Search This Blog

Tuesday, 14 June 2022

JAHA - 3

 





    Simulizi : Jaha

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Hata kama alikuwa na huzuni, Carolina alijikaza kisabuni na kumfuata daktari. Hofu yake ilikuwa ni juu ya gharama za matibabu. Alihisi kuwa Pachoto alishindwa kumudu gharama na pengine hakulipa deni alilokuwa akidaiwa. Ukweli haikuwa hivyo. Pachoto alilipa gharama zote za matibabu achilia mbali pesa alizokuwa amempatia Carolina kama malipo ya kumkubali na kubarizi naye.

    Kama ilivyokuwa kwa Pachoto, daktari alimjuza caroli-na kuwa alikuwa na virusi vya ukimwi. Alipojulishwa hali hiyo alizirai kwa mshtuko. Aliishi pasipo fahamu yake pale hospitalini kwa muda wa saa nane. Alipozin-duka na kurejelewa na fahamu yake alitamka maneno yaliyomuumiza sana daktari, alisema ;

    “Yatima mimi, Mungu!

    Mbona umeniacha niangukie majaribuni!

    Nimekuwa na chozi lisilokauka machoni kwangu

    Sifahamu ubaya wangu hata na yule atakayenisitiri.

    Eee mola!

    Aibu yangu nihifadhie.

    Sina matumaini ya jaha katika dunia hii.

    Kijakazi mimi.

    Kwa nini sithaminiki mbele za watu hadi niishi hivi?

    Nani! Nauliza nani kanipa ukimwi?” Alilia sana kwa uchungu.

    Carolina alimwomba daktari ushauri nasaha kuhusu hali yake. Alikuwa amekanganyikiwa na kusahau kama alie-lezwa. Daktari hakusita kurudia nasaha zake. Alimhuru-mia sana Carolina na hakutaka kumtoza pesa ya ziada kwa muda ule aliishi zaidi. Aliahidi atamlipia gharama hiyo na mola ndiye atakayemlipa. Aliruhusiwa kutoka pale hospitalini siku iliyofuata. Hakuwa na sehemu ya kwenda wakati huo. Ilimbidi arejee katika nyumba ya kulala wageni alikokuwa amejisitiri yeye na Pachoto na isitoshe aliacha mzigo wake pale mapokezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa na pesa zilizobakia elfu ishirini, aliamua kuuza vipande vyake vya kitenge na viatu vya wazi. Jumla ali-pata shilingi elfu arobaini. Pesa hiyo ilimtosha kulipia chumba na chakula kwa siku zaidi wakati akitafakari la kufanya. Wakati akibakia peke yake mule chumbani, alimkumbuka Pachoto na aliwaza tangu maisha yake yaanze kuwa ya shida. Alitokwa na chozi la simanzi pale alipojihisi kumwonea Pachoto pasipo kufahamu. Alijuta kwa kumwambukiza gonjwa ambalo hata yeye hakufahamu kama alikuwa na hali hiyo.

    Aliwaza kuitoa mimba wakati huo mara tu apatapo ngu-vu. Kila wakati alisita na kuyakumbuka yaliyomkumba mama yake. Kwa jinsi alivyokuwa na rindi la ushamba machoni mwake kuhusu mitaa na kutowajua watu, Carolina hakufahamu hata kuhusu athari ya utoaji mimba. Alikuwepo dada mmoja aliyekuwa mapokezi alimwomba atete naye kidogo. Aliyatapika yote yaliyokuwa sirini mwake ingawaje hakumjulisha kuwa yeye ni marehemu tarajali. Kuhusu mimba, dada yule alimshauri aitoe. Alimhakikishia ataitoa salama na haitamchukua hata dakika thelathini. Alichomjuza ni kuwa, anaye daktari wake ambaye humtumia mara anasapo na gharama yake ni shilingi elfu kumi na tano pekee. Hakika dada huyo alikubuhu kwa zoezi hilo la kukatisha maisha ya viumbe vilivyokosa hatia.

    Hatimaye ilifika asubuhi ya siku iliyofuata. Mapokezi huyo alimwendea Carolina na walielekea barabara ien-dayo Tabora nje kidogo ya mji wa Nzega. Kule ndiko aliishi daktari huyo mkatili. Hali ilienda kama walivyotarajia na hakuna kilichoharibika katika zoezi zima. Mimba iliyomsumbua Carolina ilichomolewa kiustadi na afya yake ilirejea kuwa sawia.

    Aliishi hapo akiwa mhudumu wa nyumba ya kulala wa-geni wakati huo. Hakupatiwa mshahara wowote kwa mwezi. Zaidi alipatiwa chakula na malazi pekee. Aliku-wa mwenye haiba yenye mvuto, na umbo pia sura yenye kumuita kila mwanaume. Alikusanya pesa lukuki zaidi ndani ya wiki mbili za awali kuonesha uwepo wake uli-kuwa wa thamani. Alikuwa na wateja wengi waliolipia chumba kwa malazi alimolala yeye na walimlipa pesa ya kuuthamanisha mwili wake kwa usiku. Hakika alipiga ndege wawili kwa jiwe moja .

    Madreva wa mabasi, malori pia wafanyakazi wa mgodi, watumishi wa kada mbalimbali za serikali, viongozi wakiwemo wafanya biashara maarufu, wote walitoa pesa zao kumnunua Carolina. Hakuna aliyeng’amua kuwa Carolina alioza na ni mfu tarajali hadi pale moshi ulipoanza kufuka baada ya miezi michache kupita.

    Hakika aliwavuta wanaume katika mtego usioonekana kwa macho. Carolina alikuwa adimu kama bidhaa iliyo-jiuza yenyewe na si kujitembeza. Carolina wakati huo, aliingia katika dunia ya shetani. Hakuwahi kutamka ha-pana wala nitafikiria. Wakati huu aliwaza kinachoongea ndiyo ama hapana ni kiasi cha pesa alichopanga kupati-wa kuunadi mwili wake.

    Akiwa anaendelea kumeza vidonge vya kuongeza nguvu hakika alionekana zaidi ya alivyokuwa awali. Alinenepa na ngozi yake ilizidi kun’gaa kwa vipodozi vyake ali-vyojiongezea uzuri safari hii akiikana rangi yake ya asili. Ukimuuliza kuhusu Mungu, alikuwa dhahiri amempa kisogo na hakutaka kusikia wala kuona chochote kilicho mhusu Mungu wakati huo.

    Siku moja wakati akitokea Ndala kwa mpenziwe Mwa-limu, alikutana na aliyoiita bahati wakati kuu. Punde alipofika barabara ya lami iendayo mjini Nzega na Igunga alilikuta gari moja la watu binafsi limeegeshwa pembeni linapatiwa huduma. Walipasukiwa na mpira wa nyuma kwa safari ndefu waliyosafiri. Kwa vile alivyokuwa amevaa, hapakuwa na shaka angeweza kumteka yeyote mwenye roho ya karatasi. Kushuka kwake kwenye ganagana iliyoagizwa kumleta barabara kuu ya lami, alikutana na mwanaume mmoja kutokea huko mji wa Goma. Alikuwa ni Mkongo aliyekuwa ameagizwa na ofisi moja ya Umoja wa Mataifa kwenda jijini Dar-es-salaam kufuatilia magari yaliyokuwa yameagizwa toka Japani ili yatumike katika Jamhuri ya watu wa Kongo.

    Mara tu alijikuta akiduwaa na kumfanya amkonyeze kwa kope zake. Wakati huu Carolina alikuwa ameanza kuwa taleheshi mkubwa. Hakumpenda mtu, alipenda pesa yake. Alipoiona nembo ya Umoja wa Mataifa ubavuni mwa gari iliyoharibika alijua pesa imepatikana. Ishara aliyoitoa ilikuwa ni jicho la mahaba huku akionesha miondoko ya maringo. Mkongomani Mputa hakuwa na hali, alisahau cheo alichokuwa nacho na alihisi huyo ndiye aliyekuwa bahati yake. Alishukuru na kuwaza inawezekana kuharibika kwa gari yake ilikuwa imepangwa na Mungu kuwakutanisha na msichana huyu mrembo.

    “Dada, habari yako!” Mkongomani Mputa alisabahi.

    “Salama! We mzima?” Carolina aliitikia kwa mahaba huku akimpiga kope Mputa.

    Carolina wakati huo alionekana si mwenye papara. Ali-sogea pembeni kama anasubiri vipanya vitokavyo Igun-ga ili arejee mjini Nzega kuendelea na kazi yake. Kwa kuwa alizoea kupata wa kuambatana naye, Mkongomani huyu alilazimika kumsogelea Carolina na kutaka kuzun-gumza naye. Haikuwa shida. Carolina alivyompiga ukope na kulegeza macho yake, Mputa nusura kuchizika. Hakuchelea kumtongoza pale alipo mwambia;

    “Murembo, safari –a- wapi Mamaa!”

    “Safari ya niendako! Kwani vipi?”

    “Nataka- ongea na wewe.

    We murembo!” Mputa alimtaka Carolina.

    “Asante!

    Nawe pia handsome!” Huku akitabasamu.

    “Unaitwa nani?” Mputa alihoji.

    “Naitwa Caro!”

    “Caro!

    Una maana Carolite ama Caroline?”

    “Mh! La pili ndilo sahihi.

    Naitwa Carolina!

    Vipi umelipenda?”

    “Zuri sana!

    Kama wewe unavyoonekana.” Alicheka na kufurahi.

    “Wewe je?

    Unaitwa nani?

    Pia unaonekana si mwenyeji hapa, kulikoni?”

    “Naitwa Mputa. Toka Goma-Kongo!”

    “Aaa! Sawa, jina zuri pia!”

    “Asante murembo! Sishindi wewe.”

    Alipojibiwa na Carolina hakuendelea zaidi. Yeye haku-fahamu sana lugha ya kiswahili. Alikuwa stadi wa Lin-gala na Kifaransa pekee. Alifahamu Kiingereza kwa kuibia.

    Yalipompotea maneno yote ya Kiswahili, Mputa alia-mua atamke kutumia lugha ya kiingereza kufikisha ujumbe wake. Jinsi alivyomwona Carolina alijua fika anafahamu maana ya neno lake. Ulikuwa ni ukweli, hata kama ni mbumbumbu lazima alifahamu maana ya neno “Love” likitamkwa. Mlingala huyo alitamka

    “I love you Miss!”

    “Mh! Kweli?”

    “Ndiyo!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi napenda wewe. Vipi?”

    Carolina alikuwa hana muda wa kupoteza. Hakumjibu lingine zaidi ya kumtamkia hata kama alikosea ujumbe ulifika, alisema,

    “The same, love you too!

    Hata mimi nakupenda.”

    “Nipe namba yako ya simu.” Mputa aliomba.

    Alimpatia simu yake ya kiganjani akimpa ishara aihifadhi namba yake.

    “Nitafute muda wowote ukinihitaji.” Carolina alimjuza Mputa.

    Wakati yakijiri hayo, kipanya kilikuwa kimefika. Carolina alipanda na kuondoka zake. Hakupiga hatua ya safari yake bila kuchombezwa kama ilivyotokea kwa utingo wa kipanya hiki.

    “Mrembo vipi?

    Uko poa?” Utingo alihoji

    “Niko poa.

    Vipi wewe?” Alionesha kutabasamu

    “Shwari!

    Safari ya wapi?”

    “Naenda mjini Nzega.

    Kwani vipi?”

    “La! Nimezima na pigo lako!”

    “Utazimaje?

    Kwani wewe taa?”

    “Acha uswahili wako.

    Unajidai hujui maana yangu, si ndiyo ee!”

    “Nimesha kuelewa bwana!

    Asante kwa kuzima.

    Naomba uwake hapo itakuwa poa!”

    “Unaweza kunipa namba yako ya simu?”

    “Bila shaka!

    Andika hii 0-7-6-8-32-7—2 mwisho.”

    “Poa basi!

    Nitakucheki mida mida.

    Usiniangushe.”

    “Usijali!” Carolina aliitikia huku akimrembulia kondak-ta.



    Jioni ilipofika, Carolina alipigiwa simu na Kondakta. Ilikuwa majira ya saa kumi. Carolina hakusita kumkubali yeyote ilimradi apate pesa yake ya kumsitiri. Alikuwa tayari wakati wote hakuchagua muda, pahala wala mvuto wa mtu isipokuwa pesa. Hata utingo huyo alijiunga kwenye zahama siku hiyo hiyo jioni na pesa alimpatia.

    Akiwa mwenye hamu ya kumnasa Carolina, Mputa alimtaka dereva wake asubiri gari zitokazo bandarini Dar –es-salaam ili abadili tairi. Wakati huo ilikuwa majira ya jioni alijua fika kuwa tayari gari zitokazo Jijini Dar es salaam zitakuwa zinateremka mlima wa Sekenke. Alifahamu hivyo baada ya kuwasiliana na madereva kwa simu. Alitamka mara apatapo tairi ya kubadilisha amjuze kwa simu kwani yeye aliamua kwenda mjini Nzega kukutana na Carolina. Alipofika mjini mara moja alimpigia simu Carolina.

    Ilikuwa ni palepale alipoishi Carolina wakati huu. Mputa alifika bila shaka na alimkuta Carolina na walifanya mazungumzo yao na walikubaliana. Alidai dola za kimarekani lukuki na Mputa hakusita kumpatia. Alilala naye usiku mzima huku alimtaka dereva wake arudi mjini Nzega na safari yao itaanza alfajiri.

    Kwa jinsi alichenguliwa alimtaka Carolina amtajie jumla ya pesa anayohitaji ili kuondoka naye kwa siku tano kuelekea huko Dar-es- salaam. Alikubali pia kulipa fidia ya usumbufu kwa kumtoa kazini kwake kwa siku tano. Alitaka Carolina awe kiambata wake wa kumsaidia njiani na mara wafikapo Dar-es- salaam kwani alifahamu kiswahili na alikuwa Mtanzania mzawa. Walikubaliana kuambatana pamoja katika safari hiyo yenye mashaka.

    Je, safari ya Carolina ilikuwa vipi huko Dar-es-salaam?......



    Machweo



    MAISHA YA SHOGA YAKE Carolina naye yalipata misukosuko mingi. Achilia mbali kutuhumiwa kwake na wateja wenye hila kuwa amepoteza amali zao na vito vya thamani. Usiku ule akiwa amejipumzisha na buzi lake, alipokea simu ikitokea kijijini Iditima. Kijiji hicho ambacho kipo mpakani mwa wilaya ya Kahama kilikuwa na visanga vingi.

    Ilikuwa simu ambayo haikuwa ya suhuba wala kumjulia hali wakati huo. Bali aliyempigia alimfahamisha juu ya babu yake mzee Gainda. Alikuwa ametiwa mbaroni kwa tuhuma nzito za mauaji ya mfugaji mmoja tokea wilayani Igunga ambaye ni Bwana Jinasa. Tasira alitaka apatiwe habari hiyo kwa undani baada ya yule aliyemjuza kuishiwa salio katika simu yake. Alipojaribu kumpigia alifanikiwa kufahamu kuwa, alitakiwa kufika kituo cha polisi hapo wilayani kwa ajili ya kumwekea mdhamana babu yake.

    Kwa kuwa ilikuwa ni hapohapo mjini, aliona kufanya hivyo ni jambo rahisi na la busara. Ilipofika kesho yake saa moja na nusu asubuhi alijihimu kuelekea kituo cha polisi. Tasira dada wa mapokezi katika nyumba ya kula-la wageni alijikwatua ili kwenda kituo cha polisi kuufa-hamu ukweli. Kwa kuwa alifika mara nyingi kituoni ha-po kwa tuhuma mbalimbali, haikuwa shida kwake kuwasili kituoni hapo. Alifika kabla ya wakati ikamlazimu asubiri ndipo aweze kuanza mchakato wa kumtafutia mdhamana babu yake.

    Ilipotimu saa mbili na nusu asubuhi ndipo aliliona tenga la polisi likifika kituoni hapo. Ndani yake kulikuwemo watuhumiwa watatu wa kosa la uvamizi, kuvunja na ku-pora duka lililokuwepo barabara iendayo Itobo tokea mjini Nzega. Katika harakati hiyo askari walifanikiwa kunusuru watuhumiwa watatu pekee. Kwa ujumla watu-humiwa hao walikuwa watano, wawili walikuwa tayari wameisha kuungua kwa jinsi walivyochomwa moto wa petroli na wananchi wenye hasira kali.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Palikuwa na msongamano wakati huu katika kituo cha polisi cha wilaya ya Nzega. Tasira alitumia uzoefu wake kutimiza haja yake wakati huo. Alimuomba Koplo Mbuji kuteta naye faragha ili ajue wapi anaweza kuanzia.

    “Koplo Mbuji! We Mbuji!” Tasira aliita.

    “Ahaaa! Tasira, kumbe ni wewe?” Alimsogelea

    “Ndiyo. Ni mimi. Vipi tutete kidogo?”

    “Vipi! Mchumba yupo?” Aliuliza habari za Carolina.

    “Keshaenda zake Dar es salaam.”

    “He! Mara hii! Kulikoni, kunanini huko?”

    “Mi sijui.

    Labda kuna kitu cha msingi anafatilia.

    Si unamjua alivyompambanaji!”

    “Yule si wa kawaida!

    Ama kapata buzi kanitosa baharini. Niambie.”

    “Hawezi.

    Hata kama kapata hatakutosa baharini.

    Lazima atarejea tu alikoanzia.”

    “Tuachane na hayo.

    Niambie, kulikoni tena uko hapa?

    Leo ni kitu gani kimekuleta?”

    “We achatu, ni makubwa!

    Nimefika hapa kwa swala la babu yangu toka kijijini.”

    “Vipi, kafanyaje?

    Kaiba ama kashikwa ugoni. Ama mchawi?”

    “Acha masihara basi.

    Babu yangu ana jambo kubwa linamkabili.

    Nilipokea simu jana kuwa alikamatwa kwa mauaji.”

    “He! Mauaji tena?”

    “Ndiyo!

    Angalia jinsi ya kunisaidia.

    Unajua kababu kenyewe kashajichokea.

    Kakitiwa jela ndo katakufa hapo hapo!”

    “Sikiliza.

    Jambo hili zito sana.

    Utatuzi wake pia ni mgumu.

    Pengine nahisi utapoteza muda wako bure.

    Tuhuma ya babu yako ni kubwa na nzito.

    Ni lazima afikishwe mahakamani kwanza.

    Pia si rahisi kumpatia dhamana kwa kosa lake.

    Subiri ushahidi na hukumu vitakapokamilika.”

    “Kwa hiyo utanisaidiaje Koplo?” Tasira alihoji.

    “ Hakuna njia.

    Jambo hili ni zito!

    Ingekuwa jepesi tungefanya mkato kama kawaida.

    Lakini hili, haliingiliki hata uwe na fedha kiasi gani.

    Acha sheria ifuate mkondo wake.

    Najua yataisha. Pole sana shemeji!”

    “Asante!

    Ngoja basi nisubiri tuone inavyokuwa.”

    “Sawa.

    Jipe moyo!

    Kila jambo lina suluhu yake.

    Kama hujaridhika, basi muone mwenye jalada lake.”

    “Sawa!

    Ngoja nivute muda.”

    Haikupita muda mrefu gari ikiwa na mahabusu iliwasili. Waliteremshwa mahabusu waliokuwemo kwa hadhari kubwa na ulinzi ulikuwa mkali. Tasira aliomba angalau amwone babu yake kumjulia hali.

    “Ha! Babu, kulikoni?”

    “Ndo hivi uonavyo!” Aliongea kwa sauti ya kukoroma kupitia puani. Damu zilimganda puani baada ya wanan-chi kumpatia kipigo cha mbwa mwizi.

    “Pole Babu!

    Mungu atakunusuru!”

    “Sijui hata kama nitapona.

    Hali yangu ni mbaya sana!”

    “Usijali.

    Mungu atakusaidia!

    Amini!”

    “Fanya mpango.

    Ongea na maaskari nisipelekwe mahakamani.

    Nikifikishwa huko najua sitatoka.

    Na itakuwa ndio mwisho wangu!

    Jitahidi!”

    “Usijali.

    Najua tuko pamoja Babu.

    Ngoja upatiwe matibabu tuone hili linaelekea wapi.”

    “Haya Babu.

    Jitahidi!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati huo Tasira hakuwa na cha kufanya zaidi ya kurejea pale alipoishi wakati wote. Alipata taarifa kuwa uchunguzi na upekuzi kule kijijini utafanyika mapema. Tasira alikata shauri kutumia fursa hiyo kwenda kufa-hamu yaliyojiri huko kijijini.Wakati upekuzi huo un-apangwa kufanyika, Tasira alisafiri kwenda kijijini ili kuufahamu ukweli uliokuwapo. Lilikuwa ni tukio la ku-tisha kama si kuogofya kijijini hapo. Ingawa walimficha pale nyumbani kwa babu yake, wanakijiji walimsimulia na kugubua yaliyokuwa yanajiri.

    Hapakuwa na mwenye ulimi wa Salata katika kusimulia jambo hilo lililomalizika pasipo taarifa maalumu iliyo-tangazwa na chombo cha habari. Si kwa kuliogopa uzito wake bali ni kutokana na uhaba wa waandishi wa habari na usiri juu ya uendeshaji wa jambo hili.Tasira alikuwa miongoni mwa wasichana wale wenye fuadi. Aliweza kupata simulizi lote. Alijua pahala pa kupata ukweli huo kama mpelelezi aliyekubuhu. Alifahamu fika kuwa, anaweza kupata taarifa sahihi sehemu ambapo inauzwa chang’aa. Kwa jinsi ya urembo wake na mvuto uliotoka-na na vipodozi vya mjini, alionekana malkia kati ya watwana. Alipotia mguu wake sehemu ya vilabu alipo-kelewa na wanaume wenye huba na wakware. Ilikuwa tabia ya wanaume wengi katika kijiji hiki kumtamani na kumtolea macho ya mahaba mgeni yeyote wa kike aliyeingia kijijini hapa. Hawakujali hata kama alikuwa na sura ya kuchkiza.

    Wakati huo alibahatika kukutana na Mongo. Alikuwa kijana mwendesha daladala ya baiskeli kama ilivyojuli-kana katika maeneo ya Bukene. Kwa jinsi alivyooneka-na, Mongo alionekana kama mzee mwenye miaka Aro-baini na tano. Maisha yake kuwa magumu kupita kiasi ndicho chanzo cha kumfanya uzee umkimbilie. Umri wake sahihi ni miaka ishirini na moja, lakini tayari ali-kuwa na wake watatu na watoto tisa wakati huo.

    Tasira alimtaka Mongo ampatie hadithi yote kutokana na alivyoifahamu kesi iliyomkabili Babu yake. Alimuahidi kumpatia chochote kile ambacho roho yake ilimtuma kukipata. Hakuwa na janja ya kumkwepa, kwani alilewa manukato yaliyokuwa yameufunika mwili wa Tasira. Mongo alihisi kapata bahati ya kuongea pia kumgusa mzungu. Aliamua kuyatapika yote hadharani kumjuza Tasira. Alimsimulia kuwa, mzee Gainda aliingia matatani kutokana na kifo cha mtu aitwaye Jinasa. Alikuwa ni mkazi wa wilaya ya Igunga vijijini. Kwa kuwa alikuwa mfugaji maarufu mwenye kuhamahama, alipanga kuhamia Urambo kufuata malisho pamoja na maji. Kama ilivyomwagiza nafsi yake, mfugaji huyo bwana Jinasa alifahamu kuwa mzee Gainda alikuwa na uganga ambao ungemfukuzia wabaya wote hasa wachawi na apate mafaniko yeye na mali zake kule aendako.

    Walipokubaliana na mzee Gainda, Jinasa alishauriwa arudi nyumbani kwake Igunga kurudia angalau sehemu ya kile alichotaka kuhama nacho. Aliamriwa kuwa, ka-ma atashindwa kuleta vyote basi ajitahidi kuuza baadhi ya vitu hivyo na arejee na pesa zilizotokana na mauzo hayo ndipo zifanyiwe matambiko.

    Alikuwa na shauku ya kutimiza matakwa ya moyo wake. Jinasa alikanyaga baiskeli hadi kijijini kwake Igunga. Hakuwaza hata kama maisha yake yalikuwa rehani. Hakika aliiona familia yake kwa mara ya mwisho na hapakuwa tena na salia mtume. Alipouza alivyoagizwa, alifunga safari kurejea kwa mganga wake akiwa na thamani ya kutosha.

    Ilimchukua saa kumi na tatu kufika kijijini kwa mzee Gainda kwa usafiri wa baiskeli. Alibeba fedha taslimu zaidi ya laki saba, simu ya mkononi, nguo za kubadilisha pamoja na vipande vya dhahabu alivyokuwa amejihifadhia. Jinsi safari ilivyokuwa ndefu, hakika alichoka sana.

    Kesho yake ilipowadia, Gainda alimtaarifu Jinasa kuwa, majira ya jioni ndiyo wataenda porini kufanya tambiko lao. Alimwagiza pia kuandaa kafara yake ili kuhitimisha safari yake. Hakika ilikuwa ni siku ambayo Jinasa aliisubiri kwa hamu. Mboni zake na wajihi wake ulisomeka furaha na hakujua nini kitafuatia.

    Mnamo saa kumi na moja jioni, Jinasa aliongozana na mzee Gainda ili kwenda kufanya tambiko. Jinasa alitan-gulizwa huku amebeba furushi lake la fedha na dhahabu. Alifungwa nguo nyeusi na kitambaa chekundu.

    Jinsi alivyopenda kuvaa makoti marefu yaliyofunika hadi magotini, mzee Gainda alificha jambia lake kiunoni. Walipofika sehemu ya kufanyia tambiko lao huko porini, pasipo kufahamu Jinasa aliamuliwa achimbe shimo la kufanyia uganga wao. Hakukaidi kitu, alifuata amri ya mganga wake. Ingewezekanaje kuoga akiwa na nguo zake? Ililazimu kuchojoa nguo zote na kubaki na nguo ile nyeusi aliyoandaliwa na Gainda. Wingu zito la damu lilitanda, shahidi wa unyama huo ilikuwa miti iliyokuwa imezunguka na kushuhudia sehemu hiyo. Katikati ya miti yenye huzuni, mtu mmoja kati ya wakazi wa kijiji hicho alikuwa kachelewa kutoka mawindoni alishuhudia unyama huo akiwa mafichoni.

    Aliamriwa achukue noti ya shilingi elfu kumi na atum-bukize ndani ya shimo alilochimba. Ndani ya shimo hilo kulitiwa manyoya ya mtetea pamoja na vumbi jeusi. Alitekeleza aliyo agizwa. Alipotakiwa kila jambo aliafiki. Hakuwa na ubishi wowote muda wote na mpole kama kondoo wa kizungu.

    Ilivyowadia wasaa wa kuwekwa tojo kwenye makalio, Jinasa alitakiwa kubong’oa. Alikuwa hana wasiwasi wowote. Alielekeza macho yake na kichwa ndani ya shimo ili achanjwe na kupakwa dawa. Kwa kutokuwa na wasiwasi wowote, alivyozoea kuwafanyia wagojwa wake, mzee Gainda alichomoa jambia yake kiunoni kwa mkono wake wa kuume. Mzee Gainda alisukumiza kwa nguvu jambia lake na kumchoma ubavuni na kufanya tumbo la Jinasa kutapika viungo vyake vya ndani. Palitapakaa damu zilizochuruzika na kumfanya alowe chepe. Wakati akitapatapa huku na kule alibahatika kumkanyaga Gainda mguu wake wa kuume na kumjeruhi.

    Jinasa alikata roho baada ya dakika chache. Damu yake ilifichua maovu ya Gainda sehemu zote. Mwili wa Jinasa ulibaki porini zaidi ya miezi mitatu na aliliwa na kutawanywa na wanyama wakiwemo fisi. Wakati Mongo akiyatapika yote aliyoyafahamu, simulizi yake ilikuwa kama filamu iliyokuwa ikichezwa. Tasira aliishiwa na nguvu na alitokwa na machozi. Alihisi yeye kama ndiye alifanyiwa ubedui ule. Ingawaje alilia na kutokwa na chozi jepesi, aliukaza moyo wake na kumtaka Mongo aendelee kumfafanulia.

    Kweli hujafa hujaumbika, na dunia ni hadaa isiyo na siri hata chembe. Ingawaje alifanya siri, kuna mtu mmoja kwa macho yake alibahatika kuona unyama uliotekelezwa naye. Alikuwa ni Tonja mwindaji wa digidigi aliyekuwa ameenda porini huko kukagua mitego yake. Alibakia na ushahidi alivyokuwa ameitazama sinema hiyo yenye mauaji ya kinyama. Mongo alisisitiza kuwa, kesi inayomkabili Gainda ni ngumu. Ushahidi wa kumfunga tayari ulikuwa hadharani na polisi walimpata ila tu, walitaka kuuona ushahidi wa mazingira na kuhitimisha upelelezi wao.

    Siku za mwizi kweli ni arobaini, na siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Hatimaye siku ile iliyongojewa ya upekuzi iliwadia. Ilikuwa majira ya saa nane mchana siku hiyo ambapo kamanda wa sungusungu aliwataarifu wanakijiji wote kwenda kushuhudia upekuzi.Upekuzi huo ulifanyika mbele ya mboni za makumi ya wanakijiji waliomiminika kwa wingi.

    Haikuwa siri tena. Ushuhuda ulikuwa umetolewa na aliyeona tukio pahala alipo uawa bwana Jinasa. Hawa-kupata taabu kutafuta ushahidi kule porini. Waliona na kuokota mabaki ya mifupa ya mwili wa aliyekuwa ana-hisiwa kuwa ni ndugu Jinasa. Polisi hawakujiridhisha moja kwa moja kuwa alikuwa ndiye hadi uchunguzi wa kisayansi ufanyike.

    Walipomaliza kuikusanya mifupa pamoja na fuvu waliafiki vema kurejea nyumbani alipoishi mzee Gainda ili kutafuta ushahidi wa mwisho kuhusu tuhuma yake. Walichokipata na kukiona nyumbani huko bado ni kitendawili kigumu. Hakuna hata aliyetabiri kilichopatikana huko. Nini kilipatikana wakati huko?



    *****



    Wakati Mkongomani pamoja na Carolina wakiwa wana-karibia kuwasili mjini Dodoma, njiani walipatwa na maswahibu mengi. Uchovu wa barabarani kutoka Singida mjini hadi Dodoma kupitia Manyoni ulitosha kuwahakikishia miili yao kulegea.

    Wakiwa karibu na Mji wa Manyoni, kisanga kingine kiliwatokea;

    “Carolina, naomba nipatie shilingi alfu tanotano.

    Wazee wako kazini” Mputa alimwomba Carolina.

    “Nimebakiza kama shilingi elfu thelathini pekee.

    Noti sita, je nikupe zote?”

    “Hapana, angaza macho tizama wako wangapi?”

    “Wako watatu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wanaume wawili na mwanamke mmoja.” alimpatia noti tatu za shilingi elfu tanotano.

    Wakati Mputa akiwa anaendesha gari yeye aliendelea kutafakari kisha alimwambia Carolina;

    “Hivi hizi pesa tunazowapa ni za nani?

    Hawa jamaa kila pahala wametapakaa.

    Hawapati mshahara?

    Wanakusanya pesa kwa niaba ya nani?”

    “We hufahamu.

    Pesa zote hizo ni kwa ajili yao.

    Hakuna yule humpelekea, kwani hazina hata stakabadhi.

    Lakini inasadikika, baadhi yake humpelekea mkuu.

    Humpelekea ili aendelee kuwapangia zamu barabarani.

    Hiyo ni fadhila, wakishindwa hunyimwa nafasi hiyo.”

    “Egesha gari pembeni.” Askari wa kiume aliamuru.



    “Vipi wazee, habari za kazi afande?” alisabahi huku akitoa kichwa nje akiwa bado katika usukani. Wakati askari mmoja wa kike aliendelea kuchungulia na kukagua gari kila mahala.

    “Safari ya wapi na mnatoka wapi?” Askari wa kike ali-hoji

    “Goma-Kongo afande.

    Safari ya Darisalama bwana mukubwa.” Mkongomani alijieleza.

    “Teremka chini kuna tatizo katika gari yako.

    Fanya haraka. Nipe leseni yako na kibali cha kuingia nchini.”

    “Hakuna problemu afande.

    Mambo sawa kila kitu kipo.” Alitoa hati ya kusafiria na leseni yake na kuteremka toka kwenye gari. Carolina alibaki ndani ya gari punde naye aliamua kuteremka.

    “Mbona hati ni moja, ya pili?

    Dada naomba hati yako tafadhali.”

    “Mi mbongo.

    Natakiwa kuwa na hati ama vipi?” Carolina alijibu.

    “Huyu umemtoa wapi? Ama ni........” Afande alihoji.

    “Acha hizo afande.

    Nimeomba msaada.

    Ananisaidia nifike Dar.

    Unajua usafiri ni shida.” Carolina alijitetea huku akitabasamu. Askari wa kiume alimtazama Carolina na kumkonyeza na kisha alimezea mate.

    “Dada naomba namba yako ya simu, ama.........” askari wa kiume aliingiwa na pagaa.

    “Hakuna shaka.” Alimtajia na kuinukuu.

    “Mkongomani, tuachie angalau hela ya soda.

    Huoni hata mdogo wetu umejibebea pasipo tahayari.” Askari wa kiume aliongea.

    “Hakunaga probleme afande.

    Kamata hii hapa.” Aliunyoosha mkono wake kumpatia. Alisita kuzipokea kisha aliangaza macho yake kila upande.

    “Tupia chini hapo halafu ondoka mwendelee na safari.

    Wanga wengi.” Alitekeleza kisha waliendelea na safari yao.

    “Jamaa wana njaa hawa.

    Tatizo hakuna, lakini pesa iko hitajika kila wakati”. Mkongomani Mputa alilalama.

    “Nchi ya kitu kidogo hii.

    Ulikuwa hujui nini?

    Mlungula kwao ni sawa na maji na samaki.

    Hujawahi kusikia?”

    “Nini” Mputa aliuliza.

    “Askari anamuaga mkewe ‘injika ugali mboga naileta.”

    “Kila siku nikiwa nakujaga bongo, hela mingi huenda bure. Mbona govamenti iko kimya. Haijui utumbo huu?” Mkongo alihoji.

    “Serikali wanajua sana.

    Tatizo ni kulindana!

    Kuna taasisi ya kupinga rushwa.

    lakini hakuna kinachobadilika.

    Kila wakati rushwa inaongezeka.

    Sijui wapi kuna tatizo.

    Wakulaumiwa sijui nani?

    Sisi wenyewe ama serikali?

    “Iko tatizo ndani ya gavamenti!

    Sheria haina nguvu.

    Rushwa ni haramu.

    Hii ni ndogo sana, inakuwa halali sababu wakubwa ha-wawajibishwi, mutu wadogo hujifunza kwa wakubwa.”

    “Kweli unayoyasema.

    Wakubwa katika nchi hii hulindana sana.

    Utasikia kila wakati katibu tarafa, hakimu wa mahakama ya mwanzo na hata mwalimu wa shule ya msingi kuwa katiwa mbaroni kwa rushwa ya shilingi elfu kumi. Je waliopokea mamilioni na hata kuiibia serikali mapesa ya wavuja jasho na kuingia mikataba ya ulaghai mbona hawawajibishwi? Inatia hasira sana wanapoamua kutufanya wote mbumbumbu.” Carolina alilalama.

    “Bongo watu wapole sana.

    Kama si wapole basi wajinga mingi.

    Revolution ni muhimu.

    Wabongo lazimu wake up!

    Pambana pata haki kama demokrasi iko.

    Angalia Rwanda na China, mwizi lazima akufe kwa mo-to ya bunduki!”

    “Acha watunyonye, ipo siku haki itatendeka.

    Suluhu ipo njiani, haki inakuja na yote yatapita.”



    Ilipowadia saa kumi na moja jioni, waliwasili mjini Dodoma. Kwa kuwa alichoka sana, Mputa na dreva wake walishauriana kulala mjini hapo. Walikubaliana kufanya hivyo na walienda hoteli moja kujipumzisha. Muda walio wasili Dodoma , ulikuwa wa machweo. Kwa kuwa Carolina alikuwa kunguru, hakuweza kupumzika na kulala wakati huo.

    “Nataka nitoke mara moja ninyooshe miguu.

    Nimechoka sana kukaa. Caro alimuaga Mputa. Alimka-bidhi mkoba wake pamoja na simu ya mkononi akimfa-hamisha kuwa atarejea baada ya dakika chache. Alikuwa amedhamiria kuufahamu mji wa Dodoma hata kwa dakika chache. Alitokea pale ilipokuwa Hotel iitwayo SAMIKE ANNEX. Haikuchukua hata dakika tatu akitembea mtaani na asipate wa kumpiga mkono. Wakati huo alikutana na kila aina ya mwanaume na hakusita kutongozwa. Aliukaza mguu wake hadi alipofika Dodoma Inn ambapo kuna ukumbi wa starehe na mahala pekee ambapo wenye pesa zao hubarizi kuyapunguza machungu ya siku. Aliyapepesa macho yake kila upande na kisha aliliona gari pale nje limeegeshwa. Ghafla akitaka kujipenyeza kwenda ndani ya ukumbi huu, alistaajabu kumwona kijana mmoja kateremka toka ndani ya gari lile na kumfuata. Alipomfikia alimshika bega

    “Habari yako Dada?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nani dada yako?” Aligeuka huku aking’aka. Alimtaza-ma kwa kejeli hasa alivyo na umbile dogodogo na kuhisi ni miongoni wa vijana barubaru wasio mbele wala nyuma.

    “Samahani dada, naomba unisikilize!

    Mjumbe hauawi, mi nimeagizwa na bosi.”

    “Ananifahamu ama amenifahamu baada ya kuniona?”

    “Naomba nisikilize basi.

    Kuna mheshimiwa anakuhitaji mara moja.”

    “Lo! Hata salamu?

    Kwanza unajua mimi ni nani, nafanya nini pia natoka wapi? .. unawaza hapo hapo tu...”

    “Samahani anti, naomba twende kwenye gari pale nje uongee naye. Ama vipi?”

    “Haya ngoja nimsikilize anasema nini. Lakini ana..........”.

    “Usiwe na shida, maswali yote utamuuliza na atakujibu.”

    Alikuwa ni mbunge mmoja ambaye alifika Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge la bajeti. Si kwa hali yake pengine ulimbukeni na hata kutokuwa na maadili toka kule atokako. Pengine yaweza kuwa ni tabia yake kama ilivyo ngozi na mwili. Alikuwa akijivinjari mitaani baada ya kikao cha Bunge la bajeti. alihitaji faraja baada ya mzozo na migongano ya kimaslahi kuwahusu wabunge kujiongezea kipato tofauti na utajiri wa nchi hii. Kulikuwa na mgongano pia wa kimaadili jinsi wenye dhamana walivyofikia hatua ya kujichotea amali za uma pasipo idhini ya idara zao maalumu na wananchi. Wakati huu Caro alikuwa amefika;

    “Ndiyo mrembo!

    Ingia ndani ya gari tuzungumze zaidi.

    Ama kuna tatizo?” Bwana mkubwa alichombeza kwa jeuri ya cheo chake.

    “Hakuna neno!

    Naingia usijali.”Carolina aliingia ndani ya gari la kifahari. Kiyoyozi na marashi yaliuteka mwili wake.

    “Tunafahamiana ama!” Carolina alihoji akimtazama mheshimiwa.

    “Inawezekana tunafahamiana.

    Kwani unaonaje, sura yangu ni ngeni machoni mwako?”

    “Sura yako si ngeni machoni, na..

    Inawezekana tushawahi kuonana mara nyingi.

    Lakini nikumbushe ni wapi na lini pia unaitwa nani?” Caro alihoji.

    “Nitazame mara nyingine tena, kisha nieleze Dodoma ukiisikia jambo linaloitambulisha Dodoma ni nini?”

    “Mbona sielewi. Dodoma kama Dodoma, naifahamu kupitia masomo ya shule ya msingi kwamba, ni kituo cha uzalishaji wa Zabibu pia ni Mji mkuu wa nchi yetu Tanzania. Hakuna zaidi!”

    “Kuna kimoja umesahau ambacho ni kikubwa zaidi.

    Kitu gani hukiangalia katika runinga toka mji wa Dodo-ma?”

    “Runinga!

    Inawezekana ni ......... Bunge!

    Okay nimekumbuka ni Bunge.”

    “Hujapata picha kuwa unaongea na nani?

    Kumbuka”. Bwana mkubwa alitabasamu na kumkonyeza Carolina.

    “Ah! Nimepata picha sasa.

    Nisamehe sikujua.

    Mheshimiwa Kitufya wa Mjengoni!

    Sawa, habari za kazi?

    “Njema sana mrembo.

    Umependeza sana!

    Hivi unaitwa nani?”

    “Naitwa Sharon Night.” Carolina alidanganya jina mara nyingine.

    “Jina zuri sana kama wewe ulivyo!

    Vipi umeambatana na mtu pengine nitakukwaza?”

    “Hapana, nimemwacha mwenzangu yupo hotelini.

    Naelekea Arusha kesho hivyo tunapumzika kwa muda kisha kesho safari iendelee. Ulikuwa unasemaje mhe-shimiwa.”

    “No!

    Niite Kitufya tafadhali.

    Achana na mheshimiwa, kuna muda wake!”

    “Haya Kitufya!

    Nataka niende nilikofikia.” Alitaka kufungua mlango ateremke

    “Hapana usiende.

    Kitu gani unakihitaji toka kwangu ili angalau niwe nawe usiku wa leo. Usijali gharama wala chochote, kila ukita-kacho nitakupatia. Nimekupenda sana baada ya kukuona. Fanya mambo! Huoni bahati hii, ulitegemea kukutana namimi zaidi ya kuniona kupitia runinga?”

    “No!

    Hapana mheshimiwa.

    Naomba siku nyingine si leo, nina mtu tayari.”

    “Hapana.

    Sema chochote utakacho nitakupatia.”



    Kwa kuwa aling’ang’aniwa kama ruba, hakuwa na jinsi. Alimwomba hata amkubalie kubarizi naye dakika chache kwa malipo yoyote aliyoyataka. Walikubaliana kwa malipo ya dola mia moja za Marekani. Hapakuwa na haja ya kusumbuka kwani naye aliishi katika hoteli ileile waliyofikia Carolina na Mputa ingawaje alihofu ataumbuka.

    Carolina aliuvaa ujasusi wakati huo. Alipofahamu mbunge huyo alikuwa na wadhifa serikalini, aliona ni wakati wake wa kujipatia ngawira mbali na malipo aliyolipia kule chumbani. Carolina alitamani sana kuon-doka na mkoba uliokuwa mezani ndani ya chumba cha mbunge huyo. Aliwaza mengi wakati huo, rohoni aliji-semea;

    “Itawezekanaje niondoke na kumwacha kama alivyo pasipo kumfundisha adabu?

    Leo ni leo, ngoja nifanye ubedui anitambue.

    Hizi pesa anazoringishia ni mali ya nani kama si wavuja jasho! Atanitambua leo asili yangu.” Alitamani hata kumlewesha mbunge huyo ili atoweke na mkoba huo. Alitaka kumpekua ili ajipatie nyaraka za zitakazotumika kumpatia pesa azifikishapo katika baadhi ya vyombo vya habari.

    Baada ya kubarizi na mkubwa huyo ndani ya Kitufya aliingiwa shauku ya kubaki na Carolina. Alimpatia pesa taslimu kama walivyokubaliana. Carolina alifahamu kapata mtaji wa kumpatia pesa zaidi. Alimuahidi mbunge huyo kuwa atarejea baada ya muda mfupi lakini atafute jinsi ya kufanya kwa mumewe.

    Alipoteremka palipo chumba cha Mputa, alimkuta kalala fofofo. Hakutaka kumgutusha zaidi aliandika ujumbe katika kijikaratasi kuwa I’M COME SOON HONEY BECASI I TO RETACH MY HEA. CHAUS!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roho ya Carolina wakati huo ilikuwa ya kinyama. Ha-kuwaza kama binadamu wa kawaida. Akili yake iliwaza pesa pekee. Wakati huo akitaka kuelekea mtaani kutafuta madawa ya kulevya kokote. Alimuuliza mlinzi mmoja wa hoteli aliyofikia sehemu ambayo ataweza kupata madawa hayo. Mlinzi alifahamu wahusika wote kwani naye alishirikishwa na tajiri yake. Haikumchukua muda mlinzi katika hoteli alipomweleza sehemu ambapo angepata mzigo huo. Alijieleza pasipo hadhari na mtu aliyemsimulia habari hiyo kuwa, anaye rafiki yake ambaye kazi yake ni kusambaza bidhaa hiyo hapo mjini na kwingineko nchini. Alitamka hadi jina la rafiki yake huyo kuwa kwa jina la kazi yake anajulikana kama Super Suba. Kwa kuwa alikuwa na namba za simu, mlinzi alimpigia simu kumjulisha kupatikana kwa mteja wa bidhaa hiyo. Alikuwa ni kijana tajiri mwenye magari lukuki. Mara nyingi gari hizo hutumiwa na Super kusambaza mzigo wake popote pale alipohitaji na hakuna aliyeng’amua kuhusu hilo jambo hilo.

    Wakati huo Super alimwagiza dereva wake aliyeshiriki naye katika biashara hiyo haramu. Alikuwa ni binti mrembo asili ya mzigua na mchanganyiko wa kimanga. Alifahamika kama Shamina. Dada huyo alimuia kusam-baza madawa kwa wateja wadogo wadogo kwa reja reja pasipo hofu yoyote.

    Kwa kuwa alifahamishwa kiasi kilichohitajika ni cha chini, Super alichukua kipande cha sabuni ya mche na kukiyeyusha kwenye moto na ndipo paketi aliiviringisha ndani yake kisha aliigandisha. Alikichomeka katikati yake na kukisitiri kama kilivyo kuwa awali. Hakika ilikuwa si rahisi kung’amua kilichokuwemo ndani ya kipande hicho cha sabuni. Alipokabidhiwa kipande cha sabuni, Carolina aligomba

    “Mchezo gani mnanifanyia?”

    Wafanyieni washamba si mimi.” Walimcheka na kum-wambia mjini shule, aende na sabuni ile na ndani yake atakuta mzigo wake. Aliafiki na hata akalipa fedha tas-limu kwa dola za Marekani.

    Wakati yakiendelea hayo, Carolina tayari alijiamini ku-tekeleza uafriti alioukusudia kwa Kitufya. Hakurejea chumbani kwa Mputa, alijiandaa kwenda kwa mheshi-miwa mbunge. Alipomaliza kupaka unga sehemu alizo-hisi zinhemnasa alirejea kwa mkubwa aliyekuwa tayari kapanga na kuamua kusherehekea mavuno ya jasho yake. Hakufahamu lolote kuhusu kile kilichoendelea. Carolina alifahamu kuwa, mbunge huyo angeukwaa mkenge bila shaka yoyote pale tu atakapokaa naye kari-bu. Lilikuwa jambo gumu kwa mheshimiwa na hata mtu yeyote kutonaswa katika mtego huo.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog