Simulizi : Kivuli Cheusi
Sehemu Ya Nne (4)
Akaiacha pikipiki aliyokodisha akaiendea taksi iliyompeleka hoteli ya Rayberth hotel. Hotel iliyomilikiwa na Raymond kwa fedha haramu. Hotel iliyochipuka ghafla huko pembezoni mwa ufukwe wa bahari. Hakupenda kulaza damu kabla Raymond hajapata habari za vifo vya mke wake na mfanyakazi wake wa siku nyingi.
Moses alipokuwa chini ya ghorofa ya hotel hiyo akimlipa dereva ujira wake, akaliona gari analolifahamu. Aliliona mara ya kwanza katika apartment ya rafiki yake, McCuthbert. Gari ya Jafari Hiza.
*****
Mara tu baada ya kuachana na Moses hotelini, Vannesa alienda hadi zilipo ofisi zake. Huko alikutana na Jafari Hiza akiwa anajiandaa kuondoka.
"Umekula ng'ombe mzima umelishindwa Jicho?" Akamtania Jafari Hiza.
Jafari hakucheka, akataka kutoka bila kuzungumza chochote. Vannesa akamzuia kwa kumshika kifuani
"Unaenda wapi sasa?"
"Mke wa Raymond amefariki" akajibu kwa hali ya kughafirika. Jibu hilo likamshangaza sana Vannesa "Amekufa!?" Jafari hakujibu kitu, kutokana na bumbuwazi ya kifo cha Bi Furahiya iliyomkumba ghafla Vannesa, akaongozana na Inspekta Jafari Hiza mpaka nyumbani kwa Raymond.
Vannesa akapanda gari ya Jafari kuelekea huko. Wakiwa njiani, Jafari Hiza aliamua kumpigia Raymond. Simu yake ilipopokelewa sauti haikuwa ya Raymond.
"Unasema?.. Basi tunakuja sasa hivi"
Jafari akamueleza Vanessa yote kuhusu taarifa aliyoipokea kutoka kwa mfanyakazi wa Raymond; kuwa Raymond amepoteza fahamu na amezinduka dakika chache zilizopita, hivyo amepumzika.
Vannesa akasema “Unaonaje tukapitia ofisini kwake kisha tuelekee nyumbani. Kwa sababu
tunaweza kupata chochote huko"
"Sawa"
Jafari Hiza alikubali ushauri wa Vannesa. Akaligeuza gari yake na kuelekea kawe ilipo hoteli ya Raymond. Kwa mwendo wa speed kali, kutokea zilipo ofisi za Vannesa walichukua dakika ishirini pekee kuwafikisha kwenye hoteli ya kifahari ya Raymond. Hawakutaka kupiga simu kwa kuwa walipafahamu mpaka ofisini kwake.
Jafari Hiza aliongoza mbele akifuatiwa na Vannesa.
Walikuwa wakipanda lifti kuelekea ghorofa ya tatu zilipo ofisi za Raymond. Hiyo ni baada ya kuliegesha gari yao eneo la maegesho. Walikaribishwa ofisini kwa Raymond baada ya kuonesha vitambulisho vyao. Raymond alikuwa akihema kwa uoga akashusha pumzi ndefu baada ya kumuona Jafari Hiza.
"Afadhali umekuja Jafari" Akapata nguvu ya kusimama. Machozi yakiendelea kumtoka, akawakaribisha Jafari na Vannesa. Aliwaondoa wafanyakazi wake waliokuja kumjulia hali.
"Mke wangu Jafari"
Alikuwa ameinamisha uso wake, alipouinua, ulikuwa umelowa machozi.
"Pole sana Raymond"
"Nitapoa vipi wakati amesema anaitaka roho yangu?" Raymond akawa mkali. Lakini hiyo haikumtisha vannesa kuuliza.
"Wewe unadhani ni nani anahusika"
"Wewe mwanamke una kichaa?"
Akavuta kamasi jepesi na kumuuliza kwa hasira "ina maana Jafari mnafanya nini mpaka sasa?"
"Tupo hapa kukusaidia, mzee"
"Mnanisaidia kumtafuta nani?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Muuaji wa mke wako"
"Sasa muuaji wa mwanangu ndiye muuaji wa mke wangu." Alinyanyuka akawa anazunguka kila upande wa ofisi "anajiita kivuli cheusi"
Vannesa naye alikuwa amenyanyuka na kwenda upande wa dirishani huku akimuuliza swali Raymond "Natumaini Raymond hili ni jambo unalolifahamu kuhusu..." Kabla Vannesa hajaendelea kuzungumza, alinyamaza ghafla. Alinyamaza mara baada ya kumuona
mtu ambaye anayemfahamu. Alipotazama kwa makini,
“Hapana”
Akajisemea'Inawezekana namfananisha' Bila kujua wote waliokuwepo ofisini humo wakimtazama yeye, alitoka mbio na kuikimbilia lifti ya kumshusha chini. Bila kuelewa Jafari Hiza akaelekea dirishani kuchungulia chini ya ghorofa ya hoteli hiyo hakuona cha maana.
XXXXX
Moses baada ya kuliona gari ya Jafari Hiza, akataka kumfahamu mtu huyo vizuri. Bila shaka alikuwa na hakika mtu huyo yupo katika ofisi za Raymond. Akataka kufahamu uhusiano uliopo kati yake na Raymond pamoja na Vannesa.
Sawa alijua Vannesa kuwa ni mpelelezi, mpelelezi aliyetumia kivuli cha uandishi wa habari kuficha uhalisia wake. Lakini yeye akamuona Vanessa kama shushu mwenye njaa anayependa kufuatilia mambo ya hatari kuiepusha njaa ya siku chache badala ya kifo cha milele.
Akajipa moyo na kuzifuata lift za kumpandisha mpaka juu. Aliifahamu vyema ofisi ya Raymond kwa kuwa haikuwa mara ya kwanza kuingia katika jengo hilo. Lakini alipofika ndani ya
lift na kutaka kubonyeza nambari ya kuelekea zilipo ofisi za Raymond, roho yake ikasita. Iliposita hakubonyeza kitufe cha namba na kubonyeza kile cha kufungua mlango.
"Hapana siendi"
Roho yake ilipokataa, akaitii. Alitoka mpaka nje tena, na kuifuata ilipo barabara. Ni hapo ndipo Vannesa akiwa juu ya ghorofa ndani ya ofisi ya Raymond, alimuona Moses. Kwa kuwa alihisi amemfananisha hakutaka kuamini tu kwa kumfananisha.
Alitaka kujiridhisha kwa macho.
Alitaka kumuona huyo aliyefanana na Moses kuanzia utembeaji, nguo alizovaa pamoja hata na umbo lake. Vannesa akawa ameshuka na kumuona Moses akiwa kwa mbali kidogo. Umbali uliowatenganisha kwa miguu isiyopungua ishirini. Akashindwa hata kumuita, lakini alipata uhakika kabisa ndiye Moses anayemfahamu.
Akarudi ofisini kwa Raymond akiwa na mawazo.
Mawazo ya kujiuliza Moses amefuata nini katika hoteli hiyo? Sawa ni hoteli na kila mtu alikuwa na uhuru wa kufika katika hotel aipendayo, lakini si kwa Moses aliyemuacha hotelini kule kinondoni. Kulikuwa na mtu alikuwa na miahadi naye? Akaitazama saa yake. 'Hapana' akajisemea. Haiwezekani amuache saa nne asubuhi hotelini tena kitandani halafu saa nane awe amefika katika hoteli hiyo. Ni saa ngapi ameshakutana na mtu huyo na kuzungumza naye? Kwanini awe hana gari? Kuna uwezekano ana uhusiano wowote na Raymond?
Akajiondoa hofu na kusema inawezekana alikuwa ni mteja kama wateja wengine waliofuata huduma ya hoteli ya Reyberth kama wengine. Akaufungua mlango wa ofisi ya Raymond. Hata alipoingia ndani ya ofisi ya Raymond, bado alikuwa akiwaza kuhusu Moses.
Lakini hawakukaa sana ndani ya ofisi hiyo, wote watatu walitoka kwa nia ya kurudi nyumbani kwa Raymond. Vannesa na Jafari Hiza walipanda kama walivyokuja, raymond akawa peke yake. Walipofika tu katika mtaa aliokuwa akiishi Raymond, simanzi ilionekana katika kila nyuso ya mkazi wa mtaa huo.
Ni mmoja tu ambaye alipata nguvu ya kuisimamisha gari ya Raymond.
Alikuwa ni mwanamke wa makamo aliyelowa machozi. Alilia kwa uchungu.
Raymond alimfahamu fika
"Habari yako mama Koku"
"Si nzuri jirani yangu" akajifuta machozi kwa upande wa kanga, "tafadhali usiingie ndani ya nyumba yako kwa sasa"
"Kwa nini?" Raymond alihamaki kwa mshangao. Vannesa na Jafari nao walikuwa wameshashuka kutoka katika gari lao wakisikiliza kilichokuwa kikisemwa na mama huyo aliyekuwa akivukwa na nguo kwa kilio.
"Nipo na Merce nyumbani kwangu, nusu saa zilizopita amekuja na kunieleza kuwa kuna mauaji yametokea nyumbani kwako. Ndipo akanieleza kuwa kuna mgeni aliyekuja nyumbani kwako"
Mwanamke yule akawa anamuhadithia Raymond. Mgeni huyo alifika nyumbani bila mtu yeyote kumfahamu. Ni Majura pekee mlinzi wa getini ndiye alikuwa akimfahamu. Akaeleza kuwa mgeni
huyo pia Bi Furahiya alikuwa akimfahamu hivyo alikaribishwa sebuleni na Bi Furahiya kwenda kumuandalia kinywaji. Hakukuwa na mtu sebuleni zaidi ya mgeni anayeshukiwa ni muuaji na Bi
Furahiya. Mara Merce alipoenda kuwaandalia chakula ndipo alifahamu kifo cha Bi Furahiya. Hatimaye walinzi waliokuwa wakilipwa na Raymond pia kati yao akaeleza kuhusu kifo cha Majura getini.
Wote walionekana kufa kifo kimoja.
Wote walitoa mapovu na walikufa haraka. Walilala usingizi wa milele kwa
aina moja. Hadithi hiyo ya mama koku ikazidi kumtia uchungu Raymond. Akashuka garini na kutaka kuingia ndani kwa jazba.
Mama Koku akamzuia. "Tafadhali usiingie" Raymond akasimama "naomba usubiri nimalize kuzungumza"
Baada ya kufahamika Majura na Bi furahiya wamefariki, kosa lingine likafanyika. Hapo moyo wa Vannesa ukaanza kwenda mbio. Wakasikiliza kwa makini. Jafari Hiza na Vannesa walikuwa wakisikiliza kwa makini sana. Mama koku akawa anaendelea huku akivuta kamasi jepesi lililokuwa likijipenyeza katika pua zake. Kuna mmoja kati ya wale walinzi sita aliokota kopo la manukato. Macho ya Jafari Hiza yakamtoka pima.
Mama Koku akaendelea. “Akaipuliza ile hewa aliyodhani ni manukato. Kati ya walinzi wale sita hakuna aliyehimili kusimama kwa miguu yake. miongoni mwa wafanyakazi wote wa ndani ya nyumba ya Raymond aliyepata nafuu ya kutoka nje akiwa hai alikuwa ni Merce. Hewa ile ndani ya chupa ya manukato ilikuwa ni hewa ya sumu...Mimi ndiye nilimsaidia Merce kumpa maziwa. Ndiye aliyenihadithia hadithi yote hii"
Mama Koku hakumalizia hapo akaishia kwa kumwambia kama ushauri Raymond "unaweza kuchagua kuingia ama kusubiri taarifa ya wauguzi waliokuja kuchukua miili ya watu wako"
Jafari Hiza akazungumza "Hiyo sumu ndiyo ile niliyokuambuia Vannesa" akamwangalia Vannesa kisha akagota kwenye uso uliomvimba Raymond kwa kulia "Huyu muuwaji ndiye huyu huyu aliyemuua mwanao Bertha na wote niliokupa taarifa juu ya vifo vyao. Huyu ndiye aliyewaua wamiliki wa apartment aliyofanyia mauaji ya shahidi namba moja aliyekuwa akimfahamu kule masaki kwa sumu hiyo hiyo" akawaeleza aina ya sumu ambayo aliitumia kwa kuichanganya katika chupa ya manukato. Habari hiyo haikumfanya Raymond kuacha kulia. Alilia kama
mtoto.
Jafari Hiza akaeleza kuwa "hewa hiyo yenye sumu hudumu kwa dakika tano tu hewani, hivyo hakuna shaka kama tukiingia"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wote wakaingia na kukuta miili ya watu kumi na moja ukiwemo wa bi Furahiya, Majura, walinzi sita na wafanyakazi watatu. Walikuwa wamefunikwa katika mifuko maalumu ya maiti.
******
Wakati ambao walikuwa wakizungumza pale nje, ni wakati ambao Vannesa alimuona tena yule mtu aliyemuona kule hotelini kwa Raymond. Hakuwa amebadili shati lake jeupe, alifunga tai ya pink na suruali nyeusi juu akiwa amehifadhiwa na koti jeusi. Alipendeza sana.
Ila kwa Vannesa ikawa ni tatizo.
Akajiuliza kuhusu kumuona sehemu mbili zote zikiwa ni sehemu za ajabu. Alipatwa na wasiwasi sana juu ya Moses. Akaamua kumpigia simu baada ya kujitoa pembeni kidogo katika maongezi ya Raymond, mama koku na Jafari Hiza.
"Uko wapi Moses?.. Upanga.. Na mimi nipo hapa.. Hallo.. Hallo.."
Simu ikawa imekatwa na alipojaribu kupiga mara ya pili ikawa haipatikani. Akaamua kumtafuta mwenyewe.
Akawa haonekani.
Kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Hivyo haikuwa rahisi kumuona.
Alirudi kwa Raymond kumuuliza kuhusu kufahamiana kwake na Moses. Aliamini fika kulikuwa na uhusiano fulani kati yao. Yeye hakuwa akijua kuwa Moses ndiye muhusika mkuu wa mauaji hayo,
lakini kwanini Moses awe mtu kama anayeficha jambo kila anapomuona katika mazingira ya himaya ya Raymond? Raymond alikuwa tayari yupo ndani akilia juu ya maiti ya mke wake. Alimuacha kwa muda mpaka atakapopata nafasi nzuri ya kuzungumza.
Wakati ukafika, walikuwa wawili tu majira ya jioni ndani ya gari ya Raymond. Ilikuwa ni baada ya kutoka hospitali.
"Naomba nikuulize jambo Raymond"
Raymond akaitika kiunyonge "Sema chochote Vannesa"
"Unamfahamu mtu anayeitwa Moses?" Raymond akapiga breki ya ghafla na kutumbua macho juu ya uso wa Vannesa, akamuuliza kwa mshituko "Umemfahamu vipi Moses? Umemuona? Namtafuta sana, umemuona wapi huyo kijana tafadhali niambie nitampata vipi?"
Vannesa akaonesha tabasamu tu la kutoridhisha wala kuonesha kama alikuwa anafahamu chochote kuhusu Moses. Yeye mwenyewe akajisuta kuwa hakuwa akimfahamu Moses zaidi ya kumfahamu Moses wa kitandani, alimfahamu Moses wa chumbani, juu ya kitanda cha hoteli aliyekuwa akioga naye bafuni. Hakujua kazi ya moses wala hakuwahi kumuuliza. Hakujua nyumbani kwa Moses wala ndugu zake, ndio sababu hakujibu kitu mpaka Raymond alipozungumza kwa sauti iliyoonesha kukata tama "Moses ameshakufa siku nyingi" akawasha gari na kuanza safari ya kuondoka
"Amekufa!?"
Mshangao wa Raymond akawa ameupokea Vannesa mapigo ya moyo yakamuenda mbio na jasho
likamtiririka kiasi cha kutoonekana umuhimu wa kiyoyozi. Akaropoka kwa nguvu licha ya
kuwa alikuwa anawaza tu
"Ina maana“
*****
Baada ya moses kushindwa kuingia katika hoteli ya Raymond, kuna nafsi ikamsukuma kuelekea nyumbani kwake, Raymond. Ilikuwa ni kama alivyotarajia. Umati mkubwa wa watu wakizungumza kila jambo.
Alichokisikia katika vingi walivyovizungumza ni kile alichokijua.
Jambo lile lile la watu wawili kufa kwa hali ya kushangaza. Lakini sasa hawakuwa wawili tena, waliongezeka watu tisa. Ikamshangaza sana lakini hakupenda kustaajabu sana kwakuwa alifahamu ulikuwa ni uzembe wa mtu yeyote ambaye angekuwa hafahamu kuhusu hila zake. Akajitenga na watu ambao walionekana si aina yake. Watu ambao walionekana ni waswahili na wafupi wa elimu.
Akatazama huku na huko, akavutiwa na kikundi kimoja. Kikundi hicho kilikuwa na watu wa rika lake. Watu walioonekana wenye elimu pamoja na jambo alilokuwa akilidadisi, alikuwa na hakika wao wangekuwa na majibu yake.
Akakisogelea taratibu akajiunga nao.
Ulikuwa ni wakati wa simanzi, hivyo hakuna ambaye alijali ongezeko la mtu kati ya kikundi chao kilichobeba watu sita kabla ya Moses.
"Raymond amepatikana"
Kijana aliyeukaribia uzee, akasema kwa upambe. Mwingine na mwingine wakaendelea kudakia bila kuwa na hakika na chochote. Alichokuwa akikitafuta akawa amekipata. Mmoja kati ya wale waliokaa kwenye kikao akaropoka
"Kwani nyinyi hamfahamu biashara haramu anazozifanya Raymond?" Akanyamaza kwanza. Aliwakagua kila mmoja bila kujali ugeni wa Moses kati kati yao. "Inawezekana amewadhulumu wenzake ndio maana wanamlipizia"
Mwingine akadakia kwa udaku "Unachosema kinawezekana" huyu aliyekuwa anaongea akainama kabisa "walianza kwa mtoto wake Bertha huko kijitonyama sasa wanaendeleza mauaji zaidi"
Kabla hajamaliza kuzungumza, yule ambaye Moses alimkuta akiongea akakohoa.
Moses akamtazama kama wengine walivyokuwa wamefanya. Akamkuta naye akimtazama. Yule kijana aliyetawaliwa na ufukara na shida aliyekonda kwa mawazo, akauliza
"Sijuhi wewe ni nani mwenzetu?"
Alikuwa akimuuliza Moses. Moses akajichekelesha pale bila kujibu chochote. Alipoona wote wakimtazama, akapata la kuongea
"Mimi ni mgeni katika mtaa huu ila nimeshitushwa na habari za vifo vya watu hawa" aliwatazama watu wale na kuonyesha waliridhika na majibu yake. Akamalizia "mnisamehe kama nimeingilia mkutano wenu"
Yule ambaye alikuwa kama kiongozi katikati yao, akamsimamisha Moses mara alipokuwa akigeuka na kutaka kuondoka "Hapana usiondoke" Moses akasimama na kurudi miongoni mwao "tusamehe bwana, unajua hizi habari ni nyeti sana hivyo nilishitushwa na sura yako kwa kuwa wewe ni mgeni katikati yetu"
"Hamna .."
Kabla Moses hajamaliza kuongea, akaiona gari ya Raymond. Akabaki akiwa ameduwaa kuitazama. Kwa nyuma ilikuwa inafuatwa na gari ya Jafari Hiza. Hakufahamu kama ndani yake alikuwepo pia Vannesa. Wote kati yao wakawa wanashangaa alichokuwa akikitazama Moses. Wakaliona gari ya Raymond. Kila mmoja alianza kuaga na mwisho Moses alijikuta amesimama peke yake.
Ni wakati huo alipomuona Vannesa akishuka na Jafari Hiza kutoka ndani ya gari ya jafari. Alipoendelea kutazama kwa muda wa dakika ishirini zaidi, aliyaona macho ya Vannesa yakimtazama. Alishuhudia mshangao juu ya macho hayo ya Vannesa. Lakini alijizugisha pale na kujiingiza kati kati ya vikundi vya watu kumkimbia Vannesa. Alipotazama kwa mbali akiwa ameuacha mtaa wa Raymond, alimuona Vannesa akihangaika kumtafuta.
Akacheka kwa kuuzika na kujisemea moyoni
"Hutaniona tena Vannesa"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akatokomea anapopajua.
*****
Vannesa akiwa ameachana na Raymond mawazo juu ya Moses yakazidi kumuumiza nafsi yake. Alijiuliza ni vipi Raymond atamke kuwa Moses amefariki. Moses huyu aliyelala naye chumba kimoja? Kitanda kimoja? Akaoga naye bafu moja? Hapana kuna namna juu ya jambo hilo. Akaamua kumpigia simu.
".. Haipatikani"
ilikuwa ni sauti ya mashine kutoka katika mtandao aliokuwa akitumia Moses.
'Kwanini amezima simu? Ni yeye kweli niliyemuona nyumbani kwa Raymond'
Akajiambia mara baada ya kuingia ndani ya gari yake aliyoiacha kazini.
Wakati huo Naima alikuwa tayari ameshatoka kazini. Kichwa chake kikawaza kwenda hoteli aliyokuwa akilala na Moses. Hakutumia muda mrefu mpaka kuifikia hoteli ya Caribean. Alienda moja kwa moja mpaka chumbani. Kitasa kikawa kigumu kufungua mlango. Akagonga hodi bado ukimya ukatawala. Aliamua kushuka mpaka chini kwenda kuuliza mapokezi kama mteja wao ambaye ni Moses amekwisharudi hadi wakati huo. Msichana wa mapokezi akajibu
"Ndiyo na amerudisha chumba tayari"
"Amerudisha chumba? Hajaacha ujumbe wowote?" Alikuwa akiuliza huku akijipekua pekua kuitafuta simu yake. Yule muhudumu wa mapokezi akatoa bahasha fulani ya rangi ya kaki. "Ameniachia bahasha hii hapa"
Vannesa aliiacha simu ile na kufungua bahasha hiyo kwa shahuku kubwa. Alitamani kufahamu nini kipo ndani ya bahasaha. Alipoupenyeza mkono wake ndani ya bahasha, akagusa vitu viwili. Vyote vilionekana ni kama karatasi.
Kitu alichodhani ni Karatasi kikadondoka.
Nyingine ilikuwa ni karatasi aliyoishika mkononi mwake. Hicho kitu kingine kilichodondoka, kilikuwa ni picha. Picha ambayo alikutana nayo kama ushahidi kwa watu waliokutwa wamekufa. Picha iliyopigwa na mtu aliyejitambulisha kama kivuli cheusi. Picha iliyopiga kivuli cha mtu ambacho ni cheusi. Aliishika bila kuamini kama ni ujumbe alioupata kutoka kwa Moses. Akaitoa karatasi ile iliyo mkononi mwake na kuikunjua kusoma kilichoandikwa ndani ya barua hiyo
Barua hiyo iliandikwa na Moses mwenyewe.
Ilisomeka hivi "Pole sana Vannesa kwa siku zote kukulaghai na kukufanya uniamini kuwa nilikupenda. Katika maisha yangu sikuwahi kumpenda msichana wala sijuhi nini kuhusu mapenzi. Mimi ni muuaji. Mimi ni mwanaume hatari ambaye unahangaika kunitafuta usiku na mchana. Dhumuni la ujumbe huu mdogo, ni kukujuza kuwa nitasitisha kusimamisha uhai wa watu wasio na hatia mpaka nitakapopata nafasi huru ya kuzungumza na Raymond. Na ihitaji roho yake endapo hatonieleza ukweli juu ya ninachokitafuta kwake." Akahitimisha ujumbe wake huo kwa kumwambia "wako umpendaye Kivuli cheusi"
Pumzi za Vannesa zikaongezeka, Kifua kilipanda na kushuka huku asiamini alichokuwa akikisoma. Bila kutarajia machozi yakamtoka. Uchungu ulimshika sana. Donge zito likaikamata koo yake alipojaribu kutaka kunyanyuka akahisi uzito.
Kiukweli nguvu zilimuishia. Hakuamini kama alikuwa akilala kitanda kimoja na muuaji. Hakujua kama aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba ndiye aliyekuwa akimwambia anampenda kila siku. Alikaa kwa muda mrefu bila kuchukua hatua yeyote, simu yake ndani ya mkoba ikapata uhai.
Juu ya kioo alikuwa Jafari Hiza.
"Vipi Vannesa"
Jafari Hiza alitamani jioni hiyo kukutana na Vannesa. Tamaa ya mapenzi ilimuwaka kiasi cha kushindwa kuvumilia. Alimuhitaji sana Vannesa. Akazungumza kwa mahaba ndani ya chombo cha simu.
"Unasemaje Jafari?".
Vannesa akaitika kivivu kama aliyetoka kusinzia.
"Ha!! Vannesa umeshalala mara hii?"
"Hapana"
"Okey!! sasa tunaweza kukutana sasa hivi?"
"Sipo sawa lakini ni muhimu mimi na wewe tukutane"
Hakuelewa nini alimaanisha Vannesa lakini tamaa ikazidi kumsukuma kuamini kuwa Vannesa pia alikuwa akimpenda. Hakujua kilichomkuta Vannesa kwa wakati huo.
Vannesa na Jafari Hiza wakapanga wakutane katika bar ya Caribean. Ilikuwa ni night club. Vannesa hakupata shida kwenda mbali kwa kuwa ilikuwa ni hatua chache kutoka ulipo mlango wa kuingia katia vyumba vya kulala. Bar hiyo ilikuwa ghorofa ya pili. Hakutaka kutumia ngazi kutokana na uchovu uliomkamata ukichanganya hasira zilizomjia juu ya Moses. Mwanaume aliyeamini ndiye mwanaume atakayeziba pengo la Amani. Amani aliyemsaliti na kutembea na rafiki yake Martha. Akamuona Moses mwanaume anayefaa kuwa mume wake kabisa.
Akaziendea lifti na kubonyeza kitufe cha namba mbili. Akajisogeza katika moja ya viti vilivyo pembezoni kabisa lakini mwanga ulimmulika. Aliutazama mlango huku bado machozi yakimtoka. Akakumbuka siku ya kwanza alipomuona Moses eneo hilo.
Akaijutia sana siku ile.
Siku ile ya kwanza kuingia ndani ya bar hiyo. Pombe zikamfanya kuangukia kwa Moses. Muuaji aliyeondokea kumchukia lakini kiuhalisia alimpenda sana. Aliitafuta chuki moyoni mwake juu ya Moses, lakini haikuepo.
Alimpenda sana Moses.
Licha ya kugundua Moses ni muuaji, bado alimpenda. Ubaya wa Moses ukajitenga mbali na mapenzi yake moyoni. Lakini usoni alionesha chuki za wazi na aliona ni sahihi kumchukia. Mara akajiuliza atamwambia nini Jafari hata akija? Akiwa katika kuwaza huko, alimuona Jafari akiingia. Jafari alipokuwa akiingia, aliiweka simu sikioni mwake akimpigia Vannesa.
"Nimeshakuona.."
Vannesa akamuelekeza wapi alipokaa, Wakaonana. Jafari Hiza alishangaa sana kumuona Vannesa akidondosha machozi, Akauliza kwa huba
"Vipi Vannesa, una matatizo gani?"
Huku akimpapasa papasa mikononi. Bado vannesa akaendelea kulia alilia akalia wala hakunyamaza. Mwisho Jafari Hiza alipofanikiwa kumnyamazisha Vannesa akaiweka picha yenye kivuli cheusi mezani walipokaa.
"Nini hiki?"
Jafari hiza akauliza kama hakuitambua picha hiyo. Ilikuwa ni picha moja iliyoonekana kila sehemu iliyotokea mauaji. Vannesa akajibu kwa kughadhibika
"Kwani huifahamu picha hiyo?"
"Ina maana kuna mauaji yametokea?"
"Ni heri yangetokea kuliko kilichonipata"
Vannesa hakuona sababu ya kuficha kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Akamuhadithia kila kitu Jafari tangu mwanzo walipokutana katika bar hiyo ya carribean. Habari hiyo ikawa mbaya sana kwa Jafari Hiza. Ile tamaa yake kwa Vannesa ikakatika mara baada ya kusikia kuwa Vannesa alikuwa na mahusiano na muuaji wanayemtafuta.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hisia fulani zikaingia moyoni mwake.
Hisia mbaya za kudhani huenda Vannesa ana husika katika kumrahisishia muuaji kukimbia mitego yao ya kumkamata.
Akaondoka bila kumuaga Vannesa.
******
Baada ya kuandika ujumbe ule na kuiacha picha ile, Moses akiwa anatoka nje ya hotel hiyo; aliiona gari ya Vannesa. Hakutaka kukutana na Vannesa tena, lakini hakutaka kumuua pia. Mapenzi aliyo nayo kwa Vannesa aliamini ipo siku atakuja kuwa nae tena. Licha ya kumwambia ukweli juu mauaji aliyokuwa akiyafanya, lakini aliamini yeye ni binadamu na ipo siku atamsamehe.
Aliamini hivyo ndio maana akawaza tena. Aliwaza kuwa ni vizuri kuendelea kumfuatilia Vannesa kila siku bila kukutana naye. Alitaka kujua Vannesa anafanya nini na anakutana na nani kwa siku. Kazi hiyo aliianza mara baada ya kujificha na kumtazama Vannesa alipokuwa akiingia kuelekea chumbani. Mara alimuona akirudi mapokezi. Moses alitumia gazeti pana kuficha uso wake.
Vannesa hakumuona.
Alimtazama mpaka alipokuwa akiisoma barua yake. Aliyaona machozi machoni mwa Vannesa. Akatamani kumfuata amwambie ni kiasi gani anampenda, ila hakujua maana ya machozi yale. Akaendelea kumfuatilia kila alichokuwa akikifanya.
Alimuona akiipokea simu.
Hakusimama hata alipomuona akiingia ndani ya lifti, alijua wapi alipokuwa anaenda. Akafungua mkoba wake aina ya briefcase, akayaona mavazi yake ya kizee. Ndevu nyingi zilizochoka. Akacheka kimoyomoyo.
Alielekea chooni kubadilisha muonekano wake.
Dakika tano zikawa nyingi akarudi eneo lile la mapokezi. Wakati ambao sasa anarudi pale alipokaa mwanzo, ndipo akagongana na mtu. Mtu yule alikomaa sana, kiasi cha kikumbo hicho kumdondosha mpaka sakafuni. Alipouinua uso wake huku akiugulia maumivu, alimuona mtu huyo. Mtu huyo hakuwa mwingine bali ni Jafari Hiza. Jafari Hiza hakumtambua Moses kwa kuwa hakuijua hata taswira ya muuaji. Akamuinua Moses huku akimuomba radhi kwa heshima kama mzee mwingine. Moses akajua fika Jafari alikuwa akielekea kwa Vannesa. Akamfuatilia alipokuwa anaenda.
Ni katika bar ile ile aliyokutana na Vannesa kwa mara ya kwanza. Jafari Hiza alikuwa mbele Moses nyuma kwa mwendo wa tahadhari. Moses aliziacha meza tano toka alipokaa Jafari Hiza na Vannesa. Huko baada ya muda akaona hali si shwari. Aliona Vannesa akimpatia Jafari Hiza picha ile ya kivuli cheusi. Ghafla Jafari aliondoka bila kuagana kwa heri.
"Kuna tatizo"
Kuna nafsi ikamnong'oneza. Jafari Hiza akampita pale pale alipokaa na kuondoka zake. Alipomuona Vannesa akiwa peke yake, hakuona si tatizo akimuacha na kumfuatilia Jafari Hiza. Alipanga kumfanyia kitu mbaya. Moyoni akajiambia
"Bila kumuua Jafari Hiza atamghiribu Vannesa "
*****
Baada Jafari Hiza kuondoka, Vannesa naye hakuona umuhimu wa kubaki tena; naye akaondoka. Aliamua kurudi nyumbani kwake na kukiacha chumba kilichokuwa kikimkumbusha kumbukumbu mbalimbali za Moses. Alikumbuka kipindi ambacho alikuwa akishikana na moses kila sehemu ya mwili.
Akilikumbuka tabasamu la Moses, chozi likamdondoka tena. Akatoka kinyonge ndani ya hotel ya Carribean. Akaifuata gari yake iliyopo maeneo ya maegesho ya hotel hiyo. Aliufungua mlango na kunyonga ufunguo, injini ikaitika. Aliisogeza gari yake lakini hakuwa amekwenda mbali sana. Alikutana na foleni kubwa ya magari. Bila kujua tatizo lililopo mbele, akaipiga sterling ya gari kwa hasira na kuitusi foleni hiyo. Gari hazikusogea zaidi ya dakika kumi aliyokaa kwenye foleni hiyo. Alichoka kusubiri. Aliamua kushuka na kujaribu kwenda kutazama nini kilichosababisha foleni hiyo.
Aliopishana nao walikuwa wakisema "Huenda breki zilifeli" Wengine wakadai "Ni uzembe bwana, unaweza kukuta alikuwa amelewa si unajua wikiendi hizi" Umati mkubwa wa watu ulikuwa ukishangaa ajali mbaya aliyokutana nayo Vannesa. Ajali hiyo ilitokea katika makutano ya kuiunganisha barabara ya kuelekea mwananyamala na ileile ya Jomo kenyata. Eneo lililoitwa studio. Gari ndogo iliyopondwa vibaya vioo kudondoka chini na kuwa kama unga ndio picha halisi iliyomvuta Vannesa kuzubaa kama mashuhuda wengine.
Akataka kuondoka ageuze gari apite njia nyingine, lakini kuna kitu kikamfanya asite. Kitu hicho ni aina ya gari hiyo iliyokanyagwa vibaya na Kontena lililodondoka kutoka katika gari yake. Gari hiyo aliifahamu vizuri, alikwishaipanda mara nyingi na aliizoea kuiona mara kwa mara. Akaropoka kwa nguvu "Mungu wangu"
Mara kikafuata kilio.
Ilikuwa ni gari ya Jafari Hiza. Jafari aliyeachana naye muda mchache uliopita. Akaanza kujilaumu kwa kukutana na Jafari. Alianza kudhani kuwa chanzo cha ajali hiyo huenda ni yeye kasababisha. Alikumbuka vizuri kuwa Jafari aliondoka akiwa na hasira, hakumuaga hata yeye mwenyewe.
Akalia kwa uchungu.
Akiwa katika kulia huko, alishuhudia baadhi ya vijana waliojitolea wakijaribu kuuvuta mwili wa mtu kutoka ndani ya gari iliyoangukiwa na kontena. Kontena lililodondoka baada ya gari hiyo kuigonga gari ya kontena na kusababisha ajali hiyo.
Vannesa alisogea mpaka karibu na mwili ule, alikuwa ni Jafari Hiza kweli. Alikuwa bado anapumua, hata wengi wa mashuhuda waliomtoa walimuona kuwa anapumua.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tumuahishe hospitali"
Wenye mioyo ya huruma wakaropoka huku wakishika nafsi zao. Jafari Hiza akawa amemuona Vannesa akajitahidi kutoa sauti huku damu nyingi zikimtoka mdomoni
"Nakufa Vannesa. Gari yangu ilifeli breki wakati..." Hakuimalizia sauti yake, akawa amelala ghafla. Macho yalikuwa yakimtazama Vannesa, moyo ukiwa umeacha mwili. Alikufa kistaarabu, kifo kilichohudhunisha.
Jafari Hiza akapelekwa hospitali kwa msaada wa msamaria aliyejitolea gari yake. Vannesa alipiga simu katika ofisi za Jafari Hiza na kutoa taarifa huku akiomba gari yake kuchunguzwa zaidi.
Alirudi katika gari yake na kuigeuza kuelekea nyumbani kwake. Alipoondoka Vannesa nyuma alifuatwa na gari ndogo ya Moses. Moses aliyekuwa hapo muda wote katika taswira yake ile ile ya uzee, Alimuona Vannesa wakati akiuacha umati wa watu nyuma na yeye kuupokea mwili wa Jafari Hiza. Alichukizwa sana na kitendo cha Jafari kutoka mzima na kuamini kuna kitu ambacho jafari Hiza alimwambia Vannesa, akaamua amfuatilie Vannesa ili apajue anapoishi kwanza.
****
****ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment