Simulizi : Kivuli
Sehemu Ya Nne (4)
**** **** ****
WAKAKAA kimya kwa muda, Afande Maswe akamgeukia Ndilana kumuonyesha ishara kuwa asimamishe kurekodi, Ndilana akatekeleza. Afande Maswe akawageukia ghafla na kufyatua risasi iliyopiga chini katikati yao..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tutasema..” aliropoka Bewa
Afande Maswe akamwambia Ndilana aendelee kurekodi
“Enhe..”
“Sisi ndiyo tulimnyonga wakili Pembe”
“Kwanini?”
“Alikuwa na siri ya Afande, kwa hiyo afande akajua kuwa akikamatwa ataitoa”
“Siri gani?”
Konstebo Bewa akamgeukia Koplo Malinda kisha akakaa kimya. Kwa akili za Afande Maswe alijua moja kwa moja kuwa Koplo Malinda ndiye anayejua mambo mengi kuliko Bewa au Bewa naye anayajua lakini anaogopa kusema mbele ya koplo Malinda. Afande Maswe akamsimamisha Ndilana asiendelee kurekodi kisha akawageukia Malina na Bewa.
“Nitawaweka katika vyumba viwili tofauti, atakayeficha taarifa yeyote tutamrudisha humu ndani na kumuua. Kama ni wewe Malinda tutakuacha tu ufe taratibu na hilo jeraha lako na kama utaficha wewe Bewa tutakuchapa risasi ya kichwa kama mwenzenu”
Haraka haraka wakachukuliwa na kutenganishwa, mmoja akawa anahojiwa na Afande Maswe na Mwingine akawa anahojiwa na Inspekta Ndilana. Baada ya dakika takribani 40, wote wakawa wametoa taarifa zinazokaribiana. Konstebo Bewa akawekwa rumande na Koplo Malinda akapelekwa hospitali chini ya ulinzi mkali kisha kila kitu kikawekwa sawa kama hakujatokea jambo lolote.
********
Mapema siku hiyo Afande Haruna aliwasili kituoni pale majira ya saa mbili kwa madai kuwa alikuwa anapita akaona aingie kuwasalimia kisha akaanza kuwaongelesha maaskari wa zamu akiwaweka katika mazingira ambayo watu wake wangeingia bila kuonekana na baada ya kufanikisha mambo yake akaondoka.
Baada ya lile tukio, Afande Maswe akatoa taarifa kwa mkuu wa jeshi la polisi, akaagiza ulinzi uongezwe kisha akatoa maagizo kwa askari wa zamu kuwa akija yeyote ambaye hayuko kwenye zamu au ambaye hayuko kwenye kituo kile awekwe ndani, hata kama akiwa na cheo gani labda wapate maelekezo mengine tofauti toka kwake au kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Masaa mawili tu baada ya Afande Maswe na kikosi chake kutawanyika, SSP Haruna Majaliwa aliwasili akionekana amekunywa pombe kiasi. Alikuwa akijichekesa chekesha huku akisogea ilipo kaunta.
“…leo hadi mtanichoka, nilikuwa nakunywa mitaa hii. Vipi kazi?”
Askari wawili wakatoka kuja nyuma yake kisha mmoja akamsogelea…
“Samahani afande, uko chini ya ulinzi. Tutakushikilia hadi kesho atakapokuja afande Maswe”
“Haiwezekani. Kwanini mnanikosea adabu kiasi hicho”
“Tumeagizwa tu afande na sisi tunatekeleza maagizo”
“Maswe ndiyo kawaagiza?”
“Ni maagizo toka kwa IGP”
“Ngoja nimpigie simu sasa hivi”
“Hapana afande, nadhani ungefanya tunavyosema ili tusikuvunjie heshima”
Afande Haruna akataka kufanya vurugu ili aondoke lakini walimdhibiti vilivyo na kumuweka rumande wakimuacha akitukana na kutoa vitisho mbalimbali.
Kutokana na pilika pilika za kumdhibiti Afande Haruna, hawakukumbuka kuizima simu yake, ghafla ikawa inaita mfululizo wakaitoa walipoiweka na kuizima. Baada ya dakika chache toka waizime hiyo simu akatokea dada mmoja mrembo akawa anatembea kuelekea ilipo kaunta.
“Karibu dada”
“Ahsante”
“Tukusaidie nini?”
“Samahani, namuulizia Mzee Haruna”
“Tumwambie nani anayemhitaji?”
Yule dada akakaa kimya kwa muda akijifikiria kisha akafunguka
“Nilikuwa naye kwenye gari lake akaniambia anaingia mara moja, naona hatoki na simu hake kwanza ilikuwa haipokelewi ila kwa sasa imezimwa kabisa”
“We unaitwa nani dada?”
“Daah yani maelezo yote hayo bado mnataka hadi jina? Niambieni tu kama naweza kumuona au kama sivyo niondoke zangu” alisema yule dada kwa ukali
“Tunasikitika kukwambia kuwa hakuna lolote kati ya hayo ambalo linawezekana”
“How?” aliuliza yule dada kwa kiingereza akitaka ufafanuzi
“Huwezi kumuona na wewe huwezi kuondoka, tutakushikilia hadi asubuhi”
“What?”
Wakati huo tayari alishazungukwa na kuwekwa chini ya ulinzi akibwabwaja kuwa watamkoma endapo baba yake atapata taarifa.
“Waulizeni wenzenu hapa hapa watawaambia Sekela ni nani?
Sekela ni yule mtoto wa kigogo ambaye alikamatwa pamoja na Kibope kuhusiana na namba ambayo pia ilikuwa ikiwasiliana na Wakili Hamis Mzee Pembe na ndiyo ile iliyompigia Inspekta Ndilana na kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi kuwa jichunguze na wewe.
Baada ya hapo hali iliendelea kuwa shwari hadi kunakucha.
********************
Alfajiri, Inspekta Ndilana alidamkia Kigamboni kwa Alice kwa kutumia gari nyingine, na alipofika akampigia simu Alice aje lilipo lile gari.
Mara baada ya Alice kutoka, Inspekta Ndilana akapokea simu toka kwa Sarah
“Afande, Alice anaelekea kwenye gari jeusi lenye vioo vya giza”
“Lipige picha kisha nitumie na namba za hilo gari”
“Niekusoma afande”
Wakati Alice anaingia kwenye gari la Inspekta Ndilana, na huku picha zikawa zinaingia kwenye simu yake.
“Habari za leo Jackson” Alice alimsalimia Ndilana kwa kumuita jina lake la kwanza, hali iliyomfanya Ndilana atabasamu.
“Nzuri Alice, nilitaka nikuone sura yako inakuwaje alfajiri” alimwambia akimtazama usoni na kumfanya Alice aangalie chini kwa aibu
“Nimekurupuka tu hata uso sijanawa, nikajua labda kuna tatizo”
“Hapana hakuna tatizo mpe.. ah Alice” alijikuta akitaka kumuita Alice mpenzi kabla hajajishtukia na kubadilisha kauli huku Alice akimkazia macho.
“Uliniambia kuwa ile namba niliyokuonyesha siyo ngeni machoni mwako, umeingalia kwenye simu yako?” aliuliza Inspekta Ndilana akirudisha maongezi ya kikazi.
“Hebu niione tena”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndilana alitoa karatasi lenye ile namba ya simu na kumkabidhi Alice ambaye akaichukua na kujaribu kuipika kwenye simu yake. Likatokea jina ‘SIMJUI’
“Nimeshaikumbuka hii namba”
“Enhe”
“Wakati niko Kilwa ilikuwa ikinipigia kunitongoza kila siku usiku lakini hakuwa anataka kujitambulisha, alikuwa akiniambia kuwa tukionana nitamjua”
“Enhe”
“Mimi nikawa namkatalia tu lakini vitu alivyokuwa akiongea ni kama vile ananijua”
“Vitu gani”
“Ah vitu tu”
“Hutaki kuniambia” Inspekta Ndilana akauweka uso wa kiaskari akimtazama Alice ambaye alikuwa akiongea kama anaongea na mpenzi wake. Sura ya Inspekta Ndilana ikamshtua Alice akawa akimwangalia kwa mashaka.
“Alikuwa ananiambia mara kiuno chako nakipenda, mara matiti yako mazuri mara asifie macho yangu.. ndiyo mambo ya hivyo hivyo…” alisema Alice kwa aibu
“Ila ni kweli Alice…” alijikuta akiropoka huku akiuangushia mkono wake pajani kwa Alice. Alice akatulia kwa muda bila kuutoa mkono wa Ndilana, akainua uso kumtazama Ndilana wakajikuta wakitazamana kwa sekunde kadhaa.
Alice akautoa mkono wa Ndilana kwa haraka haraka kisha akashusha pumzi ndefu akijiinamia chini.
“Mi narudi ndani” alivunja ukimya Alice
“Una habari kama Wakili Pembe kajinyonga?” aliuliza Ndilana na kumfanya Alice ashtuke sana
“Lini? Imekuwaje?” aliuliza
“Hakuna anayejua chochote hadi hivi sasa ila nadhani unakaribia kuupata uhuru wako wa zamani moja kwa moja.
“Kwa ajili ya kifo cha wakili Pembe?” aliuliza Alice
“Hapana, nadhani tunakaribia kuhitimisha hili suala”
“Nitafurahi sana Jackson, sijui hata nitakupa zawadi gani?” alisema Alice akionekana mwenye furaha
“Au kama ili uliyotaka kumpa muuaji wa Adrian Zayumba?” aliuliza Inspekta Ndilana kwa mzaha kwa kuwa katika mahojiano ya kwanza Alice alidai kuwa kwa jinsi alivyofurahishwa na kuuawa kwa Zayumba, angemjua muuaji angeweza kumpa hata penzi usiku kucha.
Alice alicheka kwa aibu…
“Husahau tu?”
“Siwezi kusahau hilo neno kwa kuwa lilinishangaza sana”
“Ukaniona Malaya eeh?’
“Hapana, sijawahi kukufikiria hivyo hata siku moja Alice. Kwangu mimi, wewe ni msichana ambaye una sifa zote za kuwa mke wa mtu” alijieleza Ndilana
“Hujamalizia”
“Nini”
“Wenzio wakisemaga hivyo wanamalizia kuwa tatizo mi nishaoa, ningekuwa bado ningekuoa wewe” alisema Alice na kusababisha wote wacheke kwa pamoja.
“Mimi sijaoa ndiyo maana sijamalizia hivyo”
“Mnh”
“Unaguna nini?”
“Ungekuwa hujaoa ungenipeleka hoteli badala ya kwako kwa jinsi ambavyo nawajua wanaume nyinyi?”
“Niliona tu kuwa usingenielewa, ungedhani natumia matatizo yako kufanikisha shida yangu”
“Kwa hiyo unasubiri yaishe?” alihoji kama ambaye anakerwa na kitendo cha Inspekta Ndilana kushindwa kuomba penzi na kubaki anausifia ‘mzigo’ kila siku.
“Sikiliza Alice” alianza kuongea Ndilana huku akiuweka mkono wake pajani kwa Alice ambaye alitulia tu bila kuutoa
“Leo nikiri mbele yako kuwa nakupenda sana. Toka mara ya kwanza kukuona ulinivutia lakini mazingira hayakuruhusu na kadiri siku zilivyokuwa zikienda nilijikuta nikizidi kukupenda. Ila sikupenda ionekane kuwa natumia matatizo yako kujinufaisha. Kwanza ingeleta mgongano wa kimaslahi katika kazi pili hata wewe usingeamini kama mapenzi yangu yanatoka moyoni, san asana ungedhani nataka rushwa ya ngono”
“Ndio nlivyokwambia nafikiria hivyo?” aliuliza Alice akiwa haeleweki eleweki
Alichokifanya Ndilana ni kuzidi kuutembeza mkono wake mapajani mwa Alice wakajikuta wamekumbatiana na kumiminiana mabusu mwisho wakajikuta wakilaza siti na kufanya mapenzi mule mule ndani ya gari.
Wakati wakiendelea simu ya Ndilana ilikuwa ikiita lakini alikuwa akiikata hadi alipomaliza raundi ya kwanza ya pambano lisilo la ubingwa akaiangalia namba iliyokuwa inapiga simu, ilikuwa ya Sarah. Akaipiga.
“Afande, gari lilikuwa linatikisika. Nijitokeza kuangalia kinachoendelea?”
“Hapana hilo ni la mpenzi wake, mwache tu” alijibu Ndilana akihema. Kisha akaitupia simu pembeni na kuanzisha tena mashambulizi.
Baada ya muda fulani, Alice akawa anatoka katika gari la Inspekta Ndilana huku akijiweka vizuri kurudi ilipo nyumba yao. Kutokana na picha alizotumia na Sarah, Ndilana alijua Sarah amekaa upande gani, akatupa macho kumwangalia akamuona ameweka simu sikioni.
Inspekta Ndilana akainyanyua simu yake kutaka kuipiga simu ya Sarah ili amshtue kwa kuwa alionekana kama ameduwaa na simu yake sikioni. Kuiangalia simu akaikuta kuwa bado iko hewani, kumbe baada ya kuongea na Sarah hakuikata ile simu, ina maana kuwa kashkash zote za malavidavi mule ndani ya gari zilikuwa zinamfikia Sarah laivu bila chenga.
Kijasho chembamba kikaanza kumtoka Inspekta Ndilana alichokifanya ni kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi kuwa ‘unaweza kwenda kupumzika kwa masaa manne’. Sarah alionekana akiusoma ujumbe mfupi wa maandishi halafu akaonekana kujibu huku akitupia macho gari la Inspekta Ndilana likiwa linageuzwa kutaka kuondoka.
Ujumbe mfupi uliingia katika simu ya Inspekta Ndilana, ‘naomba lifti afande’. Ilibid Inspekta Ndilana asimamishe gari na kumpigia Sarah ilia je kupanda kwenye gari. Siri ikawa nje. Sarah alikuja kwa unyonge na kuingia kwenye gari, pamoja na kuonekana kuwa na uchovu mwingi lakini alionekana dhahiri kuwa kitendo kilichotokea kilimzidishia unyonge.
Ikaanza safari kimya kimya kuelekea maeneo ya Kinondoni anayoishi Sarah, wakati wanavuka feri, Sarah alipitiwa na usingizi kutokana na uchovu. Ndilana hakumuamsha na ilionekana kama vile Ndilana anakujua sana anapoishi Sarah kwa kuwa hakuelekezwa hata mara moja. Na hata Sarah mwenyewe hakuwahi kuwaza kama kwamba Ndilana anakujua anapoishi.
Walipofika nyumbani kwa Sarah, Inspekta Ndilana akamuamsha Sarah, Sarah akashtuka na kujikuta amefika nyumbani kwake. Akabaki akishangaa kwa sekunde kadhaa kisha…
“Umefikaje bila maelekezo yangu” aliuliza na kumfanya Inspekta Ndilana atabasamu.
“Napafahamu unapoishi”
“Kakuelekeza nani?”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nisingeacha kupafahamu kwa muda niliokuwa nikiutumia kukufuatilia kipindi kile”
“Kwa hiyo ndiyo maana ukanipa kazi ya kumlinda demu wako kwa vile nilikukataa?”
Sarah aliongea akionekana ana donge moyoni, na Ndilana akaligundua hilo akakaa kimya kwa muda, Sarah akashtuka toka kwenye gari, akaubamiza mlango na kuelekea mlango wa kwake.
“Sarah”
“Sema” alijibu akisimama bila kumwangalia Inspekta Ndilana.
“Rudi kwanza ndani ya gari?”
“Sitaki”
“Kumbuka mimi ni kiongozi wako, na hii ni amri halali”
“Sawa afande” alijibu Sarah akirudi kwenye gari na kuingia ndani
“Sarah, kabla ya leo sikuwa na mahusiano na Alice ila kwa kuwa yeye yuko mpweke na mimi niko mpweke na matatizo yanaelekea kuisha tukajikuta ghafla tunadondokea katika mapenzi. Nisamehe kama nimekukwaza”
“Unikwaze? Kwani mimi yananihusu nini?”
“Najua hayakuhusu lakini unapaswa kujua kwa kuwa wewe ndiyo umeshuhudia kilichotokea, unastahili ufafanuzi”
“Mnh! Kweli hii kazi haina adabu, yaani mtu unaacha usingizi wako unamlinda mtu akisex na Malaya wake” aliongea Sarah kwa hasira
“Teremka kwenye gari langu, unatakiwa kuripoti pale saa sita kamili” aliagiza Inspekta Ndilana kwa sauti ya mamlaka.
Sarah aliteremka na kuelekea nyumbani kwake bila kusema neno wa kufunga mlango wa gari alipotokea. Ndilana alimwangalia kwa muda kisha akaremka kuufunga mlango wake wa gari, akaondoka kuelekea kituoni akitafakari alivyomfaidi Alice na wakati huo huo vitendo alivyoonyesha Sarah.
Kufika kituoni, kabla ya chochote akaitwa ofisini kwa Afande Maswe. Akapewa taarifa zote kuhusiana na kukamatwa kwa SSP Haruna na Sekela. Pia akaelezwa namna baba yake Sekela alivyong’ongonyea baada ya kupewa taarifa kuhusu mazingira aliyokamatiwa binti yake na mwisho akampa pongezi toka kwa IGP kwa kuwa walimtoa lawamani, kulikuwa na lawama sana aliposhikiliwa Sekela mara ya kwanza kwa madai kuwa polisi inamtafutia kashfa kigogo huyo.
Baada ya taarifa hizo Afande Maswe akabaki anamkodolea macho Inspekta Ndilana
“Inspekta Jackson Ndilana”
“Naam afande”
“Sarah kapiga simu”
Moyo wa Inspekta Ndilana ukaanza kwenda mbio, akili ikaanza kuwaza kwa kasi akipanga na kupangua cha kujitetea.
“Anasemaje afande” aliongea kwa mashaka
“Anasema hawezi kuripoti ulipompangia kwa sababu amepatwa na malaria kali sana? Mna tatizo lolote?”
“Hapana afande, kwanini?”
“Haonekana kama anaumwa, kwa kuwa alikuwa anaongea kama aliyejawa na hasira na anasema anaumwa malaria kali wakati hata hospitali anadai hajaenda. Kifupi alikuwa anachanganya tu mambo ila nimempa ruhusa kwa kuwa najua binadamu huwezi kuwa sawa siku zote”
“Mimi sina tatizo naye afande, nadhani kuna jambo kalikuta nyumbani kwake ambalo halikumfurahisha”
Afande Maswe akamwangalia kwa muda kisha akabadilisha maongezi na kumpa ahueni Ndilana
“Sekela tumeshamuachia kwa dhamana kwa kuwa anaweza kuhitajika wakati wowote ila SSP Haruna Majaliwa ataenda kuhojiwa kwenye chuo cha maafisa wa polisi Kurasini, unajua mtu kama yeye hawezi kuhojiwa hapa.”
Baada ya taarifa hizo Afande Maswe alimuagiza Inspekta Ndilana akajiandae kwa ajili ya mahojiano na SSP Haruna akimsisitiza kuwa kwanza ni mkubwa kwake kwa cheo, pili ana uzoefu mkubwa sana na masuala ya kipolisi kuliko yeye hivyo Ndilana anatakiwa kujipanga haswa japo kutakuwa na maofisa wengine.
Inspekta Ndilana akarudi kaunta kuchukua vitu ambavyo alikutwa navyo SSP Haruna pamoja na mahojiano ya awali aliyoyafanya Afande Maswe na Sekela kisha akarudi ofisini kwake akajifungia huku akijikuta ananukia ki-Alice Alice kwa kuwa hajaoga toka abinjuane na Alice.
Ili kuiweka akili yake sawa ikabidi ampigie kwanza Alice kumwambia kuwa atahitaji kuwa naye jioni ya siku hiyo na kupiga stori mbili tatu na kutaniana akakata simu na kuanza kuweka msisitizo katika kazi anayoifanya, akaanza kupekuwa kielelezo kimoja baada ya kingine na maelezo ya wote waliohojiwa huku akijenga hoja.
Baada ya saa moja kasoro akaitwa ili waelekee Kurasini kwa ajili ya kumhoji SSP Haruna Majaliwa ambaye kwa wakati huo alikuwa ameshapelekwa huko chini ya ulinzi mkali. Wakati anatoka akapokea ujumbe toka kwa Alice ‘kazi njema afande wa mwili wangu’. Akaujibu kisha akatoka akicheka.
Chumba cha mahojiano kilikuwa kina maofisa sita wa ngazi za juu waliokuwa tayari kusikiliza huku Inspekta Ndilana na SSP Majaliwa wakiwa wanatazamana wakitenganishwa na meza. SSP Majaliwa alikuwa akimwangalia Inspekta Ndilana kama chui anavyomwangalia swala kwa matamanio ya kumrarua.
“We umeoa?” alianza kuuliza swali SSP Majaliwa kana kwamba yeye ndiye yuko pale kumhoji Inspekta Ndilana.
“Hapana”
SSP Majaliwa akaigeukia timu ya maafisa akitabasamu
“Kwanini mnanipa mvulana anihoji?”
“Majaliwa, tumekupa heshima ya kuhojiwa katika mazingira haya kutokana na utumishi wako wa muda mrefu katika jeshi la polisi na pia kwa kukuheshimu kama mwajiriwa wa jeshi kwa kuwa bado hujafutwa kazi. Ukiifanya kazi ya kijana kuwa ngumu tutamuomba IGP akuondole kinga zote na utahojiwa kama raia” alizungumza Kamishna Zebadayo ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa ile timu.
Inspekta Ndilana akajua akilegea kidogo tu atadhalilishwa mbele za mabosi wake na kuonekana anapwaya, japo moyo ulikuwa ukimdunda kutokana na timu iliyokuwepo katika mahojiano yale lakini ilibidi ajikaze ‘kisabuni’.
“Una swali jingine kabla sijaanza kukuhoji?” aliuliza Inspekta Ndilana ili kujirudishia hali ya kujiamini.
Swali hiyo lilimfanya Majaliwa arudishe umakini kwa Inspekta Ndilana.
“Naam?”
“Nakuuliza una swali jingine lolote kabla sijaanza kukuuliza mimi? Maana nikianza kukuhoji sitakuruhusu uniulize swali jingine lolote…”
Maelezo ya Ndilana yaliwafanya maafisa waangaliane kisha wakaonyeshana ishara ya kumkubali Ndilana hali iliyomtoa Majaliwa kujiamini kwake.
“Sina swali jingine?”
“Ulikuwa unatoka wapi na Sekela?” alianza kwa swali ambalo hakuna ofisa yeyote aliyelitegemea na hata SSP Majaliwa mwenyewe hakuwaza kama angeulizwa swali lile.
“Matembezi”
“Wapi?”
“klabu ya Pentagon”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ya Kijichi, siyo?”
“Ndiyo”
“Unaenda kujificha Kijichi kwa kujua wazi kuwa unachokifanya siyo sahihi, sivyo”
“Kivipi?”
“Nataka majibu, muda wako wa maswali umeshaupoteza”
“Hakuna tatizo la mimi kuwa Kijichi, ni uamuzi tu”
“Sawa. Unajua kama Sekela ni mwanafunzi na baba yake, ambaye ni mheshimiwa anatumia gharama kubwa kumsomesha?”
“Mwanafunzi wa chuo ni mtu mzima, ana maamuzi yake”
“Kwanini unatumia namba isiyosajiliwa kuwasiliana naye?” SSP Majaliwa akakaa kimya kwa muda kwa sababu namba anayoisema Ndilana ndiyo iliyokuwa pia ikiwasiliana na Wakili Pembe, Alice, Kibope na hata Ndilana mwenyewe.
Na kitendo cha SSP Majaliwa kukiri kuwa alikuwa Kijichi kinathibitisha kuwa ndiye anayeimiliki ile namba isiyosajiliwa kwa kuwa kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka husika, wakati Ndilana anapigiwa na namba hiyo, mhusika alikuwa maeneo ya Kijichi. SSP Majaliwa alikuwa amekwishajiweka kwenye kona.
“Maswali gani hayo… mimi siwezi kujibu”
“Jichagulie maswali matatu unayoyaona mazuri, ujiulize mwenyewe kisha ujijibu, sisi tutakuwa tunakusikiliza.” Inspekta Ndilana alimwambia SSP Majaliwa kwa utulivu kiasi cha kumfanya afure kwa hasira.
Majaliwa alikurupuka na kutaka kumvaa Inspekta Ndilana na kuwapa kazi maafisa kuwatendanisha kwa dakika kadhaa kabla ya kufanikiwa kumtuliza Majaliwa.
“Sipendi kabisa dharau mimi” aliongea Majaliwa huku akitweta kwa hasira.
“Inspekta Ndilana, unaonaje tuahirishe mahojiano?” aliuliza Kamishna Zebadayo
“Hapana afande, nadhani tunaweza tu kuendelea, afande Majaliwa alighafilika kidogo” aliongea Ndilana kwa utulivu mkubwa kisha akamgeukia Majaliwa.
“Tunaweza kuendelea?”
“Uliza” alisema kwa hasira
“Huoni kama Sekela anakulia tu hela zako kwa kuwa umezeeka na huwezi hata kumridhisha?”
“Kamlate mama ‘ako halafu atakuhadithia muziki wangu”
“Hakuna haya ya mama yangu, Sekela keshaniambia kuwa huna lolote ila anakulia tu hela zako na anasubiri ustaafu akusaidie kutumia mafao. We unasemaje?”
“Ningekuwa nikimpigia simu hata usiku anatoroka chuoni anakuja?”
“Huwa unampigia kwa namba gani?”
SSP Majaliwa alikaa kimya kwa muda kisha akatikisa kichwa akicheka kwa huzuni.
“Mwanakharamu, una akili sana wewe!” alimwambia Inspekta Ndilana huku maafisa wengine wakishangaa. Inspekta Ndilana akawageukia maafisa
“Mimi kwa leo nimeridhika, nitamhoji tena kesho au siku nyingine” alisema Ndilana akimkodolea macho Kamishna Zebadayo ambaye aliita askar waliokuwa nje wamchukue SSP Majaliwa na kumrudisha mahabusu kisha wakabaki na Inspekta Ndilana.
“Inspekta Ndilana” alianza Kamishna Zebadayo
“Naam”
“Kwanini hujauliza chochote kuhusu tukio la jana wala kuhusu matukio yaliyopo?”
“Asingeweza kutoa majibu ambayo yangesaidia katika upelelezi kwa kuwa alikwishajiandaa kupotosha ukweli” alijitetea Ndilana
“Ulichomuuliza kimesaidia nini?” aliuliza Kamishna Zebedayo na kumfanya Ndilana atiririke
“Ushahidi wenye nguvu zaidi katika matukio yote ni namba ya simu ambayo ilikuwa iliwasiliana na Wakili Pembe muda mfupi kabla ya kifo cha Adrian Zayumba na baada ya kifo hicho. Ni namba hiyo iliyokuwa ikiwasiliana na watu mbalimbali ikionyesha kufuatilia sana mwenendo wa kesi ya mauaji hayo. Na hata mimi ishawahi kunipigia.
Kwa maswali niliyomuuliza amethibitisha wazi kuwa yeye ndiye mhusika wa hiyo namba na wakati anapekuliwa kabla ya kuwekwa mahabusu amekutwa na hiyo laini ya simu” alijieleza Inspekta Ndilana na kuwafanya maafisa wajikute wanampigia makofi.
“Una akili sana bwana mdogo”
Baada ya dakika kadhaa kikao kilifungwa na watu kutawanyika, ambapo Inspekta Ndilana aliwahi kujiandaa kwa ajili ya miadi yake ya kukutana na Alice jioni yake.
******************************
Upande wa Sarah alikuwa na wakati mgumu sana akijimiminia mvinyo huku mara kadhaa akiongea peke yake. Hasira yake kubwa ilikuwa ni kwa nini ametumika kumlinda mpenzi wa mtu lakini moyoni hata mwenyewe alikuwa akijishangaa kuhusu hasira hizo.
“Katika wanaume na Jackson naye utamuweka?” alikuwa akijiuliza kwa kumkebehi Ndilana lakini bado moyo ulikuwa ukimuuma.
Mara mlango ukagongwa ghafla, Sarah akatoka kwenda kuchungulia akaliona gari la Inspekta Ndilana. Akatoka ‘msonyo’ mrefu kisha akajitupa kwenye kochi. Mlango unaendelea kugongwa mara kadhaa, akainuka kivivu na kwenda kuufungua.
“Unataka nini” lilimtoka swali la kikatili mno na kumfanya Inspekta Ndilana ambaye alikuwa tayari amejiandaa kwa ajili ya miadi yake na Alice kupatwa na mshangao
“Tuna ugomvi Sarah?” aliuliza swali ambalo lilimfanya Sarah ajishtukie na kutabasamu kinafiki
“Hamna, unajua nimekurupuka usingizini. Samahani”
“Usijali. Unaendeleaje na malaria?” aliuliza Ndilana kwa kuutaja ugonjwa kama dhihaka kwa kuwa aliomba ruhusa kuwa anaumwa malaria kabla hata hajaenda hospitali.
Sarah alikaa kimya kwa muda akimwangalia Ndilana kisha akajikohoza kusafisha koo kidogo.
“Siumwi afande, ila sijisikii vyema tu. Nadhani ni kwa ajili ya uchovu wa kazi. Karibu ndani” alisema Sarah akimkaribisha Ndilana wakati bado kasimama mlangoni kama ambaye hataki Ndilana aingie.
Ndilana akatabasamu akimwangalia Sarah, Sarah akampisha lakini Ndilana hakuingia.
“Napita tu Sarah, kuna safari naenda nikaona nipitie kukujulia hali”
“Kwa Alice?”
“Hapana”
“Nilijua umekolea unarudi tena kuendeleza”
“Siendi huko ila ninapoenda nitakutana naye. Samahani kama nilifanya unielewe vibaya. Halikuwa lengo langu kukuharibia ‘mudi’ yako”
“Wala, mimi niko poa tu”
“Ok” alisema Inspekta Ndilana akimwangalia Sarah aliyejifunga tu kanga mbili. Japo alikuwa katika hali ya kutamanisha kimapenzi lakini ajabu ni kuwa Inspekta Ndilana alimuona wa kawaida sana kiasi kwamba hata mwenyewe alijishangaa.
“Haya safari njema” alisema Sarah akionekana wazi kuwa haupendi uwepo wa Ndilana pale mlangoni
“Oh.. haya, samahani kwa kukupotezea muda, najua labda umemuacha mwenzio chumbani” aliongea Ndilana kwa utani huku akigeuza kurudi lilipo gari lake.
“Ndiyo, kuna bwana ‘angu chumbani” aliongea Sarah akionekana fika kuwa na donge kutokana na sauti yake ya kitetemeshi aliyotamkia maneno hayo.
Inspekta Ndilana hakuonekana kujali wala kujibu lolote, akaingia kwenye gari yake wakati Sarah akiubamiza mlango wake.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta Ndilana alisimamisha gari lake ghafla, akateremka na kuelekea tena kwenye mlango wa nyumba ya Sarah. Sarah alitoka ghafla pale dirishani kwa kukimbia, kwa ile haraka na ulevi ulioanza kumuingia kutokana na mvinyo aliokunywa akajikwaa kwenye stuli ndogo na kuanguka chini vibaya akifikia mkono kisha kupigiza kichwa.
Inspekta Ndilana alisikia kishindo kikubwa kama cha mtu aliyedondoka kikiambatana na ukulele kisha akawa kimya kikatawala, akausukuma mlango, na kuingia ndani akamkuta Sarah amelala akiwa amepoteza fahamu.
Kwa hali aliyoikuta Inspekta Ndilana hakuwa tena na muda wa kujiuliza maswali. Alimnyanyua na kumuweka kwenye kochi wakati huo khanga yake zake zilikuwa zimefunguka na mwili wote ulikuwa wazi ukisitiriwa na nguo ya ngani tu.
Inspekta Ndilana alijaribu kuita mule ndani lakini hakukuonekana kama kuna mtu mwingine, akaingia kwenye vyumba akakipata chumba cha kulala cha Sarah akachukua gauni kubwa lililo karibu akarudi nalo sebuleni na kumvalisha kisha akamnyanyua kumpeleka kwenye gari kisha akarudi kuufunga mlango wa Sarah kwa kutumia funguo zilizokuwa zinaning’inia mlangoni.
Inspekta Ndilana akamkimbiza Sarah hospitali ambapo alipata huduma za dharura na baada ya muda mfupi akazinduka akaanza kushangaa akiangaza huku na kule akajikuta amezungukwa na manesi wawili na daktari kabla hajauliza chochote akaanza kusikia maumivu makali ya mkono.
“Nimefikaje hapa?” aliuliza Sarah huku akiugulia maumivu
“Umeletwa na rafiki yako ukiwa umepoteza fahamu. Vipi mkono unauma?” daktari alijibu na kuuliza
“Nasikia maumivu makali sana”
Daktari akamuangalia kisha wakamchukua kwenda kupiga X-Ray ikagundulika kuwa ameteguka kwenye kiwiko cha mkono akafungwa P.O.P na baada ya kuchekiwa na kuonekana kuwa hana matatizo mengine makubwa akaruhusiwa kuondoka ila aliambiwa asubiri kidogo kwenye benchi.
Wakati wote toka anazinduka hadi anapata matibabu mengine alikuwa akisimamiwa na nesi ambaye alikuwa ameombwa na Inspekta Ndilana na kuachiwa ‘posho ya usumbufu’ ila baada ya kuruhusiwa tu nesi akamtaarifu Inspekta Ndilana ambaye alikuwa nje muda wote. Inspekta Ndilana akaingia na kumkuta Sarah kwenye benchi.
“Pole”
“Ahsante” alijibu kwa sauti ndogo akionekana kama anayejitahidi kuvuta kumbukumbu
Inspekta Ndilana alimsaidia kwa kumsika ule mkono mzima akamuongozea kwenye gari kisha wakaanza safari ya kurudi kwa Sarah wakiwa kimya kabisa.
Ilikuwaje hadi Ndilana kufika kwa Sarah?
Baada ya kutoka kwenye mahojiano na SSP Haruna Majaliwa, Inspekta Ndilana alielekea moja kwa moja nyumbani kwake ikiwa yapata saa nane adhuhuri. Miadi ya kukutana na Alice ilikuwa ni saa kumi na mbili lakini hadi anamaliza kujiandaa ilikuwa kwenye saa 9.15 alasiri, akaona autumie muda ule kupita kumjulia hali Sarah kabla ya kwenda Kigamboni kumchukua Alice.
Muda ambao Inspekta Ndilana alikuwa akimrudisha Sarah nyumbani ilikuwa bado dakika chache itimie saa kumi na mbili ila alimuomba Alice amvumilie kidogo kwa kuwa kuna dharura imejitokeza kwa hiyo atafika saa moja kamili badala ya saa kumi na mbili kamili.
“Sikuwa nimevaa hili gauni” alivunja ukimya Sarah
“Nilikuvalisha” alijibu Inspekta Ndilana kwa utulivu
“Kwanini?”
“Khanga zako zilikuwa zimevuka na hata kama zingekuwa hazijavuka, nisingeweza kukupeleka hospitali na khanga, pia hakukuwa na mtu jirani zaidi yetu wawili. Samahani kwa hilo”
Ukimya ukatawala kwa muda huku Sarah akionekana kutafakari mambo kichwani mwake.
“Zilivuka au ulinivua?”
“Nna sababu gani ya kufanya hivyo?”
“Nauliza tu”
“Ulitaka nikupeleke hospitali na chupi tu, matiti nje au ulitaka nikiache pale pale hadi atokee mwanamke wa kukuvalisha?” alisema Inspekta Ndilana akionekana kukereka na maneno ya Sarah.
“Samahani” Sarah alijirudi
“Unajua Sarah, mimi hata nimpende vipi mtu, nikikosa tu ridhaa yake basi siwezi kufanya lolote la kulazimisha mapenzi au kufanya chuki yeyote. Mapenzi ni maridhiano ya pande mbili kutoka moyoni. Naelewa kuwa hunipendi kama ambavyo nilikuwa nakupenda na nimekubaliana na hali hiyo hivyo sina haja ya kufanya makusudi labda nikuone uchi wako au vipi, kwanza nikuone ili iweje? Nilikuja kukuona kwa vile afande aliniambia unaumwa na tulikuwa tukishirikiana katika kazi, na yalipotokea haya nikakusaidia kama binadamu mwingine yeyote kwa hiyo usinifikirie vyovyote” Inspekta Ndilana ‘alimchana’ Sarah
Maneno ya Inspekta Ndilana yalimfanya Sarah awe mpole kupita kiasi wakati huo gari lilikuwa linaingia nyumbani kwa Sarah, Inspekta Ndilana alisimamisha gari akajisachi na kumpa Sarah elfu 50. Sarah akawa anasita kuzipokea akabaki anaziangalia tu.
“Najua posho haijatoka na mshahara bado, na kwa kipindi hiki utakuwa na ahitaji ya ziada kutokana na hali yako kwa maana itabidi ukae na mtu. Fanya kama nakukopesha, ukipata posho au mshahara utanirudishia”
“Kama hivyo sawa. Ahsante” alijibu Sarah akizipokea hizo hela kisha akateremka na kuelekea mlangoni haraka haraka bila kuangalia nyuma. Kufika akagundua kuwa hana ufunguo, akageuka kutazama kwenye gari akakutana uso kwa uso na Inspekta Ndilana.
Inspekta Ndilana akaunyoosha mkono wake wenye funguo kama unaelekea kiunoni mwa Sarah, Sarah akawa ameshikwa na bumbuwazi. Inspekta Ndilana akaingiza ufunguo kwenye kitasa cha mlango na kuufungua huku Sarah akimkodolea macho wakiwa wamekaribiana kama wanaotaka kukumbatiana wakabaki wanatazamana usoni.
Sarah akashusha pumzi ndefu kisha akageuka haraka kutaka kukimbilia ndani, Inspekta Ndilana akamshika bega. Sarah akageuka ghafla na kukutana na busu la mdomoni na kumfanya apigwe na butwaa.
“Jioni njema” alisema Inspekta Ndilana akigeuka kuondoka na kumuacha Sarah kaganda pale mlangoni kama aliyepigwa na shoti ya umeme.
Inspekta Ndilana aliwasha gari lake na kuondoka eneo lile akimuacha Sarah akiwa bado kasimama mlangoni.
Ilikuwa saa moja kamili juu ya alama wakati gari la Inspekta Ndilana linawasili nyumbani kwa kina Alice, Inspekta Ndilana aliteremka akawa kaliegemea gari lake akimpigia simu Alice kumtaarifu kama ameshafika pale.
Alice alitoka akiwa amevaa gauni lake refu lililouchora mwili wake uliojaaliwa umbo la kuvutia na viatu virefu huku akiwa ametengeneza vyema nywele zake za asili kiasi cha kuonekana kama binti wa kutoka katika familia ya kifalme.
Alitembea kwa madaha kuelekea lilipo gari la Inspekta Ndilana ambaye alionekana wazi kuwa mtandao wa akili kichwani mwake unaingia na kutoka ‘network search’. Alice alifika hadi pale alipo Inspekta Ndilana na kumbusu shavuni ikawa kama ndiyo kamzindua toka ndotoni.
“Hi baby”
“Hi” Inspekta Ndilana alijibu akiwa kama aliyechanganyikiwa maana ana siku nyingi sana hajaitwa bebi, au watoto wa mjini wanasema ‘hajabebishwa’
Kwa jinsi ‘difensi ilivyopoteana’ katika akili ya Inspekta Ndilana hadi Alice akagundua kuwa hapa mtu mzima amepagawa ikabidi ampe tiba mbadala ili kumrudisha katika hali yake ya kawaida.
“Twende ukamsalimie mama” alisema Alice huku akimshika mkono Ndilana aliyekuwa akitembezwa kama mtoto anayepelekwa shule,
Wakafika sebuleni na kumkuta mama Alice akionekana kama alikuwa akisubiria Inspekta Ndilana aletwe mithili ya hakimu aliyekuwa akimsubiria mshtakiwa aletwe.
“Shikamoo mama”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Marahaba Jackson. Hujambo?”
“Sijambo”
“Alice kaniambia kuwa unamtoa jioni hii. Ni muendelezo wa upelelezi wa kesi au?”
“Hapana mama, tunanyoosha tu miguu”
“Kama mtuhumiwa na mpelelezi wa kesi, au?”
Inspekta Ndilana akakaa kimya kidogo, Alice akamwangalia mama yake kisha akamwangalia Inspekta Ndilana akatabasamu. Ilikuwa ni kiashiria cha kumwambia Inspekta Ndilana afunguke tu.
“Kiurafiki tu mama” alijibu kwa sauti ya mashaka
Mama Alice akamkazia macho Inspekta Ndilana baada ya kujibu vile. Bado kidogo Inspekta Ndilana aangalie chini ila alijikaza wakaendelea kutazamana kwa muda.
“Sawa, lakini huoni kama kuchanganya urafiki na kazi kunaweza kusababisha madhara?”
“Ndiyo maana tukachelewa kuwa marafiki mama, kwa sasa Alice anakaribia kupata uhuru wake kamili kwa kuwa tayari mwenendo wa upelelezi unamtoa katika tuhuma. Bado muda mchache tu”
“Sawa, siwezi kuwakataza kuwa marafiki kwa kuwa nyie ni watu wazima ila huo urafiki msifanye lolote la ziada kabla hamjaangalia ni kwa namna gani mtakuwa tayari kwa hicho mtakachokifanya” alisema mama alice akiwakazia macho Inspekta Ndilana na Alice huku wenyewe wakijisemea moyoni kuwa, ‘ungejua kama tayari wala usingesema’.
Baada ya kupata baraka za mama, Inspekta Ndilana na Alice walitoka kuelekea kwanza hotelini kwa ajili ya chakula cha jioni. Wakaingia katika hoteli mojawapo kubwa katikati ya jiji. Wakiwa katikati ya mlo huku wakionekana kukifurahia chakula, mhudumu alikuja na kikaratasi kilichokunjwa vizuri na kumkabidhi Inspekta Ndilana.
Inspekta Ndilana akakifungua na kukisoma kikawa kimeandikwa ‘nafurahi umejifunza kukirimu watuhumiwa wakati wa kuwahoji ila hiyo yako imepitiliza ha ha ha’
Inspekta Ndilana akaanza kupepesa macho huku na kule, wakati Alice akikisoma kile kikaratasi na baada ya kukimaliza akaungana na Inspekta Ndilana kuangaza huku na kule. Kwa mbali, Inspekta Ndilana akamuona mtu ambaye alimfanya ajihisi kubanwa na haja ndogo ghafla.
Alikuwa Afande Maswe akiwa na mkewe nao wakipata mlo kwenye meza ya saba toka walipo Inspekta Ndilana na Alice. Walipokutana macho kwa macho Afande Maswe alitabasamu na kumpungia mkono Inspekta Ndilana. Inspekta Ndilana akataka kuinuka lakini Afande Maswe akamzuia kwa ishara kuwa aendelee tu na mlo. Wakawa wanaendelea kula huku wakiwa wamepoteza amani, mara wakashtukia watu wawili wamewasimamia.
“Mmependeza sana vijana. Hamjambo?” alisema Afande Maswe
“Hatujambo shikamooni” walijibu kwa pamoja, Ndilana akitaka kuinuka na kuzuiwa na Afande Maswe.
“Marahaba” alijibu mama Maswe
“Sisi tunaenda bwalo la polisi kukumbuka kidogo enzi zetu kwenye muziki wa zamani” alisema Afande Maswe akitabasamu.
“Sawa afande, sisi bado hatujafikiria pa kwenda baada ya hapa” alijikakamua Inspekta Ndilana kujibu
“Mkikosa pa kwenda mje kutuunga mkono wazee wenu” alisema mama Maswe
“Kweli bwana mdogo. Ila kama mtajisikia huru kujichanganya na wazee”
“Tutakuja afande lakini hatutakaa sana” alijikakamua kujibu.
Baada ya masaa kama mawili hivi wote wakawa wanacheza muziki wa wazee sugu kwenye bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay. Wakaburudikwa kwa muda fulani kisha Ndilana na Alice wakaaga huku mke wa Afande Maswe akionekana kuwafurahia mno.
Ilikuwa yapata saa sita za usiku wakati Alice na Ndilana wakitoka pale bwalo kurudi Kigamboni kwa kina Alice. Japo walipanga kulala kwa Ndilana lakini waliona kuwa isingekuwa adabu kwa mama Alice kwa kuwa aliwaruhusu kutoka na hawakumtamkia kuwa Alice asingerudi.
Iliwachukua nusu saa tu toka Oysterbay hadi Kigamboni kwa kina Alice. Walipofika wakawa wamekaa kwenye gari kwa muda wakibusiana kuagana kiasi cha kutaka kupandisha mzuka.
“Utazoea kufanyia kwenye gari” Alice alimwambia Ndilana akimtoa mikono wake uliokuwa unaelekea kwenye himaya ya malkia.
Wakacheka kwa pamoja kisha Alice akatoka akijiweka vizuri na kufuatia na Inspekta Ndilana ambaye aliamua kumrudisha kama ambavyo alimtoa. Wakagonga mlango na kufunguliwa na mama Alice.
“Nimemrudisha Alice mama”
“Haya mwanangu ahsante”
“Haya mama, usiku mwema”
Taratibu Inspekta Ndilana akawa anaendesha kuelekea kwenye kivuko, wakati anakaribia kivuko akaona kuna gari ilikuwa imeegeshwa pembeni ikiwashwa taa kuingia barabarani. Alipoingia kwenye kivuko akiwa ndani ya gari lake na hiyo gari ikawa nyuma yake, akajikuta anaitilia mashaka.
Mara ghafla gari la Inspekta Ndilana likagongwa na lile gari kwa nyuma na kutumbukia baharini, watu wakaanza kuhaha huku na kule. Usiku huo huo taarifa zikawa zimezagaa kila kona ya jiji la Dar es Salaam kuwa kuna gari limetumbukia baharini.
Baada ya vyombo vya usalama kukusanya taarifa mbalimbali wakapata uthibitisho kuwa gari ambalo lilitumbukia lilikuwa ni la Inspekta Ndilana na mwenyewe akiwemo ndani. Ukawa ni msiba mzito kwa Afande Maswe, Alice na Sarah.
******
Yalikuwa yamepita masaa matatu toka Afande Maswe aingie ofisini kwake na kujifungia akiacha maagizo kuwa asibughudhiwe na yeyote kwa kuwa ana jukumu muhimu la kufanya lakini ukweli ni kuwa hakuwa na shughuli yeyote, alikuwa ametulia kimya akionekana kutafakari japo hakuwa na jambo analotafakari. Akili yake ilikuwa kama imekufa ganzi akajikuta ameduwaa tu.
Pamoja na kuwa sehemu nyingine shughuli zilikuwa zikiendelea kama kawaida lakini kila mmoja alionekana kuwa na mawazo yake, hali ilikuwa imetulia sana. Asilimia kuwa ya maaskari waliunganisha tukio lililomtokea Inspekta Ndilana na kesi aliyokuwa akiichunguza.
Kijana aliyegonga gari la Inspekta Ndilana alihojiwa sana lakini maafisa waliomhoji walijiridhisha kuwa ilikuwa ni ajali ya kawaida ila swali ambalo alikuwa akijiuliza Afande Maswe, ni kwa nini imtokee Inspekta Ndilana tena akiwa katikati ya kufanikisha uchunguzi wake.
Baada ya kumshtukia yule mwenye gari usiku ule, Inspekta Ndilana aliona kuwa kuna hatari endapo akiendelea kubaki ndani ya gari, akatoa loki za milango na wakati anaufungua mlango wa gari yake ndipo gari lake likagongwa na kutumbukia bahari ila yeye aliwahi kufungua mlango na kurukia kwenye maji wakati gari likitumbukia peke yake.
Kwa kutumia ujuzi wake wa kuogelea, Inspekta Ndilana aliogelea hadi ng’ambo ya pili kwenye maeneo ya Posta ya zamani. Akaanza kutembea pole pole hadi maeneo ya Bilicanas akakodi bodaboda hadi nyumbani kwake ambako alibadilisha tu nguo, akaziweka nguo alizozama nazo kwenye mfuko akaondoka.
Ilikuwa inakaribia saa kumi na moja alfajiri wakati Inspekta Ndilana alipokuwa akiwasili maeneo ya Kimara Baruti kwa rafiki yake wa siku nyingi, Frank Magige. Ni takribani miezi nane toka Ndilana aonane na Magige wakati huo Magige alikuwa kakamatwa akisafirisha magogo bila kibali ambapo iliishia kwa kupigwa faini na kutaifishiwa mzigo wake.
“Oya baba vipi, mbona asubuhi asubuhi?”
“We acha tu Magige, ningekuwa marehemu muda huu”
“Duh! Imekuwaje kaka?”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta Ndilana akatumia muda huo kumhadithia kila kitu Magige na kumuacha mdomo wazi
“E bwana eeh! Kama muvi vile daah!”
“Ndiyo hivyo ndugu yangu, nataka nipumzike kwanza ili nipate muda wa kutafakari”
“Kazi zenu nyinyi wakati mwingine za kiboya kweli!” Magige alianza maneno yake mabovu na kumfanya Inspekta Ndilana acheke tu na kujirusha kitandani.
Inspekta Ndilana na Magige walisoma wote kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kisha kila mtu akashika njia yake ambapo Ndilana akaendelea na shule na kuangukia kuwa askari wakati Magige akaangukia kwenye biashara za kuunga unga.
Giza lilipoingia, Inspekta Ndilana akachukua pikipiki ya Magige na kuvaa mavazi ya kujikingia na majeraha wakati wa ajali yaliyomfanya asijulikane kuwa ni nani, akatoka na kuelekea mjini. Wakati huo alishafanya mpango wa kupata simu toka kwa Magige, laini yake haikuharibika pamoja na simu japo ilikuwa pia imelowa wakati anaogelea.
Wakati huo Afande Maswe alikuwa ametulia nyumbani kwake akiwa na mkewe ambapo wote walikuwa kimya wakitafakari mambo yalivyokuwa.
“Masikini kijana wa watu” alianza kuongea mke wa Maswe.
“Ndiyo hivyo, kifo hakitabiriki. Laiti angejua asingeenda kigamboni.
Mara wakashtushwa na mlio wa simu ya Afande Maswe, Maswe aliichukua kuangalia namba inayopiga kisha ghafla akaitupa chini ikasambaratika huku mwenyewe akiwa kasimama akihemea juu juu huku mkewe akimshangaa
“Vipi?” mkewe alimuuliza kwa mshangao lakini Afande Maswe hakujibu neno. Mkewe akaichukua na kuiunga unga kisha akaiwasha ikaanza kuita tena, ikawa zamu yake kuangalia. Ghafla akabaki kaganda akitetemeka bila kusema neno.
Afande Maswe akajikaza na kuipokea
“Haloo!” alipokea kwa mashaka
“Ni mimi afande, sikufariki kwenye ajali”
“Uko wapi?” aliuliza Afande Maswe akiwa bado katika hali ya kutetemeka
Inspekta Ndilana akamuelekeza alipo Afande Maswe akamdanganya mkewe kuwa ni mtu tu aliyeokota simu ya Ndilana, hakutaka kumueleza akisubiri hadi ahakikishe.
Baada ya dakika kadhaa Inspekta Ndilana alikuwa amekaa na Afande Maswe kwenye bustani ya posta ya zamani mbele ya benki ya NBC huku Inspekta Ndilana akimueleza Afande Maswe namna tukio zima lilivyojiri ambapo Maswe alithibitisha mashaka yake kuwa ni lazima yule kijana alikusudia kusababisha ajali ya Ndilana.
Walijadili mengi na kufikia muafaka kuwa Afande Maswe amkabidhi mtu mwingine kesi ya mauaji ya Adrian Zayumba wakati huo huo Inspekta Ndilana aendelee na uchunguzi wake chini kwa chini. Maswe alimuagiza Ndilana kuwa aendelee kujificha hadi muda muafaka utakapojiri, pia alimwambia kuwa asiwasiliane na yeyote kwa muda huo hata Alice. Afande Maswe akarudi nyumbani kwake na kumuelezea ukweli mkewe.
Wakati hayo yakiendelea kulikuwa na msiba mzito sana nyumbani kwa Alice, Alice alikuwa kajifungia tu akilia na hakuna yeyote aliyeweza kumnyamazisha na hadi muda huo alikuwa amekwishapoteza fahamu mara kadhaa na hali yake ilikuwa inazidi kuwa mbaya kwa vile hakuweza kula chochote kiasi cha kumfanya atundikiwe dripu.
Asubuhi yake Afande Maswe aliikabidhi kazi ya upelelezi wa kesi ya Adrian Zayumba kwa askari mwingine ila kwa masharti kuwa kila hatua atakayoenda atatakiwa kutoa ripoti kabla kwa Maswe na baadaye kutoa taarifa ya kilichojiri.
Wakati huo huo Afande Maswe aliagiza kijana aliyemgonga Inspekta Ndilana akamatwe na kufikishwa ofisini kwake mara moja. Na baada ya masaa matatu kijana akawa mbele ya uso wa Afande Maswe.
“Unaitwa nani?”
“Moi Dinya” alijibu kijana akionekana kuwa hakuwa na wasiwasi hata chembe
“Pole na ajali”
“Ahsante”
“Unaweza kunielezea ulikuwa ukitoka wapi?”
Moi Dinya alikaa kimya kwa muda akionekana kubabaika huku akitafuta neno la kujibu
“Hujui ulipokuwa unatoka?”
“Nilitoka bichi, Mikadi Beach” alisema yule kijana kwa kubabaika.
“Una uhakika?”
“Ndiyo”
“Unaweza kuniambia kuwa mikadi kulikuwa na jambo gani lililokuwa likiendelea”
Moi Dinya alikaa kimya akiwa hana la kujibu
“Aron Chuwa”
“Naam” aliitikia chuwa anayeonekana mjanja mjanja.
Afande Maswe alihakikisha anapata maelezo yote muhimu toka kwa Chuwa kabla ya kumuweka mahabusu kwa kuwa alijua akimpa nafasi tu anaweza kurubuniwa asiongee.
******
Kutokana na maongezi ambayo waliongea Afande Maswe na Inspekta Ndilana na kwa kutumia hekima zake, Afande Maswe alimchukua mkewe na kuelekea Kigamboni kumuona Alice jioni baada ya muda wa kazi
“Hukuwa mikadi, sivyo”
Moi Dinya akaitikia kwa kichwa kukubali kuwa hakuwa akitokea huko
“Unajua kama kuna mtu alikuwa akikurekodi kila kitu ulichokuwa unafanya?”
Moi Dinya akaanza kutetemeka wazi wazi huku Afande Maswe akiwa ametulia akimtazama.
“Sikiliza Moi Dinya, wewe ni kijana mzuri sana na huonekana kama ni mhalifu ila umekubali kurubuniwa, sasa mimi nataka unijibu ukweli ili nijue jinsi ya kukusaidia.
Moi Dinya akawa anaitikia akiwa kama aliyepagawa.
“Ni nani aliyekutuma?”
“Mi siwajui nililetewa tu dili na rafiki yangu. Akaniambia kuwa nikifanikisha nitalindwa na sitapata tatizo lolote kwa kuwa itachukuliwa kama ni ajali ya kawaida”
“Anaitwa nani huyo rafiki yako?”
“Aron Chuwa”
“Ulishawahi kuonana na hao waliomtuma?”
“Ndiyo, ni mzee mmoja askari”
“Ukimuona utaweza kumjua?”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo”
“Huyo Aron Chuwa anapatikana wapi?”
Moi Dinya akatoa maelezo yote kuhusu namna ya kumpata Chuwa kisha akawekwa mahabusu ‘kwa usalama wake’. Afande Maswe akatuma vijana waende kumkamata Aron Chuwa na baada ya takribani masaa mawili akawa kaletwa mbele ya Afande Maswe.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment