Simulizi : Niache Na Moyo Wangu
Sehemu Ya Pili (2)
Ilipoishia…
Gongo la kutembelea vizuri kwakuwa alikuwa na mguu mmoja. Alimbeba yule mtoto bengani akiwa ndani ya lile begi nakuanza safari yake uku mkono mmoja akiwa ameshikilia kidumu cha maji nakutokomea zake kusikojulikana.
Songa nayo sasa…CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Levina hakulijali baridi la msitu wa Kakamega kwani ndani ya masaa machache aliyokuwepo alikuwa tayari ameshalizoea. Msitu wa Kakamega ulikuwa ukitisha kwa milio ya ajabu ya wanyama na ndege wa porini lakini kwa Levina masikio na moyo wake ulishajijenga kikakamavu. Ushupavu! Hakuogopa kitu maishani mwake.Aliona bora afe kishujaa. Alikuwa ameshajitolea kwa lolote litakalomkuta mbele yake yamkini alikuwa na mguu mmoja. Mguu mmoja uliokuwa ukisaidiwa kujikongoja kwa kutumia gongo na mgongoni akiwa amembebelea mtoto mdogo kwenye kabegi alikoachiwa na Osusu. Baada ya kuweza kujisogeza kamwendo kidogo Levina akajihisi kuchoka sana. Akakaa mpaka chini kwa uchovu uku yule mtoto akimshusha mpaka chini kutokea begani. Akamchungulia, alikuwa tayari ameshapitiwa na usingizi mkali. Levina alionesha tabasamu uku vidole vyake akivitumia kumpapasa yule mtoto usoni mwake.
“Mtoto mzuri” Alijisemea Levina kwa sauti ya chini chini.
Hakutaka kupoteza muda hata kidogo kwani aliamini kabisa kuchelewa kupumzika kwake kunaweza kuwafanya kina Butiliasi wakamkuta hapo msituni. Na hivi walikuwa hawatabiriki aliona wanaweza hata wakamduru tena. Baada ya kupumzika kidogo alimchukua tena yule mtoto kama alivyofanya awali nakumdumbukiza kwenye kile kibegi kisha akamuweka begani na kuendelea na safari yake kwa kutumia msaada wa gongo upande mmoja.
*******
“Nawauliza tena bado mnataka kunifahamu?”
Si Butiliasi, Papii, Osusu wala wale mateka wote walikuwa hoi. Walikuwa wamepelekwa gwaride la kutosha na mzee mwenye kijiji. Mzee mwenye msitu, Mzee wa siku nyingi katika msitu wa Kakamega, Aguati mwana wa thorong’ong’o.
“Kama kweli wewe ipo mwanaume, ebu batokelezee tukueneshe? Kata utum mmbo,tupilia m mmbali!” Alisema Butiliasi kwa hasira na kigugumizi cha muda.
Aguati alichowafanyia safari hii alitokea hadharani. Wote wakamshangaa kwa jinsi alivyo na ngozi nyeupe sana. Nywele ndefu kutokea masikioni. Na nyusi zilizokuwa zimejawa na mvi nyeupe na nyeusi.
“Mmeniona?” Alinenea Aguati.
“Ndio” Butiliasi alijibu kwa kujiamini. Alikuwa kama mwanaume aliyelishwa pilpili kali mdomoni mwake. Alishajitolea kwa lolote liwe ili mradi aweze kumuua kiongozi wao mkuu. Kiongozi wanayemtegemea na kumtukuza wana Kakamega.
Alichowafanyia Aguati. Alinyoosha mikono yake miwili nakuielekeza eneo walipokuwa kina Butiliasi na wenzake. Kisha ile mikono akafanya ishara kama anataka kunawa. Wale kina Butiliasi wote wakabaki kama wakikumbatiana. Wakakunjamana! Wakagusana kila mmoja kwa kushikana mikono. Wote wakawa kitu kimoja. Baada ya hapo Aguati akawaburuza kwa kutumia ishara ya mikono. Wote wakajikuta wakitambaa kutokea nje. Hawakuweza kujinasua hata mara moja. Aguati akawa mstari wa nyuma uku wale kina Butiliasi wakiwa mbele yake akiwasukuma kimiujiza kutoka nje kwa kutumia ile ile ishara ya mikono yake. Kwa mara ya kwanza Butiliasi aliweza kutoa mchozi wa kuumia uku Papii na Osusu nao wakiyapokea maumivu kwa kutoa machozi ya kimya kimya. Mzee Aguati aliendelea kuwaburuta kuelekea msituni uku wakiwapitia baadhi ya wanakijiji wenzake ambao walikuwa wameshauliwa na Butiliasi kwa risasi kali. Butiliasi alishajua wazi wanapopelekwa lakini hakuwa na nguvu ya kufanya vyovyote zaidi ya kutoa tu sauti.
“Aguati? Aguati?” Aliita Butiliasi kwa sauti ya juu .
Aguati akashusha mikono yake miwili. Kina Butiliasi wakampumzika uku wakihema hoi kwa kupelekewa mchakamchaka. Wale mateka ni kama walikuwa na kizunguzungu cha muda kwani kitendo cha Aguati kushusha mikono walijikuta wote wakidondoka mpaka chini nakuanza kugalagala mithili ya mtu anayeugua ugonjwa wa kifafa.
“Mnasemaje?” Aguati alihoji.
“Unatupeleka wapi wewe muzee?” Aliongea Butiliasi kwa kujiamini.
“Nawapelekeani kwa mungu, baba yangu. Baba amekasirika sana. Hawapendi! Tangu mmekuja uku nakuua ovyo amechukia sana sasa ni bora akawahukumu yeye mwenyewe.”
“mungu gani?” Aliendelea kuhoji Butiliasi uku akili yake yote akijua wazi wanapopelekwa.
“Shimoni, kwenye jiwe la kafara. Wacha baba yangu akawahukumu” Alimaliza kuongea Aguati kisha akafanya kama alivyokuwa akiwafanya awali. Aliinyanyua mikono yake miwili nakuweza kuwainua kwa kutumia ishara ya mikono kisha safari ya kuwapeleka ikaendelea. Butiliasi alipajua sahawia kwenye shimo la kutolea kafara. Lile shimo ambalo alimsukuma kiongozi mmoja wapo waliyekuwa wakimuita Otieno. Alikumbuka pia walivyotupwa waasi wenzake pamoja na mateka wote aliokuwa nao akiwalinda kwa muda mrefu sana toka Congo,Burundi,Rwana na Uganda.
“Imeshakuwa muvita hii wacha tufe kwa muvita!” Alinena Butiliasi kimoyo moyo.
Safari ya kupelekwa kwenye jiwe la kutolea kafara haikuwa ndefu sana. Baada ya dakika kadha walikuwa tayari tena juu ya lile jiwe uku Aguati akiwa pembeni yao. Wote walikuwa wakitetemeka mithili ya kifaranga cha kuku kikinyeshewa mvua ama kumwagiwa na maji. Si Papii wala Osusu wote suruali zao zilikuwa zimejawa na haja ndogo. Aguati alianza kwa kuwachukuwa wale mateka wote.
“mungu yangu, wachukue hao ni zawadi kutoka kwangu!!” Aliongea Aguati uku akiwadumbukiza wale mateka wote waliokuwa bado na kamba mikononi mwao.Aguati akawadumbukiza. Shimo likawameza! Wakabaki watatu,Osusu,Papii na Butiliasi.
“Tubadilishie adhabu tafadhali” Papii aliropoka.
Butiliasi alikasirishwa na kauli ya mwenzake,Papii kujishusha mbele ya Aguati na mungu wao. Alichiokifanya,kwa hasira alimsukuma Papii kwenye shimo la kutolea kafara. Aguati akatoa meno kwa kucheka na mungu wao akajibu kwa kutoa sauti kali kutoka ndani ya lile shimo. Papii akawa amemezwa rasmi na mungu wa Kakamega. Wakabaki wawili Osusu na Butiliasi.
“Aingiie mmoja hapo shimoni mungu anamtaka?” Aliongea Aguati uku akiwa amekalia jiwe pembeni ya shimo la kutolea kafara.
Butiliasi akaanza kusukumiana na Osusu kuingia mule ndani ya lile shimo. Wote walikuwa waoga. Waasi wakusalitiana wenyewe kwa wenyewe. Walijiona ni bora wakakamatwa na wanajeshi wa nchi ama umoja wa mataifa kuliko kuwa hatiani na Aguati katika shimo lao la kutolea kafara. Walivutana muda mrefu bila hata ya mmoja kulisogelea lile shimo. Aguati akapata hasira sana kwa kutokwenda hata mmoja ikabidi awasogelee mpaka karibu. Kitendo cha kuwafikia karibu kina Osusu na Butilialsi pale pale wakatumia mwanya wakumgusa rasmi Aguati na kumsukuma. Aguati akajikwaa na kudondoka mpaka kwenye shimo la kutolea kafara. Kilichofuata hapo ni makelele yasio ya kawaida. Kijiji chote cha Kakamega kikalipukwa na kelele za ajabu. Mwanga mkali ukatoka mbele yao. Kisha kilichofuata ni kitu mithili ya radi kikaruka juu kabisa kutokea katika lile shimo na kupaa juu kabisa na kiliposhuka kilishuka karibu yao nakujitandaza. Kilikuwa ni kitu cha ajabu sana kisicho na mbele wala nyuma. Kilikuwa mnyama si mnyama na hata binadamu si binadamu. Osusu na Butiliasi wakaanza kurudi kinyume nyume wakiiogopa kile kiumbe cha ajabu. Kilikuwa na nguvu ya ajabu sana. Kikainuka na kuanza kuchomoza mikono yake mingi sana. Kikawa pweza si pweza wala ng’e si ng’e.
“Mvrrooooo, Mvroooo!!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakikuweza kutoa sauti ya kueleweka zaidi ya mlio wa ajabu tena mlio kama wa pikipiki. Kikazunguka kwa nguvu zote nakusababisha eneo lote kuzungukwa na upepo mkali. Upepo usio wa kawaida. Osusu na Butiliasi wakawahi kuyashika mawe madogo kwa ajili ya kujizuia. Upepo ule ukawazidi nguvu. Wakapepea mpaka kukutana na miti chini kabisa. Wakakumbatia miti ndipo na ule upepo ukapungua nguvu. Wakaendelea kutolea macho kile kitu cha ajabu kilichokuwa kikiwapa adhabu.Kiliwaogopesha sana. Kilijizungusha tena hewani na safari hii kilipotua kilikuwa kikubwa zaidi na kuwa na vichwa vya watu wengi sana mwilini. Sura za watu mbali mbali ziliweza kuonekana sambamba na macho yao na midomo wakiikenua kwa kucheka. Butiliasi aliweza kuona sura za waasi wenzake. Machozi ya huruma yalimwingia. Moyo wake Ukalalama! lakini hakuwa na jinsi katika himaya ya watu. Alikuwa ni mtu wa kusubiri miujiza itokee. Baada ya kile kiumbe kujizungusha taratibu kwa muda. Kiliongoza mpaka kwenye shimo la kutolea kafara. Kukabaki kimya kabisa. Butiliasi aligeuza macho yake kumwangalia mwenzake Osusu lakini hakuweza kumuona. Akatetema kwa hofu! Woga ukamtawala upya. Macho akayatoa.
“Osusu, Osusu naacha mimi?” Aliita Butiliasi kwa sauti ya juu na ya masikitiko.
“Nipo mubosi yangu, nipo njoo?” Aliongea Osusu ambapo kwa uoga wake alikuwa amepanda juu ya mti kabisa na kujificha akiogopa. Butiliasi naye akataka kupanda juu ya mti ule lakini hakuweza kwakuwa mti ulikuwa ukiteleza sana. Hivyo akabaki akitolea macho eneo la shimo. Mvuke wa ajabu ukaaanza kutokea kwenye lile shimo. Ule mvuke ukapaa juu zaidi na uliposhuka ulitawala eneo lote la Kakamega. Miti yote ikaanza kupukutika majani yake. Mwanga wa ajabu ulioweza kugeuza usiku kuwa mchana. Hapakuwa na giza tena eneo lote lile. Kulikuwa kama kumeshapambazuka. Ukimya ulizidi kuwatetemesha Butiliasi na mwenzake Osusu. Muda wote hadi majani yakipukutika Osusu alikuwa akining’inia juu ya mti. Hakutaka hata kuteleza ama kuachia mti ashuke chini. Aliona kwamba mti ndio mtetezi wake aliyebaki. Baada ya kimya cha muda lile shimo likaanza tena kutoa maji si maji, uji si uji na hata damu si damu. Zikaanza kutiririka kwa kutawanyika eneo lote la Kakamega. Butiliasi kamwe asingeweza kuzikwepa zile damu damu. Zilikuwa kali sana hata zaidi ya tindikali. Ziliipitia miguu ya Butiliasi. Ikameguka yote. Butiliasi akadondoka mpaka chini napo zile damu zikammeza zote. Akamalizwa mwili wote mpaka na nguo zake zikateketea pale chini. Butiliasi akawa ameshaaga dunia rasmi. Utawala wa dakika chache ukabaki mikononi mwa Osusu. Osusu ambaye alikuwa bado amening’inia juu ya mti. Alikuwa akishuhudia tukio lote la kumalizwa kwa kiongozi wake wa muda mrefu wa kikundi chao kilichosumbua sana nchini Congo. Kikundi cha waasi kiilichoyashinda majeshi ya Uganda, Kenya , Rwanda,Burundi na hata nchini kwao Congo. Kikundi kikubwa cha M23. Osusu hakuwa na furaha hata kidogo. Aliendelea kutoa macho nakuangalia zile damu zikimalizia theluthi ya shati la Butiliasi. Baada ya kumaliza kila kitu,zile damu zikahama tena. Zikaanza safari ya kuelekea juu ya mti alipokuwepo Osusu.
“Mie siyo mutu ya Congo bana! mie sio muasi! mie sipo na Buti.. mim ni mateka.. mie sio mutu ya bolingo nangai !!” Osusu alijikuta akiongea lugha isiyoleweka. Alijikuta akiziambia zile damu zisimfuate. Alijikuta hata akisaliti cheo na alipotoka. Zile damu zilizidisha nguvu na kasi ya kupanda juu. Zilimfikia Osusu na kumteketeza kwa kumuingia mwilini. Osusu alibaki mifupa mitupu. Nayo ile damu haikukubalina na mifupa. Ikaiteketeza mifupa yote. Osusu akawa ameshafariki rasmi. Hivyo utawala wa muda wa waasi katika Msitu wa Kakamega ukamalizwa na kitu cha ajabu kutoka katika shimo lao la kutolea kafara. Ile damu ilipomaliza kumtetekeza Osusu haikutosheka. Ikaingia msituni kwa ajili ya kutafuta chochote itakachokutana nacho. Ikaanza safari ya kwenda kwa kasi uku ikiteketeza miti yote nakuwa patupu. Ilizidi kusonga na kukata mbuga.
*****
Upepo ulizidi kuwa mkali zaidi. Anga nalo lilionekana kama kuchafukwa eneo lote. Ile mbalamwezi hafifu iliokuwa ikiangaza nayo ilifutika ghafla na kubaki na mwanga mkali sana. Levina alisimama na kugeuka nyuma. Alikaa chini na kumshusha mtoto kisha akafungua ile zipu aliyokuwa ameifunga kidogo kuachia eneo dogo la mtoto kupata hewa. Levina alimchungulia yule mtoto. Alikuwa bado amepitiwa na usingizi mzito sana kwa kushiba. Levina akaliruidishia begi lake. Mwanga mkali ukaendela kuliteka eneo lake. Akajikuta ghafla kumepambazuka na kuwa mwanga kama vile machana na sio asubuhi.
“Ohhh asante Mungu, ama kweli wewe waweza!” Levina alishukuru kimoyo ,moyo uku akiliweka lile begi mgongoni. Begi lililokuwa na mtoto kisha akachukua gongo lake na kuendelea na safari. Safari ambayo kwa sasa ilimsaidia kutokana na kupambazuka kwa eneo. Pili aliweza kuona njia ya wapitao kwa miguu. Alizidisha mwendo uku akiamini wazi atakutana na barabara ya lami. Barabara ile ya kipindi kile walioiacha nakushinikizwa na waasi wapitie msituni wasiifuate barabara ya lami. Baada ya mwendo kidogo levina alichoka sana kutokana na maumivu mfululizo ndani ya mwili wake. Mabega yalikuwa hayafanyi kazi kutokana na kumbeba mtoto pia mabega hayo hayo yalikuwa yamefungwa na kina Kakamega walipompa adhabu kipindi kile kwenye himaya yao. Paja lake moja lile ambalo mguu ulikuwa haupo ulianza kumletea tabu sana. Ikambidi levina ajikokote kwa kujiburuta chini taratibu uku akiliacha gongo lake. Mkono mmoja aliutumia kwa kuburuta begi na mwigine aliutumia kwa kujivuta yeye mwenyewe taratibu. Kwa mbali badaa ya kujiburuta si mwendo sana macho yake kwa upande wa mbele yaliweza kuona gari dogo likikatisha. Levina akalinyooshea mkono lakini lile gari lilikuwa na mwendo kasi halikuwaeza hata kuona kitu. Nguvu zikamrejea Levina japo hazikuwa nguvu sana akaanza kujiburuta haraka haraka kitendo cha kuifikia barabara ya lami tu uku akiwa na kile kibegi alishangaa kwa nyuma yake kusikia sauti ya ajabu. Sauti ya kama upepo uvumao kwa kasi. Aliyageuza macho yake lakini alichoweza kuambulia ni kuona tambalare. Msitu wote ulikuwa umeshamezwa. Umemezwa na damu damu nyekundu si nyekundu na hata nyeupe si nyeupe. Zile damu zilikuwa zikitoa mvuke wa ajabu kama maji yachemkao kwa kasi. Ule mvuke ukafanya ile damu kupoa na ghafla ikapunguza kasi. Zie damu zikamsogelea Levina zikiwa zimepoa kabisa,hazikuweza kudhuru kama zilimvyowafanya Butiliasi na Osusu. Kilichofanyika zile damu zilimtanda mwili mzima Levina uku zikiliacha lile begi lililokuwa na mtoto mdogo. Hazikuweza kumdhuru mtoto wala Levina. Zilimzunguka kwa muda kidogo kisha zile damu zikanywea na kuondoka zake zikirudi msituni. Kwa jinsi zilivyokuwa zikirejea ndipo na msitu ule ukaanza kujijenga upya na kuwa msitu zaidi. Majani yakarejea upya haraka haraka msitu ukarudi kama ulivyokuwa awali. Baada ya muda kidogo kelele za watu zikasikika kama wakishangilia ushindi. Makelele yale yaliufunika msitu wote. Levina akawakumbuka sana wana Kakamega. Akaamini huenda zile damu baada ya kuja kwake zimeenda kupeleka amani. Levina akawa kama mtu asiyejiamini. Alitetemeka sana mwili mzima. Akajikuta akilala chini na kupoteza fahamu uku naye yule mtoto aliyekuwa kwenye begi akitoa makelele ya kulia kutoka usingizini.
******
Wakiwa njiani Stan na Sara mara Stan akasimama nakusita. Amani ikampotea!
“Vipi mbona unasimama?” Aliongea Sara baaada ya kuhisi kama Stan amesimama.
“Baba! Baba yangu na Devotha hao wanakuja? Baba ananitafuta na ana hasira kama mama yako vile?” Aliongea Stan kwa utani uku mwili wake ukionesha kukosa amani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Stan?? Stan” Aliita baba Devotha kwa sauti ya juu na ya ukali.
Stan alisimama na Sara kimya. Sara hakuweza hata kuiona sura ya mtu anayekuja mbele yake kutokana na upofu aliokuwa nao. Baba Devotha alipowafikia karibu tu.
“Hivi wewe Stan ni muda gani toka Devo amekuja kukuita?” Alilalama baba Devotha.
“Ndio najua baba ni muda lakini…
“Lakini nini Stan?”
Kwa hasira baba Devotha alinyanyua mkono nakumpiga nao Stan shavuni. Kibao kikamwigia Stan vilivyo. Stan hasira kali zikampanda,akaanza kutoa mchozi ya uchungu.
“Baba unanionea baba, mimi nilikuwa nakuja baba!” Alijiteteta Stan.
“Ulikuwa unakuja uku unaendelea kuzubaa na visichana vyako pumbavu.!!” Baba Devotha aliendelea kufoka uku akiuvamia mti wa jirani yake na kuchuma fimbo ndefu kiasi nakuanza kumchapa nayo Stan mfululizo mbele ya Sara na Devotha.
“Tangulia nyumbani mwenyewe, tangulia nimesema” Baba Devotha aliendelea kumkalipia Stan uku akimchapa ovyo mwilini. Stan hakuwa na jinsi zaidi ya kutoa machozi ya kimyamkimya na kuvumilia kile kichapo japokuwa kilikuwa kikivimbisha nyama za mwilini mwake. Aliamua kumuacha Sara na kwenda nyumbani kwao. Roho ya huruma ilimtawala haswa ile ahadi aliyomuhaidi Sara muda mfupi kuwa atamsaidia kuchota maji na kumrudisha mpaka nyumbani ndani ya muda mfupi. Hakuwa na jinsi kwakuwa baba Devotha ndiye mlezi wake toka amekuwa. Akaondoka akiwaacha Devotha na baba yake wakibaki na Sara.
Stan alipofika nyumbani tu alipitiliza mpaka chumbani kwake, akavua shati lake nakuchukua kioo. Akajitazama mwili wake kwa jinsi ulivyokuwa umeharibiwa ndani ya muda mfupi baada ya kichapo kutoka kwa baba yake wa kufikia,baba Devotha. Alikirusha kioo chini, Kikavunjika! Kisha akaegemea ukutani akilia kwa sauti ya juu.
“Why me! Why me God!!” (Kwanini mimi! Mungu kwanini mimi!!) Alilalamika Stan.
Aliachia kilio cha makelele. Kamasi likaanza kuomba njia katika pua zake. Likasalimiana na mdomo nakuteleza mpaka kwenye nguo. Jasho kali likaendelea kumtiririka Stan. Hasira kali na dukuduku vikamkaa rohoni. Hasira ya kudhalilishwa mbele ya Sara. Sara yule ambaye alikuwa akimshuhudia muda mfupi akipigwa na mama yake wa wakufikia na yeye Stan ilikuwa zamu yake kwa baba wake wa kufikia.
“Enhhh Mwenyezi Mungu nioneshe wazazi wangu!! nielekeze baba niwafutae popote walipo!!” Stan aliongea kimoyomoyo uku akiendelea kutoa mchozi wa hasira. Akiwa bado chumbani mara mlango ukabishwa hodi kwa nguvu.
“Stan, Stan??” Sauti ya baba Devotha ilisikika.
Stan akavuta shati lake nakujifuta haraka haraka machozi yake yaliokuwa yakimtoka mfululizo. Akaenda mpaka kwenye kitasa cha mlango cha chumbani kwake nakufungua.
“Unafanya nnini tena?? Nitakuuua?? nitakupiga nikuue Stan?? Weee endelea ukiburi wako tu!!” Baba Devotha alikmkalipia Stan.
Stan hakuweza kumjibu chochote zaidi ya kutoka nakuongoza mpaka nje yalipokuwa madumu ya maji. Akachukuwa madumu ya maji ya lita ishirini ishirini kisha akamfuata baba Devotha.
“Baba naomba hela ya kununulia maji?” Stan aliomba.
“Pumbavu na leo utajua utakapochota sitoi hata senti tano!! katafute maji na uje na maji tena masafi ole wako ukanichotee maji ya mtaroni.”
Stan alisimama kwa muda akimwangalia baba yake wa kufikia,baba Devotha kwa hasira kali. Akafikiria sana pindi alimpokuwa mtu mwema kabla hajafa mke wake mama Devotha. Akatikisa kichwa chake. Hakuwa na jinsi zaidi ya kugeuka nakuondoka zake akiwa amashikilia madumu ya maji mawili. Akili yote ikamuhama. Hakujua ni wapi ataenda kuyapata maji tena masafi bila hata kuwa na senti tano. Akili yake ilishindwa kufanya kazi ya ziada. alibaki akilalama mwenyewe kwa haisra kali. Wazo kuu alilolikumbuka ni juu ya Sara. Sara yule binti kipofu. Alitamani kujua uelekeo alipokuwepo. Alihisi kuwa na yule kunaweza hata kumsaidia na yeye kupata maji pasipo kutumia gharama yoyote. Pili aliwaza endapo atampata atamtimizia ile ahadi ya kumbebea maji mpaka nyumbani kwao. Njia nzima kichwa cha Stan kikazungukwa na jina moja tu. Jina la Sara. Alirudi mpaka lile eneo alipomuacha pindi akipokea kichapo kutoka kwa baba Devotha. Patupu!! hakukuwa na dalili yoyote ya Sara wala wapita njia. Akajindokea uku akihisi njia huenda atakuwa maeneo ya jirani jirani. Maeneo ambayo watu hupenda kuchota maji ya kununua.
**********
Baada ya kipigo cha nguvu kutoka kwa baba Devotha kwenda kwa Stan. Kilimuuma sana Sara. Sara binti kipofu. Hakuwa na uwezo wa kuona tukio lote zaidi ya kusikia kinachozungumzwa. Alikuwa akielewa lugha moja iliyokuwa ikiongelewa kutoka kinywani kwa baba Devotha. Lugha ya kukaripia ambayo hata yeye mwenyewe Sara alishaizoea masikioni mwake kutoka kwa baba na mama yake wakufikia pindi wakikasirika. Moyoni ile hali ilimuuma sana Sara. Kitendo kile cha kusikia sauti za mikwaju zikimtandika Stan. Sara alijihisi kama na yeye ni mkosaji namba moja. Alijihisi kama tukio limejitokeza na kwake. Aliona na yeye amemsababishia kosa Stan. Moyo wake ukawa hauna amani japokuwa hata kwa sura hakuwa akimjua Stan zaidi ya kusikia tu sauti yake kutokana na hali ya ukipofu aliyokuwa nayo Sara.
Baba Devotha alimgeukia Sara baada ya kipigo kile kwa Stan. Alimuaangalia sura ya Sara iliyokuwa imekosa macho mawili kisha baba Devotha akamfyonza na kumtupia fimbo Sara.
Sara aliweza kukisikia fyonzo lililotoka mdomoni mwa baba Devotha, aliumia sana moyo wake kudharauliwa. Alijua ni wazi amedharauliwa kutokana na ukipofu aliokuwa nao.
“Hujafa hujaumbika!” Aliongea sara kwa sauti ya chini chini.
Akachukuwa fimbo yake na kuondoka zake uku akiwaacha Devotha na baba yake nao wakiondoka. Njia nzima Sara alikuwa ni mtu wa kuimba nyimbo za majonzi. Nyimbo zile waimbazo watu wakiwa msibani kwenye maombolezo ya marehemu. Sara aliweza kujikongoja kwa kutumia ile fimbo aliyokuwa akichapwa nayo Stan. Hakuweza kupajua mahali anapoelekea zaidi ya kujisogeza kwa kutumia fimbo.
“Dada unaenda wapi na ndoo hii?” Aliongea kijana wa makamo.
“Niache, niacheni na moyo wangu!!” Sara alijibu. Hisia zake alihisi ni wale wale wenye roho kama za kina baba Devotha ama wazazi wake wa kufikia waliokuwa wakimtesa usiku na mchana.
“Dada kama ni maji twende nikulekeze. Lete mkono. Nipe na hiyo ndoo!!” Aliendelea kuongea jyule kijana aliyeonekana kuwa na huruma.
“Nimesema sitaki msaada wowote kama kwenda nitafika mwenyewe” Sara aliongeoa kwa sauti ya kulalamika.
“Kwangu mimi utataka!” Yule kijana alibishana na Sara. Alimshika Sara kinguvu. Sara alijitahidi kumkwepa kwa kutaka kukaa chini lakini ndio kwanza yule kijana alikaza mikono yake. Baada ya kusumbuana na Sara kwa muda mrefu. Sara ilimbidi akubaliane nalo kutokana na ukipofu aliokuwa nao. Ukipofu wa kutokujua anaenda wapi. Yule kijana akafanikiwa. hapakuwa mbali sana na eneo lililokuwa lina maji. Walipofika tu yule kijana aliwaomba watu wamsaidie yule binti kipofu ili aweze kuchotewa maji. Kuna waliokuwa wakilalamika kucheleweshewa zamu na wengine walikuwa na huruma. ndoo ya yule binti kipofu ikachotwa maji. Yule kijana akailipia.
“Kwenu wapi?” Yule kijana alimuuliza Sara.
“Asante kwa msaada wako, lakini kwetu siwezi kukuonesha nipe ndoo yangu nijitwishe” Aliongea Sara kwa kujiamini hali ilioyomfanya yule kijana ashikwe na bumbuwazi.
Kitendo cha kumbishia yule kijana mara Sara akasikia sauti ya juu akiitwa.
“Saraaa!! Saraaa!!”
Sara hakuweza kuifahamu mara moja ni sauti ya nani ikigonga katika ngome ya masikio yake. Ilikuwa ni sauti tata ambayo aliisikia muda kidogo. Kadri ilivyokuwa ikimuita ndivyo na Sara alishikwa na hisia kali ya kuweza kuigundua. Kichwa na masikio yake yakafanya kazi ya ziada kugundua. Yakashidwa!
“Nani wewe!! nani??” Sara aliongea kwa ukali.
Ile sauti ilimfikia kwa ukaribu. Ikamshika mikono. Sara akasisimkwa. Akajiona kama siyo kipofu kwa muda. Akahisi ni mtu muhimu sana ameshika mikono wake. Watu wote waliokuwa wakichota maji hata na yule kijana aliyemsaidia kuchota maji walibaki wakishangaa.Umati wote wakawazunguka nakuacha kuchota maji ukiwashangaa. Waliona kama tamthilia za wafilipino wanazoona kwenye televisheni kuhamia eneo la kuchotea maji.
“Sara? Its me Stan!” (Sara,mimi ni Stan)
“Stan, Stan??” Sara aliita uku akimpapasa mikono Stan mpaka mabegani kwa haraka haraka. Akamshika mpaka kwenye paji la uso. maeneo ya mashavuni kwa Stan. Mikono ya Sara ikakutana na mchozi wa Stan uliokuwa ukiomba njia, ukitaka kudakwa katika mikono ya Sara. Sara akayadaka nakuyapikicha mkononi mwake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Stan, polee, Pole sana Stan najua nina makosa juu yako!” Aliongea Sara kwa sauti ya utaratibu. hali iliyomfanya Stan aendelee kugumbwika machozi ya hisia. machozi makali akitetemeka mwenyewe. Wakiwa bado katika hisia kali mara gari ya kifahari ikasimama maeneo yale. Akashuka mzee mmoja alioonekana anazo. Ule umati ukampisha. Akawsogelea wote wawili Stan na Sara. Ule umati uliokuwa ukichota maji. Umati ambao ulijikusanya na kuwazingira Stan na Sara ukiwashangaa kwa kuwa na hisia za ajabu uliendelea kujaa na kushangaa. Yule mzee alipowafikia karibu tu.
“Sara?” Yule mzee aliita kwa sauti ya juu uku sura yake akiikunja kuonesha kuwa ana hasira kali.
“Abee baba” aliitika Sara. Alishajua kuwa ni sauti ya baba yake wa kufikia. Baba aliyokuwa akimnyanyasa sana akishirikiana na mama yake wa kufikia. Aliijua sauti ile vilivyo!
“Unafanyaje hapa?” Alifoka yule mzee kwa ukali.
Alichukuwa ile fimbo iliyokuwa ikimsaidia Sara katika kutembea. Fimbo ambayo alishachapiwa Stan na kurushiwa Sara, Fimbo hiyo hiyo ikatumika tena kumrarua Sara. Yule mzee hakuwa na huruma hata chembe. Alimchapa sana Sara mbele ya ule umati uliokuwa umewazunguka. Stan Akataka kuingilia kati. Akafanikiwa kuichukuwa ile fimbo kutoka kwa yule mzee. Kwa hasira kali za Stan akajikuta akimchapa yule mzee. Ule umati wa wachota maji ukageua kuwa mashabiki. Wakajiona wako uwanjani. Uwanja wa mapigano. Wakaona sinema ya bure pasipo kulipia hata senti tano. Wakaanza kushangilia kichapo alichokuwa akikitoa Stan kwa yule mzee. Wengine walipiga makofi sambamba na madumu ya maji na miluzi. Sara alikuwa ameshaanguka chini akilia kwa hasira kali iliyoambatana na kwikwi. Hasira za Stan zikaendelea kumzidia. Akachukuwa ile ndoo ya maji. Ndoo ambayo ilitumika kumwagiwa maji Sara ndio nayo ikatumika kumlowanisha yule mzee. Maji yote aliyokuwa amechotewa Sara muda mfupi na kijana msamaria mwema yakamalizika kwenye mwili wa yule mzee. Mzee suti yake ikalowa tapatapa! Stan akanyanyua mikono juu kuashiria ushindi. Ushindi baada ya mapambano, baada ya kumuona yule mzee akihema juu juu kwa kuchoka kipigo kutoka kwa Stan. Umati wote ukaendelea kulipukwa kwa makofi na vigelegele. Chini kukajawa na tope kiasi kutokana na yale maji yaliomwagika. Yule mzee hakuwa na balansi tena katika mwili wake mnene akajikuta akiteleza mpaka chini. Kila akitaka kusimama aliteleza nakurudi chini. Stan naye kwa kutumia miguu yake iliyokomazwa akamsukuma yule mzee. Mzee akabiringita mpaka kwenye madumu ya maji. Stan akamfuata Sara na kumuinua kisha akamkumbatia kwa hisia kali. Akambusu shavuni.
“Sara nipo pamoja nawe!”
***********
Sara hakuweza hata kuijua sura ya Stan imekaaje. Hakuweza kujua mwili wa Stan ukoje na hata nguo alizovaa zipoje. Hisia kali ndizo zilikuwa zimeshajijenga katika mwili wake. hisia za kusaidiwa na mtu ambaye maishani mwake hajawahi kutokea. Moyoni akafurahi kupata mtetezi mpya wa maisha yake. Kitendo cha kukumbatiwa na kupigwa busu kutoka kwa Stan kikamsisimua sana mwili wake.
“Stan!” Sara aliita kwa sauti ya upole.
“Nakusikia Sara niambie!” Stan alijibu.
“Nakuomba nikubusu!” Sara aliongea kwa sauti ya juu kidogo.
Akili yake yote ilishahama kabisa. Ule umati uliokuwa ukishangilia kwa kupiga makelele sana ukazima ghafla. Ulizima nakuanza kufuatilia hisia kali zilizokuwa zikitolewa na Sara na Stan. Hisia za binti kipofu na kijana mzima. Hisia ambazo kila mmoja aliguswa nazo. Hisia ambazo hata mara moja huwezi kuziona kwa mtu kuwa karibu na kipofu na kumtetea kwa kila kitu. Sasa Sara uzalendo ulikuwa umeshamshinda baada ya kukumbatiwa na Stan kwa muda mfupi. Akatamani japo ampige busu Stan shavuni mwake. Stan woga ukaanza kumpanda. Woga wa kupigwa busu na Sara mbele ya umati. Aliona ni sahihi kwa yeye kumpiga busu Sara na si kupigwa busu. Stan akayazungusha macho yake kuangaza uku na kule. Yakamuangalia yule mzee aliyemtembezea kichapo cha haja. Alikuwa ameshainuka akijikongoja kwenye gari lake. Ule umati ukaanza kupiga makelele baada ya kugundua yule binti kipofu anaitwa Sara. Umati ukataka kushuhudia busu kutoka kwa Sara kwenda kwa Stan.
“Sara!!, Sara!! Sara!!”
Sara hakuweza kushuhudia idadi kamili ya umati ule. Hisia zake zote alizielekeza kwa kijana ambaye alimuokoa muda kjidogo kutoka katika mikono ya baba yake wa kufikia. Baba katili ambaye alikuwa kila siku akishirikiana na mke wake katika kumtesa Sara. Sara akachukuwa mikono yake na kushika masikio ya Stan. Baaada ya hapo akavuta masikio ya Stan karibu. Kichwa cha Stan kikasogea mpaka karibu na Sar. Sara akavuta pumzi kidogo kisha akaachia busu lililofanya ule umati ulipukwe tena kwa makelele. Ukaanza kushangilia kwa sauti ya juu. Eneo lote la kuchotea maji likageuka tamthilia ya kifilipino.
“Sara nikwambie kitu?” Stan alimuuliza Sara.
“Niambia Stan!”
“Hakuna tena kuchota maji kuanzia sasa na nitakuwa nikikuchotea mimi na kukupelekea mpaka nyumbani kwenu.” Aliongea Stan kwa kujiamini mbele ya ule umati.
“Stan kwa hilo haliwezekani, na mpaka hapa nitapigwa tu nikirudi leo!” Aliongea Sara.
Wakiwa bado katika mazungumzo mara lile gari aliokuja nalo baba yake Sara wa kufikia likawashwa na kuondoka.
“Stan?” Aliita Sara.
“Naam!”
“Hilo gari linaloondoka ni la baba?” Aliuliza Sara.
“Ndio. Bora ameondoka!” Alijibu Stan uku akiwa bado wamekumbatiana na Sara kwa hisia zote. Wote walikuwa wameshajisahau kwa kukumbatiana kwa muda. Wakiwa bado hawajaachiana mara sauti ikasikika. Sauti ya ukali iliofanya ule umati wote kukaa kimya na kugeuza vichwa vyao nakuangalia eneo inapotoka ile sauti ya ukali.
“Stan nani huyo?” Sara aliuliza uku akionesha kuanza kuingiwa na woga. Akajihisi baba yake amerudi tena kivingine.
“Baba! baba yaaa ngu ana ana anakuja Sara” Aliongea Stan kwa kigugumizi.
Hofu ikamtawala Sara. akakumbuka mara ya mwisho alivyowakuta wakiwa wamesimama. Akapata hisia ya sauti zile za fimbo zilizokuwa zikimchapa Stan vilivyo. Akakumbuka dharau za baba yake na Stan alipotupiwa fimbo ile ya kipindi kile iliotumika kumchapia Stan.
Ule umati ukampisha baba Devotha, baba yake na Stan wakufikia. Kitendo cha kumpisha tu na gari la polisi nalo likaingia likiongozana na gari ya baba yake na Sara. Likapaki na kushuka mapolisi wawili kwa haraka wakafuata eneo aliokuwepo Sara na Stan wamesimama. Nyuma alijikongoja baba yake na Sara. Na walipowafikia karibu tu.
“Kijana mwenyewe huyu hapa.. “ Aliongea baba yake na Sara.
“Sio mimi? msinifunge pingu jamani!!” Stan alijitetea
Polisi hawakuwa na huruma hata kidogo, Walimfunga pingu Stan. baba yake akataka kuwa mbishi kwa kutoelewa kinachoendelea lakini akaonywa na mapolisi aache kufanya lolote. Akatakiwa afike tu ofisini kwa maelezo. Ule umati ukasikitika sana. Ukawa na masikitiko kwa kuona ‘stering’ wao anashikwa na mapolisi. Wakaona kama sinema waliokuwa wakiangalia kwa muda bila kulipia hata senti tano ndio inaishia hapa. Wote kwa pamoja wakaanza kurusha maneno kuwa wanaonea.
“Na wewe twende nyumbani?” Baba Sara alimkalipia Sara uku akimshika mkono.
Sara uchungu ukamshinda kutokana na makelele ya wale vijana. Maneno aliyokuwa akiyasikia kutoka kwa Stan juu ya kugoma kufungwa pingu yalimuingia vilivyo rohoni mwake. Duku duku likamjaa! Alitamani sana kutoa machozi lakini hakuweza kutoa kutokana na macho yake yote kufungwa. Ukipofu ulimfanya machozi awe akiyatolea moyoni mwake. Moyo wake wote ukagubikwa na machozi ya huruma na uchungu. Baba yake alimvuta mkono na kumlazimisha kumpeleka mpaka kwenye gari lake.
“Na leo ndio utanitambua vizuri mimi nani?” Aliendelea kuongea baba yake Sara.
“Polisi nisaidieni. Nitauliwa mimi?” Sara alijitahidi kuomba msaada. Akilini mwake alishajua kuwa kuna mapolisi maeneo yale na ndio waliomkamata Stan. Aliomba msaada kuokolewa kwenye mikono ya baba yake wa kufikia lakini ndio kwanza wale mapolisi na baba Sara walikuwa kitu kimoja. Wasingeweza kumtetea Sara hata mara moja kutokana na wenyewe kuitwa kumkamata Stan. Walishakula pesa za baba Sara kwa ajili ya kuja kumkamata Stan aliyedaiwa kumchafulia jina baba Sara wakufikia.
“Polisi, Polisi nisaiidieni?” Bado Sara aliendelea kulalamika akiomba msaada.
“Ingia uko.” Baba Sara alimsikuma sara baada ya kulifikia gari lake. Sara hakuweza hata kujua kama amelifikia gari. Alijigonga katika mlango hali iliyomfanya kuhisi maumivu katiika paji lake la uso. Baba yake wakufikia aliendela kumsukumiza. Sara alijikuta amekutana na siti ya nyuma ya gari. Akaingia na baba Sara naye akaingia kisha wakaanza safari ya kulifuata gari la polisi mpaka kituoni.
Baada ya dakika chache wakawa wameshafika polisi. Hapakuwa mbali na eneo lile. Walimfikisha Stan na kumshusha kwa nguvu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haya shuka shuka” Aliropoka polisi mmoja.
Wakamchukuwa Stan nakumsachi mifukoni na baada ya hapo wakamfungua zile pingu.
“Haya ingia uku, ingia?” yule polisi aliendelea kuamrisha.
Baada ya hapo yule baba yake na Sara naye akaingia peke yake nakumuacha Sara ndani ya gari. Akaanza kuandika maelezo juu ya kilichotokea yeye na Stan. Akampakazia maneno mengi sana Stan ya uongo katika maelezo yake ikiwa ni pamoja na kupigwa kwa kutumia kisu na fimbo, kutishiwa maneno makali mbele ya umati wa watu nakushushiwa heshima. Kutukanwa ovyo! Polisi wakaendelea kuandika maelezo na wakahaidiana na baba Sara wampe kesi ya kutishia kuua kwa kutumia kisu. Kitendo cha kumaliza tu kuandika malezo baba yake na Stan wakufikia akatokea. Akapishana na baba Sara katika meza ya polisi.
“Nimekuja kumuangalia mwanangu, nini tena kimemfika jamani. mimi baba yaeke?” Aliongea baba Stan kwa kulalamika.
“mwanao anakesi kubwa sana na hatuwezi kumuachia kwa dhamana yeyote.”
“Ana kesi gani?” Aliongea baba Stan kwa kulalamika.
“Ana kesi ya kutaka kuua kwa kukusudia. Amemshikia mzee yule anayeondoka kisu na kumtisha kwa maneno makali akitaka kumuua!” Aliendelea kuongea polisi.
“Mwanangu huyu huyu? Stan? Stan amekua muuaji? hapana kwa kweli. Hawezi kufanya hivyo. Nimeishi naye namjua jamani?” Aliendelea kulalamika baba yake na Stan.
Baba wa kufikia wa Stan aliendela kulalamika. Jasho lililmtoka kwa kuhaha. Hakujua nini afanye ili kuweza kumtoa mtoto wake ambaye mapolisi walimuwekea ngumu kutoka. Tayari mapolisi kimoyo moyo walikuwa wakipongezana baadaya pesa waliyolipwa awali na baba yake wa kufikia wa Sara. Kamwe isingekuwa rahisi kumtoa Stan kwa dhamana yoyote pale na lengo alilokuwa kilihitaji baba yake Sara ni Stan apelekwe jela na yeye mwenyewe atakuwa shahidi kwa lolote na atatumia kiasi chochote kuhakikisha anawekwa ndani. Kile kitendo cha kudhalilishwa na kuchafuliwa suti yake mbele ya umati wa watu kilimuuma zaidi baba Sara nakuamua kumbambika kesi Stan.
****************
Sara aliumia sana kupakizwa ndani ya gari la baba yake. Hasira kali na chuki aliziweka dhidi ya baba yake. Akajiona tena amekuwa mkosaji mbele ya Stan. Akaona yale yale ya asubuhi yamejitokeza tena. Akaumia sana moyoni. Machozi yalikuwa yameuzunguka moyo wake. Hayakuweza kutoka usoni kutokana na kuwa kipofu. Ile furaha ya mara moja aliyoipata kutoka kwa Stan. Furaha yakukumbatiwa nakupigwa busu ilifutika kabisa. Akaiona dunia chungu kwa muda. Tayari alikuwa ameshampenda Stan kwa ukarimu alioutoa ndani ya masaa kadhaa. Aliona Stan ndiye mtetezi wa kweli.
“Kwanini baba yangu kamchukulia mapolisi Stan” Alijiuliza Sara kimoyo moyo bila kupata jibu.
Hakuweza hata kuamini kama kweli Stan yule yule aliyekuwa naye amepelekwa piolisi. Maneno ya dharu na ukali kutoka kwa baba yake yalimchoma sana. Neno la kusema kuwa atahakikisha Stan wake anapelekwa segerea lilimuuma sana. Walipofika kituoni baba Sara alifunga vioo vyote vya gari na kuloki milango kisha alimwacha Sara na kuelekea kituoni.
Sara alibaki mwenyewe ndani ya gari asielewe nini cha kufanya. Akajijenga hali ya kujiamini. Hali ya kuchoshwa manyanyaso kila kukicha. Akaona hapa imefikia mwisho. kwa hisia anazotumia pasipo kuona akaanza kupapasa maeneo ya mlango kwa pembeni. Akakutana na loki ya mlango. Akabonyeza na kuufungua mlango. Ukafunguka! Kitendo cha kuufungua mlango akajikuta akiteleza na kudondoka mpaka chini. Maumivu ya ndani kwa ndani akayasikia lakini akayavumilia na kuyaona ni maumivu madogo kuliko yale anayopigwa kila siku. Sara akafanikiwa kuinuka na kuanza kuondoka uku mikono akiitanguliza mbele kwa kupapasa asijue anapoelekea. Hakuwa na fimbo yoyote ya kuweza kumuongoza. Njia nzima alitembea kwa hara haraka. Alipofika mbali kidogo aligusana na ukuta. Napo akatembea kwa kutumia ukuta aliokuwa ameushika mpaka kwenye kona ya nyumba nakuingia mpaka kwenye korido asielewe anaingia nyumbani kwa nani na yupo maeneo yapi.
“Wee binti?” Aliita mama mmoja.
“Abee!!”
“wee si ulikuwa kule ukichota maji. Masikini pole sana mwanangu, polee!!” Yule mama aliingiwa na huruma baada ya kumuona Sara akiingia kwenye korido yake moja kwa moja.
“Stan yupo wapi?” Sara aliuliza pasipokujua yupo maeneo gani.
“Stan? Stan ndio nani tena?” Aliuliza yule mama.
“Yule kijana aliyekuwa na mimi kule kwenye maji. Yule kijana aliyekuwa akipigana na baba!, Kwani kituo cha polisi kiko wapi?” Aliuliza Sara kwa sauti ya juu kidogo uku asiweze kumuona anayeongea naye kutokana na upofu aliokuwa nao.
“Mwanangu. Hapa tulipo hata kituo cha polisi siyo mbali. Muda si mrefu nimeona mapolisi wakimshusha kijana mdogo mdogo uku wakiwa wamemfunga pingu kisha baada ya hapo akaingia baba mmoja mie nikaondoika zangu hata sijakaa vizuri nakuona na wewe unaingia hapa kwani ni nani huyo Stan?” Aliuliza yule mama.
“Stan ni rafiki. Ni mtu muhimu sana kwangu. nataka nikamuombe msamaha. NImemuweka pabaya tena. Mimi ndio chanzo ewe mwenyezi Mungu nisamehe kwa kumuweka hatiani tena Stan” Sara aliendelea kulalamika akiomba. Alishindwa kutoa machozi lakini mwili wake ulijawa na hasira kali sana.
Yule mama alimuonea sana huruma Sara kwa hali aliyokuwa nayo. Hali ya upofu. Alijiuliza maswali mengi juu ya Sara na huyo Stan. Akahaidiana na Sara wasubiri ifike saa moja za usiku ndipo itakuwa rahisi kuonana na Stan kwani walishakizoea kituo hicho cha polisi kwa rushwa. Alimtuliza Sara juu ya hilo Sara akawa mdogo hakuwa Sara yule aliyetamani kurudi katika nyumba ya mateso. Alishajitoa kwa lolote litakalomtokea na siyo kurudi tena katika nyumba ya mateso. Nyumba aliyolelewa toka amechukuliwa na wasamaria wema waliogeuka na kuwa watu wabaya katika maisha yake.
masaa manne yaliokuwa yamebaki itimie saa moja za usiku yalikuwa yameshamalizika. Yule mama alikuwa ameshamtengenezea Sara chakula. Sara alikula na akaomba Stan na yeye awekewe chakula ili wampelekee. Yule mama akafanya hivyo. Akamshika Sara mkono mmoja na mwingine akashika mfuko uliokuwa na ki ‘hot pot’ kidogo wakaelekea mpaka kituo cha polisi. Haikuwachukua muda Sara na yule mama msamaria mwema wakawa wameshafika kituoni.
“Samahani baba” Aliongea mama yule msamaria mwema uku akifungua pindo la kanga yake na kutoa noti ya shilingi elfu tano iliyokuwa imefungwa vilivyo na kanga ile. Akampa polisi wa zamu.
“Baba kuna kijana wetu yupo humu ndani tunahitaji kumuona na kumpa chakula” Aliongea yule mama msamaria mwema.
Polisi akaangalia uku na kule kama kuna wanoko.
“Onja kwanza wewe kama chakula kizuri, onja kijiko kimoja.” Yule mama akaonja na Sara naye kwa ushahidi zaidi akaonja. Polisi akawalekezea waende kumuona na kumpelekea chakula haraka haraka. Hali ya uchafu na harufu kali ndani ya lokapu ya kituoni ilikuwa ya kutisha. Sara ilibidi aizoee ile hali kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza. wakafanikiwa kuingia mpaka kwenye chumba cha lokapu. Chumba ambacho kwa siku hii hakikuwa hata na mtuhumiwa yoyote zaidi ya Stan aliyekuwa ameletwa mchana. Stan aliyekuwa akipambana na harufu kali na mawazo mengi juu ya hatma yake hapo kituoni.
“Stan? Stan?” Aliita yule mama akisaidiana na sauti ya Sara.
“Naam!” Upande wa pili uliitika.
Sara akiongozwa na yule mama wakawa wameshamfikia Stan. Giza la mule ndani yule mama hakuweza kumuona hata huyo Stan vizuri.
“Tumekuletea chakula baba?” Aliongea yule mama.
“Nyie kina nani? Nani nyie?” Stan aliuliza kwa sauti ya juu kidogo. Alidhani huenda ni mama yake na Sara.
“Mimi ni Sara. Sara! nipo na mama msamaria mwema aliyeniokoa mchana wa leo” Sara aliropoka kwa sauti ya chini.
“Sara? Sara?” Stan alishtuka.
Hakuweza kuamini kama ni Sara huyu aliyemjua kwa muda mchache. Sara ambaye Stan alihisi hawezi kumuona tena kutokana na kuwekwa ndani. Alichukuwa mikono yake nakumshika sara kichwani mwake. Akakutana na nywele za mabutu mabutu ambazo Sara alikuwa amesukwa. Sara naye akatoa mikono yake na kumshika Stan masikioni. Akapata hisia kuwa ni Stan huyu aliyemuona mchana. Safari hii alimpomshika tu masikio alisisimka zaidi ya mchana. Yule mama msamaria mwema akatoka nje na kumuacha Stan na Sara wakishikana mikono kwa kukumbukana.
“Stan?” Sara aliita.
********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Naam!”
“Ni mara nyingine tena nimekusababishia haya yote” Sara alianza kulalamika.
“Nooo!! usiseme hivyo Sara. Nilishakwambia na nitaendelea kukwambia niko tayari sasa nife kwa ajili yako” Stan aliongea kwa kulalamika.
Wakiwa katika maongezo mazito na ya muda mfupi. Sara akapapasa pembeni na kufungua hot pot lililokuwa na chakula. Akatoa na kijiko akiongozwa na hisia kali kisha akachukua chakula kwa hisia nakuanza kumlisha Stan. Stan alijiona yupo dunia nyingine. Dunia ya peke yao kwa mara nyingine. Kutokuwepo hata na mtuhumiwa katika lokapu ile kwa muda kuliwafanya wabaki wawili wenye furaha wakiendelea kulishana. Stan akajiona kama yupo huru. Hata yale yaliokuwa yakimsumbua kichwa juu ya kusingiziwa kutaka kuua akayasahau. Akayaweka kando kwa muda!
“Kula basi Stan?” Aliongea Sara kwa sauti ya huruma.
“Sara?” stan aliita.
“Abee!”
“Ujio wako tu na kuwa karibu na mimi Sara tayari nimeshashiba! Siendelei tena inatosha. Mtu ambaye nilikuwa nikimfikiria nimeshamuona, ila sara nikwambie kitu tena?” Stan aliuliza
“Niambie Stan?”
“Sara, nakuomba niendelee kuwa karibu na wewe na hii yote ni kuhakikisha nakutetea katika mapito yako. Nahitaji nijifunze mengi sana kupitia kwako. Nataka nioneshe jamii kuwa wewe ni mfano wa kuigwa kwa jamii. Kwanini mnanyanyasika? kwanini mnateswa na kudharauliwa na jamii. Nitahakikisha napingana navyo popote pale” Stan alilalamika.
“Ila Stan?” Sara alisita nakuita.
“Niambie!”
“Hapa kwanza sijui hata utatoka vipi? nimechanganyikiwa na hii harufu ya humu ndani ndio inaniumiza zaidi nakujiona mkosaji ni mimi. Mimi ndio nimekusababishia yote haya Stan wewe kuwa mahali hapa? Nani atakutoa na baba nilimsikia akisema lazima tu ahakikishe umeenda segerea?” Sara alilalamika.
Alitoa sauti ya manung’uniko. Alishakata tamaa ndani ya muda mfupi alipoyakumbuka maneno ya baba yake wa kufikia. maneno
juu ya kuhakikisha Stan ameozea jela ndiyo yalikuwa yakijirudia kichwani mwake.
“Sara?” Stan aliita kwa sauti ya juu kidogo ili Sara aache kuongea tu.
“Naku si si kia.” Sara alijibu uku kwiki ikimbana.
“Kwani nimeua? nimefanya kosa gani baya mpaka nipelekwe jela? usiwe na wasiwasi nitatoka tu na nikitoka?..
Kabla Stan hajamalizia maongezi na Sara mara akaiskia Sauti ya juu ikimwita.
“Stan? Stan? Stan?”
Stan akajaribu kuivuta masikioni ile sauti. Ikamwingia katika ngome ya masikio yake sambamba na woga kwa mbali. Sauti ilikuwa ni mchanganyiko wa sauti baba Sara na ya baba Devotha kwa pamoja. Alihisi ni mauza uza yakimzunguka.
“Naam!” Stan aliitika kiuwoga.
Ile sauti ikaacha kuongea na kilichofuatia ni sauti ya viatu vikitembea. Sauti ile ya viatu ikaanza kuonesha kama inakaribia ikiwafuata. Sara hakuweza hata kuona wala kujua hata kama pahali pale pangelikuwa na mwanga asingeweza kushuhudia kitu kutokana na upofu aliokuwa nao. Alichokifanya Sara alichukuwa mikono yake na kumshika Stan kwa nguvu zote akakisogeza kifua chake na kugusana na Stan. Alishaapa na moyo wake kwamba hatothubutu amuone Stan akiteswa tena kwa ajili yake.
“Muda umekwisha wa kuonana, yule binti yupo wapi?” Ile sauti ilisikika.
Stan akashusha pumzi zake chini. Akili yake ikajijenga upya bila ya woga. Alishaitambua ile sauti baada ya kumuambia muda umekwisha. Ilikuwa ni sauti ya polisi wa zamu. Yule polisi ambaye alichukuwa rushwa na kumruhusu Sara na mama msamaria mwema kuingia ndani na kuonana na Stan sambamba na kumpatia chakula Stan. Muda wote yule mama alishajitokea zake na alikuwa meza kuu ya polisi akimsubiria Sara na Stan wakiongea mazungumzo yao. Hakutaka hata kusikia maongezi yao.
“Afande mie sitoki, sitoki mnifunge na mimi humu ndani?” Aliropoka Sara kwa sauti ya juu.
“Unasemaje wee binti?” Polisi alifoka.
“Naomba mumuachie Stan. Stan hana makosa mnamuonea bure. Muachieni jamani” Sara alilalama.
Yule polisi wa zamu hasira zikampanda. Akawasha tochi yake vizuri ili amuangalie vizuri binti alioonesha kutaka kugoma kutoka. Akamuona akiwa ameng’ang’ania shati la Stan. Alikuwa amemkumbatia Stan vilivyo.
“Wee binti? Sitaki utuletee matatizo hapa kituoni usiku huu. Ondoka mwenyewe!?”
“Nimesema sitaki, mniache na Stan. Kwanini mumfunge wakati hana hatia? amefanya nini mpaka mumlete uku?” Bado sara aliendelea kulalamika kwa polisi wa zamu.
Yule polisi wa zamu akaona sasa kazi yake ya upolisi inaweza kuharibiwa na mtu mmoja. Hakuweza kujua mara moja kama yule binti ni kipofu. Alichokifanya yule polisi aliidumbukiza tochi yake kwenye suruali kisha akachukuwa mikono yake nakuanza kumvuta Sara kwa kutumia nguvu ili aweze kuachana na Stan.
“Niacheee niacheee?” Sara alilalamika baada ya mikono yake kuachanishwa na Stan.
“Sara? Sara?” Stan alimuita.
Polisi yule wa zamu akaacha kumshika Sara. Akazubaa! Sara na yeye akaacha kutoa sauti ya kulalamika.
“Sara nakuomba uende. Kesho asubuhi uje kuniona.” Stan alimbembeleza Sara kwa upole.
“Hapana Stan!!, watakupeleka Segerea kesho!, watakupeleka gerezani ukateseke. Hapana Stan ni bora wanipeleke mimi wewe wakuache. Huna hatia Stan!!, huna kwanini wakufanye hivi?” Sara alilalamika.
Safari hii maneno yale yalimgusa sana Stan. Akajiona ni mtu muhimu sana kwa Sara. Machozi yakaanza kumlengalenga.
“Afande?” Stan aliita kwa kujiamini.
“Unasemaje?” Aliitika afande.
Nakuomba umuache huyu binti usimvute tena. Haoni huyo binti. Ni mlemavu wa kutokuona chochote, kwa hiyo unavyomvuta hivyo unamuumiza na hata mimi unaniumiza moyoni mwangu. Elewa kuwa moyo wake ni wangu na wangu ni wake katika kuhakikisha anaenda njia salama. Sipendi kushuhudia ukimburuta hivyo.” Stan aliongea kwa uchungu nakufanya yule afande awe kimya kwa muda. Alikuwa ameshaguswa baada ya kutamkiwa kuwa yule binti ni kipofu. Hakuwa akiona kitu chochote mbele. Kutokana na walivyoingia na yule mama msamaria mwema yule afande aliona kama wote ni wazima. Bumbuwazi likamshika afande!! Nafsi ikamshuta kwa kitendo ambacho alikuwa akikifanya kwa Sara. Kitendo cha kumvuta Sara kwa kutumia nguvu zote ili tu aweze kuachana na Stan.
“Binti?” Afande aliita.
“Abee!” Sara aliitika uku akivuta kamasi zake zilizokuwa zikitaka kumtoka katika pua zake. Kamasi zile za hasira.
“Samahani kwa nilichokuwa nakifanya. Pole sana sikulitambua hilo” Aliongea yule afande nakumfanya Stan na Sara kwa pamoja kusisimka kwa kuguswa. Waliguswa kwa kitendo cha afande yule kuongea ya moyoni juu ya Sara.
“Stan?” Afande aliita.
“Naam!”
“Nakuomba toka na huyo binti njoo mnifuate mpaka kwenye meza kuu.” Polisi yule aliamrisha uku akianza kusonga na Stan na Sara wakinyanyuka na kumfuata kwa nyuma wakitokea lokapu.
Walipofika meza kuu Stan macho yake yakaonana na yule mama. Mama msamaria mwema. Yakatizamana!!
Stan hakuweza kumjua kama mama huyo ndio aliyekuwa na sara. Waliomletea chakula hapo lokapu. Alijua dhahiri kuwa anaweza kuwa tena siyo mwema katika jamii. Afande mwingine wa zamu alikuwa nje akizunguka zunguka.
Walipofika katika meza kuu yule afande alichukuwa karatasi ambayo ilikuwa na maelezo yalioandikwa mchana na yule mzee aliyomleta Stan. Baba yake wakufikia na Sara. Baba mweye roho mbaya. Akaipitia vizuri ile karatasi kusoma maelezo ya kesi iliyosababisha Stan awepo pale. Chini ilikuwa imepigwa sahihi sambamba na muhuri kuthibitisha imepitishwa na kiongozi wa kituo hicho na iko tayari kwa mtuhumiwa kupakiwa kwenye karandinga kwenda lokapu kubwa. Lokapu ambayo atakutana na mahabusu tofauti wenye kesi zaidi yake.
“Stan?” Aliita yule afande.
“Naam!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kesi kama hizi huwa zinakuja nyingi sana na wewe unatakiwa tukupeleke kesho lokapu kubwa. Asubuhi na mapema defender ya polisi itakuja kukuchukua. Kumbe unakesi kubwa sana mie nilijua ni usumbvufu wa kawaida tu nikuachie sasa hivi!?”
“Hapana hapana Stan haendi popote Afande” Aliropoka Sara.
“Afande?” Mama masamaria mwema alimuita afande. Alimuita kwa kutumia kiganja cha mkono wake akimuoneshea ishara ya kuwa asogee pembeni kidogo waongee. Afande akasogea na kuachana na Stan pamoja na Sara pale meza kuu ya kituo cha polisi.
“Afande sikiliza” Aliongea yule mama msamaria mwema. Alishajitoa kwa lolote ili mradi Stan aweze kutoka. Aliona bila kuwepo Stan Sara angelipata shida mbeleni. Alichokifanya yule mama msamaria mwema alifungua tena pindo la kanga yake na kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kumshikisha afande. Afande akaipikicha nakuisogeza mpaka karibu na uso wake. Akatabasamu moyoni!!
“Ongeza kumi nyingine si umeona nipo na mwenzangu?” Aliongea yule afande.
“Sina baba!! niliokuwa nayo hiyo hiyo nakuomba unisaidie jamani hawa watoto ni wa mjomba wangu ambaye yupo Singida na ni mapacha ambao wamekuwa pamoja nakupata shida sana?” Yule mama msamaria mwema ilimbidi kudanganya ili tu Stan aweze kuwa huru. Aweze kutoka na Sara kuwa na amani.
Afande akamuita mwenzake. Wakasogea karibu nakuteta jambo kisha wakamuita na yule mama. Wakaelekea kituoni nakuandika maelezo ya uongo na kweli.
“Mama mtoto wako yupo huru na hii kesi tuachie wenyewe tumeshaifuta na tutajua cha kufanya kesho” Aliongea yule polisi.
Maneno hayo yalipenya moja kwa moja mpaka masikioni mwa Sara. Akayasikia!! Akahisi kama kupulizwa na ubaridi katika macho yake. Akajiona kama anamacho yenye mboni zake na anawaona wote sambamba na kusikia sauti juu ya kuachiwa Stan. Akahisi kama anamkonyeza Stan pembeni yake. Moyo wake ukaingia na ubarafu. barafu likateleza kuzunguka moyo. Akapapasa nakugusa mikono ya Stan. Akamshika vizuri Stan mikono yake. Ikashikamana!
Baada ya dakika chache kwa haraka haraka Stan na Sara wakaongozwa na yule mama msamaria mwema nakuondoka zao. Lengo kuu likiwa ni kuwapeleka wakakae kwanza nyumbani kwake yule mama msamaria mwema. Alishajitoa kwa kila kitu. Hatua chache mbele Stan akasita. Akasimama! macho yake angavu katika giza yalishaweza kuona kwa mbali kidogo. Aliona gari ile ile ya baba yake na Sara. Gari ambayo mchana ilitumika na baba yake Sara kuja kuwapa taarifa. gari ambayo isingekuwa rahisi kuisahau katika kichwa cha Stan.
“Sara? Sara?” Stan alimuita Sara aliyekuwa haoni chochote mbele kinachoendelea.
“Nini tena Stan tembea?” Sara aliongea baada ya kuhisi kama Stan amesimama kutokana na mikono walioshikana kukaza.
“Sara gari ya baba yako hiyo hapo inatukaribia? Baba yako anakuja hapa kituoni?” Stan alijikaza na kumwambia Sara kwa kutetemeka.
“Baba? Baba yangu? Stan nimekwisha, nitakufa? anaitafuta mimi tu Stan.. Stan niokoe tafadhali sana? Nakuomba Stan!! kumbuka ahadi uliyoniambia ndani ya kituo? Niokoe Stan?” Sara aliongea kwa kuogopa. Mwili wake ulishakuwa kama umemwagiwa maji ya baridi baada ya kusikia gari la baba yake linawafuata mbele.
**************
Sara alikosa kabisa amani moyoni mwake. Alikuwa akizunguka zunguka nyuma ya mgongo wa Stan uku aking’ang’ania shati Stan asiweze kuonekana. Akili yake na hisia zilishajijenga kuwa lazima atakuwa baba yake wa kufikia kutokana na Stan kuonekana kushtuka vile. Alijikuta kutokuwa na raha wala amani kwa muda. Yule mama msamaria mwema alibaki akiwatizama kwa huruma tu asielewe nini kitaendelea kati ya Sara,Stan na yule mzee.
Lile gari la kifahari liliwafikia mpaka karibu yao. Likasisimama!! Stan akajihisi kama kojo kutiririka katika suruali yake. Akajihisi kama vile kaigeuza suruali yake nyuma mbele mbele nyuma. Vidole vyake vya mikononi vikakosa kabisa ushirirkiano,Ushirikiano wa kugangamala!! Akajikuta akitetemeka ovyo. Macho yalimtoka sana kwa kuangalia kama kweli baba yake Sara. Na kama kweli atashuka yeye ama la!
Suti kali nyeupe, Viatu vyeusi. Sura ile ile Stan aliyokuwa akiitandika mchana kwa kutumia fimbo kama mtoto mdogo na umati wa watu ukishangilia ndio ilikuwa imeshuka.Ilishuka kimikwara uku mdomoni ikionekana ikivuta sigara na moshi ikiutoa kwa pembeni. Mwanga mkali uliokuwa ukitoka mbele ya gari ndio ukamfanya Stan amuone vilivyo! Ukali!!
“Sara? Sara? kwanini ulinitoroka? kwanini unataka tukutafute wewe tu! wewe tu kila siku?” Aliongea yule mzee uku akiwafuata Stan na Sara pamoja na yule mama msamaria mwema karibu. Yule mama katu hakutaka Sara wala Stan wakamatwe. Roho ya hasira na dukuduku zikamvaa mama msamaria mwema. Uchungu wa mzazi ukamwingia. Akamkumbuka vilivyo mzee yule toka anapigwa na Stan na toka anampeleka Stan polisi. Uchungu wa pesa zake alizotumia kumtoa Stan ndizo zikamuuma mara mbili yake. Akaona endapo atalegeza na kumuacha Stan akamatwe arudishwe tena ndani itamladhimu kufanya tena kazi ya ziada mpaka kumtoa. Kazi ya ziada ya kumaliza tena kiasi kikubwa cha pesa. Hasira zikamvuta zaidi yule mama msamaria mwema mpaka nyumbani kwake anapowekaga pesa katika kibubu chake. Pesa ambazo huwa anazipata kwa shida sana kutokana na biashara yake ya kuuza samaki. Taswira yake yote akaivuta mpaka mbele yake akimtazama yule mzee mkatili. Mkatili na mnyanyasaji kwa wasio na hatia, baba yake wa kufikia na Sara. Yule mama msamaria mwema akamfananisha baba Sara na marehemu mume wake kabla hajafa. Mumewe aliyekuwa ameshindikana kwa ujambazi na uonevu wa kila aina. Mumewe ambaye walimpangia njama wenzake na kumuua baada ya kudhulumiana mali.
Uso wa yule mama msamaria mwema sasa ukawa umetuna haswa. Umetuna kwa hasira kali kwa alichokuwa akikiona mbele yake. Akaikunja mikono yake miwili na kumfuata yule baba yake na Sara wa kufikia kwa madhumuni ya kukutana naye na kupigana naye. Wakakutana!
Baba yake na Sara akaitupa sigara chini nakuisigina. Akamtazama yule mama msamaria mwema mbele yake kwa dharau akimpulizia moshi wa sigara.
“Nani kamtoa huyu kinyaragosi? Wewe? naongea na wewe nani kamtoa?” Aliongea baba Sara kwa sauti ya ukali.
“Mimi ndio nimemtoa?” Alijibu mama msamaria mwema kwa kujiamini.
“Anhaaa!! wewe ndio umemtoa ndio? Sasa nawarudisheni wote watatu mkafie ndani, Pumbavu!” Aliongea baba Sara.
Maneno yale yakamuingiza vilivyo Stan,Sara na yule mama msamaria mwema. Yule mama duku duku lilishampanda zaidi.Dukuduku la kuhakikisha baba Sara amemtia mikononi na kumshugulikia yeye mwenyewe. Alichokifanya yule mama msamaria mwema aliivuta mikono yake nakushika suti ya baba Sara kwa nguvu zote. Akamsukuma kwa nguvu zote. Tiii!! baba Sara akadondoka mpaka chini kabisa. Hasira! baba Sara hakutaka hata mara moja katika maisha yake adharirike mbele ya msichana. Safari hii alikuja akiwa amejipanga. Alijipanga haswaa. Katika mguu wake wa kushoto kulikuwamo na soksi. Na ndani ya ile soksi alikuwa amehifadhi bastola yake. Kitendo cha kuichomoa tu jicho la Stan lkikawa haraka kuiona. Woga!!
“Mama kimbia? kimbiaaaaaa!!” Stan aliropoka kwa sauti ya juu.
Yule mama msamaria mwema hakuweza kuelewa kwanini Stan kaongea maneno yale. hakuweza kuiona bastola ambayo baba yake na Sara wa kufikia alikuwa ameichomoa katika soksi yake ya upande mmoja. Alichokifanya Stan ni kumshika Sara wake kwa nguvu zote na kutokomea kwenye giza. Sara alikuwa mbishi kwa sababu kwanza hakujua wala kuona kitu chochote kinachoendelea kwa baba yake kutokana na upofu aliokuwa nao. Pili hakujua anapoelekea na Stan.
“Stan wapi tunaenda? usinipeleke kwa baba nakuomba?” Aliongea Sara uku mikono yake ikionesha kulowa kwa jasho. Jasho la uwoga!
Kitendo cha Stan na Sara kukatisha kona kwenye giza giza,mlio mkali wa risasi ukarindima kutoka upande ule waliotokea. Wakasimama!!
“Sara” Stan aliita kwa kunyong’onyea.
“Nini tena Stan”
“Mama? mama atakuwa amekufa Sara, mama aliyejitolea kunitoa katika kituo cha polisi” Stan alilalama kwa hasira.
“Stan” Sara aliita.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana Sara wacha mie nirudi. Nakuomba nikukute hapa hapa kaa chini usiondoke tafadhali. Nakuomba tena usiondoke mpaka nihakikishe nimemuweka baba yako kiganjani kwangu, haiwezekani Sara mama afe pasipokuwa na hatia yoyote. Amefanya nini mpaka baba yako ampige risasi?” Stan aliendelea kulalamika.
Alimuacha Sara akiketi chini eneo la pembeni mwa babarabara ya wapitao kwa miguu. Kulikuwa na giza sana kiasi kwamba hata Stan mwenyewe hakuweza kuona mbele vizuri japokuwa alikuwa akiongozwa na mbalamwezi iliyokuwa imechomoza kidogo. Stan akalivua shati lake vizuri nakumpa sara amshikie. Akabaki kifua wazi Stan. Akakimbia kwa kufuata kinjia mpaka katika eneo lile aliokuwa amewaacha mama msamaria mwema na baba yake wa kufikia na Sara. Hapakuwa mbali sana, Stan alikimbia kidogo na hatimaye akawa ameshafikia eneo lile.
“Mamaaaaaa!!! mamaaaaa!!!” Stan aliita kwa sauti ya juu baada ya kulifikia lile gari alilokuwa ameliacha. Gari la baba yake na Sara. Gari lililokuwa limepaki na kuwasha taa zote. Stan aliita kwa sauti baada ya kutokumuona mtu hata mmoja zaidi ya lile gari la baba Sara pembeni yake. Haraka haraka uku akihema. Ushujaa!! Stan akafanikiwa kuingia mpaka ndani ya lile gari nakuanza kutazama hapa na pale kama ataweza kumuona baba Sara. Alikuwa ameshajitolewa kwa lolote litakalompata ili mradi aweze kumtia mikononi baba yake na Sara nakuhakikisha anammaliza kabisa.
“Upo wapi mshenzi mkubwa wewe?” Stan aliongea peke yake uku akitupa tupa vitu ovyo kutoka ndani ya gari mpaka nje.
“Stan!! Stan??” Sauti ya kike ilisikika nje ya gari.
Stan kwa haraka haraka alitoka nje ya lile gari mpaka eneo la nje kuangalia sauti inapotokea. Ilikuwa ni sauti ya taratibu sana. Ilipenya ndani ya ngome ya masikio ya Stan na kumfanya avutwe na asijue ni ya nani. Aliifananisha na ya Sara lakini moyo wake ukapingana naye kuwa siyo. Tahamaki!! Stan akatoka mpaka katika lile gari nakuangaza uku na kule. macho yake yakakutana uso kwa uso na mama yule msamaria mwema akimfuata kwa kupitia mbele ya gari kulipokuwa na mwanga wa gari. Stan akamuona vizuri. Yule mama alikuwa akitetemeka sana uku mikononi akiwa amejawa na damu nyingi sana. Mikono yake ilikuwa bado imeng’ang’ana na bastola ndogo aliokuwa ameishika akitetemeka. Stan akaichukuwa ile bastola nakuishika. Mikono yake ikajawa damu nyingi kutoka katika ile bastola. Akajifuta zile damu kwenye suruali yake nakuiweka ile bastola mfukoni kwake. Stan akakaa kwa muda akimtazama yule mama msamaria mwema. Hofu!!
“Mama ume u u uuua?” Stan aliongea kwa kigugumizi.
“Stan?” Aliita yule mama msamaria mwema uku akitaka kumshika Stan. Nguvu zilikuwa zimeshamuishia mwilini mwake. Alijikuta akimkumbatia Stan.
“Stan nime me me mmaliza yuu le ba ba!!” Aliongea yule mama msamaria mwema kwa kigugumizi cha muda. Stan akafurahia ushindi moyoni mwake. Akamshika mama yule msamaria mwema mkononi.
“Sara yupo wapi Stan?” Aliuliza yule mama. Mama ambaye ndani ya muda mfupi alikuwa ameshawafahamu majina wote Stan na Sara.
“Yupo upande wa kule. Twende,twende!” Aliongea Stan.
Waliongozana na yule mama msamaria mwema uku Stan akimshika mkono. Mama ambaye kwa muda huu alikuwa akichechemea kwa kuchoka sana. Alikuwa hajiwezi. Alihema juu juu sana. Alionekana kama mtu aliyehitaji huduma ya kwanza.Walipofika kwenye ka giza giza. Akasimama!!
“Stan? Stan mwanangu?” Aliita.
“Naam mama?”
“Naumia? naumia sana Stan upande wa uku mbavuni” Aliongea yule mama kwa kulalamika.
Stan akautoa mkono wake nakuanza kuupitisha kwenye ubavu wa yule mama. Akakutana na limbi la damu likichuruzika.
“Mama kuna nini hapa?” Stan aliuliza kwa sauti ya juu.
“Mwanangu ni ni ni li pigwa na na risass sis ii..!!” Aliongea kwa kigugumizi.
“Unasemaje mamaaa?” Stan alishangaa.
“Ba ba ba Sa a aa ara ali ni ni piga kwa riii sss aaa ssii!!”
“Na yeye yupo wapi huyo baba Sara?” Stan aliuliza akitaka kujua.
“Nimesha muu uua.. Kafa ri riiik..
Kabla hajamalizia kuongea yule mama akawa ameshakata roho. Stan hakuweza kujua kama ameshafariki. Alijua huenda kazidiwa hivyo amezimia.
“Mamaa!! maamaaa!!” Stan alimtikisa tikisa!
KImya kilikuwa kingi kwa yule mama msamaria mwema. Hakuwa akihema tena yule mama. Stan akiwa katika kumshangaa na kumtikisa yule mama msamaria mwema mara mlio wa gari ukasikika pembeni yake. Taharuki!!
Macho ya Stan yakakutana uso kwa uso na rundo la mapolisi wakishuka na kutanda lile eneo. Wananchi nao wakaanza kujaa eneo lile wakizuiwa na mapolisi. Woga!! Stan akaingiwa na woga wa ajabu. Macho yake yaliendelea kutumbua eneo la mbele yake. Macho yakaona nguo zile zile alizokuwa amezivaa Sara. Alikuwa anatangatanga kwa kurusha mikono kwa kupapasa uku mapolisi wakimsukuma.
“Saraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!” Stan aliita kwa sauti ya juu mkononi mwake akimuachia yule mama msamaria mwema aliyekuwa akimshika nakuelekea mpaka eneo alipokuwa Sara amezungukwa na mapolisi akizuiliwa.
************
Sara aliendelea kupapasa mpaka akalikaribia gari la baba yake pasipo kujua kama ni lenyewe. Akaanza kulipapasa asijue anaelekea wapi na ametoka wapi.
“Binti? Binti?” Aliita polisi mmoja baada ya kumuona akipapasa uku na kule.
“Stan wangu yupo wapi? Stan yupo wapi?” Aliongea Sara kwa sauti ya ukali.
Mapolisi wote wakabaki wakimshangaa Sara kwa jinsi alivyo mbishi pili akipapasa kwa upofu aliokuwa nao pasipo kumuona anayemtafuta.
Stan alikuwa akitembea kwa kuhema sana juu juu. Mikononi alionekana bado kuwa na zile damu damu. Bado hakuwa na hofu yoyote zaidi ya kutaka kumtia mikononi Sara wake ambaye aliamini kabisa kaondoka katika ile sehemu ambayo alimwacha awali kabla hajamfuata kumuangalia mama msamaria mwema.
Uso wake ulikuwa katika hasira kali. Alimfikia Sara,Sara aliyekuwa amezungukwa na mapolisi. Ujasiri! Stan hakuogopa kitu chochote zaidi ya kuingia kati kati ya mapolisi. Hakujali hata damu alizokuwa nazo mikononi na kwenye suruali yake. Kitendo cha kumfikia Sara tu wale mapolisi wakawa wameshamuona Stan. Wakaonesheana ishara kama kushtuka kwa kitu. Wakaangaliana wenyewe kwa wenyewe. Wakamuangalia tena Stan kwa jinsi alivyokuwa akihema juu juu.
Mmoja kati ya wale mapolisi akamuwahi nakumshika Stan mkono kwa lengo la kumzuia. Kimuhemuhe!!
“Namtaka Sara wangu? Saraaa!!” Stan aliita kwa sauti ya ukali baada ya kushikwa mkono na yule polisi.
“Stan?” Sara naye aliita.
Roho ya Stan tayari ilikuwa imeshaingiwa na ubaridi mkali. Uvumilivu kwa Stan ulikuwa mdogo sana baada ya kuzuiliwa na yule polisi.
“Damu hizi unatoka nazo wapi sasa hivi wewe kijana?” Alihoji polisi.
Kabla Stan hajajibu kitu sura yake ikakutana moja kwa moja na yule afande wa kituoni ambaye alipokea rushwa kutoka kwa mama msamaria mwema kwa lengo la kumtoa Stan. Alikuwa akija haraka na mwenzake katika lile tukio pale akidhani huenda Stan kafanya balaa baada ya kumwachia huru.
“Bwana mdogo vipi tena?” Aliita yule Afande alipowafikia karibu.
Mapigo ya moyo ya Stan yakaanza kubadilika kutoka taratibu na kuwa mwendo kasi. Aliona sasa anaweza kumpoteza Sara wake muda wowote.
“Afande nilimsahau huyu hapa mwenzangu tulipotezana hapo mbele!” Alijitetea Stan akitetemeka.
“Na mama yako yule yuko wapi?” Aliuliza Afande.
“Mama! ma ma maa yupo yupo kulee” Stan aliongea kwa kigugumizi.
Hapo hapo yule Afande akaonekana kuwa upande wa Stan. Akaongea na wenzake wale aliowakuta pale kwenye doria la mapema baada ya kutokea yale mauaji. Hawakuwa mapolisi wa kituo kile cha jirani wala maeneo yale bali walikuwa ni mapolisi wa doria wale wanaozungukaga na gari maeneo mbali mbali ya jiji. Baada ya muda Stan alikabidhiwa Sara wake pasipo kushtukiwa chochote. Katu Stan hakuweza kuamini kama ameepuka kutoka katika mikono ya wale mapolisi. Akili yake yote na hofu vilikuwa juu ya ile bastola ambayo alihifadhi katika mfuko wa suruali yake. Alimshika mkono Sara akitetemeka mikono.
“Sara ni mimi Stan twende” Aliongea Stan kwa sauti ya chini chini.
Sara aliposhikwa tu mkono na Stan zile hisia zikamjia katika mwili wake. Akalitambua kuwa ni lazima atakuwa Stan licha ya sauti iliokuwa ikitoka katika kinywani mwa Stan.
“Stan tunaenda wapi na mama yule yupo wapi?” Aliuliza Stan.
Stan alisogeza mdomo wake karibu na masikio ya Sara kisha akamnong’oneza pasipo kujua wale mapolisi.
“Yupo nimemuacha kule twende tu Sara wangu”
Mwendo wa nusu saa ulimtosha kabisa Stan kujikongoja mpaka nyumba ya jirani. Alikuwa hoi hajiwezi kwa yaliotokea. Nyumba aliokuwepo alikuwa hata haifahamu ni kwa nani. Waliingia kwa kuomba msaada. Kitendo cha kugonga tu hodi walipokelewa vizuri tofauti na walivyofikiria. Stan akawa ni mtu wa kueleza kwa yaliotokea. Akawaomba hifadhi ya yeye na mwenzake Sara waweze kulala japo kwa siku halafu itakapofika asubuhi waweze kuondoka.
Yule mzee mwenye nyumba na familia yake walikuwa wakarimu sana. Waliwahudumia Sara na Stan kwa kuwapatia chakula. Wakiwa sebuleni katika kupata chakula walianza mazungumzo na yule mzee mwenye nyumba.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Umesema wewe unaitwa Nani?” Aliuliza yule mzee.
“Naitwa Stan na huyu hapa pembeni yangu ni Sara” Aliongea Stan kwa kutetemeka uku akishika kijiko kwa kula chakula na pia kumlisha Sara.
“Mtoto wa nani?” Aliendelea kuuliza yule mzee.
“Ni mtoto wa baba Devotha” Aliongea Stan kwa kujiamini safari hii akiendelea kula.
“Baba Devotha? Baba Devotha wa kule mtaa wa pili?” Aliuliza.
“Ndio baba Devotha”
“Shit wewe ndio Stan? ama kweli! yaani umekuwa mpaka nimekusahau mwanangu? Mimi na baba Devotha tulikuwaga marafiki wa muda mrefu sana toka nikutoke lakini kukatokea mafarakano hatukuweza kupatana mpaka leo hii. Alisababisha nikamchukuia moja kwa moja na hata tukipishana naye kwenye mchezo wa bao huwa hatusemeshani. Mpumbavu sana yule mzee!” aliendelea kuongea yule mzee.
“Enhh kwani ilikuwaje na baba Devotha kukosana?” Stan aliuliza kwa utani akitaka kujua.
“Ujue mwanangu! wewe kidogo ungekuwa mwanangu sasa!”
Stani alishtuka kwa kuwa na sintofahamu. Kiwewe!! Hakuelewa kuwa kwanini yule mzee ameongea maneno yale.
“Bado sikuelewi mzee kwanini?” Aliuliza Stan.
“Wakati ukiwa mdogo mimi na baba yako baba Devotha tulikuokota wewe enzi hizo tulikuwa tukiishi kibaha hukoo? tukakupeleka kwa mchungaji kuombewa. Ulitusumbua sana Stan. Ukapona na kila mmoja akawa anakung’ang’ania kuishi na wewe”
“Ilikuwaje mkaniokota” Aliuzila Stan.
“Kwani baba yako,baba Devotha hakuwahi kukuambia kuhusu kuokotwa wewe?”
“Hapana! Hapana yeye baba alivyoniambia kuwa baba na mama yangu walipataga ajali mbaya ya meli wakazama na abiria wengi hawakuonekana tena mpaka leo.”
Mzee yule akaangua kicheko cha haja kisha akamshika Stan bega.
“Kijana wewe tayari ni mtu mzima kabisa. Baba yako yule baba Devota ni muongo sana na ndio alimlaghai mke wangu na kumpa mimba mpaka sasa unavyomuona mke wangu yupo kijijini kwao na sijui kama alijifungua au la! sitaki kumuona kaniaibisha sana! Wewe Stan tulikuokota katika gari moja hivi lililoonekana limetokea Kenya kutokana na namba za gari zilivyoonesha”
“Kwa hiyo baba na mama yangu wako wapi?” Stan aliacha kula wala kumlisha Sara na sasa akili akawa ameihamishia kwa yule Mzee.
“Tulirudi kuangalia kwenye lile gari usiku ule ule lakini kilichotokea yaani ilikuwa ni kama miujiza.” Aliongea yule mzee akitikisa kichwa nakuinamisha chini kwa muda.
“Miujiza? Miujiza ipi tena?”
“Tuliwaona wazazi wako wakitoka uchi wa mnyama na kukimbia kusikojulikana uku wakiongea maneno mara Kakamega mara sijui Dadamega sijui walikuwa wakimaanisha nini. Tulijaribu kuwakimbiza watu wakawashika tukawapeleke mpaka kwa mchungaji aliokubatiza wewe. Mchunganji John akafanikiwa kuwatoa mapepo kibao”
“Wako wapi sasa?”
“Usiwe na papara. Yale maombi ya mchungaji John hayakusaidia kitu kwani mpaka sasa bado wamekuwa ni vichaa walioshindikana katika soko kuu la mbezi”
Stan aliinamisha kichwa chake chini nakutoa machozi. Machozi ya uchungu baada ya kuvuta kumbukumbu nakukumbuka vichaa wawili waliokuwa wamezoleka sana katika maeneo ya sokoni Mbezi. Moyo wa Stan ukaingiwa na ganzi ya muda. Akahaidiana na moyo wake iwe isiwe akiamka asubuhi kazi ni moja kuhakikisha mama na baba yake wamekuwa mikononi mwake.
“Lazima niwapate hiyo kesho!” Aliongea Stan akimuangalia yule mzee kwa jicho la uchungu
*******
Pilika pilika ziliendelea na kila mmoja alionekana kuwa bize kwa kazi alizokuwa nazo. Wanawake wengi walikuwa na vitu kichwani mwao wakionekana kuelekea maeneo ya soko kuu. Wale waliokuwa na biashara za kuuza mitumba walifanikiwa kuwateka wateja wao kwa mzunguko wakiwauzia mitumba mbali mbali na hata wengine wakirusha kwa dau. Upepo ulizidi kuwa mkali sana. Kuna wengine walionekana kujikunyata, ni mama mmoja tu aliyeonekana kuzoeleka eneo hilo kwa kila mara alionekana na chizi mwenzake wakiume wakiokoteza mabaki ya vyakula na hata wakati mwingine kuwatisha wateja waliokuwa wakija kununua mahitaji mbali mbali sokoni. Walikuwa ni vichaa ambao kidogo walionekana kuzoeleka katika eneo la sokoni kwani kila baada ya miaka mitatu hadi mitano huwa wakionekana na wakati mwingine hukaa miaka miwili au mmoja kutokuonekana kabisa.
“Wameanza tena?” Aliropoka mmoja wa wafanyabiashara baada ya kuwaona tena.
“Nani?”
“Wale wale vichaa wapendanao, wale misukule wakutusumbua na kutuharibia biashara zetu. Wameanza tena!” Aliongea mfanyabiashara mmoja kwa kulalamika.
“Wallah safari hii wakisogelea meza yangu namtikisa mmoja kwenye shingo nachinjilia mbali?”
“Sio wewe tu hata mimi mara ya mwisho nilishangaa kupiga hesabu ya mauzo sina hata kumi. Lazima watakuwa hata chuma ulete wale” Alimaliza kuongea mmoja wa wafanyabisashara akimwambia mwenzake.
Wale vichaa hawakusikia lolote zaidi ya kuongozana pamoja mpaka ndani ya soko katika mabanda ya sokoni nakuanza kupita huku wakifanya vituko mbalimbali. Kuna waliokuwa wakifurahia vituko vyao kwa kuvizoea na hata wengine kuchukia kutokana na kuwatibulia wateja wao kwa kuwaogopa jinsi walivyo na mavazi yao.
“Ennnh tokeni fasta fasta sitaki kuwaona humu ndani?” Aliongea mmoja wa wafanya biashara akiwafukuza wale vichaa waondoke zao.
Wale vichaa hawakutaka kamwe kusikia lolote. ndio kwanza walikuwa kama wamechochewa kufanya vituko. Mmoja wao wa kike aliinama chini na mwingine wa kiume akawa kwa upande wa juu akikatika kwa kucheza na kuimba maneno kwa sauti ya juu akipiga makofi. Walizidisha kelele kiasi cha kufanya wafanya biashara waliokuwa na moyo mwepesi kuwafukuza. Vita vikaanza kati ya wale vichaa na wafanyabiashara wa sokoni. Wakaanza kuwatupia maneno sambamba na kuwanyooshea mifagio na hata wengine wakiwatisha kwa kuwatukana ili mradi waweze kuondoka katika eneo lile.
“Nyie ni kina nani mpaka mtufukuze? si twaongea na ninyi?” Aliongea yule chizi wa kiume.
Waliendelea kuwa wabishi sana hali iliyosababisha wafanyabiashara ndani ya soko kujikusanya na kuwatimua kwa kutumia nguvu. Wale wafanya biashara nao waliokuwa nje ya soko wakilangua mitumba nao wakaunga hoja. Wakawa msafara mmoja na wafanya biashara wa ndani ya soko. wakaungana! wakaanza kuwatimua wale vichaa na hata wengine kudiriki kuwafukuza kwa kuwatupia mawe na makopo. Wakaondoka zao!
“Mamaaa maamaaa?” Sauti iliita kwa juu zaidi.
Wakabaki wakiangaliana wale vichaa nakuicheka ile sauti iliyokuwa ikiwaita.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mamaaaa!!! Baaa baaaaa!” Sauti ile iliendelea kuita na sasa hivi ilikuwa imewasogelea kwa ukaribu. Alikuwa ni Stan akiwa na Sara amemshika mkono kwa kumuongoza.
*****************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment