Simulizi : Mama Yangu Adui Yangu
Sehemu Ya Tano (5)
Naweza kupata mwanaume mwingine mambo yakawa yaleyale."
"Nakuhakikishia matatizo yaliyotokea hayatatokea tena."
"Kivipi?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tatizo lililokuwepo nimeshalimaliza japokuwa ilikuwa kazi nzito."
"Unaweza kuniambia nani aliyefanya mchezo huu?"
"Wapo wawili, mmoja mke wa huyu mzee na mwingine nina imani naye ameachana na mchezo huu," mama Amina alinificha.
"Nani mama?"
"Hapana."
"Sasa nani?"
"Shida yako kupona au kumjua huyo mtu?"
"Vyote."
"Naomba basi nisikilize, acha kuchimbua vilivyopita. Mshukuru Mungu kukuponya."
Sikutaka kumchimbua sana na kujikuta mawazo yangu nikihamishia kwa mama. Lakini wazo hilo nilipingana nalo kutokana jinsi mama alivyopigania maisha yangu.
SASA ENDELEA...
NILIJIULIZA atakuwa nani au dada mkubwa niliyemchukulia mpenzi wake? Lakini kama dada angekuwa amefanya vile alikuwa ananionea kwani tulikubaliana.
Hata wazo hilo bado sikukubaliana nalo kutokana na matatizo ya awali kunitokea nikiwa ndani ya ndoa yangu. Swali likabakia ni nani aliyenifanyia vile, kwa nini mama Amina hakuniambia kama alivyonieleza ya mke wa mzee Sambi?
Swali lile liliniumiza kichwa, sikutaka kumuuliza sana kwani ningemuudhi na kuonesha sina adabu, kama makosa niliyofanya mwanzo. Wasiwasi wangu ulikuwa ni kutokea tatizo lingine na mama Amina kugoma kunisaidia kwa vile si msikivu.
Mama Amina alinipatia dawa za kuoga na makombe ya kunywa. Baada ya zoezi la mwisho alinieleza nifanye chochote bila tatizo. Nilirudi zangu nyumbani kichwa kikiwa kizito huku nikijiuliza kwa nini mtu huyo hatakiwi kutajwa, ni nani?
Nilipanda gari la Mbande - Tandika na kuteremkia Tandika. Kwa vile kulikuwa na njia ya mkato sikutaka kupanda usafiri wowote, nilikatiza kwenda nyumbani.
Nikiwa navuka Barabara ya Devis Kona, nilisikia jina langu likiitwa.
"Mwaija."
Sikuitika mpaka nilipogeuka na kumuona aliyekuwa akiniita. Alikuwa kaka mmoja tuliyekuwa tukikaa mtaa mmoja siku za nyuma, alikuwa kwenye gari.
"Abee," niliitika na kugeuka kumsikiliza.
"Unatoka wapi?"
"Mbagala."
"Kwema?"
"Kwema."
"Kwa vile naelekea maeneo ya kwenu naomba nikusogeze."
"Acha tu nitafika."
"Hapana Mwaija nafika karibu kabisa na kwenu, ingia twende."
Sikutaka kuwa mbishi, nilifungua mlango wa gari na kuingia. Akaondoa gari, tulipokaribia Transfoma, alianza kunisemesha.
"Leo nina bahati ya kuonana na wewe."
"Bahati ipi Juma?" nilimuuliza huku nikimtazama.
"Kwanza pole."
"Ahsante," nilimjibu kwa mkato.
"Nimekufuatilia muda mrefu."
"Kuhusu nini?" nilimkata kauli.
"Subiri basi."
"Haya endelea."
"Mwaija kama usingeolewa na Beka ningekuoa mimi."
"Kivipi?"
"Nilikupenda muda mrefu, huwezi kuamini kila hatua ya maisha yako niliifuatilia mpaka mlipoachana na Beka. Wakati najiandaa kuja kwenu nilipata safari ya ghafla.
"Niliporudi nilikuta unaumwa sana, bado niliendelea kukufuatilia. Leo hii ninaweza kusema hii ni nafasi yangu."
"Nafasi gani?"
"Ya kutuma maombi ya kukuoa."
"Juma naomba sasa hivi suala la mapenzi tuachane nalo."
"Kwa sababu gani?"
"Nahitaji kupumzika, mapenzi yamesababisha nichungulie kaburi."
"Bila matatizo hayo ungekuwa tayari?"
"Ndiyo kwa vile heshima ya mwanamke ni ndoa."
"Kwa nini usinipe nafasi hiyo?"
"Labda baadaye, lakini sasa hivi nahitaji mapumziko ya muda mrefu, kwa sasa nayachukia mapenzi kuliko kitu chochote."
"Kwa hiyo utakuwa tayari lini?"
"Niache kwanza."
Juma alinifikisha nyumbani na kuniacha huku akiniomba awe sehemu ya mawazo yangu ya kila siku. Nilimkubalia ili aniache nipumzike kwa vile bado mbaya wangu aliendelea kuwa siri iliyonitesa sana.
Baada ya kufika nyumbani, niliendelea kutumia dawa nilizopewa na mama Amina huku ombi la Juma likiwa halipo akilini mwangu.
Lakini kumbe kwa mwenzangu ilikuwa tofauti, aliendelea kunifuatilia kwa karibu. Baada ya wiki mbili kukatika, mama aliniita na kunipa taarifa ya kujitokeza mtu wa kutaka kunioa ambaye ni Juma.
"Mama naomba suala hilo tuachane nalo kwa sasa."
"Hapana mwanangu nakuomba ukubaliane nalo."
"Mama nimechoka, kila siku miye tu."
"Kwa nini unasema hivyo?"
"Mapenzi yamekuwa mateso na kutishia uhai wangu kila siku."
"Sasa hivi hayatatokea tena."CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwa nini unasema hivyo?"
"Mimi najua, naomba unisikilize mimi mama yako."
"Mmh! Sawa mama kwa vile nakupenda sana pia umenipigania maisha yangu kwa nguvu zako zote nimekubali."
"Nimefurahi mwanangu kunisikiliza mama yako."
Nilikubaliana na mama kuhusu kuolewa, huku nikishangaa mama yangu kuwa mbele katika kukubali jambo lile tofauti na siku za nyuma.
Majibu yalirudi kuwa nimekubali, mipango ya ndoa ikaanza mara moja. Taarifa ile nilimweleza mama Amina na dada Suzy na wote wakaniunga mkono. Namshukuru Mungu nilipata ushirikiano wa hali na mali kwa familia, muda wote mpaka wakati wa ndoa yangu.
Niliolewa na Juma, mfanyabiashara wa maduka ya nguo na vyombo vya umeme Kariakoo aliyekuwa amejenga Kibamba. Namshukuru Mungu baada ya ndoa nilimuweka wazi mume wangu juu ya maisha yangu niliyopitia na umuhimu na mama Amina kwangu.
Hakuwa na tatizo, alinipa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kumualika mama Amina kwetu japokuwa kwenye harusi yangu alihudhuria na kunipa ushirikiano mkubwa sana.
Kuna kitu kimoja kilinifurahisha, mama Amina japo alikuwa mganga wa jadi naye alikuwa wamo! Akiamua kujilipua na pamba huwezi kuamini kama ni yeye anayevaa kaniki wakati wa kutibu.
Siku ya harusi nilimsahau alivyolipuka na ‘migoldi' iliyomchafua kichwani mpaka mikononi. Alikuwa mganga wa kileo anayekwenda na wakati.
Namshukuru Mungu maisha ya ndoa yalikwenda vizuri, baada ya muda nilishika ujauzito. Mama Amina aliufunga ili nisiupoteze tena.
Mungu alijalia nikajifungua salama mtoto wa kike mwenye afya njema. Kwa kweli maisha niliyoishi na mume wangu yalinikumbusha mbali huku nikiwa na wasiwasi juu ya kutokea yaliyotokea mwanzo.
Nilikuwa na furaha na malezi mazuri ya mume wangu, familia yangu kwa jumla ilikuwa karibu nami. Lakini nilipokumbuka maisha ya zamani na misukosuko, moyo ulikosa raha.
Nakumbuka vizuri siku moja nikiwa Kariakoo, karibu na Kituo cha Msimbazi niliguswa bega na mtu. Nilipogeuka nilikutana na mtalaka wangu Beka.
"Mwaija," aliniita akionesha kunishangaa.
"Abee."
Japokuwa nilimpenda kuliko mwanaume yeyote lakini kitendo alichonifanyia sikumchangamkia, nilimuona mtu wa kawaida.
"Za siku?"
"Nzuri."
"Umeolewa?" aliniuliza baada ya kuona pete ya ndoa kidoleni.
"Uliponiacha ulitegemea sitaolewa tena?" nilijikuta nikizungumza huku nimebinua midomo japokuwa sikukipenda kitu kile katika maisha yangu.
"Mwaija bila vile ningebakia jina," Beka alisema kwa sauti ya majonzi.
"Si nilikuuliza nani anataka kukubakiza jina hukuniambia ikabaki siri yako na familia yako huku ukitaka kunigombanisha na mama yangu?"
"Samahani tutafute sehemu nzuri, tuzungumze vizuri."
Leo ndiyo unaweza kumsema? nilimuuliza nikiwa nimemkazia macho.
Kama mpaka leo hujui tatizo lazima nikueleze huenda likaiokoa ndoa yako ya sasa.
Kauli ile ilinifanya niwe na hamu ya kumsikiliza. Tulisogea kwenye mgahawa uliokuwa karibu na kutafuta meza ya pembeni.
Baada ya kukaa tuliagiza vinywaji, nilitulia kumsikiliza Beka mtalaka wangu, bwana na mwanaume wa usichana wangu ambaye alionekana maisha si mabaya.
Mwaija najua unaweza kunichukia na kuniona adui yako kutokana na kushindwa kusema ukweli. Lakini nilifanya hivyo kulinda amani iliyo ndani ya familia yenu.
Nina imani mama yako unampenda sana na unamuamini kwa kila kitu.
Ndiyo.
Ni vigumu kuamini mama yako ndiye aliyekuwa adui yako namba moja.
Etiii!? nilishtuka kusikia vile.
Ndiyo maana sikutaka kuyasema hayo kipindi kile kwa vile tungeweza kupotea wote kabla siri haijatoka nje.
Una maana gani? sikumuelewa alimaanisha nini.
Mwaija nina imani unanijua vizuri kuliko mtu yeyote.
Ndiyo.
Na maisha yangu unayajua vizuri?
Ndiyo.
Baada ya ndoa yetu kupigwa mizengwe na wewe kusimama kidete, mwisho tulifanikiwa kuoana. Namshukuru Mungu baada ya ndoa maisha yalikuwa mazuri sana, mpaka tukanunua kiwanja na kuanza ujenzi.
Ni kweli.
Tatizo lilianza baada ya kubeba ujauzito, uongo kweli?
Ni kweli.
Na ujauzito wako ulitoka katika mazingira ya utatanishi?
Ni kweli kabisa.
Na baada ya hapo ndipo mikosi na mabalaa yalipoanza mpaka nikakosa hata kazi na wewe ni shahidi ulifuata fedha kwenu.
Ndiyo.
Kwa kweli sikujua chochote kuhusiana na matatizo yale kwa kuamini ni mipango ya Mungu. Lakini nilishikwa mkono na rafiki yangu aliyeshangazwa na anguko langu la ghafla na kunipeleka kwa mtaalamu, Handeni, Tanga.
Nilipofika huko niliyoyasikia kwanza sikuamini, niliamini mganga ni muongo. Alinieleza mambo mengi kuhusiana na matatizo yangu mpaka ya ndani ya familia yako.
Eeh! nilishtuka kusikia vile.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-
Eeh! Ndiyo, alisema chanzo ni mama yenu ndiye aliyefanya mambo ya kishirikina kwa kukutega mlangoni, uliporuka ujauzito ukatoka kisha akaanza kuniwangia mpaka mambo yangu yakawa hayaeleweki.
Alikwenda kwenye kiwanja na kuifunga nyumba yetu iliyokuwa kwenye hali nzuri ili tusiendelee huku akifunga riziki kila kona. Baada ya kuona pamoja na hali ya maisha kuwa mbaya lakini hutaki kuachana na mimi, alianza kuitafuta roho yangu kuhakikisha ananitenganisha na wewe.
Ilionesha hata kama ningekueleza usingekubali kitu ambacho kingefanya nipoteze maisha kwa vile alikuwa na nafasi ya kuja kwetu angenimaliza kwa urahisi.
Japokuwa maneno ya mganga yalikuwa yakifanana na kweli, bado sikukubaliana naye kwa kuamini kauli ile ni ya uchonganishi ambayo ndiyo chanzo cha vitabu vya dini kuikataa ramli.
Ukweli kuamini moja kwa moja nilishindwa wala kukueleza jambo zito kama hilo ambalo lazima lingeleta mpasuko. Nilimueleza mganga jinsi mama mkwe alivyonisaidia mpaka hata kupata nauli ya kwenda kule.
Alinieleza kama siwezi kukueleza basi niachane na wewe. Ilikuwa vigumu kukubali kuachana na wewe mke wangu kipenzi ambaye naamini mpaka nakufa sitapata mwingine kama wewe.
Mwaija hata sijui kwa nini nilichukua uamuzi huo heri ningesema mapema kwa jinsi ulivyokuwa ukinipenda ungeweza kunisikiliza lakini wasiwasi wangu ndiyo ulionifanya nilie kila siku kukukumbuka mke wangu mpenzi.
Basi mganga alinieleza nichague moja katika ya matatu. Nikueleze ubaya wa mama yako, kama nikishindwa nikuache huku nikikueleza kila kitu anajua mama yako na kama ungemwambia angeujua ubaya wake au vyote vikishindikana nikubali kufa.
Maneno ya Beka yalinisisimua mwili na kuanza kuamini yote aliyosema hasa baada ya mama Amina kukataa kunitajia mbaya wangu. Niliendelea kumsikiliza mtalaka wangu huku mapigo ya moyo yakinienda kasi.
Kwa kweli bado sikuwa tayari lakini alinichambulia moja baada ya lingine kama ameniumba yeye, hata sababu ya dada zako kuachika na kutokuwa na wazo la kuolewa tena. Kama mtu akitokea anataka kuoa basi hugeuka ugomvi na kumfukuza kama mbwa.
Maneno yale yalikuwa na ukweli kwa sababu dada alimfukuza mzee Sambi baada ya kutaka kumuoa.
Basi alinipa mtihani mmoja ili kuhakikisha anachosema ni kweli, aliniambia angenipa kitu ambacho ningekuja nacho kwenu. Mama yako angeniona angeanguka.
Alinieleza baada ya tukio lile nilitakiwa nikuache na kuondoka haraka kwani kama ningeendelea kuwepo kwenu mama yako angekufa.
Ni kwa nini? niliuliza mkono shavuni.
"Kwa sababu ya ubaya wake," alisema.
"Unafikiri kwa nini amekuwa na tabia hiyo?" nilimuuliza swali ambalo nilitakiwa nilijibu mimi mwenyewe.
"Ni roho mbaya na kupenda kushiriki mambo ya kishirikina yamemfanya apende kucheza michezo ya kichawi."
"Enhee, nini kiliendelea?"
"Kwanza nilikataa na kuamua kuachana na wazo hilo. Baada ya kubahatika kupata kazi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Tanga.
"Nilifanya kazi kule kwa muda huku nikiwa na wazo la kutafuta njia mbadala tofauti na maelezo ya mganga.
"Lakini mganga alinieleza kama sijipendi nifanye kinyume na alivyonieleza. Baada ya kufanya kazi kwa muda nilipata nafasi ya kurudi nyumbani.
"Kabla ya kuja Dar nilirudi kwa mtaalamu ambaye alinieleza nifanye kama alivyonielekeza na kuniambia mambo nitakayoyakuta siku nitakayokuja kwenu na hali itakayojitokeza.
"Niliporudi Dar sikukaa, nilikuja kwenu na kila nilichoelezwa na mganga kilitokea ikiwa ni pamoja na mama yako kuanguka alipokuwa amekaa baada ya kushtuka aliponiona.
"Kwa kweli tukio lile lilinifanya nichukue uamuzi mgumu wa kukupa talaka na kukuacha na fumbo kuhusiana na talaka yako.
"Niliamini mama yako angekueleza lakini hakukueleza, nilipoondoka sikutaka kujua habari za nyuma. Leo unaponiona nina siku mbili na kesho naondoka kurudi nilipo, kwa yaliyonitokea nimejikuta sipendi tena kukaa katika jiji hili."
Mpaka Beka anamaliza kunieleza chanzo cha talaka yangu, macho yake yalikuwa yamejaa machozi. Si yeye tu, hata mimi muda wote nilikuwa nikilia huku nikitumia mtandio wangu wa kichwani kujifuta machozi.
Nilijitahidi kuzungumza japokuwa moyo wangu ulikuwa kama amechubuliwa katika kovu lililoanza kupona na maumivu yake yakawa mara mbili.
"Beka nakubaliana na wewe kwa asilimia mia kuwa, mama yangu anahusika lakini bado hukutakiwa kuutesa moyo wangu kwa maswali yasiyo na majibu.
"Najua pengine mimi ndiye niliyesababisha kwa kutoa siri ya kipato chetu kwa mama ila kwa vile ni mkeo ulitakiwa kuniweka wazi. Siamini kama kuna mwanadamu anaweza kuua bali kwa idhini ya Mungu.
"Hata kwenye riziki binadamu anaweza kuichelewesha si kuizuia kabisa.
"Beka ungekuwa wazi ningejua nifanye nini, pengine ukimya wako umenifanya nichungulie kaburi au ningezikwa ningali hai."
"Kwa nini?" Beka aliuliza macho yakiwa yamemtoka pima.
Nilimueleza yote yaliyotokea baada ya kunipa talaka, maisha niliyoishi na kufikia kuugua ugonjwa wa ajabu.
"Dah! Pole sana Mwaija, nina imani hata huyo bwana kuondoka kwake inawezekana mama yako amechangia."
"Inawezekana," nilimkubalia.
"Lazima ujiulize kwa nini mtu akukimbie wakati wa matatizo?" aliniuliza.
"Beka nashukuru kwa maelezo yako ambayo naamini yamechelewa kunifikia, nina imani leo hii tungekuwa pamoja."
"Ni kweli lakini sina wa kumlaumu bali wasiwasi wa nafsi yangu."
"Beka naomba nikapumzike kwa vile sijisikii vizuri, pia mwanangu nimemwacha muda mrefu."
"Ha! Mwaija una mtoto?" Beka alishtuka.
"Beka uliambiwa mi mgumba?"
"Mmh! Sawa," Beka alishusha pumzi nzito na kuinamisha kichwa.
"Beka naomba niondoke, kwani hali yangu siielewi nahisi mapigo ya moyo yananienda kasi," niliongea kwa shida kidogo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hakuna tabu Mwaija kwa vile nina gari nitakupeleka."
"Hapana Beka, nitakodi teksi au nitamwita mume wangu anifuate."
"Kwa nini usumbuke nitakupeleka mara moja, kwa hali hii siwezi kukuacha peke yako."
"Hakuna tatizo."
Ilibidi nikubali kwa vile sikuelewa baada ya muda hali yangu ingeendeleaje. Kila nilivyofikiria nilikosa jibu na kujikuta moyo ukiniuma kama unataka kutoka na kuachana na mwili wangu.
Beka alinipeleka mpaka kwangu kwani hata nguvu za kutembea sikuwanazo. Nashukuru nilifika nyumbani salama na kuagana na Beka huku tukipeana namba za simu kwa ajili ya kuendelea kusalimiana kama marafiki si wapenzi tena.
Nilipofika ndani hali ilizidi kuwa mbaya, kila nilipoyakumbuka mambo yote yaliyokuwa yamejificha nyuma ya pazia.
"Kumbe mama yangu ndiye adui yangu!" nilijiambia mwenyewe moyoni.
Kichwa kiliniuma na mapigo ya moyo yalinienda kasi, nilimwambia msichana wa kazi amjulishe mume wangu kwa vile hata uwezo wa kupiga simu sikuwa nao.
Mume wangu baada ya kupewa taarifa alifika mara moja na kunikimbiza hospitalini. Niliambiwa kuwa presha ilikuwa juu sana na kuwafanya madaktari kupata kazi ya kuishusha.
Walifanikiwa baada ya saa mbili ndipo nilipata usingizi mpaka asubuhi. Taarifa zilimfikia mama, naye akawa wa kwanza kufika hospitalini na kufuatiwa na dada zangu.
Siri ya matatizo yangu sikumueleza mume wangu, alijua ni matatizo ya kawaida japokuwa hali ile haikuwahi kunitokea tangu aliponioa. Mama naye alishangaa na kutaka kujua presha ile ilisababishwa na nini.
Nilishindwa kumueleza ukweli, nilisingizia imetokea ghafla japokuwa mama alikataa katakata maelezo yangu.
"Hapana Mwaija, kwa maelezo aliyonipa mumeo nahisi kuna kitu mnanificha.Hebu niambie mama nini kimekusibu? Madaktari wamesema presha ile ingeweza kukupofua macho au kukufanya upooze mwili."
"Hata sijui nimejisikia tu mwili ukikosa nguvu na kumpigia simu mume wangu ambaye alinieleta hapa," bado niliificha siri ile.
"Mwaija mi' mtu mzima maisha ya ndoa nayajua, kama kuna kitu mumeo amekuudhi niambie ili tujue tufanye nini, sitaki yatokee ya mzee Sambi."
"Haki ya Mungu, kuhusu mume wangu utamuonea. Ananitunza kama malkia, hajawahi hata kunikemea tangu anioe na ananipenda kwa mapenzi ya dhati."
"Sasa tatizo ni nini?"
"Mama ni hali umenitokea tu, hata sielewi, pengine ni mawazo ya kutaka kuzikwa ningali hai, kila nikikumbuka moyo unanipaa," nilitengeneza uongo uliomfanya mama aamini.
"Lakini mwanangu mambo hayo si yameshaisha? Sasa hivi una ndoa yako nzuri, pia una mtoto, hebu achana na mambo hayo ili kuondoa kuishi kwa wasiwasi."
"Sawa mama nimekuelewa nitajitahidi kusahau."
"Itabidi ufanyiwe na kisomo."
"Hakuna tatizo."
Kila alilokuwa akilifanya mama na kutoa maneno yenye faraja, yaliufanya moyo wangu uzidi kuwa njia panda kwa kutoamini kama mbaya ni yeye.
Niliamini lile lilikuwa fumbo zito ambalo alilifahamu mama Amina peke yake, yeye ndiye aliyekuwa na majibu ya maswali yangu. Nilipanga nikitoka hospitali na kutulia, nimfungie safari ili akanieleze ukweli, nilikuwa radhi kumpa kiasi chochote atakachokitaka ili tu anieleze ukweli.
Baada ya hali yangu kuwa nzuri niliruhusiwa na kurudi nyumbani. Mume wangu naye alitaka kujua sababu ya tatizo lile kama alikuwa amelisababisha yeye. Naye nilimdanganya sababu ile ilitokana na kukumbuka hali iliyonitokea siku za nyuma.
Alinisihi nisiwaze vitu vilivyopita kwa vile ananitunza kama mboni ya jicho lake. Nilimhakikishia hali ile haitajitokeza tena, maneno yangu yalimfariji mume wangu na kurudisha tabasamu lililopotea baada ya kuwa na wasiwasi wa tatizo langu.
Nilijitahidi kuwa katika hali ya kawaida ili niweze kuwatoa wasiwasi wote na kunipa nafasi ya kuweza kwenda kwa mama Amina. Siku zilikatika nikiwa katika hali ya kawaida.
Baada ya wote kuamini kuwa nilikuwa sawa, nilifunga safari hadi kwa mama Amina ili kujua ukweli.
Aliponiona nikiwa katika afya njema na mwili wangu ukiwa umerudi kama zamani, alifurahi sana.
Baada ya wote kuamini nipo sawa nilifunga safari hadi kwa mama Amina kutaka kupata ukweli. Aliponiona alifurahi kuniona nikiwa katika afya njema huku mwili wangu ukiwa umerudi kama zamani.
Kwa vile nilikuta watu wengi wakisubiri huduma nami nilikaa kusubiri. Baada ya muda niliitwa ndani, niliingia na kwenda kukaa kwenye mkeka.
Mwaija naona leo mdogo wangu umenitembelea, vipi familia yako?
Namshukuru Mungu haijambo.
Una habari gani?
Mama Amina naomba msaada wako ambao ni muhimu kuliko kitu chochote.
Msaada gani?
Kuna jambo umekuwa ukinificha kwa nini usinieleze ili nimjue mbaya wangu?
Mwaija, mbaya wako wa nini, tatizo limekwisha unataka kuchimbua nini?
Mama Amina ukweli nimeujua lakini nataka msaada wako ili yasijetokea tena.
Ukweli gani?
Nilimweleza yote niliyoelezwa na Beka kuhusu mama ambayo yalikuwa na ukweli asilimia kubwa. Maelezo yangu yalimshangaza sana mama Amina ambaye aliamini pengine nilichokisema nisingekijua.
Baada ya kushusha pumzi ndefu mama Amina alisema:
Unayosema ni kweli lakini hakukuwa na umuhimu wa kukueleza kwa vile mbaya wako alijisalimisha na kuzivunja nguvu zake, hivyo hakuwa na madhara tena.
Lakini aliyefanya vile ni mama yangu? nilimuuliza huku nikimtazama usoni.
Ndiyo, lakini sasa hivi hana ubaya wowote baada ya kukubali kuzivunja nguvu zake za kishirikina.
Hizo nguvu zake zimevunjwa wapi?
Hapahapa kwangu.
Ilikuwaje mpaka akakubali zikavunjwa hizo nguvu zake?
Baada ya tatizo lako kupelekwa kwa mtaalamu wake ambaye kama angeweza kulitatua tatizo la mke wa bwana uliyekuwa naye basi siri hii ingeendelea kuitafuna familia yenu.
Lakini Mungu naye ana mambo yake, baada ya kushindikana na wewe kuzidiwa sana na kuletwa kwangu. Hakuwa na jinsi ilibidi ajivue nguo ili kuokoa maisha yako.
Kabla ya kuanza kukuhudumia nilipoangalia niliyaona madudu yake. Kutokana na matatizo yako kuwa ya muda mrefu nisingeweza kukutibu juujuu bila kuanza kungoa mzizi. Hakukuwa na njia nyingine ya kuvunja nguvu za mama ili niweze kukupata vizuri.
Ilikuwa kazi kubwa, lakini kutokana na hali yako ilivyokuwa na kumuhakikishia utapona alikubali. Basi nikavunja nguzo zote alizokuwa nazo na kumsafisha kisha nikawaosha na dada zako wote.
Mama alisema alifanya vile kwa ajili gani?
Basi tu alipenda kushiriki mambo ya kishirikina ambayo sitakueleza kwa vile si sehemu yake zaidi ya kukueleza yanayokuhusu.
Ukiingia katika mchezo ule uchelewi kujiunga kwenye chama cha waharibifu, si wachawi bali wanaozunguka kwa waganga kuharibu maisha ya watu kama kuwaharibia watu kwenye kazi au kuharibu ujauzito wa mtu kwa wivu tu wa kijinga.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ina maana kuna watu wengine wanaendelea na mchezo ule aliokuwa nao mama?
Ndiyo, tena baada ya kujitoa watamsumbua sana. Juzi tu nimemtoa kitu kizito walichomtupia washirika wake kwa sababu ya kujitoa kwenye chama chao.
Mmh! Kwa hiyo sasa hivi mama ajihusishi na mchezo huo?
Umegundua mabadiliko gani kwenye familia yako ambayo siku za nyuma hayakuwepo?
Kuna tofauti kubwa sana, sasa hivi mama swala tano.
Basi shukuru Mungu mama yako amerudi kwenye mstari sahihi.
Nakubaliana na wewe kuwa kuna mambo mengi yamebadilika kwa sasa, dada wa kati sasa hivi anafanya kazi tofauti na zamani kwani alikuwa mtu wa starehe na kushinda nyumbani tu. Kingine nimeambiwa na mama kuwa dada mkubwa amepata mchumba.
Tatizo lilikuwa kwenye vifungo lakini baada ya kuvifungua na kuondolewa nuksi kila mmoja mambo yake yamemnyookea na dada yako anayetaka kuolewa ni mjamzito kwa sasa.
Usiniambie! nilishtuka kusikia vile.
Kila kitu sasa hivi tambarare mengine yakija itakuwa ni kudra ya Mungu si mkono wa mtu.
Nashukuru kwa maelezo yako pia nashukuru kwa kumuokoa mama yetu toka kwenye kundi baya.
Ndiyo kazi yetu kuona tunatumia fani yetu kutengeneza si kuharibu. Kuna kitu kimoja kinamuumiza mama yako kuhusiana na aliyoyafanya kwa kweli kinamkosesha raha, nimejitahidi sana kumtuliza.
Mama yenu anajua hamjui chochote na hataki mjue alifanya nini. Nina imani akijua umefahamu ataumia mara mbili.
Nataka kumweleza mama ukweli japokuwa sina ujasiri huo.
"Nakushauri ungeachana nayo kwa vile umeelewa nawe umekuwa tayari kumsamehe."
"Sawa, nimemsamehe mama kwa vile nampenda sana."
Baada ya maelezo ya mama Amina nilirudi nyumbani kwangu nikiwa kidogo na afadhali baada kuutua mzigo mzito ulionisumbua lakini nilijiuliza kwa nini nisimueleze ili ajue alichotufanyia wanaye.
Kutokana na maelezo ya mama Amina jinsi mama yangu anavyoumizwa na matendo yake nilishindwa kumweleza na kuamua kumsamehe kwa vile tayari alikuwa amerudi kwa mola wake.
Siyo siri nilikuwa nampenda mama yangu sana kwa malezi yake. Nilishtuka sana kusikia ndiye aliyekuwa adui yangu mkubwa.
Lakini nilifarijika baada ya kujirudi na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaye tunaishi katika mstari mzuri baada ya kupotea.
***
Siku zilikatika nikiwa na siri yangu moyoni huku nilijitahidi kuyasahau yote yaliyotokea.
Nilijikuta nikimpenda zaidi mama yangu pamoja na yote aliyonitendea. Kila nilipokumbuka yaliyonitokea, nilijifungia ndani na kulia huku nikizidi kumuomba Mungu amsamehe mama yangu.
Niliwaza sana kuhusu siri ile kuwaambia dada zangu, bado nafsi ilinisuta kwani niliamini kuwaeleza wasiyoyajua ni sawa na kumvua nguo mama yangu.
Mama alibadilika sana baada ya kuanza kuswali na kuachana na pombe, alikuwa mpole na mtu mwenye mawazo mengi sana kila alipokuwa peke yake.
Dada zangu walishangazwa na hali ya mama kurudi katika ibada, kuacha pombe na tabia zote mbaya.
Alikuwa mkali kwa mambo machafu na kuwaeleza waige mfano wangu wa kuolewa na si kuzini ovyo.
CD za taarabu alizipiga marufuku nyumbani na kuifanya nyumba kupoa huku majirani wakishangazwa na hali hiyo kwani sauti za muziki siku za nyuma zilikuwa juu na kuwakera.
Pia, mabadiliko ya mama yaliwashangaza na kuifanya nyumba yetu irudishe heshima ya wakati wa uhai wa marehemu baba.
Taarifa zilizotoka kwa dada zangu zilisema mama amebadilika sana hakai tena sebuleni kama zamani muda mwingi alikuwa akishinda ndani kwa ajili ya kuswali, muda mwingi alikuwa akipenda kukaa peke yake na alipotoka alionesha kuvimba macho akionesha alikuwa akilia.
Japokuwa mabadiliko yale yalikuwa mazuri, lakini hali ya mama ya kukosa raha na kushinda chumbani peke yake hata sisi wanawe ilitunyima raha.
Wasiwasi wangu ulikuwa labda mama anateseka na aliyotufanyia. Niliingiwa na wasiwasi wa kumpoteza mama kwa kuhofia kwamba angeweza kufa kwa kihoro.
Maana aligeuka na kuwa kama mgonjwa, alianza kupungua kila siku mpaka kupelekea kuugua vidonda vya tumbo. Hali ile ilitufanya tukutane kutaka kujua kipi kimemsibu mama yetu japokuwa niliamini aliyoyafanya ni sehemu ya maumivu ya majuto.
Kila tulipomuuliza mama kuhusu matatizo yake aliishia kulia, nilikuwa na wasiwasi wa kuwaeleza dada zangu tatizo la mama na jinsi lilivyotokea.
Niliamini mtu wa kutusaidia kipindi kile alikuwa ni mama Amina. Niliamua kwenda kwake na kumuomba ushauri kuhusu tatizo la mama.
Alinieleza tatizo la mama yetu linatokana na kuumizwa na vitendo alivyotufanyia wanawe.
"Mama yenu anashindwa kuwaeleza ukweli tatizo hilo kwa kuhofia kwamba mnaweza kumtenga na kumfanya afe kwa kihoro. Nilimhakikishia hakuna tatizo litakalotokea bila kumueleza kama wewe unajua kila kitu."
"Sasa tufanyeje? Maana hali ya mama ni mbaya. Mimi nimemsamehe leo na kesho kiama, nina imani hata dada zangu pia watamsamehe."
"Mwaija najua sasa hivi moyo wako umetulia, mfuate mama yako na umueleze unayoyajua kuhusu yeye na kuonesha umemsamehe ili kuondoa donge moyoni mwake."
"Mmh! Nitaweza, nina wasiwasi mama yangu anaweza kulia mbele yangu. Nampenda sana mama yangu na naumia na hali yake pia nitaumia zaidi akilia," nilishindwa kuzizuia hisia zangu.
"Sasa tutafanya nini?"
"Mama Amina kaa na mama na umweleze yote kisha tukutanishe wote, nina imani una nafasi ya kurejesha furaha ndani ya familia yetu. Siyo siri sisi wote kwa sasa hatuna raha."
"Nitafanya hivyo, wewe nenda kesho nitakuja."
"Mama Amina wewe ndiye tegemeo langu la mwisho kwa mama yetu."
"Shaka ondoa mdogo wangu, mama yetu atarudi katika hali yake ya kawaida maadamu mmeamua kulimaliza."
Niliachana na mama Amina na kurudi nyumbani. Sikuwa na furaha kwa kusubiri simu ya mama Amina kuhusu mama amepokeaje alichomueleza.
Siku iliyofuata nilikuwepo nyumbani lakini mawazo yangu yalikuwa mbali sana. Nilisubiri simu ya mama Amina kwa shauku kubwa. Nikiwa namalizia kumuosha mtoto simu iliita, mapigo ya moyo yalinibadilika ghafla, nilimuacha mtoto kwenye beseni na kuikimbilia simu sikutaka kumtuma msichana wa kazi aifuate niliona kama angechelewa.
Lakini haikuwa ya mama Amina, nilijikuta nikichukia. Baada ya kuzungumza nilirudi kumalizia kumuosha mtoto. Kabla sijaanza kumuosha iliita tena. Nilimtuma msichana wa kazi.
"Niletee," hamu yote iliniisha.
Alipokuwa ameishika nilimuuliza nani, akaniambia mama Amina. Nilimwacha mtoto na kuwahi kama itakatika na salio sikuwa nalo.
"Haloo," nilipokea huku mapigo ya moyo yakiwa juu.
"Vipi mbona unahema?"
"Mwenzangu, hata sijielewi mama kanichanganya sana, vipi umeishafika nyumbani?"
"Ndipo ninapoongelea."
"Umeishazungumza na mama?"CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndiyo."
"Amesemaje?"
"We upo wapi?"
‘Nyumbani."
"Njoo basi mara moja."
Nilishindwa kuendelea kumuosha mtoto nilimfuta na mimi kubadili nguo bila kuoga na kuondoka. Nilipofika barabarani nilikodi teksi kwenda Tandika kwa mama.
Bahati nzuri kipindi kile hakukuwa na foleni kubwa barabarani kama sasa. Gari lilikwenda mpaka njia panda ya Mandela na Tazara Vetenari ilikata kulia.
Nilifuata barabara ya Vetenari kabla sijafika maghorofa ya Tazara nilishangaa dereva kusimamisha gari pembeni karibu na kituo kidogo cha polisi.
"Vipi mbona unasimama?"Nilimuuliza dereva.
Kuna gari nyuma limeonesha ishara ya taa tusimame sijui ana shida gani.
"Sawa," nilitulia sikushughulika naye nilijua ni watu wake.
Baada ya muda nililiona gari la mzee Sambi likisimama mbele yetu. Nilishtuka mpaka mapigo ya moyo yakanienda mbio. Baada ya gari kusimama alishuka mzee Sambi na kuja kwenye gari letu.
Alipofika alitoa miwani yake na kusema kwa kushtuka:
"Ni wewe Mwaija?"
"Ndiye mimi, ulijua nitakufa?"
"Sivyo Mwaija ni historia ndefu."
"Ya kunitaka kuniua na kunidhurumu mali yangu?"
"Mwaija naomba tukae pembeni tuzungumze."
"Katu sitazungumza na wewe muuaji," nilimjibu kwa hasira.
"Usiniite hivyo Mwaija nipe nafasi unisikilize."
"Ili?"
"Utajua sababu ya mimi kuondoka ghafla."
"Nikijua itanisaidia nini, nilikufuata kukuliza?"
"Ha! Mwaija umeolewa?" mzee Sambi alishtuka baada ya kuiona pete ya ndoa kutokana na kurusha mikono yangu wakati nilipokuwa nikiongea.
"Ulifikiri siolewi?" nilimjibu kwa nyodo.
"Na huyo mtoto ni wako?" alizidi kushtuka kila dakika.
"Ndiyo, uliambiwa mi ni mgumba?" nilimjibu kwa nyodo.
"Mwaija angekuwa wangu huyo, mama yako anahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga uhusiano wetu."
"Aliyetaka kuniua ni mama yangu au mkeo?"
Muda wote dereva wa teksi alikuwa akitushangaa kwa jinsi tulivyokuwa tukitupiana maneno.
"Huwezi kunielewa naomba basi uje kwenye gari langu tuzungumze."
"Mlinikosa kuniua hamtanipata tena, ulimtuma mkeo aniue ili mchukue nyumba. Sawa, mmechukua vyote hivyo, lakini sijawafuata kuwaulizia kitu chochote."
"Mwaija nyumba bado ni yako."
"Usinichefue, kukusikiliza usinifanye mjinga, uliniambia nini kuhusu mkeo na matokeo yake kimetokea nini? Kwa taarifa yako najua kila kitu katika ile nyumba."
Nilimweleza yote tangu siku nilipokwenda na kumkuta na mkewe wakiwaonesha wapangaji nyumba. Nilimuona akishangaa kama kaona meli barabarani.
"Basi naomba tuzungumze Mwaija ili unielewe nipo radhi kukupa chochote ili tuondoe tofauti zetu."
"Naomba hayo tuachane nayo, endelea na maisha yako na mkeo mchawi. Acheni kuwaroga watoto wa watu kwani mnawaharibia mambo yao."
"Mwaija maneno gani hayo?"
"Tuachane na hayo, naomba uendelee na safari yako."
"Sasa?"
"Kuhusu nini?"
"Nipe hata dakika tano."
"Nimeitwa nyumbani mama anaumwa naomba uniache niwahi."
"Naomba namba yako ya simu."
"Siwezi kukupa, mume wangu ana wivu sana."
"Sasa ita.."
"Dereva hebu tuwahi safari yetu."
Dereva aliondoa gari na kumuacha mzee Sambi akiwa amesimama barabarani. Dereva hakuniuliza mpaka tulipofika kwenye kona ya Maguruwe.
"Dada vipi?"
"Achana naye," nilimijibu kwa mkato.
Nilijikuta nikiwa mtu mwenye hasira baada ya kuachana na mzee Sambi mpaka machozi yalinitoka huku kifua kikinijaa kwa hasira. Nilifika nyumbani na kumlipa dereva kisha niliingia ndani.
Nilipokelewa na mama na ndugu zangu pamoja na mama Amina.
"Karibu mama yangu," mama Amina alinitania kutokana na kumwita mwanangu jina lake kama shukurani kwake kwa kuwa sehemu ya kupatikana kwa mwanangu.
"Asante, shikamoo."
"Marahaba mama yangu."
"Shikamoo mama," nilimgeukia mama.
"Marahaba, za nyumbani?"
Mama yangu aliitikia kwa unyonge, hali ile ilizidi kuniumiza moyoni.
"Nzuri mama, shikamooni dada zangu."
"Marahaba mama Husna," waliitika wote.
Nilikwenda kukaa pembeni ya mama na kumpa mjukuu wake, alimpokea na hapohapo nikagundua mama alikuwa akitokwa na machozi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuketi mama Amina alifungua kikao kile cha kifamilia.
"Jamani nina imani mtashangaa kuuona uwepo wangu hapa kwenu kwa muda huu," alianza kuzungumza mama Amina.
"Walaa," tulijikuta tukijibu kwa pamoja.
"Basi leo sikuja kama mlivyonizoea, kuna jambo zito limenileta ambalo nina imani hamlijui lakini mama yenu anataka mlijue kabla mauti hayajamchukua.
"Nina imani hivi karibuni mmeona mabadiliko ya hali ya mama yenu?"
"Ni kweli," tulijibu kwa pamoja.
"Nina imani hali hii imewashtua sana na kukosa jibu, ni kweli?"
"Kweli," dada alijibu.
"Nina imani mi si msemaji ila mzungumzaji mkubwa ni mama yenu ataeleza kinachomtesa moyoni mwake."
"Hakuna tatizo," dada mkubwa alijibu.
"Kabla sijamkaribisha mama yenu naomba kuwauliza."
"Uliza tu," tulimkubalia.
"Je, mnampenda mama yenu?"
"Zaidi ya sana."
"Kama amewakosea mpo tayari kumsamehe?"
"Leo mpaka kesho kiama," tulijibu wote kwa vile tulikuwa tukimpenda sana mama yetu.
Haya mama Zamda hebu toa dukuduku lako wanao wamesema wamekusamehe leo na kesho kiama.
Wote tulihamishia macho yetu kwa mama aliyekuwa ameweka mkono shavuni. Mama alitoa mkono shavuni na kufuta machozi kwa mtandio kisha alikohoa kidogo na kupenga makamasi na kujifuta kwa kitambaa kidogo cha mkononi kisha alisema kwa sauti ya kujilazimisha:
Nikuwa na mtihani mzito baada ya kugundua nilichokifanya si sahihi hasa kwa mzazi kama mimi. Lakini nimekuwa na wakati mgumu kuyasema haya kwenu.
Kwangu ni sawa na kutembea bila ya nguo mbele ya kadamnasi, lakini sina jinsi lazima niseme. Namuomba Mungu anipe nguvu ya kuweza kuyasema haya.
Nina imani huenda wanangu mnasema mtanisamehe mama yenu kwa vile hamjui kipi kibaya nimewafanyia ambacho kinaweza kuwafanya mkanichukia na kutaka hata tusizikane kitu ambacho nina imani kitaniweka katika wakati mgumu sana hata kusababisha nife kwa kihoro.
Mama kwa lolote baya hata kama ulitaka kutuua mimi nakutoa wasiwasi, kwa upande wangu nilichosema sitabadili kauli yangu. Kama nitafanya hivyo basi Mungu anifufue nguruwe siku ya kiama.
Nilijikuta nikisema kwa uchungu mpaka machozi yakanitoka huku moyo ukiniuma. Niliamini mama yetu alikuwa na mzigo mkubwa moyoni mwake kuyaanika mabaya yake kwa kinywa chake.
Niliamini kuyasema yale ilikuwa njia ya kumpa nafuu mama kwa kile alichotaka kukitoa mbele yetu. Dada zangu nao waliungana nami kumhakikishia mama hakuna atakaye badili kauli ya kumsamehe.
Baada ya kauli yangu mama alishusha pumzi ndefu na kusema:
Kwanza napenda kumshukuru Mungu kunipa watoto wenye mapenzi makubwa kwangu japokuwa mama yenu nilikosa mapenzi ya dhati kwenu japo niliamini nawapenda sana lakini mapenzi yangu kwenu yaligeuka sumu.
Pia namshukuru mama Amina Mungu amzidishie, kwa umri namzidi sana lakini amekuwa mwanamke shupavu mwenye moyo wa kipekee kuipigania familia yangu, Mungu atakulipa.
Amina, aliitikia mama Amina.
Mama alianza kumwaga siri zake kwa kujilazimisha kama mtu aliyekuwa akinyweshwa shubiri. Kuanzia siri nzito ambayo hatukuijua ya kifo cha baba kuwa yeye ndiye alichangia.
Wanangu kifo cha baba yenu naweza kusema mimi ndiye chanzo. Kilitokana na mateso mazito yaliyofanya mimi mama yenu niingie kwenye mchezo mbaya.
Baba yenu aliondoka nyumbani nikiwa na ujauzito wa miezi miwili wa Mwaija na kuhamia kwa mwanamke wa nje.
Mwanzo sikushtuka kwa vile mahitaji yote ya muhimu nilikuwa nayo nilijua atarudi. Lakini adha ya mateso ilianza baada ya kuishiwa kila kitu ndani. Kwa kweli niliteseka kufikia hatua ya kushinda na njaa mimi na ninyi wanangu, kibaya nilikuwa mjamzito.
Yeye baba yenu alikuwa ameshikwa na mwanamke wa nje ambaye alimfanyia madawa na kumfanya aisahau familia yake.
Kila kukicha hali ilizidi kuwa mbaya nikawa napita kwa majirani kuwaombea chakula. Kuomba kila siku nilishindwa na kuamua siku nyingine kuwakorogea uji bila sukari.
Maisha yangu yalikuwa magumu sana kwani kuna wakati nililazimika kushinda na njaa, nikawa mtu wa kuwaza tu. Nilikuwa nakonda kila siku na kushinda nalia kutokana na mateso mliyokuwa mkiyapata wanangu.
Kuna siku mlishindwa kunyanyuka kitandani kutokana na njaa, Nilijikuta naingia nyumba ya jirani na kuiba unga. Nilishindwa na kuwa aibu mtaani.
Nilijikuta nikipata mawazo mengi kufikia kuwaza kunywa sumu, lakini moyo ulinisuta kufanya hivyo kwa vile ningetoa uhai wa kiumbe kisicho na hatia pia kuwaacha wanangu kwenye mateso mazito.
Siku moja nilipata wazo baada ya kumuona mwanamke mmoja akiuza mboga za majani huku akiwa na tumbo kubwa. Sikusita kumuuliza na kunieleza ana watoto wanne, mumewe alimkimbia na kuamua kufanya biashara ile ambayo ilimsaidia kupunguza ukali wa maisha.
Wazo lile nililiafiki na kumuomba msaada wa mimi kupata zile mboga. Alinielekeza jinsi ya kuzipata nami nikaingia kwenye biashara hiyo.
Mwanzo niliona aibu, lakini aibu ilinitoka baada ya kumaliza mapema na kununua mahitaji muhimu ya siku ile japo hayakulingana na aliyokuwa akinipa baba yenu.
Siku za kujifungua nazo zilikaribia nikawa nachoka sana. Ilibidi nipumzike na biashara ile kutokana kuelemewa na tumbo.
Ugumu wa maisha ulianza kujirudia, lakini nilipata bahati kuna dada mmoja alihamia jirani ambaye kwa kweli tulikuwa tumezoeana. Nilipomueleza matatizo yangu hakutaka kuniacha alinisaidia mahitaji madogomadogo. Namshukuru Mungu nilijifungua salama mtoto mwenye afya njema.
Kwa vile tulikuwa na vitu ndani, alinishauri niuze baadhi ili nipate fedha ya kujikimu na maisha.
Nilifanya vile kwa kuuza kabati kubwa la nguo, tivii na deki kwa bei ya kutupa. Baada ya kufanikiwa zoezi lile alinishauri nihangaike kwa vile baba yenu aliikimbia familia yake, lazima kutakuwa na mkono wa mtu. Bila hivyo nitaiua familia yangu.
Siwezi kumlaumu kwa kunipa wazo la kumuhangaikia baba yenu. Baada ya kuyafanyia kazi mawazo yake ambayo baadaye yalikuwa majuto ya milele.
Alinipeleka kwa mtaalamu mmoja ambaye alinieleza kila kitu juu ya baba yenu kushikwa kishirikina na mwanamke wa nje.
Aliniahidi kunisaidia basi alinipatia tiba ya kusafisha mwili wangu na dawa nyingine.
Niliamini uchawi upo na dawa zipo kwani baada ya kutumia zile dawa kwa wiki moja baba yenu alirudi na kuonekana kama mtu ambaye hakuelewa alikuwa wapi.
Kwa vile nilikuwa nimepewa dawa ya kumtuliza, nilimwekea kwenye chakula na kwenye maji na kuchukua nguo alizorudi nazo na kuzipeleka kwa mtaalamu ambapo alizifanyia dawa.
Baada hapo baba yenu alitulia nyumbani na hali ya maisha ilirudi kama zamani kwa kurudisha vitu vyote nilivyoviuza. Pia alinionesha na nyumba aliyokuwa akiijenga ambayo baadaye aliiandika jina la Mwaija kama zawadi ya kuzaliwa kwake bila ya wewe kuwepo.
Niliendelea kutumia dawa nilizopewa. Kila nilipokwenda kwa mtaalamu alinieleza vita iliyokuwa nje ni kubwa kwa yule mwanamke aliyetaka kumchukua tena baba yenu.
Lakini mganga alinihakikishia hawezi kufanya kitu. Nilimshukuru shoga yangu kuweza kuiokoa familia.
Wakati nikiamini mambo yametulia kumbe yule mwanamke alikuwa halali kwa ajili ya baba yenu, alizunguka pande zote za dunia. Mwaija alipofikisha miaka miwili mambo yalibadilika.
Ya mwanzo ilikuwa cha mtoto, kwanza tulianza kukosana ndani, jambo si jambo linakuwa ugomvi mkubwa. Nilirudi haraka kwa mtaalamu na kunipatia dawa. Lakini ndiyo kwanza zikamfukuza ndani baba yenu.
Baba yenu alitoweka sikujua yule mwanamke kamficha wapi. Nilihangaika kutumia dawa za yule mtaalamu bila mafanikio. Taratibu maisha yakaanza kuwa magumu tena.
Niliapa kuuza hata nguo ya ndani ili kumshikisha adabu yule mwanamke. Nilikwenda kwa kila mganga niliyeelezwa, niliuza vito vyangu vyote ili kuhakikisha namrudisha baba yenu, lakini sikufanikiwa na kujikuta nimeuza nguo zangu zote za maana ili kuhakikisha naendelea kumuhangaikia baba yenu.
Hamuwezi kuamini wanangu kipindi cha kuhangaika kwangu sikujua malezi yenu. Nilikonda nilikuwa sijijali, kuoga na kubadili nguo hakikuwa kitu muhimu kwangu kwa wakati ule kwa ajili ya kumhangaikia baba yenu.
Mpaka nakufa yule mwanamke siwezi kumsahau.
Kuna mtu alinieleza kuna sehemu nikienda baba yenu atarudi na asingetoka tena. Kwa vile kulikuwa mbali, niliwachukua na kuwapeleka kijijini kwa mama na mimi kuondoka kwenda kuhangaika.
Nilikwenda mpaka Ufipa ambako nilikaa zaidi ya miezi mitatu na kubahatika kumpata mganga ambaye alinihakikishia baba yenu atarudi na hataondoka tena kwenda kwa yule mwanamke na kama angerudi basi ningekwenda kuchoma mikoba yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Pia alinihakikishia kama yule mwanamke atatia tena mkono basi atabakia jina.
Baada ya kupata tiba nilirudi nyumbani na dawa kibao, za kuoga, kunywa, kuchoma na kuchanganya kwenye chakula. Niliandikiwa dawa zote na matumizi yake.
Baada ya kupewa dawa nilirudi nyumbani nikiwa hoi. Nilikonda mama yenu na kusawajika kwa ajili ya kuhangaika kumrudisha mume wangu nyumbani.
Nilifika nyumbani majira ya saa moja usiku, siku ileile sikutaka kulala. Nilichukua dawa zangu, nilianza kwa kuoga dawa na nyingine kumwagia kila kona ya nyumba kuondoa uchawi. Kisha nilianza kufanya kama nilivyoelekezwa jinsi ya kumvuta baba yenu.
Kwa vile nilikuwa nimefika jioni sana, usiku ulipofika nilichoma dawa huku nikimwita baba yenu kwa jina arudi nyumbani. Nilifanya vile bila kupumzika kama nilivyoelezwa mpaka nitakaposikia hodi.
Narudia tena kusema uchawi upo na dawa zipo. Nikiwa katikati ya zoezi ambalo lilikuwa linachukua zaidi ya saa moja na nusu. Nilisikia mlango ukigongwa, niliacha kunuiza na kwenda kufungua mlango.
Sikujua nani anayegonga, nilipofungua mlango kidogo nianguke kwa mshtuko baada ya kumuona baba yenu mbele yangu.
Kauli ya mama ilifanya mwili wangu usisimke, nilimuangalia mama aliyekuwa akizungumza taratibu huku akifuta machozi, moyo uliendelea kunifukuta.
Nilimuona baba yenu kama msukule aliyerudishwa baada ya kuchukuliwa kichawi. Alikuwa kama mtu asiyejifahamu. Kama mmeshawahi kuona mtu akirudishwa baada ya kuchukuliwa kichawi ndivyo baba yenu alivyokuwa.
Ile hali nilielezwa na mganga itajitokeza lakini alinieleza nimshtue kwa kumpiga na maji ya dawa usoni kisha nimuoshe kwa dawa aliyonipa na nyingine nimpe anywe, siku ya pili angeamka akiwa mzima kabisa.
Baada ya baba yenu kuingia ndani moyo uliniuma sana kutokana na hali aliyokuwa nayo. Kumbe alikuwa yupo na yule mwanamke na aligeuzwa msukule kwa kufanyishwa mambo bila kujua.
Nilifanya kama nilivyoelekezwa, nikampiga usoni na maji ya dawa ili kumzindua kwenye kifungo cha kichawi. Baada ya kuchanganya dawa kwenye maji nilimpiga nayo usoni na kumfanya ashtuke kama anatoka usingizini.
Cha kwanza kilikuwa kuwauliza wanawe, nilimueleza mmekwenda kumtembelea bibi yenu kijijini. Alijinyoosha kama mtu aliyekuwa amechoka sana na kupiga miayo.
Nilimpelekea maji bafuni yaliyochanganywa na dawa. Baada ya kuoga nilimpa dawa ya kunywa na kumuacha alale.
Mmh! Yaani baba yenu alipolala ha..ha..ku..amka tena.
Mama alianza kulia kwa kwikwi, kitu kilichofanya wote tulie kilio cha kimya kwa kutokwa machozi huku nikizidi kumuonea huruma mama yetu.
Ilibidi mama Amina aanze kazi ya kumbembeleza mama aliyekuwa akilia kilio cha kwikwi. Nilipowaangalia dada zangu kila mmoja alikuwa akilia.
Kwa kweli ilikuwa simulizi yenye kuumiza na kuupasua moyo bila ganzi. Baada ya mama kunyamaza aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio na kuzidi kuniumiza.
Kwa kweli sikuelewa sababu ya kifo cha baba yenu, nilijiuliza labda dawa niliyompa kunywa ndiyo iliyochangia kifo cha baba yenu na kama ni ile nilikosea sehemu nini? Niliumia mara mbili baada ya kuhaingaika kote kumbe natafuta kumuua mume wangu.
Kufikia hapo tena mama akaanza kulia tena.
Nilishindwa kujizuia nilijikuta nikisema kwa sauti bila kujielewa:
Mama hujamuua baba, ulifanya kwa ajili yetu lakini bahati mbaya ikatokea iliyotokea.
Hapana wanangu bila mimi msingekuwa yatima.
"Hamuwezi kuamini wanangu kipindi cha kuhangaika kwangu sikujua malezi yenu. Nilikonda nilikuwa sijijali, kuoga na kubadili nguo hakikuwa kitu muhimu kwangu kwa wakati ule kwa ajili ya kumhangaikia baba yenu.
"Mpaka nakufa yule mwanamke siwezi kumsahau.
Kuna mtu alinieleza kuna sehemu nikienda baba yenu atarudi na asingetoka tena. Kwa vile kulikuwa mbali, niliwachukua na kuwapeleka kijijini kwa mama na mimi kuondoka kwenda kuhangaika.
"Nilikwenda mpaka Ufipa ambako nilikaa zaidi ya miezi mitatu na kubahatika kumpata mganga ambaye alinihakikishia baba yenu atarudi na hataondoka tena kwenda kwa yule mwanamke na kama angerudi basi ningekwenda kuchoma mikoba yake.
"Pia alinihakikishia kama yule mwanamke atatia tena mkono basi atabakia jina.
"Baada ya kupata tiba nilirudi nyumbani na dawa kibao, za kuoga, kunywa, kuchoma na kuchanganya kwenye chakula. Niliandikiwa dawa zote na matumizi yake.
"Baada ya kupewa dawa nilirudi nyumbani nikiwa hoi. Nilikonda mama yenu na kusawajika kwa ajili ya kuhangaika kumrudisha mume wangu nyumbani.
"Nilifika nyumbani majira ya saa moja usiku, siku ileile sikutaka kulala. Nilichukua dawa zangu, nilianza kwa kuoga dawa na nyingine kumwagia kila kona ya nyumba kuondoa uchawi. Kisha nilianza kufanya kama nilivyoelekezwa jinsi ya kumvuta baba yenu.
"Kwa vile nilikuwa nimefika jioni sana, usiku ulipofika nilichoma dawa huku nikimwita baba yenu kwa jina arudi nyumbani. Nilifanya vile bila kupumzika kama nilivyoelezwa mpaka nitakaposikia hodi.
"Narudia tena kusema uchawi upo na dawa zipo. Nikiwa katikati ya zoezi ambalo lilikuwa linachukua zaidi ya saa moja na nusu. Nilisikia mlango ukigongwa, niliacha kunuiza na kwenda kufungua mlango.
" Sikujua nani anayegonga, nilipofungua mlango kidogo nianguke kwa mshtuko baada ya kumuona baba yenu mbele yangu."
Kauli ya mama ilifanya mwili wangu usisimke, nilimuangalia mama aliyekuwa akizungumza taratibu huku akifuta machozi, moyo uliendelea kunifukuta.
"Nilimuona baba yenu kama msukule aliyerudishwa baada ya kuchukuliwa kichawi. Alikuwa kama mtu asiyejifahamu. Kama mmeshawahi kuona mtu akirudishwa baada ya kuchukuliwa kichawi ndivyo baba yenu alivyokuwa.
"Ile hali nilielezwa na mganga itajitokeza lakini alinieleza nimshtue kwa kumpiga na maji ya dawa usoni kisha nimuoshe kwa dawa aliyonipa na nyingine nimpe anywe, siku ya pili angeamka akiwa mzima kabisa.
"Baada ya baba yenu kuingia ndani moyo uliniuma sana kutokana na hali aliyokuwa nayo. Kumbe alikuwa yupo na yule mwanamke na aligeuzwa msukule kwa kufanyishwa mambo bila kujua.
"Nilifanya kama nilivyoelekezwa, nikampiga usoni na maji ya dawa ili kumzindua kwenye kifungo cha kichawi. Baada ya kuchanganya dawa kwenye maji nilimpiga nayo usoni na kumfanya ashtuke kama anatoka usingizini.
"Cha kwanza kilikuwa kuwauliza wanawe, nilimueleza mmekwenda kumtembelea bibi yenu kijijini. Alijinyoosha kama mtu aliyekuwa amechoka sana na kupiga miayo.
Nilimpelekea maji bafuni yaliyochanganywa na dawa. Baada ya kuoga nilimpa dawa ya kunywa na kumuacha alale.
" Mmh! Yaani baba yenu alipolala ha..ha..ku..amka tena."
Mama alianza kulia kwa kwikwi, kitu kilichofanya wote tulie kilio cha kimya kwa kutokwa machozi huku nikizidi kumuonea huruma mama yetu.
Ilibidi mama Amina aanze kazi ya kumbembeleza mama aliyekuwa akilia kilio cha kwikwi. Nilipowaangalia dada zangu kila mmoja alikuwa akilia.
Kwa kweli ilikuwa simulizi yenye kuumiza na kuupasua moyo bila ganzi. Baada ya mama kunyamaza aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kilio na kuzidi kuniumiza.
"Kwa kweli sikuelewa sababu ya kifo cha baba yenu, nilijiuliza labda dawa niliyompa kunywa ndiyo iliyochangia kifo cha baba yenu na kama ni ile nilikosea sehemu nini? Niliumia mara mbili baada ya kuhaingaika kote kumbe natafuta kumuua mume wangu."
Kufikia hapo tena mama akaanza kulia tena.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilishindwa kujizuia nilijikuta nikisema kwa sauti bila kujielewa:
"Mama hujamuua baba, ulifanya kwa ajili yetu lakini bahati mbaya ikatokea iliyotokea."
"Hapana wanangu bila mimi msingekuwa yatima."
"Si kweli, wangapi mayatima si kwa tukio kama lako?" nilihoji.
"Lakini bila mimi baba yenu asingekufa."
"Angekufa kwa kitu kingine, mama toka ulipoanza kuzungumza sijaona sehemu uliyochangia kifo cha baba. Mama tunakuomba uondoe wazo hilo," dada mkubwa alisema.
"Basi wanangu baada ya msiba tulifanya kila kitu na kumlaza baba yenu katika nyumba yake ya milele. Nilikonda kwa mawazo, lakini ninyi ndiyo mlionifanya nisimame imara ili kuhakikisha nawasomesha na hamtetereki kimaisha.
"Sijui niseme nini, lakini baada ya kifo cha baba yenu vitu vingi vilijulikana. Alikuwa na gari na nyumba pia malipo yote ya kazini kwake nilipata.
Baada ya kupata vitu vyote hivyo nilimalizia nyumba ya Mwaija na kuipangisha. Naweza kusema nilifanya kosa kukueleza Mwaija baba yako alikuachia nyumba kubwa.
"Hilo naomba nikiri nilifanya kosa, nimekula fedha yako bila kukushirikisha kwa miaka yote hiyo. Lakini leo nitakukabidhi kila kitu.
"Kupitia mali alizoacha baba yenu niliweza kuwasomesha wote ila sikutaka msome sana kwa vile mngeondoka na kuniacha peke yangu. Hapo ndipo nilipoanza kufanya makosa makubwa.
"Baada ya Zamda na Rehema kuolewa niliona nyumba inapwaya na kujikuta nikipata wazo la kuwarudisha nyumbani, hapo ndipo nilipokwenda kwa mtaalamu na kuzisambaratisha ndoa zenu na ninyi kurudi nyumbani bila kujua mimi ndiye mbaya wenu. Niliweza kuwafanya kuzichukia ndoa kitu kilichokuwa furaha yangu.
"Nilifanya hivyo kwa Mwaija ambaye nilikuwa nampenda sana, wewe ndiyo sikutaka kabisa uondoke nyumbani. Yote yaliyokutokea niliyafanya mimi mama yako.
"Wanangu nachukua nafasi hii kuwaombeni radhi kwa yote niliyowafanyia pia namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe kwa kila baya nililowafanyia. Sijui bila mama Amina, wanangu wangeendelea kuishi maisha gani.
"Mwanangu najua nimewaumiza bila ya ninyi kujua, naomba mnisamehe nipo chini ya miguu yenu."
Mama alisema huku akinyanyuka kitini ili apige magoti. Tulinyanyuka wote na kumuwahi kabla hajapiga magoti na kumwambia tumemsamehe.
Baada ya zoezi lile, mama Amina alizungumza:
"Nina imani mmemsikia vizuri mama yenu, siku zote mtu akigundua kosa lake na kutubu hata Mungu umsamehe. Mama yenu kagundua makosa yake na leo kayasema yote bila kuacha kitu.
"Kwa vile mmemsamehe nawaomba muishi kama zamani, mpendeni mama yenu. Alifanya vile kwa mapenzi mazito kwa wanaye lakini akawa anaharibu.
"Namshukuru Mungu kwa upande wangu nimemaliza kazi yangu nina imani kila mmoja ameona mabadiliko," mama Amina alituambia.
"Ni kweli," tulijibu kwa pamoja.
"Mimi nafikiri sina cha zaidi, nashukuru tumemaliza salama acha nikimbie," mama Amina alitaka kutuaga.
"Mama Amina tunashukuru kwa kila ulilotufanyia, nina imani si kwa uwezo wetu bali ni Mungu ndiye aliyetuongoza kukujua wewe na kututoa kwenye kiza kizito.
"Kwa upande wa mama bado tunampenda sana tena sana. Alichotueleza hakitapunguza upendo wetu kwake. Tunampenda mama leo, kesho kwa vile kilichofanyika ni funzo si kwake hata sisi tutazaa na kutorudia makosa.
"Mama ondoa unyonge lililopita limepita, tumshukuru Mungu kwa kulifungua mapema kabla hujafa. Inawezekana tukio hili lilikuwa likitukumbusha kumrudia Mungu wetu.
"Namalizia kumshukuru tena mama Amina wewe si mganga tu bali ni sehemu ya familia yetu. Sisi hatuna cha kukulipa bali Mungu ndiye mwenye uwezo huo.
Wadogo zangu hatuna budi kumtunza mama yetu kwa vile amebakia kama jicho letu. Tusimuwekee kinyogo bali tumpende na kumtunza," dada mkubwa alisema kwa hisia kali mpaka machozi yakamtoka.
"Mama nakupenda nitaendelea kukupenda," dada Rehema alisema maneno mafupi.
"Mama nataka kukuambia mapenzi yangu kwako ni makubwa sana, nataka kukueleza chanzo cha matatizo yangu niliyajua muda mrefu toka nikiwa na Beka.
"Lakini bado sikuwa tayari kukuchukia mama yangu, niliamini unatupenda japokuwa sikupenda maisha tuliyokuwa tukiishi, nilijitahidi niwe tofauti na dada zangu.
"Nilikuwa na bahati iliyoishia na matatizo, hata baada ya kugundua sababu ya matatizo yangu bado moyo haukukubali mama unaweza kuwa adui yetu.
"Nimehangaika kuupata ukweli bila mafanikio, na nilipoupata bado niliendelea kukupenda mama yangu, nilitamani kukueleza lakini niliogopa.
"Inawezekana wote hamkujua kikao hiki kimeitishwaje, nataka kuwaeleza, mimi ndiye niliyemfuata mama Amina na kumuomba aitishe kikao hiki ili kuufungua moyo wa mama uliokuwa na mzigo mzito ila sijui kwa dada zangu kwa vile niliyajua haya mapema.
"Mama inawezekana ukaona nimekuvunjia heshima kwa kukulazimisha kuyasema mambo mazito kwetu. Mama naomba unisamehe nilifanya hivyo kwa ajili ya kukuweka huru.
"Nilijua unaumia na kuendelea kuteketea kama mshumaa, huwezi kujua hali uliyokuwa nayo ilitutesa sana wanao kiasi gani. Lakini leo nataka kukuambia toka moyoni kuwa tumezaliwa upya," nami nilimalizia.
"Asanteni wanangu, narudia kusema namshukuru Mungu kunipa watoto wenye mapenzi ya dhati na mama yenu. Nimejifunza kitu nina imani kila kitu ni uweza wa Mungu.
"Mama Amina nashukuru sana mdogo wangu, Mungu atakulipia, narudia wanangu mnisamehe sana."
"Tumekusamehe mama," tulisema kwa pamoja.
***
Kikao kiliisha salama kwa watoto wote kuiswafi mioyo yetu kwa mama. Kwa upande wangu niliutua mzigo mzito ulionielemea moyoni mwangu na kuwa huru huku nikiendelea kumshukuru Mungu.
Furaha ilirudi katika nyumba yetu, dada yangu aliolewa harusi kubwa na mwingine anaendelea na kazi huku akiwa na bwana ambaye alimuahidi kumuoa.
Namalizia kwa kumshukuru mama Amina kwa msaada wake wa hali na mali kuhakikisha anapigania afya yangu mpaka leo hii ninayotoa ushuhuda huu nina afya njema na watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume.
Dada zangu wote wana mtoto mmoja mmoja.
Pia namshukuru sana mwandishi wa mkasa huu kwa kukubali kupoteza muda wake kuandika mkasa mzito kama huu. Mungu atamlipia kwa kazi yake ya kujituma bila kuchoka.
Mwisho kabisa nawashukuru wasomaji wote kwa kupoteza muda wao kufuatilia simulizi yangu mpaka leo ambapo nahitimisha mkasa huu, Mungu atawalipa pia nina imani kuna kitu mmejifunza hasa wazazi nina imani mmeona madhara ya ushirikina.
Wapeni uhuru watoto wenu waishi maisha yao hata kama mnawapenda sana. Naomba kwa leo niishie hapa Mungu awabariki, ahsanteni.
Kwa kunifuatilia hadithi yangu na kuacha shughuli zenu nawapendeni nyote .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO!
0 comments:
Post a Comment