IMEANDIKWA NA : LASIMA N. NASSORO
*********************************************************************************
Simulizi
: Dunia Rangi Rangire
Sehemu Ya Kwanza (1)
"UVIVU ni adui mkubwa kwa ujenzi wa taifa, tena ndiyo usababishao njaa, ewe ndugu yangu we amka kumekucha, kamata jembe na panga twende shamba, ewe karani amka kumekucha kwani hizi ni saa za kwenda kazi, ewe mwanafunzi amka kumekucha chukua kalamu na kitabu uende shule.”
Huo ulikuwa wimbo uliokuwa unaimbwa redioni asubuhi na mapema, wakati huo Bi Marina alikuwa ameshatayarisha uji na kiporo cha mihogo alichokuwa amemwekea mwanawe. Akaenda chumbani kwa mwanawe kumwamsha,
“Kibe, Kibe mwanangu.”
“Naamu,” ilikuwa ni sauti ya Kibe akiwa bado ana usingizi.
"Jitahidi baba uamke maana kumeshakucha,”
Kibe akiwa bado ana usingizi, akajikokota kutoka kitandani na kumfata
mama yake jikoni.
“Shikamoo mama"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Marahaba, umeamkaje?”
“Nashukuru nimeamka salama, sijui wewe"
"Hata mie niamka salama, nenda ukanawe uso halafu uje upate staftahi
maana saa zimekwenda"
"Sawa mama, baba bado amelala?"
"Yupo macho, si unasikia redio inalia, msemeshe tu atakuitika.”
Baada ya kunawa uso, Kibe akaenda kumsalimia baba yake Mzee Sosongo
kisha akaenda jikoni kufungua kinywa.
“Sasa leo unaenda kuchungia upandi upi?" Marina alimuuliza mwanawe.
“Hata sijajua maana siku hizi majani yamekuwa ya shida, Hii mvua isiponyesha mifugo itapata sana shida.”
Baada ya kumaliza staftahi Kibe akafungulia mifugo,
“Mama ngoja niende maana leo nimechelewa sana, kwa nini hukuniamsha mapema?”
“Najua unachoka sana mwanangu, ndiyo maana sikuwahi kukuamsha ili walau
upunguze uchovu”
"Ngoja basi mie niende, utaniagia baba."
“Haya, nenda baba na mizimu ya mababu ikulinde na lolote baya"
"Taire mama.”
Kibe akaondoka na mifugo kwenda kutafuta malisho.
*******
Kibe alikuwa mtoto pekee wa Mzee Sosongo na Bi Marina,walikaa muda mrefu sana bila kujaaliwa kupata mtoto hadi wakakata tamaa maana walikuwa wameanza kuzeeka.
Japo kuwa Kibe alikuwa ndiye mtoto wao pekee, Mzee Sosongo na bi Marina hawakudekeza mtoto wao. Mara zote walimuasa kuwa,uvivu ni adui wa maendeleo na ili ufanikiwe lazima ujitume kwa moyo wako wote. Kibe aliporudi jioni kutoka machungani alikuta kuna wageni.
Baada ya kuingiza mifugo zizini akamfata mama yake jikoni,
"Habari za kushinda mama."
"Nzuri mwanangu, je wewe umeshindaje?"
"Nimeshinda vyema mama,ila nina njaa kweli, kuna chochote cha kula?"
"Angalia hapo kwenye kitala nimekuwekea chakula, uje uchukue na maziwa ushushie,"
Wakati Kibe anaendelea kula akamuuliza mama yake," hivi mama hao wageni
wanaoongea na baba ni kina nani?"
"Huyu wa kike si ni Teresia mtoto wa baba yako mdogo Kaborongo? Huyo mwanamume ni mumewe amemleta ili tumjue."
"nnilishamsahau,ni muda mrefu umepita toka nilipo muona".
"Alikuwa anamwambia baba yako kuwa kwasababu umemaliza darasa la saba
na hukuchaguliwa kuendelea sekondari basi uende nae mjini akakutafutie
chochote cha kufanya".
"Mie sitaki kwenda huko mjini, kwanza nikiondoka nani atakae kuwa
anachunga mifugo? Umri wa baba umekwenda sidhani kama anaweza
kukimbizana tena na mbuzi".
"Baba yako bado hajaamua,alisubiri urudi kutoka machungani ndiyo
akuelezee nawe pia utoe maoni yako".
"Maoni yangu ni kuwa sitaki kwenda huko mjini,kwanza huyu dada
mwenyewe sijamzoea sembuse kukaa naye?"
"Subiri hadi baba yako atakapokueleza ndipo nawewe utoe maoni yako,na
usije ukasema nimekueleza maana wamjua baba anavopenda kila jambo
aanze yeye kulisema."
"Sitamwambia, ngoja nikaoge maana baridi ikizidi kuniingia mwilini sitaoga tena"
Mzee Sosongo akamuita mkewe baada ya wageni kuondoka. Mkewe alifika pale alipo Mzee Sosongo akamkuta akikohoa, akasubiri hadi alipoacha kukoho,
“Baba Kibe, nimekuambia uache kuvuta sigara lakini hutaki, waona jinsi kikohozi chako hakiishi japo unakunywa dawa kila siku?"
“Mama Kibe, hiki ninachovuta siyo sigara bali ni kiko, 'KIKO' kwani huelewi?"
“Kwani ukivuta kiko au uvute sigara,moshi si ndiyo unaingia mwilini mwako?"
“Haya nimekusikia maana ukianza kuongelea kitu humalizi"
“suala si kumaliza au kutomalizi,muhimu ni kuelewa na kuchukua hatua
kwa yale uelezwayo"

“Sawa mke wangu,nimekuelewa nitajihidi kujaribu kuacha, ila siyo rahisi ufikiriavyo. sasa nilichokuitia hapa ni kuhusu haya huyu mtoto wa
Kaborongo aliyotueleza, je wewe unafikiriaje?”
“siyo wazo baya ila unatakiwa umueleze Kibe usikilize kuwa nayeye anaamuaje.”
“Kibe bado mdogo,hajafikia umri wa kujiamulia mwenyewe,sisi ndiyo
tunatakiwa tujadili kisha tumueleze tutakayoamua.”
“Sawa nimekuelewa,mfano tumeamua kuwa aende huko mjini,je ni nani
atakuwa anachunga?”
“Suala la kuchunga hilo halina shida, siku hizi kuna huyo kijanaaitwaye Sereng'ei, huwa anachukua mifugo ya wale ambao hawana mchungaji
na kuipeleka malishoni na kila baada ya miezi mitatu unampa mbuzi jike
au kondoo jike"
"sasa wewe unaamuaje? tumwambie aende huko mjini?"
"Mie naona aende akaangalie kama atapata cha kufanya,pia kutamfanya
alinganishe maisha ya mjini na ya huku kijijini,akiona kuwa maisha ya
mjini hayampendezi basi arudi."
Kibe alipoelezwa kuhusu uamuzi wazazi wake waliyofanya kuwa aende huko mjini, alipinga wazo hilo kama alivyomueleza mama yake pale mwazo
walipokuwa jikoni.
Mzee Sosongo akakohoa na baada ya kutulia akasema,
“Mwanangu, tambua kuwa yote haya ni kwa ajili yako,ni kwa faida ya maisha yako hapo baadaye, hakuna mzazi amtakiae mwanae mabaya,na furaha ya mzazi ni kumwona mwanaye akifanikiwa kimaisha, hatuja kuambia kuwa ukienda huko
mjini basi ukae huko huko na usirudi tena huku,hapa ni kwako na tambua
kwamba, hakuna tembo alemewaye na mkonga wake."
“Sawa baba nimekuelewa,nitaenda,ila nikiona mambo hayaniendei vizuri nitarudi," Mama yake ambae wakati wote huo alikuwa kimya, naye akasema,
"Na hatuombi yakawe mabaya,baba yako atachukua maziwa ili aieleze mizimu
ya mababu zako kuwa ikakutangulie na kukuongoza huko utakapo kwenda, si
ndivyo baba Kibe?"
“Ndivyo hivyo mama Kibe, kipindi nikiwa na rika kama la Kibe, baba yangu
aliniambia kuwa, kama unakwenda safari ya mbali na unaondoka bila kuiambia mizimu, basi huko uendako hutafanikiwa," baada ya siku mbili kupita toka Teresia aje nyumbani kwa baba yake mkubwa Mzee Sosongo,akarudi tena kuwaaga.
Teresia baada ya kusalimiana na Mzee Sosongo na mkewe bi Marina, akawauliza ,
"Kibe hajarudi toka machungani?"
Mzee Sosongo akasema,
"siku hizi majani yamekuwa ya shida sana,hivyo
wanakwenda kutafutia mifugo malisho mbali,hadi afike hapa giza
linakuwa limeanza kuingia,"
Teresia akamuuliza tena Mzee Sosongo,
“Na mmejadiliana kuhusu yale niliyowaeleza siku ile ya kuhusu kwenda na Kibe mjini?"
"Ndiyo ,tumejadiliana na Kibe amekubali muende wote".
"Sawa baba, sasa mie kilichonileta hapa ni kuwaaga,kesho nataka nirudi mjini"
"Na mumeo,mbona yeye hukuja kutuaga?"
"Hajisikii vizuri, toka tumekuja amekuwa akisumbuliwa na homa,amenituma niwape salaamu zake na anawaomba radhi kwa kushindwa kuja kuwaaga"
"Ukifika mwambie tumezipokea na twamuombea apone."
"Sasa baba, sikai sana maana mama ameniambia twende niwahi kurudi ili
akanitolee mihogo kwenye lile shamba letu la kule bondeni, Kibe
akirudi, mwambie aje alale kule kwetu maana tutaondoka mafungulia
ng'ombe ili tuwahi basi la mkikicho."
"Sawa mama, nawatakieni safari njema na kama ujuavo huyu mdogoako
hajawahi kutoka hapa kijijini toka azaliwe hivyo nakuomba mama, mkifika
huko mjini usije ukamwacha akapotoka, mwonye na kumpa muelekeo pale
utakapoona amekosea."
"Sawa baba nimekuelewa" Teresia akatoka na kumfata bi Marina
jikoni,

"Mama miye nataka kuondoka"
"Mbona haraka hivyo mwanangu? Siburia chakula kiive ule ndiyo uende"
"Hapana mama, ngoja niende maana mama ananisubiria ili twende katika lile shamba letu la kule bondeni tukachimbe mihogo."
"Haya mwanangu, kesho mtakapo safiri, nawatakieni safari njema"
"Amina mama, na nyie mubaki salama"
"Asante mwanangu"
Teresia alipoondoka, mama Kibe akamfata Mzee Sosongo kule alipo,
"Sasa mume wangu, Kibe atabeba nini akienda huko mjini?"
"Kuna ile ndizi iliyopo kule mwisho mpakani na shamba la bwana Kihara, nenda ukaikate ili iendelee kuchuruzika utomvu, mpaka Kibe arudi itakuwa imechuruzika utomvu wote."
"Atabeba ndizi pekeyake au tumchanganyie na viazi vitamu?"
"Fanya hivyo utakavoona inafaa,ila usije ukamuwekea mzigo utakaomlemea."
"Sawa mume wangu"
Kibe aliporudi akaambiwa ajiandae ili aende kulala kwa baba yake
mdogo, tayari kwa safari kesho.
. Baada ya Kibe kuwa tayari, Mzee Sosongo akachukua maziwa ili atambike, akamwaga kidogo chini karibu na mafiga kasha akasema.
"Thekere, chukua maziwa haya, kuwepo kwetu hapa ni sababu yako maana babu wa babu wa babu yangu alikuwa mwanao, kuna mwanao hapa anaenda huko mjini, twakuomba ukamwongoze na umfungulie njia na umwekee mkono apate hicho akifuatacho huko, umlinde na umwepushe na hila za wanadamu wabaya."
Baada ya kumaliza kusema hayo, akamwaga maziwa kidogo, yaliyobaki akanywa kidogo akampa mkewe naye akanywa kidogo kisha Kibe akaambiwa amalizie yaliyobaki. Mzee Sosongo akasimama kisha akatema mate kidogo kiganjani mwake na kumpaka Kibe katika paji lake la uso nakusema.
"Huko uendako, nyota yako ikang'ae kama mwezi, maadui wawe marafiki zako, majini yageuke kuwa malaika, wachawi wageuke kuwa waganga, wenye husda na chuki wageuke kuwa na upendo, na marafiki wazidishe urafiki wao, lolote utakalo fanya liwe na mafanikio, ukiokota jiwe libadilike liwe dhahabu."
Kisha akakaa, akasema, "Kibe mwanangu, huko uendako ni ugenini, heshima na adabu ndiyo silaha ya mafanikio yako, unapokosa omba msamaha, huko uendako utayaona mengi mwanangu, mengine mazuri na mengine mabaya, fuata yale mazuri na yatakayo kusaidia maishani, uepuke vishawishi vya mjini maana ukifata vishawishi, utasahau ulipotoka, pombe mwanangu ndiyo chanzo cha maovu yote humu duniani, epuka pombe, kufikia hapo sina la kuongezea, pengine kama Mama yako ana lake la kukuambia."
"Hayo uliyo mwambia yanatosha, mie namtakia tu safari njema"
Kibe akasimama pale alipokuwa amekaa na kwenda kupiga magoti mbele ya baba, kisha akasema, "Baba pamoja na Mama, hayo yote mliyonieleza nitajitahidi kuyatekeleza, kama nitaona maisha ya huko yamenishinda, nitarudi.”

Mzee Sosongo akamnyanyua na kusema.
"Sawa baba, chukua mizigo uende maana giza linazidi kuwa nene na usije ukatusahau ukiwa huko."
“Sitowasahau wazee wangu, kwaheri Baba, kwaheri Mama, mbaki salama.”
Taswira ya mji aliyokuwa nayo Kibe kichwani mwake ilikuwa tofauti na ile aliyoikuta, alishangaa kuona majengo marefu na barabara za lami.
“Divi dada hizi nyumba, walitumia mti gani mrefu kiasi hiki kutengeneza ngazi ya kujengea?
“Teresia akamjibu, "Hawakutumia mti, kuna chuma maalumu za kutengenezea majukwaa ndiyo walizo tumia."
"Na hizi barabara nyeusi hivi walitoa wapi unga wa udaga mwingi kiasi cha kutosha barabara zote hizi?"
"Hahaha, Kibe wanifurahisha kweli, hiyo inaitwa lami na siyo unga wa udaga uliotumika."
"Usinicheke dada, mwenzio nataka kujua, si unaelewa jinsi mazingira ya kule kwetu yalivyo?"
"Siyo kwamba nakucheka ila wanifurahisha jinsi unavyolinganisha unachokiona hapa na kule kijijini."
******
Maisha ya mjini yakampendeza Kibe, akawa akimwambia Teresia kuwa kama atafanikiwa kimaisha angependa na yeye ajenge nyumba nzuri mjini na kule kijijini. Teresia alitabasamu tu kila wakati Kibe akimweleza juu ya ndoto yake, siku moja Teresia akamwambia Kibe.
"Kibe mdogo angu, kila mtu anapenda awe na maisha mazuri, nyumba nzuri na gari la kutembelea lakini si kila mwenye ndoto hizo huweza kuzitimiza, unajua kwa nini?"
"Sijui Dada yangu, labda unifahamishe pia namna ya kutimiza ndoto hizo."
"Juhudi na maarifa ndiyo silaha ya mafanikio, ukiwa na nia ya kufikia malengo fulani, njia haikosekani si unajua mchagua jembe si mkulima?"
"Naifahamu hiyo methali, ila sijaelewa una maana gani"
"Namaanisha, ukitaka mafanikio usichague kazi ya kufanya maana huwa kiwango cha elimu cha kukufanya uchague kazi."
"Siwezi kuchagua kazi, siku nikiipata nitajibidiisha sana ili nibadili maisha yangu na ya wazazi wangu."
"Usijali, keshokutwa nitakupeleka kwa muhindi mmoja ambaye aliniahidi kuwa atakupatia kazi."
"Nitashukuru sana dada."

Siku aliyoahidiwa kupelekwa kwa muhindi ikafika, walipofika walipokelewa na mtu ambaye Kibe alifahamishwa kuwa ndie atakaye mpatia kazi.
"Bwana Kanjubai, kama nilivo kueleza kijana ndie huyu, baba na baba yangu wametoka tumbo moja, baba yake ndiye mkubwa kwa baba yangu," hayo ni maneno aliyosema Teresia baada ya kukaribishwa ndani na kukaa. Kanjubai naye akasema, "Basi mimi nimeona yeye, nilipoona umekawia kumleta, nikafikiri pengine wewe ilidanganya mimi."
"Kwa nini nikudanganye bwana Kanjubai? Nilikuwa nasubiri azoee mji, unajua hajawahi toka kijijini toka azaliwe."
"Ooh! okay, basi natumai yeye iko zoea sasa mji."
"Si saana, ila ana ndoto ya kufanikiwa maishani, anataka awe na nyumba nzuri hapa mjini."
Wakati wote huo Kibe alikuwa amekaa kimya akisikiliza mazungumzo kati ya Teresia na Kanjubai, aliposikia Teresia akimweleza Kanjubai juu ya ndoto yake, akatabasamu, Kanjubai akamwangalia kisha akamwambia.
"Kama wewe iko na ndoto ya kuwa na maisha zuri, usiwe vivu maana wazungu wanasema, work like bee and eat honey or work like fly and eat waste," Ikawa zamu ya Kibe kuongea.
"Nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kufikia hayo malengo yangu,"
Teresia akasema,
“Sasa bwana Kanjubai,mie ngoja niende tutaonana siku nyingine kunielezea mambo yatakavyokuwa yamefikia, Kibe, wewe utabaki hapa maana Kanjubai anataka akufunze kazi kwanza kabla ya kukuajiri."
"Sawa dada, hakuna shida, maadamu kazi ndiyo nimeifata huku mjini, hakuna shida nitabaki."
"Sawa, kwa heri bwana Kanjubai."
"Kwa heri Teresia, mimi tapigia wewe kukufahamisha kijana anavo endelea."
Baada ya Kibe kula chakula cha mchana, akapelekwa katika chumba chenye kitanda pekeyake na hicho kitanda kilikuwa katikati ya chumba, akaambiwa apumzike humo hadi hapo atakapo hitajika.
Baada ya mlango kufungwa Kibe akakaa katika kile kitanda, akasikia mdundo wa muziki lakini hakujua ulikuwa unatokea wapi maana hakuona redio humo chumbani, akaamua kujilaza kitandani huku akifikiria, 'kweli pesa ni sabuni ya roho, kitanda kizuri kama hiki ukute hakuna hata mtu anayekilalia'. Kibe akawa anasikiliza kwa makini maneno ya muziki uliokuwa unasikika humo chumbani.
"I'm the worm that cometh, iam him, iam hell, i'm the devil all in one, the eyes that hide the face inside come stare into my eyes. A killer is listening to horrors in my head.. He is bleeding, sliding on the razor's edge.. All pigs die, iam hell Godless , me iam pagan idolatry, kneel before the horror."

Hayo ni baadhi ya maneno yaliyokuwa katika wimbo huo. Japokuwa Kibe hakuelewa maana ya maneno ya wimbo huo, hakuupenda. Usiku ulipo ingia, Kibe aliletewa chakula, akaambiwa ale na alale maana kesho yake watasafiri kuelekea sehemu ya kazi.
Asubuhi na mapema, Kibe aliamshwa na mtu ambaye toka alipofika jana hakuwahi kumwona, alikuwa amevalia suti nyeusi na miwani mieusi.
"We dogo amka twende, utafurahia kitanda chako pindi utakapo kuwa na pesa."
hayo yalikuwa maneno ya huyo mtu aliyekuwa amevalia suti nyeusi. Kibe akaamka, akapelekwa bafuni akaoga kisha akapewa chai ya rangi na maandazi makubwa mawili. Alipo maliza kula, Kanjubai akaingia pale alipokuwa Kibe, akamuambia.
"Kibe, huyu anaitwa Moris, yeye atapeleka wewe sehemu ya kazi, kuna nguo yoyote ulikuja nayo tofauti ya hiyo uliyovaa?"
Kibe huku akimwangalia huyo jamaa mwenye suti nyeusi na miwani myeusi, ambaye anaitwa Moris kama alivoambiwa na Kanjubai, akajibu.
"Sikuja na nguo nyingine."
"Basi hakuna shida, nguo utapata huko, haya Moris mpeleke na ukifika uniambie jinsi kazi inavokwenda," Moris akasimama nakusema.
"Hakuna tabu boss, kila kitu kitakuwa shwari, twende dogo," Kibe akasimama na kumfata Morisi, wakaingia katika gari aina ambayo madirisha yake yalikuwa na giza, kisha wakaanza safari ndefu ambayo hakujua wanapoelekea.
Walisafiri siku nzima bila kusimama, walitoka sehem ya mji wakaingia mbuga, giza lilipoingia, Moris akapaki gari pembeni ya barabara na kumwambia Kibe.
"Tutapumzika hapa na alfajiri tutaendelea na safari," Kibe huku akipiga miayo, akauliza.
"Ina maana bado hutujakaribia kufika?"
"Bado sana, tukijitahidi kuwahi kesho asubuhi, pengine mpaka usiku saa nne au tano tutakuwa tumefika, kula chakula upumzike maana najua hujazoea safari ndefu."
"Sasa tulala wapi?"
"Lala kiti cha nyuma, mie nitajinyoosha hapa nilipokaa."

Safari ya kwenda kazini ndiyo hiyo imenza, Kibe anapelekwa wapi? Kanjibai na Moris ni nani?usikose sehemu ya tatu ya hadithi hii iliyojaa uhalisia wa maisha ya kijana wa kitanzania...Je ni kweli Dunia ni Rangi Rangile?...
ITAENDELEA

0 comments:
Post a Comment