Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

MAPENZI YAMENIFANYA NIWE MUUAJI - 3

 









    Simulizi : Mapenzi Yamenifanya Niwe Muuaji

    Sehemu Ya Tatu (3)





    CHANZO CHA MAUWAJI KINANZIA HAPA

    SIKU ya pili tulipanda basi lililotoka Dar na kufika Lushoto kwenye Kijiji cha Mlalo saa kumi jioni.

    Hatukukaa, tulichukua usafiri mwingine wa baiskeli na kuelekea katika vijiji vya ndani zaidi mpaka katika Kijiji cha Tewe ambacho kinasifika kwa kuwa na waganga wenye uwezo wa juu.



    Tulifika katika kijiji hicho saa kumi na moja kasoro jioni na kwenda kwa mtaalam anayeitwa mzee Kidereko.

    Alikuwa akiishi katika nyumba moja kubwa ya matofali, nyumba hiyo ilikuwa ni tofauti na nyingine kwa kuwa ilikuwa imeezekwa kwa bati.

    Pia, ilikuwa imezungukwa na uwa wa miti ya minyaa, ndani kulikuwa na nyumba zingine ndogo nne za miti na udongo zikiwa zimeezekwa kwa makuti. Tulikaribishwa na wenyeji wetu ambao walimfahamu sana Shedu ambaye alionekana kuwa ni mwenyeji sana pale.

    “Oooh, Shedu karibu,” dada mmoja aliyekuwa amejifunga kitenge kilichopauka alimchangamkia.

    “Asante Mwana, za hapa?”

    “Nzuri ka Shedu, karibu mgeni,” nilikaribishwa na miye huku nikipokewa mzigo wangu.

    “Asante.”

    Tulipelekwa hadi chini ya mti wa mwembe ambako chini yake kulikuwa na jamvi lililokuwa limechakaa na pembeni yake kulikuwa na vigoda.

    “Jamani karibuni.”

    “Asante, za hapa?” Shedu aliuliza.

    “Mmh! Kama unavyoziona maisha magumu.”

    “Mwana magumu wakati unatakata?”

    “Inatubidi tuyazoee maisha ya huku kwa lazima, kwa vile hatuna jinsi, nina imani nimekuona kidogo nitacheka.”

    “Ondoa hofu, mzee yuko wapi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amekwenda porini kuna kazi ya mtu amekwenda kuifanya, nina imani muda wowote atarejea.”

    “Ameondoka saa ngapi?”

    “Tangu saa tisa usiku.”

    “Mmh! Inaonekana ni nzito.”

    “Kwa kweli ni nzito, kuna mtu mmoja alilazwa chini na wabaya wake, akaletwa hajitambui na kutibiwa na mzee baada ya kupona aliruhusiwa.

    “Miezi minne baadaye alipigwa kombora lingine lililomkata kauli mpaka watu wakajua amekufa.

    “Taarifa zilipomfikia mzee alikwenda mjini na kumnyanyua kisha alimtaka aje huku amtengeneze vizuri. Alifika jana jioni na kulala hapa, usiku ndipo walipoamka na kuelekea porini ambako atamfanyia kinga itakayomlinda ili mtu akimgusa aondoke yeye.”

    Nilijikuta nikivutiwa na mazungumzo ya Shedu na yule msichana anayeitwa mwana.

    “Namuamini mzee hapo lazima mtu alale chini.”

    “Tena amekasirika sana kwa kitendo cha kupimwa nguvu.”

    “Mzee Kidereko tena.”

    “Mmh, na ninyi?”

    “Ndugu yangu ana shida ndogo.”

    “Shedu, shida ndogo ndiyo mpande basi kuja huku, si nasikia mjini kuna wataalam ambao wanaweza kutatua shida ndogo, wakishindwa ndipo mnakuja huku?”

    “Mwana kazi zangu zote huwa anazifanya mzee Kidereko, kwa hiyo hata rafiki yangu alipopatwa na tatizo sikutaka asumbuke kwa waganga uchwala, nikaona nimlete kwa mzee.”

    “Mmh! Sawa, tena huyo anaingia.”

    Kauli ya yule msichana ilitufanya wote tugeuke kuangalia kwenye mlango wa uzio na kumuona mzee mmoja aliyekuwa akijivuta kwa mkongojo wake, akiwa na vijana wawili waliokuwa wamebeba kapu na majani mabichi.

    Shedu alinyanyuka na kwenda kumpokea mzee Kidereko.

    “Babuuu.”

    “Babuuuu.”

    Walikumbatiana na kuja nilipokuwa nimekaa, nami nilinyanyuka kumpokea mzee Kidereko.

    “Shikamoo babu.”

    “Marhahaba karibu.”

    “Asante babu.”

    Vijana walipokelewa vikapu walivyotokanavyo porini na kupumzika kwenye mkeka. Wote walipumzika kwa kujilaza kuonesha kuwa walichoka. Kutokana na kuchoka sana vijana wale baada ya kujilaza usingizi mzito uliwachukua na kuanza kukoroma.

    Mzee Kidereko alinyanyuka na kuelekea ndani mwake na kutuacha tukiwa tumekaa kwenye vigoda. Muda nao ulikuwa unadizi kuyoyoma, kigiza kilianza kuimeza nuru ya jioni hiyo.

    “Mzee huyu kiboko,” Shedu alinieleza kwa sauti ya chini.

    “Kweli anatisha kwa maelezo mafupi imeonesha anaijua sana fani ya mizizioloji.”

    Saa moja kasorobo kililetwa chakula, kilikuwa ni wali na bata, baada ya chakula ndipo mzee Kidereko alipotuita pembeni kwa mazungumzo.

    “Jamani karibuni, sikuweza kuzungumza na ninyi nilipofika kwa kuwa tulikuwa hoi sana kama mlivyowaona wenzangu.”

    “Ni kweli babu,” Shedu alijibu.

    “Mmh! Shedu za siku?”

    “Nzuri babu.”

    “Mambo yako yanakwendaje?”

    “Yanakwenda vizuri.”

    “Kazini?”

    ”Panakwenda vizuri yale mambo yalienda kama ulivyoniahidi.”

    “Kwa hiyo asante yangu umeniletea?”

    “Ndiyo, tena nimeshukuru baada ya jamaa yangu kukubali kuja huku ili nami nipate nafasi ya kukuletea asante yako.”

    “Na mkeo katulia?”

    “Kila mtu anashangaa hata ndugu walioanza kuiandama ndoa yangu wametulia.”

    Kauli ile ilinishtua na kujiuliza, ndoa ya Shedu ilikuwa na tatizo gani lililotatuliwa na yule babu? Lakini nilitulia kimya na kupanga kumuuliza tukiwa wawili japokuwa nilianza kuhisi huenda kilichompata ndicho kilichonifikisha pale.

    “Mmh, mwenzio ana tatizo gani?” mzee Kidereko aliuliza.

    “Kama langu, lakini la kwake limezidi, mkewe kamkimbia kabisa na inasemekana ameolewa na mtu aliyemchukua.”

    “Mmh! Mjini mbona tabia za kuchukuliana wanawake zimeshamiri, wanadamu bwana, wanawake wengi lakini wanapenda wake za watu. Tatizo si kubwa kama mngekuja mapema, mngeweza kugeuka leo hii. Nitalifanya sasa hivi ili kesho alfajiri muwahi kurudi kwenu.”

    “Nitashukuru mzee wangu, kweli mke wangu atarudi?” nilijikuta nikiuliza.

    “Hiyo kazi niachie mimi, maadamu umelileta kwangu.”

    “Nitashukuru mzee wangu.”

    “Unataka aliyemchukua mkeo tumfanyeje?”

    “Vyoyote ukakavyoona inafaa mzee wangu.”

    “Tumuue?”

    “Hapana.”

    ”Tumtie uchizi?”

    “Mmh! Hakuna adhabu nyingine?”

    “Zipo nyingi utakayotaka wewe.”

    “Yoyote ya kawaida la muhimu nimpate mke wangu.”

    “Kazala lazima tumtie adabu, mzee mfanyie kama yangu.”

    Nilishtuka na kujiuliza kama yake ipo vipi? Ilibidi niulize.

    Ni adhabu gani anayotaka kufanyiwa mwanaume aliyemchukua mke wa Kazala?



    “Ulimpa adhabu gani?”

    “Nilimpoteza kwenye sura ya dunia,” Shedu alijibu kwa kujiamini.

    “Ha! Unamaanisha ulimuua?”

    “Ndiyo! Kanitesa sana yule mshenzi kasababisha mwanangu wa kwanza afe baada ya mke wangu kumuacha na kwenda kwa huyo mwanaume na kusababisha mwanangu afe kwenye beseni la maji.”

    “Mungu wangu!” nilishtuka na kushika mdomo.

    “Kibaya mtu yule hakuishia hapo, alimchanganya mke wangu kiasi cha kudai talaka. Nilimfuata na kumueleza aachane na mke wangu majibu aliyonijibu yalikuwa ya udhalilishaji. Eti aliniambia kama namuona mke wangu anafaidi yeye kuwa naye na mimi niwe mpenzi wake.”

    “Uwe mpenzi wake alimaanisha nini?”

    “Eti niwe mkewe.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mungu wangu!” kauli ile ilinishtua sana.

    “Kazala wee acha tu, mtu akiwa na fedha ana dharau ndiyo maana jambo lako nililichukua kama langu. Kazala nimeteseka mpaka nilipoletwa huku kwa mzee Kidereko.”

    “Ina maana ulikuwa humjui tokea awali?”

    “Matatizo ndiyo yaliyonifanya nifike huku, we si unajua kabila langu?”

    “Nilishangaa pale uliponileta huku na kabila lako, nikajua baba ndiye Mnyamwezi ma mama mtu wa Tanga.”

    “Walaa.”

    “Yalikuwa mateso ya muda gani?”

    “Miezi nane lakini kwangu ilikuwa miaka mia nane.”

    “Pole sana.... ikawaje?” nilijikuta nikiwa na shauku baada ya kuona matukio yetu yanafanana sana.

    “Baada ya kuletwa huku sikutaka adhabu kali, lakini babu aliniambia mtu huyo nikimchelewesha ataniwahi mimi.

    “Kutokana na mateso niliyoyapata na uchungu wa kifo cha mwanangu nilikubali.”

    “Mmh! Ikawaje?”

    “Basi mzee akatengeneza mambo, sikuwepo ila waliokuwepo na kutoa ushuhuda walisema baada ya kwenda nyumba ya wageni na mke wangu ambaye yeye alijimilikisha na kuwa mkewe. Kutokana na maneno aliyoyasema mke wangu, aliyekuwepo kwenye tukio wakiwa faragha.

    “Baada ya kumaliza mchezo wao uume haukupoa uliendelea kuwa vile vile, kama chuma na kuuma maumivu makali sana.

    “Alipiga kelele za maumivu, ilibidi achukuliwe na kupelekwa hospitali, huko alipigwa sindano za ganzi ili uume upoe lakini wapi, kila dakika maumivu yalikuwa makali alilia mpaka sauti ikakauka. Nasikia alinitaja mimi ili niende akaniombe msamaha.

    “Nguvu zilimwisha mateso yale yaliendelea kwa saa nane, jioni uume ulinywea na yeye kufariki dunia.”

    “Mmh! Aliteseka sana.”

    “Yeye kwa saa nane mimi miezi minane, kuchanganyikiwa kubaya nakumbuka kuna kipindi nilikuwa natembea nikizungumza peke yangu. Kingine hali yangu ya kimaisha ilikuwa mbaya hapo ndipo nilipozidi kuumia.”

    “Baada ya hapo nini kiliendelea?” nilijikuta nikivutwa na simulizi ya Shedu.

    “Mke wangu alirudi huku mtaani kila mmoja akiniheshimu mpaka leo hakuna mtu wa kumgusa mke wangu. Hata akija mgeni lazima atapewa taarifa za yule jamaa aliyejitia kidume na kulamba udongo. Basi akipata taarifa ile humkalia mbali mke wangu.”

    “Lakini mbona kama adhabu ni kubwa sana?”

    “Kazala acha huruma wanadamu si wa kuwachekea ona anavyoteseka kwa haki yako.”

    “Sawa lakini kuua!” bado niliona adhabu ya kuua ni kubwa.

    “Kijana acha ujinga, siku zote akuanzae mmalize,” mzee Kidereko alisema.

    “Sawa mzee wangu, mi shida yangu kumrudisha mke wangu tu si kuua.”

    “Sawa, ila lolote litakalotokea usirudi hapa.”

    “Kwa nini babu?”

    “Inaonekana hujihurumii, kwa hiyo naomba ukiondoka hapa usirudi labda uje na lingine. Mimi hupenda kufanya kazi mara moja ili usirudi hapa kwa kazi hiyohiyo. Kwa akili ya mkeo hata kama atarudi bado ataendelea kukusumbua. Nakueleza utarudi hapa nguo zipo kichwani.”

    “Kwa nini unasema hivyo?”

    “We si mtoto mdogo mambo mangapi kakufanyia mkeo nusra ujiue, kweli au uongo?”

    “Kweli.”

    “Sasa kwa nini mtu aliyetaka kukusababishia ujiue unamuonea huruma. Nataka kukueleza huruma ikizidi hugeuka uchawi wa kukuzuru mwenyewe hasa kwa adui yako.”

    Nilitulia kwa muda nikiwaza na kuwazua juu ya adhabu wanayotaka kuifanya kwa mwanaume aliyemchukua mke wangu. Kauli za kurudi nguo nimeweka kichwani zilinitisha sana na kujua kurudi pale nitakuwa mwendawazimu.





    NILIKUWA nimezama kwenye dimbwi la mawazo, mzee Kidereko akanishtua:

    “Sasa amua tufanye kazi kamili au nusunusu?”

    “Mzee Kidereko fanya kazi kamili,” Shedu alisema.

    “Shedu usimsemee mwenzako, mwache aseme mwenyewe.”

    “Mzee Kidereko usimsikilize huyu jamaa, siye ndiyo tunaojua anavyoteseka, tena kurudi na nguo kichwani umemhurumia anatakiwa abakie jina, juzi tu amechungulia kaburi.”

    “Hata kama yote hayo yamemtokea bado ana hiyari ya kuepukana na tatizo hilo au kuendelea kuteseka.”

    “Mzee tumetoka mbali na shida yetu ni kulimaliza tatizo hilo, hasa tukizingatia sasa hivi mwanamke ndiyo kaolewa kabisa,” Shedu alizidi kushadadia.

    “Bado mwenyewe uamuzi wa mwisho ni yeye mwenyewe.”

    Ubishani ule ulinifanya nikumbuke mateso mazito aliyonipa mke wangu na dharau ya yule mwanaume, kwanza kwa kumfanya mwanangu achelewe kutembea, pili kulala na mke wangu katika kitanda changu.

    Ile ilikuwa ni dharau kubwa sana na mbaya zaidi kumchukua jumla na kumuoa, japokuwa sikuwa na uhakika na jambo hilo lakini kwa mujibu wa kauli ya mke wangu alivyoniandikia barua yake siku alipoondoka ilionesha wazi kuwa jamaa huyo ndiye aliyemchukua jumla.

    Moyo uliniuma mpaka machozi yakanitoka na mishipa ya kichwa kunisimama kwa hasira.

    Nilinyanyua uso wangu na kuwaangalia Shedu na mzee Kidereko, wote walikuwa kimya wakisubiri jibu langu.

    Moyoni sauti iliingia ikiniambia mtu yule hakustaili huruma hata kidogo.

    “Babu maliza kazi,” nilijikuta nikitamka kwa sauti.

    “Kwa moyo wako au kwa kulazimishwa?”

    “Kwa moyo wangu.”

    “Kweli?”

    “Kweli kabisa.”

    “Kazala huo ndiyo uanaume,” Shedu aliniunga mkono kwa uamuzi wangu.

    “Basi ngoja tuifanye hii kazi ili kesho muweze kuondoka.”

    “Sawa.”

    Tulikwenda kwenye kibanda kimoja ambacho mzee Kidereko alikuwa akifanyia kazi zake. Kilikuwa na vitendea kazi vyake, baada ya kukaa kwenye mkeka aliagiza beseni dogo la maji ambalo lililetwa baada ya muda.

    Beseni lile likajazwa maji kisha mzee Kidereko akaniuliza:

    “Huyo bwana unamjua jina?”

    “Simjui.”

    “Nipe jina la mkeo.”

    “Anaitwa Suzana.”

    “Jina la mama yake?”

    “Maria.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kumpa majina yale alichukua dawa ya unga akaanza kuinyunyuzia kwenye maji huku akilitaja jina la mke wangu kwa sauti ya chini.

    Baada ya muda aliniita na kuniuliza:

    “Huyu si mkeo?”

    “Ha! Ndiye,” nilishtuka kumuona mke wangu ndani ya beseni lile nikawa kama natazama video.

    “Ni kweli ni yeye?” mganga aliniuliza tena.

    “Ndiyo mzee wangu.”

    “Na huyo aliyekaa pembeni yake unamjua?”

    Nilituliza macho yangu kumuangalia yule mwanaume aliyekuwa amekaa na mke wangu akiwa kifua wazi na kugundua kuwa ndiye yule mwanaume niliyemuona kitandani na mke wangu.

    “Huyu ndiye aliyemchukua mke wangu,” nilisema kwa sauti huku macho yakiwa yamenitoka pima.

    “Kweli ni yeye?” aliniuliza tena mzee Kidereko.

    “Ndiye.”

    “Sasa tunamtoa mkeo na kumbakisha huyo mwanaume kisha nitakuelekeza kitu cha kufanya.”

    “Hakuna tatizo.”

    Baada ya kusema vile alichukua dawa ya unga na kuinyunyuzia kwenye maji huku akizungumza kwa sauti ya chini sana maneno ambayo sikuyaelewa kwa ufasaha. Mara nilimuona mke wangu akinyanyuka na kuondoka na kubaki yule mwanaume peke yake akiwa amekaa kwenye kochi.

    “Sasa nuiza kifo chochote unachokitaka kimpate huyu bwana.”

    “Cha ajali.”

    “Nuiza.”

    Mganga alinipa unga ule niuweke kwenye maji kwa kunyunyizia huku nikinuiza kile ninachokitaka, nilifanya vile huku nikinuiza kutaka yule mwanaume afe kifo cha ajali kwa kuamini kuwa kifo kile hakiwezi kuwafanya watu wanifikirie vibaya kwamba labda nahusika.

    Baada ya kunuiza kimoyomoyo nilimwambia nimemaliza, baada ya kusema vile alichukua kisu kikubwa cha kuchinjia mbuzi na kukiweka kwenye maji na kusema:

    “Majibu ya kazi yetu tutayaangalia asubuhi wakati mnaondoka, kama haikukubali itabidi mbaki tufanye tena upya lakini kazi zangu ninazozifanya katika mia basi mbili tu ziligoma lakini niliporudia ilikubali.”

    Baada ya zoezi lile mganga alichukua beseni la maji na kutoka nalo nje, baada ya muda alituita nje, nasi tukamfuata.

    Tulipotoka katika kilinge cha mganga tulikwenda sehemu tuliyopangiwa kulala ili asubuhi tuondoke kurudi Dar. Tulilala kwenye mkeka, tukiwa tumejilaza nilianza kumdodosa Shedu.

    “Kazi iliyofanyika ni hiyo tu au kuna nyingine?”

    “Kwa nini?”

    “Naona tumefanya ya kumuua yule jamaa, vipi kuhusu mke wangu kurudi?”

    “Jamaa akifa tu, mkeo anarudi nyumbani.”

    “Itawezekana kweli?”

    “Kama ingekuwa haiwezekani angekwambia, yule mzee amekwishaona kila kitu.”

    “Mmh! Sawa.”

    “Usiwe na wasiwasi tukurudi mkeo naye atakuwa ameshakubali kurudi kwako na utamletea mzee zawadi.”

    “Haya.”

    Tulilala mpaka alfajiri tulipoamshwa na mzee Kidereko, akatueleza kuwa ngoma imekuwa nzito.

    “Vijana ngoma imebuma.”

    “Kivipi?”

    “Muziki mnene,” alisema huku akituonesha beseni lililokuwa na maji na kisu likiwa kama tulivyoliacha jana.

    “Mbona hatuelewi?”

    “Jamaa kajitengeneza sana.”

    “Umejuaje?”

    “Kama ingekubali tungekuta maji haya yamegeuka damu.”

    “Unafikiri ni kwa nini?

    “Jamaa anaonekana yupo sawa.”

    “Kwa hiyo?”

    “Kuna kazi ya ziada inatakiwa kufanyika, tuliyoifanya ilikuwa ya kawaida sana.”

    “Sasa itakuwaje?”

    “Safari imekufa, tutarudia tena leo jioni.”

    Kauli ile ilinitisha na kuiona kama vita yangu na mwanaume aliyemchukua mke wangu ni kubwa sana tofauti na matumaini niliyopewa.



    Hatukuwa na jinsi tulikubali kushinda pale kijijini mpaka jioni tulipongia kwenye kazi nyingine. Safari ile alichemsha maji kwenye chungu,yalipokuwa yakichemka aliweka dawa na kunieleza nishike kisu na kukiingiza ndani ya yale maji yaliyokuwa yakichemka.

    Japokuwa ndani ya chungu hakukuwa na kitu kingine lakini kila nilipoingiza kisu kiligoma.

    “Vipi mbona huingizi kisu?” mzee Kidereko aliniuliza.

    “Kimegoma kunaonesha kuna kitu ndani ya chungu,” nilimweleza mganga baada ya kisu kugoma kuingia.

    “Hebu toa kisu,” aliniamuru.

    Nilikitoa kisu, mganga alichukua dawa ya unga na kuiweka kwenye yale maji yaliyokuwa yakichemka kisha aliweka maji yaliyokuwa kwenye chupa ndogo na kunieleza nikiingize tena kisu.

    Kisu kiliingia kama kinaingia sehemu iliyokuwa ngumu, ghafla maji kwenye chungu yalibadilika na kuwa damu.

    “Endelea kukiingiza kisu kwa nguvu,” mganga alinieleza.

    Kila nilivyojitahidi kukiingiza ilifika sehemu kikagoma kabisa kwenda mbele wala kutoka nje.

    “Chomoa kwanza.”

    Nilipochomoa kiligoma kutoka.

    “Kimegoma.”

    “Hebu,” ilibidi akitoe mwenyewe ndani ya maji ambayo yalikwishaanza kutoa harufu ya damu mbichi. Baada ya kukitoa kisu maji yalirudi katika hali ya kawaida. Hali ile ilimshtua mganga na kumsikia akishusha pumzi nzito na kusema:

    “Mmh! Hapa ipo kazi.”

    Nilimuona akikuna kichwa na kukitazama chungu ambacho muda huo kiliacha kuchemka ghafla kiliacha kuchemka japo moto ulikuwa bado unawaka. Nilijikuta nikichanganyikiwa hata Shedu naye alionekana kushtushwa na tukio lile ambalo bado sikuelewa.

    Nilisikia mganga akisema, hapa lazima turoge kazi hii ifanyike saa nane za usiku hatuna jinsi mtu tunayepambana naye si mtu mdogo, kajidhatiti ndiyo maana ameamua kufanya aliyotaka. Lakini muda si mrefu atanijua mimi ni nani sijawahi kushindwa na kitu japokuwa hili ni tukio langu kubwa kunisumbua lakini lazima nitamaliza kazi.

    Kazi hii sasa hivi ninatakiwa kuifanya mwenyewe kwa vile wewe ni mwepesi, nitaondoka mwenyewe usiku nikirudi kila kitu kitakuwa kama kilivyopangwa.”

    Kulikuwa na dalili za siku inayofuata kulala palepale, nikaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba mganga kazi ile imemshinda.

    Nikaona tutachelewa hata kazini, lakini sikuwa na jinsi siku ile tulilala palepale mpaka siku ya pili.

    Siku ya pili baada ya kufungua kinywa nilipelekwa porini ambako nilichanjwa juu ya kichuguu kupewa kinga kwa ajili ya kupambana na adui yangu ambaye alionekana amejidhatiti katika nguvu za kiza.

    Baada ya kupewa kinga ambayo nilielezwa hakuna mtu wa kunigusa hata mambo yangu yatakuwa mepesi tofauti na mwanzo.

    Kutokana na kazi kuwa nzito nilitakiwa kununua mbuzi mwekundu. Nilifanya hivyo kwa kutoa fedha kisha mganga aliwatuma watoto wake kwenda kumtafuta mbuzi huyo mwekundu asiye na baka lolote.

    Watoto walirudi jioni wakiwa na mbuzi mwekundu kwa ajili ya kafara yangu ya usiku ya kumkomesha mbaya wangu. Siku ile tuliendelea kusota kwa mganga mpaka usiku.

    Ilipotimu saa mbili ndipo mbuzi yule alipovishwa sanda na kuchinjwa na damu yake kumiminiwa ndani ya shimo lililochimbwa kama kaburi kisha tulimzika yule mbuzi ndani ya shimo lile akiwa ndani ya sanda na kuelezwa tukalale kwa ajili ya kujiandaa na safari ya siku ya pili alfajiri.

    “Vijana wangu kazi imekwenda vizuri kesho safari ya kurudi mjini ipo kama kawaida.”

    “Tutashukuru mzee wangu,” nilishukuru kwa vile nilikuwa nimeishaanza kuchoka kukaa pale kijijini.

    “Kazi imekwenda vizuri inaoneka hata tiba niliyokupa asubuhi imekusaidia sana.”

    “Kwa hiyo mzee kazi itakwenda kama ilivyopangwa?” nilimuuliza.

    “Shaka ondoa, japo kazi ilikuwa ni kubwa bado usiku nitatoka peke yangu kwenda kumaliza kazi ndogo iliyobakia.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Je, ikienda kinyume?” bado nilimdadisi mganga.

    “Haiwezi, nilichokifanya ni uchawi mkubwa sana.” Mganga alinihakikishia alichokifanya.

    Kauli ile ilinishtua na kujiuliza uchawi na uganga una tofauti gani, sikutaka kuuliza kitu lakini moyoni niliomba kafara yake ifanikiwe ili turudi mjini kwani maeneo yale yalikuwa yameanza kunikera.



    Tulilala mpaka siku ya pili ambapo tuliamshwa alfajiri, saa kumi na moja, baridi lilikuwa kali sana, nilijua tulitakiwa kujiandaa kwa safari, kumbe tulipewa taarifa iliyonivunja nguvu na kutamani kulia.

    Mzee Kidereko tangu alipoondoka jana yake hakurudi, hivyo tulitakiwa kuingia porini kumtafuta.

    Kwangu yale yalikuwa mapya na kujiuliza tunakwenda kumtafutia sehemu gani huko porini. Hatukuwa na jinsi tuliondoka zaidi ya watu sita wakiwemo watoto wawili wa kiume wa mganga na wasaidizi wake, huku msaidizi wake akitangulia mbele na usinga ili kutuelekeza mzee Kidereko alipo.

    Tulitembea porini kwa saa mbili bila kupumzika wala kujua mzee Kidereko alikuwa wapi. Lakini muda wote msaidizi wake alitueleza kuwa muda si mrefu tungemuona.

    Baada ya mwendo kidogo tulishtuka kuyaona matone ya damu.

    Ningekuwa peke yangu ningetimua mbio au kubadili njia lakini msaidizi wa mganga huyo alielekea upande uleule.

    Mimi na Shedu tuliwafuata nyuma huku nikijiuliza zile damu zilikuwa ni za nini? Tuliendelea kuzifuata, ziliongezeka kila tuliposogea mbele huku majani yakionekana kuvurugika kama kulikuwa na vita nzito.

    “Huyu hapa,” sauti ya mtoto wa mzee Kidereko ilitushtua na kutufanya sote tugeuke kwenye majani yaliyoonekana kulala kama kulikuwa na ugomvi wa tembo.

    Tuliposogea nilishtuka kumuona mzee Kidereko akiwa amelala ameshikilia pembe nyeusi iliyokuwa imefungwa na kitambaa chekundu kwa chini na mwili wake hasa sehemu za kifuani na tumboni zikionesha damu iliyoanza kuganda.

    Nilijua mzee Kidereko ngoma ilimshinda na kusababisha mauti yake, baada ya kumuona, msaidizi wake alitueleza turudi nyuma. Alitoa unga mweupe na kuanza kuurusha eneo lote, kisha alitoa maji kwenye chupa ndogo na kummwagia kichwani mzee Kidereko ambaye bado alikuwa ametulia kama tulivyomkuta.

    “Kazi ilikuwa nzito,” alisema msaidizi wake aliyekuwa akifungua kichupa kidogo na kutoa dawa aliyoiweka kwenye pua za mzee Kidereko. Baada ya sekunde chake alipiga chafya mfululizo na kuamka, alikaa kitako na kututazama kisha alimuuliza msaidizi wake.

    “Umekuja na utanduo?”

    “Ndiyo”

    “Nipe.”

    Alitoa pembe ndogo na kumkabidhi, aliichukua na kuifungua kwa chini kisha alitoa unga mweusi na kuuweka mkononi na kupuliza kidogo, uliobakia aliutupia wote mdomoni na kunyanyuka. Tuliongozana naye kurudi nyumbani.

    Tulipofika alikuwa amechoka sana, baada ya kuoga na kula aliingia ndani kwake kulala.

    Tulibakia njia panda na Shedu bila kujua nini kilikuwa kinaendelea, kwani tulikuwa tumemaliza siku ya nne tofauti na ruhusa ya siku mbili tulizoomba kazini. Nikiwa nimekaa na Shedu chini ya mti nilimuuliza rafiki yangu.

    “Shedu nini kinaendelea mbona sielewi?”

    “Kazala hata mimi nimechanganyikiwa hata sijui kinachoendelea.”

    “Shedu usipojua wewe mimi si ndiyo nitazidi kuchanganyikiwa kabisa.”

    “Kazala haijawahi kutokea tangu nimemfahamu mzee Kidereko.”

    “Sasa hii ni nini?”

    “Yaani sielewi ni wazi aliyemchukua mkeo ni mtu aliyejizatiti sana.”

    “Kwa hiyo kazi imemshinda?”

    “Mmh! Sijajua hebu tusubiri aamke.”

    “Kwa kweli nimekwisha kata tamaa.”

    “Kazala huwezi kuamini hata mimi nimechanganyikiwa, tangu nimfahamu huyu mzee na sifa zake kwa kazi nzito alizowahi kuzifanya hii yako imekuwa ya kwanza kwa haya yanayomtokea. Hajawahi kushindwa na kitu hata wasaidizi wake nao wamechanganyikiwa.”

    “Sasa huku tutakaa siku ngapi wakati tumezidisha siku moja?”

    “Tumsubiri aamke ili tujue nini kinaendelea kama ameshindwa tujue moja.”

    “Na akisema hajashindwa tutafanyaje maana hawezi kukubali kirahisi namna hii, lazima anaweza kutueleza tuongeze siku.”

    “Tutamuomba tuondoke kuwahi kazini ili tupange siku nyingine ya kurudi.”

    “Siamini kama ataiweza tena, kama ametaka kufa nina wasiwasi akilazimisha anaweza kufa bure.”

    “Kweli nimeamini mwenye uwezo wa juu ni Mungu peke yake, nilivyomuamini mzee Kidereko amechemka kwa siku nne. Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha.”

    Maneno ya Shedu yalinikatisha tamaa na kurudiwa na imani yangu ya awali kuwa hakuna uchawi bali kuna mazingaombwe. Nilijikuta nikianza kumuwaza upya mke wangu na kuamini hakukuwa na suluhu ya kumrudisha zaidi ya kuendelea kuteseka.

    Mpaka jioni inaingia mzee Kidereko alikuwa bado hajaamka.

    Pale nyumbani palikuwa kimya kila mtu aliendelea na shughuli zake kama hakikutokea kitu chochote cha hatari. Jioni ya siku ile mimi na Shedu tulizunguka baadhi ya vijiji, giza lilipoingia tulirudi nyumbani.

    Tulimkuta mzee Kidereko akiwa bado hajaamka, kitu kilichotutia wasiwasi ni mtu kulala asubuhi mpaka jioni. Nilijiuliza ni usingizi wa aina gani huo au ndiyo kapitiliza kabisa.

    Hali ya utulivu iliyokuwepo ilizidi kutupa wasiwasi na kujiuliza nini hatma ya yote. Majira ya saa tatu usiku tulifuatwa na yule binti aliyetupokea siku ya kwanza tuliyofika.

    “Mzee anawaita.”

    “Mzee gani?” niliuliza.

    “Jamani kaka Kazala hapa nyumbani kuna wazee wangapi?’

    “Mmoja.”

    “Basi ndiye anayewaita.”

    “Ameamka?”

    “Ndiyo.”

    “Saa ngapi?”

    “Muda mrefu, ameoga amekula na kupumzika.”

    “Lakini hajambo?”

    “Hajambo mbona hali ile ni ya kawaida, tumeizoea kazi hii inataka moyo la sivyo utaiacha.”

    Tuliongozana na yule msichana hadi ndani ya nyumba ya mzee Kidereko, hali ilikuwa tofauti na siku zote ambazo huzungumzia pale chini ya mwembe au kilingeni kwake. Alipotuona alitukaribisha.

    “Karibuni vijana wangu.”

    “Asante mzee, shikamoo.”

    “Marahaba karibu mketi.”

    “Asante.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulikaa kwenye viti vya kukunja na kusubiri alichotuitia. Baada ya ukimya mfupi alizungumza.

    “Vijana wangu.”

    “Naam mzee,” tuliitikia kwa pamoja.

    “Kwanza poleni kwa kuwachelewesha tofauti na tulivyokubaliana.”

    “Kawaida mzee tukupe pole wewe kwa matatizo uliyokutana nayo,” nilimpa pole kwa kuamini hata kama angekufa mimi ndiye ningekuwa chanzo.



    “Wala usihofu ile ni moja ya kazi zetu, kazi nyingine lazima ujitolee uhai ufe wewe au afe yeye.”

    “Kwa hiyo kazi imekuwa nzito?”

    “Ilikuwa nzito si nzito tena japo kidogo iondoke na roho ya mtu.”

    “Unamaanisha nini?”

    “Baada ya kafara ya mbuzi mwekundu kazi iliyobakia ni kummaliza kabisa, kumbe katika sehemu ya uhai wake kuna ulinzi mkubwa uliomzunguka yaani atakayegusa lazima aondoke.

    “Baada ya kuingia porini ili kumalizia kazi kilikuja kitu cha ajabu ambacho nimepambana nacho mpaka alifajiri. Ilikuwa vita nzito ambayo kwangu ilikuwa mara ya pili japo hii ilikuwa kubwa kidogo. Lakini mpaka naishiwa nguvu nilikuwa nimemaliza kazi. Kama ningeishiwa nguvu kabla sijammaliza ningekufa mimi.”

    “Mungu wangu,” nilishtuka.”

    “Usishtuke ni jambo la kawaida kwetu waganga.”

    “Kwa hiyo?”

    “Kesho mnaweza kurudi kazi imeisha.”

    “Kuhusu yule jamaa itakuwaje?”

    “Kazi imeisha hivi mkirudi mtakuta msiba.”

    “Msiba?”

    “Ndiyo.”

    “Wa nani?”

    “Wa adui yako.”

    “Kafa lini?”

    “Alfajili ya leo.”

    “Mmh! Umejuaje?”

    “Ndiyo kazi yangu, wewe umeleta si juu yako kujua kila kitu kinachofanyika zaidi ya kufanikisha kilichokuleta.”

    “Nini kilichomuua?”

    “Wewe ulitaka afe kwa nini?”

    “Ajali.”

    “Basi kafa kwa ajali leo alfajiri, asingekufa ningekufa mimi.”

    “Mmh!”

    “Basi nina imani kazi imekwisha japo ilikuwa nzito nashukuru imeisha salama, japokuwa kuna wakati nilianza kuchanganyikiwa. Lakini niliamini nitamuweza tu asingeweza kushindana na mimi huku ndiko Tewe hakujawahi kushindwa kitu.”

    “Basi tunashukuru. Vipi kuhusu mke wangu?”

    “Atarudi mwenyewe wala hakuna haja ya kutumia dawa kwa vile aliyekuwa akimzuzua ameshakufa.”

    “Mmh! Mzee kweli atarudi?”

    “Baada ya kifo atafukuzwa na ndugu wa huyo mwanaume na kumuona yeye ndiye nuksi.”

    “Kwa hiyo?”

    “Utamuona mwenyewe anarudi kuomba radhi, nina imani atatulia, kama adhabu atakuwa ameipata.”

    Tuliagana na mzee Kidereko nikiwa siamini na kuona kama vile mzee kazi imemshinda na kuamua kutuondoa kijanja. Tulikwenda kulala baada ya kujiandaa na safari ya kesho alfajiri kurudi tulipotoka ili tuwahi kazini japo tulikuwa tumepitisha siku mbili.

    Tuliamshwa alfajiri ya siku ya pili kwa ajili ya safari. Kwa vile kulikuwa na baridi kali hatukuweza kuoga, tulinawa uso tu.

    “Kazala mwanangu kazi yangu japo ilikuwa ngumu lakini nimeimaliza vizuri sana. Ningekuwa mtu mwepesi pale uliponikuta mngekuta mzoga.”

    “Ukisema mzoga una maana gani?” nilimuuliza.

    “Mngekuta nimekufa.”

    “Dah! Pole sana mzee wangu, ahsante sana kwa msaada wako.”

    “Nawe pia. Ila nina ombi moja naomba unisaidie!”

    “Ombi gani tena?”

    “Nakuomba jambo tulilofanya huku libakie siri yako, watu wao ndiyo watakaozungumza yao kuhusu kifo cha ugoni wako. Kifo hiki ni vigumu mtu kujua kwa vile mazingira yake hakuna atakayekuwa na wasiwasi kwa kuamini amri ya Mungu.”

    “Sawa mzee wangu nitafanya hivyo.”

    “Haya nawatakieni safari njema,”

    Mzee Kidereko alimpatia Shedu kifurushi kidogo na kumwambia:

    “Hii zawadi yako.”

    “Asante,” Shedu alipokea kile kifurushi, nikajua cha dawa japo sikutaka kujua dawa ya nini. Sikutaka kuhoji kapewa nini kwa vile ile ilikuwa hainihusu.

    Baada ya kila kitu kwenda kama kilivyopangwa tulisindikizwa na vijana wa mzee Kidereko kwa baiskeli mpaka Mlalo ambako tulifika muda wa saa moja hivi za asubuhi.

    Ilikuwa ni saa moja kabla ya magari ya kuelekea Dar kuondoka. Tulibahatika kupata tiketi kwenye basi la Umba, basi la Shambalai lilikuwa limejaa. Tuliingia na kukaa kwenye siti ya watu wawili.

    Saa mbili gari liliondoka Mlalo na kuelekea Dar es salaam, Shedu alionesha alikuwa na usingizi sana, safari ilipoanza tu aliuchapa usingizi mimi niliendelea kuangalia mji wa Mlalo.

    Akili yangu ilikuwa njia panda nisipate jibu kuhusu mwanaume aliyemchukua mke wangu kufariki dunia kwa ajali kama ni kweli.

    Akili yangu haikuamini nilijua yule mzee katutoa kisiasa ili tu tusiondoke tukiwa hatuna imani naye. Sifa alizonipa Shedu na niliyoyakuta niliona kuna tofauti kubwa. Lakini sikutaka kuumiza kichwa, ukweli na uongo wa mganga nilijua ningeupata baada ya kufika mjini.





    KWA vile ilikuwa ni alfajiri nami usingizi ukaanza kuninyemelea lakini jambo hilo lilikuwa limechangiwa na mazingira ya sehemu tuliyofikia, siku zote sehemu usiyoizoea huwezi kulala vizuri, basi nami usingizi ukanichukua bila ya kujijua.

    Shedu ndiye aliyenishtua kutoka usingizini, yeye aliamka muda ambao usingizi ulikuwa umeshanikolea.

    “Kazala amka tupate chakula cha mchana.”

    “Wapi hapa?” nilimuuliza baada ya kuona tumefika kwenye kituo cha basi.

    “Korogwe.”

    “Sasa ni saa ngapi naona jua ni kali?”

    “Saa saba.”

    “He! Kumbe nimelala sana!”

    Tuliteremka Korogwe na kupata chakula cha mchana, kisha tukarudi kwenye basi na kuendelea na safari ya kurudi kwetu. Tulifika Chalinze saa tisa na nusu alasiri, tulipanda basi lililokuwa likitoka Dar saa kumi na nusu jioni tuliingia makwetu saa nne usiku.

    Kwa vile muda ulikuwa bado Shedu alikwenda kwake na mimi nilirudi kwangu.

    Nilishukuru kwa kuwa siku ya pili ilikuwa Jumamosi ambayo kwa kawaida huwa siendi kazini, hivyo niliamini ningekuwa na muda mrefu wa kupumzika.

    Baada ya kula chakula nilichonunua, nilioga na kujitupa kitandani kutokana na kutawaliwa na uchovu usingizi haukuchelewa kunichukua.

    Nilishtuka siku ya pili tena baada ya kugongewa na jirani yangu, nilifungua mlango na kutoka nje.

    “Vipi jirani za asubuhi, ulisafiri?”

    “Nzuri, eeh nilitoka kidogo.”

    “Mbona hukuaga?”

    “Ilikuwa ni safari ya ghafla sana samahani kwa hilo.”

    “Mkeo alirudi,”

    “Eeh!” nilishtuka kusikia vile.

    “Alikuja juzi pamoja na mwanao, walikusubiri mpaka usiku bila kutokea, ilipofika usiku ilibidi alale kwenye korido asubuhi ya jana ndiyo kaondoka.

    “Jana tena alikuja hapa bila mtoto alikaa mpaka saa tatu usiku akaamua kuondoka,” aliendelea kunifahamisha jirani yangu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/---

    “Atakuwa amekwenda wapi?”

    “Mmh! Kwa kweli siwezi kujua ila ameondoka na kuniomba nimuwekee mizigo yake vizuri na kusema atarudi kesho. Nia yake ilikuwa ni kuingia ndani, amesema anaweza kuja na fundi ili amfungulie mlango. Kwa nini hukuacha funguo?”

    “Kama nilivyokwambia safari ilikuwa ya ghafla sana.”

    “Basi kwangu kuna mizigo ya mkeo,”

    “Sawa,” nilichukua mizigo ya mke wangu na kuiingiza ndani.

    Baada ya kuweka vitu vya mke wangu vizuri nilikaa kwenye kochi na kuanza kuwaza na kuwazua kama kauli ya mganga na niliyoyasikia muda mfupi kuhusu mke wangu kurudi nyumbani yalikuwa na uhusiano.

    Nilijiuliza kama mke wangu amerudi ina maana ni kweli yule mwanaume amekufa kwa ajali kama alivyonieleza mganga au kuna lingine lililotokea.

    Nikiwa katikati ya mawazo Simon alibisha hodi, nilimkaribisha ndani kwa vile mlango ulikuwa wazi. Simon aliingia akionekana kuwa na jambo alilotaka kuniambia, baada ya kuketi alisema:

    “Pole na safari.”

    “Asante.”

    “Mmh! mzee unatisha.”

    “Kivipi?”

    “Jamaa tumemzika jana.”

    “Jamaa gani?”

    “Si mgoni wako.”

    “Muongo!”

    “Kweli tumemzika jana, kwa kweli mimi na wote tuliosikia sababu ya kifo chake tulijua ni kifo cha kawaida lakini aliyonieleza Shedu nimeshtuka sana.”

    “Unashtuka nini wakati hata mgoni wa Shedu naye alilamba udongo.”

    “Ni kweli alilamba udongo, kifo chake wengi walijua kilitokana na kumchukua mke wa mtu, kulikuwa kama kuna miujiza fulani hivi, lakini kifo cha mbaya wako kilikuwa cha ajali, tena baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na gari la mafuta. Waliofika kwenye tukio wanasema wala hakuomba maji, alikufa palepale.

    “He! Kumbe kweli?” nilijikuta nikishtuka baada ya kusikia vile.

    “Unashangaa nini?”

    “Unajua aliyosema yule mzee mimi nilijua anatudanganya, nilidhani alikuwa anatupa moyo baada ya kuona kazi imemshinda.”

    “Kaniambia yote Shedu yaliyotokea huko, lakini ukweli unabaki palepale yule mzee ni tishio, hasa kwenye kazi za kulipa visasi.”

    “Lakini naamini adhabu aliyopewa ni kubwa sana,” nilisema.

    “Si ndiyo uliyochagua?” Simon aliniuliza akinikazia macho.

    “Adhabu hii sikuichagua bali walinichagulia ili kumkomesha.”

    “Basi tena ni kujipanga upya, shemeji amerudi?”

    “Nasikia amerudi juzi jioni na kulala hapa, asubuhi ameondoka inaonekana labda ameenda kwao.”

    “Sasa ndiyo mkeo atulie kama umemuua huyo, akiendelea na tabia yake utaua wangapi?” Simon aliniuliza.

    “Kwanza Simon hebu ondoa hilo neno la kusema nimeua, kazi yote imefanywa na mganga,” nilijitetea.

    “Kwa sababu ya nani?”

    “Kwa sababu yangu, lakini kwa uamuzi wa wengine, mi nilikuwa namtaka mke wangu tu.”

    “Basi ndiyo hivyo mkeo atarudi jipange kuhakikisha kosa la awali halijirudii tena.”

    Tukiwa katikati ya mazungumzo mara mlango wa mbele uligongwa, ilikuwa sauti ya mke wangu. Nilitamani ninyanyuke nikampokee lakini niliona aibu mbele ya ya rafiki yangu Simon.

    Nilimkaribisha aingie ndani.

    Mke wangu alipoingia alikuja moja kwa moja hadi nilipokuwa nimekaa na kupiga magoti kuomba msamaha.



    “Samahani mume wangu najua nimekukosea kwa yote niliyokutendea, nimeamini yote ni matawi shina ni wewe. Najua nimekuumiza mume wangu kiasi cha kukufanya uchanganyike. Yote ni kiburi cha nazi kushindana na jiwe, leo hii nimegeuka bundi kila kona nafukuzwa familia ya nilipokwenda hawataki hata kunisikia mama naye hataki kuniona nitakuwa mgeni wa nani?

    “Mume wangu Kazala nakuomba nipo chini ya miguuu yako, wewe ndiye kimbilio langu la mwisho, nawe ukinifukuza sina pa kwenda. Kazala mume wangu naomba unipokee tumlee mtoto wetu Zawadi. Najuta kukukimbia, nimeamini si wajinga waliosema usiache mbachao kwa msala upitao...

    “Shemeji Simon nakuomba niombee msamaha kwa mume wangu Kazala ambaye nilimkosea kwa kuondoka bila kuaga, zilikuwa ni hasira lakini leo hii zimekuwa hasara kwangu.

    “Kazala bado nakuhitaji katika maisha yangu, rudisha moyo wako nipokee tena, nakuahidi kuwa mke mwema katika maisha yangu yote yaliyobaki chini ya jua, nakupenda Kazala, nakupenda baba Zawadi nipo chini ya miguu yako,” mke wangu alilia kilio cha uchungu kuonesha kweli ameumizwa na yaliyotokea.

    Yote yaliyotokea kwangu hayakuwa tatizo kwangu zaidi ya mke wangi kurudi tena mikononi mwangu. Nilimnyanyua na kumkumbatia na kumweleza nimemsamehe. Nilimkumbatia mwanangu ambaye alikuwa kwenye afya nzuri na mke wangu.

    Pamoja na kuumizwa roho na kifo cha mgoni wangu, lakini nilipata faraja ya ajabu mke wangu kurudi mikononi mwangu. Kwa mara ya kwanza niliamini uchawi upo na unafanya kazi.

    Maisha yalianza upya huku mke wangu kila kukicha akijutia alichokifanya, nami nilimweleza yote aliyofanya nimemsamehe toka moyoni mwangu. Hali ya utulivu ilirudi ndani bila mtu kunitilia wasiwasi juu ya kifo cha mgoni wangu kuwa nimekisababisha mimi, wengi waliamini ile ilikuwa amri ya Mungu.

    Maisha nayo yaliendelea huku nikirudi katika hali yangu ya zamani kutokana na mapenzi mazito niliyopewa na mke wangu. Haikuchukua muda toka arudi, akabeba ujauzito mwingine ambao haukuwa na matatizo nao, hakuzungumzia kuutoa zaidi ya kuulea kwa ajili ya kusubiri siku ya kujifungua.

    Hali ile ilinifanya niamini mke wangu kweli tukio lililotokea limempa fundisho. Muda ulipofika alijifungua mtoto mwingine wa kike ambaye nilimwita Happy kutokana na furaha ya kurudi kwa utulivu ndani ya nyumba yetu.

    Watoto wetu Zawadi na Happy walikua vizuri huku mama yao akionesha kuwapenda na kuwajali tofauti na Zawadi alipokuwa mdogo alivyobemendwa na mama yake.

    Siku zilizidi kwenda nami nikizidi kuyafurahia maisha, mke wangu alichukua miaka mitatu na nusu toka arudi kuanza mambo yake. Nakumbuka aliniomba sana tutafute msichana wa kazi kwa ajili ya kumsaidia kazi za nyumbani.

    Kwa vile sikutaka kubishana na mke wangu nilikubaliana naye na kumpa ruksa ya kutafuta mfanyakazi.

    Haikuchukua hata siku tatu msichana wa kazi alipatikana kuonesha alimuandaa hata kabla ya kunieleza. Tuliendelea na maisha huku familia yetu ikiwa imeongezeka mtu mwingine.

    Waswahili wanasema kaniki hata ukiifua na mito na bahari zote dunia na sabuni zote hata siku moja haiwi nyeupe. Pia hawakukosea kusema la kuvunda halina ubani. Toka aliporudi alikuwa na tabia ya kunywa pombe kitu ambacho mwanzo nilikikemea lakini alinibembeleza kwani alikuwa amezoeshwa na alipokwenda.

    Kwa vile nilikuwa nampenda nilimkubalia awe anakunywa siku mojamoja. Sehemu tuliyokuwa tukiishi kulikuwa na Grosari karibu. Mara nyingi alimtuma msichana wa kazi na kumletea ndani na kunywa.

    Siku nyingine niliporudi sikumkuta ndani, msichana wa kazi alinieleza kwamba, mke wangu alimwambia, kama nitarudi kabla hajarudi akamwite.

    Nilimtuma akamwite japo muda ule alitakiwa kuwa nyumbani, alimfuata na baada ya muda alirudi akiwa amechangamka kidogo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Vipi mume wangu umerudi zamani?”

    “Kama dakika tano, vipi umeanza lini kwenda baa kunywa?”

    “Samahani mume wangu, leo jirani yetu God alinipa ofa hapo nje kwenye Grosari.”

    “Hakuna tatizo ila usiiendekeze sana pombe.”

    “Mume wangu si leo tu, tena nimepewa ofa na jirani.”

    “Hakuna tatizo ila usiendekeze sana, kunywa siku mojamoja siyo mbaya.”

    Kumbe ukaribu na jirani yangu ulikuwa na maana pana zaidi ya ujirani, mke wangu alianzisha uhusiano na jirani yangu ambaye nikiwa kazini alimgeuza mke wangu wake.

    NAKUMBUKA siku moja usiku nikiwa kitandani nilishtuka na kujikuta nimelala peke yangu.

    Sikuwa na wasiwasi kwa kuwa niliamini kuwa huenda mke wangu alikuwa amekwenda msalani.

    Kwa vile choo na bafu vilikuwa nje nilijua amekwenda kujisaidia tu, nilijilaza, sikuchelewa sana nikapitiwa na usingizi. Niliposhtuka nilishangaa kumuona mke wangu akiwa pembeni yangu amezidiwa na usingizi.



    Siku hiyo kabla ya kulala nilijaribu kumgusa mke wangu lakini aliniomba radhi kwa kuniambia kuwa tumbo lake lilikuwa limeshtuka ghafla.

    Kwa vile ile hali haikuwahi kumtokea, nilimuacha na kuendelea kuuchapa usingizi,

    siku ya pili tena nilipomgusa alinieleza bado alikuwa akisumbuliwa na tumbo.

    “Sasa mke wangu umetumia dawa gani?”

    “Si...sijatumia dawa yoyote mume wangu.”

    “Sasa utaendelea kuilea hali hii mpaka lini? Kumbuka mumeo lazima nipate haki yangu kutoka kwako!”

    “Najua mume wangu, samahani kwa hilo, kesho nitakwenda hospitali.”

    “Mmh! sawa.”

    “Nisamehe mume wangu,” alisema huku akinibusu na kunifanya mwanaume nilegee kabla ya usingizi haujatuchukua, kama kawaida yetu tulilala tukiwa tumekumbatiana ili kupeana joto, mpaka pale kila mmoja wetu alipopitiwa na usingizi na kugeukia upande wake kwa kupeana migongo.

    Nilishtuka katikati ya usiku, usingizi ulikuwa umenipaa na kujikuta nikiwa peke yangu kitandani, hata hivyo sikuwa na wasiwasi kwa kuwa nilihisi mke wangu atakuwa amekwenda msalani, niliendelea kujilaza huku macho yangu nikiyaelekeza darini.

    Muda mrefu ulipita bila mke wangu kurejea kitu ambacho kilinitia wasiwasi labda tumbo lilikuwa limemzidia kule msalani. Nilinyanyuka kitandani na kutoka nje kwenda kumuangalia.

    Nilifika hadi msalani, sikuona dalili ya kuwepo kwa mke wangu, nilijaribu kuliita jina lake lakini hakukuwa na jibu lolote.

    Niliingia hadi msalani lakini sikumuona, nilitoka nje na kujiuliza atakuwa amekwenda wapi, nilizunguka nyumba nzima sikumuona, niliamua kurudi ndani nikiwa na mawazo tele kwa kutomuona usiku wa manane kama ule.

    Nilikaa kitandani nikijiuliza maswali mengi, nilishangaa usiku kama ule atakuwa amekwenda wapi, nilihisi labda atakuwa amezidiwa na kuamua kwenda nyumbani kwao, lakini nilipingana na wazo hilo kwa kujua kuwa kama ingekuwa hivyo ni lazima angenijulisha, asingeweza kuondoka peke yake tena kimyakimya.

    Nikiwa nimekaa kitandani niliona mlango ukifunguliwa kwa uangalifu mkubwa, mtu aliyekuwa akiufungua alitulia kwa muda, nikataka kumuona aliyekuwa akiingia kwa kunyata kwa kudhani labda alikuwa ni mwizi.

    Baada ya mlango kufunguliwa mtu aliyekuwa akiingia ulitanguliza mguu wake wa kulia, kisha mwili wake ukaonekana.

    Alikuwa ni mke wangu akiwa katika vazi la khanga moja,aliponiona alipatwa na mshtuko mpaka khanga aliyokuwa ameivaa ikamdondoka na akabakia mtupu kama alivyozaliwa, hakuiokota bali aliendelea kusimama kama mwanga aliyekamatwa wakati akijiandaa kuwanga.

    Nilimuangalia na kushindwa kumuelewa kwa nini alikuwa katika hali ile ya kutahayari.

    “Vipi mke wangu?” nilivunja ukimya baada ya kumtazama kwa muda mrefu.

    “Sa...sa...” alishindwa kusema alichokuwa amekikusudia.

    “Unatoka wapi?”

    “Msalani, tumbo lilinizidia nikachelewa kurudi.”

    “Ulienda choo kipi?”

    “Cha nje.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo mume wangu.”

    “Na sasa hivi ndiko unakotoka huko au...?”

    “Ndiyo mume wangu,” alijibu huku vidole vyake vya mkono mmoja akiwa ameviweka mdomoni.

    “Wakati mimi nilipokuwa nikiingia msalani wewe ulikuwa wapi?”

    “Kwani wewe umekwenda msalani saa ngapi?”

    “Hebu kwanza vaa nguo yako,” niliposema hivyo aliinama na kuiokota khanga yake na kujifunga, kisha akasimama palepale na kuendelea kuweka vidole vyake mdomoni kama mwanamke aliyekuwa akitongozwa kwa mara ya kwanza.

    “Mke wangu ulikuwa wapi?”

    “Msalani mume wangu,” aling’ang’ania jibu lake.

    “Si kweli, nimeshtuka kutoka usingizini muda mrefu na kukaa macho, nikawa na wasiwasi labda umezidiwa na tumbo, nikatoka hadi msalani sikukuona, nikazunguka nyumba nzima, sikukuona sasa huo msala ni msala gani uliokwenda wewe?” nilimuuliza huku nikimsogelea hadi karibu yake na niliweza kuhisi mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yakimuenda kwa kasi.

    Mke wangu alishindwa kunijibu, kitu ambacho kilinipandisha hasira na kunifanya nitambue kuwa kulikuwa na mchezo mchafu aliokuwa akinichezea.

    Nilimkazia macho na kumuuliza kwa mara nyingine tena kwa hasira huku nikiivuta khanga aliyokuwa amejifunga na kumfanya abakie mtupu.

    “ Hebu niambie ukweli, ulikwenda wapi? kama utanidanganya, nitakachokufanyia hutakuja kukisahau mpaka utakapoingia kaburini. Ni mwaka wa tatu na nusu tangu moyo wangu upone majeraha. Hujaridhika unauchubua tena, niambie ulikuwa wapi?”

    “Samahani mume wangu nilipokuwa nikirudi kutoka msalani, nilipofika kwenye mlango wa God, aliniita kwake lakini sijafanya naye kitu chochote kile.”

    “Leo hukufanya naye kitu, sawa siku zote ulizokuwa ukienda kwake ulikuwa ukifanya naye nini?”

    Swali langu lilimpa wakati mgumu kulijibu, akabakia akiumauma meno, nikapata nafasi ya kuongeza maneno mengine.

    “Mke wangu wewe ni kiumbe gani, umenifanya nimechuma dhambi kwa ajili yako, tumetulia umeanza tena, kibaya zaidi ndani ya nyumba tunayoishi. Wewe ni kiumbe gani? umerogwa na nani mpaka kuwa katika hali hii?”

    “Nisamehe mume wangu ni shetani tu, mi nipo chini ya miguu yako, sitarudia tena,” mke wangu alinisogelea na kupiga magoti.

    “Haya nieleze ukweli tangu umerudi hapa nyumbani umeshaisaliti ndoa yetu mara ngapi?”

    “Kwa haki ya Mungu ni mara nne tu.”

    “Na wanaume wangapi?”

    “Mmoja tu mume wangu, ni God tu, ukweli wa Mungu tangu nimkubalie ni wiki ya pili sasa, hata hivyo nilijitahidi kumkatalia lakini nimeshindwa kwa kuwa amekuwa akinisumbua sana.

    “Amekuwa akinipa ofa na fedha

    za pombe, siku zote shetani ana nguvu, nimejikuta nikimkubalia na kukusaliti kwa mara nyingine mume wangu.

    “ Najua ni kwa jinsi gani ninavyokuumiza lakini nakuomba usiniache, pombe ndiyo sababu mume wangu nitaiacha, siku aliyonipa ofa ya pombe ndiyo ilikuwa mwanzo wa kunisumbua kimapenzi, kwa kweli nilijitahidi lakini nilijikuta nimemkubalia bila kujua, naomba usiniache mume wangu.

    “Mama alishaniambia siku nikifanya ujinga kwako kisha ukanifukuza, basi nitafute mahali pengine pa kwenda, nisirudi kwake.

    Unataka kujua kilichotokea?



    “Nakuahidi mume wangu sitafanya ujinga tena na pombe leo ndiyo mwanzo na mwisho.”



    Japo kauli ya mke wangu haikuwa na nguvu ya kunishawishi kumsamehe hasa baada kujua kuwa ametoka kwa mwanaume baada ya kunikimbia kitandani na kwenda kufanya uchafu wake. Kikubwa kilichoniuma ni dharau zilizokuwa zikioneshwa na jirani yangu kwa kutembea na mke wangu akijua ni mke wa mtu.



    Kilichoniuma zaidi kilikuwa kumshawishi kunitoroka kitandani na kuniacha peke yangu.



    Roho iliniuma kufanywa bwege kiasi kikubwa, kwangu ilikuwa dharau kubwa sana ambayo iliuumiza moyo wangu kwa jinsi nilivyodhallishwa kiasi cha kutaka kulipa kisasi cha historia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliamini kuwa mke wangu hakuwa na kosa ila kuna watu walitaka kuniona mimi ni nani. Nilipanga mwisho wa wiki niende tena kwa babu kumtia adabu.



    Tena mtu huyu sikuwa na huruma naye hata kidogo niliapa kumbakisha jina tu.



    Nilimsamehe mke wangu na kumuomba abadilike la sivyo sitamuuliza kitu chochote tena na wala sitamfukuza.



    Mke wangu alinihakikishia kutulia kwa kusema kuwa hatarudia tena kosa kama lile, siku ile niliiacha ipite lakini moyoni nilikuwa na maumivu na hasira kama nyoka aliyekanyagwa mkiani.



    Nilijitahidi kuficha kilichonikuta kwa watu wote huku nikiomba mwisho wa wiki ufike upesi.



    Siku zote mke wangu hakuacha kuniomba msamaha, nilimwa,bia kuwa nimemsamehe toka moyoni na si mdomoni.



    Jirani yangu baada ya kugundua nimegundua hila zake ya kumchukua mke wangu, akawa anatoka alfajiri na kurudi usiku wakati siye tukiwa tumelala. Moyoni nilijisemea kuwa arukeruke lakini siku zake za kuishi duniani zilikuwa zinahesabika, nikifika kwa mzee Kidereko lazima alambe udongo.



    Niliapa kuwa siri ile hataijua mtu yeyote, baada ya kumsamehe mke wangu nilijilazimisha kuishi maisha ya kulazimisha furaha huku moyoni nikiwa na maumivu makali kutokana na tabia za watu kumgeuza mke wangu jamvi la wageni.



    Kwa vile dawa yao niliijua sikutaka kubishana na mtu zaidi ya kupanga safari ya kwenda kwa Mzee Kidereko kule Tewe.



    Hakuna aliyegundua mabadiliko yangu kazini na nyumbani, wengi walijua uhusiano wetu ulikuwa ni mzuri, pia kitabia mke wangu alikuwa amejirekebisha.



    Hata safari yangu ya kwenda Tewe niliifanya kuwa ni siri yangu, sikutaka kumwambia hata Shedu aliyenipeleka kwa mzee Kidereko kwa mara ya kwanza.



    Moyo wangu ulikuwa umeingia woga kuiogopa aibu ya kuonekana bwege kama watu wangejua kuwa mke wangu karudia makosa yaleyale.



    Ijumaa baada ya kazi nilianza safari yangu huku nikimuaga mke wangu kuwa nakwenda nyumbani kwa wazazi nimeitwa mara moja. Mke wangu alinitakia safari njema huku akinihakikishia kwa maneno mazito kuwa nimuamini.



    “Mume wangu najua huniamini tena moyoni mwako, lakini nakuahidi mbele ya muumba ambaye hakosekani kila sehemu, yeye ndiye shahidi yangu kwa haya ninayoyasema mbele yako muda mfupi kabla hujaenda kuwaona wazazi wako.



    “Ni kwamba nimekuwa kama kaniki isiyobadilika rangi hata ukifuliwa na kusuguliwa vipi.



    “Lakini hili ninalolisema mbele yako kama nitarudia tena kosa basi Mungu anigeuze kiumbe chochote cha ajabu au kuyachukua maisha yangu,” mke wangu alisema kwa sauti iliyotia uchungu.



    Alizungumza maneno mazito ambayo yalinitoa machozi na kunifanya niamini kuwa kiapo chake kile kilitoka moyoni mwake na kujutia alichokifanya.



    Pamoja na kutaka kumuamini bado nilimuona kama mjusi asiyeweza kugeuka kuwa nyoka hata ukimpaka unga.



    Nilijua kile kilikuwa ni kilio cha majuto lakini mke wangu alikuwa na akili za mbuzi, hakawii kujisahau na baada ya tukio hutulia na kujutia.



    Kwa upande mwingine kiapo cha mke wangu nilikiona kizito sana kwa kuwa alijichagulia adhabu na kama atarudia utakuwa ni upumbavu wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wazo la kusitisha safari yangu lilikuja na kuona hakuna haja ya kwenda kwa mzee Kidereko, niliona ni heri nitulie tu na kufanya mambo mengine.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog