Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

JINI MWEUSI - 4

 





    Simulizi : Jini Mweusi

    Sehemu Ya Nne (4)


    ********************
    ********************
    Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akapandishwa vyeo na mwisho wa siku akajikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.

    Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.

    Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.

    Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.

    SONGA NAYO.

    Pamela aliogopa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya mahali pale, dawa ya Fluticasone aliyoambiwa aichukue hakuwa akiiona katika droo ile ya kitanda, alihisi kuchanganyikiwa mno. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hakujua ni kitu gani cha ziada alichotakiwa kufanya.

    Sekunde zilisonga mbele, alibaki akiendelea kupekuapekua ndani ya droo ile mpaka alipofanikiwa kukiona kikopo kimoja kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na dawa, kikopo kile kiliandikwa Fluticasone, kutokana na maelezo yaliyoandikwa katika kikopo kile, ndipo alipogundua kwamba hiyo ilikuwa ni dawa ya pumu.

    Wakati anamwangalia yule mzee kitandani, ndiyo alikuwa katika hatua ya mwisho kuvuta pumzi, dawa aliipata, hakujua namna ya kufungua kikopo kile, akabaki akihangaika kufanya hili na lile lakini kikopo hakikufunguka.

    “Kinafunguliwa vipi kutoa dawa?” alijiuliza lakini hakupata jibu.

    Wakati akijiuliza hayo, hali ya yule mzee iliendelea kuwa mbaya zaidi, hakuchukua muda mrefu, akatulia pale kitandani, pumzi ikakata na kufariki dunia. Wakati mzee huyo anakufa, Pamela hakuligundua hilo, aliendelea kuangalia namna ya kufungua kile kikopo, baadaye ndipo kumbukumbu ikamjia kwamba inawezekana zile dawa walizokuwa wakizitumia Wazungu kujipulizia mdomoni ndiyo ilikuwa kama ile.

    Alipoangalia pembeni na kubonyeza kwa juu, akaona dawa ikitoka, hakutaka kuchelewa, hapohapo akamsogelea yule mzee kisha kumuweka tundu la lile kopo mdomoni mwake kisha kubonyeza kwa juu, dawa ikatoka lakini alikuwa amekwishachelewa kwani tayari alifariki dunia.

    Hakuwa akimfahamu, siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kumuona lakini kifo chake kilimuhuzunisha mno. Alibaki akimuita pale kitandani lakini yule mzee hakuweza kuamka. Pamela akaogopa, hakutaka kubaki mahali hapo, kitu alichokifikiria muda huo ni kukimbia tu.

    “Siwezi kubaki,” alijisemea, hapohapo akavaa nguo zake harakaharaka na kuondoka mle chumbani, tena huku akikimbia, akafungua geti na kutokomea gizani, hata viatu alisahau kuvaa, alivishikilia mkononi.

    * * * *

    Kichwa cha Dickson kiliwaza mapenzi tu, hakufikiria kitu kingine mahali hapo, kwa kumwangalia msichana yule, alimtamani sana, hakuona kama kulikuwa na sababu ambazo zingemfanya kumuacha hivihivi.

    Pepo la ngono alilokuwa nalo lilimuweka kwenye wakati mgumu, hakufikiria kitu kingine chochote kile zaidi ya kulala na mwanamke huyo tu. Njiani, humo ndani ya gari alikuwa akizungumza naye, alitaka kuona akizoeana kabla ya kuingia ndani.

    Walichukua muda wa dakika ishirini ndipo walipofika nje ya nyumba moja ya wageni, wote wakateremka na kuanza kuelekea ndani. Muda wote huo Dickson alikuwa na kofia yake kichwani mwake, hakutaka kugundulika, hakukuwa na kitu alichokuwa akikihofia kama kugundulika kwani aliona kama hilo lingetokea ilikuwa ni lazima ashtakiwe hata kama alikuwa kiongozi mkubwa wa jeshi la polisi.

    Wakaingia ndani, akalipia kisha kuelekea chumbani. Walipofika humo, akamlaza kitandani msichana yule na kuanza kumwangalia kwa matamanio. Hakutaka taa iwake, aliogopa kugundulika, alichokifanya ni kuifuata swichi na kuizima.

    “Mbona unazima taa?” aliuliza mwanamke yule huku akionekana kuhamaki.

    “Sasa si ninataka tuanze kufanya kilichotuleta humu ndani,” alijibu Dickson.

    “Yaani tufanyie gizani?”

    “Ndiyo! Kwani kuna ubaya?”

    “Hapana! Kufanyia gizani siwezi,” alisema mwanamke yule huku akiinuka kitandani.

    “Kwani kuna tatizo gani kufanyia gizani?”

    “Raha ya chumbani tuonane, sasa giza la nini?” alisema mwanamke yule.

    “Sasa kama mimi mteja nahitaji giza!”

    “Hapana! Kwa giza siwezi kabisa.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akiyasema maneno hayo, tayari yule mwanamke alikwishaifikia swichi iliyokuwa mle chumbani na kuiwasha. Dickson akashtuka, mwanga mkali ukampiga usoni mwake, kofia haikuwepo kichwani mwake, alikuwa amekwishaiweka pembeni tayari kwa kulala na mwanamke yule.

    Alipoiwasha taa ile akarudi kitandani pasipo kumwangalia mteja wake, alipolala tu kitandani na kumwangalia mteja wake usoni, mwanamke yule akashtuka sana, mtu aliyesimama mbele yake alimfahamu vilivyo, alikuwa yuleyule mwanaume ambaye mara kwa mara alizungumza mbele ya waandishi wa habari akipinga sana wanawake kujiuza, yuleyule ambaye aliagiza machangudoa wote wakamatwe na wapigwe faini, alikuwa kamanda Dickson.

    “Aaah! Kamanda Dick,” alisema mwanamke yule kwa kuhamaki.

    Dickson akashtuka, hakuamini kama mwanamke yule alikuwa akimwangalia usoni, hakuwa na kofia wala miwani, alionekana kuchanganyikiwa mno.

    Yule mwanamke akasimama kitandani kwa lengo la kuondoka, alipoanza kupiga hatua, Dickson akamshika mkono.

    “Niachie niondoke,” alisema yule mwanamke.

    “Kwenda wapi?”

    Kumuacha hivihivi halikuwa jambo rahisi, hata kabla yule mwanamke hajafanya chochote akashtukia akipigwa kofi moja usoni, kofi lililompepesua na kujikuta akiangukia kitandani. Alichokifanya Dickson ni kumfumba mdomo wake kwa kutumia taulo lililokuwa kitandani na kuiziba pua yake.

    Yule changudoa alibaki akikukuruka lakini Dickson hakumuacha, aliendelea kumziba mdomo na pua yake kwa lengo la kumuua tu. Hakukuwa na kingine alichotakiwa kufanya, kugundulika na yule mwanamke aliamini kwamba kungemletea matatizo makubwa hivyo ili kuficha kila kitu kilichokuwa kimetokea ilikuwa ni lazima amuue.

    “Siku zote hakuna siri ya watu wawili, ni lazima ufe kama wenzako,” alisema Dickson.

    Mwanamke yule akatulia kitandani, shuka lilikunjikakunjika, mwili wake ulivimba, Dickson akaelekea bafuni, akalilowesha maji lile taulo kisha kuurudia mwili wa yule mwanamke na kuanza kufuta sehemu zote ambazo vidole vyake vilitumika kumgusa. Alipomaliza, akatoka nje.

    “Hapo nje si kuna chipsi?” alimuuliza dada wa mapokezi.

    “Ndiyo!”

    “Oke! Ngoja nikanunue kwanza, nakuja,” alisema Dickson, dada yule akakubaliana naye, akatoka nje na kulifuata gari lake, kilichosikika baada ya hapo ni muungurumo wa gari lililoanza kuondoka mahali hapo.


    ********************
    ********************
    Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akajikuta akipandishwa vyeo na mwisho wa siku akijikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.

    Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.

    Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.

    Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.

    SONGA NAYO...

    Taarifa zikaanza kusambaa Upanga kwamba kulikuwa na mwanaume aliyekuwa amekufa chumbani kwake. Kila mtu aliyezisikia taarifa hizo alishtuka, walimfahamu mzee huyo, alikuwa mzee mpole, aliyeheshimika ambaye alisumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu.

    Watu walihuzunika mno, wengi walisema kwamba pumu ndiyo iliyokuwa imemuua mzee huyo lakini baadhi ya watu wakaibuka na kusema kwamba mzee huyo alikuwa ameuawa. Hakukuwa na aliyejua ukweli halisi wa kifo chake.

    Polisi walipoingia ndani ya chumba chake waliukuta mwili wake ukiwa kitandani, alikuwa ameishika shingo yake na pembeni kulikuwa na dawa yake iliyokuwa kwenye kichupa, dawa iitwayo Fluticasone ambayo ilikuwa maalum kwa wagonjwa wa pumu.

    Pamoja na kukuta hali halisi ndani ya chumba hicho, hali iliyoonesha kwamba mzee huyo alikuwa amekufa lakini bado baadhi ya watu waliendelea kung’ang’ania kwamba mzee huyo alikuwa ameuawa jambo lililowafanya polisi kuanza kuhoji.

    “Mnasema ameuawa?” aliuliza polisi mmoja, alikuwa mbele ya vijana wanne.

    “Siyo sisi, ni walinzi wa maeneo haya,” alijibu kijana mmoja huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Walinzi gani?”

    “Wa nyumba zile kule,” alijibu kijana mwingine huku akizinyooshea kidole nyumba mbili.

    Polisi huyo hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuelekea kule kijana yule aliponyoosha kidole, alipoifikia nyumba moja miongoni mwa nyumba zile mbili, akapiga hodi ambapo mlinzi akaufungua mlango na macho yake kukutana na macho ya polisi.

    “Kwa nini unasema kwamba mzee Ibrahim ameuawa?” aliuliza polisi yule mara baada ya salamu.

    “Jana alikuja usiku kama saa nane hivi mzee Ibrahim alifika nyumbani kwake hapa na kuliingiza gari lake ndani ya ngome ya nyumba yake. Sikujua alikuwa na nani kwa sababu gari lake lilikuwa na vioo vyeusi,” alijibu mlinzi huyo kwa kirefu.

    “Ikawaje?”

    “Baada kama ya saa moja hivi, nikamuona msichana mmoja akitoka huku akikimbia, kilichotokea ndani, sikukijua na hata wenzangu hawakujua pia,” alisema mlinzi yule.

    Maelezo ya mlinzi yalikuwa muhimu kwani yule polisi aliamini kwamba yangeweza kufanikisha kukamatwa kwa muuaji huyo, alichokifanya ni kumchukua na kutangulizana naye kituoni kwa sababu ya kutoa maelezo zaidi.

    * * *

    Ukiachana na taarifa za kufariki kwa tajiri aliyekuwa akiishi Upaga, pia kukawa na taarifa zingine za mwanamke aliyeuawa ndani ya nyumba moja ya wageni iliyokuwa Mwananyamala. Polisi waliosikia tetesi hizo hawakubaki kituoni, wakaelekea mpaka katika nyumba hiyo ya wageni kwa ajili ya kushuhudia kilichokuwa kimetokea.

    Umati wa watu uliokuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni uliwapa uhakika kwamba kile walichokuwa wamekisikia kilikuwa kweli kabisa, wakateremka kutoka garini na kuelekea ndani huku wakiwa na bunduki zao mikononi.

    Msichana mrembo wa sura, aliyekuwa na umbo la kuvutia alikuwa kimya kitandani. Mapovu yalikuwa yamemtoka mdomoni, shuka lilikuwa limechafuliwa kwa haja kubwa iliyokuwa imemtoka mara baada ya kunyongwa na muuaji.

    Kila polisi aliyemwangalia msichana yule, alimkumbuka yule msichana Fatuma aliyenyongwa bafuni alipokuwa akioga. Watu wa kwanza waliotiwa hatihani walikuwa vijana waliokuwa chumbani wakivuta bangi, walichokisema ni kwamba aliyemuua Fatuma alikuwa mwanaume aliyevalia kofia kubwa kichwani.

    Haikuwa hiyo tu, hata alipouawa msichana mmoja porini na mzee aliyeshuhudia tukio lile kusema kwamba mtu aliyefanya mauaji alikuwa amevalia kofia kubwa kichwani, iliwapa uhakika kwamba mtu huyo ndiye aliyehusika katika mauaji ya watu hao wawili.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Leo hii kulikuwa na mtu mwingine aliyeuawa, alikuwa msichana mrembo ambapo kwa maelezo ya dada wa mapokezi alisema kwamba msichana huyo alikuwa akijiuza na alikuja katika nyumba hiyo ya wageni na mteja wake, kilichotokea, baadaye yule mwanaume akatoweka, hata sura hakuwa ameiona.

    “Kwa nini? Kwa sababu ya giza?”

    “Hapana! Alikuwa amevaa kofia,” alijibu msichana huyo.

    Polisi wakachanganyikiwa, mtu mmoja mwenye utambulisho wa kuvaa kofia alikuwa amefanya mauaji ya watu watatu kwa nyakati tofauti, polisi wakaanza kujiuliza juu ya mtu huyo kufanya mauaji hayo lakini hakukuwa na yeyote aliyefahamu.

    Wapo waliohisi kwamba muuaji alitumwa na mganga kuua ili kupata utajiri lakini kitu kilichowafanya kuyapuuzia mawazo hayo ni kwamba miili ya watu hao ilikutwa na viungo vyote, hakukuwa na kiungo kilichonyofolewa.

    Taarifa zikapelekwa kwa DCP Dickson, alichokifanya ni kuwaita polisi wawili waliokuwa katika kitengo cha upelelezi na kuanza kuwauliza juu ya kile kilichotokea katika upelelezi wao.

    “Kuna mtu anavaa kofia, huyo ndiye anayeua,” alisema polisi mmoja.

    “Yaani ishu ya kuvaa kofia mmeiona kuwa sababu kubwa? Wangapi wanavaa kofia? Yaani badala ya kuja na kuniambia kwamba muuaji ni fulani, mnakuja hapa na kuniambia muuaji anavaa kofia, kweli mnaweza kuniletea taarifa ya kijinga namna hii?” aliuliza Dickson huku akijifanya kuwa na hasira.

    “Tutafanya kazi kwa juhudi mkuu! Mpaka atakapopatikana,” alisema polisi mmoja.

    “Acheni uvivu, fanyeni kazi kama watu wanaotaka kufanya kazi, siyo mnakuja hapa na kuniambia mambo ya kofia,” alisema Dickson.

    “Sawa mkuu! Tutafanya hivyo,” alisema polisi mmoja kisha wote kwa pamoja kupiga saluti kama heshima, baada ya hapo wakaondoka.

    Dickson akarudi ofisini na kutulia kitini, uso wake ulijawa na tabasamu pana lakini kwa mbali alionekana kuwa na hofu mno. Alihisi kama angeweza kukamatwa kwani staili ya kofia aliyokuwa akiivaa ingemponza.

    “Ni lazima nitoke kivingine, siwezi kukamatwa kirahisi,” alisema Dickson huku akijipanga usiku wa siku hiyo atoke na kwenda kuonana na msichana mwingine maeneo ya Kinondoni Makaburini. Alitaka soko lake lihamie huko, hivyo akajipanga.


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
    Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
    Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa.  Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
    Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kumnunua changudoa, walipokuwa hotelini na kugundulika na changudoa yule kwamba ni yeye, anaamua kumuua na mwili kwenda kuuzika porini. Wakati anauzika, kulikuwa na mzee ambaye aliona kila kinachoendelea.
    Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
    Uzuri wake uliendelea kuwa gumzo, machangudoa wengine waliogopa kwa kuwa kila alipokuwa, hakukuwa na biashara nzuri kwa upande wao. Kila mteja ambaye alifika mahali hapo na kumuona Pamela, hakutaka kumuacha, alimfuata na kumnunua kisha kuondoka naye au wakati mwingine kumaliza shida zake katikati ya makaburi.
    Machangudoa wengi walimuonea wivu na wengine kumkasirikia, ili biashara zao ziende kama inavyotakiwa ilikuwa ni lazima Pamela aondoke mahali hapo kwani uwepo wake uliwaletea shida sana.
    Baadhi ya machangudoa wakakutana na kuanza kumjadili kwamba ilikuwa ni vizuri kumfukuza au wamuache. Katika kushauriana huko, wengine wakaona ilikuwa ni lazima aendelee kubaki kwani kwa wakati huo Pamela alikuwa kivutio, wanaume wengi walifika na walipomkosa, waliwachukua machangudoa wengine.
    Maisha yaliendelea kila siku, thamani yake ikaanza kupanda, akawa msichana mwenye bahati, alitengeneza kiasi kikubwa cha fedha mpaka pale alipokuja kukutana na mwanaume aliyemfuata huku akiwa na kofia kubwa kichwani, mteja aliyekuwa na muonekano wenye fedha ambaye kwake alijitambulisha kama muuzaji wa nafaka kutoka vijijini aliyejiita kwa jina la Mandingo.
    “Mandingo!” alisema kwa mshangao.
    “Ndiyo! Mimi ni Mkurya, huwa nasafirisha nafaka kutoka huko vijijini kuja huku mjini,” alisema mwanaume huyo.
    “Aisee! Kumbe nipo na bosi!”
    “Yeah! Nipo hapa kwa ajili ya kutumbua hela, zinaniwasha sana. Kwanza gharama yako inakwendaje?” aliuliza mwanaume huyo.
    “Kwa sababu wewe ni mfanyabiashara mkubwa, mwenye fedha, nitakufanyia laki mbili kwa usiku mmoja,” alisema Pamela.
    “Mmmh! Hakuna tatizo, kwa ajili yako, kwa jinsi ulivyo, nipo tayari,” alisema mwanaume huyo.
    Huyo hakuwa mfanyabiashara kama alivyojitambulisha, alikuwa Dickson ambaye aliamua kubadilisha kiwanja cha kuchukua machangudoa na kuhamia Kinondoni Makaburini. Alipomuona Pamela kwa mara ya kwanza, moyo wake ukafarijika, alifurahia moyoni mwake kwani kwa kipindi kirefu alichokitumia kununua machangudoa, hakuwahi kukutana na changudoa aliyekuwa na umbo zuri, sura nzuri kama alivyokuwa Pamela.
    Staili yake ilikuwa ileile, hakutaka kujulikana, kichwani alikuwa na kofia kubwa ya Marlboro huku kukiwa na mwanga hafifu ambao hata ulipompiga usoni, hakuonekana vizuri.
    “Unaishi wapi?’ aliuliza Pamela.
    “Naishi Msasani, ila hatutoweza kwenda nyumbani,” alijibu Dickson.
    “Kwa hiyo tutafanyia wapi? Garini?”
    “Hapana. Tutakwenda kuchukua chumba katika gesti moja uswahilini.”
    “Mmmh!”
    “Nini sasa?”
    “Umejisifia mfanyabiashara mkubwa, halafu tuchukue gesti! Kweli jamani baby? Kwa nini tusichukue hoteli kabisa?” aliuliza Pamela huku akionekana kushtuka kwa mbali.
    “Hahaha! Si unajua sisi wengine watu maarufu Tanzania, tukionekana, siyo poa kabisa,” alijitetea Dickson.
    “Basi sawa. Cha msingi hela tu,” alisema Pamela.
    Hakukuwa na muda wa kupoteza tena mahali hapo, alichokifanya Dickson ni kuliondoa gari mahali hapo na kuelekea katika gesti moja iliyokuwa Manzese Midizini. Hakutaka kwenda katika hoteli kubwa kwa kuwa alijua fika kwamba kugundulika ilikuwa rahisi sana tofauti na gesti bubu za mitaani.
    Huko, aliamini kwamba hakukuwa na ulinzi wa kutosha, wahudumu hawakuwa na umakini wowote ule kwa wageni waliokuwa wakiingia, zaidi, wao waliangalia fedha tu. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kutokugundulika katika kila gesti aliyokwenda kule Mwananyamala.
    Garini alikuwa mzungumzaji mkubwa, alitaka kuzoeleka kwa msichana huyo ili hata watakapofika chumbani kusiwe na maswali mengi. Hapohapo garini ndipo Dickson alipomwambia Pamela kwamba hakukuwa na kitu alichokichukia kama kufanya mapenzi katika chumba kilichokuwa na mwanga mkali wa taa.
    “Kwa nini?”
    “Basi tu, unajua sisi wengine tunakuwa na aibu kubwa sana.”
    “MmmH! Kweli makubwa, halafu si kwako tu, mpo wengi wa namna hiyo, sijui huwa mnaogopa nini,” alisema Pamela.
    Maneno hayo yakawa ahueni kwa Dickson, alijiona kuwa mshindi, kitendo cha Pamela kumwambia kwamba yeye hakuwa mmoja wake akawa na uhakika kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima kuzima taa ya chumbani na hatimaye kufanya mapenzi kama alivyokuwa amepanga.
    Hakuwa na hofu tena, alijua jinsi ya kucheza na wanawake hao, kuua, wala hakuogopa, alitaka kuona mambo yake yote yanakwenda sawa kama inavyotakiwa hivyo kunapotokea kizuizi chochote cha kuitunza siri ile, hakuhofia kuua hata kidogo.
    Waliendelea na safari mpaka walipofika katika gesti hiyo iliyokuwa Manzese Midizini, tena kwa kuingia ndani kabisa. Walipofika, akasimamisha gari na kisha kuteremka. Katika kipindi chote hicho alihakikisha kofia yake haitoki kichwani mwake.
    Vijana waliokuwa wamekaa pembeni mwa gesti hiyo walibaki wakimwangalia Pamela ambaye alikuwa akipiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo na Dickson ambaye hawakuwa wamemtambua kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Umbo lake liliwaacha midomo wazi, hawakuamini kama kulikuwa na mwanamke aliyekamilika kama alivyokuwa Pamela. Sura nzuri na yenye mvuto, umbo namba nane, hipsi kubwa ambazo vijana wa mitaani walipenda kuziita kwa jina la pisto.
    “Nahitaji chumba.”
    “Vipo. Show time au mpaka asubuhi?” aliuliza dada wa mapokezi.
    “Mpaka asubuhi.”
    “Elfu sita.”
    “Hakuna tatizo,” aliitikia Dickson, akalipia, wakapewa ufunguo na kuelekea huko chumbani. Wakati Pamela akifikiria fedha, hakujua kama alikuwa katika mikono ya mtu muuaji. Endapo angejua, asingekubali kuelekea gesti na mwanaume huyo.




    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam

    kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa

    katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa

    inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya

    machangudoa kumi na moja wanapotea na

    hakuna anayejua walikopotelea. Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia

    kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapoteaDa

    katika mazingira yanayofanana. Mwanaume

    mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari

    la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda

    eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa

    na wote wanaopotea. Upande Wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano

    tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson

    Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa

    wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es

    Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha

    kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda

    kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye

    anahamishiwa Dar es Salaam. Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson

    anajikuta akinogewa na penzi la changudoa

    mmoja aitwaye Pamela, umbo lake, ngozi

    vinamchanganya na kujikuta akianza kumganda

    pasipo kujua kwamba ukaribu wake na msichana

    huyo ungeweza kubadilisha kila kitu. Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO… Huo ulikuwa mwanzo wa ukaribu baina ya

    Dickson na changudoa Pamela. Msichana huyo

    mrembo ambaye alivutia kila alipomwangalia

    aliliteka penzi la Dickson kiasi kwamba hata

    alipokuwa ofisini, hakuwa akifikiria kitu

    chochote kile zaidi ya penzi la msichana huyo

    mwenye umbo lenye mvuto. Siku zikaendelea kukatika, hakukuwa na muda wa

    kutulia, saa mbili ofisini pasipo Pamela

    zilionekana kuwa nyingi, wakati mwingine

    alihakikisha anafanya kazi zake haraka

    iwezekanavyo kisha kurudi nyumbani ambapo

    alimpigia simu Pamela na kuja nyumbani kwake.

    Wivu ukamjaa moyoni, wakati mwingine

    alimlazimisha msichana huyo alale nyumbani

    kwake kwani kila alipokuwa naye mbali, alihisi

    msichana huyo kulala na San aims wengine kitu

    kilichouumiza mno moyo wake, kwa jinsi

    alivyokuwa na mapenzi mazito kwa Pamela, kuna

    kipindi alisahau kabisa kwamba msichana huyo

    alikuwa changudoa tu ambaye alilala na

    mwanaume yeyote aliyekuwa na pesa. “Vipi tena?” aliuliza Pamela, ilikuwa mchana wa

    saa saba, alipigiwa simu na Dickson, haikuwa

    kawaida kitu hicho kutokea. “Upo wapi?” “Nipo nyumbani, kuna nini mpenzi?” aliuliza

    Pamela. “Unaweza kuja mara moja?” “Wapi?”

    “Nyumbani kwangu.” “Kwani haupo kazini?” “Haujanijibu swali langu, unaweza kuja?” “Naweza. Ila kuna nini?” “Wewe njoo, wala usiogope,” alisema Dickson na

    simu kukatwa. Kichwa chake kilichanganyikiwa mno,

    alichokitaka mahali hapo ni kumuona music hana

    huyo tu kwani hakukuwa na kitu alichokuwa

    akipenda kama kuwa karibu na Pamela. Hakutaka kuendelea kukaa ofisini, alichokifanya

    ni kuondoka na kurudi nyumbani haraka ambapo

    wala hazikupita dakika nyingi, Pamela akafika,

    moja kwa moja akampeleka chumbani na kulala

    naye, hata kazi aliamua kuachana nayo kwa Sikh

    hiyo kwani penzi la Pamela lilimchanganya. **** Magreth alibadilisha ratiba yake, kila siku akawa

    mtu wa kutembea katika viwanja mbalimbali vya

    machangudoa huku lengo lake likiwa ni kuona

    kama angefanikiwa kumpata mteja wake

    aliyemkimbia katika kipindi alichomhitaji sana. Alizunguka na kuzunguka, tena wiki nzima mpaka

    alipofanikiwa kupata taarifa ambazo aliamini

    kwamba mtu aliyekuwa akizungumziwa alikuwa

    huyohuyo aliyekuwa akimhitaji. “Umesema changed is BMW nyeusi?” aliuliza changudoa

    mmoja. “Ndiyo! Unamfahamu?”

    “Kwa kweli sijawahi kumuona, ila huyo mteja

    anafika sana hapa kiwanjani,” alijibu changudoa

    huyo. “Nitampata vipi?”

    “Kwani ni nani kwako? Mumeo?” “Hapana! Ila ninataka kuonana naye,” alisema

    changudoa huyo. Jibu pekee alilopewa ni kwamba isingewezekana

    kuonana na mteja huyo kwani siku hizo hakuwa

    akifika sana kutokana na kulipata penzi la

    kudumu kutoka kwa msichana mrembo

    aliyetokea Arusha, Pamela. Kitu alichokitaka Magreth ni kuonana na huyo

    Pamela kwa kuamini kwamba angepata taarifa

    nyingi juu ya mwanaume huyo na hata

    ikiwezekana kupafahamu kwake kwani hakukuwa

    na mteja ambaye alimpa fedha nyingi kama

    mwanaume huyo ambaye mpaka katika kipindi

    hicho hakujua alikuwa na sura gani. Alipofanikiwa kuonana na Pamela, akajaribu

    kutengeneza urafiki naye, akaanza kumzoea, kila

    siku mchana akawa mtu wa kwenda

    kumtembelea, kwa kuwa Pamela hakuwa na

    marafiki wengi na pia hakuwa amelizoea sana jiji,

    akaupokea urafiki wa Magreth pasipo kujua

    msichana huyo alihitaji nini. Mpaka siku ambayo Dickson alimpigia Pamela

    simu na kumuita nyumbani, Magreth alikuwa

    pamoja naye chumbani, alichokifanya ni kumuaga

    kwa lengo la kwenda huko. “Ndiyo unakwenda kuonana naye?” aliuliza

    Magreth. “Ndiyo! Unataka twende wote?” aliuliza Pamela

    huku akionekana dhahiri kwamba alikuwa

    akitania.

    “Hahah! Kama inawezekana! Kwani hawezi

    kulala na wanawake wawili?” aliuliza Magreth,

    naye mwenyewe alionesha kutania. Pamela hakujibu swali hilo zaidi ya kucheka kisha

    kuondoka nyumbani hapo. Kwa Magreth

    alionekana kuwa na uhakika kwamba mwanaume

    huyo ambaye Pamela alikwenda kuonana naye

    ndiye yule ambaye alifika sana katika kiwanja

    chake, Sinza Mori na kumnunua, lakini ghafla

    akapotea na hakurudi tena. “Atakuwa ndiye yeye tu, ni lazima nimtafute,

    nipajue kwake na kumrudisha mikononi mwangu,”

    alisema Magreth pasipo kujua mtu huyo alikuwa

    nani. 


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
    Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa.  Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
    Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinogewa na penzi la changudoa mmoja aitwaye Pamela, umbo lake, ngozi vinamchanganya na kujikuta akianza kumganda pasipo kujua kwamba ukaribu wake na msichana huyo ungeweza kubadilisha kila kitu.
    Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
    Magreth hakutaka kukurupuka, alitaka kufanya vitu kimyakimya, yaani kumchunguza rafiki yake mpaka pale ambapo angepata ukweli wa mambo ili ajue ni kitu gani cha kufanya.
    Alijipanga, hakutaka kushtukiwa kabisa. Siku iliyofuata ambapo Pamela alirudi nyumbani, alimtembelea na kumchangamkia kama ilivyo siku nyingine, yote hayo aliyafanya kwa sababu alihitaji kufahamu mwanaume aliyekuwa akitembea naye aliishi wapi, kwani hata yeye alikuwa akimhitaji kwa sababu alikuwa bwana wake kitambo.
    Alihakikisha hachezi mbali na simu ya Pamela, alijitahidi kufuatilia namna ya kutoa loki za kwenye simu kwa mtindo wa kuzungusha pattern, alipozikariri, kazi ikawa kwake kuifungua na kufanya yake.
    Alimvizia Pamela alipokwenda bafuni kuoga ndiyo ukawa muda wake wa kuchukua simu yake kisha kuanza kuiangalia palepale kitandani. Alitoa loki kisha kuanza kuangalia namba zilizoingia jana usiku, muda ule ambao alitakiwa kuondoka nyumbani.
    Jina alilokutana nalo lilikuwa Mapesa, akajua kwamba hiyo ndiyo namba ya huyo bwana aliyekuwa na wasiwasi naye. Alichokifanya ni kuchukua simu yake na kuangalia namba, zilikuwa za mtu yuleyule, mwanaume aliyekuwa akilala naye kwa malipo makubwa.
    “Ndiye yeye!” alisema Magreth huku akiachia tabasamu pana na la kinafiki.
    Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kazi yake ya kumtafuta mwanaume huyo. Kitu cha kwanza alichokitaka ni kufahamu mahali alipokuwa akiishi, hilo wala halikuwa tatizo, kwa sababu alikuwa rafiki kipenzi wa Pamela, ndani ya siku chache tu akafahamu mahali alipokuwa akiishi mwanaume huyo, Dickson.
    Kilichofuata ni kuanza kumvizia, kila siku usiku alihakikisha anakwenda nyumbani kwa mwanaume huyo, anakaa nje kwa mbali huku akimsubiri aingie nyumbani kwake kwa lengo la kwenda kuzungumza naye lakini kila siku aliambulia patupu, hakuwa akibahatika kuonana na mwanaume huyo, kwani mara nyingi alikuwa akilala hotelini na Pamela, aliporudi ilikuwa ni asubuhi.
    Magreth alifuatilia kwa takriban wiki mbili ndipo siku moja akafanikiwa kuliona gari la Dickson likianza kuingia ndani ya jumba hilo la kifahari. Kwa kasi kubwa, Magreth akajitoa kule alipokuwa amejificha na kuanza kupiga hatua za haraka kuelekea lilipokuwa geti la nyumba ile, alitaka kuzungumza na mwanaume huyo.
    Alipolifikia gari, kwa haraka akaenda katika mlango wa gari na kuanza kugonga kioo huku akihitaji kufunguliwa.
    Dickson aliyekuwa ndani alishtuka, akaanza kujiuliza mtu huyo alikuwa nani mpaka kupata ujasiri wa kutaka kufunguliwa mlango. Kitu cha kwanza alihisi kwamba alikuwa jambazi, alipomwangalia vizuri, alikuwa msichana ambaye wala hakumfahamu vizuri kutokana na mwanga hafifu.
    Kabla hajashusha kioo cha gari, akahakikisha anaangalia sehemu nyingine kama kulikuwa na watu wengine ambao alihisi ndiyo waliomtuma msichana huyo, alipoona amani imejaa, akashika bunduki yake kama tahadhari kisha kushusha kioo.
    “Nikusaidie nini binti?” aliuliza Dickson, garini mwake hakukuwa na mwanga mkali. Mkono wake wa kushoto ulishikilia bunduki kisiri.
    “Umenisahau mpenzi?” aliuliza Magreth, Dickson akashtuka, kwani sauti aliyoisikia haikuwa ngeni, na hata alipomwangalia vizuri msichana huyo, aligundua kwamba alikuwa Magreth.
    “Mage…”
    “Ndiyo mimi kipenzi. Nimekukumbuka sana,” alisema msichana huyo.
    “Umepajuaje hapa?”
    “Nani? Mimi? Mbona nimepajua kawaida tu.”
    “Mmh!”
    “Usijali mpenzi!
    Kitendo cha Magreth kupafahamu alipokuwa akiishi lilionekana kuwa kosa kubwa, alijua fika kwamba mwisho wa siku msichana huyo angegundua kwamba yeye alikuwa kamanda mkuu jijini Dar es Salaam.
    Alichokifanya ni kumchangamkia kisha kumchukua na kuelekea naye ndani, tena huku akihakikisha anaivaa kofia yake. Magreth alionekana kuwa na furaha mno, kitendo cha kuona kwamba mwanaume huyo amempokea kwa mapenzi motomoto, kilimfurahisha.
    Akamchukua na kumpeleka ndani huku akihakikisha gari amelipaki vizuri. Alipofika humo, hakuwasha taa sebuleni, aliunganisha naye mpaka chumbani kisha akamlaza kitandani.
    Alichokitaka ni kumuua msichana huyo tu. Alihitaji kuwa na amani, hakuhitaji presha, alijua fika kwamba endapo angemuacha msichana huyo basi kitu ambacho kingefuata ni aibu kubwa.
    Magreth angejua kwamba nyumba ile ni ya kamanda wa jeshi la polisi na mwisho wa siku kuwatangazia watu kwamba mtu huyo alikuwa bwana wake. Alipofikiria mambo yote hayo, hakuona sababu ya msichana huyo kuendelea kuwa hai.
    Alipofikishwa kitandani na kulazwa chali, alifurahi kwa kuona kwamba hatimaye alifanikiwa kumrudisha bwana wake mikononi mwake. Alijiachia kitandani pale, alijiweka vizuri tayari kwa kumkaribisha Dickson katikati ya miguu yake pasipo kujua kwamba mwanaume huyo alikuwa na vitambaa kadhaa mikononi mwake kwa ajili ya kumziba pumzi na kumuua. Hilo, Magreth hakulitambua kwa sababu ya giza.
    ********************
    ********************


    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
    Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
    Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa.  Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
    Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson anajikuta akinogewa na penzi la changudoa mmoja aitwaye Pamela, umbo lake, ngozi vinamchanganya na kujikuta akianza kumganda pasipo kujua kwamba ukaribu wake na msichana huyo ungeweza kubadilisha kila kitu.
    Je, nini kitafuatia?
    SONGA NAYO…
    Dickson hakuwa na hamu ya kufanya mapenzi na Magreth, alichokifikiria ni kumuua msichana huyo tu. Alimwangalia kitandani pale, kwa jinsi alivyojiachia, alijua fika kwamba endapo angeleta mchezo na kumuacha hai msichana huyo ilikuwa ni lazima aumbuke hapo baadaye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Vitambaa vyake vilikuwa mikononi mwake, Magreth hakuwa na hofu yoyote ile, alijiweka vizuri pale kitandani huku akianza kuchojoa nguo moja baada ya nyingine.
    “Come to me big dad…” (Njoo kwangu baba…) alisema Magreth kwa kutumia maneno ya mahaba. Dickson akakifikia kitanda kile na kumsogelea karibu.
    Hakuwa na huruma, hiyo haikuwa mara ya kwanza kuua, alikwishawahi kufanya hivyo kabla hivyo hilo halikuwa tatizo kwake, kwa kasi ya ajabu, hapohapo akaviandaa vitambaa vile na kumfunika navyo Magreth puani na mdomoni.
    Msichana huyo akaanza kukukuruka kitandani pale, akaanza kurusha mikono yake huku na kule kama mtu aliyekaribia kukata roho. Dickson hakutaka kumuacha, aliendelea kumkandamizia vitambaa vile. Kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo, Magreth akashindwa kujitoa mikononi mwa mwanaume huyo, ndani ya dakika mbili tu, nguvu zikaanza kumuisha na baada ya sekunde chache, akatulia kitandani hapo, pumzi ikakata na kufariki dunia.
    “Haina jinsi Magreth…” alisema Dickson.
    Alipohakikisha kwamba msichana huyo amekufa, akaelekea jikoni akachukua maji na kuyaweka kwenye bakuli kisha kurudi mle chumbani. Akachukua kitambaa na kuanza kuufuta mwili ule katika sehemu zote zilizokuwa na alama za vidole vyake.
    Hakutaka kugundulika, alijua fika kwamba kama asingefanya hivyo basi ilikuwa ni lazima kugundulika kwani alama za vidole zingepimwa na uchunguzi kuanza kufanyika.
    Alipoona kwamba amezifuta alama zote, akauzungushia shuka kisha kuubeba na kutoka nao nje. Alipofika nje, akaelekea katika eneo la maegesho ya magari yake, akaupakiza mwili ule ndani ya gari kisha kuondoka nao.
    Hali ya hewa ilianza kubadilika, mawingu yalijikusanya angani na upepo kuanza kuvuma hali iliyoonesha kipindi kichache kijacho mvua kubwa ingeweza kunyesha.
    Dickson akaenda stoo ambapo alichukua koleo na sururu kisha akaelekea ndani ya gari, kilichofuata ni kuanza safari ya kuelekea katika Msitu wa Pande huku lengo lake likiwa ni kwenda kuuzika mwili ule.
    Mvua kubwa ikaanza kunyesha, Dickson hakurudi nyuma, alichotaka ni kumalizana na suala la mwili wa Magreth usiku huohuo. Kwa kuwa hakuwa na foleni usiku huo, alitumia dakika kumi tu, akaanza kuukaribia msitu huo.
    “Ngoja niingie hapahapa,” alisema Dickson kisha kukata upande wa kushoto na kuingia ndani ya msitu huo.
    Aliliendesha gari katika njia iliyokuwa na nyasi ndefu zilizolowanishwa na mvua iliyoendelea kunyesha. Alikwenda mbele zaidi huku taa za gari lake zikiwa full. Aliendesha mpaka alipofika katika sehemu iliyokuwa imezungukwa na miti mingi, akasimamisha gari na kuteremka huku mkononi akiwa na bunduki kwa ajili ya tahadhari.
    Hakuutoa mwili kwanza, akachukua vifaa vyake na kuanza kuchimba shimo msituni pale. Hakutaka kujiamini kwamba alikuwa peke yake, muda mwingi aliangalia huku na kule ili kuona kama kulikuwa na mtu mwingine zaidi yake.
    Alichukua dakika zaidi ya ishirini, shimo likakamilika, alichokifanya ni kurudi garini, akauchukua mwili wa Magreth na kwenda kuuingiza kwenye shimo lile kisha kuanza kuufukia.
    ****
    “Unasemaje?”
    “Tumeletewa taarifa ya mauaji!”
    “Kutoka wapi?”
    “Mbezi! Kuna taarifa kwamba inasemekana kuna mwili umefukiwa.”
    “Wapi?”
    “Kwenye msitu wa Pande!”
    “Lini hiyo?”
    “Jana usiku wakati mvua kubwa ilipokuwa ikinyesha,” ilisikika sauti ya polisi mmoja.
    Polisi wa Kituo cha Polisi cha Mbezi walikuwa wakitoa taarifa kwa mkuu wa kituo hicho kwamba siku hiyo waliambiwa kwamba kulikuwa na taarifa zilizodai kwamba kuna mwili wa mtu ulikuwa umefukiwa msituni.
    Taarifa hizo zikapokelewa hivyo polisi wanne waliokuwa na bunduki mikononi mwao, wakiwa ndani ya gari lao kuanza safari ya kuelekea huko walipoambiwa kwamba mwili wa mtu ulipozikwa.
    Hawakuchukua dakika nyingi, wakafika katika eneo ambalo watu wengi waliingia msituni kwenda kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea, nao wakaliingiza gari kuelekea huko.
    Mbele, wakakutana na umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika kwa staili ya kuzunguka kitu, walichokifanya ni kuwasogeza watu hao na kisha kuelekea pale ambapo kulionekana kama kuna kitu kimefukiwa, wakaanza kufukua.
    “Kuna nini kwani?” alisikika mwanamke mmoja akiuliza.
    “Nasikia kuna mwili umezikwa. Ila ni tetesi, sijui kama ni kweli,” alijibu mwanaume mmoja kwa sauti ya chini. Bado polisi waliendelea kulifukua shimo lile.
    ********************
    ********************
    Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufaya katika jeshi la Polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akajikuta akipandishwa vyeo na mwisho wa siku akijikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.
    Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.
    Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.
    Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.
    SONGA NAYO…
    Do not cross’ (usivuke) yalikuwa maneno machache yaliyoandikwa katika viplastiki mfano wa kamba zilizozunguka sehemu hiyo ambayo kulikuwa na kazi maalum ya kufukua sehemu ambayo watu walisema kulikuwa na mwili uliofukiwa.
    Polisi walikuwa bize kulifukua shimo hilo, hakukuwa na kazi kubwa kwani ardhi ililowa kwa kiasi kikubwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku. Baada ya dakika kadhaa, wakaufikia mwili huo, wakayaweka makoleo pembeni kisha kuanza kufukua kwa mikono.
    “Mungu wangu!”
    Kila mmoja alishtuka, mwili wa mwanamke ukatolewa katika shimo lile, baadhi ya wanawake waliokuwa mahali hapo wakashindwa kuvumilia, wakaanza kulia, waliumia mioyo yao, kile kilichokuwa kikionekana, kilikuwa ni ukatili wa hali ya juu.
    “Utoeni kabisa, hakikisheni hamgusi sehemu zile zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi,” alisema polisi mmoja ambaye alionekana kuwa kiongozi wa polisi waliokuwa mahali pale.
    Mwili wa Magreth ukachukuliwa na kupelekwa pembeni kabisa, watu wengine hasa wanawake wakashindwa kubaki mahali hapo, wakaondoka huku wakiwa wenye nyuso za huzuni.
    “Mmewapigia simu?” aliuliza kamanda.
    “Akina nani?”
    “Watu wa uchunguzi.”
    “Ndiyo! Wamesema wanakuja mkuu!”
    Zilipita dakika kumi na tano, gari jingine likafika mahali hapo, wanaume wanne waliokuwa na mavazi maalum na glavu mikononi mwao wakateremka na kuanza kupiga hatua kule kulipokuwa na polisi wale wengine ambao walikuwa na mwili wa Magreth pembeni.
    Mara baada ya kuzungumza nao kidogo, wakaanza kuuchunguza mwili ule palepale, lengo lao likiwa ni kutaka kubaini alama za vidole, waliporidhika, wakaubeba na kuupandisha ndani ya gari na safari ya kuelekea hospitalini kuanza.
    “Hii ni hatari sana…”alisikika polisi mmoja.
    *     *     *
    ‘Mwili wa Mwanamke wakutwa Msituni’, Muuaji aibuka jijini Dar’, Dar Yageuka Machinjioni’, hivyo vilikuwa vichwa mbalimbali vya habari katika magazeti yaliyotoka siku moja baada ya mauaji ya msichana Magreth.
    Kila mtu aliyeyaona magazeti yaliyokuwa na vichwa hivyo vya habari hiyo, alishtuka, si kwamba hawakuwa wakijua kama kulikuwa na mauaji ya chinichini yaliyokuwa yakiendelea bali kitendo cha kukutwa msichana mwingine akiwa ameuawa msituni ndicho kilichowashtua zaidi.
    Waandishi wa magazeti hayo waliandika habari ndefu ambayo ilionekana dhahiri kwamba muuaji wa mauaji yote hayo alikuwa mtu mmoja. Walianza na taarifa ile ya kwanza kabisa, mauaji ya msichana ambaye aliuawa katika Msitu wa Pande, taarifa zilisema kwamba muuaji huyo alivalia kofia kubwa ili kuuficha uso wake.
    Shuhuda pekee wa tukio lile, mzee Gombana ambaye ndiye alimuona muuaji huyo na kusema kwamba alivaa kofia kubwa, mwisho naye alikufa katika kifo kilichojaa utata mkubwa baada ya kutoka katika kituo cha polisi kutoa maelezo.
    Ukiachana na mzee huyo, pia alizungumziwa msichana mwingine aliyekuwa akiishi Mwananyamala, msichana huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika gesti bubu moja aliuawa bafuni wakati anaoga huku vijana ambao walimuona muuaji huyo wakisema kwamba alivalia kofia kubwa ambayo iliwapa ugumu kuuona uso wake.
    Muuaji alikuwa nani? Kwa nini aliua? Hayo yalikuwa maswali yaliyokuwa vichwani mwa watu wengi, hakukuwa na mtu aliyekuwa na jibu lolote lile. Watu waliendelea kujiuliza juu ya muuaji lakini bado vichwa vyao viliendelea kuwa na giza.
    “Ni lazima muuaji apatikane,” alisema polisi wa Kituo cha Mbezi.
    “Sawa mkuu! Tutafanya hivyo!”
    Ilikuwa ni lazima taarifa hizo zifikishwe makao makuu ya polisi jijini Dar ambapo ndipo muuaji, kamanda Dickson alipokuwa. Ndani ya dakika arobaini, tayari taarifa za mauaji yale zilikuwa mezani kwa kamanda Dickson ambapo baada ya kuzisoma, akapigwa na mshtuko na kujiuliza ni kwa namna gani watu walifahamu kule alipouzika mwili ule usiku kwani aliamini kwamba hakukuwa na mtu aliyemuona.
    “Ni nani alimuona muuaji akiingia msituni?” aliuliza kamanda Dickson.
    “Taarifa zinasema ni wawindaji.”
    “Mmh! Waliweza kumuona wakati anachimba shimo na kuufukia mwili?” aliendelea kuuliza, alitaka kupata jibu.
    “Hapana ila walisema waliliona gari likiingia msituni, wao wakakimbia kujificha…”
    “Baada ya hapo?”
    “Gari lilipoondoka ndipo walipokwenda kuona kulikuwa na nini, wakahisi kwamba kulikuwa na mwili umefukiwa, hivyo wakatoa taarifa,” alisema polisi mmoja.
    “Sawa, unaweza kwenda.”
    “Asante mkuu,” alisema polisi huyo kisha kupiga saluti kama heshima, akaondoka zake. Kamanda Dickson akabaki ofisini akiwa na presha kubwa.


    ********************
    ********************
    Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania

    kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa

    akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania.

    Kutokana na umahiri wake, akajikuta

    akipandishwa vyeo na mwisho wa siku akajikuta

    akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam,

    DCP. Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona

    anamheshimu kutokana na utendaji wake

    mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima

    zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson

    alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko

    shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la

    Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani. Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi,

    alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa.

    Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar

    es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila

    ambaye alimuona sura yake na kumgundua,

    alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa

    liwe siri maisha yake yote. Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye

    Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata

    amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana

    na uzuri wake, anawapata wanaume wengi,

    anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata

    wanawake wenzake. SONGA NAYO. “Unaweza kuja nyumbani leo?” ilisikika sauti ya

    Dickson kwenye simu. “Mimi?”

    “Kwani nazungumza na nani mpenzi? Ndiyo!

    Wewe hapo.”

    “Mmh! Kwa leo sidhani, kuna msiba huku.” “Nani amefariki?””Rafiki yangu, anaitwa Magreth!” “Pole sana aiseee. Basi sawa, nitakucheki

    keshokutwa,” alisema Dickson na kukata simu. Muda huo, mwili wake ulimuwaka moto, alikuwa

    na hamu ya kuwa na mwanamke hata kwa saa

    moja tu. Mtu pekee ambaye kila siku aliuridhisha

    moyo wake alikuwa msichana Pamela tu.

    Alimpigia simu na kumwambia kwamba

    asingeweza kuja kwa kuwa alikuwa kwenye

    msiba wa rafiki yake. Hapo ndipo Dickson

    alipogundua kwamba kumbe Magreth

    alifahamiana na Pamela. Hakutaka kukaa nyumbani, pepo la ngono

    alilokuwa nalo lilimchanganya mno, alichokifanya

    ni kuondoka nyumbani na kwenda Ambiance

    ambapo aliamini kwamba angepata msichana

    mzuri wa kulala naye usiku wa siku hiyo. Kama kawaida yake akaingia ndani ya gari lake

    na kuanza safari ya kuelekea huko kwa ajili ya

    kumnunua changudoa na kulala naye usiku huo.

    Ndani ya gari, alijiona kuchelewa kufika huko

    alipokuwa akielekea, aliendesha kwa kasi kubwa

    na ndani ya dakika ishirini, akafika Ambiance

    ambapo pembeni kulikuwa na wanawake wengi

    waliokuwa wakijiuza. Hata kabla hajachagua yupi wa kumfuata, ghafla

    wasichana wanne wakasogea kule alipokuwa,

    walivalia mavazi tofauti, wengine taiti na wengine

    vimini vilivyoyaacha mapaja yao wazi. “Ngoo… ngoo… ngoo…” kioo cha mlango wa gari

    kiligongwa na msichana mmoja. Akakishusha na

    kuwaangalia wasichana hao. Hakukuwa na

    aliyemfahamu kutokana na giza kubwa lililokuwa

    ndani ya gari. “Karibu mpenzi…” alisema msichana mmoja huku

    akijinyonganyonga. “Asante. Bei inakwendaje?” “Kulala au show time?”

    “Kulala!” “Elfu sitini,” alisema msichana huyo. “Nyingi sana. Mwingine?” “Subiri kwanza kaka! Mbona hatujaelewana! Bei

    mazungumzo mpenzi!” “Utapunguza hadi ngapi?” aliuliza Dickson. Kilichokuwa kikiendelea mahali hapo ni

    kukubaliana kwa bei na changudoa huyo

    aliyesimama nje ya gari lake huku wale wengine

    wakiwa wamekwishaondoka kwani mwenzao

    huyo alichaguliwa hivyo ndiye aliyetakiwa

    kukubaliana bei na mteja huyo.

    Baada ya dakika kadhaa, wakakubaliana na hivyo

    msichana huyo kutakiwa kuingia ndani ya gari na

    kuondoka mahali hapo, changudoa huyo akafanya

    hivyo. Alivyoingia ndani ya gari, ndipo Dickson

    alipogundua uzuri wa changudoa huyo. Kimini

    alichokuwa nacho ambacho kiliishia mapajani,

    alipokaa kitini, kikajivuta kwa juu na kumfanya

    Dickson kuweweseka zaidi.

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika

    nyumba moja ya wageni iliyokuwa Manzese

    Midizini. Gari likasimamishwa hivyo kutakiwa

    kuteremka. Changudoa yule alibaki na mshangao,

    hakuamini kama safari yao ingeishia ndani ya

    nyumba hiyo. Ilikuwa uswahilini mno ambapo bei yake

    isingeweza kuwa zaidi ya shilingi elfu tano. Mtu

    aliyekuwa amemnunua kutoka katika kiwanja

    chake, alionekana kuwa bwana wa haja, mwenye

    pesa lakini kitendo cha kupelekwa katika chumba

    kile, ilimshangaza. “Tumefika!” alisema Dickson. “Nidiyo humu?” aliuliza changudoa yule kwa

    mshangao. “Ndiyo! Kwani tatizo nini?” “Mbona unaonekana una pesa sana, au hata hili

    gari umeazima?” “Hapana. Ni maamuzi tu. Unataka hela au

    unataka kulala kwenye kitanda cha gharama?”

    aliuliza Dickson, alionekana kuanza kukasirika. “Nataka hela.” “Kama unataka hela twendeni,” alisema Dickson.

    Kwa sauti aliyoitoa, hata changudoa yule alihisi

    kwamba alimkosea Dickson kwa kumuoneshea

    ishara ambazo moja kwa moja zilionekana kama

    kudharauliwa, alitamani kumuomba msamaha

    lakini akashindwa kufanya hivyo, kama malipo

    yake, akaahidi kufanya kila liwezekanalo

    amchanganye chumbani tu.

    Kofia yake haikutoka kichwani mwake, bado

    hakuhitaji kujulikana, kila kitu kilikuwa siri kubwa

    kwake, walipofika mapokezi, akalipia chumba na

    kwenda chumbani tayari kwa kufanya kile

    kilichowapeleka pale. “Naruhusiwa kuweka masharti kama mteja?”

    aliuliza Dickson. “Kama lipi?” “Napenda kufanya gizani, sipendi taa.” “Kweli?”

    “Ndiyo!” “Hata mimi napenda giza, hakuna tatizo,” alisema

    msichana huyo kwa furaha, tena huku akionekana

    kuchangamka sana, kwa muonekano wake tu,

    alionekana kuwa na kitu nyuma ya pazia, Dickson

    hakuelewa hilo.



    Pamela hakuamini kile alichokisikia kwamba rafiki yake kipenzi alikutwa akiwa amekufa porini huku mwili wake ukiwa umezikwa. Mara ya kwanza hakuamini kile alichokisikia lakini baada ya yeye na mashoga zake kwenda hospitali kuutambua mwili huo, hapo ndipo alipoamini kwamba rafiki yake huyo kweli alifariki dunia.
    Moyo wake ukawa kwenye majonzi mazito, alibaki akilia tu, alimzoea sana Magreth, japokuwa hawakuwa marafiki kwa zaidi ya mwaka lakini walizoeana vya kutosha. Harakati za mazishi zikaanza kufanyika, hakukosa kwenye msiba huo, alikwenda kila hatua mpaka pale mwili wa Magreth ulipozikwa katika Makaburi ya Mburahati jijini Dar es Salaam.

    Kwa kuwa alikuwa kwenye kipindi cha majonzi, hakutaka kwenda sehemu yoyote ile, alisimamisha kazi yake ya kuuza mwili kwa kuwa alikuwa kwenye majonzi makubwa. Hata Kamanda Dickson alipompigia simu na kumwambia kwamba alitaka kulala naye, alikataa, hakujisikia kabisa kulala na mwanaume yeyote.
    Siku zikaendelea kukatika, baada ya wiki kupita hapo ndipo alipoamua kurudi katika kazi yake kama kawaida. Wakati huo ambao alirudi kazini ndipo alipopata tetesi kwamba kulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakipotea, tena machangudoa ambao walinunuliwa na mwanaume mmoja kisha alipoondoka nao, hawakuweza kurudi.

    “Huwa anawaua,” alisema changudoa mmoja, alionekana kuwa na hofu.

    “Ni nani?” aliuliza Pamela.
    “Sijui! Ila hata Magreth aliuawa na huyohuyo mwanaume hata Khadija naye aliuawa na huyohuyo mwanaume,” alisema changudoa huyo maneno yaliyomtisha sana Pamela.Hakuwa na amani, moyo wake ulikuwa na hofu tele, kuanzia siku hiyo hakutaka kuchukuliwa na mwanaume yeyote yule kwenda naye kufanya mapenzi, kila mteja aliyekuja mahali hapo, ilikuwa ni lazima kufanya mapenzi makaburini au garini lakini si sehemu nyingine, hasa hotelini au nyumbani.

    “Wateja wengi wanakuwa wagumu kufanya makaburini, wanaogopa,” alisema Pamela.

    “Kweli?”
    “Ndiyo! Jana kaja jamaa wa Kiarabu, aliniahidi hela nzuri tu ila mwisho wa siku nilipomwambia kwamba makaburini, akakata kamba, huyo akaondoka zake,” alisema Pamela.

    “Kwa hiyo tufanye nini?”

    “Kwani nyie si mmesema mtu anayeua anatembelea gari nyeusi?”

    “Ndiyo!”
    “Sasa kama mtu akija na gari nyeupe, tunatakiwa kumuogopa kwa lipi? Sidhani kama ni sahihi,” alisema Pamela, kipindi cha wiki nzima alichokaa bila kuingiza chochote, ilimuumiza. Hakutaka kujali, alichokipanga ni kufanya popote pale, hata kama huyo mwanaume muuaji akija na kumchukua kwa lengo la kumuua, alikuwa tayari, alichokiangalia ni hela tu.

    * * * *

    Wanaume wengi walilizwa na machangudoa, wengi walipoteza mamilioni ya fedha na vitu vyao vya thamani kutokana na kuibiwa na machangudoa hao. Michezo michafu iliyokuwa ikichezwa na machangudoa iliwaogopesha wengi.

    Machangudoa wengi walitumia dawa za usingizi kwa ajili ya kuwawekea wanaume na mwisho wa siku wanapolewa na kulala, wanawaibia kila kitu kisha kuondoka zao. Huo ndiyo mchezo uliokuwa ukiendelea kwa machangudoa wengi, hasa wale waliokuwa jijini Dar es Salaam.
    Kitendo cha Dickson kumchukua changudoa yule, hakujua kama huyo alikuwa miongoni mwa machangudoa waliokuwa wakiwaliza wateja wao. Mara baada ya kuingia humo chumbani, kabla ya kuanza kufanya mapenzi, msichana yule akamwambia Dickson kwamba alitaka kwenda bafuni kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

    Alipofika bafuni, akachukua kikopo kidogo kilichokuwa kwenye mfuko wake wa jinsi ambacho kilikuwa na unga fulani uliochanganywa na dawa za usingizi, akaupaka kifuani na kurudi chumbani.
    Alipofika, akachojoa nguo zake, akajilaza kitandani na kumvuta Dickson. Dickson akaingia katika mikono ya changudoa huyo aliyebaki mtupu kitandani pale, kilichoendelea baada ya kupokelewa ni kushughulika na kifua cha msichana huyo.
    Wala hazikupita dakika nyingi, macho yake yakaanza kuwa mazito, mbele akaanza kuona giza nene na baada ya dakika moja tu, usingizi mzito ukampata akiwa palepale kifuani.
    Changudoa yule akamtoa Dickson kifuani, hakutaka kuwasha taa, alichokifanya ni kuzichukua nguo za Dickson na kuanza kuzipekua mifukoni. Humo, akakuta kiasi cha shilingi laki tano, hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kuzichukua na simu yake ya gharama kubwa kisha kuondoka chumbani hapo.
    Alipofika nje, alitaka kuingia ndani ya gari lakini akasita kwa kuhofia kwamba angeweza kugundulika kwa wanaume waliokuwa nje ya nyumba hiyo ya wageni. Akaelekea upande wa Kaskazini kulipokuwa na barabara ya lami, alipofika huko, akakodi bodaboda na kutokomea kurudi nyumbani kwake huku akiona kwamba amefanikiwa kufanya wizi kama ambao alizoea kuufanya kwa wateja wengine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vipi Khadija?”
    “Kama kawaida. Nishamliza mtu huko, pedeshee fulani alijitokeza, nimemuacha akiwa hoi,” alisema Khadija huku meno yote yakiwa nje.

    “Mmmh! Hongera zako aisee…”

    “Asante. Kwa hiyo bata wapi?”

    “Wewe ndiye tajiri, unataka twende wapi?”

    “Twende Savannah…tukale bata tu.”
    “Ngoja nijiandae, usiku huuhuu tunaelekea huko, tumpitie Shamila, Ashura na Mariamu, akijipendekeza mwingine huko, kama kawaida tunamliza,” alisema Khadija huku akijiona mshindi pasipo kujua ni mtu gani aliyekuwa amemfanyia mchezo huo mchafu.


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam

    kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa

    katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa

    inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya

    machangudoa kumi na moja wanapotea na

    hakuna anayejua walikopotelea. Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia

    kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea

    katika mazingira yanayofanana. Mwanaume

    mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari

    la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda

    eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa

    na wote wanaopotea. Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano

    tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson

    Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa

    wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es

    Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha

    kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda

    kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye

    anahamishiwa Dar es Salaam. Mara baada ya kufanikiwa kuwa DCP, Dickson

    anajikuta akinogewa na penzi la changudoa

    mmoja aitwaye Pamela, umbo lake, ngozi

    vinamchanganya na kujikuta akianza kumganda

    pasipo kujua kwamba ukaribu wake na msichana

    huyo ungeweza kubadilisha kila kitu. Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

    Dickson akashtuka kutoka katika usingizi mzito,

    mwili wake ulikuwa umechoka mno, akaangalia

    huku na kule, alitaka kufahamu alikuwa sehemu

    gani kwani kwa jinsi kitanda kile kilivyokuwa,

    alikuwa na uhakika kwamba hapo hapakuwa

    nyumbani kwake. Akayafikicha macho yake na kuiangalia sehemu

    hiyo, ilikuwa katika nyumba ya wageni.

    Kumbukumbu zake zikaanza kurudi nyuma ili ajue

    sababu zilizomfanya kuwa ndani ya chumba

    hicho. Hapo ndipo alipokumbuka kwamba mara ya

    mwisho kabisa alikuwa chumbani na mwanamke,

    walishikana hapa na pale, kilichofuata,

    hakukikumbuka. Akaelekea katika suruali yake,

    alitaka kuona kama fedha zake zilikuwepo,

    hakukuta kitu, si fedha tu, hata simu yake pia

    haikuwepo. Akajikuta akiuma meno kwa hasira, mwili

    ukaanza kumtetemeka mithili ya mtu anayesikia

    baridi, kwa sababu kwa mbali mwanga wa alfajiri

    ulishaanza kutokeza, akainuka, akavaa nguo zake

    na kuondoka chumbani hapo huku akiwa na kofia

    yake kichwani. Hakumsalimia dada wa mapokezi, aliunganisha

    moja kwa moja mpaka nje, akalifuata gari lake na

    kuondoka huku akiwa na hasira kali dhidi ya

    changudoa aliyemlevya na kumuibia Alichokitaka ni kulipa kisasi, hakutaka kumuacha

    changudoa huyo aendelee kuishi kwani akili yake

    ilimwambia kwamba kabla ya kuondoka,

    alimwangalia usoni na kumgundua alikuwa nani,

    hivyo akaenda kuwaambia marafiki zake. Hakutaka kuona siri hiyo ikivuja, kwa hali na mali,

    tena kwa gharama yoyote ile ilikuwa ni lazima

    amuue changudoa huyo. Hakujua alifananaje,

    alichokikariri kutoka kwake ni miguu yake, ilikuwa

    imejaajaa huku kwa mbali akiwa na matege.

    Mbali na miguu hiyo, sura yake ilikuwa na

    chunusi nyingi zilizomfanya kumpendezesha sana

    na kumfanya avutie. “Nitamtafuta, na nitamuua tu, si yeye, hadi

    marafiki zake wote ni lazima niwamalize wote

    kwa kuwa najua atakuwa amewaambia tu,”

    alisema Dickson huku akionekana kuwa mwingi

    wa hasira.

    Alichokifanya mara baada ya kufika ofisini ni

    kuagiza usiku wa siku hiyo katika sehemu zote

    ambazo zilikuwa na machangudoa waliokuwa

    wakijiuza, ilikuwa ni lazima polisi waende

    kuwakamata na ikiwezekana wawaweke ndani na

    yeye mwenyewe kwenda kuwaangalia. Polisi walishangaa sababu ya Kamanda Dickson

    kuamua hivyo lakini hakukuwa na mtu mwenye

    maswali, kwa kuwa amri ile ilitolewa na mkuu

    wao, ikawabidi waifuate kama walivyotakiwa. Usiku wa usiku huo polisi wakafanya doria

    sehemu zote zilizokuwa na machangudoa, wengi

    wakakamatwa na kupelekwa vituoni, asubuhi

    iliyofuata Kamanda Dickson akaanza kutembelea

    kila kituo na kuwaangalia machangudoa hao,

    alipoona hakuna mbaya wake aliyekuwa

    akimtafuta, akaachana nao. “Nitampata tu, ni suala la muda tu,” alijisemea

    Kamanda Dickson. * * *

    Kichwa cha Pamela kilikuwa na mawazo mengi,

    stori alizopewa kuhusu mtu mwenye gari nyeusi

    ambaye alikuwa akiwachukua wasichana na

    kwenda kuwaua ilimuogopesha. Moyo wake ulijawa na hofu lakini hiyo haikuwa

    sababu iliyojitosheleza ya kumfanya asimame na

    kuachana na shughuli zake. Alitoka jijini Arusha

    mpaka Dar es Salaam kwa sababu alihitaji fedha,

    alijipanga na katika kipindi ambacho aliishi jijini

    Dar, tayari aliyaona mafanikio, hivyo kuachana na

    biashara ya kujiuza ilikuwa ngumu. “Umakini ndiyo unaohitajika tu,” alijisemea. Machangudoa wote wa Kinondoni hawakuwa

    watokaji, ili ufanye nao ngono ilikuwa ni lazima

    iwe hapohapo makaburini au ndani ya gari lako,

    ila si kuondoka katika eneo hilo na kwenda

    hotelini au sehemu nyingine. Kwa Pamela ilikuwa tofauti, aliyatoa maisha yake

    sadaka, alijua kwamba wanaume wengi

    hawakupenda kufanya ngono makaburini kwa

    kisingizio cha kuogopa laana, hivyo kama na yeye

    angefanya kama watu wengine basi asingepata

    fedha, hivyo ilikuwa ni lazima kufanya kama

    zamani. Machangudoa wengine walimshangaa Pamela

    lakini hakuonekana kujali, alihitaji kuwa na fedha,

    hivyo hata suala la kuuawa, aliliita ajali kazini.

    Siku ya kwanza ikapita, ya pili, ya tatu mpaka

    wiki nzima, hali ilikuwa ni amani tele, hakuuawa

    wala kukutana na mtu mbaya, wote waliokuja

    kwake ambao walimtaka kwenda kulala naye,

    walikuwa watu wema mpaka kufikia hatua akahisi

    kwamba inawezekana stori hizo zilikuwa ni

    uzushi tu.

    Baada ya wiki nzima kukatika, hapo ndipo

    akajikuta mikononi mwa polisi. Hakuwa yeye,

    walikuwa na machangudoa wengine wengi,

    walifungwa pingu na kupelekwa vituoni. Kila mmoja alishangaa, hakukuwa na taarifa

    kama siku nyingine ambapo kabla ya polisi

    kufanya doria, waliletewa taarifa, doria ya siku

    hiyo ilikuwa ya ghafla sana hivyo machangudoa

    wengi kujikuta wakiingia mkenge.

    Alilala sero na wenzake, kesho yake,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hawakuachiwa bali waliambiwa wasubiri kwani

    Kamanda Dickson, mtu mwenye sura mbaya

    alikuwa akipita katika vituo vyote kwa ajili ya

    kuangalia idadi ya machangudoa hao kujua kama

    kuna muharifu aliyekuwa akimtafuta.


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea na hakuna anayejua walikopotelea.
    Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea katika mazingira yanayofanana. Mwanaume mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye anayehusishwa na wote wanaopotea.
    Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
    Hisia kali za mapenzi zinasababisha kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye anahamishiwa Dar es Salaam.
    Baada ya kuwa DCP, Dickson anakutana na msichana aitwaye Pamela, anatokea kuvutiwa naye, anafanya naye mapenzi kwa kumnunua Kinondoni. Kupitia changudoa huyo aliyetoka Arusha, anajikuta akianza kuwaua wanawake wengi jijini Dar es Salaam.
    Je, nini kitafuatia?
    SONGA NAYO…
    Hawakuchukua muda mrefu wakafika kituoni, alichokifanya polisi ni kumwambia kijana yule aliyejitambulisha kwa jina la Samto ampigie simu Hadija na kumwambia maneno yoyote yale ilimradi wakutane sehemu.
    Hiyo ndiyo njia ambayo ilionekana kufaa kutumika kwani vinginevyo wasingeweza kumkamata mwanamke huyo. Wakati Samto amepewa simu kwa ajili ya kumpigia Hadija, Kamanda Dickson akamzuia kwa kumwambia kwamba hakutakiwa kufanya hivyo, kwa kuwa alikwishaipata simu yake, haikuwa na haja.
    “Haina haja kufanya hivyo, nilichokuwa nakitaka ni simu tu,” alisema Kamanda Dickson hali iliyomfanya kila polisi kushangaa huku wengine wakimuona kuwa na roho nzuri.
    “Hakuna tatizo afande.”
    “Ila ningependa kuzungumza na huyu mtu.”
    “Sawa mkuu!” alisema polisi mmoja kisha kupiga saluti.
    Wakamchukua Samto na kumpeleka katika chumba kimoja kilichokuwa na meza moja ndefu na viti viwili. Walipofika wakamuweka kwenye kiti kimoja na kiti kingine kukaliwa na Kamanda Dickson, polisi wote wakatoka nje.
    Kamanda Dickson akabaki akimwangalia Samto huku uso wake ukionekana kuwa na hasira mno. Alivimba kiasi kwamba ubaya wa sura yake kuonekana dhahiri. Samto alimfahamu mtu aliyekuwa mbele yake, alikuwa miongoni mwa watu waliosemekana kuwa na roho mbaya, hivyo kila alivyomwangalia na kwa jinsi alivyokuwa na hasira, akajua kwamba angeweza kufanywa kitu kibaya.
    “Huyo Hadija anaishi wapi?” aliuliza Dickson.
    “Anaishi Kinondoni A.”
    “Kama kunaelekezeka hebu nielekeze,” alisema Dickson hivyo Samto kuanza kumuelekeza.
    “Sawa. Alipokuuzia simu hii alikwambiaje?”
    “Alisema kwamba ilikuwa yake hivyo nisiwe na hofu na kwa sababu huwa mara nyingi nanunua vitu kwake, nilimwamini sana,” alisema Samto.
    “Huwa anapatikana nyumbani muda gani?”
    “Mchana huwa yupo muda wote, ila kuanzia saa moja, anatoka kwenda kwenye mishe zake.”
    “Na hapo anaishi na watu wangapi?”
    “Yupo na wasichana wenzake wawili, Asha na Anita, ila pia ana marafiki zake wa karibu, Mariamu na Ashura ambao wanaishi kama nyumba ya tatu kutoka hapo anapoishi,” alisema Samto.
    “Sawa. Wanafanya kazi gani?”
    “Wanajiuza usiku.”
    “Wote hao?”
    “Ndiyo!”
    Kamanda Dickson hakutaka kupoteza muda, alichokifanya ni kuondoka kituoni hapo huku akitoa agizo kwamba Samto asitolewe kituoni wala asiwasiliane na mtu yeyote na kama alihitaji chakula, ilibidi kununuliwa lakini si kuruhusu kuonana na mtu yeyote yule.
    Ili kuonesha kwamba alimaanisha alichokisema, akaingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha shilingi elfu hamsini na kumgawia mkuu wa kituo huku akimtaka mkuu wa kituo ahusike katika ishu zote za chakula kwa Samto.
    *********
    “Dada samahani!” ilisikika sauti ya mwanaume mmoja kutoka katika sehemu iliyokuwa na giza hafifu, kichwani alikuwa na kofia kubwa huku akiwa amevaa shati lenye maua.
    “Nani? Mimi?” aliuliza msichana huyo, kwa kumwangalia tu, wala usingeweza kujiuliza mara mbili kwamba alikuwa akifanya kazi gani, mavazi yake tu, tena kwa muda kama huo alionekana kuwa changudoa, na kama hakuwa changudoa, basi alikuwa mtu wa kujirusha kwa sana usiku.
    “Ndiyo dada! Nakuhitaji mara moja.”
    “Mbona gizani?”
    “Jamani! Kwani kuna giza hapa? Halafu sisi wengine wenye familia zetu hatutaki kuonekana, si unajua mke akituoni usiku hakulaliki…” alisikika mwanaume huyo.
    Msichana yule akajisogeza karibu na mwanaume yule ila kwa mwendo ulioonesha kuwa na hofu na uwepo wa mwanaume yule mahali pale. Alipomfikia, alijitahidi sana kumwangalia usoni ili amuone vizuri lakini kutokana na kigiza kilichokuwa mahali pale, hakuweza kumgundua.
    “Nataka mechi…” alisema mwanaume huyo.
    “Nani kakwambia kama najiuza?”
    “Jamani! Nimebanwa mwenzako, hata kama haujiuzi, naomba tu uniridhishe mtoto wa mwanamke mwenzio, nitakupa hela yoyote uitakayo,” alisema mwanaume huyo.
    “Una kilo?”
    “Hiyo tu? Hakuna tatizo,” alisema mwanaume huyo, hapohapo akaingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha shilingi laki moja na kumgawia msichana huyo. Alionekana kuwa na kiu ya kutaka kulala naye kwa kisingizo cha kutoka mkoani na gari la mizigo, hivyo njiani kote alikosa mwanamke wa kumkosha roho yake. Mwanaume huyo alikuwa Kamanda Dickson na mwanamke alikuwa Shamila, rafiki yake Hadija.


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam

    kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa

    katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki

    kubwa inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu,

    zaidi ya machangudoa kumi na moja wanapotea

    na hakuna anayejua walikopotelea.

    Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia

    kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea

    katika mazingira yanayofanana. Mwanaume

    mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea

    gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa

    akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye

    anayehusishwa na wote wanaopotea.

    Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano

    tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson

    Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa

    wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar es

    Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha

    kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda

    kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye

    anahamishiwa Dar es Salaam. Baada ya kuwa DCP, Dickson anakutana na

    msichana aitwaye Pamela, anatokea kuvutiwa

    naye, anafanya naye mapenzi kwa kumnunua

    Kinondoni. Kupitia changudoa huyo aliyetoka

    Arusha, anajikuta akianza kuwaua wanawake

    wengi jijini Dar es Salaam.

    Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO… Biashara ilikuwa mbaya kwa Shamila, alishinda

    katika kijiwe chake lakini wanaume siku hiyo

    waliadimika, hakukuwa na mwanaume yeyote

    aliyemfuata mpaka mishale ya saa kumi alfajiri

    alipoamua kurudi nyumbani kupumzika kwa

    kuhesabu kwamba siku hiyo aliambulia patupu.

    Wakati akiwa amefika karibu na mahali alipokuwa

    akiishi, bahati nzuri kwake akakutana na

    mwanaume, aliyeonekana kuwa na hela nyingi

    ambaye alihitaji huduma yake kwa muda huo

    uliobakia. Shamila hakutaka kulaza damu, hiyo ilionekana

    kuwa bahati yake, yaani kama kutembea kilometa

    hamsini pasipo kuuona mwembe halafu mbele

    unakutana na embe dodo, alichokifanya ni

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kuondoka na mteja huyo na kwenda naye katika

    gesti iliyokuwa karibu na eneo hilo. “Unaonekana mzuri sana, ila unaweza au ndiyo

    utaleta usista duu?” aliuliza Kamanda Dickson

    kwa sauti ya kilevi kwa mbali, hakutaka

    kugundulika kirahisi, yaani msichana huyo ajue

    kwamba alikutana na mlevi.

    “Usije ukakimbia wewe tu.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo!” “Basi kama ndiyo hivyo, nitakuongeza fedha,

    ilimradi unifikishe ninapokwenda,” alisema

    Dickson huku wawili hao wakipiga hatua kuelekea

    kwenye gesti moja iliyokuwa karibu, kwa namna

    walivyokuwa wakitembea ilikuwa ni rahisi sana

    kusema kwamba walikuwa wapenzi wa muda

    mrefu, kwani walishikana kimahaba. Walipofika katika gesti hiyo, moja kwa moja

    wakaelekea mapokezi ambapo dada wa hapo

    alionekana kufahamiana sana na Shamila,

    wakasalimiana kwa furaha na kuomba chumba,

    wakapewa chumba namba ishirini na mbili. “Si ndiyo kile chenye wavu uliochanika na kitanda

    chenye kelele?”

    “Ndiyo! Ila wavu tulibadilisha na hata kitanda

    kipo poa, tulikibadilisha, tumeweka cha chuma,”

    alisema mhudumu. “Kama ni hivyo sawa, leo nipo na mpenzi mpya,

    sitaki presha ya kitanda cha kelele,” alisema

    Shamila pasipo Dickson kuzungumza chochote

    kile. Kwa sababu Shamila ndiye alikuwa mwenyeji,

    alichokifanya ni kuchukua ufunguo wa chumba

    hicho na kuanza kuelekea huko. Bado walikuwa

    wakishikana kimahaba mpaka walipofika

    chumbani ambapo yeye kama mteja, Dickson

    akahitaji kufanya mapenzi kwenye giza kwa

    lengo la kutokuonekana. “Nyie wateja wa siku hizi mna masharti kama

    waganga…mnapenda sana kufanya mapenzi

    gizani kama paka,” alisema Shamila kwa sauti

    iliyoashiria kutania, alipomaliza kusema hayo,

    akampiga Dickson kibao cha mahaba kisha

    kuanza kuvua nguo zake.

    Uso wa Dickson ulionesha tabasamu pana lakini

    moyo wake ulikuwa na hasira kali, hakumpenda

    Shamila, alimchukia kwa kudhani kwamba huyo

    Hadija alimwambia kuhusu yeye hivyo kupania

    kumuua humohumo ndani. Shamila alijichekesha huku akizungumza maneno

    ya mahaba ambayo alidhani kwamba yangeingia

    ndani ya moyo wa Dickson na kuubadilisha

    hatimaye kuwa mteja wake wa kila siku hasa

    baada ya kubadilishana namba za simu.

    “Nataka nikupe mapenzi ya kisasa baby…”

    alisema Shamila.

    “Yapoje hayo?” “Wewe subiri, nitakuonesha kwa nini wananiita

    Shamila mkia wa taa,” alijigamba msichana huyo. Dickson alitulia tu, alibaki akimwangalia

    msichana huyo ambaye alionekana kupania sana

    usiku wa siku hiyo pasipo kujua kwamba usiku

    huo ndiyo ungekuwa kwisho wa kuvuta pumzi ya

    hii dunia. Baada ya kumaliza manjonjo yake yote,

    akamsogelea Dickson pale kitandani na kulala juu

    yake. Dickson akamgeuza Shamila na kumuweka

    chini huku akileta unafiki wa kumbusu hapa na

    pale hali iliyomfanya msichana huyo kufumba

    macho kimahaba.

    “Bila shaka unaitwa Shamila…” alisema Dickson,

    Shamila akashtuka.

    “Kumbe unanifahamu?” aliuliza Shamila huku kwa

    mbali akionekana kushtuka.

    “Ndiyo! Hadija yupo wapi?” “Nani? Hadija? Ndiye nani?” aliuliza Shamila huku

    akijidai kutokumjua Hadija kwa kuhofia

    kuchukuliwa mteja wake.

    “Haumfahamu?”

    “Wala simjui kabisa.” “Una uhakika?”

    “Ndiyo! Kwanza ndiyo nini kumtajataja mtu

    kwenye muda kama huu jamani baby? Mbona

    unataka kuniumiza?” aliuliza Shamila huku

    akijifanya kama kutaka kulia eti kwa kuumizwa

    na wivu mkali. “Na wewe si ndiye uliyetumia naye fedha zangu

    alizoniibia gesti? Bila shaka mlifurahi na kula

    bata sana kwa hela za mwanaume msiyemjua ni

    nani,” alisema Dickson, maneno hayo yakaanza

    kumtia shaka Shamila, akataka kujitoa pale

    kitandani, akashindwa, mikono yake ilizuiliwa

    vilivyo, Dickson alikuwa juu yake. “Wewe ni nani?” aliuliza Shamila huku akiwa na

    hofu tele.

    “Mwenye simu na fedha! Nimekuja kwa ajili ya

    kuwaonesha ni jinsi gani mali za mwanaume

    haziendi bure,” alisema Dickson, hapohapo pasipo

    kuchelewa akaanza kumkaba Shamila kooni. Msichana huyo alikukuruka huku na kule,

    alijitahidi kuitoa mikono ya Dickson shingoni

    mwake lakini hakufanikiwa, alikabwa vilivyo,

    macho yakaanza kubadilika na mishipa ya shingo

    kumsimama, Dickson hakumwacha, aliendelea

    kumkaba kwa lengo la kumuua


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam, machangudoa wengi wanaanza kuuawa katika mazingira ya kutatanisha. Hakuna anayemjua muuaji, kila changudoa anayenunuliwa na mwanaume aliyekuwa kwenye gari aina ya Volkswagen nyeusi, anauawa kikatili.
    Kila mmoja anaogopa, machangudoa wengine wanaacha kujiuza, wanajifungia vyumbani mwao, ila kwa wengine ambao hawakuweza kuishi bila kufanya biashara hiyo, wanakwenda huko, bado wengine wanaendelea kuuawa.
    Nyuma ya kila kitu, kuna mwanaume mmoja mwenye sura mbaya, tena akiwa ni Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, (DCP) Dickson ndiye ambaye anafanya mauaji hayo pasipo kugundulika.
    Kazi yake ni kununua machangudoa na yeyote atakayemgundua, humuua kikatili na kuondoka zake.
    Polisi wanachanganyikiwa, wanamtafuta muuaji, wanamkosa kwani anaonekana makini hasa kwenye kufuta alama za vidole vyake.

    Hali ya hofu inaendelea kutanda jijini Dar es Salaam.
    Je, nini kitafuatia?
    SONGA NAYO…
    Kule chooni alikoingia, Happy alifungua kipochi chake na kutoa bastola ndogo tayari kwa kumuweka chini ya ulinzi Kamanda Dickson pasipo kujua kwamba mtu huyo alikuwa hatari zaidi yake.
    Hakutaka kuchelewa kule, akatoka huku akijiamini kwani alikuwa na uhakika kwamba mwanaume huyo hakuwa akijua yeye alikuwa nani na chooni alikwenda kufanya nini. Akaufungua mlango kwa ajili ya kuingia chumbani, kitu kilichomshtua, ngumi moja nzito ikatua usoni mwake, akabaki akipepesuka, hapohapo akaanguka chini.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kamanda Dickson hakutaka kuchelewa, tena alipoiona bastola ile akagundua kwamba mtu huyo alikuwa hatari na kama angemuacha basi ilikuwa lazima afe, hivyo kitu cha haraka kilichomjia kichwani, iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumuua.
    Akamsogelea pale chini kwa lengo la kukamilisha alichokitaka, kwa ustadi mkubwa kama mtu aliyepitia mafunzo ya karate, Happy akainyanyua miguu yake na kuikamata shingo ya Kamanda Dickson na kumwangusha chini.
    “Kamanda…” alijikuta akiita Happy huku akionekana kuwa na mshtuko, hakuamini kile alichokiona, mkuu wake wa kazi ndiye aliyekuwa naye chumbani, tena akipambana naye kwa ajili ya kuuokoa uhai wake.
    “Koh koh koh…” Kamanda Dickson alijikuta akikohoa huku akijitahidi kuiondoa miguu ya Happy ambayo iliikaba shingo yake vilivyo.
    Dickson hakutaka kukubali, hakuwa tayari kuona akikamatwa kirahisi namna hiyo hivyo alichokifanya ni kujinyanyua pale chini alipokuwa, akamnyanyua Happy huku miguu ya msichana yule ikiendelea kuing’ang’ania shingo yake.
    Alimbeba juujuu na kumbamiza chini kwa kuanguka naye. Sauti kubwa ya maumivu ikasikika kutoka kwa msichana huyo, hata kabla hajajua nini cha kufanya, Dickson akajisogeza pembeni, akaishika shingo yake iliyokuwa na maumivu na kuanza kukohoa mfululizo.
    “Who the hell are you?” (Wewe ni nani?) aliuliza Dickson huku akimwangalia mwanamke huyo kwa macho ya mshangao, hakuamini kama kungekuwa na changudoa aliyekuwa na mbinu za kujihami namna ile.
    “I don’t know, I am here to kill you,” (Sijui, nipo hapa kwa ajili ya kukuua)

    Wote walisimama na kuanza kuangaliana, Happy alimwangalia kamanda wake ni kweli alimfahamu vilivyo, wakati mwingine alipokea amri kutoka kwa mkuu wake huyo na kuambiwa nini cha kufanya lakini kwa hali ilivyokuwa chumbani humo, hakukuwa na muda wa kupeana heshima tena, ulikuwa ni wakati wa hatari, wakati wa kuiokoa nafsi yake.
    “Kama unataka kuniua, niue kama utaweza! Ukishindwa, nakuua wewe,” alisema Dickson huku akikunja ngumi. Hakukuwa na kingine kilichofuata zaidi ya kupigana. Kila mmoja alipitia mafunzo makali lakini kwa Dickson alionekana kuwa hodari katika kurusha ngumi mfululizo, mateke na hata ukwepaji wake ulionesha kabisa kwamba alikuwa mzuri katika kupambana tofauti na Happy.
    Dakika kumi na tano zilikatika huku wakiendelea kuoneshana kazi, tena kimyakimya pasipo kuwasumbua wateja wengine waliokuwa kwenye vyumba vingine. Happy akaishiwa nguvu, akashtukia akipigwa ngumi mfululizo zilizomchanganya na kujikuta akiangukia kitandani huku uso wake ukiwa umevimba vilivyo na damu zikimtoka. Akabaki akipiga kelele tu. Akawahiwa kwa kuzibwa mdomo.
    “Nyamazaaa…” alisema Kamanda Dickson kwa ukali huku akimziba mdomo.

    Wakati akiwa amemtuliza pale kitandani, mara akasikia mlango ukigongwa, akajua fika kwamba mgongaji alikuwa mhudumu wa gesti ile hivyo akaufuata mlango na kuufungua, hata kuvaa kofia yake alisahau kuivaa.

    “Nikusaidie nini?”
    “Nimesikia kelele kaka…”

    “Ndiyo! Ni kelele za mahaba… na wewe unataka?”

    “Hapana! Samahani, nilifikiri mnahitaji msaada,” alisema msichana yule huku akitetemeka.
    Dickson hakutaka kuzungumza sana, akaufunga mlango na kumfuata Happy kitandani pale, kilichofuatia ni kuendelea kumpiga ngumi za uso mfululizo na mwisho kabisa akainyonga shingo yake kwa kumkaba.
    “Kwisha kazi…” alijisemea Dickson huku akikaa pembeni.

    Alikaa kwa dakika kama kumi hivi ndipo alipokumbuka jambo moja la muhimu sana. Wakati ameufungua mlango na kuzungumza na dada wa mapokezi, hakuwa na kofia ya kuuficha uso wake na ndiyo maana dada yule alikuwa akizungumza naye huku akitetemeka, hasa baada ya kugundua alikuwa akizungumza na nani.
    “Kanigundua…kanigundua…ni lazima nimuue,” alisema Dickson huku akionekana kuchanganyikiwa.
    Harakaharaka akainuka kutoka pale kitandani, akaufuata mlango na kutoka. Breki ya kwanza ilikuwa mapokezi, alipofika hapo, dada huyo hakuwepo, alichanganyikiwa zaidi, akaanza kuita kwa kuhisi labda msichana huyo alikuwa sehemu, hakuisikia sauti iliyoitikia.
    Huku akiangalia huku na kule, ghafla akasikia sauti za watu nje wakija, maneno aliyoyasikia ni koplo, kamanda na mkuu, mbali na maneno hayo, akasikia sauti ya msichana, akajua kwamba dada huyo wa mapokezi alikwenda kuwaita polisi, alichokifanya, akaufunga mlango wa kuingilia ndani ya gesti ile, polisi wale wakaanza kugonga kwa nguvu.
    “Fungua mlango… fungua mlango kabla hatujauvunja,” alimsikia polisi mmoja ambaye alizungumza huku akiikoki bunduki yake, Dickson akabaki akiwa amesimama, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alichanganyikiwa, hakujua kama alitakiwa kuufungua mlango au la.
    Kilichomchanganya zaidi, aligundulika kama alikuwa yeye, maiti ya kule ndani ilimtia hofu kubwa, hakujua afanye nini, kwanza akasimama na kuanza kujifikiria, polisi waliendelea kugonga mlango wakitaka wafunguliwe.
    “Siwezi kukamatwa kijinga…” alijisemea Dickson, kweli, kwa jinsi hali ilivyokuwa, lingekuwa jambo gumu kwa mtu kama yeye kukamatwa kizembe namna ile. Ghafla, polisi wale wakaanza kupiga teke mlango kwa lengo la kuuvunja huku yeye akiwa amesimama, tena amepigwa butwaa.


    ********************
    ********************
    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam

    kufuatia kupotea mfululizo kwa machangudoa

    katika mazingira ya kutatanisha. Taharuki kubwa

    inazuka kwani ndani ya kipindi kifupi tu, zaidi ya

    machangudoa kumi na moja wanapotea na

    hakuna anayejua walikopotelea. Jambo hilo linasababisha jeshi la polisi kuingilia

    kati. Kinachozidi kuzua utata, wote wanapotea

    katika mazingira yanayofanana. Mwanaume

    mmoja asiyejulikana, aliyekuwa anatembelea

    gari la kifahari aina ya Volkswagen, aliyekuwa

    akienda eneo hilo usiku wa manane ndiye

    anayehusishwa na wote wanaopotea. Upande wa pili, kijana aliyekuwa na mwonekano

    tofauti na binadamu wa kawaida, Dickson

    Maduhu au Zinja kama wenzake walivyokuwa

    wakimtania, amejiunga na Chuo Kikuu cha Dar

    es Salaam. Hisia kali za mapenzi zinasababisha

    kijana huyo aanze kutoka usiku na kwenda

    kutafuta machangudoa. Hivyo baadaye

    anahamishiwa Dar es Salaam. Baada ya kuwa DCP, Dickson anakutana na

    msichana aitwaye Pamela, anatokea kuvutiwa

    naye, anafanya naye mapenzi kwa kumnunua

    Kinondoni. Kupitia changudoa huyo aliyetoka

    Arusha, anajikuta akianza kuwaua wanawake

    wengi jijini Dar es Salaam. Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO… Idadi kubwa ya watu ilikusanyika nje ya gesti

    ya Mkombothi iliyokuwa Kinondoni jijini Dar.

    Minong’ono ilisikika kila kona kwamba ndani ya

    gesti hiyo kulikuwa na msichana aliyekuwa

    ameuawa. Kila mmoja aliyesikia minong’ono hiyo

    alishindwa kuamini hivyo watu wengi kutaka

    kwenda ndani kujionea wao wenyewe. Wanaume

    waliokuwa na nguvu ambao ndiyo walikuwa watu

    wa kwanza kupewa taarifa hiyo walifanya kazi

    ya ziada ya kuwazuia watu kuingia ndani. Waliokuwa na simu zenye kamera, kama

    kawaida yao walikuwa bize kupiga picha,

    walitaka kuwa wa kwanza kutoa taarifa katika

    mitandao ya kijamii. Hakukuwa na mtu

    aliyekumbuka kuwapigia simu polisi,

    walichokifikiria kwanza kilikuwa ni mitandao ya

    kijamii tu. Umati wa watu ulizidi kuongezeka huku kila mtu

    akiongea lake, baadhi ya wanawake waliopewa

    nafasi ya kwenda chumbani, waliporudi

    walikuwa wakilia huku wakisema kwamba

    mwanamke aliyeuawa kikatili alikuwa Shamila. “Shamila!” Haiwezekani! Ni jana tu nilikuwa

    naye!” alisema kijana mmoja huku akionekana

    kutokuamini kabisa. Jina la Shamila likaanza kusikika masikioni mwa

    watu. Walimfahamu msichana huyo, japokuwa

    alikuwa maarufu kwa kujiuza lakini alikuwa

    msichana wa tofauti kabisa. Alikuwa

    mchangamfu na aliyependa kuzungumza na kila

    mtu, hakuwa msichana wa majivuno, hata kwa

    kidogo alichokuwa nacho, alikuwa radhi

    kumpatia hata na mwingine. “Ni kweli Shamila au nimemfananisha?” aliuliza

    jamaa mmoja. “Ni yeye! Ni Shamila kweli!” Pamela akafika mahali hapo, alipoambiwa

    kwamba Shamila alikutwa akiwa ameuawa

    chumbani kwake, hakuamini. Alitaka kujionea

    kwani usiku uliopita tu alikuwa naye Kinondoni

    mpaka alipoamua kuondoka kwa sababu alikosa

    wateja. Akaruhusiwa kwenda ndani. Hazikuwa tetesi,

    kile alichokisikia ndicho alichokutana nacho

    ndani. Mwili wa Shamila ulikuwa kitandani,

    mdomoni alikuwa na alama zilizoonesha

    kwamba kabla ya kuuawa alitokwa sana na

    mapovu mdomoni.

    Pamela akashindwa kuvumilia, hapohapo

    machozi yakaanza kumtoka, picha aliyoiona

    kitandani ilimsisimua sana hivyo kujikuta akitoka

    nje huku akilia kwa sauti. Lilikuwa pigo kubwa kwa machangudoa

    wengine. Hazikupita dakika nyingi, polisi

    wakafika katika gesti hiyo na kuingia ndani, mtu

    wa kwanza kabisa kumshikilia kama mtuhumiwa

    namba moja alikuwa dada wa mapokezi.

    “Jamani sijui chochote kile,” alisema msichana

    huyo.

    “Sawa! Ila twende kituoni, tunataka uisaidie

    polisi,” alisema polisi mmoja, dada yule wa

    mapokezi akafungwa pingu, mwili wa Shamila

    ukatolewa ndani. Watu walipouona ukitolewa, hawakuamini,

    wakabaki wakilia, ni kweli, mtu aliyekuwa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ameuawa ndani ya chumba kile alikuwa Shamila,

    hivyo akaacha vilio vikubwa katika mtaa

    aliokuwa akiishi.

    Muuaji hakujulikana, hata dada yule alipoulizwa

    juu ya muuaji huyo, alishindwa kumfahamu ila

    kitu pekee alichokisema ni kwamba mwanaume

    huyo alivalia kofia kubwa ya Marlboro, hivyo

    hakuweza kumgundua usoni. “Alivalia kofia ya Marlboro?” aliuliza polisi kana

    kwamba hakuwa amesikia. “Ndiyo!” “Haukuweza kuuona uso wake?” “Ndiyo afande.”

    Maelezo ya dada yule yakawarudisha nyuma

    kabisa na kukumbuka kwamba wanawake

    kadhaa waliouawa kipindi cha nyuma, waliuawa

    na mtu huyohuyo ambaye kila siku alionekana

    kuvalia kofia kubwa. Hawakujua mtu huyo alikuwa nani na kwa nini

    aliwaua wanawake tu. Polisi walichanganyikiwa,

    hawakujua pa kuanzia kwani hata nyakati za

    usiku walipokuwa wakitembea kama kufanya

    doria, walikutana na watu wengi waliovalia kofia

    za namna hiyo hivyo kuwa na wakati mgumu wa

    kumfahamu mhusika. “Ila huyu muuaji ni nani?” aliuliza polisi mmoja,

    alionekana kuchoka, walizunguka sehemu kubwa

    jijini Dar kufanya doria lakini hakukuwa na dalili

    zozote zile.

    “Hata mimi sifahamu! Hapa inabidi tuongeze

    kasi, la sivyo wanawake wengi hapa Dar

    watauawa,” alisema polisi mmoja. Wakati polisi wakiendelea na doria yao, upande

    wa pili Kamanda Dickson alikuwa na mawazo

    tele, moyo wake ulianza kuridhika kutokana na

    kile alichokifanya, aliambiwa kwamba mbali na

    Hadija kulikuwa na wasichana watatu na mmoja

    alikuwa amekwishamuua na walibaki wawili

    kabla ya kumalizia na mhusika mwenyewe

    ambaye ni Hadija. Usiku wa siku hiyo, alishinda akinywa pombe

    nyumbani kwake, kichwa chake bado kilikuwa na

    mawazo tele, kila kitu kilichokuwa kikiendelea,

    kilimchanganya sana. Alijiona kuwa na roho mbaya lakini hakuwa na

    jinsi, alihitaji kuificha siri yake ili aishi kiamani

    na hakukuwa na kitu kingine cha kufanya

    kuificha siri hiyo zaidi ya kuua kama alivyokuwa

    akifanya. Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Pamela,

    japokuwa msichana huyu alikuwa changudoa

    lakini moyo wake ulimpenda, alikuwa radhi kwa

    kila kitu, kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa

    ajili ya msichana huyo kwake halikuwa tatizo

    kutokana na uzuri aliokuwa nao, aliona kustahili

    kufanyiwa mambo yote ili awe na furaha maisha

    yake yote. “Wa pili ni huyu Asha, nikimalizana naye,

    nahamia kwa Anita kisha kumuua Hadija

    mwenyewe, bila kufanya hivi, najua itakula

    kwangu tu,” alisema Kamanda Dickson kisha

    kujitupa kitandani kwake, akili yake ilichoka

    mno



    ********************
    ********************

    Hali ya sintofahamu inazuka jijini Dar es Salaam, machangudoa wengi wanaanza kuuawa katika mazingira ya kutatanisha. Hakuna anayemjua muuaji, kila changudoa anayenunuliwa na mwanaume aliyekuwa kwenye gari aina ya Volkswagen nyeusi, anauawa kikatili.
    Kila mmoja anaogopa, machangudoa wengine wanaacha kujiuza, wanajifungia vyumbani mwao, ila kwa wengine ambao hawakuweza kuishi bila kufanya biashara hiyo, wanakwenda huko, bado wengine wanaendelea kuuawa.
    Nyuma ya kila kitu, kuna mwanaume mmoja mwenye sura mbaya, tena akiwa ni Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, (DCP) Dickson ndiye ambaye anafanya mauaji hayo pasipo kugundulika. Kazi yake ni kununua machangudoa na yeyote atakayemgundua, humuua kikatili na kuondoka zake.
    Polisi wanachanganyikiwa, wanamtafuta muuaji, wanamkosa kwani anaonekana kuwa makini hasa kwenye kufuta alama za vidole vyake. Hali ya hofu inaendelea kutanda jijini Dar es Salaam.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
    Pamela alibaki akitetemeka pale kitini, kila alipomwangalia mwanaume yule aliyeingia, hakuonekana kuwa na utani, muonekano wake tu ulionesha kwamba alitaka kuambiwa ukweli juu ya kilichokuwa kikiendelea, vinginevyo asingeweza kueleweka.
    Mwanaume huyo akakaa kwenye kiti na kuweka zile karatasi juu ya meza, macho yake akayatuliza kwa Pamela ambaye tayari kijasho chembamba kilianza kumtoka huku kwa mbali akitetemeka kama mtu aliyeanza kuhisi baridi kali.
    “Unamfahamu huyu?” aliuliza mwanaume yule huku akimuoneshea Pamela picha ya Kamanda Dickson, yaani hata kumsalimia hakutaka, kwake, maswali yalikuwa muhimu zaidi ya salamu.
    “Nd..iy..o..” alijibu Pamela huku akitetemeka.

    “Ulishawahi kumuona wapi?”

    Hapo ndipo Pamela alipoanza kuhadithia namna alivyokutana na Kamanda Dickson tangu siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho kuachana naye. Katika kipindi chote hicho cha kuhadithia, mwanaume yule alikuwa kimya akimsikiliza, pale alipoona kulikuwa na jambo la muhimu kuandika, aliandika kwenye moja ya karatasi zake.
    “Ulishawahi kumuuliza kwa nini alikuwa akificha sura yake siku za kwanza?” aliuliza mwanaume yule.“Hapana! Sikutaka kujali sana kwa kuwa nilihisi kwamba yeye ni mume wa mtu hivyo hakutaka kugundulika, sikuwa na hofu, nilichokiangalia ni fedha tu,” alijibu Pamela.
    “Unahisi kwa nini aliwaua wanawake aliokuwa akiwachukua?”

    “Nahisi walimgundua. Hata siku ya kwanza nilipouona uso wake akaniuliza kwa nini sikushtuka au kuogopa? Kwa kuwa sikuwa namfahamu, nikamwambia siwezi kushtuka wala kuogopa. Nahisi wale waliomgundua ndiyo aliowaua kwa kudhani siri yake ingegundulika,” alisema Pamela.
    Kila swali aliloulizwa mahali pale, alijibu kiufasaha kabisa. Mahojiano hayo yalichukua zaidi ya dakika thelathini ndipo akaruhusiwa kuondoka huku akiambiwa kwamba alitakiwa kufika pale kituoni kila atakapokuwa akihitajika.

    * * * *

    Watu walijaa katika meza za wauza magazeti, walichokuwa wakikiona, hawakukiamini hata kidogo. Minong’ono ya hapa na pale ilikuwa ikisikika katika kila meza ya magazeti iliyokuwa imekusanya idadi kubwa ya watu.
    Habari iliyokuwa imeandikwa katika magazeti hayo, ilimshtua kila mmoja, hakukuwa na aliyeamini kwamba mtu aliyekuwa akiwaua wanawake wale katika kipindi chote hicho alikuwa Kamanda Dickson, mtu aliyeheshimika na kuogopwa mno na wahalifu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hiyo ndiyo ikawa habari ya mjini, kila gazeti lililokuwa na habari hiyo, lilinunulika na mpaka kufikia saa sita mchana, hakukuwa na gazeti lolote mitaani lililokuwa na habari kuhusu Kamanda Dickson.
    Habari hiyo haikuwa peke yake bali hata uthibitisho wa picha ya gari lake likiwa nje ya gesti moja Mwananyamala ilisindikizia habari hiyo kitu kilichowafanya watu wengi kuamini kwamba kamanda huyo ndiye alikuwa muuaji wa wanawake wale.

    “Mimi siamini mwenzenu…” alisikika mwanamke mmoja aliyesimama mbele ya meza moja ya magazeti.
    “Wewe ndiyo kama mimi! Eti Kamanda Dickson muuaji, sasa huku kuchafuana kumezidi, kwanza magazeti haya bora yafungiwe tu,” aliisema mwanaume mmoja aliyeonekana kukasirishwa mno na habari hiyo.
    “Kwanza haya magazeti yafungiwe kwa kumchafua kamanda wetu, mchapakazi na anayejitolea sana, pili ni lazima jeshi la polisi liingilie kati, haiwezekani lichafuliwe kiasi hiki tena kwa habari ya kuungaunga kama hii,” aliingilia mwanaume mwingine, kila mtu aliyekuwa mahali hapo alionekana kukasirishwa na habari ile.
    Mijadala iliendelea mitaani, watu walikuwa wakibishana kwamba inawezekana habari hizo zilikuwa ni za kutengenezwa kwa ajili ya kumchafua mtu fulani. Japokuwa ukweli uliandikwa gazetini lakini hakukuwa na mtu aliyeuamini, kila mmoja alihisi kwamba taarifa hizo zilikuwa kwa lengo la kumchafua kamanda huyo.
    Taarifa hazikutolewa gazetini tu, ilipofika saa saba mchana, karatasi zenye picha zake zikaanza kubandikwa katika vituo mbalimbali vya daladala, mitaani kwamba Dickson alikuwa mtu hatari na yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwake basi kitita cha shilingi milioni ishirini kingekuwa kama zawadi yake.
    Hapo ndipo wale watu ambao hawakuamini kilichoandikwa magazetini wakaamini. Hoja zikaibuka tena, mijadala ikaanza kwenye mitandao ya kijamii, watu wengi walikuwa wakilishutumu jeshi la polisi kwa kutokulivalia njuga suala hilo mpaka pale wanawake wengi walipouawa.
    “Polisi wazembe sana…” alilalamika jamaa mmoja pasipo kukumbuka kwamba mtu aliyekuwa akifanya mauaji alikuwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam.
    Kila mtu alizihitaji hizo milioni ishirini. Kumgundua Kamanda Dickson halikuwa jambo gumu, alijulikana kila kona, ubaya wa sura yake ulikuwa gumzo. Watu wakawa makini mitaani, wengi waliokuwa hata wakifanana naye walichukuliwa na kupelekwa kituoni.

    Siku ya kwanza ikapita, wananchi walikuwa makini kila kona lakini hawakuweza kumpata. Siku ya pili ikaingia, ya tatu mpaka ya nne lakini bado polisi na wananchi waliendelea kumtafuta pasipo mafanikio.
    Wakati polisi wakiendelea kumtafuta kwa kufuatilia hata akaunti zake benki, wakagundua kwamba siku moja nyuma, kiasi chote cha fedha alichokuwa nacho kilihamishwa na kupelekwa katika akaunti ambayo hawakuiona, walishindwa kufahamu ni nani aliyefanya hivyo na fedha hizo zilikuwa katika akaunti ya nani.
    Kama fedha zilihamishwa kisiri, ilimaanisha kwamba alikuwa sehemu. Yeye hakuwa na utaalamu wa masuala ya kompyuta, je ni nani aliyemsaidia kuhamisha fedha hizo pasipo benki kujua mahali zilipopelekwa? Mbali na hiyo, je, huyu Kamanda Dickson alikuwa wapi? Hilo ndilo swali alilojiuliza kila mtu pasipo kupata jibu.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

Blog