Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

KIVULI CHEUSI - 3

 





    Simulizi : Kivuli Cheusi

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Wasiwasi huo ukamshitua kuitazama kila gari na chombo cha usafiri. Ndipo vinyweleo vikamsimama alipohisi bajaji iliyokuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu, ikiambatana naye kila alipokuwa anaenda mara alipokiacha kituo cha bamaga sheli.

    Hata alipofika jirani na apartment aliyokuwa anaifuata, hakushuka. Aliichunguza bajaji ile ilipokuwa inaelekea. Haikusimama kama alivyotarajia. Bajaji ile iliendeshwa na mzee wa makamo aliyesahau matumizi ya kiwembe juu ya kidevu chake. Bajaji ikampita pale pale na kutokomea.

    Vannesa alishuka na kuiendea apartment ile. Ikawa rahisi kwa kuwa alikutana na mke wa McCuthbert, alifahamiana naye siku ya msiba wa mumewe. Akaieleza shida yake na hakukuwa na kikwazo. Kwa kutumia kompyuta ya mapajani, walizitoa cd ndani ya kamera zile na kuzichomeka kwenye deki ya kompyuta. Picha iliyoonekana ndani ya cd ile ikamfanya Vannesa kuhamaki. Hasira zikampanda na kumfanya aropoke

    "Haiwezekani"



    MASAA MACHACHE KABLA YA KIFO CHA EVA

    Moses akiwa ndani ya tafakuri nzito, ndipo alipomkumbuka McCuthbert. Rafiki yake wa muda mrefu. Alipotoka katika pub ya Gq, alimfuata katika moja ya casino zake tatu iliyopo pembezoni mwa fukwe ya bahari. Uzuri alimkuta akiwa ameshapata kilaji, hivyo hakutumia pesa yake kumlewesha.

    Mazungumzo yalianza kikawaida wakijaribu kukumbushiana baadhi ya biashara zao haramu zilizowakutanisha pamoja. Ni huyo ndiye alikuwa mwenye roho ya mwisho aliyotumwa kuiangamiza na Raymond. Hakuwa akielezwa sababu ya kwanini alitumwa kuitoa roho ya fulani na fulani, alichopaswa ni kufuata oda huku pesa yake ikiwa mezani.

    Alipewa kiasi cha shilingi milioni hamsini kuitoa roho ya McCuthbert. Alipewa picha na maelekezo ya namna ya kumpata. Hakujua nguvu na utajiri alionao McCuthbert. Mholanzi mwanaharamu wa madawa ya kulevya.

    Siku hiyo alipomtafuta, alimkuta katika moja ya fukwe za kifahari huko kunduchi bichi. Sigara yenye moshi mzito kinywani mwake huku akiwa amezungukwa na warembo

    kadhaa waliofaa kuitwa walimbwende. Alikaa kistaarabu baada ya kukaribishwa kinywaji. McCuthbert akawafukuza wale wasichana mazungumzo yakaanza.

    "Nimetumwa nikuue?"

    Ulikuwa ni kama mzaha kwa McCuthbert. Ni nani ambaye hafahamu kiasi kikubwa cha pesa alichonacho McCuthbert. McCuthbert, akamtazama Moses kwa dharau kisha akajifanya kumuonea huruma.

    Akamuuliza "kijana unajiamini nini?"

    Moses alifahamu hilo hivyo hakupata shida, akamueleza yote. Akamueleza kuwa ametumwa kumuangamiza kwa dau la shilingi milioni hamsini. Akamtaja Raymond kama ndiye tajiri wake. Moses akaingiwa na tamaa ya pesa nyingi, hivyo akataka kubadilisha biashara. Akajitia kunyanyuka, uoga uliomvaa McCuthbert ukamfanya ahamaki.

    Akaongea kwa pupa "unaenda wapi sasa kijana?" ikabidi awe mpole "tafadhali nahitaji kufanya biashara na wewe" Uso wa Moses ukachanua kwa tabasamu akamgeukia McCuthbert.

    "Shilingi milioni 120 pamoja na kukuletea kichwa chake" Moses akadanganya hakumaanisha alichokuwa akikisema. Kutokana na kukiogopa kifo, McCuthbert akapandisha dau

    "milioni 150"

    Moses akampa akaunti yake ya benki na huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana. Japo hakufahamu McCuthbert alimtenda nini Raymond ila akamsaliti. Usaliti ule ukazaa upendo wa kudumu kati yao.

    Moses akamueleza shida yake McCuthbert licha ya kujali ulevi alionao.

    "Ninahitaji nyumba yako ya masaki"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hilo halina shaka Moses"

    Akiwa anachezea chuchu za msichana fulani aliyekuwa akimchezea kifua chake

    "Ngoja nimpigie Andrew akupe ufunguo"

    "Hapana nipo njiani kwenda huko" Moses akasema

    "Bila shaka una bibi leo" McCuthbert akabeua kiulevi huku akitoa kitita cha pesa "hadi umeshindwa kulipia hela ya hotel" kama pesa McCuthbert alikuwa na jeuri nayo haswa.

    Moses akaondoka huku mipango yake ikiwa inaenda sawa. Huko alikutana na Andrew pamoja na wasaidizi wengine. Hakuwa na wasiwasi nao kwa kuwa yeye ni zaidi yao. Yeye alikuwa rafiki wa karibu wa mmiliki wa apartment hizo, amuogope nani ikiwa ufunguo alikuwa nao? Simu ilikwishapigwa kwao na waliufahamu ujio wake, hivyo hakuogopa juu ya maswali ambayo angeulizwa nao.

    Alikuwa huru kufanya lolote.

    Alipishana nao nje ya nyumba ile baada ya salamu na kuingia ndani. Huko aliutumia utundu kidogo kugundua ulipo moyo wa kamera zote zilizofungwa katika nyumba hiyo. Aliukata waya fulani uliosaidia kuonesha picha na kuacha ule wa sauti.

    Akauchomeka waya wake aliokuja nao huo haukuwa na kazi ya maana lakini ulikuwa maalumu. Umuhimu wa waya ule ni kuonesha kivuli peke yake baadala ya picha kamili. Akaujaribu na kutazama. Picha ya nje mara baada ya kuufunga, vilikuwa ni vivuli pekee. Akatabasamu kwa furaha huku akiamini ameupoteza ushahidi wa mauaji kabla hajayafanya.

    Akatokomea baada ya kuweka kila jambo sawia ndani ya nyumba hiyo.

    XXXXX

    Hali ya kuikosa picha ya mgeni aliyeongozana na mwanamke aliyeuawa, ilimchanganya sana. Video ilipoanza, Vannesa macho yalimtoka haswa. Shahuku ya kujua sura ya muuaji, ikawa inampeleka puta pumzi zake. Mke wa McCuthbert naye akajawa na shahuku

    huku wakiitazama kwa mara ya kwanza pamoja na Vannesa. Video haikuwa video kama walivyotegemea, bali video iliyokosa uhalisia. Vilionekana vivuli tu badala ya taswira kamili ya

    mwanadamu. Hakuna aliyepatwa na wazo lolote juu ya kufahamu au kuyagundua maumbo ya vivuli vile. Vannesa akahamaki

    "Haiwezekani"

    Akamgeukia Andrew ambaye pia alikuwa amechanganyikiwa kupita kawaida.

    "Mchezo gani huu?"

    kigugumizi cha kustaajabu, kikamponza Andrew. Vannesa akaanza kuhisi huenda Andrew anahusika juu ya hilo. 'pesa' akazidi kufikiria uwezo wa kipesa alionao muuaji au wauaji. Harufu ya kuwa makini, ikasumbua fikra zake.

    "Sifahamu chochote mimi jamani dada Vannesa"

    Andrew akajitetea lakini hakuaminika. Vannesa akampigia simu Jafari Hiza. "naomba uje umchukue huyu kijana hapa kwa McCuthbert Hana analolitoa nikamuelewa.. Ndio.. Kijitonyama hapa hapa"

    Baada ya kukata simu, akaaga.

    “Sina uwezo wa kukukamata kwa kuwa mimi sio askari lakini nadhani maafisa watafanya kazi yao” Alipotoka nje, akaelekea kwenye gari yake huku mawazo ya mzee mwenye bajaji yakimyeyuka.

    Alipoufungua mlango wa gari yake, simu ikaita. Juu ya kioo mpigaji alikuwa ni Moses, Vannesa akahifadhi namba ya Moses "Honey" Alitabasamu. Akaipokea kwa sauti ya

    madeko

    "mpenzi... Nipo kijitonyama.. Uko wapi?... Kwa hiyo nikufuate ulipo... Kwanza nimechukia... Kwanini tangu asubuhi hujanitafuta? .. Anha.. Haya ninakuelewa mpenzi. Nakupenda.. Nipo njiani.."

    vannesa akaiwasha injini na kuingiza gari barabarani.

    XXXXX



    Baada ya kufahamu kile kilichomfanya aamue kuingia ndani ya hotel ya New Africa, sasa hata kahawa Aliyoiagiza hakuitaka tena. Alitoka nje kwa mwendo wa kukimbia huku akihisi kama alikuwa anachelewa.

    Bahati ikawa kwake.

    Mpaka alipotoka nje, ikawa ndio Vannesa anatoka akiwa amesimama na Naima pembezoni mwa gari lake Vannesa. Alifahamu fika Vannesa alikuwa anatoka. Akapiga simu kwa mshirika wake mmoja wanayefahamiana. Yeye aliitwa Chanduru. Alikuwa akikodisha gari zake kwa ujira mdogo. Chanduru hakujali juu ya kazi ambayo gari yake ilienda kufanyiwa. Pesa kamili mezani na masharti ya gari lake kurudi salama. Kwa kuwa Moses na Chanduru ni marafiki wa muda mrefu, wakaaminiana.

    Moses akamuomba Chanduru dereva wa kike. Dakika chache kabla Vannesa hajaondoka, gari

    ya Chanduru iliingia. Aliyeiendesha ni msichana mrembo aliyetumiwa katika biashara haramu kadhaa. Alikuwa Meriana. Wakati ambao anaingia yeye na ndipo gari ya Vannesa ilikuwa inaondoka. Akaingia ndani ya gari harakaharaka. Hawakusalimiana na Meriana akazungumza kama hayawani

    "Ifuate, ifuate" Meriana hakufahamu chochote. Alikuwa akigeuka huku na kule akitafuta gari hili na lile. Hakuelewa. Akauliza "Nifuate nini?" gari ya Vannesa ikawapita mbele yao. Moses akanyoosha mkono lilipokuwa likitokomea kuitafuta barabara ya bibi titi. Meriana akaliacha gari moja likiwa katikati ya gari ya Vannesa na gari yake.

    Akamuuliza Moses "lakini tunalifuata gari ile kwa nini?"

    "tangu lini ukauliza juu ya kazi isiyokuhusu?" alimgeukia na kumwambia "kazi yako ni kuendesha gari na kufanya ninachokuagiza"

    Gari ya Vannesa ilipokipita kituo cha Mwenge, gari zao zikawa zinafuatana. Ni hapo Vannesa alipoanza kuhisi kuwa alikuwa anafuatiliwa. Mpaka Vannesa alipoikunja gari yake na kuingia barabara ya sinza. Moses akaongea usikunje kona kwanza" mwendo wa gari aliyokuwa akiiendesha Meriana ukapunguzwa. Gari ya Vannesa ikakunja kona iliyo pembezoni mwa bar ya Hongera. Moses akamwambia tena Meriana

    "Ifuate"

    Meriana akaifuata gari ya Vannesa ilipokuwa inaelekea. Moses alikwisha gundua kuwa gari ya Vannesa ilikuwa ikielekea Gq pub. Kwa mbali aliiona ikiwa imesimama sehemu ya maegesho. Mita chache yaani miguu kumi kutoka walipo akamuamuru Meriana kusimama.

    Walikaa kwa zaidi ya dakika thelathini, Moses akamuona Vannesa akitoka. Akamvuta Meriana na kuanza kubadilishana naye mate. Kitendo hicho kikamshangaza sana Meriana. Lakini ikawa ni sehemu ya njama za Moses. Moses alifahamu Vannesa asingekuwa mjinga. Mjinga wa kutofahamu alikuwa akifuatiliwa. Hiyo ilitokana na kuwa hakuwa akimuamini tena Vannesa. Wasiwasi ulikuwa kwenye fikra zake kuwa Vannesa alikuwa akimfuatilia yeye. Alikuwa akimtafuta kutokana na mauaji aliyokuwa akiyafanya. Alikuwa na uhakika kuwa Vannesa ni mpelelezi mwenye kunusa hatua zake.

    "Hawezi kuharibu mipango yangu ni lazima nimuue Raymond"

    Gari ya Vannesa ikatokomea. Wakiwa njiani kumfuatilia Vannesa ndipo Moses akayabadilisha mavazi yake. Gari ya Vannesa ikawa umbali wa magari matano mbele ya gari la Meriana na Moses. Moses akamuacha Meriana mara walipofika posta, Meriana alicheka sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "umefanana na wazee kabisa"

    Moses alikuwa amejibadilisha muonekano wake na kuwa mzee aliyechoka sana. Akairukia moja ya bajaji zilizojipanga pembezoni mwa bank ya NBC. Dereva wa bajaji hiyo alishangaa kumuona mzee aliyeifuata bajaji yake kwa pupa, Kitita cha noti za shilini elfu hamsini kikamchanganya. Akaenda kila alipokuwa akielekezwa na mzee ambaye alihisi kuwa hana pesa hapo mwanzo wakati anaipanda bajaji yake.

    Bajaji aliyoipanda Moses ikaifuata nyuma gari ya Vannesa. walipokipita kibonde

    kilichokuwa kikiwaletea mihemko wasafiri wengi waliokipita, akatambua alipokuwa akielekea Vannesa.

    Akaendelea kumfuata nyuma huku akiamini kuwa Vannesa anahitajika kufa kabla hajapata anachokitafuta. Akaliona gari la Vannesa likiwa linaegeshwa mbele ya nyumba aliyomuua Eva ndani yake.

    Akazungumza na dereva wa chombo kile "naomba ushuke" Dereva akahamaki

    “Unasemaje wewe?"

    kitita cha noti za shilingi elfu kumi zaidi ya saba zikamfanya kumuachia ufunguo wa bajaji mzee yule asiyemfahamu. Alimuachia lakini kwa miahadi ya kuchua taksi ambayo itamfuatilia mpaka atakapomkabidhi bajaji yake kwa shughuli yake binafsi anayotaka kuifanya peke yake.

    Moses akaipita gari ya Vannesa. Huko alikaa kwa muda mrefu akifuatilia ni saa ngapi Vannesa angetoka.

    Akiwa amesubiri kwa muda mrefu, ndipo akamuona Vannesa akitoka, akaamua kumpigia simu. Ndiyo simu ambayo aliipokea Vannesa wakati ule ambao anatoka ndani ya apartment, baada ya kuikosa taswira ya muuaji. Alipomaliza maongezi ya kwenye simu na Vannesa, Akajinong'oneza kwa hasira

    "Jioni ya leo" tabasamu la chuki likamponyoka Moses "Roho yako nitaitafuna Vannesa kama ukienda kinyume na mimi"

    Baada ya Vannesa kuondoka kichwani akiwa na wazo la kwenda kumuona Mfaume, alichokiwaza Moses; ni muendelezo wa mauaji yake. Baada ya gari la Vannesa kutokomea na kutoonekana kabisa, akajitokeza na kusimama kabisa karibu na gari la Vannesa lilipoegeshwa mwanzo. Taswira aliyo nayo ni ile ile ya kizee. Hakuna ambaye angemfahamu kwa taswira hiyo. Akajipa uhakika wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kummaliza Andrew. Kummaliza Andrew ingekuwa ni kuufuta ushahidi wake.

    Alikagua ilipo sumu yake ambayo alitegemea kuitumia kwa Andrew na kuipata katika mifuko ya suruali yake. Akatazama huku na huko, kisha akagundua kuwa hakukuwa na mtu; akaingia ndani ya nyumba aliyotoka Vannesa dakika chache zilizopita. Alipogonga akakaribishwa na mke wa McCuthbert.

    "Oh! Nani wewe" kabla Moses hajaingi, mke huyo aliuliza.

    Muonekano wa Moses haukuonesha hata punje kama alikuwa ni mteja wa kuhitaji nyumba hiyo. Andrew naye aliliacha kochi na kujisogeza mlangoni. Alipomuona Moses, akacheka. "Unataka nini babu?"

    Moses alikohoa mfululizo huku akijitia kucheka kizee. Akazungumza kwa sauti ya mikwaruzo

    "Nahitaji nyumba ya kulala" akiwa analitafuta kopo lake mfano wa manukato mazuri akawauliza kwa hila “au kisa mnaniona mimi ni mchafu na ndio maana mnadhani sina fedha? Au kwa sababu nguo zangu zinanuka na mnadhani kuwa sina manukato ya kunukia?” akatoa kopo lake na akajipulizia kwenye nguo zake kuu kuu kwa hila.

    "Hamnikaribishi ndani?" Akauliza huku tabasamu la ushindi likimponyoka.

    Hakujibiwa, kimya kilichokaribishwa na kishindo cha miili ya Mke wa McCuthbert na Andrew ikaisalimia sakafu. Moses akatabasamu baada ya kuona wakidondoka chini kama gunia. Akaitema kitu alichokuwa akikitafuna mfano wa plastiki aliyokuwa akiitafuna tafuna wakati aliokuwa akijipulizia sumu ile iliyo ndani ya kopo la manukato.

    Akaiingiza miili ile ndani.

    Wakati ambao alikuwa akifunga mlango, aliona magari ya polisi yakija katika mtaa ambao nyumba ile ipo. Akayavua mavazi yale na uzee wake, kisha akarudi katika hali ya ujana. Alikumbuka ndevu za bandia ambazo zingewapumbaza wachache ambao wangemuona ni kijana wa kawaida anayevutia. Akajificha juu ya paa, ndani ya dari kutokana na uzoefu wake ndani ya nyumba hiyo aliijua sehemu gani ya kuingilia.

    Akiwa ndio kwanza anafunika tu mfuniko wa kumruhusu kujificha vizuri darini, mlango wa nyumba hiyo nayo ukafunguliwa. Alisikia sauti tu "Imekuaje?" Sauti ya mmoja wa walioingia ndani, ikauliza. Hiyo ilikuwa ni sauti ya Inspekta Jafari Hiza. Moses akaisikia sauti ya mwingine ikijibu

    "Hawapumui mkuu" Jafari hiza akawa ameshika nguo za Moses na madevu yake ya kizee. Akiwa katika kutazama chini ya paa alimojificha kupitia tundu dogo lililoachwa kimakosa na fundi wa paa hilo, Jafari Hiza alikuwa akipiga simu kwa Vannesa.

    "Halo Vannesa?" Moses akasikia sauti ya Jafari Hiza japo hakumfahamu, akiliita jina la Vannesa. Jafari Hiza akaendelea baada ta simu kupokelewa "Ndani ya nyumba ya McCuthbert ulitoka saa ngapi?... Kuna mauaji ya utata zaidi yametokea... Kuna mwanamke na yule Andrew tuliyekuwa tumekuja kumchukua.. Vitu.."

    Kabla Jafari Hiza hajamaliza kuzungumza, kutoka katika moja ya makoti ya kizee aliyoyaokota chini chupa ile yenye sumu ikadondoka.

    ".. Jafari.. Jafari"

    Ilikuwa ni sauti ya Vannesa ikikoroma ndani ya spika za simu ya Jafari Hiza. Aliita bila kupokelewa upande wa pili mpaka alipoanmua kuikata simu yenyewe. Jafari Hiza akaiokota chupa ile kwa uangalifu huku akiwa amevaa gloves. Alipotaka kuipuliza, mmoja wao ambaye ana aina ya udaktari ndani yake ambae pia ni mpelelezi akamzuia.

    "Hatujajua bado kifo cha hawa watu wawili, huenda ikawa ni sumu"

    Wazo hilo likapita ndani ya fikra za Jafari Hiza. Kila kitu ndani ya nyumba hiyo kikaokotwa kama kithibitisho na kwenda kupimwa. Miili ya Andrew na mke wa McCuthbert ikabebwa kwenye gari maalumu la hospitali lililoitwa punde na kwenda kuhifadhiwa mochwari. Jafari Hiza pamoja na jopo lake walipotaka kutoka, kuna kijana akawazuia. Alikuwa ni yule dereva wa boda boda.

    “wewe ni nani?" Jafari Hiza aliuliza.

    "Kuna babu namtafuta ameingia humu mimi ni dereva wa bodaboda"

    Mwili wa Jafari Hiza ukamsisimuka, vinyweleo vikamsimama kuhisi kuwa muuaji wanayemtafuta hakuwa mbali. Aliwaamuru askari wake wamsake mtu yeyote ambaye angeonekana kuwa ndani ya nyumba hiyo na kumtia nguvuni.

    Msako uliendeshwa kwa dakika ishirini zaidi. Hakuna kilichopatika na zaidi ya kila kitu kutolewa katika mpangilio wake maalumu. Jafari Hiza akaondoka na yule dereva wa boda boda kwa ajili ya kumsaidia yeye katika upelelezi wake.

    XXXXX



    Vannesa akawa amechelewa zaidi ya dakika nyingi mpaka kufika masaki ilipo nyumba ya kupanga yalipofanyika mauaji mengine. Hakuwakuta wakina Jafari Hiza. Lakini Moses pia hakuwa mbali na eneo hilo. Alikuwa sehemu ambayo alijificha mara ya kwanza na boda boda ile ya kijana aliyeondoka na Jafari Hiza. Alikaa hapo baada ya sekunde chache alizotoka juu ya dari alipojificha mara baada ya jafari Hiza na wenzake kutokomea. Alimuona Vannesa wakati akijaribu kukigusa kitasa cha mlango huo lakini hakikufunguka. Yeye akakumbuka alivyotokea ndani ya nyumba hiyo kupitia dirisha la jikoni. Alimuona akihangaika kurudi kwenye maegesho ya magari.

    Akaamua kumpigia simu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea kwa upole akijaribu kumchota kujifanya tayari yupo ndani ya chumba cha hoteli.

    "Mpenzi uko wapi... Kazini hadi saa moja ya jioni?.. Ni chombo gani cha habari kinakunyanyasa kiasi icho hakikupi muda wa kupumzika na mwenza wako?.. Nakuhitaji bwana sasa hivi.."

    Kutokana na tabasamu la Moses alilotoa baada ya simu kukatika ikaonesha kuwa Vannesa alimpa jibu zuri. Akajiambia huku akiingia barabarani kuita taksi itakayomrudisha kinondoni ndani ya hoteli aliyolala yeye na Vannesa

    "Vannesa"

    Taksi ikawa imesimama kama ndiye Vannesa. Alipofungua mlango na kuufunga akamwambia Dereva

    "Nipeleke Kinondoni"

    "Shilingi elfu kumi na tano"

    "Nitakupa ishirini" dereva alipomgeukia, Moses akamwambia huku akitabasamu "naomba ipae"

    Maneno hayo hayakumsumbua dereva yule akaziingiza gia kwa fujo na kumuonesha mteja wake yeye ni zaidi ya madereva wa magari ya mashindano. Moses akamalizia wazo lake

    "Lazima nikuue"

    Akacheka kifedhuli mpaka dereva akashangaa. Taksi aliyopanda Moses ikafika mpaka kwenye hoteli hiyo. Kwenye maegesho ya magari, gari la Vannesa halikuwepo. Moses akamlipa dereva ujira wake kisha aliifuata lift ya hotel hiyo kivivu. Alibonyeza gorofa namba tatu, kilipo chumba chake. Akaingia chumbani kwake kwa kadi maalumu. Milango ya hotel hii, haikuwa na funguo.... Kadi hiyo hiyo ilitumika pia kuwashia taa.

    Ufahari, ufahari haswa.

    Akiwa amejipumzisha, akamuwaza sana Vannesa. Kuna nafsi ilimwambia kuwa bado mapema kumuua, kuna nyingine ikamwambia akichelewa kumuuwa basi roho yake ni ya Vannesa. Hakutaka hilo litokee. Akanyanyuka kama amepigwa na shoti ya umeme. Akiwa ndio kwanza anasimama, simu yake ikaita.

    Aliitoa haraka kumtazama mpigaji.

    Simu hiyo ya mkononi, aliisajili kwa jina la bandia na wala hakuna aliyeifahamu. Ni simu ambayo ameinunua kwa kazi hii nzito ya kulipiza kisasi. Kisasi cha kuitafuta roho ya Raymond pamoja na watu wake wa karibu wanaomuhusu. Alipoitazama simu iliyokuwa inaendelea kuita, juu ya kioo alikuwa ni Vannesa.

    "Habari mpenzi.. Upo sehemu gani?.. Sawa nakusubiri mpenzi.."

    Kisha simu ikakatwa. Moses akalitoa tabasamu la shetani tabasamu lililoudhi kulitazama. Akaiendea moja ya mifuko katika begi lake alilokuja nalo, akaitoa ile nyongo ya mamba. Ilikuwa inakaribia kuisha, lakini alikuwa na hakika kuwa kwa unga huo mdogo ndani ya juice ingetosha kuupokonya uhai wa Vannesa.

    Akiwa amemaliza kuagiza juice kupitia kwenye simu ya chumbani hapo. Aliingia bafuni kuoga. Alipomaliza, mlango nao ukawa unagongwa. Akajifuta maji huku akiwa na taulo kiunoni, akaufungua mlango.

    Alikuwa ni Vannesa.

    Macho yake Vanessa yakanasa juu ya kifua cha Moses. Ndiyo walikwishalala pamoja, lakini hakupata nafasi ya kukiona sawia kama sasa waliposimama pamoja mlangoni. Vannesa japo alikuwa mchovu, hakujali yote. Alizivamia papi za Moses na kuanza kubadilishana mate. Moses naye alimbeba na kumuingiza ndani. Huko nako mchezo wa kubadilishana mate uliendelea kwa muda mrefu zaidi mpaka Vannesa alipokuwa mtupu kabisa. Moses naye akalitupa taulo pembeni, wakaanza kucheza michezo ya kuchezeana viungo kadhaa katika miili yao. Nusu saa baadaye wote wakawa hoi.

    Moses ndiye akawa hoi zaidi.

    Kilichobaki akawa anamuhitaji Vannesa, hakutaka tena kusubiri. Alipotaka kumuingilia kimwili, Yule muhudumu wa Juice alikuwa mlangoni akigonga mlango. Moses akajifunga taulo akiwa na hasira kupitiliza. Alizipokea juice zile na kuziweka mezani. Akarudi kitandani alipojilaza Vannesa. Michezo ikaendelea. Safari hii alipotaka tena kumuingilia Vannesa, Vannesa akamwambia kwa sauti nyororo ya upole

    "Unaonaje tukioga pamoja kwanza mpenzi?"

    Kama mbuzi wa hitima, Moses akakubali. Waliingia bafuni wakaoga, huku wakiogeshana kila mmoja akitumia mikono yake kuchezea kila kiungo cha mwenzake kwa ustadi mkubwa. Hakika kila mmoja akawa hajiwezi tena.

    Si Vannesa wala Moses.

    Wakaliacha bomba la mvua na kurudi tena kitandani. Moses alikuwa kiboko kwenye nyanja ya mapenzi. Alijua kumdatisha Vannesa mpaka Vannesa akapiga ukunga wa raha. Vannesa naye si kwamba alilala kama gogo. Alijitahidi kukumbuka miaka ya nyuma alipokuwa na mpenzi wake Amani. Yeye ndiye alimfundisha mapenzi, yeye ndiye aliyemfundisha hiki alichokuwa anamfanyia Moses. Moses licha ya ukatili na ujasiri wake mtaani, Vannesa akawa mshindi wa kumtoa chozi. Hakulia kwa huzuni bali kile kilio cha raha.

    Saa tatu usiku Moses alikuwa amelala fofofo. Vannesa alijinyanyua taratibu na kuingia bafuni. Huko aliingia kuoga. Bomba la mvua, ikawa limemuamsha Moses. Moses akawa amekumbuka kuwa aliumwaga ule unga wenye sumu kwenye juisi akiwa pale mlangoni bila Vannesa kumuona. Nafsi yake ikakataa kabisa kumuangamiza Vannesa. Kutokana na penzi zito alilolipokea kutoka kwa Vannesa dakika chache zilizopita, akajiambia

    "Hapana" akasimama huku akijifunga taulo "nitamlinda milele aendelee kunipa furaha ya mapenzi"

    Vannesa akawa anatoka bafuni. Wakakumbatiana tena, Vannesa akasema kwa sauti ya huba

    "Nakupenda mpenzi" Kutoka moyoni Moses akajibu kwa dhati "Nakupenda sana Vannesa"

    Walipoachiana, Vannesa akaifuata mojawapo ya glass ya juice.

    "He! Kumbe kuna juice hapa"

    Moyo ukamlipuka Moses. Alipomuona Vannesa akiichagua juice ileile aliyoimwagia unga wa sumu, akashindwa kujizuia.

    "Mpenzi hiyo ya ukwaju ninmeichagua mimi"

    "Lakini mpenzi"

    Bila Vannesa kumalizia alichoanza kukisema, hakutegemea kilichotokea. Mkono wake ulipigwa kikumbo na glass ya juice ikamponyoka. Ikawa kama bahati mbaya na Moses ndivyo alivyoigiza. Sumu iliyo ndani ya juice ikamwagilka, hivyo roho ya Vannesa ikapona. Moses aliingia bafuni akaoga kisha wakajiandaa na Vannesa kwenda kupata chakula katika mgahawa wa hoteli hiyo.

    Wakiwa huko majira ya saa nne usiku, simu ya Vannesa ikapata uhai.

    Mpigaji alikuwa Jafari Hiza.



    Baada ya upimwaji wa vifaa ambavyo vilikutwa ndani ya nyumba ya McCuthbert. Ilipimwa ile sumu iliyowekwa ndani ya chupa ya manukato. Sumu ambayo ni hatari sana kwa binadamu. Sumu iliyotengenezwa kwa kuchukua mate ya nyoka aina ya kobra anayejulikana kwa jina la egyptian cobra.

    Sumu ya nyoka huyo inajulikana kwa jina saikrotiki.

    Sumu hii huaribu mfumo mzima wa ubongo wa kati na kusimamisha mfumo wa upumuaji. Historia ya nyoka huyo hata kuitwa jina hilo ni kwa sababu alimng'ata malkia wa misri aliyeitwa Cleopatra.

    Daktari mkuu katika idara ya upelelezi akatoa ripoti ya kifo kilichosababisha watu wale wawili kufa. Ikapimwa pia ile plastiki ambayo Moses aliitema pale mlangoni. Ikagundulika ni dawa ambayo ilizuia sumu hiyo. Mtafunaji wa plastiki ile aliitafuna ili tu sumu ile isimdhuru. Jafari Hiza alimpigia simu Vannesa kumpa taarifa hiyo.

    "Tunaweza kuonana?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana Hiza. Kuna nini tena" Vannesa alijibu upande wa pili wa simu, huku Moses akimkodolea macho kwa umakini.

    "Kuna ripoti juu ya chanzo cha kifo cha yule mke na kibaraka wake waliokufa kule masaki"

    Macho yakamtoka pima Vannesa, lakini akajizuia kutojionesha hofu yake mbele ya Moses. Akajibu kiutulivu

    "Tunaweza kuonana pale pale kwenye meeting point yetu"

    Simu ikakatwa Jafari Hiza akachukizwa na tabia mpya aliyoianzisha Vannesa. Tabia ya kutojali kabisa kazi tofauti na zamani. Si kweli kwamba Jafari hiza alichukizwa tu na tabia ya Vanessa pia alitamani kesi hii isiishe mapema ili imuweke karibu na mwanamke huyu. Ilikuwa ni hatari kugundulika kama Jafari hiza alikuwa akimtumia mtu mwingine tofauti na aliyeajiriwa katika kitengo cha usalama wa taifa, lakini yeye hakujali kwa kuwa alimuhusudu sana Vanessa.



    *****

    Baada ya kumaliza chakula mgahawani, Vannesa na Moses waliongozana pamoja mpaka chumbani. Vannesa hakukaa zaidi kitandani akiwa macho. Usiku ulikuwa mnene uliomlevya, akalala fofofo.

    Moses hakulala wala usingizi haukuonekana kuwa karibu na kope zake. Akajiegesha kwenye kiti kilicho pembezoni mwa meza ndogo ya duara. Aliiacha whisky iliyomuunguza koo, akachomoa kasha lake la sigara nene. Aliiwasha ya kwanza huku akiuvuta moshi wake taratibu. Tafakuri zake zikaingia huruma. Aliwaza ni damu za wangapi zimeingia katika mkondo usiofaa. Mkondo wa kulipiza kisasi kwa ajili ya damu ya baba yake aliyemlea kwa muda mrefu. Alimlea akidhani kuwa ndiye baba yake mzazi. Alimuua kwa mkono wake bila kufahamu kuwa alikuwa akitoa uhai wa mtu muhimu katika maisha yake. Alitoa roho ya pamela kwa hila zake za kutoa siri kutokana na mauaji ya Bertha. Wa pili akawa Omary aliyefuatiwa na Eva kabla hajaitoa roho ya McCuthbert hatimaye za wawili ambao ni mke wake McCuthbert kisha Andrew.

    Vifo vyao visingemtia uchungu Raymond ndio maana akaona ni vifo visivyo na thamani katika mipango yake. Alikumbuka jinsi ambavyo alimfahamu Raymond. Kipindi hicho alikuwa bado mtoto sana. Alikuwa ameimaliza elimu yake ya msingi akisubiria majibu ya kumpeleka shule ya sekondari. Mama yake alishindwa kupumua kwa kutumia mashine akiwa mgonjwa mahututi, mauti ukampokonya roho yake.

    “Inasemekana aligongwa na gari kwa makusudi” Mashuhuda ajali hiyo walisema.

    Haikujulikana ni nani alimgonga hivyo hakukuwa na mtu wa kumuhukumu. Kwa kuwa mzee Carlos alikuwa na urafiki wa karibu na Raymond, hata katika msiba wa mke wake Carlos alikuwepo pia. Huko ndipo alipofahamiana na Raymond. Hapo ndipo zile siku mbaya anazozichukia mpaka leo ndio zilipojizaa.

    Raymond alijiweka karibu na familia ya Moses kama rafiki wa Carlos, mzee tajiri aliyemlea Moses tangu akiwa mdogo kipindi hicho Bi Tunu mama yake Moses amekataliwa mimba na kufukuzwa nyumbani na mwanaume. Mwanaume ambaye Carlos alimfahamu fika na Bi Tunu hakumueleza Moses hata alipokuwa mpaka anakufa.

    Hivyo ikamfanya Moses kuamini Carlos ndiye baba yake.

    Aliendelea kuishi huku akimuona Raymond kama rafiki wa karibu na Carlos. Ikafika ile siku Raymond alimtembelea shuleni na kumuomba afanye naye biashara

    "Baba"

    Alimuheshimu na kumuita hivyo kwa kuwa alikuwa mtu wa karibu na Carlos "mimi bado mwanafunzi nitafanya biashara gani na wewe mzee wangu?"

    Raymond alicheka na kumwambia "mimi huwa sikosei katika maamuzi yangu ndiyo maana nimekufuata wewe. Kama upo tayari kuungana na mimi katika biashara yangu nitafurahi ukinijuza mapema"

    Raymond akaondoka huku akimuachia kitita cha pesa ambazo hakuwahi kutegemea kuzishika licha ya utajiri mkubwa alio nao Carlos, baba yake.

    Zilikuwa ni shilingi milioni moja.

    Wakati akiendelea kukumbuka yaliyopita, sigara ikawa imezima ikiwa mdomoni kwake. Akachomoa kasha na kuiwasha nyingine. Akaendelea kuzama zaidi katika mawazo yake. Alikumbuka jinsi alivyojiingiza rasmi katika biashara haramu za madawa ya kulevya bila Carlos kufahamu. Biashara hiyo ikaendelea mpaka alipokuja kufahamu kuwa hata makampuni ya baba yake Carlos, pamoja na utajiri wake wote ni kutokana na biashara hiyo hiyo pia. Hakufahamu kuwa biashara hiyo ndiyo iliyowaweka kwa ukaribu Raymond na Carlos. Moses akaendelea na shule huku akisambaza madawa ya kulevya.

    Ni ile siku alipotumwa kuua. Raymond alimtuma Moses kuua mtu. Si mtu wa kwanza kumuua kutokana na kazi alizokuwa akizifanya, lakini kwa Moses mtu huyu alimfanya hana hatia ya kumuua. Kwanza jinsi ya kumuua ilikuwa ni tofauti na watu wote ambao alitumwa kuwauwa. Mtu huyu alifungwa uso kwa kuvalishwa kitambaa fulani na ilikuwa ni usiku. Moses akaichomoa bastola yake kiunoni kila alipotaka kubonyeza kitufe cha kufyatulia risasi, moyo wake ukawa mzito.

    Hakujua kwa nini.

    Lakini kutokana na roho ngumu huku akihaidiwa dau kubwa la kuitoa roho ya mtu huyo na Raymond, akafanya kile kitu ambacho nafsi yake fulani ilimnong'oneza asifanye, akampiga risasi ya kifua mtu yule. Raymond na jopo lake likaondoka eneo hilo huku wakimuacha Moses akiwa anamfuata yule mtu aliyempiga risasi.

    Moses hakuaamini alichokiona baada ya kumfunua kitambaa mtu yule. Alikuwa ni mzee Carlos, baba yake. Carlos alikuwa akiongea kwa shida sana huku akimueleza ukweli wote kuhusu maisha yake. Alipomaliza kumueleza roho yake nayo ikapaa.

    Tafakuri hizo za Moses zilikatishwa ni kikohozi kikavu kilichomvamia Vannesa. Naye akaitupa sigara katika kasha la kuhifadhia jivu na kupanda kiutandani kulala.



    *****



    Raymond hakuishi kwa amani licha ya kuhisi hali ilianza kuwa shwari. Bado aliamini kuwa Kivuli cheusi alikuwa pahala fulani kajibanza akipanga jambo baya zaidi la kumfanyia. Binafsi hakujua sababu ya huyo mtu aliyejitambulisha kama kivuli cheusi kumtafuta kwa uchu kiasi hicho, lakini aliamini ni mmoja kati ya wabaya wake.

    Hakuweza kuwaza kabisa kama Moses angekuwa ni mbaya wake anayeitafuta roho yake usiku na mchana. Yeye pia alimtafuta Moses kuyamaliza yale yote yaliyotokea kumsababishia kifo Carlos ambaye ni baba yake. Raymond akawa amesahau kabisa kama aliwahi kumpa mwanamke fulani ujauzito na kumfukuza nyumbani kwake. Mwanamke yule alizaa mapacha lakini mmoja kati ya watoto wale alifariki. Hakufahamu kuwa Moses ndiye mtoto wa Bi Tunu aliyemgonga na gari kwa makusudi kule maeneo ya kimara baruti na kukimbilia maeneo ya mbezi akikatisha barabara ya maramba mawili na kukimbia kesi ya mauaji hiyo ilikuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

    Bi Tunu mwanamke aliyebeba ujauzito wake ndiye mwanamke aliyetambulishwa na rafiki yake kuwa ni mkewe. Rafiki yake wa muda mrefu Carlos. Ndiyo!! alimfukuza Tunu kutokana na ujauzito lakini si kwamba alikuwa hampendi. Alimpenda sana lakini kutokana ujana na kazi aliyokuwa akiifanya, hakuhitaji mtoto kwa wakati huo. Roho ikamuuma sana kumkuta Tunu akiwa na Carlos. Akaapa kumuangamiza Tunu na Carlos bila kujali ukaribu wao wa siku nyingi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndiyo sababu alimuingiza Moses katika biashara zake akiamini kuwa Moses ni mtoto wa carlos. Hivyo angemtumia Moses kumuua baba yake. Hakufahamu siku zote hizo kuwa yule Moses aliyemuona tangu akizaliwa mpaka amekuwa ni mtoto wake aliyemkataa tangu tumboni. Hakujua sababu ya Moses kuwa na mahusiano na Bertha mara walipokutana chuoni. Raymond akawa amelipiza kisasi kwa kuiangamiza familia ya Moses. Moses akawa ameingia katika kisasi cha kuiangamiza familia ya Raymond.



    ******



    Moses aliamini kuwa Raymond hatakuwa nyumbani hivyo ugeni wake wa ghafla ungemshitua sana Bi Furahiya. Kupotea kwake muda mrefu kungemshitua sana. Bila shaka angestaajabu na kuduwaa kwa kuwa ni muda mrefu tangu kifo cha Bertha nyuma yake ni zaidi ya miezi nane iliyopita.

    Aliichukua bajaji iliyomfikisha moja kwa moja katika nyumba ya Raymond. Nyumba iliyolindwa na mitambo maalumu, getini akiwemo Majura.

    Mlinzi aliyemfahamu vizuri Moses.

    Nyumbani kwa Raymond kukawa na ulinzi mkali uliongezwa ili kuilinda familia hiyo. Ulinzi wa askari maalumu waliolipwa kwa ajili ya kuilinda familia. Majura aliwatambulisha kwa Moses askari hao na kuruhusiwa kupita.

    Moses alicheka moyoni kwa kuwa aliamini ulinzi huo ni kutokana na uoga na mtu aliyejiita Kivuli cheusi, ambaye ni yeye. Aliingia ndani kwa mapokezi ya heshima.

    Kama alivyotarajia, Bi Furahiya alishituka sana huku akifurahi sana kumuona Moses.

    Alimpokea kwa maswali mengi huku akiongea kwa furaha na machozi yakibaki kidogo yamdondoke.

    "Ulikuwa wapi Mose jamani? Kaka yako Ray, amekutafuta sana kwenye simu amekukosa"

    Ray huyo ambaye Bi Furahiya alikuwa akimuita Kaka, ndiye huyo Moses alikuwa akiitafuta Roho yake. Raymond ambaye ndiye mtu pekee anayemchukia kuliko yeyote duniani. Moses alikaa kochini baada ya salamu za hapa na pale, Alijitia kucheka cheka kumpoteza wasiwasi Bi Furahiya.

    Huo ndio ukawa wakati ambao Moses aliupenda sana. Aliiona glass ya juisi ya machungwa juu ya meza. "Bila shaka alikuwa akiinywa huyu mwanamke" Moses akajisemea.

    Hakutaka kufanya kosa. Aliutoa ule unga wake wa sumu ndani ya moja ya mifuko yake ya suruali. Unga wa nyongo ya mamba ambayo imekaushwa juani hatimaye ikasagwa uliobaki na kuumalizia hapo katika bilauri ya juisi aliyokuwa akiinywa bi furahiya.

    Dakika chache baadaye Bi Furahiya, alirudi akiwa na Glass nyingine ya juisi. Alimpatia Moses, yeye akaenda kuifakamia ya kwake.

    Hakufahamu kuwa anainywa sumu.

    Alipotaka kuongea, dakika tatu zilikuwa nyingi. Moyo wake ukapunguza kasi ya kusukuma damu. Mapigo ya moyo yalikuwa yanapiga kwa mbali sana. Jasho jingi lilikuwa likimtoka Bi Furahiya. Moses alinyanyuka huku akijikung'uta kung'uta koti lake. Alitoa

    picha ya kivuli cheusi, kwenye moja ya mifuko ya koti lake. Akampatia mkononi Bi furahiya. Bi Furahiya alizungumza neno moja tu ambalo halikusikika vizuri.

    "Nakufa"

    Moses akacheka kwa kejeli, akaropoka neno la kuudhi zaidi "Labda nikuongezee sumu nyingine uliyoifakamia kwa uroho" Akacheka kwa nguvu kisha akatoka nje.

    Nyumba hiyo ilikuwa na wafanyakazi lakini wote walikuwa nje hivyo hakuna ambaye ingekuwa ni rahisi kumshitukia Moses kabla hajatoka nje ya geti kabisa.

    Wafanyakazi wote walikuwa katika sehemu zao za kazi. Moses aliwaaga askari wale ambao walionekana kutomjali kabisa mgeni huyo. Akiwa anamfikia Majura huku akitafuna plastiki ile kama dawa ya kuzuia sumu, akalitoa kopo lililofanana na kopo lililohifadhi manukato. Kopo ambalo kama lile ambalo alilitumia kumuua mke wa McCuthbert na Andrew.

    Alipomfikia Majura baada ya stori za hapa na pale, wakati anaondoka akajipulizia ile sumu. Baada ya kuhakikisha sumu ile imefanya kazi ya kupokonya uhai wa Majura, aliondoka bila yeyote kushitukia chochote.

    Baada ya Moses kutokomea, ni dakika nyingi zilipita mpaka ambapo maiti ya Bi Furahiya kufahamika. Aliyetoa taarifa kuhusu maiti hiyo, alikuwa ni mfanyakazi aliyehusika na chakula. Wakati ambao alikuwa akimfuata chumbani kwake kumuuliza kama alikuwa anahitaji chakula, ndio wakati aliomuona Bi Furahiya akiwa anathema povu kaikumbatia sakafu pale pale sebuleni alipokuwa amekaa na Moses.

    Alipiga ukunga, uliowafanya walinzi wa nje kutimua mbio kuelekea sauti ile ya kike ilipotokea silaha zao zikiwa mbele. Waliingia ndani wakiwa wanaangaza huku na kule. Walimshuhudia Bi furahiya akiwa wa baridi, kaikumbatia sakafu juu ya povu lilokuwa likimtoka mdomoni.

    Mmoja wa walinzi hao, alitoka nje na kukimbilia getini kwa Majura. Mbio hazikuwa ndefu sana mpaka alipokifikia kibanda cha Majura, alimkuta Majura naye akiwa amelala usingizi kama wa Bi Furahiya, mapovu mdomoni, picha yenye kivuli cheusi pembeni ya kichwa chake.

    Mlinzi huyo, hakuamini alichokuwa akikiona.

    Alirudi ndani ya nyumba na kuwapa taarifa wenzake wanne waliobaki.

    "Majura amekufa?"

    Wote walishituka.

    Mmoja alitoka bila kuongea chochote mpaka nje ya geti kabisa. Alijaribu kuangaza huku na huko kama anayemtafuta mtu. Akarudi ndani mbio jasho likimtoka pumzi zikipishana

    kwa kasi.

    "Ameshaondoka"

    "Nani?" Mmoja wao akauliza

    "Aliyefanya mambo haya, ni yule aliyetoka hapa punde"

    Wote kwa pamoja walionyesha kuelewa jambo fulani. Wazo la kupiga simu katika ofisi za ambulance. Haikuchelewa kupokelewa

    "Upanga mheshimiwa... Tunashukuru sana"

    Wote wakiwa hawajui la kufanya, wakiwa katika mawazo mazito. Si mfanyakazi wa jikoni, yule aliyekuwa anafua nguo ndani ya chumba chenye mashine za kufulia wala walinzi wote sita

    waliokuwa wamekaa pembeni ya maiti zote mbili.

    Mmoja wao ndipo akakumbuka kuuliza

    "Hivi jina la yule mgeni mnalikumbuka?"

    Mwingine akadakia kwa huzuni "Anha! Siunajua umapepe wa Majura?"

    Mwingine akajisemea "mimi sikumsikia akimtambulisha yule mtu"

    Yule aliyekatishwa akamalizia "majura amezidi umapepe sana alituchekesha chekesha wala hatukumfahamu jina lake"

    Yule aliyegundua maiti ya Bi Furahiya aliuliza jambo. "Mmekumbuka kumpigia baba?" Wakashituka kwa pamoja. Mmoja akakiri kusema

    "Dah! Sisi ni wajinga tumesahau" Ndipo wakati ambao iliingia simu mbaya kwa Raymond na kumfanya apoteze fahamu.

    "Mzee.. Mzee!!?"

    Mmoja wa walinzi aliyejitolea kumpigia Raymond, aliishia kuita bila kufahamu

    nini kimemkuta bosi wao.



    ******CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Raymond akiwa ofisini kwake jumanne tulivu yenye manyunyu na umande mande, alipokea ujumbe mfupi uliosema "Bi Furahiya amefariki dunia kwa sumu, kifo kikihusishwa na muuaji yule yule wa Bertha, Kivuli cheusi"

    Akili ya Raymond ikawa imeleemewa na ujumbe huo mzito, akapoteza fahamu kwa kuikumbatia meza yake pana yenye umbo bapa.

    Baada tu ya jua kuchomoza, Vannesa aliamshwa na simu iliyokuwa ikipiga kelele. Ilikuwa ni simu ya Naima. Katibu muhtasi wake wa ofisi yake ya kuwapumbaza wengine. Kuwapumbaza wasiofahamu kazi yake kubwa ya upelelezi. Alipotaka kuipokea, nayo ikawa imekatika. Kumbe iliita muda mrefu. Alipotaka kumpigia, simu ikaanza tena kuita.

    Akaipokea

    "Habari yako Naima?.. Yah nimechoka sana aisee.. Vipi mbona asubuhi asubuhi.. Jafari Hiza? .. Amefuata nini asubuhi asubuhi?.. Anha mwambie nakuja .."

    Baada ya simu kukatika, alijinyanyua kivivu na kukiacha kitanda. Aliingia bafuni kuoga. Alipotoka, alimkuta Moses amekwishaamka. Alikuwa akiivuta sigara yake taulo kiunoni.

    “oh! Mpenzi umeamka?”

    uso wa Moses haukuwa na furaha licha ya kuongeleshwa kwa huba na Vannesa. Alipomgeukia Vannesa, Vannesa ndipo alifahamu roho mbaya ya Moses kwa mara ya kwanza. Ile sura iliyokuwa ikimchekea na kumuonesha tabasamu siku zote, haikuwepo. Sura iliyojitutumua mbele yake kwa hasira ikaongozwa na maneno ya chuki ya Moses.

    “hivi huyo Jafari Hiza ni nani?” wakati ambao Vannesa alitaka kujibu, alikatishwa “haiwezekani jana wakati tunakula akupigie simu, leo asubuhi asubuhi akupigie simu. Na wewe unakurupuka na kumfuata?” Vannesa akataka kujitetea, Moses akamkatisha tena "Sipendi na nabidi uchague moja"

    Hilo likawa jambo gumu kwa Vannesa kukubaliana nalo. Alijua jinsi ambavyo serikali ilikuwa ikimtegemea. Bila yeye kumpata huyo muuaji ilikuwa ni ngumu kwa jeshi la polisi kumpata. Muuaji ambaye yupo naye karibu na ndiye huyo anayemtazama kwa hasira.

    Vannesa hakujua yeye akawa anatumia akili na nguvu za kibinadamu. Alimtazama kwa hasira, akijuta kwanini aliamua kuwa na mwanaume? Alimuona mwanaume huyo kama ni kizuizi kipya katika kazi yake. Kuna dakika alipokuwa akizitazama ndita za Moses, hakutamani kuendelea kuwa naye. Akajibu kwa hasira

    "Moses, mimi na wewe tumekutana tu barabarani. Hunijui vizuri na pia bado sijakujua vizuri, hii ni kazi yangu inayonipa kula siku zote tafadhali naomba uheshimu kazi yangu"

    Vannesa aliongea kwa hasira hata Moses akaliona hilo. Vannesa akavaa na kujiandaa kuondoka. Alimuacha Moses akiwa bado anapasha mapafu yake kwa moshi wa sigara..



    ******



    Moses alianza kujihisi mwepesi kutokana na jambo alilolifanya. Kumuua Bi furahiya kwake alianza kuona akikaribia ushindi wa kumaliza kisasi chake. Lakini kabla hajamaliza kumuua Raymond, alitaka kufahamu ni nini kilimpata hata akamtelekeza mama yake. Ni nini hasa kilichomfanya amsababishe yeye Moses amuue baba yake kwa mkono wake? Na kwanini amuingize katika kazi haramu za kutoa roho za watu?

    Alifanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila uoga lakini hakuipenda. Alimchukia Raymond lakini hakuwa na jinsi kwa kuwa tayari alishajiingiza kwake. Siku alipotoroka katika himaya yake, ndiyo siku aliyopanga kulipiza kisasi kwa Raymond. Alimchukua Bertha kutoka kwa Yesaya, akifahamu fika ni dada yake wa baba mmoja lakini ikawa ni sehemu ya kisasi chake. Akatembea naye mara nyingi, bila kuwa na mapenzi yoyote moyoni.

    Alifahamu kuwa kuna siku atamaliza chuo na kumiliki rasmi miradi aliyoachiwa na Carlos. Kipindi hicho ndio alitaka aanze kwanza kuitoa roho ya Bertha. Aliamini kuwa akiwa na pesa

    pamoja na nguvu sehemu fulani, basi Raymond asingekuwa tishio kwake. Akamiliki makapuni kwa muda mrefu huku wazo la kuiangamiza familia ya Raymond ikiendelea kumpotezea muda mwingi kuwaza.

    Hakujali kuibeba damu ya Raymond ndani ya mwili wake.

    Alichotaka ni kuingamiza damu yake kama Raymond alivyoiangamiza ya kwake. Akiwa njiani bila kufahamu alipotaka kwenda, akapata nia ya kwenda ofisini kwa Raymond. Alipanga kuonana na Raymond, amuulize hadithi nzima ya mauaji aliyokuwa akiiyafanya huku akitumia mkono wake kuyaficha maovu yake.

    Alitaka afahamu yote kabla ya kumtoa roho yake.

    Akaiacha pikipiki aliyokodisha akaiendea taksi iliyompeleka hoteli ya Rayberth hotel. Hotel iliyomilikiwa na Raymond kwa fedha haramu. Hotel iliyochipuka ghafla huko pembezoni mwa ufukwe wa bahari. Hakupenda kulaza damu kabla Raymond hajapata habari za vifo vya mke wake na mfanyakazi wake wa siku nyingi.

    Moses alipokuwa chini ya ghorofa ya hotel hiyo akimlipa dereva ujira wake, akaliona gari analolifahamu. Aliliona mara ya kwanza katika apartment ya rafiki yake, McCuthbert. Gari ya Jafari Hiza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog