Simulizi : Kivuli
Sehemu Ya Tatu (3)
***** ***** *****
ALIPOONA hapati ushirikiano akatoa visingizio kadhaa na kudai kwa sasa yuko katika nafasi ya kusaidia, japo hawakuwa wamefanikiwa kumpata wakili mwingine, mama yake Alice alimwambia kuwa wameshapata wakili kwa hiyo hawahitaji tena msaada wake.
“Wakili Rwehumbiza? Yeye kaniambia kuwa hamjakubaliana naye bado. Najua kwa sasa mna hasira kwa kudhani niliamua kuwakatalia wakati mnanihitaji ila mjue kuwa ilikuwa nje ya uwezo wangu. Kama mtaona yafaa mtanijulisha, niko tayari kuwasaidia.” Aliongea Wakili Pembe na kuwaacha kina Alice wamebaki kimya naye akaondoka.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hivi huyu baba anakutakia nini?” lilimtoka swali Mama Alice akimkazia macho Alice
Mama Alice akamwangalia kwa muda Alice kisha akaingia ndani kuendelea na shughuli zake.
Siku iliyofuatia, Alice alikuwa anatakiwa kwenda kuripoti polisi kama masharti ya dhamana yake yanavyosema. Wakakutana asubuhi sana na Salome na Hadija kisha wakaongozana kuelekea kituoni ambapo walipofika kituoni askari wa zamu aliwaambia wamsubiri askari mwenye kesi, wakatoka nje na kukaa sehemu kumsubiria.
Wakati wanaendelea kumsubiri Inspekta Ndilana, aliwasili Wakili Hamis Mzee Pembe akaenda moja kwa moja walipokaa kina Alice, wakajikuta wanaguna wote watatu kwa pamoja kisha wakatazamana na kutabasamu.
“Alice”
“Abee”
“Naomba tuongee kidogo” aliongea Wakili Mzee Pembe akijisogeza pembeni.
Alice aliangaliana na wenzake kisha akainuka kumfuata wakili Pembe, wakaenda kusimama pembeni mbali kidogo na walipokaa kina Hadija.
“Usifanye hasira Alice, hii ni kesi ngumu sana kwako. Unapomsikiliza mama yako ujue mwisho wa siku wewe ndiyo utakaoenda jela” alianza kujieleza Wakili Pembe huku akimwangalia Alice kwa umakini.
“Siyo hasira, ni kwamba hatuhitaji tu tena huduma yako”
“Ndivyo unavyodhani? Hawa polisi hawana urafiki, sasa hivi wanajifanya kama hawana habari na wewe lakini ghafla wanaweza kukukamata na kukupeleka mahakamani na ukahukumiwa haraka haraka. Mimi nakuonea huruma kwa kuwa bado umri wako ni mdogo na hujaitumia kabisa elimu yako halafu uje kuishia jela”
Alice akakaa kimya kwa muda akitafakari, Wakili Pembe akamsogelea na kumshika begani
“Hebu kwanza niambie, ni nini kinaendelea kwenye kesi yako? Nataka tuimalize kesi hii halafu tufungue madai ya kumtaka mtoto kwa kuwa baba yake amekwishafariki”
Wakati akifanya hivyo Inspekta Ndilana ndiyo akawa anaingia kituoni na kukiona kitendo hicho, akawapita bila kuwasalimia japo aliwapita karibu kabisa.
“Habari za leo afande” Alice alimsalimia Inspekta Ndilana aliyevalia kiraia.
“Nzuri” aliitikia Ispekta Ndilana akiishia kuingia kituoni bila kumwangalia.
Alice akamsindikiza kwa macho Inspekta Ndilana kisha akamgeukia Wakili Hamis Mzee Pembe ambaye muda wote alikuwa akimwangalia.
“Unaona Alice, polisi hawana urafiki. Acha nikusindikize”
Hadija na Salome wakawa wamefika walipo Alice na Wakili Hamis Mzee Pembe, Alice akawageukia kisha akamgeukia Wakili Pembe.
“Ngoja nikasikilize kwanza”
Wakatoka wakiongozana wote watatu hadi ofisini kwa Inspekta Ndilana ambaye asubuhi hiyo alikuwa akionekana kuwa na macho mekundu sana na uso wa pombe.
Walimchangamkia sana hasa Hadija lakini hakuonyesha ushirikiano wa aina yeyote kabla ya kuwatoa nje na kubaki na Alice.
“Nitakurudisha ndani Alice” alianza kuondea akimkazia macho Alice.
Maneno ya Inspekta Ndilana yalimfanya Alice apate hofu ghafla na kupoteza tabasamu lake usoni, akaanza kutetemeka kwa woga
“Tafadhali afande, naomba usifanye hivyo niko tayari kufanya lolote lakini usinirudishe ndani” alisema Alice kwa mashaka huku Inspekta Ndilana akiwa bado amemkazia macho.
“Umekumbuka nilikwambiaje kuhusu kuanzisha mahusiano?”
“Mbona sijaanzisha uhusiano wowote afande?”
“Pale nje ulikuwa unafanya nini?”
“Yule ni wakili aliyekuwa anaisimamia kesi yangu wakati marehemu ananidai mtoto”
Inspekta Ndilana akabaki kimya akimwangalia Alice. "Kweli tena afande, yule ndiye wakili Hamis Mzee Pembe”
“Ilikuwaje asije wakati uko ndani aje wakati umetoka?” aliuliza Inspekta Ndilana akimkazia macho Alice. "Nikuja jana kusema yuko tayari kutusaidia, mama akamkatalia akaondoka ndipo akaja hapa leo”
“Mlipata hela ya kumlipa?”
“Hapana, anasema kipindi kile alikuwa katingwa na matatizo ya kifamilia ila sasa yuko sawa”
“Mlifahamiana vipi?”
Alice alianza kujieleza…..
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Adrian Zayumba alipofungua kesi ya kudai mtoto na habari kuandikwa kwenye magazeti watu wengi walijitokeza siku ya kesi kuanza kusikilizwa. Wakati natoka kwenye kesi Wakili Pembe alinifuata na kudai kuwa anataka kunisaidia katika kesi ile.
Nilipomwambia kuwa sina uwezo wa kumlipa akaniambia amejitolea tu kunisadia bila malipo yeyote kwa kuwa amehisi kuwa naweza kudhulumiwa haki yangu. Baada ya mashauriano na mama nikamkubalia na toka hapo akawa mstari wa mbele kwenye kila jambo linalohusu kesi.
Mara zote mama alikuwa akimtilia mashaka kutokana na moyo aliokuwa akiuonyesha akawa anadhani labda nina mahusiano naye ya kimapenzi lakini namficha ila baadaye akaona kuwa hatukuwa na ukaribu wowote zaidi ya masuala ya kesi tu.
Tukawa karibu sana na hata baada ya kesi tukawa tunawasiliana japo siyo mara nyingi kama ilivyokuwa wakati wa kesi. Mara nyingi alikuwa akiniuliza kama bado nina hasira na Zayumba nikawa namwambia kuwa lazima nimfanye kitu kibaya kiasi kwamba hata akipona asinisahau katika maisha yake yote.”
“Siku ambayo ulitoka kwa nia ya kwenda kumdhuru Zayumba ulimwambia chochote?” Baada ya kukaa kimya kwa muda akisikiliza, Inspekta Ndilana akaanza kumpiga tena maswali Alice.
“Hapana, hakuna yeyote aliyekuwa anajua”
“Kuna mtu kwenu alimjulisha?”
“Mama anavyodai, nilipotoroka na wakaona sipokei simu yeyote wala kujibu ujumbe walimpigia kujua kama anajua nilipoenda, akadai kuwa hana habari”
“Mama yako alipata wapi taarifa kuwa Zayumba ameuawa?”
“Alipewa naye..”
“Alimwambiaje?”
“Alimwambia kuwa mwanao keshamuua Zayumba, na ndicho kitu kinachomfanya mama amchukie hadi leo?”
“Na wewe si ulisema ulipewa naye?”
“Ndiyo”
“Wakati unatoka mahabusu ulimtaarifu?”
“Hapana”
“Alijuaje?”
“Hicho ndicho kitu ambacho kilinishangaza, na kilichonishtua zaidi anajua pia kuwa tulitafuta wakili mwingine na bado hatujafikia makubaliano naye.”
“Ulimwambia kama unakuja kuripoti?”
“Hapana, nimeshtukia tu yuko hapa na akaniambia kuwa anisaidie kwa kuwa mnaweza kunigeuzia kibao muda wowote, mkanifungulia mashtaka na nikahukumiwa haraka”
Inspekta Ndilana akakaa kimya kwa muda akionekana kutafakari maneno ya Alice. Ghafla akashtuliwa na mlango uliogongwa na kuingia Koplo Asha na kutoa heshima.
“Jambo afande”
“Jambo”
“Afande Idrisa anataka faili la kesi ya mauaji ya Adrian Zayumba”
“Afande Idrisa?” aliuliza Inspekta Ndilana kwa mshtuko kwa kuwa pamoja na kuwa SSP Idrisa ni mkubwa wake kicheo lakini hahusiki chochote na mwenendo wa kesi ya Adrian Zayumba. Wakati Inspekta Ndilana akijifikiria akaingia Afande Idrisa, wote wakatoa heshima.
“Koplo Asha, mpeleke huku binti mahabusu kesho apandishwe mahakamani. Inspekta Ndilana nipe faili lake. Kesi ndogo tu inachukua muda namna hii wakati mtuhumiwa unaye?” aliongea afande Idrisa.
Alice akachukuliwa mkuku mkuku na Koplo Asha kupelekwa mahabusu wakati afande Idrisa akiondoka na faili la kesi na kumuacha Inspekta Ndilana ameduwaa.
Yalipita masaa mawili Inspekta Ndilana akijiuliza maswali mengi bila kujua afanye nini. Kikubwa alijua kuwa ndiyo amepoteza rasmi kazi yake kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku ya mwisho aliyopewa kumtafuta muuaji kwa kuwa alishindwa kuthibitisha kuwa Alice anahusika. “Sasa imekuwaje tena?” alijiuliza kila mara.
Ghafla mlango ulifunguliwa wakaingia Hadija na Salome.
“Imekuwaje afande?”
“Hata mimi sielewi” alijikuta akiropoka Inspekta Ndilana.
Ukimya ukatawala kwa muda kisha Inspekta Ndilana akapata wazo jipya akainuka.
“Mnisubiri nje”
Salome na Hadija wakatoka nje wakiwa wamechanganyikiwa wasijue la kufanya.
Inspekta Ndilana alitoka moja kwa moja kuelekea kwa Afande Maswe. Msaidizi wa afande Maswe alimzuia kuingia kumuona kwa vile alidai ana kazi nyingi. Inspekta Ndilana alipatwa na hasira akawa hajali tena kwa vile alijua keshapoteza kazi mpaka muda ule, akaamua kuingia kinguvu.
..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Afande Maswe ambaye alikuwa akisoma tu gazeti akashtuka kumuona Inspekta Ndilana akiingia kama anayegombana na mtu.
“Vipi?”
Inspekta Ndilana akatoa heshima na kuanza kumuelezea kilichotokea Afande Maswe ambaye alikuwa anamsikiliza kwa umakini.
“Ulikuwa umefikia wapi?”
Inspekta Ndilana akaanza kumuelezea Afande Maswe kuhusu mwenendo mzima wa Wakili Pembe na kumtupia zigo wakili huyo kuwa anahisi anahusika kwa namna moja au nyingine na tukio zima la mauaji ya Zayumba kwa vile mienendo yake inaacha maswali mengi sana.
“Nilikuwa nashangaa ni kwanini hukuliona hilo toka mwanzo, na ndicho ambacho kingenifanya nikuvue cheo. Ukisikiliza tu vizuri mahojiano na Alice lazima utashawishika kufuatilia miendendo ya huyo wakili wake. Ya hapa niachie mimi, wewe pata namba ya simu ya Alice na aliyokuwa akiitumia wakili wake kisha ukachukue rekodi zote kwenye kitengo chetu”
Inspekta Ndilana alitoka pale akijiona mwepesi kama aliyetua gunia la kilo mia. Nje akawaambia Salome na Hadija kuwa wasiwe na wasiwasi. Kila kitu kitaenda sawa, wakapumzike tu nyumbani.
“Hapana sisi hatutaondoka hadi tujue hatma ya shoga yetu”
Inspekta Ndilana akatoka pale akiwa na matumaini kibao.
Huku nyuma Afande Maswe aliamrisha faili la kesi lirudishwe kwake na akafutwa zuio la kuachiwa Alice lililowekwa na SSP Idrisa. Na Inspekta Ndilana aliporudi kuleta ripoti akapewa tena uhuru wake wa kuendelea na uchunguzi, kitu cha kwanza akaenda kumtoa Alice.
Alice alipoletwa tena kwa Inspekta Ndilana baada ya kutolewa mahabusu alikuwa tayari macho yameshamvimba kwa kulia. Inspekta Ndilana akajikuta akimwangalia kwa huruma Alice ambaye kwa ukweli ni mrembo wa ukweli.
“Pole Alice”
“Mimi hata sielewi tena afande”
“Unaweza kuniita tu Jackson. Unajua Alice hii kesi yako inaelekea kuwa inawagusa watu wengi sana na ndiyo maana nikakwambia kuwa uwe makini katika kutembea na usianzishe kabisa uhusiano mpya katika kipindi hiki.” Alimwambia Alice kwa upole
“Yaani afan.. ah Jackson, mimi nafuata kila ambacho unaniambia kwa kuwa naamini wewe ndiye utakayenisaidia” alisema kwa upole Alice akionekana kumaanisha anachokisema.
“Ukifanya kinyume tu mimi nitajua. Na kwa siku hizi tatu inapidi uwe unaripoti kila siku asubuhi”
Alice alionekana kukosa raha baada ya kuambiwa suala la kuripoti mfululizo, machozi yakaanza kumtoka upya, ikabidi Inspekta Ndilana awaite Salome na Hadija awaelezee upya kile alichomwambia Alice.
“Sisi tunaamini kuwa unatusaidia afande, maana hali ya asubuhi ilikuwa ni mbaya sana, na bila juhudi zako Alice angekuwa bado yuko ndani” alisema Hadija
“Alice nampenda sana, siwezi kumuachia adhurike” aliropoka Inspekta Ndilana kabla ya kurekebisha kauli “namaanisha napenda atendewe haki” alirekebisha na kuwafanya Salome na Hadija wachekee chini chini.
Alice aliondoka na rafiki zake, Hadija na Salome huku nyuma wakimuacha Inspekta Ndilana akifanyia kazi taarifa za simu kabla ya kuzipeleka kwa Afande Maswe.
Katika taarifa inaonekana kuwa baada ya kupigiwa simu na namba ya mama yake Alice, saa kumi na mbili za asubuhi, wakili Pembe alikuwa akiwasiliana na namba moja mara nyingi kati ya muda huo na saa mbili asubuhi, akaja kuwasiliana nayo tena kati ya saa tatu na saa nne na saa sita dakika chache kabla ya kuwasiliana na Alice.
Inspekta Ndilana pia akasoma jumbe zote fupi walizokuwa wakitumiana Alice na wakili Pembe ambazo zilionyesha kuwa wakili Pembe alikuwa anamsukuma Alice ili ajione kuwa ni mhusika wa mauaji hayo.
Inspekta Ndilana akaandaa taarifa na kumpelekea afande Maswe ila ilibidi asubiri kwa muda kwa kuwa afande alikuwa katika kikao kizito na SSP Idrisa ambapo mara kadhaa afande Maswe alisikika akifoka kwa hasira. Alipotoka mule ndani SSP Idrisa alionekana kuwa na macho mekundu sana na alitoka kwa hasira kama nyati aliyejeruhiwa.
Inspekta Ndilana alipoingia alimkuta afande Maswe akiwa na chupa kubwa ya maji akiinywa huku akionekana macho mekundu kama aliyetoka kupuliza moto wa kuni. Kabla hajasema chochote afande Maswe alimuwahi.
“Inspekta Jackson Ndilana” aliita afande Maswe kama mwendesha mashtaka anayemuapisha mtu mahakamani.
“Naam afande”
“Kwanini uliamua kumuachia Alice mara ya kwanza?”
“Nilihisi huenda kuna watu wako nyuma ya hii kesi kwa hiyo nikajua akiwa nje tutapata mengi zaidi yatakayosaidia katika kesi kuliko akiwa ndani” aliongea Inspekta Ndilana kwa uhakika.
“Niliambiwa kuwa kilichokufanya umuachie Alice ni tamaa za kimapenzi. Unajua toka mwanzo nilihisi hii kesi ina maslahi na watu, ndicho kitu ambacho kilifanya nifuatilie hii kesi tofauti na nyingine. Lakini hatua ya leo iliyofanywa na SSP Idrisa ni ya kushangaza kwa hiyo kuwa makini katika uchunguzi wako. Haya nipe ripoti.” Aliongea afande Maswe akionyesha kuwa anamaanisha anachosema.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta Ndilana akamuelezea Afande Maswe ripoti kuhusu taarifa za simu.
“Ushajua kuwa hiyo namba aliyokuwa anawasiliana nayo ni ya nani?”
“Hapana haikuwa imesajiliwa”
“Unafikiriaje?”
“Kwanza inabidi tufuatilie taarifa za hiyo namba, tukijua wengine ambayo wanawasiliana na hiyo namba tutamjua mwenyewe. Pili ninaomba askari mmoja afuatilie nyendo za Alice kujua kama kuna watu wanamfuatilia na mwisho ningependa wakili Hamis Mzee Pembe akamatwe na ashikiliwe kwa mahojiano.” Alijieleza Inspekta Ndilana
“Ruksa!”
Inspekta Ndilana akatoka ofisini kwa afande Maswe akijututumua utafikiri stelingi wa sinema ya kihindi kuelekea ofisini kwake. Alipofika ofisini kwake alifanya utaratibu wa kumuombea ruhusa Sarah, yule askari mwenziye wa kike aliyekuwa akimvizia Kinondoni siku ile aliyokutana na Hadija, kisha akampigia.
“Sarah!”
“Yes afande!”
“Umepewa taarifa na kiongozi wako”
“Ndiyo afande”
“Nakupa nusu saa uwe kivukoni, tumia usafiri wowote”
Na kweli baada ya dakika takribani ishirini Sarah, aliyevalia kiraia alikuwa tayari ameshafika Kivukoni kuonana na Inspekta Ndilana. Ndilana baada ya kumuona tu moyo ukaanza kwenda kasi kiasi cha kujishtukia kuwa huenda unaonekana juu ya nguo alizovaa.
Ilibidi Inspekta Ndilana azuge kwa dakika kadhaa mapigo ya moyo yarudi katika hali ya kawaida ndipo akanzisha mazungumko ya kazi aliyomuitia. Akamuelekeza kila kitu kuhusiana na Alice na kumwambia kuwa hakuna yeyote anayejua zaidi ya yeye Inspekta Ndilana, Sarah na Afande Maswe na kumtaka ahakikishe kuwa hakuna dakika yeyote inayopotea bila Alice kuwa chini ya uangalizi wake na ahakikishe hajui kama anafuatiliwa.
Baada ya kutoka pale Inspekta Ndilana aliongozea moja kwenye kitengo chao kupata taarifa za namba ziliyokuwa zikiwasiliana na wakili Pembe na alipozipata akarudi ofisini japo muda wa ofisi ulikuwa umeisha. Akaanza kuzifanyia kazi na kupata watu wawili ambao alipocheki majina yao mmojawapo ni Shabani Kibope na Mwingine alijulikana kama Sekela Mwaijage. Lilibaki zoezi moja tu la kumtia nguvuni wakili Hamis Mzee Pembe.
Usiku huo huo kwa amri ya Afande Maswe ikaanza operesheni ya kuwakamata watu hao wawili kuanzia kwa Shabani Kibope ambaye haikuwa kazi sana kumkamata. Ngoma ikawa kumkamata Sekela…
Sekela ni binti wa afisa wa ngazi za juu serikalini kwa hiyo nyumba anayokaa kwanza ina ulinzi wa polisi halafu baba yake alikuwa na sauti kubwa sana kiasi kwamba ilibidi Afande Maswe atoe maelezo ya kina kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi na baada ya majadiliano makali ikabidi Sekela afanyiwe mahojiano usiku ule ule mbele ya wakili wa baba yake.
Kwenye simu yake hakuwa kaihifadhi namba iliyokuwa inawasiliana naye akadai kuwa ni mtu ambaye kwanza alimpigia na kudai kuwa alikosea namba na kuanzia hapo akawa akimpigia kumsalimia lakini hamjui na wala hajawahi kumuona na bahati mbaya hakukuwa na mawasiliano ya meseji hata mara moja.
Ikashindikana kupata chochote toka kwa Sekela japo kwa jinsi alivyoonekana Sekela ni kama anamjua huyo mtu na inaelekea wana uhusiano wa karibu ila kutokana na hali ilivyokuwa wakati wa mahojiano chini ya mwongozo wa wakili wake, kina Inspekta Ndilana wakachemka. Ikabaki kete moja tu, kwa Shabani Kibope.
Ilikuwa yapata saa kumi na moja alfajiri wakati Inspekta Ndilana alipokuwa akirudi nyumbani kwake alipopokea simu kutoka kwa Sarah…
“Niambie Sarah”
“Kuna tukio”
Inspekta Ndilana akaliegesha gari lake pembeni.
“Nini?”
“Kuna gari la polisi limekuja nyumbani kwa kina Alice, wamemchukua na hivi wanaondoka naye”
“Piga picha unitumie kwenye mtandao sasa hivi, pia nitumie namba za hiyo gari haraka”
“Vyote nishafanya afande, nakutumia sasa hivi afande”
“Ukishanitumia nenda kapumzike ila saa tisa kamili alasiri uwe umeripoti kwenye sehemu yako”
Baada ya kama dakika tano hivi picha zikawa zimefika kwenye simu ya Inspekta Ndilana. Ndilana akampigia simu afande Maswe kumueleza na baada ya kama robo saa ikatangazwa kwenye redio ya polisi kuwa gari lenye namba alizonitumia Sarah linatakiwa kufika kituo cha kati likiwa na mtuhumiwa wanayemshikilia.
Yalipita mawasiliano kadhaa kama dakika arobaini kisha ikatumwa taarifa kuwa limeshawasili kituo cha kati ambapo tayari afande Maswe alikuwa amekwishafika na Inspekta Ndilana ndiyo alikuwa anaingia.
Wale askari baada ya kuhojiwa wakasema kuwa wametumwa na mkuu wao wa kituo wakamkamate Alice baada ya kuripotiwa kuwa mtoto wa Alice, Catherine ameibwa na imeachwa karatasi iliyoandikwa ‘nimemchua mwanangu, msinifuatilie’. Kwa hiyo mtuhumiwa wa kwanza ni Alice.
“Ilikuwa muda gani wakati tukio linatokea?” aliuliza afande Maswe
“Saa saba za usiku” alijibu askari mwenye cheo cha sajenti ambaye ndiye alikuwa kiongozi wao
“Hiyo saa saba za usiku ndiyo muda ambao waliripoti tukio au lilitokea?”
“Lilitokea, waliripoti saa 9.05 usiku”
Afande Maswe akampigia simu mkuu wao…
“Kifupi kamtafuteni anayehusika, huyu hahusiki kwa sababu kila hatua yake anayokanyaga tunaijua na ndiyo maana mara tu baada ya kumkamata nikajua na nikawaambia mumlete hapa. Hawa nawaachia warudi huko na ntataka kujua kila hatua mtakayokuwa mnafikia kuhusu uchunguzi wenu.”
“Sawa afande”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya wale maaskari kuondoka, Afande Maswe akamuagiza Inspekta Ndilana akamtoe mahabusu Alice kisha ampeleke hadi kwake. Ahakikishe anakuwa katika mikono salama. Alipomtoa tu mahabusu, Alice alimvamia Inspekta Ndilana na kumkumbatia kwa nguvu akilia.
Inspekta Ndilana akawa anaangaza huku na huku kama watu wamemuona akimwambia
“Niko kazini Alice ngoja tutoke hapa tutaongea,kisha ntakupeleka hadi nyumbani”
Ilikuwa yapata saa nne kasoro dakika chache asubuhi wakati Inspekta Ndilana akitoka na Alice kwa kutumia gari lake ambapo kwa kutumia simu ya Inspekta Ndilana, Alice aliwapigia simu nyumbani kwao ili kuwatoa wasiwasi. Inspekta Ndilana aliendesha moja kwa moja hadi nyumbani kwake kinyume na maelekezo ya Afande Maswe.
Njia nzima walikuwa kimya kila mmoja akionekana mwenye mawazo mengi sana hadi wakati wanafika kwenye hoteli moja ambayo iko jirani na nyumbani kwa Inspekta Ndilana.
“Nakuchukulia chumba hapa upumzike kwa masaa matatu kisha ntakurudisha nyumbani. Unaweza kuwaita kina Salome ukawa nao kwa kuwa si hawakai mbali na hapa?” akimweleza Alice na kutekeleza alichoongea kabla ya yeye kwenda nyumbani kwake kwa mapumziko mafupi.
******
Baada ya kuachwa peke yake, Alice alibaki akiwaza kuhusu kutoweka kwa mtoto wake kutoka katika nyumba ya dada yake Adrian Zayumba. Aliwaza mengi sana na sababu za yeye kuhusishwa na utowekaji wa mtoto huyo. “Au wanatengeneza mazingira ya mimi kutompata tena mwanangu?” alijiuliza bila kupata majibu sahihi.
Ilikuwa yakaribia saa saba kamili wakati Inspekta Ndilana anarudi hotelini alipomuacha Alice ambapo alimkuta peke yake amejilaza kitandani akionekana mwenye mawazo mengi huku mlango umerudishiwa.
Kuna kitu ambacho Inspekta Ndilana hakuwa kakigundua tokea mwanzo lakini sasa alikuwa akikiona bayana. Ni kwamba Alice hakuwa amevaa sidiria na bado matiti yake yalikuwa yamekaa vyema kifuani pake, akajikuta muda mwingi macho hayataki kubanduka kifuani kwa Alice.
“Habari za mapumziko”
“Hivyo hivyo tu!”
“Nilidhani ungewaita rafiki zako wakupe kampani”
“Hapana. Nilihitaji kukaa mwenyewe kwa muda kutafakari hii hali inavyoendelea” alisema Alice akionekana kuchoshwa na misukosuko ya kila siku.
Ndilana alibaki akimwangalia Alice kwa huruma huku ukimya ukiwa umetawala kabla ya Alice kuuvunja ukimya huo.
“Kwanini umenileta huku badala ya nyumbani?”
“Kwa sababu za kiusalama Alice, nitakurudisha kwenu saa tisa” alijitetea huku macho yake yakiwa yameganda kifuani kwa Alice. Safari hii Alice mwenyewe akashtukia, akajiangalia kifuani kisha akamwangalia tena Ndilana. Ikabidi Inspekta Ndilana aone aibu akazuga kutoa kijitabu kidogo na kumuonyesha Alice.
“Unaijua hii namba?” Ndilana alimuuliza akimuonyesha namba iliyomfanya awakamate Sekela na Kibope
Alice aliiangalia kwa muda kisha akawa kama anayekumbuka jambo fulani.
“Hii namba siyo ngeni kwangu” alijibu kwa uhakika
Inspekta Ndilana akashtuka na kujiweka vizuri utafikiri kafumwa na mkwewe akiwa bila nguo.
“Unaweza kukumbuka vizuri kuwa ni ya nani?”
“Siyo rahisi kuikumbuka labda nikirudi nyumbani nikacheki katika simu yangu nione kama nnayo”
Inspekta Ndilana akajifikiria kwa muda akikodolewa macho na Alice kisha Alice akamtupia swali la kizushi.
“Ulijuaje kama nimekamatwa?”
“Nna mtandao mrefu sana” alijibu bila kujifikiria huku macho yake yakirudi kwenye matiti ya Alice.
“Unadhani haya matatizo yataisha kweli jamani?” aliuliza Alice akiuchukua mto kuukumbatia ili kuficha matiti yake, kitendo kilichomfanya Inspekta Ndilana atabasamu.
“Vipi?” aliuliza Alice
“Una matiti mazuri sana, sikuwahi kugundua kabla. Samahani kwa kuingiza mada nyingine katikati ya maongezi ila ndiyo ukweli” Inspekta Ndilana alijikaza kutoa yake ya moyoni na kumfanya Alice amwangalie kisha ainamie chini kwa aibu.
Inspekta Ndilana akarudisha maongezi ya kikazi ili kujaribu kumrudisha Alice katika hali yake ya kawaida kisha wakapata chakula cha mchana pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kigamboni anapoishi Alice.
“Kwanini unaonekana kunilinda sana?” Alice alimgonga Inspekta Ndilana swali ambalo hakuwa na jibu lake na hata yeye mwenyewe hakuwahi kujiuliza ni kwanini anamfanyia Alice mambo yaliyo tofauti na watuhumiwa wengine.
Inspekta Ndilana alikaa kimya kwa muda akitafuta jibu la haraka haraka lakini hakuweza kulipata ikabidi amgeukie Alice “kwani hupendi kulindwa?”
“Hapana, nauliza tu”
“Ni kawaida yangu kuwalinda ambao nahitaji taarifa muhimu toka kwao na ndiyo maana hata Hadija nilienda kumtoa alipokamatwa” Inspekta Ndilana alionekana kupata pointi ya kusimamia.
“Sawa, nashukuru sana kwa kuwa mmojawapo kati ya wanaolindwa na wewe, vinginevyo ningekuwa napigwa makofi nikihojiwa na wale askari walionikamata”
“Siku ile ilitokea bahati mbaya tu, siyo kawaida yetu polisi kupiga raia”
Alice alikaa kimya kidogo akionekana kutafakari jambo kisha akaguna kidogo.
“Vipi Alice”
“Hamna kitu nawaza tu namna mapenzi yanavyoweza kumuweka mtu katika matatizo yasiyokwisha”
“Usiyalaumu mapenzi, matatizo yanaweza kukukuta katika hali yeyote sio lazima iwe katika mapenzi” Inspekta Ndilana akajaribu kutetea mapenzi
“Kwangu mimi maisha ni mazuri nikiwa nje ya mapenzi, ningekuwa sijachelewa ningekuwa tu mtawa nijue moja. Mapenzi yamenitumbukia nyongo na sidhani kama nitakuja kupenda tena hapa duniani, labda nife halafu nizaliwe tena upya”
Maneno ya Alice yalikuwa kama msumari wa moto moyoni mwa Inspekta Ndilana, yalimfanya akae kimya kwa muda mrefu akiyatafakari kabla ya kushtuliwa na mlio wa simu yake. Akaiangalia kwa muda, ilikuwa ni namba ya Sarah.
***** ***** ***** *****

“Vipi Alice”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hamna kitu nawaza tu namna mapenzi yanavyoweza kumuweka mtu katika matatizo yasiyokwisha”
“Usiyalaumu mapenzi, matatizo yanaweza kukukuta katika hali yeyote sio lazima iwe katika mapenzi” Inspekta Ndilana akajaribu kutetea mapenzi
“Kwangu mimi maisha ni mazuri nikiwa nje ya mapenzi, ningekuwa sijachelewa ningekuwa tu mtawa nijue moja. Mapenzi yamenitumbukia nyongo na sidhani kama nitakuja kupenda tena hapa duniani, labda nife halafu nizaliwe tena upya”
Maneno ya Alice yalikuwa kama msumari wa moto moyoni mwa Inspekta Ndilana, yalimfanya akae kimya kwa muda mrefu akiyatafakari kabla ya kushtuliwa na mlio wa simu yake. Akaiangalia kwa muda, ilikuwa ni namba ya Sarah.
“Nimesharipoti afande” aliongea akitoa taarifa kwa Inspekta Ndilana kuwa ameshawasili kwenye maeneo ya kumlinda Sarah.
“Ok. Hunijui na hatujawahi kuonana” alijibu Ndilana kwa maneno ambayo Sarah aliyaelewa yalikuwa yanamaanisha nini.
Baada ya muda mchache, Inspekta Ndilana akawa maeneo ya kina Alice. Pamoja na kuwa Sarah aliona kila kitu na wakati Fulani walitazamana kabisa na Inspekta Ndilana lakini hawakusalimiana wala kuonyesha dalili yeyote kuwa wanafahamiana.
Alichokifanya Inspekta Ndilana ni kumteremsha tu Alice na kuondoka akiacha Alice akilakiwa na mama na ndugu zake. Alichofanya Inspekta Ndilana ni kurudi kituoni kwa lengo la kumhoji Shabani Kibope ambaye ndiye atakayewasaidia kumjua mwenye namba iliyokuwa ikiwasiliana na Wakili Hamis Mzee Pembe.
Jambo la kwanza alilokuta kituoni ni habari ya uhamisho wa ghafla aliopewa SSP Idrisa, yule afande aliyekuwa akiingilia uchunguzi wa kesi anayoichunguza . SSP Idrisa alikuwa amerudishwa makao makuu ili kupangiwa shughuli nyingine. Jambo hilo lilimshtua sana Inspekta Ndilana, aliona kuwa kuna kila dalili kuwa ile kesi anayoichunguza ni nzito kuliko anavyoifikiria.
Alituma aletewe Shabani Kibope akaletwa akionekana kuchoka sana kwa masaa yale machache aliyowekwa rumande. Inspekta Ndilana na Shabani Kibope wakabaki wanaangaliana kwa sekunde kadhaa huku Kibope akionyesha chuki ya wazi kwa Ndilana.
“Nimekuita kwa jambo moja tu, jibu utakalonipa ndilo litakalonifanya nikuachie uende zako au tuendelee kukushikilia” alianza Ndilana huku Kibope akiwa kimya amemkazia macho. Inspekta Ndilana akatoa karatasi la namba na kumuonyesha Kibope.
“Unaijua hii namba hii”
Kibope aliiangalia kwa muda kisha akatabasamu kivivu wakati Inspekta Ndilana akimwangalia kwa umakini.
“Hii namba ilinisumbua sana kipindi fulani, ilikuwa inanipigia, nikipokea inaniwekea muziki. Mara ya kwanza nilidhani ilikuwa ikijipiga bila mwenye nayo kujua nikawa na nakata halafu naipigia lakini ikawa inapokelewa na kuachwa hewani hadi nakata”
“Enhe ikawaje?”
“Nikaanza kuifuatilia kujua ni ya nani kwa kutumia huduma za pesa kwenye simu, nikawa kama nataka kumtumia salio ili nione litatokea jina gani lakini ilikuwa ikitokea namba tu bila jina kumaanisha kuwa hakuwa ameisajili kwenye huduma za pesa. Ila baadaye ikaacha kunisumbua”
Alipoona hana tena anachoweza kupata kutoka kwa Kibope, Inspekta Ndilana akautumia muda ule kujaribu kumuweka sawa Kibope kuwa alimuweka ndani kwa usalama wake kutokana na hali ilivyokuwa ikiendelea katika uchunguzi wake na kumfanya Kibope arudi katika hali ya kawaida, mwisho akamchomekea swali.
“Unamfahamu Sekela?”
“Sekela?” aliuliza Kibope na kufanya Inspekta Ndilana ampe maelezo kuhusiana na Sekela
“Ah yule! Kama umepiga afande umeumia, mtoto Malaya kishenzi yule. Anamtia aibu sana baba yake. Sijui kama kuna mwanamme maaarufu hapa bongo ambaye hajapiga pale!” alisema Kibope akionekana mwenye uhakika na anachokisema.
Inspekta Ndilana alibaki kaka kimya kwa muda akionekana kutafakari cha kufanya kwa haraka haraka bila kupata jibu kisha akamgeukia Kibope…
“Anapata wapi muda wa kufanya uchafu huo wakati kwao analindwa kiasi kile?”
“Yule akiwa chuo ndio watu wanamkamatia huko huko…” alielezea Kibope akitaja chuo anachosoma Sekela na mengineyo ambayo yalikuwa ni msaada mkubwa kwa Inspekta Ndilana.
Kitu ambacho toka awali Inspekta Ndilana alikigundua kwa Shabani Kibope ni kuwa, ukitaka kumfanya aongee kwa kujiachia, ongea naye kuhusu masuala ya wanawake na ndiyo udhaifu ambao alikuwa akiutumia katika mahojiano na Kibope.
Alipojiridhisha, alimuachia Kibope na kumpa taarifa kwa Afande Maswe pamoja na kumueleza nia yake kuwa anataka kumkamata Wakili Hamis Mzee Pembe. Baada ya majadiliano kuhusu masuala kadhaa, Afande Maswe akampa ruhusa Ndilana aendelee na alichokipanga.
Kwa maelezo aliyoyapata Ndilana ni kwamba wakili Mzee Pembe huwa anapatikana mahakama ya Kisutu kila siku asubuhi, akaona ni vyema autumie muda huo kuliko kuanza kutafuta nyumba anayoishi. Inspekta Ndilana akaamua kuitumia jioni ile kwa kustarehe, akawa anarudi nyumbani huku akiwaza ayatumiaje mapumziko yake.
Wakati akikatibia nyumbani kwake, akapigiwa simu ambayo ilimshtua kiasi cha kufanya gari lake analoliendesha liyumbe kidogo kabla ya kukaa sawa. Ilikuwa ni namba ile ambayo anaichunguza, Inspekta Ndilana akaipokea kwa tahadhari kubwa. Akakutana na muziki, wimbo wa Bao la Kete wa mwanamuziki AT.
Ndilana akawa anasikiliza kwa makini lakini hakuwa akisikia kitu kingine chochote zaidi ya wimbo huo. Baada ya muda hiyo simu ikakatwa, ukaja ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka…
‘haya na wewe jiweke mahabusu ujichunguze sasa’
Ingawa lengo la mtu huyo lilionekana kama ni kumchanganya Inspekta Ndilana lakini kitendo hicho kilichukuliwa kwa namna tofauti na Ndilana. Haraka haraka alifanya mawasiliano na Afande Maswe ambaye naye akafanya mawasiliano mawili matatu katika mamlaka husika na baada ya muda, ripoti ilikuja kuwa mpigaji wa simu hiyo alikuwa maeneo ya Mtoni Kijichi.
Ilikuwa ni hatua moja mbele katika uchunguzi wake, pia kutokana na ujumbe huo ilikuwa wazi kuwa hiyo namba inatumiwa na mtu ambaye anaifuatilia hiyo kesi na anajua kila hatua ya uchunguzi inayopigwa. Ila kikubwa katika yote, ni mtu ambaye anaifahamu namba yake ya simu ambayo ni watu wachache sana wanayo.
Inspekta Ndilana huwa anatumia laini mbili katika simu yake, moja anayo kila mtu hadi watu wa nje wanayo halafu kuna namba rasmi ambayo huitumia kwa shughuli za kiofisi tu na ndiyo hiyo iliyopigiwa na namba anayoichunguza. Hiyo ina maanisha kuwa aliyempigia ni mtu wa ndani ya polisi au ambaye ana mtandao ndani ya jeshi la polisi. Atakuwa nani, SSP Idrisa?
Saa sita za usiku, Ndilana alikuwa katikati ya sehemu ya kuchezea. Alikuwa anavurugika haswa na muziki uliokuwa unaporomoshwa na bendi ya Msondo Ngoma. Inspekta Ndilana ni mgonjwa sana wa muziki wa msondo ngoma, huwa anenda disko au kwenye mabendi mengine kuwafurahisha wanawake anaokuwa nao lakini akiamua mwenyewe kustarehe huwa anaitafuta bendi hiyo ilipo.
**** **** ****

Wakati kibao cha Ndoa ya Manyanyaso kikiendelea huku mwimbaji Edo Sanga akitiririka, Inspekta Ndilana alishtukia anashikwa bega kwa nyuma na alipogeuka alipigwa na butwaa kwa dakika sekunde kadhaa.
Kwa jinsi ambavyo Ndilana alikuwa amevaa ilikuwa ni vigumu sana kwa mtu ambaye anamjua kwa juu juu kumtambua, alivalia suruari yake ya jinsi na shati la drafti huku juu akiwa amevaa kapero iliyofunika sehemu kubwa ya uso wake..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikuwa ni Shabani Kibope aliyeonekana kalewa kiasi fulani, wakasalimiana kwa kupeana mikono kisha wakawa wanacheza pamoja, askari na aliyekuwa mtuhumiwa wake. Baada ya wimbo kuisha Ndilana aliongozana na Kibope sehemu aliyokuwa amekaa Kibope kwa muda.
Meza aliyokaa Kibope ilikuwa na jamaa mmoja na wanawake watatu weupe wenye maumbile makubwa sana yale ambayo msukuma yeyote akiyaona anaweza kutoa hata ng’ombe mia ili kuoa tu. Kibope akatoa utambulisho wa kijuu juu ila hakumtambulisha Ndilana kama ni askari nadhani alikuwa anakwepa Ndilana kurudishia kuwa naye alikuwa mtuhumiwa wake. Ikawa jinsia zimebalansi, watatu kwa watatu.
Kwa kadiri walivyokuwa wakiendelea kunywa na kuinuka mara kwa mara kucheza, wakajikuta wamekwisha gawana kuwa nani ni wa nani ila Ndilana hakuonekana kuufurahia mgao ule.
Ilipotimia mishale ya saa nane hivi Inspekta Ndilana akainuka kama anaenda chooni, akakunja kona na kutokomea zake kurudi nyumbani.
Ila katika muda aliotumia kukaa pale na kina Kibope aligundua jambo fulani, maana mwanzoni walikuwa wanachangamkiana kikawaida wakipiga stori za hapa na pale ila kuna wakati Ndilana alitoka kwenda chooni na aliporudi alikuta hali kama kuna kitu kilizungumzwa wakati yeye hayupo.
Japo Kibope na jamaa yake walionekana kujilazimisha kuendeleza uchangamfu, wale wanawake walikuwa wakitoa ujumbe fulani kwenye macho yao. Ilikuwa ni kama wanamwambia fanya fanya uondoke ili uturudishie uhuru wetu. Ila hakutilia maanani sana alijua ni kawaida kwa raia wengi kutofurahia kuwa karibu na maaskari.
Wakati anakaribia nyumbani kwake akapokea taarifa kuwa mtoto wa Alice amepatikana na watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano, lakini taarifa za awali zinasema kwamba wao walimuokota tu akiwa majira ya saa mbili za usiku akiwa kama amepotea. Na kwa mujibu wa mtoto mwenyewe ni kwamba aliletwa na gari akaacha maeneo aliyookotwa. Muda huo huo akamjulisha Alice kuhusu kupatikana kwa mtoto wake.
Kesho yake asubuhi, Inspekta Ndilana alifika kwenye maeneo ya mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kumvizia wakili Hamis Mzee Pembe. Alikaa takribani masaa matano bila dalili zozote za kumuona wakili huyo, ikabidi arudi ofisini kwake akapitie rekodi kuona kama anaweza kupapata anapoishi.
Hadi inafika saa tisa tayari Inspekta Ndilana alikuwa akitoka kuelekea maeneo anayoishi wakili Hamisi Mzee Pembe. Wakili huyo alikuwa akiishi maeneo ya Kimara Baruti.
Kufika maeneo hayo akaanza kufuatilia ramani aliyopewa hadi akakazibia kabisa na maelekezo yanavyodai kuwa ni nyumbani kwa wakili huyo. Cha kustaajabisha akakuta kundi la watu wakiwa wamekusanyika, na baada ya kuulizia akambiwa wakili huyo amejinyonga usiku wa kuamkia siku hiyo.
Ikabidi haraka haraka aanze kufuatilia habari hiyo akapewa taarifa kuwa wakili huyo hakuonekana kuwa na tatizo lolote siku kabla ya kujingonga na hakuacha ujumbe wowote. Baada ya kupata taarifa hizo ikabidi awahi hospitali ya Muhimbili ambako mwili ulipelekwa kwa ajili ya uchunguzi, akakuta madaktari ndiyo wamemaliza kuufanyia uchunguzi chini ya usimamizi wa polisi.
“Ni kweli kuna alama ya kamba nene aliyotumia kujinyongea, lakini kuna alama nyingine ya kitu chembamba kama waya ambao upo shingoni nan i kama ulitumika kwanza kabla ya kamba” alianza kuelezea daktari kiongozi wa uchunguzi
“Kwa hiyo kuna uwezekano kuwa alinyongwa kwanza na waya ndipo akatundikwa na kamba kwa sababu haiwezekani ajinyonge mwenyewe na waya kisha ajimalizie na kamba wakati amaeshafariki” alitoa maoni yake Inspekta Ndilana.
“Ndivyo inavyoelekea” alisisitiza mmojawapo wa maaskari mbele ya ndugu aliyoshiriki katika kuangalia uchunguzi wa mwili.
“Unasemaje?” askari mwingine alimuuliza ndugu wa marehemu wakili Hamisi Mzee Pembe
“Mi nadhani tuache tu kama yalivyo, tumzike ndugu yetu. Hata tukianzisha uchunguzi haitasaidia kitu zaidi ya kuendelea kuumiza tu mioyo yetu”
Wakati wote huo akili ya Inspekta Ndilana ilikuwa ikizunguka kama feni bovu isijue uamuzi wa kuchukua waka sehemu ya kuanzia. Akachukua nakala ya taarifa zote muhimu katika uchunguzi wa tukio hilo kisha akarudi ofisini kwake akajifungia kwa ufunguo kiasi cha kutojulikana kama kuna mtu ofisini humo au hamna na kuamua kujiegemeza kidogo apumzike kabla ya kujikuta akiuchapa usingizi mzito kutokana na uchovu.
Inspekta Ndilana alishtuka mida ya saa tatu usiku na kilichomshtua ni minong’ono ya watu ambao walikuwa kama wanabishana mlangoni mwa ofisi yake. Akaitoa mlio simu yake haraka haraka, akamtumia ujumbe mfupi Afande Maswe halafu akategesha sehemu ya kurekodia sauti kisha akaiweka sehemu ya kujificha kidogo.
Kwa haraka haraka akatumia meza ya ofisini kwake kupata ili kuichomoa balbu kisha akarudi kutulia nyuma ya mlango huku akiwa kaishikilia vyema bastola yake, wakati huo zilikuwa zikisikika juhudi za kuufungua mlango wa ofisi yake kwa funguo ambazo sio zake. Kwa jinsi walivyokuwa wakiongea ni kama vile walikuwa watatu.
Mara mlango ukafunguliwa na kusukumwa kwa nguvu kiasi cha kumgonga kwenye paji la uso Ndilana aliyekuwa nyuma ya mlango, akawa amezibwa na mlango.
“Niliwaambia hakuna haja ya kuvunja mlango, hizi funguo zinaingiliana” alisema mmojawapo akiwatambia wenzake huku.
“Tumekuaminia mtaalam” alisema mwingine huku wakiingia ndani
“We zunguka zunguka hapo nje uangalie usalama” alisema yule wa kwanza ambaye alikuwa anatambia kuufungua mlango kwa funguo zake huku akijaribu kuwasha taa ya mule ofisini.
“Poa, ila fanyeni fasta” alisema mmoja mwenye sauti ya kukwaruza kama ambaye koo lake limekubuhu kwa kupitisha vitu vikali.
“Dah! Taa haziwaki, sasa?”
“Mi nna simu ya tochi” alisema yule mwenye sauti ya kukwaruza huku akiwawashia tochi toka kwenye simu yake ya kichina.
“Tunakutaniaga kuwa simu yako sabufa lakini leo imetuokoa” alisema mwingine
“Acha ufala wewe fanya kazi iliyokuleta” alitoa fedhuli yule mwenye sauti ya kukwaruza.
Wakaanza kupekua mule kwenye droo za meza ya ofisini kwa Inspekta Ndilana huku wakisema maneno ya kashfa kuhusu Ndilana. Japo maneno hayo yalikuwa yakimchoma lakini ilibidi avumilie tu ili aone wanachotaka kukifanya. Wakawa wanatoa mafaili ya Ndilana na kuanza kupekua wakionekana kutafuta kitu.
“Tuyabebe tu yote, muda unaenda” alipendekeza yule aliyefungua mlango
“Hapana, tukichukua na makaratasi ya upelelezi wa kesi ya yule Malaya lazima Afande Maswe ataingilia kati, sijui naye kamgonga yule demu maana alivyoshupalia hii kesi utadhani kesi ya kubakwa binti yake”
“Mimi kale katoto ka afande lazima nikachape”
“Wewe unatafuta kesi, ukachape katoto ka kidato cha pili?”
“We unachezea watoto wa siku hizi eeh? Utashangaa unavyopelekwa pelekwa kama Taifa Star inacheza na Hispania. We si unakaona kanavyobinua kiuno kakitembea”
Wakacheka huku wakiendelea kupekua mafaili.
“Hizi hapa!!” alisema mmojawapo akizitoa karatasi za uchunguzi wa kifo cha Wakili Pembe kutoa kwenye faili la mojawapo la Inspekta Ndilana
“Ndilana boya kweli, kila kitu anataka kuweka pua yake utadhani hili jeshi ni la baba yake. Atakuja kuchukuliwa roho ndiyo ajue kuwa watu si watu”
“Turudishie fasta tuondoke zetu”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakaanza kurudishia mafaili haraka haraka kisha wakawa wanaangalia kama kila kitu kiko sawa, mara ukasikika mlio wa gari linaloingia kwa kasi. Wakati huo yule mwenye sauti ya kukwaruza akawa anasikika akikimbia huku akiwahamasisha watoke haraka kuna noma. Wakakurupuka kutaka kuondoka wakashtusha na mlango uliokuwa unajifunga.
“Tulieni hivyo hivyo mlivyo” alisema Ndilana akiwa ameishikilia bastola yake vyema.
Kabla hawajajua la kufanya, mlio mkubwa wa risasi ulisikika toka nje kisha yule mwenye sauti ya kukwaruza akasikika akipiga kelele kumuita mama yake kisha kukawa kimya ikisikika miguu ikitembea kwa tahadhari kuelekea ilipo ofisi ya Inspekta Ndilana.
“Mwenzenu keshatangulizwa ahera kwa risasi, na nyinyi mkifanya ujanja wowote mtamfuata. Kaleni chini!” aliwaamrisha wakati huo sauti za miguu zikiwa zimefika mlangoni.
“Inspekta Ndilana!” ilisikika sauti ikiita toka nje, ilikuwa ni auti ya Afande Maswe. Inspekta Ndilana alisangaa kwa kuwa alitegemea kuwa Afande Maswe angewatuma askari wadogo watangulie lakini yeye kaamua kuwa mbele.
“Kila kitu kiko sawa afande. Nimewadhibiti”
Mlango ukafunguliwa ikamulikwa tochi yenye mwanga mkali kisha akaingia Afande Maswe kwa tahadhari kubwa akiwa na bastola mkononi akifuatiwa na askari wawili wenye SMG. Inspekta Ndilana akarudishia balbu kisha akaichukua simu yake na kumwekea afande Maswe mazungumzo ya wale askari mbele yao.
Lengo la Inspekta Ndilana lilikuwa ni kumtia hasira Afande Maswe ili awe upande wake moja kwa moja kwa kuwa binti waliyekuwa wakimzungumzia ndiyo kipenzi cha afande na anamsomesha kwa gharama kubwa kwenye shule ya kimataifa.
Baada ya kumalizika kwa maongezi yao Afande Maswe alionekana kutetemeka kwa hasira akiwaangalia kama anayetamani kuwashambulia kwa meno.
“Hapa hapa mtasema kila kitu, mkificha neno lolote nawachapa risasi mwenyewe na naandika maelezo kuwa tulidhani majambazi kwa kuwa hakuna taarifa yeyote kuwa tungepokea ugeni wenu usiku huu” alisema Afande Maswe akionesha kuwa hatanii.
“Kabla sijawajua nyie ni kina nani, nataka mniambie ni nani kawatuma”
Wale jamaa wawili wakawa kimya wakitegeana kuongea, Afande aswe akamuonyeshea bastola mmojawapo, yule mwenye mafunguo..
“Anza wewe”
Jamaa akakaa kimya bila kujibu neno, Afande Maswe akampiga risasi ya mguu bila bastola yake kutoa mlio wowote. Wakati anaugulia akamgeukia mwingine…
“Enhe, wewe?”
“Afande Haruna” alijibu kwa kutetemeka. Afande Maswe akamuonyesha ishara Inspekta Ndilana arekodi maongezi, alipomaliza akamgeukia yule jamaa.
“Unaitwa nani?”
“Konstebo Rajabu Bewa, natokea FFU Ukonga.”
“Na wewe?”
“Koplo Malinda natokea huko huko” alijibu yule jamaa aliyechapwa risasi ya mguu huku akiugulia maumivu.
“Na yule mwenzenu marehemu?”
Swali hilo liliwafanya washtuke na kuanza kuona kuwa hakukuwa na chembe ya masihara pale
“Koplo Riwa kafa?” aliuliza kwa mshangao Konstebo Bewa akionekana kupagawa
“Yule naye ni wa huko huko?” aliuliza Afande Maswe
“Ndiyo” alijibu Bewa
“Mmetumwa na nani na mmekuja kufanya nini? Nijibu wewe hapo” akimuonyeshea kidole koplo Malinda aliyekuwa akilia kwa maumivu kama mtoto
“Tumetumwa na SSP Haruna Majaliwa, katuambia tuje kuchukua makaratasi ya taarifa za uchunguzi wa kifo cha wakili Hamisi Mzee Pembe toka kwenye ofisi ya Inspekta Ndilana. Naomba nipelekeni hospitali nitakufa mimi” alijibu koplo Malinda huku akilalamika.
“Mlijuaje ofisi ya Ndilana wakati hamfanyi kazi hapa na huyo mnayemtaja hafanyi kazi hapa?”
“Alituelekeza kila kitu, na hata hapa tulikuja naye akawa anaongea na askari wa zamu ili kutupa nafasi ya kuingia humu ndani na ilikuwa aje kututoa”
“Mnajua nini kuhusu hii kazi mliyotumwa?”
Wakakaa kimya kwa muda, Afande Maswe akamgeukia Ndilana kumuonyesha ishara kuwa asimamishe kurekodi, Ndilana akatekeleza. Afande Maswe akawageukia ghafla na kufyatua risasi iliyopiga chini katikati yao.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**** **** ****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment