Simulizi : Mama Yangu Adui Yangu
Sehemu Ya Tatu (3)
Mwaija.
Abee.
Mzee Sambi.
Naam.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Majibu yenu yametoka, sasa sijui niyatoe kwa kila mmoja au kwa wote?
Kwa wote, sababu ya kuja pamoja kila mtu anataka kujua afya ya mwenzake.
Vizuri, je, mpo tayari kupokea majibu yenu?
Daktari acha mbwembwe we tupe jibu tujue tunasuka au tunanyoa, mzee Sambi ilibidi amweleze daktari aliyeonekana jambo dogo anataka kulikuza kitu ambacho humuongezea mtu hofu moyoni.
Sawa nimekuelewa mzee, majibu yenu yapo kama ifuatavyo wote wawili kwa vipimo vya awali vinaonesha mpo sawa.
Una maanisha? nilimsikia lakini sikumuelewa.
Damu yenu wote inaonesha ipo safi.
Ooh! Alhamdulilah, japokuwa nilikuwa na uhakika na afya yangu lakini nilimshukuru Mungu kwa vile sikuwa na uhakika wa uaminifu kwa mtalaka mwenzangu kwa asilimia mia moja.
Lakini upande wa mzee Sambi yeye alikuwa yupo katika hali ya kawaida zaidi ya kutabasamu na kuninyanyua na kunikumbatia kwa furaha.
Hongera mpenzi wangu.
Asante.
Jamani kama nilivyosema vipimo vya awali ndivyo vinavyoonesha mpo salama.
Ina maana kuna majibu mengine? nilijikuta nikiuliza kwa sauti huku nikijitoa kifuani kwa mzee Sambi.
Hapana ila mnatakiwa msikutane bila kinga mpaka mchukue vipimo vya pili ambavyo ni baada ya miezi mitatu.
Kwa upande wangu sihitaji kurudia kwani nina zaidi ya miaka miwili, simjui mwanaume.
Mmh! Hongera.
Hata mimi nilikuwa najijua nipo salama, lakini ili kuzidi kumtoa hofu nitafikisha miezi mitatu nitapima tena ndipo tuanze uhusiano rasmi, mzee Sambi alinitoa hofu.
Basi mi niwapeni hongera kwa kutunza afya zenu, majibu yasiwape kiburi bali yaongeze uaminifu katika uhusiano wenu, daktari alituasa.
Asante daktari.
Baada ya kuchukua majibu na kupata nasaha za daktari tuliondoka kurudi nyumbani. Njiani moyo wangu ulijikuta ukijaa furaha na kuanza kumuamini mzee Sambi ambaye tokea mwanzo alionesha nia njema kwangu.
***
Mzee Sambi aliendelea kunipeleka na kunirudisha nyumbani kwa mtindo wa kuniacha njiani na kunipa fedha ya teksi. Wiki mbili baadaye alinijulisha kiwanja kimepatikana na mwisho wa wiki alinipeleka kwenda kukiona.
Kiwanja kilikuwa kizuri sana kilichokuwa maeneo ya Boko, hakikuwa mbali na Barabara ya Bagamoyo. Kilikuwa kikubwa cha kutosha kujenga nyumba kubwa na kubakia eneo la kupumzikia.
Kwa kweli siku ile kwa mara ya kwanza nilifurahi sana na kumkumbatia mzee Sambi kwa furaha ya kweli toka moyoni.
Asante mpenzi wangu.
Huu ni mwanzo tu, nataka uamini sipo na wewe kukupotezea muda wako bali kuhakikisha nayabadili maisha yako.
Asante mpenzi naanza kuamini.
Utaamini siku moja, najuta kuchelewa kukufahamu mapema.
Hayo achana nayo tugange yaliyopo nayajayo.
Basi mpenzi tukirudi kwenye gari nitakuonesha ramani ya nyumba yako inatakiwa kuwa vipi?
Ramani yake ipo wapi? nilijikuta nimepata kimuhemuhe mtoto wa kike.
Ipo kwenye gari.
Twende nikaione, mtoto wa kike shauku ikanipanda.
Utaiona tu wala usiwe na wasi.
Lakini mpenzi huku mbali sana na mji?
Si utakuwa na usafiri wako ili kukurahisishia kwenda popote bila tatizo.
Mmh! Hapo sawa.
Baada ya kuzunguka eneo la uwanja wangu tulirudi kwenye gari. Kabla ya kuondoka alinionesha ramani ya nyumba yangu pia picha ya nyumba iliyokuwa imeishajengwa ambayo ilionekana nzuri pembeni kukiwa na gari la kifahari na bustani nzuri.
Basi nyumba yako ikiisha itakuwa kama hivi.
Muongo! nilishtuka kuambiwa nyumba kama ile nzuri itakuwa yangu.
Ikiwa tofauti na hii picha ikatae.
Na hili gari la kifahari lililopo pembeni ya nyumba nitakuwa nalo?
Lazima kila kitu kiwe kama kinavyoonekana kwenye picha.
Wawooo! Jamani asante mpenzi wangu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hizi ni rasharasha tu, mambo mazuri yanakuja.
Tulitoka kwenye kiwanja changu na kunirudisha nyumbani, kama kawaida aliniteremshia mbali na nyumbani. Nilipofika nilijikuta kila dakika nikitabasamu baada ya kukumbuka picha ya jumba la kifahari nililooneshwa na mpenzi wangu na kunihakikishia nyumba yangu ndivyo itakavyokuwa.
Nilijikuta nikiyaona maisha yangu yakibadilika na kunifanya niwe mtu mbele za watu. Nilikumbuka baadhi ya wanawake waliokuwa wakija kazini na kuwatetemekea kwa vile walikuwa na magari au wake wa watu wenye fedha nami nilijua tayari nimewafikia. Moyo uliniuma baada ya kujua sina haki ya asilimia mia moja hata nikiwa naye. Nilijiuliza kwa upendo alionionesha angekuwa wangu peke yangu sijui ingekuwaje! Naamini ningekuwa juu zaidi ya mawingu.
Siku iliyofuata ilikuwa Jumatatu, nilikwenda kazini kama kawaida. Da Suzy aliniuliza mchakato wangu na mzee Sambi. Nilimweleza yote sikumficha hata moja.
Unaona mdogo wangu ulitaka kuupiga teke mfuko wa fedha!
Lakini kumbuka si wangu wa kufa na kuzikana, Lakini ndiyo hivyo cha kuazima hakisitiri ------.
Mdogo wangu usifikirie visivyo kuhusu, ridhika na unachokipata. Amekuahidi mambo mengi na moja ameanza kulitekeleza. Ningekuwa ndiyo mimi mbona ningemzalia mtoto kwa vile mmepima na kuzijua afya zenu.
Mmh! Sawa, huwezi kuamini nimeanza kumpenda hata bila kujijua.
Chezea faranga wewe? Dada Suzy alitania.
Walaa, si kwa ajili hiyo bali ameonesha upendo wa dhati kwangu, ni mtu mwenye huruma, mkweli pia mwenye nia njema kwangu.
Basi mdogo wangu usiipoteze nafasi hiyo.
Dada sasa hivi mimi na mzee Sambi kama chanda na pete.
Hongera mdogo wangu, la muhimu mzalie mtoto ndicho kilio chake.
Atampata tu muda si mrefu tukianza kujirusha.
Ina maana hujampa? Dada Suzy alishtuka kusikia siku zote hizo sikuwa nimempa mwili wangu mzee Sambi.
Dada sikutaka kuwa naye kibiashara bali kujua hatima ya maisha yangu.
Kweli mdogo wangu una msimamo.
Tuliendelea na kazi, jioni kama kawaida mpenzi wangu alinipitia na kunirudisha nyumbani. Gari lilipofika makutano ya Barabara ya Changombe na Nyerere nilishangaa kuona likinyooka kufuata Barabara ya Nyerere badala ya kukata kushoto.
Sikutaka kumuuliza kwa kujua labda ameamua kupitia Barabara ya Mandela na kuingilia barabara ya kuelekea maghorofa ya Tazara. Lakini tulipofika njia panda ya Nyerere na Mandela alikata kulia badala ya kushoto kitu kilichonishtua.
Vilevile sikuhoji nilitaka nione mwisho wake utakuwa vipi. Gari lilielekea Buguruni, lakini tuliongoza hadi Tabata Dampo. Tulipinda kulia kufuata barabara ya kuelekea Tabata.
Tulipofika Bima alikata kulia kuelekea Tabata Kimanga nami nilikuwa kimya nimetulia nione ananipeleka wapi. Tulipofika Savana alikata kulia na kusimamisha gari nje ya nyumba moja yenye geti, akateremka na kufungua geti.
Aliporudi kwenye gari nilimuuliza.
Mpenzi wewe si una mke?
"Ndiyo."
"Sasa unanipeleka wapi?"
"Ondoa wasiwasi mpenzi."
"Kama kwako naomba unishushe."
"Hapana mpenzi, kwani nilikuambia nakaa wapi?"
"Sasa huku tunakwenda wapi?"
"Bebi mbona una wasiwasi? Siku zote nayajali sana maisha yako kuliko kawaida."
"Najua lakini naomba uniambie huku unanipeleka wapi?"
"Unaniamini?"
"Nakuamini."
"Basi niachie mimi kila kitu."
"Haya baba."
Mzee Sambi aliliingiza gari ndani ya geti na kulisimamisha mbele ya nyumba nzuri.
"Tumefika," alisema huku akinitazama usoni.
Sikumjibu nilitulia nikimuangalia, baada ya kuzima gari alinieleza:
"Tushuke."
Bila kuhoji kitu niliteremka na kufunga mlango wa gari, nikasimama nje ya gari kusubiri kujua pale nimeletwa wapi. Wazo langu la kwanza labda nyumba ya wageni.
Lakini katika makubaliano yetu ilikuwa mpaka akamilishe kila kitu ndipo na mimi nimpe mwili wangu. Lakini moyoni nilijikuta nikiwa tayari kumsikiliza atakachokitaka na kuusihi moyo wangu kutokuwa na swali kwa lolote litakalokuja mbele yangu.
Mzee Sambi baada ya kufunga mlango wa gari alikwenda hadi kwenye mlango wa nyumba ile na nilishangaa kuona akitoa ufunguo mfukoni na kufungua mlangoni. Baada ya kuzungusha funguo alinyonga kitasa na kuusukuma mlango kwa ndani.
Baada ya mlango kufunguka aliingia ndani na kutoka kisha aliniita.
"Bebi njoo."
Nilimfuata bila kusema kitu nikijua siku ile sikuwa na ujanja wa kukataa kufanya chochote na mzee Sambi, kutokana na kila alichokuwa akifanya mbele yangu kilianza kuivunja ngome ya moyo wangu.
Nilipofika mlangoni alinishika mkono na kuniingiza ndani ya nyumba ile, ambayo sebule yake ilikuwa imekamilika na kuwa na kila kitu kwa mtu mwenye maisha ya juu.
"Karibu mpenzi."
"Asante," nilijibu huku nikipepesa macho.
"Unapaonaje hapa?"
"Mmh! Pazuri."
Alinishika mkono na kunipeleka mpaka chumbani nikajua shughuli imefika, sikuwa na uwezo wa kupinga, kwa vile mpaka kukubali kuingia mle ndani nilikubali kwa hiyari yangu sikulazimishwa na mtu.
"Karibu bebi."
"A..a..sante."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mbona una wasiwasi?"
"Walaa," nilikataa tu lakini mazingira yale yalinifanya nipoteze kujiamini.
"Unakionaje chumba?"
"Kizuri," nilijibu kwa mkato.
"Bebi naomba nikuambie kitu."
Nilijua hana cha kuniambia zaidi ya kuniomba kufanya mapenzi kutokana na kunionesha vitu vya kunijali. Lakini bado nilikuwa na maswali pale ni kwa nani?
"Niambie tu bebi."
"Naomba nikuambie toka moyoni mwangu, Mwaija nakupenda."
"Hata mimi nakupenda," nilijibu nikiwa bado sijiamini.
"Nimefurahi kusikia hivyo."
"Hata mimi nafurahi kwa yote unayonifanyia na mengine utakayonifanyia."
"Naomba kwanza tutoke nje."
"Hakuna tatizo."
Tulitoka hadi nje ya nyumba na kunizungusha kuiangalia ile nyumba iliyokuwa kwenye hali nzuri sana. Bado sikumuelewa alinitoa nje kufanya nini.
"Mwaija."
"Abee."
"Hii nyumba unaionaje?"
"Mmh! Nzuri."
"Basi mpenzi kuanzia sasa utakaa hapa."
"Na ile nyumba unayonijengea Boko?"
"Hapa nimekupangia kwa muda wakati unasubiri nyumba yako kuisha ili nami nipate muda wa kuwa na wewe baada ya kazi kwa nafasi."
"Mmh! Asante mpenzi," nilimshukuru kwa kumkumbatia.
"Basi vitu vyote unavyoviona ndani vimenunuliwa juzi na kupangwa jana. Baada ya kuridhika ndiyo nikakuleta ujionee nyumba yako."
"Asante sana," nilijikuta nikiwa na furaha ya ajabu moyoni na kuona kama Mungu kaamua kunifanyia muujiza.
"Haya ni matunda ya msimamo na tabia zako, sijawahi kuona msichana kama wewe katika kipindi hiki."
"Mbona tupo wengi tu basi mmekuwa wavivu kuchagua vinavyong'aa barabarani mkadhani vyote ni dhahabu."
"Nimekubali na kauli yako."
Tulirudi ndani, kwa vile muda ulikuwa umekwenda nilimuomba aniwahishe nyumbani.
BASI mpenzi kuanzia sasa utakaa hapa.
Na ile nyumba unayonijengea Boko?
Hapa nimekupangia kwa muda wakati unasubiri nyumba yako kuisha ili nami nipate muda wa kuwa na wewe kwa nafasi baada ya kazi.
Mmh! Asante mpenzi, nilimshukuru kwa kumkumbatia.
Basi vitu vyote unavyoviona ndani vimenunuliwa juzi na kupangwa jana. Baada ya kuridhika ndiyo nikakuleta ujionee nyumba yako.
Asante sana, nilijikuta nikiwa na furaha ya ajabu moyoni na kuona kama Mungu kaamua kunifanyia muujiza.
Haya ni matunda ya msimamo na tabia zako, sijawahi kuona msichana kama wewe katika kipindi hiki.
Mbona tupo wengi tu basi mmekuwa wavivu kuchagua vinavyongaa barabarani mkadhani vyote ni dhahabu.
Nimekubaliana na kauli yako.
Tulirudi ndani, kwa vile muda ulikuwa umekwenda nilimuomba aniwahishe nyumbani.
Bebi kwa nini leo usilale hapa?
Mmh! Peke yangu jumba lote hili?
Tutalala wote.
Hapana siku nyingine, si unajua mimi mtoto wa mama lazima nikaage nyumbani kuwa naanza kujitegemea!
Hakuna tatizo nakusikiliza wewe.
Basi kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.
Hakuna tatizo.
Tulikubaliana kuondoka tulizima taa na kufunga mlango wa nyumba na geti na kunirudisha nyumbani. Tulipofika maeneo ya Mwembe Yanga alinikodia teksi hadi nyumbani.
Nilifika nyumbani na kuwa na mawazo mengi juu ya mzee Sambi. Baada ya kuoga na kupata chakula cha usiku, nilimfuata mama chumbani kwake na kumweleza siri yangu.
Aliposikia namgongea alitoka na kuniuliza, kwa vile sikuwa na kawaida ya kumfuata muda ule. Toka nilipoanza kazi baada ya kazi nilikuwa chumbani kwangu nikiangalia CD za filamu.
Sikutaka kukaa nje kwa kuhofia kujiingiza kwenye vishawishi vibaya. Mama aliponiona aliniuliza:
Vipi mama?CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikuwa na mazungumzo na wewe kidogo.
Sawa, nisubiri sebuleni nakuja.
Hapana mama nataka tuzungumzie chumbani kwako.
Mmh! Makubwa mazungumzo ya chumbani kwangu?
Ndiyo mama.
Haya karibu.
Niliingia chumbani kwa mama na kukaa kitandani kwake karibu yake. Mama alimaliza kuweka vitu vyake vizuri kisha alinigeukia.
Haya mama niambie.
Mama kuna kitu ninacho muda mrefu, ilikuwa vigumu kukueleza mwanzo kwa vile sikuwa na uhakika nacho.
Kitu gani hicho?
Mama nimepata rafiki wa kiume ambaye amejitolea kila kitu katika maisha yangu.
Nilijua, nilisubiri kuambiwa ningekuuliza ningeonekana muongo.
Inawezekana lakini mwanzo ilikuwa ngumu kulisema.
Haya mwanangu ulikuwa unasemaje?
Mama mtu mwenyewe unamfahamu.
Mwanangu nimfahamu vipi bila kunifahamisha.
Mzee Sambi.
Mzee Sambi aliyekuwa mpenzi wa dada yako?
Ndiyo.
Mmh! Makubwa, kwa nini umekubali kuchangia mapenzi na dada yako? nilimshangaa mama kuniuliza swali kama lile.
Hata mimi mwanzo sikutaka kukubali, lakini mzee yule alinieleza mambo mengi kuhusiana na dada kumfukuza na alivyotaka kumfanyia ambavyo vyote dada alivipiga teke.
Vitu gani?
Alitaka awe nyumba yake ndogo na kumuahidi kumjengea nyumba na kumnunulia gari.
Muongo wanaume wa mjini utawaweza, wanataka wakutumie wakitimiza haja zao wanaondoka bila kwa heri. Dada yako aliniambia nikamkatalia.
Mama makubaliano yetu ni kuwa naye baada ya kunikamilishia kila alichoniahidi.
Atawahi muongo mkubwa, atakuletea nyaraka za uongo ili uamini lakini mwishoni atazichukua.
Kwangu tofauti, hivi ninavyo kwambia ameisha ninunulia kiwanja na ujenzi utaanza mara moja.
Muongo? mama alishtuka.
Tena mama nyumba ikiisha litakuwa bonge la jumba pia amesema ataninunulia gari la kifahari.
Mmh! Hongera.
Asante na sasa hivi amenipangia nyumba nzima hivi ndiyo nimetoka kuiona yenye kila kitu ndani.
Dada yako akijua itakuwaje si unaujua ukorofi wake.
Yeye ndiye aliyeniambia kama namtaka nimchukue.
Basi mimi sina tatizo, kwa hiyo nyumba aliyokupangia itakuwaje?
Nitahamia wakati wowote.
Kwa hiyo utakuwa unakaa naye?
Hapana, hatujakubaliana hilo bali ametaka niwe huru na kuweza kuonana naye na kupanga mambo yetu kwa uhuru mkubwa.
Sawa, umeona ulijifanya mlokole yote haya ungeyapatia wapi?
Mama nilitaka kusahau, amesema eti nikimzalia mtoto wa kike atanipa milioni kumi na kiume ishirini.
Masuala ya nyumba na gari yanakufa?
Walaa hiyo ni bonasi ya furaha ya kupata mtoto.
Mmh! Makubwa.
Mama mbona unaguna.
Ndiyo nasikia kwako kumzalia mtu mtoto akulipe fedha.
Mama amesema mkewe hana kizazi hivyo anategemea kwangu.
Wewe ndiyo unacho?
Mama maneno gani hayo? maneno ya mama yalinivunja nguvu.
Siyo maneno gani, kwani huyo mkewe alilokosa kwa Mungu nini?
Sasa mama yeye kukosa kizazi na mimi kunaingiaje?
Siyo kuingiaje bali nenda na mawili, isije ahadi ya milioni kumi na ishirini ikayeyukia hewani ukachanganyikiwa bure. Mtoto ni majaliwa ya Mungu na si kwa ahadi ya fedha ingekuwa hivyo mkewe angemzalia.
Sawa mama nimekuelewa, nilikuja kukufahamisha tu.
Hicho kiwanja chenu kipo wapi?
Boko.
Utanipeleka lini nikakione?
Mwisho wa wiki.
Basi mwanangu nakutakia kila la heri.
Asante mama yangu.
Niliagana na mama na kwenda kulala japokuwa nilichelewa kulala kwa kauli ya mama labda sina kizazi kwa kweli iliniumiza sana.
Nilijikuta nikiyadharau yote kwa kuamini kila kitu chini ya jua muwezeshaji wa yote ni Mungu pekee si mwanadamu.
Niliamini hakukuwa na haja ya kuendelea kuwa nyumbani kwa vile sifa ya nyumbani kwetu sikuipenda siku zote. Ilionekana Mungu alisikia kilio changu cha kuishi kwenye nyumba yenye sifa mbaya kilipokelewa.
Pamoja na furaha ya kutoka nyumbani lakini suala la kuanza kuishi na mzee Sambi kama mke na mume sikuliafiki kwa vile ilikuwa mapema sana.
Kukaa peke yangu jumba lile niliona haifai lazima nilitakiwa kuwa na mtu wa karibu. Nilikumbuka kuna msichana mmoja aliyekuwa akifanya kazi za ndani kwa jirani yetu niliye kuwa nimezoeana naye. Kuna siku alinifuata kabla ya kuanza kazi super market kuniomba aje pale kwetu au nimtafutie kazi kutokana na manyanyaso na ugumu wa kazi aliokuwa akikutana nao pale.
Niliamini nikiwa naye angenisaidia kazi pia kunichangamsha nikiwa nyumbani peke yangu. Nilijikuta nikipata tumaini la kuwa na mtu wa kukaa naye. Baada ya kuwaza sana usingizi ulinichukua.
***
Siku ya pili kabla ya kwenda kazini nilibahatika kumuona yule msichana ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na saba.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kweli alifurahi sana kumpa habari ambazo ilionekana alikuwa akizisubiri kama wokovu.
Nilimweleza nitampitia jioni ya siku ile nikitoka kazini na kwenda naye kwangu. Nilikwenda kazini na kumweleza da Suzy ambaye alizidi kuusifia uamuzi wangu wa kukubali kuwa na mzee Sambi.
Jioni mzee alinipitia, nikamweleza kuanzia siku ile nitahamia kwangu. Alifurahi sana kwa kitendo changu cha kukubaliana naye bila masharti magumu.
Lakini mpenzi nitakuwa na msichana wa kazi.
Wala usiwe na wasiwasi, nilikuwa na wazo hilo maana jumba ni kubwa unatakiwa kuwa na mtu kama mimi sipo, mzee Sambi alinifurahisha sana, hakuwa mtu wa kunipinga jambo.
Basi sasa hivi nakwenda kumpitia ili tuende naye kwangu.
Hakuna tatizo.
Tulikwenda hadi Temeke na kumpitia msichana wa kazi ambaye nilimkuta amejiandaa. Kabla ya kuondoka niliwaaga ndugu zangu ambao walishtuka.
Vipi tena?
Nawakimbia kidogo.
Wapi?
Tabata.
Mmh! Vipi Beka karudi nini? dada mdogo aliuliza.
Walaa, yupo mwingine, dada anamjua.
Siku hizi yupo na mzee Super.
Mzee Sambi? dada mdogo alishtuka.
Ndiyo, mdogo wetu kaamua kujimilikisha mzee mzima.
Ha! Wee Mwaija umekosa wanaume wote mpaka umchukue mpenzi wa dada yako? We si ulikuwa mlokole, imekuwaje leo kuchangia bwana na dada yako? dada alizidi kushangaa.
Kila kitu dada anajua.
Mwache kwa raha zake, mzee yule mshamba nilimtimua. Eti ataninunulia gari, ooh atanijengea nyumba, utongozaji wa kizamani. Nilimpa penzi la muda siyo kunganganiana kama ruba.
Alichonichefua zaidi eti tukapime ili nimzalie mtoto kwa madai kuwa atanipa milioni kumi, nilimwambia mimi nina shida ya mtoto? Aliambiwa mi kiwanda cha kuzalisha watoto? Mdogo wangu kamzalie mtoto upate hiyo nyumba, gari na milioni kumi.
Mmh! Kumbe nimekuwa -----, yaani mambo yanapita juu yangu bila kujua? Kwa hiyo umemruhusu mdogo wako atembee na bwana ako?
Kipi cha ajabu? Si afadhali Mwaija aliniuliza kuliko wewe uliyekuwa ukitembea na bwana yangu mpaka ukaniwekea fitina nikaachwa, dada mkubwa alimjia juu dada mdogo.
Niliona mjadala wangu utavumbua yasiyonihusu. Nikaamua kuwaaga.
Jamani dada zangu mi nawahi, naamini tutaonana mwisho wa wiki.
Hakuna tatizo, ukitulia uje utuchukue.
Hakuna tatizo.
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda niliondoka kwa kumpitia msichana wangu wa kazi na kwenda naye hadi kwangu, Tabata Savana. Nilipofika nilimweleza kuwa nitaishi naye kama ndugu yangu japokuwa nitamlipa mshahara kama kawaida. Alinishukuru kwa kumtoa kwenye mateso.
***
Niliyaanza maisha mapya ya kuishi kwangu nikiwa na mzee Sambi ambaye wakati huo alikuwa akinitafutia eneo kwa ajili ya kunifungulia mini super market maeneo ya karibu na aliponipangia kati ya Tabata Mawenzi au Shiba.
Niliendelea kumshukuru Mungu kwa kuyabadili maisha yangu huku bado nikiwa namkumbuka mume wangu Beka juu ya kunipa talaka bila sababu.
Kila nilipokuwa peke yangu nilimkumbuka sana Beka, mwanaume ambaye niliamini ndiye wa maisha yangu. Nilikuwa na mzee Sambi ambaye nilimpenda kutokana na kujitoa kwa ajili yangu huku akijitahidi kuona naishi maisha ya furaha muda wote. Lakini mapenzi ya kweli yalikuwa kwa Beka.
Lakini lazima niseme ukweli mzee Sambi sikumpenda kwa asilimia zote. Niliapa kumsamehe Beka kama atagundua makosa yake na kuja kuniomba msamaha.
Unaweza kunishangaa, lakini nilikuwa radhi kuishi maisha yoyote na Beka na kuwa tayari kuachana na kila kitu nilichoahidiwa na mzee Sambi.
Beka nilimpenda naye alinipenda hilo nililitambua, lakini kilichovunja mapenzi yetu sikukielewa mpaka siku ile alipokuja na kunipa talaka iliyokosa maelezo ya kina.
Mara nyingi nilipokuwa peke yangu nilijisahau na kuweka mkono shavuni na machozi kunitoka nikimkumbuka. Pamoja na raha nilizopewa na mzee Sambi huku ujenzi wa jumba langu la kisasa ukiendelea, bado nilikuwa na jeraha kubwa moyoni mwangu ambalo siku zote halikupona kwa vile sikujua sababu ya kupewa talaka bila kuelezwa kisa.
Siku zote mtu akihukumiwa kwa kosa analolijua hata kama ni dogo na hukumu kuwa kubwa hujua kosa lake. Lakini kwangu hata nilipokuwa katikati ya furaha, kila nilipokumbuka mazingira tata ya talaka yangu, furaha ilinipotea na kujikuta nikitokwa machozi na kuweka mkono shavuni.
Mara nyingi msichana wangu wa kazi alikuwa akinishtua na kutaka kujua sababu ya mimi kuwa vile. Siku moja uvumilivu ulimshinda na kuamua kuniuliza:
Dada una tatizo gani?
Nipo sawa.
Hapana dada si mara ya kwanza kukuona hivi, mara nyingi ukiwa peke yako unakuwa umeshika tama machozi yanakutoka kisha unatikisa kichwa na na kufuta machozi.
Mmh! Mdogo wangu ya dunia.
Yapi dada, mbona mimi yangu nimemwachia Mungu.
Ni kweli mdogo wangu, lakini langu linanitesa kila nikilikumbuka, kwa akili ya kawaida unaweza kulidharau lakini langu ni donda ninalolitonesha kila mara.
Kwani dada una tatizo gani? Mariamu aliniuliza akiwa ananitazama kwa jicho la huruma.
Kwa vile alikuwa msichana aliyepevuka nilimweleza yote. Baada ya kunisikiliza alinipa pole.
Duh! Dada unataka kuniambia mpaka leo hujajua sababu ya kupewa talaka?
Sijajua, na kibaya dua na maombi yangu yote yalikuwa kwa mume wangu. Hata katika maisha yetu hatukuwahi kugombana.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi si angekuambia kuliko kukupa mtihani usioujua?
Wee acha, kila nikikumbuka moyo unaniuma sana.
Lakini dada mbona Mungu kasikia kilio chako.
Mungu hajasikia kilio changu, bali kanipandisha kutoka chini lakini jibu la swali langu bado sijalipata.
Ungeachana nalo tu.
Najitahidi kufanya hivyo, lakini moyo wangu umekataa kupinduka.
Na mama anasemaje?
Mama ajue nini ikiwa talaka kanipa Beka kwani mama yangu ni familia ya mtalaka wangu?
Mmh! Lakini Mungu mkubwa ipo siku utasahau.
Ndicho ninachokiomba usiku na mchana mawazo juu ya mtalaka wangu yafutike kichwani mwangu.
Maisha yaliendelea huku nikiwa sina pingamizi la kumpa mwili wangu mzee Sambi kwa vile sikuona sababu ya kumnyima kwani tuliishi kama mke na mume.
Siku moja tukiwa kitandani tumejilaza, ilikuwa siku ya mapumziko, ambazo mzee Sambi alizitumia kuja kwangu kushinda mpaka jioni.
Mwaija, aliniita kwa sauti ya chini.
Abee.
Unayaonaje maisha?
Namshukuru Mungu mazuri.
Kuna kitu umepungukiwa?
Kinaweza kuwepo, lakini kwa sasa nina imani hakuna.
Vipi kuhusu ombi langu?
Lipi? nilimuuliza huku nikijigeuza na kumtazama.
Kuhusu mtoto.
Hakuna tatizo.
Upo tayari kuzaa na mimi?
Ndiyo.
Asante sana mpenzi wangu.
Ni wajibu wangu kukufurahisha mpenzi wangu kwa vile nawe unanifurahisha. Mungu akijalia nitakuzalia watoto hata kumi.
Usiniambie!
Tatizo lipo wapi baba ana uwezo na malezi si tatizo.
Mi nataka wawili kwanza.
Basi baba jitahidi kuwatafuta hao watoto.
Kwa furaha hata kabla ya kuwapata leo nitakupa hundi ya milioni kumi kama asante ya kuonesha una mapenzi ya dhati na mimi.
Siku ile alinipa hundi ya milioni kumi, nami mara moja nikaanza kuitega mimba kwa kutumia kalenda ya kupata mtoto. Sikuwa mvivu siku zote za hatari nilijitahidi kukutana na mpenzi wangu.
Siku zilikatika bila kuonekana dalili za kushika ujauzito kitu kilichonishtua sana. Mwezi wa tatu ulipokatika nilijikuta nikipata wazo labda mzee Sambi ndiye mwenye tatizo na kumsingizia mkewe ndiye hazai.
Siku moja tukiwa tumejilaza kitandani, nilimdodosa mzee Sambi juu ya mkewe kushindwa kumzalia mtoto.
Samahani mpenzi.
Bila samahani.
Eti tatizo la mke mwenzangu lilikuwa nini?
Tatizo gani?
La kushindwa kubeba mimba?
Ni historia ndefu haina muhimu kwa sasa.
Hapana, nina sababu zangu.
Sababu zipi?
Naomba kwanza uniambie.
Sababu kubwa mke wangu hana mfuko wa uzazi.
He! Tatizo nini? nilishtuka kusikia vile.
Alipata matatizo kwenye mfuko wa uzazi ukaondolewa.
Wakati huo mkiwa ndani ya ndoa?
Hapana.
Ina maana tatizo alilipata kabla ya ndoa?
Ndiyo.
Sasa kipi kilichokufanya umuoe wakati ukijua kabisa hazai na kukufanya sasa hivi uhangaike nje ya ndoa kutafuta mwanamke akuzalie mtoto?
Ni historia ndefu, mke wangu kabla ya tatizo hilo alikuwa mpenzi wangu wakati huo alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita. Wakati anajiandaa na mtihani alijigundua ana ujauzito.
Sasa wewe unajua mwanafunzi kwa nini hamkutumia kinga au kalenda ya mzunguko wa hedhi?
Wee acha huwezi kuamini, mke wangu nimeanza naye mapenzi tangu akiwa kidato cha tatu. Muda wote tulikuwa makini, hata sikumbuki tulikosea wapi.
Ehe!CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa vile alikuwa amebakiza miezi mitano afanye mtihani na ujauzito ulikuwa wa miezi mitatu ilibidi tufanye mpango wa kutoa.
Mmh! Ikawaje?
Kumbe aliyemtoa hakumsafisha vizuri, baada ya muda alianza kusumbuliwa na tumbo. Hata mtihani wa kidato cha sita aliufanya kwa shida. Hatukujua tatizo mapema kutokana na yeye kusafiri kwenda kwa bibi yake kwa miezi mitatu.
Huko alipokwenda hali ilizidi kuwa mbaya na kulazwa hospitali. Alinieleza alisafishwa tena na kupata nafuu. Lakini ugonjwa wa tumbo ndiyo ukawa tatizo lake.
Aliporudi Dar nilimchukua na kumpeleka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake. Vipimo vilionesha mfuko wa uzazi umeharibika na hakukuwa na njia yoyote ya kumnusuru na hali yake zaidi ya kutolewa.
Mke wangu alilia sana huku akinilaumu nimemuharibia maisha yake. Sikuwa na jinsi zaidi ya kumuahidi kumuoa na kuishi naye mpaka Mungu atakapomchukua mmoja wetu.
Basi ilinibidi nijikomiti na kujifunga kwa maandishi kwamba sitamuacha.
Baada ya miaka saba alitaka tuasili mtoto, lakini nilimshauri kwa nini nisitafute mtoto wa nje ya ndoa. Mwanzo alikataa katakata kwa kuamini mwanamke nitakayezaa naye atamdharau kwa vile hawezi kuzaa.
Nimbembeleza na kumweleza siri ile itabakia kati yake na mimi na nusu ya mali yangu nitampa yeye ila niwe na mtoto wa damu yangu kutoka kwa mwanamke wa nje atakayenizalia kwa mkataba.
Ilibidi tukubaliane atakayeingia ndani ya nyumba yetu ni mtoto na si kitu kingine. Hapo ilibidi nianze kusaka mtu wa kuzaa naye. Kwa kweli kila niliyemgusia kuzaa naye alitaka ndoa.
Kwangu ilikuwa vigumu kutokana na masharti ya mke wangu. Ndipo nilipokutana na dada yako ambaye nilimuahidi kama atakubali kunizalia mtoto ningempa zawadi kubwa.
Tatizo lingine ambalo lilimtibua dada yako na ndiyo chanzo cha kunifukuza lilikuwa kumwambia kama atakuwa tayari tukapime. Hicho ndicho kilichosababisha mimi na dada yako tukosane.
Lakini nashukuru sasa hivi nimeangukia kwenye mikono salama.
Kama mlikubaliana na mkeo kupata mtoto, kwa nini unatumia fedha nyingi kunijengea nyumba na kuninunulia gari wakati ningekuzalia mtoto tu na kuachana?
Pamoja na yote niliyokueleza, mke wangu mkorofi sana kiasi cha kunifanya nyumba niichukie, jambo dogo anaomba talaka.
Labda unamnyanyasa kutokana na hali yake.
Haijatokea hata siku moja, basi siku hizi kabadilika amekuwa mtu wa kukasirika bila sababu.
Sasa akijua umenifanyia vitu hivi tofauti na makubaliano yenu unafikiri itakuwaje, si ndiyo kuuana? nilijikuta nikiingia woga.
Hawezi kufahamu hata siku moja.
Sababu ya kuuliza hivyo inatokana na mimi kukutega siku zangu za hatari bila mafanikio.
Kwa hiyo ulitaka tufanyeje?
Tukacheki afya zetu tujue sababu ya kuchelewa kupata mimba ni nini.
Hakuna tatizo.
Tulikubaliana siku ya pili kwenda hospitali kuangalia tatizo la kuchelewa kupata mimba linatokana na nini au kati yetu kuna mwenye tatizo linalosababisha nisishike ujauzito.
***
Siku ya pili alinipitia kazini mapema na kwenda naye kwenye moja ya hospitali kubwa jijini. Tulipofika tulipokelewa na daktari ambaye alionesha anamfahamu sana mzee Sambi aliyekuwa maarufu jijini.
Karibu mzee Sambi.
Asante John.
Karibu dada, alinikaribisha na mimi.
Asante.
Ndiyo mzee za siku?
Nzuri tu ndugu yangu.
Naona mmefika hapa mna shida?
Ndiyo.
Mna shida gani?
Nina imani unajua raha ya nyumba mtoto? mzee Sambi alisema.
Ndiyo, lakini mtoto ni majaliwa.
Ni kweli, lakini lazima ujue kama una tatizo na kama unalo linatatulika vipi?
Kwa hiyo mna shida gani?
Tunataka tuangalie afya zetu ili tujue kwa nini tunalima lakini hatupati mazao.
Hakuna tatizo mtajua kila kitu.
Daktari alituandikia karatasi ya kwenda kuchukua vipimo. Tulikwenda hadi kwenye chumba cha maabara. Tulipofika tulichukuliwa, nilitangulia mimi ndani na kufanya uchunguzi kwa kuangaliwa kwa Ultra Sound kuangalia mirija ya uzazi na uwezo wa mayai kukomaa na kubeba mimba.
Kwa upande wa mwenzangu sikujua kwa vile kila mmoja alipimwa peke yake. Baada ya kumaliza kupimwa nilielekezwa kwenda kukaa sehemu kusubiri.
Baada ya muda mzee Sambi naye alikuja nilipokuwa nimekaa. Tulikaa sehemu ile kusubiri kuitwa, kwa upande wangu sikuwa na wasiwasi kwa vile niliishawahi kupata ujauzito na kutoka.
Wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa kwa mzee Sambi kwa kujua huenda ana tatizo lakini hakutaka kuliweka wazi. Baada ya kukaa zaidi ya saa tatu tuliitwa kwa daktari.
Baada ya kuingia tulitulia kusubiri majibu ya daktari kuhusiana na afya zetu.
Jamani majibu yenu yamerudi, vipimo vyetu vinatazama kwa umakini mkubwa na majibu yake hayana ubabaishaji. Hivyo basi majibu yanaonesha kila kona haina tatizo kila mtu ana uwezo wa kupata mtoto.
Sasa tatizo nini? niliuliza.
Hii huwa ni hali ya kawaida tu wala haina tatizo kwa mtu kuchelewa kupata mtoto. Muda ukifika mtapata tu.
Sasa mpaka lini? mzee Sambi naye aliuliza.
Kwani mna muda gani kwenye uhusiano?
Mwezi wa pili sasa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mbona mapema, kuna watu hupata mtoto ndani ya miaka sita mpaka kumi ya ndoa.
Okay, tumekuelewa daktari.
Baada ya kupata ukweli wa afya zetu tulirudi kuendelea kumtega mtoto kwa kuzitumia siku zote za hatari ili niweze kumzalia mtoto mzee Sambi. Alionesha ana hamu na mtoto kama uzima kwa mtu aliyesimama mbele ya malaika mtoa roho.
Wakati huo, ujenzi wa nyumba yangu ulikuwa ukiendelea vizuri. Kutokana na ujenzi wake wa kisasa isingewezekana kukamilika kwa miezi miwili. Mafundi walinieleza mpaka nahamia kwangu itachukua miezi saba mpaka nane.
Mwezi wa nne nilifikiria kumpeleka mama kwenye saiti yangu. Sikutaka kufanya kosa kama la awali la kumpeleka mama bila idhini ya mpenzi wangu.
Nilipomuuliza mzee Sambi alikubali nimpeleke kwa vile yule ni mama yangu hata ikiisha lazima angefika. Mwisho wa wiki nilimpeleka nikiwa na mzee Sambi.
Mama alishtuka kuliona jumba lililokuwa kwenye hatua za mwishomwisho. Nilimuona akishtuka lakini aliuficha mshtuko wake. Wakati mzee Sambi akizungumza na mafundi mama alinivuta pembeni na kuniuliza.
Unasema hii nyumba ya nani?
Yangu.
Wewe?
Ndiyo mama, huamini?
Muongo! Unataka kuniambia mzee Sambi ndiye aliyekujengea?
Ndiyo mama, mbona mambo mazuri yanakuja, muda si mrefu nitaacha kazi na kufungua duka langu ambalo lipo katika matengenezo.
Mwezi ujao litajazwa vitu na kulifanyia matangazo kisha nitalifungua.
Mmh! Wapi?
Maeneo ya sehemu ninayokaa.
Hongera.
Asante mama.
Wakati huo mzee Sambi alikuwa amemaliza kuzungumza na mafundi alikuja tuliposimama na kusema:
Mama si ungezunguka kuliona jengo la m wanao?
Nimeliona baba inatosha.
Hapana mama hebu twende ukakague nyumba ya mwanao.
Nilimshika mkono mama na kumzungusha sehemu zote za kiwanja changu na nyuma ya nyumba. Mama aliisifia nyumba yangu na kunifanya nifarijike moyoni.
Baada ya kumuonesha mama nyumba yangu, tulimrudisha mpaka Temeke kisha nilirudi nyumbani kwangu kupumzika. Moyoni nilifurahi mama yangu kuona jumba langu la kifahari, mshtuko aliouonesha nilijua ulitokana na kutoamini macho yake.
***
Pamoja na maisha na malezi mazuri kutoka kwa mpenzi wangu, lakini kuchelewa kupata mtoto kulinikosesha raha. Siku moja nikiwa kazini muda mwingi nilikuwa nimetawaliwa na mawazo kitu kilichomshtua da Suzy.
Mwaija mdogo wangu nakuona haupo sawa, nini kinakusibu?
Ni kweli.
Tatizo nini?
Sikumficha nilimweleza kila kitu kuhusiana na kuchelewa kumzalia mtoto mzee Sambi.
Sasa kama mlionekana hamna tatizo kipi kinachelewesha kupata mtoto?
Hapo ndipo ninapochanganyikiwa.
Mmeshatumia tiba mbadala?
Sasa kama huna tatizo tiba mbadala ya nini?
Mdogo wangu huenda ni chango, ukipata dawa za asili zitakusaidia.
Dada kama lingekuwa chango nisingepata ujauzito.
Mdogo wangu, lazima uangalie na jicho la tatu huenda una chango lisilouma na kusababisha mimba isiingie.
Mmh! Sijawahi kutumia dawa za asili tangu nizaliwe.
Ndiyo unatakiwa ukatumie uone kwani wengi walikuwa na matatizo kama yako leo hii wana watoto.
Hizo dawa nitazipata wapi?
Nitakupeleka kwa mtaalam.
Wapi?
Mbagala Maji Matitu.
Hiyo dawa itanisaidia kweli? niliingiwa na wasiwasi japokuwa nilimuamini sana da Suzy.
Dada nakwambia ndani ya wiki ukitumia kitu hicho.
Shoga nakuahidi nikishika mimba nitakupa milioni moja.
Wee iandae tu, nakuapia mwezi haukatika bila kunasa.
Basi dada naomba unipeleke, nilijikuta nikipata shauku ya kwenda kwa huyo mtaalam ili niweze kumzalia mtoto mzee Sambi.
Hakuna tatizo.
Tulikubaliana mwisho wa wiki anipeleke kwa huyo mganga ili anisaidie kupata mtoto. Maneno ya dada Suzy yalinipa faraja kwa asilimia ndogo.
Mwisho wa wiki nilimpitia dada Suzy na kukodi gari mpaka Mbagala Maji Matitu. Tulipofika tulikwenda moja kwa moja kwa mtaalam aliyekuwa akikaa ndani kidogo kupita kituo kidogo cha polisi cha Maji Matitu. Tulifika kwenye nyumba iliyokuwa imezungushiwa uzio wa makuti. Tuliingia ndani tulikuta watu kama sita wakiwa wamekaa kwenye mkeka na ndani kulikuwa na watu wawili.
Mganga alikuwa akitoka ndani alipotuona alitufuata na kutukaribisha. Alikuwa dada mmoja aliyekuwa na umri wa kawaida, pia hata mavazi yake yalikuwa ya kawaida kuonesha si mganga wa kizamani wa kuvaa kaniki na ngozi.
Alikuwa na umbile fupi na alivaa dela lililompendeza, mikononi mwake alikuwa amevaa pete za rangi ya fedha kila kidole na shingoni alikuwa na mkufu wa rangi ya fedha pia, kichwani alikuwa ameseti nywele, ukimuangalia haraka huwezi kuamini kama ni mganga.
Jamani karibuni, alitukaribisha kwa uchangamfu mkubwa.
Asante dada, tulijibu kwa pamoja.
Samahani jamani, vumilieni kidogo sina kazi kubwa nitawaiteni baada ya muda mfupi.
Hakuna tatizo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mganga alituachia na kuelekea ndani tukiwa tumekaa kwenye benchi lililokuwa pembeni ya mkeka.
Baada ya muda alituita ndani, tuliingia chumbani ambako ndiko kwenye kilinge, kulikuwa na vitu vyake vya kiganga na dawa. Baada ya sisi kuketi mganga alikaa mbele yetu kwenye kigoda na kutulia kwa muda kisha alisema:
Ndiyo, karibuni.
Asante, tulijibu kwa pamoja.
Mna tatizo gani?
Mwenzangu anahitaji mtoto.
Anahitaji vipi? aliuliza huku akitutazama kwa zamu.
Amekwenda hospitali na kuonekana hana tatizo lakini mtoto hapati, alisema da Suzy aliyeonekana mzoefu wa sehemu zile.
Na mwenzake naye alikwenda?
Ndiyo wote wapo sawa.
Basi tumuombe Mungu nina imani dawa nitakazompa zitamsaidia.
Halafu tulitaka kujua talaka yake ya mwanzo ilisababishwa na nini? da Suzy aliuliza kwa niaba yangu.
Hakuna tatizo, mganga alisema huku akinyanyuka na kuchukua lubega wa Kimasai na kujifunga kisha alivaa taji la Kimasai na chini alivaa viatu vya matairi na kushikilia mkuki, pembeni yake alilaza sime.
Nilijikuta nikiingiwa na hofu na kujiuliza alikuwa akitaka kufanya nini lakini dada Suzy hakuonesha wasiwasi wowote.
Baada ya kutulia kwenye kigoda chake alimwita mwanaume aliyekuwa nje ambaye alikuja kukaa pembeni yetu.
Jamani nina imani mwalimu atakayepanda kuna maneno yatakushindeni kuyaelewa. Huyu atawasaidia kuwaelewesheni.
Hakuna tatizo.
Baada ya kusema vile alichoma udi na kuuweka pembeni kisha akashika mkuki wake na kuuinamia kwa muda, akatulia kupandisha jini la Kimasai lililokuwa likiitwa Lukuki.
Heloo habari, alisema baada ya kupandisha, nilitulia tuli kuangalia kwani jambo lile kwangu lilikuwa ndiyo siku ya kwanza.
Nzuri, da Suzy aliitikia.
Alianza kwa kutusalimia kwa kutushika mikono na kugusanisha kichwa chake na kila aliyekuwemo mle ndani.
Alianza kuelezea matatizo yangu huku nikibahatisha mawili matatu yaliyonishinda mkalimani alinisaidia kunifafanulia.
Rafiki una matatizo makubwa sana, matatizo yako si ya leo hata najiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu, kweli?
Ndiyo, ndiyo nilijibu.
Tatizo lako limeanza baada ya ndoa yako, ikiwa pamoja na kuharibikiwa mimba, mume kuharibikiwa maisha na kukosa kazi. Kuharibikiwa maisha na kila kitu kusimama ni kweli? mganga aliniuliza, yote aliyosema yalikuwa ni ya kweli alikuwa kama mtu anayejua maisha yangu.
Ni kweli, nilikubali.
Mumeo aliondoka na aliporudi alikupa talaka isiyo na maelezo ni kweli?
Ndiyo ila alisema mama anajua.
Tatizo lako nitakutibu wala sitaki kulichimba sana kwa vile nitazalisha visivyotakiwa, kingine unatafuta mtoto bila mafanikio japo huna tatizo lolote, ni kweli?
Kwa nini usinieleze mbaya wangu? nilitaka kujua.
Huna moyo huo wa kusikia vitu vizito vilivyo kuzunguka, ila nakuahidi kukutibu na kukuondoa vifungo ulivyofungwa.
Tatizo lako nitakutibu wala sitaki kulichimba sana kwa vile nitazalisha visivyotakiwa, kingine unatafuta mtoto bila mafanikio japo huna tatizo lolote, ni kweli?
Kwa nini usinieleze mbaya wangu? nilitaka kujua.
Huna moyo huo wa kusikia vitu vizito vilivyokuzunguka, ila nakuahidi kukutibu na kukuondoa vifungo ulivyofungwa. Hivyo ndivyo vilivyosababisha upewe talaka, mshindwe kumaliza nyumba yenu na mumeo awe na maisha magumu, pia usishike ujauzito, ungemeza kila aina ya dawa bila ya mafanikio.
Mungu wangu! Na nani? nilishtuka kusikia habari zile zilizokuwa zinafanana na maneno ya mume wangu.
Matatizo yako siwezi kukueleza nani ameyasababisha kwa vile najua wanadamu mna mioyo midogo, ila naweza kukutibu. Kwa kukufungua vifungo hivyo kwa uwezo wa Mungu utashika ujauzito tu.
Nitashukuru.
Leo nitakupa dawa ya kuoga ila kesho njoo asubuhi nitakuosha nuksi, pia kukufungua vifungo na kukupa dawa ya kunywa. Mwezi haufiki utashika ujauzito.
Nitashukuru.
Kesho njoo na pea mbili za khanga mpya za kukuoshea.
Sawa.
Baada ya kunipa maelezo ya kina kuhusu maisha yangu na kumruhusu jini la Kimasai kuondoka. Yule dada alirudi katika hali ya kawaida na kuelezwa yote aliyosema Lukuki.
Alinipa dawa ya kuoga na kutakiwa siku ya pili asubuhi na mapema sana nifike kwa mganga ili nifanyiwe tiba yangu kwanza. Nilirudi nyumbani nikiwa bado siamini kama kweli kupitia dawa za yule dada nitapona na kupata mtoto.
Nilipofika nyumbani nilijipumzisha kwenye kochi huku msichana wa kazi akiniletea juisi. Baada ya kunywa nilikwenda chumbani na kujifungia ili kupumzisha akili yangu kutokana na kuzongwa na mawazo mengi. Sikutaka kelele za aina yoyote, nilishukuru siku ile mzee wangu alikuwa amesafiri na kupata uhuru mkubwa wa kutulia.
Kichwa kilikuwa kizito kutokana na kugubikwa na mawazo mazito yaliyojifungafunga na kunifanya nishindwe kuelewa niliyoelezwa kama yana ukweli kwa asilimia kubwa.
Swali likabakia nani mtendaji wa ubaya ule. Kila nililoliwaza lilikuwa halikubaliki na kuona kama najichanganya kwa kufikiria vitu ambavyo hata kwa mtutu visingewezekana.
Mpaka usiku unaingia bado nilikuwa kwenye fumbo zito, chakula kilinishinda na kunifanya nipande kitandani mapema. Nilikumbuka nilitakiwa kuoga dawa nilizopewa na mganga. Nilikwenda bafuni na kujimwagia maji ya dawa mwili mzima na kupanda kitandani kujilaza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Usingizi ulikuwa mbali nilijikuta nikiwa na mawazo mengi kuhusiana na maelezo ya mganga kwa kuijua historia yangu kama vile nilimhadithia na kuona hata ujauzito wangu haukuharibika kwa amri ya Mungu bali kulikuwa na mkono wa mtu.
Hata kuvurugikiwa maisha na kupewa talaka yenye utata na fumbo zito kulikuwa na sababu ambayo bado nilifichwa.
Maneno ya mganga yalizidi kunichanganya sana baada ya kurudia kusema siri nzito za moyoni mwangu ambazo nyingine hata dada Suzy sikuwahi kumwambia.
Pamoja na kunieleza sababu ya kuharibikiwa maisha na kuniahidi kunisaidia kwa kunifungua vifungo vyote, bado nilibakia na swali ni nani aliyenifanyia hivyo.
Nilijikuta nikiyakumbuka maneno ya mtalaka wangu na kuamini alichokisema, nikaon alikuwa na sababu ya kunipa talaka. Lakini nilijikuta nikiendelea kumlaumu kama alijua kuna mtu katia mkono kwa nini hakuniambia aliyetenda vile.
Hata kama ni mama yangu mzazi, japokuwa jambo hilo nililipinga kwa nguvu zangu zote, bado niliamini sikuwa na kosa la kupewa talaka.
Nilijikuta nikiwaza peke yangu:
Mmh! Inawezekana kweli aliyefanya vile ni mama yangu mzazi? Hapana ...hapana... mama yangu mzazi hawezi kufanya kitu hicho, afanye ili iwe nini? nilijiuliza.
Wazo la mama yangu mzazi ndiye aliyenifanyia mchezo ule nililikataa kwa nguvu zote. Swali lililoniumiza akili lilikuwa kwa nini mtalaka wangu alisema mama ndiye anayejua kila kitu alikuwa na maana gani?
Nilijiuliza nani aliyenifunga au dada zangu kwa wivu wa mimi kuolewa? Lakini mbona wao waliolewa na kuachika iweje wanionee wivu?
Kwa kweli kila nililolifikiria kwangu lilikuwa zito kiasi cha kutaka kunipasua kichwa. Usingizi ulinipitia baada ya kukaa sana kitandani na kushtuka siku ya pili baada ya kupigiwa simu. Nilipoangalia nilikuta ni da Suzy ndiye aliyenipigia.
Niliangalia saa ya juu ya droo ya kitanda na kuona kumekucha ilikuwa saa moja kasoro. Niliichukua simu huku kichwa kikiwa kizito kutokana na mawazo kunizidi uwezo, pia kutokana na kuchelewa kulala.
Haloo da Suzy.
Abee, vipi umeshatoka nyumbani?
Dada wee acha tu, yaani simu yako ndiyo iliyonishtua usingizini, bila hivyo sijui ningeamka saa ngapi?
Kwani mzee leo kalala nyumbani?
Walaa, mawazo tu dada yangu.
Lakini yule dada si kasema atakusaidia?
Ni kweli lakini maneno aliyosema mganga na aliyosema Beka yanafanana lazima niseme ukweli nimechanganyikiwa sana ninaposhindwa kumjua mbaya wangu.
Mdogo wangu yote hayo yataisha, kwanza mshukuru Mungu umeachwa na Beka lakini sasa hivi una maisha mazuri. Wengine wakiharibikiwa huwa wanachanganyikiwa na kukata tamaa ya maisha, kwani wanaandamwa na mikosi kila kukicha.
Mmh! Sawa.
Basi usiyape sana nafasi mawazo yanayoumiza, sisi tusingekuwa hapa.
Lakini nani kanifanyia hivi?
Mwaija hebu kwanza kaoge ili tuwahi kwa mganga.
Sawa.
Nilinyanyuka kitandani na kwenda kuoga harakaharaka na kutoka kumuwahi da Suzy. Sikutaka hata kufungua kinywa kwa vile nilikuwa nyuma ya muda tuliokubaliana kufika kwa mganga.
Dada chai tayari, msichana wa kazi alinishtua aliponiona naondoka bila ya kufungua kinywa.
Mmh! Mdogo wangu kuna sehemu nimechelewa nitakunywa nikirudi.
Sawa dada lakini ungekunywa hata nusu kikombe cha maziwa ya moto?
Nisamehe mpenzi nimechelewa sana.
Sawa dada.
Nilitoka hadi barabarani na kukodi teksi mpaka Changombe kwa Da Suzy, niliyempitia kuelekea kwa mtaalam Mbagala Maji Matitu. Kabla ya kufika tulisimama sehemu na kununua doti mbili za kanga mpya nilizoagizwa na mganga.
Tulipokelewa na mganga aliyekuwa na wateja wengi zaidi ya jana yake.
Nilijikuta nikijawa na mawazo mengi kichwani na kujiuliza uwepo wa watu wengi pale ulitokana na nini!.
Nilipomuuliza da Suzy aliniambia ukiona watu wengi ujue ni ubora wa tiba zake umewavuta.
Yule dada alipotuona alitukaribisha kwa furaha kwani siku zote uso wake ulijaa ucheshi. Baada ya kutukaribisha mganga alituchukua na kutupeleka katika chumba kimoja kilichokuwa kimejengwa peke yake ndani ya uzio wa nyumba yake na kutueleza:
Jamani nisubirini hapa kila kitu nimekiandaa kwa kazi yenu. Ngoja nikaandae kisha nitawaita.
Hakuna tatizo.
Mganga aliondoka na kutuacha tukiwa tumekaa kwenye kochi la mbao lililokuwa halina mito tulilolikuta nyuma ya nyumba.
Baada ya muda aliniita, nikaingia ndani ambapo yule mganga aliniambia niingie chumbani.
Nilipoingia alinieleza nivue nguo zote kisha nijifunge upande mmoja wa kanga na mwingine nijifunge kichwani kama kilemba.
Baada ya kufanya hivyo, alinipeleka kwenye bafu lililokuwa pale uani na kunieleza nikae kwenye stuli.
Pembeni ya stuli kulikuwa na beseni lililokuwa na maji na kamba za ukindu saba zilizofungwa na dawa ya unga kama aliyonipa jana yake nikaweke kwenye maji ya kuoga.
Tukiwa bafuni, alisimama nyuma yangu na kunishika katikati ya kichwa na kuzungumza maneno anayojua, lakini yote yakiwa kumuomba Mungu kunifungua katika matatizo yangu na kuisafisha nyota yangu iliyofifia.
Nyota yangu Ilikuwa imeingia ukungu na kushindwa kutoa mwanga wake halisi.
Baada ya kusema kwa muda maneno hayo, alitoa mkono kichwani mwangu na kunimwagia maji kwa kutumia kata kuanzia kichwani huku akisema maneno kisha mikononi na kumalizia miguuni.
Alinimwagia juu ya kanga niliyokuwa nimejifunika kisha mwili wote.
Baada ya kunimwagia maji mwili mzima kwa kumwagia juu ya kanga nilizojifunga aliiondoa kanga ya kichwani na kuchukua ukindu mmojammoja uliofungwa na kuzungusha kwenye mikono na kuufyatua.
Alifanya vile kwa sehemu za viungo vya mwili ambavyo wanasema ndimo watu wanatumia kuingiza uchawi wao kama kwenye magoti, kifuani na kiunoni.
Kufungua kamba za ukindu alikuwa akifungua vifungo mwilini mwangu. Baada kumaliza zoezi lile alinieleza nioge maji yaliyobaki mwili mzima bila nguo kisha yeye alitoka nje.
Niliondoa nguo mwilini na kuoga mwili nzima, wakati huo alikuwa amekwenda ndani kisha alirudi akiwa na kanga nyingine mpya na kunieleza nikimaliza nivae zile na nilizoogea alinieleza nizianike bila kuzikamua.
Nilifanya kama alivyonieleza na kutoka nje nikiwa nimejifunga kanga mpya, kisha niliingia kilingeni. Nilielezwa nivae nguo zangu.
Nilifanya vile na kukaa kwenye mkeka na kupata dua, nilipewa makombe ya kunywa na kuoga kwa siku tatu na miti ya kuchemsha kwa ajili ya kukifungua kizazi na dawa ya kunawa kabla ya kukutana na mwenzangu.
Nilitoa kiasi alichonieleza huku nikimuahidi nikishika ujauzito nitampa zawadi kubwa sana.
Mdogo wangu tumuombe Mungu kila kitu kitakwenda vizuri.
Niliagana na mganga na kumpitia da Suzy aliyekuwa bado nyuma ya nyumba ameegemea ukutani na kushikwa na usingizi.
Da Suzy, nilimwita huku nikimtikisa.
Abee, vipi tayari? alishtuka usingizini na kufikicha macho huku akipiga miayo.
Ndiyo twende zetu.
Mmh! Usingizi ulianza kuninyemelea.
Basi twende zetu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mmh! alinyanyuka na kujinyoosha kisha akasema:
Acha nikamuage mama Amina, mama Amina lilikuwa jina la mganga.
Kabla hatujaenda mgang alikuja na kusema alisahau kitu.
Samahani kuna kitu muhimu nilitaka kukisahau kukuelezea.
Kitu gani? Nilimuuliza.
Ukishika ujauzito njoo mara moja tufunge ili usiweze kutoka.
Sawa dada nimekuelewa nitafanya hivyo.
Tuliagana na mganga na kwenda kutafuta usafiri. Kwa vile tulikuwa hatujala tulitafuta sehemu ya kupata kifungua kinywa kisha nilimpeleka da Suzy kwake na kurudi zangu kwangu.
Kutokana na uchovu nilipofika nyumbani nilipanda kitandani na usingizi mzito ulinichukua.
***
Nilitumia zile dawa kwa siku tatu kwa umakini mkubwa na kumaliza. Baada ya kumaliza kutumia makombe na dawa za kunywa nilikaa kusubiri matokeo ya dawa zile japokuwa sikuwa na uhakika wa kushika ujauzito kama nilivyoahidiwa na mganga.
Baada ya siku nne mzee Sambi alirudi, niliamini ule ulikuwa muda muhimu kutega mtoto.
Usiku kabla ya kukutana naye, nilifanya kama nilivyoelekezwa na mganga.
Nilifanya vile kisha tulikutana na mwenzangu, niliendelea kufanya zoezi hilo kwa wiki nzima huku nikiwa na matumaini madogo ya kushika ujauzito.
Mwezi ulikatika huku duka langu likiwa tayari limejazwa vitu vyote vya muhimu na kuanza kulifanyia matangazo kwenye magazeti na kwenye baadhi ya redio.
***
Kupitiliza kuziona siku zangu kulinishtua lakini bado sikuamini kwa kuwa hali kama hiyo ilishawahi kunitokea hata nilipokuwa na mume wangu kwa kupitiliza miezi miwili, lakini mwezi wa tatu niliziona siku zangu na ziliendelea kama kawaida.
Mabadiliko ya hali yangu yalinishtua kidogo, nilimweleza mwenzangu ambaye alinishauri twende hospitali kuangalia afya yangu.
Tulikwenda kufanya vipimo, baada ya daktari kuangalia majibu alisema:
Vipimo vinaonesha upo sawa, ila...
Alishusha pumzi na kututazama usoni na kutabasamu kitu kilichonifanya nijiulize mbona anatabasamu ameona nini.
Ila nini dokta...? mzee Sambi aliuliza wakati huo nilikuwa nimemuegemea begani.
Hongereni.
Hongera ya nini? mzee Sambi aliuliza.
Inaonekana mambo si mabaya.
Kivipi? safari ile niliuliza mimi.
Inaonesha wewe ni mjamzito.
Nooo...nooo, nilijikuta nikitikisa kichwa kukataa kama vile dokta ni muongo.
Kwa nini unakataa? aliniuliza akinishangaa.
Hata siamini.
Kwa nini huamini.
Nimeitafuta sana mimba, siamini kama kweli Mungu kasikiliza maombi yangu.
Basi mama hongera sana kweli una ujauzito.
Nashukuru Mungu, nilisema kwa sauti ya kilio, furaha ya ujauzito ilinifanya niangue kilio cha kwikwi.
Basi mpenzi, tumshukuru Mungu kwa kila jambo, mzee Sambi alinibembeleza.
Baada ya maelezo ya daktari jinsi ya kuitunza mimba changa tulirudi nyumbani. Njiani nilibakia na maswali ujauzito ule ni kudra za Mungu au dawa za mganga mama Amina ambaye naye alimuomba Mungu?
Lakini kwa upande mwingine nilikubaliana kuwa mama Amina ni mganga wa kweli kwa jinsi alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa. Nilipanga kumpelekea zawadi kubwa kwa ujauzito ule, pia zawadi nyingine kama nikijifungua.
Kwa kweli ilikuwa furaha kubwa moyoni mwangu kushika ujauzito. Nilipofika nyumbani nilimjulisha da Suzy ambaye naye alifurahi sana. Nilimsikia akipiga vigelegele upande wa pili kuonesha naye alifurahia shoga yake kupata ujauzito.
Ujauzito wangu ulifanya nigeuke malkia kwa mzee Sambi, muda mwingi alihakikisha yupo karibu yangu huku akihakikisha sifanyi kazi yoyote ngumu mpaka nitakapojifungua.
Nilimfikishia taarifa mama kuhusiana na ujauzito wangu, alifurahi sana mwanaye kupata ujauzito. Furaha ya mama ilinifariji na kujisikia faraja moyoni mwangu.
Mwaija angalie usirudie makosa ya awali ya kupoteza ujauzito wako, mama alinionya.
Mama sasa hivi nazingatia maelekezo ya madaktari ili kuifanya mimba yangu ikue vizuri.
Kama hivyo ni vizuri, mama yako nina hamu ya mjukuu.
Najua mama, tumuombe Mungu akupe mjukuu.
Inshaallah.
Ukaribu wa mzee Sambi uliongezeka, muda mwingi hakucheza mbali na mimi huku akiniahidi ujauzito ukifika miezi minne angenipeleka Afrika Kusini na kukaa huko mpaka nitakapojifungua.
Mwaija, katika kitu ambacho nilikiomba usiku na mchana basi ni hiki cha wewe kubeba ujauzito. Ujauzito ukifikisha miezi minne nakupeleka Afrika Kusini ambako utakaa mpaka utakapojifungua.
Kwani hapa kuna nini?
Katika kitu chenye thamani chini ya jua, ni hilo tumbo lako ambalo nataka nilitunze kuliko hata mboni za macho yangu.
Mpenzi unataka mtoto gani?
Japokuwa nataka wa kiume lakini yeyote atakayezaliwa ni zawadi yangu.
Ukaribu wa mzee Sambi ulinifanya nikose muda wa kurudi kwa mganga kumueleza matokeo ya dawa aliyonipa ilinisaidia kushika ujauzito. Sikupenda kumweleza bwana angu kuwa ujauzito wangu ulipatikana kupitia kwa mganga.
Wakati huo mzee Sambi alikuwa ameninunulia Rav 4 kwa ajili ya kunipeleka popote kama hayupo. Kwa vile nilikuwa sijajua kuendesha gari vizuri alinitafutia dereva kijana mmoja jirani yetu.
Muda mwingi alikuwa kijiweni nikiwa na shida nilimpigia na kuja mara moja kunisikiliza. Niliendelea kuona neema ya Mungu ikinifungukia kwa mambo yangu kuninyookea.
Miezi miwili ilikatika huku maendeleo kwenye ujenzi wangu yakipungua kasi japokuwa ilikuwa kwenye hatua za kumalizia. Mzee Sambi alinieleza nisiwe na wasiwasi muda si mrefu nyumba yangu itaisha.
Hali yangu ya ujauzito ilifanya niwe mtu wa kupumzika nyumbani, hata kwenye super market yangu nilichelewa kuifungua mpaka hali yangu itakapokuwa vizuri, lakini kwa shauku ya mtoto aliyokuwa nayo mzee Sambi niliona mpaka nitakapojifungua.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hospitali walisema tatizo la kuchoka sana litaisha baada ya ujauzito kukua, ile hali ilikuwa ya mpito. Pamoja na kuwa nachoka lakini nilipata huduma zote muhimu.
Mzee Sambi alihamia kwangu kwa wiki mbili akinieleza ameaga kwa mkewe amesafiri kikazi. Mtoto wa kike nilinenepa, mbona nilideka! Nini nilichokitaka nikakosa.
Siku moja nikiwa nimejipumzisha nyumbani, msichana wangu wa kazi alinieleza kuna mgeni nje.
Dada kuna mgeni.
Mwanaume au mwanamke?
Mwanamke wa makamo.
Mwambie aingie.
Baada ya muda aliingia mama mmoja aliyekuwa amevaa gauni la kitenge na kitenge kingine alijifunga chini na juu alivaa kilemba.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment