Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

KITANZI, KISU NA BASTOLA - 4

 





    Simulizi : Kitanzi, Kisu Na Bastola

    Sehemu Ya Nne (4)



    ILIPOISHIA

    “Unamjua yule msichana mpya?” alisema Madam Bernadeta kwa kunong’ona huku akiendelea kumshikashika Julieth.

    “Namjua si yule anayeitwa Salima?”

    Salima alishtuka baada ya kusikia jina lake likitajwa, akatega masikio yake ajue ni nini kilichokuwa kikitaka kuongelewa kuhusu yeye.

    Songa Nayo...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unamwonaje mzuri eee?” aliongea Madam Bernadeta huku mikono yake ikiwa kifuani kwa Julieth.

    “Usiniambie kama tayari umeshampenda ukaniacha mimi!” Julieth alijibu kwa hasira zilizochanganyika na wivu huku akijitoa mikononi mwa Madam Bernadeta na kuketi kitandani.

    “Aaa...hapana siyo hivyo ni hivi, kesho atahamia chumbani kwa Diana, ninataka uwe naye karibu. Hakikisha anafuata kila kitu atakachotakiwa kukifanya. Kikubwa ninataka uwe rafiki yake. Mpeleleze na uniambie kila kitu atakachokuwa akikifanya wakati mimi sipo karibu naye.”

    “Usijali, ni hilo tu?” aliuliza Julieth na kushusha pumzi ndefu kifua chake kikiyeyusha chuki nzito na wivu ulioanza kujijenga moyoni mwake baada ya kumsikia Madam Bernadeta akimtaja huyo msichana mpya mbele yake.

    Akasimama na kuufungua mlango, taratibu akatoka nje ya chumba hicho kisha akaufunga kama ulivyokuwa awali na kutembea hatua kadhaa hadi chumbani kwake, bila kujua kama kuna watu walikuwa makini wakiwasikiliza kila kitu walichokuwa wakizungumza Mr. John Chakos na Salima.

    Ni wazi kuwa Salima alikuwa msichana mzuri wa umbo na sura, kila mtu aliliona hilo. Kwa Julieth uzuri wa Salima ukawa kikwazo kikubwa kwa kuwa alianza kuhofia taji lake la urembo wa ‘Serenity’ kunyakuliwa na msichana huyo mpya. Siku zote yeye ndiye aliyeonekana msichana mrembo kuliko wote humo ndani. Uzuri wake uliifanya thamani na hadhi yake iwe juu zaidi ya wasichana wote ambao huuzwa ndani ya jengo hilo.

    Kila mgeni muhimu alipoingia nchini Tanzania, Julieth ndiye aliyepewa kipaumbele kutembea naye kuliko msichana mwingine yeyote. Hivyo ujio wa msichana mrembo na mzuri zaidi yake ulikuwa kikwazo kwake, alihisi kila kitu alichokuwa akiringia kilikuwa mashakani kuchukuliwa na Salima; kuanzia wateja, hadhi, marafiki na mwisho kabisa, penzi la Madam Bernadeta. Julieth hakufikiria kuruhusu hayo yote yatokee, aliwaza kufanya kila atakachoweza kupambana na adui yake.

    ***

    Muda wote huo Salima alikuwa akitafakari kitu gani kilichowapa haki wasichana hao wawili wapange kumbembeleza yeye. Alijiuliza kwa nini alikuwa akitakiwa kuhama chumba chake kesho asubuhi na kuhamia chumbani kwa msichana waliyemtaja kwa jina la Diana?

    Akili yake haikuweza kufikiria sawasawa katika hali hiyo, alitaka kuwa huru kwa kutoka humo ndani kwanza na kurudi chumbani kwake kabla muda haujazidi kuyoyoma.

    Kama vile paka mwizi, aliinua shingo yake na kumchungulia Madam Bernadeta ambaye alionekana kuanza kukolea usingizi mzito kwa uchovu mwingi wa yote waliyoyafanya dakika chache zilizopita na Julieth.

    Wataalamu wa saikolojia husema kwamba mtu akiwa katika dakika arobaini za mwanzo za usingizi, mfumo wake wa fahamu huwa katika hali isiyoeleweka kiasi kwamba mtu huyo hawezi kuamka mwenyewe wala kuamshwa hata kama kungetokea kitu cha kushtusha kiasi gani.

    Salima alijifunza kuhusu hilo sehemu fulani lakini hakujua ilikuwa wapi moja kwa moja. Akilenga kutumia mbinu hiyo alisimama na kunyata taratibu akikipita kitanda cha Madam Bernadeta aliyekuwa akijigeuza mara kwa mara na kuusogelea mlango.

    Kama mahesabu yake yalikuwa sawa, Madam Bernadeta hata kama angejigeuza vipi asingeweza kuamka muda huo, lakini kama mahesabu yake yalikuwa na hitilafu basi siku hiyo ndiyo ingekuwa arobaini yake japo kuwa siku thelathini na tisa zilizopita hakuzitumia kuchunguza vitu vya watu kama ilivyokuwa siku hiyo.

    “Mungu nisaidie,” Salima alijikuta akisema kimoyomoyo na kunyonga komeo la mlango kisha akafungua haraka akatoka nje na kushuka ghorofa hilo isiyomhusu ambapo moja kwa moja aliingia chumbani kwake na kujifungia huku akihema kwa nguvu.

    ***

    Asubuhi ya siku iliyofuata Side alijua lazima atakuwa na la kujibu kwa mkewe Sonia, hasa kumueleza kuhusu kila kitu ambacho kilitokea usiku wa jana yake na kuhusu huyo mwendawazimu aliyemhifadhi siku nzima ndani ya chumba cha wageni kwenye nyumba yao.

    Huku macho yake akimkazia Side, Sonia alichukua sahani kubwa ya matunda na kumsogezea Dedan ambaye alitazama ulaji wake kwanza na kuiga mfano kutoka kwa mwenyeji wake Side ambaye aliyazoa matunda hayo na kuyameza huku mbegu tu akizitema kama sehemu isiyofaa kuliwa ya tunda hilo la zabibu.

    Kwa utamu wa matunda hayo Dedan alijikuta akimaliza sahani nzima na kutaka tena na tena jambo ambalo liliendelea kumfanya Sonia azidi kumkazia macho mumewe Side.

    Ghafla alamu ya mlango ikalia. Sonia akakimbilia chumbani kwake na Side akamficha Dedan mahala kisha akaenda kufungua mlango.Kwa kuwa kuua kulikuwa ndani ya damu yake, Henry hakuona shida yoyote zaidi ya kufurahia amri hiyo. Tofauti na zamani, siku hiyo wala dhamira yake haimsuti juu ya damu za watu alizozimwaga kwa mikono yake. Alikuwa akizidi kuendelea kufanya ushetani wake kwa furaha kabisa kama vile kuua ilikuwa ni aina fulani ya mchezo.

    Si kilio cha Sonia wala machozi ya Dedan yalimfanya awaonee huruma na kuwaachia mateka wake hao. Badala yake Henry alikuwa akiwaangalia na kucheka kila mara Sonia alipolia kwa uwoga baada ya kumgusagusa na mdomo wa bastola yake.

    Henry alichagua sehemu nzuri mbali kabisa na makazi ya watu kiasi kwamba hakupata bugudha yoyote kuwahifadhi mateka wake. Sauti ya vilio vya kimyakimya ndivyo ambavyo vilisikika eneo hilo kutoka kwa Sonia ambaye huenda angepiga makelele kwa nguvu kama tu asingefungwa kwa kitambaa kizito mdomoni.

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Side aliingia kila chumba ili kuhakikisha kama kweli mkewe Sonia hakuwemo ndani; kitu ambacho kilikuwa sahihi. Akawaza labda alikuwa nje mahali fulani. Labda aliondoka bila kuaga!

    Alitafakari wazo hilo na kutolipa uzito kwani Sonia hakuwa na tabia ya kutoka nje, alikuwa ni mtu wa kukaa ndani muda wote akihofia kujulikana na watu. Hata mavazi yake yalikuwa ni yale yaliyomficha mwili mzima na kuacha macho tu.

    Alipokuwa akitembea kuelekea mlango wa nyuma ambao ndiyo ulikuwa umefunguliwa, Side aligundua alama za viatu asivyovifahamu kwenye ardhi ya mlango wake. Ni wazi mtu asiyemjua aliingia na kutoka ndani ya nyumba yake.

    Kama vile mchunguzi wa masuala ya uhalifu (forensic), Side alitafuta kila mahala alama yoyote itakayomdhihirishia alichokuwa akikiwaza, kuwa jambo lililotokea muda mfupi nyumbani kwake lilikuwa ni utekaji nyara na si vinginevyo.

    Mara akagundua kuchunika kidogo kwa rangi kwenye kichuma cha loki ya mlango ulioachwa wazi jambo lililomfanya agundue kuwa mlango huo ulisukumwa kwa nguvu na aliyeingia ndani. Moyo wa Side ukaanza kudunda kwa kasi kiasi cha jasho jingi kumtoka kama vile mtu aliyechanganyikiwa.

    Side alishindwa kutoa taarifa polisi wala sehemu yoyote ya usalama kwa kuwa alihofia kwa kufanya hivyo atamuanika Sonia mbele ya wabaya wake.

    Kuna ule muda mtu huwa hafikirii chochote zaidi ya kuwa na hofu isiyokuwa na mfano, muda huo ulikuwa juu ya Side kwa siku hiyo akaanza kutetemeka kwa woga. Moyo wake mara ulifanya pah! Aliwakumbuka watoto wake mapacha ambao alizaa na mkewe Sonia wote walikuwa katika shule ya malezi ya awali kwa watoto ‘Msami Day Care.’

    Kwa kasi ya ajabu Side alifika shuleni lakini jibu ni kwamba hawakuwepo hapo na walimu hawakujua wapi walipokwenda ingawa ushahidi wa watoto hao kuripoti shuleni asubuhi ulikuwepo.

    Kwa uchungu Side alifumba macho yake kwa nguvu, machozi yakimtiririka mashavuni kama mtoto mdogo. Kitu alichokuwa akikitaka kujua zaidi ni nani aliyekuwa akimfanyia mambo yote hayo?

    Akiwa mwenye kukosa matumaini, simu yake ya mkononi iliita kwa namba asiyoifahamu akaipokea na kusikiliza:

    “Haloo Side, kama unamthamini mkeo na watoto wako rudi nyumbani kwako haraka sana, nina zawadi yako,” iliongea sauti ya mtu asiyemfahamu kwa kujiamini.

    “Sema unataka shilingi ngapi nikupatie, naomba uniachie familia yangu,” alisema Side kwa pupa huku machozi yakimtoka.

    “Usiwe kama mwanamke Side, inuka uje mara moja na nikukumbushe tu, uje peke yako ukifanya ujanja wowote mkono wangu sitauzuia juu ya watoto wako.”

    “Nakuja naomba usiwafanyie jambo lolote baya.”

    “Kuna usemi unaosema kuwa muuaji akilia hulia machozi ya kweli siyo bandia unajua maana yake? Ngoja nikwambie ni vile tu muuaji hujua maumivu ya mateso kuliko mtu yeyote yule, naamini unafahamu fika jinsi inavyokuwa. Una dakika kumi au nitaanza na mkeo,” alisema muuaji huyo na kukata simu.

    Bila kupoteza muda, Side alikimbilia nyumbani kwake pasipo kujali hatari itakayomkuta.

    ***

    Salima aliburuzwa mpaka ghorofa ya tatu, safari yake wakati huu ikaishia ndani ya chumba kimoja ambacho aliamini ndicho kilichokuwa kinakaliwa na msichana aliyesikia akizungumziwa usiku wa jana yake, Diana.

    “Kuanzia leo hautaruhusiwa kukaa na simu wala kitu chochote kitakachokuwezesha kufanya mawasiliano nje ya jengo hili, mimi ndiye utakayepaswa kunisikiliza na kuniuliza kila kitu unachokiona haujakielewa. Sheria zetu zipo kila mahali ndani ya jengo hili kuwa makini uzisome kwanza kabla ya kufanya jambo lolote mahali popote, jambo la mwisho kuanzia leo jina lako litakuwa Carolina,” alimaliza kusema mwanamke huyo ambaye sauti yake, Salima aliikumbuka vyema kwa kuwa aliisikia jana yake.

    “Huyu lazima atakuwa Madam Bernadeta,” aliwaza Salima masikio yake yakishindwa kuamini kama alipewa jina la mwanamke ambaye alikuwa hasimu wake wa muda mrefu kabla ya kuelewana naye dakika chache zilizopita.

    Kwa kuwa kuua kulikuwa ndani ya damu yake, Henry hakuona shida yoyote zaidi ya kufurahia amri hiyo. Tofauti na zamani, siku hiyo wala dhamira yake haimsuti juu ya damu za watu alizozimwaga kwa mikono yake. Alikuwa akizidi kuendelea kufanya ushetani wake kwa furaha kabisa kama vile kuua ilikuwa ni aina fulani ya mchezo.

    Si kilio cha Sonia wala machozi ya Dedan yalimfanya awaonee huruma na kuwaachia mateka wake hao. Badala yake Henry alikuwa akiwaangalia na kucheka kila mara Sonia alipolia kwa uwoga baada ya kumgusagusa na mdomo wa bastola yake.

    Henry alichagua sehemu nzuri mbali kabisa na makazi ya watu kiasi kwamba hakupata bugudha yoyote kuwahifadhi mateka wake. Sauti ya vilio vya kimyakimya ndivyo ambavyo vilisikika eneo hilo kutoka kwa Sonia ambaye huenda angepiga makelele kwa nguvu kama tu asingefungwa kwa kitambaa kizito mdomoni.

    ***

    Side aliingia kila chumba ili kuhakikisha kama kweli mkewe Sonia hakuwemo ndani; kitu ambacho kilikuwa sahihi. Akawaza labda alikuwa nje mahali fulani. Labda aliondoka bila kuaga!

    Alitafakari wazo hilo na kutolipa uzito kwani Sonia hakuwa na tabia ya kutoka nje, alikuwa ni mtu wa kukaa ndani muda wote akihofia kujulikana na watu. Hata mavazi yake yalikuwa ni yale yaliyomficha mwili mzima na kuacha macho tu.

    Alipokuwa akitembea kuelekea mlango wa nyuma ambao ndiyo ulikuwa umefunguliwa, Side aligundua alama za viatu asivyovifahamu kwenye ardhi ya mlango wake. Ni wazi mtu asiyemjua aliingia na kutoka ndani ya nyumba yake.

    Kama vile mchunguzi wa masuala ya uhalifu (forensic), Side alitafuta kila mahala alama yoyote itakayomdhihirishia alichokuwa akikiwaza, kuwa jambo lililotokea muda mfupi nyumbani kwake lilikuwa ni utekaji nyara na si vinginevyo.

    Mara akagundua kuchunika kidogo kwa rangi kwenye kichuma cha loki ya mlango ulioachwa wazi jambo lililomfanya agundue kuwa mlango huo ulisukumwa kwa nguvu na aliyeingia ndani. Moyo wa Side ukaanza kudunda kwa kasi kiasi cha jasho jingi kumtoka kama vile mtu aliyechanganyikiwa.

    Side alishindwa kutoa taarifa polisi wala sehemu yoyote ya usalama kwa kuwa alihofia kwa kufanya hivyo atamuanika Sonia mbele ya wabaya wake.

    Kuna ule muda mtu huwa hafikirii chochote zaidi ya kuwa na hofu isiyokuwa na mfano, muda huo ulikuwa juu ya Side kwa siku hiyo akaanza kutetemeka kwa woga. Moyo wake mara ulifanya pah! Aliwakumbuka watoto wake mapacha ambao alizaa na mkewe Sonia wote walikuwa katika shule ya malezi ya awali kwa watoto ‘Msami Day Care.’

    Kwa kasi ya ajabu Side alifika shuleni lakini jibu ni kwamba hawakuwepo hapo na walimu hawakujua wapi walipokwenda ingawa ushahidi wa watoto hao kuripoti shuleni asubuhi ulikuwepo.

    Kwa uchungu Side alifumba macho yake kwa nguvu, machozi yakimtiririka mashavuni kama mtoto mdogo. Kitu alichokuwa akikitaka kujua zaidi ni nani aliyekuwa akimfanyia mambo yote hayo?

    Akiwa mwenye kukosa matumaini, simu yake ya mkononi iliita kwa namba asiyoifahamu akaipokea na kusikiliza:

    “Haloo Side, kama unamthamini mkeo na watoto wako rudi nyumbani kwako haraka sana, nina zawadi yako,” iliongea sauti ya mtu asiyemfahamu kwa kujiamini.

    “Sema unataka shilingi ngapi nikupatie, naomba uniachie familia yangu,” alisema Side kwa pupa huku machozi yakimtoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usiwe kama mwanamke Side, inuka uje mara moja na nikukumbushe tu, uje peke yako ukifanya ujanja wowote mkono wangu sitauzuia juu ya watoto wako.”

    “Nakuja naomba usiwafanyie jambo lolote baya.”

    “Kuna usemi unaosema kuwa muuaji akilia hulia machozi ya kweli siyo bandia unajua maana yake? Ngoja nikwambie ni vile tu muuaji hujua maumivu ya mateso kuliko mtu yeyote yule, naamini unafahamu fika jinsi inavyokuwa. Una dakika kumi au nitaanza na mkeo,” alisema muuaji huyo na kukata simu.

    Bila kupoteza muda, Side alikimbilia nyumbani kwake pasipo kujali hatari itakayomkuta.

    ***

    Salima aliburuzwa mpaka ghorofa ya tatu, safari yake wakati huu ikaishia ndani ya chumba kimoja ambacho aliamini ndicho kilichokuwa kinakaliwa na msichana aliyesikia akizungumziwa usiku wa jana yake, Diana.

    “Kuanzia leo hautaruhusiwa kukaa na simu wala kitu chochote kitakachokuwezesha kufanya mawasiliano nje ya jengo hili, mimi ndiye utakayepaswa kunisikiliza na kuniuliza kila kitu unachokiona haujakielewa. Sheria zetu zipo kila mahali ndani ya jengo hili kuwa makini uzisome kwanza kabla ya kufanya jambo lolote mahali popote, jambo la mwisho kuanzia leo jina lako litakuwa Carolina,” alimaliza kusema mwanamke huyo ambaye sauti yake, Salima aliikumbuka vyema kwa kuwa aliisikia jana yake.

    “Huyu lazima atakuwa Madam Bernadeta,” aliwaza Salima masikio yake yakishindwa kuamini kama alipewa jina la mwanamke ambaye alikuwa hasimu wake wa muda mrefu kabla ya kuelewana naye dakika chache zilizopita.



    Baada ya kuongea hayo, Madam Bernadeta na hao wanawake alioingia nao wakaondoka na kumuacha Salima peke yake.

    Akili yake ikiwa juu ya maneno makali aliyoambiwa na Caro kupitia ujumbe wa simu dakika chache zilizopita, alihisi yalikuwa yakianza kutimia kwa kuwa walishaanza kumkataza kuwa na mawasiliano na mtu yeyote wa nje bila kuambiwa sababu za msingi pia sauti ya Madam Bernadeta ilikuwa yenye mamlaka na amri tofauti na vile alivyoongeleshwa na mtu yeyote tangu alipoingia mara ya kwanza katika jengo hilo.

    “Labda wamenisikia nikiongea na Caro?” alijiuliza Salima huku akiyakumbuka vyema maneno aliyotumiwa na Caro kwa njia ya ujumbe mfupi muda mchache uliopita ukisomeka: “Kila unachokiongea na kukifanya kuna mtu anakutazama.”

    ***

    Kama ilivyo kwa mwanaume yeyote, akili ya Dedan iliwaka ari ya kutaka kujiokoa toka kwenye kifungo alichomo. Japo alikuwa amefungwa vyema mikono na miguu yake, tena akiwa na kitambaa kizito mdomoni, alihisi lazima afanye jambo ili kujisaidia yeye na mwanamke aliyekuwa mkarimu kwake tangu alipofika nyumbani kwake usiku uliopita.

    Mwanamke huyo hakuwa mwingine zaidi ya Sonia ambaye ingawa Dedan hakujua vyema wasifu wake, lakini aliamini hakustahili kupitia mateso hayo pamoja naye siku hiyo.

    Moyoni aliazimia kuurudisha wema wa Sonia na mumewe Side kwa kuwaokoa na hatari yoyote ambayo ingewakuta siku hiyo bila kujua kuwa yeye ndiye alikuwa chanzo cha yote kwani kama Side asingejihangaisha kumuokoa yeye, Madam Flaviana angejuaje kama alikuwa akificha siri hadi kumtuma Henry amchunguze?

    Dedan alijitahidi kwa shida kujinyonganyonga mpaka akafanikiwa kuigeuza mikono yake iliyofungwa kwa nyuma na kuwa mbele kama ambavyo huwa kwa kawaida. Kwa muda mrefu Dedan aliisuguasugua kamba ngumu aliyofungwa mikono yake kwenye ncha ya gogo la mti lililokuwa karibu yake mpaka ikalainika na kukatika.

    Kwa kuwa mikono yake ilikuwa huru aliweza kuifungua kwa wepesi kamba iliyokuwa miguuni mwake na baadaye kumfungulia Sonia kisha wote wakaondoka maeneo hayo.

    “Fanya haraka tuondoke asije kurudi hapa na kutukuta,” Sonia alisema kwa hofu wote wakielekea nyumbani kwao bila kujua kama Henry alikuwa huko tayari na watoto wake.

    ***

    Side alifika nyumbani kwake mara moja. Hakuwa na muda wa kujihami hata kidogo. Kitu alichokifikiria mbele yake ni jinsi atakavyoweza kuiokoa familia yake toka kwa bedui mmoja aliyetumwa na Serenity mara baada ya siri zake kufichuka.

    Kwa kuwa alikuwa akifanya nao kazi kwa muda mrefu, alijua fika kiwango cha adhabu yake kwa makosa aliyoyafanya. Alijua hakuna hata chembe hai moja katika mwili wake itakayosalia. Kifo chenye maumivu makali ndiyo adhabu ndogo aliyojikadiria kupewa pindi Madam Flaviana na Mr. Chakos atakapomtia mkononi.

    Side alijua hakuwa na cha kufanya. Alitambua wajibu wake ni kuitetea familia yake kuliko kitu kingine chochote. Akapiga moyo konde na kuvuka barabara ya mwisho kuingia nyumbani kwake, saa yake ya mkononi ilionesha kuwa aliwahi kwa dakika nne kati ya kumi alizopewa na mtekaji nyara.

    Hatua mbili kabla hajafika kwenye geti la nyumba yake alihisi mkono mzito ukimshika begani alipogeuka tu!

    ***

    Side hakukumbuka kitu chochote tokea hapo zaidi ya kushtuka akiwa katika moja ya vyumba vyake huku mikono na miguu yake ikiwa imefungwa hali kadhalika midomo yake.

    Masikio yake yaliruhusiwa kusikia sauti za watoto wake wadogo wakilia chumba cha pili kutoka kile alichopo. Kwa upendo uliopitiliza juu ya wanae, Side alijikuta akimwaga machozi kama mtoto mdogo akijilaumu kwa kila jambo alilolifanya.

    Akiwa katika hali hiyo, mara mlango ukafunguliwa na mtu asiyemfahamu. Alipoangalia kiatu chake aligundua kuwa ndiyo kiatu chenye soli alizoziona mapema siku hiyo nje ya nyumba yake.

    Alipomsikiliza sauti yake kwa makini, aliitambua kuwa ndiyo ileile iliyozungumza naye muda mfupi ikimtaka arejee nyumbani kwake mara moja. Woga ulimshika akatulia kimya akisubiri nini kitafuatia kwani alishamjua mtekaji wake kuwa ni Henry ‘Ze Deader’ maana yake ni ‘Muuaji Wauaji’ kama ambavyo aliwahi kumsikia Madam Flaviana na Mr. Chakos wakimzungumzia mara kadhaa huko nyuma.

    Akiwa amekosa msaada wowote, Side alijigaragaza sakafuni kila muuaji wake alivyozidi kumsogelea.

    Kwa mikogo, Henry aliichukua simu yake na kupiga kutoa maagizo kwa mtu fulani.

    “Muda ndiyo huu, hakikisha unaipeleka hiyo mizigo Serenity mara moja ikiwa kama ilivyo. Wakikuzidi nguvu ua!” alisema Henry bila kujali jinsi gani Side aliumia kwani alishajua kuwa mizigo iliyokuwa ikizungumziwa ni mkewe Sonia na Dedan.

    “Inaonekana Madam Flaviana anakupenda sana. Eti ameniambia nikumalize mara moja ila hakuniambia kwa njia gani, so i will make it faster and painless (kwa hiyo nitafanya haraka bila maumivu) kwa ajili ya heshima yake,” alisema Henry huku akimtazama Side aliyekuwa akihangaika kujaribu kujifungua kamba alizofungwa baada ya kujua hatima yake. Bila huruma, Henry aliichomoa bastola yake na kuifunga ‘silenser’(kidhibiti sauti) kisha akafyatua risasi kadhaa zilizotua vyema katika mwili wa Side. Mithili ya paka shume Henry akaondoka ndani ya jengo hilo akiwa tayari ameliwasha moto akilenga kuwateketeza watoto wa Side ndani yake.

    ***

    Wakiwa bado mbali na makazi ya watu, Dedan na Sonia walihangaika huku na huko kuitafuta barabara na makazi ya watu. Kila kona walikuwa wamezungukwa na vichaka wasijue waendako.

    Dedan ndiye alikuwa wa kwanza kusikia mngurumo wa gari upande wake wa kushoto. Akamshika mkono Sonia na wote wakakimbilia upande huo na kulisimamisha gari hilo wakapanda bila kujua muendeshaji wake kuwa ni mtu yuleyule aliyetumwa na Henry dakika chache zilizopita.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***

    Madam Flaviana aliketi pembezoni mwa Mr. Chakos, kama kawaida yao walikuwa wamezungukwa na kompyuta nyingi zilizounganishwa na kamera za CCTV zilizotegwa vyema ndani ya jengo la Serenity wakiangalia kila kitu kilichokuwa kikifanyika ndani ya jengo hilo.

    Hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiijua siri ya kamera hizo isipokuwa wao tu na bosi wao Mr. George ambaye bado hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa akimjua kwa sura.

    “Haya Sonia ameishapatikana vipi kuhusu Caro?” Madam Flaviana alimuuliza Chakos.

    “Caro atapatikana tu. Nimewatuma watu wamtafute kwenye mtandao kupitia simu ya mwisho aliyompigia Salima. Wewe hakikisha hakuna kinachoharibika, tumebakiza mwezi mmoja tu kabla Prince Khalfani hajafika jijini,” alisema Chakos na kunyamaza ghafla macho yake yakiangalia kwa makini video iliyomuonesha Julieth akigonga mlango wa chumba cha Salima aliyepewa jina la Carolina muda mfupi uliopita.

    ***

    Salima aliufungua mlango na kushtushwa na msichana mrembo aliyekuwa amesimama mbele yake.

    “Naitwa Julieth nimesikia wewe ni mgeni hapa. Unaitwa Caro si ndiyo?” alisikika Julieth huku akijikaribisha mwenyewe ndani ya chumba cha Salima na kukaa kitandani.

    Kwa sauti ile, Salima aligundua mara moja kuwa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa chumbani kwa Madam Bernadeta siku ile.

    “Njoo huku,” aliita Julieth na kusimama. Bila ubishi Salima akamfuata kwa nyuma.

    Walipita korido ndefu na kuingia ndani ya chumba kimoja kilichoandikwa ‘Restroom.’ Salima alipigwa na butwaa baada ya kuwaona wasichana wengi wasiopungua thelathini wote wakiwa wamevalia nguo zinazofanana na zile alizovaa yeye na Julieth.

    Wasichana wote waliokuwa ndani ya chumba hicho walikuwa wakimtazama yeye peke yake huku wengi wao wakionekana kumtazama zaidi mpaka akainama chini kwa aibu akitamani kujificha nyuma ya Julieth.

    “Jamani huyu ni Caroline. Atakuwa na sisi kuanzia leo,” Julieth alimtambulisha Salima huku wasichana wale wote wakimsikiliza kwa makini.

    “Vipi amepitia ‘initiation’ au bado?” aliuliza msichana mmoja, kufumba na kufumbua macho wote wakamvamia Salima wakimshambulia.

    “Pole Caro sote tumepitia hilo,” alisema Julieth huku naye akijiunga nao.

    Salima alibaki akipiga makelele akiomba msaada na kujitetea kila alivyoweza lakini hakuna hata mmoja aliyemuogopa zaidi ya kuzidi kumuandama

    Ilikuwa kama jambo la utamaduni, endapo msichana mpya atatambulishwa basi lazima apitie sharti gumu la kuvuliwa nguo zake zote na wasichana waliomtangulia kama utaratibu wa kuingia ndani ya jengo hilo. Shughuli hiyo ndiyo huitwa ‘initiation.’

    Akiwa hajui kuhusu jambo hilo, Salima alipiga makelele bila msaada wowote huku wasichana hao wakimvua nguo zote na kumuacha kama alivyozaliwa akitetemeka kwa hasira.

    Cha ajabu baada ya kuhakikisha Salima hakuwa na nguo yoyote mwilini mwake, wale wasichana wote wakaangua vicheko na kumfafanulia maana ya kitendo walichomfanyia ambapo Salima mwenyewe alijikuta akicheka pamoja nao huku na yeye akiapa kulipiza kisasi kwa msichana mwingine mgeni atakayetambulishwa siku zijazo.

    ***

    Dereva wa gari walilopanda akina Dedan aliendelea kukata kona toka mtaa mmoja kwenda mwingine. Mwanzoni Sonia alifikiri mtu huyo alikuwa akiwapa lifti kwa kuwapeleka nyumbani kwao kama alivyowaahidi saa chache zilizopita, lakini haikuwa hivyo.

    Sonia alipomtazama vizuri dereva yule aligundua kuwa alikuwa makini sana akiwaangalia kwa kioo cha juu yake kilichomruhusu kuwaona abiria wote waliokaa kwenye siti za nyuma yake ambao ndiyo yeye Sonia na Dedan.

    Bila kuonesha hofu yake, Sonia aligeuza shingo na kuitazama milango ya gari hilo na kugundua kuwa ilikuwa imelokiwa. Akaangalia aina ya viio vyake akagundua kuwa vilikuwa vile vya ‘tinted’ ambavyo mtu wa ndani huweza kuona nje pasipo wa ndani kuonekana. kwa mazingira hayo Sonia alihisi yalikuwa mazuri kwa utekaji nyara kama akili yake ilifikiri kwa usahihi.

    Kwa uoga Sonia alishindwa kuhoji wapi walikuwa wakipelekwa maana hata Dedan mwenyewe alianza kupatwa na wasiwasi na kugeuka mara kwa mara akimwangalia Sonia.

    Sonia alizidi kupepesa macho yake akiangalia vyema kila kitu ndani ya gari hilo. Zaidi alikuwa akiangalia kitu chochote kitakachoweza kugeuka silaha kama tu dereva huyo atageuka na kuwa mmoja kati ya majambazi waliotumwa kuwadhuru.

    Alipopapasa juu ya kiti alichokaa, akagundua kulikuwa na peni. Akaificha akitumaini kuitumia baadaye kama silaha yake. Akaendelea kupapasa zaidi kwa kificho ili asije kushtukiwa na dereva yule aliyekuwa makini kila saa akitupia jicho lake kwenye kioo akiwaangalia Sonia na Dedan nyuma yake.

    “Sonia najua mpaka sasa utakuwa umeshajua ninatokea wapi, kwa hiyo hakuna haja ya kuhangaikahangaika. Mimi ni dereva tu na jukumu langu ni kukurudisha nyumbani,” aliongea dereva huyo akiuvunja ukimya baada ya kushtukia mbinu za Sonia.

    “Sonia ni nini kinaendelea?” Aliongea Dedan akimgeukia Sonia aliyekuwa amepigwa butwaa akishangaa ‘Serenity’ wamejuaje kama alikuwa hai!

    “Usiogope Dedan, usiogope..” aliongea Sonia akizama kwenye siti ya kiti alichokaa, taratibu akaishiwa nguvu na kuzirai.

    “Sonia!” Dedan alimwita Sonia kwa kumtingishatingisha huku akiwa katika bumbuwazi asijue nini kilichokuwa kinaendelea kwenye maongezi ya Sonia na dereva huyo kiasi cha Sonia kuwa katika hali hiyo.

    Baada ya mwendo mfupi, dereva alikunja kona na kuingia ndani ya geti kubwa lililojifungua na kujifunga lenyewe na kuzidi kutokomea ndani zaidi na baadaye kupaki.

    Mara mlango wa siti aliyokaa sonia ukafunguliwa kisha mtu mwingine akatokeza mikono yake na kumtoa nje Sonia akiwa bado amezirai.

    “Wewe shuka unifuate!” Ilisikika sauti yenye amri kutoka nje ya gari ikimwamrisha Dedan ashuke mara moja, jambo ambalo alilifanya haraka bila kupoteza muda.

    Mbele kulikuwa na mlango mwingine mkubwa uliokuwa ukiingia ndani ya ghorofa refu lililopambwa kwa rangi nzuri huku juu ya mlango maandishi yaliyoandikwa ‘Serenity’ yakionekana kwa ukubwa.

    “Huyo ndiyo Dedan na hatimaye Sheila amepatikana umemuona jinsi alivyo?” Aliongea Madam Flaviana akimwambia Mr.Chakos kama kawaida yao wakiwa hawabanduki kwenye kompyuta zao.

    “Nasikia alikuwa akijiita Sonia, tumpe haki yake tumwite hivyohivyo,” aliongea Chakos mara simu yake ya mkononi ikaita, akaongea kwa muda kidogo kisha akageuka na kumtazama Madam Flaviana akiongea kwa sauti: “Carolina naye amepatikana andaa mchezo!”



    “Carolina! umempataje?” aliuliza kwa mshangao Madam Flaviana.

    “Usishangae sana hakuna kitu kinachonishinda nikiamua,” alijibu Mr. Chakos kwa kujiamini huku akikenua meno yake meupe huku meno mawili ya pembeni yakiwa yenye



    kuchongoa kama yale ya wanyonya damu; kama umeishawahi kuona filamu za ‘Dracula.’

    “Yupo wapi?” aliuliza kwa shauku Madam Flaviana.

    “Subiri muda mfupi ujao atapelekwa Serenity kama wenzake.”

    ***CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Iliwachukua takriban nusu saa majirani wa Side kugundua kuwa moto mkali ulikuwa ukiwaka ndani ya nyumba ile. Taarifa zilienea kila mahali kwa kasi ya ajabu huku watu



    wakimiminika toka kila kona ya Ulongoni.

    Watu wachache walio jasiri walijitolea kumwaga maji na mchanga ili waupunguze moto ule au kuuzima kabisa. Wengine walitoa taarifa kwa kitengo cha zimamoto na polisi



    ambao kama kawaida yao walitumia muda mrefu kufika kwenye tukio.

    “Nani mmiliki wa nyumba hii?” aliuliza afande Luka akichukua maelezo kutoka kwa mmoja wa jirani zake Side.

    “Samahani afande, sikufundishi kazi lakini kwa nini tusitoe msaada kwanza hayo mambo mengine yafuate baadaye?” aliongea afande John na kupata sapoti kubwa kutoka kwa



    wakazi wa eneo hilo.

    “Unataka kufanya nini John! Wewe huoni huo moto ulivyo? Hakuna kiumbe chenye uhai humo. Subiri amri toka kwangu siyo unapayuka tu. Kama unataka kuingia ukafe, nenda!”



    Aliongea afande Luca kwa ghadhabu.

    Kufumba na kufumbua, afande John alijitosa ndani ya nyumba hiyo iliyochachamaa kwa moto bila uoga wowote huku kila mmoja akimshangaa.

    “Mwanaharamu huyu anataka kufanya nini?” alisema afande Luca kwa hasira akikunja kitabu chake alichokuwa akiandika maelezo huku jasho likimtiririka kwa hofu.

    Baada ya dakika chache…

    “Njooni huku,” ilisikika sauti ya afande John ikitokea ndani na kumfanya kila mmoja ageuke na kuelekea upande ambao ilisikika sauti hiyo.

    Katikati ya moshi mzito alichomoza afande John mkononi mwake akiwa amewabeba watoto wawili aliopokewa na polisi wenzake kwa ajili ya huduma ya kwanza na kuwahishwa



    hospitali mara moja.

    “Nyumba nzima sijamuona mtu yeyote zaidi ya hao watoto wawili,” aliongea afande John kwa taabu akimwambia afande Luca ambaye aliachama mdomo kwa mshangao akizitazama



    nguo za afande mwenzake zikifuka moshi, akili yake ikikataa kuamini ujasiri uliooneshwa na afande mwenzake.

    Wakati watoto wale wanapakizwa kwenye ‘ambulance’, afande John aliweza kuona kamba zikiwa mikononi mwao na vitambaa vizito midomoni mwao. Haraka akahisi kwa vyovyote



    vile tukio la kuungua kwa nyumba kumefuatia baada ya uharifu fulani kufanyika.

    Kwa muda mfupi aliokuwa hapo, aligundua kuwa wakazi wa nyumba hiyo iliyotajwa kuwa ya bwana Saidi maarufu kama Side hawakuwa na ushirikiano mzuri na majirani zao kiasi



    cha watu hao kujulikana sana. Maelezo ya jirani mmoja yalionesha kuwa familia hiyo ni ya baba na watoto wadogo wawili wa kike, lakini mara nyingine kumekuwa na maelezo



    kuhusu kuonekana kwa mwanamke mwenye ushungi kuanzia juu mpaka chini ndani ya nyumba hiyo.

    Kwa maelezo ya majirani hao, walisema ni nadra sana mwanamke huyo kuonekana hadharani na mara kadhaa huisikia sauti yake kutoka ndani.

    Kwa maelezo hayo afande John alihisi kwa vyovyote Side na huyo mwanamke aliyekuwa akiishi naye kwa siri walikuwa wakihusika katika mpango wa kutaka kuwaua watoto wao



    kwa kuwasha moto kwa makusudi.

    Akafungua kitabu chake kisha akachora michoro kadhaa na kuweka alama ya viulizo katika jina la Side na katika jina jingine alilolipachika ‘nani.’

    Kikosi cha zima moto hatimaye kikafika na kuanza kazi yake. Muda huo nusu ya nyumba ilikuwa imeteketea pamoja na mali zote huku kuta zenye masinzi mazito zikibakia



    kama kumbukumbu kuwa eneo hilo awali liliwahi kukaliwa na jengo zuri.

    Upesi askari wakawatawanya watu na kulizungushia eneo hilo utepe kama kidhibiti na kuwatenga raia wa kawaida kutoka sehemu hiyo ili wafanye uchunguzi wa chanzo cha



    tukio hilo.

    ***

    Salima alirudia na hali yake ya furaha na kwa mara ya kwanza akapata marafiki wapya ndani ya jengo hilo. Katika hayo kamwe hakusahau kuwa Julieth alitumwa kumpeleleza



    kama ambavyo aliwasikia wakizungumza chumbani na Madam Bernadeta.

    Usiku ule Salima alilala kwa amani kana kwamba hakuwahi kulala kama vile maishani yake yote, lakini ghafla katikati ya njozi zake doa la giza liliingia na kusambaa



    likiharibu weupe wote ulioangaza juu ya ndoto yake. Mapigo ya moyo yakapiga kwa kasi, mara akazinduka kitandani akiwa na hofu asijue maana ya ndoto ile.

    Akiwa hana hata lepe la usingizi, akawasha taa ya chumbani na kubaki akizungukazunguka kama vile alikuwa akikatafuta kitu alichokipoteza.

    Ghafla macho yake yakatua pembeni ya kitanda chake na kuuona mchoro wa ajabu ulioonekana nyuma ya ubao wa kitanda kile.

    Mwanzoni alishindwa kuelewa maana ya mchoro ule ulioonekana wazi kuchorwa kwa kitu chenye ncha kali. Lakini alipobadilisha mtazamo yaani kwa kuuangalia tokea upande wa



    kulia kwenda kushoto alianza kuuelewa taratibu.

    Shepu ya mchoro huo ulikuwa ni ramani ya chumba, kama vile wachoravyo wataalamu wa majengo. Ramani hiyo ilikuwa na sehemu ya wazi katikati, mara moja Salima aliigundua



    sehemu hiyo iliwakilisha mlango wa chumba hicho.

    Kwenye kona ya mchoro huo, alama mfano wa jicho ilionekana na kona nyingine kulikuwa na alama mfano wa sikio.

    Kwa tafakari ya harakaharaka, viungo hivyo huwa na kazi ya kuona na kusikia ni wazi kuwa mchoraji wa ramani hiyo alikuwa na maana yake ambayo Salima hakuijua. Hofu



    ikaanza kumpanda huku akiukumbuka ujumbe wa mwisho aliotumiwa na Carolina kuwa chochote atakachofanya kuna mtu anamuona na kumsikia.

    Akazima taa na kuanza kufuatilia kimyakimya maana ya jicho na sikio kama alivyoiona kwenye ramani. Akaelekea upande wa kushoto kama mchoro ulivyoonesha. Kwa mshangao



    akakiona kitufe kidogo chenye lenzi kikiwa kimefichwa vyema katika ua la plastiki lililopambwa ukutani.

    “Mungu wangu, kamera!” alijisemea Salima kimoyomoyo huku akiiacha kama ilivyo na kuelekea upande mwingine ambapo alikiona kinasa sauti.

    Fumbo lote lilikuwa limefumbuliwa mbele yake, akatambua kuwa jicho ilikuwa ni kamera na sikio kilikuwa ni kinasa sauti. Kwa uwoga na aibu, Salima aliishia kusikitika



    na kujilaza kitandani akiwaza juu ya kila kitu alichokifanya kuwa alikuwa akionwa na kusikiwa na mtu mahali fulani.

    ***

    Baada ya huduma ya kwanza, hatimaye Sonia alishtuka akiwa katika chumba asichokifahamu. Akavuta kumbukumbu zake na kugundua kuwa kabla hajazirai alikuwa akizungumza na



    dereva wa gari alilolipanda akiwa na Dedan. Kuanzia hapo hakukumbuka chochote zaidi. Moja kwa moja akajua tayari ameshaingia katika mikono ya Serenity.

    Akiwa bado amejilaza kitandani kwa uchovu mwingi, Sonia alijigeuza taratibu upande wake wa kushoto na kumuona msichana mwingine akiwa amelala kitanda cha pembeni yake

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akihema taratibu mfano wa mgonjwa mahututi.

    Haukupita muda mrefu msichana huyo akashtuka na kugeuka akishangaa huku na huko na mara macho yake yakatua kwa Sonia.

    “Naitwa Sonia, nani wewe?” Kwa tabu Sonia alianza kujitambulisha yeye mwenyewe.

    “Caro,” alijibu msichana huyo kwa shida huku akijipapasa shingoni mwake kana kwamba kuna kitu alikuwa anakitoa bila mafanikio.

    “Kwa nini upo hapa?” Sonia aliendelea kuuliza kwa shauku huku akijaribu kukaa kitandani lakini alishindwa na kulala tena.

    “Shhh!” Caro alimkatiza usemi Sonia. Mara sauti ya viatu vilisikika vikisogea kwenye chumba hicho. Ghafla Madam Flaviana akaingia na kujongea taratibu mpaka kwenye



    vitanda walivyokuwa Caro na Sonia.

    “Karibuni warembo, I’m so happy to see you again (ninafuraha kuwaona tena),” aliongea Madam Flaviana kwa mbwembwe huku akiwatazama Caro na Sonia jinsi walivyopigwa na



    butwaa.

    “Najua mnajisikia uchovu sana, hiyo inatokana na nusu kaputi tuliyowawekea kabla ya kuwafanyia oparesheni maalumu.‘Infact’ tumewawekea vipandikizi karibu kabisa na uti



    wa mgongo upande wa shingo.

    Vipandikizi hivyo ni hatari kama mtataka kuviondoa kwa kuwa tumevishikiza karibu kabisa na sehemu ya uti wa mgongo. Niwaambie tu kwamba hakuna daktari yeyote



    atakayeweza kuviondoa vipandikizi hivyo bila kuutoa na uhai wenu pia. Tunahitaji jambo dogo sana kutoka kwenu. Nina uhakika hamuwezi kukataa,” aliongea Madam Flaviana



    kwa nyodo huku akiondoka.

    “Oh! Nimesahau kuwaeleza kuhusu hivyo vipandikizi tulivyovifunga miilini mwenu. Kama mtajaribu kutoroka kwa hali yoyote ile ndani ya jengo hilo vipandikizi hivyo



    huweza kuripuka na kukumaliza moja kwa moja. So be careful,” alimalizia Madam Flaviana na kuondoka akiwaacha Sonia na Caro wakilia kwa uchungu. Hakuna ubishi wote



    walijijua wapo ndani ya mikono ya Serenity.

    ***

    Kama askari wa kitengo cha upelelezi, Afande John alijitahidi kufanya kila kitu kwa ustadi mkubwa. Ubaya wa kazi yake ni kwamba kila siku amekuwa akishughulika na



    upande hasi wa mwanadamu kwa maana ya maovu wanayoyafanya watu kila siku iendayo kwa Mungu.

    Siku hiyo pia alikuwa akishuhudia matokeo ya maovu hayo. Mbele yake kulikuwa na maiti ya mwanadamu iliyoiva kwa moto kiasi cha kutotambulika hata kidogo.

    Kama maelezo yatakuwa sahihi basi mtu huyo atakuwa ndiye Side aliyetajwa kama mmiliki wa nyumba hiyo iliyoungua.

    Kwa umakini mkubwa alivaa glovu zake na kuugeuza mwili huo. Mara akaona matundu ya risasi katika maiti hiyo.

    “Huyu alikuwa ameuawa kabla ya moto kumuunguza,” aliwaza Afande John huku akiendelea kuchorachora kwenye kitabu chake, saa hiyo juu ya yale jina la Side likaunda



    kiboksi kingine na kuweka kiulizo.

    “Huyu alikuwa ameuawa kabla ya moto kumuunguza,” aliwaza Afande John huku akiendelea kuchorachora kwenye kitabu chake. Saa hiyo juu ya jina la Side akaunda kiboksi



    kingine na kukiwekea kiulizo.



    “Vipi kuna maiti nyingine zaidi ya hiyo?” Afande Luca alimuuliza Afande John huku akipiga miayo mfululizo kutokana na uchovu uliochanganyika na usingizi kwani tayari



    kiza kilikuwa kimeshaanza kutanda.

    “Hapana, ni hii tu,” alijibu Afande John.

    “Fasta tuipakize kwenye gari tuondoke hapa,” alisema Afande Luca.

    Baada ya kumaliza zoezi la kuibeba maiti ile, Afande John aligeuka kana kwamba machale yake yalimtuma afanye hivyo. Mara macho yake yakakutana uso kwa uso na mtu mmoja



    aliyepotelea haraka kwenye vichaka vilivyokuwa karibu yake huku giza la usiku likimficha.

    “Kuna mtu anatutazama upande ule haraka tumfuatilie,” alisema Afande John na kukimbilia huko mara moja akimwacha Afande Luca aliyebakia akimlaani kwa kujifanya



    kiherehere kwenye kila jambo.

    Japo kuwa mtu yule alikuwa na spidi kali, lakini hakuweza kufua dafu mbele ya Afande John aliyekuwa akiruka viunzi kama vile hakuwa na akili nzuri.

    Kwa kasi ya ajabu, Afande John alifanikiwa kumfikia na kulidaka shati lake akijaribu kumvuta ili kumpunguza kasi. Kama vile mtu yule alikuwa akiyasoma mawazo ya Afande



    John, upesi akabonyea chini kidogo, kufumba na kufumbua shati pekee ndilo lililobakia mikononi mwa Afande John, huku mtu yule akipepea kifua wazi na kutokomea



    vichakani.

    “Yuko wapi sasa huyo mtu?” alitamka Afande Luca huku akihema bila mpangilio baada ya kufika kwenye tukio.

    “Nusu nimkamate, lakini amefanikiwa kunitoroka afande.”

    “Umeona eee! Nilishakuambia tuondoke, wewe unang’ang’ania kufanya mambo yasiyokuhusu. Sitaki urudie upuuzi kama huo ukiwa unafanya kazi na mimi.”

    “Sawa afande tuondoke,” alijibu Afande John huku mikono yake ikiwa bize ndani ya mifuko ya shati alilolipata kutoka kwa mtu yule aliyemchoropoka. Mara akachomoa kadi



    fulani na kuanza kuikagua.

    “Tazama afande!” alisema Afande John akimwonesha Afande Luca ambaye alikuwa bado amekunja ndita kwa hasira kama vile mtu aliyekusudia kulamba ndimu lakini kwa bahati

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mbaya ndimu ikamlamba yeye.

    “Nini? Giza limeingia tuondoke bwana!” Alifoka Afande Luca kwa hasira.

    “Angalia ni kadi ya kampuni, halafu hii nembo nadhani nimeishawahi kuiona mahali lakini sikumbuki ni wapi,”

    “Hebu leta kwanza,” alisema Afande Luca hasira zake zikiwa zimepungua kidogo na kuipokonya kadi ile akijifanya hodari kutoa majibu mambo yaliyoshindikana.

    “Mh! Hata mimi alama hii nimeshawahi kuiona kwenye jengo moja, ngoja tufike ofisini kwanza.”

    Wote wakakubaliana kuihifadhi kadi hiyo na kuondoka eneo hilo.

    Kama kawaida yake, Afande John alifungua kitabu chake, akaandika neno ‘mvamizi’ pembeni ya jina la Side kisha akakifunga vizuri na kukirudisha mfukoni.

    ***

    Mr.Chakos, Madam Flaviana na mwanaume aliyeonekana kula chumvi nyingi walionekana wakimtazama kwa umakini mkubwa Dedan kupitia kompyuta zao.

    “Kwa kumuangalia unamwonaje, ni mzima au?” aliuliza Mr.Chakos akimtazama huyo mzee aliyekuwa pembeni yake.

    “Yap, vipimo vya nje vinaonesha kuwa ni mzima, ila bado hana kumbukumbu ya mambo ya zamani. Katika hatua aliyopo anaweza akapandikizwa uongo wowote na kuuamini kuwa ni



    kweli kwa kipindi chote cha maisha yake,” alijibu mwanaume huyo ambaye kitambulisho chake kiliandikwa ‘Dr. Eugene Harry’.

    “Madam, kafanye kazi yako,” Mr. Chakos alimgeukia Madam Flaviana aliyesimama na kutoka mle ndani.

    ***

    Akiwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea, Dedan alitulia tuli akisubiri hatima yake. Masaa yalikuwa yakienda taratibu sana ndani ya chumba alichofungiwa.

    Chumba kizima kilikuwa na kitanda na televisheni peke yake. Kwa muda huo alitamani kuwaza kitu fulani kuhusu maisha yake, lakini hakuwa na kitu chochote katika



    kumbukumbu zake zaidi ya Sonia na Side watu aliowafahamu siku moja tu iliyopita kabla hawajatengana.

    Mara sauti ya ufunguo ilisikika mlangoni pake. Mlango ukafunguliwa na mwanamke wa makamo aliingia ndani kwa kujiamini akimfuata mahali alipokaa Dedan huku akimwachia



    tabasamu pana kana kwamba walikuwa wakifahamiana.

    “Hallow Dedan! Naitwa Madam Flaviana,” alisema Madam huku akimpa mkono wa salamu Dedan ambaye aliupokea kwa heshima.

    “Nafahamu haujui uko wapi na kwa nini upo hapa, ila tambua tu kuwa upo sehemu nzuri na salama, ondoa hofu,” alisema harakaharaka Madam Flaviana akimtoa uwoga Dedan



    aliyekuwa kimya akimsikiliza.

    “Nafahamu una maswali mengi sana kichwani mwako, nipo hapa kukujibu machache ambayo nina imani ndiyo ya msingi.

    Najua umemsahau Salima lakini ngoja nikukumbushe,” alichombeza Madam Flaviana huku akichomoa ‘laptop’ yake. Akafungua upande wa picha na kuanza kumuonesha Dedan picha



    za Salima huku akimpa mkanda mzima kuhusu uhusiano wake yaani yeye Dedan na msichana huyo.

    Baadaye alimsimulia kuhusu Caro kama chanzo cha matatizo yake huku akidanganya kuwa mara kadhaa hapo zamani msichana huyo alijaribu kumuua na kuokolewa na Salima jambo....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog