Simulizi : Kivuli Cheusi
Sehemu Ya Tano (5)
Jafari Hiza akapelekwa hospitali kwa msaada wa msamaria aliyejitolea gari yake. Vannesa alipiga simu katika ofisi za Jafari Hiza na kutoa taarifa huku akiomba gari yake kuchunguzwa zaidi.
Alirudi katika gari yake na kuigeuza kuelekea nyumbani kwake. Alipoondoka Vannesa nyuma alifuatwa na gari ndogo ya Moses. Moses aliyekuwa hapo muda wote katika taswira yake ile ile ya uzee, Alimuona Vannesa wakati akiuacha umati wa watu nyuma na yeye kuupokea mwili wa Jafari Hiza. Alichukizwa sana na kitendo cha Jafari kutoka mzima na kuamini kuna kitu ambacho jafari Hiza alimwambia Vannesa, akaamua amfuatilie Vannesa ili apajue anapoishi kwanza.
****
Jafari hiza bila kujua alikuwa akiongozana na Moses ambaye ndiye muuaji, alisimama mapokezi ambapo alikuwa akizungumza jambo na muhudumu wa mapokezi hiyo. Hakujali nini ambacho Jafari alikuwa akichunguza kwa wakati huo, licha ya kujua Jafari alikuwa akichunguza kitabu cha wateja. Aliuona wakati huo ni sahihi kufanya kile alichodhamiria.
Alipanga kumuua Jafari.
Hakutaka kumuua kwa kuacha ushahidi, lakini angejiua mwenyewe. Akakumbuka kuwa alikuwa ana utundu fulani juu ya kuchezea magari na alilijua vyema gari ya Jafari Hiza. Akatoka moja kwa moja mpaka eneo la maegesho ya magari na kuliendea gari ya jafari Hiza. Alipoinama chini ya uvungu wa gari hiyo, akaukata ule mrija ambao ulikuwa ukipitisha mafuta ya breki katika gurudumu za gari ya jafari hiza.
Alipomaliza alimuona Jafari Hiza akija huku akiwa amechanganyikiwa. Alitoka chini ya uvungu wa gari hiyo na kujificha pembezoni mwa magari mengine. Jafari Hiza aliondoka mara baada ya kuiwasha injini ya gari yake, mwendo aliokuwa akiuendesha ulitisha sana.
Ulikuwa ni mwendo wa kasi kuliko wa magari ya mashindano.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moses naye alimfuatilia kwa mwendo ule ule huku akiwa na tahadhari kubwa. Hatua chache kabla hajafika eneo ambalo alipata ajali, Jafari Hiza alionekana kukosa muhimili wake. Kupoteza huko kwa muhimili kulisababishwa na gari lililokuwa likipita mbele ya gari la jafari hiza, Gari hiyo ilibeba kontena. Jafari Hiza aliigonga gari hiyo na kusababisha kontena lililopoteza mhimili wake kutokana na kona kali pia, hivyo likadondoka.
Mlio wa sauti kubwa iliyosikika uliwashitua watu wengi. Hatua chache gari la Moses liliegeshwa pembezoni mwa barabara kama magari mengine. Alitoka ndani ya gari yake na kwenda kushuhudia kifo cha jafari Hiza. Alikuwa na tabasamu pana usoni mwake. Alihisi ushindi kwa kila jambo alilokuwa akilitenda mbele yake.
Akiwa eneo la tukio dakika chache baadaye alimuona vannesa. Alichukizwa sana kumuona Vannesa eneo hilo. akiwa bado anashangaa, akashangazwa kumuona Jafari Hiza akitolewa ndani ya gari lile. Kelele za kusikia kuwa anapumua, zikamchanganya. Akatamani kujitokeza lakini dakika chache baadaye alisikia kuwa amekufa.
Lakini alikuwa amekufa katika mikono ya Vannesa. Alitaka kufahamu nini Vannesa aliambiwa na Jafari Hiza. Vannesa alipoondoka, Moses akamfuata nyuma kama mkia mpaka alipofahamu kuwa Vannesa anaishi kurasini eneo la uhasibu katika kota za bandari.
Vannesa alipofika na kuingia ndani kwake aliwasha taa na kuweka chupa ya whisky mezani kwake. Alipoimimina whisky kwenye glass kiwiliwili kilichojikaribisha kikamshitua ghafla. Akatumbua macho zaidi kwa kuwa aliizima taa. Alipenda kuzima taa alipokuwa akijiweka katika tafakuri nzito. Tafakuri ambazo zilihitaji utulivu mkubwa huku akizisindikiza kwa pombe kali iliyomuunguza koo.
Moyo wake ukamuenda mbio na kuipapasa bastola yake ndogo aliyoisunda kiunoni mwake. Yule aliyekuwa akiingia kama mwizi, akaongea kwa kebehi.
"Huna haja ya kutaka kuniua nimekuja kuzungumza na wewe Vannesa"
Sauti hiyo ilikuwa ile ile ya Moses. Vannesa akaing'amua.
Akanyanyuka na kuiwasha taa.
Sura ilikuwa ni ya Moses. Moyo wake ukaanza kwenda mbio zaidi ya mara kwanza. Si kwamba aliogopa, ila hisia za mapenzi zikampeleka puta. Alimtazama vizuri Moses hakuamini kama ndiye Moses muuaji.
Jamani moses hana sura ya uuaji mbona?
Alipingana na nafsi yake kana kwamba alikuwa akizungumza na kikundi cha watu. Vannesa alimrukia mdomoni mwake Moses na kuanza kubadilishana mate. Kiukweli Vannesa alichanganyikiwa na Moses hata Moses alichanganyikiwa na Vannesa. Zilitumika dakika tano mpaka walipochokana na wote wakakaa kwenye kochi. Vannesa alikuwa na maswali mengi lakini alianza kumuuliza hivi.
"Ilikuwaje mimi na wewe tukawa na uhusiano?"
Akanyamaza kama alikuwa akilisubiri jibu la Moses lakini Moses alipotaka kuzungumza, vannesa akaendelea kuulizia "nilikuwa na kutafuta muda mrefu Moses. Umenikosesha usingizi kutokana na mauaji uliyokuwa ukiyafanya nilitamani nikikutana na wewe, nikuue kabla sijakufikisha polisi. Sababu ya kufanya haya yote ni nini?"
Moses akacheka alipokuwa akiyatazama machozi ya huba yalikuwa yakimtoka Vannesa. Moses akamjibu
"hiki ni kisasi cha damu ya wazazi wangu Bi Tunu na mtu niliyedhani kuwa ni baba yangu Mzee Carlos. Vannesa, ukatili nilio nao na mbinu zote za kikatili amenifundisha Raymond. Raymond ameiteketeza familia yangu na mimi niliapa kuisambaratisha ya kwake"
Maswali bado hayakumuisha Vannesa.
Moses akamuhadithia Vannesa kila kitu. Na hata kuwa ni yeye ndiye amehusika kumuua Jafari Hiza. Jambo hilo likamuuza zaidi Vannesa. Lakini kama aliyerogwa na mapenzi, Vannesa hakumchukia sana Moses.
Alimtazama Moses kama mwanaume au binadamu yeyote mwenye uchungu. Hivyo aliongozwa na hasira kufanya mauaji aliyokuwa akiyafanya. Vannesa akamuuliza
"Kwa hiyo umekuja kufanya nini kwangu na umepajuaje?"
"Nilikufuatilia tangu ulipokuwa katika ajali na ulipoenda kuongea na Jafari Hiza sekunde kadhaa kabla hajafa na mpaka hapa kwako. Nilikuja kukueleza kila kitu kuhusu mimi na ujue ni kiasi gani nakupenda. Nilipanga kukuua tangu siku nilipogundua ulikuwa ukinitafuta. Lakini mapenzi niliyo nayo kwako yamenifanya niwe boya nisisikie chochote juu yako. Nakupenda sana Vannesa na ndio ujumbe ulionileta kwako"
Vannesa alimwangalia Moses huku akitabasamu. Akazivamia papi za Moses na kubadilishana mate kwa mara ya pili. Makochi hayakutosha kufanya walichotaka kukifanya, wakahamia chumbani kwa Vannesa. Chumba kilichohifadhi kitanda kipana chenye umbo la duara. Zuria la manyoya jekundu na sofa mbili zilizotenganishwa na meza ndogo ya duara pia. Moses akawa kama mwenyeji katika chumba cha Vannesa. Alimyanyua na kumtupa juu ya shuka nyeupe zilizotandikwa kwenye godoro pana la sita kwa sita.
Vannesa akawa anatoa miguno ya kimahaba na kumdatisha zaidi Moses kila alipomshika. Moses naye akafanyiwa hivyo hivyo kama vile walikuwa wakilipiziana. Wote wakawa hoi baada ya dakika kadhaa baadaye.
*****
Raymond akashitushwa sana na kifo cha Jafari Hiza. Taarifa hizo alizipata kutoka katika ofisi ya jafari hiza. Ni saa chache tangu mwili wa jafari hiza ulipoingizwa ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.
Raymond akamkumbuka Vannesa.
Akajaribu kupiga simu yake muda mrefu ikawa inaita bila kupokelewa. Akajaribu tena ikawa inakatwa mfululizo baadaye ikazimwa kabisa. Ni wakati huo ndipo Moses alikuwa akitafuna tunda la Vannesa. Vannesa mwenyewe alikuwa ahitaji usumbufu mara baada ya kumaliza raundi ya kwanza wakisubiri ya pili.
Raymond hakulijua hilo.
Hakujua kuwa yule malaika mlinzi ametekwa na shetani. Hakujua pia marafiki zake wote ndio wabaya wake. Moses huyu si ndiye alikuwa akimfundisha na kumtuma kumuua fulani na fulani basi huyu huyu aliyemuahidi kumletea mtuhumiwa wa muuaji ambaye ni Vannesa ndiye aliahidi kumlinda Muuaji asikamatwe pia. Akawa hana mtu aliyebaki naye pia, akawa peke yake. Kukatiwa simu na kuzimiwa kabisa kukamuudhi sana.
Akaamua kulala.
Wiki ikapita huku asimuone Vannesa wala kupata simu yake. Akiwa ofisini kwake ndani ya mawazo mengi jinsi maisha yalivyombadilikia kwa kipindi kifupi, mlango wake ukafunguliwa. Alikuwa ni katibu muhtasi wake.
"Unasemaje Veronika?"
"Kuna wageni wanahitaji kukuona"
"Sina apointmnent leo hufahamu"
“Nafahamu bosi ila wamenisihi sana"
"Ni nani na nani?"
"Mwanamke alijitambulisha kwa jina la Vannesa" macho ya Raymond yakamtoka pima, vero akaendelea "na mwanaume amejitambulisha kuwa yeye ni Moses"
"Moses?"
Raymond alihamaki kwa sauti ya juu.
"Ndiyo bosi"
"Waruhusu waingie"
Alijishika kiuno na kukiinamisha kichwa chake chini asiamini kama moses yupo hai. Akajiuliza wakati ambapo Moses na vannesa alikuwa akiingiaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Moses yupo hai?.."
Kabla hajamaliza, alikuwa kama anayetazamana na mzimu. Macho yake yalimtoka pima alipotazama eneo la mlangoni. Akapiga kelele kama asiyeamini. "Moses!!?"
Moses na vannesa walikuwa wakitabasamu kwa pamoja walipokuwa wakiingia katika ofisi ya Raymond. Macho yake hayakuwa macho ya kawaida yamtazamayo mwanadamu wa kawaida. Yalikuwa ya uoga mwingi, mshangao wa kushangaa kitu kilichoshitusha na haswa asichokitegemea. Kumuona Moses, ilikuwa ni kama aliyeona mzimu. Alikumbuka mara baada ya kumkosa Moses kwenye simu, alipokea taarifa kuwa Moses amefariki.
Alishangazwa kumuona Moses akipumua, akitabasamu na kutembea kwa furaha zaidi.
"Sasa huyu ni nani?" Kabla hajajibiwa lolote na yeyote ambaye hajamsikia, Vannesa na Moses walijikaribisha juu ya viti mbele ya meza pana ya ofisi ya Raymond. Bado mshangao ulikuwa juu ya uso wa Raymond. Alipokuwa akikaa, alikuwa akimtazama Moses kwa kumshangaa kiajabu. Akamgeukia Vannesa kama ndiye alikuwa na jibu hilo.
Vannesa akatabasamu zaidi.
Raymond hakuelewa nini kilichokuwa kikiendelea kwa kuwa bado Moses hakuweka mezani ujumbe uliomleta huku akiongozana na Vannesa. Raymond alitambua kuwa Vannesa ni mpelelezi anayefanya kazi zake kwa kujitegemea, hiyo ni siri aliyofichuliwa na Jafari Hiza. Siri ambayo Jafari Hiza alipoamua kuvunja miiko ya kazi kutoa siri kutokana na kulaghaiwa na pombe iliyomlewesha huku akisunda kibindoni kitita kikubwa cha pesa, akaongea kilevi
"Yule ni mwanamke mjanja sana" Raymond akawa anamkodolea macho Jafari Hiza kwa shahuku. Jafari hiza akasema "Kalikataa ofa ya mheshimiwa raisi" akabeua kidogo na kumalizia "yule ni mpelelezi lakini, lakini si wa kuajiriwa. Ujanja janja wake wa uandishi wa habari na kuyahatarisha maisha yake alipojiunga katika jeshi ndiyo vinampa kiburi"
Hiyo ndiyo sababu ya kufahamu kazi ya siri aliyokuwa akiifanya Vannesa. Baada ya kushangaana huko, ndio kwanza Moses akakumbuka kusalimia.
"Habari yako Raymond" Raymond akaitikia kwa uchangamfu sana.
"Salama simba wangu ulikuwa wapi siku zote? Nimekutafuta sana"
Tabasamu likazidi kumpanuka. Akajikoolesha pale kwa uongo kisha akajibu
"Nilikuwa hapa hapa nikiitafuta roho yako" aliutazama uso wa Raymond. 'Ndiyo' alikuwa amesikia
kilichozungumzwa lakini hakuelewa. Moses akaendelea "lakini sintokuua mpaka unieleze ukweli kuhusu mama yangu. Kwanini ulimfukuza akiwa na ujauzito pamoja na kumtelekeza bila kufahamu kama alikuwa ana mimba yako"
Raymond akacheka. Alicheka sana mpaka akashika kitambi chake. Alimuangalia Vannesa akamuuliza
"Umemtoa wapi kijana wangu?" Akacheka tena kwa kuongeza kasi zaidi ya kucheka huku akimgeukia Moses tena akamgeukia Vannesa "Ulimuokota mtaani? Jalalani? Umemtoa wapi?"
Akaongeza tena kicheko.
Moses na Vannesa wote walikuwa wakimtazama bila kupitiwa na kicheko wala tabasamu. Raymond akaendelea "labda nikuulize" akaitengeneza koo yake kwa kikohozi na kuendelea kuzungumza "nimekaa na wewe siku zote, ni mama yupi unayemzungumzia?"
"Tunu, Tunu baganda" Raymond akashituka alishituka sana hata kikohozi cha kushangaa kikamlipuka. Akauliza bila kujielewa alichokuwa akikizungumza
"Unamfahamu.. Una.. Tunu?" Moses alikuwa akitabasamu huku akitingisha kichwa. Raymond akauliza
"umemfahamu vipi Tunu? Ni siku nyingi? Haiwezekani"Moses akamwambia
"Ndio ni siku nyingi sana ndio maana ulimfukuza akiwa na mimba yangu"
Raymond akainamisha kichwa chake akijaribu kuwaza mambo yanayomtokea. Yalikuwa mazito kiasi cha kumuumiza sana. Ni juzi tu alitoka kumzika mke wake aliyetanguliwa na mtoto wake wa pekee anayemfahamu, Bertha. Aliona dunia ikimuadhibu kabla ya muda sahihi wa adhabu kufika. Mawazo ya Raymond yakawa mbali, miaka mingi iliyopita.
*****
Miaka 28 iliyopita, Ilikuwa majira ya kipindi cha baridi kati kati ya vitongoji vya kijiji cha kanazi huko bukoba. Tunu Baganda alikuwa anatoka shuleni Raymond akitoka kukata tikiti ya kurudi mjini Dar esa salaam.
Tunu akiwa anasoma katika shule ya kansenene kidato cha tano. Nani asingesimama kumtazama Tunu, huku akiusifu uumbaji wa mwenyezi Mungu? Tunu mwenye macho malegevu, mapaja yaliyovimba, chuchu zilizomsimama kifuani na mzigo alioubeba nyuma chini ya mgongo.
Huyo ndiye Tunu aliyeimeza miaka kumi na nane pekee. Majira ya saa 12:30 jioni ndipo alikutana na Raymond karibu na shamba lao la kahawa.
"Samahani dada"
Tunu naye akasimama.
Ilikuwa ni sauti ya Raymond aliyeshindwa kuvumilia. Alishindwa kuitazama sura iliyoshabiahana na warembo aliokutana kati kati ya jiji la Dar es salaam. Weusi wake na uzuri wa asili ndiyo uliomvutia. Alipompita na kupata nafasi ya kumtazama nyuma ndipo hakuvumilia akaamua kumuita.
Tunu akasimama.
Baada ya kumuita hakujua amwambie nini sasa. Alimsogelea mpaka alipo na
kumsalimia tena
"Habari yako?"
"Nzuri"
‘Aibu’ Raymond akaiona aibu usoni mwa Tunu. Akauhisi ushindi, japo hadi wakati huo bado hakujua kama yalikuwa ni mapenzi yalikuwa kweli alikuwa ametamani.
"Naitwa Raymond naishi hapo jirani baada ya shamba la pili kwenye nyumba ya mzee Jonathan, sijuhi mwenzangu unaitwa nani?"
"Mimi?"
Tunu akawa amecheka, kana kwamba hakuwa akiongeleshwa yeye. Raymond naye akacheka na kuitika
"Ndiyo nazungumza na wewe"
"Naitwa Tunu"
"Tunu nimetokea kukupenda sana tafadhali usinishangae kwa kukuambia haya ila nimeshindwa kujizuia mara baada ya kukuona"
Hakujibu haraka, lakini Raymond alilitarajia hilo. Wakiwa wamesimama muda mrefu bila kuzungumza chochote huku wakitazamana, Tunu akaukata ukimya huo
"Mimi sijazoea naomba niende"
"Kwani unakaa wapi ?"
"Ha! Sikukuambia n'na kaa kwa mzee Baganda hapo mbele?"
"Hukuniambia. Sasa naweza kukuona kesho? Kwa kuwa siku tano mbele nasafiri" Tunu akaonesha kushangaa. Akauliza
"Una safiri?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndiyo nilikuja kusalimia ndugu zangu baba na mama yangu wanaishi huku mimi naishi Dar es salaam"
"Dar es salaam?"
Akili ya Tunu ikawa imevurugwa sana na kusikia jina la jiji hilo. Hiyo ni baada ya ule ugonjwa kwa wale wanaoishi vijijini kipindi hicho cha miaka ya themanini kutamani sana kuja Dar es salaam. Hiyo ndio sababu hata Tunu na Raymond walipoachana, kuna kinafsi kilichokuwa kikimchombeza Tunu kuingia katika uhusiano na Raymond.
Usiku kucha alikuwa akimuwaza Raymond. Akalikumbuka tabasamu lake na yeye akacheka kwa sauti. Kutokana na nyumba yao kutokuwa na umeme na kuwa na mazoea ya kulala mapema, leo Tunu alilala saa sita usiku.
Mawazo yote yakawa juu ya Raymond.
Akapanga akikutana naye tena atamkubalia na kutoroka naye kuja mjini pamoja naye. Huo ndio ukawa mwanzo wa Tunu na raymond.
Ilipofika asubuhi ambayo bado ilikuwa haijalichomoa jua lake jekundu vizuri,
Tunu alizivaa sare zake za shule kama alikuwa akielekea shule. Nani angegundua kuwa kama alikuwa haendi shule? Ikiwa alionekana sana kuipenda shule? Walikutana na Raymond katika shamba la ndizi walipoahidiana kuwa wangekutana hapo siku mbili zilizopita. Nani angefahamu kama ameshakubali kulaghaiwa? Ikiwa mwenyewe ameamua kufanya hivyo?
Alipenda kufika mjini siku moja.
Hakupenda kila siku kuwa msikilizaji, akatamani siku moja na yeye kuwa msimuliaji kwa aliyoayaona huko aendako. Kwakuwa Raymond alikwisha kata tikiti, ikawa kama bahati ya kupata siti ya pamoja wote wawili.
Gari ikapita barabara ya kati.
Barabara mbovu iliyopita kahama na kuwalazimu kulala singida. Saa 11:45 walianza safari kwa kuipita Dodoma kisha morogoro na kuingia Dar es salaam saa 12 jioni. Tunu alishangaa kila alichokiona.
Raymond alimkaribisha Tunu katika chumba chake kimoja huko Ubungo kibangu. Kabla ya mwaka kusubiri mwezi mmoja ukatike, kuna kitu kikamtembelea Tunu. kichefuchefu na kutamani vitu vichachu vichachu.
"Mimba!"
Akajisemea kama anayejinong'oneza. Si mimba pekee iliyoingia ndani ya nyumba ya Raymond. Tabia mpya ya Raymond ilimfanya Tunu kuwa mnyonge. Tabia ya ulevi na kurudi usiku
wa manane nani angeivumilia. Kipindi hicho chote Raymond alikuwa hafahamu kama Tunu ana mimba. Hivyo alimpiga bila huruma kila mara alipokuwa analewa.
Tunu akapanga kuondoka.
Alitamani kurudi nyumbani lakini akakumbuka kuwa alitoroka, aliogopa kurudi. Akajipa ujasiri kuwa angeyaweza maisha ya kubangaiza mtaani. Alihamia huko buguruni kwa mnyamani. Kazi ya kuchoma vitumbua ndiyo ikawa chanzo cha kumuingizia pesa ya kula na kumudu hali yake ya ujauzito.
Aliweza kumudu gharama za kulipia chumba cha kupanga maeneo hayo hayo jirani na alipokuwa akichomea maindi. Raymond aliporudi nyumbani, kama kawaida yake akipepesuka huku na huko matusi yakimtoka kinywani, Hakumkuta Tunu.
Maisha ya upweke nayo yakamtafuna kadri siku zilivyozidi kwenda. Tunu alijulikana na wengi kutokana na kuwa na wateja wengi waliopenda vitumbua vyake. Jumapili moja baada ya kumaliza
kuuza vitumbua vyake barabarani, akiwa amejipumzisha ndani kwake alisikia hodi. Wasiwasi ukampaa akidhani huenda alikuwa mwenye nyumba,lipofungua mlango hakuwa yeye.
Carlos alikuwa mlangoni.
Kijana mtanashati wa mavazi na mzuri wa sura.
"Karibu"
"Hapana ahsante, nina jambo nahitaji kukuambia"
Carlos na Tunu walikuwa wanafahamiana kutokana na vitumbua. Carlos alikuwa anapenda sana kununua vitumbua vya Tunu. Haikujulikana kama alipenda vitumbua tu ama hicho kilichomleta.
Hicho ambacho kilimfanya asiingie ndani na kuishia mlangoni. Tunu akiwa amesimama kumsikiliza Carlos anataka kusema nini.
"Tunu nahitaji kuwa na wewe muda mrefu nimejisikia kukuambia kuwa nakupenda ila sikujua ni vipi nitaanza kukuambia."
Tunu alilichukia sana neno hilo, alichukia kuambiwa anapendwa. Kwa kuwa alishadanganywa akaiacha shule na aliachwa baada ya kuhisi kuwa alichezewa na kupewa ujauzito huo. Carlos alitumia dakika 45 kumshawishi Tunu.
Alifanikiwa kumnasa.
Zikiwa zimebaki siku chache ajifungue. Alikuwa tayari amehamia nyumbani kwa carlos. Asubuhi ya Jumatatu tarehe 14 mwezi wa kumi wa mwaka 1986, Tunu akapata watoto wawili mapacha. Watoto wa kiume ambao aliwaita Mariano na Moses. Wiki chache baadaye Mariano alisumbuliwa sana na pumu iliyombana usiku kucha. Siku chache baaaye Mariano akawa amefariki na kumuacha, mdogo wake.
Moses akalelewa kwa amani na furaha huku akikua na kuamini kuwa Carlos ndiye baba yake mzazi. Akaupata umri wa kwenda shule baada ya miaka kwenda zaidi. Tunu hakufahamu kuwa Raymond na Carlos walikuwa wakifahamiana. Hakufahamu kuwa wao ni marafiki wa karibu kwa muda mrefu sasa. Ni siku hiyo ambayo Carlos alimkaribisha Raymond nyumbani kwake bila kufahamu kama Tunu pia alifahamiana na Raymond.
Raymond akatafunwa na wivu.
Hakujua kama Carlos ndiye alimficha Tunu wake muda wote huo aliosumbuka akimtafuta. Alitamani kumueleza rafiki yake kuwa huyu ndiye msichana wake aliyewahi kumueleza lakini kuna nafsi ikamkataza. Alibaki akimtazama Tunu kwa jicho la hasira. Moyoni akajiapiza
"Nitakufanyia kitu ambacho ni heri mimi na Carlos wote tukose"
Kipindi hicho pia ndio ilikuwa mara ya kwanza kumuona Moses, Akavutiwa naye. Alipoondoka alipanga nini afanye juu ya kuitekeza familia ya Carlos. Urafiki wake na Carlos ukamtoka. Akapanga atamuanza Tunu kisha Moses ambaye alidhani ni mtoto wa Carlos na Tunu atamuua baba yake kwa nguvu yake ya ushawishi na huo ungekuwa mwisho wa Moses pia baada ya kumuangamiza baba yake.
Baada ya wiki chache baadaye baada ya Tunu kumueleza kila kitu Carlos kuhusu Raymond, Carlos akapokea taarifa za kifo cha ghafla kwa kugongwa na gari kilichompata Tunu. Carlos akafahamu ni njama zilizotengenezwa na Raymond.
Uadui mkubwa ukaibuka kati yao.
Hawakuwa tena na uhusiano mzuri zaidi ya kila mmoja akimtafuta mwenzake na kulipiza kisasi. Bila kufahamu Carlos, Moses alikuwa karibu sana na Raymond kwa kipindi hicho.
XXXXX
Hiyo ikawa hadithi iliyomfumua Moses ufahamu wake kwa kiasi kikubwa. Moses alifahamu vizuri kuhusu kaka yake mama yake na alimjua baba yake. Lakini kitu ambacho bado kikawa kitendawili ni kuwa Raymond hakufahamu kuwa Moses ni mtoto wake.
Baada ya hadithi hiyo, ndipo Moses naye alizungumza
“baba”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Raymond alishituka. Alikuwa amejiinamia wala hakujua kuwa alipokuwa akikukumbuka kila jambo lililotokea hapo zamani, alikuwa akizungumza kwa sauti. Sauti ambayo Moses na Vannesa walikuwa wakimsikia.
Jina hilo la ‘baba’ ndiyo lilimshitua.
“wewe ni baba yangu” Moses akajibu huku Vannesa akitabasamu. “hukufahamu jambo hili kwa kuwa ulimfukuza mama yangu, mimi na kaka bado tukiwa tumboni”
Raymond akashituka “kaka? Kaka yako yupi?”
“Tulizaliwa mapacha ila yeye kaka alifariki wiki chache baadaye”
Moses akamueleza kila kitu huku machozi yakimtiririka. Raymond naye alisikiliza hadithi hizo kwa hisia kiasi cha kumtiririsha machozi yaliyokuwa magumu kumtoka siku zote. Wakiwa wote wanalia yaani Moses na Raymond, Moses alinyanyuka akitoa bastola yake aliyoipachika kwenye kiuno.
Vanessa alipoiona hali hiyo, akamzuia kufanya alichotaka kufanya.
Ikiwa tayari Vannesa alikwishawatumia askari anaofahamiana nao ujumbe kwenye simu zao kisirisiri na kuwaelekeza maeneo hayo. Askari hawakuchelewa sana. Walikuja na silaha nzito za moto kutokana na kumuogopa sana kivuli cheusi.
“naomba unisamehe Moses” Moses alikuwa ametiwa pingu baada ya Kurudishwa mikono yake kwa nyuma. Moses alishangazwa na hali hiyo. Aliduwaa akimshangaa Vannesa huku akijiuliza nini kinatokea? Hali hiyo ikamkumba vile vile Raymond. Hakuelewa kwanini pia naye alitiwa mbingu. Vannesa akadondosha chozi huku akijifuta kwa kiganja chake. Akasema kwa huzuni.
“Moses naomba unisamehe kwa kukulaghai kuwa nilikupenda sana. Zilikuwa ni njama tu kukuingiza katika mtego wangu. Nilikupenda mwanzo lakini si kabla hujamuua Jafari Hiza. Rafiki yangu wa toka utoto wetu. Nilikuchukia tangu nilipofahamu una sura ya binadamu lakini roho ya mnyama ndani yako. Nitahakikisha wewe na baba nyako mnapata adhabu inayostahili. Kutokana na visasi vyenu, mmepoteza uhai wa wengi wasio na hatia”
…. MWISHO ….
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TOA MAONI YAKO TAFADHALI!!!!........
ASANTENI
0 comments:
Post a Comment