Simulizi : Mikono Michafu
Sehemu Ya Tatu (3)
Nilijikuta nikiutoa mkono wangu kiunoni mwa Mwajuma na kumfanya atabasamu kwa huzuni kisha akashusha pumzi ndefu.
“Mimi ni askari Musa, na najua kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa na wewe ni askari lakini wa kiwango cha juu kwa kuwa muda wote niliokuwa na wewe nilishindwa kujua chochote kuhusu kazi yako ya uaskari” Mwajuma alinieleza maneno mazito ambayo yalinifanya nijihisi kutetemeka.
“Kwanini umeamua kuniambia maneno hayo yote?” nilijikakamua kumuuliza
“Nahisi uko hatarini kutokana na mambo unayoyafanya kuuingilia mtandao, kuna mtandao wa baadhi ya viongozi walioko madarakani unaojilimbikizia mali kwa njia haramu na halali ili uweze kuwa na nguvu kwenye uchaguzi ujao na kuchukua kiti cha urais” Mwajuma aliongea akiushika mkono wangu na kuukumbatia.
“Kuna baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi wanatumiwa na wanasiasa hao kwa kuwa waliingia madarakani kwa nguvu za hao wanasiasa, ila wenzangu na miye tunapewa tu amri na kazi za kufanya. Kwa kweli mimi nimechoka, niko tayari kushirikiana na wewe ili tuokoe nchi yetu. Tunakoelekea ni kubaya sana” Mwajuma aliongea maneno mazito sana kiasi cha kunifanya nikaribie kupoteza ujasiri wangu.
“Kwanini ulitumwa kunifuatilia na nani aliyekutuma?” nilimuuliza Mwajuma
“Hayo siyo ya umuhimu kwa sasa, ila cha muhimu ni kwamba matukio mengi ya ujambazi yanakuwa yamepangwa na biashara nyingi haramu zinajulikana na zina mikono ya baadhi ya wakubwa na zina lengo la kukusanya nguvu kwa ajili ya uchaguzi mkuu hivyo wewe unaonekana kikwazo na usipoangalia utapotezwa” aliniambia Mwajuma akionekana mwenye uhakika na anachokisema.
Nilishtuka sana ila sikutaka kumuonyesha Mwajuma kuwa nimejali zile habari alizoniambia huku akionekana kuingiwa na hofu. Nilimvuta na kumkumbatia kwa nguvu nikimpiga busu kwenye paji la uso huku nikimpapasa mgongoni kisha nikamuachia na kuacha nafasi kati yetu.
“Boimanda ni nani?” nilimuuliza kwa upole.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hata mimi simfahamu vizuri, ila ndiye mratibu mkuu wa harakati zote zinazofanywa na mtandao huo. Ila kitu ambacho naweza kukuthibitishia ni kuwa Boimanda ni mtu hatari sana. Maneno yako uliyonieleza siku ile yalinichoma sana, toka siku ile nikawa nayatafakari, leo nikaona nikuite kwa vile hakuna anayejua kwa nimekuja kwenye hii kitchen party”
“Ah achana na hizo habari” nilimjibu nikimkaribia kiasi cha kuhisi pumzi zake akiwa anahema.
Kitendo hicho kilimfanya Mwajuma ashtuke na kuniangalia kama ambaye haamini anachoshuhudia. Nikauzungusha mkono wangu kiunoni mwake na kumkumbatia nikipeleka mdomo wangu kumnong’oneza jambo, kitendo kilichomfanya asisimkwe na mwili.
“Umeniamsha hisia za mapenzi juu yako, najihisi kukupenda kama vile mwanzo japo umekiri tofauti” nilimnong’oneza maneno hayo nikawa nahisi mikono yake ikinipapasa mgongoni mwangu.
Nikamwangalia usoni huku nikiwa bado nimemkumbatia, Mwajuma alikuwa anaonekana kuhitaji jambo ambalo nililijua wazi. Nikampelekea mdomo na kumpiga busu zito la mdomoni, akauacha wazi mdomo wake kuuruhusu ulimi wangu upenye. Tukanyonyana ndimi kwa muda kabla ya kukatishwa na taa za gari lililokuwa likitoka katika maegesho.
“Bado busu lako ni tamu vile vile” nilimwambia Mwajuma na kusababisha atabasamu.
“Hujaacha tu mambo yako?” aliniambia kwa aibu.
“Twende nikupeleke nyumbani mpenzi” nilimwambia nikimvutia nilipoliacha gari.
Tulipofika nyumbani kwa kina Mwajuma, aliteremka akawa anaelekea mlangoni na mimi nikateremka na kumuwahi. Nikamvuta tukaanza tena kubusiana huku tukipapasana kabla ya jambo lililonitia mashaka kutokea. Tulimulikwa tena na taa za gari, hili la sasa hivi lilikuwa linapita. Nikahisi kuwa kuna kitu hakiko sawa ila sikujua ni nini.
“Ntakutafuta kesho kwa namna ntakayoijua mimi kisha tutaongea vizuri zaidi na kuona kuwa tutawezaje kufanya kazi pamoja” nilimwambia maneno ambayo kwa mwenye kutafakari angejua moja kwa moja kuwa nimekiri kuwa mimi ni askari.
Baada ya kuagana na Mwajuma nikarudi kwa Tausi wangu nikiwa nimejipa jukumu la kumjua Boimanda kupitia Mwajuma.
Nilifika nyumbani na kumkuta Tausi wangu yuko macho akiwa amejilaza kitandani kajikunyata, alionekana kuwa alipatwa na hofu sana kwa kitendo cha mimi kuitwa usiku ule. Moyo uliniuma sana nilipokumbuka namna nilivyombusu Mwajuma. Niliapa kuwa haitatokea tena nifanye jambo kama lile na hata kwa kumjua Boimanda ntatumia njia nyingine badala ya kumuweka karibu Mwajuma.
Nilimkumbatia Tausi wangu, nikamuona akijiachia na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Kuna kazi italazimika niifanye kwa haraka” nilianza kujiongelesha nitafute pozi la kumhadithia kilichojiri ambacho kwa uhakika ningemficha ufisadi nilioufanya.
“Umefikiriaje wazo langu?” aliniuliza swali ambalo sikulitarajia kwa muda ule.
Tausi aliniambia kuwa angefurahi kama ningeacha kazi na kujihusisha na biashara ili niepukane na maisha ya hatari ninayoishi kutokana na kazi ninayoifanya. Kimsingi nilimkubalia kuwa wazo lake ni zuri ila utekelezaji wake unahitaji umakini wa hali ya juu ili nisije kujiingiza katika hatari zaidi kwa kuwa mengi nimeyaona na kuyajua, siwezi kondoka kirahisi.
“Nishaanza kulifanyia kazi wazo lako mpenzi” nilimjibu huku nikimkumbatia kwa nguvu zaidi na kummiminia mabusu kadhaa kabla hatujaishia katika usingizi ambao ulitupeleka hadi saa tatu asubuhi.
Kitu cha kwanza baada ya kuamka tu niliwatuma watu wangu wakamcheki Mwajuma na kufuatilia mienendo yake yote kwa masaa 24 kisha wakijiridhisha kwa vitu maalum ambavyo niliwaagiza waviangalie, wamchukue na kumpeleka sehemu ambapo ningekutana naye kwa mahojiano zaidi juu ya habari alizonipa.
“Nimekwisha” niliongea mwenyewe baada ya kuwaza ‘kitakavyonuka’ endapo Tausi akiziona. Nikawa nazichambua moja baada ya nyingine, kikadondoka kikaratasi. Nikakiokota haraka na kukisoma.
‘Ukionyesha ushirikiano, Tausi hataziona na polisi hazitafika. Njoo ufukweni na usiwasiliane na yeyote. Kumbuka hapo ulipo tunakuona!’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jasho jembamba lilianza kunitoka. Sikuwa nahofia kuuawa kwa kuwa kama nia yao ingekuwa hiyo, badala ya kunipiga picha wangenipiga risasi. Halafu ukiona mtu anajitahidi kutafuta mambo ambayo yatakutisha ujue anakuogopa. Niliamini kuwa ni watu wanaonifahamu fika ila ukweli ni kwamba wamenishika pabaya.
Baada ya masaa machache nilipokea habari ambayo ilinishtua sana. Mwajuma alikutwa ameuawa chumbani kwake na watu wasiojulikana na polisi walikuwa katika uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo. Akili yangu ilisimama kwa muda kufanya kazi, nilijikuta natokwa na machozi bila kujijua. Nikawahi kutoka nje na kukimbilia ufukweni ili Tausi asije kushtuka.
Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwepo, majirani zake wanadai alirudishwa usiku sana na gari, baada ya muda gari hilo likarudi tena. Zikasikika purukushani za hapa na pale kisha kukawa kimya, wao wakajua ni mambo ya mapenzi tu, asubuhi wakashtuka kukuta damu zikichuruzika toka chumbani kwake ndipo wakatoa taarifa polisi.
Kwa kweli nina muda mrefu sana sikuwa nimelia lakini siku ile nilijikuta nikilia kama mtoto mdogo, nililia haswa pale ufukweni. Niliwaza mambo mengi sana kuhusiana na Mwajuma, nilitamani kama kungekuwa na mtu wa kumhadithia kuhusu nilichojihisi kutokana na kifo cha Mwajuma.
Kutwa nzima nilijitahidi kumficha Tausi lakini mwisho ilibidi nimwambie kuwa yule dada aliyenipigia simu kunipataarifa muhimu amekutwa ameuawa muda mfupi baada ya kuongea naye. Sikuweza kumwelezea kiundani kuhusu uhusiano wangu na Mwajuma lakini alihisi kuwa msiba ule ulinigusa sana. Tukalala na majonzi, sikuthubutu kwenda msibani japo ndiyo ingekuwa fursa ya kuwajua wazazi halisi wa Mwajuma.
Baada ya siku mbili, walisafirisha mwili wa Mwajuma kwenda Mwanza kwa ajili ya mazishi na kama zilivyo taratibu za kiislamu hakuna aliyeuona mwili wa Mwajuma kwa kuwa ni watu maalum waliuandaa.
Kama ilivyo kawaida yangu huwa ninaanza mazoezi mapema sana na kumaliza wakati jua linaanza kutoa mwanga hivyo baada ya mapumziko ya siku tatu ya msiba niliamka kama kawaida na kutoka nje kwa ajili ya mazoezi. Nilishtuka kuona bahasha ya khaki imelala karibu kabisa na mlango wangu. Nikaanza kuangaza huku na kule bila kuona dalili zozote za mtu.
Nikaiokota kwa tahadhari na kuifungua. Kilichomo kilinifanya nitake kuzimia, ni picha zangu nikibusiana na Mwajuma pale nje ya ukumbi na kule nyumbani kwao. Kumbe wasiwasi wangu nilipomulikwa na taa za gari mara mbili haukuwa wa bure.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimekwisha” niliongea mwenyewe baada ya kuwaza ‘kitakavyonuka’ endapo Tausi akiziona. Nikawa nazichambua moja baada ya nyingine, kikadondoka kikaratasi. Nikakiokota haraka na kukisoma.
‘Ukionyesha ushirikiano, Tausi hataziona na polisi hazitafika. Njoo ufukweni na usiwasiliane na yeyote. Kumbuka hapo ulipo tunakuona!’
Jasho jembamba lilianza kunitoka. Sikuwa nahofia kuuawa kwa kuwa kama nia yao ingekuwa hiyo, badala ya kunipiga picha wangenipiga risasi. Halafu ukiona mtu anajitahidi kutafuta mambo ambayo yatakutisha ujue anakuogopa. Niliamini kuwa ni watu wanaonifahamu fika ila ukweli ni kwamba wamenishika pabaya.
Nikaanza kutembea pole pole kuelekea ufukweni nikiwa na mawazo mengi kichwani, ila nilikuwa sina wasiwasi kutokana na utaratibu wangu wa kiusalama niliojiwekea. Kutembea kwangu pole pole ilikuwa ni kuvuta muda zitimie dakika tano.
Wakati nakaribia ufukweni, nilimuona mtu mmoja aliyesimama ufukweni hapo akimulikwa na mwanga wa mbalamwezi. Nilikuwa na uhakika kwamba hakuwa peke yake pale ila aliyekuwa anaonekana ni yeye tu.
“Musa Njiwa! Naamini hatutapata tabu ya kushirikiana na wewe kwa kuwa hutakuwa tayari kumpoteza Tausi wakati huo huo kushitakiwa kwa kesi ya mauaji” aliongea bwege yule akionekana kujiamini sana.
“Hakuna haja ya kunielezea jambo ambalo nalijua na wewe unalijua, nenda moja kwa moja kwenye jambo uliloniitia. Mnataka nini toka kwangu?” nilimjibu kwa kujiamini kwa kuwa ilikuwa imebakia dakika moja tu zitimie dakika tano za wao kujidai katika eneo langu. Pia nilimkatiza kuendelea kutoa historia kwa kuwa saa niliyoivaa huwa inarusha mawimbi ya sauti yanayonaswa kwenye mashine ya kurekodia sauti iliyoko ndani yangu.
Kutokana na kazi ambazo nimezifanya niliwekewa aina fulani ya ulinzi ili nisidhurike. Huwa nikiamka kwa mazoezi kuna vitu fulani huwa navifanya kumjulisha Tausi kuwa kila kitu kiko sawa.
Asiposikia chochote kutoka kwangu kwa muda wa dakika tatu kuna namba alizotakiwa kubonyeza na ndani ya dakika mbili au tatu tayari kikosi kinakuwa kimewasili. Endapo angeona kimya kinaendelea, kuna mtandao wetu wa siri aliotakiwa kuujulisha baada ya dakika nyingine tano.
“Tuko kwa ajili ya maslahi ya taifa na wananchi wote wa Tanzania kwa jumla, na wewe tunakutambua kuwa ni kijana mwadilifu na mchapakazi. Ila mienendo yako kwa siku chache hizi inatupa mashaka” aliongea kwa majivuno.
Wakati huo nilikuwa nikijihisi kutetemeka na ujasiri wangu wote ulianza kuyeyuka. Sio kwa sababu ya maneno aliyoniambia bali muda ambao tayari ningekuwa nimeokolewa toka mikononi mwa ile mijamaa. Hali hiyo ilinifanya nijue kuwa wale watu hawakuwa wa kawaida, walikuwa na nguvu kubwa.
“Ongea moja kwa moja, mnataka nini?” pamoja na wasiwasi ulioanza kuniingia nilijikuta nikimuuliza kwa hasira. Kwa kawaida huwa nachukia sana kufanya maongezi na watu ambao wanazunguka zunguka katika kuongea.
“Safi! Tunataka utuambie ni kazi gani unayoifanya sasa hivi na ni nani aliyekutuma?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sifanyi kazi yeyote, kwa hiyo hakuna aliyenituma” nilimjibu kwa kifupi bila kujifikiria
“Nadhani hujui unaongea na watu wa aina gani katika nchi hii”aliongea kwa majivuno mjinga yule.
“Napata shida ya kujua uwezo wenu katika nchi hii kwa sababu kama mngekuwa na uwezo mnaodhani mnao, usingeniuliza kuwa nafanya kazi gani na nimetumwa na nani, mngekuwa mnajua kuwa sifanyi kazi yeyote kwa muda huu na msingesumbuka kunitafutia vitu vya kunishinikiza” niliendelea kumjibu jeuri ili nimtie hasira afunguke.
Jamaa lilikaa kimya kwa muda kisha likajikohoza kusafisha koo lake, nikajua nishamkamata kwenye eneo nnalomtaka.
“Sikia kijana, tunajua unachunguza mienendo kadhaa ambayo kimsingi haikuhusu na hakuna agizo lolote ulilopewa kiofisi kufanya kazi hiyo, unahatarisha usalama wa taifa bila kujijua. Tumekuita kukufahamisha kuwa tunajua unachofanya na tuna uwezo wa kukushughulikia” aliongea jamaa yule kwa sauti iliyojaa chuki.
“Kitu ambacho napenda kukuthibitishia ni kuwa, sina lolote ninalotafuta, ila kubwa zaidi ninalotaka kukuthibitishia ni kuwa hamna uwezo mnaodhani mnao. Kwanza mna mbinu za kizamani za kutaka kubambikia watu kesi wakati iku hizi kuna kila aina ya teknolojia inayoweza kubainisha ukweli na mnajua wazi nna uwezo wa kuzitumia” nilimjibu kwa jeuri vile kwa kuwa nilishaona ishara za kuwasili watu wa mtandao wangu.
Jamaa akawa anaangaza huku na kule akitweta kwa hasira kisha akatoa amri kwa kujiamini, “hebu mchukueni huyu tukashughulikie”.
“Kamshughulikie baba ‘ako mzazi aliyeko shamba” nilimjibu kwa dhihaka.
Ukapita ukimya bila yeyote kujibu wala kuchukua hatua yeyote. Nikamuona jamaa akipoteza ujasiri, ikawa zamu yangu kucheza naye.
“Wenzako wote tayari wako mikononi mwa wananchi wenye hasira kali na hivi sasa wanaweza kuwa tayari washauawa, umebaki peke yako. Umeamini kuwa waliokutuma hawana nguvu wanayodhani wanayo?” Nilimwambia kwa kujiamini ila kimsingi nilikuwa natoa maagizo kwa mtandao wangu juu ya hukumu ya wale wenzake.
Nikaanza kumsogelea huku yeye akirudi nyuma kwa woga, nikawa nazidi kumfuata kwa kuwa nilishamuona mmoja wa watu wangu akiwa kasimama kwa nyuma yake. Nikatisha kama nataka kumfukuza, akageuka kutaka akimbie, akajikuta yuko uso kwa uso na Jerome Masola.
“Kaa chini mbwa we” aliamrisha Jerome.
Jamaa lilikaa chini utafikiri limepigwa virungu vya magoti.
Nikamuagiza Jerome amchukue yule ‘boya’ pamoja na picha zangu na Mwajuma wakamhoji sehemu yetu maalum kwa kuwa nilijua kuwa muda si mrefu watu kutoka ofisini wangekuja. Jerome akamchukua kutaka kutokomea naye wenzetu walipojipanga wakiwa na wale wengine waliokamatwa kabla.
Baada ya takribani dakika arobaini tangu mtandao wangu usafishe hali iliyotokea ndipo walikuja watu waliotumwa na idara ya usalama Taifa wakiwa na silaha, eti kuitikiwa wito wa hatari. Kwa kweli bila ya kuwa na malengo maalum, ningewatukana matusi ya nguoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hatukuwa na tatizo lolote na hakuna aliyetoa taarifa yeyote, labda mmepokea taarifa toka kwa mtu mwingine” niliwaeleza huku nikijifanya niko katika hali ya usingizi.
Wakajizungusha zungusha pale wakishindwa kuendelea kuniuliza chochote. Nadhani walikuwa wameshapewa majibu ya kunipa wakawa wanatafuta namna ya kunipa ila sikuwapa nafasi ya kuniambia upuuzi wao.
Lakini pia kikubwa nilikuwa najaribu kuwapa ujumbe kuwa na mimi ni mtu wa aina gani. Chezea mimi wewe?
Tukio la kuvamiwa nyumbani kwangu niliendelea kulikalia kimya, sikulitolea taarifa yeyote ofisini wala sikuilamu ofisi kwa kutochukua hatua ndani ya muda uliotakiwa ila tukio hilo na maneno ya yule lofa vilinipa ujumbe kuwa siko salama tena na ofisi inashiriki kwa namna moja au nyingine kwenda kinyume na mimi.
“Mi nadhani mtuache tupumzike na nyinyi mkaendelee kutafuta huyo mwenye matatizo” niliwaambia kuwafukuza kimtindo huku nikiingia ndani ya nyumba yangu na kufunga milango nikiwaacha wamechanganyikiwa wasijue mpango wao unaendaje au umeishia wapi.
Kutokana na aina ya kazi tunazozifanya na hatari inayotukabili kulingana na uadui tuliyojijengea, kuna baadhi yetu tunaoaminiana tulianzisha mtandao mdogo wa kulindana nje na utaratibu wa kiofisi. Na ndiyo uliniokoa siku hiyo mikononi mwa wanaojiita wanalinda maslahi ya taifa.
Siku hiyo kwenye taarifa za habari za usiku huo zikatangazwa habari kuwa majambazi sita wameuawa na wananchi wenye hasira kali maeneo ya Mbagala Majimatitu usiku wa kuamkia siku hiyo na polisi wanaendelea na uchunguzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment