Simulizi : Kivuli
Sehemu Ya Tano (5)
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***** ***** ***** *****
“KWA hiyo afande mtaniacha nimhoji peke yangu au mtaendelea kuwepo?” aliuliza Mwita
“Unaonaje kijana?”
“Mi nadhani mniache naye tu afande”
“Hapana afande msiondoke ataniua huyu” aliropoka SSP Majaliwa
“Ukimjibu anavyotaka, mtamaliza haraka kwa hiyo tutasubiri lakini ukiendelea na masihara sisi tutaondoka tuwaache mshughulikiane” alisema Kamishna Zebadayo
“Ntajibu” alisema Majaliwa akiwa kajawa na hofu
“Sikiliza, Koplo Malinda na Konstebo Bewa wameshatueleza kila kitu hivyo hata usipotoa maelezo yako tutayatumia yao kukufikisha mahakamani. Nieleze unachokijua upande wako ili haya yaishe mi nikaendelee na mitikasi yangu. Una dakika kumi” alisema Mwita akimwangalia kwa macho yake mekundu.
Maafisa wote walikuwa kimya wakisilikiza kwa makini wakati SSP Haruna Majaliwa akijiandaa kutoa maelezo yake.
“Nilikuwa nakuonjesha athari za bangi, na leo hapa sikuachii hadi unambie kila kitu. Na ukizingua nakuchapa kisha tunaendelea labda ufe ghafla ndio nitakuachia”
“Inspekta Mwita” aliita ofisa mmoja kati ya wale waliokuwa kwenye jopo lile na kumfanya Mwita amgeukie.
“Unasemaje afande?”
“Naona ubadili kidogo utaratibu wa mahojiano”
“Afande! Sikaidi agizo lako ila kila mtu ana mbinu zake za kumhoji mhalifu, halafu boya kama huyu ukimhoji kwa kuremba atatuwekea tu usiku. Au kama vipi mniache naye tu maafande nitawapa mrejesho
Maafisa wote wakabaki kimya kisha kiongozi wa maafisa hao Kamishna Zebadayo akamruhuru aendelee kumhoji kwa namna ambayo ataiona yeye kuwa inafaa. Kamishna Zebadayo alijua maana ya ACP Maswe kumpa kesi ile Inspekta Mwita.
Moi Dinya akatoa maelezo yote kuhusu namna ya kumpata Chuwa kisha akawekwa mahabusu ‘kwa usalama wake’. Afande Maswe akatuma vijana waende kumkamata Aron Chuwa na baada ya takribani masaa mawili akawa kaletwa mbele ya Afande Maswe.
“Aron Chuwa”
“Naam” aliitikia chuwa anayeonekana mjanja mjanja.
Afande Maswe alihakikisha anapata maelezo yote muhimu toka kwa Chuwa kabla ya kumuweka mahabusu kwa kuwa alijua akimpa nafasi tu anaweza kurubuniwa asiongee.
*********
Kutokana na maongezi ambayo waliongea Afande Maswe na Inspekta Ndilana na kwa kutumia hekima zake, Afande Maswe alimchukua mkewe na kuelekea Kigamboni kumuona Alice jioni baada ya muda wa kazi
Kutokana na hali waliyomkuta nayo, walibaki katika mtihani mzito wa au kumwambia arudi katika hali yake ya kawaida au kutomwambia adhurike. Ilibidi waamue kumchukua Alice ili hata wakimwambia asije akavujisha siri kuwa Inspekta Ndilana yuko hai.
Baada ya mabishano ya hapa na pale na kumthibitishia Mama Alice kuwa wanampeleka kwa mtaalamu ambaye ataweza kumfanya arudi katika hali yake ya kawaida, aliwakubalia waondoke naye kwa masharti kuwa wawe wanampa taarifa kwa kila kitakachokuwa kikiendelea.
Badala ya kwenda naye kwao wakaenda hoteli mojawapo iliyoko katikati ya jiji, wakaagiza vinywaji na Afande Maswe akaanzisha mazungumzo.
“Alice binti yangu”
Alice aligeuza macho kumwangalia Afande Maswe
“Hutakiwi kuwa katika hali hiyo kwa kuwa hakuna aliyethibitisha kuwa Jackson Ndilana amefariki”
“Unamaanisha nini?” aliuliza Alice kwa sauti ndogo ya kinyonge
“Kilichothibitishwa ni kuwa gari alilokuwa analiendesha limetumbukia baharini, ila hakuna anayejua kama alikuwemo ndani ya hilo gari au lah”
“Najua unataka kunipa moyo tu, angekuwa hajakuwemo asingeweza kukubali avumishiwe kifo”
“Yule ni askari kumbuka, anaweza kuwa na mipango yake”
Alice akamkazia macho Afande Maswe huku mkewe Maswe akiwaangalia.
“Naomba uniambie ukweli baba”
“Ndilana yupo hai”
Alice alikaa kimwa kwa muda akimwangalia afande Maswe kama ambaye hajasikia vizuri alichokisema.
“Ila jua kuwa uhai wake uko mikononi mwako, ukitoa habari kuwa hajafariki watamuua kweli. Nisingekwambia, ni mama yako hapa ndiye kanishinikiza nikwambie kwa vile alikuwa anakuonea huruma kwa hali uliyokuwa nayo”
“Yuko wapi?” Alice alikurupuka na swali
Kuna mtu atakuja kukuchukua akupeleke alipo.
Baada ya dakika chache Afande Maswe aliongea na simu kisha akamchukua Alice na kutoka naye nje ambako kulikuwa na pikipiki likisubiria na dereva.
“Huyu atakupeleka alipo Ndilana”
Safari ikaanza kimya kimya hadi Kimara kwa Magige. Walipoteremka Alice akawa kasimama akisubiri dereva ampeleke alipo Ndilana. Dereva akatoa helmet , alikuwa ndiye Ndilana.
Alice alibaki ameduwaa akimuangalia Ndilana kama ndiyo kwanza anamuona kisha bila kujua nguvu zilipotokea, Alice alikurupuka na kumdandia Ndilana akimkumbatia kwa nguvu kisha akamuachia na kuanza kumkagua kama ni kweli binadamu au mzuka.
“Alice, unajua ni jinsi gani nakupenda?”
“Najua Jackson”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Niambie ambacho hujawahi kuniambia”
Alice akashtuka na kurudi nyuma hatua moja akibaki kumkodolea macho. Ndilana akamshika mkono Alice na kuingia naye ndani.
“Baba, vita unaiweza” aliropoka Frank Magige na kumfanya Ndilana acheke.
Ndilana alipitiliza na Alice moja kwa moja chumbani bila kumpa nafasi Alice ya kusalimiana na Magige
“Jackson”
“Niambie”
“Kwanini unaniuliza hivyo?”
“Nimeambiwa jinsi ulivyokuwa baada ya kusikia nimekufa”
“Sasa badala ya kunipa pole unaniuliza swali gani hilo?”
“Kwa namna ulivyokuwa ni kama ulikuwa na uwezo wa kuepusha tukio lile halafu hukuchukua hatua. Ni jambo gani unalolijua?”
“Hakuna ninalokufischa”
“Nakupa muda, unieleze kila ambacho unakijua. Ukishindwa, uchukulie kuwa nimeshakufa na nakurudisha kwenu usiku huu huu” alisema Ndilana akimuwekea uso mkavu Alice
Ukimya ulitawala kwa muda wakitazamana.
“Najua waliomuua Adrian Zayumba, japo sina uhakika wa asilimia mia moja na sababu ya kumuua siijui”
“Nani?”
“Afande Majaliwa na wenzake”
“Unakumbuka ulinambia kuwa Majaliwa alikuwa anakupigia kukutaka?”
“Ndiyo”
“Ni wakati gani, kabla au baada ya kifo cha Zayumba?”
“Wakati wote”
“Una uhakika kuwa hakuna ambacho unanificha?”
“Hakuna”
Wakaangaliana kwa muda na kuanza kufurahia mapenzi yao.
********
Kitu cha kwanza alichofanya Inspekta Mwita, aliyekabidhiwa upelelezi wa kesi ya mauaji ya Adrian Zayumba ni kufuatilia taarifa zote toka uchunguzi wa kesi hiyo uanze. Alipoenda kukagua ofisi ya Inspekta Ndilana akaikuta imesafishwa, hakuna faili wala karatasi lolote.
Taarifa zilipomfikia Afande Maswe hakushtushwa sana kwa kuwa alishaambiwa na Inspekta Ndilana mahali alipohifadhi taarifa zote hivyo alichoofanya ni kumwambia kuwa aendelee na mahojiano na SSP Haruna Majaliwa wakati anashughulikia suala hilo.
Siku iliyofuatia, Inspekta Mwita akaandaliwa tena mahojiano na SSP Majaliwa mbele ya lile lile jopo la maafisa wa polisi ambao hawakuwa na habari kama Inspekta Ndilana yuko hai. Kutokana na makubaliano waliyofikia Inspekta Ndilana na Afande Maswe, Maswe hakusema chochote kuhusiana na kunusurika kwa Ndilana.
“Mmeniletea mvulana mwingine?”
“Afande nakuheshimu, ukiniletea dharau ntakuvuruga sekunde yeyote kuanzia sasa” alisema Inspekta Mwita ambaye sifa yake kubwa ni ukorofi.
Uamuzi wa Afande Mwita wa kumpa kesi hiyo Inspekta Mwita ilikuwa ni makusudi kutokana na tabia za ajabu ajabu za Inspekta Mwita ambaye huonekana kama mvuta bangi mbele ya viongozi na SSP Majaliwa ndiye alikuwa kiongozi wa kundi linalompaka matope Inspekta Mwita hivyo wawili hao ni chui na paka.
“Umeoa? Mvulana ni kijana ambaye hajaoa”
“Nimemuoa mama ‘ako mzazi”
“Unasemaje?” SSP Majaliwa aliuliza kwa ghadhabu.
Badala ya kujibu Inspekta Mwita alimkaba kwa nguvu SSP Majaliwa akitumia mkono mmoja huku mkono mwingine akiwa anamuonyeshea ngumi na kumfanya Majaliwa agwaye huku viongozi wengine wote wakiwa wametulia kimya.
“Nshakwambia sitaki tupotezeane muda kibwege bwege” alisema akimuachia kwa kumsukumia nyuma na kumfanya ayumbe yumbe na kujiachia kwenye kiti.
“Una siri gani na Wakili Pembe hadi ukaogopa ataisema ukaamua kumuua?” alianza kuuliza Mwita
“Sina siri wala sijamuua huyo mtu unayemtaja”
“Nimemtaja nani?”
“We ndiye umemtaja halafu unaniuliza mimi?”
“Unaona dhamira inavyokusuta, umemuua mtu hata kutaja jina lake unaogopa?”
Majaliwa anakaa kimya
“Au kwa sababu anajua kama umemuua Adrian Zayumba kwa vile mlikuwa mnagombea demu?”
“Unaongea nini wewe mvuta bangi” alifungua mdomo Majaliwa na kumfanya Mwita amchape makofi mawili makali sana kiasi cha kufanya maafisa wengine wasisimkwe na mwili.
“Nilikuwa nakuonjesha athari za bangi, na leo hapa sikuachii hadi unambie kila kitu. Na ukizingua nakuchapa kisha tunaendelea labda ufe ghafla ndio nitakuachia”
“Inspekta Mwita” aliita ofisa mmoja kati ya wale waliokuwa kwenye jopo lile na kumfanya Mwita amgeukie.
“Unasemaje afande?”
“Naona ubadili kidogo utaratibu wa mahojiano”
“Afande! Sikaidi agizo lako ila kila mtu ana mbinu zake za kumhoji mhalifu, halafu boya kama huyu ukimhoji kwa kuremba atatuwekea tu usiku. Au kama vipi mniache naye tu maafande nitawapa mrejesho”
Maafisa wote wakabaki kimya kisha kiongozi wa maafisa hao Kamishna Zebadayo akamruhuru aendelee kumhoji kwa namna ambayo ataiona yeye kuwa inafaa. Kamishna Zebadayo alijua maana ya ACP Maswe kumpa kesi ile Inspekta Mwita.
“Kwa hiyo afande mtaniacha nimhoji peke yangu au mtaendelea kuwepo?” aliuliza Mwita
“Unaonaje kijana?”
“Mi nadhani mniache naye tu afande”
“Hapana afande msiondoke ataniua huyu” aliropoka SSP Majaliwa
“Ukimjibu anavyotaka, mtamaliza haraka kwa hiyo tutasubiri lakini ukiendelea na masihara sisi tutaondoka tuwaache mshughulikiane” alisema Kamishna Zebadayo
“Ntajibu” alisema Majaliwa akiwa kajawa na hofu
“Sikiliza, Koplo Malinda na Konstebo Bewa wameshatueleza kila kitu hivyo hata usipotoa maelezo yako tutayatumia yao kukufikisha mahakamani. Nieleze unachokijua upande wako ili haya yaishe mi nikaendelee na mitikasi yangu. Una dakika kumi” alisema Mwita akimwangalia kwa macho yake mekundu.
Maafisa wote walikuwa kimya wakisilikiza kwa makini wakati SSP Haruna Majaliwa akijiandaa kutoa maelezo yake..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nakiri kuhusika na yote, nipelekeni mahakamani”
“Hakuna njia ya mkato we mzee, hapa utaongea neno kwa neno. Bila hivyo huendi mahakamani miaka mia na kila siku nakutia mikofi” aliropoka Mwita kwa hasira akimalizia na kumtia singi kichwani.
Kamishna Zebedayo akainuka na kuwaonyesha ishara maafisa wengine wainuke. Wakainuka.
“Endelea naye tu Mwita” alisema Kamishna Zebedayo akiwaongoza wenziye kutoka nje huku Majaliwa akipiga kelele kuwa wasiondoke.
Alichokifanya Inspekta Mwita alimkamata na kuanza kuugongesha uso wake kwenye meza ya mahojiano mara kadhaa na alipomuachia dawa zikawa zinamtoka puani na mdomoni kisha akaanza kumporomoshea matusi akimtishia kuwa lazima amtie kilema kabla ya kwenda mahakamani.
“Utaniua bure Mwita”
“Yaani nikikuua ndiyo moyo wangu utaridhika, umeninyanyasa sana hanithi wewe kwa kutumia cheo chako. Lazima nikutolee hasira na maumivu yangu yote”
Inspekta Mwita akaanza tena kumgongesha uso Majaliwa kabla hajakatizwa na ujio wa Afande Maswe.
“Shikamoo afande”
“Marahaba” aliitikia Afande Maswe akimwangalia SSP Majaliwa aliyekuwa hoi huku akivuja damu puani na mdomoni.
“Afande Maswe” aliita Majaliwa kwa sauti ya uchovu
“Naam”
“Kwanini mmeamua kunifanyia hivi?”
“Si ndivyo mnavyowafundisha vijana wenu kuwafanyia wahalifu, au?”
Majaliwa akabaki kimya akimwangalia Maswe kwa huruma. Maswe akamgeukia Mwita
“Tupishe kidogo Inspekta”
Mwita akatoka nje akionekana kuwa bado anamtamani SSP Majaliwa.
“Kamishna kaniambia kuwa amekuacha na huyu chizi, moja kwa moja nikajua kuwa anaweza hata kukuua na ndiyo maana nimekuja. Nieleze ukweli uondokane na hii adha ili uende mahakamani ukahukumiwe kwa haki, bila kusema ukweli na mimi nitashindwa kukusaidia” alisema afande Maswe kwa utulivu akimwangalia Majaliwa.
“Wale vijana wamewaelezaje?”
“Majaliwa, tunajua kila kitu na ingekuwa mimi ndiyo mwamuzi wa mwisho ningeipeleka mahakamani kwa ushahidi huu huu uliopo, lakini wewe ni afisa wa ngazi za juu katika jeshi na haiingii akilini kuwa unaweza kujihusisha na mambo hayo kwa jambo jepesi tu.”
“Ni jukumu lenu kujua, siyo mimi kuwaambia”
“Sawa Majaliwa, mimi naenda” aliongea Maswe akigeuka na kuanza kuondoka.
“Afande Maswe”
Afande Maswe akageuka kumwangalia Majaliwa
“Unasemaje?”
“Kulikuwa na mzigo wa tajiri mmoja ambao ulitakiwa kusindikizwa kwenda Arusha na yule tajiri alikuwa anamtumia Adrian Zayumba kama mtu wa kati kuwasiliana na mimi ili tumfanyie utaratibu. Tajiri huyo aliunganishwa kwangu na Shabani Kibope ambaye ni mmojawapo ya watu mliowahoji mara kadhaa” alianza kujieleza Majaliwa na kumfanya Afande Maswe arudi kumsikiliza.
“Enhe”
“Mimi ile kazi nikawapa Riwa ambaye mlimuua kwa risasi, Koplo Malinda na konstebo Bewa ambao wako mahabusu. Tukapewa kianzio na ilikuwa baada ya kuufikisha mzigo huo huyo tajiri atumalizie kiasi kilichobaki. Vijana wakafanya kazi kwa uaminifu na huyo tajiri akawa mwaminifu kumpa kiasi kilichobakia Adrian Zayumba lakini badala ya kutulipa, Zayumba akabana hela zetu. Na ndipo ulipoanza ugomvi kati yetu na Adrian Zayumba”
Maswe akawa kimya akiendelea kumwangalia Majaliwa usoni.
“Baada ya kutokea suala la kudaiana mtoto kati ya Zayumba na Alice tukawa tunalifuatilia kwa iyokaribu kwa kumtumia wakili Hamis Mzee Pembe na alipotoa taarifa kuwa Alice ametorokwa kwa lengo la kumuua Zayumba tukaamua kuutumia upenyo ule ili tumtumie Alice kama kivuli”
“Alice alikuwa anajua kama anatumika kama kivuli”
“Ndiyo”
“Muda gani alijua kama anatumika kama kivuli, mara tu baada ya mauaji, Alice mimi ni mpenzi wangu ila hatukuweza kuendelea kipindi hiki kutokana na tatizo la hii kesi”
Ghafla Afande Maswe akaanza kujihisi mapigo ya moyo yanaongezeka na damu ikienda kwa kasi baada ya kupata habari ile ya Alice.
“Ni tajiri gani?” akazuga kuuliza swali jingine
“Nasikitika kuwa siwezi kukutajia kwa maana hata nikikutajia hutakuwa na ushahidi wa kumhusisha na chochote”
“Said bin Mahmood?”
Majaliwa akashtuka na kujiweka vizuri kwenye kiti
“Umejuaje?”
“Nilishakwambia Majaliwa kuwa tunajua kila kitu na lengo langu ilikuwa unieleze ukweli ili nijue nI kwa namna gani nitakusaidia, kwa kuwa kama ujuavyo umefanya kazi miaka mingi hivyo sitafurahi endepo nikikuona unapoteza haki zako zote”
“Unataka kujua nini zaidi ya haya niliyokwambia?”
“Mmemuua Ndilana kwa ajili ya kupeleleza kesi au kwa kuwa anatembea na Alice”
“Alice ni Malaya tu, siwezi kumuua mtu kwa ajili yake kikubwa ni nilitaka kulinda mafao yangu”
“Nieleze kuhusu Alice nami nitakulinda”
“Kwanini uko unataka sana kujua kuhusu Alice?”
“Utanieleza au?”
“Siwezi kukueleza mengi kuhusu Alice lakini ni mwanamke ambaye hajui kumkataa mwanamme ila pale bwana mdogo Ndilana alijiona kapata sana. Wakati yuko Kilwa mara nyingi nilikuwa namfuata ila mara ya mwisho nilienda bila taarifa nikamfumania na Mzungu nikaamua kumpotezea kwa muda, yule na wale wenzake lao moja tu, wanajiuza”
“Unajua yuko wapi hivi sasa?”
“Yuko Kimara ila najua atakuwa kapata tu bwana mpya”
“Umejuaje?”
“Hawezi kwenda mahali bila mimi kujua”
“Umewasiliana naye vipi wakati uko ndani?”
“Kuna watu anawasiliana nao wananifikishia taarifa”
“SSP Idrisa anahusikaje na masuala yenu?”
“Hajui chochote, kwa kuwa najua ni mtu wa kufanya maamuzi kwa jazba nilikuwa nikikutana naye baa ‘namtia ndimu’ kuhusiana na kesi naye anakuja kuwacharukia kituoni”
“Sawa. Nikuache na Mwita?”
“Hapana afande, ataniua”
Afande Maswe akaagiza Majaliwa arudishwe mahabusu.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
******
Ulifanyika mpango wa ‘kumrudisha Inspekta Ndilana duniani’ ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku. Siku hiyo usiku, ilikuwa Ndilana akajilaze ufukweni akiwa na mavazi yake yale yale kisha mtu aliyepandikizwa amuokote na kumpeleka kwenye hospitali moja ya binafsi kisha mtu huyo atoe taarifa polisi katika kituo kilichopangwa.
Mambo yote yakaenda kama yalivyopangwa, wakati Ndilana ameandaliwa tayari kuokotwa na msamaria mwema aliyepangwa. Zikaonekana boti mbili za kizamani zikijongea maeneo yale na kuzimwa taa za karabai zilizokuwa zikitumika kutoa mwanga na kutia nanga maeneo yale yale.
Baada ya dakika chache wakatitokeza askari watano wenye silaha na kuanza kuranda randa huku na kule wakionekana kama wanalinda jambo fulani. Baada ya kujiridhisha kuwa kila kitu kiko sawa wakawaonyesha ishara wale watu waliokuwa kwenye boti kisha wale watu wakaanza kuteremsha shehena ya mizigo.
Wakati huo yule msamaria aliyekuwa amepandikizwa alikuwa ndiyo anawasili kwa ajili ya zoezi la kumuokota Ndilana, ikabidi ajibanze sehemu ili kuangalia kinachoendelea. Baada ya watu wale kumalizia kushusha mizigo yao, wale askari wakaangaza huku na kule wakizunguka zunguka mara mmojawao akamulika tochi yake kwenye mwili wa Ndilana.
Yule askari akamuita kiongozi wao
“Afande Ditu”
Musa Kasongi Ditu akakurupuka na kukimbilia eneo lile kwa tahadhari kubwa, kuona hivyo yule msamaria mwema akakurupuka na kutimua mbio jambo lililowashtua wale askari wengine watatu waliobaki na kupiga kelele
“Afande kuna mtu”
“Mkamateni”
Wale askari wakaanza kumkimbiza yule msamaria mwema ambaye sasa alikuwa akikimbia huku akipiga kelele.
“Piga risasi” aliagiza Ditu
Mara milio ya risasi ikasikika kisha ukatoka ukulele mkubwa na baadaye kutawaliwa na kimya kikubwa.
“Safi sana” alisema Kasongi Ditu na kuvunja ukimya ule.
Baada ya dakika kadhaa wakaonekana watu watatu wakiuburuta mwili wa mtu mmoja gizani wakijongea walipo Kasongi Ditu na yule askari mwingine.
“Inabidi tuondoke na huo mwili tukaufukie sehemu, na huyu tumbebe tukammalizie mbele ya safari”
Mara wakawa wanamulikwa na taa za gari jingine kitendo kilichowafanya washtuke sana, Kasongi Ditu alipowageukia wenzake akakuta kuwa wale watatu waliokuwa wanauburuza ule mwili siyo wenzake, ni maaskari wengine ila ule mwili uliokuwa unaburutwa ndiyo wa mwanzao.
“Mko chini ya ulinzi” ilisikika sauti ya Afande Maswe ikitokea kwenye gari.
Wakabebwa wote, pamoja na wale wenye mizigo na mizigo yao hadi kituo cha kati.
Mpango wa kumrudisha Inspekta Ndilana ukawa umevurugika ikabidi aingie moja kwa moja kwenye kazi ila wakati wanaingia pale kituoni, askari waliokuwa kaunta ilibidi watimue mbio kwa kudhani kuwa wameingiliwa na mzuka.
Ilichukuwa muda kuweka kila kitu sawa, wakawa kwenye chumba cha mahojiano wakiwahoji waliokamatwa mmoja mmoja kwa zamu kwa kuanzia na Musa Kasongi Ditu aliyekuwa kiongozi wa zoezi lile.
“Mlipata wapi silaha wakati leo wote mliokamatwa mko mapumziko”
“Kwenye ghala la kikosi cha kuzuia fujo”
“Ilikuwaje mkapewa”
“Mbona watu wengi tu wakiwa na kazi zao binafsi wanapewa? Ni hela yako tu”
Walipomaliza tu mahojiano na Kasongi, watu wote waliokuwa zamu katika stoo ya silaha wakakamatwa huku mahojiano na wengine yakiendelea.
Mahojiano yalipokamilika, ikagundulika kuwa ile mizigo ilikuwa ni ya mfanyabiashara mmoja maarufu sana nchini ambaye naye akatiwa nguvuni.
Ikabidi Mkuu wa Jeshi la aunde timu maalum ya kuchukuza mienendo ya maaskari polisi akiihusisha idara ya usalama wa taifa.
*******
Baada ya kurudi rasmi duniani, Inspekta Ndilana alifika ofisini kwake na kutulia kimya akitafakari masuala yote yanayojitokeza toka alipoanza upelelezi wa kesi ya Adrian Zayumba. Kilichokuwa kikimtatiza haswa ni kitendo cha nguvu kubwa kutumika kumzuia ili asiendelee na uchunguzi wa kesi yake.
Wakati akitafakari hayo na mengineyo, mlango wake ulifunguliwa ghafla, Afande Steven Maswe akaingia na kumfanya Inspekta Ndilana ainuke na kutoa heshima kisha akampisha Afande Maswe kwenye kiti chake naye kukaa cha wageni.
“Alice umerudi naye toka Kimara?”
“Ndiyo, amerudi kwao”
“We unamuonaje Alice”
“Sijakuelewa afande”
“Namaanisha kwa kipindi ulichokuwa naye karibu, unamuona ni mwanamke wa aina gani?”
Inspekta Ndilana akakaa kimya kwa muda akionekana kutafakari. Akilini mwake alijua kuwa kuna jambo ambalo afande wake anataka kumwambia kuhusu Alice japo hajajua ni jambo gani.
“Swali gumu Inspekta?”
“Hapana afande, nilikuwa najaribu kuvuta kumbukumbu zangu vyema. Kwa kweli sijafanya juhudi zozote za kumfahamu Alice nje na masuala yanayohusu kesi niliyokuwa naichunguza”
“Ushawahi kumhoji kuhusiana na namba ya SSP Haruna Majaliwa?”
Ndilana akashtuka kidogo na kuongeza umakini akijibu “ndiyo”.
“Alisemaje?”
“Alidai kuwa ilikuwa ikimpigia kumtongoza, na ilionekana kuwa ni ya mtu anayemfahamu ila yeye hakuwahi kujua kama ni ya nani”
Afande Maswe alimwangalia Ispekta Ndilana kwa umakini akitingisha tingisha mguu wake mmoja hali iliyofanya mapigo ya moyo ya Inspekta Ndilana yaanze kwenda kasi.
“Uliyaamini maelezo yake?”
“Sikuyatilia maanani afande kwa kuwa lengo lilikuwa ni kumjua mwenye namba na tayari tulikuwa tushamjua, ila baada ya wewe kuniuliza muda huu ndipo nimegundua kuwa nilitakiwa kuingia ndani zaidi”
“Vyema. Ingia ndani zaidi”
“Samahani afande, unajua ni kwa namna gani najitoa katika kazi yangu, naomba kama una lolote la kuweza kunisaidia katika hili uniambie”
Afande Maswe akamwangalia kwa muda kisha akatoa kifaa kidogo cha kurekodia akakiwasha, yakaanza mahojiano kati ya Maswe na SSP Haruna Majaliwa…..
Mwita: Shikamoo afande
Afande Maswe: Marahaba
SSP Majaliwa (sauti ya uchovu): Afande Maswe
Afande Maswe: Naam.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SSP Majaliwa: Kwanini mmeamua kunifanyia hivi?
Afande Maswe: Si ndivyo mnavyowafundisha vijana wenu kuwafanyia wahalifu, au?
Kimya kinatawala kidogo kisha…
Afande Maswe: Tupishe kidogo Inspekta
Vinasikika vishindo vya miguu kisha…
Afand Maswe: Kamishna kaniambia kuwa amekuacha na huyu chizi, moja kwa moja nikajua kuwa anaweza hata kukuua na ndiyo maana nimekuja. Nieleze ukweli uondokane na hii adha ili uende mahakamani ukahukumiwe kwa haki, bila kusema ukweli na mimi nitashindwa kukusaidia
SSP Majaliwa: Wale vijana wamewaelezaje?
Afande Maswe: Majaliwa, tunajua kila kitu na ingekuwa mimi ndiyo mwamuzi wa mwisho ningeipeleka mahakamani kwa ushahidi huu huu uliopo, lakini wewe ni afisa wa ngazi za juu katika jeshi na haiingii akilini kuwa unaweza kujihusisha na mambo hayo kwa jambo jepesi tu.
SSP Majaliwa: Ni jukumu lenu kujua, siyo mimi kuwaambia
Afande Maswe: Sawa Majaliwa, mimi naenda
Vinasikika vishindo vya miguu kisha…
SSP Majaliwa: Afande Maswe
Afande Maswe: Unasemaje?
SSP Majaliwa: Kulikuwa na mzigo wa tajiri mmoja ambao ulitakiwa kusindikizwa kwenda Arusha na yule tajiri alikuwa anamtumia Adrian Zayumba kama mtu wa kati kuwasiliana na mimi ili tumfanyie utaratibu. Tajiri huyo aliunganishwa kwangu na Shabani Kibope ambaye ni mmojawapo ya watu mliowahoji mara kadhaa
Afande Maswe: Enhe
SSP Majaliwa: Mimi ile kazi nikawapa Riwa ambaye mlimuua kwa risasi, Koplo Malinda na konstebo Bewa ambao wako mahabusu. Tukapewa kianzio na ilikuwa baada ya kuufikisha mzigo huo huyo tajiri atumalizie kiasi kilichobaki. Vijana wakafanya kazi kwa uaminifu na huyo tajiri akawa mwaminifu kumpa kiasi kilichobakia Adrian Zayumba lakini badala ya kutulipa, Zayumba akabana hela zetu. Na ndipo ulipoanza ugomvi kati yetu na Adrian Zayumba. Baada ya kutokea suala la kudaiana mtoto kati ya Zayumba na Alice tukawa tunalifuatilia kwa iyokaribu kwa kumtumia wakili Hamis Mzee Pembe na alipotoa taarifa kuwa Alice ametorokwa kwa lengo la kumuua Zayumba tukaamua kuutumia upenyo ule ili tumtumie Alice kama kivuli
Afande Maswe: Alice alikuwa anajua kama anatumika kama kivuli
SSP Majaliwa: Ndiyo
Inspekta Ndilana anashtuka na kujiweka vizuri huku Afande Maswe akimwangalia kwa umakini huku mahojiano ya Afande Maswe na SSP Majaliwa yakiendelea…
Afande Maswe: Muda gani alijua kama anatumika kama kivuli
SSP MAjaliwa: Mara tu baada ya mauaji, Alice mimi ni mpenzi wangu ila hatukuweza kuendelea kipindi hiki kutokana na tatizo la hii kesi
Afande Maswe: Ni tajiri gani?
SSP Majaliwa: Nasikitika kuwa siwezi kukutajia kwa maana hata nikikutajia hutakuwa na ushahidi wa kumhusisha na chochote
Afande Maswe: Said bin Mahmood?
SSP Majaliwa: Umejuaje?
Afande Maswe: Nilishakwambia Majaliwa kuwa tunajua kila kitu na lengo langu ilikuwa unieleze ukweli ili nijue nI kwa namna gani nitakusaidia, kwa kuwa kama ujuavyo umefanya kazi miaka mingi hivyo sitafurahi endepo nikikuona unapoteza haki zako zote
SSP Majaliwa: Unataka kujua nini zaidi ya haya niliyokwambia?
Afande Maswe: Mmemuua Ndilana kwa ajili ya kupeleleza kesi au kwa kuwa anatembea na Alice
SSP Majaliwa: Alice ni Malaya tu, siwezi kumuua mtu kwa ajili yake kikubwa ni nilitaka kulinda mafao yangu
Afande Maswe: Nieleze kuhusu Alice nami nitakulinda
SSP Majaliwa: Kwanini uko unataka sana kujua kuhusu Alice?
Afande Maswe: Utanieleza au?
SSP Majaliwa: Siwezi kukueleza mengi kuhusu Alice lakini ni mwanamke ambaye hajui kumkataa mwanamme ila pale bwana mdogo Ndilana alijiona kapata sana. Wakati yuko Kilwa mara nyingi nilikuwa namfuata ila mara ya mwisho nilienda bila taarifa nikamfumania na Mzungu nikaamua kumpotezea kwa muda, yule na wale wenzake lao moja tu, wanajiuza
Afande Maswe: Unajua yuko wapi hivi sasa?
SSP Majaliwa: Yuko Kimara ila najua atakuwa kapata tu bwana mpya
Afande Maswe: Umejuaje?
SSP Majaliwa: Hawezi kwenda mahali bila mimi kujua
Afande Maswe: Umewasiliana naye vipi wakati uko ndani?
SSP Majaliwa: Kuna watu anawasiliana nao wananifikishia taarifa
Afande Maswe: SSP Idrisa anahusikaje na masuala yenu?
SSP Majaliwa: Hajui chochote, kwa kuwa najua ni mtu wa kufanya maamuzi kwa jazba nilikuwa nikikutana naye baa ‘namtia ndimu’ kuhusiana na kesi naye anakuja kuwacharukia kituoni
Afande Maswe: Sawa. Nikuache na Mwita?
SSP Majaliwa (kwa hamaki):Hapana afande, ataniua
Afande Maswe (kwa sauti kubwa): Mwitaaa!
Mwita (kwa mbali): Naam Afande
Vinasikika vishindo vya miguu, kisha
Afande Maswe: Mrudishe mahabusu
Inspekta Ndilana alijikuta akishindwa kuwaza wakati huo Afande Maswe alikuwa akizima kifaa chake cha kurekodia sauti. Jasho lilikuwa likimtiririka Inspekta Ndilana kiasi cha kulowesha nguo zake mithili ya mtu aliyetoka kunyeshewa na mvua.
“Una mtazamo gani kuhusiana na mahojiano uliyoyasikiliza?”
“Kwa kweli afande, sijui cha kuwaza hadi muda huu”
“Sawa, jifikirie kisha kati ya saa tisa na saa kumi uje ofisini kwangu”
Afande Maswe aliinuka na kutoka akimuacha Ndilana anatweta kama jogoo lililotoka kufukuza tembe halafu likamkosa.
Yalipita masaa mawili, Inspekta Ndilana akiwa ameduwaa asijue cha kufanya, wakati huo tayari alikuwa amezima simu yake baada ya kupata ujumbe kutoka kwa Alice kuwa amemmiss naye kukosa jibu la haraka haraka la kumpa.
Mwanzoni alitaka kutoamini maneno ya SSP Haruna Majaliwa lakini kitendo cha Majaliwa kujua kuwa Alice alikuwa Kimara ndicho kilimfanya awe na uhakika kuwa aliyoyasema Majaliwa ni ya kweli. Ndilana akawa akiwaza maneno ambayo Alice alikuwa akimwambia wakati wako kitandani akajikuta anadondosha mchozi..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Inspekta Ndilana akakumbuka maneno aliyoambiwa na mzee mmoja miaka mingi iliyopita kuwa duniani kuna vitu viwili tu ambavyo hutakiwi kuviwekea uhakika, ni hali ya hewa na wanawake. Alisema kuwa mwanamke anaweza leo akakuhakikishia kuwa anakupenda kuliko chochote halafu kesho yake akakuacha na kumrudia bwana wake wa zamani aliyemfukuza kwa matusi. Halafu akiulizwa akasema tu kuwa we unamboa kwa kuwa unampenda sana, yeye anataka mwanamme wa kumtimua timua.
Inspekta Ndilana akaamua kwenda kwa Afande Maswe na kumuomba binafsi ampe mapumziko ya siku tatu ili akili yake ikae sawa.
“Pole Jackson”
“Ahsante afande”
“Sipendi ukae peke yako, nakuhitaji sana kwa kazi kipindi hiki”
“Kwa akili yangu ilivyo afande, sidhani kama nitaweza kukusaidia chochote”
“Nakujua Inspekta, wewe ni kijana imara sana ambaye unaweza kutumia matatizo kupata faida unayotaka . nakutaka uendelee na kazi, sikupi hata robo saa ya mapumziko”
“Sawa afande, nipe majukumu name nitayatekeleza lakini kwa kupanga mwenyewe cha kufanya siwezi. Akili yangu imegoma kuzunguka”
“Nataka ukaongee vizuri na Sarah, nadhani anaweza kuwa na taarifa zaidi ya alizokuwa anakupa”
“Sawa Afande” Ndilana alijibu kwa unyonge huku akitoka taratibu ofisini kwa Afande Maswe.
Wakati Inspekta Ndilana akitoka, Afande Maswe alikumbuka kuwa Sarah anaweza asiwe na taarifa kama Ndilana hakufa ikabidi ampigie simu kumtaarifu kwa namna ambayo haikuwa rahisi kwa Sarah kujua kama alikuwa anataarifiwa kwa kuwa Maswe alimpigia kama kumjulia hali na katika maongezi akagusia hilo.
Ilikuwa yapata saa moja jioni wakati Ndilana anayeonekana kama amefiwa akiwasili nyumbani kwa Sarah. Sarah alionyesha kuupuuzia sana ujio wa Ndilana tofauti na matarajio ya Ndilana. Kitu kingine kilichomshangaza Ndilana ni kwamba hata pole hakupewa na Sarah pamoja na yote yaliyomtokea. Ndilana akabaki anang’aa ng’aa macho mule ndani huku Sarah akiwa kama ambaye anamwambia ongea uondoke zako.
“Unaweza kunielezea kuhusu ujio wako”
“Sarah”
“Sema”
“Hujapendezwa na mimi kuja hapa?”
“Kwani kukuuliza ni tatizo?”
“Ok. Tuyaache, nilikuwa hapo baa ya jirani nikaona nipite kukusalimia”
“Ahsante mimi nipo”
Maongezi yakawa wameishia hapo, Ndilana akawa hana tena cha kuongea na Sarah akawa anamwangalia kama anayemwambia kuwa kama huna la ziada safari njema. Baada ya kutazamana kwa dakika kadhaa ikabidi Ndilana aage bila kufanya kilichomleta.
“Mimi niko hapo baa”
“Uko hapo baa au mko hapo baa?”
“Niko hapo baa”
“Mwenzio umemuacha wapi leo?”
“Nisingependa kuzungumzia mambo hayo” alijibu Ndilana akiinuka kutaka kuondoka.
“Subiri kidogo” alisema Sarah akiinuka kuelekea chumbani kisha akarudi akiwa na noti tano za elfu kumi kumi.
“Mzigo wetu huu”
Ndilana alibaki akimtazama Sarah aliyekuwa anamlipa elfu hamsini za kipindi kile alipokuwa akitoka hospitali baada ya kuumia. Ndilana kwa kumuonyesha ukauzu akazipokea kisha akatoa waleti yake iliyokuwa na karibia laki nne, akaziongezea zile elfu hamsini na kuirudisha waleti mfukoni ikionekana kutuna sana.
Ndilana akageuka bila kusema neno na kutoka.
“Niagizie Saint Anne kama hutajali” aliagizia Sarah
“Uje kufuata”
Alijibu Ndilana bila kusimama.
Baada ya kunywa mbili tatu huku akitafakari haya na yale, Ndilana alishtuliwa na mtu aliyesimama karibu yake kabisa. Kuangalia alikuwa Sarah…
“Inaelekea una mawazo sana leo”
“Ah! Najihisi nimevurugwa tu”
“Poa, nimefuata wine yangu”
“Nenda kaunta waambie wakupe ntalipa”
“Mnh!”
“Unaguna nini?”
“Si uniagizie, hujui kumhudumia mwanamke! Loh!”
“Maigizo siyawezi” Ndilana alijibu akimuonyesha ishara mhudumu aje
“Unamaanisha nini?”
“Wanawake ni watu wasioleweka, akikupenda hujui akikuchukia hujui na mbaya zaidi ukiwa unampenda kweli hakuamini ukiwa unamzuga ndiyo anadhani unampenda kweli. Upuuzi mtupu, mi sasa hivi ninachoamini kwa mwanamke ni ngono tu kwa kuwa huwezi kufanya naye ngono ikawa anakudanganya kuwa mnafanya wakati hamfanyi” alitiririka maneno Ndilana na kumfanya Sarah abaki kaduwaa wakati Mhudumu akifika.
“Karibu ukae dada”
“Hapana sikai, niletee mzinga wa Saint Annie, naondoka nao”
Mhudumu anaondoka huku Sarah akiwa bado anamkodolea macho Ndilana.
“We kweli leo umevurugwa”
“Na wewe ukazidisha kunivuruga”
“Nimefanya nini”
“Mtu nimefunga safari toka kwangu kuja kwako nipate mtu wa kupiga naye stori, matokeo yake unaniletea niaje niaje”
Mhudumu alirudi na alichoagizwa huku Sarah akimwangalia Ndilana. Mhudumu anamkabidhi Sarah. Inspekta Ndilana alijimiminia kinywaji chake na kuiweka glasi mezani kwa nguvu huku Sarah akiendelea kumkodolea macho. Inspekta Ndilana anatoa waleti yake na kuchomoa noti kadhaa na kumkabidhi mhudumu.
“Kalipie na ulete mahesabu yote hapa, nianze kula vitu upya” alisema Ndilana akimwangalia mhudumu
“I’m sorry afande, sikuwa na nia ya kukufukuza” aliongea Sarah akionekana kujawa na aibu kutokana na tabia aliyomuonyesha Ndilana.
“Usiwaze. Beba mzinga wako katulie nyumbani, acha niwaze na kuwazua hapa”
“Twende ukanywee kwangu afande” alisema Sarah kwa kuwa alimuona Inspekta Ndilana akielekea kuzidiwa na kinywaji.
Inspekta Ndilana akacheka wakati mhudumu anakuja na karatasi la mahesabu, Ndilana analiangalia kisha anamwambia amuongeze kinywaji na kumgeukia Sarah…
“Una baa nyumbani kwako?”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Si iko karibu, nitakuwa nafuata mimi vinywaji”
“Hapana Sarah, nahitaji kuwa peke yangu”
“Utakuwa peke yako lakini ukiwa kwangu siyo hapa, hapa siyo pazuri sana kiusalama na wewe unafanya kazi zinazotengeneza maadui wengi” alisema Sarah akikusanya vinywaji vya Inspekta Ndilana ambaye alikuwa akicheka kimoyomoyo kuwa mtego wake umeitika.
Baada ya masaa kadhaa, Sarah na Inspekta Ndilana wakawa wanakunywa huku wanapiga stori mbalimbali za maisha kabla Sarah hajarudisha stori za Alice.
“Umepita muda mrefu sisikii ukitafutwa japo kwa simu, mpenzi wako yuko wapi?”
“Tumeachana”
“Imekuwaje wakati penzi lilikuwa limenoga hadi kupitiliza”
“Nimemgundua kuwa siyo”
“Ndiyo maana ukapagawa hivyo?”
“Mnh! Una maswali mengi…”
“Mi ni polisi, unashangaa?”
Walicheka kwa muda kisha Inspekta Ndilana akamdanganya Sarah kuwa amemfumania Alice, Sarah akakaa kimya kwa muda kisha…
“Hivi ulimchunguza kabla ya kuwa naye?”
“Hapana. Ukimchunguz asana bata humli”
“Yule ni mmojawapo wa mademu wanaotumika katika uhalifu”
“Umejuaje Sarah?”
“Nisiwajue wanawake wa mjini mimi?”
Sarah akaanza kumpa Inspekta Ndilana stori za Hadija, Salome na Alice. Kwa mara ya kwanza Inspekta Ndilana akajiona kuwa alikuwa anachoreka ile mbaya kuwa katika uhusiano na Alice japo ni kweli anampenda sana.
Inspekta Ndilana akaanza kuwaza stori alizopewa na Alice kuwa hapendi sana wanaume akalinganisha na ‘mavituz’ aliyokuwa akipewa na Alice kitandani, akajiona mjinga sana kwa kumuamini Alice. Alice alionekana ni fundi kupita kiasi kunako kitanda kiasi kwamba wakati mwingine Ndilana alikuwa akionekana kama mwanafunzi wa chekechea.
Inspekta Ndilana akatumia fursa hiyo kupata habari za mtandao wa uhalifu unaohusisha polisi na raia, waliongea mengi sana na Inspekta Ndilana akapata taarifa za kutosha kuhusiana na kila ambacho Afande Maswe alikuwa akikitaka.
Kwa kadiri muda ulivyokuwa unaenda, pombe zilikuwa zikiwakolea huku stori zikiwaishia mwisho wakajikuta wakinywa kimya kimya huku mawazo ya ngono yakianza kumtawala Ndilana, akawa anaukagua mzigo kimoyomoyo akipanga namna ya kuvunja ukimya. Wakati akikaribia kupata jawabu, mlango ukagongwa na kuwashtua, akaingia kijana mmoja mtanashati na kukaa kwenye kochi mojawapo akitingisha tingisha mguu kama anayefuatisha mdundo wa muziki kutafuta namna ya kuanza kurap.
“Afande huyu ni mchumba wangu anaitwa Harison”
“Nimefurahi kumfahamu” alisema Ndilana akiwa amejawa na donge kubwa moyoni
“Harison, huyu ni afande wangu, anaitwa Inspekta Jackson Ndilana”
“Uafande hadi home, inakuwaje?”
Sarah anainuka haraka haraka na kumshika mkono Harison kutaka kumnyanyua
“Tukaongee kwanza ndani”
“We chanika tu hapa hapa, siendi kokote”
Inspekta Ndilana akakaa kimya akiangalia tu kinachoendelea.
Sarah anakaa pembeni ya Harison
“Siyo hivyo unavyofikiria mpenzi”
“Kumbe?”
“Amekuja tu kunisalimia, ndiyo yule niliyekwambia kuwa alizama baharini”
“Ndiyo alikuwa anafanya unililie hovyo? Mi si nilikwambia atakuwa bwana ‘ako? Mtu hivi hivi huwezi kumlilia siku zote kama huna uhusiano naye.”
“Kwa nini hunielewi mpenzi?”
“Mi nilijua tu mademu wa kipolisi siyo? Kila mtu anajua kuwa nyie mnamalizana wenyewe kwa wenyewe” aliongea Harison na kumfanya Sarah ainuke kwa hasira.
“Huwezi kuwa nyumbani kwangu halafu ukanitukana kiasi hicho, toka” aliongea kwa hasira na kumfanya Harison akae kimya kwa muda. Kisha akapata cha kuongea akionekana kuishiwa pozi
“Simaanishi hivyo mpenzi”
“Ondoka, sitaki! Huwezi kunikosea adabu kiasi hiki, unanipa nini cha ajabu hadi unikashifu kiasi hiki” alisema Sarah akionekana kuchanganya pombe na hasira.
Harison akainuka na kutoka kwa unyonge, Sarah akaubamiza mlango na kuuegemea. Akaanza kulia. Ikawa kazi ya Inspekta Ndilana kumbembeleza, upembelezaji ulioishia kwa kubambiana na hatimaye kuivunja amri ya sita pale pale kwenye kochi. Kisha wakaishia usingizini kutokana na ulevi na uchovu.
Ilikuwa yapata saa tisa za usiku wakati wanashtuka pale kwenye kochi wakiwa wamekumbatiana, bila kusema neno Inspekta Ndilana akainuka na kumbeba Sarah hadi chumbani. Wakaendelea na habari zao kisha wakaingia bafuni kuoga na hatimaye wakawa kitandani wamelala huku wamekumbatiana.
“Imetokea kama ajali, unadhani iishie kama ajali au?” Sarah alimuuliza Inspekta Ndilana
“Mimi nimetimiza ndoto yangu na sitaki iishie hivi hivi ila itategemea kwako”
“Kama ni ndoto yako ilikuwaje ukalala na yule Malaya?”
“We si ulikuwa hunitaki”
“Ulijuaje kama sikutaki?”
“Si ulikuwa unanitolea nje kila mara?”
“Haukuwa sirias halafu ulikuwa unaonekana una mambo mengi”
“Leo ndiyo umeona niko sirias au?”
Sarah anamfinya Inspekta Ndilana kisha wanaangaliana na kunyonyana midomo kabla ya Sarah kutoa kauli.
“Na ole wako nikuone tena na yule Malaya”
**********
Siku iliyofuatia, Inspekta Ndilana alidamkia moja kwa moja kazini, alichokifanya ni kuvaa tu fulani aliyopewa na sarah na suruari aliyokuja nayo jana yake. Kituo cha kwanza kikawa ofisini kwa Afande Maswe ambapo alimueleza kila kitu kuhusiana na taarifa za kuwepo kwa mitandao ya kifalifu kati ya polisi na raia.
“Unajua kuwa IGP aliunda tume?”
“Ndiyo afande”
“Kuna askari wengi sana watapoteza ajira kwa kuwa tume imeshagundua hicho unachokisema ila nilitaka nijiridhishe kwa taarifa kutoka upande mwingine. Kinachofanyika sasa hivi ni kuwatumia asari wote waliokamatwa kwa makosa mbalimbali wakati unafanya uchunguzi wako pamoja na raia walioshirikiana nao kuweza kuwapata washiriki wote.”
“Na raia?”
“Nasikitika kukwambia kuwa hata Alice itabidi akamatwe upya ili kuisaidia polisi”
“Atashitakiwa kwa kosa gani”
“Hawezi kushitakiwa ila atakuwa chini ya uangalizi maalum. Najua ni kiasi gani unampenda ila usalama wa raia na mali zao ndicho kipaumbele chetu cha kwanza”
“Naelewa afande”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa unaweza kwenda”
“Nna ombi moja afande”
“Lipi?”
“Naomba yale mahojiano yako na afande Majaliwa”
Afande Maswe alimwangalia Inspekta Ndilana kwa muda kisha akampa alichokitaka.
Inspekta Ndilana alitoka moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake akiwa na mawazo tele kichwani. Alipofika alikuta mlango umefungwa, akaufungua na kujitupa kwenye kochi sebuleni. Akawasha yale mahojiano na kuanza kuyasikiliza upya. Alijikuta anashindwa kujizuia kulia kutokana na donge lililomkaba moyoni.
Ghafla alihisi uwepo wa mtu mule ndani, kugeuka akajikuta akiwa uso kwa uso na Alice aliyevaa khanga tu akionekana macho yamemvimba kama aliyelia kwa muda mrefu, wakabaki wakitazamana huku wate wakiwa na sura za kulia.
Kumbe wakati huo wote, Alice alikuwa ameshazunguka kila mahali kumtafuta Inspekta Ndilana na alipomkosa akaamua kumsubiria nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa na nakala za funguo za mlango wa kuingilia na wa chumbani.
“Jackson”
“Alice”
“Nimesikia alichosema huyo mshenzi, yote ni ya kweli”
Inspekta Ndilana alishtuka akawa anamwangalia Alice kama vile hajawahi kumuona toka kuzaliwa kwake
“Unasemaje Alice”
“Alice alishakufa siku nyingi, mimi ni kivuli cha Alice. Ulikuwa unakaribia kumfufua Alice lakini nadhani Mungu hakupenda Alice afufuke”
“Sikuelewi Alice”
“Nafsi yangu ilikufa zamani sana, nilikuwa msichana mwenye mapenzi ya kweli na niliyeamini katika mapenzi kabla ya kutokea na mfululizo wa matukio yaliyonifanya nisione tena thamani ya mapenzi na moyo wangu kufa.”
Alice alitembea pole pole na kuja kukaa karibu na Inspekta Ndilana
“Ila amini jambo moja Jackson, ulianza kunifanya nione tena thamani ya mapenzi kwa kuwa ulikuwepo kila pale ambapo nilihitaji mkono wako unishike, ulijitoa kwa ajili yangu kwa kiasi ambacho kilikuwa kinanishangaza. Unajua ni kwa nini nilichanganyikia baada ya kupata taarifa kuwa umekufa?”
Inspekta Ndilana alitikisa kichwa kukataa
“Nilikuwa nasikitika kuwa umekufa bila kukueleza ukweli kuhusu mimi na kukushukuru. Najua huna tena moyo wa kuwa na mimi na hata kama ungekuwa nao, siko tayari kuwa na wewe kwa sababu unastahili kuwa na mwanamke bora zaidi yangu”
Alice aliunyanyua mguu wake na kuuweka juu ya mguu wa Ndilana ikawa kama kamkalia nusu, akausogeza mdomo wake sikioni mwa Inspekta Ndilana.
“Nataka nikupe ahsante yangu ambayo hautaisahau maishani”
Inspekta Ndilana akabaki amezubaa tu kama anayeota asijue afanye nini kutokana na kuchanganyikiwa na mambo mengi yaliyojitokeza kwa wakati mmoja. Ghafla wakashtushwa na askari walioingia mule ndani na kumchukua Alice.
“Naombeni dakika moja nimuage Jackson wangu” alisema Alice baada ya kusindikizwa na askari wa kike kuvaa na akawa tayari kutoka.
Wakamuachia akatembea pole pole hadi aliposimama Inspekta Ndilana, akambusu mdomoni na kusababisha wanyonyane midomo kwa muda kisha akamwambia.
“Hii ni ya kutoka kwa Alice, siyo kwa kivuli cha Alice”
Alice akachukuliwa na kuondoshwa pale huku Inspekta Ndilana akijitupa kwenye kochi.
Ripoti ya tume ya IGP iliwafukuzisha askari arobaini na nane na wengine wakashtakiwa pamoja na wafanyabiashara waliokuwa wakishirikiana nao na wambambe wao kina Shabani Kibope. Alice pamoja na wenzake, Hadija Mashushu na salome waliweka chini ya uangalizi.
Inspekta Jackson Ndilana na Afande Maswe wakapandishwa vyeo na kuhamishiwa makao makuu na hatua iliyofuatia ni ya maandalizi ya ndoa ya Inspekta Ndilana na Sarah.
MWISHO
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****HUO NDIO MWISHO WA RIWAYA YETU HII. MDAU UNAKARIBISHWA KUTOA MAONI*****
0 comments:
Post a Comment