Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

LET'S CALL IT A NIGHT - 4

 





    Simulizi: Let's Call It A Night

    Sehemu Ya Nne (4)



    “Kuna nini?” aliuliza mchungaji huku akionekana kubadilika, maneno aliyoyaongea Maimartha yalionyesha kabisa kwamba mtoto wake, John alikuwa akimtongoza.

    “Mwambie sasa,” alisema John.

    “Eti Maimartha kuna nini?” aliuliza mchungaji, Maimartha akabaki kimya.

    “Ngoja nikueleze kilichotokea,” alisema John.

    “Kumetokea nini?”

    “Bwana amenionyesha kwamba Maimartha ndiye atakuja kuwa mke wangu, ninajaribu kumwambia kuhusu hilo, anaipinga sauti ya Bwana,” alisema John, kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa ‘serious’ na kile alichokuwa akikizungumza.

    “Maimartha, ni kweli?’ aliuliza mchungaji.

    “Baba mchungaji, John amekuwa akinisumbua sana,” alisema Maimartha.

    “Si kwamba ninamsumbua, najaribu kumwambia juu ya kile ambacho Bwana amenionyesha, siwezi kuipinga sauti yake,” alisema John.

    “Hebu twendeni ofisini.” Alisema mchungaji na wote kuanza kuelekea ofisini.

    Hofu yote aliyokuwa nayo John ikatoweka, alijua fika kwamba baba yake alikuwa mkali na hakuwa na masihala yoyote yale hasa kuhusu ishu nzima ya kumtumikia Mungu, kitendo ambacho Maimartha alikuwa amekizungumza kilimkasirisha mno.

    “Nitakupenda siku zote Maimartha,” alisema John kwa sauti ya chini ambayo baba yake hakuisikia kule mbele alipokuwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sikutakiiii,” naye Maimartha alisema kwa sauti ya chini.

    “Huwezi kuipinga sauti ya Mungu, wewe ni wangu tu.”

    “Tutaona.”

    Walipofika ofisini kwa mchungaji, wakaambiwa wakae chini na Maimartha kupewa nafasi ya kuzungumzia sula hilo toka mwanzo mpaka mwisho. Hakuficha kitu, alielezea kila kitu kilichokuwa kimetokea, toka siku ya kwanza John alipoanza kumfuatilia mpaka siku hiyo. Mchungaji alikarika mno, kitu alichokuwa akitaka kukiona ni kwamba mtoto wake huyo anakuwa na tabia nzuri itakayokuwa mfano mzuri kwa vijana wengine, kitendo cha kumtaka Maimartha kimapenzi kilimkasirisha.

    “Umeanza lini tabia hii John?”

    “Baba, kwani kuna tatizo kumwambia mtu kile ambacho nimeonyeshwa kwenye maono?” aliuliza John.

    “Nipo ofisini, niite mchungaji.”

    “Sawa mchungaji. Nimwambia Maimartha kile kilichokuwa moyoni mwangu. Nimeonyeshwa kwamba yeye ndiye mke wangu wa baadae, nilichokuwa nikikifanya ni kumwambia kile nilichoonyeshwa.”

    Japokuwa alikuwa akidanganya lakini usingeweza kumgundua kwa kumwangalia. Uso wake ulionyesha kwamba kila kitu alichokuwa akikizungumza mahali pale kilikuwa kweli kabisa.

    Alijua kwamba mtoto wake alifanya kosa lakini utetezi wake juu ya kosa lile alilokuwa amelifanya ulikuwa ni wa kiwango cha juu kabisa.

    “Mchungaji, na wewe unataka kuyapinga maono ya Mungu?” aliuliza John, aliupa ujasiri moyo wake.

    “Una uhakika ni Mungu?”

    “Asilimia mia moja.”

    “Maimartha, Mungu amekuonyesha kitu chochote?”

    “Hapana. Hajanionyesha hata mara moja.”

    “Mchungaji, wala asijali, Mungu hufanya vitu kwa zamu, katoka kwangu basi atakwenda kwake,” alisema John.

    Kwa sababu alikuwa muongeaji sana, John akashinda kwa ushindi mkubwa. Mchungaji hakuwa na cha kusema yaani ilikuwa ni sawa na kutokumkutia hatiani mtuhumiwa, alichokifanya ni kuwapa ushauri wa kimaandiko na kisha kuwataka waondoke.

    Hiyo ikawa imechochea moto, John hakuacha zaidi ya kuendelea kasi zaidi za kumfuata Maimartha mpaka kikafika kipindi ambacho msichana huyo akajua kwamba ni kweli Mungu alikuwa amemuonyesha John kwamba alitakiwa kuwa mke wake hapo baadae.

    Katika hali ya kushangaza, Maimartha akajikuta akianza kumpenda John. Kila alipokwenda kanisani, alipokuwa akimuona John moyo wake ulifarijika sana.

    Hakutaka hali hiyo itokee moyoni mwake lakini alishindwa kuizuia kabisa, alijiona kuwa kwenye mapenzi ya kweli na kijana huyo.

    “Please stooooooop,” alisema Maimartha katika kipindi alichokuwa kitandani usiku, aliyaambia mawazo yake yaache kumfikiria sana John.

    Hilo lilikuwa jambo gumu kutokea, kila alipogeukia huku na kule, mawazo juu ya John yaliongezeka zaidi. Alibaki akigalagala kitandani pale, John aliutesa moyo wake kwa kipindi kirefu kitandani pale.

    Moyo wake ukaanza kuingia kwenye mapenzi ya dhati kwa mvulana huyo mpaka kufikia kipindi kilimpelekea kujutia uamuzi wake wa kumkatalia mvulana huyo toka kipindi cha nyuma.

    “Nahisi naye Mungu ameanza kunionyeshea kwamba John ndiye mume wangu wa maisha yangu,” alijisemea Maimartha

    Usingizi ulipaa kabisa, moyo wake ulisumbuliwa na taswira ya John tu. Mapenzi yalimzidi nguvu, yaliunyanyasa mno moyo wake mpaka kufika hatua iliyompelekea kulitamka jina la mvulana huyo kila wakati chumbani humo.

    Kadiri dakika zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele, mapenzi juu ya John yalizidi kuongezeka, kila alipogeuka kitandani pale, aliusikia moyo wake ukisema John, John, John, John.

    ****

    Maisha yake hakuyatuliza kwa Mungu tu ambaye kila siku alikuwa akimuabudu kanisani bali yalijaa mchanganyiko, mguu mmoja alikuwa amekanyaga upande wa Mungu na mwingine alikuwa amekanyaga upande wa shetani.

    Mbele yake kulikuwa na pande mbili ambazo zote hizo alikuwa akitaka kuzitumikia kwa wakati mmoja. Alishindwa kusimama upande mmoja kwa sababu pande zote hizo mbili zilimvutia.

    Kila alipokuwa akisimama mbele kanisani na kuanza kuimba, watu walikuwa wakitetemeka, sauti yake ilikuwa ni ya kipekee sana na hata nyimbo za kuabudu alizokuwa akiziimba zilionekana kuwa na upako, machozi yalivyokuwa yakimtoka, alionekana kweli alikuwa mtakatifu hata zaidi ya mchungaji wa kanisa hilo.

    Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku. Mapenzi yaliusumbua sana moyo wake, kila alipokuwa akimuona John, alikuwa akiweweseka huku kila siku akijiona kuogelea kwenye dimbwi la mahaba.

    Kwa sababu ya maneno yake aliyompa John kipindi cha nyuma kwamba hakuwa akimtaka, naye kijana huyo hakutaka kumfuata tena, kila alipokuwa akimuona, alipishana naye bila kumpa salamu yoyote ile.

    Hicho kilikuwa miongoni mwa vitu vilivyomuumiza mno, hakuamini kama John yule aliyekuwa akimpenda ambaye katika siku za nyuma alimfuata na kumwambia maneno mengi ya kimapenzi leo hii alikuwa akimpita bila hata salamu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “John, naomba usinifanyie hivi, naomba unisamehe kwa kila kitu nilichokufanyia,” alisema Maimartha huku akimwangalia John katika kipindi alichosimama mbele akiwaongoza watu kwenye kipindi cha kuabudu, macho yake aliyafumbua kificho na kumpiga kijana huyo jicho la wizi.

    “Mapenzi yananiumiza sana, kwa nini imekuwa hivi? Hivi ni nani ninayeweza kumwambia juu ya tatizo langu? Ni nani atakayemwambia John juu ya ninavyojisikia moyoni?” alijiuliza Maimartha lakini hakupata jibu zaidi ya kuendelea kuumia kila siku.

    Alipoona kila kitu kinashindikana ndipo alipoanza kwenda nyumbani kwa mchungaji mara kwa mara. Lengo lake si kwenda kumtembelea mchungaji au mama mchungaji kama alivyokuwa akisema bali lengo lake kubwa lilikuwa ni kumuona John tu.

    Alipomkosa nyumbani huko, alisikitika zaidi lakini kila alipomuona, alijihisi kuburudika moyoni mwake. Hata kama hakuwa na ishu yoyote ile, alikuwa akikaa nyumbani hapo kwa muda mrefu tu.

    Hakujua ni kwa jinsi gani alitakiwa kumuingia John ili aweze kumueleza kile alichokuwa akijisikia. Alijiona kuwa na mzigo mzito moyoni mwake huku mtu pekee ambaye alitakiwa kuutua mzigo huo akiwa John, mtoto wa mchungaji.





    Salvation Christians lilikuwa moja ya mashirika ya dini ambayo yalikuwa
    yakizunguka katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya kusambaza Neno la Mungu.
    Shirika hili la dini ya Kikristo katika Dhehebu la Kipentekoste lilikuwa na kazi
    kubwa ya kusambaza Injili katika mataifa mbalimbali ili kwa wale waliokuwa
    hawamjui Mungu basi waweze kumjua, wafunuliwe na kuokolewa maishani mwao.
    Shirika hili lilianzishwa mwaka 1980 huku likiwa na Wamarekani wawili tu, bwana
    Simpson na mkewe, bi Katie. Hawa walikuwa Wainjilisti ambao kila siku walikuwa
    wakisafiri huku na kule kueneza Neno la Mungu hasa katika sehemu ambazo Neno
    hilo halikutapakaa sana.
    Kwa mara ya kwanza kazi ikaanza nchini China. Huko walikutana na ugumu
    mkubwa wa kuwabadilisha watu wamfuate yule Mungu aliyeandikwa katika Biblia
    na vitabu vingine vya dini kwani katika nchi hiyo, asilimia tisini na tano ya watu
    walikuwa wakiabudu miungu ya udongo, miti ambayo kwao ilijulikana kama
    buddha.
    Wachina hawakuonekana kuwa wepesi kukubaliana na ukweli waliokuwa
    wakiambiwa, hawakutaka kumuabudu Mungu ambaye hawakuwa wakimuona,
    walibaki na msimamo wao kwamba mungu wa kweli alikuwa buddha na si huo
    ambaye bwana Simpson alikuwa akimzungumzia na mke wake.
    Ndani ya mwezi mmoja ambao walikaa nchini China, walifanikiwa kujenga kanisa
    dogo lililokuwa na washirika ishirini na kisha kuondoka zao kuelekea katika nchi
    nyingine.
    Kazi kubwa waliyokutana nayo ilikuwa katika nchi nyingine ndani ya Bara la Asia.
    Kulikuwa na idadi kubwa ya miungu kiasi kwamba kila walipokuwa wakienda, watu
    waliendelea kutoa sababu kwamba kamwe wasingeweza kumwabudu Mungu
    wasiyemuona.
    Kazi ya kuisambaza injili ndani ya Bara la Asia iliwachukua miezi sita na ndipo
    walipoamua kurudi nchini Marekani. Kwa kuwa shirika lao hilo liliendelea
    kujitangaza, watu wakaanza kujiunga nao huku michango mingi ikitolewa kwa ajili
    ya kuendesha kazi za shirika hilo.
    Mpaka inafika mwaka 1990, tayari shirika hilo lilikuwa limejikusanyia watu zaidi ya
    elfu sabini na walikuwa wametapaa katika ncini mbalimbali duniani huku wakiwa
    na kiasi cha zaidi ya dola bilioni mbili katika akaunti yao.
    Ilipofika mwaka 1992, bwana Simpson akafariki dunia huku akiwa na miaka sabini,
    kazi kubwa akaiacha kwa mkewe ambaye naye mwaka uliofuata, akafariki dunia
    huku akiwa na miaka sitini na nane.
    “Gospel of God never dies” (Injili ya Mungu haifi)” alisema Williams, kijana
    aliyeachwa na kuwa kiongozi.
    Kadiri miaka ilivyozidi kwenda mbele shirika hilo liliendelea kukusanya watu wengi
    huku makanisa yakizidi kufunguliwa katika nchi nyingi duniani. Mpaka kufika
    mwaka 1993, Shirika la Salvation Christian likawa moja ya mashirika yenye fedha
    nyingi duniani huku likiongozwa na Shirika la Msalaba Mwekundu.
    Mwaka 1994 shirika hilo likaanza kuzitembelea nchi za Afrika. Nchi ya kwanza
    kutembelewa ilikuwa Misri, huko, walikwenda watu mia moja ambao walikuwa
    wamegawanyika katika makundi tofautitofauti.
    Walikuwepo watu waliohusika katika kuhubiri kila walipokuwa, walikuwepo wale
    waliohusika katika kupiga muziki, walikuwepo wale waliokuwa na kazi ya kuimba
    na wa mwisho walikuwepo wale waliokuwa maalumu kwa ajili ya kufanya
    maombezi tu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Wakafanikiwa kufungua makanisa mawili huku wakiwapata wakiwaacha Wamisri
    thelathini na mbili makanisani na kisha kuendelea na safari yao.
    Ilikuwa ni safari ngumu kupita kawaida. Wakati mwingine walikuwa wakikutana na
    vizuizi vya wanajeshi wa majini kwa sababu usafiri wao mkubwa ulikuwa meli
    ambayo waliinunua maalumu kwa ajili ya kazi yao tu.
    Mwaka huo walipanga kutembelea nchini Rwanda kwa ajili ya kuendeleza Injili
    ndani ya nchi hiyo. Kwa bahati mbaya, wakakutana na vita vya wenyewe kwa
    wenyewe kitu kilichowapa ugumu mno katika kukamilisha mipango yao.
    “Tulitaka kwenda katika Chuo cha Usharika Nkuluwele, lakini haitowezekana, vita
    vimesambaa mpaka chuoni hapo na kuna taarifa kwamba zaidi ya wanachuo
    ishirini wameuawa,” alisema mchungaji Randy mara baada ya kupokea taarifa
    kutoka kwa mwenyeji wao, Ndizeyi.
    Taarifa hiyo haikuwa nzuri walichokifanya ni kuendelea na safari yao mpaka nchini
    Tanzania ambapo wakaweka ukaribu na Dhehebu la Praise And Worship kwamba
    kila walipokuja nchini Tanzania, wenyeji walikuwa ni dhehebu hilo kubwa nchini
    Tanzania.
    ****
    “Unanipenda mimi? Umeanza lini? Umekuja kunifuata ili baadae uwatagazie watu
    kanisani kwamba nimekutongoza ili nitengwe kanisani? Hebu acha upuuzi wako,
    ujanja wako naujua sana,” alisema John huku akiwa pembezoni mwa nyumba yao,
    mbele yake alikuwepo Maimartha aliyekuwa akililia kuwa naye.
    Kila siku alikuwa mtu wa kuvumilia tu, moyo wake uliumia kwa kipindi kirefu,
    alikosa raha kwa sababu mapenzi aliyokuwa nayo moyoni hayakuwa yakielezeka.
    Kwa kipindi kirefu mno alikuwa akitamani sana kumwambia John ukweli lakini
    alijawa na hofu kubwa.
    Siku zilikatika mpaka kufikia kipindi ambacho kwake akakiona kuwa sahihi
    kuzungumza kile alichokuwa akikisikia moyoni mwake, kumwambia ukweli namna
    alivyokuwa akimpenda.
    “Ninakupenda John, ninakuhitaji,” alisema Maimartha huku akijitahidi kuyatafuta
    machozi ili aonewe huruma.
    “Umeanza lini kunipenda? Unanishangaza sana. Nilikwambia hivyo kipindi cha
    nyuma ukaniletea pozi, sasa shobo za nini?”
    “John, naomba unielewe.”
    “Hebu nipe muda kwanza nijifikirie, nyie watumishi wa Mungu mnakuwa na mitego
    sana,” alisema John.
    John hakutaka kumuelewa msichana huyo, kila siku naye akawa mtu wa kumfikiria
    Maimartha tu. Maneno aliyomwambia yalimshtua, alikumbuka fika kwamba katka
    kipindi cha nyuma yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumwambia maneno ya
    kimapenzi lakini matokeo yake suala hilo likafika kwa mchungaji.
    Leo hii, msichana yuleyule ndiye aliyemwanzishia maneno hayo ya kimapenzi, ndiye
    aliyemfuata na kumwambia vilevile kama alivyomwambia kipindi cha nyuma, John
    alichanganyikiwa kwani hakuwa akijua kama Maimartha alikuwa akimaanisha au
    alimwambia hivyo kwa kuwa kulikuwa na kitu fulani.
    “John, hakuna kitu, ninakupenda, nipo tayari kuwa mke wako,” alisema Maimartha.
    Mapenzi mapenzi tu, Maimartha alionekana kuchanganyikiwa kwa mvulana huyo,
    kila neno alilokuwa akiliongea lilionekana kutokutosha kabisa kitu kilichomfanya
    kutamani kuwepo na neno jingine zaidi ya ‘nakupenda’
    “Kuna kitu,” alisema John.
    “Hakuna kitu.”
    “Lakini kwa nini iwe sasa hivi na isiwe zamani?”
    “Sijajua John. Ninakupenda.”
    “Nashukuru.”
    “Ninataka uwe mpenzi wangu.”
    “Maimartha....”
    “Abeee.”
    “Wewe ni mtumishi wa Mungu.”
    “John. Naomba usilizungumzie hilo. Ninakupenda.”
    “Ooppss....”
    “Please John, love me” (Tafadhali John, nipende)
    “Maimartha, do you remember the first time when I came to you? What did you tell
    me? I am not deserve to be your husband, right? Bad enough, you told my father.
    Maimartha, why now? How do I look, handsome than the way I was last few
    weeks? Tell me, what do you think I have,” (Maimatha, unakumbuka kara ya
    kwanza nilipokufuata? Uliniambia nini? Sistahili kuwa mume wako, sawa? Mbaya
    zaidi, ulimwambia baba yangu. Maimartha, kwa nini iwe sasa hivi? Ninaonekana
    vipi, mzuri zaidi ya nilivyokuwa wiki chache zilizopita? Niambie, unafikiri nina nini)
    John aliuliza maswali mfululizo.
    “I love you John” (Ninakupenda John)
    “Nina kitu gani ambacho sikuwa nacho kabla?”
    “You have everything I want” (Una kila kitu ninachokitaka)
    Kwa muonekano wake tu, Maimartha alionekana kumaanisha kile alichokuwa
    akikizungumza mbele ya John. Mapenzi yalimpelekesha kupita kawaida, alikuwa
    radhi kufanya kitu chochote kile salama lakini kumuona John akimkataa na
    kwenda kuwa na msichana mwingine.
    Katika kila swali aliloulizwa alitoa majibu yanayojitosheleza kitu kilichomfanya
    John kukubaliana na uamuzi wa msichana huyo na hatimae kuanzisha uhusiano
    wa kimapenzi uliotakiwa kuwa siri kubwa.
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya miaka mingi kupita huku wakiendelea kwenda huku na kule katika
    kusambaza Neno la Mungu, hapo ndipo wakafika nchini Rwanda kwa mara
    nyingine tena kwani mara ya mwisho kufika nchini hapo hawakuwa
    wamefanikiwa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa
    vikiendelea.
    Kila kitu kwa wakati huo kikaenda vizuri, hakukuwa na ugumu wowote kwani
    zaidi ya watu elfu kumi waliamua kuyabadilisha maisha yao na kuokoka. Hiyo
    ikawa furaha kubwa kwao, kile kilichokuwa kimewapeleka nchini humo
    kilifanikiwa kwa zaidi ya asilimia sitini.
    Hawakurudi nyuma, waliendelea kusonga mbele zaidi. Walipotoka hapo,
    wakaelekea mpaka nchini Burundi, kote huko walikuwa wakiendelea kuhubiri
    kwa watu mbalimbali na kwa mafanikio makubwa wengi wakaokoka.
    Baada ya miezi miwili ya kutembelea Rwanda, Burundi, Kongo, Kenya na ndipo
    walipoamua kuweka mikakati ya kufika nchini Tanzania.
    Zaidi ya watu mia moja walipangwa kuelekea nchini Tanzania ambapo huko
    wangefanya ziara kwa kipindi cha miezi miwili na kisha kuondoka kuelekea
    nchini India kabla ya kurudi nchini Marekani kuendelea na mambo mengine.
    Kwa sababu walijigawa kimakundi, wote wakakutana nchini Kenya na kisha
    kuanza safari ya kuelekea nchini Tanzania huku kila mmoja akionekana kuwa
    na furaha kutokana na nchi waliyokuwa wakielekea katika kipindi hicho ilikuwa
    moja ya nchi iliyosifika kwa amani duniani.
    “After two months, we are going back home” (Baada ya miezi mitatu, tunarudi
    nyumbani) alisema mchungaji wao ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa shirika
    hilo kwa kipindi hicho, Simon Pegg.
    ****
    Mapenzi yalikuwa motomoto baina ya mtoto wa mchungaji, John na msichana
    aliyekuwa akisifika kwa kuwa na sauti nzuri, Maimartha. Mapenzi hayo
    yalikuwa ni siri kubwa na waijitahidi kujificha ili mtu yeyote asiweze kugundua
    kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yao.
    Mara kwa mara walikuwa wakikutana maeneo ya Jangwani ambapo huko
    walikuwa wakifanya yao na kisha kurudi nyumbani. Walipendana mno huku kila
    mmoja akiona kwamba wangeweza kuwa mke na mume hapo baadae.
    Kama kuimba, Maimartha hauacha kufanya hivyo, bado aliaminika kanisani na
    wala hakukuwa na mtu ambaye aligundua au hata kuhisi kwamba msichana
    huyo alikuwa katika mapenzi mazito na mtoto wa mchungaji wa kanisa hilo,
    John.
    Wiki ya kwanza ya mapenzi yao ikakatika, kila mmoja akaonekana kuwa na
    furaha huku akihitaji kila wakati awe karibu na mpenzi wake. Wiki ya pili, ya
    tatu na ya nne zikaingia na kupita, mapenzi yao yaliendelea kuwa motomoto
    huku mara kwa mara wakiwa karibu.
    John ambaye hakuwa akifika kanisani mara kwa mara, naye akaanza kwenda
    mpaka katika ibada za katikati ya wiki, mazoezi ya kwaya, yote ikiwa ni kutaka
    kumuona mpenzi wake huyo.
    “Najifikiria siku kanisa likijua, aiseee, hakutokalika,” alisema Maimartha huku
    akiwa amemlalia John kifuani, walikuwa ndani ya nyumba ya wageni ya
    Mwaipopo iliyokuwa Tandale.
    “Unafikiri watajua vipi? Watatufumania au wataambiwa na mtu?” aliuliza John.
    “Vyovyote vile, yaani nahisi kama watajua.”
    “Hakuna kitu kama hicho. Tutaitunza siri hii, siku wakija kujua, tayari tutakuwa
    tumekwishaoana,” alisema John na kuanza kumchojoa Maimartha nguo
    alizokuwa amezivaa.
    Siku hiyo, kuanzia asubuhi mpaka jioni walishinda katika nyumba hiyo ya
    wageni. Hawakutaka kutoka nje kwani wote wawili waliwaaga wazazi wao
    kwamba walikuwa wakienda katika makundi ya kujisomea kwa ajili ya
    kujiandaa na mitihani ya mwisho ya kidato cha sita.
    “Wiki ijayo ni siku yangu ya kuzaliwa,” alisema John kwa sauti ya chini.
    “Itakuwa lini?”
    “Ijumaa bila shaka. Nitataka tuwe wote siku hiyo. Tusafiri tuelekee Bagamoyo.”
    “Mhh! Itawezekana kweli?”
    “Kwa nini tushindwe? Fedha ipo, tatizo kutumia tu.”
    “Sawa, tutaangalia mpenzi, hakuna tatizo.”
    Siku ambayo waliahidiana kwamba wangekwenda Bagamoyo ikawadia, kila
    mmoja alionekana kuwa na furaha, chumbani hotelini, walikuwa na kazi moja
    tu, kufanya ngono.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Siku hiyo ilikuwa ni ya furaha kwao, hakukuwa na mtu aliyefikiria maisha ya
    baadae yangekuwa vipi, kwa sababu walikuwa wakipendana kupita kawaida,
    hawakuonekana kama kuna ubaya wowote wa kufanya kile walichokuwa
    wakikifanya mahali hapo.
    Siku zikaendelea kukatika, baada ya siku kadhaa, Maimartha akaanza kujisikia
    mabadiliko mwilini mwake. Mwili wake ukaanza kupata uchovu mwingi, katika
    kila hali aliyokuwa nayo kipindi hicho, alikumbuka kwamba ilikuwa vilevile kama
    kipindi kile alichokuwa amepata mimba ya John.
    “Mmmh! Ni mimba tena?” alijiuliza Maimartha.
    Hakutaka kubaki nyumbani, dalili zile zikamfanya kuondoka na kuelekea
    hospitalini kwa ajili ya vipimo ili awe na uhakika juu ya kile alichokuwa
    akikihisi, alipofika, mkojo wake ukachukuliwa na vipimo kufanyika, hisia zake
    zilikuwa kwenye ukweli, alikuwa amepata mimba.
    “Mungu wangu! Nina mimba?” alimuuliza Dokta aliyempima huku akionekana
    kushtuka.
    “Ndiyo, ni ya mwezi mmoja,” alisema dokta huku akionyesha tabasamu pana.
    Maimartha hakutaka kubaki ndani ya chumba hicho, huku akionekana
    kuchanganyikiwa, akachomoka na kuelekea nje. Akaanza kupiga hatua kuelekea
    kituoni, muda wote alikuwa mtu wa kulia tu.
    Majuto yakaanza tena, akajuta kwa nini aliruhusu mimba itunge kwa mara
    nyingine na wakati alikuwa amejiahidi kwamba kamwe asingeweza kupata
    mimba kama ilivyokuwa kwa Mark.
    Japokuwa alijilinda sana kwa kumtaka John atumie mpira, mwisho wa siku
    alishindwa, hasa siku ile ambayo mvulana huyo alikuwa akisherehekea siku
    yake ya kuzaliwa, siku ambayo walikuwa chumbani kwa kipindi kirefu.
    Mtu ambaye alikuwa akimfikiria mahali hapo alikuwa John tu, huyo ndiye
    alikuwa mpenzi wake ambaye alitembea naye na alikuwa na uhakika kwamba
    mimba hiyo ilikuwa yake.
    Ndani ya daladala, Maimartha alikuwa mtu wa kulia tu, machozi yalikuwa
    yakibubujika mashavuni mwake, hakuamini kwamba angeweza kupata mimba
    japokuwa alijitahidi kujilanda kwa asilimia mia moja.
    Kuna wakati mwingine alikuwa akimalaumu Mungu kwa kuruhusu jambo lile
    kutokea maishani mwake kwani aliamini kwamba alikuwa muumini mzuri wa
    Mungu japokuwa kuna nyakati alikuwa akianguka kama binadamu.
    Janga la mimba lilimtesa mno, katika umri huo wa miaka ishirini, hiyo ilikuwa
    ni mimba ya pili kuipata. Huku akiwa kwenye mawazo lukuki juu ya nini
    alichotakiwa kumwambia John, kondakta akatangaza kituo cha Magomeni
    Usalama ambapo Maimartha akateremka na kuanza kuelekea nyumbani kwa
    kina John.
    “Ametoka,” alisema mama yake mara baada ya kumuulizia.
    “Amekwenda wapi?”
    “Kwa rafiki yake, Michael.”
    “Atachelewa sana kurudi?”
    “Sidhani. Maimartha, mbona upo hivyo? Macho mekundu, ulikuwa unalia?”
    “Hapana mama.”
    “Unaumwa?”
    “Hapana mama. Mimi mwenyewe nashangaa.”
    Maimartha hakutaka kuwa mkweli, usiri mkubwa ulikuwa moyoni mwake juu ya
    hali aliyokuwa nayo. Siku hiyo, hakutaka kuondoka mahali hapo, alikuwa
    akimsubiria John ili aweze kumwambia ukweli juu ya afya yake.
    Baada ya masaa matatu, John akafka nyumbani hapo, alipomuona Maimartha,
    akashtuka, hli aliyokuwa nayo ilikuwa tofauti kabisa, muonekano wake
    ulionyesha kwamba alikuwa na tatizo.
    “Kuna nini?” aliuliza John.
    “Naomba tukaongelee nje ya hapa.”
    Wote wakaaga na kuondoka. Huko, Maimartha akaanza kumwambia John
    ukweli juu ya hali aliyokuwa nayo kipindi hicho, John akashtuka mno.
    “Unasemaje?”
    “Nina mimba.”
    “Ya kwangu au?”
    “Sasa unafikiri itakuwa ya nani?”
    “Hapana. Unanidanganya Maimartha.”
    “Nina mimba yako John.”
    “Hapana, hiyo itakuwa ya mwingine tu. Sisi tulikuwa tukitumia mpira,
    hukumbuki?” aliuliza John huku akionekana kuchanganyikiwa.
    “John, sikuwa na mwanaume mwingine zaidi yako, hii ni mimba yako,” alisema
    Maimartha huku akianza kulia tena.
    “Haiwezekani Mai, unakumbuka kwamba sikukukuta bikira?”
    “John, hii ni mimba yako,” Maimartha alisema kwa sauti ya juu.
    “Hiyo si mimba yangu. Mtafute mweye mimba yake,” alisema John tena kwa
    sauti ya juu zaidi ya ile aliyoitoa Maimartha.
    Maimartha akashindwa kuvumilia, akajikuta akigeuka nyuma na kuanza
    kukimbia huku akilia kama mtoto mdogo. Mwaka huo ukaonekana kuwa mbaya
    kwake, ulikuwa mwaka uliojaa majanga ya mimba tu katika maisha yake,
    hakuamini kama John alikataa mimba ile, alibaki akijuta moyoni mwake.
    Alipofika nyumbani, moja kwa moja akapitiliza mpaka chumbani kwake,
    hakutaka kutoka, alilala kitandani huku akiwa ameukumbatia mto na wakati
    mwingine akiuficha uso wake katika uso huo huku akilia tu.
    “Mungu kwa nini umeruhusu mimba nyingine katika maisha yangu?” aliuliza
    Maimartha, hakukumbuka kwamba mstari aliokuwa si ule ambao alitakiwa
    kuwepo, kila alichokuwa akikisema, kwa Mungu kikawa kama hakisikiki kwani
    maisha yake yalijaa dhambi japokuwa kwa nje alionekana kuwa mtakatifu zaidi
    ya mchungaji.
    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Mpaka wazazi wake wanarudi nyumbani bado alikuwa akilia tu. Mimba
    aliyokuwa nayo ilimtia wasiwasi kwamba kulikuwa na uwezekano wa watu
    kufahamu na mwisho wa siku jina lake kuchafuliwa.
    “Ni lazima niitoe, haina jinsi, ila John, sitokusahau mpumbavu wewe, unaniona
    mimi malaya!” alisema Maimartha huku akionekana kuwa na hasira.
    Maimartha hakutoka chumbani kwake, hakutaka kuwaona wazazi wake kwa
    kuhisi kwamba wangeweza kumshtukia, alibaki chumbani mule huku kichwa
    chake kikiwa kwenye mawazo lukuki.
    “Ngo, ngo, ngo,” ulisikika mlango ukigongwa, tayari ilikuwa ni saa tatu usiku.
    Maimartha hakutaka kujisumbua kunyanyuka kwenda kuufungua mlango ule,
    kwa wakati huo hakuwa na ‘mood’ ya kuongea na mtu yeyote yule, alitaka
    kubaki peke yake chumbani ili akifikirie kile kilichokuwa kikiendelea katika
    maisha yake.
    “Maimartha....Maimartha, kama upo ndani fungua mlango,” alisikika mama
    yake, bi Estelina.
    Maimartha aliisikia vema sauti hiyo lakini hakuwa radhi kufungua mlango
    kwani bado alitamani kuendelea kubaki chumbani peke yake, hakutaka
    kusumbuliwa na mtu yeyote yule.
    Kadri sekunde zilivyoendelea kukatika na ndivyo ambavyo mama yake alivyozidi
    kuugonga mlango ule. Kwake, hali hiyo ikaanza kuonekana kuwa usumbufu
    mkubwa, hakukaa na kuwaza vizuri, kila alipogeuka, sauti ya mlango ilikuwa
    ikisikika kitu kilichomfanya kusimama na kwenda kuufungua mlango.
    “Kuna nini?” lilikuwa swali la kwanza lililotoka kwa bi Estelina.
    “Ninaumwa mama.”
    “Na mbona umefunga mlango?”
    “Nijisikia kuwa peke yangu mama. Sijisikii kuongea,” alisema Maimartha kwa
    sauti ya kichovu.
    “Umekunywa dawa?”
    “Ndiyo.”
    “Sawa. Subiri kwanza tukemee hiyo roho ya magonjwa ishindwe kwa jila la
    Yesu,” alisema bi Estelina na kukaa kitandani.
    Akaanza kumfanyia maombezi binti yake kwa kuamini kwamba kweli
    Maimartha alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kichwa. Muda wote huo
    Maimartha alikuwa akilia tu, unafiki aliokuwa akiufanya uliuumiza moyo wake.
    “Amen. Pumzika kwanza,” alisema bi Estelina na kumuacha Maimartha
    chumbani mule.
    Hakulala usiku mzima, alikesha kama popo. Muda wote, mawazo yake yalikuwa
    juu ya John tu, moyo wake uliumia mno kwani hatua alizokuwa akizipitia
    zilikuwa ngumu kumaliza salama.
    Wazo lililokuwa limekitawala kichwa chake ni kwamba alitakiwa kuitoa mimba
    ile tu, japokuwa alikuwa akiogopa kufanya hivyo lakini kwa hali aliyokuwa nayo
    kipindi hicho alikuwa tayari kukifanya kitendo hicho kwa mara ya pili tena.
    Asubuhi ilipofika, saa moja akaondoka na kuelekea Manzese katika ile
    dispensari ambayo aliitumia kipindi cha nyuma kwa ajili ya kutolea mimba.
    Alipofika, kwa kuwa ilikuwa ni asubuhi sana, haikua imefunguliwa hivyo
    kutakiwa kusubiri.
    Ilipofika saa 3:00 asubuhi, dispensari ikafunguliwa na kutakiwa kuingia ndani
    huku akiwa ni mgonjwa wa kwanza kabisa.
    “Nikusaidie nini?” aliuliza Dk. Nkini, maarufu wa kutoa mimba Manzese.
    “Nimekuja nina tatizo dokta.”
    “Tatizo gani?”
    “Mimi ni mwanafunzi na kwa bahati mbaya nimepata mimba.”
    “Kwa hiyo?”
    “Nataka kuitoa.”
    “Ni ya muda gani hiyo?”
    “Mwezi mmoja.”
    “Ulishawahi kufika hapa kabla? Sura yako si ngeni machoni mwangu.”
    “Nilikwishawahi kufika.”
    “Kwa tatizo hilihili?”
    “Ndiyo.”
    “Daah! Binti unachezea sana kizazi, kuwa makini,” alisema Dk. Nkini.
    Akatajiwa gharama zote alizotakiwa kulipa na kisha kazi kuanza mara moja.
    Japokuwa ilimuuma sana lakini hakuwa na jinsi, kwa wakati huo alichokuwa
    akikitaka ni kuitoa mimba hiyo ili asiweze kuahibika kwani alikuwa akionekana
    mtakatifu kanisani.
    ****
    Shirika la Kimishionari, Salvation Christian likaingia nchini Tanzania, miongoni
    mwa nchi ambayo kila siku walitamani kuiingia. Kila mmoja alionekana kuwa
    na furaha maokezi mazuri kutoka kwa washirika wa makanisa ya Kipentekoste
    ya Praise And Worship.
    Siku hiyohiyo, hawakutaka kwenda hotelini, breki ya kwanza ilikuwa ni katika
    Kanisa la Praise And Worship lililokuwa Mwenge ambapo wakaanza
    kumshukuru Mungu kwa kuwafikisha salama nchini Tanzania.
    Miongoni mwa washirika waliokuwepo katika kanisa hilo siku hiyo alikuwa
    Maimartha. Kama kawaida yake sauti yake ilimchanganya kila mmoja, alikuwa
    na sauti nzuri ambayo kila aliyeisikia aligundua kwamba binti huyo alikuwa
    amepata bahati ya upendeleo kutoka kwa Mungu.
    Katika kila wimbo wa kuabudu aliokuwa akiuimba kanisani hapo, nguvu za
    Mungu zikawa zinashuka kitu kilichompelekea hata yeye mwenye kuona
    kwamba bado Mungu alikuwa akimtumia japokuwa maisha yake yalijaa uovu.
    Walipomaliza, washirika wakatawanyika na wageni hao kuelekea katika hoteli
    ambazo walipangiwa ila kwa gharama zao wenyewe.
    Usiku, mchungaji Peggy alikaa na viongozi wengine wa shirika hilo la kidini na
    kuanza kuzungumza nao kuhusu binti mrembo waliyekutana naye mwenye sauti
    nzuri ya kumsifu na kumuabudu Mungu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Kwa kipindi kirefu walikuwa wakitafuta muimbaji kama Maimartha lakini kila
    muimbaji waliyekuwa wakimpata, alikuwa tofauti na yule waliyekuwa
    wakimtaka. Kwa Maimartha, msichana huyo akaonekana kuwa sahihi wa
    kuwepo katika shirika hilo kwa ajili ya kuwa muimbaji wao kwani sauti yake
    ilikuwa ni ya kipekee mno.
    Kikao hicho cha dharura kilichukua saa moja, kikakamilika na makubaliano
    kuwekwa kwamba Maimartha achukuliwe na kuanza kutumika katika shirika
    hilo la dini ambalo husafiri katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuhubiri
    Neno la Mungu.
    “When she sings, I see the glory of God comes upon me” (Anapoimba, ninauona
    utukufu wa Mungu unakuja juu yangu) alisema mchungaji Peggy.
    “Let’s talk to her, we have an opportunity to take her” (Tuzungumze naye, tuna
    nafasi ya kumchukua) alisema mke wa mchungaji Peggy, bi Regina.
    “No problem” (Hakuna tatizo)


    Wiki moja baada ya kumaliza mitihani yake, Maimartha akafuatwa na mchungaji Peggy pamoja na uongozi wa shirika lile la dini na kuambiwa kwamba alitakiwa kujiunga nao kwani walivutiwa na huduma yao kanisani.
    Hiyo, kwa Maimartha ikaonekana ni nafasi ya kipekee kwake, kitendo cha kumsifu Mungu huku akitembea katika nchi mbalimbali duniani kwake ikaonekana kama baraka kubwa.
    Makubaliano yakafanyika huku akiahidiwa kwamba taratibu zote za vibali vya safari vitaaanza kufanyiwa kazi.
    “Siamini mama,” alisema Maimartha mara baada ya mchungaji na viongozi wengine kuondoka.
    “Amini mwanangu, unajitoa sana kwa Mungu, kamwe hawezi kukuacha hivyohivyo,” alisema mama yake, bi Estelina.
    Maimartha akaondoka na kuelekea chumbani, bado hakuweza kuamini kile kilichokuwa kimetokea katika maisha yake. Wakati mwingine alijiona kama yupo usingizini ambapo baada ya muda angeshtuka na kujikuta akiwa chumbani, lakini kila kitu kilichokuwa kikitokea, hakikuwa ndoto.
    Furaha aliyokuwa nayo ikamfanya kupiga magoti chini na kumshukuru Mungu kwa kile kilichokuwa kimetokea, baada ya miaka kadhaa ya kumuabudu Mungu kwa kusifu kanisani, leo hii, Mungu aliyemwabudu aliamua kufungua milango zaidi.
    Kuanzia hapo, hakutaka tena kusikia habari za John wala Mark, aliamua kwa moyo mmoja kwamba kipindi hicho ndicho kingekuwa kipindi pekee ambacho kingemfanya kusimama sawasawa na Mungu wake.
    “Nitakuabudu maisha yangu yote Mungu wangu, sitotaka kujichanganya tena,” alisema Maimartha huku akiwa amepiga magoti na uso wake akiwa ameuelekezea juu.
    Baada ya mwezi mmoja, mchungaji Peggy akarudi ndani ya nyumba hiyo kwa mara nyingine huku akiwa na wasaidizi wake na kisha kuondoka na Maimartha huku akiwa amekabidhiwa kila kitu alichotakiwa kuwa nacho.
    Hakutakiwa kuishi nchini Tanzania, alitakiwa kuiendeleza karama yake ya uimbaji kwa watu mbalimbali duniani kwani Mungu alitakiwa kusifiwa sehemu mbalimbali kupitia sauti ambazo ametupa.
    Siku hiyo, hakuamini kama alikuwa akiingia katika meli ya kifahari tayari kwa kuanza maisha yake mapya. Ilikuwa ni meli kubwa yenye kila kitu ndani. Kulikuwa na vyumba vikubwa vyenye vitanda, televisheni, mashne za kufulia na vitu vingine vingi.
    Mbali na hivyo kulikuwa na chumba kikubwa kilichotumika kama sehemu ya kujisomea biblia na vitabu vingine. Kulikuwa na chumba kilichokuwa maalumu kwa kufanyia maombi, kufundishia neno la Mungu na vyumba vingine vingi, yaani kwa kifupi, meli hii ilijulikana kama ‘Nyumba inayoelea’.
    Alipofika ndani ya meli hiyo, Maimartha akakabidhiwa kwa watu wengine ambao muda wote waionekana kuwa na furaha kutokana na ujio wa msichana huyo mahali hapo.
    “Nitamsifu Mungu mpaka shetani anishangae,” alijisemea Maimartha katika kipindi alichokwenda ndani ya chumba kiichotumika kama kanisa kwa ajili ya kufanyia ibada.
    ****
    Sauti ya Maimartha ilikuwa ni ya kipekee sana, kila alipokuwa akiimba, hata kama ulikuwa mbali ungejua tu kwamba msichana huyo alikuwa amebarikiwa kuwa na sauti nzuri. 
    Nguvu za Mungu zilionekana kushuka kila alipokuwa akiimba, aliimba kwa hisia kali, kila alipokuwa akikumbuka uovu aliokuwa ameufanya katika maisha yake, alikuwa akibubujikwa na machozi tu.
    Maisha ya melini yalikuwa tofauti, hayakuwa sawa na maisha ya nyumbani. Kule, hakukuwa na mambo ya kuzurura au kupanda gari kwamba unaelekea sehemu fulani, huko ilikuwa ni kukaa ndani tu.
    Ukubwa wa meli, mitambo mingi ya kisasa iliyowekwa melini iliifanya kuwa imara na hata kama bahari ilikuwa ikichafuka, ndani kulionekana kuwa salama kabisa.
    Nchi ya kwanza kwa Maimartha kwenda ilikuwa ni India. Mkutano mkubwa wa Injili ambao ulitangazwa nchini humo ulitarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Eden Garden uliokuwa ndani ya jiji la West Bengal
    Ingawa matangazo ya mkutano huo yalikuwa yametangazwa kwa muda wa mwezi mzima, lakini muitikio wa watu uwanjani hapo haukuwa mkubwa kabisa, hawakuzidi hata watu elfu moja.
    Ilikuwa ni hali mbaya, hakukuwa na mtu aliyefikiria kwamba kitu kama kile kingeweza kutokea, walichokuwa wamekifikiria ni kwamba uwanja huo ungejaza sana lakini mwisho wa siku, walikuwa wamefika watu wachache mno.
    Kuna kipindi kingine walijuta juu ya sababu iliyowafanya kuleta mkutano huo ndani ya Jiji la West Bengal badala ya kupeleka Mumbai au Delhi.Hawakutaka kujuta sana kwani waliamini inawezekana Mungu alikuwa na makusudi na watu hao wachache.
    “Mungu atafanya jambo,” alisema mchungaji Peggy, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na imani kubwa.
    Siku ya kwanza ikapita, zikawa zimebakia siku sita tu za kufanya mkutano huo wa Injili ndani ya uwanja huo. Siku hiyo, ilikuwa ni afadhali ya siku ya jana, watu walifika wachache mno tena wengi wao wakiwa wale waliookoka siku iliyopita.
    “Unajua kuziimba zile nyimbo za Don Moen, zile za kuabudu?” aliuliza Christopher, kiongozi wa sifa na kuabudu ndani ya shirika hilo la kidini.
    “Ninazifahamu zote,” alijibu Maimartha.
    “Kumbe unazifahamu, tulidhani hauzifahamu. Sasa leo utaongoza sifa mkutanoni,” alisema Christopher.
    “Hakuna tatizo.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuongoza sifa na kuabudu mbele ya umati mkubwa wa watu. Sauti yake iliposikika katika spika zilizokuwa uwanjani hapo tu, watu waliokuwa nje ya uwanja huo wakaanza kuingia ndani ya uwanja huo ktu kilichomshangaza hata mchungaji Peggy.
    Sauti ya Maimartha ilikuwa ni ya kipekee mno, kwa jinsi ilivyokuwa ikitoka, hakukuwa na mtu aliyetarajia kuona kama kulikuwa na mtu mwenye sauti kama ile, hata wale waimbaji wa nyimbo zao za Kihindi, hawakuwa na sauti nzuri kama ya Maimartha.
    Maimartha akageuka lulu mkutanoni hapo, kila alipokuwa akiimba nyimbo za kuabudu, Wahindi wote walikuwa kimya wakimsikiliza. Idadi chache ya watu mia tatu waliofika mkutanoni pale ikaongezeka, mpaka mkutano ulipomalizika, kulikuwa na watu zaidi ya elfu tano.
    Mitaani siku hiyo, kila mtu akawa anaizungumzia sauti ya Maimartha, ilikuwa ni ya kipekee sana kitu kilichowapelekea watu wasiofika katika mkutano ule kutamani kufika na mwisho wa siku kuisikia sauti hiyo.
    Siku ya tatu ya mkutano, kutokana na sifa zilizokuwa zikisikika mitaani, zaidi ya watu elfu tano wakawa wamekusanyika. Hayo yakaonekana kuwa mafanikio makubwa, kwa sababu wengi walifika mahali hapo kwa ajili ya kuisikia sauti ya Maimartha, hata mchungaji Peggy alipokuwa akihubiri, katikati ya mahubiri alikuwa akimruhusu Maimartha kusimama na kuimba pambio moja na kuendelea na mahubiri yake.
    Watu wakajikuta wakianza kumkabidhi Mungu maisha yao, watu kutoka sehemu nyingine nchini India kama Tamil Nadu, Maharashtra, Mumbai na sehemu nyingine wakafika mkutanoni kwa ajili ya kuisikia sauti ya binti huyo mrembo.
    “Ana sauti nzuri mno, aisee sijawahi kusikia sauti kama hii,” alisema jamaa mmoja, alikuwa Muhindi aliyekuwa akiabudu buddha.
    Kwa watu wengi waliokuwa wakifika uwanjani hapo kwa ajili ya kusikiliza sauti nzuri ya Maimartha, hawakuondoka hivihivi, wengi waliokoka na kuachana maisha yao ya kuiabudu miungu ya kuchonga, buddha.
    Maimartha akaonekana kuwa na thamani kubwa, kutumiwa kwake hakukuishia hapo, mpaka walipokwenda katika nchi nyingine, bado aliendelea na huduma yake ya kuimba na aliendelea kupendwa na kila mtu hasa sauti yake nzuri.
    Mwaka wa kwanza ukakatika, bado alikuwa mtu wa kukaa ndani ya ndege hiyo na kama walikuwa wakitoka, basi ni kukaa nchini Marekani na baada ya miezi kadhaa kuondoka kuendelea na huduma kama kawaida.
    Siku ziliendelea kukatika, mwaka wa pili ukaingia na kupita, baada ya miezi kwenda kwa kasi, mwaka wa tatu ukaingia na kijana mmoja mtanashati mwenye asili ya Kigiriki akajiunga na shirika hilo la kidini.
    Kwa kumwangalia, alikuwa kijana mpole mno, mtanashati na ambaye hakuwa muongeaji sana. Kila alipokuwa akikaa, kijana huyu aliyeitwa Damian Dimitri alikuwa mtu wa kusoma Biblia tu.
    Ndani ya meli hiyo, kila mtu akafurahi kumpata mtu kama huyo ambaye alijitolea maisha yake yote kumtumikia Mungu. Hakuwa muimbaji wala mpiga vyombo, kwa Damian, yeye alikuwa ni mtu wa kuhubiri tu, aliijua vema Biblia na hata kila alipokuwa akisimama mbele za watu, maandiko aliyokuwa akiyasoma na kuyafafanua, yalimshangaza kila mmoja. Watu wote wakakubaliana kwamba jamaa alikuwa na karama ya uhubiri hali iliyomfanya kuaminika na kila mtu akiwepo mchungaji Peggy.


    Alikuwa miongoni mwa watu masikini waliokuwa wakiishi katika kijiji masikini cha Kiryas Joel kilichokuwa katika mji wa Monroe ndani ya Jiji la New York nchini Marekani.
    Kijana huyu aliyejulikana kwa jina la Damian Dimitri, alikuwa tofauti na vijana waliokuwa wakiishi kijijini hapo. Muda mwingi alikuwa mkimya, hakuwa mzungumzaji sana kama walivyokuwa watu wengine.
    Maisha yake hayo yakamfanya kuwa na marafiki wachache kwani tangu alipohamia kikijini hapo miaka kumi iliyopita, hakuwa na marafiki wengi.
    Ukimya wake ukamfanya kupendwa na wazee wengi, vijana wengi wakatakiwa waige mfano wa maisha yake kitu kilichoonekana kuwa kigumu kwao.
    Miaka ikakatika, Damian aliendelea kuonekana tofauti kwa vijana wengine waliokuwa mahali hapo. Hakukuwa na mtu aliyejua maisha yake ya nyuma yalikuwa ni ya namna gani, hakukuwa na mtu aliyefahamu kwa undani kuhusu Damian.
    Kuna wakati watu walimuona kama mzimu ambao uliibukia ndani ya kijiji hicho lakini kulikuwa na watu wengine waliofikiri kwamba kijana huyo alikuwa F.B.I kwani maisha yake yalikuwa ni ya kujificha sana.
    Baada ya kukaa kwa kipindi fulani ndani ya kijiji hicho, Damian akapotea kabisa, hakuwa akionekana na hata pale alipokuwa akitafutwa, hali ilikuwa ileile, hakuwa akionekana.
    Hiyo ikazua hofu kwa watu wa kijiji kile, kwa wale waliosema kwamba Damian alikuwa mzimu, wakapigilia misumali maneno yao na hatimae kuaminika kwa asilimia mia moja kwamba Damian alikuwa mzimu.
    Siku zikaendelea kukatika, kutoweka kwa Damian kuliwaogopesha watu lakini mara baada ya mwaka mzima kupita, kijana huyo akarudi tena kijijini hapo hali iliyomshtua kila mmoja.
    “Where has he been? (Alikuwa wapi?) aliuliza mwanakijiji mmoja.
    “We know nothing, why don’t we ask him?” (Hatujui kitu chochote kile, kwa nini tusimuite na kumuuliza?) aliuliza kijana mmoja.
    “Maybe, he is a ghost” (Labda ni mzimu)
    Hakukuwa na mtu aliyekuwa radhi kumuita na kumuuliza maswali, akaanza kuogopeka kijijini kwamba alikuwa mzimu lakini baada ya wiki moja kupita, Damian akawa mshirika mzuri wa ibada kanisani.
    Hapo ndipo watu walipopigwa na butwaa zaidi. Ilikuwaje ‘mzimu’ huo kwenda kanisani huku muda wote akionekana kuwa na Biblia? Ilikuwaje mzimu kujifungia chumbani na kuanza kuomba? Kila walichokuwa wakijiuliza, hawakuwa na majibu yoyote yale.
    “Oooh! My God! I saw him reading a Bible, what does this mean?” (Oooh! Mungu wangu! Nimemuona akisoma Biblia, hii inamaanisha nini?) alisema kijana mmoja huku akiwa na mshangao.
    “Impossible” (Haiwezekani)
    Hakukuwa na mtu aliyeamini kile alichokisema kijana yule, walichokifanya ni kuanza kuongozana naye kule alipomuona Damian akisoma Biblia ili kuamini kama lile lililosemwa lilikuwa kweli au la! Walipofika huko, kile kilichozungumziwa ndicho kilichoonekana, mtu waliyedhania kwamba ni mzimu alikuwa ametulia akisoma Biblia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Maisha yake yalijaza maswali mengi vichwani mwa watu, kila mtu alikuwa akijiuliza lake lakini hakukuwa na mtu aliyepata jibu juu ya maswali hayo. Siku zikaendelea kukatika zaidi, bado Damian alionekana tofauti kabisa na watu walivyokuwa wakijisikia, baada ya mwezi mmoja tangu aanze kusoma Biblia, matangazo yakaanza kuonekana kwamba Shirika la Kidini la Salvation Christians lilikuwa njiani kuja kijijini hapo kwa ajili ya kufanya mkutano mkubwa wa Injili.
    Watu wakajiandaa vilivyo kuwapokea, baadaya wiki moja, watu hao walifika mahali hapo na kuanza mkutano huo ambao ulikuwa na mafanikio makubwa.
    Wengi waliookoka lakini sauti ya msichana Maimartha ndiyo iliyowavutia watu zaidi, alikuwa na sauti ya kipekee ambaye kila aliyeisikia hakuamini kama duniani kulikuwa na mtu aliyekuwa na sauti kama yake.
    Watu wakajikuta wakimiminika mkutanoni kisa kikiwa ni kuisikia sauti hiyo yenye mvuto mkubwa. Mpaka mkutano unakwisha, kulikuwa na watu zaidi ya elfu tatu ambao walikuwa wameokoka, kisa kikiwa ni kuvutiwa na sauti ya msichana huyo ambayo iliwaita kutoka huko walipokuwa.
    Katika kipindi chote ambacho Maimatha alikuwa akiimba, Damian alikuwa kimya akimwangalia, sauti ya msichana huyo iliutetemesha moyo wake na hakuamini kama kweli kulikuwa na mtu aliyekuwa na sauti nzuri kama aliyokuwa nayo.
    Ukiachana na sauti yake, kwa jinsi alivyokuwa, muonekano wake ulikuwa ni wa kipekee mno, alikuwa na sura nzuri, umbo zuri ambalo nalo liliutetemesha moyo wake na kumfanya kujisikia kuwa na uhitaji wa sichana huyo.
    Hakukuwa na njia yoyote ya kumpata Maimartha zaidi ya kutaka kujiunga na shirika hilo la kidini, alichokifanya, siku hiyohiyo akamfuata mchungaji Peggy na kumwambia nia yake ya kutaka kujiunga nao.
    “Tutalifikiria hilo, “ alisema mchungaji Peggy.
    “Ninahitaji kumtumikia Mungu zaidi, kuisambaza Injili yake duniani kote,” alisema Damian huku akionekana kuhitaji kweli nafasi ile.
    “Una karama gani?”
    “Karama ya kuhubiri.”
    “Sawa. Tutakutafuta, subiri kwanza tukaangalie kwanza kama kuna nafasi nyingine zaidi,” alisema mchungaji peggy.
    Hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake kwa wakati huo. Uzuri wa Maimartha ulikuwa umeshamchanganya mno, hakutaka kumuacha, alikuwa akimhitaji kwa gharama yoyote ile. 
    Kila siku alikuwa akimuomba Mungu apate nafasi hiyo, hakutaka kumuacha Maimartha, alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini mwisho wa siku awe na msichana huyo mrembo. 
    Siku zikakatika, mwezi wa kwanza ukapita na wa pili kuingia lakini kukawa kimya. Hakukata tamaa aliendelea kusubiri zaidi. Mwezi wa tatu ulipoingia hapo ndipo alipopewa barua kwamba alitakiwa kusafiri kwenda Washington kwa ajili ya kujiunga na wenzake.
    “Asante Yesu!” alisema Damian kwa sauti kubwa, hakuamini kama kweli alikuwa amefanikiwa.
    Siku iliyofuata, akapanda basi lililompeleka mjini, huko, akachukua treni ambayo ikampeleka mpaka Washington huku akiwa amechukua masaa nane njiani. Alipofika huko, akaelekea katika mtaa alioelekezwa ambao ulikuwa karibu na Kanisa la River Jordan.
    Alipoingia, akajitambulisha na kukaribishwa ndani. Mchungaji Peggy alipokuwa tayari, akamuita ofisini kwake na kuanza kuongea naye, alipoona anafaa, akampeleka kwa wenzake ambao walikuwa katika chumba cha maombi wakiomba tayari kujiandaa na safari ya kuzunguka dunia kama kawaida yao.
    “Maimartha....” alijiitia moyoni mara baada ya macho yake kukutana na msichana mrembo aliyesimama mbele yake, alikuwa msichana aliyemfanya kuwa mahali hapo, msichana aliyemfanya kutamani kujiunga na shirika hilo la dini, msichana ambaye kila siku alikuwa akimfikiria sana, alikuwa Maimartha.


    “Ninataka kumfahamu zaidi kijana huyu,” alisema Godwin, mmoja wa vijana waliokuwa wakiendelea na huduma ya kulitangaza Neno la Mungu duniani.
    “Nani?”
    “Damian.”
    “Kwa nini unataka kumfahamu?”
    “Ni kijana wa kipekee sana, ni mpole, sijawahi kukutana na mtu kama huyu maishani mwangu,” alisema Godwin.
    “Sasa unataka kujua nini kuhusu yeye?”
    “Mengi tu, alianza vipi kuwa mhubiri.”
    “Sawa. Mfuate na uanze kumuuliza.”
    Damian alivisumbua vichwa vya wengi, maisha yake ndani ya meli hiyo yalikuwa ni ya kipole sana, hakuwa mzungumzaji kama watu wengine, hata kama ulikuwa ukimkasirisha, yeye ndiye alikuwa akikuomba msamaha.
    Maisha yake hayo yalimshangaza kila mtu, upole wake na utaratibu ukawajengea watu kumuamini bila kujua kwamba kijana huyo alikuwa ndani ya meli hiyo kwa ajili ya Maimartha tu ambaye alikisumbua kichwa chake kila siku.
    “Nitampata tu,” alijisemea Damian kila alipokuwa akimwangalia msichana huyo.
    Siku zikaendelea huku maisha ndani ya meli hiyo yakiendelea. Japokuwa alikuwa akimpenda mno Maimartha hakutaka kumfuata na kumwambia ukweli, kila kitu kikabaki na kuwa siri moyoni mwake.
    Kikafika kipindi ambacho Damian akashindwa kuvumilia kabisa, walipofika nchini Ubelgiji ndani ya Jiji la Brussels, ndipo alipoamua kumfuata Maimartha na kumwambia ukweli kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.
    “Yesu wangu!” alisema Maimartha huku akionekana kushtuka.
    “Huo ndiyo ukweli Maimartha, nimeshindwa kuvumilia kabisa, moyo wangu umekuwa katika mapenzi ya dhati juu yako, ninakupenda Maimartha,” alisema Damian, wakati huo walikuwa nyuma ya jukwaa la mkutano wa Injili.
    “Muogope Mungu Damian, wewe ni mchungaji,” alisema Maimartha huku akiwa amemkazia macho Damian.
    “Najua Maimartha, sipo kwa ajili ya kukuchezea, ninakupenda kweli na nipo tayari kukuoa,” alisema Damian.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Mapenzi yalionekana kushamiri kila sehemu, katika sehemu zote alizokuwa akienda, mapenzi yalikuwa yakichukua nafasi kubwa maishani mwake. Ndani ya meli hiyo ilionekana kuwa sehemu salama ya kutokuambiwa kitu chochote cha mapenzi lakini hali ilikuwa imekwishabadilika.
    Mwanaume ambaye alikuwa akimuamini sana kutokana na wokovu wake na hata kuhubiri kwake ndiye aliyemfuata na kuamua kumtongoza kwa ahadi ya kumuoa. Huo ulikuwa mtihani mkubwa kwa Maimartha kwani kila alipokuwa akiwakumbuka watu aliowahi kuwa nao katika mahusiano ya kimapenzi, hakumwamini mwanaume yeyote yule.
    “Siwezi kuwa naye, nimekwishaamua kumtumikia Mungu maisha yangu yote,” alisema Maimartha wakati alipokuwa chumbani akiendelea na kazi zake za uimbaji.
    Siku zikaendelea kukatika huku Maimartha akiendelea kupokea usumbufu kutoka kwa Damian. Hakuwa mwanaume aliyetulia hata mara moja, kila siku alikuwa akimfuata na kumwambia maneno ya kimapenzi kana kwamba alikuwa amenuia kumpata.
    “Naomba unikubali, ninataka kukuoa na tufunge ndoa,” alisema Damian.
    “Haiwezekani.”
    “Nakuomba Maimartha, nipo tayari kukuoa kabisa, sitaki uwe mpenzi wangu tu,” alisema Damian.
    Maimartha hakutaka kukubali hata kidogo, kwake, wanaume walionekana kama sumu kali inayoua kwa haraka sana. Hakutaka kumuamini mwanaume yeyote yule na ndiyo maana hata Damian alipokuwa akimfuata, alimwambia ukweli kwamba hakuwa akitaka kuingia naye katika mahusiano ya kimapenzi.
    Kwa Damian yalikuwa mateso makubwa, hakukubali kabisa kuuona akimkosa Maimartha, kwa sababu alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati, akaamua kumwambia mchungaji Peggy ambaye kwake ilikuwa ni furaha tele kwa kuona vijana wake walikuwa wamefikia hatua hiyo.
    Alichokifanya ni kumuita Maimartha na kumwambia juu ya maneno aliyoambiwa na Damian, mpaka kufikia hatua hiyo, tayari Maimartha akaona kwamba Damian alikuwa ‘serious’ juu ya kile alichokuwa amemwambia, akakubaliana na mchungaji na mwisho wa siku, uchumba baina ya watu hao wawili kutangazwa ndani ya meli ambayo ndiyo ilikuwa nyumba na kanisa lao.
    “Ila hamtakiwi kuonana kimwili mpaka mtakapooana,” alisema mchungaji Peggy.
    “Hakuna tatizo mchungaji, tutakuwa waaminifu katika hilo,” alisema Damian.
    Hawakuwa na maisha ya maigizo, kila mtu alikuwa amepanga kuishi na mwenzake, hata meli ilipotoa nanga nchini Ubelgiji, mahusiano yao yaliendelea zaidi.
    Mara kwa mara walikuwa pamoja, walikuwa wakifanya mambo mengi pamoja yakiwepo yale ya kutoa huduma katika nchi mbalimbali duniani. Uchumba wao uliendelea mbele, kitu walichokuwa wakikisubiria kwa wakati huo kilikuwa ndoa tu.
    “Ninakupenda Maimartha,” alisema Damian huku akiiangalia pete ya uchumba aliyokuwa ameivaa.
    “Nakupenda pia mpenzi,” alisema Maimartha.
    Damian akabaki kimya, alimwangalia Maimartha kwa mtazamo ambao ulikuwa tofauti kabisa, alionekana kuwa na kitu fulani alichokuwa akitaka kukizungumza mahali hapo lakini alionekana kuhofia.
    “Kuna nini?” aliuliza Maimartha.
    “Hakuna kitu.”
    “Nakufahamu Damian mpenzi, niambie kuna nini.”
    Damian hakutaka kujibu kitu chochote, aliendelea kubaki kimya kwa muda. Macho yake yalikuwa yakiangalia kifua cha Maimartha, kila wakati alipokuwa akimwangalia, tamaa za mwili zikaanza kumshika.
    “Ninakupenda.”
    “Najua Damian. Ila kuna nini?”
    “Nahitaji japo kuuona mwili wako usiku wa leo,” alisema Damian, Maimartha akashtuka.
    “Unasemaje?” aliuliza Maimartha kwa mshtuko. Damian akabaki kimya, mapigo ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi kana kwamba moyo ulitaka kuchomoka.


    Damian alibaki kimya huku akimwangalia Maimartha, mdomo wake ulikuwa mgumu kufunguka kwamba ni kitu gani alichotakiwa kukiongea. Alimwangalia msichana huyo mara mbilimbili, mapigo yake ya moyo bado yalikuwa yakidunda kwa nguvu, kijasho chembamba kikaanza kumtoka.
    Tamaa ya mwili wake ilikuwa imemshika, ilikuwa katika kiwango cha mwisho kabisa kitu kilichompelekea kuanza kumuomba msichana huyo kwa nguvu zote. Macho yake yakaanza kubadilika, yakaanza kuwa mekundu, kila alipojiangalia, alijiona kuwa tofauti na siku nyingine, tamaa ya mwili ilimuwaka.
    Japokuwa alikuwa akiomba sana lakini Maimartha hakutaka kumuelewa, alikuwa na msimamo wake uleule kwamba hakutakiwa kufanya naye mapenzi mpaka pale ambapo wangeoana na kuwa mume na mke.
    Siku hiyo ikapita, Damian hakuambulia kitu zaidi ya Maimartha kusema kwamba alitakiwa kuvumilia mpaka watakapooana. Kwa Damian, huo ukaonekana kuwa mtihani mkubwa, kiu ya kufanya mapenzi ilikuwa imemshika na hakutaka siku hiyo ipite hivihivi tu.
    “Nitamlevya tu, subiri,” alijisemea Damian.
    Kwa sababu ilikuwa ni asubuhi, alichokifanya ni kwenda katika chumba cha kuhifadhia dawa na kisha kuchukua aina tatu ya vidonge na kisha kuvisagasaga, alipoona kwamba imetosha, akavichukua na kuviweka katika karatasi.
    Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kumpata msichana huyo, kwa kuwa alikuwa amekwishashikwa na tamaa ya kufanya mapenzi huku akiuona muda wa kusubiri ukiwa mkubwa, alichokifanya ni kutumia dawa za kulevya tu.
    Jioni ya siku hiyo, akamuita Maimartha na kuanza kuzungumza naye. Walikuwa sehemu ya kawaida ambayo ilikuwa kama sebule ndani ya meli hiyo. Damian akachukua juisi na kisha kumimina kiasi katika glasi aliyotakiwa kumpa Maimartha na kisha kujimiminia na mwenyewe.
    Wakaanza kunywa huku wakiongea, kila mmoja alionekana kuwa na furaha mahali hapo, kwa Damian, kitu alichokuwa akikihitaji mahali hapo ni kufanya mapenzi na Maimartha tu. Tamaa ya mwili wake iliendelea kumuwaka.
    Alichokuwa akikisubiria mahali hapo ni ‘timing’ tu, alikuwa akimvizia Maimartha ainuke aende sehemu yoyote ile ili aweze kufanya kile alichotaka kukifanya mahali hapo.
    Damian akaona kama Mungu yupo upande wake, Maimartha akaomba ruhusa ya kuelekea chooni, akamruhusu. Hiyo ikaonekana kuwa nafasi ya kipekee kwake, alichokifanya ni kuchukua unga ule wa dawa zenye mchanganyiko na kisha kumuwekea katika glasi yake.
    Mpaka Msichana huyo anarudi, tayari alikuwa amekwishaichanganya vizuri. Kitendo cha Maimartha kuinywa juisi ile, baada ya dakika tano, macho yake yakaanza kuwa mazito na usingizi kumpitia.
    Hiyo ilikuwa ni nafasi ya kipekee sana, alichokifanya Damian ni kumbeba na kumpeleka chooni. Huko, tamaa yake ya mwili ikazidi kumpanda, alichokifanya ni kumvua nguo zake na kuanza kumbaka.
    Maimartha hakushtuka, bado aliendelea kubakwa. Baada ya dakika kumi kwa Damian kumaliza, akavaa nguo zake na kisha kutoka nje huku akimwacha Maimartha chooni tena akiwa amemvalisha nguo zake kama kawaida.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Baada ya saa moja, kelele za msichana zilisikika chooni mara baada ya kumuona Maimartha akiwa amelala chini. Watu wengine waliokuwepo ndani ya meli hiyo, wakatoka vyumbani mwao na kwenda huko.
    Hakukuwa na mtu aliyeamini kile alichokuwa amekiona, Maimartha alikuwa chini chooni huku akionekana kutokujitambua. Wakambeba na kumpeleka chumbani na kisha kuanza kumfanyia maombezi.
    Ilikuwa ni vigumu kugundua kwamba Damian alikuwa nyuma ya kila kitu kilichokuwa kimetokea, alikuwa akishughulika kwa asilimia mia moja huku akijifanya kuchanganyikiwa kwa kile kilichokuwa kimetokea.
    Maombezi yalifanyika kwa takribani nusu saa, wakamuacha apumzike. Ilipofika saa nne usiku, Maimartha akarudiwa na fahamu. Kitu cha kwanza kilichomshangaza ni juu ya mahali alipokuwa. Alikuwa chumbani huku pembeni akiwepo mchumba wake, Damian.
    Akabaki akimwangalia, kumbukumbu zake zikaanza kumrudia, akakumbuka kwamba mara ya mwisho alikuwa na Damian wakinywa juisi, baada ya hapo akaenda chooni na kurudi, kilichoendelea, hakukikumbuka.
    “Damian, uliniwekea dawa ya usingizi?” aliuliza Maimartha kwa sauti ya chini, macho yake yalikwishaanza kuwa mekundu kutokana na machozi kuanza kujikusanya.
    “Mpenzi......”
    “Damian uliniwekea dawa ya usingizi?” alilirudia swali lake kwa mara ya pili, akajifunua shuka na kisha kuupeleka mkono wake sehemu za siri na kujikagua.
    “Umenibaka pia! Kwa nini umenifanyia hivi?” aliuliza Maimartha huku machozi yakianza kumbubujika mashavuni mwake.
    Moyo wake uliumia kupita kawaida, hakuamini kama mpenzi wake huyo angewezakufanya kitu kama hicho. 
    Baada ya dakika kadhaa, mchungaji Peggy na viongozi wengine wakaingia, walipomuuliza, hakutaka kuwaambia ukweli, aiwadanganya kwa kuwaambia kwamba alidondoka chooni kwa bahati mbaya na kupoteza fahamu.
    Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kila kitu, kilichoendelea kilikuwa ni kufanya mapenzi tu tena kwa siri kubwa. Mara kwa mara walikuwa wakionana chooni na kufanya mchezo huo mchafu. 
    Hakukuwa na mtu aliyefahamu kilichokuwa kikiendelea, maisha yao ya kinafiki yaliwapa upofu watu wote ndani ya meli hiyo. Miezi ikakatika, kikafika kipindi ambacho Maimartha akaanza kujisikia tofauti, kichefuchefu kikaanza, mwili ukaanza kujisikia uchovu mwingi, akagundua kwamba alikuwa na mimba.
    “Mungu wangu! Nina mimba,” alijisemea Maimartha huku akionekana kuwa na wasiwasi.
    Hakutaka kukaa na jambo hilo kisiri, alichokifanya ni kumwambia Damian juu ya kilichokuwa kimetokea, kwa Damian, hakuonekana kuwa na wasiwasi, alijiamini kupita kawaida.
    “Itatupasa kuondoka humu,” alisema Damian.
    “Kwenda wapi?”
    “Popote pale. Itatupasa kuondoka.”
    “Tutaondoka vipi na wakati tupo katikati ya bahari?” aliuliza Maimartha.
    “Usijali. Kila kitu niachie mimi,” alisema Damian.
    Mpaka kufikia hapo, Maimartha akaonekana kuwa na hofu na Damian. Hakumuelewa kabisa kile alichokuwa amekisema kwamba walitakiwa kuondoka hata kabla watu wengine hawajagundua kwamba alikuwa mjauzito.
    Meli ilikuwa imeweka kambi katikati ya bahari, sehemu ambayo kwa lugha nyepesi ungesema sehemu ya kimataifa. Hakukuwa na meli upande wowote ule na hata kama ulikuwa ukiangalia pande zote, usingeweza kuiona nchi kavu, pamoja na hayo yote, Damian alisema kwamba ilikuwa ni lazima waondoke.
    “Damian, hebu niambie ukweli, wewe ni nani? Nimekuwa nikiwa na hofu sana juu ya maisha yako,” aliuliza Maimartha.
    “Utanijua tu, ni lazima tuondoke.”
    “Niambie kwanza, siwezi kuondoka na wakati sijui ninaondoka na mtu gani.”
    “Maimartha, utanifahamu, nitakwambia kila kitu, usijali,” alisema Damian huku akimsihi Maimartha kwamba ilikuwa ni lazima usiku wa siku hiyo waondoke japokuwa hakujua wangeondoka vipi.
    “Damian....”
    “Mpenzi, ni lazima tuondoke, ipo hivi, tunaondoka na boti usiku wa leo, tunakwenda Urusi, baada ya hapo, utajifungulia huko, kuna kazi nataka kumalizia nchini Marekani,” alisema Damian.
    “Mpenzi....” alisema Maimartha, akaanza kulia, maneno aliyoyazungumza Damian yalimchanganya kupita kawaida. Kichwa chake kilikuwa na maswali mengi kwamba Damian alikuwa nani.
    Kitu ambacho hakuwa akipenda kitokee ni juu ya kugundulika kwamba alikua mjauzito. Aliaminika sana ndani ya meli hiyo, kitendo cha kugundulika kwamba alikuwa mjauzito kingeweza kumshushia heshima kubwa aliyokuwa nayo ndani ya meli hiyo.
    “Nimekubaliana nawe, tutaondoka. Ila ninakuamini, naomba usivunje uaminifu wangu kwako,” alisema Maimartha.
    “Usijali....niamini mpenzi,” alisema Damian.
    “Sawa.”


    Kichwa cha Maimartha hakikutulia, muda wote alikuwa akimfikiria Damian, kwake, tayari mwanaume huyo alionekana kuwa tofauti, aligundua kwamba alikuwa na mambo mengi ambayo hakutaka kuyaweka wazi.
    Kichwa chake kilijaza maswali mengi juu ya mwanaume huyo lakini hakupata jibu lolote lile. Usiku wa siku hiyo alitakiwa kutoroka na Damian kuelekea nchini Urusi huku akiwa hafahamu wangetoroka vipi na kwa kutumia nini kwani kila alipokuwa akiangalia huku na kule, hakukuwa na sehemu ya nchi kavu kabisa.
    “Tutatoroka vipi? Mbona huyu Damian simuelewi kabisa?” alijiuliza Maimartha lakini hakuwa na jibu lolote lile.
    Usiku wa siku hiyo mara baada ya ibada ya usiku, Maimartha akajiandaa vilivyo, akafungasha vitu vyake tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini Urusi. Kwa zaidi ya masaa manne, hakuwa amemuona Damian ndani ya meli hiyo kitu kilichompa uhakika kwamba alikuwa akiandaa mikakati ya safari yao.
    Ilipofika saa sita na nusu usiku, Damian akaingia ndani ya chumba alichokuwa akilala Maimartha na wasichana wengine wawili. Wote walikuwa wamelala isipokuwa Maimartha tu ambaye muda wote alikuwa macho akisubiria muda wa kuondoka ufike aweze kuondoka.
    “Shiiiiiiiiiiiii,” Damian alitoa sauti ya kumtaka Maimartha kutokupiga kelele zozote zile.
    Alichokifanya Damian ni kumtaka Maimartha kuchukua mizigo yake na kuanza kumfuata. Japokuwa kila kitu walichokuwa wakikifanya mahali hapo kingeweza kufanyika kwa sauti kubwa, lakini kutokana na kutotaka kugundulika, walikuwa wakifanya kimyakimya.
    Maimartha alikuwa radhi kwa kila kitu, alikuwa mjauzito, hakutaka kitu hicho kijulikane kwa kuogopa kuonekana vibaya kwa watu wengine, alikuwa tayari kuondoka kuelekea mbali lakini si kugundulika kwamba alikuwa mjauzito.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    Wakaanza kutembea kwa mwendo wa kunyata mpaka katika stoo ya kuhifadhia vyakula. Huko ndipo ambapo ilipokuwa sehemu yao ya kutorokea kuelekea nchini Urusi.
    “Subiri,” alisema Damian.
    Alichokifanya mwanaume huyo ni kuchukua simu yake na kuanza kupiga sehemu. Maimartha alibaki kimya huku akiwa amepigwa na mshangao. Walikuwa katikati ya bahari, sehemu ambayo haikuwa na minara ya simu lakini kitu cha ajabu, simu ya Damian ilikuwa ikitumika vizuri.
    Kila kilichokuwa kikitokea, Maimartha alikuwa akishangaa tu, hakujua kama mwanaume aliyekuwa naye muda huo alikuwa jini, mpelelezi au mtu wa aina gani. Maimartha akabaki akimsikiliza Damian tu, lugha aliyokuwa akiitumia kuwasiliana na watu wa upande mwingine hakikuwa Kingereza bali aliongea Kirusi, lugha ambayo kwa Maimartha haikuwa ikieleweka kabisa.
    “??? ???, ?? ??????”(Tunawasubiri nyie tu, sisi tupo tayari) alisema Damian kwa Kirusi.
    “?? ???????” (Mpo tayari?) aliuliza jamaa wa upande wa pili.
    “??” (Ndiyo)
    “?? ? ????” (Upo na mtu mwingine?)
    “??” (Ndiyo)
    “??? ???????? ???? ? ??? ?? ????? ??? ?? ?????? ???? ? ?????? ????????????” (Imekuwaje tena na wakati ulitakiwa kuwa peke yako?)
    “??? ??????? ???????” (Ni habari ndefu.)
    “?? ?? ????? ??????? ??????? ???????? ??????, ??? ??” (Hatuwezi kumchukua mtu mwingine zaidi yako.)
    “? ????? ???, ????? ?????? ???. ? ?? ???? ???????? ??” (Naomba mnisaidie katika hilo. Siwezi kumuacha.)
    “?????? ??????. ?? ?? ??????,” (Haiwezekani Damian. Tupo kazini.)
    “? ????. ??????????, ???????? ???, ? ?? ???? ???????? ??, ??? ????? ?????? ???????” (Najua. Naomba mnisaidie, siwezi kumuacha, ana mtoto wangu.)
    “?? ????????? ????” (Yaani umempa mimba mwanamke?)
    “??” (Ndiyo)
    Maimartha alitulia tu, hakuwa akiielewa lugha iliyokuwa ikizungumziwa mahali hapo, Damian aliendelea kuongea na watu hao mpaka pale alipoona kwamba ameelewana nao na ndipo alipomwambia asubiri.
    Ndani ya stoo hiyo, hakukuwa na amani hata kidogo, kila wakati macho yao yalikuwa yakiangalia huku na kule, kila waliposikia milango ikifunguliwa, walijificha zaidi kwa kuhisi labda watu hao wangeingia ndani ya stoo hiyo na kuwaona.
    Ilipofika saa saba na nusu usiku, Damian akabipiwa simuni, alichokifanya ni kuufungua mlango mdogo uliokuwa kule stoo kwa upande wa baharini. Baridi kali likaingia ndani mpaka kumfanya Maimartha kuanza kutetemeka, mawimbi yalikuwa yakipiga huku kukiwa na mawingi mazito yaliyokuwa yakipiga katika meli ile, kwa kifupi, hali ilikuwa ikitisha mno.
    “Tuondoke,” alisema Damian huku akimvalisha boya, tayari boti ndogo ilikuwa imekwishafika karibu na meli ile.
    “Hapana Damian, ninaogopa,” alisema Maimartha huku uso wake ukionekana kuogopa.
    “Unaogopa nini?”
    “Maji. Yananitisha.”
    “Usiogope, hautozama. 
    Haikuwa kazi nyepesi kumshawishi Maimartha kujitosa baharini. Bahari haikuwa imetulia, mawimbi yalikuwa yakipiga kwa nguvu. Japokuwa alikuwa na boya lakini bado alionekana kuwa na hofu moyoni mwake.
    Alipoona muda unazidi kwenda huku msichana huyo akiwa anajiuliza na moyo wake kutawaliwa na hofu, akamsukuma na kuangukia baharini na kisha na yeye kujitosa huku akiwa na mizigo ya Mamartha.
    Mawimbi yaliyokuwa yakipiga kwa nguvu yalizifanya kelele zake kutokusikika kabisa. Damian akaanza kupiga mbizi na kumshika Maimartha, alipoona ameshikwa, akamng’ang’ania Damian.
    Kwa taratibu wakaanza kuusogelea mtumbwi ule, walipoufikia, kwa msaada wa majaa wawili waliokuwa ndani ya mtumbwi huo, wakawavuta na kuwaingiza ndani.
    Bahari ilitisha, sauti za mawimbi ya maji zilikuwa zikisikika kila sehemu, boti ile ilikuwa ikiyumbizwa huku na kule lakini wala haikuzama. Maimartha alikuwa akitetemeka kwa hofu, kila wakati alikuwa akimuomba Mungu amnusuru kwa jambo lolote baya ambalo lingeweza kutokea maharini mule.
    Japokuwa alipewa blanketi na kujivisha lakini bado baridi liliweza kupenya mwilini mwake na kumfanya kutetemeka sana huku meno yake yakigongana kila wakati. 
    “Tunakwenda wapi?” aliuliza Maimartha, boti iliwashwa na kuanza kutokomea kusipojulikana.
    “Hii ni safari ya kwenda Urusi.”
    “Na boti hii?”
    “Hapana. Kuna meli inatusubiri.”
    “Sawa. Ila wewe ni nani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    “Usijali. Utanifahamu tu. Kwanza twende Urusi,” alisema Damian na kumbusu Maimartha shavuni.
    Busu lile halikuleta faraja yoyote ile, moyo wake ulikuwa na wasiwasi tele, kila alipokuwa akimfikiria Damian alikosa jibu kabisa. Walitumia nusu saa kuifikia meli kubwa zaidi ya ile waliyokuwa wametoka. 
    Walipoifikia, wakaisogelea na kila mmoja kushushwa kwa kutumia kamba ndefu ambayo ilipelekwa mpaka kwenye meli ile. Hapo, kidogo Maimartha akawa na amani moyoni mwake japokuwa kwa jinsi watu walivyokuwa wakionekana ndani ya meli ile, hawakuonekana kuwa watu wema hata kidogo.
    Wote walikuwa wanaume, japokuwa alijitahidi kutafuta kama kulikuwa na mwanamke, hakuweza kumuona jambo lililomfanya kujua kwamba hakutakiwa kumshukuru Mungu bali alitakiwa kuomba sana ili aweze kumuokoa kutoka katika mikono ya watu hao.
    Damian ndiye alikuwa msimuliaji mkuu, aliwaambia watu wale kule alipokuwa ametoka na msichana Maimartha kwamba alikuwa mpenzi wake aliyekuwa na mimba yake. Kila mmoja alionekana kushtushwa na maneno ya Damian.
    Huku wakionekana kukasirika, wakaanza kumlalamikia Damian kwamba kitu alichokuwa amekifanya hakikuwa sahihi lakini Damian aliendelea kujitetea kwamba kile alichokuwa amekifanya, kilitokea tu hivyo asingeweza kuufunika ukweli.
    “Hatujafurahishwa na ulichokifanya. Vipi kuhusu kazi yetu?” aliuliza jamaa mmoja, kwa sababu ni lugha ya Kirusi ndiyo iliyokuwa ikitumika, Maimartha hakuelewa kitu.
    “Kazi niliifanya, ila sikuimalizia.”
    “Na vipi kuhusu huyu mbwa?”
    “Naomba mtangulie naye Urusi, nitakuja huko.”
    “Una uhakika utatufanyia kazi yetu ndani ya muda?”
    “Nina uhakika huo.”
    “Sawa. Tunakupa miezi sita mitatu, ukishindwa tunamuua huyu malaya wako.”
    “Sawa. Hakuna tatizo. Nitafanikisha ndani ya muda huo.”
    “Sawa.”
    Hali iliyokuwa ikiendelea ndani ya meli ile bado iliendelea kumtia wasiwasi Maimartha, hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea na watu wale walikuwa ni wakina nani. Kila alipokuwa akiwaangalia, kwa sababu aliwahi kutembelea nchi nyingi, aligundua kwamba baadhi yao walikuwa Wagiriki na wengine Warusi.
    Maimartha akaanza kujuta sababu iliyompelekea kukubaliana na Damian kuelekea ndani ya meli ile, hapo ndipo alipogundua kwamba uamuzi aliouchukua haukuwa mzuri, ilikuwa ni bora kubaki ndani ya meli ya walokole kuliko kukubaliana kuongozana naye.
    “Niambie ukweli,” alisema Maimartha huku akitaka kulia.
    “Mimi ni mpelelezi.”
    “Hilo tu?”
    “Ndiyo. Nilitumwa nchini Marekani kwa ajili ya kukamilisha kazi moja tu.”
    “Kazi gani?”
    “Daaah!”
    “Niambie, kazi gani?”
    “Kuna kazi niliagizwa.”
    “Ipi?”
    “Kuna kazi niliagizwa, wewe jua kwamba kuna kazi niliagizwa. Hilo tu.”
    “Una uhakika tutatoka salama humu?”
    “Asilimia mia moja.”
    “Lini sasa? Kesho?”
    “Hapana.”
    “Lini sasa? Niambie.”
    “Sijajua, ila tutatoka salama mpenzi.”
    “Sikuamini.”
    “Kwa nini?”
    “Macho yako yapo tofauti na unachokisema.”
    “Niamini mpenzi.”
    “Ila niambie ni kazi gani uliyoagizwa?”
    “Wanataka nilipue Daraja la Brooklyn nchini Marekani,” alisema Damian na kukaa kimya.
    “Ukalipue daraja? Wewe ni mpelelezi au gaidi?”
    “Ni mpelelezi tu, nimelazimishwa kufanya hivyo, sina jinsi, wameiteka familia yangu, wamewateka wazazi wangu, nisipofanya hivi, wataniua,” alisema Damian.
    “Usipofanya hivyo watawaua wazazi wako? Inamaanisha hata mimi wataniua, si ndiyo?”
    “Sijajua.”
    “Kwa nini umenileta humu? Ulisema ni sehemu salama kwa maisha yetu, kweli hii i sehemu salama? Unadhani tutaweza kuondoka humu salama?” aliuliza Maimartha, tayari machozi yalikuwa yakimtoka.
    “Usijali, nitafanya kazi yao, tutaondoka na kwenda kuishi Ugiriki,” alisema Damian.
    Maimartha hakuongea kitu, akaondoka na kuelekea pembeni, akakaa chini na kuanza kulia. Tayari mpaka kufikia hatua hiyo alijiona ni mfu mtarajiwa. Usalama aliokuwa ameahidiwa na Damian kuhusiana na meli hiyo, ukaondoka, amani ikatoweka, sehemu hiyo ikaanza kuonekana kama jehanamu maishani mwake. Mbaya zaidi, endapo Damian asingeweza kukamilisha kazi aliyotumwa, basi alikuwa na uhakika kwamba hata yeye mwenyewe angeweza kuuawa na watu hao ambao kwa kuwatazama tu, walionekana kutokuwa na huruma hata kidogo. 
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog