Simulizi: Let's Call It A Night
Sehemu Ya Tano (5)
Maisha ndani ya meli ile yalikuwa yakiendelea kama kawaida, kila mtu alionekana kuwa bize, hakukuwa na mtu aliyekuwa akimuongelesha kwa kitu chochote kile. Rafiki yake pekee alikuwa Damian ambaye ndiye aliyekuwa akila naye na kufanya naye mambo mengine.
Kila siku watu waliokuwa ndani ya meli hiyo walionekana kutokuwa watu wa kawaida kabisa, jicho ambalo walikuwa wakitumia kumwangalia halikuwa jicho salama, walionekana kuwa na chuki za waziwazi.
Kila siku Damiana alikuwa na kazi moja ya kumtia moyo kwa kumfariji kwamba kusingekuwa na tatizo lolote ambalo lingetokea hivyo alitakiwa kuendelea kuamini kwamba kuna siku wangeondoka na kuendelea na maisha yao sehemu nyingine kabisa tofauti na melini hapo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa Maimartha, maneno yale hayakumuingia hata mara moja, kila siku kichwa chake kilikuwa kikiwafikiria watu wale, kwa mtazamo tu, hawakuonekana kuwa watu wazuri, kwa jinsi walivyoonekana, tayari alijiona kuwa marehemu.
Damian aliligundua hilo na kazi yake kubwa ilikuwa ni kuendelea kumtia moyo Maimartha.
“Wataniua hawa,” alisema Maimartha.
“Hapana, hawawezi kukuua kabisa, nipo hapa kwa ajili yako, amini kwamba utakuwa salama mikononi mwangu,” alisema Damian maneno yaliyomuingia Maimartha na kujiona kumpata mlinzi wa uhakika maishani mwake melini humo.
Siku ziliendelea kukatika, baada ya miezi kadhaa kukatika, Damian alitakiwa kuondoka ndani ya meli hiyo na kutakiwa kuelekea nchini Marekani. Hiyo ilikuwa ni taarifa mbaya kwa Maimartha lakini hakuwa na jinsi.
Siku ambayo alikuwa akiambiwa kuhusiana na safari hiyo, alibaki akilia sana, machozi yalimbubujika usiku mzima kwa kuamini kwamba na yeye huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yake kwa kuamini kwamba watu wale wasingeweza kumuacha hata kidogo.
“Wataniua.”
“Hawawezi kukua hata kidogo. Ngoja nikafanye kazi yao kisha nitarudi na kukuchukua, umekwishakuwa familia yangu, yeyote atakayekugusa kwa ubaya, nitamuua,” alisema Damian kwa ushujaa mkubwa.
“Naomba twende wote.”
“Hiyo haiwezekani, hawawezi kukubali.”
“Umekwishawaambia juu ya hilo?”
“Niliwagusia, walinikatalia katakata.”
“Mungu wangu! Kwa hiyo maisha yangu ndiyo yanaishia humu melini?”
“Hapana. Hayawezi kuishia humu, utaondoka ukiwa salama kabisa.”
Japokuwa aliambiwa maneno mengi lakini hayo yote hayakuweza kumuingia. Tumbo lake lilikwishakuwa kubwa, alikuwa akikaribia kujifungua kabisa na kujifungulia ndani ya meli hiyo kulimaanisha kwamba maisha yake yasingekuwa mazuri kabisa, tena angeweza kuuawa, yeye na mtoto wake kutupwa baharini.
Hicho ndicho kitu kilichomtia wasiwasi zaidi, hakutaka kujifungulia ndani ya meli hiyo lakini hakuwa na sehemu nyingine yoyote ile.
Baada ya siku mbili, Damian akapanda boti iendayo kasi na kuondoka melini hapo. Kwa Maimartha, majonzi aliyokuwa nayo kipindi hicho yalikuwa ni zaidi ya msiba, kitu kilichokuwa kikimjia moyoni mwake, kilimwambia kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wake wa kuonana na Damian kitu kilichomliza kupita kawaida.
“Haiwezekani, atarudi tena tu,” alijisemea Maimartha,
Kama alivyokuwa ametabiri ndicho kilichokuwa kimeanza kutokea. Watu wale ambao wote walikuwa wazungu wakaanza kumuonyeshea chuki kubwa, kuna siku nyingine hakupewa kabisa chakula na kila alipokuwa akiuliza aliambiwa kwamba chakula hakikuwepo.
Moyoni mwake aliumia mno lakini hakuwa na jinsi, mtu ambaye kila siku alimtegemea kwa kumletea chakula alikuwa ameondoka melini hapo. Alitamani sana kuwasiliana na wazazi wake na kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea kule alipokuwa lakini hakuweza kupata simu kabisa.
Alipoona maisha yanazidi kuwa magumu, hapo ndipo alipoanza mishemishe ya kujitafutia chakula mwenyewe ndani ya meli hiyo. Alianza kwa kwenda stoo, alipekua huku na kule, hakukuwa na kitu chochte zaidi ya chupa za pombe kali ambazo kwake hazikuwa salama kabisa na hakuwa amewahi kunywa pombe maishani mwake.
Hakukata tamaa, aliendelea kutafuta zaidi na zaidi. Akaamua kwenda katika sehemu ambayo haikuwa ikifikiwa na watu kutokana na joto kubwa lililokuwepo huko kwani ilikuwa ni karibu na injini.
Alipoifikia sehemu hiyo tu, joto la mwili wake likaanza kuongezeka na jasho kuanza kumtiririka kama maji. Hakusimama, bado alikuwa akisonga mble kwani moyo wake ulimwambia kwamba huko kulikuwa na chakula hivyo alitaka kwenda kuchukua na kula.
Alipofika karibu na chumba kimoja kilichokuwa pembeni, kwa mbali akasikia minong’ono, kwanza akashtuka, hakuamini kama huko kungekuwepo na watu kwani joto lililokuwepo mahali hapo lilikuwa kubwa.
Alichokifanya ni kuanza kusogea, alitaka kujihakikishia kama ile minong’ono aliyoisikia ilikuwa ni ya watu au kitu kingine. Huko moyo wake ukimdunda kwa nguvu, Maimartha aliendelea kusogea na kuufungua mlango wa chumba kile, mwili wake ukamsisimka kupita kawaida. Macho yake yakagongana na macho ya vijana watano weusi ambao walikuwa wamejificha mahali hapo huku pembeni kukiwa na pakti kadhaa za biskuti na soda.
Maimartha alitamani kupiga kelele na kuondoka mahali hapo, lakini kila alipotaka kufanya hivyo, alisita kwa kuona kwamba watu hao wangepata matatizo kwani alikwishagundua kwamba vijana wale walikuwa wazamiaji kutoka katika Bara la Afrika.
“Who are you? (Nyie ni wakina nani?)” aliuliza Maimartha, hakukuwa na mtu aliyejibu, wote walikuwa kimya.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wazamiaji wale
walionekana kuwa na hofu, kila walipokuwa wakimwangalia Maimartha walijua kwamba
msichana huyo angeweza kupiga kelele na hivyo kuwaharibia mishemishe zao za
kwenda barani Ulaya.
Walijitahidi kumuhimiza Maimartha anyamaze lakini
msichana huyo hakutaka kufanya hivyo, alichokuwa akitaka kukifanya ni kupiga
kelele tu.
“Please, dont shout out” (Tafadhali, tunakuomba usipige
kelele) alisema mwanaume mmoja, kwa jinsi lafudhi yake aliyoitoa, alikuwa
Mnigeria.
“Why shouldn’t I shout out?” (Kwa nini nisipige
kelele?)
“Please help us, they will kill us, we are black people,”
(Tunaomba utusaidie, watatuua, sisi ni watu weusi) alisema kijana
yule.
Usalama wa maisha yao ulikuwa mikononi mwa Maimartha tu, hiyo
ilimaanisha kwamba endapo angepiga kelele basi Warusi wale na Wagiriki wale
wangeweza kufika mahali hapo, kuwachukua na kuwatosa
baharini.
Maimartha hakutaka kitu hicho kitokee, moyo wake ulikuwa na
huruma tele, kama angepiga kelele na watu wale kuuawa basi roho ya mauaji
ingeeanza kumsumbua milele.
Tofauti na hivyo, watu wale walikuwa na
chakula, tumbo lake halikuwa na kitu na siku hiyo hakuwa amepewa chakula
chochote kile, japokuwa watu wale walikuwa na biskuti tu, kwake, chakula hicho
kilionekana kuwa kingi.
Kadri alivyoendelea kukaa sehemu ile, joto
lilikuwa likiongezeka zaidi. Kila wakati alikuwa akijiuliza ni kwa namna gani
watu wale walikuwa wamevumilia kipindi chote hicho kukaa sehemu iliyokuwa na
joto kali namna ile.
Kwa kipindi cha dakika kadhaa tu alichokuwa
amekaa mahali hapo, tayari nguo zake zilianza kulowanishwa na jasho lililokuwa
likimtoka, hakupata picha watu wale walikuwa wakijisikiaje.
“Why are
you here? (Kwa nini mpo hapa?)
“We are going to Europe” (Tunakwenda
Ulaya)
“Do you know where you are going?” (Mnapajua
mnapoelekea?)
“No, can you tell us your destination?” (Hapana, unaweza
kutuambia mnaishia wapi?)” aliuliza jamaa yule ambaye alionekana kuwa kiongozi
wa msafara.
“We are going to Rusia” (Tunakwenda
Urusi)
“Rusia?” Jamaa mmoja aliuliza kwa mshtuko
Wote
wakashtuka, hawakuamini kama walikuwa ndani ya meli iliyokuwa ikielekea Urusi.
Wakaangalia huku kila mmoja akionekana kutokuamini kile alichokuwa amekisikia
kutoka kwa Maimartha.
Lengo lao kwa wakati huo halikuwa kwenda Urusi
bali walitaka kwenda katika nchi yoyote nyingine, nchi ambayo haikuwa na baridi
kali kama ilivyokuwa katika nchi hiyo. Kila mmoja akaonekana kuwa na wasiwasi,
kitendo cha kwenda Urusi kwao kilionekana kama kujiua kwa sababu mbali na baridi
kali la huko, hakukuwa na maisha mazuri hasa kwa wageni wenye ngozi
nyeusi.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Maimartha kufahamiana na wazamiaji
hao, akawaomba chakula kile na kuanza kula. Japokuwa zilikuwa biskuti ambazo
hazikuwa zikishibisha lakini akavumilia hivyohivyo kwa kulidanganya tumbo lake
na kujikuta akishiba chakula hicho.
Yeye ndiye ambaye alikuwa
akiwaambia juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea, kitu ambacho kwa vijana
wale kilikuwa msaada mkubwa.
Siku zikaendelea kukatika, mwili wa
Maimartha ukaanza kudhoofika, hakuwa akila, alikuwa akishinda katika hali ya
kuwaza tu kitu kilichoudhoofisha sana mwili wake. Hakukuwa na mtu aliyemuonea
huruma hata mara moja, Warusi wale walionekana kuwa makatili ambayo hayakutakiwa
kuishi katika dunia hii.
“??? ?????” (Huu ni mzigo) alisema Mrusi
mmoja, alikuwa akimzungumzia Maimartha.
“??? ??? ?? ??? ???????” (Kwa
hiyo tufanye nini?)
“????????? ????? ??? ? ????” (Tumtoseni baharini)
alisema jamaa mmoja.
Huo ndiyo uamuzi walioufikia, hawakutaka
kuendelea kuishi na Maimartha ndani ya meli hiyo kitu pekee walichokuwa wakitaka
kukifanya ni kumtosa baharini tu.
Kila siku walikuwa wakiendelea
kuishi naye lakini vichwa vyao vilikuwa vikifikiria namna ya kumtosa baharini
binti huyo huku wakati mpenzi wake, Damian atakaporudi basi waweze
kumuua.
Wakati wanafikiria hilo, tayari Maimartha alianza kuwa na
urafiki na wazamiaji waliokuwa ndani ya meli hiyo kificho. Kila siku ilikuwa ni
lazima kwenda huko na kuongea nao na hapo ndipo alipogundua kwamba miongoni mwa
wale wazamiaji, kulikuwa na mmoja aliyekuwa raia wa Kenya.
“Tukifika
Urusi, tunaondoka tu kuishi na maisha ya mitaani, najua ajira zipo tu, daah! Ila
hii meli ingekuwa inakwenda Marekani, ningefurahi sana,” alisema Ongowi,
mwanaume huyo kutoka Kenya.
“Mnachofuata huko ni nini
hasa?”
“Tunakwenda kuishi huko, Afrika pagumu sana, hakuna ajira,
tupotupo tu,” alisema kijana mwingine.
Kila siku walikuwa watu wa
kuongea tu, kila siku Maimartha alikuwa akiwahadithia maisha ya nchi nyingine
kitu ambacho kiliwachanganya mno na kujiona kama walikuwa wakichelewa kuingia
barani Ulaya.
Maimartha hakutaka kuwaficha, hata alipoulizwa juu ya
mimba aliyokuwa nayo, akaanza kuwaelezea historia ya maisha yake toka
alipojiunga na watu wa dini wa Shirika la Christian Salvation kitu
kilichomhuzunisha kila mmoja.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo huyo
Damian hayupo?”
“Ndiyo, aliondoka kwenda kufanya kazi yao waliyomtuma,
baada ya hapo, akirudi tutaondoka,” alisema Maimartha.
“Kwa jinsi
ulivyotuhadithia, mmh! Sidhani kama utaondoka salama.”
“Kwa
nini?”
“Wanaweza hata kukuua.”
“Hapana. Hawawezi
kuniua.”
“Kuna mwingine unayemjua ndani ya meli
hii?”
“Hapana. Hakuna yeyote.”
“Basi wanaweza kukua. Warusi
huwa ni watu wenye roho mbaya sana, ukiachana na Warusi, pia kuna Wagiriki, nao
kama Warusi, wana roho mbaya hata shetani akiwaona anashangaa wameitoa wapi roho
hiyo. Sasa chukulia hao watu wawili wameungana pamoja, nini kitatokea dhidi
yako? Watakuua tu,” alisema Ongowi.
Maneno aliyoyasema kijana yule
yalikuwa sahihi kabisa, kwa chuki walizokuwa wakimuonyeshea huku likiwepo suala
la kumnyima chakula ilionyesha kabisa watu hao wasingeweza kumuacha salama,
hivyo alitakiwa kujinasua mapema.
“Kwa hiyo nifanye
nini?”
“Haina jinsi. Kaa na sisi, tukifika Urusi, tunaondoka
zetu.”
“Sawa.”
Moyo wake ulikuwa mweupe kabisa kukubaliana
na wazamiaji wale, alikuwa radhi kuishi nao lakini si kuendelea kuishi na wale
mabaharia walioonekana kuwa na rioho mbaya.
Hakutaka kurudi tena, naye
akaanza kushindia biskuti huku hali yake ikiendelea kuwa mbaya sana. Alizidi
kukonda huku mara kwa mara akilia kwamba tumbo lilikuwa
likimuuma.
Ukiachana na hayo yote, kila kilipokuwa kikifunguliwa
kidirisha kidogo, Maimartha alikuwa akipiga kelele kwamba alikuwa akisikia
baridi kali kitu kilichowafanya kugundua kwamba mtu waliyekuwa naye tayari
alikuwa mgonjwa.
“Nini tena?”
“Kichwa
kinauma.”
“Kingine?”
“Tumbo nalo linauma. Ongowi, ninakufa,
tumbo linasokota,” alisema Maimartha huku akilishikilia tumbo lake lililokuwa
kwenye maumivu makali.
“Usilie Maimartha, ngoja tuanye
kitu.”
Hawakuwa na dawa, kitu walichokuwa wamekikumbuka ambacho
walikuwa nacho mikononi kilikuwa ni vyakula na soda tu. Walijitahidi kumfunika
nguo lakini bado hali yake iliendelea kuwa vilevile, alitetemeka
mno.
Siku hiyo aliishi kimateso sana, hakutaka kula, hamu ya kula
ikatoweka huli muda mwingi akitapika maji tu. Kwa kumwangalia, alitia huruma
sana lakini hakukuwa na kitu ambacho wangeweza
kumsaidia.
“Ninakufaaaaa,” alisema Maimartha huku akionekana kutokuwa
na nguvu.
“Hauwezi kufa…utaishi tu,” alisema Ongowi.
“Naomba
usniache Ongowi, naomba unisaidie.”
“Nitakusaidia siku
zote.”
Kwa mateso aliyokuwa akipitia Maimartha ndani ya meli ile, kila
mmoja alikuwa akimuonea huruma. Kwa kumwangalia tu, alikuwa binti mdogo ambaye
hakustahili kuyapitia mateso aliyokuwa akiyapitia.
Baada ya wiki moja
kupita huku akiendelea kuwa ndani ya chumba kile, uchungu ukaanza kumshika kitu
kilichomletea maumivu makali na kuanza kupiga
kelele.
“Shiiiiiiii…..shiiiiii….” walijaribu kumtolea sauti ya
kunyamaza lakini Maimartha hakunyamaza, alikuwa akiendelea kupiga kelele kwamba
alikuwa akisikia uchungu wa kutaka kujifungua.
BAdo alikuwa akiendelea
kulia, akajilaza chini na kuipanua miguu yake, damu zikaanza kumtoka kitu
kilichowafanya Ongowi na wenzake kugundua kwamba msichana huyo alikuwa njiani
kujifungua.
Hawakuwa madaktari wala hawakuwahi kusomea kitu chochote
kuhusu uuguzi, suala la Maimartha kutaka kujifungua halikuwa jambo zuri kutokea
kwani hawakuwa wamelitegemea.
“Tufanye nini
sasa?”
“Tumuhudumieni, hakuna jinsi.”
“Lakini anapiga sana
kelele. Hawezi kunyamaza? Washikaji watakuja na kutokea msala,” alisema jamaa
mmoja.
“Sijui. Hebu tumsaidieni kwanza.”
Huo ndiyo uamuzi
waliokuwa wameufiki, walichokifanya ni kuanza kumsaidia Maimartha aliyeonekana
kuwa kwenye hali mbaya. Bado alikuwa akipiga kelele za uchungu, damu ziliendelea
kumtoka sehemu za siri.
Ongowi alikuwa akitetemeka kwa hofu, aliingiza
mikono yak echini ya kiuno cha Maimartha na kisha kuanza kumtoa mtoto ambaye
tayari alikuwa amekwishaanza kuonekana
kichwa.
“Sukumaaaaa….sikumaaaaa…” alisema
Ongowi.
“Nimechoka, nimechoka kusukuma,” alisema
Maimartha.
“Amechoka kusukuma. Kwa hiyo tufanye
nini?”
“Nakumbuka niliwahi kusoma sehemu kwamba mwanamke akisoma
kusukuma huwa anapigwa vibao.”
“Kweli?”
“Kweli. Huwa
inasiadia.”
“Basi sawa. Kazi ya kumpiga vibao niachieni
mimi.”
Maimartha akaanza kupigwa vibao vya nguvu, vibao hivyo vikaanza
kumpa nguvu ya kuanza kusukuma tena. Japokuwa ilikuwa ni kazi ngumu lakini
alitakiwa kuifanya kwani mtoto angeweza kufa endapo tu angeacha na kubaki kichwa
kikiwa nje.
Huku akipiga kelele, kazi iliendelea na kumalizika huku
Maimartha akiwa hoi. Mtoto wa kike alikuwa kimya, walichokifanya ni
kumtingishatingisha na ndipo alipoanza kulia tena. Kila mmoja akafurahi kwa
kuona kwamba walikuwa wamefanikiwa kile walichokuwa
wamekitaka.
“Ataitwa Ameria.”
“Kwa nini asiitwe
Esta?”
“Acha aitwe Ameria. Mtoto mzuri sana. Demu wangu alipozaliwa
alikuwa na sura hiihii,” alisema jamaa mmoja, alikuwa raia kutoka
Uganda.
****CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yupo wapi huyu
Malaya?” aliuliza Usmanov, mwanaume mwenye misuli mikubwa kutoka nchini
Urusi.
“Alikuwepo hapa. Sasa amekwenda wapi?”
Hebu
mtafuteni. HAwezi kututoroka. Yaani atoroke kipindi tulichopanga kumuua,
haiwezekani. Mtafuteni,” alisema Usmanov kwa hasira.
Kila mmoja
alikuwa amechanganyikiwa, kutoweka kwa Maimartha kuliwachanganya kupita kawaida.
Mipango waliyokuwa nayo ni kumuua tu na si kuona akitoroka kiwepesi kama
alivyofanya.
Walichokifanya ni kuanza msako ndani ya meli hiyo. Kila
walipokwenda, Maimartha hakuwepo kitu kilichowapa wasiwasi mkubwa.
“Au
amejitosa baharini?”
“Hapana. Hawezi kufanya hivyo. Tuendeleeni na
msako.”
Hawakuishia hapo, msako uleiendelea zaidi, kitu walichokuwa
wakitaka ni kumpa na kumuua tu. Walimtafuta kila sehemu, walisukuma makabati,
waliangalia chini ya vitanda lakini Maimartha hakuonekana jambo lililomchanganya
kila mtu.
Wiki ya kwanza ikakatika, Maimartha hakuonekana sehemu
yoyote ile. Wazo lililokuwa limewajia vichwani mwao ni kwamba walitakiwa kwenda
kumtafuta katika chumba kilichokuwa karibu na injini lakini wakasita kufanya
hivyo kutokana na joto kali lililokuwepo huko.
“Vyumba vyote tayari,”
alisema kijana mmoja
“Kuna chochote kilichobaki?” aliuliza
Usmanov.
“Kipo kimoja, ila sidhani kama yupo huko.”
“Chumba
kipi?”
“Kile kilichokuwa karibu na injini.”
“Mmmh! Sidhani
kama itawezekana mtu kukaa huko. Achaneni naye, kama mmemkosa kote, inawezekana
amejiua” alisema Usmanov.
Hicho ndicho kilichoamuliwa, hawakutaka
kuendelea kumtafuta, walichokifanya ni kutulia na kuendelea na
maisha.
Baada ya siku kadhaa kupita, huku wakiwa wameizima meli
katikati ya bahari karibu na Urusi, usiku wa manane wakaanza kusikia kelele za
mwanamke, wote wakajikuta wakiamka na kuanza kusikiliza vizuri.
Sauti
ile ilikuwa ikipiga kelele kwa nguvu kana kwamba alikuwa akipatwa na maumivu
makali. Walichokifanya ni kutoka vitandani mwao na kuanza kuifuatilia sauti
ile.
Haikuwa kazi nyepesi kuipata, waliisikia zaidi lakini hawakujua
ilitokea mahali gani.
“Inatokea wapi?”
“Hata mimi
sijui.”
“Mmmh! Ni maajabu.”
Hawakutaka kukata tamaa,
walidhamiria kuifuatilia sauti hiyo mpaka watakapoipata, wala haukupita muda
mrefu, wakaanza kusikia sauti ya mtoto, hiyo ilikuwa ikitoka kwa sauti kubwa
kuliko sauti ya Maimartha.
Walichokifanya ni kuanza kufuatilia na
mwisho wa siku wakagundua kwamba sauti ile ilikuwa ikitoka katika chumba
kilichokuwa karibu na injini, sehemu ambayo waliogopa kwenda kwa kuwa
hawakuamini kama kuna mtu angeweza kukaa huko kutokana na joto kali lililokuwepo
sehemu hiyo.
Kwa sababu walikuwa wamesikia sauti ya mtoto kutoka huko,
wakaamua kuelekea huko. Sauti ya mtoto yule iliendelea kusikika zaidi,
walipokikaribia chumba kile, wakaufungua mlango, japokuwa kulikuwa na giza,
mwanga hafifu uliokuwa ukipita kupitia kidirisha kidogo, waliweza kuwaona zaidi
ya watu watano akiwepo Maimartha.
“?????? ????” (Watu weusi) alisema
Usmanov huku akionekana kupandwa na hasira.
Hiyo haikuwa mara yao ya
kwanza kukutana na watu weusi waliokuwa wakizamia melini kwa ajili ya kwenda
Ulaya, na kila walipokuwa wakiwapata, walikuwa wakifanya kitu kimoja tu, kuwapa
mapipa na kisha kuwatosa baharini.
Walikuwa wakiwachukia mno watu
weusi, hawakuwapenda, kila walipokuwa wakiwaona, kitu walichokuwa wakikifikiria
ni kuwaua tu.
Walichokifanya ni kutoa bunduki zao. Japokuwa walikuwa
na hasira nao lakini hawakutaka kuwaua kwa kuwa lengo lao kwa kila mzamiaji
aliyekuwa akikamatwa hakuwa akiuawa zaidi ya kutoswa baharini
tu.
Wakawasogelea na kuanza kuwapiga kwa mateke na ngumi huku
wakimnyanyua Maimartha aliyekuwa hoi na kuanza kumpiga
vibao.
Hawakuionea huruma hali aliyokuwa nayo, walimchukia kwa kuwa
alikuwa mtu mweusi tu. Waliwapiga vya kutosha, waliporidhika, kama kawaida yao
wakachukua mapipa na kuanza kuyatupa baharini.
“??????? ?x” (Watupeni)
alisema Usmanov, wakawachukua Waafrika wale na kuwatupa baharini huku
wakiwaambia kama walikuwa na uwezo wa kuogelea, wapige mbizi kuyafuata mapipa
yale.
“??? ? ????” (Tumfanye nini?) aliuliza jamaa mmoja akimaanisha
Maimartha.
“Mtupeni yeye na mtoto wake, hatuwezi kumlea mtoto mweusi)
alisema Usmanov, kijana mmoja akamchukua Maimartha, wakampa mtoto wake na kisha
kumtosa baharini huku akiwa amemkumbatia mtoto wake na huku akilia. Kwa
kuitazama tu, ilikuwa picha mbaya sana, ila kwa Warusi na Wagiriki wale,
hawakuonekana kujali.
Wakamtosa
baharini!!
Bahari ya Pacific ilikuwa
miongoni mwa bahari zilizokuwa na baridi duniani. Kuna kipindi sehemu nyingine
kulikuwa kukitokea mabarafu makubwa yaliyowapa wakati mgumu manahodha waliokuwa
wakiziongoza meli.
Katika kipindi hicho, kulikuwa na baridi kali
katika bahari hiyo. Kitendo cha kutoswa baharini tu, kiliwapa wakati mgumu mno.
Wakabaki wakilia huku wakiendelea kuomba msamaha na kurudishwa melini lakini
hakukuwa na mtu aliyewaelewa, Warusi na Wagiriki wale wenye roho mbaya
wakaondoka zao.
Maimartha alikuwa akilia. Mwili wake ulikuwa kwenye
maumivu makali, bado hakuwa na nguvu kwani kipindi kichache kilichopita alikuwa
ametoka kujifungua. Kwake, alikuwa na wakati mgumu zaidi kujilinda yeye na mtoto
wake.
Alishindwa kujua ni kipi alitakiwa kukifanya, tayari alianza
kunywa maji kitu kilicholifanya tumbo lake kujawa na maji. Msaada wake mkubwa
baharini hapo alikuwa Ongowi ambaye alipiga mbizi, alipomfikia akamshika mkono
na kuelekea naye kwenye moja ya mapipa yaliyokuwa yakielea.
“Kaa hapa
kwanza,” alisema Ongowi huku akitetemeka baharini pale. Kila alipokuwa akiongea,
mdomo wake ulitoa aina ya moshi fulani uliomaanisha kwamba alikuwa akisikia
baridi mahali hapo.
Mtoto wa Maimartha, Ameria alikuwa akilia tu,
hakujua ni kitu gani alitakiwa kukifanya. Alikuwa mtupu kabisa. Kila alipokuwa
akimwangalia, moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama Mungu alikuwa amempa mtoto
katika kipindi cha mateso kama alichokuwa nacho wakati huo.
“Ongowi,
mtoto wangu anakufa,” alisema Maimartha huku akilia.
Mtoto Ameria
alikuwa akilia tu huku akitetemeka, kila aliyekuwa akimwangalia alimuonea
hukuma. Mkono mmoja wa Maimartha ulikuwa umeshikilia pia huku mkono mwingine
ukiwa umemshikilia mtoto wake.
Dakika zilindelea kukatika, sauti ya
kilio aliyokuwa akiitoa mtoto Ameria ikakatika na mwisho wa siku kuwa kimya
kabisa.
“Ongowi, Ongowi, mtoto wangu kanyamaza, Ongowi, mtoto wangu
amekufa,” alisema Maimartha huku akijaribu kumtingisha mtoto wake, alikuwa kimya
kabisa.
“Unasemaje?” aliuliza Ongowi huku akionekana
kushtuka.
“Mtoto wangu ame………”
Maimartha hakuweza kuvumilia,
akaanza kulia kwa sauti kubwa. Moyo wake ukawa kwenye maumivu makali, hakuamini
kile kilichokuwa kimetokea, binti yake ambaye alikaa tumboni mwake kwa takribani
miezi tisa alikuwa amekata roho huku akiwa ameishi chini ya nusu saa katika
dunia hii.
Mawimbi yaliendelea kuyapiga mapipa yale, yalikuwa
yakipelekwa huku na kule lakini hawakutaka kuyaachia. Hiyo ilikuwa siku mbaya na
yenye mateso kuliko siku zote katika maisha yake, kila alipoiangalia maiti ya
mwanaye aliyokuwa ameishika, moyo wake uliendelea kumuuma.
Siku hiyo
walishinda baharini huku Maimartha akiendelea kuishikilia maiti ya mtoto wake
kwa kudhani kwamba angeweza kuyafumbua macho yake na kuanza kulia tena. Hilo
halikutokea, alitakiwa kukubaliana na ukweli kwamba mtoto wake kipenzi, Ameria
alikuwa amefariki dunia.
“Maimartha…” aliitwa
Ongowi.
“Abee.”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Pole sana kwa
kufiwa na mtoto wako.”
“Inaniuma sana, moyo wangu umekuwa katika
maumivu makali. Kwa nini mimi?”
“Pole sana. Kazi yake Mungu haina
makosa. Muachie mtoto wako, haina jinsi,” alisema Ongowi huku akionekana
kumuonea huruma.
“Siwezi Ongowi, siwezi kumuacha mwanagu awe chakula
cha samaki. Sitoweza kumuachia, labda nife,” alisema Maimartha.
“Sawa.
Ngoja tuone tutaishia wapi. Kama Mungu akipenda, basi tufike salama tuendapo, na
kama haitokuwa hivyo, hata kifo si kibaya kwa wakati kama huu,” alisema Ongowi
huku akitetemeka.
“Naomba mnisamehe Ongowi, mimi ndiye nilikuwa chanzo
cha kila kitu. Naomba unisamehe kwa kila kitu.”
“Usiseme hivyo
Maimartha, hakuna anayetakiwa kukulaumu kwa wakati kama huu. Tulikuwa tunajaribu
kuyaokoa maisha yako,” alisema Ongowi.
Waliendelea kukaa baharini kwa
zaidi ya masaa kumi, bado Maimartha alikuwa ameishikilia maiti ya mtoto wake
huku akilia. Kila alipokuwa akimwangalia, moyo wake bado uliendelea kumuuma
mno.
Kila walipokuwa wakiangalia huku na kule, hakukuwa na eneo la
nchi kavu lililokuwa likionekana, katika kila upande, kulikuwa na maji na
hakukuwa na alama zozote za kuwepo na sehemu yoyote ya nchi kavu ikiwepo
kisiwa.
“Ninakufa Ongowi.”
“Hapana. Hauwezi kufa, shikilia
pipa vizuri,” Ongowi alimwambia Maimartha.
Kutokana na mawimbi
yaliyokuwa yakipiga huku na kule, mapipa yakaanza kupelekwa sehemu nyingine
kabisa, baada ya saa moja, wakajikuta wakiwa wamepotezana, wale wazamiaji wengi
ambao kila mmoja alikuwa na pipa lake hawakuonekana.
Walijaribu
kuangalia huku na kule kuona kama wangeweza kuwapata lakini hilo likaonekana
kuwa gumu. Ilipofika usiku wa saa nane, Maimartha akachoka kulishikilia pipa kwa
mkono mmoja, alichokifanya ni kuiachia maiti ya mtoto wake huku
akilia.
Hakuwa na jinsi, mkono wake mmoja ulikuwa taabani, japokuwa
aliumia sana lakini hakuweza kulizuia jambo lile lisitokee. Alilia mno na
machozi yake kupelekwa na maji, hakuamini kwamba angeweza kuyapitia maisha
aliyokuwa akiyapitia kwa wakati huo.
“Nahisi tumbo linauma,” alisema
Maimartha huku akilia.
“Vumilia, tutapata msaada tu.”
Hivyo
ndivyo alivyoambiwa na Ongowi, aliendelea kusubiri huku moyo wake ukisali kila
wakati lakini hakukuwa na msaada wowote ulioweza kuja.
Mawimbi
yaliendelea kupiga, pipa nalo liliendelea kupelekwa huku na kule, hakutaka
kuliachia pipa lile, aliendelea kuling’ang’ania.
“Mungu, ninakufa,
naomba uipokee roho yangu,” alisema Maimartha, alichoka kushikilia, nguvu zake
zilimuisha, taratibu akaanza kuliachia pipa lile na kuanza kuzama, alikuwa
tayari kufa kwani asingeweza kuvumilia kuyapata mateso yale. Alikuwa akifa huku
akijiona, akazama, macho yakaanza kujaa giza, mwisho, hakuweza kuona kitu
chochote kile, akajua tu kwamba tayari mtoa roho alikuwa
amekwishamfikia.
Maimartha alikuja
kupata fahamu akiwa mchangani, kwanza alishangaa, akaanza kujiuliza maswali
mengi kwa nini alikuwa mahali pale na nini kilikuwa
kimetokea.
Alikumbuka kwamba mara ya mwisho alikuwa baharini, tena
amezama majini, baada ya hapo, aliona giza, kumbukumbu zake zikaishia hapo,
hakujua kitu chochote kilichoendelea.
Wakati akijiuliza hayo, akaamua
kusimama, alikuwa katika sehemu moja ambapo mbele yake kulikuwa na bahari,
akajua kwamba inawezekana sehemu aliyokuwepo ilikuwa
kisiwani.
“Nimefikaje? Ilikuwaje mpaka niwe hapa?” alijiuliza
Maimartha lakini akakosa jibu. Alipogeuka nyuma, kulikuwa na miti mingi,
kulifanana na pori japokuwa huko kulikuwa na mchanga mwingi.
Jua
halikuwa kali, hakuwa akijua ilikuwa ni saa ngapi lakini kwa kuliangalia jua tu,
aliweza kuhisi kwamba ilikuwa saa mbili asubuhi. Baridi lilikuwa kali, alikuwa
akitetemeka mno kitu kilichomfanya kila wakati kujikunyata lakini haikuweza
kusaidia.
Alichokifanya ni kuanza kupiga hatua kuelekea katika miti
ile, alipofika huko, akaingia ndani. Hali haikuwa ya kawaida kabisa, hakukuwa na
ndege yeyote yule, kwa jinsi ilivyoonekana, hakukuwa na kiumbe chochote kile
hasa wanyama.
Maimartha aliendelea kuingia zaidi huku kichwa chake
kikiendelea kujiuliza ni kwa namna gani aliweza kufika pale alipokuwa. Baada ya
dakika ishirini tu, akatokea upande mwingine, napo, kwa mbele akakuta bahari,
hapo ndipo alipokuwa na uhakika kwamba pale alipokuwa kilikuwa ni
kisiwa.
“Nimefikikaje? Mbona hakuna mtu?” alijiuliza
Maimartha.
Alichoamua kukifanya ni kurudi kule alipotoka, kama
alivyotumia muda wa kuja hapo alipokuwa ndiyo muda aliotumia kwenda kule
alipotoka, alipofika, akakuta kukiwa na kuni zimewekwa huku zikiwa zinateketezwa
kwa moto, yaani kama walivyokuwa wanatumia watu wanaotaka kuota
moto.
“Mmmh!” aliguna Maimartha.
Hakukuwa na mtu aliyemuona
mahali hapo, kutendo cha kukuta kuni zikiwa zimewashwa moto kilimshtua ila
hakuwa na jinsi. Kwa kuwa alikuwa akisikia baridi, akajisogeza na kuanza kuota
moto.
Hapo ndipo kumbukumbu za maisha yake ya baharini zikaanza
kujirudia kichwani mwake, alikumbuka kila kitu mpaka kipindi ambacho mtoto wake
alikufa na kuiachia maiti yake izame baharini.
Maimartha akaanza kulia
tena, bado moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kama alikuwa
amepata mtoto na mwisho wa siku alikuwa amekufa baharini baada ya kupigwa na
baridi kali.
Kuna wakati alihisi kwamba Mungu aliruhusu jambo lile
litokee kwa kuwa alikuwa ametoa mimba mbili.
“Mungu! Haya ndiyo
malipo ya nilichokifanya? Mbona umenilipia kwa pigo kubwa sana?” aliuliza
Maimartha huku akiangalia juu kana kwamba alikuwa akimuona
Mungu.
Wakati akiwa anajiuliza maswali hayo, ghafla akasikia akiitwa
kwa nyuma, sauti aliyoisikia haikuwa ngeni masikioni mwake, alipogeuka, macho
yake yakakutana na macho ya Ongowi, akajikuta akisimama, akaanza kumfuata na
kisha kumkumbatia kwa furaha.
“Nini kilitokea Ongowi?” aliuliza
Maimartha.
“Kwanza tule, nimeleta samaki. Ushawahi kula samaki wa
kizungu?” aliuliza Ongowi.
“Wa kizungu! Nishawahi kula nilipokuwa nje
ya Afrika,” alisema Maimartha.
Hawakuwa na chombo chochote kile,
walichokifanya ni kuwachoma samaki wale na walipomaliza wakaanza kula. Muda wote
huo Maimartha alikuwa akiendelea kujiuliza juu ya namna ambavyo aliletwa ndani
ya kisiwa kile, walipomaliza kula tu, akaanza kuuliza.CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ilikuwaje mpaka
nipo mahali hapa?” aliuliza Maimartha.
“Uliliachia pipa tayari kwa
kuzama, sikutaka nione hilo linatokea, nilichokifanya ni kuzama majini na kuanza
kukufuata. Ilikuwa kazi ngumu sana lakini nashukuru Mungu kwamba nilifanikiwa
kukupata, nikakuchukua na kuja nawe juu na kukupakiza juu ya pipa langu,”
alisema Ongowi na kuendelea:
“Baada ya hapo, nililiacha pipa liendelee
kuelea, masaa manne baadaye ndipo nilipokiona kisiwa hiki kwa mbali, nikaanza
kulisukuma pipa na mwisho wa siku kufika mahali hapa, haukuwa ukijitambua, mara
ya kwanza nilidhani umekufa ila niliposikiliza mapigo yako ya moyo, yalikuwa
yakidunda kwa mbali sana,” alisema Ongowi.
“Nashukuru sana. Sasa
tutatoka vipi hapa?”
“Bado sijajua. Najua tutaondoka tu japo sijajua
tutaondoka vipi. Sina hamu ya kuishi Ulaya tena, bora nirudi Kenya tu,” alisema
Ongowi.
“Kwa hiyo tusubiri
meli?”
“Ikiwezekana.”
Hawakuwa na cha kufanya zaidi ya
kusubiri meli tu, siku hiyo wakabaki katika kisiwa hicho huku wakiongea mambo
mengi yaliyotokea katika maisha yao. Muda mwingi Maimartha hakuonekana kuwa na
furaha, bado mawazo mengi juu ya mtoto wake yalikuwa yakimuumiza.
Kila
alipokuwa akilia, Ongowi ndiye alikuwa mtu pekee aliyekuwa akimbembeleza, kila
alipokumbuka kwamba alikuwa ndani ya meli ya walokole na mwisho wa siku kuingia
kwenye meli ya Warusi na Wagiriki, Maimartha alijiona kufanya kosa kubwa la
kuondoka ndani ya meli ile japokuwa alikuwa na mimba.
Huo haukuwa muda
wa kujilaumu tena, alitakiwa kukubaliana na ukweli kwamba alifanya makosa na
hivyo alitakiwa kuanza upya kwa mara nyingine tena.
Siku ya kwanza
ikapita kisiwani hapo, waliendelea kuishi wawili tu huku kila mara wakiwa
wanaota moto tu. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuchoma samaki na kula huku
wakivumilia sana kunywa maji ya bahari ambapo kwa kipindi hicho kwao yalionekana
kuwa ya kawaida sana.
Siku ya pili ikaingia, maisha yaliendelea zaidi
ndani ya kisiwa hicho. Waliendelea kusubiri meli yoyote ile lakini hakukuwa na
meli iliyopita karibu na kisiwa kile.
“Kweli tunaweza kuondoka hapa
kisiwani?”
“Tuendelee kusubiri Maimartha, sijui chochote kile.
Ningependa kuondoka na kurudi nyumbani, huku Ulaya ishakuwa
balaa.”
Siku ziliendelea kukatika lakini hakukuwa na meli yoyote ile
iliyoonekana baharini. Mpaka wiki inamalizika bado hali iliendelea kuwa
vilevile. Walikata tamaa na kuona kwamba wangeweza kufa katika kisiwa hicho
hicho.
Baridi kali ndilo lililokuwa likiwaumiza kila siku. Kuna wakati
sehemu ya maji baharini ilikuwa ikiganda na kuwa barafu tupu, wakati mwingine
theluji ilikuwa ikidondoka kitu kilichowaletea tabu mno na mateso yasiyoweza
kuelezeka.
Waliendelea kusulubika huku kila siku chakula chao kikiwa
ni samaki wa kuchoma tu ambao walikuwa wakiletwa na Ongowi aliyekuwa akijitosa
baharini na mti wake wenye ncha kali na kuwakamata kwa kuwachoma, japokuwa
ilikuwa ni kazi kubwa mno lakini alikuwa akifanikiwa kwa kiasi
kikubwa.
“Tutakaa hapa mpaka lini? Mbona meli haziji?” aliuliza
Maimartha.
“Sijajua Martha. Mbaya zaidi msimu wa baridi kali ndiyo
unaanza huku Ulaya, sijui tutaishi vipi,” alisema Ongowi.
Waliendelea
kukaa katika kisiwa hicho ambacho wala hawakujua kiliitwaje. Kila siku theluji
ziliendelea kudondoka kitu kilichowaletea wakati mgumu mno. Siku zikaendelea
kukatika, bahari ikaanza kuganda, maji yote yakaganda na barafu zito kutawala
kwa juu.
“Nahisi nitakufa, mifupa yangu inauma kwa sababu ya baridi,”
alisema Maimartha.
“Vumilia tu. Ila nina wazo,” alisema
Ongowi.
“Wazo gani?”
“Kutembea, yatupasa
kutembea.”
“Kutembea?”
“Ndiyo. Hakuna maji, sehemu yote ni
barafu, kwa nini tusitembee?”
“Ooppss…”
“Ndiyo hivyo Martha.
Tutembee tu hakuna jinsi.”
“Na ikitokea barafu likayeyuka tukiwa
njiani?”
“Hatujui itakuwaje. Haina jinsi. Kwa hali jinsi ilivyokuwa,
hakuna meli itakayokuja kwani bahari ishaanza kuganda,” alisema
Ongowi.
Japokuwa lilikuwa suala gumu lakini hawakuwa na jinsi,
wakaanza kutembea juu ya bahari iliyokuwa imeganda huku theluthi ikiendelea
kudondoka. Wote walikuwa wakitetemeka, walikuwa wameshikana kwa kung’ang’aniana.
Kwa Maimartha ilikuwa afadhali kwa kuwa alikwishazoea kuishi katika nchi za
Ulaya, hata tabu aliyokuwa akiipata mahali pale haikuwa kubwa kama kwa Ongowi
ambaye hakuwahi kuishi katika nchi yenye baridi kali.
Hawakujua
walipokuwa wakielekea, wao walijiendea tu ili mradi wafike wanapotakiwa kufika.
Kadri muda ulivyozidi kwenda na ndivyo barafu lilivyozidi kuongezeka baharini
hapo.
Ilikuwa ni safari ndefu iliyowapa
tabu mno, kutokana na theluji nyingi kujaa katika mabarafu yale, iliwapa wakati
mgumu sana katika kuinyanyua miguu yao kwani walipokuwa wakikanyaga, miguu
ilikuwa ikizama mpaka magotini.
Waliendelea kutembea, kwa kuangalia
tu, hata kama ungepewa taarifa kwamba pale walipokuwa wakikanyaga kulikuwa na
bahari usingeweza kukubali, hakukuwa hata na tone la maji.
Walitembea
kwa umbali mrefu mno, baada ya masaa mawili ya matembezi yao, kila mmoja
akaonekana kuchoka na hivyo walihitaji kupumzika. Hiyo ilionekana kuwa ngumu
kufanyika kwani hakukuwa na sehemu ngumu yoyote ya kukaa, waliendelea kusonga
mbele kwani napo waliogopa kuyeyuka kwa bahari ambapo ungewapa wakati mgumu
sana.
“Hivi tutafika?”CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Inategemea na
upande tunaokwenda. Hali inatisha, sijui kama tunaelekea kaskazini, kusini au
upande gani,” alisema Ongowi.
Waliendelea kumuomba Mungu, bado kazi
ilionekana kuwa kubwa, theluji ziliendelea kudondoka mpaka kipindi kingine
wakahisi kwamba wangeweza kukwama na wasingeweza kusogea mbele
zaidi.
Safari iliendelea zaidi, baada ya masaa kumi, mbele wakaanza
kuiona miti kwa mbali. Haikuwa ikionekana vizuri kwa kuwa ilikuwa imetawaliwa na
theluji iliyokuwa ikiendelea kudondoka ardhini.
Kidogo wakaanza
kupata faraja kwa kuona walikuwa wamefika sehemu salama kabisa katika maisha
yao. Wakaendelea kupiga hatua mpaka walipoifikia miti ile na kuangalia vizuri,
kulikuwa na nyumba moja iliyotengenezwa kwa mbao, wakaifuata na kuingia
ndani.
Hakukuwa na mtu, ukimya mkubwa ulikuwa umetawala, mbele,
kulikuwa na sehemu maalumu iliyokuwa ikiwaka moto, pembeni kulikuwa na sanamu la
mbwa mwitu lililokuwa limewekwa kwa juu, mbali na hivyo, kulikuwa na meza
iliyojaza pombe kali.
“Tumefika sehemu salama, sijui wapi hapa,”
alisema Maimartha.
Usiseme sehemu salama, subiri mpaka tuhakikishiwe
usalama,” alisema Ongowi.
Walichokifanya ni kuusogelea moto ule na
kukaa pembeni yake. Kila mmoja alikuwa akitetemeka huku nguo zao zikiwa
zimetawaliwa na theluji, lakini baada ya kukaa karibu na moto ule, theluji
zilizokuwa mwilini mwao zikaanza kuyeyuka.
Baada ya masaa mawili ya
kuwepo ndani ya nyumba ile, wakaanza kusikia sauti kutoka nje ya nyumba ile.
Hawakuwa wakiongea Kingereza, walikuwa wakizungumza Kirusi. Wakajificha nyuma ya
kabati lilokuwa ndani ya nyumba ile huku wakitetemeka kwa hofu kubwa kwani
tayari hawakuonekana kuwaamini Warusi kutokana na matendo ya kikatili waliyokuwa
wakiyafanya.
Mlango ukafunguliwa na watu hao wawili kuingia ndani. Kwa
kutumia jicho la wizi wakaanza kuchungulia ili kuona walikuwa wamekuja na nini.
Wakawaona wakiwa wamebeba mnyama waliyetoka kumuwinda na kumuweka juu ya
meza.
Nyuso zao hazikuwa za kawaida, walionekana kuwa makatili,
inawezekana walikuwa zaidi ya wale waliokuwa katika meli
ile.
“Tuwaombe msaada, watusaidie, tayari tumefika nchi kavu,” alisema
Maimartha kwa sauti ya chini kule nyuma ya kabati.
“Hapana. Hatuwezi
kuwaamini, tusubiri waondoka na sisi tutoke,” alisema
Ongowi.
“Wanaonekana kuwa ni watu wema.”
“Hapana. Si watu
wema. Inawezekana hawa kuwa hatari zaidi ya wale wa kule kwenye
meli.”
“Kwa hiyo tufanye nini?”
“Tuendelee kukaa tu huku
nyuma ya kabati, tukitoka hapa, ni safari kuelekea St. Petersburg au Moscow, ni
mbali sana kutoka hapa?” aliuliza Ongowi.
“Sijajua. Sijawahi kufika
Urusi kabla na mbaya zaidi sijui hapa ni wapi.”
“Basi tuendelee
kukaa.”
Huo ndiyo uamuzi waliokuwa wameufikia, walichokifanya ni
kuendelea kusubiri mpaka watu wale watakapoondoka na wao kuendelea na safari
kama kawaida. Muda ulizidi kusogea, ilipofika saa kumi na mbili jioni, wakasikia
watu hao wakitoka nje na kuondoka zao.
“Wameondoka.”
“Na
sisi tuondoke. Ila nimeanza kusikia njaa.”
Wakatoka na kuanza kutafuta
kama kulikuwa na chakula chochote kile. Kila walipokuwa wakiangalia, walikuwa
wakikutana na pombe kali tu.
“Niliwaona wameleta mnyama, yupo
wapi?”
“Sijajua. Tuendelee kutafuta, mimi mwenyewe njaa imeanza
kunikamata,” alisema Ongowi.
Waliendelea kutafuta zaidi, mwisho wa
siku wakafanikiwa kukuta nyama ya kuchoma ikiwa imefunikwa katika bakuli
lililowekwa ndani ya kabati, wakaanza kula.
“Tuondoke. Chukua hayo
makoti,” alisema Ongowi na Maimartha kuchukua makoti makubwa yalilotengenzwa kwa
ngozi ya mnyama na kuyavaa.
Safari yao ikaanza upya, wakaanza kuondoka
mahali hapo na kuelekea katika upande wa Kaskazini kulikupokuwa na Mji wa Tiksi.
Walipofika umbali kama wa kilometa kumi, wakaanza kusikia sauti kwa nyuma,
walipogeuka, kulikuwa na zaidi ya watu wanne waliokuwa wakiwataka kusimama,
walikuwa kama umbali wa robo kilometa.
Hawakutaka kusimama,
walichikfanya ni kuanza kukimbia, watu wale nao wakaanza
kuwakimbiza.
Hawakukimbia kwa kasi kama ilivyokuwa, theluji nyingi
iliyokuwa imedonda chini kwa wingi iliwapa wakati mgumu. Hawakuzoea kuwa kwenye
eneo kama hilo ila watu waliokuwa wakiwakimbiza, walionekana kuwa na kasi zaidi
yao.
“Kimbia…kazana Maimartha,” alisema Ongowi huku akimshika mkono
Maimartha.
Hawakutaka kusimama, tayari hatari kubwa ilionekana mbele
yao na kama wasingeweza kukimbia, basi wangekamatwa na hivyo kufanyiwa kitu
kibaya na Warusi wale waliokuwa wawindaji eneno hilo.
Ghafla milio ya
risasi ikaanza kusikika nyuma yao kutoka kwa wale watu waliokuwa wakiwakimbiza,
hapo ndipo walipoongeza kasi kwa kuona kwamba hisi zao zilikuwa kweli kabisa,
watu wale waliokuwa wakiwakimbiza hawakuwa watu salama kabisa.
Kila
risasi iliyokuwa ikipigwa, iliwakosa, ilikuwa ikipiga katika theluji au katika
miti iliyokuwa kwenye kila njia waliyokuwa wakipita.
Kutokana na
baridi kali lililokuwepo, hawakuchoka na wala hakutokwa na jasho, walikuwa
wakavu kabisa na waliendelea kukimbia kama kawaida.
“Mama
nakufaaaaaaa……” ilisikika sauti ya Maimartha, alipiga uyowe mmoja mkubwa
uliomfanya Ongowi kusimama na kumwangalia. Alikuwa amedondoka chini huku damu
zikimtoka, alikuwa amepigwa risasi iliyozama katika paja
lake.
“Maimartha, inuka…” alisema Ongowi huku watu wale wakija kwa
kasi.
“Nimepigwa risasi, nimep….” alisema Maimartha kwa tabu, kabla
hajamaliza sentensi yake, akaanza kulia tena.
Ongowi akawa kwenye
wakati mgumu, alishindwa kuelewa ni kitu gani alitakiwa kukifanya, alipoyatupia
macho yake kwa wale wawindaji wa kirusi, walikuwa wakija kwa
kasi.
Hakutaka kumuacha Maimartha mahali hapo kwa kuamini kwamba
angeweza kuuawa kinyama, alichokifanya ni kumnyanyua na kumuweka begani,
kilichofuata ni kukimbia naye tu huku risasi zikiendelea kupigwa
mfululizo.
Maimartha alikuwa mzito lakini Ongowi hakutaka kumuacha,
bado alikuwa amembeba mgongoni huku akiendelea kukimbia naye. Theluji ilikuwa
usumbufu mkubwa, kila alipopiga hatua, aliuona mguu wake kama kukwamba, ilikuwa
ni sawa na mtu aliyekuwa akikimbia ndani ya maji.
Alijitahidi kuongeza
kasi lakini hali ilikuwa ileile. Alijitahidi hivyohivyo, alipofika kwa mbele
njiani, macho yake yakatua katika nyumba moja ambayo kwake ikaonekana kuwa
kimbilio, akaanza kuifuata huku Maimartha akilia na damu zikiendelea
kumtoka.
“Vumilia, kuna nyumba nimeiona,” alisema Ongowi huku
akiendelea kuisogelea nyumba ile.
Alipoifikia, hakutaka kusubiri,
akaufungua mlango na kuingia ndani. Kama ilivyokuwa nyumba ile ya nyuma, hata
nyumba hii haikuwa na mtu yeyote yule. Alichokifanya ni kuufuata mlango na kisha
kuufunga, akamuweka Maimartha kochini.
“Mguu unauma, ninaumwa mguu
Ongowi, ninakufa,” alisema Maimartha huku akiugulia mguu.
“Vumulia.
Subiri kwanza,” alisema Ongowi na kulifuata kabati la vyombo lilikuwa mahali
hapo. Akalifungua, macho yake yakatua katika kiboksi kido kilichoandikwa ‘firsy
Aid Kit’ yaani kiboksi cha huduma ya kwanza, akakifungua, akatoa pamba na dawa
aina ya ‘Kentrophyn’, akachukua mkasi mdogo na kumrudia Maimartha kochini
pale.
“Ngoja niitoe risasi.”
Hakukuwa na cha kusubiri, kila
kitu kilichofanyika mahali hapo kilifanyika harakaharaka, alichokifanya ni
kuuchukua mguu wa Maimartha na kuuweka mapajani mwake, akachukua wembe mdogo na
kuichana ngozi kidogo na kuingiza kile kimkasi.
Maumivu yake
hayakuelezeka. Maimartha alikuwa akipiga kelele mno huku akitaka kuutoa mguu
wake kwa Ongowi lakini mwanaume huyo hakuliruhusu hilo, aliendelea
kuung’ang’ania kuitoa risasi ile.
Alichukua dakika mbili tu, risasi
ikatoka. Akaanza kuifuta damu ile. Huku zoezi likiendelea, ghafla mlango ukaanza
kugongwa kifujo, watu wale waliokuwa wakiwakimbiza, tayari walikuwa
wamekwishafika mlangoni, wakataka kufunguliwa mlango.
Hilo lilikuwa
gumu kufanyika, wakatulia huku wakiangalia ni kitu gani walichotakiwa kukifanya.
Huku wakijifikiria, mlango ukaanza kupigwa risasi, komeo lile la ndani likaanza
kuachia.
“???? ?? ????? ?? , ????????? ????? ??” (Tukiwaona, tuwaueni)
alisema jamaa mmoja, wenzake wakakubaliana naye, wakaendelea kuupiga risasi
mlango ule, zilibakia kama risasi tatu mlango uachie. Muda wote huo, Ongowi na
Maimartha walikuwa wakisali sala ya mwisho mule ndani. Tayari waliona kwamba
ilikuwa ni lazima wauawe.
Wote wawili,
Maimartha na Ongowi walikuwa wakiendelea kusali sala zao za mwisho, Warusi
waliokuwa nje waliendelea kupiga risasi ambazo zilionekana kwamba ilikuwa ni
lazima kitasa kiharibike na hivyo mlango kufunguka.
Waliendelea
kusali, mbele yao hawakuwa na tumaini lolote lile, kitu walichokuwa wakikifahamu
ni kwamba walikuwa wakienda kuuawa mahali hapo. Kila mmoja alikuwa amepiga
magoti chini wakisubiri mlango uvunjwe na watu hao kuingia na kuwauawa
tu.
Wakati Warusi wale wenye roho mbaya wakiendelea kujitahidi
kuuvunja mlango ule, Ongowi akahisi kwamba kulikuwa na kitu alichotakiwa
kukifanya kama mwanaume na si kusubiri kuuawa kirahisi namna
ile.
Alichokifanya ni kuinuka na kuufuata mlango wa upande mwingine.
Kwa jinsi ulivyoonekana, ulikuwa mlango chakavu ambao haukuwa umetumika kwa
miezi kadhaa kwani hata kitasa chake kilianza kushikwa na
kutu.
“Maimartha, Maimartha, inuka tuondoke,” alisema Ongowi, alipoona
msichana huyo anachelewa, akamfuata na kumuinua.
Akaufungua mlango huo
na kutoka nje huku akiwa amemshika msichana huyo begani kama mtu aliyekuwa
akimsaidia. Upande wa pili, kulikuwa na barafu kubwa, na kwa mbele kulikuwa na
pikipiki itumikayo katika sehemu za barafu, akaanza kuifua huku watu wale wakiwa
wamekaribia kuuvunja mlango ule.
“Kaa hapa, tunaondoka,” alisema
Ongowi.
Hakukuwa na sababu ya kupoteza muda mahali hapo, kila kitu
alichokuwa akikifanya mahali hapo alikuwa akikifanya harakaharaka. Walipopanda
tu, wakawasikia watu wale wakiingia ndani na kuanza kuulizana mahali
walipokuwa.
Ongowi akaiwasha pikipiki ile ya kwenye barafu na kuanza
kuondoka mahali hapo huku Maiamartha akiwa kwenye maumivu makali ya
mguu.
Milio ya risasi ikaanza kusikika kwa Warusi wale lakini hakukuwa
na risasi yoyote iliyowapata. Safari ya kuelekea wasipopajua upande wa Kaskazini
ikaanza tena.
Theluji bado ziliendelea kudondoka, majani ya miti
hayakuwa yakionekana, yote hayo yalikuwa yamefunikwa na theluji iliyoendelea
kudondoka ardhini.
Safari yao ilikwenda kwa zaidi ya saa moja na
ndipo wakaingia katika Mji wa Kozhiva ambao ulikuwa kilometa elfu mbili kutoka
katika Jiji la Moscow.
Hapo, wakateremka na kuanza kwenda kwenye
mghahawa uliokuwa katika kituo kimoja cha mafuta na kuhitaji msaada wa dawa wa
mguu wa Maimartha ambao ulikuwa kwenye hali mbaya.
“Do you speak
English? (Unaongea Kingereza?) aliuliza Ongowi.
“What can I help you?
(Nikusaidie nini?) aliuliza msichana aliekuwa katika mghahawa
huo.
Hapo ndipo Ongowi akaanza kueleza shida yake, msichana yule
mwenye sura ya kipole akawachukua na kuwapeleka katika chumba cha huduma ya
kwanza. Warusi waliokuwa kwenye mghahawa ule walibaki wakiwaangalia, kwa
muonekano tu, Maimartha na Ongowi walionekana kuhitaji msaada wa hali na mali
mahali hapo.
Walipofika katika chumba hicho, akafungua kiboksi cha
kuhifadhia dawa na kisha kuanza kumhudumia Maimartha. Muda wote msichana huyo
alikuwa akipiga kelele, maumivu ya mguu wake yalikuwa makubwa, kila aliposhikwa
hivi, yeye alikuwa akipiga kelele tu.
Baada ya dakika ishirini,
Maimartha akaonekana kuwa fiti, alifungwa bandeji. Kwa sababu msichana yule
alionyesha nia ya kuwasaidia, akaanza kumwambia kuhusu historia ya maisha yao
yalipoanzia toka walipokuwa katika meli ile na kutupwa
baharini.
Msichana huyo alisikitika na hivyo kuamua kuwasaidia kiasi
cha euro elfu moja na kuwataka kuondoka mahali hapo na kuelekea katika jiji la
Moscow ambapo huko ndipo wangepata msaada zaidi.
****
Henry
alikuwa kimya, masikio yake aliyategesha kwa msichana huyo, muimba injili ambaye
aliamua kufunguka kuhusu maisha yake. Kama kufuta machozi yake yaliyokuwa
yakibubujika mashavuni mwake, aliyafuta sana, katika kila hatua ambayo Maimartha
alikuwa akiisimulia historia ya maisha yake huku akiwa kitandani, moyo wake
ulikuwa kwenye maumivu makali.
“Ooopsss” Henry alivuta pumzi ndefu na
kutulia.
“Nimepitia mengi Henry, usinione hivi,” alisema
Maimartha.
“Pole sana. Kuna yeyote anayejua historia ya maisha yako
uliyopitia?” aliuliza Henry.
“Hakuna, hata wazazi wangu ndiyo kwanza
wanaisikia leo hii,” alisema Maimartha.
Wazazi wake walikuwa pembeni
wakimsikiliza binti yao, kwa kila neno alilokuwa akiongea mahali hapo,
waliumizwa mno kwani binti yao alikuwa amepitia maisha magumu na wakati wao
walikuwa hai.
Mama yake, bi Asteria alikuwa kwenye maumivu makali,
historia ile ilimuumiza kupita kawaida. Akamsogelea binti yake kitandani pale na
kumkumbatia, bado alikuwa amepooza kama kawaida yake.
Henry akashindwa
kuvumilia, akasimama na kuaga mahali hapo huku akiahidi kurudi siku inayofuatia.
Alipofika hotelini, akatulia kitandani na kuanza kuikumbuka historia ya maisha
ya Maimartha.
“Ni maisha yenye maumivu mno, ukimwangalia, muda wote
yupo kwenye furaha, kumbe amepitia maumivu kiasi hiki, hakika acha amshukuru
Mungu. Lakini nini kiliendelea baada ya pale mghahawani nchini Urusi? Mmmh!
Ngoja kesho nirudi tena, hiki kitabu ni kizuri sana na ninaamini watanzania
wengi watakipenda japokuwa kitawatoa machozi,” alisema Henry.
Pamoja
na kila kitu kilichokuwa kimetokea katika maisha ya msichana huyo aliyepooza
kitandani, bado moyo wake uliendelea kuwa kwenye mapenzi ya dhati, alimpenda
Maimartha kuliko msichana yeyote yule.
Usiku wa siku hiyohiyo akaanza
kuiandika historia ya maisha ya maimartha, katika kipindi chote alichokuwa
akiandika, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno. Alitumia masaa manne,
tayari aliandika theluthi ya kitabu cha msicha huyo na kulala.
Siku
iliyofuatia, kamakawaida yae akajiandaa na kuanza kwenda kwenye hospitali ya
Ganga ya hapo nchini India kwa ajili ya kuendelea kuiskiliza historia ya maisha
ya msichana huyo.
Alipofika, moyo wake ukamlipuka, hakuamini kile
alichokuwa amekiona mbele yake, wazazi wa msichana huyo walikuwa nje wakilia
kama mtoto hali iliyoonyesha kwamba kulikuwa na kitu kibaya kilichokuwa
kimetokea.
Kwa hatua za harakaharaka akaanza kuwafuata huku akiwa na
begi lake lenye laptop yake, alipowafikia, hata kabla hajauliza swali lolote,
mlango wa chumba kile alichokuwa amelazwa Maimartha ukafunguliwa na machela
kutolewa, hakumuona mtu aliyekuwa amelala ila kitu pekee alichokuwa amekiona ni
shuka la kijani lililozunguka machela ile iliyokuwa ikisukumwa kwa
harakaharaka.
“Maimartha amefariki, itakuwaje kuhusu historia ya
maisha yake? Mungu, kwa nini umemchukua hata kabla hajamalizia kunihadithia nini
kiliendelea? Mungu, tafadhali, naomba umrudishe Maimartha, ninamuhitaji,
ninahitaji kumpa furaha baada ya mapito aliyoyapitia,” alisema Henry huku
akiiangalia machela ile.
Akashindwa kuvumilia, akaanza kububujikwa na
machozi, picha ambayo alikuwa akiiona ilikuwa mbaya kwake, msichana aliyekuwa
akimpenda ambaye alikuwa ameisimulia histoeia ya maisha yake alikuwa
amefariki.
“Henry...Maimartha amefariki...” alisema mzee Paul, moyo wa
Andrew ukapigwa ganzi, akahisi kuchanganyikiwa. Kilichomchanganya zaidi,
historia ya Maimartha ilikuwa ikikaribia kumalizika, akaambiwa kwamba
amefariki.
“Nooooooo!!!!” alijikuta akipiga kelele, akaanza kukimbia
kuelekea kule machela ilipokuwa ikisukumwa, tayari alionekana kama chizi, hata
begi lake la laptop lilikuwa
chini.
Wakati mwingine Henry alijiona
kama yupo ndotoni ambapo baada ya muda wa dakika kadhaa angeshtuka na kujikuta
yupo kitandani huku akijiandaa kuandika kitabu cha maisha ya Maimartha, kile
kilichokuwa kimetokea, hakika hakikuwa ndoto, kilikuwa ni kitu halisi
kilichokuwa kikitokea katika maisha yake.
Bado alikuwa akikimbia
kuelekea kule machela ilipokuwa ikisukumwa, moyo wake aliuhisi ukiwa umepigwa
ganzi, hakuamini hata mara moja kwamba pamoja na safari ndefu ya kuja nchini
India kwa ajili ya matibabu, mwisho wa siku msichana aliyekuwa akimpenda ambaye
aliimba nyimbo za injili, Maimartha Paul angefariki dunia.
“Maimartha,
haiwezekani,” alisema Henry.
Alikuwa amechelewa, mpaka anafika kule
kulipokuwa na machela, tayari manesi wale walikuwa wamekwishaiingiza katika
chumba kilichosomeka Mortuary (Mochwari) kwa nje.
Akaanza kuugonga
mlango huku akilia kama mtoto lakini mlango haukufunguliwa, alitakiwa kubaki
pale nje kwani ndiyo kwanza taratibu zilikuwa zikitaka kufanyika kuhusu
kuuhifadhi mwili huo kwenye jeneza na mambo mengine kuendelea.
“Open
the door, please open the door I want to give her my last kiss, please open the
door” (Fungua mlango, tafadhali fungua mlango ninataka kumpiga busu la mwisho,
tafadhali fungua mlango) alisema Henry lakini mlango ule
haukufunguliwa.
Miguu yake ikakosa nguvu, akajikuta akikaa chini na
kuanza kulia. Machozi yaliendelea kumbubujika mashavuni mwake, bado kile
kilichokuwa kikiendelea hakikuwa kikiaminika kabisa.
Aliifikiria
safari ndefu ya kutoka nchini Tanzania, kuacha muda wake na kumsindikiza
msichana aliyekuwa akimpenda. Pamoja na muda wake kupotea, kumuonyeshea mapenzi
mazito lakini bado Maimartha alikuwa amefariki, hakika yalikuwa ni maumivu
yasiyosimulika moyoni mwake.
“Usiniache Maimartha, ninakupenda, naomba
usiniache,” alisema Henry, ghafla kama mtu aliyekumbuka kitu, akasimama na
kuanza kuwafuata wazazi wake na Maimartha, mzee Paul na mkewe, bi
Asteria.
Tayari mwili wake ulikuwa umelowa jasho, alionekana kama
alikimbia umbali mrefu kama wafanyavyo wakimbiaji wa mbio ndefu, alikuwa akihema
kwa harakaharaka kama mbwa, alipowafikia, akaanza kuwaangalia, nao walikuwa kama
yeye tu, machozi yaliwabubujika.
“Maimartha hajafa,” alisema Henry,
maneno hayo yakamshtua kila mmoja.
“Unasemaje?” aliuliza mzee Paul kwa
mshtuko.
“Maimartha hajafa na hawezi kufa kabla ya kitabu chake kutoka
na mimi kumuoa. Nimemleta Maimartha nchini India kwa ajili ya kutibiwa,
amenihadithia kitu nilichokuwa nikikitaka, bado hajamaliza, inakuwaje afe na
wakati ninataka kujua waliondokaje Urusi? Inakuwaje Maimartha afe na wakati
nilikwishamwambia kwamba ninampenda na ninataka kufunga naye ndoa? Kuna kitu,
bado Mungu ana makusudi na maisha yake, anataka mpaka tukio hili niliandike
kwenye kitabu huku nikisema kwamba moyo wake ulisimama kwa dakika kadhaa.
Ninaamini Maimartha hajafa,” alisema Henry.
Alionekana kama kichaa
lakini maneno aliyoyaongea yalikuwa yenye nguvu sana mioyoni mwao. Walimwangalia
mara mbilimbili, mapenzi mazito juu ya binti yao yalionekana machoni mwake,
walichokifanya ni kumsogelea na kisha kumkumbatia.
Kumbatio hilo
likaongeza kilio kwa Henry, akazidi kulia tena kwa sauti ya juu iliyowafanya
madaktari wengine kumsogelea na kuanza kumbembeleza lakini
hakunyamaza.
“Ninahitaji Maimartha arudi, tushikane mikono na tuanze
kumuombea,” alisema Henry kwa ujasiri mkubwa, wakashikana mikono na kuanza
kumuombea.
****
“Hali ya mgonjwa inazidi kuwa mbaya zaidi,”
alisikika Dk. Mandak, alikuwa akiwaambia wenzake kuhusu
Maimartha.
“Kwa nini?”
“Ametumia muda mrefu sana kuzungumza,
sijajua anazungumza nini na ndugu zake, inatakiwa apumzike kwa takribani wiki
nzima bila kuongea chochote, anapoongea, anailazimisha mishipa yake kufanya kazi
kitu ambacho hakitakiwi kwa sasa,” alisema Dk. Mandak.
“Kwa hiyo
tufanye nini?”
“Usiku wa leo tunatakiwa kumuhamisha chumba,
hatutotakiwa kuwaambia wazazi wake, kitu pekee ambacho tutawaeleza ni kwamba
mgonjwa hatoweza kuzungumza kwa sasa, hii inaweza kusaidia.”
“Sawa.
Basi tufanye hivyo.”
Hicho ndicho kilichozungumziwa mahali hapo. Kadri
muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hali ya Maimartha ilizidi kuwa
mbaya. Kitendo cha kukaa kwa muda mrefu akizungumza na ndugu zake kuhusu
historia ya maisha yake kiliifanya hali yake kuwa mbaya zaidi, hivyo alihitajika
kupumzika.
Usiku wa siku hiyo wakati ambao wazazi wake hawakuwepo,
wakamtoa Maimartha na kumpeleka katika chumba kingine kabisa na chumba kile
kumuingiza mgonjwa mwingine aliyekuwa na tatizo la figo kujaa maji ambapo kwa
kitaalamu zaidi hujulikana kama Nephrotic syndrome
Mgonjwa huyo
hakukaa sana, ilipofika saa kumi na mbili alfajiri, akafariki dunia. Wakati
madaktari wakikimbizana ndani ya chumba hicho, mzee Paul na mkewe, bi Asteria
wakashtushwa sana hasa baada ya nesi mmoja asiyejua chochote kuwaambia kwamba
mgonjwa aliyekuwa ndani ya chumba hicho alikuwa amefariki, wakaanza
kulia.
Wakati Henry anaingia hospitalini hapo, madaktari ndiyo wakawa
wanautoa mwili huo, kuona hivyo, bila kugundua kwamba aliyetolewa hakuwa
Maimartha, Henry akaanza kulia kama mtoto.
****
Dk. Mandak
ndiye alikuwa wa kwanza kukumbuka kwamba hawakuwa wamewapa taarifa ndugu wa
Maimartha kuwa mtu waliyekuwa wamemtoa hakuwa mgonjwa wao bali alikuwa mtu
mwingine.
Huku akionekana kukurupuka, akaanza kukimbia kuelekea kule
walipokuwa Henry na wenzake, wote walikuwa wameshikana mikono huku wakisali kwa
kumuomba Mungu ayarudishe mapigo ya moyo wa Maimartha kama
ilivyokuwa.
“Samahanini,” alisema Dk. Mandak, wakabaki
wakimwangalia.
“Kuna nini? Amerudiwa na fahamu?” aliuliza
Henry.
Hapo ndipo Dk. Mandak alipoanza kuwaambia kila kitu
kilichoendelea usiku na dhumuni lao la kufanya kitendo kile,kila aliyesikia,
akapiga magoti chini na kuanza kumshukuru Mungu kwa kile alichokuwa amekitenda.
Wakakumbatiana na kuanza kushangilia.
Machozi yao ya uchungu
yakabadilika na kuwa machozi ya furaha, hawakuamini kama kweli kile walichokuwa
wameambiwa kilikuwa kweli. Katika hali ya kushangaza na furaha kubwa aliyokuwa
nayo, Henry akamkumbatia mpaka Dk. Mandak.
Alichokuwa amewaambia
ndicho walichotakiwa kukifanya, hawakutakiwa kuzungumza na Maimartha hata neno
moja, kama alivyokuwa kitandani, walitakiwa kumuacha hivyohivyo.
Kitu
kilichompa wakati mgumu ni kwamba Henry alikuwa na shauku kubwa ya kutaka
kuendelezewa historia ya maisha ya Maimartha, kitendo cha kuzuiwa kilimuumiza
kupita kawaida.
Kwa muda wa wiki nzima hawakuongea na Maimartha,
walikuwa wakifika ndani ya chumba hicho na kumwangalia tu kitandani kana kwamba
alikuwa mdoli.
Bado alikuwa amepooza kitandani pale, hakuweza kuinua
kiungo chochote cha mwili wake, alikuwa kama gogo tu, ajali ambayo aliipata
nchini Tanzania iliyabadilisha maisha yake.
“Ila bado miezi mingapi?”
aliuliza Henry.
“Wala sijui, ngoja tusubirisubiri kwanza,” alijibu
mzee Michael.
“Daah! Nina hamu ya kumuona akisimama
tena.”
Baada ya kukaa tena kwa wiki nyingine ndipo waliporuhusiwa
kuzungumza na mgonjwa kwani kidogo hali yake ilikuwa na unafuu na si kama
ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
“Mpenzi...ilikuwaje?” aliuliza Henry
huku akijiweka vizuri
kitini.
Safari ya
kuelekea Moscow haikuwa ya kawaida, ilikuwa ni moja ya safari yenye kuchosha
sana. Japokuwa usafiri ulikuwa ni treni za umeme lakini bado walijisikia mchoko
mwingi.
Maimartha ndiye ambaye alipata tabu zaidi, mguu wake ulikuwa
umejeruhiwa na risasi ile iliyomuweka katika hali mbaya ya kuchanwachanwa nyama
za paja lake, kadiri baridi lilivyokuwa likipiga na ndivyo ambavyo maumivu
yalivyokuwa yakiongezeka.
“Tuombe Mungu tufike salama, siwezi kuishi
tena Ulaya, bora nirudi Afrika kwenye amani,” alisema Ongowi huku akionekana
kutokulipenda kabisa bara la Ulaya kutokana na kile kilichokuwa
kimetokea.
“Siwezi kuishi huku, ni bora nirudi nikaungane na familia
yangu na hata kama kufa, bora nife nikiwa mikononi mwao,” alisema Maimartha huku
akibubujikwa na machozi.
Walichukua saa moja, treni ikaingia ndani ya
Jiji la St. Petersburg ambapo hapo wakatakiwa kupumzika na baadae kuendelea na
safari ya kuelekea Moscow, jiji lililokuwa upande wa Kusini kutoka katika jiji
la Petersburg.
Hawakuchukua masaa mengi, wakaingia ndani ya jiji hilo,
kitu cha kwanza kabisa walichokifanya ni kutafuta sehemu ilipokuwa na ubalozi wa
Kenya, hawakutaka kabisa kuishi nchini humo huku wakiwa hawana vibali
vitakavyowawezesha kuishi kwa amani.
Waliuliziaulizi na mwisho wa siku
kupelekwa katika ubalozi huo ambapo Ongowi akajitambulisha na kumtambulisha
Maimartha na kuanza kuhadithia kile kilichokuwa kimetokea katika maisha
yao.
“Mmmh! Mbona mmepitia maisha ya mateso namna hiyo?” aliuliza
balozi wa Kenya nchini Urusi, mwanamke mcheshi aitwaye Christine
Onyango.
“Matatizo mama. Hapa tulipo, tunataka kurudi Afrika, sina
hamu tena na Ulaya,” alisema Ongowi.
Kwa kuwa walifika katika sehemu
iliyo salama, wakaanza kushughulikiwa kila kitu na baada ya wiki mbili walikuwa
ndani ya ndege wakirudi barani Afrika.
Kwao, ikaonekana kama ndoto,
hawakuamini kwamba mwisho wa mateso yote yale wangeweza kurudi barani Afrika.
Waliyakumbuka vilivyo maisha waliyokuwa wamepitia katika kisiwa kile ambapo
baadae maji yakaganda na kuanza kutembea, hakika yalikuwa mateso makubwa ambayo
hayakuweza kuelezeka.
“Na vipi kuhusu mumeo?” aliuliza
Ongowi.
“Nani?”
“Huyo Damian.”
“Sijui chochote
kile, kitu ninachokitaka ni kurudi nyumbani tu. Sijui kama alikufa au yupo hai,
ninachotaka ni kurudi nyumbani,” alisema Maimartha.
Baada ya kukaa
masaa thelathini na nane ndani ya ndege na ndipo ndege hiyo ikaanza kutua katika
Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyata ambapo kulikuwa na watu waliokuwa wakiwasubiria
wakiwepo waandishi wa habari, kwani tayari taarifa zilikwishatolewa
mitandaoni.
“Kumbe ni binti mdogo. Mungu wangu! Mwangalie
anavyosikitisha,” alisikika mtangazaji mmoja wa Kituo cha televisheni cha KTN,
alikuwa akimwangalia Maimartha.
Wote wawili wakajisikia amani, kitendo
cha kurudi barani Afrika kiliwafariji mno. Baada ya wiki mbili za kuishi nchini
Kenya huku afya yake ikiwa imeimarika, Maimartha akaruhusiwa kurudi nchini
Tanzania.
“Waooo! Karibu mwanangu,” alisema bi Asteria huku akionekana
kuwa mwenye furaha tele.
“Asante mama,” aliitikia Maimartha huku
akijitahidi kuyazuia machozi yake yaliyoanza kujikusanya machoni
mwake.
Kuanzia siku hiyo hakutaka kusikia tena safari za kwenda Ulaya.
Kwa sababu alikuwa na kipaji cha kuimba na huku akiwa na fedha nyingi katika
akaunti yake ya benki kutokana na mshahara aliokuwa akilipwa melini kuagizwa
uwekwe humo, akaanza kufanya muziki kwa kurekodi nyimbo zake
mbili.
Nyimbo hizo ndizo zilimpa jina nchini Tanzania, zilikuwa
zikipigwa sana katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni, kila
aliyezisikia nyimbo hizo, moyoni alisikia kubarikiwa mno.
Taratibu
jina lake likaanza kutangazika Tanzania nzima, akawa akiitwa kwenye mikutano
mbalimbali huku akipokea mialiko mingi ndani na nje ya Tanzania. Maimartha yule
akabadilika, akawa Maimartha aliyetembea juu ya fedha. Akajenga nyumba zake
kubwa mbili, maisha yakabadilika kabisa.
Hakukuwa na mtu aliyeifahamu
historia ya maisha yake, kila alipotaka kuwaeleza wazazi wake kule alipokuwa
amepitia, alisita kufanya hivyo kwa kuamini kwamba duniani hakukuwa na siri
zaidi ya mtu mmoja.
Moyo wake ukabeba mzigo mzito, kuna upande mmoja
wa moyo wake ulimwambia kwamba ni lazima aisimulie historia ya maisha yake ili
watu wajifunze lakini upande mwingine wa moyo wake ulimkataza kufanya hivyo
kwani angejidhalilisha.
Watanzania hawakuchoka kuuliza, kadri miaka
ilivyozidi kwenda mbele walihoji kuhusiana na ndoa ya Maimartha lakini moyoni
mwake msichana huyo hakutaka kuolewa, alitaka kuishi peke yake maisha yake
yote.
“Sipendi kuolewa,” alisema Maimartha, alikuwa akimwambia
Jonathan, kijana aliyekuwa akimfuatilia kwa kipindi kirefu
kanisani.
“Kwa nini sasa?”
“Wewe elewa kwamba sipendi
kuolewa.”
“Jamani, mbona unanifanyia hivyo? Bwana amenionyesha kwamba
wewe ndiye mke wangu,” alisema Jonathan.
“Yaani akuonyeshe wewe na
mimi asinionyeshe? Huyo bwana ni wa kichina, angalia asije kuwa shetani,”
alisema Maimartha na kuondoka mbele ya macho ya Jonathan.
Wanaume
hawakukata tamaa, kila siku waliendelea kumfuatilia msichana huyo lakini jibu
lake lilikuwa lilelile kwamba hapendi kuolewa. Kulikuwa na maswali mengi
yaliyokuja vichwani mwa watu juu ya msimamo wake lakini hakukuwa na majibu
yaliyotolewa.
Wachungaji, askofu walikwishamuita sana na kumuuliza
kuhusu hilo lakini bado jibu lake lilikuwa lilelile na msimamo wake hakutaka
kuubadilisha.
“Siwezi kuolewa maishani mwangu....siwezi,” alisema
Maimartha huku akiwa ndani ya gari lake aina ya Range SV alilolinunua kwa zaidi
ya milioni sitini.
****
Mpaka anamalizia kuisimulia historia
ya maisha yake, kila mmoja alikuwa akilia, alikuwa binti mdogo kulinganisha na
maisha aliyokuwa amepitia hapo nyuma. Pamoja na hayo yote, Henry alimuahidi
kumpa furaha ya milele.
“Ninahitaji kukuoa Maimartha,” alisema henry
huku akikifunga kitabu chake.
“Unioe
mimi?”
“Ndiyo.”
“Haiwezekani.”
“Kwa
nini?”
“Siwezi kuzaa tena.”
“Utazaa tu, kwani dokta
amekwishawahi kukwambia hilo?”
“Hapana.”
“Sasa kwa nini
usizae?”
“Nimetoa mimba mingi.”
“Usijali. Kwa jina la yesu
kristo utazaa tu, amini hilo,” alisema Henry kwa ujasiri mkubwa.
Miezi
iliendelea kukatika zaidi, madawa ambayo alikuwa akipewa yalizidi kuleta
mabadiliko maishani mwake. Baada ya miezi sita ya mateso kitandani, hatimae
viuongo vyake vya mwili vikaanza kucheza.
“Mama,” aliita Henry,
alikuwa kama mtyu aliyekurupushwa kutoka kwenye hali fulani.
“Kuna
nini?”
“Nimeona vidole vya Maimartha vimecheza.”
“Unasemaje?
Ulikuwa ukiota?”
“Hapana mama. Nimeviona vikicheza,” alisema Henry
huku akimsogelea msichana huyo kitandani.
“MmmH! Haiwezekani bwana,
Haiwezi kuwa hivyo.”
“Hapana mama, Mungu amefanya maajabu, amemletea
uponyaji,” alisema Henry kwa furaha. Alichokifanya ni kuuinua mkono wa Maimartha
na kuanza kuviangalia vidole vile, kwa mbali vilikuwa
vikichezacheza.
“Mama angalia, Maimartha anaanza kupokea upoyaji,”
alisema Henry.
Hayo ndiyo mabadiliko ya mwili wake yalipoanza. Baada
ya kukaa nchini India kwa zaidi ya miezi sita, leo hii viungo vya mwili wa
Maimartha vilianza kucheza na mwisho wa siku akaweza kujigeuza huku na
kule.
Ilikuwa ni furaha kwa familia yake, lakini zaidi ilikuwa ni kwa
Henry, hakuamini kama mpenzi wake alikuwa amepona na kurudiwa katika hali ya
kawaida.
Taarifa zile zilipowekwa kwenye mitandao, waandishi
wakazichukua na kuanza kuziweka kwenye magazeti yao.
Ulikuwa ni
muujiza wa hali ya juu, wakristo wakaitakna katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na
kuanza kumshukuru Mungu kwa muujiza mkubwa aliokuwa ameufanya.
Miezi
miwili baadae, wote wanne walikuwa ndani ya ndege wakirudi nchini Tanzania.
Hakika ilikuwa ni furaha ya kila mtu, msichana aliyepata ajali ambaye alipooza
kitandani kwa muda wa zaidi ya miezi sita, leo hii alikuwa amepona na kuwa kama
zamani.
Kwa Henry, alikuwa amekamilisha safari yake ndefu,
alichokifanya ni kuendelea kukiandika kitabu kile kilichopewa jina la MY PATH
(NJIA ZANGU) akimaanisha kwamba kitabu kile kilihusu kila njia zote alizopitia
katika maisha yake zikiwepo zile njia zilizojaa mateso, maumivu lakini mwisho wa
siku akapita katika njia zilizojaa faraja na amani.
Baada ya miezi
minne baadae, kitabu kikawa tayari na kopi kuwekwa mitaani. Ndani ya mwezi wa
kwanza tu, zaidi ya kopi laki tano zilikuwa zimenunuliwa na hivyo nyingine
kuongezwa.
Kitabu chake kiliuzwa kwa zaidi ya kopi milioni mbili,
kupitia kitabu hicho, akapata fedha nyingi ambazo zilimfanya kuyaendeleza maisha
yake zaidi kwa kufungua biashara.
Kitabu kile kilionekana tofauti na
vingine, kila aliyekisoma, moyo wake ulimsisimua, wengi walikuwa wakibubujikwa
na machozi, kilikuwa kitabu chenye kuumiza lakini mwisho wa siku kilimfariji
kila mmoja.
Japokuwa alipata fedha nyingi, hakumsahau Ongowi ambaye
alikuwa na uhakika kwamba bado hakuwa na maisha mazuri mpaka kufikia hatua ya
kutaka kuzamia Ulaya.
Akamtumia kiasi cha fedha cha zaidi ya shilingi
milioni mia mbili na kumjengea nyumba huku akimtaka kufungua biashara, ushauri
ambao ulichukuliwa na Ongowi na kufungua biashara hizo.
“Na vipi
kuhusu Damian, hukuniambia aliishia wapi,” aliuliza Henry.
“Sijui
chochote kile. Sijui kama alikufa au alipona. Sitaki kukumbuka maisha ya nyuma,
mpaka hapa nilipofikia, sina budi kumshukuru Mungu,” alisema Maimartha na
kumkumbatia Henry.
Ukaribu wao ukaongezeka na mwisho wa siku kutangaza
uchumba kanisani. Henry akaonekana kuwa mwanaume aliyeishi na bahati kubwa, na
baada ya miezi miwli, wawili hao wakafunga ndoa kanisani, wakawa mume na
mke.
“Nataka uuone muujiza mkubwa maishani mwako. Unataka kufanyiwa
muujiza gani na Mungu?” aliuliza Henry.
“Wowote ule mume wangu.
Unahisi ninapenda nifanyiwe muujiza gani?”
“Tutapata mtoto ndani ya
miezi tisa na jina lake tutamuita Upendo,” alisema Henry.
“Atakuwa wa
kiume au wa kike?”
“Wewe unataka tuanze na yupi?”
“Wa
kiume.”
”Basi sawa. Ngoja tumwambie muumbaji atuumbie mtoto wa kiume
tumboni mwako,” alisema Henry.
Japokuwa waliongea kimasihara lakini
mioyo yao ilijawa na imani kubwa, baada ya mwezi mmoja na nusu, Maimartha
akaanza kutapika ovyo na dalili zote za mimba kuonekana. Alipokwenda kupima,
akagundulika kwamba ana mimba ya mwezi mmoja na nusu.
“Nilikwambia mke
wangu. Umeona? Mungu amefanya, bado tu kuufanya muujiza mmoja, tunataka awe wa
kiume,” alisema henry kwa furaha.
Ukaribu wao kama mke na mume ulikuwa
ukindelea, walikuwa miongoni mwa matajiri wakubwa nchini Tanzania. Henry hakuwa
mwandishi tena, aliiacha kazi hiyo na kusimamia biashara zao.
Baada ya
miezi tisa, Maimartha akajifungua mtoto wa kiume na kumpa jina la Upedo. Alikuwa
mtoto mzuri aliyechukua sura ya Henry lakini mikoni, miguu alichukua kutoka kwa
Maimartha.
Mtoto huyo akaongeza upendo maishani mwao, wakaendelea
kupendana zaidi. Hawakuacha kumshukuru Mungu kwa kila kitu. Waliendelea kuwa
pamoja huku mapenzi baina yao yakizidi kuchanua kila
siku.
“Ninakupenda mume wangu,” alisema Maimartha kitandani, alikuwa
amemkumbatia mume wake, Henry.
“Ninakupenda pia. Umepitia matatizo
mengi maishani mwako, yoooooote hayo, tufanye umeyapitia wakati wa mchana, kwa
sasa, Lets call i a night kwa sababu unalala na hivyo kuikaribisha siku nyingine
yenye mafanikio,” alisema henry kwa sauti ya kimahaba.
“Yeah! Kila
kitu kilichoppita, naomba kiwe historia, nimekifunika kitabu changu chakavu,
sasa Mungu anakwenda kukifungua kitabu changu kingine,” alisema Maimartha na
kumkumbatia zaidi mume wake. Wakaanza kupeana mabusu
mfululizo.
MWISHO
Asanteni
kwa kuwa nami katika simulizi hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
0 comments:
Post a Comment