Simulizi : Kwa Udi Na Uvumba
Sehemu Ya Tatu (3)
***** ***** ***** *****
INSPEKTA Materu alikunja uso kidogo na kuguna. “Haiwezekani,” hatimaye alisema. “Taarifa nyingine toka Kibaha ndiyo inayonipa picha kuwa watu hao hawakuelekea mbele ya Kibaha; wamerudi huku.”
“Taarifa gani?”
“Kuwa gari lililotumiwa na majambazi hao limetelekezwa kiasi cha kama kilometa kumi hivi toka Maili Moja kama unakuja huku.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitowela alitikisa kichwa akiashiria kutoyaafiki maneno ya Materu. Kisha: “ Kutelekezwa kwa gari hilo siyo sababu ya kutufanya tuamini kuwa wamekuja huku. Kwani hawawezi wakafanya kama wanakuja huku halafu wakalitelekeza gari hapo kisha wakadandia gari jingine, wakapita Kibaha palepale na kutokomea kusikojulikana?”
“Wanaweza. Lakini jambo hilo litafanikiwa kama askari wa Kibaha watakuwa wamelewa chakari!”
“Afande, una maana kuwa askari wa Kibaha watakuwa wamejizatiti katika doria kuhusu ishu hii?” Kitowela alimkazia macho.
“Kwa vyovyote lazima iwe hivyo,” Inspekta Materu alijibu kwa msisitizo mkali. “Mzee Kibangu anastaafu mwishoni mwa mwaka huu. Hatapenda kuacha kazi huku akiwa na doa la uzeeni hususan katika kipindi hiki cha ARI MPYA, KASI MPYA NA NGUVU MPYA. Atataka kuondoka akiacha sifa kedekede na ikiwezekana apewe nishani ya Askari Bora na Shupavu wa Jeshi la Polisi barani Afrika.”
Kichwani mwa Kitowela, maneno hayo yalikuwa na maana mbili; ukweli na masikhara. Lakini, zaidi aliamini kuwa masikhara hayana nafasi kwa kipindi hicho. Akacheka kidogo kisha akasema, “Kuna jambo ninalotaka kujua.”
“Lipi?” Materu akamkazia macho.
“Unadhani hilo gari lililotelekezwa ndilo lililokodiwa toka huku na hatimaye dereva wake kutupwa kando ya barabara huko Kibamba?”
“Inaweza kuwa hivyo. Mara nyingi mhalifu huwa hayuko tayari kutumia gari lake katika uhalifu hata kama analo. Na inaonyesha kuwa yule dereva siye mmiliki wa gari. Mlangoni kuna jina la Maftah Mohammed.”
Kitowela aliachia kicheko kikali kisha akahoji, “Afande, una maana kuwa unawafahamu hao wahusika?”
Kwa mara ya kwanza Inspekta Materu akajiona mjinga. Akajilaumu kwa kutoa jibu ambalo hata mwendawazimu angemshangaa. Ukweli ni kwamba hadi wakati huo yeye na Sajini Kitowela hawakuwafahamu wahusika wa mauaji yale.
Hata hivyo katika kuhakikisha kuwa heshima yake haiporomoki kutokana na kauli hiyo, akawahi kujisahihisha. “Siyo kwamba nawafahamu wahusika hao, bali kuna mazingira yanayoonyesha kwamba walikuwa wameliteka gari lile,” alisema.
“Mazingira gani?”
“Kitambulisho,” Inspekta alijibu. “Kitambulisho cha maiti iliyokutwa kando ya barabara. Kwenye mifuko ya suruali ya marehemu kulikuwa na kitambulisho chenye picha na jina lake. Aliitwa Andrew Kessy. Na kulikuwa na leseni ya udereva ya class C.”
Kitowela aliguna. “Afande, nadhani bado tuko mbali katika suala hili,” hatimaye alisema na kuongeza, “maiti ya huyo Andrew Kessy imekutwa Kibamba, na gari limekutwa maeneo ya Kibaha. Kwa nini tuamini kuwa marehemu Andrew ana uhusiano wowote na gari hilo? Isitoshe, magari meupe aina ya Toyota Mark 11 au Chaser ni mengi sana. Siuoni ulazima wa kuamini kuwa gari lililokutwa limetelekezwa pale Kibaha ndilo lililotekwa Kibamba. Na kwani kuna mtu yeyote aliyekuja kuripoti kuwa kapotelewa na gari?”
“Kwa swali lako la kwanza, naona ni kweli kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina kupata ukweli,” Materu alijibu. “Kwa swali la pili, ni mapema mno kumpata mlalamikaji wa kupotelewa gari. Hazijapita hata saa sita tangu mambo haya yatokee. Madereva wengi huwasiliana na matajiri wao usiku baada ya kufunga kazi na wengine huonana nao hata baada ya wiki. Kwa hali hiyo, kama marehemu alikuwa amekabidhiwa tu gari ili azungushe mchana kutwa na jioni alipeleke kwa tajiri, basi huyo tajiri mwenyewe bado hajajua kinachoendelea.”
Ukimya ulitawala kwa muda mfupi. Kisha Sajini Kitowela alishusha pumzi ndefu. “Ipo kazi,” alisema huku kakunja uso.
“Si uongo,” Materu aliungana naye. “Na kazi yenyewe si mchezo, ni nzito kupindukia. Kuwasaka watu msiowajua sura wala majina. Tunatafuta sindano katikati ya giza nene.”
************
MWEZI MMOJA BAADAYE
DHAMIRA ya Panja alikuwa palepale; kumsaka Kipanga kwa udi na uvumba, kazi aliyoamini kuwa lazima ingefanikiwa. Ndiyo, aliamini kuwa lazima angefanikiwa kumpata, japo hakuyajua matokeo ya kukutana naye.
Hata hivyo, kuhusu hilo hakupenda kukisumbua kichwa chake kulifikiria. Hii ilikuwa ni siku ya thelathini na tatu baada ya kuzidiwa kete na Kipanga. Na tangu aliporudi nyumbani hakuthubutu kutembea mitaani mara kwa mara nyakati za mchana kwa kuhofia kukamatwa.
Asubuhi hii, akiwa kitandani, alijaribu kupanga hili na lile katika kutekeleza kazi ya kumsaka Kipanga. Takriban kila alilolifikiria aliuona ugumu katika kulitekeleza. Hatimaye akaanza kukata tamaa. Na alikuwa na sababu ya kuanza kukata tamaa.
Jiji la Dar es Salaam ni kubwa na lina zaidi ya wakazi milioni tano. Ilikuwa ni ndoto ya mwendawazimu kujenga imani ya mafanikio ya kumpata Kipanga kwa kupita hapa na pale, kitongoji hiki na kile, uchochoro huu na ule, gesti hii na ile na hata baa moja hadi nyingine kwa matumaini ya kufanikisha lengo hilo.
Na alitambua fika kuwa, hata kama angetumia njia nyingine katika msako huo, bado angehitaji kutumia fedha zisizo haba. Isitoshe, alijua kuwa Kipanga ana bastola, hivyo hata kama wangekutana uso kwa uso, Kipanga asingehitaji kutumia hata dakika moja kuamua afanye nini kama angesumbuliwa tena kuhusu mgawo wa pato la Kibaha. Angemlipua!
Bastola aliyoachiwa na Kipanga haikuwa na risasi hata moja na kwa hali hiyo, haikuwa na faida yoyote kwake kwa kipindi hicho. Alihitaji risasi walao tatu tu ili ajione yu mkamilifu. Azipate wapi risasi hizo? Hili lilikuwa jambo jingine gumu, jambo lililompasa kukisumbua tena kichwa katika kulipatia ufumbuzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hata hivyo, kama aliyeoteshwa ndoto, wazo likamjia, wazo ambalo aliamini kuwa ni la kumtatulia tatizo hilo la upatikanaji wa risasi. Alimkumbuka mtu mmoja, askari wa Jeshi la Wananchi, aliyeitwa Masumbuko Kambi. Masumbuko alikuwa katika kambi moja kubwa jijini Dar es Salaam akiwa ni mtunza silaha.
Askari huyo alikuwa ni mtu wa matumizi makubwa na ya kifahari. Hakuwa radhi kuwa na upungufu wa pesa za starehe. Alizipenda bia, aliwapenda wanawake. Kila jioni alipotoka kazini, aliripoti nyumbani na kuyavua magwanda ya kazi kisha akatinga nguo za ‘kutokea’ na kwenda katika baa maarufu zenye wateja wa kike ambao walikuwa tayari kwa yeyote na kwa wakati wote. Gari lake dogo aina ya Toyota lilikuwa likimrahisishia kazi ya kufika popote alipotaka kwenda.
Lakini ili azipate bia kila alipozihitaji, na kuwanasa wanawake wa aina yoyote na kwa wakati wowote, alilazimika kutumia pesa zisizo haba, tena za ziada; siyo mshahara halali anaoutumikia kwa mwezi mzima! Alikuwa na mke mmoja na watoto watatu, wakiishi katika nyumba ya kupanga huko Mwenge. Je, kwa kutegemea mshahara huo angeweza kuihudumia familia yake mahitaji yote muhimu sanjari na kutanua mitaani kwa kugida bia na kubeba vimwana?
Isingewezekana. Hivyo alitumia mbinu zake za siri ili aweze kupata pesa za kutanulia mitaani. Kuuza risasi kwa siri kubwa na kupata pesa za harakaharaka, ilikuwa ni mbinu pekee iliyomrahisishia upatikanaji wa pesa, asilimia kubwa ya wateja wake wakiwa ni majambazi.
Panja alikumbuka kuwa siku moja aliwahi kwenda na Kipanga kwa Masumbuko na wakapata risasi kumi baada ya Kipanga kuongea naye faragha.
Kipanga na Masumbuko walifahamiana sana, tofauti na Panja ambaye japo siku ile walionana lakini hawakuwa na ukaribu kibiashara. Lakini hilo hakuliona kuwa ni kikwazo. Aliamini kuwa mbele ya pesa Masumbuko hatakuwa na kipingamizi chochote.
Ndipo alipokurupuka kitandani na kujifunga taulo kiunoni kisha akatwaa sabuni tayari kwenda bafuni.
Hilda aliyekuwa bado kitandani, alimtazama kwa mshangao na kumuuliza, “Wewe vipi?”
“Poa tu,” Panja alimjibu bila ya kumtazama.
“Imekuwaje? Mbona unakurupuka mapema ivo?”
“Nakwenda kuoga.”
“Njoo kwanza…”
Panja hakutii wito huo. Alijua alichoitiwa. Ni kilekile walichokwishafanya kabla ya alfajiri. Na kwa kawaida walikuwa na tabia ya kuikaribisha siku kwa kukifanya kitu hichohicho muda mfupi kabla ya kukiacha kitanda. Hata hivyo, hiyo ilikuwa ni kawaida, haikuwa sheria, kwa hali hiyo Panja aliendelea na safari yake ya bafuni.
Alipomaliza kuoga alivaa harakaharaka na kisha akaifungua saraka ya kabati ambako alihifadhi akiba ya pesa zake alizopata kutokana na kazi walizofanya na Kipanga siku chache zilizopita. Alipozihesabu akagundua kuwa mambo yanazidi kuwa mabaya. Akiba pekee iliyokuwamo zilikuwa ni shilingi 250,000 tu.
Hazikuwa ni pesa za kujivunia hata kidogo, ni wazi zingeteketea siku chache zijazo. Na ni katika akiba hiyohiyo alipaswa kutoa fungu la kwenda kumpa Masumbuko ili aweze kupata walao risasi tatu!
Hata hivyo, hakujali kupungua kwa kiwango hicho, alijali kupata risasi. Hivyo, bila ya kuwaza zaidi alichomoa noti zenye thamani ya shilingi 60,000 na kuzipachika mfukoni. Akamtupia macho Hilda ambaye bado alikuwa amejilaza kitandani kihasarahasara.
“Natoka kidogo,” alimwambia. “Kuna tatizo lolote? Naweza kuchelewa kurudi.”
Hilda alijinyonganyonga, akijifunika shuka vizuri kisha akatupa swali, “Kwani unatarajia kurudi saa ngapi?”
“Haitakuwa kabla ya saa sita.”
“Hujaniachia pesa ya kulipia umeme.”
“Shi’ngapi?”
“Elfu tano.”
“Chukua elfu kumi kwenye droo. Jingine?”
“Hakuna.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwanamume alitoka. Saa 1.45 alikuwa akiteremka kwenye daladala katika kituo cha Mwenge. Akachepuka mtaa huu na ule hatimaye akafika kwa Masumbuko Kambi. Wakazungumza kibiashara, mazungumzo ambayo japo yalikumbana na kipingamizi kutoka kwa Masumbuko hata hivyo mwafaka ulipatikana.
Awali Masumbuko alitaka malipo ya shilingi 20,000 kwa risasi moja, lakini Panja alimbembeleza hadi akakubali kuchukua 50,000 kwa risasi tatu.
“Nimekufanyia hivyo tu kwa kuwa uko na msh’kaji wangu, Kipanga,” Masumbuko alisema. Kisha kama aliyekumbuka kitu, akamuuliza, “Kwani leo umemwacha wapi?”
“Hayupo hapa Dar,” Panja aliongopa. “ Kaenda mikoani. Labda atarudi baada ya wiki moja, hivi.”
Panja hakuwa tayari kugusia mkasa kati yake na Kipanga hata kidogo. Alitaka iwe siri, zaidi aliyejua ni Hilda tu! Nani mwingine ajue? Na kwa nini awepo mwingine wa kujua?
Alitoka hapo huku moyo wake ukiwa umesuuzika. Sasa alijiona kapiga hatua moja mbele katika mafanikio ya utekelezaji wa mpango wake. Hakupanda tena daladala, badala yake alikodi teksi ya kumrudisha nyumbani, Kinondoni.
Akiwa njiani alinunua magazeti mawili, moja lililoitwa KIMBEMBE likiwa na habari za udaku huku jingine, HAMASA likiwa ni katika daraja la yale yanayoitwa magazeti makini.
Akiwa ameketi kwa utulivu ndani ya teksi hiyo, kushoto mwa dereva, Panja alianza kupitia vichwa vya habari vya magazeti hayo harakaharaka na kujikuta akivutwa na kichwa cha habari katika gazeti la KIMBEMBE kilichochukua uzito wa juu katika ukurasa wa mbele; ‘BILIONEA’ AGOMBANIWA NA WANAWAKE UBUNGO.
Mara nyingi aliyapenda magazeti ya udaku kwa kuandika habari za ajabu-ajabu mathalani matukio ya fumanizi kwa wanandoa na matukio ya burudani za dansi, bongo fleva na taarabu.
Akaamua kuisoma habari hiyo ya ‘BILIONEA’kwa undani kabla ya kuendelea na nyingine.
Ilikuwa ni habari iliyosema kuwa mtu mmoja ambaye amepanga chumba katika ‘gesti bubu’ iliyoko eneo la Ubungo amekuwa akisababisha wanawake wapigane kwa ajili yake katika kile kilichoaminika kuwa ni kugombea penzi.
Ilidaiwa kuwa mtu huyo alikuwa na siku takriban thelathini tangu aingie ndani ya gesti hiyo na alionekana kuwa ana pesa lukuki kutokana matumizi yake makali yaliyohusisha unywaji pombe na uhongaji wa pesa nyingi kwa wanawake.
Mtu huyo alikuwa na desturi ya kutotembea-tembea mitaani na kama alitoka ndani ya gesti hiyo basi hakwenda zaidi ya mita hamsini kununua magazeti. Pia katika matumizi yake hayo ya kutisha, ‘bilionea’ huyo alidaiwa kuwa alikuwa akijichimbia chumbani na kugida bia na kuku kadhaa wa kuoka na nyama ya mbuzi huku akiwa na wanawake wawili, watatu hata wanne ambao mitaani hujulikana bayana kuwa ni watu walio tayari kwa mwanamume yeyote na kwa kutendwa vyovyote kulingana na uwezo wa kiuchumi alionao mwanamume husika.
Kilichomshangaza zaidi Panja ni kiwango cha shilingi 50,000 hadi 100,000 zilizodaiwa katika habari hiyo kuwa ndicho kiwango alichotoa kwa kila mwanamke aliyebahatika kuingia chumbani humo na kumtuliza kiu yake.
Ilikuwa ni habari iliyomshangaza na kumsisimua Panja kwa kiasi kikubwa. Akayainua macho na kutazama mbele, kisha akamgeukia dereva na kusema, “Kuna watu wanaojua kula raha hapa duniani. Wameiweka dunia mikononi mwao.”
Dereva aliachia tabasamu dhaifu bila ya kumtazama Panja. Kisha akahoji, “Kwa nini unasema hivyo? Au umesoma hiyo habari ya kwenye gazeti la KIMBEMBE? ”
“Nd’o maana’ake,” Panja alijibu. “Ukisikia mafisadi, basi huyu ni mmojawao. Mtu huwezi kutumia pesa kwa mfumo huu kama kweli una uchungu nazo. Au vinginevyo, tuchukulie kuwa stori hii ni ya kutengenezwa kibiashara ili gazeti linunulike.”
“Hapana!” dereva alipinga haraka. “Hiyo stori ni ya kweli! Ni ukweli mtupu! Hata mimi namjua huyo jamaa. Majuzi nilimpeleka mteja mmoja kwenye gesti hiyo, nd’o nikasikia watu wakimzungumzia huyo ‘bilionea.’ Kwa bahati, kabla sijaondoka jamaa alitoka nje na kwenda kununua gazeti. Ndipo msh’kaji mmoja akanitonya.
“Sikuweza kuimaki sura yake kwa kuwa alikuwa amevaa miwani mieusi, na hata hivyo sikuwa na haja ya kumjua. Yaani pale kila mtu anamzungumzia. Sijui kazichota wapi pesa za kutupa kiasi kile. Unaweza kukuta ni jambazi au fisadi , nd’o maana kajichimbia gesti muda wote baada ya dili lake kuwini.”
Sentensi hiyo ya mwisho ilimpeleka Panja mbali kimawazo. Akamtazama dereva huyo kwa macho makali. “Unamfahamu?” hatimaye alimuuliza.
“S’o kwamba namfahamu, nilimwona tu pale kwenye gesti. Kwan’vipi?”
“N’na shida naye,” Panja alijibu kwa utulivu.
“Una shida naye?” dereva alishangaa. “Kwani unamjua huyo jamaa mwenyewe?”
“Sina uhakika, lakini nadhani ni huyohuyo anayezungumziwa. Jamaa mwenyewe si ni mrefu?”
“Ndiyo.”
“Pandikizi la mtu?”
“Hivyohivyo! Amekaa kibaunsa-baunsa.”
“Kidevuni yukoje? Ana sharafa?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Anaonyesha hivyo, lakini siku nilipomwona hakuwa na ndevu.”
“Una siku ngapi tangu ufike pale?”
“Haijapita hata wiki. Kama siku nne, tano hivi.”
“Kichwani yuko vipi?” Panja aliendelea kudadisi.
“Ki-vipi?”
“Ana nywele au hana?”
“Ana mzinga wa para, mwanangu.”
“Macho yake?”
“Ningeyaonaje wakati nimekwambia alikuwa katinga miwani ya giza?” dereva naye alihoji huku akibadili gia na kupunguza mwendo. Walikuwa wamekaribia kwenye taa za Usalama Barabarani makutano ya barabara za Rashid Kawawa na Ali Hassan Mwinyi.
“Wakati anatembea ulimwangalia vizuri?”
Dereva aliitika kwa kutikisa kichwa.
“Uliicheki tembea yake?”
Taa ya kuwaruhusu iliwaka. Dereva hakulijibu swali la Panja, akili ilizama barabarani. Wakashika Barabara ya Rashid Kawawa. Mbele kidogo ndipo dereva akaipata sauti yake: “U
meulizia tembea yake, sio?”
“Yeah.”
“Anatembea kibabe-babe.Yaani anaonyesha kujiamini sana, kama unavyojua, mtu akiwa na tuvijisenti kidogo, basi anajiona kaibeba dunia mikononi mwake. Wengine huwa hawajui kama kuna suala la kufa duniani.”
Uso wa Panja ulichanua tabasamu kubwa, tabasamu lililofuatiwa na tamko la chini sana: “Ni mwenyewe.”
Ikawa ni kauli iliyomfanya dereva ajenge imani kuwa kuna kazi nyingine ya kumpeleka Panja huko Ubungo. Papohapo akamuuliza, “Vipi, twende Ubungo, mzee?”
Panja alifikiri kidogo kisha akasema, “No. Twende kwanza nyumbani. Suala la Ubungo halikuwa kwenye programu. Limezuka-zuka tu. Kama tutakwenda, basi hilo nitalijua baada ya kufika kwanza home.”
Dakika chache baadaye dereva aliegesha gari kando ya nyumba moja chakavu, jirani na Kanisa la Kilutheri, Usharika wa Kinondoni.
“Subiri,” Panja alimwambia dereva huku akiteremka na kufuata uchochoro uliomwingiza ndani zaidi ya eneo hilo. Alikuwa makini, hakutaka huyu dereva apajue kwake. Bado hakutaka kujiweka wazi kwa kila mtu na hasa kwa akiamini kuwa bado Polisi inamsaka.
Alitembea harakaharaka ili kufanya dereva asione kuwa anacheleweshwa. Dakika chache baadaye alikuwa ndani ya nyumba aliyoishi.
Huko ndani alimkuta Hilda akijishughulisha na usafi. Hakuhangaika naye, aliifuata ile saraka iliyohifadhi bastola, akaifungua. Bastola kubwa ya Kirusi G- Peacemaker -231 ikajaa kiganjani! Haraka akaifungua na kupachika zile risasi tatu alizozinunua Mwenge, kisha akatwaa shilingi 30,000 katika ile akiba yake.
Alipojitazama kidogo akajiona hayuko kamili. Akavua hii suruali nyeusi ya kitambaa chepesi na hili shati la miraba yenye mchanganyiko wa rangi nyeusi na nyeupe, badala yake akatinga suruali pana ya ‘cadet’, yenye mifuko mingi na mikubwa, shati pana na kofia ya Parma kichwani.
Akajitazama kwenye kioo na kutabasamu kidogo, akiridhishwa na mabadiliko haya. Akaipachika bastola katika mmoja wa mifuko ya suruali hiyo, mfuko ambao haikuwa rahisi kwa mtu asiyehusika kuweza kubaini chochote kuhusu silaha hiyo. Pesa zilitumbukizwa katika mfuko wa shati.
Akatoka huku akimwacha Hilda kaduwaa. Alipofika kwenye gari akafungua mlango na kuingia kisha akamtupia swali dereva: “Chaji yako ni kiasi gani?”
“Kutoka Mwenge mpaka hapa au mpaka Ubungo?”
“Mpaka Ubungo.”
Dereva alifikiri kidogo kisha akajibu kwa upole, “Tufanye arobaini tu.”
“Nitakupa thelathini.”
“Mafuta, mwanangu,” dereva alilalamika. “Mafuta yamepanda sana. Si unaona hata watu wa daladala wameshapandisha nauli zao?”
“Pamoja na hayo, tumalize biashara mimi na wewe, mambo ya daladala hayatuhusu! Mwishowe utaniambia na treni ya Mwakyembe imepandisha bei. We’ vipi msh’kaji wangu? Kama inashindikana, basi nipe chaji ya kutoka Mwenge hadi hapa, tuachane!”
Dereva alifikiri kidogo kisha akasema, “ Ok, twende.”
*************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
SAA 5 asubuhi, ndani ya chumba fulani, katika gesti –bubu eneo la Ubungo, Kipanga alikuwa ameketi kitandani huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa. Mbele yake, stuli tatu zilikuwa zimebeba chupa kadhaa za bia. Pale kitandani alipoketi, kulia kwake alipakana na mwanamke mweupe na mwenye mwili mkubwa ambaye pia, kama Kipanga, hakuwa na vazi lolote mwilini.
Macho ya mwanamke huyo yalionyesha wazi kuwa bado ‘hajatulia,’ na vituko alivyovifanya mwilini mwa Panja akihusisha mikono na kinywa, vilidhihirisha ni jinsi gani amekubuhu katika nyanja ya kuhudumia wanaume faragha.
Upande wa kushoto kulikuwa na mwanamke mwingine, huyo pia akiwa na ujazo wa minyama katika baadhi ya maeneo ya mwili wake, ujazo ulioweza kuyavuta macho ya mkware yeyote pale alipopita mitaani akitembea kwa madaha. Huyu pia alikuwa mtupu kama alivyozaliwa!
Wanawake hao waliingia humo chumbani asubuhi ya siku hiyohiyo baada ya kujipitisha-pitisha nje ya gesti hiyo kwa lengo la kumnasa Kipanga.
Ni baada ya kuona kuwa huenda wangeambulia patupu, ndipo aibu zikawekwa pembeni, wakamvaa mhudumu wa gesti na kumtobolea ukweli kuwa wamesikia eti hapo kuna ‘pedeshee’ ambaye anamwaga sana pesa kwa vimwana hususan wale watakaoweza kumfanyia vimbwanga vizito vya mapenzi chumbani mithili ya waigizaji wa sinema za ngono. Wale wanawake wasiojua kuwa aibu ni mdudu wa aina gani na kinyaa ni nini.
Mhudumu naye hakuwa na hiyana, akamfuata Kipanga na kumtaarifu juu ya ujio wa wanawake hao. Kipanga angekataa? Akatae wakati usiku uliopita alilazimika kumtimua mwanamke mmoja ambaye aligoma kumhudumia ipasavyo licha ya kumpa shilingi 50,000?
“Wanalipa?” Kipanga alimuuliza mhudumu.
“Nakwambia wako bomba kishenzi, mwanangu.”
“Hawataleta za kuleta katikati ya shughuli?”
“Mi’ nawajua,” mhudumu alijibu haraka. “Ni mi-shangingi iliyobobea katika fani. Nakwambia, utaikimbia mwenyewe.”
“Poa, kailete.”
Dakika chache baadaye ndipo wanawake hao wakajitoma chumbani humo. Naam, Kipanga akakubali kuwa ni wanawake wanaostahili kuwahudumia wanaume wenye njaa. Takriban saa nzima baada ya wanawake hao kukitekeleza kile kilichowaingiza humo chumbani, hatimaye Kipanga aliagiza tena bia na wakawa wakinywa taratibu.
Ni kipi kingine ambacho Kipanga angehitaji, zaidi ya wanawake wa aina hiyo chumbani humo? Wanawake waliokuwa radhi kumridhisha kimapenzi kwa namna yoyote aliyotaka! Nani kama yeye katika dunia hii? Ni starehe ipi duniani zaidi ya hiyo aliyopewa na warembo hao?
‘Haya ndiyo maisha,’ alijisemea kimoyomoyo huku akiwatupia macho kwa zamu wanawake hao, akivutiwa na uzuri wa maumbile yao, maumbile yaliyoichemsha damu yake kiasi cha kujikuta akitaka tena na tena, ikibidi wote kwa mkupuo, jambo lililokuwa gumu kutekelezeka.
************
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani lililivalia njuga suala la mauaji ya Waarabu watatu, Nassor Khalfan na wenzake. Jambo la kwanza baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, walimchukua mtoto Abdul hadi kituo cha Polisi. Huko, askari wa kitengo cha upelelezi, Maftah na Chopa wakachukua maelezo yake.
“Unaitwa nani?” Maftah alimhoji.
“Abdul.”
“Umri wako?”
Abdul alifikiri kidogo kisha akasema, “Sijui.”
Maftah na Chopa walitazamana. Hatimaye Maftah akayarejesha macho kwa mtoto Abdul na kuendelea, “Unasoma?”
“Ndiyo.”
“Uko darasa la ngapi?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“La nne.”
Chopa na Maftah walitazamana tena. Chopa akasema, “Hatazidi miaka kumi na miwili.”
“Yeah. Ni kati ya kumi na kumi na miwili,” Maftah aliongeza.
Maftah akamgeukia tena mtoto Abdul. “Leo ulikuwepo nyumbani tangu asubuhi?”
“Ndiyo.”
“Hukwenda shuleni?”
“Sikwenda.”
“Kwa nini?”
Abdul hakujibu.
“Tangu asubuhi marehemu baba yako hakuwa ametoka nyumbani?”
“Hakutoka.”
“Alikuwa na shughuli gani tangu alipoamka?”
“Alikuwa akiangalia tivii.”
“Mama yako alikuwa wapi?”
“Mama hayupo.”
“Yuko wapi?”
“S’jui.”
“Hayupo kwa siku nyingi?”
“Ndiyo.”
“Wakati baba yako anaangalia tivii unaweza kuwakumbuka wageni wa kwanza waliokuja nyumbani?”
“Ndiyo.”
“Walikuwa ni akina nani?”
Abdul alifikiri kidogo kisha akasema, “Ni wale rafiki zake wawili.”
“Wale waliokuwa pamoja naye wakati walipovamiwa?”
“Ndiyo.”
“Na wale unaosema kuwa ndio waliowavamia walikuja saa ngapi?”
Abdul alitulia kidogo, akatazama sakafuni kisha akasema, “S’jui.”
Chopa akasema, “Hilo si tatizo. Hebu tuambie, hao wavamizi walipokuja ni nani aliyewapokea mlangoni?”
“Mimi.”
“Walikwambiaje?”
“Eti wao ni wageni wa baba, wametoka Dar.”
“Halafu?”
“Halafu baba akatokea na kuwakaribisha.”
“Baba yako alikuwa akiwafahamu?”
“Ndiyo.”
“Na walipoingia walipiga risasi moja kwa moja au waliongea kwanza na baba yako?”
“Waliongea kwanza na baba.”
“Wakati wanaongea wewe ulikuwa wapi?”
“Chumbani.”
“Kwa hiyo hukuyasikia maongezi yao, eti Abdul?”
“Niliyasikia. Mlango wa chumba ulikuwa wazi.”
Chopa na Maftah wakatazamana tena kisha wakamkazia macho mtoto Abdul.
“Walikuwa wakizungumza kuhusu nini?” Chopa aliendelea kumwaga maswali.
“Gari. Walikuwa wakitaka baba awape pesa ili wamwachie gari.”
“Yaani walikuwa wakiuza gari?”
“Ndiyo.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hilo gari walikuwa wamekuja nalo?”
“Ndiyo.”
“Uliliona?”
“Ndiyo, nililiona.”
“Hebu njoo,” afande Chopa alimtoa nje Abdul.
****DOLA IKO KAZINI. ASKARI WANAMHOJI MTOTO ABDUL AMBAYE ALIWAONA PANJA NA KIPANGA WALIPOKUJA KWA MZEE NASSOR KHALFAN. KWA UPANDE MWINGINE KIPANGA YUKO GESTI AKITANUA NA 'WAREMBO.' NI KIPI KITAFUATA?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment