Simulizi : Kwa Udi Na Uvumba
Sehemu Ya Nne (4)
CHOPA na Maftah wakatazamana tena kisha wakamkazia macho mtoto Abdul.
“Walikuwa wakizungumza kuhusu nini?” Chopa aliendelea kumwaga maswali.
“Gari. Walikuwa wakitaka baba awape pesa ili wamwachie gari.”
“Yaani walikuwa wakiuza gari?”
“Ndiyo.”
“Hilo gari walikuwa wamekuja nalo?”
“Ndiyo.”
“Uliliona?”
“Ndiyo, nililiona.”
“Hebu njoo,” afande Chopa alimtoa nje Abdul. Huko kulikuwa na magari ya aina mbalimbali. “Kuna gari lolote hapa ambalo unaweza kulifananisha na lile gari walilokujanalo hao wageni?” alimuuliza.
Abdul alitazama huku na kule kisha akasema, “Ni kama lile, na lile… na lile… na lile…” Alimwonyesha magari manne, meupe aina ya Toyota Mark 11 ambayo yalikuwa yameegeshwa, yakiwa yamechanganyika na magari mengine.
Wakarudi ndani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nadhani kuna haja ya kumwonyesha picha za wahalifu sugu tulizonazo,” Chopa alimwambia Maftah.
Dakika chache baadaye majalada kadhaa ya wahalifu sugu yalikuwa mbele yao sanjari na picha zao. Baadhi ya wahalifu hao walikuwa wakitumikia vifungo magerezani, baadhi walikwishakufa, baadhi walikuwa rumande kesi zao zikiunguruma na wengine walikwishamaliza vifungo.
Hawakutaka kubagua picha za kumwonyesha Abdul, waliamua kumwachia kazi ya kuzitazama na kuzipambanua mwenyewe kabla ya hatua itakayofuata.
“Abdul, ni wewe uliyewakaribisha hao wageni ndani,” Chopa alimwambia. “Kwa hali hiyo kwa vyovyote ulipata muda mzuri wa kuweza kuwatazama. Kama ikitokea ghafla mmoja wao au wote wakitokea hapa unaweza kuwakumbuka?”
“Ndiyo.”
“Una hakika?” Maftah alimtazama Abdul kwa makini.
“Ndiyo! Nitawakumbuka vizuri!” Abdul alijibu kwa msisitizo.
Ni hapo rundo la picha kumi na tatu lilipomwagwa mbele yake.
“Kazi kwako,” Chopa alimwambia. “ Zitazame kwa makini picha hizi. Kama utaiona picha yoyote ambayo unaitilia shaka kuwa inafanana na mmoja wa wale wavamizi, iweke pembeni.”
Mtoto Abdul aliingia kazini. Akaitazama picha moja baada ya nyingine kwa utulivu. Mara macho yakaganda kwenye picha moja.
Akaikodolea macho picha hiyo bila ya kupepesa. Hatimaye akaiweka kando na kuendelea kuzichunguza picha nyingine. Alipozimaliza, akairudia picha ile aliyoiweka pembeni. Kwa mara nyingine akaikodolea macho kwa makini. Kisha akampatia Chopa.
Ilikuwa ni picha ya mmoja wa majambazi sugu yenye rekodi mbaya katika Jeshi la Polisi. Aliitwa Kipanga Sukasuka. Rekodi yake ilionesha kuwa kiasi cha miaka kumi iliyopita, Kipanga alihukumiwa jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu. Lakini rekodi hizohizo hazikuweka bayana kuwa Kipanga alikwishamaliza kifungo hicho.
Picha hiyo ilimwonesha Kipanga akiwa amevaa suruali aina ya Jeans, raba miguuni na fulana kubwa yenye picha ya mcheza sinema maarufu wa Marekani. Macho yake yalikuwa makali, yaking’ara ukatili ilhali kichwani upara ukitawala.
“Kwa nini umeichagua picha hii?” Chopa alimhoji mtoto Abdul.
Abdul alikumbwa na kigugumizi.
Maftah akamwahi, “Vipi, Abdul, huyu mtu ni mmoja wa wale uliowafungulia?”
“Ndiyo.”
“Ni huyu pekee? Si umesema uliwafungulia wawili?”
“Ndiyo, niliwafungulia wawili.”
“Sasa mbona umeichagua picha moja tu?” Chopa alimuuliza.
“Yule mwenzake simwoni kwenye picha hizi,” Abdul alijibu.
“Lakini huyo mwenzake ukimwona sasa hivi utamkumbuka?”
“Ndiyo.”
“Huyu mwenye picha hii una hakika ndiye aliyekuja au ni kwamba tu anafanana-fanana naye?” Chopa aliendeleza maswali.
Abdul hakujibu.
“Unaweza kuwa unamfananisha, eti?”
“Ndiyo.”
“Na pia anaweza kuwa ni mwenyewe, si nd’o maana’ake?”
“Ndiyo.”
“Ok, kapumzike kule kwene benchi nje.”
Uchunguzi haukuishia kwa mtoto Abdul pekee. La hasha. Mama mmoja, mkazi wa jirani na nyumba yalikotokea mauaji naye alipopewa zoezi la utambulisho kwa kutumia picha, akaitilia uzito zaidi picha ya Kipanga. Vijana wawili wapita njia waliowaona Kipanga na Panja wakitoka ndani ya jumba lile na kutokomea na gari, japo walitatanishwa na wingi wa picha walizooneshwa, hata hivyo bado waliitilia shaka zaidi picha ya Kipanga.
“Yeah, hii ni hatua ya kwanza muhimu,” Chopa alimwambia Maftah. “Inabidi tule sahani moja na Kipanga kwanza. Na kwa kuanzia ni vyema tufanye mawasiliano na watu wa Dar, mara moja. Matukio mengi ya kihalifu, Kipanga aliyafanya akiwa Dar. Na Dar ndiyo makazi yake. Najisikia kuamini kuwa huenda watakuwa wamekimbilia Dar na kujichimbia mahala fulani, pesa zikiwa ni nyenzo madhubuti kwa kuwaficha.”
***************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
DAKIKA ishirini tu baada ya picha ya Kipanga pamoja na taarifa kamili kuhusu tuhuma za Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani dhidi yake kutumwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao, nyumba ya Kipanga ilioko mtaa wa Jangwani ilivamiwa na askari kanzu. Upekuzi wa hapa na pale sanjari na maswali kwa huyu na yule vikatawala. Kipanga hakuwepo, na wapangaji walidai kuwa tangu alipoondoka asubuhi alikuwa hajarudi.
Ilikuwa ni taarifa iliyowatia gizani askari hao. Kazi iliyokuwa mbele yao ikawa ngumu zaidi. Japo waliwabeba baadhi ya wapangaji hao na kuwapeleka kituoni ambako waliwasumbua kwa mateso ya wastani na mlolongo wa maswali, hata hivyo bado haikusaidia kitu.
Wiki moja ikapita.
Ya pili ikakatika.
Ya tatu ikatinga.
Mwezi ukatimia!
Bado Chopa na mwenzake, Maftah huko Kibaha, na Inspekta Materu na mwenzake Sajini Kitowela wa jijini Dar Es Salaam hawakuwa wameambulia lolote katika msako dhidi ya wahusika wakuu wa mauaji ya wafanyabiashara watatu wenye asili ya Kiarabu huko Maili Moja, Kibaha na wanaoaminika pia kuwa ndiyo walioiba fedha lukuki ambazo bado hesabu yake haikuweza kufahamika.
Hatimaye ikaja siku. Ilikuwa ni asubuhi, saa nne, Inspekta Materu akiwa ndani ya gari lake dogo akielekea Makao Makuu ya Polisi. Gari lilikuwa katika mwendo wa taratibu kutokana na msongamano ulioigubika barabara hiyo ya Bibi Titi Mohammed.
Alikumbuka kuwa, jana yake mkuu wake alimtaka ampe taarifa ya maendeleo ya msako wa wahusika hao wa Maili Moja. Akiwa katikati ya msongamano wa magari, jirani na kituo cha daladala cha Akiba, wazo moja lilimjia. Kwamba, inaaminika kuwa majambazi wale waliua na kuondoka na fedha nyingi sana.
Aliwajua majambazi wengi hususan wa Dar jinsi wanavyojitupa kwenye anasa pale pesa zinapowatembelea mifukoni, tena zile pesa za kutakata. Wengi wao huzama kwenye kwenye anasa. Baadhi yao ni wanywaji wa pombe na wengine wamebobea katika ufuska.
Kipanga ni mpenzi wa vyote viwili; pombe na wanawake. Inspekta Materu hakuhitaji kujiuliza kuhusu hilo. Kipanga hakuwa mgeni kwake. Alimfahamu, na aliifahamu vizuri tabia yake. Ni kwa kulijua hilo, ndipo alipomwita muuza magazeti aliyekuwa akipitapita kando ya magari akinadi biashara yake. Kilichomfanya amwite kijana huyo ni pale alipoliona gazeti la KIMBEMBE lenye kichwa cha habari; ‘BILIONEA’ AGOMBANIWA NA WANAWAKE UBUNGO.
Alivutwa na kichwa hicho cha habari, hivyo wakati magari yalipoanza kuserereka tena barabarani, alilitupa kwenye kiti cha pili gazeti hilo huku shauku ya kulisoma ikizidi kumjaa. Alipokaribia kwenye makutano ya Barabara za Maktaba na hiyo ya Bibi Titi, taa nyekundu ikawaka na kusimamisha tena msafara. Akashusha pumzi ndefu na kulitwaa tena gazeti hilo. Papohapo akaanza kuisoma habari hiyo kwa utulivu na haraka.
Dakika moja baadaye alikuwa amemaliza. Na ndipo alipokata shauri kufika huko Ubungo kujionea mwenyewe huyo mtanuzi anavyofanya vitu vyake. ‘Huenda tukawa tumepiga hatua moja mbele,’ alijisemea kimoyomoyo.
Lakini pamoja na kujiwa na wazo hilo, pamoja na kuchukua uamuzi huo, bado kulikuwa na tatizo. Hakuijua vizuri Ubungo. Isitoshe hakuvijua vichochoro vya Ubungo. Hadi taa zilipowaruhusu na kuanza kukanyaga moto, alijiona kama mpuuzi aliyepanga mpango usiopangika. Alikaribia kuachana na wazo hilo wakati alipokuwa akiingia Barabara ya Ohio lakini mara akamkumbuka Koplo Kendo, askari aliyezaliwa, akakulia, kusomea na hatimaye kupafanya Ubungo maskani ya kudumu. Akajenga imani kuwa Kendo atakuwa msaada mkubwa kwake.
Kilichompeleka Makao Makuu ya Polisi hakikuwa cha kumchukua zaidi ya robo saa hivyo kabla ya saa 5 akawa amesharudi ofisini kwake ambako jambo la kwanza alilofanya ni kumwita Koplo Kendo na kumhoji kuhusu hiyo gesti bubu.
“Naijua,” Kendo alimwambia. “Ni gesti ambayo hupendwa na kutumiwa na wanaume wanaoiba wake za watu na wanawake wanaoiba waume za watu.”
“Iko vichochoroni sana?”
“Hapana. Lakini iko mbali kidogo kutoka Morogoro Road.”
“Gari inafika?”
“Yeah. Ni mtaa safi wenye barabara nzuri tu.”
“Ni gesti tu, au hata baa ipo hapohapo?”
“No,” Kendo alijibu haraka. “Kwa anayetaka bia, wahudumu humletea kutoka nyumba kama ya tatu, nne hivi toka hapo. Kuna vijibaa viwili maeneo ya jirani na hapo.”
Kwa kiasi fulani hiyo ilikuwa ni habari njema kwa Inspekta Materu. Shauku ya kufika huko Ubungo ikazidi kumjaa. Lakini kama kawaida yake, hakupenda kumkosa Sajini Kitowela katika masuala ya kutatanisha kama hilo. Hivyo muda mfupi baadaye walikutana, na Materu akapasua.
“Nafikiri twende Ubungo.”
“Kuna nini, afande?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tukamcheki huyu mshenzi anayetanua kama hana akili nzuri katika kipindi hiki ambacho wengine tunalia njaa kutokana na mafisadi kuifilisi nchi,” Inspekta Materu alisema huku akimwonesha Kitowela habari iliyochukua uzito wa juu katika gazeti pendwa la KIMBEMBE.
Kitowela alilitwaa gazeti hilo na kutulia kwa muda akiisoma habari hiyo. Muda mfupi baadaye alicheka na kuhoji, “Afande, sasa tunaanza kufanya upelelezi kwa kuongozwa na magazeti?”
“Nilijua utasema hivyo,” Materu alisema huku akikunja uso. Alionyesha bayana kutofurahishwa na swali hilo. Akaongeza, “Kumbuka mpaka sasa hatujapiga hatua yoyote ya maana. Tayari mwezi u’shakatika, hatuna mbele wala nyuma. Na jana nimeulizwa kuhusu ishu hii-hii. Unadhani tutafanya nini? Inabidi tuguse kila mahali ambapo huenda tunaweza kupata picha yoyote.
“Jambo unalopaswa kujua ni kwamba uandishi ni taaluma kama taaluma nyingine. Waandishi siyo vichaa wa kuweza kuzushazusha mambo tu ili wauze magazeti. Wanajua walifanyalo. Kwa kweli idara yetu haiwezi kuwa na uwezo wa Ki-Mungu wa kujua kila kitu kinachotokea bila msaada wa mtu yeyote mwingine au taasisi nyingine isiyokuwa chini ya Jeshi la Polisi. Ndiyo maana tuna Polisi-Jamii katika kupata ushirikano toka kwa wananchi.”
Akatulia na kumkazia macho makali Sajini Kitowela. Kisha akaendelea, “Kwa vyovyote kuna zaidi ya robo tatu ya ukweli katika stori hii. Isitoshe, Koplo Kendo anaishi hukohuko Ubungo, na anaifahamu vizuri gesti hiyo. Hajawahi kumwona mtanuzi huyo, lakini anakiri kuzipata habari hizo toka maeneo hayo. Ni habari iliyozagaa kabla hata waandishi hawajaichangamkia kwenye kompyuta zao.”
“Kuna uhusiano gani kati ya mtanuzi huyu na mhusika wetu?” Kitowela alirusha swali.
Inspekta Materu alilitafakari swali hilo na alipolipima kwenye mizani akaliona likiwa na uzito wa unyoya. Hakutarajia kuwa mtu kama Sajini Kitowela angeuliza swali la aina hiyo katika kipindi hicho wanachotapatapa kuwasaka wahusika wa mauaji ya watu watatu sanjari na wizi wa fedha huko Kibaha, Maili Moja.
Hata hivyo hakutaka kulizungumzia hilo. Alilipuuzia. Badala yake alisema, “Ninachozingatia hapa ni tabia ya Kipanga. Ni mtu, ni jambazi kama majambazi wengine ambao mara tu mifuko yao inapojaa huhamia baa au gesti.”
“Kwa hiyo tutakachokifanya sisi ni kama kubahatisha, si nd’o maana’ake?” Kitowela alimng’ang’ania Inspekta Materu.
“Inaweza kuwa hivyo ingawa si lugha nzuri kusema kuwa tunakwenda kubahatisha,” Inspekta Materu alijibu. “Cha kuzingatia ni kwenda tukiwa kamili, tumetimia. Chukua silaha yako, robo saa isitukute hapa. Sawa?”
“Sawa, afande,” Sajini Kitowela aliitika huku akitoka.
“Halafu,” Materu aliongeza, kauli iliyomfanya Kitowela asite kuondoka na kugeuka.
“Ndiyo, afande.”
“Hatutatumia gari la ofisi. Tafuta teksi nzuri. Sehemu za aina ile hapastahili kwenda na Ma-defender yetu.”
Kitowela alipoondoka, Inspekta Materu aliichukua picha ya Kipanga na kuipachika katika mfuko wa kushoto wa shati lake.
***************
DEREVA teksi alikanyaga breki za gari nje ya baa ya Kitamba, Ubungo likiwa ni eneo ambalo lilikuwa geni kwa Panja, sehemu iliyostahili kuitwa Ubungo-vichochoroni.
“Unaiona nyumba ile?” dereva alimwonesha kwa kidole.
Kutoka hapo walipokuwa hadi kwenye hiyo nyumba ambayo Panja alionyeshwa kulikuwa na umbali wa mita kama mia moja, hivi.
“Ipi, ile yenye maua mengi nje?”
“Acha hiyo. Ile inayofuatia.”
“Pale ilipopaki ile Land Rover ya bluu, wan-teni?”
“Yeah. Hapohapo. Unasemaje, nikufikishe mlangoni?”
“No,” Panja alipinga haraka. “Kama gesti yenyewe ina sifa ya kuwa na wateja wanaoendekeza ngono, kwa vyovyote mtu yeyote akiniona nateremka pale atajua ni ngono tu inayonipeleka. Hapahapa panatosha.”
Dakika iliyofuata Panja alikuwa ndani ya Kitamba Bar akinywa bia iliyochanganywa na toti tatu za pombe kali. Na alikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Ujasiri. Mara kwa mara alipokuwa akipata vinywaji vya aina hiyo alikuwa mwepesi wa kumtongoza mwanamke yeyote atakayemtia machoni pake kama ambavyo pia alivyokuwa tayari kumchinja mtu yeyote kama kuku.
Bia ilipokatika, alitoka. Lakini bado alihitaji ujasiri mkubwa zaidi, hivyo alikwenda chooni ambako alijifungia na kuwasha msokoto wa bangi yake. Mikupuo mitatu ya nguvu ikiambatana na unuiziaji, ilitosha kumfanya ajione kuwa yeye ndiye baba wa dunia.
Nani kama yeye?
Alipotoka chooni alipitiliza moja kwa moja nje. Sasa hakuwa na jingine kichwani, zaidi ya kuifuata ile ‘gesti bubu’ akiamini kuwa huenda siku hiyo akawa amepata kitu cha kueleweka. Huenda akaondoka hapo huku akiwa ameutokomeza umaskini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alipovuta hatua tatu alijipapasa mfuko wa kulia wa suruali yake pana. Akashusha pumzi ndefu, pumzi za matumaini na kujawa na nguvu maradufu baada ya kubaini kuwa bastola yake yenye risasi tatu ilikuwemo.
Kichwani mwake alikuwa na mambo mawili; kwamba, kama atamkuta mtu huyo mwenye sifa ya utanuzi ni Kipanga, basi liwalo na liwe, ama anaondoka hapo na pesa, tena pesa za kueleweka, ikibidi ziwe zote atakazozikuta, au aiache maiti ya Kipanga ikivuja damu. Vinginevyo, yu radhi kufa kuliko kurudi nyumbani bila pesa.
Kitu fulani kilimjia akilini na kumwambia kuwa kwa vyovyote mtanuzi huyo ni Kipanga, na kwamba bado ana pesa nyingi, pesa zinazoweza kumwingiza yeye, Panja katika daraja jingine la maisha, daraja la juu katika mafanikio. Ni pesa hizo zilizomleta hapo, na alidhamiria kuzipata hata kama itamlazimu kuipindua Ubungo juu, chini.
Akaongeza kasi ya kutembea, safari hii kwa ukakamavu zaidi, macho mbele huku mkono wa kulia ukiwa ndani ya mfuko wa suruali, ukiikamata bastola yake tayari kwa lolote. Naam, alikuwa tayari kwa lolote!
Tayari kuua.
Tayari kufa.
***************
WANAWAKE hawa wawili ni kama vile walikuwa wakiigiza sinema ya ngono. Kila mmojawao akiwa ameshakabidhiwa kitita cha shilingi 50,000 na bia kadhaa kutua matumboni mwao kiasi cha kuwafanya nusu- vichaa, walidhihirisha kuwa wao ni wanawake waliofundwa, wakafundika.
Walimfanyia Kipanga yale aliyoyapenda na aliyoyahitaji. Naam, waliviachia huru viungo vyao vyote, wakamruhusu Kipanga awatumie kwa jinsi apendavyo katika kuuburudisha moyo wake.
Mtu mmoja aliwahi kukaririwa akidai kuwa mwanamke mwenye umbo kubwa na teketeke, huwa ni mbumbumbu wa kutisha pindi awapo faraghani na mwanamume. Mtu wa pili alipingana na kauli hiyo, akisema kuwa umbumbumbu wa mtu katika starehe ya mapenzi hauna uhusiano wowote na ukubwa au udogo wa umbo la mhusika hususan mnene na mwembamba.
“Siyo kwamba mwanamke mnene huwa mzito na kwamba mwanamke mwembamba ndiye mwepesi wakati wa shughuli hiyo, hapana. Wepesi unatokana na juhudi binafsi za mtu. Kama mwanamke mnene atajiweka kizembezembe na minyama- uzembe yake, basi lazima hatakuwa na chochote cha ziada katika zoezi hilo.” Hayo ni maono ya mtu wa pili.
Kwa namna moja au nyingine huyu mtu wa pili alikuwa sahihi kwa kulinganisha na hawa wanawake waliokuwa wakimhudumia Kipanga. Ndiyo, wote walikuwa wanene, lakini unene wao wa hadharani uliotoa taswira ya kuwa ni wazito sana sirini, ulikuwa ni unene uliodhihirisha kuwa umahiri katika tendo la ndoa hauna uwiano wowote na umbo la mhusika.
Kila mmoja kwa zamu yake alijipinda na kujipindua bila ya kuchoka na kuonekana kama vile alikuwa akitumia nguvu za ziada ambazo binadamu wa kawaida hakujaaliwa kuwa nazo. Kwa Kipanga, alijiona kapata watu wanaostahili; wanawake wenye sifa kuu mbili kati ya tatu muhimu kwa wanawake wanaostahili kuitwa ‘wanawake wazuri.’
Aliamini kuwa mwanamke mzuri ana sifa kuu tatu. Ya kwanza; awe mrembo sana hadharani, ya pili; hodari sana jikoni, na, ya tatu;
malaya sana kitandani.
Hawa wanawake wawili wenye miili mikubwa na teketeke huku weupe wao ukiwa umekolezwa na vipodozi vilivyotoka ng’ambo ya Afrika vyenye wingi wa kemikali, walijaaliwa sifa mbili kati ya tatu; urembo wa hadharani na watundu sana chumbani. Kwa Kipanga, sifa hizo zilitosha kumfanya aifurahie burudani aliyopata kutoka kwao.
Waliendelea, wakaendelea na kuendelea zaidi.
***************
TEKSI iliyowabeba Inspekta Materu, Sajini Kitowela na Koplo Kendo ilikomea mita kama mia tatu hivi kutoka katika gesti bubu ambayo askari hao waliifuata.
“Tumefika?” Materu alimuuliza Kendo.
“Siyo mbali kutoka hapa hadi kwenye gesti yenyewe,” Kendo alijibu. Kisha kama aliyeonyesha kushangazwa na swali la Kitowela, akahoji, “Afande, au twende mpaka mlangoni?”
“Hapana. Hapahapa panatosha.”
Kutoka hapo walitembea taratibu lakini kwa kujiamini, wakihakikisha hakuna mtu ambaye atawashangaa au kuwatilia shaka. Wakaiacha barabara na kupita uchochoro huu hadi ule, Kendo akiwa kiongozi wa msafara.
Hatimaye wakajikuta wanatokeza kwenye Baa ya Kitamba ambako kwa muda huo, saa 6 mchana, idadi ya wateja haikuwa kubwa. Zaidi kulikuwa na wachache waliokuwa wakila nyama-choma na soda. Kwa jumla ukumbi huo ulipooza. Koplo Kendo akawaongoza ndani ya baa hiyo ambako waliagiza soda na kuanza kunywa taratibu.
Ni wakati wakiendelea kunywa soda ndipo Kendo alipowaonyesha sehemu waliyoihitaji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa pale walipokaa, hawakuhitaji kunyanyuka na kutoka ili wapaone vizuri hapo ilipo gesti bubu.
“Ok,” Materu alisema kwa sauti ya chini. “Kazi yako imetosha. Sasa unaweza kurudi. Kama tutafanikisha lengo lililotuleta hapo, suala la msaada wako nitalifikisha ngazi za juu, na matunda yake utayaona.”
”Sawa, afande,” Koplo Kendo alijibu huku akiachia tabasamu la mbali kisha akanyanyuka na kutoka taratibu.
**************
AKIWA hamfahamu Panja, wala kuijua dhamira ya ujio wake, mfanyakazi wa gesti-bubu alimwonesha chumba alichokuwemo Kipanga. Haikuwa kazi ngumu kwa Panja kumrubuni kijana huyo wa mapokezi hadi akamwonesha chumba hicho. Aliingia kwa kujiamini na kutoonyesha ugeni wowote, hali iliyowafanya wengine waliokuwa hapo wasimtilie shaka wala kumtazama-tazama.
Ndipo, baada ya kuchangia maneno mawili, matatu na vijana wengine waliokuwa hapo wakizungumzia soka la Uingereza, hatimaye akamsogelea yule mhudumu aliyekuwa ndani ya chumba kidogo chenye kijidirisha maalumu kwa minajili ya kutoa huduma kwa wateja.
“Anko, mambo vipi?” alimwinamia hapo dirishani.
“Poa tu. Karibu.”
“Samahani msh’kaji wangu. Kuna jamaa yangu, kaniagiza nimfuate hapa leo.”
Kijana Yule alikunja uso kidogo huku akimtazama Panja usoni sawia. Kisha akamuuliza, “Anaitwa nani?”
“Kipanga.”
Jina hilo halikuwa geni masikioni mwa kijana huyo. Ni kwamba, japo Kipanga alipoingia hapo kiasi cha mwezi mmoja uliopita alitumia jina bandia, lakini kadri siku zilivyokwenda ndivyo alivyokuwa akijisahau mara kwa mara na kujikuta akilitamka jina lake halisi pindi alipoulizwa na mwanamke yeyote waliyekuwa pamoja baada ya kufakamia bia kwa fujo na kuendelea na starehe nyingine.
Leo alijisahau na kumtamkia mwanamke huyu, kesho yule, keshokutwa, yule. Ikawa hivyo hatimaye jina la Kipanga likazoeleka, jina la Kakinga likatokomea taratibu na hatimaye likajizika kabisa. Na ikawa ni hali iliyoondoa utata na shaka pale Panja alipolitamka kwa mhudumu huyo.
Mhudumu huyo alikuwa katingwa na shughuli za hesabu za mapato na matumizi, hivyo hakuiona haja ya kuendelea kumhoji maswali huyu mgeni anayeonekana yu mstaarabu na asiyekuwa na matatizo.
“Kamcheki namba kumi,” alimwambia huku akiyarejesha macho kwenye leja yake ya hesabu. Na bila ya kuuinua tena usowe, aliongeza, “Nadhani atakuwepo, na atakuwa na wageni wake. Lakini kamcheki.”
Panja alishusha pumzi ndefu na kuupeleka mkono kwenye mfuko uliohifadhi bastola yake. Akaigusa bastola hiyo na kuiacha. Akautoa mkono na kuangaza macho kushoto na kulia. Hakukuwa na mtu yeyote mwingine. Akamrudia mhudumu huyo na kumuuliza, “Namba kumi ndiyo wapi?”
Ni hapo mhudumu huyo alipoahirisha kufanya kazi yake. Akaunyanyua uso na kumwambia, “Fuata korido hiyo,” akamwonyesha kwa kidole. Kisha akaongeza, “Ukifika mbele, kata kushoto. Siyo kulia. Huko kushoto, hesabu mlango wa kwanza, wa pili, wa tatu, ukifika wa nne utaiona hiyo namba kumi. Ni hapohapo.”
Panja alitaka kumshukuru kwa sauti lakini akajikuta akiikosa sauti yake. Badala yake, aliinama kidogo huku akiukita mkono wa kulia kifuani, tabasamu la mbali likichanua usoni, akionyesha ishara ya shukurani. Kwa hatua fupifupi, lakini kwa kujiamini, alifuata maelekezo ya mhudumu huyo, mkono wa kulia ukiwa umezama mfukoni akiikamata bastola yake tayari kwa lolote.
Alipoufikia mlango wenye maandishi: No.10 akasimama bila ya kubisha hodi. Akaangaza pande zote za korido hiyo na kutomwona mtu yeyote, hali iliyompa matumaini ya kutoshindwa kuitekeleza azma yake. Akaunyanyua mkono ili agonge mlango, lakini akasita. Na alikuwa na sababu ya kusita.
Masikio yake yalinasa miguno tofauti, miguno ambayo haikuhitaji mtu mzima, mwenye akili timamu ashindwe kujua ni kipi kilichoendelea.
Hasira zikampanda, hasira zilizotokana na kumbukumbu ya tukio la kiasi cha mwezi mzima huko Maili Moja, Kibaha, tukio lililompa Kipanga utajiri wa wastani kiasi cha kuja kutanua huku Ubungo, akitumia pesa kama ‘mwendawazimu.’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuendelea kuvuta subira, alikurupuka kugonga mlango. Aligonga mara mbili. Kimya. Sasa hata ile miguno iliyotoa taswira ya starehe ya mapenzi na maneno ya kimahaba-mahaba ilikatika ghafla. Akatulia kama sekunde kumi hivi na kurudia kugonga, safari hii ikiwa ni mara tatu na kwa nguvu zaidi.
*****PANJA YUKO MLANGONI ANAGONGA. ASKARI NAO HAOOOO...KAZI IPO
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment