Simulizi : Jaha
Sehemu Ya Pili (2)
Tutaongea baadae tukipata muda.
Acha niangalie kwanza barabarani nahisi askari wana-weza kutukamata. Tunaingia mjini sasa, unaona hapa ni mnadani. Unapafahamu?”
“Ndiyo! Napafahamu ingawaje si saaana!”
Waliwasili mjini Nzega majira ya jioni. Kuonesha anajiramba kwa Carolina, Tora alimpitisha Makubaliano Bar ili kumchomea mishikaki na chipsi pamoja na kumnunulia soda ya kopo. Hapo Carolina alianza kuingia kwenye mitego ya ibilisi hata kabla siku haijaisha. Alipomaliza kutumia alichokuwa amekarimiwa na Tora, hatimaye alichukuliwa na kupelekwa nyumbani alikotakiwa kuishi kama kijakazi. Mama Tora aliandaa hafla ya kumkaribisha Carolina. Alifurahia ujio wake hadi alimyongoa. Alimpikia vunana la mchele ambalo Carolina hakuwahi kulitia mdomoni mwake. Alikula na alitosheka. Alipokuwa akiwatazama wanawake ndani ya nyumba hiyo, hakika walikuwa wakipendeza kwa mavazi yao marefu yenye staha.
Kabla hajalala, Mama Tora aliitisha baraza la utambuli-sho kumtabulisha Carolina.
“Ndugu wanafamilia, huyu ni Carolina.
Ndiye msaidizi wetu humu ndani.
Huyu ndiye maisha na hewa ya kila mmoja wetu.
Naomba mpendeni sana zaidi ya chochote.
Yeye ni kila kitu.
Ni mtoto wangu pia wala si kijakazi tena.”
“Haya mama karibu sana jisikie nyumbani” Mzee Miembe aliongea.
Mama Tora alimuasa Carolina kuwa, wajibu wake wa kwanza ni kutogubua lolote nje ya familia. Alimhalalisha kuwa yeye ni mmoja wa familia hasa ni mtoto kati ya watoto wake. Aliwataka wote katika familia yake, kumheshimu sana Carolina na kumchukulia mtoto wa nyumbani. Alimweleza kuhusu ulimbukeni wa mjini hasa habedari yake ilikuwa juu ya wanaume guberi wa miili ya wasichana. Carolina hakufahamu kitu kwani alikuwa usungo maishani mwake.
“Carolina, wewe ni ua changa kondeni. Kila mdudu ana-vutwa na harufu nzuri ya ubichi wako. Anatamani kujit-walia na kulinusa kama si kulimiliki. Anagalia sana, usiwe ua la konde ama saa ya jiji.
Kila mmoja huitamani na kuitumia lakini punde tu ama-lizapo haja yake hutoweka na kutofahamu umuhimu wake. Isitoshe ua la konde halina mtunzaji, japo litamvuta mwanadamu basi hulichuma na kulinusa kwa mkono wake wa kuume. Limchoshapo kulibeba na hulitupa kwa mkono wake wa kushoto. Hapa jua huliangaza na kulikausha kabisa. Likaukapo binadamu huyo huyo, hulitwaa kwa fagio na kuliviringa kwenye vumbi mchanganyiko na kila uchafu. Kamwe hakumbuki kama lilimpendeza. Hapo hulitia katika jalala na kulitia kiberiti pasipo huruma. Mwisho wake ni majivu hujipatia kusafishia choo. Hapo ndiyo mwisho wake.”
“Mama mbona sikuelewi? Unamaana gani?”
“Wewe bado binti mbichi usiyejua kitu.
Hapa mjini kuna kila aina ya afriti.
Nina maana jitunze kama ua la uani.
Ua la uani hutiwa maji na mbolea kisha hustawi.
Ukijirahisi hapa mjini, kila mwanaume atakufanya kito-weo wakati wa njaa yake. Si asubuhi, mchana, jioni hata usiku watakuhitaji. Jitahidi kuishi maisha ya imani. Waepuke wanaume hadi upate mmoja utakayemwita mmeo.
Umenielewa?”
“Ndiyo mama, nimekuelewa.
Asante sana kwa maneno yako mazuri.
Nitajitahidi kuishi kwa nikaha”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipoyaanza maisha mapya, Carolina alipatiwa chumba cha kulala. Kilikuwa ni chumba cha uani chenye nakshi na mvuto kwake. Alipatiwa karibu kila kitu cha msingi ikiwemo redio. Miongoni mwa majukumu aliyopewa yalikuwa ni kupika chakula cha familia na kuiweka nyumba katika hali ya usafi wakati wote. Hawakupan-giana mshahara kwani tajiri yake alimtaka aone kwanza tija ya kazi zake ndipo wazungumze kuhusu malipo.
Hatimaye juma moja lilimalizika. Carolina ilimbidi naye kuishi kwenye mfumo na sheria za wenyeji wake zilivyo muhitaji kuishi. Hakuwa na pingamizi, alijua hiyo ni njia mahsusi ya kusitiri utu wake. Binti Carolina hakuwa msununu mpenda shari bali alikuwa ni chemichemi ya furaha kwa yeyote mwenye huzuni. Alikuwa ni msaada katika nyumba ya Mzee Miembe. Kila mgeni aliyeitembelea familia hiyo enzi za Carolina, alijisikia faraja na mwenye furaha isiyo kifani.
Ilimlazimu mama Tora kumwandika kazi Carolina kwa mshahara wa shilingi elfu kumi. Hakikuwa kiasi cha kutosha kulinganisha na kazi alizofanya wakati huo. Familia nzima ilibadilika na kuwa yenye furaha. Carolina aliruhusiwa maramojamoja kwenda matembezini akiushangaa mji na ndipo wengi waliyaona maungo yake ya thamani. Aliumbika sawia, kila mwanaume rijali aliyemtupia macho alimtamani awe ahali wake. Maisha yaliendelea sawia pasipo kikwazo chochote. Alihisi maisha yamemnyokea na kujiita mwenye bahati.
Ramsa ya Carolina ilionekana itadumu ndani ya familia ya Mzee Miembe. Stahifu alizotegemea kama mtoto wa familia hiyo aliiweka mikononi mwa Mungu. Je kitu gani kinamnyemelea Carolina wakati huu wa Furaha? Ataongezewa mshahara ama ataambulia matusi na ma-simango? Mengi ni bashiri! Endelea kusoma wasifu wa mrembo wetu.
Adhuhuri
SAFARI YA CAROLINA katika maisha ilikuwa si rahisi ndani ya familia ya kigeni. Ilikuwa juu ya barabara yenye mashimo, milima pamoja na mizunguko ambayo ilionekana kwa fikra ilivyomkabili. Hakufika katika ki-lele cha ustawi na mafanikio pasipo kukumbana na kik-wamo.
Wakati hajafikia hata nusu ya safari yake akisaka maisha bora ya ndoto zake, alipambana na vizingiti vingi visivyohesabika. Alilazimika kupigania roho yake kwa uchungu wa moyo na mwili kwa kufanya bidii mfululizo.
Ama kweli maisha yamejaa pingamizi mbalimbali. Carolina alipigana kiume kutaka kujinasua ili kufaulu alivyotegemea. Hii ilimfanya ajitahidi kila hali kuyazuia maswahibu kumvaa. Harufu aliyoivuta ya umasikini na uchungu wa kifo cha mama yake na hata kutomfahamu baba yake, alitia juhudi kujitegemeza.
Punde Carolina alianza kuandika historia tofauti baada ya nusu mwaka wa maisha yake mjini tangu azaliwe na kuliona jua mara ya kwanza. Ingawaje alionesha uwezo mkubwa sana na bidii kuliko ilivyotazamiwa, hakuche-lea kuonja shubiri.
Ungemtazama wakati huo, Carolina alikuwa sawia ame-nenepa na alistahili kuitwa tipwatipwa. Wakati hajafikia utu uzima ni shayiri kuwa alikuwa amebobea katika kazi za ndani. Wakati wote alipokatiza kuelekea sokoni hata upepo uliompunga pamoja na miali ya jua la asubuhi vilimpigia saluti. Hakuweza kusimamishwa mlingoti na kiboya wa kiume alivyokuwa imara. Njia yake ilikuwa nyoofu kama miale ya jua. Alipafahamu fika alipoelekea kutwaa mahitaji yake. Wakati wote alipokuwa njiani na mitaani toka ama kuelekea sokoni wakware walimchombeza kwa maneno ya kumzoea. “Habari malikia?” Hakujibu kingine zaidi ya salamu. “Malikia si sifa yangu” na mara zote alitoa majibu ya mkato ili kuwakatisha wasimzoee. Aliamini mwanzo wa salamu ni mazoea.
Ama kweli, kikulacho ki nguoni mwako. Hakufahamu wala dunia haikuota kamwe kama ndani ya familia aliyoishi kuna afriti waliomendea kuugusa mwili wake. Alifahamu kuwa anastaha ya familia. Tora na abu yake walimmezea mate wakati wote alipokatiza mbele zao. Iliwapa mtihani mioyo yao ya karatasi pale alipokatiza kuwatengea chakula. Macho yao yaliwatoka mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango. Mwili na maumbile yake vilionekana barabara hata kama alijisitiri ndani ya vazi lililofunika hadi unyayoni kwake.
Dada huyu hakuwa mmoja wa baradhuli wengi wali-owahi kuishi katika uso wa dunia hii. Carolina hakuwa na tabia ya utalakeshi kama asili aliyozaliwa nayo. Ha-kuwahi kujianika kama unga juu ya jabali ama kama chaza mwambani. Zaidi alijisitiri kuficha maumbile yake. Na kama watu wote waliokuwa na akili njema, hakupenda ustawi wake utokane na mapendeleo yoyote. Alitaka utokane na ustahili wa jasho lake mwenyewe.
Alijizolea umaarufu katika mji wa Nzega. Si kwa tabia chafu wakati huu, lakini, kwa tabia yake ya kujilinda na kujiheshimu. Alijulikana na kila mtu na alivuma kama mchaguliwa uraisi wa Marekani. Upepo na mwanga, vyote vilimsitiri na kumfanya mwenye heri. Watu wa kila rika, wanaume na wanawake, wafanyabiashara, ma-dreva, wachuuzi na hata watumishi wa serikali wa mji huu walishikwa na hamu ya kuzipenda tabia zake. Asilani hapakuwa na mtu aliyetabiri kuwa Carolina siku moja angeoza na kuwa mwiba ulioelekezwa katika mboni za wakware.
Iwe suheli wala kaskazini, magharibi hata mashariki sehemu waliyoishi alikuwa mwaminifu. Hakufaulu kuanzisha usuhuba na yeyote jinsia ya kiume zaidi ya salamu. Kwa watu wa jinsia yake wote walikuwa mwan-ga na hewa aivutayo kwa maisha yake na kumfanya aishi nao vizuri kama ndugu.
Ilifika siku yenye kuukabili utelezi katika safari yake. Kwa kuwa alivaa madaluga yenye meno, matumaini ya kushinda aliyahisi. Hakupata kuisahau siku ambayo ali-patwa na tashwishi iliyokuu hasa kutokana na ubedui alioanza kupambana nao ndani ya mji alioishi. Hakuto-kea mwanaume tofauti toka nje ya nyumba alimoishi Carolina na kuzitibua furaha zake. Matumaini na imani yake vilianza kufifia kama kibatari kilichoishiwa mafuta. Tora ndiye aliifurusha furaha ya Carolina katika mji wake. Achilia mbali kushindwa kwa Carolina, Tora alikuwa ukuba na thakili mkubwa machoni pia rohoni mwa Carolina. Aliposhindwa juhudi zake kumnyenga, aliishia kunawa.
Katu Tora hakukubaliwa kwa hiari. Ilikuwa kazi ngumu kwa Carolina pia aibu ilimjaa machoni mwake. Kwa kuwa alikuwa hajamjua mwanaume zaidi ya kupigana vikumbo wakati alipokatiza palipo halaiki, alikuwa mwenye hofu. Kwa ushupavu na uchu wake, Tora haku-kubali kushindwa. Alianza kumchukia Carolina na kum-tishia maisha yake. Pengine alihisi ana bwana ambaye alimpa jeuri. Hata hilo halikuwa jawabu sahihi zaidi ya ono lenye mzizi wa wivu uliomea rohoni mwa Tora.
Binti huyu mwenye mwanya, alikuwa bado ni mbichi. Alikuwa bado malikia asiyenyang’anywa furaha yake. Hakuwahi kuingiwa na pepo wabaya katika maisha yake. Aliwaza kila wakati kuwa angependa kuishi pekee na kama angelishindwa angeliolewa na mwenye huba wa kumpenda awe ahali yake ndiyo angeruhusu kuwa mfalme katika maisha yake. Mawazo ya Carolina yali-kuwa ni ndoto na simulizi za ‘nge’ na ‘nga’ wakati ya-meshajiri.
*****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ukiacha sabihi yake katika maisha, Carolina alikuwa na subira. Ilikuwa jioni moja ambapo kulifanyika harusi ya mpwake mzee Tora. Hafla hiyo ilifanywa katika kijimji cha Tinde ambako familia nzima ilipaswa kushiriki. Kwa kuwa ratiba na siku ya harusi ilifahamika kwa Tora, alijiandaa kwa hila zake. Alijadili kichwani mwake na kujidai mgonjwa taabani siku mbili kabla ya harusi. Alijipeleka hospitali na alimhonga daktari ampatie cheti cha kupumzika kwa siku tatu. Yote hiyo ilikuwa hila ya kutka kutimia haja zake.
Janja ya Tora ilikuwa ngumu kuinusa na kuing’amua. Siku ya harusi ilipofika wote nyumbani isipokuwa Tora na Carolina walielekea Tinde. Huwezi kuamini furaha aliyoihisi ikijaa rohoni mwake kijana huyu. Alipobaki yeye Tora na Carolina ndani ya nyumba, aliona ni bahati kubwa. Hakuonesha tena kama ni mwenye homa. Alifahamu atatumia kila hila kumnasa Carolina na kutimiza haja zake hata hakuhofu lolote la kumuumbua.
Alivyokuwa na huruma, Carolina alimtayarishia mgonj-wa staflahi kwa ajili ya kuianza siku kama stahifu yake. Alipotenga kikombe kimoja cha chai mezani, Tora alimtaka alete na cha pili ili wote wapate kushiriki chai. Alisikika akisema;
“Caro! Naomba uongeza kikombe kingine tupate chai pamoja” ilikuwa agizo la Tora. Aliogopa Caro, na isi-toshe hakuwahi kula meza moja na mwanamume. Kweli Carolina alikuwa mwenye sinya kuhusu tabia hiyo. Kwa kuwa alilazimishwa ilimpasa aheshimu amri hiyo.
“Sawa kaka Tora. Lakini naomba kuta unaendelea!” ali-jibu binti huyo kwa upole.
Kwa raghba yake Carolina, sura ilijaa machoni mwa Tora na ghafla Tora aliingiwa na pagaa. Hali hiyo ilim-fanya roho yake imtoke na mapigo yake ya moyo yam-wende mbio kama mbwa aliyekoswa na fisi.
Wakati huu hakuwa na saburi. Alikata shauri kuwa lolote na liwe. Alivyokuwa, alijiandaa kwani hila na jeuri. Alipanga kumfedhehesha Carolina. Hali hiyo ilikuwa ya ufidhuli zaidi ya sakarani ama fisadi mla cha watu alijikuta akiongea;
“Caro! Naomba uketi hapa karibu.
Ninajambo nataka tuzungumze.
Si unakumbuka siku ile?
Hatukumaliza mazungumzo yetu.” Tora aliongea kwa unyenyekevu huku akiyabinya macho yake.
“Sawa, lakini acha nikae hapahapa nilipo.
Nina imani utanisikia nami nitakusikia!” Caro alijibu kwa hadhari.
Wakati huo Tora alinyanyuka kitini alipokuwa kaketi na alieleka kuliko lango kuu la kuingilia. Alilifunga kisha alirejea ndani. Wasaa huo aliwaza nje ya ubinadamu. Akili yake ilitawaliwa na uchu wa kujua Carolina ni na-ni. Haraka aliingia na kumkodolea macho huku akitam-ka;
“Caro, nakupenda sana!
Hujui nini nakuwazia.
Ungejua fika ungenisikiliza ninachokueleza!
Nakupenda sana mrembo!”
“Kuna nini kaka Tora?
Mbona hivyo?
Halafu.......!”
“Caro sikiliza. Mimi siumwi wala sihisi maumivu. Zaidi nimefanya hivi ili angalau nipate muda wa kuwa na wewe laazizi wangu, mke wangu mtarajiwa.” Anatamka huku akimsogelea Caro.
“Mwendawazimu nini?”
“Kila umwonaye wamtamani, ukoje wewe?”
“Mbona maneno yako na wewe ulivyo….ah! Caro aliyauma maneno huku hasira zikiwa zimemjaa. Alijari-bu kunyanyuka ili kumuepa. Tora naye alimsogelea. Alimkamata kwa nguvu na kumrusha kwenye sofa.
“Niache Tora!
Mwanaharamu wewe.
Unataka nini kwangu?” Pumzi alizikokota.
“Tulia Caro!
Mimi nakupenda.
Nipatie pato langu.
Ujira wa kukupatia kazi hapa.
Ungepata kazi bila mimi wewe? Tora alisisitiza.
“Achana na mimi nasemaaa!
We—we!” Carolina alijaribu kujinasua.
Akiwa amebanwa ukutani kaegemea kochi, aliangaza macho yake na kuona mezani kuna birika la chai aliyo-kuwa ametenga. Ghafla alibadilisha kauli kumhadaa Tora:
“Ngoja nikwambie Tora.
Unajua nini?”
‘Unanipenda?” Tora alihoji kwa shauku.
“Ndiyo, nakushangaa sana.
Niachie basi kidogo ni…..”
“Fanya haraka basi, kwani unatakaje?”
“Nataka utulie.
Kwani wewe jimbi?
Huwezi kubeba mishale kuwinda njiwa wako.
Tulia wala usijali shida yako naijua.
Najua unahitaji nini kwangu….”
Carolina aliutuma mguu wake wa kuume kulibana birika la chai moto kwa kutumia dole gumba lake. Miguu pamoja na birika alivivuta hadi mgongoni kwa Tora na kulitua ambapo chai yote ilimwagikia na kumuunguza sawia mgongoni.
“Caro!
Unaniunguza!
Nitakuua leo!
..kwa nini unilipe moto!
Una jeuri eee!” Tora alilalama huku akimwachia Caro-lina aende zake. Tora aliungua na kujisikia mwenye maumivu makali.
Wakati yakijiri hayo, Carolina alitoa siahi zilizosikiwa na baadhi ya majirani, lakini hawakujali. Alikimbilia chumbani kwake kujinusuru. Aliingia kisha aliufunga mlango kwa komeo na kujitupa kitandani akihema juu juu.
Aibu ilimhama Tora na bado hakukoma. Kwa nyuma Tora alichukua sime na kumfuata. Ingawa hisia zilim-hama wakati huu alitaka kulipa kisasi kwa nini Caro alimuunguza kwa chai.
“Caro! Fungua mlango!”Alimtaka Caro amfungulie mlango. Aliyapepesa macho yake pande zote. Hakuona mtu akiwa karibu na kumwona. Alikuwa na uchu wa kumtia Caro himayani. Alichukua uamuzi wa kuvunja mlango, aliukanyaga mlango na makomeo yote yal-ing’oka na moja kwa moja macho yake yalikutana na umbile mwanasesere la Carolina. Alikuwa akitaka kuba-dili nguo zake, akizitoa zile zilizokuwa limelowana chai.
“Nikubali. Nitakuoa Carolina.” Alimtaka amkubali. Ali-poonekana haeleweki kakazana kujisiiri kwa ngu zake, Tora alitoa sime na kumgusisha shingoni. Walibaki wa-metazamana kama Jimbi waliopigana na kuchoshana vibaya. Carolina alikuwa na hasira sana wakati huo. Tora yeye alikuwa na uchu hasa alipomtazama Carolina akiwa mwanasesere mtupu.
Roho ya utu ilimtoroka Tora na kubaki kivuli. Tora alii-weka roho yake ya utu rehani na kubaki kama jinamizi. Alimfanyia kitendo cha haya na cha kinyama ambacho hufanywa na binadamu firauni wasio utu. Ni wale tu wenye roho za paka shume.
Sifa ya Carolina tayari ilikuwa imeanza kuandikwa vin-gine pasipo matkwa yake. Baada ya hapo Tora aliufunga mlango na kwenda zake. Baada ya unyama alioufanya akili ilimjia na alijiona punguani. Aliwaza sana jinsi angeweza kuikabili tuhuma hiyo.
‘Alah! Hatimaye….” Alijiwazia.
Alikata shauri kuwa lolote na liwe. Alihisi Carolina ali-kufa. Ilimchukua zaidi ya saa tatu kuzinduka na kurejea katika hali ya dunia. Aliporejewa na fahamu yake alihisi hakuwa yeye aliyejifahamu. Alilia na kuilani nafsi ya Tora. Alifahamu kuwa tayari alifanyiwa unyama mkub-wa. Wakati akilia alijenga taswira ya kile kilimtokea mama yake na kufanya azaliwe yeye. Alijihisi maumivu makali sana yakiuteka mwili wake. Aliwaza na kuwazua akiwa na mawazo mengi. Aliwaza kuwataarifu majirani lakini alihisi aibu kubwa kuwa angeanzaje.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijikaza na kuchukua taulo pamoja na kitenge ili anga-lau apate maji ya kuoga. Aliitekeleza azma yake kwa shida. Hakuwa na hali, matumaini yake yaliingia dosari. Alipotaka kujisemea peke yake, alishikwa na tambaza na kumfanya alie sana kwa uchungu. Wakati mambo yakimwendea upogo, Carolina aliwaza hata kujiua. Alihisi aibu ya kuishi duniani hapa. Aliupiga moyo konde alipofahamu ni kosa kubwa kujiua. Yote ya baadaye aliyakabidhi kwa jalali.
Aibu ziligubika sura na akili ya Tora. Ilimlazimu kwen-da Kachoma kujipatia mzinga wa Chag’aa. Alifanya hivyo ili apoteze aibu usoni kwake. Haikuwa mazoea yake, watu wengi walistaajabu kumwona huko. Alilewa na kurejea kulala chumbani kwake na alilala usingizi fofofo.
Ilitimia saa kumi jioni Carolina akiwa bado taabani ki-tandani. Aliwaza jinsi ya kufanya. Hili hata lile aliliwaza na hakupata jawabu lililo sahihi. Aliwaza sana hasa alihofu kama hakuambukizwa juliana hata gojwa lolote lenye kuambukiza. Pengine aliwaza kama atapata mimba atakuwa mgeni wa nani. Wazo lake wasaa huo aliwaza kuwa ataishi vipi.
Wakati huo alijenga kiburi na aliamua kutofanya cho-chote. Alikata shauri kumweleza mama Tora ili alitatue tatizo lililomkabili. Lo! Ilikuwa ni vigumu kwake kum-weleza moja kwa moja Mama Tora. Alijiuliza ataanzaje kuelezea tukio hilo. Wakati mwingine, alihofu kutosiki-lizwa kwa kuwa ni kijakazi. Alivyofahamu umbuji wa Tora hakika angeweza asimshinde kutoa ushahidi inga-waje kweli aliutenda unyama huo. Kitu kigumu alichoo-gopa ni kama angetakiwa kwenda kupimwa ili kupata ushuhuda. Ilikuwa ni nvigumu kwake na alikata shauri, lolote na liwe.
Ilipowadia saa kumi na mbili na nusu za jioni, alifahamu kuwa alipaswa kutayarisha chakula cha jioni. Alijua pia kuwa, mzee Miembe na familia yake walikuwa njiani kutokea Tinde kwa kuwa ndoa waliyohudhuria ilichukua muda mfupi. Aliona jambo la busara aandike barua kumjulisha mama Tora yaliyomsibu.
Katika barua yake Carolina, aliandika maneno yasiyo-weza kusahaulika kichwani mwa Mama Tora na yalim-fanya kushindwa ustahimili. Carolina aliandika:
Carolina Mnyonge.
Mpendwa Mama Tora!
Fahari ya Bwana iwe nawe. Mola aliyeadimu akujalie daima dumu. El Amiri ndiye stahili ya wote.
Katika jumla ya maisha yangu yote, sijamfahamu mwa-naume. Nimejitahidi kulinda stahifu yangu na familia yako ili nipate sona. Kwa barua hii Mama, sitakuwa na stara kwani mficha maradhi mauti humuumbua. Hakika mimi siwezi kukumbatia ng’e mikononi mwangu. Nafa-hamu ataning’ata na nitamtupa apotee wakati amenid-huru.
Ujumbe wangu kwako na barua hii ni kuwa, mwanao Tora kanifanyia ubedui usiopimika. AMENIBAKA pasi-po tahayari. Pengine kuwa yatima ndiyo maana hani-tambui asili yake.
Nahisi maumivu makali sana kwa sasa, hata siwezi ku-tabawali. Nahisi zilizala kunipeleka kaburini. Kifo changu kipo njiani kunitwaa. Sikufahamu kama nitakumbwa na mikasa yote hii nilivyoiheshimu familia hii.
Sabihi nitamtumaini Manani. Kama mwenye shufaa mwano, nimemsamehe hajui alitendalo na kama anajua atajutia nafsi yake.
Nilifahamu TORA ni mtu wa imani, kumbe ni afriti asiyemfano. Usishangae wala kustaajabu japo itatokea ahamani hapa wakati wowote. Janati inaniita kumfuata Mama yangu.
Tamati siwezi kuendelea. Machozi yananilenga. Rabi akupe maisha, wewe pamoja na wako ghulama. Mauko yangu jalali atanisitiri. Sitaendelea kuishi kwa amani.
Caro-yatima!
Barua hiyo aliifunga kwenye bahasha na kuandika juu yake. MAMANGU, MA TORA- NZEGA. Aliiweka barua katika meza kilipo kiti ambacho alipenda sana kuketi Mama huyo. Alifahamu angeikuta na kuiona hata kabla ya kumwona alipo yeye.
Ilipowadia saa moja jioni, Tora alikuwa bado kalala fo-fofo. Mzee Miembe na mkewe walirejea nyumbani. Mama Tora alikuwa na mazoea ya kumwita Carolina ma-mdogo mara tu arejeapo kutoka sehemu yoyote. Na siku hiyo alisikika akiita;
“Ma mdogo!
Caro ma mdogo!” Hakusikia akiitika wakati huo.
Aliita na hakupata jawabu. Ilivyo ada aliketi kwenye kiti na aliiona barua hiyo.
“He! Nani tena kanikumbuka?” Akili yake ilimtuma yaweza kuwa mtoto wake aliyekuwa anasoma shule ya upili Uchama. Alistaajabu alipoisoma barua hiyo na kubaki mdomo wazi kaduwaa.
“Yarabi Toba!
Maafa haya!
Kulikoni tena mikosi hii? Alikosa jawabu na ilibidi any-anyuke kuelekea chumbani kwa Carolina.
“Carolina!....ma mdogo!. Alinyanyua shingo yake ku-chungulia chumbani. Kwa mbali alimuona kajilaza ki-tandani na shuka kajifunika gubi. Alihisi amebwia sumu na kujimaliza.
Kwa aibu ilivyoikumba familia, Mama Tora alimwomba na kumpigia magoti Carolina.
“Carolina mwanangu!
Nakuomba mamangu usinivue nguo!
Haya kweli yametokea ama la?
Kweli ama unamsingizia mwanangu?
Caro! Naongea nawewe!” alionekana kung’aka. Wakati huo Caro alimtazama bila hata kuongea jambo.
“Naomba nieleze kama kweli amekufanyia hivyo.
Msamehe mwanangu na mtunzie siri!
Aibu mwanangu!” alimsihi.
“Naomba usiudhuru mwili wako kwa hili lililotokea.
Amini Mungu atakusaidia uwe salama. Tafadhali, fanya jambo hili siri kubwa jirani asifahamu.”
Mama Tora alikuwa na lengo la kuuficha uozo.
“Caro mama! nitakupeleka hospitali.
Nitakulipa fidia ili mradi tu usiseme kwa mtu.
Hata wanangu wa kike na baba yao wasifahamu.” Ali-pokuwa akiongea yote hayo, Caro alikuwa akimtazama, machozi yakimbubujika na macho kumuiva sawia. Ha-kujibu lolote zaidi ya kilio chenye huzuni.
Mama Tora alitoka chumbani na kuelekea kule hujisitiri Tora mtoto wake. Alitaka kuujua ukweli. Alimkuta kaji-laza;
“Tora mwanangu.
Kulikoni kunivua nguo mchana mchana!
Umekumbwa na nini leo? Tora alimkodolea macho pasipo kujibu kitu.
“Tora, naongea na wewe, kulikoni?
Umemfanyia nini mtoto wa watu?
Utaficha wapi aibu hii!
Jamani, shetani gani kakukuta wewe?” mama Tora alifok kwa ukali.
“Naomba niache nipumzike!
Mbona unanifatafata!
Hayakuhusu bwana!” Alifoka kumkemea mama yake. Mama yake alinyog’onyea. Aliamua kuondoka ingali alizidi kuzungumza maneno kwa Tora.
“Mtoto gani wewe?
Hata ubebweje, mbeleko unaichana!
Lione!” Mama Tora aligundua kuwa Tora alikuwa kab-wia mtama. Hakuona wala kuhisi aibu sababu alikuwa chakari amelewa. Mama Tora alitoka chumbani kwa Tora akijiwazia atakalolifanya. Hakuwa na ubishi na aliufumba mdomo wake. Alistaajabu jinsi familia yake ilivyoingiwa na pepo wabaya.
*****
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi kesho yake, Mama Tora alimchukua Caro aki-wa mnyonge kwenda hospitali. Wakiwa njiani hawaku-semeshana neno. Kila mmoja alikuwa akitafakari matatizo yake.
“Daktari, naomba umpime mwanangu.” Mama Nasoro alimwagiza daktari.
“Mama, nimpime nini?
Malaria ama kitu gani?” Daktari alihoji
“Njoo basi nikuume sikio.
Naomba mpime ujauzito.
Nahisi anaweza kuwa na mimba.
Kama hadhari, mchunguze.
Usihoji kitu nitakulipa.
Nitakulipa utakacho baba!” Alimnong’oneza.
Alikanganyikiwa. Iweje mimba ipimwe na ionekane siku moja hasa tu baada ya kubakwa? Baada ya Caro kupimwa alipatiwa majibu na kupatiwa huduma stahiki. Alitakiwa kurudi baada ya miezi mitatu kufahamu hatma ya afya yake. Baadae walirejea nyumbani. Mama Tora aliwaarifu wanafamilia kuwa, Carolina ni mgonjwa wa malaria hivyo amepewa pumziko la siku saba. Aliomba wamsaidie kazi za ndani apumzike.
Wakati siku ya pili ilivyojiri, Mama Tora ilimlazimu amwondoshe mtoto wake ili kupunguza hasira za Caro-lina. Alimwagiza Tora kwenda Zanzibar kwa Shangazi yake. Mama yake alimtaka abaki huko hadi hapo ange-muita. Tora hakupinga, aliona dhahiri Mama yake kam-sitiri. Hakuchukua muda, baada ya siku mbili alitoweka. Siku ya kuondoka ilikuwa ya furaha kwa Tora. Alijua ataficha aibu zote. Wakati huo majirani hawakufahamu pia kuhisi jambo hilo. Kweli mchelea mwana kulia hulia yeye.
Baada ya siku nane hali ya Carolina ilianza kutengemaa kama awali. Aliendelea na kazi ingawa hakuwa na fura-ha kama alivyokuwa mwanzo.
****
Muda ulizidi kuyoyoma, masaa yalikatika na siku zika-hesabika. Caro aliendelea na kazi zake kama awali na kujihisi amani ikimrejea. La hasha! Alijidanganya wakati huo. Mengi yaliyomnyima furaha yalizidi kumkumba. Hakuwahi kuwaza kama Mzee Miembe alikuwa tayari akielekea ushaibu wake kama angeweza kumuwazia na kumtamani Carolina.
Siku moja, Mzee Miembe alirukwa na usingizi baada ya kuota amekumbatiwa na Carolina kitandani. Aliposhtuka alienda moja kwa moja chumbani kwa Carolina. Ilikuwa baada ya miezi miwili kupita na hakuwa ameyasahau maumivu yaliyomkumba hapo awali. Alipofunguzwa Carolina hakuufungua mlango mara moja zaidi ya kuhoji.
“Nani?
Unataka nini usiku huu?”
“Fungua Mama!
Mimi Mzee Miembe tajiri yako!” Alijitambulisha. Wa-kati huo alijizoazoa toka kitandani kwenda kuufungua mlango. Aliufungua mlango kwa hadhari.
“Nahitaji tuzungumze ndani.
Nina machache ya kukueleza.” Wakati huo Carolina ali-hisi pengine Mzee Miembe amesikia habari ya kubakwa kwake. Alitii amri ya mwenyeji wake, mwenye nyumba aliyemwajiri aliafiki.
“Karibu Baba!
Mbona usiku hivi?
Kuna tatizo?” Carolina alihoji mfululizo.
“Tatizo lipo! Lakini.......!” Alishikwa tambaza.
“Tatizo gani?
Mama anaumwa, ama kuna nini?” Aliendelea kuhoji huku wote wamesimama ndani ya chumba.
“Naomba niketi!
Ama hutaki?” Mzee Miembe aliuliza huku kamkazia macho Caro.
“A..Ha.! Ee...! sawa.” Alijibu kwa hofu.
“Carolina.
Nahitaji uwe mke wangu wa tatu mama.
Nakupenda sana tangu utue humu ndani.
Unasemaje?” Mzee Miembe alijifaragua.
Wakati hajajibiwa kitu alitaka mkumbatia Caro kwa nguvu.
“Niache tafadhali.
Naomba niache!” Caro aling’aka
“Naomba utambue mimi ndiye mwenye nyumba hii.
Nitakupa kila kitu ukitakacho.
Halafu usipige kelele, Mama yako atasikia.” Mzee Miembe alibembeleza.
“Sikutaki kizee!
Hata haya huna! Lo!
Nyumba hii vipi? Nenda kwa binti yako sasa!” Caro ali-foka.
Mzee Miembe hakuelewa. Alifunua kiunoni alikofunga kitenge. Kutazama Caro aliona kunakisu kimeviringwa. Mzee Tora wakati huo alitumia ubabe wake kumpata Carolina.
“Nitakufanyia kibaya.
Utake usitake lazima unikubali!
Usijaribu kufunua mdomo wako nitakumaliza!
Iweje binti mzuri kama wewe uishi kama mtawa?” Mzee alitoa kitisho.
Wakati huo Carolina aliwaza cha kufanya. Mara hiyo alijaribu kutafuta jinsi lakini hakupata ufumbuzi. Alia-mua kuketi kitandani huku Miembe kamwelekezea kisu chake. Alivaa kanga kujisitiri wakati huo wa usiku.
Mzee Miembe alimsukuma na kumrukia. Caro alipiga makelele kisha alinyamazishwa baada ya kujazwa ki-pande cha kanga mdomoni. Mzee huyu bila aibu alizifu-ata nyayo za mtoto wake. Mtihani mwingine ulimkuta Caro. Alijua tayari keshapoteza mwana na hakuwa tayari kupoteza maji ya moto pia. Haikuwa matakwa yake kufanya hivyo, lakini mazingira yalimfanya awe hivyo. Baada ya jambo hio kumkuta, Caro alianza kutafuta namna ambayo angeiepuka nyumba hiyo. Alificha siri hata Mama Tora hakufahamu zaidi ya kuhisi tabia za Carolina kubadilika siku hadi siku. Alikuwa tayari ameanza maisha ya mapenzi pasipo kupanga. Alipata hata shauku ya kumpata kijana mtaani ambaye angemsaidia japo lolote la msingi. Hakufahamu hata kama siku itafika atalia machozi ya buriani.
Koba ndiye alikuwa mwamume wa tatu kummendea Carolina. Hakufahamu kilichojiri. Alikuwa ni kiwembe karibu mji mzima walimfahamu. Ingawaje alipendelea sana kushinda mtaa wa Makoroboi, hapakuwa na msi-chana aliyekatiza mbele yake pasipo kumchombeza ha-takama angekuwa na sura ya ajabu. Alijiita baharia wa nchi kavu huku hajulikani wapi maskani kwake.
Kwa kuwa duniani hakuna siri. Mambo yote yalikuwa hadharani. Uhusiano wa Carolina na Koba ulianikwa hadharani na karibia kila mtu alifahamu ukweli huo na walijisemea. “Ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bo-vu” Carolina aliukwaa mkenge.
Baada ya miezi miwili baadae kupita, mambo yalianza kubadilika. Carolina alikuwa ni mtu wa kutapika na ki-chefuchefu wakati wote. Afya yake ilianza kudhoofika hasa kwa kuwa alikuwa hafahamu kilichokuwa kikiendelea. Baada ya hali hiyo kutokea na fununu mbaya za Carolina juu ya Koba aliwafanya waajili wake wamtupie virago nje akaendelee na maisha yake ya kawaida. Mama Tora alimtamkia;
“Caro!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naona maisha ya nyumba hii yamekushinda.
Tunaona afya yako inayumba hata kazi tena hazifanyiki. Naomba uondoke!
Ondoka tafadhali usitufie sie.
Hakuna kazi ya mgonjwa.
Kama una mimba shauri yako na kama una nini hukohu-ko…”
“Mama, kwani kazi sifanyi?
Nitaenda wapi mama yangu. Nisamehe nitabadilika.”
“Hayawani mkubwa.
Mama yako nani? Eti nitaenda wapi.
Mfate mama yako kaburini.
Msichana hunastaha wala chembe ya heshima.
Iweje tuchangie mume katika umri huo? Muone Malaya! Toka nyumbani kwangu nitaku….” Alinyanyuka mama huyu na kumkamata masikio Carolina. Alimvuta na kumgongesha ukutani. Carolina alichoropoka. Mama Tora alienda chumbani na kuokoteza nguo za Carolina na kumrushia. Carolina alitupiwa mizigo yake nje. Hakuwa na pa kwenda zaidi ya kulia kama mtoto. Koba alikuwa karubandika hakujulikana alikolala. Hapakuwa na nyumba yeyote ya kulala wageni ambapo alikuwa hafahamiki. Kumpata ilikuwa mtihani mgumu.
Maisha yalianza kuwa kama achali kwa Carolina. Huzu-ni yake wakati huo ilikuwa ni ataishi wapi, hiki ndicho kitendawili kilichokosa mteguaji. Maisha yake yalizidi ugumu na kutotambulika kama tui la nazi na maziwa.
Akiwa amebeba kifurushi chake, alienda ovyo. Hakujua aelekee wapi. Alijawa na simanzi na alijisemea,
“Masikini mimi!
Kwa nini?
Tangu alfajiri hadi kiama maisha yangu kizungumkuti.
Kwa nini nizaliwe nihangaike namna hii!
Tazama, matatizo yameniandama kila pahala.
Kwa nini nisife angalau nimfuate Mama yangu?” Alilia kwa uchungu wakati wote.
“Angalia, hata niliowaamini wamenigeuka.
Sijui nifanyeje hata pesa zangu wameninyang’anya.
Mola-e! Nichukue Baba!”
Wakati yamejiri hayo, aliwaza wapi aelekee. Aliwaona wanaume wabaya kipindi hicho. Ingali hakujua wapi atapata msaada alijua fika kuwa hawezi kuyafikia mam-bo yote yaliyokuwa katika ndoto zake za maisha. Aliji-wazia kuwa tabia ilikuwa jambo muhimu sana kwa binadamu kama yeye. Alijilaumu sana wakati huo;
“Kwa nini nimevunja agano la roho yangu.
Nimesaliti agano langu mwenyewe.
Ee Mola nifanye niishi katika ahadi zangu.
Lakini, ah!….” Suluhisho lake lilimjia aelekee pale se-hemu ambayo huegeshwa magari ya mizigo. Wakati huo palijulikana kama ‘PARKING ambapo alijua ni sehemu sahihi kwake. Alipokaribia katika eneo hilo alipepesa macho yake aliona maandishi kwenye kibanda kimoja kilichojengwa kama jukwaa juu yake kumeandikwa “ACHA NGONO UKIMWI UNAUA!” Hakutilia maanani na aliendelea akajiegesha karibu na mchoma mahindi barabarani. Hakuwa na senti moja mkononi mwake wala chochote baada ya kutimuliwa. Kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Giza lilimwishia Carolina na kumfanya alizoee kama ndugu yake wakati huo.
Je alienda wapi binti huyu? Je Carolina alipatwa nini maishani mwake? Nani alimsaidia ama aliamua kuishi maisha
Alasiri
CAROLINA ALIPATA MTIHANI usio mtahini. Hakumfa-hamu nani angekuwa mwokozi wake. Alivyosongwa na mawazo hakuweza kuwasikia waliopita na kumsabahi. Hamu ya kula na kunywa chochote ilimhama. Hata kama angeshikwa na hamu asingeweza kukipata cha kumsitiri shida yake kwa kuwa hakuwa na senti ya kumsaidia. Kwa maisha aliyozoea kuishi hakubahatika kupata rafiki wa kumsitiri hata pa kulala. Aliyazoea maisha ya uani ya kuishi kama mwali ama bata aliyefugwa. Kila jambo alilowaza, aliishia ukingoni.
Wakati hajala wala kunywa, ugumu ulimkabili na kum-nyang’anya furaha yake. Aliwaza wapi pa kulala wakati huo. Hakupata jawabu zaidi ya kububujikwa na machozi. Alipowaza arudi kijijini alikotokea kwa walezi wake, hakika alihisi kukanganyikiwa. Alikosa cha kuwaeleza endapo angerudi huko. Ilivyokuwa hawezi kusimulia, familia yake wote walitoweka duniani. Kifo chao kilitokana na kupondwa na nyumba ya matope iliyoenda mrama kutokana na mvua kubwa zilizonyesha msimu huo wa masika. Cha kuumiza zaidi roho yake, hakupata taarifa mapema kwani maisha yalimtenga na nduguze.
Alichofahamu ni kuwa, kuna mjomba wake na binamu yake walikuwepo huko Isagenhe na wote walikuwa tara-jali wa kifo. Wote wawili waligundulika na virusi vya ukimwi. Hakuwa na msaada na hakujua aelekee wapi. Wakati huu aliishi kama nzi akisadifu usemi kuwa, ushikwapo shikamana uchwewapo na jua lala.
Majira ya saa kumi na mbili unusu ilivyo kawaida ya wakatisha tiketi waliojipatia kipato, hurejea makwao kupeleka riziki walizojipatia kwa kutwa nzima. Haikuwa tarajali yake msichana Carolina kukumbana na hatimaye kuangukia mikononi mwa Pachoto. Huyu alikuwa mkatisha tiketi hapo mjini. Hapakuwa na aliyekuwa hamfahamu kijana huyu. Alikuwa mtanashati na mwingi wa maneno. Akiwa amepanda baiskeli yake ndogo mfano wa baiskeli zilizozagaa miji yote Afrika ya mashariki. Alipiga mluzi na kuimba wimbo kwa sauti;
Safari safari ee!
Safari safari
ee mama,
Kaja Tuma anadai noti-ee!
Safari kaahirisha-ee!
Msafiri kafiri-ee!
Ee mama,
Abiria chunga pesa zako-ee!
Vijaluba wasikuteke-ee!
Kuwa macho ee!
Ee mama,
Stendi mbwa mwitu ee!
Usikae koroboi ee!
Kaa rada oooo!
Ee mama.
Baada ya wimbo alijisemea.
“Maisha gani haya kero kutwa?
Stendi kelele.
Nyumbani ukifika ndo usiseme.
Kuna haja ya kuwa na kajumba ka uani.
Katanisitiri nikichoka kelele.
Mke wangu mdomo mrefu kama kasuku.
Ukikanyaga tu-we mamaaa!
Heshima hakuna, dharau mwanzo mwisho.
Mara e-unanuka kikwapa cha stendi.
Siku nyingine, he-hujapiga mswaki! Jamani….”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alitokea barabara yaingiliapo magari yatokayo jijini Dar-es-salaam. Wakati huo alikuwa anarudi mjini akito-kea kwake huko Burunde ambako ndiko alikuwa ame-jenga na kuishi na mkewe wa ndoa na watoto wake wa-wili. Alidhamiria kufuata mahitaji ya nyumbani kwani kutwa nzima hakupata chochote. Alitamani aingie katika hoteli moja iliyomtaa huu wenye biashara zenye thamani. Hoteli hii ilipendwa na wengi hasa wakazi wa mji wa Nzega na wageni mbalimbali kutoka nje.
Pachoto angejiita mwenye bahati kama asingekutana na Carolina. Alipokuwa akipata kikombe cha maziwa, ma-cho yake aliyaelekeza nje alipo egesha baiskeli yake. Alihofu kama angekwapuliwa ingekuwa vigumu kuipata baiskeli hiyo kwa muda ule.
Asiye hili wala lile, macho yake yaliongezwa upeo kati-ka giza na gari lililokuwa limechelewa kufika mjini likitokea Dar-es-salaam. Malaika wa kifo walimuunganisha kuiona sura ya Carolina akikatiza katika mwanga ule. Alibeba furushi alimokuwa amefungasha nguo zake. Carolina aliamidi kuelekea maeneo ya Mwaisela karibu na kiwanja cha Samola. Kiu yake ilikuwa ni kumtafuta dada yake mzee Malecha ambaye aliolewa katika maeneo hayo.
Pachoto hakuyaamini macho yake. Alihisi macho yake yalikuwa yakimfisadi na kumsanifu. Aliiangalia saa yake kwani hakuamini kama kweli Carolina, mwali wa kwa Mzee Miembe, mtoto wa uani, angekuwa mtaani anaswampa peke yake wakati huo. Aliamua kukiacha kikombe cha maziwa nusu angali tayari amekilipia kwa uchu wa kumfuatilia Carolina. Alipokuwa amemkaribia akiwa anajitahidi kuvuka ng’ambo ya pili ya barabara iendayo Singida, akiongozwa na taa za baiskeli yake, Pachoto aligundua kweli alikuwa Carolina.
Wakati huo alijihisi fahari. Pachoto alimuita Carolina kwa sauti ya upole na huba.
“Dada Caro!”
Dada Caro!......” Wakati huo Caro alisikia na aliitika pasipo kugeuka kumwona aliyemwita;
“Abee!
Unasemaje?” Hapa Carolina aligeuka na kuangaza ma-cho yake.
“Ni wewe?
Nipe habari, unasemaje? Carolina alionesha ukaribu machoni mwa Pachoto. Alijikanyaga kanyaga wakati huo hasa kwa kuufahamu msimamo wa Carolina wakati angali katika familia ya Miembe.
“Ni mimi ndiyo!
Mambo poa!
Hu .... ah! Anyway!” Pachoto aligugumia. Kijana huyu alikuwa guberi kuzidi kiasi. Alijikaza
“Safari ya ..a wapi saa hizi?
Mbona pia ni usiku... si kawaida yako!
Aliendelea kuya-kokota maneno. Kwa kuwa jasiri haachi asili, Carolina alibaki mkimya kidogo kisha aliendelea;
“Safari yangu inanichukua kule nisikokujua.
Nafahamu hutaamini kilichonisibu leo!” Alikatiza.
“Una maana gani?
Kusikojulikana!
Ndio wapi huko?” Pachoto alihoji.
“Ndiyo! Pasipofahamika.
Nimefukuzwa na tajiri yangu.
Kosa langu silijui!” Carolina alijieleza.
“Sema koma!
Wewe ufukuzwe!
Mtoto wa uani!
Kweli makubwa!” Alikuwa kaduwaa macho kayatum-bua.
“Niambie, tatizo gani tena?
Ama ndio ka mchezo ka uani?” Pachoto alisema kwa kejeli.
“Acha maneno yako! Ka mchezo ka uani gani!” Usini-udhi sasa!
“Nisamehe dada yangu.
Huo ni utani tu!” Pachoto alimwelekea Carolina.
“Tatizo kwani ni nini?” Alihoji.
Carolina alimweleza Pachoto yote yaliyomsibu. Alimweleza kinagaubaga kule alikokuwa akielekea muda huo. Baada ya kumsikiliza Carolina, Pachoto alifahamu kajipatia kivuno. Alifahamu kuwa kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Wakati huo akiutekeleza usemi kuwa, vita vya panzi ni furaha ya kunguru. Sasa aliamua kumrubuni Carolina kwa maneno ili avune usingizi.
Kupiga domo na kubemba ilikuwa jadi yake Pachoto. Aliweza kumshawishi msafiri apande gari la kusubiri na aliache lililokuwepo kituoni. Iweje leo ashindwe kumbadilisha msimamo Carolina aliyeishi kama popo kwenye nyumba iliyobomolewa paa wakati huo.
“Caro!
Shida kaumbiwa binadamu.
Nawe pia kubali kukabili hali hii.
Eh!......ninaombi moja,...
Sijui niseme……!
“Hofu yako ni nini juu yangu?” Carolina alihoji.
“Mimi si nduguyo.
Yanini pilipili nile mie wewe ikutoe kamasi?
Achana na porojo zako.
Shida haizoeleki.”
“Hapana Carolina.
Najua hasira zimekutawala wakati huu.
Tuliza moyo wako.
Ongea na watu uvae viatu.
Nipo tayari kukusaidia kwa kila hali.
Upo tayari?” Pachoto alikazia.
“ Pachoto! Nafahamu maisha yenu watu wa stendi.
Maneno mengi kama kasuku.
Mimi si msafiri, mimi ni mtembezi mjuvi.
Fuata hamsini zako niachie hamsini zangu pia!
Nielewe!” Caro aling’aka.
“Sikiliza Carolina.
Unamwamini Mungu? Alihoji.
“Ndiyo!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha yangu yote namwamini yeye.
Najua madomo yenu stendi yamejaa matusi na uongo.”
“Acha kunitusi.
Maisha huenda vile uonavyo yakiwa.
Ya kituo cha basi waachie wapiga debe nay a nyumbani halali kwa wenye miji. Mimi ni Pachoto na maisha yan-gu. Humpasa mtu kufanya kile aonacho kitamfaa. Ki-kubwa ni kushibisha tumbo lake. Maisha ndivyo yalivyo ukweli wake. Hatuishi kwa ndoto bali uhalisia. Nielewe Carolina!”
“Unaweza kunisaidia kwa lipi sasa?
Naona usiku wazidi kuingia.
Acha niende!” Alianza kuondoka.
“Hapana!
Naomba nisikilize mara moja!
Naomba!”
“Mara ya mwisho!
Sema utanisaidia lipi?” Caro aling’aka kwa hasira.
“Vyovyote utakavyo nifanye nitafanya.
Una chochote?
Hela za kukusitiri?
“ Mh! Si....!” anakumbuka kweli hana hata chembe ya kumfanya aishi na kuingoja kesho.
“sina!”
“Naomba!
Naku.....!
mh!
Nakupenda Carolina!
Sana!
Nakupenda naomba unikubali.” Alichombeza Pachoto huku akiwa amepiga magoti akijidai kutoa machozi.
Alipiga domo la kumtaka Carolina apumzike naye siku hiyo. Ilimchukua dakika kumi na tano wakiwa wamesi-mama njia panda ya kuelekea hospitali ya Mwaisela. Haikuwa rahisi kumng’oa Carolina kama mbuyu uli-okomaa. Kwa usanifu wake wa kubemba alimwimbia mashairi yenye urari na vina.
“ Caro, najua wewe ni binti mwema na mrembo sana.
Sipendi nikuone unapata taabu kama hizi.
Nitakusaidia lolote ulitakalo.
Nitauza hata nyumba yangu nikusaidie.
Fahamu, ukimwona mtu usimdharau.
Mheshimu kwani hujui kesho atakuwaje.
Kumbuka, wengi watakutamani, lakini atakupenda mmoja pekee. Mimi nimekupenda si kukutamani.”
Maneno matamu yalipenyeza masikioni mwake na kubisha hodi kwenye ubongo wake. Wakati huo mguu wake aliutumia kuchorachora chini kuashiria ameshindwa. Caro aliyameza maneno yote yaliyotoka mdomoni mwa Pachoto na kushibisha roho yake. Alipowaza hali aliyoishi nayo muda huo, alihisi ni heri akamkubali Pachoto kwa ajili ya kumchuna. Alijua fimbo ya mbali haiui nyoka. Alikubali na ndipo kiu ya Pachoto ilianza kupata kinywaji alichokitamani.
“Naomba nyanyuka Pachoto.
Nitakupa sharti moja la msingi kama kweli unanipenda.” Aliyatamka maneno hayo huku akimvuta Pachoto.
“Nitakupenda milele amini.
Nipo tayari kwa lolote.
Sema nifanyeje?” Pachoto alitamka.
“Nimekubaliana na wewe.
Lakini naomba nisaidie kwanza.
Rafiki wa kweli ni yule akufaaye wakati wa dhiki.
Jiite mwenye bahati, kwani tutazidi kufahamiana.”
“Asante!
Asante Caro!” Alimshika na kumrukia kwa furaha.
Ushindi wasaa huo uliangukia kwa Pachoto. Kilichoku-wa kimebaki kutekelezwa wakati huo ni juu ya Pachoto kutafuta pahali salama pa kujisitiri. Hapakuwa na fikira nyingine wakati huu. Wote wawili waliambatana kuele-kea magharibi tokea walipokuwa wamesimama. Pachoto hakuwa na fedha mfukoni wakati huo. Aliamua kwenda palipo muamala ya NMB ili kujipatia pesa ya dharura. Alichomoa shilingi elfu hamsini kulipa gharama ya malazi na chakula katika moja ya nyumba za kulala wageni zilizokuwa karibu na fikra zao.
Pachoto alijua kuwa amejipatia kilichobora walichokikosa wengi. Aliamini Carolina ni kifaa ambacho hakikufahamu mwanamume. Kama si hivyo, basi kuendesha baiskeli ndiko kwaweza kuwa kulinyang’anya usichana wake. Aliamini sana hata zaidi ya asilimia mia wakati anaisaliti ndoa yake. Walijivinjari na Carolina usiku ule pasipo hadhari. Ilikuwa ni hatari, kwani alifanya upasuaji pasipo kuzuia hatari yoyote tarajali.
Alipanga kumwoa Carolina kutokana na vile alivyolewa na mvuto wake.
“Nakupenda sana Caro!
Nipo tayari kukuoa hata leo.
Niahidi hutanisaliti.” Alinena Pachoto.
“Usiwe na wasiwasi.
Bado ni mapema mno kutamka hivyo.
Kila jambo lina wakati wake.
Vumilia siku itakuja kama kweli umeamua.” Caro aliongea kwa sauti ya huba huku akimpapasa Pachoto kidevuni.
Wakati huo wote walikubaliana kuoana huku fika Pa-choto alikuwa na ndoa tayari. Wakati huo wa usiku siku ya pili, Malaika wa mwanga pamoja na maulana el fad-hili aliamua kumpiga kofi la fahamu Pachoto. Ama kweli ilikuwa mtihani wenye hila uliomuumbua Pachoto. Haikuwa tarajio lake. Carolina alishikwa na maumivu ya tumbo ghafla huku akitapika kwa sababu ya jelezi iliyomkumba. Ilikuwa kengele ya tahadharisho kubwa. Pachoto alijihoji maswali mengi kuwa nini kimetokea. Katu hakufahamu lililojiri wakati huo. Alihisi kamchezo kalizidi furaha ya Caro hivyo hali itakuwa tulivu muda usio mrefu.
Kwa kuubeba mzigo uliomkabili, Pachoto alilazimika kumchukua Carolina kumpeleka hospitali moja ya kuji-tegemea iliyokuwa karibu nao. Ni karibu hapohapo Mwaisela. Kufikishwa kwake wodini alitundikiwa chupa ya maji ili kufidia kiasi alichokuwa amekipoteza.
Ilipotimu saa tatu asubuhi, ilikuwa tayari saa tano tangu Carolina afikishwe pale hospitalini zimepita. Daktari aliyekuwa zamu aliafiki mara hii kuchukua vipimo vya afya ya Carolina. Alitaka kufahamu kama kuna tatizo lolote lililo msumbua.
“Dada yangu.
Kaa vema tufanye uchunguzi wa afya yako zaidi.” Dak-tari alimwomba Caro.
“Kwani kuna nini daktari?
Naomba nipumzike kidogo.
Nahisi sina nguvu kabisa.” Caro alimwomba daktari.
“Hapana!
Naomba nikupime sasa.
Ni muda mfupi utapumzika.
Nahisi kuna jambo linalokufanya utapike.
Kama si malaria, acha tuangalie.
Naomba jikaze tufanye vipimo.” Alisisitiza daktari huku akirudishia mlango wa chumba alimolazwa mrembo huyu.
Daktari alibobea katika kazi yake. Ilimchukua muda mfupi sana kuufahamu ukweli. Carolina hakuwa na hili wala lile juu ya afya yake. Hakuwahi kuugua malaria, taifodi wala kisukari. Majibu ya vipimo vyake yalipati-kana. Daktari hakutaka kumpa majibu mgonjwa moja kwa moja kwa hofu ya kupoteza hali yake kwa mshtuko. Ilikuwa si rahisi wakati huu kumweleza Carolina. Ilim-chukua muda mfupi kusafiri dunia ya saba ndiko aliko-kuwa akivinjari kwa usingizi. Aliyekuwepo wakati huo alikuwa Pachoto pekee mtu ambaye alijilengesha kuubeba mzigo wa Carolina. Alikuwa kaketi mapokezi kusubiri taarifa ya daktari.
“Pachoto!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Pachoto!” Daktari aliita huku akichungulia ma-pokezi toka ofisini kwake.
“Naam!
Nakuja daktari!” Alikuwa na shauku ya kufahamu mpenzi wake wa hamu alitatizwa na nini.
“Naomba keti hapo.” Alimwonesha pa kuketi.
“Ndiyo Daktari!
Nimeitika wito.
Nieleze, anasumbuliwa na nini bibie?” alihoji Pachoto.
“Mr Pachoto!”... Daktari aliita.
“Naam daktari!”
“Carolina ni mkeo ama nduguyo wa kawaida?”
Akiwa mwenye kujiamini, Pachoto alijibu kwa majivu-no yaliyotokana na wajihi wa Carolina kuwa alifaa ku-wa ahali wa mtu mwenye pesa pia heshima.
“Ni mke wangu daktari!
Kuna tatizo?” Pachoto alijigamba.
“Ndugu Pachoto, una roho ya kiume?” Lilikuwa swali kutoka kwa daktari. Swali ambalo lilimuingiza Pachoto katika ulimwengu wa mashaka.
“Kwa nini unauliza hivyo daktari?.. alihoji badala ya kujibu ndiyo ama hapana kwa swali la daktari. Daktari aliendelea kumpatia ushauri pamoja na maneno yenye nasaha ambayo hakuwahi kuyasikia popote. Pachoto alipatwa na wasiwasi.
“Bwana Pachoto, hongera sana!”
“Kwa lipi daktari?” Pachoto alihoji. Hakufahamu kitu chochote, alihisi kama kuna miujiza inayomtia kiwewe na kuikanganya akili yake. Wakati huu angalau alihisi si tatizo kama ni mimba wangeitoa wakati wowote na ku-endelea na maisha yao ya kinyumba.
“Ndugu Pachoto.
Zingatia sana ushauri nitakao kupatia.
Nataka uendelee kuishi na kutimiza ndoto zako.
Wewe pamoja na mkeo pia kichanga anaye tarajiwa nusu mwaka uliobakia,...
Eee! Kwa kuwa binadamu alizaliwa kwa uchungu na pia huru, hapa duniani kuna minyororo iliyofunga furaha yake. Ni vema kuyachukulia yote kawaida. Hata siku ya ndoa yenu kasisi aliwaasa kuwa, mtaishi pamoja katika shida na raha......... ( Alikaa kimya kidogo na aliendelea). Mkeo Carolina, kutokana na vipimo vilivyo ni kwamba, ana mimba ya miezi mitatu. Hongera sana!”
“Asante daktari!” Alijibu kwa wasiwasi wa akisikiacho.
“Mbali na mimba, analo tatizo lingine.”
“Lipi daktari, nieleze.” Kiwewe kilimpanda.
“Mkeo analo ambukizo la vijidudu vya ukimwi!
Ni heri kama nawe unaafiki kupima afya yako ili nyote mjiunge na dawa za kurefusha maisha.
Pole sana mdogo wangu!”
Wakati daktari alipomalizia neno “pole sana” Pachoto alikuwa akibubujikwa na machozi kama chemchemi zitokazo mlima Kilimanjaro. Alijitahidi kuyafumba na kuyakodoa macho kulizuia chozi hilo adimu juu ya jaha bila mafanikio. Aliposhindwa kuuhimili uchungu huo, aliangua kilio hadharani. Daktari alimsihi kwanza asim-julishe mkewe. Pachoto alikanganyikiwa na hakuweza kuwaza kama angekuwa na hali hiyo. Akili ilimjia kuwa aondoke zake kurejea numbani kwake.
Bila shaka Pachoto alitoka nje na kupanda baiskeli yake kwenda nyumbani kwake. Wakati huohuo daktari alitoka nje na kumwona Pachoto akitokomea barabara iendayo Singida. Alielekea mashariki kuliko makazi yake.
*****
Alipozinduka usingizini, Carolina alihisi hali yake im-ekuwa sitiri. Alijihisi buheri wa afya ingawaje ndani aliwaza sana. Wakati akijiwazia kuhusu wapi ataishi, ghafla daktari aliingia chumbani alimokuwa amepatiwa kitanda. Alitaka kufahamu ukweli pia kutoka upande wa pili. Alipouliza kuhusu uhusiano wake na Pachoto, Carolina hakuficha kitu. Alimjuza daktari kuwa alikuwa hawara pekee aliyekutana naye siku mbili zilizopita. Alistaajabu sana daktari na hakuchelea pia kumpa pongezi kuwa anao ujauzito wa miezi mitatu. Jambo hilo halikumfurahisha Carolina. Alionekana kutowekwa na hali yake aliyoamka nayo. Alipoulizwa hali yake ikoje, alimfahamisha daktari kuwa alijisikia mzima walau. Alimjulisha angemruhusu kutoka hospitalini hapo muda wowote. Wakati ule, alimtaka amfuate ilipo ofisi yake ili amuage na kumruhusu kurudi nyumbani.
Hata kama alikuwa na huzuni, Carolina alijikaza kisabuni na kumfuata daktari. Hofu yake ilikuwa ni juu ya gharama za matibabu. Alihisi kuwa Pachoto alishindwa kumudu gharama na pengine hakulipa deni alilokuwa akidaiwa. Ukweli haikuwa hivyo. Pachoto alilipa gharama zote za matibabu achilia mbali pesa alizokuwa amempatia Carolina kama malipo ya kumkubali na kubarizi naye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment