Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

LET'S CALL IT A NIGHT - 3

 





    Simulizi: Let's Call It A Night

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Mawazo juu ya Paul yaliendelea kumtesa, hiyo haikuwa kawaida kabisa kutokea katika maisha yake. Kila siku alipokuwa akikaa chini moyo wake ulikuwa ukimfikiria paul ambaye hakurudi tena machoni mwake.

    Kila siku akawa mtu mwenye mawazo tu, mpaka mwaka unakatika bado Paul hakuwa amerudi ndani ya baa hiyo. Hilo lilimsumbua sana moyoni mwake, alikuwa amekwishajaribu kila njia kumtafuta mwanaume huyo lakini hakufanikiwa kumuona.

    Kuna kipindi alifikiria kwamba ingesaidia sana kama angekuwa na angalau picha yake ili kila atakapokuwa akiiangalia basi aweze kufarijika, kwa wakati huo, hakuwa hata na picha.

    Mwaka ukakatika, kwenye mwezi wa nne, huku akiwa hana hili wala lile, kwa mbali alimuona kijana mmoja mtanashati amekaa katika moja ya viti vilivyozunguka meza.

    Kwanza akashtuka, japokuwa mtu huyo alikuwa kwa mbali lakini alipomwangalia vizuri, aliweza kumgundua, alikuwa Paul. Huku akionekana kuchanganyikiwa kwa furaha, Estelina akaanza kumfuata Paul kule alipokuwa, alipomkaribia, akapokelewa na tabasamu pana.

    Bila kutarajia, Estelina akajikuta akimfuata Paul na kumkumbatia jambo lililowaacha midomo wazi watu waliokuwepo mahali hapo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimekukumbuka Paul,” alisema Estelina huku akibubujikwa na machozi ya furaha.

    “Nimekukumbuka pia Estelina,” alisema Paul.

    Muda wote Estelina alionekana kuwa na furaha tele, hakuamini kama mwanaume aliyekuwa akiusumbua moyo wake hatimae alikuwa amefika katika baa hiyo. Kama kawaida yake, hakuwa mnywa pombe, kinywaji alichokiagiza kilikuwa kilekile cha siku zote, soda.

    “Ulikuwa wapi? Mbona uliadimika sana?” aliuliza Estelina.

    “Nilikwenda Dar es Salaam, siishi Singida kwa sasa, ninaishi Dar,” alisema Paul.

    Siku hiyo walikaa na kuongea mengi, katika kipindi chote cha maongezi, Estelina alikuwa akimsisitizia Paul kutokuondoka mpaka pale atakapomaliza kuimba. Hilo halikuwa tatizo kwa paul, akamsubiria.

    Aliimba kwa kuzikonga nyoyo za watu, aliimba kwa manjonjo makubwa huku wakati mwingine akipiga hatua kumfuata Paul pale alipokuwa amekaa na kumuimbia karibu yake.

    Paul alikuwa mwanaume mwenye aibu nyingi, kila alipokuwa akisogelewa na kuimbiwa, alikuwa akichekacheka tu huku akijisikia aibu. Walevi hawakuwa na hiyana, kila Estelina alipokuwa akipita, walikuwa wakimshika makalio kitu ambacho kwa Paul, kilimuumiza kupita kawaida. Alipomaliza kuimba, akamfuata Paul na kuanza kuongea naye huku akisubiria ngwe ya pili ya uimbaji.

    “Estelina.....” aliita Paul.

    “Niambie.”

    “Una sauti nzuri sana.”

    “Asante Paul.”

    “Kuna kitu unatakiwa kufanya, hakika sauti yako itakuwa nzuri zaidi,” alisema Paul.

    “Kitu gani?”

    “Mungu amekupa sauti hii si ya kumuimbia shetani na kumpa utukufu, yakupasa kumuimba Yeye aliyekupa sauti hii,” alisema Paul.

    “Unamaanisha nini?”

    “Yakupasa kuokoka na kumuimbia Mungu,” alisema Paul.

    Estelina akashusha pumzi na kumwangalia vizuri Paul. Ni kweli aliona kwamba mwanaume huyo aliongea suala moja la muhimu sana. Katika kipindi cha nyuma, alikuwa ameokoka lakini maisha ya shida aliyokuwa akiishi yakamfanya kuuacha wokovu na kujiingiza katika maisha ya kumtumikia shetani.

    Hilo, kwake likaonekana kuwa gumu. Alikuwa maarufu Singida nzima kutokana na nyimbo alizokuwa akiziimba baa, angeeleweka vipi endapo angeamua kuokoka na kuanza kuimba kanisani, hakutaka kukubaliana nalo, alihitaji kukusanya fedha zaidi.

    “Haiwezekani.”

    “Estelina, niamini, utabarikiwa zaidi,” alisema paul.

    “Yaani niurudie wokovu?”

    “Kwani uliwahi kuokoka kabla?” aliuliza Paul na Estelina kuanza kumuhadithia historia ya maisha yake, Paul akashusha pumzi.

    “Fedha si kila kitu Estelina, mrudie Mungu wako,” alisema Paul.

    Haikuwa kazi kubwa kumshawishi Estelina amrudie Mungu na wakati katika maisha aliyokuwa akiishi alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kukusanya fedha nyingi.

    Japokuwa hakumruhusu mwanaume yeyote kumvua nguo yake lakini kupitia uimbaji, kushikwashikwa makalio na walevi kulimpatia sana fedha mbali na mshahara aliokuwa akilipwa kila siku.

    Ushawishi wa Paul ukaanza kufanya kazi, maneno yake yakaanza kumuingia Estelina na mwisho wa siku akakubaliana kuokoka, ila hakutaka kukaa hapo, alitaka kuambatana na Paul popote atakapokwenda.

    “Basi hakuna tatizo, tutakwenda Dar es Salaam, nimepanga vyumba viwili, tutaishi pamoja,” alisema Paul, na bila shaka, Estelina akakubaliana naye.

    ****

    Katika kipindi ambacho Estelina alikuwa akiaga, mzee Mapunda alitamani kulia, maneno aliyokuwa akiongea Estelina yalimuumiza mno. Alipenda kuwa na msichana huyo, hakutaka aende sehemu yoyote ile kwani yeye ndiye alikuwa chanzo cha mapato makubwa katika baa yake ya Mapesapesa.

    Kuondoka kwake mahali hapo likaonekana kuwa pigo kubwa, hii ilimaanisha kwamba kusingekuwa na idadi kubwa ya watu kama iliyokuwa ikifika mahali hapo kila siku.

    Japokuwa alimsisitiza sana Estelina kubaki katika baa yake lakini msichana huyo alikataa, alimwambia ukweli kwamba katika wakati huo aliamua kumrudia Mungu hivyo asingeweza tena kuimbaimba katika baa hiyo, alitaka kujikita zaidi kanisani.

    Kwa miaka sita aliyokuwa amekaa katika baa hiyo, mzee mapunda alikuwa amejiingizia kiasi kikubwa mno kupitia Estelina, alijenga nyumba nyingi, alifungua baa nyingine katika sehemu mbalimbali hapo Singida, yaani mafanikio yote hayo, yalitokana na sauti ya Estelina.

    Leo, msichana huyo alikuwa akiaga na kutaka kuondoka kuelekea Dar es Salaam, japokuwa alikuwa akiumia moyoni mwake lakini hakutaka kumzuia kwani kitu alichokuwa akitaka kwenda kukifanya ni kumtumikia Mungu na si kufanya kazi katika baa nyingine, akakubaliana naye.

    “Ila hauendi kwenye baa nyingine?” aliuliza mzee Mapunda huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Hapana, Ninakwenda Dar es Salaam kumtumikia Mungu. Mimi na baa urafiki wetu umeishia hapa,” alisema Estelina.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati mwingine alitamani ile ingekuwa ndoto, alimpenda sana msichana huyo kwa sababu alimpa mafanikio makubwa maishani mwake, hakutaka kumuacha kabisa lakini kipindi hicho, msichana huyo alionekana kuwa radhi kuondoka, alionekana kuwa na kiu kubwa ya kumtumikia Mungu.

    “Kama ni kweli, nakutakia maisha mema,” alisema mzee Mapunda huku akimgawia Estelina kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kuanzishia maisha huko atakapokuwa.

    Siku iliyofuata, Estelina, Paul na mtoto wake, Maimartha aliyekuwa na miaka sita walikuwa ndani ya treni wakielekea Dar es salaam. Moyoni mwake alikuwa na furaha sana kwani toka azaliwe alikuwa akisikia tu kuhusu mkoa huo lakini hakuwa amewahi kufika.

    Kutoka Itigi walipopandia treni, walichukua siku moja, kesho wakawa wamefika Dar es Salaam ambapo moja kwa moja wakapumzika nyumbani na kesho kuelekea katika Kanisa la Praise and Worship alipokuwa akisali Paul na kuongea na mchungaji kuhusu Estelina.

    “Yesu ashindwi kitu, hatimae amemrudisha kundini mtumishi wake,” alisema mchungaji wa kanisa hilo lililokuwa Manzese, mchungaji Mushi.

    “Ila hana pa kukaa, ningeomba niweze kuishi naye mpaka hapo atakapopata chumba cha kukaa,” alisema Paul.

    “Hakuna tatizo. Katika kipindi chote atakachokuwa nyumbani kwako, ishi naye kama dada na kaka,” alisema mchungaji Mushi.

    “Hakuna tatizo.”

    Waliishi pamoja kwa muda wa mwezi mmoja, na ndipo Estelina alipopata chumba ambacho hakikuwa mbali na hapo alipokuwa akiishi Paul. Kila siku walikuwa wakionana na kwenda kanisani pamoja huku wakati mwingine wakikutana na kuanza kumuomba Mungu pamoja.

    Kwa sababu alikuwa akipenda kumuona mtoto wake akisoma, Estelina akaamua kumuanzisha Maimartha darasa la kwanza katika shule ya Turiani iliyokuwa Magomeni.

    Kila siku, watu hao walikuwa wakikutana nyumbani na kufanya maombi kwa ajili ya maisha yao. Waliendelea kuwa katika hali hiyo kwa miezi sita tu,hapo ndipo walipokubaliana kwamba sasa walitakiwa kuoana na kuishi pamoja kama mume na mke. Baada ya miezi mitano, harusi ndogo ikafungwa na wawili hao kuoana.



    Japokuwa alikuwa ameishi katika maisha ya kawaida mkoani Singida, alipofika jijini Dar es Salaam na mama yake kuamua kumrudia Mungu, mtoto Maimartha akaanza kuishi maisha ya kilokole.

    Kila siku ya Jumapili alikuwa akipelekwa kanisa asubuhi na mapema kwa ajili ya kuwahi darasa la Sunday School kwa watoto kwa kuamini kwamba kupitia darasa hilo hakika maisha yake yasingeweza kuharibika huko mbeleni.

    Umri wake ulikuwa ni miaka sita tu lakini alionekana kuwa na uwezo mkubwa darasani. Katika kila mitihani waliyokuwa wakifanya shuleni, alikuwa hakosi kwenye idadi ya watu kumi ambao walikuwa wakifanya vizuri.

    Alikuwa na umri mdogo lakini katika maisha yake kila siku akawa muombaji mzuri tu kanisani. Wazazi wake walimlea katika maisha ya kumjua Mungu kwa hiyo kila siku hayo ndiyo yalikuwa maisha yake.

    Kanisani, kila siku alikuwa akipenda kuimba, alimuimbia Mungu kila alipokuwa akifika kanisani hapo. Sauti yake ilikuwa nzuri, kila siku mwalimu wa Sunday School alikuwa akimwambia Maimartha awaongoze wenzie katika kusifu na kuabudu kitu ambacho alikuwa akikifanya kwa moyo mmoja.

    “Nataka kuwa muimbaji,” alisema Maimartha, wakati huo alikuwa na miaka kumi na nne.

    “Usijali. Utakuwa muimbaji mzuri sana, Mungu atakuinua na kukuweka juu,” alisema Estelina, kila alilokuwa akiongea mtoto wake, Maimartha alikuwa akimuunga mkono.

    Kwa jinsi sauti yake ilivyokuwa ikisikika, alionekana kuwa na kipaji kikubwa cha kuimba, kipaji hicho alichokichukua kutoka kwa mama yake kiliendelea kukua moyoni mwake huku akionekana kuwa na uwezo wa hali ya juu.

    Wazazi wake hawakutaka kumrudisha nyuma, kila siku walimwambia kwamba alikuwa muimbaji mzuri ambaye Mungu angetenda mambo mengi katika maisha yake kitu ambacho kilimfariji mno.

    ***

    Alipomaliza darasa la saba, hakufanya vizuri sana na hivyo kujiunga na Shule ya Sekondari ya Makongo. Akiwa huko, bado Maimartha aliendelea kuwa muimbaji mzuri. Katika kwaya za shule ambazo mara nyingi zilikuwa zikitumbuiza katika sherehe mbalimbali ikiwepo Sherehe ya Siku ya Wazazi, Maimartha ndiye alikuwa muimbaji kiongozi.

    Suati yake ilikuwa nzuri na yenye kuvutia mno kiasi kwamba kwa kila mtu aliyekuwa akiisikia, alivutiwa nayo. Hakuacha kwenda kanisani, kila alipokuwa akihitajika, alikwenda huko huku napo akiwekwa na kuwa kiongozi wa sifa na kuabudu.

    Akiwa ameingia kidato cha nne, Maimartha akajikuta akianza kuingia katika mahusiano kwa kijana mmoja, huyu aliiwa Mark.

    Katika kipindi cha nyuma hata kabla hajaingia katika mahusiano ya kimapenzi na mvulana huyo, kila alipokuwa akimuona alijihisi kuwa na kitu cha tofauti moyoni mwake jambo lililompelekea kuivumilia hali hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele, hali ile ilizidi kuongezeka kiasi kwamba akaanza kuwa na hamu ya kumuona Mark kila wakati na kama ilitokea kwa zaidi ya masaa matatu hajamuona, moyoni alijisikia maumivu makubwa.

    Shuleni hakuwa muongeaji sana, alikuwa msichana mkimya aliyeonekana kuwa na maamuzi yake katika kila kitu alichotaka kukifanya. Hali ya kuanza kumpenda na kumhitaji Mark, ikamfanya kuwa mtu wa tofauti kabisa.

    “Yesu nisaidie,” alisema Maimartha mara baada ya kuona kwamba maji yalimfika shingoni.

    Alijitahidi kuomba na kuikemea hali hiyo lakini hakukuwa na kitu chochote kile kilichobadilika, bado alijihisi kuwa na uhitaji na mvulana huyo. Hisia kali za kimapenzi zikaanza kumpelekesha, kila alipokuwa akijitahidi kujiweka bize ili asiweze kuwa katika hali hiyo, ilishindika kabisa.

    Maimartha akawa kama mtu aliyepagawa mapenzini, kila alipokuwa akikaa darasani alikuwa akiliandika jina la mvulana huyo katika mapaja yake na hata baadhi ya madaftari yake yalikuwa yakijazwa jina la Mark katika ukurasa wa nyuma kabisa.

    Maimartha alikuwa muoga, japokuwa aliona kuwa na nafasi kubwa ya kumwambia ukweli Mark jinsi alivyokuwa akijihisi moyoni mwake lakini alikuwa akiogopa mno.

    Hakuwahi kuwa na uhusiano na mvulana yeyote yule na wala hakuwa amewahi kuzisikia hisia za kimapenzi moyoni mwake, kwa Mark, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa katika maisha yake, hakujua angeanza vipi.

    “Shetani shindwa...shetani shindwa...” alikemea Maimarthakwa kuona kwamba mawazo juu ya Mark yangeweza kumtoka lakini hiyo haikuweza kuondoka kabisa.

    “Mark nakupenda...ninashindwa kabisa kujizuia,” alijisemea Maimartha katika kipindi alichokuwa chumbani kwake.

    Japokuwa alikuwa msichana aliyeokoka lakini katika kipindi hicho aliamua kuuweka wokovu wake pembeni, alikuwa akitaka kuwa na Mark ambaye kila siku alikuwa akiutesa moyo wake tu.

    Halikuwa jambo jepesi kwake kumfuata na kumwambia ukweli kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake jambo lililomfanya kila siku kuumia bila kupata msaada wowote.

    Upendo mkubwa aliokuwa nao juu ya Mark ulikuwa siri yake, kama kuumia aliumia kivyakevyake lakini kamwe hakutaka kumwambia mtu yeyote yule kwani hakujua jamii ingemchukuliaje na wakati kila mtu alijua kwamba alikuwa ameokoka.

    Mara baada ya kuona kwamba aliumia sana moyoni mwake, Maimartha hakutaka kuendelea kuumiza tena, kitu alichokitaka kwa wakati huo ni kumwambia Mark ukweli juu ya mapenzi makubwa aliyokuwa nayo juu yake.

    Siku ambayo aliipanga kumwambia Mark ukweli, alikuwa amejipanga vilivyo, toka alivyokuwa akitoka nyumbani, akili yake ilikuwa ikifikiria kumwambia mvulana huyo jinsi alivyojisikia.

    Japokuwa alikuwa msichana mkimya, siku hiyo ukimya wake ulikuwa maradufu, hakutaka kuongea na marafiki zake, alikuwa amekwishayapanga maneno kichwani mwake, kuongea sana na watu, aliogopa kusahau.

    “Tokea basi Mark, mbona unachelewa hivyo!” alijisemea Maimartha huku akionekana kuwa na hamu ya kumuona Mark na kumwambia ukweli juu ya kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.

    Ilipofika saa 1:20 asubuhi, Mark akafika shuleni hapo, begi lilikuwa mgongoni mwake, kama kawaida yake, mwendo wake ulikuwa wa taratibu, alikuwa akipiga hatua kuelekea darasani.

    Maimartha alipomuona mvulana huyo, moyo wake ukamlipuka, mapigo yake ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi kubwa kana kwamba moyo ulitaka kuchomoka.

    Kadri Mark alipokuwa akipiga hatua kuelekea katika darasa alilokuwa, Maimartha alihisi kuchanganyikiwa kabisa.

    Siku hiyo Mark alionekana tofauti mbele ya macho yake, uzuri ambao alikuwa nao ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana. Moyoni alijisikia faraja, mapenzi aliyokuwa nayo juu ya Mark yakaongezeka zaidi.

    Mpaka Mark anakaa kitini, Maimartha alikuwa kimya akimwangalia. Alikuwa na hamu kwa kipindi kirefu, alitamani sana Mark afike shuleni hapo ili aongee naye, kwa wakati huo, huyo Mark alikuwepo ndani ya darasa alilokuwa, lakini aliogopa kumfuata na kumwambia ukweli.

    “Jamani Mark, mbona unanitesa hivi?” aliuliza Maimartha kwa sauti ya chini ambayo hata mwanafunzi aliyekuwa pembeni yake hakuweza kuisikia.

    Huku akiwa anajifikiria ni kitu gani alitakiwa kukifanya mahali hapo, mlango ukafunguliwa na mwalimu kuingia. Kwa siku hiyo, macho yake yalikuwa kwa Mark tu, hakuwaelewa kabisa walimu waliokuwa wakiingia na kufundisha kwa zamu.

    Muda wa mapumziko ulipofika, Maimartha akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni kuchukua kipande cha karatasi na kisha kuanza kuandika maneno fulani, alipomaliza, akaifuata meza ya Mark na kisha kuiweka karatasi ile juu na yeye kuondoka zake.

    Muda wa mapumziko ulipokwisha, wanafunzi wakarudi darasani, kwa haraka hata kabla Mark hajarudi, Maimartha alikuwa amekwishafika darasani, alitaka kumuona Mark angekuwa kwenye hali gani.

    Mvulana huyo alipoingia darasani na kukaa kitini, macho yake yakatua katika kikaratasi kile kilichokuwa juu ya meza, kwanza akaonekana kushtuka kwani katika kipindi alichokuwa amekwenda nje, kikaratasi kile hakikuwepo mezani pale., alichokifanya ni kuangalia huku na kule, kila mtu alikuwa bize na mambo yake.

    Kila kitu kilichokuwa kikiendelea Maimartha alikuwa akimwangalia tu. Mark akakichukua kipande cha karatasi kile, akakifungua, kilikuwa kimeandikwa maneno machache sana yaliyosomeka:

    To The One I Love The Most,

    ‘Ninakupenda Mark, nimeshindwa kuvumilia kukaa kimya, nimeamua kuzifikisha hisia zangu kupitia mwandiko wangu, baadae nitazifikisha kupitia sauti yangu nzuri’

    A Slave (Precious Mapple)

    Mark akashtuka.



    Hicho hakikuwa kitu cha kawaida kutokea, kikaratasi kile alichokikuta katika meza yake kilimshtua kupita kawaida. Huku akiangalia huku na kule, kichwa chake kilikuwa kikifanya kazi kubwa ya kumfikiria mtu ambaye kulikuwa na uwezekano wa kukiweka kikaratasi kile juu ya meza yake.
    Kichwa chake kilichekecha na mwisho wa siku hakuambulia kitu. Ukiachana na hivyo, akaanza kujifikiria mtu ambaye alikuwa akijiita kwa jina la Precious Mapple, hakukuwa na mtu aliyejiita jina hilo darasani humo.
    “Ni nani? Huyu Precious Mapple ndiye nani?” alijiuliza Mark lakini alikosa jibu kabisa.
    Hakutaka kuendelea kukisumbua kichwa chake kwa kujiuliza maswali mengi, alichokifanya ni kuachana na habari za kikaratasi hicho na kuendelea na mambo yake kama kawaida.
    Maimartha alikuwa kwenye hofu kubwa, mapigo yake ya moyo yaliendelea kudunda kwa nguvu, moyo wake ulionekana kugawanyika sehemu mbili, sehemu ya kwanza alisikia ikimwambia amfuate Mark na kumwambia ukweli lakini sehemu nyingine ilimwambia aachane naye na kuendelea na maisha yake ya kumtumikia Mungu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Maimartha hakukubali, moyo wake ulikuwa umekwishazama katika mapenzi ya mvulana huyo kwa asilimia mia moja hivyo asingeweza kuvumilia siku hiyo ipite bila kumwambia kitu chochote kile. 
    Alijifikiria kwa sana juu ya namna gani alitakiwa kumfuata Mark na kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea, baada ya kuona anateseka sana na wakati dokta wake alikuwepo, akaamua kuupiga moyo konde na kumfuata.
    “Mambo Mark!” alisalimia Maimartha huku akionekana kujishtukia.
    “Poa, karibu Mai,”
    “Asante,” aliitikia Maimartha na kushusha pumzi ndefu, akabaki kimya.
    Mark alikuwa ameyatuliza macho yake usoni mwa Maimartha, alionekana binti mpole na mkimya hata kwa mtu ambaye alikuwa akimuona kwa mara ya kwanza. Maimartha hakutaka kuongea kitu chochote kile kwani kila alipotaka kumwambia Mark juu ya kile kilichokuwa moyoni mwake, alijisikia aibu.
    “Nakusikiliza Maimartha. Au wewe ndiye Precious Mapple?” aliuliza Mark, kwa mbali Maimartha akaonekana kushtuka.
    “Precious Mapple?”
    “Yaap! Huyo mtu kaniletea kikaratasi hapa. Au unamjua msichana anayejiita jina hilo?” aliuliza Mark.
    Mapigo ya moyo ya Maimartha yakazidi kudunda kwa kasi zaidi, swali alilokuwa ameulizwa jibu lake lilikuwa dhahiri na kingekuwa ni kitu cha harakaharaka kumjibu mvulana huyo kwamba huyo mtu aliyekuwa amemuulizia alikuwa yeye.
    “Mmmh! Wala simfahamu, amefanyaje?” aliuliza Maimartha.
    “Kama haumfahamu, poa.”
    “Lakini niambie amefanyaje.”
    “Hajafanya kitu.”
    Mpaka mwalimu anaingia darasani, Maimartha hakuwa amezungumza chochote na hata kile kitu kilichompeleka kwa Mark hakuwa amekiongea. Hilo likamfanya kunyong’onyea, alitamani kwa kipindi kirefu kumwambia Mark ukweli lakini bado ilikuwa imemtawala moyoni mwake.
    Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo moyo wake ulivyozidi kuteseka, kila siku kilio chake kilikuwa ni kumwambia Mark ukweli kwamba alikuwa akimpenda mno.
    Hakujua angeanzia wapi lakini ilikuwa ni lazima kumwambia kijana huyo ukweli wa moyo wake. Maimartha alivumilia kila siku lakini mwisho wa siku akaamua kumfuata Mark kwa mara nyingine, leo hii alikuwa ameamua, alijitoa mhanga kwamba ilikuwa ni lazima amwambie Mark ukweli, hata kama angemchukulia vibaya, asingejali chochote.
    “Mark...” aliita Maimartha, Mark alipogeuka, moyo wa Maimartha ukapiga ‘paaaa’.
    ***
    Siku hiyo Maimartha alikuwa amedhamiria kumwambia Mark ukweli juu ya kile kilichokuwa kimeujaza moyo wake, hakuwa tayari kujiona akiwa kwenye mateso makali na wakati dokta wa maumivu yale alikuwepo, alitaka kufanya kile alichokuwa amekipanga kwa siku nyingi.
    Mark alibaki akimwangalia Maimartha kwa uso uliojawa na tabasamu pana ambalo lilimfanya kuonekana mzuri zaidi machoni mwa msichana huyo. Alibaki akimwangalia huku uso wake akiuweka katika hali ya kutaka kusikia kitu gani ambacho msichana huyo alitaka kumwambia mahali hapo.
    “Ninakupenda,” Maimartha alijishukia akisema maneno hayo yaliyosikika vema masikioni mwa Mark.
    Aliumia sana, kila siku alisononeka, ukimya wake wa kutokumwambia Mark vile alivyokuwa akijisikia kulimfanya kuteseka mno. 
    Neno ‘nakupenda’ alilokuwa amesema mahali hapo si kwamba alikuwa amepanga kulitamka bali uzuri, uso uliojawa na tabasamu ukampelekea kulitamka neno hilo.
    Akaufumba mdomo wake, akabaki akiwa na mshangao juu ya neno lile kwani hakulitegemea kama lingetoka kinywani mwake. Alipomwangalia Mark, alikuwa akitabasamu zaidi, yaani hakuonesha mshtuko wowote ule.
    “Waooo!! Kumbe unanipenda!” alisema Mark huku tabasamu likiendelea kubaki usoni mwake.
    “Samahani,” alisema Maimartha huku akionekana kujishtukia.
    “Samahani ya nini tena?” aliuliza Mark.
    “Limenitoka tu?”
    “Inawezekana ikawa kweli limekutoka. Ila lina maana yoyote kutoka kwako juu yangu?” aliuliza Mark.
    “Samahani.”
    “Usijali Maimartha.”
    Maimartha akashusha pumzi ndefu na nzito, aliulaumu mdomo wake kwa kulitamka neno hilo ambalo lilimfanya Mark kugundua kile kilichokuwa moyoni mwake.
    Alijulikana kama msichana aliyeokoka, hivyo shule nzima walijua kwamba alikuwa akiishi katika maisha matakatifu. Hilo ndilo lilikuwa kubwa ambalo lilimfanya kujishtukia
    Alimpenda sana Mark lakini siku zote alitaka jambo hilo liwe siri yake, alikubali kuendelea kuumia moyoni mwake lakini si kumwambia Mark kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.
    Leo hii, kwa bahati mbaya kabisa alijikuta akimwambia Mark kwamba alikuwa akimpenda jambo lililomfanya kujiona mkosaji mkubwa.
    Kuanzia siku hiyo, neno hilo moja likaonekana kuleta maendeleo katika maisha yao. Urafiki wao wa karibu ukaanzia hapo. Mara kwa mara Mark alikuwa akikisogeza kiti chake mpaka pale alipokuwa amekaa Maimartha na kuanza kuongea naye.
    Ukaribu huo ndiyo uliocholeta mapenzi moyoni mwa Mark, taratibu akajiona akianza kuwa karibu na Maimartha jambo lililmfanya kumthamini msichana huyo.
    Mpaka wanamaliza kidato cha nne shuleni hapo, wawili hao walikuwa wapenzi, katika kila sehemu waliyokuwa, walikuwa pamoja huku hata wakati mwingine wakitembeleana kama marafiki, na si kama wapenzi kama walivyotaka iwe.
    “Kwa nini nisijiweke wazi moja kwa moja?” alijiuliza Maimartha.
    “Nitamwambia ukweli kabla matokeo hayajatoka,” alijisemea na kutulia kitandani.
    Kitandani hakukulalika vizuri, kila wakati alikuwa akimfikiria Mark ambaye kwake, kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele alijiona akimpenda mvulana huyo kwa mapenzi ya dhati kutoka moyoni.
    Kasi yake ya kwenda kanisani ikawa imepungua, siku za ibada za kati ambazo alikuwa akitakiwa kanisani hakuwa akielekea huko, alikuwa akienda nyumbani kwa kina Mark, wanapiga stori na hata kama siku itatokea amekwenda kanisa, alipokuwa akirudi ilikuwa ni lazima kupitia nyumbani kwa mvulana huyo, japo kumuona sura yake, moyo wake uliridhika.
    “Mark...” aliita Maimartha.
    “Unasemaje Mai,” aliitikia Mark.
    “Kuna kitu nataka kukwambia,” alisema Maimartha.
    “Kitu gani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Maimartha akashusha pumzi ndefu na nzito. Aliuhisi mwili wake ukianza kupata joto la ghafla huku moyo wake ukidunda kwa kasi kubwa, yaani kama ulitaka kuchomoka.
    “Mai...” aliita Mark mara baada ya kumuona msichana huyo amekuwa kimya sana.
    “Abeee...”
    “Nakusikiliza.”
    “Mark. Naomba nikuulize kitu kimoja,” alisema Maimartha.
    “Kitu gani?”
    Hapo, hakujibu tena swali hilo, kama kawaida yake akabaki kimya. Siku hiyo, kumwambia ukweli Mark likaonekana kuwa suala gumu kwake, hakuamini kama angeweza kumwambia kile kilichokuwa kimeujaza moyo wake, bado alikuwa akiogopa.
    “Ninakupenda Mark, ninataka uwe mpenzi wangu” alisema Maimartha huku kwa mbali mwili wake ukianza kutokwa na kijasho chembamba, kitu alichokitegemea ni kwamba Mark angechukia na kuusitisha urafiki wao.
    Mark akashusha pumzi ndefu na nzito. Alihisi masikio yake kuwasha.


    Mark hakusema kitu, alibaki kimya huku akitabasamu tu. Maimartha hakuamini, tabasamu lile lilikuwa ni tofauti na kile kitu alichokifikiria kabla. Alichokijua ni kwamba Mark angekasirika na kumuoneshea utofauti usoni mwake lakini hali haikuwa hivyo.
    Tabasamu alilolionesha Mark likazidi kuutesa moyo wake, hakuamini kama Mark aliongezeka uzuri na kuwa kama alivyokuwa, Maimartha akajikuta naye akianza kutabasamu.
    “Maimartha...” aliita Mark.
    “Abeeee...”
    “Mbona hukuniambia toka mapema?” aliuliza Mark.
    “Kwa nini?”
    “Nina msichana anayenipenda. Hapa nilikuwa katika hatua za mwisho kuja kumtambulisha kwako,” alisema Mark.
    Maimartha alihisi mwili wake ukianza kutetemeka, tabasamu alilokuwa amelitoa, ghafla likapotea, mwili wake ukapigwa ganzi, hakuamini kile alichokuwa amekisikia.
    Wakati mwingine alijiona kusikia vibaya, alitamani kumwambia Mark alirudie kile alichokuwa amekizungumza ili ayategeshe vema masikio yake, lakini pamoja na hayo, alijua kabisa hakuwa na matatizo ya kusikia hivyo kile alichokuwa amekisikia ndicho alichokuwa amezungumza mvulana huyo.
    “Mark...”
    “Umechelewa Maimartha. Yaani kipindi chote hicho unakuja kuniambia leo! Yaani toka shuleni haukuniambia, unakuja kuniambia leo hii, Mai, kwa nini?” alisema mark na kumalizia na swali.
    “Nilikwambia.”
    “Lini?”
    “Siku ya kwanza.”
    “Haukumaanisha Mai.”
    “Ninakupenda Mark.”
    “Nina mtu Mai. Umechelewa.”
    Kati ya siku mbaya maishani mwake, siku hiyo ilikuwa ya kwanza, aliuhisi moyo wake ukiingia katika maumivu makali mno ambayo hakuwahi kuyapata katika maisha yake yote.
    Mtu aliyekuwa akimpenda na kumthamini, mtu ambaye alichukua muda mrefu kujenga naye ukaribu, leo hii alikuwa ameamua kumwambia ukweli juu ya kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake lakini alimwambia kwamba alichelewa, hayo yalikuwa ni zaidi ya maumivu.
    Hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akilia. Hakutaka kumuona tena Mark kwani aliamini kwamba endapo angemuona basi angekumbuka maneno aliyokuwa amemwambia kwamba alikuwa amchelewa kumwambia maneno hayo.
    Kuanzia siku hiyo, hakutaka kuwasiliana na Mark, kila alipokuwa akipigiwa simu, alikuwa akiikata na hata alipokuwa akitumiwa meseji hakuwa akizijibu. Akajikuta akianza kumchukia mark, rafiki yake wa kipindi kirefu, ghafla akabadilika na kuwa adui mkubwa maishani mwake.
    “Sikupendi Mark...... Ninakuchukia Mark, sitaki kukuona tena Mark,” alisema Maimartha huku akiwa kitandani mwake, machozi yalimbubujika tu mashavuni mwake.
    Mto wa kulalia ukawa faraja yake kubwa, kila alipokuwa akibubujikwa na machozi, alikuwa akiuchukua mto ule na kuanza kujifutia machozi yake huku wakati mwingine akiukumbatia.
    Wiki nzima, hakutaka kuwasiliana na Mark, alijiona kuwa na chuki na mvulana huyo kwa sababu aliutesa moyo wake tu. Akajitahidi kujiwekea mazingira yote ya kumuepuka mtu huyo.
    Matokeo ya kidato cha nne yalipotoka, Maimarthaalikuwa amefaulu vizuri na baadae kujiunga na Shule ya Wasichana ya Jangwani huku Mark akijiunga na Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
    Bado kumbukumbu za mapenzi zilikuwa zikimtesa, alikuwa akiendelea kumpenda Mark japokuwa kila siku alisema kwamba alimchukia mvulana huyo. Mdomo wake ukashindwa kabisa kuweka upinzani na moyo wake, kile kilichokuwa kimeamuliwa moyoni kilikuwa na nguvu kuliko maneno aliyokuwa akiyazungumza.
    “Lakini kwa nini nateseka hivi? Kwa nini nautesa moyo wangu namna hii?” alijiuliza Maimartha lakini akakosa jibu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kumbukumbu za mapenzi juu ya Mark ziliendelea kuishi moyoni mwake japokuwa alikuwa akikutana na wanaume wengi lakini mvulana huyo alikuwa mtu pekee aliyeuteka moyo wake.
    Mara kwa mara Maimartha alikuwa na kazi ya kuelekea katika Shule ya Sekondari ya Benjamin kwa ajili ya kumuona Mark ambaye alimwambia kwamba alikuwa na mtu hivyo asingeweza kuwa naye.
    Hilo tu wala halikutosha kumzuia Maimartha, kama kawaida yake, bado alihitaji kuwa karibu na mvulana huyo ambaye kwa kumwangalia tu alionekana kutokusomeka.
    “Mark....” aliita Maimartha, mvulana huyo alikuwa akipita mbali na alipokuwa amesimama, alipogeuza macho na kumuona Maimartha, kwa haraka akaanza kupiga hatua kumfuata.
    “Niambie,” alisema Mark huku akiwa amemfikia msichana huyo.
    “Nimekufuata wewe hapa shuleni,” alisema Maimartha.
    “Kweli?”
    “Ndiyo. Ninataka kuongea nawe mara moja.”
    “Kuhusu nini?”
    “Utajua tu.”
    “Kama ni yaleyale naomba uniache,” alisema Mark, kwa mbali Maimartha akaonekana kunywea, hakutegemea kuyasikia tena maneno kama hayo kutoka kwa Mark.
    Maimartha alibaki na mawazo lukuki, kile alichokuwa amekisema Mark kilimuingia masikioni mwake lakini hakutaka kukubaliana naye. Hakuwa radhi kubaki kimya bila kumwambia Mark kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.
    Ni kwa kipindi kirefu mno alikuwa amebaki kimya na hicho kilikuwa kipindi chake cha kumkumbushia kile ambacho mara kwa mara alikuwa akimwambia toka walipokuwa shuleni.
    Kwa Mark, alionekana kuwa tofauti, hakuwa na dalili zozote za kukubaliana na Maimartha juu ya kile alichotaka kumwambia. Alimkanya lakini Maimartha hakuonekana kukubaliana naye.
    “Una jipya?” aliuliza Mark, walikuwa wamesogea pembeni kabisa, karibu na mti mkubwa wa mwembe.
    “Mark, siwezi kujizuia, ni lazima nizungumze lilelile,” alisema Maimartha kwa sauti ya chini, alishindwa kujizuia kabisa.
    “Umeanza,” alisema Mark.
    “Hapana. Si kwamba nimeanza, huu ni muendelezo juu ya kile nilichokuwa nikikwambia kila siku,” alisema Maimartha, katika kipindi hicho alisahau kabisa kama alikuwa binti aliyeokoka aliyetarajia kuwa muimbaji mkubwa.
    Kwa kila kitu alichokisema, Mark hakutaka kumuelewa, aliendelea kuweka msimamo kwamba asingeweza kuwa naye kwa sababu alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na msichana mwingine.
    “Haiwezekani,” alisema Maimatha.
    “Haiwezekani nini sasa?”
    “Hauwezi kuwa na msichana. Kama ungekuwa naye, ningemjua toka zamani,” alisema maimartha.
    “Mai, naomba achana na mambo ya mapenzi, zingatia shule na mzingatie Mungu wako unayemsifu kila siku,” alisema Mark.
    Japokuwa alikuwa ameongea maneno ya msingi lakini kwa wakati huo, moyoni mwa Maimartha yalionekana kuwa maneno ya kipuuzi, mapenzi yalimlevya kiasi ambacho hakutaka kusikia kitu chochote kile. Alimhitaji mno Mark lakini mbaya zaidi mvulana huyo hakuonekana kuwa radhi kuwa mpenzi wake.
    Siku hiyo aliambulia patupu, kile alichokuwa amekifuata shuleni hapo hakikufanikiwa hata kidogo, Mark aliendelea kumkatalia.


    Kilikuwa ni kipindi cha ubaridi ndani ya Jiji la Dar es Salaam, lile joto
    lililokuwepo kwa miezi kadhaa lilipotea. Ingawa halikuwa baridi kali kama la
    mikoa mingine lakini kwa wakazi wa jiji hilo ikaonekana kuwa shida, katika kila
    kona waliyokuwepo, makoti mazito yalikuwa miilini mwao.
    Saa 2:00 usiku, Mark alikuwa amejikunyata pembezoni mwa nyumba ya mzee
    paul, alifika mahali hapo kwa sababu alipigiwa simu na Maimartha kwamba
    alitaka kuongea naye.
    Ingawa hakutaka kuwa na ukaribu mkubwa na msichana huyo lakini siku hiyo
    Mark akajikuta akielekea huko, hapo, alikuwa akimsubiria msichana huyo
    aliyeahidi ndani ya dakika chache angekuwa mahali hapo.
    Alisubiri sana, mpaka inafika saa 2:45, Maimartha hakuwa ametoka nje ya uzio
    wa nyumba yao japokuwa kwa mbali sauti yake ilikuwa ikisikika. Mark
    akaonekana kukasirika, hakutegemewa kukaa kwa muda mrefu mahali hapo na
    wakati alikwishawasiliana na msichana huyo na kumwambia kwamba ndani ya
    dakika chache atakuwa mahali hapo.
    Mark akakata tamaa, akafikiria kuondoka mahali hapo lakini hata kabla
    hajaanza kuondoka, akasikia geti likifunguliwa, alipoangalia, alikuwa
    Maimartha.
    “Pole,” alisema Maimartha kwa sauti ya chini, mwilini mwake alikuwa na sweta
    zito.
    “Utaniua kwa baridi, niambie unataka kuniambia nini,” alisema Mark huku kwa
    mbali akitetemeka kutokana na baridi lile kali.
    “Nimekukumbuka mno. Bado nauliza kuhusu lilelile,” alisema Maimartha.
    “Nilikwambia kwamba nina mtu.”
    “Hapana. Ulinidanganya kwamba una mtu, hebu niambie kwa nini
    ulinidanganya,” aliuliza Maimartha.
    “Sikukudanganya, nilikwambia ukweli.”
    “Hapana, si kweli. Mimi siyo mtoto Mark. Naomba uniambie sababu za
    kunidanganya.”
    Mark akanyamaza, akaanza kumwangalia Maimartha usoni, alipoona kwamba
    anaanza kusikia aibu, akaangalia chini. Ni kweli maneno aliyoongea Maimartha
    yalikuwa ni kweli kabisa, katika kipindi chote alikuwa akimdanganya kwamba
    alikuwa na mtu lakini ukweli ni kwamba hakuwa na mtu yeyote yule.
    Aliulizwa swali lakini hata kabla ya kujibu alitakiwa kujifikiria kutoa jibu la
    uhakika na si kukurupuka tu.
    “Maimartha...” aliita Mark.
    “Niambie, kwa nini umekuwa ukinitesa hivi?”
    “Subiri kwanza.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Niambie kwanza, kwa nini umekuwa ukinidanganya kila siku?” aliuliza
    Maimartha, hapohapo akaanza kupiga hatua kumsogelea Mark.
    Kibaridi bado kiliendelea kupuliza, miili yao ikaanza kusisimka na kuwaweka
    katika hali nyingine kabisa. Maimartha alipomshika Mark mkono, mwanaume
    huyo akapata msisimko wa ajabu.
    Maimartha hakuacha, alianza kama utani lakini mwisho wa siku wakajikuta
    wakisogea lembeni kabisa, sehemu iliyokuwa na kificho, hapo ndipo kila kitu
    kilichotakiwa kufanyika, kifanyike.
    Pumzi nzito walizokuwa wakizitoa ziliwachanganya, bila kutarajia, wakajikuta
    wakianza kuvuana nguo. Kutokana na giza lililokuwepo mahali hapo, hakukuwa
    na mtu yeyote aliyewaona hapo walipokuwa wamejificha.
    “Mark....” Maimartha aliita kwa sauti ya chini, alionekana kuzidiwa kabisa.
    “Unasemaje?”
    “Sijawahi kufanya mchezo huu,” alisema Maimartha.
    “Ndiyo siku yako ya kwanza?”
    “Ndiyo.”
    “Basi usijali, umekutana na mwalimu,” alisema Mark, wakajikuta wakiwa
    watupu, hapo ndipo mchezo mchafu ulipoanza.
    Muda wote Maimartha alikuwa akilia tu, kuna kipindi alikuwa akijuta kufanya
    kitendo kile lakini katika kipindi alichokuwa akipapaswa huku na kule, akajikuta
    akihisi raha ambayo hakuwahi kuipata kabla.
    Ndani ya dakika kumi, usichana wake aliokuwa nao ukatolewa, kiasi kidogo cha
    damu kikawa kimetoka sehemu zake za siri, kuanzia hapo, akaanza kuitwa
    msichana aliyekamilika.
    “Nakupenda Mark,” alisema Maimartha.
    “Nakupenda pia. Ila umenisumbua sana,” alisema Mark huku akivaa nguo zake
    tayari kwa kuondoka.
    “Sijazoea, siku nyingine sitokusumbua.”
    “Sawa. Hakuna noma,” alisema Mark, wakaagana na kuondoka mahali hapo
    huku kukiwa hakuna ajuaye kile kitakachotokea baada ya hapo.
    ****
    Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilikuwa siri kati ya watu wawili. Hakukuwa na
    mtu yeyote aliyetakiwa kujua. Japokuwa alijua fika kwamba alikuwa akimtenda
    Mungu dhambi lakini hakuacha kufanya mapenzi na Mark.
    Mara kwa mara walikuwa wakikutana kisiri katika nyumba ya wageni iliyokuwa
    Kigogo na huko ndipo walipofanyia uchafu wao mbele za Mungu.
    Kama kuimba kanisani, hakuacha, sauti yake nzuri bado iliendelea kuwa tishio
    kwa watu wote. Huku akiwa na miaka kumi na tisa, Maimatha alikuwa akitisha
    sana kiasi kwamba watu wote walimtabiria kuja kuwa mwanamuziki mkubwa
    hapo baadae.
    “Una sauti nzuri, kama malaika,” alisema kijana mmoja, aliitwa John, mtoto wa
    mchungaji wa kanisa hilo la Praise And Worship.
    “Asante John. Sifa na Utukufu kwa Bwana,” alisema Maimartha.
    “Ila samahani, nawez kuonana na wewe baadae?”
    “Kuna kitu gani?”
    “Ningependa niongee nawe, baadhi ya mambo tu,” alisema John.
    “Muda gani?”
    “Jioni.”
    “Sawa. Tutaongea nikija kanisani kwenye ibada ya jioni,” alisema Maimartha.
    “Hapana. Sitaki iwe kanisani.”
    “Sasa wewe unataka iwe wapi?”
    “Popote ambapo kutakuwa na utulivu.”
    “Kama wapi?”
    “Popote tu.”
    John hakuonekana kujiamini, kitu pekee alichokuwa akikifikiria mahali hapo
    kilikuwa ni gesti tu. Kutamka waziwasi hakuwa radhi, alichokuwa akikitaka ni
    Maimartha ajiingize mwenyewe kwa kuitaja sehemu hiyo.
    Moyo wake ulikuwa na hofu kubwa, alikuwa mtoto wa mchungaji
    aliyeheshimika lakini halikuwa jambo jepesi kwake kuacha kumfuatilia
    Maimartha.
    Alimpenda msichana huyo na kila siku macho yake yalimuonyeshea kila kitu
    lakini msichana huyo hakutaka kuelewa kitu chochote kile.
    Wengi walivutiwa na sauti ya Maimartha ila kwa John, alivutiwa zaidi ya watu
    wote. Moyo wake uliteseka mchana na usiku, kila alipokuwa akitaka
    kumwambia msichana huyo ukweli wa moyo wake alikuwa akishindwa.
    “Hivi atanichukuliaje?” alijiuliza bila kupata jibu.
    Siku ziliendelea kukatika, Maimartha aliendelea kuonekana mtakatifu na wakati
    maisha yake yalijazwa na uchafu mwingi. Kila mtu alimuona kuwa msichana
    pekee ambaye alijiheshimu kanisani hapo.
    Wasichana wengi waliambiwa wafuate tabia yake kwani kwa kila mwanamke
    aliyekuwa akimwangalia, alitamani kama angekuwa binti yake.
    “Yesu wangu!” alisema Maimatha mara baada ya kuambiwa na John kwamba
    alikuwa akimpenda.
    “Usishtuke Maimartha, ninakupenda sana,” alisema John, macho yake yalikuwa
    yakionyesha kila kitu kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.
    “John, wewe ni mtotowa mchungaji,” alisema Maimartha huku uso wake ukiwa
    kwenye mshangao mkubwa wa kinafiki.
    “Kwani watoto wa wachungaji hawatakiwi kupenda?”
    “John, niondolee upuuzi wako,” alisema Maimartha kwa sauti ya juu huku
    akijifanya kukasirika.
    “Ninakupenda Maimartha.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    John hakukoma, kila siku kilio chake kilikuwa kwa msichana huyo, aliendelea
    kumsisitizia kwamba alimhitaji lakini hiyo ilikuwa ni sawa na kumpigia ngoma
    mbuzi ukimtaka acheze. Maimartha alikataa katakata.
    “Sikutakiiiiiii,” alisema Maimartha kwa sauti ya juu yenye ukali.


    Mpaka Maimartha anaingia kidato cha sita, bado mapenzi yake ya siri na Mark yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Sehemu kubwa waliyokuwa wakikuta ilikuwa ni pembezoni mwa Shule ya Msingi ya Turiani iliyokuwa karibu na nyumba ya mtabiri, Sheikh Yahya, hapo, waliongea mengi lakini kwenye kufanya mapenzi, kama kawaida yao walikuwa wakikutana katika Gesti ya Kipelepele iliyokuwa Kigogo.
    “Hivi siku kanisani kwenu wakijua?”
    “Watajuaje?”
    “Mapenzi kikohozi Mai,” alisema Mark.
    “Lakini si unaweza kukohoa bila watu kusikia.”
    “Kakudanganya nani? Wewe subiri siku watu wajue, nitakuruka,” alisema Mark na kuanza kucheka.
    Huku maisha ya kimapenzi baina ya watu hao wawili yakiendelea, mabadiliko yakaanza kutokea kwa Maimartha. Kitu cha kwanza akaanza kujisikia akiumwa na tumbo huku wakati mwingine akiwa mvivu kupita kawaida.
    Hilo wala halikuwa tatizo kubwa, alijaribu kutumia vidonge kwa kuamini kwamba ulikuwa ugonjwa wa kawaida, kitu cha ajabu, tatizo hilo halikumuisha, aliendelea kujisikia hivyohivyo.
    Mabadiliko hayakuishia hapo, baada ya siku kadhaa, akaanza kutapika huku mdomo wake ukiwa na hamu ya vitu vichachu mdomoni mwake. Maembe ndiyo yalikuwa vitu pekee yaliyoiridhisha hamu yake hiyo.
    “Nataka nikuone leo,” alisema Mark huku mkononi akiwa na simu kubwa kama mche wa sabuni, simu ya Motorola, kipindi hicho ndicho ambacho simu zilianza kuingia.
    “Upo wapi?” aliuliza Maimartha.
    “Kama kawaida, kwenye ukuta wa shule.”
    “Sawa. Ila sijisikii vizuri sana.”
    “Unaumwa?”
    “Ndiyo. Najisikia kichefuchefu, natapika, mwili umekuwa na uchovu mwingi sana,” alisema Maimartha.
    “Hebu njoo nikuone kwanza, inawezekana kwa sababu hajaniona siku ya jana ikawa sababu,” alisema mark.
    “Sawa. Nakuja.”
    Ndani ya dakika kumi Maimartha alikuwa pembeni mwa Mark. Huyo ndiye alikuwa mtu pekee aliyekuwa akimpenda kwa mapezi ya dhati. Alimthamini na alikuwa tayari kwa kitu chochote.
    “Ninaumwa mpenzi,” alisema Maimartha kwa sauti ya kudeka, ilikuwa saa mbili usiku.
    “Pole sana. Usijali, utapona tu. Umekwenda hospitali?”
    “Hapana.”
    “Fanya kesho uende. Utaweza kwenda peke yako?”
    “Siwezi, nataka unisindikize.”
    “Usijali. Tutakwenda.”
    Siku iliyofuata, wawili hao wakaonana na kuamua kwenda katika Hospitali ya Mwembechai kwa ajili ya kupima kile kilichokuwa kikimsumbua Maimartha.
    “Nafikiri itakuwa homa kali,” alisema Maimartha huku akimwangalia dokta.
    “Itatupasa tuchukue vipimo, kwanza tutaipima damu na kisha mkojo,” alisema dokta.
    “Sawa.”
    Katika kipindi chote hicho Mark alikuwa pembeni ametulia, macho yake hayakutulia, mara alikuwa akimwangalia dokta na mara Maimartha.
    Maimartha na Mark wakatoka chumbani humo na kuelekea sehemu iliyokuwa na vyoo. Walipofika mlangoni, Mark akabaki nje huku akimwacha Maimartha akiingia ndani ya choo hicho na baada ya muda akatoka huku akiwa na mkojo wake katika chupa ndogo.
    Wakarudi katika chumba kile cha dokta na kumpa mkojo ule kisha kuchukuliwa damu yake.
    “Subirini nje kwa dakika kadhaa, nitawaita,” alisema dokta yule.
    Wote hawakuonekana kuwa na raha, ugonjwa wa Maimartha ulivisumbua vichwa vyao. Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba alikuwa akisumbuliwa na homa au U.T.I (Urinary Tract Infections) uliokuwa maarufu kwa wanawake.
    “Nitakuwa na UTI tu,” alisema Maimartha huku akilia, alikuwa akisikia maumivu makali.
    “Itakuwa hivyo tu. Usijali, tutanunua dawa za kutosha,” alisema Mark.
    Walikaa kwa zaidi ya dakika arobaini na tano na ndipo mlango ukafunguliwa na dokta kuwaambia kwamba walitakiwa kuingia ndani. Walipofika ndani, karatasi ya matokeo ilikuwa mikononi mwake. Uso wake haukuwa wa kawaida, alionyesha kuwa na wasiwasi mno.
    “Kuna nini?” aliuliza Mark, uso wa dokta ulimuonyeshea wasiwasi.
    “Nimechukua vipimo vyote.”
    “Imekuwaje? Umegundua ana tatizo gani?” aliuliza Mark.
    “Maimartha ana mimba ya mwezi mmoja,” alisema dokta, wote wakshtuka.
    “Unasemaje?” aliuliza Maimartha huku akionyesha mshtuko wa wazi.
    “Una mimba,” alisema dokta. 
    Maimartha akahisi kuzimiazimia.
    ****
    Lilikuwa pigo kubwa maishani mwake, alimuona Mungu kumuacha na hivyo kuruhusu kupata mimba. Unafiki aliokuwa akiuleta kanisani ndiyo ambao ulisababisha kila kitu kuwa hivyo ili ijulikane kwamba maisha aliyokuwa akiishi hayakuwa yale ambayo watu walifikiria.
    Usiku hakulala, kichwa chake kilikuwa na mawazo lukuki, alikuwa akifikiria ni kwa jinsi gani angeweza kuwaambia wazazi wake kwamba alikuwa na mimba.
    Maimartha akachanganyikiwa, lawama zake zote zikaenda kwa Mark kwa kuruhusu kufanya mapenzi bila kutumia kinga ambayo ndiyo iliyosabisha kile kilichokuwa kimetokea. Moyo wake uliendelea kujuta zaidi, mpaka anakuja kupata usingizi wa mang’amung’amu, ilikuwa saa nane usiku.
    Alipoamka, hakuweza kusahau kile kilichokuwa kimetokea siku iliyopita, alikumbuka vilivyo kwamba aliambiwa ni mjauzito, akasimama na kisha kuanza kulisogelea kabati lake na kuanza kujiangalia kwenye kioo, alionekana kutia huruma.
    “Naomba unisamehe Mungu,” alisema Maimartha kwa sauti ya chini.
    Akaifunua fulana yake aliyokuwa ameivaa na kisha kuanza kuliangalia tumbo lake, hakuamini kama kweli alikuwa amepata mimba huku akiwa kidato cha sita, yaani alikuwa akijiandaa kuingia kidato cha sita, mtu pekee ambaye alitakiwa kushauriana naye juu ya mimba hiyo alikuwa Mark.
    “Tufanye nini sasa?” alisikika Mark akiuliza simuni.
    “Sijui, siwezi kuwaambia wazazi wangu, sitaki wajue kilichoendelea, sitaki wajue kama nina mimba,” alisema Maimartha huku akilia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Upo tayari kuzaa?” aliuliza Mark.
    “Hapana, sipo tayari, sitaki kuwa na mtoto kipindi hiki,” alijibu Maimartha huku akilia.
    “Inatupasa tufanye kitu.”
    “Kitu gani?”
    “Kutoa mimba,” alijibu Mark, Maimartha akashtuka.
    “Kutoa mimba?”
    “Ndiyo.”
    “Mimi nitoe mimba?” aliuliza Maimartha huku akishtuka.
    “Ndiyo. Au unataka kuzaa?”
    “Hapana, siwezi kutoa mimba.”
    “Kwa hiyo upo tayari kuzaa?”
    Maimartha akabaki kimya, hakujua ni kipi alichotakiwa kujibu mahali hapo. Alijua fika kwamba tukio la kutoa mimba lilikuwa baya na lenye kuhatarisha maisha yake, hakutaka kufanya hivyo.
    Japokuwa hakuwa akitaka kutoa mimba lakini pia hakuwa tayari kuzaa. Alijiona kuwa binti mdogo mwenye ndoto nyingi maishani mwake, kuzaa kwake kulimaanisha kwamba ni lazima baadhi ya ndoto ambazo alikuwa nazo zingefutika.
    “Maimartha....” aliita Mark.
    “Mark...nisaidie mpenzi,” alisema Maimartha huku akilia.
    “Kutoa mimba ni suluhisho la mwisho.”
    “Naogopa kumtenda dhambi Mungu wangu,” alisema Maimartha.
    “Mpenzi, umemtenda dhambi Mungu mara ngapi? Yaani unaogopa kumtenda Mungu dhambi kwa kitu ambacho kitakusaidia maishani mwako! Yaani unataka uzae, uachane na shule na usitimize ndoto ulizojiwekea?” aliuliza Mark, naye mwenye alikuwa akiogopa.
    “Mark! Kwa nini tumefanya bila kutumia mpira? Kwa nini Mark?”
    “Mai, huu si wakati wa kupeana lawama, tuangalie ni jinsi gani tunaweza kuepuka aibu iliyokuwa mbele yetu,” alisema Mark.
    Huo ndiyo ulikuwa wakati wa majuto. Kila mmoja alijutia kile walichokuwa wamekifanya. Maimartha hakutaka kuendelea kuongea zaidi, alichokifanya ni kukata simu.
    Alilia mno, siku hiyo ikaonekana kuwa mbaya kwake, mimba aliyokuwa nayo ilimpa mawazo kupita kawaida. Kama ilivyokuwa kwamba majuto ni mjukuu, Maimartha akaanza kujuta kwa kila kitu kilichotokea.
    Akajuta kwa kuiacha njia ambayo Mungu alimtaka aifuate na kufuata njia aliyotaka kuifuata mwenyewe na matokeo yake kupata mimba katika umri ambao hakuutarajia.
    Suala la kutoa mimba ndilo lilizozidi kumuumiza kichwa chake zaidi, hakujua ni kipi alichotakiwa kukifanya, hakujua kama alitakiwa kukubaliana na Mark kuitoa mimba ile au aiache iendelee kukua.
    Siku nzima alilifikiria suala hilo na mwisho wa siku akaamua kuungana na Mark kwamba ilikuwa ni lazima mimba itolewe.
    “Nimekubali kuitoa,” alisema Maimartha huku akilia.
    “Safi sana. Naomba tuonane Manzese,” alisema Mark na kukata simu.
    Saa 8: 20 walikuwa nje ya maabara ndoto ya Dk. Antony Lumanyika, daktari mzuri aliyekuwa akifanya baadhi ya kazi kimagendo kama kuchoropoa mimba za wasichana waliokuwa wakifika mahali hapo.
    Japokuwa ilikuwa ni kazi hatari hasa kwa wanawake lakini hakutaka kuiacha, ndiyo ilikuwa kazi pekee ilimyopatia kiasi kikubwa cha fedha kwa siku moja tu.
    Maimartha alipoletwa ndani ya maabara yake, akawasikiliza tatizo la msichana huyo.
    “Ya muda gani?”
    “Mwezi mmoja.
    “Gharama ni shilingi elfu kumi na tano,” alisema Dk. Lumanyika.
    “Hakuna tatizo.”


    Mwili wa Maimartha ulichoka, kazi ya kutolewa mimba ikafanyika kwa mafanikio makubwa. Japokuwa alikuwa akiogopa lakini hakupata tatizo lolote lile.
    Kutokana na mchoko huo, alishindwa kwenda nyumbani, alichokifanya ni kwenda nyumbani kwa kina Mark na kulala huku akitaka mwili wake urudiwe na nguvu tena.
    Alishinda asubuhi yote hiyo kitandani. Machozi yalikuwa yakimtoka, hakuamini kama alikuwa amefikia hatua ya kutoa mimba. Aliaminika kanisani kwamba alikuwa mtakatifu na katika nyimbo zote za kusifu na kuabudu, yeye ndiye alikuwa kiongozi kanisani kwao huku kila walipokuwa wakija wachungaji mbalimbali wa kitaifa na kimataifa, yeye ndiye alikuwa kiongozi wa kusifu na kuabudu.
    Leo hii, kiongozi huyo alikuwa ametoa mimba, lilikuwa suala moja lililomsikitisha mno, hakuamini kama kweli alifikia hatua hiyo iliyomsononesha kupita kawaida.
    Japokuwa alijaribu kumuomba Mungu msamaha lakini aliona kwamba asingeweza kumsamehe kutokana na uovu huo aliokuwa ameufanya.
    “Nimekutenda dhambi Mungu wangu,” alisema Maimartha huku akiwa ameufunika uso wake na mto, staili ya kigubigubi.
    Kama kulia, siku hiyo alilia na kuomboleza, kila kitu kilichokuwa kimetokea kwake alikiona kama yupo ndotoni na baada ya muda fulani angeamka kutoka usingizini.
    Katika maisha yake yote, hakufikiria kama kuna siku angefanya jambo kama hilo, hakika lilimsikitisha kupita kawaida.
    Huku akiwa katika hali hiyo, Mark akaingia chumbani humo, akaanza kumsogelea Maimatha kitandani pale, alipomfikia, akamuinua na kumuegemeza mapajani mwake.
    “Usilie mpenzi wangu,” alisema Mark kwa sauti ya chini.
    “Nimemtenda Mungu dhambi.”
    “Najua. Hautakiwi kujuta namna hiyo mpenzi. Futa machozi yako,” alisema Mark.
    “Mark....”
    “Naam.”
    “Kweli nimetoa mimba?”
    “Ooopppsss....”
    “Siamini kama ningepitia katika hatua hii Mark, siamini kama ingetokea siku ambayo ningetoa mimba,” alisema Maimartha na kuanza kulia tena.
    Asubuhi hiyo, Mark alikuwa na kazi ya kumbembeleza kipenzi chake tu, hakupenda kumuona akiwa kwenye hali hiyo, alimthamini kwa kuwa alikuwa sehemu ya maisha yake.
    Kila alipokuwa akibembelezwa, Maimartha alilia zaidi. Kila alipokuwa akikumbuka kile kilichokuwa kimetokea, moyo wake ulimuuma mno.
    Ilipofika jioni, Maimartha akaondoka kuelekea nyumbani kwao. Alipofika huko, akaingia chumbani na kutulia kitandani. Siku nzima kwake ilikuwa mbaya, macho yake yalikuwa makundu kwa sababu ya kulia sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Una nini?” aliuliza bi Estelina alipoingia chumbani na kumkuta binti yake akilia.
    “Ninaumwa mama.”
    “Unaumwa nini?”
    “Nahisi homa na kichwa kinagonga,” alidanganya Maimartha.
    “Ngoja tukemee roho hiyo ya magonjwa,” alisema bi Estelina na kisha kuanza kumuombea Maimartha.
    Maombezi hayo yalimuumiza kupita kawaida. Aliuhisi moyo wake kuingia kwenye hukumu ya Mungu, kile kilichokuwa kimetokea na maombezi ambayo alikuwa akifanyiwa na mama yake, yalionekana kama kuwa mzaha mbele za Mungu.
    Hakumzuia mama yake, alimwacha aendelee kumuombea japokuwa alijua fika kwamba kile alichokuwa amemwambia kilikuwa ni uongo.
    Kuanzia siku hiyo, Maimartha hakutaka kuonana na Mark, tendo la kutoa mimba lilibaki kama alama kubwa moyoni mwake ambayo isingeweza kufutika maisha yake yote.
    Akamrudia Mungu, akaanza kumuomba msamaha huku kila wakati akijitakasa. Hakutaka tena kujihusisha katika mapenzi, mimba aliyokuwa ameipata na kuitoa tayari lilikuwa fundisho kubwa kwake.
    Siku ziliendelea kukatika, mtoto wa mchungaji, John hakutaka kumuacha, kila siku alikuwa akimfuata na kumwambia jambo lilelile kwamba alitaka awe mpenzi wake, waingie kwenye uchumba na hatimae wafunge ndoa kanisani.
    Hilo lilionekana kuwa jambo lisilowezekana hata kidogo, uhusiano na Mark ulimfundisha mambo mengi likiwepo lile la kupata mimba na mwisho wa siku kuitoa. Hakutaka kurudia kosa mara mbili.
    “Maimartha, hautaki kuwa mama mchungaji?” aliuliza John.
    “Nimesema sitaki John, wewe nielewe tu, sitakiiii,” alisema Maimartha.
    “Hapana Maimartha. Lakini kwa nini unakuwa hivi?”
    “Nimekuwaje?”
    “Mkali tofauti na siku nyingine. Hebu punguza ukali jamani, unanionea ukifanya hivyo,” alisema John kwa sauti ya kubembeleza.
    “Nitaliambia kanisa ukiendelea kunifuatilia,” alitoa mkwara Maimartha.
    “Hakuna tatizo. Wewe liambie tu, kwani ninaamini kila kitu utakachowaambia kitakuwa kweli kwamba ninakutaka, waambie tu, tena bora kila mtu ajue hapo ndiyo utaamini ni kwa jinsi gani mapenzi yangu yalivyokuwa makubwa kwako,” alisema John.
    “Nimesema sikutaki, mbona unanilazimisha wewe mwanaume?” alisema Maimartha kwa sauti ya juu kidogo, watu waliokuwa pembeni kanisani hapo wakasikia, mchungaji akaanza kuwafuata, alionekana kuchukizwa.
    “Bora mchungaji aje nimwambie ukweli,” alisema Maimartha maneno yaliyomfanya John kuanza kutetemeka. 


    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog