Simulizi: Let's Call It A Night
Sehemu Ya Pili (2)
Matibabu bado yalikuwa yakiendelea kila siku, Maimartha alikuwa kimya
kitandani huku akionekana kama mtu ambaye tayari alikuwa amekata roho. Kila
alipokuwa akimwangalia Maimartha kitandani pale, henry alijisikia uchungu
moyoni mwake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni kweli alikuwa akiwaona watu wengi vitandani wakiteseka, alikuwa
akiwachukulia kawaida, kuumwa kwa Maimartha lilionekana jambo zito sana
moyoni mwake, alilichukulia kwa uzito tofauti na watu wengine walipokuwa
wakiumwa wakiwepo ndugu zake.
Kila wakati swali lake kwa madaktari lilikuwa atapona lini na atayafumbua
macho yake lini. Hakukuwa na dokta aliyekuwa akilijua hilo, kitu walichokuwa
wakikitaka ni kuendelea na tiba hiyo kama kawaida.
Picha za vipimo vya Magnetic Resonance Imaging (MRI) vikasafirishwa na
kupelekwa katika Hospitali ya Ahmedabad Civil ambayo ilikuwa ikipatikana
Ahmedabad. Ukiachana na India, hiyo ndiyo ilikuwa hospitali kubwa barani
Asia.
Wagonjwa wengi waliokuwa wakishindikana katika hospitali nyingine walikuwa
wakipelekwa katika hospitali hiyo ambayo ilikuwa na madaktari waliokuwa
wazoefu katika kuzifanya kazi zao.
Walipoyapokea majibu ya vipimo vya MRI kutoka katika Hospitali ya Ganga,
walichokifanya ni kumtuma daktari wao ambaye alikuwa mzoefu na matatizo
ya mifupa, Amir aende huko kwa ajili ya kumuona mgonjwa huyo, Maimartha.
Alipofika, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuangalia taarifa nzima ya mgonjwa huo
hata kabla hajaanza kazi yake. Kila kitu alichokisoma katika ripoti hiyo
kilionesha kwamba pamoja na kuvunjika kwa uti wa mgongo, Maimartha
angeweza kupooza na kubaki hivyo maisha yake yote.
“Tunatakiwa kufanya haraka hata kabla miezi sita haijatimia, vilevile tunatakiwa
kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha hizo chembechembe zilizotoka
zinatolewa kuepuka matatizo zaidi,” alisema Dk. Amir.
“Hatua ya kwanza ni ipi?” aliuliz Dk. Sunil.
“Kumchukua tena vipimo vya MRI.”
“Mmmh! Hivyo si tumekwishachukua na ripoti kukutumia?”
“Najua, natakiwa kuanza upya, kwa kufanya hivyo, nadhani itaweza kusaidia na
nitajua tatizo kubwa ni lipi,” alisema Dk. Amir.
Kwa sababu yeye ndiye alikuwa mtaalamu zaidi, hakukuwa na mtu aliyelipinga
hilo, walichokifanya ni kufanya kama alivyosema. Vipimo vya MRI vikachuliwa
kwa mara nyingine tena, majibu yalivyokuja, akagundua tatizo jingine kwamba
mbali na kuvunjika kwa uti wa mgongo, pia picha iliyopigwa ilionesha kwamba
ulikuwa umepinda kidogo.
“Hili ni tatizo ambalo sikuwahi kukutana nalo,” alisema Dk. Amir huku
akionekana kushangaa.
“Tatizo gani?”
“Uti wake wa mgongo umepinda, kazi ya kwanza tunayotakiwa kupambana
nayo ni kuurudisha uti huo kwenye hali yake ya kawaida na matibabu yaanze
rasmi,” alisema Dk. Amir.
“Mmmh! Itachukua muda gani mpaka unyooke?”
“Miezi miwili.”
“Sasa baada ya hapo, tutafanikiwa kumtibia kwa miezi sita? Itakuwa imebaki
miezi minne.”
“Tutaweza tu. Kupinda kwa uti wa mgongo ndiyo tatizo lililoleta tatizo lake la
kutokurejewa na fahamu. Kwanza tushughulikie suala hili,” alisema Dk. Amir.
Usiku hakulala, muda wote alikesha na vitabu vyake huku akiangalia ni kwa
namna gani angeweza kumsaidia Maimartha. Mgonjwa huyo alionekana kuwa
kwenye hali mbaya, alijua fika kwamba alikutana na wagonjwa waliokuwa na
matatizo ya uti wa mgongo lakini kwa Maimartha tatizo hilo likaonekana kuwa
kubwa zaidi.
Kichwa chake kilimuuma, kwa kutumia mitandao mbalimbali ya madaktari
wenzake, hakuweza kugundua namna ya kuurudisha uti wa mgongo wa
Maimartha kama ulivyokuwa, kwake, tatizo hilo likaonekana jipya.
Mbele yake alijiona kuwa na mtihani mkubwa, kufanikisha matibabu ya
Maimartha kulimaanisha kwamba uwezo wake ungekuwa juu zaidi kwani tatizo
hilo lilionekana kuwa jipya kabisa.
Alipekua kila kitu alichoona kufaa kupekuliwa usiku huo lakini wala haikusaidia.
Akajaribu kuufungua mtandao wa Google na kuanza kutafuta labda tatizo la
kupinda kwa uti wa mgongo lilikuwa limeelezewa, napo hakukuta kitu hali
iliyomuumiza kichwa zaidi.
“Nifanye nini sasa? Hivi kweli naweza kushindwa namna hii? Hapana, kusoma
kwangu kwa miaka thelathini halafu tatizo hili kweli nisilitatue, basi bora
nirudishe vyeti endapo tu itatokea kushindwa kulitatua tatizo hili,” alijisema Dk.
Amir.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata, asubuhi na mapema akafika hospitalini hapo, kitu cha kwanza
alichokifanya ni kuonana na ndegu wa Maimartha na kuanza kuongea nao.
Aliwaelezea tatizo lililokuwa likimsibu msichana huyo, kila mmoja alionekana
kusikitishwa.
“Atapona?” aliuliza bi Estelina huku akilia.
“Atapona tu, cha msingi muendelee kumuomba Mungu,” alisema Dk. Amir.
Kuunyoosha uti wa mgongo wake haikuwa kazi nyepesi, ilikuwa ni kazi ngumu
iliyohitaji umakini wa hali ya juu. Kila siku kazi ilikuwa ni hiyohiyo tu. Madaktari
walikuwa wakikusanyika katika chumba hicho kila siku ambazo Dk. Amir
alikuwa akifika mahali hapo.
Mwezi wa kwanza ukakatika, kwa mbali dalili zikaanza kuonekana kwamba uti
wa mgongo ungeweza kunyooka endapo wangeongeza juhudi zaidi.
Hawakukata tamaa, waliendelea mbele na mwezi wa pili ulipoingia, kazi ilikuwa
imefanyika, uti wa mgongo ulikuwa umenyooka, bila kutegemeam, wakajikuta
wakipiga makofi ya shangwe kana kwamba Maimartha alikuwa amepona.
“Asante Mungu kwa msaada wako, hongera sana dokta,” madaktari wengine
wakajikuta wakimpongeza Dk. Amir.
Wazazi wake, Henry na Dk. Mshana walipopewa taarifa kwamba madaktari
walikuwa wamefanikisha kuunyoosha uti wa mgongo wa Maimartha, wakabaki
wakimshukuru Mungu tu kwani waliamini kwamba yeye ndiye alikuwa dokta
mkuu aliyeujua zaidi mwili wa binadamu kuliko madaktari hao.
“Tunamshukuru Mungu, kwa hiyo atapona vizuri lini?” aliuliza bi Estelina.
“Tuna miezi minne, tusipofanikisha ndani ya miezi minne inamaanisha kwamba
mgonjwa wenu atapooza maisha yake yote,” alisema Dk. Amir.
“Kwa hiyo amepooza?”
“Kila mtu anayepata tatizo hilo ni lazima apooze,” alijibu Dk. Amir.
“Na vipi kuhusu kurudiwa na fahamu zake?”
“Alishindwa kurudiwa na fahamu kwa sababu uti wa mgongo wake ulikuwa
umepinda, tatizo limekwisha, tegemeeni kwamba atarudiwa na fahamu na
kuongea muda wowote ule,” alisema Dk. Amir, wote wakajikuta wakibubujikwa
na machozi, kuambiwa kwamba Maimartha alikuwa amepooza, kuliwaumiza
zaidi ila kuhusu kurudiwa na fahamu muda wowote ule, kidogo kuliwafariji.
Siku ziliendelea kukatika kama kawaida, kila siku Dk. Amir alikuwa na jukumu
la kufika hospitalini hapo na kumtibia mgonjwa wake. Moyoni mwake alikuwa
na imani kubwa kwamba Maimartha angekwenda kurudiwa na fahamu na
mwisho wa siku angepona kabisa.
Mpaka kufikia hapo, jina lake liliendelea kuwa kubwa, kazi aliyokuwa ameifanya
haikuwa ndogo, ilikuwa ni kazi moja kubwa ambayo ilimpa heshima kubwa.
Siku ya kwanza ikakatika, katika mwezi huo wa pili, ulipofika katikati, kama
muujiza, Maimartha akaanza kuyafumbua macho yake na kuanza kuangalia
hapo alipokuwa.
Madaktari walikuwa wamemzunguka, kila alipokuwa akiangalia alipokuwa
hakupafahamu lakini mara ya kuwaona madaktari hao, dripu alizokuwa
ametundikiwa na mashine ya oksijeni iliyokuwa imeziba pua na mdomo wake,
akagundua kwamba alikuwa hospitalini.
Madaktari waliomzunguka, hakukuwa na daktari mweusi, kila mmoja alikuwa
mweupe, hiyo ikaacha maswali kichwani mwake kwamba alikuwa wapi.
“Welcome to the world” (Karibu ulimwenguni)” alisema Dk. Amir huku uso wake
ukipambwa na tabasamu pana.
“Nipo wapi?” aliuliza Maimartha kwa sauti ya chini.
“Just relax....relax,” (Tulia...tulia)” alisema Dk. Amir.
Hapo ndipo ambapo Maimartha akaanza kukumbuka, mara ya mwisho kabisa
alikumbuka kwamba alikuwa ndani ya gari na alikuwa akisikia honi kwa nyuma,
alipogeuka, aliliona gari kubwa la mafuta likija kule alipokuwa, likaigonga gari
lake kwa nyuma, baada ya hapo, hakukumbuka kitu chochote kile
kilichoendelea.
Akaanza kujiangalia, akataka kuitoa mashine ile ya oksijeni, akashindwa
kuunyanyua mkono wake. Hakuishia hapo, akataka kuisogeza miguu yake,
akashindwa kabisa kufanya hivyo jambo lililomfanya kugundua kwamba
alipooza.
“Nimepooza, nimepooza,” alisema Maimartha huku akipiga kelele.
Alichokifanya Dk. Amir ni kuchukua sindano iliyokuwa na dawa ya usingizi na
kumchoma Maimartha, hapohapo akalala usingizi mzito.
Mpaka kufikia hatua hiyo, wakaanza kupongezana, kazi waliyokuwa
wameifanya ilikuwa kubwa iliyohitaji pongezi, hawakuamini kama kweli
walikuwa wamefanikiwa kwa kiasi hicho mpaka Maimartha kurudiwa na
fahamu, kazi kubwa ambayo ilikuwa imebakia ni kumrudisha katika hali yake ya
kawaida.
Walipopewa taarifa kwamba Maimartha alikuwa amerudiwa na fahamu, wote
kwa pamoja wakarukaruka kwa furaha na kukumbatiana, hawakuamini kama
mwisho wa siku Maimartha angeweza kurudiwa na fahamu kwani siku
ziliendelea kukatika na alikuwa kimya.
“Can she talk?” (Anaweza kuongea?) hilo lilikuwa swali la kwanza alilouliza
Henry.
“Yes, she can,” (Ndiyo, anaweza)
“We want to talk to her” (Tunataka kuongea naye) alisema Henry huku
akilengwa na machozi ya furaha. Kwa furaha aliyokuwa nayo moyoni,
haikuweza kuelezeka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Dk. Amir hakutaka kuwaruhusu muda huo kwani hata kama wangekwenda
ingekuwa kazi bure tu kwa sababu Maimartha alikuwa katika usingizi mara
baada ya kuchomwa sindano ile, alichowaambia ni kwamba wajiandae
kumwangalia siku inayofuatia.
“No problem” (Hakuna tatizo)” alisema Henry.
Siku hiyo ikaonekana kuwa siku yenye furaha kuliko siku zote katika maisha
yake, alifurahia kusikia kwamba hatimae Maimartha alikuwa amerudiwa na
fahamu zake huku akiwa na uwezo wa kuzungumza.
Ndani ya chumba cha hoteli, Henry alikuwa akimshukuru Mungu, hakuamini
kwamba mwisho wa siku alikuwa ametenda muujiza na kumrudishia fahamu
zake Maimartha. Mpaka analala saa tano usiku, bado Henry alikuwa mwenye
furaha tele.
Kwa sababu yeye ndiye alikuwa mwandishi pekee aliyejua hali ya Maimartha
ilivyokuwa ikiendelea nchini India, siku iliyofuata akaandika taarifa kuhusiana
na hali aliyokuwa nayo Maimartha hospitalini hapo.
Zilikuwa ni taarifa zilizowashtua Watanzania kwa furaha, hatimae maombi
waliyokuwa wakiyafanya kwa kipindi kirefu, wakati huo Mungu alikuwa
ametenda.
Magazeti yote na vyombo vingine vya habari vikaanza kuandika kuhusu taarifa
hiyo ila jambo la kusikitisha lililoandikwa ni kwamba Maimartha alikuwa
amepooza.
Wakristo hawakucha kuomba, kila siku Jumapili jioni walikuwa wakikutana
katika Kanisa la Praise And Worship na kuanza kumuombea Maimartha ili afya
yake itengemae na kuwa kama zamani.
Picha zake wakati yupo kitandani zilimsisimua kila mtu. Alionekana kama mfu
kitandani hapo, wengi waliokuwa na moyo mwepesi wakaanza kulia,
muonekano wake aliokuwa nao kitandani pale ulimuumiza kila mtu.
“R.I.P Maimartha,” alisema jamaa mmoja ambaye alishika Gazeti la Uwazi, kila
alipoiangalia picha ya Maimartha, hakuwa na matumaini kama msichana huyo
angeweza kuamka tena.
Siku ambayo Henry na wazazi wake Maimartha walipofika hospitalini hapo kwa
ajili ya kumwangalia Maimartha, hawakuamini kama siku hiyo wangeweza
kuongea na mgonjwa huyo kutokana na kipindi kirefu kuwa kimya kitandani.
Hawakuacha kumuomba Mungu, katika viti ambavyo walikuwa wamekaa huku
wakisubiri kuingia ndani, walikuwa wakiikutanisha mikono yao na kuanza
kusali.
Walimwamini Mungu, walijua kwamba hata kupata fahamu kwa Maimartha
ulikuwa ni muujiza mkubwa wa Mungu ambao alikuwa ameufanya katika
maisha yake.
Mpaka Dk. Amir anafika na kuwaambia kwamba mgonjwa alikuwa
amekwishaandaliwa na kuanza kuingia ndani, hawakuamini kama wangemkuta
Maimartha akiwa macho huku akiwaangalia.
Walichoambiwa ndicho walichokutana nacho chumbani. Maimartha alikuwa
ameyafumbua macho yake, alikuwa akiangalia huku na kule, watu hao
walipoingia, machozi yakaanza kumbubujika.
Hakuwa na raha, moyo wake haukufurahi kabisa kila alipokuwa akikumbuka
kwamba kwa wakati huo mwili wake ulikuwa umepooza. Alitamani kutembea
kama watu hao waliokuwa wameingia ndani ya chumba hicho, alitamani
kuchezesha viungo vyake kama watu hao lakini kwa kipindi hicho
haikuwezekana kabisa.
Alikuwa kitandani hapo kama gogo, hakuwa na nguvu ya kugeuka kutoka
upande mmoja kwenda upande mwingine.
“Henry...” Maimartha alijikuta akiita kwa sauti ya chini, Henry akamsogelea.
“Maimartha, hatimae umerudiwa na fahamu,” alisema Henry huku machozi ya
furaha yakianza kumtoka.
“Nimepooza Henry, siwezi hata kuugeuza mwili wangu kutoka sehemu moja
kwenda nyingine,” alisema Maimartha, bado sauti yake ilikuwa ikisikika kwa
chini kabisa.
Kana kwamba hakuwaona wazazi wake mahali pale. Maimartha alikuwa
akiongea na Henry tu kwani huyo ndiye mtu ambaye alikuwa naye karibu hata
kabla hajapatwa na majanga aliyokuwa ameyapata.
“Naomba unisamehe Maimartha, mimi ndiye niliyesababisha yote haya,”
alisema Henry kwa sauti ya chini, machozi ya furaha yaliyokuwa yakimbubujika
yakabadilika na kuwa machozi yenye maumivu makali moyoni mwake.
“Si kosa lako Henry, ulifanya kile ulichotakiwa kufanya,” alisema Maimartha.
Bado sauti yake ilikuwa ni ya chini mno, kulikuwa na kazi ya ziada kumsikia
kile alichokuwa akikiongea mpaka ulisogeze sikio lako na kumsikiliza kwa
umakini.
Wazazi wake wakakisogelea kitanda kile, japokuwa binti yao alikuwa
amerudiwa na fahamu lakini bado waliendelea kumuonea huruma kitandani
pale. Ule, kwao ukaonekana kuwa mkubwa katika maisha ya Maimartha,
hawakutarajia kama ingetokea siku ambayo Maimartha angekuwa katika hali
hiyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Maimartha...” aliita mama yake, bi Estelina.
“Mama...umekuja kuniona,” alisema Maimartha.
“Nimekuja mwanangu, nisingeweza kukuacha, hali yako inanisikitisha sana, kila
siku nimekuwa nikimuomba Mungu urudi katika hali nzuri,” alisema bi Estelina
huku naye akianza kububujikwa na machozi.
Bado mioyo yao haikupata faraja ile waliyotakiwa kuipata, japokuwa mtoto
wao, Maimartha alikuwa amerudiwa na fahamu na kuweza kuzungumza tena
lakini bado hawakufurahishwa kumuona akiwa katika hali ile, walitaka aweze
kusimama na kutembea kama ilivyokuwa zamani.
“Mungu atatenda tu, nitasimama na kutembea kama zamani,” alisema
Maimartha kwa sauti ya chini.
Japokuwa alikuwa akipitia mateso makali kitandani pale bado moyo wake
ulikuwa na imani kubwa kwamba kuna siku angeweza kusimama tena na
kutembea kama ilivyokuwa zamani.
Hiyo ilikuwa ni imani yake ambayo kila siku ilikuwa ikitenda kazi moyoni
mwake. Mpaka kufikia kipindi hicho, bado aliendelea kujisaidia na kula kwa
kutumia mipira ile ambayo baada ya siku kadhaa ikatolewa na kuanza kutumia
njia ya kawaida.
Hakika Maimartha aliendelea kuwa kwenye mateso makali kupita kawaida.
Alitamani kutembea kama alivyokuwa zamani lakini katika kipindi hicho, ajali
aliyokuwa ameipata ilibadilisha kila kitu.
“Kama Yesu aliwaponya watu waliopooza na kuwafanya vipofu kuona, kweli
atashindwa kuniinua katika kitanda hiki?” aliuliza Maimartha.
“Anaweza. Bado haujamaliza kazi yake, itakupasa uendelee kuwa hai kwa ajili
ya kuifanya kazi yake,” alisema Henry huku kwa mbali akiachia tabasamu.
“Kama ataniponya, ni lini sasa?”
“Siku yoyote. Mungu huwa hawai na wala hakawii, anafanya mambo yake kwa
wakati ulio sahihi.”
“Henry....”
“Naaam.”
“Unanipenda?”
“Umekuwa rafiki yangu kwa kipindi kirefu, ninakupenda Maimartha.”
“Simaanishi urafiki, macho yako yananionyeshea kila kitu, unanipenda?” aliuliza
Maimartha.
“Maimartha....” aliita Henry, akakaa kimya huku akijifikiria jibu la kutoa mahali
hapo.
“Naomba unijibu Henry,” alisema Maimartha.
“Najisikia hivyo moyoni mwangu, sijui kwa nini, nilikuwa nakuchukulia kama
mtu wa kawaida, ila kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, nahisi kukupenda
kwa mapenzi ya dhati,” alisema Henry kwa sauti ya chini, hakutaka wazazi wa
Maimartha wasikie.
“Nimepooza Henry, utanipenda vipi mtu kama mimi?” aliuliza Maimartha.
“Ninaamini utapona tu, na hata kama hautopona, bado hiyo si sababu ya
kunifanya nisikupende maishani mwangu. Najihisi kuwa na mapenzi mazito
kwako, sijajua kwa nini, moyo wangu unaniambia kwamba wewe ndiye mke
sahihi wa maisha yangu,” alisema Henry, yalikuwa maneno yenye kuumiza
mno, yakamfanya Maimartha kububujikwa na machozi.
“Nimepooza Henry,” alisema Maimartha, alikuwa akijisikia uchungu kuwa katika
hali ile.
“Maimartha, Mungu ameruhusu jambo hili kutokea, huwa hafanyi makosa
anaporuhusu jambo fulani litokee. Labda ameruhusu hili kwa kuwa anataka
kuona ni kwa jinsi gani nitaweza kukuoneshea upendo wa dhati kutoka moyoni
mwangu. Maimartha, umepooza, ndiyo, lakini huu ni muda wangu wa
kukuonyeshea mapenzi ya dhati. Ninakupenda Maimartha,” alisema Henry, naye
akajikuta akianza kububujikwa na machozi.
Alikuwa ameamua, kila siku alipokuwa hospitalini hapo,kila alipokuwa
akimwangalia Maimartha, aliuhisi moyo wake kuwa kwenye mapenzi ya dhati
kwa msichana huyo.
Moyo wake ulikuwa umekufa na kuoza, hakutaka tena kuwa na msichana
mwingine zaidi ya Maimartha ambaye alikuwa kitandani akisubiri kufa tu. Moyo
wake ulizidiwa na mapenzi juu ya msichana huyo, hata kama alikuwa
amepooza kitandani, hilo hakujali, kitu alichokuwa akikisikiliza ni mapenzi
yaliyoanza kuchipuka moyoni mwake tu.
Henry alijikuta akiwa kwenye mapenzi ya msichana Maimartha kwa asilimia
mia moja. Kipindi cha kwanza aliona ni kitu kisichowezekana kwa mtu kama
yeye ambaye alikuwa amepanga kutokujiingiza katika mahusiano ya mapenzi
kuanza kumpenda msichana yeyote yule.
Kwa Maimartha, ilimshangaza sana. Hakuwa na wazo la kuwa na msichana
huyo, si kwamba alikuwa amepooza tu bali hata kwenye kipindi alichokuwa
mzima wa afya, bado hakuwa akimpenda, kila siku alimchukulia kama mtu wa
kawaida.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Leo hii, msichana huyo akiwa kitandani huku akiwa amepooza mwili mzima,
akajikuta akianza kuanguka katika mapenzi ya msichana huyo. Bado hakujua
kitu hicho kilisababishwa na nini kwani kama ni ukaribu, aliwahi kuwa karibu na
wasichana wengi lakini jambo hilo halikuwahi kutokea.
“Ninampenda Maimartha, nikisema simpendi nitakuwa najidanganya tu,”
alisema Henry katika kipindi ambacho alikuwa katika chumba cha hoteli.
“Lakini kwa nini imekuwa hivi? Mbona sikuwa nikimpenda toka kipindi cha
nyuma, kwa nini imekuwa leo?” alijiuliza Henry lakini hakupata jibu, suala
lilikuwa ni lilelile kwamba alikuwa kwenye mapenzi ya dhati na msichana huyo.
Siku iliyofuatia, aliamka kitandani na kujiandaa kwa ajili ya kwenda hospitalini
kumuona Maimartha. Siku hiyo hakutaka kwenda mikono mitupu, alipitia katika
duka la maua na kununua maua kadhaa na kadi ya kumtakia afya njema.
Alipofika hospitalini hapo, akamuwekea Maimartha maua yale pembeni na kisha
kumbusu kwenye paji la uso. Japokuwa alikuwa amepooza kitandani, akahisi
kabisa kwamba busu lile lilikuwa limemletea kitu cha tofauti mwilini mwake,
akaachia tabasamu.
“Henry...” aliita Maimartha kwa sauti ya chini.
“Unasemaje kipenzi.”
“Mwili wangu umesisimka.”
“Mwili wako umesisimka?” aliuliza Henry kwa mshtuko.
“Ndiyo. Mwili wangu umesisimka,"alisema Maimartha huku akianza
kububujikwa na machozi
“Hapana. Haiwezekani mwili wako kusisimka na wakati umepooza,” alisema
Henry.
“Kweli Henry, mwili wangu umesisimka, busu lako lilitaka kunirudisha katika
hali ya kawaida,” alisema Maimartha huku akionekana kumaanisha kile
alichokuwa amekisema.
“Hebu jaribu kuunyanyua mkono wako,” alisema Henry na Maimartha kujaribu
kufanya hivyo.
“Siwezi. Nashindwa kufanya kitu chochote kile,” alisema Maimartha kwa sauti
ya chini huku akionekana kuwa na majonzi.
Henry akanyong’onyea, kitendo cha kuona kwamba Maimartha hakuweza hata
kuufanyisha kazi mwili wake kuliendelea kumpa uhakika kwamba bado
msichana huyo hakuwa amepona na hata ile kauli ya kusema kwamba aliuhisi
mwili wake ukisisimka haikuwa kweli.
“Kuna siku utasimama na kutembea tena,” Henry alimwambia Maimartha,
ilionekana kuwa kauli uliyojaa imani kubwa.
“Namtumaini Mungu, nitarudi kama nilivyokuwa,” alisema Maimartha.
Huku mapenzi baina ya watu hao wawili yakianza kuchipuka, hapo ndipo
ambapo Henry akamuomba Maimartha kumwadithia maisha yake ya nyuma
kwa ajili ya kuandaa kitabu cha maisha yake.
Hilo halikuwa tatizo tena, alichokifanya Maimartha ni kumuahidi Henry kwamba
kesho yake ingekuwa siku maalumu ya kuanza kumuhadithia kila kitu
kilichokuwa kimetokea katika maisha yake ya nyuma.
Henry akaifurahi, hicho ndicho kitu alichokuwa akikitaka kwa kipindi kirefu kwa
kuamini kwamba kingempa jina kubwa zaidi ya lile alilokuwa nalo katika kipindi
hicho.
Siku iliyofuata, Henry alikuwa amejiandaa kwa kila kitu, mkono mwake alikuwa
na vitendea kazi vyote kama kalamu na notebook yake tayari kwa kuanza kazi
aliyotarajia kuifanya hospitalini.
Alipofika, mara baada ya maongezi ya hapa na pale likiwepo la kumjulia hali,
Henry akajiweka sawa tayari kwa kusikiliza kile alichokuwa akitaka kuhadithiwa
na Maimartha huku yeye akiwa tayari kwa kuandika baadhi ya vitu.
“Henry, naomba usinichukie,” alisema Maimartha.
“Siwezi kukuchukia, kilichopita, kimepita, kamwe hakiwezi kunifanya
nikuchukie,” alisema Henry.
“Kweli?”
“Niamini.”
“Nashukuru kama unamaanisha.” alisema Maimartha.
Henry akajiweka vizuri, akaishika vizuri kalamu yake tayari kwa kuanza kazi
aliyokuwa akitamani kuifanya kwa kipindi kirefu. Maimartha akameza mate,
kabla hajaanza kuongea kitu chochote kile, machozi yakaanza kumtoka,
alionekana kuumizwa na matukio yake ya nyuma yaliyotokea katika maisha
yake.
“Nitaanza mwanzo kabisa kipindi ambacho mama alikuwa amejifungua.
Sikuona ila alinihadithia kila kitu, nadhani natakiwa kuanzia hapo,” alisema
Maimartha.
“Hakuna tatizo,” alisema Henry huku akijiweka sawa, notebook ilikuwa
mapajani mwake na kalamu mkononi mwake, alichokuwa akikitaka ni kuandika
vitu muhimu ambavyo Maimartha angevitamka mahali hapo.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
1987, Nungi,
Singida.
Msichana mjamzito alikuwa akilia kwa
maumivu makali alipokuwa katika
barabara ndogo iliyokuwa ikielekea
katika Kijiji cha Muhalala mkoani Singida.
Wapita njia waliokuwa
wakipita karibu na njia ile, wakaanza kumfuata msichana
yule aliyekuwa
akiendelea kulia kwa maumivu makali ya kutaka kujifungua
huku
akionekana kuhitaji msaada.
Tayari damu zikaanza
kumtoka kitu kilichowafanya watu wale waliomfuata
kushikwa na wasiwasi
kwamba kuona endapo wasingefanya kile kilichotakiwa
kufanywa basi hali
ingeweza kuwa mbaya.
Kwa haraka sana msichana yule akalazwa chini na
mwanaume mmoja
miongoni mwa watu wale waliomsogelea kukaa katikati ya
miguu yake na
kuanza kumtoa mtoto.
“Sukumaaaa...sukuma....”
alisema mwanaume huyo huku akiwa ameiweka
mikono yake tayari kwa
kumvuta mtoto ambaye alionekana kuwa tayari kutoka.
Haikuwa kazi
nyepesi, yalikuwa ni maumvivu makubwa mno aliyosikia
msichana huyo.
Aliambiwa asukume, aliendelea kusukuma mpaka ukafika
wakati ambacho
akaanzakukosa nguvu kabisa za kuendelea kusukuma.
“Nimechoka,” alisema
msichana yule, sauti yake tu ilimaanisha kile
alichokuwa
akikiongea.
“Sukuma, sukuma,” alisema mwanaume
yule huku mikono yake ikiwa tayari
katikati ya mapaja ya msichana
yule.
Walipoona kwamba kila walipoongea kipole msichana yule hakuwa
akisukuma,
wakaanza kumpiga vibao mfululizo mashavuni kitu
kilichomfanya kuanza kazi
ya kusukuma kwa mara
nyingine.
Ingawa kulikuwa ni njiani kwenye vumbi lakini hakukuwa na
mtu aliyejali hilo,
kitu walichokuwa wakikitaka kwa wakati huo ni
kuona mtoto huyo akizaliwa tu.
Damu hazikukoma, bado ziliendelea
kutoka kama kawaida, njia ikajaa damu na
majimaji ambayo yaliendelea
kutoka kwa msichana yule, baada ya dakika kumi
za maumivu, mwanaume
yule akafanikiwa kumtoa mtoto huyo.
Mtoto alikuwa kimya, macho yake
yalikuwa yamefumba, alichokifanya ni
kukikata kitovu na kisha kuanza
kumtingishatingisha mtoto yule, akaanza kulia
huku akikunjakunja ngumi
hali iliyomfanya mwanaume yule kutoa tabasamu
pana.
“Wa
kike,” alisema mwanaume huyo.
Hapo ndipo walipoanza kushughulikia
suala la kumpeleka katika zahanati
ndogo iliyokuwa katika Kijiji cha
Muhalala.
Kijijini hapo, hakukuwa na maendeleo yoyote yale. Hakukuwa
na usafiri wa
hospitalini, wanakijiji wenyewe hawakuwa wakimiliki hata
baiskeli, ukiachana na
hayo, hata vyakula vyenyewe vilikuwa ni vya
shida mno.
Hali ilikuwa mbaya sana, japokuwa mwanamke yule alikuwa
akitokwa na damu
na hakukuwa na usafiri wowote ule, wakaanza kumbeba
kumpeleka katika
zahanati ya kijiji hicho ambacho kilikuwa na umbali
wa zaidi ya kilomita tatu.
Mwendo ulikuwa mrefu wenye kuchosha lakini
hawakutaka kuacha kuelekea
katika zahanati hiyo. Mwanamke yule
wasiyemjua alikuwa akiendelea kupiga
kelele za maumivu huku damu
zikiendelea kumtoka hali iliyoonyesha kwamba
angeweza kufariki muda
wowote ule.
“Subirini kwanza,” alisema mzee mmoja.
“Kuna
nini?”
“Damu zinamtoka sana. Hatuwezi kupata ngadungadu?” aliuliza
mzee huyo.
“Ngoja tuangalie.”
Mzee mmoja akaingia porini.
Ngadungadu yalikuwa ni aina ya majani ambayo
yalikuwa yakiota sana
porini huku kazi yake kubwa waliyokuwa wakitumia
wanakijiji wa vijiji
vya Singida ni kukaushia damu mwilini.
Hata kama mwili ulikuwa umepata
jeraha la aina gani huku damu zikitoka,
ukipaka majani ya ngadungadu
damu inakata kabisa.
Hayo ndiyo majani waliyokuwa wakiyataka mahali
hapo. Haikuwa kazi ndogo
kuyapata, baada ya dakika tano, mzee yule
akawarudia mahali hapo huku
akiwa na majani hayo ambapo kwa kutumia
meno yao, wakayasaga na kisha
kumpaka mwanamke yule sehemu za siri,
damu ikakata.
“Tuondokeni,” alisema mzee yule ambaye alionekana kuwa
kiongozi na safari
kuendelea.
Kwa shida kubwa, kupata vilima
na kushusha, kutembea katika sehemu
tambarare na mabondeni, mwisho wa
siku wakajikuta wakiingia katika Kijiji cha
Muhalala ambapo
wakampeleka mwanamke yule katika zahanati ndogo huku
akiwa amepoteza
fahamu.
“Mleteni,” alisema nesi mmoja miongoni mwa manesi wanne
waliokuwepo nje
ya zahanati ile.
Msichana yule akachukuliwa
na kupandishwa juu ya kitanda, hakuwa
akijitambua na alikuwa amepoteza
damu nyingi sana njiani, Hapo ndipo
matibabu
yalipoanza.
Kwanza akasafishwa na kulazwa huku dripu ikining’inizwa
juu na maji yakiingia
kidogokidogo kwenye mshipa wake. Baada ya dakika
ishirini, nesi mmoja
akawafuata wanaume wale.
“Mnamfahamu
huyu msichana?” aliuliza nesi mmoja.
“Hapana. Tulikutana naye njiani,
tukaamua kumsaidia,” alijibu mwanaume
mmoja.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo
hamumfahamu kabisa?”
“Ndiyo dada. Kuna nini?
Amekufa?”
“Hapana. Dokta anataka kuongea na ndugu
zake.”
“Labda tuseme sisi ndiyo ndugu zake, kwa hiyo kuna
nini?”
“Nifuateni.”
Yule nesi akaanza kuingia ndani, wanaume
wale watatu wakainuka na kuanza
kumfuta. Nesi akaingia katika chumba
kidogo kilichokuwa kikitumika kama ofisi
ya daktari mkuu wa zahanati
ile, nao wakaingia.
Macho yao yakatua usoni mwa mzee mmoja mwenye
ndevu nyingi aliyekuwa
amevaa miwani usoni. Uso wake haukuwa na
tabasamu hata kidogo, alionekana
kuwa ‘serious’ kila
wakati.
Wanaume wale walipoingia, akaishusha miwani yake na kuanza
kuwaangalia,
aliporidhika, akachukua faili lililokuwa mezani na kuanza
kulifungua.
Akaanza kuyapitisha macho yake ndani ya faili lile,
aliporidhika, akayainua
macho yake na kuanza kuwaangalia
tena.
“Mgonjwa wenu amepoteza kiasi kikubwa cha damu, inabidi
asafirishwe
kuelekea Singida Mjini,” alisema dokta yule.
“Na
vipi kuhusu mtoto wake?”
“Mtoto wake tumemwangalia, anaendelea vizuri
japokuwa naye tulimkuta na
tatizo kidogo, ila anaendelea vizuri.
Itampasa asafirishwe na mama yake
kuelekea Mjini,” alisema dokta
yule.
“Hilo si tatizo. Gari si lipo?”
Gari lipo ila kwa sasa
lipo Mwasa, kwenye saa nane mchana watakuwa
wamekwishafika hapa. Si
unajua tuna gari moja tu la hospitali,” alisema
dokta
yule.
“Basi hakuna tatizo.
Tutasubiri.”
“Sawa. Ila inabidi mchangie mafuta,” alisema dokta
yule.
“Hakuna tatizo.”
Ilipofika saa nane mchana, gari aina
ya ‘defender’ likasimama nje ya hospitali
ile, kwa haraka manesi
waliokuwepo ndani ya zahanati wakatoka huku wakiwa
wamembeba msichana
yule na mtoto wake, wakamuweka ndani ya gari lile.
“Na sisi si
tunakwenda?” aliuliza mwanaume mmoja.
“Ndiyo. Ila hela ya mafuta iko
wapi?” aliuliza dokta yule. Mwanaume mmoja
akamfuata na kumpa kiasi
cha shilingi mia tano ambacho walikuwa
wamechanga na dokta kumpa
dereva.
“Ongozana nao,” alisema dokta akimwambia nesi
mmoja.
Safari haikuwa fupi, kutokana na ubovu mkubwa wa barabara
iliyokuwa na
mashimo mengi, gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa
taratibu sana hali
iliyowapelekea kuchoka kupita
kawaida.
Kila wakati, walikuwa wakimwangalia mwanamke yule waliyekuwa
wakimsaidia,
kwa muonekana wake alionekana kuwa binti mdogo ambaye kwa
kukadiria tu
alikuwa na miak isiyozidi ishirini.
Vichwa vyao
vilikuwa na maswali mengi ya kuuliza lakini katika kipindi hicho,
kila
mmoja alikuwa kimya akiifuatilia safari hiyo ambayo kwa ujumla
ilionekana
kuwa kero kutokana na mashimo mengi
barabarani.
Walichukua masaa matatu, wakafika Singida Mjini ambapo
wakampeleka katika
Hospitali ya Mkoa na matibabu kuanza rasmi huku
wanaume hao wakibaki
kwenye mabenchi.
“Hapa tutachelewa.
Tukatoeni taarifa kwa manesi ili kama vipi tuondoke,”
alishauri
mwanaume mmoja.
“Hakuna tatizo,” aliunga mkono mwanaume mwingine na
wote kumfuata dokta
na kumweleza kila kitu kuhusiana na safri yao
mpaka walipomkuta mwanamke
huyo.
“Hakuna tatizo. Nyie
nendeni, nawaahidi atapona tu,” alisema dokta huyo na
wanaume wale
kuondoka zao.
Namtaka mtoto wangu,
dokta, mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza msichana yule
kwa sauti ya juu
iliyoonekana kuwa kelele hospitalini hapo.
“Nyamaza, mtoto wako yupo
salama,” alisema nesi mmoja.
“Yupo wapi? Nionyesheeni mtoto wangu
kwanza,” alisema msichana yule.
Kwa sababu alikuwa akipiga sana
kelele, walichokifanya manesi waliokuwa
ndani ya chumba kile ni
kumletea mtoto wake ambaye alionekana kuwa katika
hali ya
usafi.
Msichana yule akaonyesha tabasamu pana usoni mwake, kumuona
mtoto wake
kukampa faraja kubwa, akamchukua na kuanza kummwagia mabusu
mfululizo
usoni
“Nakupenda mwanangu,” alisema msichana
yule.
Kuanzia siku hiyo, msichana huyo akawa mtu wa kukaa hospitalini
hapo. Uso
wake ulionekana kuwa na majonzi makubwa, hakuamini kama
aliweza
kujifungua mtoto yule salama.
Kila alipokuwa
akimwangalia, alikuwa akilia tu. Moyo wake ulijawa na
maumivu, maisha
yake ya nyuma yalimuumiza kupita kawaida, hakuamini
kama mwisho wa
siku alikuwa amemshika mtoto wake mikononi mwake.
Kila walipokuwa
wakimwangalia, manesi walikuwa wakimshangaa. Kwa
muonekano wake tu,
alionekana kuwa na kitu moyoni mwake, alionekana
kuumizwa na kitu
fulani lakini hakuwa radhi kukizungumza mahali hapo.
Manesi hawakutaka
kukaa kimya, walichokifanya ni kuanza kumdadisi ili kujua
ni kitu gani
kilichokuwa kikiendelea kwa msichana yule, kwa nini
alijifungulia
njiani? Alikuwa akitoka wapi? Na ndugu zake walikuwa
wapi?
“Nilifukuzwa na baba baada ya kumwambia kwamba nilikuwa na
mimba,”
alisema msichana yule kwa sauti ya chini.
“Umetoka
wapi?”
“Kijijini kwetu.”
“Wapi?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakutaka kulijibu
swali hilo, akabaki kimya kwa muda. Kilio cha kwikwi kilianza
kusikika
kutoka kwake. Alilia kwa sekunde kadhaa, akajitahidi kunyamaza
na
kuyafuta machozi yake.
“Nimetokea Nungi,” alijibu
msichana yule.
“Sawa. Ni nani aliyekupa ujauzito
huu?”
“Sijui. Ninachokumbuka ni kwamba kuna siku nilibakwa na vijana
wanne kijijini
kwetu wakati natoka kwenye mkutano wa injili,” alisema
msichana yule.
“Ulibakwa na vijana
wanne?”
“Ndiyo.”
“Ikawaje sasa?”
“Nilipokwenda
nyumbani, sikuwaambia wazazi, nilijifungia chumbani nikilia tu
kwani
nilijisikia maumivu makubwa moyoni mwangu. Nilimuomba Mungu
anipe
amani na furaha kama niliyokuwa nayo lakini ilishindikana
kabisa. Baada ya
miezi miwili, kwenda kupima, nikaambia nina
ujauzito,” alisema msichana huyo.
“Pole sana. Wazazi wako
wameokoka?”
“Hakuna aliyeokoka. Nilipoamua kuokoka, wakanitenga, wao
ni wapagani,
hawalijui kanisa wala msikiti, wapowapo tu. Kwa kipindi
kirefu walikuwa
wakinisisitizia kwamba sikutakiwa kwenda kanisani,
niliwabishia sana na ndiyo
maana hata nilipowaambia kwamba nina mimba,
wakanifukuza,” alisema
msichana huyo.
“Ukaenda kuishi wapi
baada ya hapo?”
“Nilikuwa katika cha Mbwenini, huko, nikajiunga na
kikundi kimoja cha ngoma
kilichokuwa kikimilikiwa na mwanamke mmoja
aliyekuwa akiitwa Ebeza.
“Nikaishi na mwanamke yule kwa miezi kadhaa,
mimba yangu ilipoanza
kuonekana ndipo hapo alipoanza kuninyanyasa.
Siku moja kabla ya kujifungua,
nikaamua kutoroka kwani mambo yalikuwa
magumu mno,” alisema msichana
huyo.
“Pole sana. Unaitwa
nani?”
“Naitwa Estelina.”
“Pole Estelina,” alisema nesi
mwingine.
“Asante dada.”
Estelina aliendelea kukaa
hospitalini pale kwa takribani siku mbili na ndipo
aliporuhusiwa
kuondoka nyumbani. Siku hiyo ilikuwa ni ya majonzi kwake,
hakuwa na
sehemu ya kwenda na wala hakutaka kurudi nyumbani kwao wala
kwa bi
Ebeza.
Japokuwa hakutaka kwenda huko lakini hakuwa na sehemu yoyote
ile ya kuishi
jambo lililomfanya kuwa na wakati mgumu
mno.
Manesi walipoligundua hilo, wakaamua kuchanga fedha na kisha
kumgawia,
kilikuwa ni zaidi ya shilingi elfu moja, hicho ndicho
ambacho alitakiwa kuanza
nacho maisha. Kwa mwaka huo 1988, kiasi hicho
kilikuwa kikubwa sana.
“Nitabaki hapahapa mjini, mpaka nipate fedha
zaidi,” alisema Estelina.
Huo ndiyo uamuzi aliokuwa ameufikia muda
huo, alitaka kuendelea kubaki hapo
mjini kwa ajili ya kukusanya fedha
ili akizipata ajue ni kitu gani
kilichokuwa
kikifuatia.
“Nitafanya kazi baa,” alijisemea
Estelina.
Hakutaka kuchagua kazi, hakuwa na sehemu yoyote ya kulala na
wala hakuwa
na uwezo wowote wa kupanga chumba hivyo maisha yake kwa
wakati huyo
alitegemea kuishi mitaani tu.
Mtoto, kwake
akaonekana kuwa usumbufu mkubwa, kuna wakati alitamani
kumtupa sehemu
ili aendelee na maisha yake lakini kuna wakati roho ya
huruma ilikuwa
ikimjia na kuona kwamba kile nacho kilikuwa ni kiumbe
cha
Mungu.
Akaamua kumvumilia, japokuwa alikuwa mtoto wa
kulialia kila wakati lakini
hayo yote akaona si kitu, hakuona kama
hizo zilikuwa sababu zilizojitosheleza
za kumtupa mtoto
wake.
“Naomba kazi,” alisema Estelina, alikuwa katika chumba kimoja
ambacho
kilitumika kama ofisi ya meneja wa baa ya Mapesapesa iliyokuwa
hapo Singida
Mjini.
“Nani kakwambia kuna kazi hapa?”
aliuliza meneja huyo, alikuwa mzee mwenye
mvi huku mdomo wake
ukionyesha kwamba alikuwa mzuri wa kuvuta tumbaku.
“Nimeona tangazo
hapo nje.”
“Si kwa mabinti waliozaa, tunataka wasichana
wabichiwabichi, ili hata
wakiangaliwa na wateja, wavutiwe,” alisema
meneja yule, mzee Mapunda.
“Naomba unipe nafasi,” aliomba Estelina
huku akipiga magoti.
“Hakuna kazi kwa wakimama, tunataka
mabinti.”
“Ila naweza kuwaburudisha wateja hata kwa kuimba,” alisema
Estelina.
“Unajua kuimba?”
“Najua.”
“hebu imba
kidogo nisikie,” alisema mzee Mapunda.
Hapo ndipo Estelina alipoanza
kuimba. Sauti yake ilikuwa ni ya kipekee mno,
kila alipozidi kuimba
zaidi na ndipo mzee Mapunda akaonekana kuvutiwa zaidi
mpaka wakati
mwingine kutikisa kichwa chake, juu kwenda chini, chini
kwenda
juu.
“Safi sana. Nilikuwa natafuta muimbaji, nahisi
utatufaa,” alisema meneja
Mapunda.
Kwa sababu alikuwa na
kipaji cha kuimba, hiyo ikaonekana kuwa nafasi yake
ya kipekee ya kuwa
muimbaji ndani ya baa hiyo. Akapewa chumba ambacho
alikuwa akilala na
wenzie wawili ambao kuishi na Estelina ilionekana kuwa
mzigo
mkubwa.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila wakati mtoto
wake alikuwa akilia tu, haikujalisha kama ni usiku au
mchana. Mtoto
akawa kero kwa wenzake, kuna wakati walikuwa wakimwambia
ukweli kwamba
mtoto wake alikera lakini kila siku walipoona hali hiyo
inazidi,
wakaamua kukaa kimya huku wakikereka mioyoni
mwao.
Kila siku kazi yake kubwa katika baa hiyo ilikuwa ni kuimba tu.
Japokuwa
alikuwa akipenda sana kufanya hivyo lakini kazi ile
ikaonekana kuwa kero
kwake.
Kila wakati wanaume waliokuwa
wakija hapo kunywa walikuwa
wakimshikashika makalio yake na hata
wengine wakidiriki kumwambia waende
wakalale pamoja kitu ambacho kwake
hakikuweza kukubalika.
Kutokana na mvuto wa nyimbo nzuri alizokuwa
akiziimba, wateja wengi
wakaanza kumiminika ndani ya baa hiyo, sifa
zikaanza kusambaa kila sehemu
kwamba ndani ya baa hiyo kulikuwa na
binti mdogo aliyekuwa akiimba nyimbo
nzuri.
“Huwa ninakuja
hapa kwa ajili ya huyu mwanamuziki tu,” alisema jamaa
mmoja ambaye
alikuwa amekaa kwenye meza moja na wenzake watano.
“Ana sauti nzuri
sana. Unajua sauti hii inaweza kumtoa nyoka pangoni!”
alisema jamaa
mwingine na wote kuanza kucheka.
Mameneja waliokuwa wakimiliki baa
nyingine walipoona hivyo, nao wakaanza
kuwaweka waimbaji katika baa
zao. Hiyo haikusaidia, sauti ya Estelina ilikuwa
ni ya kipekee sana
ambapo kila alipokuwa akiimba, hata kama ulikuwa wapi,
pale
unapoisikia tu ilikuwa ni lazima uende huko kushuhudia.
Baa ya
Mapesapesa ikaanza kupata watu wengi, hata wale ambao
hawakuwa
wanywaji, kila walipokuwa wakipita na kumuona Estelina
akiimba, walisimama
na kuanza kumsikiliza.
Taarifa juu ya
Estelina hazikuishia hapo, kila siku zilizidi kusambaa
sehemu
mbalimbali kwamba kulikuwa na msichana aliyekuwa akiimba kwa
sauti nzuri
kama malaika jambo lililoendelea kuwakusanya watu ndani ya
baa hiyo.
Wageni kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine, kila
walipokuwa wakiingia
ndani ya Singida, waliambiwa kuhusu Estelina kitu
kilichowafanya kumiminika
zaidi ndani ya baa hiyo.
“Aiseee,
huyu dada anaimba balaa, sauti yake naifananisha na Diana
Rose,”
alisema mwanaume mmoja na kumtaja mwanamuziki huyo wa
Marekani
aliyekuwa akivuma sana kipindi hicho.
“Hebu
isikilize sauti yake, hii ni sauti ya mrembo haswa,” aliingilia
jamaa
mwingine.
Mbali na kipaji cha uimbaji alichokuwa
nacho, kwa uzuri, Estelina alikuwa
ameumbika sana. Alikuwa mrefu wa
saizi ya kati, mweupe, nyuma alikuwa
amejaziajazia huku sura yake
ikiwa ni ya kitoto ambayo kwa wazungu
wangeiita
‘Babyface’.
Ukiachana na hayo, Estelina alikuwa na mguu iliyojaa,
kiuno chake kilionekana
wazi na kila alipokuwa akipiga hatua, huku
nyuma milima miwili ilikuwa
ikipishana, huu ukienda huku, ule
unakwenda kule.
Mbali na umbo hilo, kuwa na mtoto, bado Estelina
alikuwa na kifua kizuri.
Matiti yake hayakuwa yamelala kama ilivyokuwa
kwa wanawake wengine
waliozaa, chake, kilikuwa kimesimama kitu
kilichoonyesha kama alikuwa
ametoka kuvunja ungo juzi.
Umbo
lake liliwatoa udenda wanaume wengi kitu kilichowapelekea
umtongoza
mara kwa mara lakini msichana huyo hakutaka kuwaelewa
kabisa.
Mameneja wa baa nyingine wakagundua kwamba mafanikio ya Baa
ya
Mapesapesa ilikuwa ni sauti nzuri ya Estelina. Japokuwa walikuwa
na
wasichana wao waliokuwa wakiimba lakini kwa Estelina alionekana
kuwa
tofauti kabisa.
Waliwaita wasichana kujaribu kuimba,
wengi waliweza lakini kamwe
hawakuufikia uwezo wa sauti nzuri
iliyokuwa ikisikika kutoka kwa Estelina.
“Tunataka uje kufanya kazi
kwetu,” alisema jamaa mmoja, alikuwa meneja wa
Baa ya
Polepole.
“Mtanilipa shilingi ngapi kwa siku?” aliuliza
Estelina.
“Kwani hapa unalipwa kiasi gani?”
“Elfu
moja.”
“Sisi tutakupa elfu moja na mia tano.”
“Sawa. Ngoja
nijifikirie.”
“Tukupe muda gani?”
“Wiki
moja.”
Dunia haikuwa na siri, japokuwa walikuwa wamekaa wawili tu
wakiongea,
baada ya siku mbili maneno hayo yakamfikia mzee Mapunda
ambaye kwa
harakaharaka akamuita Estelina ofisini na kuanza kuongea
naye.
“Naomba usituache, nitakulia elfu mbili na mia tano kwa siku,”
alisema mzee
mapunda.
“Hiyo tu?” aliuliza
Estelina?”
“Na chumba. Kitakuwa chumba cha peke yako, nitamuajiri
mfanyakazi awe
anakaa na mtoto wako,” alisema mzee
Mapunda.
“Hakuna tatizo.”
Sauti yake nzuri iliendelea
kuwavutia watu wengi. Mzee mapunda
alikwishagundua kwamba wateja wengi
walimiminika katika baa yake kwa ajili
ya Estelina tu na ndiyo maana
hakutaka kumpoteza mtu huyo.
Alijiahidi kumfanyia kila kitu
kuhakikisha kwamba anamshikilia, anakuwa wake
na kuendelea kuwavutia
wateja mahali hapo. Baa ya Mapesapesa iliendelea
kukua zaidi, kila
siku watu walikuwa wakimiminika katika baa hiyo, ghafla bin
vuu,
Estelina akajikuta akianza kuukwaa ustaa hapo Singida Mjini kutokana
na
umahiri wake katika kuimba.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Estelina
aliendelea kuimba kama kawaida, akapata umaarufu mkubwa huku Baa
ya
Mapesapesa ikizidi kupata wateja wengi. Sauti yake bado iliendelea
kuwa
kivutio kwa watu wengi. Jina lake lilikua na kuheshimika kila
kona.
Sifa zake, mbali na Singida, watu kutoka Dodoma wakaanza kusikia
mengi
kuhusu Estelina kitu kilichowafanya kusafiri kuelekea huko, nao
walitaka kuisikia
hiyo sauti ambayo ilijulikana kama ya kumtoa nyoka
pangoni.
Walipofika huko, waliamini kile kilichokuwa kimeongelewa,
sauti yake ilikuwa ni
zaidi ya ile iliyozungumziwa kwamba ni ya kumtoa
nyoka pangoni.
Kabla ya Estelina kufika katika baa hiyo, kwa siku
zilikuwa zikiletwa kreti za
pombe kumi na mbili lakini mara baada ya
msichana huyo kufika katika baa
hiyo, bosi, mzee Mapunda akaanza
kuleta zaidi ya kreti mia mbili kwa siku na
zote zilikuwa
zikiisha.
Yalikuwa ni mafanikio makubwa na ndiyo maana kila siku
alikuwa akipambana
kuhakikisha kwamba anambakisha Estelina ndani ya
baa yake, hakutaka aende
sehemu yoyote ile.
Kwa Estelina,
maisha yake yalikuwa yamebadilika, alianza taratibu kupokea
kiasi
kidogo cha fedha na mwisho wa siku dau lilipanda na kufikia kiasi
cha
shilingi elfu tano.
Hiyo ilikuwa mwaka 1991, kiasi hicho
kilikuwa kikubwa ambacho kiliyabadilisha
maisha yake kwa ujumla. Mtoto
wake, Maimartha alikuwa amekua, kwa wakati
huo alikuwa na miaka
mitatu.
“Estelina, ninataka kukuoa, haki ya Mungu tena,” alisema
Steven, jamaa
aliyekuwa akiendesha magari ya mizigo kutoka Singida,
kwenda Dar na sehemu
nyingine nchini Tanzania.
“Unataka
kunioa?” aliuliza Estelina.
“Ndiyo, nataka nikuweke ndani kabisa,
halafu tunakwenda Mjini Dar es Salaam
kuishi pamoja,” alisema
Steven.
“Hapana, sitaki kwenda Dar.”
“Kwa nini Estelina?
Unajua Dar kuzuri, ukienda kule, kuna baa nyingi, utakuwa
ukiimba na
kulipwa kiasi kikubwa cha fedha,” alisema Steven.
“Sitaki kwenda Dar
na sitaki kuolewa.”
Steven alikuwa mmoja miongoni mwa vijana wengi
waliokuwa wakimtaka
kimapenzi Estelina. Hakuwa msichana mwepesi wa
kuwakubali wanaume, kila
alipokuwa akiambiwa kwamba anataka kuolewa,
Estelina alikuwa akikataa
kabisa.
Aliyathamini sana maisha
yake, aliwafahamu watu wengi ambao walikuwa
wakiteseka ndani ya ndoa
zao, walikuwa wamefuatwa vizuri na wanaume kwa
ahadi ya kuolewa, baada
ya kuingia kwenye ndoa, matatizo yalianza.
Yeye kama yeye alikuwa
akijiweza kimaisha, alilala sehemu nzuri, alikuwa vizuri
na alilipia
matumizi ya kila kitu alichokuwa akikihitaji, hakuona kama kulikuwa
na
sababu ya kuolewa.
Kila mwanaume aliyekuwa akimfuata, alimkatalia kwa
kumwambia kwamba
alijisikia vizuri kuishi peke yake kuliko kuishi na
mtu.
Kuimba katika baa ya Mapesapesa hakukuisha, kila siku watu
walikuwa
wakikusanyika katika baa hiyo, viti havikutosha na hata eneo
lilikuwa dogo
lakini mzee Mapunda hakutaka kubadilisha eneo, alitaka
kubaki hapohapo.
Mwaka wa tano ulipoingia, bado Estelina alionekana
kuwa msichana mrembo
sana ambaye alimvutia kila mtu aliyekuwa
akimwangalia. Figa yake ilikuwa
matata, nyuma alikuwa amejaa, sura
ilikuwa nzuri.
“Dada habari yako,” alimsalimia kijana mmoja, huyu
alikuwa Paul.
“Nzuri. Mambo vipi.”
“Poa tu. Wewe ndiye
muimbaji hapa?” aliuliza kijana huyo.
“Ndiyo mimi. Kuna
lolote?”
“Yeah! Nilipita hapa jana, niliisikia sauti yako, hakika
umebarikiwa,” alisema
kijana
yule.
“Nashukuru.”
Estelina hakuwa na muda wa kuongea na
wanaume, kila mwanaume aliyekuja
mbele yake, aliongea naye kidogo na
kuondoka zake. Aliwajua vilivyo wanaume,
wengi walikuwa wakija katika
sura ya upole lakini mioyo yao ilikuwa mikali
zaidi ya
simba.
Mwanaume huyo, Paul hakuacha kuja mahali hapo, kila siku
alikuwa akija na
kumsalimia Estelina, alipoanza kuimba tu, Paul
alikuwa akiondoka zake.
Hali hiyo ikaendelea kwa mwezi mzima mpaka
Estelina akaijua ratiba kamili ya
Paul kuja hapo baa na kuongea naye.
Kwake, kijana Paul alionekana kuwa
tofauti na wanaume
wengine.
Paul alikuwa kijana mpole kupita kawaida, kila alipokuwa
akiongea naye,
alikuwa akisikika kiupole sana. Japokuwa alikuwa
amemzoea kwa kipindi kirefu,
lakini kamwe kijana huyo hakuwahi
kumtongoza, alikuwa akipiga naye stori
kawaida tu na kuondoka
zake.
Hakuwa mlevi, kila alipofika hapo baa, alikuwa akiagiza soda na
chakula,
anakula, Estelina alipokuwa akitaka kuimba, ananyanyuka na
kuondoka zake.
Taratibu, Estelina akaanza kuumia moyoni, alitamani
sana Paul aisikie sauti
yake kila alipokuwa akiimba lakini mwanaume
huyo alikuwa akiondoka kila
Estelina alipotaka
kuimba.
Tayari moyoni mwake kukaanza kujengeka kitu cha tofauti sana,
kila alipokuwa
akimuona Paul, alijisikia kabisa kuwa na furaha zaidi
na kila mwanaume huyo
alipokuwa akiondoka, moyoni alijisikia
mnyonge.
Hali hiyo ilimuumiza mno, alivumilia zaidi lakini mwisho wa
siku akashindwa
kuvumilia, alichokifanya ni kumsubiria mwanaume huyo
afike tena hapo baa na
kumuuliza ni kitu gani kilichokuwa kikimsibu
mpaka kuondoka kabla ya yeye
kuanza kuimba.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika siku hiyo
ambayo alikuwa akimsubiri Paul kwa hamu kubwa, hakuweza
kutokea mahali
hapo. Estelina akaanza kupatwa na wasiwasi, hakujua ni kitu
gani
kilikuwa kimemsibu.
Siku hiyo akajipa moyo kwa kuona kwamba
inawezekana alikuwa bize,
akasubiri siku inayofuatia, nayo hakutokea,
Estelina akanyong’onyea. Hatimae
wiki nzima ikapita, bado Paul
hakutokea.
Mwezi wa kwanza ukatimia, mwezi wa pili ukaingia na wa tatu
kukatika, Paul
hakurudi tena hapo baa kitu kilichomsononesha mno
Estelina.
“Paul, upo wapi? Rudi mahali hapa japo hata siku moja tu,
nimekukumbuka
mno,” alisema Estelina, maneno hayo hayakusaidia kitu
chochote, mwezi wa
sita ukakatika, Paul hakuonekana machoni
mwake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment