Simulizi : Kivuli
Sehemu Ya Pili (2)
***** ***** ***** *****
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hata mimi sielewi hadi hivi sasa. Baada ya wewe kuondoka pale, niliongea na yule wakili na tukafikia muafaka. Nikarudi nyumbani kujiandaa kwa ajili ya kuja kuonana na wewe, wakati natoka nikawakuta askari nje ya nyumba yangu. Wakaniambia kuwa wamepata taarifa kuwa nafanya biashara ya dawa za kulevya, wakapekua nyumba yangu lakini hawakukuta kitu ndipo wakanichukua kunileta hapa kwa madai kuwa wanasubiri taarifa nyingine ila wameshaniambia wazi kuwa wanataka hela ndiyo waniachie” alijieleza Hadija.
“Wewe unafikiria ni kwa nini umehisiwa unafanya biashara hiyo?”
“Kwa kweli sijajua, japo kwanza nilidhani umewatuma lakini sikuona sababu ya wewe kunifanyia hivyo. Sijui ni nani aliyewapa taarifa hizi za uongo na sijui ni kwa lengo gani. Ila ni nani aliyekupa taarifa kuwa niko hapa?”
“Nilipiga simu yako haikupokelewa, baada ya muda nikapigiwa na Salome kwa simu yako, ndiye aliyenipa taarifa” alijitetea Ndilana
“Naomba unisaidie nitoke humu afande” aliongea akiwa katika hali ya uhitaji kweli
“Usiniite afande, sijajitambulisha kuwa mimi ni askari”
“Haya naomba unisaidie basi, mimi hela ya kuwapa sina. Nina hela ya kumpa wakili tu na nikiitoa hiyo tutakwama kwa Alice. Au umekubali kunisaidia niitoe hela ya wakili niwape?”
“Sikiliza Hadija, nitakuacha ulale humu kwa usiku huu kwa kuwa sijapata taarifa kamili na mkuu wa kituo hayupo muda huu, kesho alfajiri nitawatuma watu wakufuate. Ukinipa ushirikiano tutatatua tatizo lako kisha tutaendelea kuangalia tatizo la Alice. Umekula?”
“Nina njaa kama kidonda”
Inspekta Ndilana akajikuta anabeba majukumu, akatoka kwenye kumtafutia chipsi na kuku, akamletea na juisi na maji ya kunywa. Wakati wanakula Ndilana aliamua kuutumia muda ule kuulizia mawili matatu.
“Wewe una undugu na Alice?”
“Hapana ila ni rafiki sana wa mdogo wangu Salome, naye namuona kama mdogo wangu”
“Kwanini hadi leo ndiyo mnamtafutia wakili?”
“Tulikuwa tunamtegemea wakili wa kesi yake ya awali na marehemu mzazi mwenziye lakini amekuwa akituzungusha tu kisa hela. Alikuwa anataka hela nyingi sana”
“Ndiyo wakili Hamisi Mapembe?”
“Ndiyo, Hamisi Mzee Pembe! Kwenye kesi ya awali alikuwa anajitolea tu lakini alikuwa anajituma sana lakini safari hii anaonekana kama hataki. Wanasema huenda ni kwa sababu ile ilikuwa ya madai na hii ni ya jinai” alitoa ufafanuzi Hadija huku akikata sehemu ya kipande cha kuku na kukiweka mdomoni.
“Mlipokuwa huko Kilwa, Alice hakupata bwana kweli?”
Ilibidi Hadija atulie kwa muda akimuangalia Ndilana kisha akabinua midomo na kuguna. Ndilana akajishtukia na kutoa tabasamu akimwangalia Hadija.
“Najua kuwa wewe huwezi kukosa kutokana na urembo ulio nao, ndiyo maana naulizia kuhusu Alice” alijitetea kwa hoja za kichovu.
“Hakuna yeyote kati yetu aliyekuwa na bwana japo wengi walikuwa wakijitokeza. Ila sidhani kama huu ni muda mzuri wa kuyaongea hayo, wewe ukitoka hapa unaenda kulala kwenye godoro mimi naenda kulala sakafuni” aliongea kwa huzuni na kumfanya Ndilana apoteze tabasamu lake usoni.
“Usiwe na wasiwasi Hadija, kama hukufanya kosa lolote utaachiwa tu”
Ilikuwa yakaribia saa saba usiku wakati Hadija na Inspekta Ndilana wakiagana.
“Usiwaambie kuwa mimi ni askari” aliongea kwa sauti ndogo kabla ya kuondoka wakati wakimrudisha Hadija mahabusu.
“Afadhali nimepata cha kusema kwa afande” alijisemesha Inspekta Ndilana akiingia kwenye gari lake na kuondoka.
Kesho yake saa moja kamili asubuhi, Inspekta Ndilana alikuwa mlangoni kwa Afande Maswe, baada ya kukaribishwa alimuelezea kuwa eti alienda kumfuata Hadija nyumbani kwake kwa mahojiano akamkuta na wakili wanayemuomba amsimamie Alice akawaacha kwanza ila aliporudi mara ya pili akakuta kakamatwa. Kuanzia hapo ndipo akamueleza afande Maswe ukweli.
“Anaishi wapi?” aliulizwa kaswali kadogo na afande Maswe na kujikuta akipata kigugumizi kwa kuwa hakuwahi hata kumuuliza Hadija kuwa anaishi wapi, mwisho akapata cha kujitetea
“Nilienda Magomeni kwa Salome anielekeza anapoishi naye nikamkuta hapo hapo”
“Sawa”
Afande Maswe akapiga simu kutaka maelezo kwa mkuu wa kituo cha Urafiki, akaelezwa tu kuwa walipata taarifa toka kwa msamaria mwema kuwa Hadija anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya ndipo wakaenda kupekuwa nyumbani kwake lakini hawakukuta kitu.
“Sasa ni kwa nini bado mnamshikilia?”
“Tulikuwa bado tunataka kujiridhisha” alijitetea mkuu wa kituo
“Hebu niambie mnafanyaje ili kujiridhisha wakati mmepata tu taarifa na nyinyi hamjachukua muda kuzifuatilia mkakimbilia kumkamata na kupekua nyumba yake?”
Mkuu wa kituo alikaa kimya kidogo kisha akajitetea kuwa wanasubiri taarifa zaidi toka kwa chanzo chao ili waone kama kuna namna watakayoweza kuitumia kuthibitisha.
“Kwa hiyo mwanzo hamkuchukua taarifa kamili?” aliuliza Afande Maswe
“Hapana afande”
“Ila?”
Ukimya ulitawala upande wa Mkuu wa Kituo huku Afande Maswe naye akiwa ametulia akishubiri jibu. Baada ya kupita sekunde kadhaa bila jibu, Afande Maswe aliagiza Hadija apelekwe pale kituo cha kati mara moja kisha akakata simu na kumgeukia Inspekta Ndilana.
“Mnalipeleka wapi jeshi nyie vijana? Nyie ndiyo askari wasomi tunaowategemea mliboreshe jeshi la polisi lakini matokeo yake mmekua hamfanyi kazi kabisa kwa kutumia akili. Au mmeingia tu polisi kwa kuwa mlikosa kazi kwingine?” aliongea Afande Maswe kwa masikitiko kisha akamwagiza amuachie Hadija baada ya kumaliza kumhoji anayotaka.
“Sawa afande, ahsante” alisema Ndilana bila kujibiwa neno na Afande Maswe.
Ilikuwa yapata saa mbili na robo wakati Hadija anaingizwa ofisini kwa Inspekta Ndilana na kuachwa peke yao. Ndilana akamfanyia utaratibu wa chai kisha wakawa wanaangaliana huku wakiwa na vikombe vyao vya chai mkononi.
“Ahsante bebi, maana sijui umewaambia nini, nimeogopwaje? Alianza Hadija kwa maneno yake ya kishangingi.
“Mnh! Toka afande hadi bebi?” alijiuliza Ndilana kichwani bila kutoa sauti ila usoni alionekana kutabasamu kidogo kisha akarudi katika uso wa kazi.
“Sikiliza Hadija, ukinipa ushirikiano nitakuachia na nitakusaidia katika tatizo la Alice. Ukinidanganya kidogo tu urafiki wetu unakufa hapa hapa. Sawa?”
“Sawa”
“Unaitwa nani?” aliuliza Ndilana swali ambalo lilimfanya Hadija atabasamu.
“Jamani? Hujui jina langu?”
“Unaitwa nani?” aliuliza tena Ndilana akiwa kamkazia macho Hadija
“Hadija Mashushu” alijibu Hadija kwa urahisi.
Inspekta Ndilana aliinuka ghafla na kumwangalia kwa macho makali Hadija na kumfanya Hadija aingiwe na hofu..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nawaita wakurudishe Urafiki, halafu tusijuane kuanzia sasa. Naona unaanza kunizoea vibaya” aliongea Ndilana akizunguka kwenye meza yake kutaka kutoka. Hadija akamdaka mkono, Inspekta Ndilana akasimama akibaki anamwangalia.
“Nimekosa nini afande?”
“Nilikwambia kuwa ukinidanganya kidogo tu urafiki wetu unakufa hapo hapo, nawe jibu la swali la kwanza tu umenidanyanya”
“Kaa tafadhali, naitwa Hadija Ayub Mwinyimvua. Ila wamezoea kuniita Hadija Mashushu na ndiyo maana kote ninapoenda na hata kule Urafiki niliandikisha hilo hilo Hadija Mashushu”
Inspekta Ndilana akarudi kukaa sehemu yake na kuliandika jina kamili la Hadija. Kisha akainua uso kumwangalia.
“Hili ni onyo la mwisho”
“Sawa”
“Unaishi wapi?”
“Sinza Madukani”
“Unafanya biashara gani?”
“Naleta bidhaa mbalimbali toka Dubai, Thailand na China”
“Ulikamatiwa wapi?”
“Kwa Salome, ila walinichukua hadi kwangu madukani kupapekua”
“Unaishi na nani?”
“Kwa sasa niko peke yangu ila nina bwana mwarabu huwa anakuja kwa msimu”
“Kwanini unapenda kuwa kwa Salome wakati una kwako?”
Swali hili lilimfanya Hadija akae kimya kwa muda akijiuma uma huku Inspekta Ndilana akimkazia macho.
“Kumbuka makubaliano yetu. Hutaki kujibu?” aliuliza tena Ndilana
“Kusema kweli nikiwa kwa salome ndiyo nakuwa huru kuvaa ninachotaka, kunywa pombe na hata kutoka na marafiki ila kule siwezi kwa kuwa najulikana kama niliyeishika dini kutokana na mavazi ninayovaa na hata aina ya maisha ninayoishi. Na sifanyi hivyo kwa nia mbaya ila bwana ‘angu akija kuna watu wanamwambia maneno maneno kama unavyojua tena waswahili tulivyo” alijieleza Hadija kwa kusita sita.
“Kwa hiyo ulienda Kilwa na Alice na mkakaa miezi hiyo mitatu ili mjiachie, sivyo?” aliuliza Ndilana kiwivu wivu.
“Hapana nilikuwa siko vizuri kutokana na kugombana na bwana ‘angu, unajua waarabu huwa hawapendi sana ndugu yao akiwa na uhusiano wa kimapenzi na mswahili kwa hiyo yalizuka maneno maneno yaliyonikosesha raha ndipo nikaamua kwenda sehemu ambapo hataweza kupahisi ili niweze kutuliza kichwa changu”
“Wakati Alice anakamatwa, we ulikuwa naye?”
“Ndiyo”
“Ilikuwaje?”
Hadija alijiweka vizuri kisha akaanza kuhadithia…
“Watu wengi pale Kilwa walikuwa wakijiuliza kuwa tuko kule kwa shughuli gani kutokana na kukaa tu hotelini na kuzunguka huku na kule kufurahia maisha. Kwanza walidhani kuwa tumeenda kujiuza kwa wazungu wanaoenda kule kutalii, lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda hawakuona dalili zozote za sisi kuwa makahaba kwa kuwa hatukuwa tukichangamkia kabisa wanaume. Na uzuri wenyewe kila mtu alikuwa na matatizo yake, mimi ya bwana ‘angu na Alice ya mzazi mwenziye.
Wakawa wakiendelea kuhisi hili na lile kama ilivyo kawaida yetu waswahili, kupumzika waende wazungu tu, tukienda waswahili wenzao inakuwa nongwa. Baada ya habari za uwepo wetu kuendelea kuvuma tukahisi kuwa tunafuatiliwa na askari kwa kuwa kuna watu walikuwa wakituvaa kutuuliza mambo mawili matatu ya kutuchimba
Siku hiyo jioni tulikuwa tunaogelea, baada ya hapo tukawa ufukweni tukinywa na kupiga stori, mara wakatokea jamaa watatu na mwanamke mmoja. Wakajitambulisha kuwa ni askari kishwa wakasema kuwa wanamtaka Alice kituoni na tulipofika kule wakasema kuwa anatuhumiwa kwa mauaji ya Adrian Zayumba na ndipo wakamleta huku na mimi nikarudi.”
“Ulikuwa unamjua marehemu kabla umauti haujamfika?” aliuliza Inspekta Ndilana
“Ndiyo, mara nyingi alipokuwa akitoka na Alice tulikuwa tunatoka wote” alijibu Hadija
“Unaweza kumuelezeaje marehemu Adrian?”
“Marehemu hazungumzwi kwa mabaya lakini kusema ukweli Adrian alikuwa Malaya ila tu tulikuwa tunashindwa kumwambia Alice kwa kuwa alikuwa kama kipofu wa mapenzi” alisema Hadija akionekana kuwa na uhakika na anachokisema.
“Unaweza kufafanua?”
“Alikuwa hashindwi kumtaka Salome au mimi wakati Alice katoka kidogo kama kwenda msalani. Kuna siku tulitoka naye kwenda Bagamoyo kisha tukalala hoteli moja, usiku akamtoroka chumbani Alice tukamfuma anatoka bafuni na msichana mwingine. Ila tulikuwa tunamsema tu mwenyewe bila kumwambia Alice kwa kuogopa kumuumiza kwa kuwa alikuwa anampenda sana”
Ndilana alishusha pumzi akimwangalia Hadija huku akijisemea moyoni “kwa ulivyo mwepesi atakuwa kakukosa wewe?” kisha akamuuliza…
“Unadhani marehemu alikuwa na maadui?”
“Uwezekano wa marehemu Adrian kuwa na maadui ni mkubwa sana kwa kuwa hata huyo msichana tuliyemfuma naye wakitoka bafuni, mchana tulimuona na jamaa yake. Hatujui walitongozana saa ngapi hadi wakutane kumalizana kwa mtindo ule. Sasa hapo mwanamme wa yule dada angejua, siyo uadui kweli?”
Inspekta Ndilana alitikisa kichwa kuonesha kukubaliana na mawazo ya Hadija, hali iliyomfanya Hadija apate nguvu ya kutupa karata yake…
“Ndiyo maana najua rafiki yetu hana kosa lolote na anastahili kuwa huru” aliongea Hadija.
“Mliwahi kumwambia chochote Alice kuhusu tabia ya Adrian baada ya Alice kuachana na Adrian?” Inspekta Ndilana alitupa swali la kizushi
“Kwa kweli tulimwambia, maana baada ya kumfumania Adrian tena wakati akiwa na ujauzito, Alice alikosa raha sana na akakonda vibaya. Ikabidi tumwambie ukweli kuwa aangalie tu afya yake na ya mtoto kwa kuwa Adrian ni Malaya mbwa, na tukamueleza mengi ambayo hakuyajua. Japo alitulaumu kwa kuchelewa kumwambia ila alituelewa na mwenyewe akakiri kuwa hata tungemueleza kipindi kile wako wote asingekubali”
Wakati Ndilana akitafakari huku akiangaliwa na Hadija, mlango ulifunguliwa ghafla akaingia Koplo Asha na kusimama kwa muda akiwaangalia. Hadija aligeuka kumwangalia kisha akaendelea kuangalia mbele alipo Inspekta Ndilana wakati Ndilana akiendelea kumwangalia Koplo Asha.
Koplo Asha akaguna na kugeuka kutaka kutoka nje, Inspekta Ndilana akamsimamisha.
“Una shida gani koplo Asha?”
“Endelea tu naona uko na mgeni…”
Kabla Inspekta Ndilana hajasema kitu, Koplo Asha alikuwa keshatoka na kuubamiza mlango akiwaacha Hadija na Inspekta Ndilana wakiangaliana.
“Hadija”
“Abee”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ulikuwepo wakati Alice anapata taarifa ya kifo cha Adrian Zayumba”
“Ndiyo”
“Hebu nielezee ilikuwaje, kumbuka kinachotufanya tuendelee kuwa marafiki ni ukweli wako tu”
Hadija akaanza kujieleza….
“Kwa kweli siku hiyo, Alice alifika kwa Salome asubuhi na mimi nikiwepo. Alionekana kama aliyekosa amani, tukamhoji sababu akatueleza kuwa alipanga kwenda kumuua Adrian ili amchukue mtoto wake. Tukamkalisha chini na Salome tukaongea naye kwa kirefu sana na kumuomba awe mvumilivu na Mungu atampa haki yake. Baada ya maongezi marefu, Alice akawa kama ameanza kurudi katika hali yake ya kawaida.
Kama baada ya masaa mawili hivi, sikumbuki ilikuwa ni saa ngapi, Alice akapigiwa simu na wakili wake Hamisi Mzee Pembe. Ilikuwa ni dakika chache baada ya kuiwasha kwa kuwa toka anafika pale simu yake ilikuwa imezimwa. Alipoipokea alisikiliza kidogo na kuanza kushtuka kisha akaanza kujitetea kuwa siyo yeye aliyemuua Adrian Zayumba.
Baada ya kumaliza kuongea na simu akatuambia kuwa wakili wake kampigia kumlaumu eti kwa nini alienda kumuua Zayumba. Tukamuuliza yeye kama wakili ni kwanini akulamu moja kwa moja bila kukuuliza? Akasema hata yeye anashangaa ila anajua ni kwa sababu alitoroka nyumbani kwa lengo la kumuua Zayumba.
Tuliongea kwa kirefu, akasema kuwa wakili wake kamshauri kuwa azime simu na atafute sehemu ya kwenda hadi mambo yatakapotulia ndipo arudi ila atakapokuwa awe anampigia simu kujua mambo yanaendeleaje. Ndipo nikaamua kwenda naye safari yangu ya Kilwa”
Inspekta Ndilana akabaki anamwangalia Hadija kama aliyeishiwa na maswali huku Hadija akijitahidi kumbembeleza Ndilana amsaidia yeye pia amsaidie kumtoa Alice katika kesi inayomkabili na yuko tayari kufanya chochote atakachotaka Inspekta Ndilana.
“Wewe kuanzia sasa nakuachia huru ila uwe makini na nyendo zako na kuhusu Alice, ukitoka hapa katafute wadhamini wawili wa uhakika na uje nao hapa kabla ya saa saba”
Hadija alikurupuka na kumbusu Inspekta Ndilana mdomoni kama aliyepagawa kiasi cha kumpakaza mate kwenye midomo yake. Ndilana akawahi kumzuia na kumrudisha alipokaa.
“Samahani afande, nilizidiwa na furaha”
“Samahani nini, sema tu umalaya unakusumbua” alimjibu kimoyo moyo kisha akamjibu kwa sauti
“Hakuna tatizo ila jitahidi kukontroo furaha zako. Ila nina swali moja la mwisho”
“Uliza tu afande”
“Alice ana bwana mwingine?”
Hadija alimwangalia Inspekta Ndilana kwa muda kisha akamjibu kwa kifupi “Hana”
“Sawa, kwa muda huu asianzishe mahusiano yoyote hadi kesi itakapokwisha ili asije kuingia kwenye matatizo mengine.”
“Afande umekolea nini?” alitania Hadija huku akionekana kuwa hafurahishwi na kitendo cha Ndilana kumuulizia ulizia Alice
“Wewe si una mwarabu Hadija? Ila nasema tu hivyo kwa ajili atakuwa nje kwa dhamana, sasa akiingiza mambo mengine kesi inaweza kumuwia ngumu hii” alijitetea Ndilana kwa hoja nyepesi
“Nimekuelewa afande”
Hadija aliachiwa huru akijua kuwa Inspekta Ndilana ndiyo kila kitu, wakati huo Inspekta Ndilana alikuwa akielekea ofisini kwa Afande Maswe. Na baada ya muda mchache afande Maswe alikuwa tayari kumsikiliza Inspekta Ndilana.
“Nimeamua kumuachia Alice kwa dhamana” Inspekta Ndilana alianza kumuelezea afande Maswe
“Kwanini?”
“Kutokana na uchunguzi wangu unavyoenda, nadhani nitapata vitu vingi sana endapo Alice atakuwa nje kuliko akiwa ndani”
Afande Maswe alimwangalia Inspekta Ndilana kwa muda kisha akamtupia swali
“Unavyodhani ameua yeye au hajaua yeye?
“Yote yanawezekana japo uwezekeno mkubwa zaidi kuwa aliuawa na mtu mwingine kwa wivu wa kimapenzi” alijibu Ndilana kwa ufasaha.
“Siyo kwamba umeona kuwa leo ntamuachia halafu utakuwa huna namna tena ya kumrudisha katika upelelezi wako? Afande Maswe aliongea jambo ambalo ndiyo ukweli wenyewe uliomsukuma Ndilana atake kumuachia Alice ka uharaka kiasi kile.
Inspekta Ndilana alijikuta akishindwa kuuficha mshangao wake mbele ya afande Maswe jambo lililomfanya afande Maswe atabasamu.
“Hata kama ndicho ulichokuwa unakiwaza umenifurahisha kwa kuwa unaonekana sasa unaanza kuzitumia akili zako badala ya kuzitumia kupatia mabibi mitaani. Haya fanya ulichoamua”
Inspekta Ndilana allitoa heshima yake kwa afande Maswe kisha akatoka akiwa hana hamu na mzee huyo.
“Huyu mzee sijui atakuwa mchawi” alijikuta akiwaza Inspekta Ndilana akielekea ofisini kwake ambapo aliagizwa Alice aletwe.
Alice aliingizwa ofisini kwa Ndilana akiwa kavalia suruari ya jeans iliyoukamana vilivyo mwili wake na fulana kubwa lakini nyepesi. Japo alionekana kuchoshwa sana na mazingira ya mahabusu, hali yake ngumu haikuweza kuufunika urembo wake aliojaaliwa.
“Karibu Alice”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alice alikaa kimya bila kujibu neno lolote akaketi sehemu aliyoonyeshwa na askari wa kike aliyemleta. Baada ya kuketi akabaki akimkodolea macho Inspekta Ndilana ambaye naye alikuwa akiduwaa kumkodolea macho kuanzia kwenye macho yake, akashuka hadi kwenye pua kisha kwenye midomo akaanza kuwazia namna Zayumba alivyokuwa akifaidi kuibusu.
“We ni mrembo sana Alice”
“Najua” alijibu Alice kwa ujeuri lakini Inspekta Ndilana hakuonekana kujali
“Nilikuwa na Hadija hapa, nikamuahidi kuwa nitakuachia kwa dhamana endapo ataleta wadhamini wawili wa uhakika”
Alice alishusha pumzi ndefu kama mtu aliyeshusha mzigo mzito sana kisha akajikuta akiropoka kwa kiingereza “thanks God” akimshukuru Mungu.
“Nimempa na sharti jingine….” Aliongea Ndilana maneno yaliyomfanya Alice ajiweke vizuri na kusikiliza kwa umakini.
“Usijihusishe na mahusiano ya mapenzi kwa sasa, usije kuingia matatani” aliendelea Inspekta Ndilana kwa msisitizo ila badala ya Alice kuzingatia alionekana kupuuza
“Mimi mapenzi?! Wala sina shida nayo, na siyo kwa kipindi hiki tu ambacho nina kesi, hata baada ya hiyo kesi. Yaliyonikuta yanatosha. Ningekuwa na mambo hayo hata humu ningefanya, mbona kuna baadhi ya askari wanawachukua mahabusu wa kike na kuwarudisha alfajiri?” aliongea Alice bila mashaka yeyote.
Maneno ya Alice yalimshtua sana Inspekta Ndilana siyo tu kwa kuwa Alice ameonyesha kuwa ni mgumu kiasi gani lakini hizo tuhuma kuwa kuna askari ambao wanajirusha na mahabusu ilikuwa ni habari mpya kwake.
“Unasema?” aliuliza kama ambaye hajasikia vyema
“Kwani wewe hujui mnayofanya humu?”
“Mimi ni ofisa, ni vigumu sana kujua vitu kama hivyo tena ambavyo ni kinyume na taratibu za jeshi la polisi. Imekuwaje leo unaongea na mimi hivi Alice? Siku ya kwanza ulikuwa hutaki kuongea kabisa”
“Nilitembelewa na Hadija, akanieleza kuwa wewe ni mtu mzuri, huna matatizo. Na hata kuhusu dhamana aliniambia lakini sikumuamini kwa kuwa nilidhani ananipa moyo” alisema Alice akionyesha kuwa na uhakika huku Inspekta Ndilana akishangilia kimoyo moyo kwa kuwa alifagiliwa.
Baada ya maongezi yale Alice alirudishwa rumande na Inspekta Ndilana akitoka maeneo ya kazini lakini aliacha maagizo kuwa wakija wadhamini wa Alice aruhusiwe ila awe anaripoti mara mbili kwa wiki.
**********************************
Inspekta Ndilana alikuwa amebakiza masaa kadhaa na siku tatu za kumtafuta muuaji wa Adrian Zayumba. Njia iliyobaki ni kufanya upya mahojiano na watu wa karibu na Zayumba ili kujua kuona kama anaweza akapata popote pa kuanzia.
Mtu wa kwanza aliyemfikiria kumhoji upya alikuwa ni Shabani Kibope, huyu jamaa alikuwa karibu sana na marehemu Adrian Zayumba hasa masaa ya jioni kwa kuwa Kibope ni mwajiriwa wa serikali. Ndilana akawasha gari lake hadi Tegeta anapoishi Kibope.
“Mlifahamiana vipi na Adrian Zayumba?” lilikuwa ni swali la kwanza baada ya Ndilana kumpata Shabani Kibope na kukaa sehemu kwa ajili ya mahojiano.
Swali la Ndilana lilionekana kumshtua sana Kibope, alionekana wazi kuwa anajipanga kujibu kwa tahadhari ili asije akajikoroga. Inspekta Ndilana alivyoona hivyo akajua kuwa hawezi kupata maelezo yeyote ambayo yatamsaidia katika upelelezi wake, akatumia akili ya haraka haraka. Inspekta Ndilana akacheka sana kwa ghalfa kisha akapiga funda la bia yake iliyokuwa mezani wakati Kibope akiwa anamwangalia kwa mshangao.
“Nimekuitia pombe wewe, unadhani kila muda watu wanakuwa kazini? Kesi ishafungwa ile muuaji kakamatwa tayari. Hebu lete stori” aliongea Ndilana akionyesha kweli mwanzoni alikuwa akifanya mzaha.
Pamoja na maneno yale, bado Kibope alikuwa akinywa kwa tahadhari kubwa huku akichagua maneno ya kuongea na Ndilana. Muda wote alikuwa akijiuliza iweje askari afunge safari huko alikotoka amfuate kwa ajili ya pombe tu wakati hawana ukaribu wa aina yeyote zaidi ya kuwa aliwahi kumhoji kuhusiana na mauaji ya rafiki yake Adrian Zayumba?
Baada ya kupata bia mbili tatu, Ndilana akajifanya amekolea pombe akaenda chooni akijiyumbisha kidogo na aliporudi akabadilisha maongezi.
“Bwana kuna demu mmoja nilimuona mitaa hii, ndiyo nilikuja kumvizia nikaona nikutafute unipe kampani kidogo” Ndilana aliongea maneno ambayo yalimgusa kidogo Kibope, akajiweka sawa na kuonekana akianza kuhema kawaida.
“Demu gani huyo?”
“Anakaa mitaa ya nyuma hapo, anaitwa Hamisa”
“Dah! Mtoto mchoyo kweli yule! Si yule anayefanyia kwenye duka la dawa za mifugo pale Kijitonyama?” aliuliza Kibope kwa shauku. Inspekta Ndilana akajua kuwa mbinu yake imefanikiwa.
Wakati Inspekta Ndilana akimtafuta Kibope ili afanye naye mahojiano aliambiwa kuwa alikuwa mara nyingi anakaa na marehemu Zayumba kwenye baa ya ‘Simba kapakatwa’ maeneo ya Kijitonyama kumvizia huyo Hamisa lakini alipoenda maeneo yale hakumkuta ila aliambiwa wanakaa jirani na huyo Hamisa mitaa ya Tegeta.
“Ndiyo huyo kaka. Nilikuwa namfukuzia muda mrefu sana ila nilisimama kumfuatilia baada ya kubanwa sana na kazi”
“Yule kahama huku siku hizi yuko mitaa ya Mbezi ya Kimara. Mtoto anajifanya mgumu sana yule, hata marehemu alifukuzia sana pale akagonga mwamba” alijivua Kibope akimsukumia tuhuma marehemu Zayumba..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mimi kwangu alishajaa kwa vile nilitangaza ndoa, si unajua vipindi vya harusi kwenye runinga vinavyowahamasisha mabinti wa siku hizi kutaka kuolewa? Tatizo nikabanwa na kazi halafu namba yake nikaipoteza. Ila poa siyo ishu, nitamfuata kazini kwake kesho” alijieleza Ndilana akimjaza Kibope kwenye mtego wake.
Baada ya hapo zikaendelea pombe na hadithi za wanawake, lakini kwa kadiri hadithi zilivyokuwa zikiendelea ndivyo Kibope alivyokuwa akifunguka kuhusu mambo yake na marehemu Zayumba. Na hadi kufikia saa sita za usiku wakati Ndilana anaagana na Kibope tayari alikuwa kapata kila ambalo alilitaka.
Kutokana na maelezo ya Shabani Kibope, Adrian Zayumba alikuwa akipendwa sana na wanawake hasa walio katika ndoa ambapo kwa mujibu wa Kibope alivyomnukuhu marehemu, asilimia kubwa ya wanawake walio ndani ya ndoa huwa hawafurahi mapenzi. Hali hiyo ilimfanya Zayumba atembee na wake za watu wengi sana jambo ambalo lilimsababishia kutengeneza maadui wengi sana.
Kwa kuwa Zayumba hakuwa na kituo cha ushauri wa masuala ya ndoa, ilikuwa ngumu kwa mume na mke kuwasiliana naye kwa pamoja ili aonane nao wote na mara nyingi wanawake ndiyo walikuwa wakimtafuta sana.
Tatizo lilikuwa likianzia alipokuwa akiwaelekeza mambo ya kufanya ili kuboresha mahusiano yao ya kimapenzi katika ndoa na wao ikawa ngumu kutekeleza kwa sababu mamlaka yote ya ndani iko kwa waume zao, basi wakawa wakijikuta wanaangukia mikononi mwa Zayumba ili awaridhishe kimapenzi.
Kati ya stori nyingi alizopiga Kibope, Inspekta Ndilana alivutiwa na stori tatu za kuhusu wake za vigogo ambao walikuwa wakimpa hela nyingi sana Zayumba ili awaridhishe kimapenzi na mmoja wapo ni yule Salma aliyetajwa na Alice kwenye maelezo yake.
Nilitoka pale na wazo moja, kumtafuta Salma, na kutokana na maelezo ya Kibope haikuwa shida tena kumpata.
******************************
Kesho yake saa yake saa tatu asubuhi, gari la Inspekta Ndilana lilikuwa likiwasili kwenye hekalu moja la kifahari maeneo ya Masaki ambapo anaishi Salma na mumewe ambaye ni mkurugenzi wa taasisi fulani nyeti katika masuala ya fedha nchini. Zile siku tatu ambazo alitakiwa na Afande Maswe awe amempata muuaji ndiyo zilikuwa zimeanza rasmi.
“Salma ni mtu haswa…” alijikuta anajisemea moyoni baada ya kujieleza kwa walinzi, kutoa kitambulisho chake na kuitiwa Salma ambaye wakati huo alikuwa ndiyo anatoka ndani kuitikia wito.
Wakati anaitwa walinzi walimshauri ampe taarifa ‘mzee’ kuwa kuna askari kaja kumhoji lakini Salma aliwakataza kwanza hadi pale atakapojua kilichomleta huyo askari, baada ya sekunde chache ndipo Ndilana na Salma wakawa wanatazamana uso kwa uso huku pembeni yao akiwa amesimama mlinzi
“Karibu afande”
“Ahsante”
“Nikusaidie nini”
“Ungependa nikuhoji mbele ya mlinzi kijana wako?”
“Endelea tu” alidakia mlinzi aliyesimama pembeni ya Salma na kumfanya Salma ashtuke na kumwangalia kwa jicho kali.
“Si mmeshaona kitambulisho chake? Hebu rudi sehemu yako” alimshushua yule mlinzi mdaku.
Mdaku akaanza kutembea taratibu kwa aibu kurudi kwenye kibanda chao ambayo utadhani cha kufugia Nungunungu.
Inspekta Ndilana akabaki akimwangalia Salma wakati Salma anamwangalia mlinzi anavyoishia kiunyonge utafikiri toto dowezi lililonyimwa wali kwa jirani.
“Naweza kukaribia?”
Maneno ya Ndilana yalikuwa kama yamemshtua Salma usingizini.
“Ah! Karibu kiti” akamkaribishia kwenye viti vya maongezi vilivyo nje ya nyumba ya kigogo huyo, mumewe Salma. Wakaketi tayari kwa maongezi.
“Salma, tufanye maongezi yawe mafupi ili kuwaondoa mashaka walinzi na wewe upate chochote cha kumueleza mzee akikuuliza kuhusu ujio wangu. Lakini ufupi wa maongezi yetu utategemea ushirikiano wako, yaani wewe ndiye utakayeamua kuwa mambo yawe magumu kwako au yawe mepesi” alianza Inspekta Ndilana.
“Mbona sikuelewi afande?”
“Utanielewa tu Salma, nilikuwa nakutahadharisha kabla ya maongezi rasmi ili tusifanye mambo yakawa magumu kwako. Mrembo kama wewe hutakiwi kupewa misukosuko na ndiyo maana mzee akakupa maisha mazuri na kukuwekea walinzi” aliongea Ndilana akitabasamu huku Salma akishusha pumzi.
“Nimeelewa”
“Safi… Salma, najua kuwa uliwahi kuwasiliana na marehemu Zayumba kuhusu ushauri wa masuala ya kimapenzi, mkakutana katika hoteli maeneo ya mnazi mmoja ambapo alikuja na msichana wake na picha tunazo kutoka kwenye kamera za usalama za hoteli ile” alianza maelezo Ndilana huku Salma akionekana kuanza kuhemea juu juu.
“Najua pia kuwa mkaanza mahusiano ya mapenzi ukimpa Zayumba mahitaji yote ya msingi kiasi cha Zayumba kuamua kuachana na msichana wake. Na mkaendelea hadi ulipokuja kugundua kuwa Zayumba siyo mwaminifu ukaamua kuachana naye na kutulia kwenye ndoa yako” aliendelea kumuelezea akichanganya taarifa alizozipata toka kwa Alice na kwa Shabani Kibope.
“Niambie unataka nini tafadhali” aliuliza Salma akionekana kujawa na wasiwasi.
“Ulijuaje kama Zayumba siyo mwaminifu?”
Salma alikaa kimya kwa muda akijiuma uma huku Inspekta Ndilana akiwa amemkazia macho. Ukimya ulitawala kwa muda kisha Salma akajikohoza kidogo.
“Nakusikiliza Salma”
“Naomba nitakachokiongea kibaki kati yetu”
“Endapo utanieleza bila kuficha jambo, sitahitaji kuongea na mwingine yeyote ili kuujua ukweli lakini ukinificha utakuwa unanishawishi nitoe siri ili nipate ukweli, na endapo hutaniambia kabisa nitaondoka na wewe na yote tunayoyajua kuhusu wewe yatakuwa wazi kwa mumeo. Nadhani kusema kuna faida kubwa kuliko kuficha, au unaonaje?” Inspekta Ndilana alimwambia Salma maneno ambayo yalikuwa ni kama kisu kinachopita kwenye mfupa wake.
“Yote uliyosema ni kweli” alianza Salma
“Enhe, ulijuaje kama Zayumba siyo mwaminifu?” alikazia swali lake Ndilana
Salma akaanza kujieleza…
“Kuna rafiki yake Adrian Zayumba alikuwa pia akinitaka, akawa ananifuatilia kwa muda mrefu kupitia kwenye simu na mara nyingine tukiwa na marehemu na yeye alikuwa akisubiri muda Adrian akiwa anatuacha peke yetu naye anaanza mambo yake. Mimi sikumkubalia kwa vile niliona fika kuwa alikuwa ananitaka kwa kujua kama nini hela, ila lililonikera zaidi ni kwamba alikuwa akiniona kama Malaya hivi.
Baada ya kuona nina msimamo, akaanza kunieleza mambo aliyokuwa akiyafanya Zayumba ili nami nitoke naye kama kulipizia kisasi.
Ila kwangu mimi habari hizo nilizichukulia kama tahadhari kwangu kwa sababu dunia sasa hivi imeharibika, nikaona kuendelea na Zayumba kunaweza kunifanya nikambukizwa maradhi mwishowe nikaja kumuua mume wangu kwa maradhi wakati hana kosa lolote zaidi ya kuwa alikuwa hanitimizii haja zangu za ndoa ipasavyo” alimalizia kujieleza Salma
“Anaitwa nani huyo jamaa?”
“John Nkongolo” alijibu Salma kabla ya kumuelezea huyo jamaa kuwa ni mrefu, mwembamba anayefuga manywele marefu au maarufu kama ‘bunda’. Kisha akampa Ndilana namba ya simu ya Nkongolo.
“Uliwezaje kufanya yote haya wakati unalindwa kiasi hiki?” aliuliza Inspekta Ndilana akionekana kustaajabu mambo yaliyokuwa yakijiri..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kaka yangu mwanamke akiamua lake hazuiliki” alijibu akitabasamu kwa aibu.
Inspekta Ndilana alianza kumuuliza mfululizo maswali ambayo hayana kichwa wala miguu kwa muda mrefu hadi walinzi wakaanza kuingiwa na hofu wakawa wanapitapita. Hali ile ilimkosesha amani Salma na kutamani Ndilana aondoke haraka iwezekanavyo. Ndilana alipoiona hali ile ndipo akajua muda muafaka umefika.
“Unadhani ni sababu gani iliyosababisha kifo cha Zayumba?” Ndilana alimuuliza Salma kwa kumshtukiza
“Umalaya wake tu” alijibu Salma bila kujifikiria
“Unadhani ni nani atakuwa amemuua?”
“Kwa kweli siwezi kujua, ila atakuwa kakodiwa watu na waume wa wanawake zake”
“Kama ni wewe umepewa kazi ya kuchunguza kifo chake ungeanzia wapi upelelezi wako?” Inspekta Ndilana aliuliza swali la kijinga lakini lilibeba maana nzito sana nyuma yake.
“Kwa mwanamke wake wa mwisho”
“Unamjua mwanamke wake wa mwisho?”
“Hapana. Naomba uondoke, inatosha tafadhali” Salma aliongea akisimama huku akiwa kama anamsubiri Ndilana ainuke. Ndilana akainuka taratibu akitabasamu.
“Ukikumbuka chochote nipigie” Inspekta Ndilana alikuwa akiongea huku akitoa kadi yake ya mawasiliano na kumpa Salma. Salma anaipokea.
“Wakikuuliza waambie nimekuja kukuomba uniombee kwa mzee atufadhili kwenye klabu yetu ya mpira ya mtaani inayoshiriki ligi ya taifa. Ila nikihitaji ushirikiano wako nitakuja tena” Ndilana alimpa ushauri Salma.
“Yangu niachie mwenyewe na kuhusu kuja tena hapa nakuomba usije tena, nitakupigia kukupa namba yangu, ukihitaji chochote nipigie nitakuja ulipo”
“Chochote?” aliuliza Ndilana kwa mzaha na kumfanya Salma aishie kuguna tu.
***** ***** *****
“SIYO hasira, ni kwamba hatuhitaji tu tena huduma yako”
“Ndivyo unavyodhani? Hawa polisi hawana urafiki, sasa hivi wanajifanya kama hawana habari na wewe lakini ghafla wanaweza kukukamata na kukupeleka mahakamani na ukahukumiwa haraka haraka. Mimi nakuonea huruma kwa kuwa bado umri wako ni mdogo na hujaitumia kabisa elimu yako halafu uje kuishia jela”
Alice akakaa kimya kwa muda akitafakari, Wakili Pembe akamsogelea na kumshika begani
“Hebu kwanza niambie, ni nini kinaendelea kwenye kesi yako? Nataka tuimalize kesi hii halafu tufungue madai ya kumtaka mtoto kwa kuwa baba yake amekwishafariki”
Wakati akifanya hivyo Inspekta Ndilana ndiyo akawa anaingia kituoni na kukiona kitendo hicho, akawapita bila kuwasalimia japo aliwapita karibu kabisa.
“Wakili Rwehumbiza? Yeye kaniambia kuwa hamjakubaliana naye bado. Najua kwa sasa mna hasira kwa kudhani niliamua kuwakatalia wakati mnanihitaji ila mjue kuwa ilikuwa nje ya uwezo wangu. Kama mtaona yafaa mtanijulisha, niko tayari kuwasaidia.” Aliongea Wakili Pembe na kuwaacha kina Alice wamebaki kimya naye akaondoka.
“Hivi huyu baba anakutakia nini?” lilimtoka swali Mama Alice akimkazia macho Alice akamwangalia kwa muda Alice kisha akaingia ndani kuendelea na shughuli zake.
Siku iliyofuatia, Alice alikuwa anatakiwa kwenda kuripoti polisi kama masharti ya dhamana yake yanavyosema. Wakakutana asubuhi sana na Salome na Hadija kisha wakaongozana kuelekea kituoni ambapo walipofika kituoni askari wa zamu aliwaambia wamsubiri askari mwenye kesi, wakatoka nje na kukaa sehemu kumsubiria.
Wakati wanaendelea kumsubiri Inspekta Ndilana, aliwasili Wakili Hamis Mzee Pembe akaenda moja kwa moja walipokaa kina Alice, wakajikuta wanaguna wote watatu kwa pamoja kisha wakatazamana na kutabasamu.
“Alice”
“Abee”
“Naomba tuongee kidogo” aliongea Wakili Mzee Pembe akijisogeza pembeni.
Alice aliangaliana na wenzake kisha akainuka kumfuata wakili Pembe, wakaenda kusimama pembeni mbali kidogo na walipokaa kina Hadija.
“Usifanye hasira Alice, hii ni kesi ngumu sana kwako. Unapomsikiliza mama yako ujue mwisho wa siku wewe ndiyo utakaoenda jela” alianza kujieleza Wakili Pembe huku akimwangalia Alice kwa umakini.
“Ukikumbuka chochote nipigie” Inspekta Ndilana alikuwa akiongea huku akitoa kadi yake ya mawasiliano na kumpa Salma. Salma anaipokea.
“Wakikuuliza waambie nimekuja kukuomba uniombee kwa mzee atufadhili kwenye klabu yetu ya mpira ya mtaani inayoshiriki ligi ya taifa. Ila nikihitaji ushirikiano wako nitakuja tena” Ndilana alimpa ushauri Salma.
“Yangu niachie mwenyewe na kuhusu kuja tena hapa nakuomba usije tena, nitakupigia kukupa namba yangu, ukihitaji chochote nipigie nitakuja ulipo”
“Chochote?” aliuliza Ndilana kwa mzaha na kumfanya Salma aishie kuguna tu.
*********
Masaa mawili baadaye Inspekta Ndilana alikuwa ameshampata John Nkongolo na kufanya mahojiano naye lakini ilikuwa inaonekana kuwa umalaya tu ndiyo ulikuwa unamsumbua Nkongolo, hakuwa na taarifa zozote za kusaidia katika kumpata muuaji wa Zayumba.
Inspekta Ndilana alirudi ofisini kwake akiwa bado hajapata mwelekeo wa kumpata muuaji waAdrian Zayumba, na hata wazo la Salma ambalo lilionekana wazi lilitokana na hasira za kimapenzi kwa kuwa kwa mtu kama Zayumba ambaye alikuwa na wanawake wengi kwa wakati mmoja siyo rahisi kujua nani atakupa habari za kukusaidia.
Nje ya ofisi yake ikawa inasikika sauti ya Afande Maswe akiwasemesha maaskari japo hakuwa akiyasikia maneno yenyewe kwa ufasaha. Inspekta Ndilana akaamua kuwasha mahojiano ya Afande Maswe na Alice ayasikilize kuzugia muda ili hata afande akiingia ajue yuko katika kazi.
Mara mlango ukafunguliwa, Afande Maswe akaingia. Inspekta Ndilana akatoa heshima za kijeshi kisha akazima kifaa kilicho na mahojiano na kubaki kimya akimsikiliza afande wake.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kazi inaendeleaje inspekta?”
Inspekta Ndilana akamueleza afande Maswe kila kitu kilichojiri katika uchunguzi wake na hatua aliyofikia. Wakati wote huo Afande Ndilana alikuwa akimwangalia Ndilana kwa umakini mwisho akatabasamu.
“Walahu safari hii unaonekana kujituma, japo bado hujatumia akili yako na utaalamu wako wa upepelezi” alianza kuongea afande Maswe maneno ambayo yalionekana kumkera sana Inspekta Ndilana
Kwa juhudi ambazo alizifanya Ndilana, hakutegemea kama bosi wake angemwambia maneno kama yale ambayo aliyatafsiri kama dharau kwa juhudi zake alizozionyesha.
“Unajua Ndilana, kadiri unavyoutanuka na wigo wa upelelezi wako ndivyo unavyozidi kupotea, mwisho utajikuta una vitu vingi halafu huna pa kushika”
“Lakini afande, wewe si ndiyo uliniambia nitanue wigo wa upelelezi wangu ili niweze kufanikiwa?”
“Wewe hutanui wigo wa upelelezi unatanuka na wigo wa upelelezi, mwishowe utachanika msamba! Sikiliza dogo, nilichokukuta unakisikiliza na ulichoniambia ni hali mbili tofauti”
Ukimya ulitawala huku Ndilana akionekana wazi kuwa kachanganyikiwa, mwisho akapata kauli.
“Sijakuelewa afande, naomba unifafanulie”
“Una mahojiano na Alice, ukaenda kuchukua tena mahojiano na Hadija, ukamhoji huyo Kibope, ukaenda kwa Salma mwisho ukamalizia kwa huyo anayemtaka Salma. Wakati huo, mahojiano ya Alice bado hujayafanyia kazi na siku zimebaki mbili. Umekuwa kama mfa maji badala ya kuwa mweledi. Fanya kazi, shauri yako.”
Afande Maswe alimwambia Inspekta Ndilana kisha akaufungua mlango na kuondoka.
Inspekta Ndilana alikaa kwa muda akiwa kachanganyikiwa mwishowe akaamua kumfuata Afande Maswe ofisini kwake.
“Samahani afande, naomba unisaidie kunielekeza cha kufanya” alisema Inspekta Ndilana akimwangalia Afande Maswe kwa ukakamavu.
“Unataka nikusaidie nini kati ya mengi ambayo umenieleza? Mara zote mbona nimekusaidia hadi kumtoa yule dada kule urafiki…”
“Nahitaji unisaidie kunielekeza chochote ambacho utaona wewe kinafaa”
“Mahojiano yangu na Alice uliyasikiliza mara ngapi?” alianza kumuuliza Ndilana
“Zaidi ya mara tano afande”
“Hebu nihadithie toka mwanzo hadi mwisho”
Inspekta Ndilana akaanza kushuka maelezo kwa afande wake hadi mwisho kisha akabaki kimya akimwangalia Afande Maswe.
“Sawa. Kuna sehemu yeyote uliyokuwa unaandika vitu vilivyo kugusa?”
“Ndiyo afande”
“Hebu nione”
Inspekta Ndilana akatoka kwenda kuchukua kidaftari chake na kukileta kwa afande Maswe. Afande Maswe akakiangalia kwa muda kisha akatabasamu na kumwangalia Ndilana.
“Inspekta Jackson Ndilana”
“Naam afande”
“Kabla hujamkamata Alice ulikuwa unawaza kuwa huenda Alice alimuua Zayumba kutokana na chuki ya kuchukuliwa mtoto wake. Sivyo?”
“Ndiyo afande”
“Baada ya kumkamata na kuyasikiliza haya mahojiano inaonekana kuwa akilini mwako unawaza kuwa huenda ni chuki za mapenzi ndizo zimesababisha Zayumba auliwe, sivyo?”
“Ndiyo afande”
“Upelelezi wako wote unaangalia sababu za kuuliwa Zayumba na ndizo ambazo unazipata, lakini hutafuti nani aliyemuua. Sivyo?”
“Hapana afande, najua kuwa kwa kupata sababu ya kifo chake itakuwa rahisi kumpata muuaji” alijitetea Ndilana na kumfanya Afande Maswe acheke.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa si ushajua kuwa sababu ni chuki za kimapenzi, haya niambie muuaji ni nani?” Afande Maswe aliuliza swali ambalo lilimfanya Inspekta Ndilana abaki kama juha akimwangalia afande wake.
“Nimeelewa unamaanisha nini afande” alijibu Inspekta Ndilana kwa aibu.
“Haya nenda kamtafute muuaji, umebakiwa tu na siku mbili”
Inspekta Ndilana alitoka akiwa kama aliyechanganyikiwa.
Ikabidi anunue mzinga wa pombe kali, akala akashiba kisha akaanza kujidunga mipombe nyumbani kwake hadi akazima.
*********
Baada ya kutoka mahabusu, Alice alienda moja kwa moja nyumbani kwao. Alice alikuwa akiishi na mama yake na wadogo zake wawili wa kiume kwa kuwa baba yake alifariki wakati yuko kidato cha sita.
Siku ya pili tu baada ya kuachiwa toka mahabusu alipokea ugeni wa wakili Hamis Mzee Pembe aliyekuwa akitaka kujua maendeleo ya kesi ya Alice, kitendo hicho kiliwakera sana kwa kuwa walitumia muda mwingi sana kumuomba awasaidie wakati Alice kakamatwa lakini alikuwa akiweka vikwazo vya hapa na pale na mwishowe akawatajia malipo ya hela nyingi kama sharti la kusimamia hiyo kesi.
Alipoona hapati ushirikiano akatoa visingizio kadhaa na kudai kwa sasa yuko katika nafasi ya kusaidia, japo hawakuwa wamefanikiwa kumpata wakili mwingine, mama yake Alice alimwambia kuwa wameshapata wakili kwa hiyo hawahitaji tena msaada wake.
*****INSPEKTA NDILANA KACHANGANYIKIWA BAADA YA KUPEWA SIKU MBILI TU ZA KUMPATA MUUAJI. AKILI SI YAKE. KAAMUA KUNYWA POMBE HADI HOI! JE NI KIPI KITAENDELEA?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment