Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

MAMA YANGU ADUI YANGU - 4

 





    Simulizi : Mama Yangu Adui Yangu

    Sehemu Ya Nne (4)



    Vazi lile lilikuwa limempendeza sana yule mama ambaye alikuwa na umri wa dada zangu.

    "Karibu dada," nilimkaribisha nikiwa nimejilaza kwenye kochi.

    "Asante," alijibu na kwenda kukaa kwenye kochi lililokuwa likitazamana na kochi langu.

    "Shikamoo," nilimwamkia huku nikijitahidi kukaa kitako.

    "Marahaba, za hapa?"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mmh! Nzuri, karibu."

    "Asante, mzee Sambi nimemkuta?"

    "Ametoka."

    "Ametoka saa ngapi?" aliniuliza huku akitembeza macho kila kona ya nyumba kama anakagua kitu.

    "Asubuhi lakini hachelewi kurudi."

    "Samahani mama unatumia kinywaji gani?" msichana wangu wa kazi alimuuliza mgeni.

    "Asante, situmii kitu," mgeni alishukuru. Nilipomuangalia kwa chati mkononi alikuwa ameshika ufunguo wa gari, pia alikuwa na mkufu na hereni za dhahabu na mkononi alikuwa na pete katika vidole vitatu, hakika yule mama alikuwa anaonekana ni mtu mwenye maisha mazuri.

    "Mama yangu ungekunywa hata juisi basi," nilimbembeleza mgeni.

    "Usihofu, siku nyingine."

    "Ulikuwa na shida gani?"

    "Aah! Basi nitaonana naye."

    "Kwa hiyo akija nimwambie nani aliyekuja?"

    "Nitamuona tu wala usihofu, naomba niwakimbie."

    "Japokuwa hukutaka kutuambia wewe ni nani, nikuruhusu dada yangu."

    Yule mama alinyanyuka na kutoka na kuniacha nikimsindikiza kwa macho. Baada ya kutoka nilijiuliza yule ni nani aliyekuja kumuulizia mzee Sambi.

    Alikuwa mtu wa kwanza kuja kumuulizia mzee Sambi tangu nihamie pale, wazo la haraka lilikuwa labda mwenye nyumba ambaye nilielezwa kwamba ni mwanamke ambaye hakai maeneo yale.

    Nilijiuliza alikuwa na shida gani kwani kodi yake alishalipwa ya mwaka mzima. Niliachana naye na kuendelea na yangu.

    Muda mfupi baada ya yule mama kuondoka, aliingia mzee Sambi. Kama kawaida nilimpokea kwa kujilazimisha huku akinikataza kunyanyuka.

    "Aah! Tulia unaenda wapi mpenzi?"

    "Mpenzi unafikiri nisipofanya mazoezi si nitalemaa ulimsikia daktari alivyosema?"

    "Asubuhi si ulifanya, pumzika sitaki uteseke."

    "Sawa, lakini kukupokea ni moja ya mazoezi siyo mateso."

    "Haya mpenzi."

    Baada ya kupumzika nilimweleza kuhusu yule mgeni aliyefika kumuulizia muda mfupi kabla hajarejea.

    "Mpenzi kuna mtu alikuja kukuulizia."

    " Mtu?"

    "Ndiyo."

    "Alikuja kuniulizia hapa?"

    "Ndiyo."

    "Mmh! Mtu gani huyo anayejua naishi hapa?"

    "Kuna mama mmoja alikuja kukuulizia, inawezekana ni mwenye nyumba wako."

    "Mmh! Ana shida gani namba yangu ya simu si anayo!"

    "Mi nitajuaje."

    "Amesemaje?"

    "Amesema mtaonana baadaye."

    "Hakuacha ujumbe wowote?"

    "Hakuacha."

    "Kwani yupo vipi?"

    "Mrefu mweusi, amevaa vitenge kuanzia juu mpaka chini."

    "Ana mwanya?"

    "Ndiyo."

    "Na ana meno mawili ya dhahabu?"

    "Ndiyo, una mfahamu?"

    "Ndiyo."

    "Ni nani?"

    "Achana naye ni mwenye nyumba."

    "Sasa mbona amekuja bila taarifa?"

    "Nitaonana naye, kama ana shida lazima atanipigia tu."

    "Mmh! Inaonekana mwenye nyumba anajipenda sana."

    "Kawaida, baada ya kuniuliza ukamjibu sipo alisema kitu gani kingine?"

    "Amesema mtaonana."

    "Ni hilo tu?"

    "Ndiyo."

    "Mmh! Sawa."

    "Kwani vipi mbona kama umeshtuka?"

    "Kawaida tu."

    Sikutaka kumuuliza sana niliamini yule ni mama mwenye nyumba. Usiku wa siku ile aliniaga kurudi kwake japokuwa awali alipanga kurudi jioni ya siku ya pili.

    "Vipi mbona ghafla?" nilimuuliza.

    "Hapana kesho nitarudi."

    Pia, sikutaka kumzuia kwa vile nilikuwa naye kwangu kwa wiki moja na nusu kitu ambacho kilikuwa hakijatokea, siku za nyuma alikuwa akilala mara mojamoja na kuondoka siku ya pili.

    ***

    Ilikuwa ajabu baada ya mzee Sambi kuondoka ilipita wiki bila kufika kwangu kitu ambacho hakikuwa cha kawaida. Baada ya wiki moja ndipo alikuja. Vilevile sikutaka kumuuliza niliamini ni mihangaiko na nilizingatia ni mume wa mtu.

    Siku aliyokuja tulikutana faragha na saa tano aliondoka kwenda kwake. Nilala vizuri mpaka asubuhi wakati huo nilikuwa nalala na msichana wa kazi kwa ajili ya msaada wa usiku.

    Siku ya pili nilipoamka nilipokwenda kuoga nilishtuka kukuta kwenye nguo ya ndani kuna damu kidogo. Haikunishtua sana japokuwa nilijiuliza damu ile ilitokana na nini!

    Sikutaka kukaa kimya nilimjulisha mzee Sambi kuhusiana na hali niliyoikuta asubuhi.

    "Mmh! Au jana nimetumia nguvu?"

    "Walaa, kawaida, mbona nipo sawa tu ila kilichonishtua ni damu kidogo kwenye nguo ya ndani."

    "Unasikia mabadiliko yoyote mwilini?"

    "Nipo sawa."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Fanya hivi fika hospitali mara moja mi nitakuja baadaye ila nijulishe maendeleo yako."

    "Hakuna tatizo."

    "Basi fanya hivyo."

    Baada ya kuzungumza na mzee wangu nilioga na kumpigia dereva aliyekuwa akinisaidia kunipeleka popote kwa vile nilikuwa sijajua vizuri gari, pia kutokana na hali yangu ya ujauzito sikutaka kuendesha.

    Baada ya kufika nilimweleza anipeleke hospitali.

    Sele alinipeleka mpaka Hospitali ya Madona iliyopo Tabata Aroma. Nilipofika nilimweleza daktari hali niliyokutana nayo asubuhi naye alishtuka sana. Lakini baada ya kunifanyia vipimo ilionesha hakukuwa na athari zozote kwenye ujauzito wangu.

    Alinipa dawa na kunieleza nisifanye kazi yoyote ngumu kwa kipindi kile. Nilimshukuru Mungu kukuta ujauzito wangu ukiwa salama. Jioni alipokuja mzee Sambi nilimweleza niliyoelezwa hospitali kuhusu ujauzito wangu.

    Alinipa dawa na kunieleza nisifanye kazi yoyote ngumu kwa kipindi kile.

    "Nina wasiwasi labda nilitumia nguvu bila kujua."

    "Mmh! Labda, sasa tutafanyaje?"

    "Itabidi tuvumilie mpaka hali itakapokuwa sawa."

    Tulikubaliana kutokutana kimwili kwa kipindi kile. Kwa vile muda wake wa kuwepo kwangu uliisha saa nne usiku aliondoka. Kama kawaida niliendelea kulala na msichana wangu wa kazi ambaye alikuwa mtu muhimu sana kwangu kwa kipindi hicho.





    Siku ya pili nilipoamka, kabla ya yote niliangalia nguo yangu ya ndani na kukuta tena damu kidogo. Lakini ya siku ile ilizidi kidogo ya jana yake.

    Nilishtuka sana na kumpigia simu daktari mmoja shoga yangu aliyekuwa serikalini ambaye pia alikuwa akifanya kazi kwenye hospitali binafsi ambaye tulianza naye urafiki nilipokuwa dukani.

    Baada ya simu kuita kwa muda, ilipokelewa upande wa pili, nilimweleza hali yangu. Alishtuka baada ya kumweleza kuwa ni mjamzito lakini natokwa damu kidogo hasa usiku nikilala.

    "Unataka kuniambia baada ya kuiona hiyo damu huendelea kutoka kama upo kwenye siku zako?"

    "Hapana, ikitoka mara moja basi mpaka siku ya pili asubuhi kitu ambacho sikielewi."

    "Unasema ya leo imezidi kidogo tofauti na ya jana?"

    "Ndiyo."

    "Mmh! Itakuwa nini? Mtu uwe na ujauzito halafu damu zitoke? Kuna kitu chochote ulichokifanya ambacho kinaweza kusababisha hali hiyo?"

    "Juzi usiku nakumbuka nilikutana kimwili na mwenzangu."

    "Hamkutumia nguvu katika tendo?"

    "Wala, kawaida tu."

    "Tumbo unalisikiaje?"

    "Lipo kawaida tu."

    "Haliumi?"

    "Haliumi."

    "Hebu njoo hospitali mara moja tufanye uchunguzi wa kina."

    "Sawa nakuja."

    Nilikata simu na kumueleza msichana wangu wa kazi hali iliyonitokea, ambaye jana yake sikumweleza ile hali. Baada ya kumweleza alishtuka.

    "Dada kuwa makini, damu itatoka vipi ikiwa tayari una ujauzito, tumbo linauma?" naye aliniuliza kama daktari.

    "Walaa."

    "Sasa kitakuwa nini?"

    "Hata najua? Naona maluweluwe tu."

    "Unasema jana ulikwenda hospitali na kuambiwa hakuna tatizo? Basi hebu isikilizie hali na leo kama itazidi basi urudi hospitali," alinipa ushauri.

    "Hapana, kuna daktari wangu mmoja ameniambia niende leo."

    "Dada kama kurudi si ungerudi kwa daktari aliyekutibu jana kuliko kubadili?"

    "Siyo mbaya, siendi kwenye tiba bali kufanya uchunguzi wa kina ili kujua hali hii inasababishwa na nini."

    "Kama ni hivyo hakuna tatizo."

    "Ngoja nimjulishe shemeji yako."

    "Bado hujamwambia?"

    "Bado, nilitaka kwanza kupata maelezo ya kitaalamu kwa vile ilinitisha. Kwa vile natoka nitampigia na Sele aje anichukue."

    Nilimpigia simu mzee Sambi na kumweleza hali iliyonitokea asubuhi, alishtuka na kunieleza nirudi hospitali.

    "Duh! Sasa ni nini hicho?"

    "Yaani hata mwenyewe nashangaa."

    "Tumbo linauma?"

    "Lipo kawaida."

    "Basi ungerudi Madona."

    "Nakwenda kwa Dokta Hindu."

    "Si mbaya inabidi afanye vipimo vya kina ili tujue tatizo nini na tiba yake ifanyike haraka."

    "Sawa mpenzi."

    Nilikata simu na kumpigia dereva anifuate asubuhi ile. Nilikwenda kuoga na kujiandaa kwenda hospitali. Baada ya kufungua kinywa nilielekea kwa Dokta Hindu aliyekuwa mtaalamu wa magonjwa ya wanawake.

    Nilisahau kuwaeleza kitu kimoja kuhusu da' Suzy, wakati huo alikuwa amepata bwana na kuamua kuacha kazi pale Super Market. Kitu kingine kilichosababisha aache kazi kilikuwa ugomvi kati yake na Meneja Emma, bwana‘ake wa zamani waliyeachana.

    Kutokana na habari nilizopewa, Meneja Emma baada ya kujua da' Suzy ana bwana mwingine tena mwenye uwezo ambaye alikuwa akimpitia baada ya kazi, roho ilimuuma.

    Kitendo kile kilimuumiza sana Emma na kutaka kutumia ubosi wake kurudisha uhusiano wa zamani, kitu kilichosababisha usumbufu kwa da' Suzy na kuamua kuacha kazi.

    Hata baada ya kuacha kazi, bado aliendelea kupata usumbufu toka kwa Emma wa kupigiwa simu bila kuzingatia yupo wapi na nani. Pia alikuwa akimtumia ujumbe wa vitisho kitu kilichosababisha kubadili namba yake ya simu ambayo mimi sikuwa nayo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taarifa hizo nakumbuka nilipewa na mmoja ya wasichana tuliokuwa tunafanya kazi pamoja aliyekuwa akiendelea na kazi.

    Kwa kipindi kile sikuwa na shida naye kwa vile nilijua ana namba yangu lazima angenipigia na kunipa michapo yote. Niliamini alichokifanya kilikuwa na maslahi kwake.

    Baada ya dereva kuja alinichukua na kunipeleka hospitali. Nilipofika nilikuta wagonjwa wengi, nilisubiri kwa saa nzima ndipo nilipopata nafasi ya kuonana na Dokta Hindu.



    “Mwaija usione nimekuweka shoga yangu, nilitaka niwapunguze watu ili nipate nafasi nzuri ya kuzungumza na wewe kwa kina.”

    “Hakuna tatizo shoga yangu.”

    Sikuwa na maelezo mengine ya kumueleza zaidi ya yale niliyomwambia kwenye simu. Baada ya kuniuliza maswali alinifanyia vipimo vyote kisha alipima ujauzito wangu na kukuta kila kitu kikiwa sawa.

    “Mmh! Sasa hiki kitakuwa nini?” dokta Hindu alishtuka.

    “Hata najua!”

    “Kila kitu kinaonesha kipo sawa, ujauzito pia uko sawa, inawezekana ni hali ya kawaida ambayo haiathiri kitu.”

    “Nina wasiwasi hali hii inaweza kuendelea.”

    “Mmh! Sidhani kwa vile nimecheki hakuna dalili zozote za damu kuendelea kutoka.”

    “Mmh! Ilinitisha sana.”

    “Ondoa wasiwasi ujauzito wako upo sawa hata viungo vya karibu na mfuko wa uzazi vipo sawa.”

    Baada ya kuona hakuna tatizo nilirudi nyumbani kidogo moyo wangu ulikuwa umetulia. Wazo la kumwambia mama nilikuwa nalo lakini kutokana na maelezo ya daktari niliamini huenda damu iliyotoka usiku wa kuamkia siku ile ilikuwa ya mwisho.

    Nilirudi nyumba na kujipumzisha huku msichana wangu wa kazi akitaka kujua majibu ya hospitali.

    “Vipi dada za huko?”

    “Mmh! Nzuri, majibu ni yaleyale.”

    “Unamaanisha nini?”

    “Hakuna tatizo.”

    “Sasa na hizo damu?”

    “Inaonekana zimekata.”

    “Ooh! Afadhali yaani hata mimi nilikuwa na wasiwasi sana.”

    “Nashukuru kuguswa na matatizo yangu.”

    “Yaani dada wewe kama Mungu wangu.”

    “Aah! Hapana siwezi kuwa Mungu wako.”

    “Kweli dada umeniokoa kwenye mateso.”

    “Pamoja na hilo, lakini nitabakia kuwa mwanadamu wa kawaida,” pamoja na wema wangu niliamini siwezi kufikia hata robo ya utukufu wa mitume nini Mungu!

    “Basi wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”

    “Hapo sawa.”

    Kwa vile alikuwa ameniandalia juisi alinipatia na kunywa kisha nilijipumzisha. Siku ile nilishinda katika hali nzuri japokuwa wasiwasi wangu ulikuwa ni kuumwa na tumbo, lakini hali ile haikujitokeza mpaka jioni ilipoingia.

    Usiku ulipofika nililala vizuri mpaka siku ya pili. Nilipoamka cha kwanza kilikuwa kuangalia nguo ya ndani ambayo nilishangaa kuikuta ikiwa safi. Nilijichunguza na kujiona nilikuwa sawa, nilikwenda kuoga na kuisikilizia ile hali ambayo pia siku ilikatika nikiwa sawa. Mchana wa siku ile dokta Hindu alinipigia simu kutaka kujua maendeleo ya hali yangu nikamjulisha kwamba nilikuwa nikiendelea vizuri.

    Sikujiamini moja kwa moja niliendelea kuisikilizia hali ile kwa siku tatu bila kuona mabadiliko.

    Wiki ilipokatika bila kuiona damu, niliamini kuwa nimepona na tatizo lile limeisha.

    Baada ya wiki ya pili kukatika nikiwa katika hali nzuri, niliamini naweza kukutana kimwili na mpenzi wangu.

    Kama kawaida siku hiyo alikuja jioni kabla ya kuondoka nilimuomba akidhi haja zangu.

    Japokuwa alitaka tuendelee kusubiri mpaka mwezi ukatike lakini nilimhakikishia kwamba nilikuwa sawa. Alinikubalia na tukakutana, safari ya kwanza tulienda vizuri.

    Safari ya pili tukiwa katikati ya tendo nilihisi tumbo likivurugika kama vile nilikuwa nikitaka kuhara na nikamuomba mzee Sambi anyanyuke kwanza.

    “Samahani mpenzi hebu toka.”

    “Kuna nini?”

    “Tumbo limenivurugika ghafla.”

    Aliponyanyuka nilihisi kama nimeshikwa na haja ndogo. Nilikimbilia msalani na kuchutama na kusukuma kwa nguvu.

    Ajabu haja ndogo iligoma kutoka lakini maumivu ya kutaka kujisaidia yalikuwa makali.

    Niliendelea kulazimisha kusukuma huku mvurugano tumboni ukiwa mkubwa. Niliamini lile ni tumbo la kuhara, niliendelea kusukuma haja kubwa ambayo niliamini lazima nitaharisha kutokana na tumbo lilivyokuwa likinivuruga.

    Lakini baada ya kujikamua sana nilitoa kinyesi kidogo kama cha mbuzi na kunishangaza, tumbo lilivyokuwa likinivuruga kutoa kinyesi kama kile wakati nilijua nitaharisha.

    Niliendelea kujikamua huku haja ndogo ikiuma lakini iligoma kutoka. Niliendelea kujikamua huku maumivu chini ya kitovu yakiwa makali sana.

    Nilijiuliza kile ni nini? Nilijuta kulazimisha kufanya mapenzi, japokuwa hayakuwa ya nguvu zaidi ya kufanya kwa tahadhari kubwa.

    Mzee Sambi alinifuata msalani baada ya kuniona nimechelewa kutoka na kuniuliza:

    “Vipi mpenzi?”

    “Yaani hii hali wala siielewi.”

    “Kwa nini?”

    “Haja ndogo imenishika mpaka kinena kinauma lakini haitoki. Tumbo nalo limevurugika lakini choo hakitoki hata sijui...yaani mbona nateseka mtoto wa kike,” nilisema huku nikiuma meno kwa uchungu.

    “Sasa itakuwa nini! Au twende hospitali?”

    “Su...su...mmh,” nilisema huku nikiuma meno na kusukuma kwa nguvu baada ya kusikia kama kitu kikisogea mithili ya mtu anayejifungua.

    Niliuma meno na kusukuma kwa nguvu zote. Mara kitu kilifyatuka kwa mbele na kufuatiwa na damu nyingi nyeusi.

    Niliendelea kujikamua, damu iliendelea kutoka ikiwa mabongemabonge na kufika robo ya sinki la choo.

    Ilikuwa damu nyeusi iliyokuwa ikinuka kama kitu kilichokuwa kimeoza.

    Wakati huo nilianza kuharisha mfululizo kitu kilichonifanya niishiwe na nguvu na kuanguka msalani.

    ***

    Niliposhtuka nilijikuta nikiwa hospitali, niliponyanyua macho niliwaona watu kwa shida, macho yangu yalikuwa kama yana ukungu.



    Hata hivyo, nilibaini kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wamejazana kitandani kwangu huku nikiongezewa damu.



    Uwezo wa kuona vizuri sikuwa nao kwa vile nilipojitahidi kutizama vizuri niliona kitanda kikizunguka na kunifanya nifumbe macho, nilikuwa nimeshikwa na kizunguzungu kikali.

    Niliisikia sauti ya mama ikiniita:

    “Mwaija...Mwaija.”

    Nilimsikia lakini sikuwa na uwezo wa kufumbua mdomo japokuwa nilijitahidi kuitikia. Nilikuwa najisikia vibaya na kizunguzungu kilikuwa kikali sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilitulia nikiwa nimefumba macho, kizunguzungu nacho kilipungua taratibu na usingizi ulinipitia.

    Niliposhtuka nilijikuta nikiwa kitandani na mama na dada zangu walikuwa pembeni wakionesha kuwa na nyuso zenye huzuni.

    Mara aliingia daktari na kusogea kitandani kwangu.

    “Mwaija,” aliniita kwa sauti ya upole.

    “Abee,” safari hii sauti ilitoka.

    “Unajisikiaje?”

    “Kizunguzungu.”

    “Kitaisha tu, damu uliyopoteza ilikuwa nyingi.”

    “Damu!?” Nilishtuka.

    “Ndiyo, ulikuja ukiwa na hali mbaya sana, mpaka sasa hivi unazungumza kweli Mungu mkubwa.”







    “Mimba yangu ipo salama?” lilikuwa swali lililonitoka kinywani kwangu, kwani haikuwa tofauti na tukio la awali la kuharibika mimba yangu.” “Bado tunaangalia kwanza hali yako, mengine ata baadaye.” “Mama,” nilimwita mama aliyekuwa amesimama



    pembeni ya kitandani. “Abee mwanangu unaendeleaje?” “Kizungumzungu, lakini kwa sasa afadhali kidogo.” “Pole.” “Asante mama.” “Pole Mwaija,” dada zangu nao walinipa pole. “Asante.” Kuna kitu kimoja nilikigundua katika nyuso za mama na dada



    zangu. Walionekana wamevimba macho kuonesha kama walikuwa wakilia.



    “Mama,” nilimwita kwa kujilazimisha. “Abee mama.” “Mbona kama wote mlikuwa mkilia?” nilimuuliza mama. “Mmh! Wee acha tu



    kweli Mungu mkubwa.” “Kwa nini mama?” “Sikuamini kama ungeweza kuzungumza hivi.” “Kwa nini?” “Hali tuliyokukutana nayo



    ilituchanganya, mimi ndiye kidogo niliyejitahidi lakini dada zako walipokuona waliangua vilio. Hatukuamini kama utapona.” “Kwani



    ilikuwaje?” “Tulipigiwa simu na bwana yako akilia, huwezi kuamini tulivyoondoka nyumbani ndivyo tulivyokuwa, hakuna aliyekumbuka viatu wala khanga ya kujifunga juu.



    “Tulikukuta umelazwa sebuleni damu chapachapa huko msalani ndiyo usiombe utafikiri kumechinjwa ng’ombe na harufu kali kama kuna kitu kimeoza.” “Mungu wangu, ujauzito wangu



    upo salama?” “Hatujajua, huwezi kuamini mimi na dada yako mkubwa tuna siku ya pili tupo hospitali hatujarudi nyumbani.” “Kwa nini mama?” nilishtuka kwani niliamini tukio lile lilikuwa la siku ileile. “Kwa hali uliyokuwa nayo tulijua umefariki kwani hata mapigo



    ya moyo yalionesha kusimama. Pamoja na kuelezwa turudi nyumbani hatukukubali. Tulilala nje ya hospitali kwa siku mbili mpaka ulipofumbua macho lakini hukuweza kuzungumza. “ Lakini tulielezwa kwamba damu waliyokuwekea ungeweza kurudi katika hali



    yako ya kawaida. “Damu uliyopoteza ni nyingi sana. Yaani tungechelewa kidogo tungekupoteza kwani ulikuwa umeishiwa damu kabisa mwilini, kwani tatizo nini mwanangu?” mama aliniuliza akiwa ameniinamia. Nilijitahidi kuelezea hali yangu tangu siku ya



    kwanza na siku ile nilipotokewa na tatizo lile. “Mmh!” waliguna wote. “Kwa nini ulikaa kimya?” dada mkubwa aliniuliza. “Nilijua labda ni hali ya kawaida kwa vile sikuwa na maumivu yoyote.” Kuguna kwao kulinishtua na kujiuliza kulikoni kuguna wote kwa



    mpigo. Nilichowaeleza mbona kilionekana kuwashtua na kutazamana wote. “Jamani kuna nini?” niliuliza baada ya kuingiwa na hali ya woga. “Mwaija hebu kwanza tuangalie tiba za hospitali.” “Kwa nini unasema hivyo mama?” “Kauli yako imenitisha mtu kupatwa



    na tatizo baada ya kukutana na mwenzio. Pia hata yule mwanamke nina imani hakuwa mwema kwako.” Kauli ya mama ilinishtua na kunifanya nijiulize inamaa aliyekuja alikuwa mke wa mzee Sambi na kama ni yeye mbona hakuniambia ukweli. Nilikubaliana na kauli ya mama kutokana na mshtuko alioupata mzee Sambi juu ya ugeni ule baada ya kuufahamu wajihi wa mke wake. “Kwani



    mama aliyekuja si mwenye nyumba?” “Tutajua tu kama amri ya Mungu au mkono wa mtu.” Jioni alipokuja mzee Sambi kuniona alionesha uso wa furaha baada ya kunikuta nikiwa katika hali nzuri. Niliamini siku mbili nilizokuwa sina fahamu zilimchanganya sana.



    “Karibu mpenzi,” nilimkaribisha.“Asante, pole sana.”“Asante.”“Vipi unaendeleaje?” “Sijambo.” “Vipi umekula?” “Ndiyo.” Baada ya muda mama na dada zangu walitoka nje na kuniacha na mzee Sambi. Niliamini ile ndiyo ilikuwa nafasi yangu ya kupata ukweli



    kama aliyekuja siku ile alikuwa nani. “Eti mpenzi aliyekuja siku ile alikuwa mkeo?” “Mbona unauliza hivyo?” “Nijibu swali langu,” nilikuwa mkali kidogo. “Ndiyo.” “Ndiyo nini?” “Ni mke wangu kweli.” “Mzee Sambi, mkeo alikuja kwangu kufanya nini?” “Sijui.”







    "Eti mpenzi aliyekuja siku ile alikuwa mkeo?"

    "Mbona unauliza hivyo?"

    "Nijibu swali langu," nilikuwa mkali kidogo.

    "Ndiyo."

    "Ndiyo nini?"

    "Ni mke wangu kweli."

    "Mzee Sambi, mkeo alikuja kwangu kufanya nini?"

    "Sijui."

    "Amepajuaje?"

    "Hata mimi nashangaa."

    "Na kwa nini ulinificha ukanidanganya?"

    "Nilihofia kukushtua kwa vile nilikwenda nyumbani tukayamaliza."



    "Huu ugonjwa wangu nina wasiwasi na mkeo."

    "Kafanya nini?"

    "Nitajua tu, ila kama ni yeye nitakufa naye."

    "Hawezi kufanya mchezo wowote mchafu."

    "We mtetee labda nife."CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mpenzi usiwe na mawazo potofu, kwa vile upo hospitali ngoja tuone kitakachoendelea."

    Siku ya pili niliamka nikiwa na nguvu na chupa za damu nilizoongezwa ziliisha na kujiona nikiwa sawa. Nilichotaka kujua ni kuhusu



    ujauzito wangu. Majibu ya vipimo yalipatikana jioni ya siku ile baada ya mzee Sambi kuja.

    Vipimo vilionesha ujauzito wangu umetoka. Baada ya kupewa taarifa ile nilipata mshtuko uliosababisha nipoteze fahamu.

    Baada ya kurudiwa na fahamu na kukumbuka kilichonitokea nililia sana. Niliamini siku ile kama ningekuwa ghorofani basi



    ningejitupa au kama kungekuwa na sumu karibu yangu ningekunywa.

    Roho iliniuma kama kidonda na kujiuliza hali ile itaendelea mpaka lini.

    Nilijiuliza ule ndiyo utakuwa mchezo wa kushika ujauzito na kutoka katika maisha yangu?

    Taarifa za kupoteza ujauzito wangu zilimliza mzee Sambi kama mtoto.

    Kwa kweli lilikuwa pigo lingine kubwa maishani mwangu. Tangu siku niliyopewa taarifa ya kuharibika kwa ujauzito wangu



    mwingine, chakula kilikataa kupita mdomoni japokuwa mama na dada zangu walinilazimisha nile angalau kidogo.

    Siku nne kwangu zilikuwa sawa na mwezi mzima kwa mawazo na kushindwa kula, kutokana na kufikiria mateso yanayonipata ya



    kupoteza ujauzito wangu kila mara.

    Nilikonda kama niliugua kwa muda mrefu. Mama na dada zangu walitumia muda mwingi kuwa karibu yangu huku



    wakinibembeleza angalau nile kidogo, lakini wapi chakula kilikataa kupita mdomoni, muda mwingi nilikuwa nikilia tu.

    Kingine kilichoniumiza akili kilikuwa ni maumivu ya tumbo na kuendelea kutoka damu kama ya hedhi kwa muda mrefu. Nilikuwa



    nashinda na pedi ili nisijichafue.

    Ugonjwa wa tumbo ukanitia wasiwasi labda sikusafishwa vizuri. Ilibidi nifanyiwe usafi upya.

    Nilimshukuru Mungu kidogo hali ya maumivu ya tumbo ilitulia na kuamini maumivu yale yalisababishwa na uchafu uliobaki.

    Kuendelea kutokwa na damu kulinichanganya sana japokuwa haikutoka nyingi lakini bado nilibakia na swali kwa nini iendelee



    kutoka.

    Nilifanya vipimo vyote lakini haukuonekana ugonjwa wowote. Nilianza kuingiwa na wasiwasi yale ni mambo ya Kiswahili au



    kishirikina. Kila kukicha hali yangu ilizidi kubadilika, nikawa siwezi kunyanyuka.

    Nikawa mtu wa kulala kitandani, miguu ilikuwa kama vile imepooza. Kutokana kukosa ufumbuzi wa ugonjwa wangu, daktari



    mmoja alimshauri mama tuhangaike upande wa pili.

    Ilibidi nitolewe hospitali, ungeniona siku ile ungelia kwa uchungu. Nilikuwa nimekwisha kama mgonjwa wa kifua kikuu. Mama



    alinichukua na kunipeleka kwa mtaalamu Temeke Yombo.

    Mwaija miye nilikuwa wa kubebwa kama mtoto mdogo, sura yangu kwa muda mfupi ilibadilika na kuwa kama mzee, kila aliyeniona



    alitokwa na machozi.

    Nilipelekwa kwa mganga wa kiume ambaye aliponiona kabla ya kunitibu alishauri kwanza nikapimwe damu kwani nilikuwa na dalili



    zote za ugonjwa wa kisasi kama kukonda na nywele kubadilika rangi.

    Nilipelekwa hospitali kupima na majibu yakaonesha kwamba sikuwa na tatizo lolote. Mganga baada ya kupata majibu alianza



    kunitibu, kwanza kwa kuangalia tatizo langu lilikuwa ni nini.

    Japokuwa nilikuwa siwezi kukaa lakini alichokuwa akikisema nilikisikia:

    "Mgonjwa wenu amechezewa na mwanamke."

    "Kivipi?"

    "Ametupiwa jini."

    "Na nani?" mama aliuliza.

    "Na mwanamke mmoja aliyemtembelea kwake."

    Kauli yake iliwafanya mama na dada zangu waangaliane na kushusha pumzi ndefu.

    "Ni nani?"

    "Mwenyewe anamjua, kuna siku alitembelewa na mgeni saa tano asubuhi akiwa amevaa vitenge kuanzia juu mpaka chini. ni



    kweli?"

    "Ni kweli kabisa," nilijibu.

    "Basi yule ndiye mbaya wenu japokuwa siku ile hakuja kwa shari."

    "Ni nani?"

    "Huyu ana mwanaume ambaye ana mke na yule ndiye mkewe. Bahati mbaya alikuwa hajulikani ila alitaka kupata ukweli baada yaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    kuujua ukweli ndipo alipokwenda kufanya mambo yake.

    "Alitumia uchawi wa jini kupitia kwa mumewe, jini lile lilikuwa likitembea naye bila kujua na muda wa kukutana jini lilitangulia



    mbele ili kuuharibu ujauzito.

    Baada ya kukutana na mwenzako ndipo lilipopata nafasi ya kutangulia na kusababisha utokwe na damu ukiwa mwanzo wa



    kuuharibu ujauzito wako.

    "Kwa vile ulitokwa na damu hukufahamu tatizo, ulikwenda hospitali na kufanikiwa kuzuia damu isitoke. Kwa vile ulikuwa hujui



    kilichokuwa kikiendelea uliamini tatizo lako lilikuwa limekwisha.

    "Kwa vile jini lile lilitumia njia ya wewe kukutana na mwenzako, lilisubiri mtakapokutana tena. Siku mliyokutana lilitumia nafasi



    hiyo kuharibu ujauzito wako ulioambatana na kutokwa na damu nyingi sana."

    "Sasa mbona baada ya ujauzito kutoka kila siku hali yake inazidi kuwa mbaya, damu imekuwa haikomi kutoka?" mama aliuliza.

    "Lile jini lililotumwa kwake lilikuwa na kazi mbili kubwa, kazi ya kwanza limeifanya vizuri na sasa linafanya kazi ya pili."

    "Kazi gani?" mama aliuliza.

    "Kwanza ilikuwa ni kuiharibu mimba, pili kummaliza taratibu mpaka azimike kabisa."

    "Mungu wangu! Kwa hiyo bado jini hilo lipo?"

    "Ndiyo."

    "Kwa hiyo utatusaidiaje?"

    "Kumtibu tu."

    "Na aliyemfanyia?"

    "Ngoja kwanza tumtibu kisha mambo mengine yatafuata."

    Nilianza kupata tiba kwa kupewa dawa ya majani mabichi na kutakiwa kuinywa ambayo ilisababisha nitapike na kuharisha. Baada



    ya muda nilipewa uji uliochanganywa na dawa.

    Baada ya kunywa nilipitiwa na usingizi kwa muda mrefu tangu nianze kuumwa siku hiyo ndiyo niliyopata usingizi mzito.

    Nilipoamka nilikuta tayari imeandaliwa nyungu ambayo nilifukizwa kwa kufunikwa na shuka. Kwa vile sikuwa na uwezo wa kukaa



    peke yangu nilishikiliwa mpaka huduma ilipokwisha.

    Nilirudishwa na kulazwa kwenye mkeka huku nikiwa navuja jasho kama maji mwili mzima kutokana na joto kali la nyungu.

    Baada ya mapumziko nilipatiwa chakula, ajabu ni kwamba nilikula vizuri sana.

    Siku ile nililala pale na kubaki na dada kwa ajili ya kunisaidia kwa vile miguu haikuwa na nguvu. Nilikaa kwa mganga kwa wiki mbili



    nikiendelea kupata tiba.

    Tiba ile ilinisaidia, niliweza kusimama na kutembea lakini kwa shida, hata hivyo nilikuwa na mabadiliko makubwa katika afya



    yangu, ilikuwa tofauti na nilivyokwenda nikiwa mtu wa kubebwa. Mpaka naondoka kwa mganga damu ilikuwa imekata, hata hamu



    ya kula nilikuwa nayo. Tatizo lilikuwa kwenye nguvu za miguu, nilikuwa siwezi kusimama au kutembea kwa muda mrefu.





    Pia nilikatazwa nisirudi kwangu mpaka mganga atakapokwenda kupatengeneza. Kipindi chote nilichokuwa kwa mganga sikumuona mzee Sambi.



    Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa hospitali siku nilipomuuliza kuhusu mkewe kuja nyumbani kwangu.Tangu siku ile alipoondoka sikumuona tena.

    Nilijikuta najawa na mawazo kuhusu kupotea kwa mzee Sambi kwa sababu niliamini matatizo yote yanatokana na yeye. Nilijiuliza kuna nini kimemsibu mpaka kunikimbia?



    Lakini muda ule sikumfikiria sana yeye zaidi ya afya yangu, niliendelea kutumia dawa nilizopewa na mganga ili kuimarisha afya yangu. Nilitumia zile dawa kwa wiki lakini miguu ilikuwa bado haijapata nguvu.



    Nilirudishwa tena kwa mganga baada ya miguu kuanza kupasua na kuwaka moto. Usiku nilikuwa silali kutokana na ukali wa maumivu, nilikuwa nakesha nikilia. Mbona niliteseka! Vitu vingine visikie kwa mtu lakini usiombe vikukute.



    Kutokana na kusikia maumivu makali hata kutembea nilishindwa kwani kwenye nyayo kulikuwa kama kuna vidonda. Nilipofika nilianzishiwa dozi nyingine.



    Baada ya kunywa siku ya pili mwili ulianza kubabuka ngozi kama nyoka, kitu kilichonitisha sana.

    Mganga alisema ile ni sumu iliyokuwa mwilini hivyo ilikuwa inatoka. Nilitakiwa kujipaka mafuta mazito mwili mzima usiku kabla ya kulala ili asubuhi nikiamka nikute ngozi iliyobabuka imebanduka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuwa najipaka kopo lote la mafuta, mwili ulikuwa kama nimetumbukia kwenye tope la mafuta. Ngozi iliyotoka ilibanduka taratibu, ilichukua zaidi ya wiki kumalizika.



    Baada ya kukoboka mwili, kazi ikabakia nguvu kwenye miguu ambayo haikuonesha mabadiliko. Maumivu ya miguu yaliisha tatizo likabaki kwenye nguvu. Kuwaka miguu kuliisha na kubadilika kuwa ya baridi na kuonesha dalili zote za kupooza.



    Hali ile ilizidi kunichanganya akili, kila kukicha nilikonda mtoto wa kike na kubakia kichwa kama guruguja. Duniani watu wanateseka, nilikuwa namaliza mwezi kwa mganga, kazi yangu ilikuwa kukaa kwa muda wote mpaka hata mgongo ukaanza kunisumbua. Muda mwingi nikawa nalala kama nyoka.



    Ilionesha wazi mganga alichemsha kuniponyesha japokuwa hakutaka kusema. Miguu ilianza kukonda na kuwa midogo. Nilijikatia tamaa na kuanza kukataa dawa kwa kuamini nilikuwa nakunywa kama maji kwa vile hakukuwa na mabadiliko yoyote ya dawa nilizokunywa.



    Niliwaomba wanirudishe nikafie nyumbani lakini mama na dada zangu waliniomba niendelee kuvumilia kwa vile mganga alisema hajakata tamaa.

    “Jamani kama mmenichoka naomba mnirudishe nikafie kwangu.”

    “Mwaija mwanangu sisi wote tunaumiza vichwa juu yako. Hakuna mwenye furaha kila mmoja anateseka kwa ugonjwa wako.”



    “Sasa kama siponi kuna faida gani kuendelea kukaa kwa mganga, mi najua nakufa kwa nini msinirudishe nikafie nyumbani?”

    “Mwaija usiseme hivyo, kuugua siyo kufa.”

    “Jamani mimi nimeshakufa, nasubiri kuzikwa.”

    “Hapana mwanangu, basi tufanye mpango wa kukupeleka kwa mganga mwingine.”

    “Sitaki mwenda kwa mganga yoyote niacheni nife.”



    Ilibidi nirudishwe nyumbani baada ya kushindikana kutibika. Nilirudishwa nyumbani kumalizia siku zangu za kuishi zilizobakia. Kila kukicha hali yangu ilikuwa mbaya.

    Nilikonda mpaka uti wa mgongo ulitoka, nilipolala nilihisi naumia kwa vile nilikuwa nalalia mifupa. Kula nilishindwa, chakula changu kikuu kilikuwa uji tena nusu kikombe.



    Jamani maradhi mengine yasikie kwa watu si ya kuugua, nikawa kila siku lazima nipoteze fahamu. Kuna siku kutokana na maelezo ya mama walidhani nimekufa, kilio cha dada zangu kilikusanya watu nje.



    Ilikuwa ni baada ya kupoteza fahamu kwa siku mbili, kilichositisha kuzikwa kwangu ni joto la mwili ambalo wazee walisema wanaweza kunizika ningali hai.



    Baada ya hapo sikuelewa kinachoendelea mpaka niliposhtuka baada ya kupiga chafya mfululizo. Nilipofumbua macho nilijikuta sehemu ambayo haikuwa ngeni lakini bado sikuwa na uhakika nayo.



    Nilipojaribu kunyanyuka nilishindwa, nilipojipapasa bado nilikuwa kwenye mifupa mitupu. Kutokana na harufu niliyokuwa naisikia nilijua pale ni kwa mganga.



    Nilijiuliza pale ni wapi na kwa nini wamenipeleka tena kwa mganga ikiwa tulikubaliana nisubiri mauti yangu. Nikiwa bado nipo katikati ya mawazo kwa nje ya chumba nilichokuwa nimelala, nilisikia sauti ya watu wakizungumza.

    Nilisikia sauti ya mama akizungumza na sauti nyingine ambayo ilinishtua.



    Siku ile nililala pale na kubaki na dada kwa ajili ya kunisaidia kwa vile miguu haikuwa na nguvu. Nilikaa kwa mganga kwa wiki mbili nikiendelea kupata tiba.



    Tiba ile ilinisaidia kwani niliweza kusimama na kutembea lakini kwa shida. Pia nilikuwa na mabadiliko makubwa katika afya yangu, nilikuwa tofauti na nilivyokwenda kwani awali nilikuwa mtu wa kubebwa tu.



    Mpaka naondoka kwa mganga, damu ilikuwa imekata, hata hamu ya kula nilikuwa nayo. Tatizo lilikuwa kwenye nguvu za miguu, nilikuwa siwezi kusimama au kutembea kwa muda mrefu.



    Pia nilikatazwa nisirudi kwangu mpaka mganga atakapokwenda kupatengeneza. Kipindi chote nilichokuwa kwa mganga sikumuona mzee Sambi.



    Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa hospitali siku nilipomuuliza kuhusu mkewe kuja nyumbani kwangu.Tangu siku ile alipoondoka sikumuona tena.

    Nilijikuta najawa na mawazo kuhusu kupotea kwa mzee Sambi kwa sababu niliamini matatizo yote yanatokana na yeye. Nilijiuliza kuna nini kimemsibu mpaka kunikimbia?



    Lakini muda ule sikumfikiria sana yeye zaidi ya afya yangu, niliendelea kutumia dawa nilizopewa na mganga ili kuimarisha afya yangu. Nilitumia zile dawa kwa wiki lakini miguu ilikuwa bado haijapata nguvu.



    Nilirudishwa tena kwa mganga baada ya miguu kuanza kupasua na kuwaka moto. Usiku nilikuwa silali kutokana na ukali wa maumivu, nilikuwa nakesha nikilia. Mbona niliteseka! Vitu vingine visikie kwa mtu lakini usiombe vikukute.



    Kutokana na kusikia maumivu makali hata kutembea nilishindwa kwani kwenye nyayo kulikuwa kama kuna vidonda. Nilipofika nilianzishiwa dozi nyingine.



    Baada ya kunywa siku ya pili mwili ulianza kubabuka ngozi kama nyoka, kitu kilichonitisha sana.

    Mganga alisema ile ni sumu iliyokuwa mwilini hivyo ilikuwa inatoka. Nilitakiwa kujipaka mafuta mazito mwili mzima usiku kabla ya kulala ili asubuhi nikiamka nikute ngozi iliyobabuka imebanduka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikuwa najipaka kopo lote la mafuta, mwili ulikuwa kama nimetumbukia kwenye tope la mafuta. Ngozi iliyotoka ilibanduka taratibu, ilichukua zaidi ya wiki kumalizika.



    Baada ya kukoboka mwili, kazi ikabakia nguvu kwenye miguu ambayo haikuonesha mabadiliko. Maumivu ya miguu yaliisha tatizo likabaki kwenye nguvu. Kuwaka miguu kuliisha na kubadilika kuwa ya baridi na kuonesha dalili zote za kupooza.



    Hali ile ilizidi kunichanganya akili, kila kukicha nilikonda mtoto wa kike na kubakia kichwa kama guruguja. Duniani watu wanateseka, nilikuwa namaliza mwezi kwa mganga, kazi yangu ilikuwa kukaa kwa muda wote mpaka hata mgongo ukaanza kunisumbua. Muda mwingi nikawa nalala kama nyoka.



    Ilionesha wazi mganga alichemsha kuniponyesha japokuwa hakutaka kusema. Miguu ilianza kukonda na kuwa midogo. Nilijikatia tamaa na kuanza kukataa dawa kwa kuamini nilikuwa nakunywa kama maji kwa vile hakukuwa na mabadiliko yoyote ya dawa nilizokunywa.



    Niliwaomba wanirudishe nikafie nyumbani lakini mama na dada zangu waliniomba niendelee kuvumilia kwa vile mganga alisema hajakata tamaa.

    “Jamani kama mmenichoka naomba mnirudishe nikafie kwangu.”

    “Mwaija mwanangu sisi wote tunaumiza vichwa juu yako. Hakuna mwenye furaha kila mmoja anateseka kwa ugonjwa wako.”



    “Sasa kama siponi kuna faida gani kuendelea kukaa kwa mganga, mi najua nakufa kwa nini msinirudishe nikafie nyumbani?”

    “Mwaija usiseme hivyo, kuugua siyo kufa.”

    “Jamani mimi nimeshakufa, nasubiri kuzikwa.”

    “Hapana mwanangu, basi tufanye mpango wa kukupeleka kwa mganga mwingine.”

    “Sitaki mwenda kwa mganga yoyote niacheni nife.”



    Ilibidi nirudishwe nyumbani baada ya kushindikana kutibika. Nilirudishwa nyumbani kumalizia siku zangu za kuishi zilizobakia. Kila kukicha hali yangu ilikuwa mbaya.

    Nilikonda mpaka uti wa mgongo ulitoka, nilipolala nilihisi naumia kwa vile nilikuwa nalalia mifupa. Kula nilishindwa, chakula changu kikuu kilikuwa uji tena nusu kikombe.



    Jamani maradhi mengine yasikie kwa watu si ya kuugua, nikawa kila siku lazima nipoteze fahamu. Kuna siku kutokana na maelezo ya mama walidhani nimekufa, kilio cha dada zangu kilikusanya watu nje.



    Ilikuwa ni baada ya kupoteza fahamu kwa siku mbili, kilichositisha kuzikwa kwangu ni joto la mwili ambalo wazee walisema wanaweza kunizika ningali hai.



    Baada ya hapo sikuelewa kinachoendelea mpaka niliposhtuka baada ya kupiga chafya mfululizo. Nilipofumbua macho nilijikuta sehemu ambayo haikuwa ngeni lakini bado sikuwa na uhakika nayo.



    Nilipojaribu kunyanyuka nilishindwa, nilipojipapasa bado nilikuwa kwenye mifupa mitupu. Kutokana na harufu niliyokuwa naisikia nilijua pale ni kwa mganga.



    Nilijiuliza pale ni wapi na kwa nini wamenipeleka tena kwa mganga ikiwa tulikubaliana nisubiri mauti yangu. Nikiwa bado nipo katikati ya mawazo kwa nje ya chumba nilichokuwa nimelala, nilisikia sauti ya watu wakizungumza.

    Nilisikia sauti ya mama akizungumza na sauti nyingine ambayo ilinishtua.









    Ilikuwa baada ya kupoteza fahamu kwa siku mbili, kilichositisha kuzikwa kwangu ni joto la mwili ambalo wazee walisema wanaweza kunizika nikiwa bado hai.



    Baada ya hapo sikuelewa kilichokuwa kikiendelea mpaka niliposhtuka pale nilipopiga chafya mfululizo.

    Nilipofumbua macho nilijikuta sehemu ambayo haikuwa ngeni lakini bado sikuwa na uhakika nayo.



    Nilipojaribu kunyanyuka nilishindwa, nilipojipapasa bado nilikuwa mifupa mitupu. Kutokana na harufu niliyokuwa nikiisikia nilijua pale ni kwa mganga.



    Nilijiuliza kwa nini wamenipeleka tena kwa mganga ikiwa tulikubaliana nisubiri mauti yangu. Nikiwa bado katikati ya mawazo kwa nje ya chumba nilichokuwa nimelala, nilisikia sauti ya watu wakizungumza nje ya chumba.



    Nilisikia sauti ya mama akizungumza na sauti nyingine ambayo ilinishtua. Ilikuwa ya mtu ninayemfahamu lakini nilijua labda zinafanana na nyingine ilinishtua zaidi ilikuwa kama ya mama Amina mganga aliyenitibu mwanzo.

    Nilimsikia akizungumza:



    “Mmesikia chafya atakuwa amerudiwa na fahamu.”

    “Hata mimi nimesikia.”

    “Mmh! Akipona nitashukuru,” nilimsikia mama akisema.

    “Tumuombe Mungu, lakini mwanao yote kayataka mwenyewe, nilimueleza arudi akadharau. Wagonjwa wengi wakipata nafuu huwa hawajali kumalizia tiba na kujiona wapo sawa matokeo yake ugonjwa unamrudia tena kwa kazi kubwa kwa vile vita inakuwa mara mbili.”



    “Hakuniambia, kama angenieleza haya mapema ningemleta pengine hata ujauzito wake usingetoka.”

    “Nilimwambia arudi niufunge lakini akadharau matokeo yake ni haya. Lakini nakuhakikishia Mwaija atatembea na kurudia katika hali yake ya kawaida.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kweli?” mama aliuliza.



    “Tatizo alilonalo likitoka mbona mwanao mzima, hilo nina uhakika wa kulitoa.”

    Nilishangaa kusikia mganga akijiamini kupita kiasi, kwani hata mganga wa Yombo alisema hivyo lakini mwisho wa siku alichemka.

    “Ngoja nikamuangalie.”



    Baada ya kimya cha dakika chache nilisikia sauti za nyayo za miguu zikija ndani.

    Nilitulia nikitizama juu kwa vile sikuwa na nguvu ya kujigeuza, nilivyolazwa ndivyo nilivyolala.



    Baada ya muda nilisikia nikiitwa.

    “Mwaija.”

    “Abee,” niliitikia.



    Baada ya kuitikia aliyeniita alisogea karibu yangu ndipo nilipomtambua vizuri kuwa ni mama Amina.



    “Pole.”

    Badala ya kuitikia nilianza kulia, mama Amina alinibembeleza:

    “Mwaija utapona japo umechelewa sana.”



    Lakini kumbe sikuwa nalia kwa maumivu bali aibu ya kumkimbia baada ya kupata ujauzito na kuondoka bila kurudi, pia kuwa muongo kwa niliyomuahidi.



    “Silii hilo dada.”



    “Unalia nini?”

    “Nimekuwa muongo na hii ndiyo adhabu yangu.”

    “Hebu achana na hayo, naomba nikupe uji wa dawa kwa vile sasa hivi huwezi kula chakula kigumu ili niendelee na tiba yako.”

    “Sawa.”



    Mama Amina alitoka na kuniacha nikiwa na maswali mengi, huku nikijiuliza ni nani aliyenipeleka kwake.



    Baada ya muda alirudi na bakuli la uji akiwa ameongozana na mama pamoja na da’ Suzy hapo ndipo nilipojua aliyenileta kwa mama Amina ni da’ Suzy.



    Nilijikuta nikisahau ugonjwa wangu na kutabasamu baada ya kumuona da’ Suzy japokuwa niliamini sura yangu ilikuwa kama ya mzee kutokana na kukonda kwa ugonjwa.



    “Mwaija,” da Suzy aliniita

    “Abee.”

    “Pole mdogo wangu.”

    “Sijapoa.”

    “Utapona tu dada.”



    “Mmh! Nitashukuru japokuwa imani yangu imekuwa ndogo sana.”

    “Mwaija kwa uwezo wa Mungu utapona tu mdogo wangu,” mama Amina alinipa moyo.



    Walisaidiana kunikalisha kisha nilipewa uji uliochanganywa na dawa. Japokuwa nilikuwa mgonjwa niliweza kuunywa wote uliokuwa kwenye bakuli.



    Baada ya kunywa waliniacha nipumzike kwa muda. Baada ya muda nilifuatwa na kutolewa nje, ilionesha ni majira ya jioni inayokimbilia usiku kutokana na kigiza kuanza kuimeza nuru ya mchana.



    Kama kawaida nilitolewa kwa kubebwa, ilikuwa yataka moyo kwani kila aliyenishika alishika mifupa. Nilitolewa uani na kulazwa kwenye mkeka.



    Nilielezwa natolewa mdudu (jini) niliyetupiwa, kazi ya kumtoa ilianza mara moja.



    Nilipewa dawa ya maji ambayo nilielezwa ni miti zaidi ya nane iliyokuwa imechangwanywa pamoja.



    Baada ya kunywa nilianza kujisikia vibaya tumbo likaanza kunichanganya na kusikia kichefuchefu. Nilianza kutapika lakini hakuna kilichotoka nilipoanza kujigogoa, mama Amina alikuja na kuingiza vidole mdomoni kwangu kama anatafuta kitu na kukitoa kwa kukwangua.



    Aliingiza vidole mpaka kwenye koromeo na kukwangua na kutoa vitu kama malenda na kusema anatoka. Sikuelewa anatoka nani, aliendelea kufanya vile na kutupa nje yale malenda.



    Alifanya vile zaidi ya mara tano kisha alisema:

    “Lilikuwa limeanza kukomaa lakini bahati nzuri limetoka lote.”



    Bado sikuelewa lilikuwa limekomaa nini. Baada ya muda nilipewa uji wa dawa ambao ulinifanya niharishe mpaka nguvu ziliniishia. Mauti niliyaona mbele yangu, baada ya zoezi lile nilirudishwa ndani.



    Kutokana na mshikemshike nilioupitia usingizi mzito ulinichukua.



    Niliamshwa usiku sana na kupewa ndizi zilizopondwa na kulazimishwa kula japo mwili haukuwa na nguvu hata kidogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kula nilirudi kitandani kulala. Siku ya pili niliamshwa na kupewa uji wa dawa na kupumzika. Majira ya saa nne nilipata kifungua kinywa cha nguvu. Nilishangaa siku ile nilikula vizuri.



    Mama Amina aliniambia mdudu aliyekuwa akinisumbua ametoka. Japokuwa nilikuwa naumwa lakini nilikuwa na uwezo wa kuzungumza.



    “Mdudu ndiyo nini?”



    “Jini ulilotupiwa.”



    “Unamaanisha limetoka?” sikuamini.



    “Ndiyo.”



    “Mbona yule mganga wa mwanzo alisema limetoka na kupata nafuu lakini matatizo yalizidi?”



    “Hakumtoa.”



    “Alifanya nini?”



    “Alimpoza, waganga wengi huwapoza tu lakini hawawatoi.”



    “Kwa hiyo wewe umemtoa?”



    “Ndiyo.”



    “Hatarudi tena?”



    “Ndiyo.”



    “Kwa hiyo nimepona.”



    “Kwa vile kilichokuwa kikikumaliza tumekitoa nina imani sasa hivi afya yako itaimarika.”



    Kauli ya mama Amina niliiamini kwa asilimia ndogo sana, niliamini alikuwa akinitia moyo tu. Ajabu mwili wangu ulikuwa



    mwepesi tofauti na siku za nyuma ambapo nilikuwa nikiusikia kuwa mzito kama nimebebeshwa mzigo, hata kuhema



    kwangu kulikuwa kwa shida lakini baada ya zoezi lile nilihema vizuri.



    Nilikaa kwa mama Amina kwa siku kadhaa huku nikiendelea kutumia dawa zake. Alinieleza jini nililotupiwa lilitaka kufanya



    viungo vyangu kupooza, kama ningechelewa mwili mzima ungekufa ganzi na kupooza kabisa.







    Nilijiuliza hata kama ndiyo mke wa mzee Sambi kanifanya hivi kosa langu nini ikiwa alikubaliana na mumewe. Kama alikuwa akimtaka mumewe angenieleza kama ningekataa ndiyo angenitenda.



    Moyoni niliwaza mengi baada ya kupina nami lazima nilipe kisasi kama alivyonifanyia. Baada ya tiba ile niliweza kukaa peke yangu baada ya wiki, nilishangaa mama kumsifia mama Amina, kwangu sikuona kigeni sana japokuwa nililetwa nusu mfu lakini haikuwa na tofauti na kwa mganga wa kwanza.



    Niliendelea kukaa kwa mama Amina kwa kutumia dawa za kunywa na kufusha. Kila siku nilichuliwa sehemu zote zilizo kufa ganzi kama miguu ambayo ilikuwa haina nguvu.



    Baada ya wiki moja nyingine niliweza kunyanyuka na kutembea kwa kushikwa. Niliendelea kutumia dawa ya kuchua na kunywa na kuweza kutembea mwenyewe japo kwa shida.



    Pamoja na kutolewa kwenye umauti bado sikuwa na imani ya kurudia hali yangu ya zamani. Baada ya afya yangu kuimalika niliruhusiwa kuondoka lakini baada ya kupata kinga.

    Niliweza kutembea lakini miguu bado ilikuwa haijakaa vizuri. Nilijiuliza yatakirudia ya mwanzo japo kulikuwa na tofauti na mganga wa mwanzo kwa kiasi kikubwa.



    Niliendelea kutumia dawa ya kuchua kwa ajili yakuondoa ganzi miguuni ambayo iliondoka taratibu. Lakini ajabu muda wote sikumuona mzee Sambi.



    Nilimuuza mama ambaye alinieleza niachane naye kama kila kitu kimekwenda vizuri.

    “Lakini mama mtu niliyekuwa naishi naye kama mume na alikuwa mstari wa mbele katika matatizo yangu apotee ghafla lazima kutakuwa na kitu.”



    “Sasa sisi tutajuaje, tulitakiwa kukuuliza wewe kwa vile baada ya siku ile ambayo ulisema ulimbana kuhusu yule mwanamke aliyekuja kwako kuwa ni mkewe alipoondoka hatujamuona tena.

    “Ilitakiwa utumbie baada ya mazungumzo yale kuna kitu gani kingine kilitokea.”

    “Mbona yalikuwa mazunguzo ya kawaida wala hakukuwa na kitu chochote kibaya.”



    “Ndiyo maana nasema uachane naye, kama hamjakosana ameondoka akijua wewe ni mgonjwa. Hivi leo upo hivi nimuone nitamfukuza kama mbwa.”

    “Lakini mama lazima nijue sababu.”

    “Kama hakukwambia, mimi nitajuaje?”



    “Mamaa ina maana naye anaweza kuondoka kana Beka?” kauli ya mama ilinishtua sana.

    “Kwani Beka ulimfukuza?”

    “Sijamfukuza, lakini aliniachia fumbo zito.”

    “Fumbo gani?”



    “Kwamba wewe unajua, lakini wewe umekataa. Kabla sijapata jibu inawezekana mzee Sambi naye kakimbia!”

    “Hata akikimbia wewe umepungukiwa nini, hukutibiwa?”

    “Nimetibiwa.”

    “Sasa tatizo nini?”

    “Mama hawezi kuondoka hivihivi lazima kuna sababu.”

    “Mwaija mi nitajuaje, wewe ndiyo unanihusu wengine sijui chochote.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama sasa hivi sikubali lazima nijue sababu ya mzee Sambi kupotea ghafla tena kipindi cha matatizo mazito ambayo kwa upande mwingine ameyasababisha yeye.”



    “Mwanangu wanaume wa sasa wanakupenda kwenye uzima yakikukuta unakula wewe na familia yako.”

    “Mmh! Nitajua tu.”



    “Utajua, lakini sasa hivi endelea kwanza kuimalisha afya yako. Sambi si muhimu kama afya yako ila sitaki kumuona kwa vile alikusudia kukuua.”

    “Kivipi?”

    “Mkewe aliyofanya madogo?”



    “Sawa, lakini akija naomba usimfukuze ili aniambie sababu ya kunikimbia.”

    “Hiyo mtajuana lakini kwangu sitaki kumuona.”

    “Sawa, lakini kila kitu kitakuwa wazi.”



    Kwa vile bado nilikuwa nahitaji msaada wa familia yangu kutokana na hali yangu kutengemaa taratibu sikuweza kurudi kwangu, niliendelea kukaa nyumbani.



    Kwa vile muda ule kodi nayo ilikuwa imekaribia kwisha niliwatuma watu kuhamisha vitu vyangu vyote na kuvirudisha nyumbani. Kichwa changu kilikuwa kizito kuhusu kutoweka mzee Sambi bila taarifa. Pamoja na kujua mkewe ndiye mbaya wangu niliamini bado nikuwa nahitaji msaada wake.



    Da’ Suzy ambaye alikuwa amekuja kwa muda Dar baada ya kuhamia Mwanza na mumewe. Alinieleza alivyonikuta siku aliyokuja kunitembelea.



    “Mwaija Mungu mkubwa,” alisema huku akiniangalia kwa jicho la siamini.

    “Kwa nini?”



    “Nilivyokukuta siku ya kwanza na leo hii tunaongea hivi naamini Mungu mkubwa na Mungu yupo pia mama Amina mganga.”

    “Kwani ilikuwaje?”

    “Baada ya kufika Dar nilikuwa na hamu ya kuonana na wewe kipenzi changu japo niliondoka bila kukuaga na kubadili namba kwa ajili ya Emma.”

    “Taarifa niliisikia.”



    “Basi niliamua kuishi bila mawasiliano na mtu yeyote zaidi ya ndugu zangu. Baada ya kufika nilishinda siku moja na siku ya pili ndipo nilipokuja kwako ambako sikukuta mtu na ilionekana hakuna dalili za kuwepo watu



    Niliamua nije kwenu kukuulizia ndipo nilipofika na kukutana na mshtuko. Nilikuta watu wamekusanyika, nilipouliza niliambiwa umefariki.



    Nilishindwa kuamini niliingia mpaka ndani na kushangaa kukuta watu wakijadiliana kuhusu hali yako. Wapo waliosema umekufa lakini mzee mmoja alikataa na kusema hujafa kwa vile kwa muda wote bado mwili wako ulikuwa na joto.

    Walisema wasubiri siku mbili kama hali yako itabakia hivyo basi wakuzike. Mungu alinifungua akili ghafla ya kumkumbuka mama Amina.



    Nilimpigia simu na kumwelezea hali yako, aliniambia nimpe muda kidogo. Baada ya muda alinipigia na kunieleza kuwa wewe ni mzima ila kilichotumwa kilikuwa katika hatua ya mwisho kukutoa uhai wako,” mmh! Zilikuwa habari zilizofanya nihisi mwili kusisimka.



    Nilitulia nikimsikiliza da’ Suzy macho yamenitoka pima mkono shavuni kama akinihadithia mkasa wa kusikitisha wa mtu mwingine lakini ulikuwa wangu kwa vile yote yale yalipotokea sikuwa na fahamu nilikuwa nusu mfu.

    Nimeamini katika maisha kama hujafa hujaumbika na kisemwacho kipo. Habari zilizokuwa zinanihusu nilisimuliwa na mtu mwingine nami kuwa msikilizaji.



    Da’ Suzy aliendelea kunisimulia mkasa wangu mzito baada ya kuyaonja mauti na kuamini bila yeye ningezikwa ningali hai.

    “Basi mdogo wangu baada ya kumuomba msaada wake wa haraka mama Amina, alitoa masharti tukubebe tukupeleke kwake kwa vile kwenu isingewezekana kukutibu.”



    Kauli ile ilinishtua na kujiuliza kwa sababu gani tiba yangu isingewezekana nyumbani kwetu?

    “Basi nilimweleza mama na kina dada kuhusu kukupeleka Mbagala kwa mama Amina walikataa kwa vile ilionesha familia yako ilikuwa imeisha kata tamaa na wewe kuwa hai.



    “Kuna kipindi waliniambia maiti hii uipeleke wapi, nikuache ili mwili upoe waweze kukuzika.

    Niliwakatalia kuwa wewe si maiti bali upo hai na kuwahakikishia ukipata tiba utapona. Kwa kweli ushindani ulikuwa mkubwa na kujikuta nikiangua kilio ili nikupeleke kwa mama Amina.



    Walinikubalia huku nikipewa masharti kama umekufa basi mwili nitaurudisha mwenyewe bila kuwashirikisha. Huwezi kuamini Mwaija hali niliyokuona nayo ilinipa ujasiri wa ajabu na kukuchukua mpaka kwa mama Amina.



    Nilipokufikisha nilishtuka kumuona hata mama Amina naye akishtuka baada ya kukuona jinsi ulivyokuwa. Mwaija ulikuwa mfu kabisa mdogo wangu na kuniuliza.

    “Mmh! Wewe mbona kama mgonjwa ameisha kufa?”

    “Yupo hivi siku ya pili leo na ulipo angalia yupo hivihivi.”

    “Mmh! Ipo kazi.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Tulikuingiza ndani na haraka alianza kazi ya kukutibu ikiwa kupakwa mafusho ambayo alisema yalipunguza nguvu ya mdudu aliyekuwa amekushika.



    Alichukua dawa ya majani na kukuwekea puani na kutueleza baada ya muda utapiga chafya. Na kweli ilichukua nusu saa ulipiga chafya ndipo mama Amina alipokuja ndani kukuangalia na kusema umerudiwa na fahamu.



    Mama yako hakuamini alikuwa na hamu ya kukuona. Tuliingia na kumsaidia mama Amina kukunywesha uji. Hali uliyokuwa nayo pamoja na mama Amina kutupa moyo bado sikuamini kama ningeweza leo kuongea na wewe hivi kweli Mungu mkubwa,” da’ Suzy alinisimulia kwa uchungu mpaka machozi yalimtoka.



    Maelezo ya Da’ Suzy yaliusisimua mwili wangu na kujiuliza mateso kama yale mpaka lini. Moyo uliniuma lakini nilishindwa nifanye nini. Nilimshukuru da’ Suzy kwa ujio wake kwa kuamini kama asingetokea basi nilikuwa nazikwa hai. Pia nilimshukuru kwa



    kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha afya yangu inaimarika ikiwa pamoja na kunipeleka kwa mama Amina.



    Kutokana na moyo wa utu ilibidi apitishe muda wake wa kuondoka ili kuhakikisha anakuwa na mimi mpaka muda ule. Siku za mwanzo kuwa kwa mama Amina nilikuwa na da Suzy pamoja na ndugu zangu.



    Aliendelea kunipa moyo na kunihakikishia matatizo yanayonikabili yataisha na kurudi kwenye hali yangu.

    “Da Suzy kwa nini kila maisha yangu yakianza kuwa mazuri napata matatizo makubwa? Unafikiri lini nitayafurahia maisha kama wengine?”



    “Mdogo wangu kila kitu chenye mwanzo hakikosi mwisho, ipo siku utasahau yote haya yatakuwa simulizi kwa wanao.”

    “Mmh! Sina uhakika wa kupata mtoto kwani kila tatizo huanzia kwenye ujauzito.”

    “Mwaija hili umelitaka mwenyewe, mama Amina alikueleza urudi lakini kwa kiburi chako ukaona ulielezwa mambo ya kitoto,” da’ Suzy alinilaumu.

    “Dadaa, niliogopa kumshirikisha mzee Sambi kuwa ujauzito wangu umetokana na kutumia miti shamba. Kingine muda mwingi alikuwa karibu yangu na wewe ukaondoka ghafla nikakosa mtu wa kunisukuma kwenda kwa mama Amina.”

    “Umeelezwa matatizo yako unafanya mchezo, Mwaija wewe si mtoto mdogo dunia ya leo bila kuhangaika unakufa unajiona.”

    “Unajua mpaka sasa sielewi kabisa.”

    “Kitu gani?”

    “Alivyoondoka mzee Sambi hana tofauti na mume wangu Beka.”

    “Mwaija kwa nini usimweleze mama Amina nina imani atakusaidia.”

    “Sawa, itabidi nikifuata dawa ya kuchua nitamweleza.”

    “Vipi kwanza miguu?”

    “Sijambo, sasa hivi naweza hata kukimbia. Sijui mama Amina nimpe zawadi gani.”

    “Yoyote, mbona yule mama hana tamaa za kijinga.”



    Baada ya wiki da’ Suzy aliondoka kuelekea Mwanza. Nilimtakia safari njema na kumuombea kila lenye heri limtangulie na kumuepusha na kila la shari. Niliamini sikuwa na uwezo wa kumlipa yote aliyonifanyia bali Mungu peke yake.



    Nami hali yangu ilitengemaa na kuweza kufanya kitu chochote bila msaada wa mtu. Nilitoka siku moja bila kumtaarifu mtu na kwenda saiti kuangalia nyumba yangu japokuwa mama alinikataza niachane na kila kitu cha mzee Sambi.



    Nilipanda daladala hadi Mwenge na kuunganisha kuelekea Bunju. Nilipofika kwa mbali niliona jumba limependeza likiwa limekamilika.

    Uzio ulikuwa umeisha jengwa na kuwekwa geti la chuma. Nilisogea mpaka pale getini, bahati nzuri mlango mdogo wa geti la kuingilia ulikuwa wazi.



    Niliingia ndani, nilipotupa macho kwa mbele nilishtuka kumuona mzee Sambi na mkewe na mwanaume mwingine akiwa na mkewe wakizungumza.



    Sikujua walikuwa wakizungumza nini na wale watu. Nilirudi nje haraka ili wasinione, wakati huo nao walionekana wanatoka, niliwachungulia kupitia kwenye tundu la mlangoni na kuona wote wakiingia kwenye magari yao ili waondoke.



    Nilimuona mlinzi akisogea mlangoni kufungua geti, nilijificha nyuma ya mti uliokuwepo pale. Baada ya muda gari zilitoka na kuelekea mjini. Pamoja na kuyaona yale yote bado sikujua nini kinaendelea.



    Magari yalipotoka na geti kufungwa nilisogea getini ili kutaka kujua zaidi kuhusu ile nyumba yangu. Niligonga geti na mlinzi alitoka na kuniuliza:



    “Nikusaidie nini dada, kama kazi sasa hivi hakuna nyumba imemalizika. “

    “Sina shida hiyo.”

    “Una shida gani?”

    “Samahani kaka una muda gani hapa?”





    “UNAMAANISHA kuwepo hapa kivipi?”

    “Kikazi.”

    “Huu mwezi wa pili, kwani vipi?” mlinzi alionesha kunishangaa.

    “Ndiyo maana hunifahamu.”

    “Kwani wewe ni nani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Mimi...”

    Nilianza kujitambulisha kwa kifupi.

    “Sasa mbona sijawahi kukuona pia nyumba hii ni ya mkewe mzee Sambi.”

    “Ndivyo wanavyosema?” niliuliza macho yamenitoka pima.

    “Ndiyo, muda wote ulikuwa wapi?”

    “Nilikuwa naumwa.”

    “Mmh! Pole sana, kwa kweli siwezi kuchangia chochote labda muonane na mzee.”

    “Sawa, na wale watu wamekuja kufanya nini?”

    “Ni wapangaji ambao nielezwa wanaingia wiki ijayo.”

    “Mmh! Ahsante.”

    “Pole sana dada yangu kama unayosema ni kweli, siamini kama mzee yule anaweza kukufanyia ubaya huo. Basi hata ugonjwa wako naamini mkewe anahusika.”

    “Kaka yangu acha niende.”

    “Lakini kama una hati za kiwanja utapata haki yako.”

    “Aliichukua.”

    “Basi nenda mahakamani, nina imani utetezi wako utakusaidia kupata haki yako.”

    Japokuwa maneno ya yule kaka yalikuwa yana ushauri mzuri lakini muda ule yalikuwa yakinivuruga. Niliondoka bila kumuaga na kuelekea zangu barabarani ambako nilichukua daladala hadi Mwenge kisha nilipanda la Tandika mpaka nyumbani.

    Njia nzima sikupata jibu kuhusu mzee Sambi kwenda na mkewe kwenye nyumba yangu. Kilichonishtua zaidi kusikia ile nyumba ni ya mke wa mzee Sambi. Moyo uliniuma na kutokwa machozi njia nzima. Mtandio haukucheza mbali uso wangu kwa ajili ya kufuta machozi.

    Nilipofika nyumbani nilikwenda chumbani kwangu na kuendelea kulia mpaka kichwa kikaniuma na kumuona mzee Sambi ni muuaji asiye na huruma.

    Nilijiuliza kama matatizo ya ugonjwa yaliyotaka kuchukua uhai wangu sababu ni mkewe. Baada ya kuamini siponi alinikimbia bila kujua hatma yangu. Nilishindwa nifanye nini kwani kichwa kiliniuma sana kama kinataka kupasuka.

    Mama baada ya kugundua hali yangu alinifuata ndani na kutaka kujua nina tatizo gani. Sikuwa na jinsi nilimueleza yote niliyokutana nayo siku ile, japokuwa alinikataza kufuatilia chochote kwa mzee Sambi.

    “Mwaija mbona mwanangu umekuwa na masikio magumu, nimekueleza achana na kila kitu chake, una shida gani toka alipokukimbia?”

    “Sina mama lakini roho inaniuma, ile ilikuwa tayari nyumba yangu.”

    “Kama haki yako utaipata kwa njia nyingine mwache kama anajifanya mjanja.”

    “Kwa hiyo nifanye nini?”

    “Achana naye, jipange kwa maisha mapya.”

    Nilikubaliana na mama japokuwa moyo ulikuwa ukiniuma sana kwa unyama alionifanyia mzee Sambi na kuamua kumuachia Mungu.

    Siku iliyofuata niliamua kwenda kwa mama Amina ili kumuomba anieleze matatizo yangu kinagaubaga na kumuomba asinifiche hata kitu moja.

    Kama kawaida nilipofika nilikuta wagonjwa wengi, baada ya kunisalimia aliendelea na kazi zake. Baada ya saa moja aliniita ndani, nilipoingia na kukaa kwenye mkeka kwanza aliniuliza hali yangu.

    “Namshukuru Mungu naweza kusema sasa nimepona.”

    “Kazi imebakia moja kuhakikisha nasafisha ndoa yako, kwa vile nyota yako bado ipo juu nina hakika kwa uwezo wa Mungu mambo yako yatakuwa vizuri muda si mrefu.”

    “Nashukuru sana mama Amina, ila nilikuwa na ombi moja.”

    “Lipi hilo?”

    “Kuhusu kufanana kwa matukio yangu.”

    “Matukio gani?”

    “Ya kuondokewa na wapenzi wangu bila kuelezwa tatizo, naomba leo unieleze kinagaubaga hata kama mama yangu anahusika naomba uniweke wazi nifahamu kisha tujue tufanye nini.”

    “Mwaija mambo mengine hayatakiwi kuchambuliwa, kwa vile tatizo lako limekwisha angalia maisha yako yajayo kwa sasa, yaliyopita achana nayo.”

    “Hapana mama Amina huu utakuwa mchezo wa kuigiza, naweza kupata mwanaume mwingine mambo yakawa yaleyale.”

    “Nakuhakikishia matatizo yaliyotokea hayatatokea tena.”

    “Kivipi?”

    “Tatizo lililokuwepo nimeshalimaliza japokuwa ilikuwa kazi nzito.”

    “Unaweza kuniambia nani aliyefanya mchezo huu?”

    “Wapo wawili, mmoja mke wa huyu mzee, na mwingine nina imani naye ameachana na mchezo huu,” mama Amina alinificha.

    “Nani mama?”

    “Hapana.”

    “Sasa nani?”

    “Shida yako kupona au kumjua huyo mtu?”

    “Vyote.”

    “Naomba basi nisikilize, acha kuchimbua vilivyopita. Mshukuru Mungu kukuponya.”

    Sikutaka kumchimbua sana na kujikuta mawazo yangu nikihamishia kwa mama. Lakini wazo hilo nilipingana nalo kutokana na jinsi mama alivyopigania maisha yangu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog