IMEANDIKWA NA : DOTO NSHIMBA (WISE JOHN)
*********************************************************************************
Simulizi : Jaha
Sehemu Ya Kwanza (1)
Alfajiri
ILIKUWA SAA 8:00 mchana baada ya kazi za bustani. Carolina alirejea nyumbani alipolelewa. Wakati huo ali-jihisi uchovu na alionekana mwingi wa mawazo hasa alipovuta kumbukumbu ya maisha aliyoishi wakati huo. Begani kwake mkono wa kuume alipachika jembe, mko-no wake wa kushoto alionekana kabeba dumu la maji na kichwani kaibeba ndoo yenye maji. Ungemtupia macho ungeona mgongoni akiwa na furushi la kanga alilokuwa kalibeba kama mtoto. Alikaza mwendo kwa ushupavu, shingo ikimcheza na ndoo kuyumbayumba. Kisha alifika upenuni kwa familia aliyokuwa kaizoea na kupaita kwao. Aliitua ndoo chini kisha kusimama kando. Aliyaagiza macho yake kulitazama gauni lake lililokuwa limelowa na kuchafuka matope na kufanya rangi yake kufifia kwa uchafu. Wazo lilimtawala wakati huo akajiuliza, kwa nini ndoto zake za elimu hazikutimia. Hakuishia hapo, Carolina alijisemea,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Carolina mie. Nitakuwa mgeni wa nani?
Kwa nini, kila nikitia juhudi zinaishia karaha?
Hivi, iweje baba yangu na utajiri wote huu asinipeleke shule? Ah!....”
Carolina aliwaza na kuwazua mengi wakati huo. Tayari macho yake ya gololi yalitekwa na vijito vya machozi yaliyokuwa yakishindana kwenda chini na kufanya mi-chirizi kwenye mashavu yake mororo. Alijikaza kuyazuia, kamwe hakufanikiwa. Kifua kilimtuna kwa huzuni na uchungu ukamnyima furaha. Kwikwi ya kilio ilibisha hodi na kuiteka furaha yote. Alijiinamia kuruhusu ma-chozi yaisabahi ardhi. Ardhi iliyomyima furaha na kum-fanya akose chachu ya bahati yake. Jicho lilikuwa je-kundu kama kaa la moto. Hakufahamu hata suluhu ya matatizo yake. Ilisikika sauti ikimwita naye kushtuka;
“Dada Caro. Mbona unaonekana mwenye huzuni?”
Sauti ilikuwa ni ya Huruma mtoto wa mwisho wa Mzee Malecha. Wakati huo naye alikuwa katokea kisimani. Aliitua ndoo yake chini sambamba na pale Carolina alii-tua ndoo yake. Alimsogelea na kumshika begani akimta-zama kwa huruma na upole. Carolina aliyafikicha macho yake kwa Kanga harakaharaka na kujibu;
“Si kitu Huruma.”
“Hapana. Mbona naona huna raha, hata macho yamekui-va! Kulikoni?”
Huruma alimpangusa machozi yaliyokuwa yakimbubuji-ka. Aliendelea kumdadisi ili kujua ukweli wa kilichoku-wa kimejiri.
“Dada, mbona huna raha, tena unalia-kwani kuna nini?”
“Hapana Huruma. Amini nipo sawa. Hakuna tatizo lolote mdogo wangu!”
“Huwezi kunificha Dada. Lazima kuna tatizo. Angalia, hata macho yako yanakushitaki, yameiva na kusinyaa kwa huzuni!”
“Hapana Huruma.” Carolina alijibu kwa haraka.
“Sasa kuna nini?” Huruma alihoji.
“Nimewaza mengi sana mdogo wangu. Kwa nini mimi naishi maisha haya kama kijakazi? Kwa baba yangu, tena naishi maisha yasiyo na mbele wala nyuma. Shule naitamani sana, na sijui kitatokea nini. Kutosoma nahisi uchungu sana kwani hata ndoto zangu nahisi kufifia.” Carolina alinyanyuka kwa hasira na kujiburuza akielekea chumbani.
“Nisubiri Dada Caro.” Huruma naye alichepua mguu kumfuata mule chumbani. Alijaribu kumtuliza ili aache kulia na kuishi katika simanzi. Je alifanikiwa?
*****
Kila kiumbe huzaliwa na bahati yake hapa duniani. Vi-levile, kila mmoja Mungu humchorea ramani kuwa ata-toka wapi na wapi ataishia. Sote hatulijui hilo hata kama tutakuwa wasomi wenye mrundikano wa shahada na sta-shahada. Kamwe hatuwezi kung’amua siri hiyo. Allah! Dunia isingelikuwa haki kama asingelizaliwa Binti huyu mrembo. Alizaliwam pengine pasipo utashi wa muumba. Maana katika siku yake ya kwanza kuinusa dunia alianza kuonja shubiri. Hakuyapenda maisha kwenye sayari yenye kiu ya kumficha kila kiumbe aonekanaye juu yake.
Dunia kamwe haizeeki na haimwogopi kiumbe yeyote juu yake. Ingekuwa kama ilivyo kwa wanadamu, basi ingekuwa tayari imezeeka na kuwa ajuza ama kikongwe asiyetambua wala kuhisi chochote. Hii ni kwa kutokuwa erevu na sahaulifu wakati wote. Ingawaje kuna mashaka yaliyotapakaa juu ya uso wa mrembo huyu, Carolina ba-do ni almasi iliyo lulu mbele ya wachuuzi wa miili ya warembo. Wakati wote mahangaiko na rasharasha ya furaha ni sehemu ya maisha yake. Aliyakumbuka maneno yaliyouchoma moyo wake. Huruma alitibua furaha za Carolina wakati huo.
“Da caro, kwani Mama na Baba yako ni wazee wetu ama?”
“Kwa nini uniulize hivyo? Huruma!”
“Ninataka kujua dada. Nilisikia siku moja minong’ono kuwa wewe si ndugu yetu wa damu”
“Ndiyo Huruma. Nasikitika sana kufahamu hili wakati huu ingali sijui la kufanya.” Carolina alijibu kwa un-yonge.
“Nieleze, ilikuwaje ukawa nasi hata leo tunaamini wewe ni ndugu yetu wa damu?” Huruma alihoji huku akimpa-pasa Carolina mabegani.
“Siku ya kuzaliwa kwangu inatosha kuelezea mapungufu katika maisha yangu. Ilikuwa mwezi wa pili tarehe ya mwisho wa mwezi, wenye tarakimu mbili ya mwisho ikiwa tisa ndiyo nilizaliwa. Ilimaanisha kuwa miaka mingine hata kama nitajiandaa na sherehe ya kuzaliwa kwangu, nisingepata wasaa huo kutokana na siku hiyo kutofikiwa wala kupatikana katika majira ya ulimwengu. Ingawaje nilizaliwa mwezi wa wapendanao, kuzaliwa kwangu kilikuwa ndiyo kifo cha Mama yangu aliyejuli-kana sana kama Binti Majaliwa. Mama alifariki kutokana na uchungu alipotokwa damu nyingi wakati wa ugeni wangu nilipotaka kuinusa dunia. Hakika ilikuwa ishara mbaya pengine nuksi isiyotabiriwa mapema juu ya mai-sha yangu na Mamangu. Kweli Mama aliibeba mimba iliyonibeba mimi kwa zaidi ya miezi kumi na mitano pasipo matarajio ya kujifungua. Hii ilikuwa tofauti na mimba za wanawake wengine”
“Halafu ikawaje?” Huruma aliuliza.
“Ingawaje wahenga walisema, uchungu wa mwana au-juaye mzazi, kwa Mama yangu haikuwa hivyo. Mara nyingi alijitahidi kubwia madawa ya kienyeji ili kuipo-romoa mimba iliyotungisha wasifu wangu.”
“Kwa nini alitaka kuitoa mimba hiyo wakati kwa imani zetu ni dhambi kubwa?” Huruma aliuliza kwa sauti ya upole.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni kweli, hofu yake kubwa hadi kutaka kufanya hivyo ilikuwa kutofahamu nani ndiye mhusika wa mimba hiyo.”
“Yeye aliipataje, alikuwa....... Ah?”
“Hapana Huruma.”Carolina alidakia kwa haraka.
“………. mimba aliipata katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuleweshwa. Alileweshwa na wavulana siku ya mkesha wa noeli baada ya kutiliwa madawa ya kulevya kwenye soda na hatimaye alilewa na walimbaka kwa uchu.”
“Kwani hapakuwa na sheria za kuweza kumtetea? Hata hivyo, kwani hakuwafahamu waliombaka na kumpatia ujauzito?” Huruma alizidi kudadisi.
“Ilikuwa vigumu sana kuwafahamu kwani alikuwa ka-leweshwa na hajitambui. Hata hivyo japo alijua waliom-nunulia soda haikuwa rahisi moja kwa moja kueleweka kwa watu”
“Halafu, mbona..........” alikatishwa na Carolina alipoen-delea kumsimulia.
“ …… baada ya kitendo hicho kumfika, Mama alihisi dunia inamteta katika mboni zake. Alihisi aibu ikijaa juu ya uso wake. Alitumia kila aina ya uganga kuiharibu mimba hiyo. Alitumia shubiri, majani ya kisamvu kibichi na miarobaini aliyoichemsha na madawa mengine ya kienyeji, lakini katu hakufaulu. Mama hakukata tamaa, alikuwa mwenye fuadi, hakukata tamaa ingawaje ali-shindwa kutimiza unyama alioukusudia.”.
“Wewe ulifahamu vipi kuhusu yote haya?” Huruma ali-hoji.
“Nilisimuliwa na Marehemu Bibi yangu hata majirani walinijuza baada ya utando kunitoka machoni.”
“Dada, inaonesha mengi yaliyojiri. Baadaye ilikuwaje hadi tunaongea hapa?”
“Mama yangu hakubahatika kuinusa siku ya mahangaiko itakuwa lini hapa duniani. Ulikuwa usiku mmoja wenye huzuni ambapo Mama alishikwa na uchungu mkali uliomfanya ateremke chini ya sakafu yenye vumbi. Ali-teremka kutoka katika kitanda alichokuwa amezoea ku-kilalia tangu kuzaliwa kwake. Kilikuwa kitanda chenye matendegu ya miti na kilisanifiwa kwa ngozi ya ng’ombe na kufumwa sawia. Hakika kilikuwa kigumu pia imara sana. Kilikuwa ni kitanda mbadala wa kile kilichosukwa kwa waya, yaani teremka tukaze. Kwa kuwa waliishi katika hali ya ukata ulionuka, hakukuwa na kiberiti cha kuwasha kibatari walichoita koroboi nyakati zote. Mama alitegemea kijinga cha moto alichokuwa ameingiza chumbani kingemmulikia na aone pahala pa kujisitiri wakati huo. Haikuwa rahisi, mvua ilinyesha kwa fujo sana. Nyumba yao iliyoezekwa kwa majani, ilivuja kama mwembe. Matone ya mvujo yalizima moto wote na kubaki giza. Alitumia miali ya radi iliyokuwa ikimulika ikamsaidia kuona hali halisi katika sehemu aliyokuwa amejiegesha. Kwa kuwa nguvu zilimwisha, hakuweza hata kuita watu wamsikie wala hakusikiwa na waliokuwa chumba cha pili wamejipumzisha. Ilikuwa huzuni kubwa haielezeki.” Carolina anliangua kilio cha huzuni. Alishindwa kujizuia kwa yaliyompata yeye na mama yake.
“Mama yangu! Siijui sura yake mimi!”
“Usilie dada Carolina.” Huruma alimnyamazisha kwa upole.
“Mungu yupo atakujalia. Amini! Nafahamu kuwa ukiwa na kijeba rohoni dawa ni kukitoa. Jikaze yote yataisha na utasahau.”
Mrembo Carolina hakuwa na hali. Alijikaza kisabuni na kuendelea kumsimulia Huruma ili apunguze ujazo wa kijeba rohoni mwake. Carolina aliendelea;
“Kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Uzazi wa mama ulikuwa kama wa kinyonga. Kuwaona watoto wake mwenyewe si jambo rahisi hasa kutokana na kufa mara tu baada ya kujifungua. Hakuna ambaye alifahamu hata kutabiri kuwa Mama angepoteza maisha yake kwa kunizaa mimi. Wengi walihisi pengine angejifungua watoto mapacha kwa jinsi tumbo lake lilivyokuwa kubwa. Kitendawili kingine kilichokosa mteguaji katika kijiji cha Idubula alikoishi, ni juu ya nani ndiye abu wa ujauzito wa Mama yangu.”
Carolina alizidi kububujikwa na machozi. Alijikaza akaendelea baada ya kupangusa machozi yaliyokuwa yamefunika mashavu yake.
“Nani aliweza kumshawishi hadi asiishi katika kiapo chake pasipo kumwoa? Wengi walifahamu fika kuwa aliishi mbichi hadi umri wake wa miaka ishirini. Hakika alifanyiwa unyama mkubwa” Wakati huo Caro ali-shindwa kuendelea na simulizi lake. Alionekana mwenye majonzi yasiyo kifani.
Kwa mujibu wa bibi yake Bi Maua, alipozaliwa Carolina usiku ule wa shida, hakuna yeyote aliyefahamu katika nyumba hiyo. Carolina hakulia na wala hakutapatapa baada ya kuzaliwa ilivyo jadi ya kichanga aliyezaliwa punde. Ungeweza kushawishika kusema kuwa, Carolina alizaliwa taahira. Lakini haikuwa hivyo. Alikuwa ni mzima mwenye siha njema. Alikuwa anaomboleza kifo cha Mama yake pengine ndicho kilimfanya awe mkimya na asiweze hata kulia kama waliavyo vichanga wengine.
Naam! Binti Majaliwa hakuwa mzima tena. Ilipo wadia asubuhi baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza na wa mwisho, ambaye hata hakubahatika kumwona alikata kauli. Alitokwa na damu nyingi sana iliyomfanya apitil-ize kuliko mauti. Hali ya umauti ilimkuta kutokana na kukosa msaada pia mwangalizi ambaye angeweza ku-gundua hali hiyo mapema na kuinusuru.
Binti Majaliwa aliishi na wadogo zake wawili, Nyamizi na Endengula. Wote hawa walikuwa wasichana ambao pia walilala vyumba vyao tofauti. Kutokana na tabia za wasichana hawa hasa Nyamizi, zilikuwa si za kumcha Mungu wala kumsimulia jirani. Kweli kifo hufichua mengi. Hadi inagonga saa kumi na mbili asubuhi, Nya-mizi alikuwa ndio anarejea nyumbani akitokea kwa ha-wara yake. Ilivyokuwa kawaida yake, alirudi saa kumi na moja za alfajiri akihofu macho ya majirani kumshan-gaa. Kwa siku hiyo, alichelewa kurudi kutokana na mvua kubwa iliyomwagika hadi asubuhi ilivyojiri. Endengula yeye alilala fofofo kama maiti kutokana na kiubaridi kilichokuwa kimetanda wakati wa mvua hizo kali za masika kukatika.
Mara baada ya Nyamizi kuingia ndani ya nyumba yao akiusukuma mlango wa matete alihisi rindi la mtu aliyejilaza mlangoni kwa chumba cha dada yake. Alitaka kufahamu kinachojiri. Kwa kuwa alikuwa amehongwa tochi na bwanake, ilimlazimu amulike afahamu kulikoni juu ya kile akionacho. Alichokutana nacho, hakuamini macho yake na wala hakuweza kustahimili zaidi ya kububujikwa machozi kwa uchungu ulioishika nafsi yake.
“Mamaa!” Nyamizi alipiga makelele kuashiria tatizo.
Yalikuwa ni majonzi yasiyoweza kusimulika katika ujio wa Carolina. Binti Majaliwa alikuwa zamani alikwisha-kata kauli na alikakamaa kuashiria hana tena hali wala kauli na dunia hii isiyohuruma.
“Endengula! Endengula!.. amka – dada ame....”
Ilimbidi Nyamizi amwamshe Endengula na kumfahami-sha yaliyoisibu nyumba yao. Walilazimika kujikaza ki-sabuni wakizishauri nafsi zao kuamini kuwa yaliyopita si ndwele heri kuganga yajayo. Walishauriana kuwa wawajulishe majirani juu ya yale yaliyowasibu. Waliwajulisha majirani zao akiwemo Mzee Makaranga pamoja na mkewe. Hawa walikuwa watu wa kwanza kupata taarifa na walimfunika vema Binti Majaliwa kabla ya wanakijiji wengi kuwasili. Walifahamu pia kuwa, Carolina alikuwa amepoteza maisha yake. Wakati wakitaka kumhifadhi kichanga Carolina, Mama Makaranga alishtushwa na mtikisiko wa nguo waliyokuwa wamemfunika. Aligundua kuwa Carolina alikuwa mzima ndipo alipokimbilia mafuta ya karanga nyumbani kwake. Aliyachemsha na kisha kumsafisha akarejelea hali ya mtoto wa kawaida. Baada ya hapo, wote kijijini walijuzana kuhusu tukio hilo lililokuwa likiendelea kama ada yao.
Mzee Malecha aliipaza sauti yake kwa wanakijiji wali-pokusanyika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndugu zangu, yaliyopangwa yamepangwa. Binti yetu katutoka ingali tunamhitaji sana. Pamoja na hayo, inatupasa kutilia maanani miiko yetu. Wana Idubula wote tunafahamu mila zetu ni zipi hasa kutokana na aina ya tukio kama hili.”
Mzee Makaranga alidakia, “Kweli mzee Mwenzangu! Mila zetu zinatuzuia kumsitiri mtu ambaye alipata mimba wakati akiwa hana mume atambulikanaye katika jamii. Hii ni ishara mbaya hasa wakati wa mababu zetu. Je, leo bado hali hii ipo? Tukishiriki jambo hii tutakuwa tumetibua mikosi katika ardhi yetu! Ama kuna nini kitatokea?”
Mzee Makaranga aliendelea.... “Kwenu Wana Idubula! Binti yetu Binti Majaliwa hii leo ametutoka kwa aibu. Je tufanyeje wazee wangu? Mzee Malecha, tutumie kanuni zetu tulizoachiwa na mababu zetu. Mwili wake hautakiwi kuzikwa katika ardhi yetu. Tunatakiwa kwenda kuutupa mwili wake katika mto nje kidogo ya kijiji chetu. Hiyo itanusuru hali zetu.”
Mzee Malecha alidakia wakati huo, “Mtoto je?”
“Naye hukohuko! Hatufai kuwa naye. Ni mkosi! Huoni, Mama yake hakuwa na mume, hakuwahi kuolewa, ali-bakwa na pia amekufa pasipo kumwona na kasababisha kifo chake! Huyu ni mikosi! Naye tumpeleke, atamlea nani na wapi atamlelea?” Mzee Makaranga alisisitiza.
Wakati huu mzee Malecha alionekana mwenye mawazo mengi kichwani. Alishindwa kutangua zozo lililokuwa limetawala.
“Ndugu zangu, tunahitaji mabadiliko katika ardhi yetu. Nawaomba tuyape kisogo maisha ya gizani. Ulimwengu umebadilika sana siku hizi. Mimi siamini yote yale, Mzee Makaranga anasema.”
“Basi mchukue kamle nyama!” Makaranga aling’aka.
Wazee pembeni walinong’ona chini chini. “Hapana! Haiwezekani! Lazima tuwale masumle watu hawa. Walichokifanya si chema, kwani wao wanaona alichokifanya ni chema sana. Ng’ombe watatu walete hapa tuwachinje ndipo tufanye kazi hii.”
“Wazee wangu, naomba mniwie radhi kwa haya ya-nayoendelea hapa.” Mshauri wa kijiji aliomba kwa un-yenyekevu. “Nawaombeni sana tufanye la Mungu kama maagizo yake. La Mungu halina ibilisi wazee wangu. Tunao wajibu wa kuyarejea mafundisho ya Mungu kwa umoja wetu. Marehemu hajatukosea na wala hatuna haja ya kumkosea. Yeye aliyesirini anajua mapungufu yake. Sisi tutimize wajibu wetu. Tusihukumu kwani hata nasi siku moja tutahukumiwa!”
Kimya kinlitawala. Wakati huo wazee walijigawa ma-genge magenge. Waliteta, baadhi yao walianza kutoka na kususia shughuli hiyo.
“Ndugu Wanakijiji, kijiji chetu kinamatatizo mengi sana. Pamoja na hayo, leo tumepata la kuondokewa na mzinzi mmoja. Tumshukuru Mungu katupa fundisho juu ya tabia za ibilisi! Aliyebeba ujauzito na kusingizia kabakwa hata hakuwa na mume katutoka! Hii ni aibu sana! Kuweza kufuta aibu hii, sote turejee makwetu, wenzangu tukaje na kuni mbilimbili. Familia ya wafiwa watulipe masumule kwa kulifumbia macho jambo hili. Kwa nini waliruhusu haya yafanyike? Wote tunajua, mchelea mwana kulia, hulia yeye na samaki usipomkunja angali mbichi atakushinda akikauka. Ng’ombe watatu tunawahitaji wachinjwe ili tusafishe tawala yetu kwa damu. Palipo chafuka damu husafishwa kwa damu ndugu zangu!” Mzee Makaranga alikazia kauli yake.
“Wazee wangu, dada yangu alikuwa muumini wa ma-tendo mema hata hajawahi kwa makusudi yake kumtendea mtu hata jamii yetu ubaya. Tunaomba tumzike kwa utu wake, mashetani walimfanyia unyama!” Endengula alisisitiza kwa huruma.
“Sawa kabisa, hilo ndilo wazo sahihi.” Mshauri wa kijiji aliunga mkono hoja.
“Wewe mtoto, kati yako na sisi wazee wa ardhi hii, nani alitangulia kuliona jua? Nakuuliza, nani?” Angalia! Ku-na mamlaka gani inayoruhusu uchafu aliokuwa nao dada yenu! Wazazi wenu waliwafundisha mfanye ukahaba kisha mkivuna uozo msingizie shetani? Mzee Makaranga aliropoka bila tahayari kama mropo toka shimoni.
“Mzee Makaranga, naomba shuka kidogo tuelewane.” Mshauri alimsihi Makaranga.
“Marehemu hakufanya kosa hili kwa makusudi. Ilikuwa nje ya matakwa yake. Tambueni, alibakwa pasipo hiari yake. Hatuelewani?”
“Naunga mkono maoni ya ndugu Mshauri, ni ya kujen-ga. Tumzikeni kwa imani yake. Kama ni mdhambi ata-hukumiwa na aliyemuumba, kwani sisi hatuna alilotukosea na hatujamuumba, iweje leo tumhukumu?” alisema Malecha.
Makaranga alikataa katakata akitaka kujiengua. Wazee wa kijiji baadhi yao walionekana kuingiwa na maneno ya watetezi wa marehemu. Mzee mmoja alijitokeza na kuuamsha ulimi wake. Alikuwa mpigadomo ayari mwenye ulimi mtamu. Alinyanyuka na kusema, “Ndugu zangu, naomba tukumbushane mafundisho ya wazee wetu waliosema.. mauti ni siri kubwa zaidi ya uumbaji wa mwanadamu yeyote. Na je, nani afahamuye kesho kutatokea nini kwake na hata apange na atoe kila kilicho chema kumpatia maskini ili asamehewe? Kama tunawe-za kumsamehe tudhanie ni mwovu, basi tumezisamehe nafsi zetu. Tusitengane kwa jambo dogo. Tumzikeni watakavyo, katu hatutapata makovu!”
Alipokwisha kuyanena maneno hayo, Mzee Malecha na mshauri wa kijiji walimuunga mkono mzee huyo. Mazi-shi yalandaliwa na walikubaliana kumsitiri mama huyu katika makaburi ya kijiji yaliyoko pembeni kidogo ya kijiji cha Idubula. Ingawaje minong’ono ilikuwepo, wote waliafiki kutimiza jambo hilo.
Ilikuwa safari yake ya mwisho katika uso wa dunia hii. Hakika ilikuwa ni majonzi yaliyotanda katika familia ya Mzee Majaliwa na mkewe Maua. Bibi Maua alijawa na simanzi hasa baada ya kuona wanae tayari wameshafika wanne kuwekwa kwenye kaburi la sahau. Watatu walifariki kwa sababu ya ndui na wakati huo binti yao alifariki kwa uzazi. Alihesabu uzao wa tumbo lake, aliona amebakiza watoto wanne. Watoto wake watatu wote ni wakike na mmoja pekee ndiye mtoto wa kiume aliyeamini ndiyo kichwa cha nyumba yake.
*****
Ili kudhihirisha kuwa Carolina alikuwa kiumbe mwenye karama kwa Mungu na duniani, alibahatika kulelewa na mama mmoja aliyejitolea. Mama huyu alijulikana kama Mama Saraganda. Mama huyu alijifungua usiku uliofuata baada ya kifo cha Binti Majaliwa na alijaliwa mtoto wa kiume aliyempatia jina Saraganda. Mama huyo alijitolea kumlea Carolina. Alinyonya pamoja na mwanae hadi pale alipokoma akiwa na miaka mitatu. Carolina aliendelea kuishi na familia ya mama huyo na alimzoea kama mzazi wake. Wakati wa utoto wake, maanani alimwepusha na majanga mengi. Hakuugua wala kupatwa na tatizo lolote kiafya. Alichokuwa anafahamu ni kwamba, Mama yake ndiye Mama Saraganda na alijua walizaliwa mapacha na mvulana aliyeitwa Saraganda. Hadi alipofikia umri wa miaka kumi na mitatu, alifahamu hivyo. Alifahamu pia kuwa, Nyamizi na Endengula ni ndugu zake wa kawaida wala si mama zake wadogo kwa vile aliishi nao mbali mbali.
Wakati akiendelea na masomo ya shule ya msingi hapo kijijini, binti huyu alikuwa nyota isiyoweza kuzimwa hata na mawingu yatandayo angani. Alikuwa na akili nyingi darasani achilia mbali sauti yake ya kasuku kama si chiriku. Aliposhiriki katika mashindano ya Umta-shumta kwaya yao ilishinda kwaya zote zilizoshiriki. Hakika wengine wote hawakufua dafu.
Hakujaliwa sura pekee, Maulana alimtunuku mwili ulio na mvuto. Umbo lake lilikuwa la kuvutia. Namba nane iliyosimama, kiuno kama dondola na makalio yenye mvuto ambapo kila nguo aliyovaa ilimkaa ipasavyo. Hata kama alivaa nguo ronya zilizochukiza wengine na kuwafanya manungayembe, kwake yeye alionekana ni malkia. Ngozi yake ilikuwa mororo kama mgongo wa chupa. Hakutumia vipodozi vya aina yoyote kuuchuna mwili wake. Kwake ilimtosha kutumia mafuta ya mgan-do baada ya kuogea sabuni ya mche pasipo wasiwasi wowote. Hakumfahamu mwanamume kitu ambacho ki-limfanya sikumoja wakati wa somo la sayansi kuhusu uzazi aulize na wenzake kumcheka sana. Aliuliza…. eti mwalimu, --- una mfupa?
Carolina alikuwa na tabia njema zilizoipendeza shule nzima. Alikuwa mwenye bidii ya kazi shuleni hata nje ya shule. Katika mashindano ya wilaya alifika hadi mkoani ingawaje alionekana ni mshamba. Sauti yake ilimfanya ateuliwe peke yake kutoka mkoani akiliacha kundi lake ili kujiunga na timu ya mkoa kushiriki mashindano ya Taifa. Mafanikio hayo yote yalikuwa ni kwa sababu ya sauti yake iliyoweza kumtoa nyoka pangoni. Ingekuwa leo hii sauti yake ingemtajirisha maradufu. Angejijengea majumba ya kifahari na pengine angemiliki magari na kutukuka kote Afrika mashariki kwa sauti yake. Kama angeimba bongo fleva na hata kama angeimba taarabu pengine sauti yake ingekonga nyoyo za wengi zaidi ya Bi Kidude na kuwafanya wanaume wenye uchu wa kufisadi maisha ya warembo wamtafute wauone wajihi wake.
Ingawaje wahenga husema, Mungu hamtupi mja wake, mola alimtelekeza Carolina. Alikuwa si mbumbumbu wala si mbongompozeni, alipokuwa darasani. Cha ku-shangaza, matokeo ya darasa la saba yalivyotangazwa katika wilaya ya Nzega, yeye hakuchaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza. Ilionesha hakuwa na bahati ya maisha ya elimu. Jambo hili liliiumiza sana nafsi yake. Alibubujikwa na machozi ya huruma akiihurumia nafsi yake. Alipenda sana kusoma binti huyu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika familia aliyolelewa walikuwa ni wafugaji wa ng’ombe. Familia hiyo kwa kadirio la karibu walikuwa na ng’ombe wasiopungua mia mbili. Kila rangi na kila aina ya ng’ombe walifugwa. Alikuwa akijihesabu ni mzaliwa pacha wa familia hiyo. Alijua hata kama an-geamua kusoma katika shule za watu binafsi angeweza kufanya hivyo kwani mali ilikuwepo. Kwa kuwa alifa-hamu abu yake ni mzee Malecha, mwenye mifugo isiyohesabika ilibidi amvae jioni moja. Alimweleza hisia zake kama baba yake. Tabia za Carolina za kuwa kama ahali mwenye bashasha wakati wote zilimpendeza Mzee Malecha. Alitaka kumsaidia ipasavyo. Kilichokuwepo kwanza ni kumweleza ukweli kuhusu yeye. Nani alimweleza Carolina ukweli wa mambo? Na je alielewa kuhusu hilo?.
Ama kweli siku hazigandi kama mwanamuziki binti machozi alivyoimba. Hatimaye siku iliwadia. Walipata wasaa wa kuketi faragha baada ya kuwaita mama zake wadogo na nduguze wengine pamoja na familia ya mzee Malecha. Kabla ya kumweleza waliketi na kumuita Car-olina toka chumba alikokuwa akilala.
Waliporejelea mazungumzo walianza kwa kupeana taarifa za maisha ya kawaida ya binadamu waliopitia shida. Waliongea maneno mengi, miongoni mwa maneno aliyoyatoa Mzee Malecha baada ya kupata fursa hiyo yalikuwa ya hekima. Alitumia utajiri wake wa lugha kufikisha ujumbe kwa Carolina aliposema,
“Chausiku mtoto wangu! Wewe ni ashirafu katika fami-lia yangu. Ukweli wa Mungu unanituma kusema hivyo kwa kuwa wewe si ayari wa maneno ya mitaani. Napen-da nitumie fursa hii hapa leo kukutanabahishia yote ku-husu maisha yako. Mwanangu, kama ndugu zako wataa-fiki mimi nipo tayari kujitolea kukusaidia usome kama ilivyokuwa kukulea hadi leo hii.”
Alipoyatamka maneno “kama ndugu zako wataafiki mi-mi nipo tayari kujitolea kukusaida”…….. Carolina alishtuka sana.
“Unataka kujitolea?” Carolina alihoji kwa ukali.
“Iweje baba yangu mzazi atake kujitolea kama si wajibu wake kufanya hivyo?”
Baada ya kupata mshtuko huo ilibidi afafanuliwe na ku-elezwa ukweli wote wa mambo na jinsi alivyolelewa katika familia hiyo.
Mzee Malecha aliendelea, “Carolina Mama, nakusihi uwe mtulivu. Nafahamu jambo hili litakuumiza nafsi yako. Hakuna jinsi kwani itatuwia vigumu kuendelea kuuficha ukweli wa mambo.”
“Mbona siwaelewi?” Carolina aling’aka.
“Iweje mnazungumza maneno nisiyo yafahamu. Mna maana gani?”
“Mwanangu, tunakupenda, hata baada ya mazungumzo haya tutaendelea kuishi nawe kama mazoea yetu yalivyo. Kwa ufupi, wewe ni Carolina! Mama yako si huyu umwonaye hapa. Si Mama Saraganda! Mama huyu alikulea tangu siku ukiwa na siku ya pili hapa ulimwenguni mara baada ya kifo cha Mama yako Binti Majaliwa. Mama huyu alikunyonyesha na kukujali hadi hii leo unavyoishi nasi hapa na kumwita.”
“Mbona sielewi! Na Baba yangu je?” Carolina alizidi kukanganyikiwa wakati huo. Machozi yalimtoroka ma-choni na kuchuruzika mashavuni. Midomo yake ilimtikisika kwa huzuni.
“Baba yako hakupata kufahamika. Mama yako aliupata ujauzito baada ya kuwa amebakwa na vijana wakati wa mkesha wa noeli.” Mzee Malecha alisisitiza.
Baada ya kuelezwa aliangua kilio. Machozi yalizidi kumtiririka kama mito itokayo nyikani. Hakumfahamu baba yake wala mama yake ni nani. Mafuriko yalivamia macho yake ya gololi kwa chozi lililobubujika kwa uchungu. Si chozi la furaha ya kufahamu ukweli wala huzuni ya kifo cha mamake bali alilia akiihurumia nafsi yake.
Wakati yakijiri hayo, hapakuwa na mtu aliyebaki mkame machoni kwake. Waliokusanyika katika faragha hiyo wote walitokwa na machozi ya huruma na kumhurumia sana yatima Carolina. Ukweli ni kwamba, waliiumiza nafsi yake hasa baada ya kufahamu jinsi mama yake alivyopoteza maisha wakati yeye anazaliwa. Alimhurumia mama yake jinsi alivyoteseka na hadi kupoteza maisha. Hakika hakupata taswira kichwani mwake, na alijisemea;
“Mola wangu, wajua shida zangu!
Nakutegemea kuyategemeza maisha yangu.
Iokoe nafsi yangu!
Eee mola, nioneshe njia nikufuate hadi kufa kwangu!” Aliikusanya mikono yake kwa unyenyekevu na kupiga magoti akisujudu.
Baada ya kauli hiyo aliwataka radhi pia alitoa neno la shukrani kwa familia ya mzee Malecha hasa kwa yote waliyomfanyia naye kuyafanya pahala hapo. Hakuchelea kunena kuwa;
“Ndugu zangu, asiyeshukrani ni mwivi wa fadhila.
Nawashukuruni sana kwa kunihifadhi hadi leo.
Mama Saraganda! Nakupenda Mama yangu!
Nakupenda sana!
Nawaomba mnisamehe kama kuna jambo niliwakwaza kwa muda wote.
Nafahamu, nilitenda na kuishi kama mtoto halali ingali haramu.
Naomba mnisamehe!” Carolina aliangua kilio na Mama Saraganda alimkumbatia kumnyamazisha naye akiwa anabubujikwa na machozi.
Alitoa shukrani na kuipongeza familia ya mzee Malecha hasa kwa jinsi walivyomlea bila ubaguzi wowote na kumpatia kila hitaji lake la msingi. Alipatwa na simanzi ambalo hakulitegemea kugubika furaha yake. Kwa kuwa mtu hawezi kuzuia mvua kunyesha, haikuwa budi yake kumshukuru Mungu kwa yote hayo. Aliyafuta machozi yake na macho yake yalikolea kuwa mekundu kama vile ameyatia pilipili manga.
Asili yake kuwa mshairi, Carolina aliona kuna haja ya kujiunga na makundi ya uimbaji katika kijiji cha Idubu-la. Aliamua kufanya hivyo angalau kujiliwaza na ma-chungu yalomkabili wakati wote. Alishiriki kama mwi-baji aliyekamili hadi pale alipobadili mfumo wake wa maisha. Katika maisha yake alipenda sana aitwe ‘Caro-lina mwimbaji’ akilipa kisogo jina la asili alilozaliwa nalo la Chausiku. Alipenda sana aitwe jina la marehemu mama yake yaani Carolina. Alilipenda sana jina hilo ili kulienzi kwa heshima ya mama yake aliyeshindwa kuu-ona wajihi wake hata mara moja.
Ingawaje aliendelea kuishi katika familia ya mzee Malecha, furaha yake ilififia wakati huo. Hakuwa mwenye furaha na huru kama alivyokuwa awali. Alikuwa mwenye kuzongwa na mawazo mengi hatimaye mwili wake ulianza kudhoofika mithili ya mgonjwa wa unyafuzi. Waimbaji wenziwe walimshauri sana ajitahidi kutoonesha huzuni. Yote yaliwezekana, lakini usiku ilikuwa ni ngoma isiyoweza kushinda. Alikosa hata lepe la usingizi wakati wote. Alipata usingizi wa mang’amung’amu kwa ndoto za mara kwa mara akijaribu kuiumba taswira ya marehemu mama yake na hata kutaka kufahamu kuhusu baba yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati akishiriki uimbaji wa kuburudisha Carolina ha-kuchelewa kuwatembele Mashehe na Makasisi ili wam-patie ushauri wa kiroho. Aliposhindwa kufanya hivyo alitembelea familia za watu ambao walijulikana kwa tabia zao njema na hekima za kujenga. Kwa ukarimu wao walimsaidia sana na hatimaye taratibu alianza kuyazoea machungu hayo. Hakutaka tena kuendela kuomba familia ya mzee Malecha imsomeshe. Wakati huo aliwaza ni jinsi gani angeweza kujitegemea. Carolina hakuwa na bahati wakati huo. Kila alipojaribu yote yaliishia ukingoni. Hakuna shaka alijiwazia sana wakati wote. Kila mara alijiuliza kwa nini azaliwe katika mateso yote hayo. Mara zote alikuwa akiimba shairi alilojitungia nyakati za usiku kabla ya kulala na hata wakati ambapo usingizi ulimruka. Shairi alilolitunga Carolina aliliimba;
Asilani sisahau, hakuna mwenye fuadi
Kweli dunia jahimu, amebakia adili
Walah sioni hamu, nashukuru wewe mwali
Chozi langu la huruma, unisamehe manani.
Abadani sina hamu, mamangu simfahamu
Nimebaki sina hamu, sina baba wala babu
Wajihi wangu kwa Mungu, ndugu zangu ni adimu
Chozi langu la huruma, unisamehe manani.
Sifahamu kifo changu, nimekuwa ni kikono
Kama changu baragumu, baharini na mikoko
Mola nitoe jahimu, siyo kama koromeo
Chozi langu la huruma, unisamehe manani
Jomba wangu simjui, kuolewa naogopa
Si shangazi wala bibi, wala siyo ni mgumba
Nani atanisitiri, bali woga wangu kufa
Chozi langu la huruma, unisamehe manani
Shoga zangu wanitusi, nywele zangu ka arufu
Waniita mkimbizi, sura yangu ina uzu
Napenda ani kuishi, natembea mi ni mfu
Chozi langu la huruma, unisamehe manani
Nawaombea kwa mola, niongoze wewe mola
Wote wanaonipenda, nawaombea kwa Mola
Awazidishie mola, si andisi nimekuwa
Chozi langu la huruma, unisamehe manani
Amali zangu kwa Mungu, ami we nakutafuta
Ali yangu si kwa mtu, si maisha ya anasa
Alifu ndo nilikuwa, si maisha ya anasa
Chozi langu la huruma, unisamehe manani
Beti zangu nakatiza , niombeeni kwa Mungu
Sina raha ni karaha, Mamangu ye hakutubu
Sina ajira ya maka, Kifo chake si juzuu
Chozi langu la huruma, unisamehe manani
Wakati akiimba shairi hili, Carolina alitokwa na machozi. Hisia zake zilimfikisha mbali katika bahari ya akali. Angali kijijini aliamua kujitegemeza na kilimo. Alizoa mbolea na kuanzisha bustani ya mboga. Alifanya hivyo ili kuhakikisha mkono wake unaenda kinywani achilia mbali kujipatia amali zake mwenyewe pasipo kumtegemea mtu. Hakika alifanikiwa sana na mola hakumtupa sana wakati huo. Alijulikana kijiji kizima kwa tabia zake njema. walimuita mtoto mwenye heri mshiriki wa matendo mema.
*****
Ilimchukua miezi minane ndoto yake ya kusoma ilipo-mrejea kichwani tena. Aliamua ajiunge na shule ya ufundi sanifu angalau apate vya kwake. Hisia zake zilimtuma kukimbilia mjini. Hakufahamu aanzie wapi ili kutafuta maisha. Wazo lake lilimea rohoni kama mmea wa msonobari. Alijiweka mikononi mwa Manani amfungulie njia ya kwenda mjini. Hakika penye nia pana njia, mola alimsikia na kumjaza fanaka rohoni mwake.
Mawio
CAROLINA AKIWA KIGOLI mwenye mvuto, aliyapa kisogo maisha ya kijiji. Alipofanikiwa kuishika njia ielekeayo mjini, safari yake ilikuwa yenye fanaka wala hakukwa na ajizi.
Ingawa wahenga husema, aliyebahati habahatiki, Caroli-na alipata bahati dume. Ilikuwa bahati iliyoshinda huzuni yake yote. Kwake ilikuwa kama anaota ndoto, ndoto ya mchana peupe. Adhuhuri moja akitokea bustanini kwake, alikuwa amechoka sana na alilowa chepechepe kwa maji ya lambo. Si ajabu hali hiyo aliizoea kwa kumwagilia mazao yake. Kanga yake yenye rangi ya manjano aliibeba mkono wake wa kushoto, ndani yake aliviringa nyanyachungu. Ndoo ya maji alijitwisha kichwani kama kawaida yake. Mkono wake wa kuume alibeba galoni la lita tano ambamo pia alitia maji ya chemchemi. Mabegani alipachika jembe akirejea maskani.
Wazo lilimvamia na lilipasua kichwa chake. Aliwaza ataishi vipi wakati huo. Wavulana wengi walimfuata ilhali alisimama asadi. Vijana wengi barubaru magwiji walimmendea. Asilani hakulewa kwa maneno yenye gube. Alijiwekea habedari, kutolewa maneno ya kumru-sa. Hakupenda gubu, alipenda heri.
Aliukaza mguu wake kuwahi nyumbani. Alipowasili palipo miembe saba, aliwaona vijana wawili. Kijana mmoja alikuwa Sinde ambaye huimba naye ngomani. Mvulana wa pili waliyefuatana naye alikuwa ni Tora, kijana huyu alikuwa mwembamba mwenye maringo. Wote wawili walimkodolea macho hata kabla ya kumsabahi. Walipomtazama walimwonea huruma na kisha walimsalimu. Kwa pamoja walitamka
“Habari yako dada!” Naye aliwaitikia kwa upole baada ya kugumia kwa sekunde chache.
“Salama! Habari za kutwa?” Caro alihoji.
Sauti yake ilikuwa ya mihemo kutokana na shehena ali-zobeba. Wote kwa pamoja walitoa maneno ya tahamia kwa juhudi alizoonesha.
“Nzuri sana! Pole na kazi ngumu za kutwa!”
“Asante!” Aliendelea na hatua zake kuelekea maskani alikoishi.
Wakati huo Sinde na Tora walibaki wakiendelea kuka-gua maembe mtini. Tora aliagizwa na baba yake am-baye hufanya biashara zake katika mji wa Nzega. Mama yake ambaye ni Mama Tora alimwagiza amtafutie kija-kazi toka kijijini. Alipokutanisha macho yake kwa mara ya kwanza na Carolina, Tora moja kwa moja aliingiwa na bashasha ya kutaka kujua zaidi kuhusu binti huyo. Alipomuomba Sinde amwelezee kuhusu wasifu wa Carolina, hakika alimsimulia yote mema;
“Sinde, binti huyo ni nani?” Tora alihoji.
“Anaitwa Carolina. Vipi unamfagilia nini? Maana watu wa mjini, hutembea lisani wazi..usha..”
“Si hivyo Sinde! Kuna jambo naliwaza hasa baada ya kumwona. Anaishi wapi?”
“Anaishi katika familia moja ya wafugaji. Palee kwa Mzee Malecha!” aliunyanyua mkono wake kumwonesha sehemu ile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama aliniagiza wakati nakuja huku. Alinitaka kumta-futia msichana wa kazi wa kusaidiana naye kazi za nyumbani. Vipi atafaa?” Tora alizidi kudadisi.
“Hana shida. Ana tabia nzuri sana. Kila mtu anamheshi-mu kijijini. Lakini kwa jinsi anavyoonekana kufanya kazi za nguvu, nahisi atakubali kwenda mjini. Vipi tum-julishe nini?” Sinde aliongeza.
“Bila shaka. Tafuta muda kulifanya hili. Inaonesha ata-faa katika familia yetu.”
Wakati huo Tora alielezwa kila jambo. Alivutiwa sana na wasifu aliokuwa nao Carolina achilia mbali uzuri aliokuwa anaonekana nao msichana huyo yatima. Alimwona kama lulu itakayokuwa ndani ya familia yao.
*****
Akiwa mwenye shauku, Tora alirejea mjini Nzega. Kitu cha kwanza alimjuza mamake juu ya Carolina.
“Mama!.Mama!” Tora alimwita mama yake.
“Abee mwanangu! Unasemaje? Mama Tora aliitika huku akielekea aliko Tora.
“Unasemaje? Umekuja na kipya? Mama Tora alihoji huku kamkazia macho Tora.
“Keti kwanza Mama. Mbona unaonekana mwenye hara-ka kama muuza mitumba?
“Nieleze ulichoniitia, nina kazi jikoni. Unamfahamu baba yako akirudi. Patakuwa hapatoshi. Anaogopa njaa kama nini!”
“Haya, nimetega sikio. Lete habari maana mwenda bure si mkaa bure bali huenda akaokota!” Mama Tora alisubiri kuambiwa.
“Nimepata binti!”
“Binti! Umepata mchumba! Ama una maana gani?”
“Mamaa! Mbona hivyo?
“Basi, binti gani huyo? Unatakiwa kuoa Tora! Umekua na sasa ni muda muafaka mwanangu!”
“Achana na hayo Mama! Wewe uliniagiza na videko vyako dada zangu!...Ni msichana wa kazi!”
“Ahaaa! Kumbe ndo hilo! Umenitia kiwewe nikajua umepata jiko unataka kuoa! Nikajua muda wa kujim-wayamwaya umefika. Haya, nipe habari. Binti huyo ni nani? Ni hawa wa mjini wanaoning’inia kama maembe dodo wakati wa kimbunga? Mama Tora alidodosa.
“Hapana Mama! Si wa mjini hapa. Ni binti mmoja hu-koo kijijini. Anafaa! Hasa kwa vile nimemwona na kusikia kauli yake. Yaelekea anaweza kuwa mwema na mwenye staha. Tora alimpamba Carolina.
“Ni vema. Mbona hujaja naye?”
“Nilitaka kukuuliza kwanza ili ukaonane na walezi wake. Mimi pekee nilihisi hawawezi kunielewa. Wan-gedhani pengine nataka kumtorosha. Uzee dawa! Kama vipi nikupeleke. Panga siku.”
“Haya! Umefanya vema kunijuza juu ya jambo hili. Mi niendelee na shughuli yangu jikoni. Wakati ukifika nita-kueleza.”
Ilimpasa mama Tora amhimize mwanaye kumpeleka kijijini. Siku iliwadia ya kwenda kumwona Carolina mbele ya walezi wake. Njiani Tora ndiye aliendesha gari yao aina ya Nisan patrol waliyoitumia mara zote kukusanya maembe. Ilipowadia majira ya saa tano asubuhi waliwasili kijijini hapo. Walishindwa waanzie wapi. Iliwalazimu Tora na Mama yake wafike kwa wazazi wa Sinde kufahamu ukweli zaidi. Sinde alikuwa ni mgonjwa siku hiyo, hakupata nafuu ya kumfanya azunguke zaidi ya kwenda hospitali. Sinde pia alirejea kuwaeleza kila kitu kuhusu Carolina na alimsifu kwa juhudi na asadi yake. Mama Tora alifurahi sana na kutaka kumtia machoni mwake.
Wakati uliendelea kuyoyoma na kuyeyuka kama mshu-maa uliowashwa kwenye upepo mkali. Ilipofika saa sita unusu, Tora na mama yake waliondoka kwa pamoja na gari yao hadi nyumbani kwa mzee Malecha. Haikuwa-chukua dakika kufika katika uchanjaa alipoishi Carolina. Walimwona binti mmoja mrembo amesimama chini ya mwembe. Kwa kumtazama, alikuwa amependeza zaidi ya ahali wa mtu. Tora alimnong’oneza mamake.
“Mama, unamwona huyo? Umwonaye mbele yako ndiye Carolina!”
Mama Tora alishtuka na kujisemea;
“Authubillahi! Huyu binti alifaa awe mwanangu wa kumzaa! Kwa jinsi alivyo na bashasha!”
Carolina aliwakaribisha na kuwalaki wote kwa pamoja. Aliwahudumia maji ya kunywa pia akawapatia maziwa ya mgando. Hali hiyo ilitosha kwa Mama Tora kumpatia Carolina asilimia mia ya uhodari wa kazi za kutunza mji. Hakuwa na ubishi. Kilichofuata aliamua kumpongeza Tora akisema;
“....Wewe ni fundi haswa hukosei kitu.
Leo nimekiri ustadi wako mwanangu!” Tora alicheka na aliendelea kuzungumza na Carolina. Walitaka kujua kule walikoelekea walezi wake. Naye pasipo ajizi aliwafahamisha kuwa walienda kumsabahi mgonjwa ambaye ni dada yake mzee Malecha ambaye aliolewa huko ng’ambo ya kijiji chao.
Jinsi alivyokuwa amependeza, gauni lake lenye mshono wa jongonene na msuko wake wa mkusi alionekana mwanaharusi aendaye kufunga ndoa. Tora alitokwa na udelele kwa jinsi alivyokuwa mkware na hakuna ambaye hakumfahamu katika mji wa Nzega. Alisadifu kuishi maisha ya nikaha hasa kuwa na wake wengi.
Mama Tora aliamua kuuvunja ukimya na kumweleza Carolina shida yake.
“Binti, bila shaka unaitwa Carolina!”
“Ndiyo Mama! Naitwa Carolina!”
“Unaifahamu sura hii?” Mama Nasoro alihoji akimwo-nyesha Tora.
“Ndiyo! Kaka huyu huwa namwona nyakati fulani akiwa na Sinde.”
“Sawa! Unionavyo hapa, huyu ni mwanangu. Na mguu huu ni wako.”
“Kwa vipi Mama? Carolina alihoji huku akichora chora chini.
“Bila shaka umeshahitimu Darasa la saba?”
“ Eee! Siku nyingi sana. Lakini sikuchaguliwa”
“Basi usijali. Kila jambo lina wakati wake. Mimi nakuhitaji nyumbani kwangu.”
“Unanihitaji! Kuna nini? Alionesha hofu fulani.
“Wala usiwe na wasiwasi.
Nataka tukaishi sote mjini.
Ukanisaidie kazi mwanangu.
Nitakulipa!” Carolina aliposikia hayo alitabasamu. Mwanya wake mdomoni ulionekana sawia na kisha ali-jibu baada ya kukaa kimya kwa muda.
“Mjini! …..
Sawa! ….Lakini Mama na Baba hawapo.
Wao ndio wenye mamlaka.
Waulizeni wao! Wakiafiki sina ubishi nitaenda!”
Ingawaje Carolina alionesha kukubali, alihofu tofauti ya mazingira ya mjini na kijiji ingekuwa kikwazo. Aliamua kuyamezea kwani alifahamu nchi ya Tanzania ni moja na watu wake ni wamoja. Utengano hata tofauti ya mazingira haitambulishi tofauti zao. Alijua, hapana shida angeweza kuyakabili maisha ya mjini.
Wakati huo hawakutegemea punde kuwaona mzee Ma-lecha na mkewe. Ililazimu warudi kungojea wasaa mwingine. Walirejea nyumbani kwa kina Sinde waliko-kuwa wamefikia. Majira ya saa kumi na moja unusu wa-lifunga safari ya pili kwenda kupatiwa jawabu. Mzee Malecha hakuwa na pingamizi. Alichosema, hofu yake ni umri na jinsia ya Carolina kuwa ni hatari kwa maisha ya mjini. Alisema, mjini kuna kila aina ya fataki pamoja na wanaume afriti wanaoweza kumharibia Carolina maisha yake. Aliwakubalia lakini aliwataka warejee baada ya juma moja kumchukua Carolina. Alisema;
“Ndugu zangu, uungwana ni kitendo. Ombi lenu nime-liafiki kama anayehusika kaafiki pia. Ninachowataka kufanya ni kumlinda, kumtunza na kumlea kama mtoto wa familia yenu. Msimtenge. Maisha ya mjini ni kizun-gumkuti. Mjitahidi kumlinda na awe salama kama mli-vyomkuta hapa.” Mzee Malecha aliwaasa.
Hakika siku yenye furaha ilikuwa kwa mama Tora. Wa-liaga na kuomba Carolina awasindikize. Mama Tora alitoa alfeni mkobani kwake na kumpatia Carolina.
“Shika vijisenti vitakufaa kwa chochote.” Alimpatia Carolina.
Alitabasamu hadi gego lake la mwisho kuonekana na kushukuru huku akiikunja kunja pesa aliyopewa
“Asante Mama!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mungu akubariki!...asante!” Hatimaye Tora na Mama yake walirejea mjini.
Wakati huo Carolina alihisi ndoto zake zimetimia. Ali-waza na kuwazua jinsi ya maisha mapya. Alihisi kuvuta pumzi mpya katika maisha ya nyumba yenye umeme. Aliwaza hata kuangalia video itakuwa sehemu ya maisha yake. Aliupiga moyo konde na kujiita mwenye bahati.
“Mungu wangu.
Nakushukuru kwa mapaji yako!
Nilinde hadi kifo changu.
Leo ni siku ya furaha kubwa kwangu.
Maisha gani nitaishi mjini kama ulaya! Umeme! Kideo! Hata kulalia godoro itakuwa sehemu ya maisha yangu!
La! Kweli dhiki ikizidi faraja inakaribia.
Carolina mie, nimpe nini Mungu kwa hili!
Asante Mungu!” Carolina alionekana mwenye furaha. Hakuamini kilichotokea. Wakati huu aliziangalia nguo zake zilizomo kwenye mfuko wa rambo. Alitafakari sa-fari itakuwaje hata begi hakuwanalo.
Maisha yaliendelea kwa wote kama kawaida huku akin-gojea. Ilipowadia siku ya agano lao Tora ndiye alimfuata Carolina. Alivyokuwa muungwana binti huyu aliwaaga rafiki zake na waimbaji ngoma wenziwe wote. Aliwataka wamwombee aendako naye pia aliahidi atawaombea. Alipata wosia wa kila hali toka kwa walezi wake kabla ya kuwaaga. Mzee Malecha alisema;
“Tora kijana wangu.
Nakukabidhi binti huyu mdogo mikononi mwako. Naomba mfikishe salama salimini kwa mama yako. Ka-ma kawaida ya mlezi ama mzazi yeyote,
naomba mkaishi kama ndugu.
Mpendane na mheshimiane.
Naomba pia uwe mstari wa mbele kumtetea.
Jaribu kumwepusha na mabaya yote.
Huyu ni dada yako.
Pia wewe Carolina, huyu ni kaka yako.
Mnanisikia?” Mzee Malecha alisisitiza
“Ndiyo Baba!” Tora aliitikia kwa haraka.
“Sawa Baba! Nimesikia na nimeelewa.
Nitatenda yote mema kama nilivyoishi nanyi.
Nitawakumbuka sana.
Hakuna jinsi nitafanya zaidi ya kuwaombea.
Nanyi pia naomba mniombee.
Nawapenda.” Caro alitokwa na machozi. Aliwaza yote tangu ohola na ohoriba katika maisha yake. Baada ya hapo waliianza safari akiwa na picha kichwani mwake kuwa angefikia nyumba ipi na pia aliwaza angelala wapi. Hakuwahi kuishi mjini zaidi ya siku tatu. Hata wakati ule wa mashindano ya umtashumta, mara nyingi alilala vijiji vya jirani na aliwahishwa na ganagana mapema asubuhi.
Tora alikuwa ayari mkubwa. Alimsimulia njiani Caroli-na hadithi nyingi. Alijitahidi sana kujisifu ilimradi aonekane si lofa machoni mwa Carolina. Alifungulia mziki wa kila aina ilimradi kumfurahisha mrembo huyu. Alifahamu kajipatia windo la kupoza njaa yake. Alijisifu kuwa yeye ni mtu wa Mungu kwa minajili ya kumbemba na kumteka Carolina. Ingawaje Carolina alitoka familia uchochole, hakuingiwa na neno lolote wala hakupata hisia yoyote ya kudanganywa na Tora.
“Carolina, wewe ni mrembo sana!
Sijui kwa nini ulikuwa na maisha magumu hivi?” Tora alichombeza huku akiendesha gari.
“Asante! Namshukuru Mungu kwa kila jambo.
Yote ni makusudi yake. Kila kitu kina mwanzo na mwi-sho wake” Caro alijibu kwa upole huku akitabasamu.
“Eee!..... Unajua mimi nafanya kazi gani? Tora alihoji.
“Hapana. Sijui. Kwani unafanya kazi gani?”
“Hujui! La!...kweli uko nyuma sana.
Nina kaka yangu yuko mbele!
Yeye ni meneja wa shirika la ndege huko.
Kanifungulia duka la vifaa vya michezo na vifaa vya maofisini. Wilaya nzima nasambaza vifaa hivyo.” Wakati huo Tora alijisifu na kumdanganya Carolina.
“Hivyo vyote ni vyako ama vya kaka yako?” Caro aliho-ji
“Ah! unauliza swali ama hasa ndilo jibu!
Vya kwangu!”
“Mshukuru Mungu kwani yeye ndiye mpaji.
Tumia mali zako vizuri na Mungu atakubariki.”
“Hivi Caro, umeshawahi kufika mjini Nzega?”
“Ndiyo! Nimeshafika marachache sana.
Yapata mara tatu ama nne hivi.
Nilifika wakati wa michezo ya umtashumta nilipokuwa mwanafunzi.” Caro alijieleza huku akiangaza macho yake kutazama kingoni mwa barabara na kuona majum-ba yaliyomvutia.
“Mimi sijapata mke bado.
Natarajia punde nitampata, wewe je?
Unamchumba ama una mpango gani?” Tora alihoji.
“Kwani ni lazima kuwa na mke ama mume?
Yote ni mipango ya Mungu.
Kwanza mimi bado ni msichana mdogo sana.
Siwezi hata kuwaza hayo leo.
Nawaza kusoma tu! Na si vingine.”
“Unatamani kusoma!
Sawa, inaonekana una hamu sana na shule.
Basi usijali, ongea na watu uvae viatu Caro.
Mi nitakusaidia usome.
Pesa ninayo na kila kitu nitakusaidia.
Nawe utatakiwa uwe muungwana kulipa fadhila.”
“Usijali kaka Tora.
Mimi nitafurahi sana kama nitasoma.
Mungu atawabariki na kuwalipa nyote!” ghafla alijiwa na swali kichwani... “hii gari ni ya nani?”
“ Ni ya kwangu!
Kwani vipi?’ Tora alijisifu.
“Mbona imeandikwa Tora Miembe? “
“Hilo ni jina tu.
Nilimpatia mzee wangu gari hii aitumie kama zawadi ya kunizaa. Kuna ubaya?”
“Hapana ni vema tu!” Caro aling’amua uongo na majisifu ya Tora. Alimhoji tena swali lingine.
“Umenidokeza kuwa, kaka yako yuko mbele, mbele wa-pi? Tunakoenda!
‘Ha! Hata mbele hupajui! Yuko Ulaya, Mamtoni.
“Mh! Sawa nimekuelewa. Na hii biashara ya maembe ya nani? Kwani kaka yako hampendi mzee wake hadi asimsaidie biashara za maana?”
“Achana na hayo.
Tutaongea baadae tukipata muda.
Acha niangalie kwanza barabarani nahisi askari wana-weza kutukamata. Tunaingia mjini sasa, unaona hapa ni mnadani. Unapafahamu?”
“Ndiyo! Napafahamu ingawaje si saaana!”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment