Search This Blog

Thursday, 2 June 2022

MIKONO MICHAFU - 2

 





    Simulizi : Mikono Michafu

    Sehemu Ya Pili (2)





    ***** ***** ***** *****



    NILIPOINGIA ndani ya nyumba ile kitu cha kwanza kilichovuta macho yangu katika nyumba hiyo inayodaiwa ni ya Mzee Kibwana ni picha ya baba wa taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ni picha inayoonekana kuwa ni ya siku nyingi iliyopigwa wakati kiongozi huyo akiwa kijana. Pamoja na kuonekana ni ya zamani sana lakini imewekwa kwenye fremu nzuri na kuonekana kutunzwa vizuri.



    Jambo la pili lililonitia mashaka ni mapokeo ya wale watu wawili wakati Mwajuma ananitambulisha kwao, ni kama kuna mambo ambayo wanadhani kuingia kwa mtu kutoka nje kutayafanya yajulikane. Nikabaki najiuliza, ni kweli kuwa mzee Kibwana anahusika na ujambazi? Na kama anahusika na kwa umri alio nao ina maana kaanza toka ujanani, je ana maisha yanayoendana na ujambazi? Na kama kaanzia uzeeni, ni jambo gani lilimsukuma?



    Ukweli ni kuwa ilikuwa ni kesi ndogo sana kufuatiliwa na mtu wa nafasi yangu, ile ni kazi ya wapelelezi walioko chini ya jeshi la polisi. Nilikuwa nafanya unoko tu wa ‘kiboya’ ambayo hata mwenyewe siupendi lakini upande mwingine uzoefu unaonyesha kuwa huwa hakuna jambo dogo.



    Hadi baada ya muda mfupi tukiingia maeneo ya Kinondoni Shamba iliyopo nyumba ya mzee Kibwana, tayari nilishahisi uwezekano kuwa tukio la kupeleleza mwenendo wa lile gari nililoliona uwanja wa ndege linahusiana na kesi ya yule mzee pamoja na ujio mpya wa Mwajuma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa maelezo ya mzee Kibwana, mwenendo wa mwajuma nnaoufahamu, na muonekano wa watu wale tuliokuwa nao mahakamani nilihisi kuwa kuna igizo kubwa lilikuwa linaendelea na mimi nimeingizwa katikati bila kujijua.



    Mzee yule alidai kuwa kazi yake ya udereva wa taxi inamuwezesha kuhudumia familia yake ya watu saba, lakini pale walikuwa Mwajuma na ‘mama yake’ tu.



    Kwa kusema ukweli starehe yangu kubwa huwa ni kuwaangalia mabinti warembo, nakumbuka toka wakati nasoma sekondari nilikuwa kila nikitoka shule jioni hukaa pale Posta mpya na kuanza kuangalia wasichana warembo wakienda na kurudi. Nafsi yangu ikishiba napanda daladala kurudi nyumbani. Basi nimejikuta hata sasa napenda kukodolea macho warembo kisha nawaacha waende zao bila kuwasemesha.



    Baada ya kuegesha tu gari nikaanza juhudi za kuiona sura yake ili nione kama kuna uwiano kati ya sura na umbile lile, niliona kuwa ni vyema niitendee haki nafsi yangu kabla ya kuingia ndani kusikiliza kesi niliyoifuata. Nikajifanya natoa simu kuongea na mtu huku nikielekea upande aliopo mlimbwende yule aliyekuwa akionekana anamsubiri mtu.



    Nilipofika kama hatua nne hivi kabla ya kumfikia, mrembo akanirahisishia kazi kwa kugeuka. Nilijikuta nimeshikwa na bumbuwazi nikimkodolea macho kama nimefumaniwa, kumbe alikuwa Mwajuma! Mwajuma alikuwa akinisubiri ili tuingie wote ndani. Tukaingia kwa kuongozana kama mke na mume wanaoingia kanisani kufunga ndoa. Hatukuongea chochote zaidi ya kusalimiana na Mwajuma kunishukuru kwa kuitikia mwito wake wa kufika mahakamani kutoka msaada.



    Kwa kweli kwangu kama mume wa mtu mwenye ndoa changa, haikuwa dalili nzuri kuvutiwa namna ile tena na mtu ambaye alishawahi kuwa mpenzi wangu huku bado kukiwa kuna uwezekano wa kumrudisha kwenye himaya yangu. Ila nilipiga moyo konde na kumkemea shetani.



    Ilikuwa yapata saa tatu hivi wakati kesi inaanza kwa washitakiwa kupewa nafasi ya kutoa maelezo yao ya utetezi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu ya kuwekwa ndani. Waliongea kwanza watu watatu kati ya saba waliokuwa wakituhumiwa kufanya tukio la ujambazi kwa kuvamia benki mojawapo iliyokuwa katikati ya jiji pamoja na kuua askari wawili ndipo ikafika zamu ya baba yake Mwajuma.



    Kwa mujibu wa maelezo waliyotoa wale waliotangulia na ushahidi wao haraka haraka ilinijia picha kuwa kilichofanyika baada ya tukio la ujambazi kutokea ni kwa polisi kuwakamata watu wenye rekodi za uhalifu na kuwapa kesi hiyo ya ujambazi.



    Kimsingi maelezo ya watuhumiwa wale yalinikera sana, ilionyesha dhahiri kuwa kuna kazi ya ziada kulinoa jeshi letu la polisi hasa kitengo cha wapelelezi wa kesi. Ilionekana kama kuna uvivu fulani katika ufuatiliaji wa matukio ili kupata wahusika sahihi.



    “Mimi ni dereva wa taxi toka mwanzoni mwa miaka ya themanini na ndiyo kazi inayonipa mahitaji ya kila siku mimi na familia yangu ya watu saba. Siku ya tukio nilikuwa nimeegesha gari eneo la stesheni, nikafuatwa na jamaa wanne waliokuwa na mabegi makubwa wakitaka niwapeleke Kimara. Tukaanza safari, kufika maeneo ya Ubungo Kibo kukawa na pikipiki ya askari inayokuja nyuma yetu.” Alianza kujieleza mzee huyo anayejulikana kwa jina la Jamali Kibwana.



    “Kila tulipokuwa tukienda wale askari walikuwa kama wanatufuata sisi. Kufika Kimara Korogwe, ghafla nikasikia mlio. Kuangalia kwenye kioo nikakuta wale askari wanadondoka na pikipiki yao kisha wale jamaa wakaniamuru nisimame. Wakanirushia noti nne za elfu kumi kumi na kushuka wakikimbia kuingia njia mojawapo” aliendelea kujieleza kwa ufasaha.



    “Nikapiga simu polisi kutoa taarifa, ila polisi walipofika pale wakanichukua kwa ajili ya kusaidia upelelezi kabla hawajaniunganisha na hii kesi.” Alimaliza kujieleza mzee Kibwana huku umati wote unaosikiliza kesi ile ukimsikitikia mzee huyo aliyekuwa akitia huruma kutokana na umri wake, kazi yake na mashtaka yanayomkabili.



    Watu wakaanza kunung’unikia jeshi la polisi kwa chini chini. Pamoja na kuwa kila mtu aliamini yule mzee angeachiwa, watu walikuwa wakisikitika kutokana na muda aliopotezewa kukaa mahabusu na mateso ambayo huenda yalikuwa yakiipata familia yake.



    Ila mimi nilikuwa na mawazo tofauti kwa kuwa kuna maswali

    mengi nilikuwa najiuliza bila kupata majibu. Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza tukio hilo ila tatizo lilikuwa moja, ntamshirikisha nani ambaye atanielewa na mkuu ndiyo hivyo keshatoweka duniani?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wale waliobaki waliendelea kutoa maelezo yao kisha kesi ikaahirishwa hadi siku iliyokuwa ikifuatia. Tukatoka nikiwa nimeongozana na Mwajuma ambapo nje alinitambulisha kwa ndugu zake kadhaa kama mtu niliyesoma naye shule ya msingi ila nina ujuzi kidogo na mambo ya kisheria kwa hiyo aliniomba niwasaidie. Najua watu wazima walidhani kuwa mimi ni mpenzi wake kutokana na utambulisho ule usio na mashiko.



    Baadhi walionekana kuufurahia ujio wangu, lakini kuna mzee mmoja ambaye nilitambulishwa kama rafiki wa karibu wa Mzee Kibwana alionekana kuniangalia sana kama aliyetaka kunifahamu zaidi ya alivyoelekezwa au kama anayetakakujua nilichohisi, pia kuna tatizo nililiona kwa kijana mmoja ambaye wana undugu na familia ya Mzee Kibwana. Huyu alionekana dhahiri kuwa hakufurahia ujio wangu pale.



    “Umeionaje kesi baba?” aliniuliza kwa shauku niliyetambulishwa kama mama yake Mwajuma, au ‘mzaa chema’.



    “Hana kesi mzee, naamini ataachiwa tu. Wala msipoteze gharama ya kutafuta mwanasheria” nilijibu kuwaridhisha wote, waliopenda ujio wangu na wale wasiopenda. Ila pamoja na kujibu ili kuwaridhisha, niliamini kuwa ni kweli mzee Kibwana angetoka kutokana na hali niliyoiona na uzoefu wangu.



    Hapo kidogo nikaona naenda sawa hadi na ‘wapinzani’, nikawa nimefanikiwa kuwaondoa mashaka kwa kiasi fulani.

    “Mimi toka mwanzo nawaambia, mzee hana kesi, atatoka tu. Mmeona hata mtaalam anasema?” alijinadi yule kijana anayejulikana kama Mateso.



    Baada ya maongezi mawili matatu nikaamua kumpa lifti Mwajuma, mama yake na yule mzee ambaye baadaye nilikuja kujua kuwa anaitwa Boimanda. Nilikuwa nishafikia uamuzi kuwa nipoteze muda fulani kujiridhisha kuhusiana na mambo niliyokuwa nayoyahisi.



    Nadhani utanishangaa kwa nini nilipatwa na wasiwasi huo. Kwa namna mzee Kibwana alivyohadithia ni kwamba baada ya tukio lile alipiga simu polisi. Nikuulize wewe katika hali kawaida, una namba za polisi hapo ulipo? Na hata kama hizo namba unazo, tukio kubwa kama lile likikutokea hatua yako ya kwanza itakuwa ni kutoa ripoti polisi? Akili iliyonijia ghafla ni kwamba mzee Kibwana anahusika kwa namna moja au nyingine.





    Jambo la pili lililonitia mashaka ni mapokeo ya wale watu wawili wakati Mwajuma ananitambulisha kwao, ni kama kuna mambo ambayo wanadhani kuingia kwa mtu kutoka nje kutayafanya yajulikane. Nikabaki najiuliza, ni kweli kuwa mzee Kibwana anahusika na ujambazi? Na kama anahusika na kwa umri alio nao ina maana kaanza toka ujanani, je ana maisha yanayoendana na ujambazi? Na kama kaanzia uzeeni, ni jambo gani lilimsukuma?

    Ukweli ni kuwa ilikuwa ni kesi ndogo sana kufuatiliwa na mtu wa nafasi yangu, ile ni kazi ya wapelelezi walioko chini ya jeshi la polisi. Nilikuwa nafanya unoko tu wa ‘kiboya’ ambayo hata mwenyewe siupendi lakini upande mwingine uzoefu unaonyesha kuwa huwa hakuna jambo dogo.

    Hadi baada ya muda mfupi tukiingia maeneo ya Kinondoni Shamba iliyopo nyumba ya mzee Kibwana, tayari nilishahisi uwezekano kuwa tukio la kupeleleza mwenendo wa lile gari nililoliona uwanja wa ndege linahusiana na kesi ya yule mzee pamoja na ujio mpya wa Mwajuma.

    Kwa maelezo ya mzee Kibwana, mwenendo wa mwajuma nnaoufahamu, na muonekano wa watu wale tuliokuwa nao mahakamani nilihisi kuwa kuna igizo kubwa lilikuwa linaendelea na mimi nimeingizwa katikati bila kujijua. Mzee yule alidai kuwa kazi yake ya udereva wa taxi inamuwezesha kuhudumia familia yake ya watu saba, lakini pale walikuwa Mwajuma na ‘mama yake’ tu.

    Nilipoingia ndani ya nyumba ile kitu cha kwanza kilichovuta macho yangu katika nyumba hiyo inayodaiwa ni ya Mzee Kibwana ni picha ya baba wa taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ni picha inayoonekana kuwa ni ya siku nyingi iliyopigwa wakati kiongozi huyo akiwa kijana. Pamoja na kuonekana ni ya zamani sana lakini imewekwa kwenye fremu nzuri na kuonekana kutunzwa vizuri.

    Ukiiangalia sebule yake kwa juu juu huwezi kuiona thamani yake kwa kuwa fenicha zake zinaonekana ni za kizamani sana, lakini ukitafakari mbao zilizotengenezewa zile fenicha, na mapambo ya kiasili yaliyopamba sebule ile utapata mtazamo tofauti.

    Sikuonyesha kushtuka na hali niliyoikuta mule, wakati huo Mwajuma na mama yake walikuwa wameingia ndani, nadhani kubadilisha mavazi wakiniacha na soda. Kwanza nilijaribu kuishia nje lakini wakaniomba niingie ‘kuwapa Baraka zangu’ japo kwa kunywa maji ya kunywa, hapo nikapata nafasi niliyoihitaji.

    Kitu ambacho kilikuwa kikitembea akilini mwangu ni kuwa pale sio kwa Mzee Kibwana, na uwezekano wa familia ile kuwa ya Mzee Kibwana ni ndogo sana. Kila kitu kilionekana kuwa kimepangwa vyema, ila kwa wenye upeo na michezo ya ajabu ajabu kama mimi utagundua tu kuwa hakukuwa na uhalisia. Nikaingiza mkono mfukoni, nikaibonyeza namba moja kwa muda bila kuiachia.

    Simu ilikuwa imejipiga kwenye mojawapo ya namba za dharura na kwa muda ule nikawa na uhakika kuwa niko hewani, kwa maana mtu wa upande wa pili atakuwa anasikia kila ninachoongea.

    “Hapa ndiyo nyumbani Nas… ah Musa” aliniambia Mwajuma akitokea chumbani kwake huku akionyesha kubabaika jina.

    “Lolote utakaloliita ni sawa, Naitwa Musa Nasib Njiwa” nililazimisha kuliingiza jina la Nasibu kujaribu kuondoa aibu ya kuonekana mwongo mwongo huku nikimalizia soda.

    Mwajuma akaniangalia kama anayekagua kama ninachosema kina ukweli, nami nikabaki namwangalia kabla hatujakatizwa na Boimanda aliyeingia kama mtu anayeingia kumfumania mkewe. Mzee huyu anayeonekana kuwa amejaaliwa ukorofi, tulimuacha nyumba takribani kumi kutoka pale kwa mzee Kibwana.

    “Ndiyo kijana, karibu sana” alikuwa anaongea huku akikaa kwenye mojawapo ya viti vilivyomo pale sebuleni.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapa wanapaita Kinondoni Shamba eeh?” niliwapiga swali lakini kwa mtindo wa kutoa maelekezo kwa mtu ambaye atakuwa amepokea simu upande wa pili.

    “Ndiyo bwana mdogo, ukitaka kumuelekeza mtu unamwambia tu Kinondoni shamba nyumba namba 288 karibu na kiwanda cha wachina” alijibu Boimanda huku akinikazia macho.

    Damu ilinisisimka kwa vile mzee yule alikuwa ananipa ujumbe kuwa anajua ujanja ninaoufanya.

    “Sawa sawa, mi ngoja niwaage sasa hivi” niliongea huku nikiinuka.

    “Nimekufukuza?” aliongea Boimanda kwa kujishtukia. Tukaishia kuzuga kucheka tu bila kujibu lolote. Nikamuaga mama Mwajuma kisha nikatoka na kuondoka zangu nikisindikizwa na Mwajuma hadi kwenye gari langu.

    “Nakumbuka tulivyokuwa tukilala kitandani huku tumekumbatiana tukihadithiana mambo mbalimbali, Mwajuma uliniahidi mambo mengi sana yaliyonifanya nikukabidhi moyo wangu na kuamini kila uliloniambia lakini mwisho wa yote uliamua kuondoka bila hata kusema kwa heri” nilianza kumueleza Mwajuma nikiwa kwenye gari na yeye amesimama chini.

    “Jamani, hayaishi?” aliuliza Mwajuma kwa aibu

    “Nakwambia yote haya kwa sababu nahisi umejitokeza ili uniongezee maumivu katika maisha yangu, na safari hii nadhani utaniua kabisa. Najua fika mwisho utakuwa siyo mzuri ila nimeamua kukusikiliza ili damu yangu iwe juu ya binti ninayempenda” nilimwambia makusudi maneno yale ili yamchome moyoni

    “Musa nakupenda sana ila yanayotokea yanakuwa juu ya uwezo wangu” Mwajuma aliongea maneno ambayo sikuwa na shaka kuwa yalimtoka moyoni kisha akageuka na kurudi ndani.

    Nilielewa Mwajuma alimaanisha nini, ina maana kuna watu wako nyuma yake wanampangia mambo ya kufanya na wakati wa kuyafanya. Nilipata uhakika kuwa simfahamu Mwajuma kama nilivyodhani, mbali na Boimanda, ni kina nani na kwa nini wameweza kumkontroo? Na Mwajuma hasa ni nani?

    Mzee Kibwana alikuja kuachiwa huru kama ambavyo kila mmoja alitarajia lakini hadi wakati huo kuna hatua kadhaa nilizokuwa nimezifanya ambazo zilipelekea kuzidi kuingiwa na mashaka na tukio zima lililopelekea mzee Kibwana kuwekwa ndani. Tatizo linaonekana lipo kwa Boimanda.

    Siku ya tukio, gari la mzee Kibwana lilikodiwa na Boimanda kwa ajili ya shughuli zake kitu ambacho ni nadra sana kutokea. Walipofika maeneo ya stesheni, Boimanda alimuacha mzee Kibwana pale amsubiri ila akampa tahadhari kuwa akimsubiri kwa nusu saa bila kutokea anaweza kuondoka.

    Na baada ya tukio la majambazi kuwapiga risasi polisi, simu ya kwanza kupokelewa na mzee Kibwana ilikuwa ya Boimanda kuulizia kama bado anamsubiri stesheni wakati huo saa nzima ilikuwa imepita toka amuache pale na kumwambia aondoke baada ya nusu saa. Boimanda ndiye aliyemshauri mzee Kibwana apige simu polisi na kumuelekeza namba za kupiga.

    “Boimanda ni nani?” hili ndilo lilikuwa swali ambalo nilipaswa kulijibu kabla ya kuendelea na chochote kuhusiana na uchunguzi wangu.

    Tatizo lililokuwa mbele yangu ni ruhusa ya kujiingiza kikamilifu kwenye kazi hiyo. Angekuwepo mkuu ingekuwa rahisi sana kumweleza na kupata msaada wowote ambao ningeuhitaji, lakini nafasi yake ilikuwa inashikiliwa na kiumbe mmoja aitwaye Kazikanda Moluwi ambaye sifa yake kuu ni mgumu kuelewa hasa kitu ambacho hakiko kwenye orodha ya kazi anazotakiwa kuzifanya.

    Kazikanda Moluwi alijulikana zaidi kwa jina la KM, na kabla ya kushika nafasi ya mkuu alikuwa anatumika sana kwenye shughuli za kulazimisha mambo yafanyike kwa namna yeyote. Mtu huyu hutumia nguvu zaidi kuliko akili kwa kuwa akili yake ni ya ‘kushikiwa’.





    NILISHTUKA sana ila sikutaka kumuonyesha Mwajuma kuwa nimejali zile habari alizoniambia huku akionekana kuingiwa na hofu. Nilimvuta na kumkumbatia kwa nguvu nikimpiga busu kwenye paji la uso huku nikimpapasa mgongoni kisha nikamuachia na kuacha nafasi kati yetu.

    “Boimanda ni nani?” nilimuuliza kwa upole.

    “Hata mimi simfahamu vizuri, ila ndiye mratibu mkuu wa harakati zote zinazofanywa na mtandao huo. Ila kitu ambacho naweza kukuthibitishia ni kuwa Boimanda ni mtu hatari sana. Maneno yako uliyonieleza siku ile yalinichoma sana, toka siku ile nikawa nayatafakari, leo nikaona nikuite kwa vile hakuna anayejua kwa nimekuja kwenye hii kitchen party”

    “Ah achana na hizo habari” nilimjibu nikimkaribia kiasi cha kuhisi pumzi zake akiwa anahema.

    Kitendo hicho kilimfanya Mwajuma ashtuke na kuniangalia kama ambaye haamini anachoshuhudia. Nikauzungusha mkono wangu kiunoni mwake na kumkumbatia nikipeleka mdomo wangu kumnong’oneza jambo, kitendo kilichomfanya asisimkwe na mwili.

    Tatizo lililokuwa mbele yangu ni ruhusa ya kujiingiza kikamilifu kwenye kazi hiyo. Angekuwepo mkuu ingekuwa rahisi sana kumweleza na kupata msaada wowote ambao ningeuhitaji, lakini nafasi yake ilikuwa inashikiliwa na kiumbe mmoja aitwaye Kazikanda Moluwi ambaye sifa yake kuu ni mgumu kuelewa hasa kitu ambacho hakiko kwenye orodha ya kazi anazotakiwa kuzifanya.

    Kazikanda Moluwi alijulikana zaidi kwa jina la KM, na kabla ya kushika nafasi ya mkuu alikuwa anatumika sana kwenye shughuli za kulazimisha mambo yafanyike kwa namna yeyote. Mtu huyu hutumia nguvu zaidi kuliko akili kwa kuwa akili yake ni ya ‘kushikiwa’.

    Wakati nikitafakari namna ya kuiingia kazi hiyo, muda wa Tausi kurudi nchini uliwadia. Nikaenda kumpokea uwanja wa ndege nikiwa na shauku na hamu ya mahaba ya mke wangu.

    Nilipoona tu mfumo wa ulinzi pale uwanja wa ndege nikajua kuna mchezo unaotaka kuchezwa. Kwa haraka nikawasiliana na mtu ninayemuamini katika kikosi cha ulinzi wa viwanja vya ndege na baada ya nusu saa maaskari wote waliokuwa zamu walibadilishwa kwa dharura.

    Hadi wakati ndege iliyomleta Tausi ikiwasili, tayari kulikuwa na askari wapya tofauti na waliokuwa zamu tena waliongozwa na huyo mtu niliyemwamini na kulikuwa na pilika za hapa na pale kwa baadhi ya wapokeaji katika uwanja huo wa ndege.

    Abiria wote waliteremka akiwemo Tausi ambaye nilimpokea kwa furaha na mapenzi makubwa, nikawa namzubaisha ili nihakikishe abiria wote wameteremka kwenye ile ndege. Baada ya abiria kuwa kama wameisha, aliteremka msichana mrembo sana ila mwili wake unaonekana fika kuwa umetengenezwa kimazoezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikamwangalia yule askari niliyemuamini, naye akajua namaanisha nini. Mimi nikaondoka na mpenzi wangu huku nikipanga kichwani namna ya kuburudika naye usiku huo. Laiti kama angejua mawazo niliyokuwa nayo kichwani angeona kweli ameolewa na mume ‘mcharuko’ kwa maana nilikuwa najitengeneza kisaikolojia.

    Usiku huo ilikuwa kama ndiyo mara ya kwanza kumuona Tausi. Unajua uzuri wa kuoa mwanamke mrembo? Hata ikifikia wakati maisha yamewapelekea kuchokana, unajikuta ukimtamani tu kwa jinsi alivyo. Sasa hebu fikiria mke wangu ni mrembo halafu penzi ndiyo kwanza limenoga, unajihisi kama upotelee humo humo.

    Kwenye vyombo vya habari katika siku iliyofuatia ilitawala habari za yule dada kuwa amekamatwa na shehena kubwa ya dawa za kulevya, Tausi alistaajabu sana kwa kua walikuwa wamepanda ndege moja. Moyoni nilijisifu kwa kazi nzuri niliyoifanya.

    Baada ya siku tatu toka nilipompokea Tausi, nilipigiwa simu iliyonishtua sana. Ilikuwa yapata saa saba za usiku niliposhtushwa na mlio wa simu yangu ya kiganjani. Kuangalia ikawa inaonyesha jina la Mwajuma, nikageuka kumwangalia Tausi ambaye naye alikuwa ameshtushwa na mlio wa simu hiyo kisha nikarudi kuiangalia simu hiyo.

    “Pokea mpenzi” aliniambia Tausi akiwa kwenye hali ya usingizi

    “Haloo!” Mwanamme nikajikaza kuipokea simu huku nikihisi jasho linanivuja.

    “Nifuate haraka niko kwenye kitchen party Kijitonyama” aliniambia akimalizia kwa kutaja jina la ukumbi.

    “Unajua unaongea na nani?” nilijikakamua kuuliza lakini ukweli ni kwamba kijasho kilikuwa kikinitoka.

    “Najua, wewe ni Musa au Nasibu na naamini utakuwa umelala na mkeo. Kuna jambo la muhimu sana kwako” aliongea Mwajuma na kukata simu.

    Nikageuka kumwangalia Tausi nisijue la kumwambia ila yeye alijua cha kuniambia.

    “Naijua kazi yako mpenzi na nakuamini, nenda tu kama utaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo” aliniambia Tausi kwa utulivu.

    Wakati najiandaa kwenda aliponielekeza Mwajuma, mambo mengi yalikuwayakipita kichwani mwangu nikijaribu kutabiri kitakachojiri huku nikijaribu kupanga na kupangua hatua za kufanya kukabiliana nacho. Sikuwa na mashaka na Mwajuma ila hao walioko nyuma yake ndio walikuwa wananipa mashaka.

    Baada ya muda mchache nilikuwa aliponielekeza Mwajuma na kweli nilimkuta pale, sikujua kama alifanya makusudi kunitega au ndivyo alivyotakiwa kuvaa kwenye ile kitchen party, alivaa kigauni kifupi cha khanga, viatu vya chini na nywele zake alizitengeneza kirahisi mno. Japo alionekana simpo lakini alikuwa amependeza sana.

    Nilipomfikia sikutaka kuonyesha kama niliutilia mashaka wito wake, nikamshika mkono na kumvutia kwenye kisehemu chenye giza giza karibu na maegesho ya magari katika ukumbi huo kasha nikauzungusha mkono wangu kwenye kiuno chake na kumvuia kwangu ikawa kama kajibinua. Nikawa namtazama usoni kama ninayeomba ridhaa ya kumpiga busu.

    “Mke wako ana moyo sana, mimi nisingeweza” alianza kuniambia akionyesha kawivu kwa mbali

    “Anajiamini” nilimtupia kijembe Mwajuma.

    “Niambie kweli Musa, we unafanya kazi gani?” nilisisimkwa kwa swali la Mwajuma, nikajua kuna habari nzito nyuma ya swali hilo.

    “Kazi yangu unaijua Mwajuma, kuna nini?”

    “Nimekudanganya mengi Musa,ukweli ni kuwa katika maisha yangu siamini katika mapenzi. Sijawahi kukupenda kabla, nilikuwa na wewe kwa kuwa ilibidi iwe hivyo japo nikiri kuwa uliweza kunifanya niyafurahie mapenzi kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Muda wote tuliopoteana nilikuwa nakukumbuka sana hasa nilipokuwa na hamu ya mwanamme” alianza kujieleza Mwajuma huku nikiwa bado nimemshika kiunoni.

    Nilibaki nikimtazama usoni Mwajuma nikitafakari maneno yake yaliyokuwa kama kisu kinachoukata moyo wangu. Sikuwahi kudhani kuwa kuna mwanamke ambaye angeweza kufanya yote aliyokuwa akiyafanya Mwajuma bila ya kuwa na chembe ya mapenzi moyoni mwake.

    “Ina maana urembo wote wa Mwajuma ni kama mashine tu isiyokuwa na moyo ndani yake” nilijikuta nikijisemea moyoni nikikumbuka vitabu mbalimbali nilivyowahi kuvisoma kuhusu mahusiano ya kimapenzi upande wa mwanamke. Hadi wakati huo, nilichokuwa nikikijua mimi ni kuwa penzi la mwanamke hujengeka taratibu na likishakolea limekolea kwani kulitoa huchukua muda mrefu zaidi.

    Nilijikuta nikiutoa mkono wangu kiunoni mwa Mwajuma na kumfanya atabasamu kwa huzuni kisha akashusha pumzi ndefu.

    “Mimi ni askari Musa, na najua kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa na wewe ni askari lakini wa kiwango cha juu kwa kuwa muda wote niliokuwa na wewe nilishindwa kujua chochote kuhusu kazi yako ya uaskari” Mwajuma alinieleza maneno mazito ambayo yalinifanya nijihisi kutetemeka.

    “Kwanini umeamua kuniambia maneno hayo yote?” nilijikakamua kumuuliza

    “Nahisi uko hatarini kutokana na mambo unayoyafanya kuuingilia mtandao, kuna mtandao wa baadhi ya viongozi walioko madarakani unaojilimbikizia mali kwa njia haramu na halali ili uweze kuwa na nguvu kwenye uchaguzi ujao na kuchukua kiti cha urais” Mwajuma aliongea akiushika mkono wangu na kuukumbatia.

    “Kuna baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi wanatumiwa na wanasiasa hao kwa kuwa waliingia madarakani kwa nguvu za hao wanasiasa, ila wenzangu na miye tunapewa tu amri na kazi za kufanya. Kwa kweli mimi nimechoka, niko tayari kushirikiana na wewe ili tuokoe nchi yetu. Tunakoelekea ni kubaya sana” Mwajuma aliongea maneno mazito sana kiasi cha kunifanya nikaribie kupoteza ujasiri wangu.

    “Kwanini ulitumwa kunifuatilia na nani aliyekutuma?” nilimuuliza Mwajuma

    “Hayo siyo ya umuhimu kwa sasa, ila cha muhimu ni kwamba matukio mengi ya ujambazi yanakuwa yamepangwa na biashara nyingi haramu zinajulikana na zina mikono ya baadhi ya wakubwa na zina lengo la kukusanya nguvu kwa ajili ya uchaguzi mkuu hivyo wewe unaonekana kikwazo na usipoangalia utapotezwa” aliniambia Mwajuma akionekana mwenye uhakika na anachokisema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog