Simulizi : Mama Yangu Adui Yangu
Sehemu Ya Pili (2)
Nilijikuta nikikosa jibu na kukifanya kichwa kisitulie, kwani kilikuwa kikiniuma kama kidonda kila nilipolazimisha kuwaza kitu kilichokuwa hakina jibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku ile sikutoka mpaka siku ya pili nilipofuatwa na mama ndani kunibembeleza.
Mwaija mwanangu mbona unataka kukufuru Mungu kwa kupewa talaka, kwani wewe ndiye wa kwanza?
Mama heri ningefanya kosa ningekuwa tayari kuachika, lakini kumsubiri mume wangu zaidi ya miezi nane, uvumilivu wangu zawadi yake kunipa talaka? Heri angenieleza kosa langu nikajua moja, mama inauma, inaumaa.
Mwanangu lazima ujue kama hukumkosea mumeo basi miezi hiyo nane lazima amepata mwanamke amerudi kukuacha, siku zote fimbo ya mbali haiui nyoka.
Lakini mbona maneno yake yamenichanganya sana.
Maneno gani?
Eti sababu ya wewe kuanguka.
Amekwambiaje?
Aniambie nini zaidi ya kuniacha njia panda, mara sijui sababu ya talaka wewe ndiye unajua mara sijui kunipa talaka ni salama ya maisha yake, yaani hata sielewi, nilisema huku moyo ukiniuma.
Sasa yote hayo kakuweka wazi?
Wapi mama!
Yule mwanaume mbaya sana, amekuacha na mafumbo ili atugombanishe. Lakini yule mwanaume amepata mwanamke mwingine. Kwa jinsi mlivyoagana mpaka unampa fedha za kuanzia maisha, hakutakiwa kukupa talaka mpaka angekueleza kosa lako, maneno ya mama yalinigusa.
Hapo ndipo ninapozidi kuumia moyoni mama yangu.
Mwaija wewe bado msichana mdogo, nina imani ukitaka kuolewa huchukui hata wiki utaolewa. Kwa hivyo asikuumize akili.
Sawa nitaolewa, lakini kwa nini nimeachwa? hilo ndilo lililoniumiza.
Mwanangu siku zote ukiona penzi limefika mwisho basi ujue ndiyo mwanzo wa penzi jipya.
Mama yangu alifanya kazi ya ziada kunipoza moyo, kwa upande mwingine niliona kama kulikuwa na kosa alitakiwa anieleze hata kama la kusingiziwa kwa vile mimi nilikuwa mkewe.
Kitendo cha kunipa talaka na kuniachia maswali yasiyo na majibu kilinifanya nikubaliane na maneno ya mama.
Wazo la haraka lilikuwa kwenda nyumbani kwa wazazi wa mume wangu kuulizia sababu ya kupewa talaka huenda aliwaeleza.
***
Siku tatu zote nilikuwa kwenye mawazo mazito juu ya kupewa talaka bila kosa na kusababisha nipoteze hamu ya kula. Moyoni niliona heri mume wangu angepotea hata miaka kumi nikajua bado nipo naye kuliko kitendo kile cha kunipa talaka bila sababu.
Nilijikuta nikianza kuvikaribisha vidonda vya tumbo, kutokana na kuwa na mawazo pia kukaa muda mrefu bila kula hata nilipojilazimisha kilinishinda kutokana kukiona hakina ladha.
Niliamua kwenda ukweni kuuliza sababu ya kupewa talaka labda wao aliwaeleza. Wakwe zangu walikuwa wakikaa Buguruni kwa Mnyamani.
Nilipofika nilishtuka kukuta nyumba yao ya udongo wameanza kunyanyua upande kwa kujenga kwa tofali za udongo ulaya. Nilijua mambo ya mume wangu na kuonesha alipokwenda mambo yamemnyookea. Niliwakuta wazazi wake wote wapo nje, waliponiona walinipokea kama zamani, hakukuwa na tofauti yoyote wakati nikiwa na mtoto wao na nilipoachika. Mapokezi ya wakwe zangu yalinishtua na kuamini huenda talaka niliyopewa hawana taarifa nayo.
Baada ya kukaribishwa na kusalimiana na wazazi wa mtalaka wangu, baba mkwe aliniaga alikuwa akitoka kwenda zake Buguruni Chama. Kwa vile nilikuwa nimewafuata wao wote nilimuomba asiondoke ili nizungumze nao kwa pamoja.
Samahani mama mi nafika Buguruni Chama, baba mkwe aliniaga.
Baba samahani nilikuwa na mazungumzo na ninyi wote wazazi wangu.
Hakuna tatizo mama.
Baba mkwe alirudi kunisikiliza, baada ya kukaa alinisubiri mimi nieleze kilichonipeleka pale. Kwanza nilianza kwa kuwaomba msamaha.
Kwanza samahani wazazi wangu.
Bila samahani mama, alijibu mama mkwe.
Nina imani mnajua kilichotokea karibuni kuhusu mimi na mwenzangu?
Ndiyo.
Kauli yao ilinishtua kidogo kuonesha wanajua kila kitu lakini waliamua kukaa kimya. Ile ilinifanya niamini nitaweza kujua sababu ya mimi kupewa talaka.
Wazazi wangu mpaka sasa nipo njia panda, ni kweli nimeachika talaka moja. Lakini mpaka sasa sijajua sababu ya kuachwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hujui sababu ya kuachwa! Unamaanisha nini kwani ilikuwaje?
Amekuja na kunipa talaka bila maelezo.
Mmh! Sasa mwanangu amekupa talaka bila maelezo inakuja kweli, au kuna kosa ulilolifanya mwenzio kagundua?
Wazazi wangu, Mungu ndiye anajua lakini toka mume wangu ameondoka nimekuwa mtulivu na mvumilivu kumsubiri yeye huku nikimuombea kwa Mungu afanikiwe.
Lakini amerudi mume wangu kapendeza, furaha yangu ya kumuona ikageuka shubiri.
Wee mwana, unataka kutuambia mume wako amefika tu na kukupa talaka? mama mkwe alionesha kushtuka.
Ndiyo wazazi wangu.
Kakwambia tatizo nini?
Wazazi wangu kila nikimuuliza aniambie tatizo la kunipa talaka haniambii zaidi ya kusema nimuulize mama yangu ndiye anajua, mama naye kumuuliza kanijia juu kuwa mume wangu hana adabu, talaka atoe yeye sababu atoe mama.
Mmh! Makubwa, ina maana hakuna tatizo lolote kabla ya kuondoka mumeo?
Hakuna wazazi wangu.
Amekuja na kukupa talaka bila kosa?
Ndiyo mama, nimemuuliza sababu ya kunipa talaka haniambii. Hata kama alikuwa na nia ya kuniacha angeniambia nikajua moja. Inauma mtu kumsubiri siku zote hizo halafu faida ya uvumilivu wangu kwake ni talaka? Inauma...Inauma sana, nilianza kulia kwani moyo ulikuwa ukiniuma.
Basi mwanangu nyamaza kulia.
Mama inauma, jinsi tulivyopendana na Beka si wa kunipa talaka kama ameniokota baa.
Kwa hiyo hakukueleza sababu? walirudia swali la awali.
Ndiyo wazazi wangu ndiyo maana nimekuja hapa mnieleze sababu ya mimi kupewa talaka ili nijue kosa langu huenda kweli nilimkosea mwenzangu bila kujua.
Eti mama Beka mwanao alikueleza sababu ya kumpa talaka mkewe? baba mkwe alimgeukia mkewe.
Hajaniambia.
Wazazi wangu nakuombeni nipo chini ya miguu yenu niambieni sababu ya Beka kunipa talaka.
Uongo mbaya mi sijui, labda mama yako, baba mkwe alimtupia mpira mkewe.
Mume wangu, Beka aliporudi alitueleza amempa talaka mkewe. Nina imani wote tulishtuka kwa sifa alizokuwa akikumwagia kabla ya kuondoka na aliporudi siku ile hata bila kupumzika alikuja kwako.
Aliporudi alitushtua kwa kutuambia kuwa amekupa talaka. Tuliingia wasiwasi labda amekuja huko kwa vile ni muda mrefu uko peke yako basi kakukuta na mwanaume.
Hapana wazazi wangu, amekuja ametukuta tupo sebuleni, alipofika alitusalimia na kuniomba tuzungumze, tukaingia chumbani kwetu, amesema ananipenda sana na hata pata mwanamke kama mimi lakini hana jinsi ameamua kunipa talaka.
Nimembembeleza anieleze sababu ya kuniacha amekataa zaidi ya kuniambia kila kitu mama anajua. Basi niliamini wazazi wangu lazima aliwaambia.
Kama mama yake hakumwambia sijui nani anajua sababu ya talaka, tulitegemea mzazi wako kuja lakini amekaa kimya basi tumejua sababu mnaijua wenyewe.
Mama haki ya Mungu sijui lolote, niliamini ninyi mnajua.
Mwanetu tumembembeleza, lakini amesema wewe unajua.
Mimi? nilisema nikijishika kifuani kushangaa kauli ya mume wangu.
Ndiyo.
Jamani Beka mbona ananionea, mi nijue sababu halafu nije niulize?
Ndiyo maana hata sisi tunashangaa wewe kusema hujui.
Wazazi wangu kama Beka kapata mwanamke mwingine angeniambia kuliko kunikosanisha na mama yangu. Japo nampenda lakini suala la kuachwa siwezi kulipinga japokuwa linaniuma sana.
Mmh! Sasa huu mtihani, mama mkwe alisema.
Kwani mama, Beka yupo wapi?
Beka aliondoka siku ya pili baada ya kutoka kwenu bila kutupa jibu lolote.
Amekwenda wapi?
Kwa kweli, kama yeye mwenyewe hakukuambia sisi itakuwa vigumu.
Sawa wazazi wangu, kama mmekataa kuniambia alipokwenda Beka nina imani hata sababu za kuniacha mnazijua.
Hilo hatujui.
Nashukuru wazazi wangu kwa kunificha, lakini siwezi kuwalaumu, ila siku zote nitamlaumu Beka kwa kunitendea unyama.
Baada ya kusema vile nilinyanyuka na kuondoka bila kuaga. Baada ya kutoka nilisikia nyuma wakiniita lakini sikugeuka baada ya kuona napoteza muda wangu bure.
Nilikwenda kwa mwendo wa haraka hadi Buguruni nilipochukua daladala mpaka Mikoroshini kisha nilielekea nyumbani. Nilipofika niliingia chumbani kwangu na kujifungia, nikajilaza kitandani.
Nilijikuta moyo ukiniuma kwa kuonewa bila kosa, nilijiuliza kosa langu nini, kwa nini nimekosa ushirikiano na kuwa peke yangu kama nimerogwa. Machozi yalizidi kunitoka kama maji.
Sauti nisiyoielewa niliisikia ikisema: Machozi siyo dawa ya maumivu wala ufumbuzi wa matatizo. Dawa ni kupambana, acha kulia futa machozi songa mbele.
Nilishtuka na kujikuta nipo peke yangu chumbani, niligundua nipo kwenye mawazo makali yaliyonifanya nizisikie sauti za watu. Lakini niliikumbuka kauli ile tulielezwa na mwana harakati mmoja aliyekuja shule wakati nipo kidato cha nne na kutupa moyo wasichana tunapotokewa na matatizo ya kukatisha tamaa. Nilinyamaza na kufuta machozi na kujikuta nikirudia mlolongo mzima wa maisha yangu mpaka kupewa talaka na yote niliyokutanana nayo baada ya kupewa talaka.
Nilijikuta nikikubaliana na kauli ya mama kuwa Beka alipokwenda alipata mwanamke na aliporudi aliamua kunipa talaka akisingizia mama anajua ili kunikosanisha na mama yangu.
Nilinyanyuka na kwenda kuoga huku nikiapiza kusahau yote yaliyopita. Baada ya kuoga nilitoka hadi nje nilipowakuta dada zangu wakiendelea kunywa pombe.
Nilisimama kwa muda nikiwaangalia jinsi walivyokuwa wakiyafurahia maisha. Hawakuwa na wanaume lakini kila siku mioyo yao ilijaa furaha tofauti na mimi niliyekuwa nimeolewa kila kukicha maumivu yaliutawala moyo wangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilijikuta nikijilaumu kuchelewa kutoa uamuzi wa kutafuta mwanaume kwa mtu aliyenitenda. Moyoni niliamini unaweza kuishi bila mwanaume na maisha yako yakasonga. Nilikumbuka maisha ya mama toka baba afariki ambaye sikubahatika kumuona. Aliweza kuishi maisha ya furaha japokuwa niliamini kwa umri wake baada ya kifo cha baba alikuwa na uwezo wa kuolewa.
Lakini mama hakutaka kuolewa alikuwa akiishi maisha yake mwenyewe. Japokuwa mwanzo tabia yake ya kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja na wote wakiwa waume za watu sikuipenda.
Baada ya maumivu niliyopewa na Beka nilikubaliana na mama anaona hakukuwa na faida ya kuishi maisha ya ndoa au kuwa muaminifu kwa mwanaume asiyekuwa muaminifu.
Baada ya kuwaza sana huku nikiendelea kuwatazama dada zangu waliokuwa wakifurahia maisha.
Waliponiona waliniita ili nikaungane nao kupunguza mawazo.
Njoo mdogo wangu, kunywa kidogo upunguze mawazo.
Nilijisogeza karibu na kupewa glasi iliyokuwa na bia nusu. Niliichukua na kuipeleka mdomoni na kuinywa kama maji. Ilikuwa chungu kiasi nilifumba macho na kuipitisha kooni kwa shida. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilianza kunywa bia kwani niliamini humpunguzia mtu mawazo. Nilijikuta nikipingana na mawazo yangu ya awali kuwa pombe ni uhuni.
Dada zangu walifurahia kitendo changu cha kujaribu bia. Waliniongezea kwenye glasi kila nilipomaliza, japokuwa sikuwahi kunywa lakini haikuwa mbaya sana.
Nilijilazimisha kuinywa mpaka nikamaliza bia moja. Dada aliniongezea nyingine ambayo niliendelea kunywa bila kujua kipi kitafuata.
Nilijikuta nikihisi kizunguzungu, dada aliendelea kunilazimisha nimalize bia nyingine, kitu kilichonifanya nilewe na kulala pale nilipokuwa nimekaa.
Nilishtuka siku ya pili na kujikuta nimelala kitandani kwangu nikiwa nimejisaidia haja ndogo bila kujua huku nikisikia njaa kali. Nilinyanyuka na kwenda kuoga na kufanya usafi kisha nikaanza kutafuta supu.
***
Nilijikuta nikijiingiza katika ulevi ili kupunguza mawazo, pamoja na kufanya yote bado sikuwa tayari kuutoa mwili wangu kama asusa kwa wanaume kwa kuhofia maradhi.
Japokuwa dada zangu walinikuwadia kwa wanaume ikiwa pamoja na kuniletea fedha walizopewa, lakini sikuwa tayari kujiingiza kwenye ukahaba.
Niliamua kujiingiza kwenye ulevi kama mfariji wangu kwa kipindi kile kilichokuwa kigumu sana kwangu, kwa vile mpaka muda ule bado sikujua sababu ya kupewa talaka ambayo ilionekana kuwa na siri nzito ambayo sikuwa nikiijua.
Lakini kulikuwa na tatizo lililokuwa likinisumbua mpaka mama akanikataza kunywa pombe kwa kuwa ilikuwa ikinishinda.
Kila nilipokuwa nikinywa pombe na kuanza kulewa, niliangua kilio kumlilia mume wangu.
Kwa wenzangu ilikuwa ni karaha na kuonekana kama nilikuwa nikiwapigia makelele wakati awali tulilizungumza na kukubaliana. Nilijitahidi kumsahau mume wangu mtu ambaye nilimzoea na kuamini kifo ndicho kingetutenganisha, lakini talaka ilikuwa pigo na kovu kubwa maishani mwangu.
Kila nilipolia na kukemewa niliwaahidi dada zangu kuwa sitalia tena, pia niliahidi nitaachana na mawazo ya mtalaka wangu aliyeniacha bila sababu za kueleweka. Lakini kila nilipokunywa pombe na kulewa yote yalijirudia na kuanza kulia huku nikitawaliwa na mawazo mabaya ya kunitaka ninywe sumu ili niepukane na aibu ya kuachwa.
Wakati kwangu likiwa pigo mujarabu moyoni mwangu, dada zangu waliotangulia kuachika hawakuteteleka waliendelea na maisha kwa kutumia miili yao kama mitaji ya kuwaweka mjini bila kuhofia hali ya hatari.
Niliamini njia ya kumuondoa mume wangu akilini ni kuwa bize kuliko kuendelea kukaa nyumbani na kujilazimisha kunywa pombe ambayo kila nilipolewa nilimlilia mtalaka wangu.
Niliamini ubize pekee ndiyo ungeweza kunisaidia kuchosha mwili na nikirudi nyumbani mchovu, nitafikia kuoga kula na kulala kuliko kushinda nyumbani kusubiri wanaume.
Mwanaume mmoja wa dada mkubwa alikuwa anafanya kazi serikalini, niliamini anaweza kunisaidia kupata kazi. Nilimweleza dada amweleze anitafutie kazi popote.
Baada ya kumweleza dada amwambie alinihakikishia kunipa jibu ndani ya wiki.
****
Baada ya siku nne dada aliniletea taarifa kuwa kazi imepatikana kwenye super market iliyopo katikati ya jiji. Kwa kweli nilifurahi sana kupata kazi nikiamini kuwa bize kutanifanya niwe mbali na vishawishi vibaya.
Nilielezwa Jumatatu nilitakiwa nianze kazi, bwana wa dada alisema atanipitia asubuhi ya siku hiyo, hivyo nilitakiwa niamke mapema kujiandaa kabla hajafika.
Kwa vile taarifa nilizipata siku tatu kabla, nilijiandaa kwa kutafuta nguo itakayoendana na maeneo husika, japokuwa siku zote sikupenda kuvaa nguo fupi kwani zilininyima uhuru na kujiona nakaa uchi lakini siku hiyo sikuwa na budi kuivaa.
Jumatatu niliamka alfajiri na kujiandaa kwa ajili ya kuelekea kazini. Saa moja kasoro bwana wa dada Sauda alifika na gari lake na kunichukua kunipeleka kwenye hiyo super market.
Tulikwenda mpaka katikati ya jiji. Tulipofika alipiga simu na nilimsikia akizungumza.
Haloo..eeh..nimefika.... haya nakuja.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ILIPOISHIA;
Kwa vile taarifa niliipata siku tatu kabla, nilijiandaa kwa kutafuta nguo itakayoendana na maeneo yale, japokuwa siku zote sikupenda kuvaa nguo fupi kwani zilininyima uhuru na kujiona nakuwa mtupu.
Siku ya Jumatatu niliamka alfajiri nikajiandaa na kuelekea kwenye kazi hiyo. Saa moja kasoro bwana wa dada Sauda alifika na gari lake na kunichukua kunipeleka kwenye hiyo super market.
Tulikwenda mpaka kwenye super market iliyokuwa katikati ya jiji. Tulipofika alipiga simu na kumsikia akizungumza.
Haloo...eeh...nimefika...haya nakuja.
Baada ya kukata simu aliniambia.
Twende.
Sikumjibu nilimfuata, tuliingia naye ndani na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye ofisi moja iliyokuwa ya vioo vitupu na kuingia ndani.
Ndani tulimkuta kaka mmoja mtanashati, baada ya kuingia nilikaribishwa kwenye kiti. Nilikaa na kutulia huku bwana wa dada akisalimiana na yule kaka kisha alisema:
Sasa bibie mi acha niwahi, kila kitu atamalizia huyu mwenyeji wako.
Hakuna tatizo.
Bwana wa dada alitoka na kuniacha na yule kaka ambaye aliniomba radhi na kutoka. Baada ya muda alirudi na fomu ambazo zilikuwa za kuajiriwa. Baada ya kukaa aliniuliza maswali mawili matatu kisha alinipeleka sehemu, nikapigwa picha.
Baada ya zoezi lile nilirudi ofisini kwa yule kaka aliyekuwa meneja wa duka lile kubwa sana. Alinyanyua simu na kuagiza chai, baada ya muda ililetwa na kunywa kisha alimwita dada mmoja.
Alipofika alimweleza:
Suzy huyu ni mfanyakazi mpya, naomba umpe ushirikiano wa hali ya juu.
Hakuna tatizo bosi.
Kampatie sare na aanze kazi.
Hakuna tatizo, atakuwa sehemu gani bosi?
Mweke kwa keshia.
Hakuna tatizo, kitambulisho?
Muone Sam nina imani kitakuwa tayari.
Haya shem, nina imani Suzy atakusaidia, kazi njema.
Asante.
Nilitoka na Suzy mpaka kwenye chumba kimoja kilichokuwa na sare na kunichagulia inayonitosha kisha tuliongozana mpaka kwenye chumba kingine na kukuta kitambulisho changu kipo tayari.
Nilipewa na kukivaa kisha nilipelekwa sehemu na kuelekezwa kama mtu akishalipia bidhaa aliyonunua namuwekea kwenye mfuko na kuwakaribisha tena.
Haikuwa kazi kubwa sana lakini nilichoka sana kwa vile sikuwa nimezoea kusimama muda mrefu. Jioni bwana wa dada alinipitia. Kabla ya kuondoka da Suzy niliyekuwa nimemzoea kwa haraka, alinieleza muda wa kuingia kazini na umuhimu wa kuwahi.
Nilimshukuru na kumuahidi kuwahi siku ya pili. Niliingia ndani ya gari la shemeji na kurudishwa nyumbani. Njiani shemeji aliniuliza mambo mengi kuhusiana na kazi.
Sikusita kumshukuru kwa msaada wake ambao ulikuwa muhimu kuliko kitu chochote kwa wakati ule.
Tokea siku ile nilianza kazi ya kuuza kwenye super makert na jioni shemeji alinipitia kama kawaida. Siku zote nilirudi nimechoka baada ya kuoga na kula muda mwingi niliutumia kitandani kwangu kupumzika.
Taratibu nilianza kumsahau mtalaka wangu Beka na kuamini kuna maisha mengine baada yake kwa kujua kila linalomtokea mwanadamu lina makusudio yake.
Kazi niliizoea na kuwa maarufu kutokana na ucheshi wangu. Lakini nilikuwa na wakati mgumu kazini kutokana na wanaume wengi wakware kunitaka kimapenzi.
Pamoja na ahadi nyingi nilizopewa kama nitakubali kujitoa kwao kimapenzi, sikuwa tayari kujiingiza katika dunia iliyoniumiza na kufikia hatua ya kuwachukia wanaume, japokuwa sikutakiwa kumhukumu mtu kwa kosa la mwingine.
Moyoni nilipanga baada ya miaka miwili ndipo niufungue moyo wangu. Najua unaweza kushangaa uamuzi wangu lakini kila aliyekumbwa na mkasa wa mapenzi hawezi kunishangaa kwa vile mapenzi yanaumiza sana hasa uachwe na mtu unayempenda tena bila kujua kosa lako.
Siku zilikatika huku nikizidi kuifurahia kazi yangu na maisha yangu mapya ya kuishi kama mdudu wa sikio bila kuwa na mshirika. Mwanzo niliamini maisha yale yangekuwa magumu ya kuishi bila mwanaume, lakini kila kitu ukiamua unaweza nami niliweza kabisa.
Nakumbuka siku moja wakati natoka kazini nikiwa ndani ya gari la shemeji bwana wa dada. Baada ya kutoka kazini tulikwenda mwendo wa dakika tano, alinigeukia na kuniuliza:
Mwaija una mpango gani?
Kuhusu nini shemeji?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Si nilisikia umeachana na mumeo?
Ndiyo.
Sasa una mpango gani baada ya kuachana naye?
Mmh! Bado sina mpango wowote nimeamua kupumzika kwanza.
Mwaija wewe bado msichana mdogo kwa nini ujifuje?
Sijifuji bali nimeamua kupumzika, kilichonikuta Mungu anajua.
Mwaija siyo Mungu anajua, mwanaume uliyekuwa naye hakuwa sahihi kwako.
Ukisema hivyo sikubaliani na wewe, Beka namjua vizuri kuliko mtu yeyote, kuna kitu tu ambacho kimesababisha aniache.
Kitu gani?
Wee shemu, tuyaache tu yalishapita hayo, kwa kweli sikupenda kuzikumbuka habari za mtalaka wangu.
Kama anatokea leo na kutaka kukurudia utakubali?
Naweza kukubali kama atanieleza sababu ya kuniacha na mimi kuikubali.
Sasa Mwaija tuachane na hayo kuna kitu nataka kukuambia japokuwa ninacho muda mrefu, lakini naamini leo ni siku muafaka.
Kitu gani hicho shemeji yangu?
Kuhusu wewe.
Mimi! Nimefanya nini?
Siyo kwamba umefanya kitu ila kuna jambo nimejifunza kwako kwa muda mrefu.
Kipi?
Mwaija unatabia tofauti na dada zako.
Kivipi?
Unajiheshimu pia unajifahamu.
Nashukuru kwa kulifahamu hilo.
Baada ya kuligundua hilo nilikuwa na ombi moja ambalo nina imani litakuwa na faida kubwa kwako.
Ombi gani?
Nataka nitabadili maisha yako uweze kumiliki nyumba na gari.
Kivipi?
Nafikiri unajue mimi na dada yako tukoje?
Ndiyo najua.
Basi nimeishamfumania na wanaume zaidi ya watatu.
Shemeji alitulia kuzungumza akasimamisha gari kuwaruhusu watu waliokuwa wakivuka barabara eneo la Changombe Maduka Mawili wavuke. Baada ya watu kuvuka alibadili gea na kukanyaga mafuta kisha alinigeukia na kusema:
Unajua nilikuwa nina mipango mikubwa na dada yako.
Mipango gani?
Nimjengee nyumba na kumnunulia gari.
Tatizo nini?
Hataki nimuoe zaidi ya kupenda maisha anayoishi, wewe ni mdogo lakini una akili sana.
Shem, si nasikia umeoa?
Ndiyo, lakini angekuwa nyumba yangu ndogo.
Mmhu, na mimi unataka kuyabadilisha maisha yangu kivipi?
Mwaija nataka uwe mpenzi wangu, nakuhakikishia kwa jina la Mungu kukufanyia mambo yote niliyokuahidi hata kabla ya kukutana nawe kimwili ili uniamini.
Na dada?
Mwaija, dada yako hajitambui pia hajui hatima ya maisha yake na kusahau uzuri una mwisho.
Lakini kumbuka kufahamiana na wewe ni kupitia kwa dada huyohuyo ambaye amekuwa waluwalu.
Mwaija nina malengo mazuri na wewe, ukikubali nitahakikisha nakuachisha hii kazi na kukufungulia mini super market utakayoimiliki mwenyewe.
Yote umesema mazuri ambayo kila mwanamke anayatafuta kuyapata kwa mpenzi wake. Lakini tatizo siwezi kushea mwanaume na dada yangu, ni matusi kwetu.
Mwaija, dada yako si mke wangu ni mpenzi wangu, hata nikimuacha bado ana wanaume wengine. Naomba usiipoteze nafasi hii.
Samahani kwa hili siwezi, pamoja na ahadi nono sikuwa tayari kujidhalilisha.
Inawezekana nimekushtua ila nakuomba nenda nyumbani jifikirie taratibu kisha utapata jibu. Ila naomba usinifikirie vibaya kwa vile nimekutafutia kazi ndiyo sababu ya kukutaka.
Walaa, ila tu siwezi kushea penzi na dada yangu.
Najua utasema hivyo, lakini kama utamwambia mtu yeyote nilichokuahidi atakushangaa kama utakataa.
Ni kweli atanishangaa, lakini heshima ya mtu haibebwi na mtu mwingine bali yeye mwenyewe.
Najua Mwaija, ila naomba nilichokuambia kipe muda akilini mwako ili uweze kunipa jibu ambalo najua litakuwa zuri kwako na kwangu.
Sidhani kama nitakuwa na jibu tofauti na nililokueleza.
Najua una msimamo, naomba utafute mawazo hata kwa rafiki zako wa karibu nina imani utabadilika.
Sawa, lakini siamini kama kuna mabadiliko zaidi ya hili nililokueleza. Japokuwa sikuwa tayari kuufungua moyo wangu kwa sasa, lakini kwa ukarimu wako na kuonesha kunijali kama ungekuwa huna uhusiano na dada ningeweza kukupa nafasi ya kukufikiria.
Sawa Mwaija, bado nasisitiza sitakuwa na wewe kwa ajili ya kukuumiza. Najua umeumizwa hivyo nitajitahidi kuwa mfariji wako.
Halafu kuna kitu kingine ambacho nakiogopa, kama usingekuwa na uhusiano na dada bado suala la kutembea na mume wa mtu linanitisha.
Mwaija, mke wangu hana kizazi nami nina pesa leo hii nikifariki nani atakuwa mrithi wangu? Nilitaka kuzaa na dada yako lakini alikataa hawezi kuzaa.
Hebu fikiria nitabadili wanawake wangapi wakati kipindi hiki hali ni mbaya kama usipokuwa makini?
Ni kweli, lakini umenipa mtihani mzito.
Wala si mzito, upe muda moyo wako kwa vile kitu nitakachokifanya kina manufaa makubwa sana kwako. Mwaija fedha sina sana ila nina uhakika wa kukufanya uishi maisha ya ndotoni.
Mmh! Bado mtihani kwangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwaija kama hilo huwezi naomba unisaidie kitu kimoja.
Kitu gani?
Basi nizalie mtoto mmoja akiwa wa kiume nitakupa milioni 20 akiwa wa kike milioni 10.
Tatizo si kukuzalia bali kushea penzi na dada yangu.
Mwaija naomba katika hayo mawili moja lifanyie kazi.
Wakati huo tulikuwa tumefika nyumbani, kabla ya kuteremka bwana wa dada alinipa bahasha.
Ya nini?
Kaifungulie ndani.
Sikutaka kuhoji, nilipokea. Kabla ya kuondoka alinishika mkono mmoja kwenye bega na kuniangalia kwa muda mpaka machozi yakamtoka.
Shemu unalilia nini? nilimuuliza.
Basi, naomba tulilozungumza usimwambie mtu.
Hata siku moja sina tabia hiyo.
Nimefurahi kusikia hivyo, naomba uyafanyie yote kazi niliyokueleza.
Sawa.
Tuliagana na mimi kuteremka kwenye gari na kuelekea ndani. Bwana wa dada naye alipaki gari pembeni na kuingia ndani kuonana na dada. Mimi nilikwenda moja kwa moja kuoga ili nipate muda wa kupumzika.
Baada ya kuoga na kula nilijilaza kitandani na kuifungua bahasha ambayo ilikuwa na fedha mpya, nilipohesabu nilikuta laki saba taslimu. Niliziweka kwenye kabati langu na kurudi kitandani kujilaza. Nilijikuta nawaza vitu vingi kuhusiana na maneno ya bwana wa dada. Machoni kwake alionesha hafanyi mzaha lakini bado sikutakiwa kumkubalia kwa vile ingeonesha jinsi gani familia yetu isivyojiheshimu.
Nilikuwa na wazo la kulitupilia mbali, lakini niliamini mama anaweza kunisaidia hata kuweza kulimaliza bila kumuudhi bwana ya dada pia kutogombanish a na dada yangu japokuwa niliamini kabisa katika tabia yake hata kama yule bwana angeamua kuachana naye hakuna chochote kingemgusa moyoni mwake.
Wazo lile sikutaka kuliacha lipite vilevile japokuwa moyoni nilikuwa na uamuzi wangu ambao niliamini utabakia kama ulivyo.
Wazo la kwenda kumueleza mama nilisitisha kidogo na kupanga kwanza kwenda kumwambia da Suzy ili nijue atanipa mawazo gani. Da Suzy toka nianze kazi pale alikuwa mtu wangu wa karibu ambaye tulifikia hatua kila mtu kumweleza mwenzake mambo ya ndani, japokuwa kuna baadhi ya tabia za familia yangu nilimficha.
Siku ya pili nilipokwenda kazini wakati wa chakula cha mchana nilimweleza da Suzy kuwa nina mazungumzo naye baada ya kazi, naye alinieleza atanisikiliza.
Baada ya muda wa kazi tulikwenda kwenye mgahawa uliokuwa karibu na kazini kwetu.
Kwa vile nilijua mazungumzo yetu yatachukua muda kidogo, nilimpigia simu bwana wa dada kuwa asijekunichukua nitachelewa kidogo. Lakini mwenzangu alinielewa tofauti na kujua ninataka kumkimbia kutokana na kauli yake ya kunitaka kimapenzi.
Mwaija, usifike huko nililofikisha kwako ni ombi tu si lazima. Ulitakiwa kulifanyia kazi na kuliangalia lina uzito gani kama halina mashiko ungeachana nalo na si kukimbiana.
Hapana shemu, kuna kitu kitanichelewesha kwa leo, lakini kesho utanichukua kama kawaida, nilijaribu kumtoa wasiwasi.
Mwaija mi nipo tayari kukusubiri kwa muda wowote, lakini leo nikurudishe nyumbani kama kawaida. Mmh! Shemu bado alikuwa kinganganizi.
Hapana shemu leo naomba nisikusumbue.
Mwaija najua umekasirika, bado nasisitiza ni ombi wala si lazima. Wewe ni mtu mzima mwenye kujua zuri na baya kama ulishawahi kuolewa hakuna kigeni tena kwako.
Shemu umeenda mbali sana, kama kungekuwa na mabadiliko yoyote ningekueleza. Unavyonifahamu ndivyo nilivyo.
Basi naomba ukubali nikusubiri, shemu alikuwa kinganganizi. Ilibidi nimkubalie anipitie ili niondoe wasiwasi wake.
Basi hakuna tatizo nikimaliza mambo yangu nitakutaarifu.
Hapo sawa, kauli ya bwana wa dada ilinishtua na kujiuliza nini mwisho wa yote kama sitakubaliana na yeye kitu ambacho kilikuwa kwenye mawazo yangu.
Baada ya kukubaliana na bwana wa dada, nilimgeukia da Suzy ambaye alionekana kunishangaa muda wote niliokuwa nikibishana.
Vipi Mwaija? aliniuliza baada ya kukata simu.
Ndiyo yaliyonifanya niombe ushauri wako.
Yepi hayo?
Ndiyo maana tupo hapa.
Mmh! Haya.
Vinywaji tulivyoagiza vililetwa wote tuliagiza juisi ya embe mchanganyiko na parachichi. Kila mtu alichukua glasi yake na kunywa kidogo kisha da Suzy alikaa mkao wa kunisikiliza.
Baada ya kutulia kwa muda nilimwita da Suzy.
Da Suzy.
Abee mdogo wangu, aliniitikia huku akinitazama usoni.
Kuna jambo nimekutana nalo jana limenipa wakati mgumu. Japokuwa nilikuwa na uamuzi wangu. Lakini sikutaka kuamua peke yangu kwa vile naliona zito.
Jambo gani mdogo wangu?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliamua kumpa historia fupi ya maisha yetu na nilichoelezwa na bwana wa dada jana yake. Da Suzy alionesha kunishangaa, baada ya kunitazama aliniuliza.
Mwaija unataka kuniambia mzee Sambi si mpenzi wako?
Ni shemeji yangu bwana wa dada yangu.
Basi sote tunajua yule ni mtu wako.
Walaa, ni shemeji yangu.
Basi Emma hajui lolote, angejua wewe si mtu wa mzee Sambi lazima angekutongoza. Yule mwanaume mchafu sana, pale ofisini ameisha tembea na robo tatu ya wafanyakazi.
Lakini wewe naona anakuheshimu sana.
Kauli yangu ilimfanya da Suzy kucheka kitu kilichonifanya nishtuke.
Dada mbona unacheka?
Mwaija we mtu wangu wa karibu siwezi kukuficha kitu. Emma alipokuja kazini mimi ndiye nilikuwa mtu wake wa kwanza.
Nilijikuta nikishtuka lakini nilificha mshtuko wangu. Da Suzy aliendelea kunipasha nisivyovijua.
Kwa kweli nilimpenda toka siku ya kwanza kuanza kazi. Kwa vile nilitaka kumvuta karibu yangu, nilitumia muda mwingi kumfundisha kazi.
Lakini baada ya muda alipanda cheo kwa vile alikuja na elimu yake. Hapo ndipo aligeuka mchafu sana kwa kutembea ovyo na kila msichana mzuri anayekuja kufanya kazi.
Si kazini hata huko anapokaa simu yake kila siku nilikuwa nakamata ujumbe wa mapenzi wa wanawake tofauti.
Nilijaribu kumshauri na nia yetu ilikuwa tuoane lakini hakuonesha kubadilika, niliona kuchangia mwanaume ni kujidhalilisha, nikaamua kuachana naye.
Da Suzy alijikuta akinipa historia ya uhusiano wake na bosi wetu Mr Emma.
Mmh! Pole sana, sasa kazi mlifanyaje?
Kwa vile maisha nayajua nilijielekeza kwenye kazi na kumpa uhuru.
Lakini wewe si umeolewa?
Ndiyo, tena na rafiki wa karibu wa Emma.
Mmh! Ilikuwaje?
Huwezi kuamini yule mkaka alikuwa akinipenda muda mrefu lakini nilimtolea nje. Baada ya kutendwa na Emma nilimfungulia milango ili kumkomesha Emma.
Mmh! Baada ya kuoana nini kilifuata?
Hakuna kitu zaidi ya kuheshimiana tu.
Ninavyowajua wanaume lazima kuna siku huwa anataka kukumbushia, inakuwaje akiomba?
Huwa namueleza tuheshimiane, mwanzo alikuwa mbishi lakini sasa amenielewa.
Mmh! Wanaume ukiwachekea wanaweza kukuharibia ndoa bure,
Umeona eeh, mdogo wangu.
Lakini naona kama umri ulikuwa umemzidi?
Ni kweli, Emma nimemzidi miaka mitano, lakini nilimpenda sana huwa sipendi kukumbuka penzi langu lililo peperushwa kama vumbi kwenye upepo mkali.
Mmh! Pole sana dada.
Asante.
Da Suzy alitulia kwa muda akiwa ameinama kuonesha jinsi gani mapenzi yalivyomuuliza kumpenda mtu asiye muaminifu. Baada ya muda alinyanyua uso wake na kuchukua glasi ya juisi na kunywa kidogo na kunitaza kisha alisema:
Mdogo wangu una mtihani mzito ambao ni sawa na kuitumia turufu moja iliyokuwa mkononi, ikutoe mrithi au ikutoe kapa.
Una maana gani da Suzy?
Mpaka mzee anakueleza jambo kama hilo ujue basi kakufuatilia muda mrefu. Malengo yake ni makubwa sana kwako.
Lakini kumbuka tayari ameshatembea na dada yangu.
Ni kweli lakini kwa tabia ya dada yako ya kutokuwa na bwana mmoja. Hiyo ni nafasi ambayo naamini unaweza usiipate mpaka unakufa.
Mtu akujengee nyumba na kukununulia gari kwa ajili ya mapenzi? Ni wachache katika dunia ya leo ambayo wanaume wengi ni matapeli.
Kama huwezi kukubali kuwa nyumba ndogo basi mbebee ujauzito ili upate hayo mamilioni. Naamini mzee Sambi alivyo na hamu ya mtoto lazima ahadi zote tatu atatimiza ukimzalia mtoto.
Mmh! Dada unanipa mtihani.
Hakuna mtihani, yupo wapi Beka uliyempenda kuliko kitu chochote chini ya jua? Mdogo wangu, Waswahili wanasema bahati haiji mara mbili na mchuzi wa mbwa unywe ungali wamoto, ukipoa haunyweki.
Kwa hiyo unanishauri nimkubalie?
Mwaija mkubalie, nafasi kama hiyo mdogo wangu wenzako tunaiendea kwa waganga wewe inakujia miguuni unataka kuipiga teke?
Lakini naogopa kugombana na dada.
Fanyeni hata penzi la siri nina imani litakusaidia katika maisha yako.
Mmh! Nitajaribu kwa vile umeivunja ngome ya moyo wangu sina budi kukubaliana na wewe, nilijikuta nikilegeza msimamo.
Tena nakuomba mdogo wangu usiipoteze bahati hii. Hebu angalia jinsi Mungu alivyosikia kilio chako baada ya kukimbiwa na Beka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tena amekwambia humpi mwili wako mpaka akamilishe alichokuahidi, Mungu akupe nini? Waache dada zako watakuja kuuanika wakati jua limekuchwa na kuutwanga mbichi.
Nilikuwa nawaza kumshirikisha mama suala hili, nilimweleza wazo langu la awali.
Mwaija utaharibu kila kitu, kama una wasiwasi wa kugombana na ndugu zako mbebee mimba ule maisha. Tena mtoto anazaliwa akiwa na uhakika wa maisha yake tayari.
Mwaija mizee kama hii ndiyo inatafutwa mjini, hela zao hazina chenji. Mdogo wangu kwangu mimi hata angekuwa mpenzi wa mama yangu mzazi, kama angenitangazia bingo kama hiyo nisingelaza damu.
Naweza kumkubalia lakini sijui kama yupo sawa?
Kivipi?
Kiafya, si unajua dada yangu mwingi wa habari, tusije chuma janga tulile wenyewe.
Mmh! Kweli hilo umenena mdogo wangu.
Kwa hilo utanisaidiaje?
Usimpe mwili wako labda mtumie kondomu.
Tukitumia kondomu mtoto tutampaje?
Sikiliza mdogo wangu, hilo kwa sasa achana nalo, akishatimizia kila kitu kwa jina lako, sharti lako kubwa ili umpe mwili wako ni kwenda kupima kwanza.
Mmh! Dada nimekueleza itabidi nifanye hivyo.
Na majibu yake usiyacheleweshe ili asibadili uamuzi, si unajua wanawake tupo wengi wote tunataka hichohicho!
Nashukuru dada yangu kwa ushauri wako.
Baada ya mazungumzo nilimpigia simu bwana wa dada kuwa nimemaliza kilichonichelewesha naye alinieleza atafika muda si mrefu. Baada ya robo saa alifika kunichukua, kwa vile da Suzy alikuwa akikaa njiani kwenda kwetu, tuliondoka naye na kumteremshia njiani.
Baada ya kumteremsha da Suzy, tulibakia wawili kwenye gari, tulikwenda mwendo mfupi, bwana wa dada akaanza kunisemesha akiwa ameangalia mbele.
Mwaija za kazi?
Nzuri shemeji, shikamoo.
Marahaba, sasa wewe wasiwasi wako nini? aliniuliza swali bila kunitazama.
Wasiwasi! Wa nini?
Naona umeshaanza kuniogopa, nimekueleza lile ni ombi wala haliingiliani na mambo mengine.
Nikuogope kivipi? sikumuelewa.
Najua huniamini na kuona natumia turufu ya kukusaidia ili niweze kufanikisha mambo yangu. Lakini siyo hivyo, sina nia mbaya na wewe. Ningeweza kumpa mtu yeyote fedha niliyonayo lakini naamini kwako haitapotea.
Uliyosema nimekuelewa lakini sikuwa na maana hiyo. Nilikuwa na mazungumzo kidogo na da Suzy, nikaona nitakuchelewesha.
Niliyeamua kukuleta kazini na kukurudisha ni mimi wala sikulazimishwa na mtu.
Sawa, lakini kunipitia si adhabu, kama kuna dharura lazima tuambiane.
Nimekuelewa, ila nilipata wasiwasi, jana kuzungumza leo upatwe na dharura.
Walaa, wasiwasi wako siku zote wanadamu si wapangaji bali kila kitu hupanga wenyewe.
Ni kweli, vipi mzigo uliuona?
Ooh! Samahani kwa kuchelewa kushukuru, asante sana shemeji yangu, nilijikuta nikiona aibu ya kuchelewa kutanguliza shukurani mapema.
Usihofu ni kawaida, nia yangu siku moja, uishi maisha kulingana na heshima yako.
NILIJIKUTA nikipata kigugumizi cha kumpa jibu kuwa nimekubali, nilitaka mwenyewe kwanza aniulize kuliko kukurupuka.
Kwa vile tulikuwa tumekaribia maeneo ya nyumbani, nilishangaa siku ile kusimamisha gari mbali kidogo na nyumbani na kunigeukia kisha aliniita jina langu.
Mwaija?
Abee.
Vipi, nina imani umepata muda wa kufikiria.
Nini? nilijifanya sijui.
Au basi, shemeji naye alipindisha swali lake.
Shemeji, nilimwita huku nikimtazama usoni.
Naam.
Wewe na dada mpoje? nilimtupia swali.
Kwa nini unauliza hivyo?
Jibu swali si sikuuliza swali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwaija mbona hilo tuliisha lizungumza toka jana?
Sina maana ya unayofikiria ila jibu nililokuuliza.
Tulikuwa wapenzi.
Mlikuwa wapenzi, sasa hivi?
Si wapenzi tena.
Hilo halinihusu.
Ulikuwa unasemaje?
Nina imani tabia za dada unazijua vizuri?
Tabia zipi?
Za kutokuwa na mwanaume mmoja.
Ndiyo.
Nina imani katika starehe zenu kuna kipindi hamkutumia kinga?
Sina kumbukumbu hiyo, lakini sijawahi kukutana naye bila kinga.
Basi kupata uhakika tukapime.
Ili?
We si unataka kuzaa na mimi.
Mwaija mi nipo sawa mbona!
Sijakataa, ila muhimu tukapime, hata mimi najijua nipo sawa. Lakini kwa uhakika zaidi tukapime pamoja, nilimwambia nami nipo tayari ili kumtoa hofu.
Mmh! Sawa.
Mbona kama nakulazimisha?
Walaa nipo tayari.
Kwa hiyo tutakwenda lini? nilimuuliza kumsikiliza.
Siku yoyote utakayotaka.
Kesho ukinipitia wakati wa kutoka kazini.
Hakuna tatizo, Mwaija ila leo nitakushushia hapa sifiki kwenu.
Ajabu siku ile mzee Sambi hakutaka kufika nyumbani kitu kilichonishtua sana.
Vipi mbona leo hufiki nyumbani?
Sitakiwi.
Na nani?
Na dada yako.
Utakiwi una maanisha nini?
Dada yako hataki nifike kwenu.
Kwa sababu gani?
Anasema yeye si mke wangu hivyo anahitaji uhuru.
Mmh! Sasa itakuwaje?
Kila kitu nimekihamishia kwako.
Tokea lini umekatazwa na dada kufika nyumbani?
Leo inatimia wiki?
Wiki! Muongo!
Kweli kabisa.
Mbona kila siku ulikuwa ukifika nyumbani?
Sababu nilikuwa nakurudisha nyumbani pia nilizungumza na mama na dada yako mdogo.
Kwa hiyo itakuwaje?
Basi tena, kama utakuwa tayari kuwa na mimi sitafika tena kwenu, tutajua tukutane wapi?
Tukutane wapi ili iweje? nilishindwa kumuelewa tukutane ili iwe nini.
Si kama unavyofikiri, nia kubwa kukutana baada ya kazi na kuzungumza kisha anarudi nyumbani kwenu.
Makubaliano yetu mpaka unipatie tulivyokubaliana pia kwenda kupima, sasa habari hiyo inakuwaje? pamoja na kuonesha dalili za kukubali lakini sikutaka kujirahisi.
Kupima tunakwenda kesho, kwa vile nimekuahidi lazima nitafute kiwanja nikununulie na kuanzisha ujenzi.
Mmh! Hiyo si itakuwa kazi ya mwaka mzima?
Hapana ni ya miezi miwili, nilichokuwa nasubiri jibu lako tu.
Mi nimekubali.
Basi kila kitu niachie mimi, ungependa wiki hii uanze kuendesha gari lako?
Hapana nimalizie kwanza nyumba.
Basi Mwaija ndani ya miezi miwili utakuwa ndani ya nyumba yako.
Basi nikuache uwahi nyumbani.
Niliagana na mzee Sambi aliyenipa elfu hamsini ya kupandia bajaj japokuwa nyumbani hapakuwa mbali. Sikutaka kukodi bajaj nilichepua kwa mguu hadi nyumbani.
Nilipofika dada alishtuka na kuniuliza.
Vipi shemeji yako ndiyo kasusa?
Kwani vipi?
Achana naye kapewa lifti anataka kupiga mpaka honi.
Una maana gani?
Kumpa penzi mara moja kanigeuza mkewe, ooh! Nataka kukuoa ooh, nataka kuzaa na wewe nani kamwambia mi kiwanda cha kutotolea watoto?
Lakini dada, yule jamaa ana fedha zake kwa nini usimkubalie.
Mwaija nawe msichana kama mimi hujapungukiwa kitu. We si mtu wa kuolewa, mkubalie.
Dada nikimkubalia si utakasirika.
Mwaija nikasirike ili iweje?
Si tutakuwa tumechangia mwanaume mmoja.
Angekuwa mume wangu hapo kidogo afadhali, lakini mpita njia, wee kama katuma maombi mkubalie maisha yenyewe yapo wapi, dada alisema kama alikuwa akijua nini kinaendelea.
Mmh! Basi acha nikapumzike.
Haya mdogo wangu, kama katia timu kazi kwako hela zinamuwasha.
Dada baadaye basi.
Haya mdogo wangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliagana na dada na kwenda chumbani kwangu kubadili nguo ili niende nikaoge. Baada ya kuoga na kula nilijilaza chali kama kawaida yangu mikono niliweka kichwani. Nilijikuta nikipata wazo la kumweleza dada kuwa mzee Sambi ananitaka kimapenzi.
Niliamini kutokana na maneno yake hawezi kushtuka, lakini kwa upande wangu niliona ni mapema sana kumwambia jambo lile ambalo bado lili--kuwa halijakamilika. Nilijiuliza nini hatima ya maisha yangu kama nitakuwa na mzee Sambi mwanaume mwenye mke.
Niliamua kufanya kwanza siri mpaka kila kitu kitakapokuwa wazi, kwa vile nilikuwa nimechoka na kazi usingizi haukuchelewa kunichukua.
***
Siku ya pili, baada ya muda wa kazi mzee Sambi alinipitia kutokana na makubaliano yetu ya kwenda kuangalia afya zetu, alipofika tu nilimueleza tuliyokubaliana jana yake. Naye hakuwa na pingamizi, alikubali twende tukapime.
Tulikwenda kwenye hospitali moja iliyopo Keko Maduka Mawili. Kama kawaida, tulifika na kupokelewa na dada mmoja aliyekuwa mapokezi.
Baada kuandika kadi, alituelekeza kwa daktari, chumba kilichokuwa mbele kidogo. Tulielekea moja kwa moja kwa vile muda ule hakukuwa na wagonjwa wengi, wengi walionekana wamekuja kupata huduma ya sindano za saa.
Baada ya kuingia ndani ya chumba cha daktari tulipokelewa na kaka mmoja mtanashati.
Karibuni.
Asante, tulijibu kwa pamoja.
Ndiyo niwasaidie nini?
Tunataka kuangalia afya zetu.
Kuangalia kivipi?
Kupima Virusi vya Ukimwi.
Mmh! daktari aliguna kidogo na kututazama wote kwa zamu kisha aliuliza.
Mpo vipi?
Ni marafiki.
Wa kimapenzi?
Ndiyo, alijibu mzee Sambi.
Mna muda gani katika uhusiano wenu?
Mwezi sasa, alijibu mzee Sambi.
Sasa katika huo mwezi mlipokutana mlitumia kinga?
Hatujawahi kukutana, tumekuja hapa kupima ili tujue afya zetu kabla ya kuanza uhusiano rasmi.
Kwa mfano mmoja akikutwa na tatizo mtafanyaje?
Kwa upande wangu hakuna kitakachopungua kwa vile nina mapenzi ya dhati na mpenzi wangu, alijibu mzee Sambi huku akiushika mkono wangu na kuupapasa.
Na dada yangu kama utamkuta mzee ana matatizo?
Kwa upande wangu naamini mapenzi ndiyo yataishia hapa.
Kwa nini?
Kumbuka mi bado msichana mdogo nahitaji kuwa na familia halafu leo mwenzangu awe hivyo unafikiri raha ya ndoa ipo wapi?
Lakini kuna njia ya kuweza kupata mtoto bila tatizo.
Hiyo njia ndiyo siitaki kabisa kwa vile haipo salama asilimia mia moja.
Mzee umemsikia mama? daktari alimuuliza mzee Sambi huku akimtazama.
Kwangu hakuna tatizo, ikiwa hivyo namruhusu aamue chochote anachotaka lakini kama tatizo litakuwa kwake bado nitaendelea kumpenda na kumpa huduma zote muhimu kama nilivyomuahidi.
Sawa, basi nitawapa karatasi mtaingia chumba cha kwanza mkono wa kushoto mkapime damu.
Hakuna tatizo.
Daktari aliinama na kuandika karatasi ya vipimo na kutupa, tulizipokea na kufuata maelekezo. Tulitoka na kuingia chumba cha pili, kwa upande wangu sikuwa na wasiwasi kwa vile sikuwa na tabia ya kurukaruka, pia hata mtalaka wangu naye hakuwa na tabia mbaya japokuwa sikuwa nashinda naye muda wote tulipokuwa pamoja.
Mzee Sambi naye hakuonesha wasiwasi wowote, baada ya kuingia chumba cha maabara tulikaribishwa kwenye kiti. Tulikaa na kumpa vyeti vyetu, baada ya kusoma alichukua vifaa na kutuchukua damu mmoja mmoja. Baada ya kumaliza zoezi lile alituomba tukakae sehemu ya mapumziko kusubiri majibu yetu.
Tulitoka hadi kwenye makochi na kukaa kusubiri majibu, muda wote tulikuwa kimya, hakuna aliyeanzisha mazungumzo. Baada ya robo saa tuliitwa kwa daktari, nilijua majibu yameishatoka.
Tuliingia kwa daktari na kukaa kimya kusubiri majibu yetu.
Baada ya kukaa kwenye viti, ndani ya chumba kukiwa kimya, daktari alikuwa akipitia karatasi ya majibu yetu. Muda ule niliutumia kumsoma anachokisoma kwa kumuangalia usoni kwake nikiamini atakachokisoma kitaonekana kwenye uso wake.
Nilimuona akisoma akiwa ametuliza macho, muda wote aliosoma karatasi ya kwanza alikuwa ametuliza macho. Aliiweka pembeni na kuchukua nyingine ambayo ndiyo iliyokuwa na jina langu. Aliisoma taratibu kama ya kwanza lakini kuna kipindi niliona kama amekodoa macho. Baadaye aliyarudisha katika hali ya kawaida.
Aliichukua karatasi ya kwanza na kuisoma upya na kuirudia yangu harakaharaka kisha alitutazama. Macho yake yalionesha kuna kitu amekiona kwenye karatasi, sikujua yangu au ya mzee Sambi.
Alikohoa kidogo na kutuita majina yetu kupitia kwenye vyeti vyetu.
Mwaija.
Abee.
Mzee Sambi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Naam.
Majibu yenu yametoka, sasa sijui niyatoe kwa kila mmoja au kwa wote pamoja?
Kwa wote, sababu ya kuja pamoja kila mtu anataka kujua afya ya mwenzake.
Vizuri, je, mpo tayari kupokea majibu yenu?
Daktari acha mbwembwe we tupe majibu tujue tunasuka au tunanyoa,
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment