa pembeni kwani hiyo ndiyo ilikuwa sehemu
alipomuona Dickson akimzika mwanamke na kuondoka zake.
Kwa jinsi eneo
lile lilivyokuwa, hawakuwa na shaka kwamba muda mchache uliopita sehemu hiyo
ilichimbwa na kufukiwa, walichokifanya polisi wale ni kuchukua makoleo
yaliyokuwa garini na kuanza kufukua lile shimo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bila shaka huyu
mzee yupo sahihi kabisa, humu kutakuwa na maiti, si unaona udongo unavyoonesha?”
alisema polisi mmoja huku wengine wakiendelea kufukua lile shimo.
Kazi
haikuwa ndogo, japokuwa walikuwa wengi lakini walipata kazi kubwa kulifukua lile
shimo. Mzee Gombana alisimama pembeni, alikuwa akifuatilia kila kitu kilichokuwa
kikiendelea mahali hapo huku moyoni akimuomba Mungu mwili wa mtu huyo ukutwe ili
aweze kuaminika kwa taarifa aliyoitoa.
Baada ya dakika kadhaa, makoleo
yao yakaanza kudunda mwilini mwa maiti na kugundua kwamba tayari walikuwa
wameifikia, hivyo wakayatupa makoleo yao pembeni na kuanza kutoa mchanga kwa
kutumia mikono.
“Ni msichana!” alisema polisi mmoja na hivyo
kusaidiana kuutoa mwili ule.
Kila mmoja akapigwa na mshtuko,
alionekana kuwa msichana mrembo wa sura na umbo, kila mtu aliyemwangalia
alishindwa kuelewa kipi kilichotokea katika maisha yake mpaka huyo mtu aliyemuua
na kumzika aliamua kufanya hivyo.
Walichokifanya ni kuubeba mwili ule
na kuondoka nao kwa ajili ya uchunguzi wa kujua ni kitu gani kilisababisha kifo
chake hata kabla ya kuzikwa. Hawakutaka kumuacha mzee Gombana, bado alihitajika
kwa ajili ya kuisaidia polisi juu ya kile kilichokuwa kimetokea.
“Kuna
chochote unachokikumbuka kuhusu muuaji?” aliuliza mkuu wa
polisi.
“Ndiyo! Nililiona gari lake!”
“Aina gani? Unazijua
namba zake?”
“Ndiyo! Nakumbuka kila kitu.”
“Safi sana, ngoja
tufike kituoni kwanza,” alisema polisi yule.
Hawakutaka kuendelea
kubaki pale, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika kituo chao kwa ajili ya
mahojiano zaidi na mzee Gombana ambaye alitakiwa kutaja kila kitu alichokuwa
amekiona, likiwemo suala la namba za gari ambalo kwao lilionekana kuwa
muhimu.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya
kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba
ni yeye, anaamua kumuua na mwili kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika,
kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kilichoendelea.
Je, nini
kitafuatia? SONGA NAYO…
Dickson alikuwa na furaha tele kwani alijua
huo ndiyo ungekuwa mwanzo wa kuficha siri juu ya kile kilichokuwa kimetokea
msituni. Hakutaka ajulikane na mtu yeyote kama yeye ndiye aliyehusika na mauaji
ya msichana yule kisha kumzika msituni.
Mzee Gombana alikuwa na furaha
tele, kwake kuwa mikononi mwa Dickson kulimpa faraja na kuona alikuwa kwenye
mikono iliyo salama. Garini, mzungumzaji mkubwa alikuwa yeye, alimhadithia namna
alivyomuona mwanaume huyo akiutoa mwili kutoka garini kisha kuuzika katika shimo
alilokuwa amelichimba.
“Kuna watu katili sana aiseee, nilishuhudia
kila kitu mkuu, yaani mpaka nikatetemeka,” alisema mzee Gombana
“Ni
lazima tuhakikishe anakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema
Dickson huku akiendesha gari.
Bado furaha ilikuwa moyoni mwake,
hakuamini kama kazi ingekuwa nyepesi namna ile, alichokuwa akikifikiria kichwani
mwake kwa wakati huo ni kumuua mzee Gombana tu ili ile siri iendelee kuwa
siri.
Alimshukuru Mungu kwani kile ambacho mzee Gombana alikiona kule
msituni, hakutoa ushahidi wa kutosha kuhusiana na lile gari hivyo kuona kwamba
hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya kumnyamazisha milele.
Hakutaka kuwa na
presha, kwa kuwa tayari alikuwa ameaminika vya kutosha, alichokifanya ni
kuelekea ofisini kwake ili huko ndiyo uwe mwanzo wa kufanya kile alichotaka
kukifanya. Wakati wakiwa wamefika Manzese Tip Top, Dickson akalipaki gari lake
pembeni kisha kuteremka.
Akaanza kuelekea katika duka la dawa ambapo
akanunua dawa za mafua, piriton. Akazichukua na kuondoka dukani hapo kurudi
garini pasipo kuzungumza chochote, mzee Gombana hakusema kitu, alinyamaza huku
kwa kumwangalia alionekana kuwa mtu mwenye furaha tele.
“Samahani!
Mafua yananisumbua mno,” alisema Dickson na kuingia garini.
“Pole sana
mkuu.”
“Asante.”
Akaingia ndani ya gari na safari kuendelea.
Hawakuchukua dakika nyingi wakaingia katika jengo la makao makuu ya polisi
ambapo wakateremka na kuanza kuelekea ndani huku kila polisi aliyekutana naye,
alipiga saluti kama kumpa heshima.
Walipofika ofisini, akamwambia mzee
Gombana akae kitini kwa lengo la kuzungumza naye. Ila kabla ya mazungumzo hayo
kuanza, akainuka, akaelekea nje ya ofisi ile ambapo alichukua zile dawa za
priton, akazisagasaga kisha kuchukua sumu aina ya phenomenon yenye makali ya
kuua hapohapo na kuiweka kwenye kikombe ambacho alitaka kumuwekea kahawa mzee
Gombana.
Kwa sababu phenomenon ilikuwa miongoni mwa sumu zilizoua kwa
haraka sana mara ziingiapo mwilini mwa binadamu, alichokifanya ni kupunguza
makali yake na dawa ya piriton ambayo nayo aliisaga na kuiweka ndani ya kile
kikombe kisha kurudi ofisini.
Aliporudi ofisini, akachukua chupa ya
kahawa na kuimimina katika vikombe viwili na kumgawia mzee yule kikombe
kilichokuwa na kahawa yenye sumu na kuanza kunywa. Dickson akafurahi, kitendo
cha mzee yule kunywa kahawa ile kikamuoneshea kwamba alikuwa mshindi juu ya
kilichokuwa kimetokea, hivyo alijiona kushinda vita kubwa na nzito iliyokuwa
mbele yake.
“Kwenye maisha nimejifunza mengi mno,” alisema
Dickson.
“Umejifunza nini mkuu?”
“Unapokuwa kiongozi ni
lazima uwe mnyenyekevu pia. Siku kama ya leo huwa sipendi niandaliwe kahawa,
ninapenda kuandaa mwenyewe, ninapenda kuwaoneshea watu wengine jinsi kiongozi
unavyotakiwa kuwa,” alisema Dickson huku akitoa tabasamu.
“Wewe ni
kiongozi bora, jinsi ulivyo, ukarimu wako na matendo yako ni vitu viwili
tofauti. Wengine wanakuona una roho mbaya sana, ila tangu nimekutana nawe,
hakika umekuwa tofauti na nilivyokuwa nikifikiria,” alisema mzee
Gombana.
“Ninapokuwa kazini huwa ninauvaa mwili wa kazini, huwezi
kwenda kupambana na majambazi huku uso wako ukiwa na tabasamu pana, unatakiwa
kubadilika, uso uwe kwenye muonekano wa kikazi. Ninapofanya vitu kwa ujasiri na
kuingia kazini huku nikionekana mwenye hasira, wengi wanafikiri nipo hivyo, ila
nipo tofauti,” alisema Dickson huku tabasamu pana likiwepo usoni
mwake.
Hawakuzungumza mengi kwani tayari alijua kwamba ile sumu
iliyoingia mwilini mwa mzee Gombana ingeweza kufanya kazi muda wowote ule.
Alichokifanya ni kumshukuru mzee huyo kwa ushirikiano wake huku akimtaka kwenda
na yeye kuendelea na kazi.
Mzee Gombana akasimama kisha kuondoka
ofisini hapo huku akiwa ameiacha ile namba ya gari aliloliona msituni ambalo
ndilo lilikuwa gari la Dickson aliyekuwa Mkuu wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam.
Kwa Dickson, ilikuwa ni furaha tele.
*****
“Vipi tena mbona
unaonekana hivyo?” aliuliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mbezi.
“Kuna
taarifa mbaya mkuu!” alijibu polisi mmoja.
“Mbona unanitisha! Taarifa
ipi?”
“Yule mzee kafariki jana usiku.”
“Mzee
yupi?”
“Yule aliyeleta taarifa juu ya lile gari porini. Amekufa baada
ya kulalamika maumivu makali ya tumbo.”
“Unasemaje?”
”Ndiyo
hivyo mkuu!”
Mkuu wa kituo cha polisi
akachanganyikiwa.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya
kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba
ni yeye, anaamua kumuua na mwili wake kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika,
kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kilichoendelea.
Je, nini
kitafuatia? SONGA NAYO…
Taarifa iliyofika kituoni ilimshtua kila
polisi aliyeisikia kwamba shahidi waliyekuwa wakimtegemea kuwaambia juu ya gari
lile lililokuwa msituni kufariki dunia ghafla nyumbani kwake.
Mkuu wa
kituo hicho hakutaka kubaki ofisini, haikuwa taarifa nzuri hata kidogo kwani
viongozi wake walitaka kufahamu kila kitu akiwemo Dickson ambaye alihusika
katika kifo cha shahidi huyo, mzee Gombana.
Ofisini hakukukalika tena,
alichokifanya ni kuondoka ofisini hapo kuelekea nyumbani kwa marehemu. Hakwenda
peke yake, alikuwa na polisi kadhaa ambao wote kwa pamoja walichanganyikiwa kwa
kilichokuwa kimetokea.
“Haiwezekani, hapa kuna kitu,” alisema mkuu wa
kituo.
“Kweli mtu anaweza kufariki ghafla? Tena kwenye kipindi
tunachomuhitaji sana?” aliuliza polisi mmoja huku akimwangalia mkuu wake
usoni.
“Haiwezekani, hapa kuna kitu, subiri
tufike.”
Japokuwa barabara ilikuwa mbaya lakini dereva hakujali,
aliendesha kwa mwendo wa kasi huku wakitaka kufika msibani hapo haraka
iwezekanavyo. Kitu cha kwanza walichokuwa wakihitaji ni kuuchunguza mwili wake
kwani waliamini hakikuwa kifo cha kawaida, kulikuwa na mtu aliyekuwa amemuua
mzee Gombana kwa kutaka kuficha siri juu ya kile kilichokuwa kimetokea kule
msituni.
Bado muuaji wa msichana yule na mzee Gombana aliwachanganya,
hawakujua ni nani aliyekuwa nyuma ya mauaji yale, walichokuwa wakikifanya ni
kuhakikisha muuaji anapatikana haraka iwezekanavyo hata kabla wakuu wao
hawajachukua uamuzi mbaya.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika msibani
hapo, hata kabla gari halijasimamishwa, kama makomandoo, polisi wale wakaruka,
watu wote waliokuwa msibani wakashangaa, hawakujua sababu iliyowafanya polisi
hao wafike msibani hapo huku wakiwa na bunduki mikononi, amani iliyokuwepo
ikaanza kupotea.
Hawakuzungumza na mtu yeyote yule, walichokifanya ni
kuingia ndani na kuonana na wafiwa ambapo wakazungumza nao na kuwaambia kwamba
kabla ya mwili kuzikwa ilikuwa ni lazima ufanyiwe uchunguzi ili kuona kama
ulijeruhiwa sehemu yoyote au kulikuwa na kitu kingine kilichosababisha kifo
chake.
Hawakuwa na jinsi, japokuwa walipanga kufanya mazishi yake siku
hiyo ikabidi waahirishe ili polisi wafanye kazi yao. Mpaka siku iliyofuatia,
majibu ya uchunguzi yakatolewa na kuonesha kwamba mzee Gombana alikufa baada ya
kunywa sumu iitwayo Phenomenon iliyokuwa na nguvu ya kummaliza mtu kwa haraka
mno.
“Nani alimnywesha?”
“Hatujui, labda tumuulize mkewe,”
alisema polisi mmoja.
Hawakutaka kuchelewa, bado akili zao hazikuwa
sawa mpaka pale ambapo wangehakikisha kwamba kila kitu kinajulikana siku hiyo,
walichokifanya ni kurudi tena nyumbani ambapo huko wakakutana na mke wa
marehemeu na kuanza kuzungumza naye.
“Tumerudi mahali hapa, tunahitaji
kuzungumza nawe,” alisema mkuu wa kituo cha polisi, wakamchukua na kwenda naye
pembeni, watu wote walibaki kimya wakimwangalia.
“Kuna
nini?”
“Mumeo alikula nini jana usiku?”
“Hakula chochote
kile, aliniambia kwamba hakujisikia kula, hivyo akataka alale kwani pia
alilalamikia maumivu makali ya tumbo,” alijibu mke wa marehemu.
“Kuna
sehemu alikwenda?”
“Ndiyo! Aliniaga asubuhi kwamba anakwenda kituo cha
polisi, hakurudi mpaka ile jioni,” alijibu mwanamke huyo.
Bado
walichanganyikiwa, majibu aliyokuwa akiyatoa mke wa marehemu hayakuwaridhisha
kabisa, walichokifanya ni kuondoka na kuelekea kituoni kwa kuahidi kwamba
wengerudi tena nyumbani hapo lakini bado walihitaji kufanya upelelezi wa siri
juu ya kilichokuwa kimetokea.
Bado walikuwa kwenye giza kubwa,
hakukuwa na polisi aliyejua au hata kuhisi kwamba mtu aliyemuua msichana yule na
kumzika msituni alikuwa mkuu wao wa kazi na hata kifo cha mzee Gombana kilitokea
baada ya kunyweshwa kahawa yenye sumu na kamanda wao, Dickson.
Kila
kitu kilichoendelea, taarifa zilipelekwa kwa kamanda huyo ambaye muda wote uso
wake ulikuwa kwenye tabasamu pana kwa kuamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote
ambaye angejua kama yeye ndiye aliyekuwa amehusika katika vifo vya watu hao
wawili.
Ili kuuficha uovu wake, aliendelea kuwasisitizia polisi hao
kufanya kazi mchana na usiku kuhakikisha kwamba muuaji wa watu hao anapatikana
haraka iwezekanavyo. Kwa kuwa ilikuwa ni amri, hawakubisha, wakazidi kufanya
upelelezi kwa hali ya juu, tena kwa ukimya kabisa pasipo kufahamu kwamba yule
aliyekuwa amewasisitizia kumtafuta muuaji ndiye huyo aliyekuwa amewatuma kufanya
upelelezi kwa hali na mali ili muuaji apatikane.
* *
*
“Umependeza sana dada! Gharama yako inakwenda vipi?” alisikika
Dickson akimuuliza msichana mmoja aliyekuwa amemuita, msichana aliyekuwa
akijiuza maeneno ya Sinza Mori.
“Asante baby. Mpaka asubuhi laki moja
tu,” alijibu msichana huyo huku akiachia tabasamu pana.
Dickson
hakutaka kuacha tabia yake, alikuwa na sura mbaya ambapo aliamini kusingekuwa na
mwanamke yeyote angeweza kumkubali, hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kununua
wanawake na kufanya nao mapenzi.
Alikuwa kamanda mkuu wa Jiji la Dar
es Salaam, hakutaka kujulikana na mtu yeyote yule, kila kitu alichokifanya,
ilikuwa siri kubwa. Tabia yake ya kununua machangudoa iliendelea, hakuiacha kwa
kuamini ndiyo ilikuwa njia nyepesi ya kuuridhisha mwili wake kingono. Akabaki
akimwangalia msichana huyo, muonekano wake ukamfanya kumuona anafaa kulala naye
usiku
huo.
********************
********************
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya
sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya
kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba
ni yeye, anaamua kumuua na mwili wake kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika,
kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kilichoendelea.
Je, nini
kitafuatia? SONGA NAYO…
Taarifa iliyofika kituoni ilimshtua kila
polisi aliyeisikia kwamba shahidi waliyekuwa wakimtegemea kuwaambia juu ya gari
lile lililokuwa msituni kufariki dunia ghafla nyumbani kwake.
Mkuu wa
kituo hicho hakutaka kubaki ofisini, haikuwa taarifa nzuri hata kidogo kwani
viongozi wake walitaka kufahamu kila kitu akiwemo Dickson ambaye alihusika
katika kifo cha shahidi huyo, mzee Gombana.
Ofisini hakukukalika tena,
alichokifanya ni kuondoka ofisini hapo kuelekea nyumbani kwa marehemu. Hakwenda
peke yake, alikuwa na polisi kadhaa ambao wote kwa pamoja walichanganyikiwa kwa
kilichokuwa kimetokea.
“Haiwezekani, hapa kuna kitu,” alisema mkuu wa
kituo.
“Kweli mtu anaweza kufariki ghafla? Tena kwenye kipindi
tunachomuhitaji sana?” aliuliza polisi mmoja huku akimwangalia mkuu wake
usoni.
“Haiwezekani, hapa kuna kitu, subiri
tufike.”
Japokuwa barabara ilikuwa mbaya lakini dereva hakujali,
aliendesha kwa mwendo wa kasi huku wakitaka kufika msibani hapo haraka
iwezekanavyo. Kitu cha kwanza walichokuwa wakihitaji ni kuuchunguza mwili wake
kwani waliamini hakikuwa kifo cha kawaida, kulikuwa na mtu aliyekuwa amemuua
mzee Gombana kwa kutaka kuficha siri juu ya kile kilichokuwa kimetokea kule
msituni.
Bado muuaji wa msichana yule na mzee Gombana aliwachanganya,
hawakujua ni nani aliyekuwa nyuma ya mauaji yale, walichokuwa wakikifanya ni
kuhakikisha muuaji anapatikana haraka iwezekanavyo hata kabla wakuu wao
hawajachukua uamuzi mbaya.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika msibani
hapo, hata kabla gari halijasimamishwa, kama makomandoo, polisi wale wakaruka,
watu wote waliokuwa msibani wakashangaa, hawakujua sababu iliyowafanya polisi
hao wafike msibani hapo huku wakiwa na bunduki mikononi, amani iliyokuwepo
ikaanza kupotea.
Hawakuzungumza na mtu yeyote yule, walichokifanya ni
kuingia ndani na kuonana na wafiwa ambapo wakazungumza nao na kuwaambia kwamba
kabla ya mwili kuzikwa ilikuwa ni lazima ufanyiwe uchunguzi ili kuona kama
ulijeruhiwa sehemu yoyote au kulikuwa na kitu kingine kilichosababisha kifo
chake.
Hawakuwa na jinsi, japokuwa walipanga kufanya mazishi yake siku
hiyo ikabidi waahirishe ili polisi wafanye kazi yao. Mpaka siku iliyofuatia,
majibu ya uchunguzi yakatolewa na kuonesha kwamba mzee Gombana alikufa baada ya
kunywa sumu iitwayo Phenomenon iliyokuwa na nguvu ya kummaliza mtu kwa haraka
mno.
“Nani alimnywesha?”
“Hatujui, labda tumuulize mkewe,”
alisema polisi mmoja.
Hawakutaka kuchelewa, bado akili zao hazikuwa
sawa mpaka pale ambapo wangehakikisha kwamba kila kitu kinajulikana siku hiyo,
walichokifanya ni kurudi tena nyumbani ambapo huko wakakutana na mke wa
marehemeu na kuanza kuzungumza
naye.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kumnunua changudoa wa kwanza na kumgundua, Dickson akamuua na kumzika msituni.
Baadaye, kuna mzee alimuona lakini kabla hajatoa ushahidi, akaamua kumuua. Siri
imebaki kuwa siri. Baada ya wiki moja na nusu kupita tangu amuue changudoa yule,
Dickson amerudi tena kununua mwanamke kwa ajili ya kulala naye usiku kucha.Je,
nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Dickson alibaki akimwangalia changudoa
yule kimahaba, tayari uchu wa kufanya naye mapenzi ulikwishampanda. Vazi
alilovaa, sketi fupi ambayo iliishia mapajani mwake ilimuacha hoi, kila
alipokuwa akiyaangalia mapaja yake, akili yake ilichanganyikiwa
mno.
Kilipita kipindi cha wiki moja na nusu tangu mara ya mwisho
kumnunua changudoa ambaye mwisho wa siku aliamua kumuua kutokana na kumuona
usoni na kugundua kwamba alikuwa yeye, tangu siku hiyo mpaka siku aliyosimama na
msichana huyo, hakuwa amelala na msichana yeyote yule.
“Ingia basi
twende,” alisema Dickson.
“Twende
wapi?”
“Hotelini.”
“Mimi nataka tutumie hoteli ile pale,”
alisema msichana yule huku akiinyooshea kidole Hoteli ya Maradava iliyokuwa
pembeni ya eneo hilo.
“Jamaniiiii...”
“Ndiyo! Tena ile ni
bei chee”
“Za bei rahisi si nzuri, mimi nataka ile iliyokuwa ya
gharama, si unaona hata gari langu linaongea mimi ni mtu wa aina gani,” alisema
Dickson huku akijisifia.
Msichana yule alibaki njia panda, ni kweli
alikuwa na shida ya kuhitaji hela lakini kwenda mbali na mwanaume kwake
lilionekana kuwa tatizo kubwa. Kwa kipindi cha wiki nzima stori za rafiki yao
ambaye alikutwa amefukiwa porini ziliwatisha, wasichana wengi waliogopa kutoka
na mwanaume yeyote yule kwenda naye hotelini, kwa jinsi alivyokuwa Dickson,
msichana yule alijawa na hofu.
“Unajua kuna kitu kilitokea wiki moja
na nusu iliyopita ndiyo maana hatutaki kwenda mbali na sehemu hii,” alisema
msichana yule huku akionekana kuwa na hofu.
“Kama unaogopa, basi sawa
haina noma,” alisema Dickson, akapandisha kioo cha gari, akaliwasha kwa lengo la
kuondoka.
Biashara haikuwa ya uhakika sana, mara baada ya mwanamke
yule kuona kwamba mteja wake alikuwa siriazi kuondoka mahali hapo, akakipigapiga
kioo kisha Dickson kukiteremsha na kuanza kumsikiliza.
Kipindi chote
hicho changudoa yule hakujua kama mtu aliyekuwa akizungumza naye alikuwa Kamanda
wa Kanda ya Dar es Salaam kutokana na giza lililokuwemo ndani ya gari ambalo
halikuruhusu uso wake kuonekana kwa urahisi.
“Subiri
kwanza!”
“Nisubiri nini na wakati unaniletea pozi?”
“Naomba
unisikilize kwanza!”
“Wewe sema!”
“Niongezee hamsini!
Tutalala mpaka asubuhi!”
“Daah! Sawa! Haina noma! Ingia
twende!”
Changudoa yule akazunguka upande wa pili. Alipopita mbele ya
gari lile na taa kummulika, umbo lake lilionekana vizuri machoni mwa Dickson,
alikuwa msichana mrembo aliyeumbika, msichana aliyekuwa na nyonga zilizoweza
kumtia matatani mwanaume yeyote yule.
Dickson akameza mate kwa uchu,
kila alipomwangalia, jinsi alivyotembea na umbo lake kutingishika vilivyo,
alijikuta akipagawa mno. Alipoufikia mlango, akaufungua na kuingia ndani.
Dickson akashusha pumzi ndefu.
“Kumbe huwa kunakuwa na wasichana
warembo hivi!” alisema Dickson huku akiachia tabasamu.
“Kwani hujawahi
kuchukua msichana huku?”
“Ndiyo! Hii ni mara ya
kwanza.”
“Wazuri tupo, kama vipi tutabadilishane namba za simu ili
tuwe tunashtuana,” alisema msichana yule.
“Hakuna
tatizo!”
Dickson hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya
ni kutekenya ufunguo kisha kuliondoka gari. Kadiri walivyokuwa wakiendelea
kusonga mbele ndivyo uchu wa kufanya mapenzi ulivyozidi
kumshika.
Ndani ya gari kulikuwa na mwanga hafifu ambao haukumfanya
changudoa yule kumuona Dickson usoni, gari lilizidi kwenda na wala hakuwa na
shida ya kumuona kwani kitu alichokuwa akikitaka ni fedha tu na si kitu
kingine.
Njiani, Dickson alijipa uchangamfu mkubwa, alitawala
mazungumzo kwa kipindi kirefu mno, alihitaji changudoa huyo amzoee ili hata
watakapofika chumbani kusiwe na tatizo lolote lile. Hiyo wala haikuwa shida,
walizungumza mno kiasi kwamba ilionesha kama walikwishakutana tangu miaka mitatu
iliyopita.
Baada ya dakika kumi, gari likaanza kuingia katika nyumba
ya wageni ya Chenchebe iliyokuwa Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Alijua
kwamba alikuwa na fedha nyingi lakini kwa kuwa alikuwa kamanda wa jeshi la
polisi na kujulikana mno, kwenda hotelini aliona ni lazima angejulikana kutokana
na umakini uliokuwepo kwenye hoteli nyingi, hivyo alichoamua ni kutumia gesti
bubu.
Huko hakukuwa na uchunguzi, pamoja na kofia yake kubwa
aliyoivaa, akalipia kisha kuelekea chumbani huku akiwa amekishikilia kiuno cha
changudoa huyo. Walipoufikia mlango wa chumba hicho, wakaingia ndani, kama
kawaida hakutaka taa iwashwe, mwanga hafifu uliokuwa ukitoka kwenye taa ya nje,
uliwatosha mno.
“Huwa sipendi taa kabisa,” alisema
Dickson.
“Kumbe wewe kama mimi, sipendi pia,” alijishaua msichana yule
maneno yaliyoonekana kuwa uongo ila alitaka kuwa naye pasipo kujua sababu ya
mwenzake kutopenda mwanga wa taa. Hapohapo akamshika kiuno na kumvutia
kitandani.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea na tabia yake ya kununua machangudoa
pasipo watu kufahamu kwamba yeye ndiye aliyekuwa amefanya mauaji ya msichana
aliyeuawa siku kadhaa zilizopita.Je, nini kitafuatia? SONGA
NAYO…
Mzuka wa kufanya mapenzi ulikwishampanda Dickson, alimchukua
changudoa yule na kumvuta kitandani pale, akili yake ilichanganyikiwa, umbo zuri
na ngozi nyororo aliyokuwa nayo msichana yule ilizidi kumhamasisha kufanya naye
mapenzi mle chumbani.
“Subiri kwanza,” alisema msichana
yule.
“Kuna nini?”
“Mbona una haraka?”
“Sasa si
tumelipia short time, tufanye fasta,” alisema Dickson, hata sauti aliyoitoa
chumbani hapo ilionesha ni jinsi gani alikuwa kwenye mhemko mkubwa wa kufanya
mapenzi.
Dickson hakutaka kusikia kitu chochote kile, alichokuwa
akikitaka ni kufanya mapenzi tu. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa
kasi, damu ilizunguka kwa kasi mno, kilipita kipindi kirefu kufanya mapenzi
kabla ya siku hiyo, ule mzuka wa wiki mbili zote alikuwa nao ulimzidi
nguvu.
Alimchojoa changudoa nguo zake katika haraka ambayo hata yeye
mwenyewe aliishangaa, alipomaliza, akamlaza kitandani. Katika kila kitu
alichokuwa akikifanya mahali hapo hakutaka kugundulika kama alikuwa Kamanda wa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kila alipomgeuza huku na kule,
alihakikisha kwamba mwanga wa taa iliyokuwa nje haimpigi usoni
mwake.
Walitumia muda huo vilivyo, baada ya saa mbili baadaye, kila
mmoja alikuwa hoi, Dickson alibaki akimwangalia changudoa yule huku hata hamu ya
kuendelea hakuwa nayo kabisa.
“Kiasi gani?”
“Unataka unilipe
ipi? Ya mpaka asubuhi au short time?” aliuliza changudoa yule.
“Mpaka
asubuhi japokuwa nataka kuondoka.”
“Laki moja na
nusu.”
“Hakuna tatizo.”
Dickson akaivuta suruali yake na
kutoa pochi yake ambapo akaifungua na kuanza kuhesabu fedha zake. Hakukuwa na
hela ndogo, noti zote zilizokuwa ndani ya pochi ile zilikuwa ni elfu kumi tu,
hivyo akazihesabu mpaka zilipofika kiasi hicho akamgawia msichana
yule.
“Laki moja na nusu hii?” aliuliza msichana
yule.
“Ndiyo!”
“Mmmh! Usije ukawa umenipiga changa la macho,
ngoja niwashe taa nizihakikishe,” alisema msichana yule huku akisimama kitandani
pale. Dickson akamshika mkono.
“Baby...”
“Abee
kipenzi!”
“Huniamini?”
“Kwenye suala la fedha, hautakiwi
kumuamini mtu, hata shemasi tu anaiba sadaka kanisani” alijibu msichana
yule.
“Siwezi kukufanyia mchezo huo, niamini kipenzi. Kwanza hebu
andika namba yako hapa,” alisema Dickson, aliamua kuliingizia suala la namba
kwani hakutaka changudoa yule aendelee kuweka msisitizo wake juu ya kuwasha taa
ile.
Dickson akafanikiwa kumlaghai msichana yule na mwisho wa siku
hakuweza kabisa kuwasha taa ile kitu kilichomfurahisha sana Dickson. Mpaka
alipoamua kuondoka na kumuachia changudoa yule fedha za kutosha zaidi,
wakaahidiana kwamba kuanzia siku hiyo angekuwa mteja wake, yaani kuhusu suala la
fedha hakutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.
Kila siku usiku Dickson
alipokuwa akifika Sinza Mori, hakutaka kumchukua msichana mwingine zaidi ya
huyohuyo aliyejitambulisha kwa jina la Magreth, ila awapo kazini alipenda sana
kuitwa Mage.
Uwepo wa Dickson ukawa gumzo mahali hapo, machangudoa
wengi wakamfahamu kama mwanaume aliyekuwa akija na gari jeusi, kila walipoliona
usiku mahali hapo, walijua fika kwamba alifika mahali hapo kwa ajili ya
kumchukua Magreth, hivyo hawakutaka kumuingilia.
Katika kipindi cha
wiki mbili, Magreth hakuweza kugundua kwamba yule mtu aliyekuwa akimchukua kila
usiku alikuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Siku
zikaendelea kukatika, kutokana na fedha alizokuwa akizipata Magreth, akawa
changudoa aliyekuwa na maendeleo kuliko yeyote mahali hapo.
“Niitie
Magreth...” alisema Dickson, kama kawaida alikuwa amefika Sinza Mori kwa ajili
ya kumchukua Magreth na kuondoka naye kama kawaida yake.
“Hajafika!”
alijibu msichana mmoja aliyevalia kimini.
“Amekwenda
wapi?”
“Hajafika. Anaumwa tumbo!”
“Sawa!
Asante.”
“Hutaki huduma?”
“Nataka, ila kama
ye....”
“Hata mimi naweza kukupa huduma, tena zaidi ya huyo Mage,”
alisema msichana huyo.
“Kweli?”
“Kweli
kabisa.”
“Basi ingia twende nikaone,” alisema
Dickson.
Kutokuwepo kwa Magreth hakukuwa na tatizo lolote lile,
alichokuwa akikitaka mahali hapo ni kufanya mapenzi tu, hakujali chochote kile,
akamchukua msichana yule na kuanza kuondoka naye mpaka kwenye gesti bubu ya
Chenchebe iliyokuwa maeneo ya Mwananyamala. Walipofika, wakateremka na kuingia
ndani pasipo dada wa mapokezi kuhoji sana kwani alikuwa mteja wake ambaye
hakuwahi hatakumuona uso, alimzoea mno na hata wakati mwingine aliachiwa kiasi
fulani cha fedha.
“Nataka unionyeshee ulichonacho sasa,” alisema
Dickson.
“Usijali,” alisema msichana yule, akakifuata kitanda na
kuanza kujinyonganyonga maungo yake, alipomaliza akazivua nguo zake na Dickson
kumfuata pale kitandani.
“Anza na kifua changu kwanza,” alisema
msichana yule, kwa haraka pasipo kuuliza chochote Dickson akafanya kama
alivyoambiwa pasipo kujua kwamba huo ulikuwa mtego mkubwa, msichana yule alitaka
kumlevya na madawa ya usingizi aliyoyapaka
kifuani.
********************
********************
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya
sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Huko, tabia
yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa
mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja
anapokwend hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa
mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni
Kamanda Dickson.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Usiku
ulikuwa mkubwa, milio ya risasi ilisikika kila sehemu, watu waliokuwa ndani ya
nyumba zao, wakafunga milango na madirisha ili kuyaokoa maisha yao. Wale
waliokuwa wakipita njia kuelekea kule kulipokuwa na kituo kikubwa cha polisi
ambapo milio kadhaa ya risasi ilisikika, wakasimama na kurudi walipotoka, tena
wakikimbia kwa mwendo wa kasi.
Polisi walikuwa wakishambuliana na watu
waliokisiwa kuwa majambazi. Walifika kituoni hapo kwa malengo mawili tu, kuwaua
polisi kisha kuiba silaha kama walivyofanya katika vituo vingine vilivyokuwa
katika mikoa mingine.
Polisi hawakukubali, kwa kuwa nao walikuwa na
silaha nzito, wakaanza kushambuliana na majambazi hao walioonekana moto wa
kuotea mbali katika kutumia silaha hizo na hata ukwepaji wao.
Polisi
walidondoka chini, damu ziliwatoka, risasi zilipenya miilini mwao, hakukuwa na
aliyemuokoa mwenzake wakati huo, kila mmoja alikuwa bize kutetea nafsi yake,
majambazi wale waliendelea kuwamiminia risasi mfululizo.
“Wanakuja…”
alisema polisi mmoja, alionekana kuchanganyikiwa mno.
“Wapigie simu
makao makuu uwaambie tunahitaji msaada,” alisema polisi
mwingine.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, hapohapo akapiga simu, jina la
mtu lililomjia kichwani mwake ni Kamanda Dickson, hapohapo akampigia simu, simu
ikaanza kuita. Majambazi wale waliokuwa wamevaa kininja waliendelea kuwasogelea
polisi wale, eneo zima la kituo hicho likabadilika na kuwa uwanja wa vita. Ni
polisi watano ndiyo waliobakia kati ya polisi kumi waliokuwepo kituoni
hapo.
* * *
Dickson alikuwa na mhemko mkubwa, alipoambiwa
kwamba kifua cha changudoa yule kiliachwa kwa ajili yake, akaanza kukisogelea
pasipo kujua kwamba kilikuwa kimepakwa dawa ya usingizi, ili alewe na kukombwa
kila kitu.
Wakati akiwa tayari amekikaribia, mara akaanza kusikia simu
yake ikiita. Haikuwa kawaida kupigiwa simu usiku, hakuwa na familia, hakuwa na
marafiki wa karibu kutokana na ukali wake na hata polisi wake alikwishawaambia
kwamba hataki kupigiwa simu usiku mpaka kuwe na kazi kubwa hasa
majambazi.
Alihitaji muda wa kupumzika kutokana na kazi ngumu
alizokuwa akizifanya kila siku. Kitendo cha kusikia simu yake ikiita, alijua
kwamba kulikuwa na tatizo sehemu, hakutaka kuendelea, aliheshimu sana kazi
kuliko mapenzi, alichokifanya, huku akionekana kama mtu aliyeshtuka, akaifuata
suruali yake na kuichukua simu.
“Nani wewe?” aliuliza
kibabe.
“Mkuu! Tumevamiwa hapa Kituo cha Polisi cha Jangwani, tunaomba
utusaidie…” ilisikika sauti ya polisi mmoja simuni huku milio ya risasi
ikiendelea kusikika mahali hapo.
Hakutaka kuuliza kitu chochote kile,
tayari akajua kwamba kulikuwa na majambazi yaliyokuwa yamevamia kituo hicho.
Hiyo ndiyo hali iliyokuwa ikiendelea nchini Tanzania, vituo mbalimbali
vilivamiwa na polisi kuuawa kisha bunduki kuibwa, alichokifanya ni kuanza kuvaa
harakaharaka.
“Nini tena mpenzi?” aliuliza changudoa yule, wakati huo
alikuwa akimalizia kuvaa shati lake.
“Chukua hiyo,” alimwambia
changudoa yule huku akimtupia noti za shilingi elfu kumi kitandani, ilikuwa elfu
sabini.
Hakutaka kuchelewa, akatoka mle chumbani huku akikimbia kiasi
kwamba hata dada wa mapokezi alimshangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa
kimetokea chumbani mpaka Dickson kukimbia, alipojaribu kumuita, Dickson
hakugeuka, akalifuata gari lake, kitu cha kwanza kabisa akaangalia kama bastola
yake ilikuwepo pale alipokuwa akiiweka, akaiona, akawasha gari na kuanza
kuelekea huko.
Kutoka Mwananyamala mpaka Jangwani hakukuwa mbali, tena
kwa sababu alitumia gari binafsi huku ikiwa ni usiku sana ambapo hakukuwa na
magari mengi barabarani, aliendesha kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba baadhi ya
watu waliokuwa barabarani walimshangaa.
Alipofika Magomeni, kitu cha
kwanza akazima taa za gari lake na kuendelea kusogea kule kulipokuwa na kituo
kile. Bado milio ya risasi iliendelea kusikika mahali hapo, alipokaribia zaidi,
akasimamisha gari lake kisha kuteremka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kunyata
tena kwa kuinamainama huku akisogea kule kulipokuwa na kituo.
Mbele
kabisa, aliwaona wanaume watano wakitembea kuelekea kituoni huku wakiwa na
bunduki mikononi mwao. Hakutaka kujiuliza mara mbilimbili, akajua wale ndiyo
walikuwa majambazi na walikuwa wakikisogelea kituo huku wakipiga risasi,
hakukuwa na majibu kutoka kwa polisi hali iliyoonesha walikuwa wameishiwa
risasi.
“Paaa…paaa…paaa…” ilisikika milio mingine ya risasi mahali
hapo, alifyatua risasi tatu mfululizo, kutokana na shabaha aliyokuwa nayo,
hapohapo majambazi watatu wakaanguka chini, damu zikaanza kuwatoka shingoni na
vichwani mwao.
Wale wengine wawili wakaonekana kuchanganyikiwa, wenzao
walikuwa chini, hawakujua risasi zilitoka upande gani, walichokifanya ni kuanza
kurudi nyuma.
Mpaka kufikia hapo, Dickson akaona hiyo ndiyo ilikuwa
nafasi pekee, alichokifanya ni kuwasogelea kwa mwendo wa kuinama tena kwa kasi.
Majambazi wale waliokuwa wamepaki pikipiki zao pembeni, wakazichukua na
kuziwasha kwa lengo la kukimbia.
“Paaa…” ulisikika mlio mmoja wa
risasi, jambazi mmoja akadondoka chini.
Dickson hakutaka kuchelewa,
kwa mwendo wa kasi akamfuata jambazi aliyetaka kutimua mbio na pikipiki,
alipomkaribia, kama ndege, akamrukia kwa nyuma, wote wakadondoka
chini.
Jambazi akachukua bunduki yake ili amfyatulie risasi Dickson,
bunduki haikuwa na risasi, Dickson alipoichukua bunduki yake na kujaribu
kumfyatulia risasi jambazi yule, nayo haikuwa na risasi. Wakabaki wakiangaliana,
kilichobakia ni kuoneshana kazi kama wanaume, kila mmoja akakunja ngumi. Hiyo
ndiyo ilikuwa nafasi ya kila mmoja kuiokoa nafsi yake.
“Fight like a
man,” (Pigana kama mwanaume) Dickson alimwambia jambazi
yule.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Huko, tabia
yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa
mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja
alipokwenda hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa
mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni
Kamanda Dickson. Hata kabla hajafanya mapenzi na changudoa huyo, anapigiwa simu
na kuambiwa kituo kimoja cha polisi kimevamiwa.
Je, nini kitafuatia?
SONGA NAYO…
Walibaki wakiangaliana tu, hali ya ukimya ilikuwa
imetawala mahali hapo mara baada ya milio ya risasi kutawala sekunde chache
zilizopita. Dickson akabaki akimwangalia jambazi yule kwa umakini mkubwa huku
akionekana kuwa na hasira mno.
Tayari alikunja ngumi, kilichofuata ni
kumsogelea na kuanza kupigana. Mpaka kufikia hatua ya kuwa DCP wa Kanda ya Dar
es Salaam, alifanikiwa kupitia mafunzo mengi, kupambana kwa kutumia risasi au
kwa kutumia mikono na miguu.
Hakutaka kuchelewa, mara baada ya
kumsogelea jambazi yule ambaye alionekana kutokuwa na mafunzo yoyote ya
mapigano, akampiga teke moja zito la mbavu ambalo lilimfanya kupepesuka huku
kabla hajaamua nini cha kufanya akapigwa ngumi moja ya shavu ambayo ilimpeleka
chini moja kwa moja na kuanza kugaragara kwa maumivu makali.
Haikuwa
kazi kubwa, ni ndani ya sekunde thelathini, kila kitu kilikuwa tayari
alichokifanya ni kulichukua jambazi lile na kulipeleka kituoni ambapo askari
wenzake bado walikuwa wamejificha wakiogopa kupigwa
risasi.
“Kamanda..” aliita polisi mmoja aliyekuwa amejificha nyuma ya
meza kubwa ya kaunta, alikuwa na wenzake wawili, wakasimama na kuanza kupiga
saluti.
“Hebu liwekeni ndani kwanza,” alisema Dickson.
Mara
baada ya ukimya mkubwa kutawala hapo ndipo watu waliokuwa ndani ya nyumba zao
wakafungua milango na kutoka ndani kuona ni kitu gani kilichokuwa kimetokea.
Macho yao yakatua katika miili ya majambazi na polisi iliyokuwa chini huku damu
zikionekana kukauka.
Polisi waliokuwa mahali hapo wakaanza kuwazuia
raia wasisogee kule ilipokuwa miili ile. Ni ndani ya dakika kadhaa, tayari
polisi wengine wakafika kituoni hapo wakaichukua miili ya majambazi wengine na
kuondoka nayo.
“Nani kafanya haya yote?” aliuliza raia mmoja,
alionekana kutokuamini kilichotokea.
“Nilisikia polisi mmoja akisema
ni kamanda Dickson,” alijibu raia mwingine.
“Kamanda
Dickson?”
“Ndiyo! Kama kweli ni yeye, huyu mtu kweli hatari, tukipata
makamanda watano tu kama yeye, mbona amani itakuwepo,” alidakia raia
mwingine.
Siku iliyofuata, vyombo mbalimbali vya habari vikaanza
kutangaza kilichotokea katika Kituo cha Polisi cha Jangwani, kila aliyesikia
hakuamini, kitendo cha kishujaa alichokifanya kamanda Dickson kiliendelea
kuwaonesha watu ni jinsi gani alikuwa shupafu.
Sifa zake ziliendelea
kutapakaa kila kona, kila alipoitwa alipongezwa kwa kazi kubwa aliyokuwa
ameifanya ambayo kwa namna moja au nyingine ilionesha namna alivyo hatarisha
maisha yake kwa ajili ya kuleta heshima katika kazi ngumu ya
kipolisi.
Japokuwa alionekana kuwa mwanaume shupavu, mwenye umakini
mkubwa awapo kazini lakini bado tatizo lake lilikuwa palepale kwamba alikuwa mtu
wa kupenda kununua mno machangudoa barabarani pasipo kujulikana.
Sura
yake ikamfanya kukosa mke, hakupendwa na wanawake wengi kwani pamoja na sura
yake mbaya bado wengine walimuogopa kutokana na matukio aliyokuwa akiyafanya
kila majambazi walipokuwa wakifanya uhalifu sehemu fulani.
* *
*
Alikuwa miongoni mwa wanawake wazuri, waliojaliwa kuwa na umbo zuri
ambalo watu wanaojua jinsi mwanamke alivyo, wangeliita umbo namba nane. Uzuri
wake ulimvutia kila mtu aliyekuwa akimwangalia, alikuwa na sura nyembamba, lipsi
nene huku macho yake muda wote yakionekana kuwa mazito kama mtu aliyekuwa na
usingizi mzito.
Kwa jina aliitwa Pamela Samsoni, msichana mwenye kimo
cha wastani, mweupe na mwenye mwendo wa maringo mithili ya twiga. Katika Mtaa wa
Sakina jijini Arusha alipokuwa akiishi, Pamela alikuwa gumzo kila kona,
alipendwa na wanaume wengi, kila alipopita, alipokuwa akipigiwa miluzi, kwa kasi
ya ajabu kama feni izungukayo, aligeuka na kuangalia mluzi
ulipotoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Japokuwa alikuwa
mzuri mno aliyewatetemesha wanaume wengi lakini hakuuthamini uzuri wake, alikuwa
radhi kulala na mwanaume kwa kuwa tu alichokiangalia ni pesa. Alipendwa na watu
wenye fedha, hakutaka kujua mwanaume alikuwa mzuri kiasi gani, kitu cha kwanza
alichokuwa akitaka kuona ni mifuko na pochi, zilikuwa zimetuna au
zilidhoofika.
“Umeumbika vizuri, una sura nzuri, kwa nini usiolewe?”
aliuliza mwanaume mmoja, alikuwa akimwangalia Pamela kwa macho ya
matamanio.
“Una sura nzuri, kifua kipana, kwa nini usioe?” naye
alimrudishia swali mwanaume huyo.
“Mmh! Aya nimeelewa unamaanisha
nini.”
Alikubalika mitaani, alipendwa kila kona, si kwa wanaume tu
bali hata wanawake waliokuwa wakimwangalia Pamela walisema wazi kwamba alikuwa
miongoni mwa wasichana wazuri mno. Mbali na uzuri aliokuwa nao, tabia ya kujiuza
kwa wanaume mbalimbali, Pamela alikuwa na udhaifu mmoja tu.
Alipokuwa
akimpenda mwanaume, alimpenda haswa, katika mapenzi, alikuwa na hasira za
karibu, kumshambulia mtu kwa ajili ya mapenzi ilikuwa moja ya sehemu ya maisha
yake. Wanawake wengi walilifahamu hilo, kila mwanaume aliyekuwa akimpata,
hakukuwa na mtu aliyemuingilia kwani waliujua fika ukorofi wake, walijua namna
ambavyo binti huyo alikuwa radhi kukurushia chupa ilimradi mwisho wa siku ujutie
kitendo cha kumchukulia mwanaume wake.
Siku zikaendelea kukatika huku
Pamela akiendelea kujiuza kwa mteja mmojammoja lakini baada ya kipindi cha miezi
sita, hapo ndipo alipoanza kujiuza karibu na Hoteli ya Chibuchibu iliyokuwa
jijini Arusha ambapo hapo alipata wateja wengi.
“Twende Mererani,”
alisema rafiki yake mmoja.
“Kufanya nini?”
“Sasa swali gani
hilo Pamela? Kwani unaweza kuchimba madini?” aliuliza rafiki yake
huyo.
“Kuchimba madini?”
“Sasa umeniuliza kufanya nini kwani
hujui kazi yako inayokuweka mjini?’ aliuliza rafiki yake huyo kwa sauti ya
chini.
Siku iliyofuata wakaanza safari ya kuelekea Mererani, bado
maisha ya kujiuza yalimsumbua, alikuwa radhi kuzunguka sehemu yoyote ile lakini
mwisho wa siku aweze kuingiza kiasi kikubwa cha fedha.
Huko alipokuwa
akienda na rafiki yake huyo, walikuwa na kazi moja tu, kujiuza kwa wanaume
waliokuwa na fedha nyingi baada ya kuuza madini yao. Kwake, hivyo ndivyo maisha
yalivyokwenda.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Huko, tabia
yake ya kununua machangudoa inaendelea kama kawaida. Akaweka mazoea na changudoa
mmoja aitwaye Magreth, kila alipokuwa akimhitaji, alimchukua. Siku moja
anapokwenda hapo, anaambiwa kwamba Magreth ni mgonjwa hivyo anamchukua changudoa
mwingine ambaye alikuwa na lengo la kumlevya chumbani pasipo kujua kama yule ni
Kamanda Dickson.
Je, nini kitafuatia?
SONGA
NAYO…
Hata kabla Pamela na rafiki yake hawajafika Mererani, tayari
watu wenye fedha zao wakapata taarifa juu ya ujio wao, stori iliyokuwa ikienea
tena kwa kasi kubwa ni kwamba msichana mrembo, mwenye umbo matata aliyekuwa
akikaa katika Mtaa wa Sakina, leo hii alikuwa akiingia Mererani kwa ajili ya
kuwasalimia wanaume wa sehemu hiyo.
Waliokuwa na fedha zao, wakaziweka
tayari, walikuwa tayari kwa kila kitu, hawakutaka kuona msichana huyo akifika na
kuondoka huku wakiwa hawajafanya kitu chochote kile, hivyo wakamsubiria kwa hamu
kubwa kama walivyomsubiria mbunge wao.
Ilipofika majira ya saa nane
mchana, Pamela akafika hapo Mererani, wanaume walipomuona tu, wakakiri kwamba
kweli msichana huyo alikuwa mrembo mno na alistahili kulitingisha Jiji la
Arusha.
Watu wenye pesa zao, waliopata mzigo wa maana wakaanza
kuwekeana madau wao wenyewe, kwa Pamela, ilikuwa furaha yake, alichokifuata
Mererani hakikuwa kitu kingine zaidi ya pesa tu. Alizaliwa akiwa maskini,
aliwalaumu sana wazazi wake na hivyo kupambana huku akijiahidi kwamba siku
atakapokufa, awe ameweka kiasi kikubwa sana cha fedha katika akaunti
yake.
Wanaume wakapangwa kwa zamu, leo Pamela alikuwa akilala na huyu
kesho na yule. Hayo yalikuwa maisha yake ya kila siku, hayakuanzia hapo Mererani
bali tangu alipokuwa Arusha Mjini alilala na wanaume mbalimbali.
Baada
ya kukaa kipindi cha mwezi tena huku akiwa amepata kiasi kikubwa cha fedha, hapo
ndipo alipopanga kwenda jijini Dar es Salaam. Hakuwahi kufika katika jiji hilo,
alisikia sifa nyingi kwamba lilikuwa jiji zuri, lenye starehe za kila aina,
hivyo naye alitaka kwenda huko.
“Ninataka kwenda Dar,” alisema
Pamela.
“Kufanya nini?” aliuliza rafiki yake.
“Kufanya hiki
ninachokifanya hapa,” alijibu Pamela.
“Mmmh! Shosti, yaani pamoja na
kupata fedha hapa bado unataka kwenda Dar?” aliuliza rafiki yake huku
akishangaa.
“Ndiyo! Sifuati fedha, ninataka kwenda kupaona, natamani
niishi sehemu Ikulu ilipo,” alisema Pamela huku akiachia tabasamu
pana.
“Sawa! Utafikia wapi?”
“Hilo nalo ni swali
jamani?”
“Ndiyo! Una ndugu?”
“Sina ndugu ila nina pesa,”
alijibu Pamela.
Hakutaka kubadilisha mawazo yake, alichokuwa
amekifikiria mahali hapo ilikuwa ni lazima kwenda jijini Dar es Salaam, alitaka
kufanya matanuzi, alitaka kuwa katika jiji lililosifika kwa starehe na kuwa na
wanaume wengi waliojua kuhonga.
Katika wiki ya mwisho kukaa Mererani,
aliamua kukusanya fedha nyingi mno, kila mwanaume aliyelala naye katika siku
hizo, alimlipa kiasi kikubwa cha fedha na baada ya siku kadhaa, alikuwa ndani ya
ndege akielekea jijini Dar.
Hakuwahi kufika huko, hakuijua mitaa ya
huko zaidi ya kuisikia tu. Hakuwa na presha, aliamini katika pesa kwamba
unapokuwa nazo kila kitu kitakwenda sawa. Baada ya saa kadhaa, ndege hiyo
ikaanza kushuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,
akateremka, hakuamini kama mwisho wa siku miguu yake ingekanyaga ardhi ya Jiji
la Dar, akaanza kupiga hatua na abiria wengine kuelekea katika jengo la uwanja
huo kwa ajili ya kuchukua mabegi yake, kila alipokuwa akitembea, hakuamini kama
alikuwa jijini Dar.
*****
Kama kawaida yake, Dickson alikuwa
amesimamisha gari lake pembezoni mwa baa maarufu ya Caspinho iliyokuwa Sinza
Mori jijini Dar. Macho yake hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule,
alionekana kuwa bize kumtafuta msichana fulani.
Wanawake wengi
walijipanga barabarani, kila mwanaume aliyekuwa akipita karibu na eneo
walilosimama, walimfuata na kumwambia kiasi walichokuwa wakijiuza, ili kama
mnunuzi asimame na kununua na kama si mnunuzi basi aendelee na safari
yake.
Machangudoa wengi walioliona gari la Dickson, hawakutaka
kulisogelea, walizoea kuliona mahali hapo, mara kwa mara alikuwa akifika na
kumchukua changudoa mmoja ambaye kwa siku mbili tatu hakuwepo, changudoa huyo
alikuwa Magreth.
Aliendelea kuangalia huku na kule, mara kwa mbali
akamuona msichana mmoja akimfuata, akamwangalia vizuri, hakuwa mgeni, alikuwa
Magreth ambaye alikuwa akitembea kwa kasi kumfuata kule aliposimamisha gari
lake, alipofika, akaufungua mlango na kuingia ndani.
“Nimekumisi
mpenzi,” alisema Magreth kwa sauti ndogo, garini kulikuwa na mwanga hafifu mno,
hakuweza kumuona vizuri Dickson.
“Nimekumisi pia, upo tayari?”
aliuliza Dickson.
“Ndiyo! Ushindwe wewe tu,” alisema Magreth, hapohapo
akawasha gari na kuondoka.
Njiani walizungumza mengi, walizoeana na
kuwa marafiki wa damu, Dickson alikuwa na maswali mengi mno, yote hayo alitaka
kufahamu mahali alipokuwa Magreth kipindi cha nyuma kwani alifika mahali hapo
mara ka mara lakini hakuwa akimkuta.
“Niliumwa sana, ila kwa sasa nipo
fiti,” alisema Magreth.
“Hahaha! Usije ukanifia
kitandani.”
“Usijali kipenzi,” alisema Magreth, muda wote huo alikuwa
akiongea kwa sauti ya kimahaba.
Walipofika katika gesti ya Chenchebe
iliyokuwa Mwananyamala A, wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Dickson akalipia
na kuingia ndani huku akiwa amemshikilia kiuno Magreth, tena kofia ikiwa
kichwani mwake.
Walipoingia chumbani, hata kabla ya kufanya kitu
chochote, Dickson akachukua taulo na kuelekea bafuni kuoga. Alitaka kujiandaa
hata kabla ya kufanya kile kilichompeleka ndani ya gesti ile.
Wakati
anatoka, huku akiwa amejisahau, tena taa ikiwaka, macho yake yakatua usoni mwa
mhudumu wa kike wa gesti ile aliyekuwa akielekea chooni. Macho ya mhudumu yule
yalipotua usoni mwa Dickson, akaonesha mshtuko mkubwa, akakumbuka kwamba hata
kofia yake aliisahau bafuni.
“Mungu wangu! Kamanda Dickson..!!”
alisema mhudumu yule huku akionesha mshtuko wa waziwazi. Dickson
akachanganyikiwa, akajikuta akirudi bafuni haraka kuchukua kofia yake na kuanza
kumtafuta yule mhudumu.
Licha ya kumtafuta mapokezi na nje ya gesti
hiyo, hakuweza kumuona yule mhudumu, akaanza kuiona aibu ikianza kumsogelea.
Akapagawa!!
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea na tabia yake ya kununua machangudoa na
kwenda nao gesti. Siku moja akiwa huko na changudoa aliyeitwa Magreth, ghafla
mhudumu wa gesti hiyo anamuona na kugundua kwamba alikuwa DCP Dickson, anashtuka
mno na kuanza kukimbia.
Je, nini kitafuatia? SONGA
NAYO…
“Samahani kaka!”
“Bila samahani!”
“Nataka
nifike kwenye hoteli moja ya kawaida.”
“Poa! Panda twende! Unataka ya
chumba kiasi gani kwa siku?”
“Hata elfu
thelathini!”
“Umefika! Ingia!”
“Ipo
wapi?”
“Kinondoni, kuna hoteli nzuri tu, usijali.”
Pamela
alikuwa akizungumza na dereva ambaye alikuwa nje ya teksi yake iliyokuwa imepaki
nje ya jengo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Macho yake yaliangalia huku
na kule, hakuamini kama pale alipokuwa kwa kipindi hicho alikuwa jijini Dar es
Salaam.
Alilisikia tu jiji hilo alipokuwa Arusha, aliambiwa kwamba
lilikuwa jiji la raha lenye wanaume wengi waliojua kuhonga huku kukiwa na
starehe za kila aina na ndiyo maana katika kipindi hicho aliamua kufika jijini
humo ili kushuhudia kile alichokuwa amekisikia.
Gari likaanza safari,
katika njia nzima, Pamela alikuwa akiangalia huku na kule, kulikuwa na idadi
kubwa ya watu. Alihitaji kulizoea jiji kwani aliamini kwamba humo ndimo
yangekuwa maisha yake yote katika miaka yote.
Walichukua dakika
arobaini na tano ndipo wakaingia katika Hoteli ya Swing iliyokuwa Kinondoni B.
Mlango ukafunguliwa na Pamela kuteremka, akamlipa dereva kiasi cha fedha
alichokuwa akikihitaji kisha kuelekea mapokezi.
Hakuwa mshamba wa
hoteli, aliwahi kukaa katika hoteli nyingi, zenye gharama kubwa na kulala chumba
chochote alichokihitaji, kuwa ndani ya hoteli hiyo kwake lilionekana kuwa suala
la kawaida. Macho yake hayakutulia, bado alikuwa akiangalia huku na kule,
alitamani kuyazoea mazingira kwa haraka sana ili pale atakapoanza kufanya kazi
basi asiweze kupata shida yoyote ile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipopewa chumba na
kuelekea chumbani, akalala kitandani, mawazo yakamsonga, akili ikachemka.
Alikuwa ndani ya jiji jingine, alikuwa mgeni, hakumfahamu mtu yeyote yule,
kwake, kila kitu kilikuwa kigeni. Hakujua ni wapi angeanzia kufanya biashara
yake ya kuuza mwili, hakujua viwanja, kiwanja pekee alichokuwa amekisikia ni
kile kilichoitwa Kinondoni Makaburini ambacho hakujua kilikuwa mahali
gani.
Usiku hakutaka kukaa ndani, akatoka nje ili kuona ni kitu gani
kilichokuwa kikiendelea. Nje ya hoteli ile aliwaona wasichana wengi wakiwa
wamesimama pembezoni, walivalia nguo fupi na kuyaacha mapaja yao wazi kabisa
huku wengine wakiwa wameshika sigara.
Hakutaka kujiuliza hao walikuwa
akina nani, kitu kilichomjia kichwani ni kwamba wanawake wale aliokuwa amewaona
walikuwa machangudoa kama alivyokuwa.
“Kumbe hapa napo kuna biashara,
nitaanza kufanya,” alisema Pamela.
Kitu alichokifanya hata kabla ya
kuanza kufanya biashara hiyo ni kumtafuta msichana ambaye aliamini kwamba
kupitia yeye angeweza kumwambia mambo mengi ili hata siku atakapoanza kufanya
biashara hiyo asiweze kupata usumbufu wowote.
“Wapi kupo poa tu, kodi
yako ndiyo inahitajika,” alisema msichana huyo.
“Hiyo kodi inalipwa
wapi?”
“Paleee…kwenye ile kaunta. Kama mnunuaji atakuwa bahili,
utawaambia wenye Bajaj, wote watu wetu, unaweza kumalizia shida zako humo,”
alisema changudoa huyo, maneno hayo yakamwingia akilini
Pamela.
*****
Hakukuwa na siku ambayo Dickson
alichanganyikiwa kama siku hiyo, msichana wa mapokezi ambaye alimuona uso wake
na kumgundua hakuwepo, alikimbia na kwenda kusipojulikana. Dickson akarudi
chumbani kwake, alionekana kuwa na haraka mno, kijasho chembamba kikaanza
kumtoka japokuwa alitoka kuoga.
“Vipi tena?”
“Unasemaje?”
aliuliza, hata hakumsikia vizuri Magreth, tayari alianza kuvaa nguo zake
haraka.
“Mbona unavaa nguo?”
“Nimepigiwa simu
nimefiwa!”
“Umefiwa? Hiyo simu umepigiwa wapi na wakati ilikuwa kwenye
nguo yako?” aliuliza Magreth.
“Subiri kwanza. Ni lazima
niondoke.”
Uondoke tena?”
“Ndiyo!”
Hakutaka
kuzungumza sana, kichwa chake kilichanganyikiwa, kitendo cha msichana yule wa
mapokezi kuondoka na kuelekea asipopafahamu kilionekana kuwa tatizo kubwa kwa
upande wake, hakutaka kubaki ndani ya chumba kile.
Alichokifanya ni
kumpatia Magreth kiasi cha shili laki moja kisha kutoka mle chumbani kwa
kasi.
Alipofika mapokezi, msichana yule hakuwepo, alichanganyikiwa
zaidi, hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kuelekea nje.
Alijua kwamba msichana yule hakuwa mtu wa kukaa mbali na gesti ile, alikuwa na
uhakika alikuwa akiishi karibu na maeneo hayo.
Huku akiwa na kofia
yake kichwani, akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika upande
waliokuwepo wanaume fulani waliokuwa wamekaa wakipiga stori kwenye banda la
muuza chipsi. Alipowafikia, akawasalimia na kuanza kuzungumza
nao.
“Kuna dada namuulizia,” alisema Dickson huku akiwaangalia wanaume
hao, hawakuwa wakimtambua kutokana na giza pamoja na ile kofia kubwa aliyokuwa
ameivaa.
“Dada yupi?”
“Yule anayehudumia kwenye ile gesti!
Mnamfahamu?”
“Nani? Fatuma?”
“Sijui, ni mweupe, mrefu kidogo
ana kidoti hapa karibu na pua.”
“Ni Fatuma huyo! Anaishi nyumba ile
pale.”
“Ipi?”
“Ile inayowaka taa nyekundu yenye bustani ya
maua kwa nje,” alisema kijana mmoja.
“Asante sana.”
“Kwani
kuna nini braza? Tumemuona ametoka huku akikimbia!”
“Hakuna kitu,
asanteni,” alisema Dickson na kuanza kupiga hatua kuelekea kule ilipokuwa nyumba
ile. Hakuonekana kuwa na masihara, alichokuwa amekipanga, ilikuwa ni lazima
Fatuma
afe.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa na kuwa DCP Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Dickson anaendelea na
utaratibu wake wa kununua machangudoa mitaani. Akiwa kwenye harakati hizo
anakutana na changudoa mmoja aitwaye Magreth, wanakuwa marafiki na kila
anapofika pa kununulia machangudoa, anamtafuta Magreth kwani ndiye
aliyemzoea.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Dickson aliendelea
kuisogelea nyumba ile, alichokuwa akikitaka ni kumuona Fatuma tu, yule msichana
wa mapokezi kwani alihisi kama angemuacha ilikuwa ni lazima kutoa siri kwamba
alikwenda katika gesti ile usiku akiwa na mwanamke kitu ambacho kwake alikiona
kuwa aibu kubwa.
Mishipa ya shingo ilimsimama, mzunguko wake wa damu
ukazidi kuongezeka mwilini mwake, alikuwa na hasira iliyochanganyikana na hofu
kubwa kwa kuhisi kwamba ilikuwa ni lazima kwa mtu kama Fatuma kuwaambia watu
kile alichokiona mle ndani.
Alipoifikia nyumba ile, hakutaka kupiga
hodi, kwanza akatulia na kusikiliza ndani kama kulikuwa na sauti za watu
waliokuwa wakiongea, aliposikiliza kwa kutegesha sikio lake, ukimya mkubwa
ulitawala.Alichokifanya ni kuanza kuusogelea mlango wa kuingilia ndani, alitaka
kuufungua na kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa na vyumba vingi vya kupanga.
Alijaribu kuusukuma mlango, haukufunguka.
“Ngoja...” alijisemea,
alichokifanya baada ya hapo ni kuanza kupiga hodi. Alitaka kufunguliwa mlango,
aingie ndani kisha kutekeleza kile alichotaka kukifanya mahali hapo. Haukuchukua
muda mrefu, mlango ukafunguliwa, mwanaume mwenye kipensi akatoka
ndani.
“Karibu,” alisema kijana yule huku macho yake yakiwa mazito kwa
usingizi.
“Fatuma yupo?” aliuliza Dickson hata kabla ya
salamu.“Fatuma! Sasa hivi? Mmmh! Sidhani! Hebu subiri,” alisema kijana yule,
akarudi ndani.
Dickson hakutaka kubaki pale mlangoni, akaanza kumfuata
kijana yule kwani alijua dhahiri kwamba endapo msichana huyo angejua kwamba
kulikuwa na mtu aliyekuja kumuulizia, ni lazima angesema hayupo, ili kumkamata
kirahisi, naye akaanza kumfuata kijana yule ambaye aliishia katika mlango wa
chumba kimoja na kuanza kuugonga huku akiliita jina la Fatuma.
“Hayupo
kaka! Kwanza huwa harudi muda huu,” alisema kijana yule.
“Huwa anarudi
muda gani?”
“Mpaka asubuhi! Analala hukohuko kazini
kwake.”
“Ila kuna vijana wameniambia amekuja huku!”
“Mmhh!
Sidhani! Au amekwenda kwa bwana wake, kwa sababu huko ndipo huwa anakwenda,”
alisema kijana yule.
“Anaishi wapi?”
“Nani? Huyo bwana
wake?”
“Ndiyo!”
“Hapo mbele, kuna nyumba fulani hivi
kalikali, ila kuwa makini, kuna wavuta bangi wengi wasije wakakutoa roho,”
alisema kijana yule kama kumtahadharisha.
“Usijali.”
Kila
kitu alikifanya harakaharaka, hakutaka kupoteza muda, kwa kuwa alikwishaambiwa
juu ya nyumba ambayo ilisemekana kuwepo kwa Fatuma, akaanza kwenda huko.Hakutaka
kusikia kitu chochote kile, kile alichokitaka ni kumuua msichana huyo tu.
Aliifikiria nchi ya Tanzania, akawafikiria watu wake, akaifikiria heshima
aliyojijengea na kukumbuka siku alizokuwa akiongea kwa msisitizo kwamba
machangudoa wote wakamatwe kwani hakupendezwa na uwepo wao, kweli walikamatwa,
sasa leo hii, yeye mwenyewe alionwa gesti akiwa na changudoa, alijaribu
kuiifikiria aibu yake, ilikuwa kubwa mno.
Nyumba ile haikuwa mbali
sana na alipotoka, baada ya dakika mbili, akafika na kulifuata geti. Pua yake
ikaanza kunusa harufu kali ya bangi iliyotoka ndani ya nyumba hiyo, hapo akajua
kwamba hiyo ndiyo nyumba aliyokuwemo msichana Fatuma hivyo hakutakiwa kugonga,
alitaka kuingia moja kwa moja ndani.
Ndivyo alivyofanya, geti
lilifungwa ila kwake haikuonekana kuwa tatizo, akauparamia ukuta na kurukia
ndani, akaanza kupiga hatua kuelekea kulipokuwa na chumba ambacho kwa nje
kilikuwa na viatu vingi. Hata kabla hajaingia, akaanza kusikiliza ndani kulikuwa
na watu wangapi, alizisikia sauti ambazo zilimpa uhakika kwamba watu waliokuwamo
mle ndani hawakuzidi watatu.
Akakishika kitasa, akajaribu kuufungua
mlango, ukafunguka, hapohapo akaanza kuingia ndani kwa mwendo wa kunyata. Taa
ilikuwa inawaka, alipoingia tu, macho yake yakatua kwa vijana watatu waliokuwa
wamekaa kitandani, walikuwa wakivuta bangi huku pembeni yao kukiwa na karatasi
iliyokuwa na madawa ya kulevya.
“Oyaa! Mbona unaingia bila hodi
mwana?’ aliuliza jamaa mmoja, kila mmoja alikuwa amelewa kutokana na kubwia
madawa yale na kuvuta bangi kwa kiasi kikubwa.
“Fatuma yupo
wapi?”
“Nani? Fatuma! Wewe nani mpaka umuulizie demu wangu?” aliuliza
kijana mmoja kwa sauti yake ya kilevi.
Hakuwa na muda wa kupoteza
mahali hapo, kuulizwa maswali yasiyokuwa na msingi, maswali aliyojua kabisa
kwamba yaliulizwa na mtu aliyefahamu fika alizungumzia nini, akajikuta zile
hasira alizokuwa nazo zikiongezeka zaidi.
Akakunja ngumi na
kuwasogelea vijana wale kitandani pale kisha kuanza kuwapiga ngumi mfululizo.
Alikuwa na nguvu, alipitia mafunzo makali hivyo kuwapiga vijana hao watatu
halikuwa tatizo kabisa, aliwashushia ngumi mfululizo.
“Fatuma yupo
wapi?’ aliuliza huku akiwa amekasirika mno.
“Yupo bafuni anaoga,”
alijibu kijana mmoja, uso wake ulikuwa umejaa damu.
Alichokifanya
Dickson ni kuchukua ufunguo wa chumba hicho, akatoka ndani kisha kuufunguka
mlango kwa nje na kuelekea bafuni. Akaanza kupiga hatua kulifuata bafu ambapo
kulisikika sauti ya maji yaliyokuwa yakimwagika,
kaufuata mlango,
hakutaka kupiga hodi, akaupiga teke, ukavunjika, naye akaingia ndani. Macho yake
yakagongana na macho ya Fatuma aliyekuwa akioga.
“Naomba
unisamehe...sitomwambia mtu,” alisema Fatuma mara baada ya kugundua kwamba yule
aliyeingia bafuni alikuwa kamanda Dickson.
“Hakuna siri ya watu
wawili, ili siri itunzwe, lazima mmoja afe,” alisema Dickson, hapohapo
akamsogelea Fatuma na kuanza kumkaba. Japokuwa msichana huyo alianza kukukuruka
lakini Dickson hakuitoa mikono yake shingoni mwa Fatuma, alimkaba vilivyo,
alitaka kumuua
tu.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinunua machangudoa kwa kuwa tu hakuwa
na sura nzuri ya kumpata mwanamke. Kila anapokwenda kuwanunua, kofia kubwa
inakuwa kichwani mwake huku akimzuia msichana yeyote kumfahamu alikuwa nani na
kila aliyebahatika kumuona na kumgundua, ilikuwa ni lazima auwawe.
Je,
nini kitafuatia? SONGA NAYO…
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Pamela hakuishi
sana hotelini akafanikiwa kupata chumba katika nyumba moja ambayo haikuwa mbali
na eneo la Makaburini hapohapo Kinondoni. Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na
wanawake wanne ambao wote hao walikuwa na kazi ya kuuza miili yao nyakati za
usiku katika eneo la Majaburini.
Wakajikuta wakianza kuwa karibu naye,
Pamela alionekana kuwa msichana mrembo, mwenye sura nzuri na umbo matata ambalo
hata machangudoa hao walipomwangalia, walibaki wakimsifia tu.
Kuishi
ndani ya nyumba moja, wakajikuta wakianza kuwa marafiki, uchangamfu wa Pamela
ulimvutia kila mmoja, wakajikuta wakimuuliza maswali mengi mpaka pale
walipogundua kwamba mawazo yao yalikuwa sahihi kwamba msichana huyo alitaka kuwa
changudoa na kufanya kazi pamoja nao.
“Kwa hiyo umekuja kwa ajili ya
kazi hii?” aliuliza msichana mmoja, aliitwa Juliana.
“Ndiyo! Ila kule
hotelini wameniambia nilipie,” alijibu Pamela.“Achana nao, wamekaa kitamaa na
hakuna wateja wengi, kama vipi njoo kambini kwetu,” alisema
Juliana.
“Wapi?”
“Makaburini.”
“Hakuna tatizo,
ninashukuru, kesho tutakuwa pamoja.”
Alifika jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kazi hiyo tu, alitaka kuwa na fedha nyingi, alitaka kuwa tajiri,
ajijengee heshima kubwa nchini Tanzania. Hakukuwa na kitu alichokitegemea kwa
wakati huo zaidi ya kujiuza tu.
Siku ya kwanza kufika katika eneo la
Makaburini, Pamela alikuwa gumzo, kila changudoa aliyemuona alishtuka, umbo lake
liliwaacha midomo wazi, miguu minene, ngozi yake yenye kung’ara na sura ya
kitoto iliwafanya machangudoa wote kumkubali na kumuonea wivu.
Kuanzia
siku hiyo, hapo ndiyo ilikuwa ofisi yake, kila siku usiku alifika hapo na
kujiuza kama walivyofanya wengine. Wale wateja wazoefu waliojiwekea mazoea ya
kufika makaburini hapo kununua machangudoa walipomuona Pamela walichanganyikiwa,
hawakuamini kama katika eneo hilo kungekuwa na msichana mrembo kama Pamela, umbo
na mvuto wake walizoea kuwaona wasichana wa namna hiyo katika klabu kubwa jijini
Dar au hata kwenye makasino mbalimbali.
“Mmmh! Wewe ni mgeni?”
aliuliza mwanaume mmoja, alikuwa mtu wa miraba minne, kichwani alinyoa upara,
pembeni alipaki gari lake la kifahari, kwa kumwangalia, alionekana kuyazoea
mazingira ya eneo hilo.
“Siyo sana, wiki yangu ya pili
hii.”
“Ooh! Kumbe, basi nilikuwa napitwa sana. Mbona sikuwa
nikikuona?”
“Mara nyingi huwa natoka na wateja.”
“Sawa,
hakuna tatizo. Gharama yako iko vipi?”
“Showtime au kuamsha
popo?”
“Kuamsha popo, mpaka asubuhi.”
“Elfu
hamsini.”
“Hakuna tatizo.”
Mara baada ya kukubaliana,
wakalifuata gari na kuingia ndani kisha kuondoka. Machangudoa wengine
walionekana kumchukia Pamela, tangu kufika kwake ndani ya eneo hilo, biashara
ikawa ngumu, wateja wengi waliofika mahali hapo, mtu waliyekuwa wakimtaka
alikuwa Pamela tu.
Safari iliendelea mpaka walipofika Upanga ambapo
gari hilo likasimama nje ya nyumba moja ya kifahari iliyozungushiwa ukuta. Mzee
yule akapiga honi, hapohapo mlinzi akafungua geti na kuanza kuliingiza gari
ndani. Pamela akabaki akiishangaa nyumba hiyo, ilikuwa ni ya kifahari sana,
ilionesha ni jinsi gani mzee huyo alivyokuwa na fedha.
* * * *
*
Hakukuwa na kitu kingine alichokuwa akikitaka zaidi ya kumuua
Fatuma. Hakutaka kuamini kama kulikuwa na siri ya watu wawili duniani, alikuwa
na uwezo wa kumuacha Fatuma lakini kwa jinsi alivyomuona msichana huyo, hakuwa
na moyo wa kutunza siri ile.
Hakutaka kujulikana, hakutaka kupata aibu
baada ya kugundulika kwamba hata yeye ambaye kila siku alikuwa mkemeaji mzuri wa
uwepo wa machangudoa naye alikuwa mmoja wa wanunuzi waliofika katika viwanja vya
machangudoa.
Alimkaba vilivyo, Fatuma alikukuruka huku na kule lakini
mkono wa Dickson haukutoka shingoni mwake, aliendelea kumkaba vilivyo. Wala
hazikuchukua dakika nyingi, Pamela akaanza kulegea, mapovu yaliyochanganyikana
na damu yakaanza kutoka mdomoni mwake, mishipa ikamtoka na hapohapo pumzi
ikakata na kufariki dunia.
Alichokifanya Dickson ni kuanza kuufuta
mwili ule kwa taulo la Fatuma kwa ajili kuficha alama za vidole vyake,
alipomaliza akatoka mle bafuni na kuondoka zake huku akiwa na uhakika kwamba
kile kilichokuwa kimetokea kingeendelea kuwa siri
milele.
*****
“Mnasemaje?”
“Kuna mwanaume aliingia
ndani jana usiku.”
“Mwanaume gani?”
“Mfupi kiasi fulani,
alikuwa na mwili uliojazia.”
“Unaweza kumfahamu hata
ukimuona?”
“Hapana! Alivalia kofia kubwa ya Marlboro, sikuweza kumuona
vizuri.”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu tena.”
“Na kwa
nini alimuua Pamela?”
“Sijui mkuu.”
“Sawa. Mpelekeni sero,
tutamhitaji tena. Mleteni mwingine.”
Vijana wale waliokuwa wakivuta
bangi na madawa ya kulevya katika nyumba aliyouawa Fatuma walifikishwa kituo cha
polisi kwa ajili ya kutoa ushahidi juu ya mauaji yaliyokuwa yametokea usiku
waliokuwa ndani ya nyumba ile.
Kila aliyeulizwa, majibu yake yalikuwa
yaleyale kwamba hawakuweza kumfahamu muuaji kwa sababu kichwani alikuwa na kofia
kubwa hivyo uso wake kutokuonekana vizuri. Polisi wakachanganyikiwa, mauaji yale
yaliwachanganya mno.
Mwili ulipelekwa katika chumba cha uchunguzi
hospitalini kwa ajili ya kumbaini muuaji kwa njia ya kuangalia alama za vidole
mwilini mwake lakini majibu yaliyotoka yalionesha mwili ulioshwa na kufutwa,
hivyo alama za vidole hazikuonekana kitu kilichowafanya polisi kugundua kwamba
mtu aliyefanya mauaji alifahamu mengi, hasa yote walivyokuwa wakifanya
wapelelezi. Kukaonekana kuwa na ugumu wa kumpata muuaji huyo. Hawakujua kama
kiongozi wao ndiye aliyehusika kwa kila
kitu.
********************
********************
Hali
ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa
machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani
ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna
anayejua walikopotelea.
Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi
kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira
yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la
kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye
anayehusishwa na wote wanaopotea.
Upande wa pili, kijana aliyekuwa na
mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake
walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za
mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta
machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
Mara baada ya
kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anaendelea kununua machangudoa sehemu mbalimbali na
kila changudoa anayegundua kwamba ni yeye, anamuua. Sasa hivi amekutana na
changudoa aitwaye Magreth, wametokea kuzoeana mno. Mbali na Dickson, upande wa
pili kuna changudoa aliyetoka Arusha, anaitwa Pamela, anasafiri kwenda Dar kwa
ajili ya kufanya biashara zake.
Je, nini kitafuatia? SONGA
NAYO…
“Unasemaje?” aliuliza kamanda Dickson huku akijifanya
kushtuka.
“Kuna mwanamke aliuawa jana, taarifa hizo zililetwa saa kumi
na mbili asubuhi,” alisema polisi aliyepeleka
taarifa.
“Wapi?”
“Mwanayamala.”
“Na muuaji
mmemkamata?”
“Hapana. Ila anaonekana kufahamu mambo mengi hasa
yanayohusu uchunguzi katika mwili wa marehemu. Tulijaribu kuchunguza ili tupate
hata alama za vidole, hatukuambulia kitu,” alisema polisi huyo.
“Kwa
hiyo baada ya hapo mkaamua tu mrudi ofisini, mkalie viti, mkunje nne na
mgongesheane glasi?” aliuliza Dickson.
“Hapana
mkuu.”
“Kumbe?”
“Bado tunalishughulia suala hilo, nakuahidi
baada ya wiki moja tutakuwa na majibu,” alisema polisi huyo.
“Sawa.
Nenda.”
Polisi yule alipotoka ndani ya ofisi yake, Dickson akashusha
pumzi ndefu, akakenua meno kwa furaha. Moyo wake ukafarijika baada ya kuona
kwamba alifanya mauaji na mpaka kipindi hicho polisi bado waliendelea kumtafuta
muuaji.
Hakuacha kwenda kununua machangudoa usiku, kila baada ya siku
tatu ilikuwa ni lazima kwenda huko na mtu ambaye alimchukua alikuwa Magreth.
Kwake alikuwa msichana mrembo lakini kitendo cha kumchukua mara kwa mara
kikamchosha, akahitaji kuwa na wanawake wengine.
Kumwambia Magreth
lilikuwa jambo gumu, alimzoea na hakujua ni kwa namna gani angeweza kumwambia
ili amchukue changudoa mwingine. Baada ya kuona ameshindwa kabisa, hapo ndipo
alipoamua kufanya maamuzi yaliyoonekana kuwa magumu kwake.
Siku hiyo
alipofika katika eneo la kununua machangudoa, kama kawaida yake alilisimamisha
gari lake mbali kabisa, akashusha kioo cha dirisha kisha kuchungulia nje.
Machangudoa walipoliona gari hilo, wakaanza kujipitisha mbele yake huku
wakiinadi miili yao, wengine walivaa suruali za jeans na wengine sketi fupi.
Dickson akatoa ishara ya kumuita changudoa mmoja, mwenye umbo namba nane huku
akiwa amezibana nywele zake kwa nyuma.
“Niambie baby,” alisema
msichana yule mara baada ya kulifikia gari lile.
“Umependeza sana,
nahisi nitakuwa mtu mwenye bahati sana kama nitapata huduma yako leo,” alisema
Dickson, kama kawaida kofia ya Marlboro ilikuwa kichwani mwake, mwanga hafifu
uliokuwa ndani ya gari ulimfanya kutokuonekana vizuri.
“Hakuna tatizo.
Laki mbili mpaka asubuhi.”
“Mmmh!”
“Nini
tena?”
“Mbona gharama?”
“Wewe unanionaje? Unalionaje hili
umbo? Hili ni umbo la kulipia vijisenti hivyo kweli baby wa mie?” aliuliza
changudoa yule, ikambidi Dickson amwangalie vizuri, alikuwa msichana mwenye umbo
la kuvutia mno.
“Ingia twende,” alisema Dickson, msichana yule
akaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea katika nyumba ya wageni
ikaanza.
* * *
Gari likaingizwa ndani, Pamela akabaki
akiliangalia jumba lile la kifahari, hakuamini kwamba kungekuwa na mtu ambaye
alimiliki jumba kubwa kama hilo tena ndani ya nchi kama Tanzania, nchi iliyokuwa
na wananchi wengi maskini.
Wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Muda
wote mzee yule aliyemnunua alionekana na furaha tele, kila alipokuwa
akimwangalia Pamela, alijiona kuwa miongoni mwa watu ambao wangefaidi usiku wa
siku hiyo.
“Twende tukaoge kwanza,” alisema mzee huyo, hivyo wakavua
nguo zao na kuingia bafuni.
Muda wote huo mzee yule alibaki
akimwangalia Pamela kwa macho ya matamanio, hakuamini kama kweli amekutana na
mwanamke aliyekuwa na umbo zuri kama alivyokuwa Pamela. Wasichana wa aina hiyo
hawakuwa wakipatikana kirahisi katika eneo kama Kinondoni Makaburini, wengi wao
walipatikana katika makasino makubwa, tena wakilipwa kwa dola kuanzia mia moja
kwenda juu.
Walipomaliza, wakatoka bafuni na kuelekea chumbani, huko,
mzee yule aliyeonekana kuwa na uchu mkubwa alibaki akimwangalia Pamela, hakutaka
kusikia kitu chochote kile, aliituliza akili yake ipasavyo na hata simu yake
aliizima, hakutaka kupata usumbufu wowote.
Baada ya kuvua nguo zote,
wakapanda kitandani, Pamela aligundua kwamba mzee yule alikuwa tajiri hivyo
alipania kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha anamteka kimapenzi.
Alijiandaa vilivyo mahali hapo lakini hata kabla hajafanya lolote lile, mzee
yule akaanza kujishika koo yake na kuanza kukukuruka kitandani pale kama mtu
aliyehitaji msaada hali iliyomfanya Pamela kushtuka.
“Nini tena?”
aliuliza Pamela, mzee yule alibaki akijikunjakunja huku mikono yake ikiwa
mdomoni.
“Give me Fluticasone,” (Nipe Fluticasane)
“What is
that?” (Ni nini hicho?)
“I am dying, give me Fluticasone,” (Ninakufa,
nipe Fluticasane) alisema mzee yule huku akionesha kidole chake katika droo
ndogo iliyokuwa pembeni mwa kitanda.
Mpaka kufikia hatua hiyo Pamela
alikuwa amechanganyikiwa, hakujua mzee huyo alikuwa akiumwa ugonjwa gani na hiyo
Fluticasane kilikuwa kitu gani. Kwa kuwa yule mzee alionesha kidole katika droo
ile ndogo, akaifungua na kuanza kuangalia ndani.
Alikutana na vitu
vingi, kulikuwa na dola zaidi ya elfu tano, kamera, bastola, picha na vitu
vingine vingi. Hakujua atoe kipi na aache kipi, alibaki akishangaa
tu.
“Fluticasone ndiyo nini?” aliuliza Pamela lakini hata kabla
hajajua nini cha kuchukua ndani ya droo ile, mzee yule akatulia kitandani, pumzi
ikakata, akafariki dunia, Pamela akapata
mshtuko.
********************
********************
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment