IMEANDIKWA NA : ANDREW CARLOS
*********************************************************************************
Simulizi : Niache Na Moyo Wangu
Sehemu Ya Kwanza (1)
Waasi wa kundi la M23 la kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo walikuwa wakiendelea kushindana na Jeshi la FRDC la nchini Congo lakini ilishindikana. Umoja mataifa nao haukuwa mbali nao. Walisumbuana nao sana kwa kipindi kirefu.Walijitahidi sana kuweka amani lakini M23 ilizidi kuwachefua zaidi. Waasi hawa walizidi kuwa mwiba mkali kila kona. Walikuwa na mbinu nyingi sana. Mbinu za kuingia nchi yeyote kimya kimya na kufanya watakavyo. Safari yao ya kutoka Congo mpaka pembezoni mwa nchi ya Uganda, Bunagana iliwezekana kwa asilimia mia. Ngome ya Bunagana yote ilikuwa chini yao. Walijidai kwa kufanya watakavyo,kuteka na hata kuua watakavyo. Waliweka kambi kubwa Bunagana kwa muda. Siku,wiki mpaka miezi ilisonga wakiwa Bunagana na mateka chini ya mia moja.
Butiliasi,kiongozi wa waasi wa M23 kamwe hakutaka mchezo katika kazi yake. Hakutaka kuona wafuasi wake wakilazia damu mwili wa binadamu ama kukamatwa wao wenyewe. Furaha yake kuu ilikuwa ni kuhakikisha umekuwa mfuasi wake kama mateka ama umeuliwa kama hutotaka. Ndivyo maisha yake yalivyo toka alipokuwa mtoto wa miaka kumi na mitano na kufanikiwa kumuua baba yake mzazi nchini Congo kwa kumchoma kisu tena bila kujali kisu hicho hcho akakimalizia kwa mama yake mzazi na kisha kutoroka na kutokomea kusikojulikana. Butiliasi alikuwa katili kupindukia. Ubabe wa haja! Mwili wa haja! Nguvu ya haja! Umbishie nini Butiliasi kama hajakutoa utumbo. Uonevu wake ulimfanya kuwa bora, waasi wenzake walimteua kama mkuu wa kikundi chao cha M23. Alipokenua kwa ukali walikaa kimya! Butiliasi ndiye aliyetoa wazo la kutorokea Bunagana,Uganda na kuweka kambi na waasi wenzake.
Giza liliendelea kutanda kuashiria usiku unaendelea. Muda wote Butiliasi alikuwa kama mtu mwenye machale. Usingizi kwake haukuwepo, kila muda alihisi masikio yake kuwa na miito ya risasi zikipishana. Tangu walipoweka kambi Bunagana hali kama hiyo haikuwahi kumtokea. Uzalendo ulianza kumshinda.
“ Hooo, inze bhazee!!” Butiliasi aliongea kwa ukali na wafuasi wake akimaanisha waame kambi.
“Nzooo dee maaa!!” Waliitikia wafuasi wake.
Wakazikoki silaha zao tayari kwa mapambano muda wowote. Wakawapakiza mateka wao kutoka mpakani mwa Uganda na wengine waliowachukuwa nchini mwao Congo.Butiliasi akaingia siti ya mbele. Nyuma wakajijaza wafuasi wake na mateka ndani ya lori kisha wakalifunika kwa turubai. Safari ikaanza ya kutoka Bunagana kuelekea Nairobi kupitia Kabale. Njia nzima Butiliasi alikuwa hana amani. Alijihisi kama kuna kitu kikinyemelea katika moyo wake uliozungukwa na ukasi wa maisha. Mwendo wa kama masaa manne mvua ya manyunyu ilianza kushuka taratibu kutoka katika anga. Manyunyu yale yalizidi kasi nakuwa mvua kubwa. Wenge! Butiliasi akamwamuru dereva azidishe mwendo zaidi. Dereva wa waasi naye akafanya hivyo. Lori likazidi mwendo. Kuna wakati liliyumba na mateka kupiga sana kelele nyuma ya lori. Butiliasi hilo hakulijali. Alizidi kumsihi dereva akanyage mafuta zaidi kwani alihisi eneo lile ni la hatari ana endapo watasimama itakuwa rahisi kushikwa. Baada ya mwendo tena mrefu lile lori lilimzidi dereva nguvu. Lilimyumbisha! Dereva wa waasi alijitahidi kulirekebisha kwa woga akimwogopa Butiliasi pembeni yake lakini haikuwezekana. Likaenda kugota katika mti mkubwa. Taa zote na shepu ya mbele ikawa imeharibika. Nyang’anyag’a! Butiliasi akapumua kwa muda huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini. Akakiinua kile kichwa kisha akamtazama dereva kwa jicho la ukali. Akalivuta gobole lake kwa pembeni nakulikoki vizuri. Hasira! Akamlenga dereva kichwani na kuachia kishikio. Papo hapo mlio mkali wa gobole ukatanda na kilichofutia ni vipande vya nyama nyama ya uso wa dereva na nyama nyama za shingoni ndizo zilizobakia. Butiliasi akafungua mlango wa mbele wa lile lori kisha akashuka ndani ya lori.Taharuki! alishangaa kuona lori likivuja mafuta nakuelekea nyuma walipokuwa wafuasi wake.
“ Mpumbavu, pumbavu sana!” Butiliasi aliongea kwa ukali peke yake.
“ Nani tena bosi”
“ Dereva, Dereva yetu”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haraka haraka Butiliasi aliingiza mkono mfukoni mwake nakutoa kitochi kidogo. Alitumia mkono wake mmoja kulifungua lile turubai nakuchungulia kwa ndani kujua mateka wake wanaendeleaje.
“Hakuna iliyekufa?” Butiliasi aliuliza.
Mateka karibia wote walijikuta wakishindwa kutamka kwa mdomo. Walitikisa vichwa vyao kana kwamba hakuna tatizo lolote. Butiliasi aliwaita wafuasi wake wote wakamzunguka. Akanong’ona!
“Mambo imeharibika hapa, Dereva bazee kashaharibu kila kitu”
“Lakini Buti, mie na wazo!” Aliropoka mmoja wa waasi.
“Wazo lipi hilo”
“Lori letu si zima linatembea?”
Butiliasi hakutaka kupoteza muda. Alihisi swali hilo linamzidishia hasira wakati tanki lote la mafuta linaonekana kabisa likiwa chini na mafuta yakimalizikia kumwagika. Butiliasi alimwangalia tena mara ya pili yule mfuasi wake. Akakitupa kile kitochi chake na kulitoa gobole lake kwapani. Akalikoki na kutaka kuiachia ili amuue yule mfuasi wake. Akiwa bado katika kuikoki. Mara mwanga mkali wa gari ukaangaza eneo waliopo. Mwanga ule ulizidi kuwa mkubwa ukiashiria kuna gari kubwa linakuja. Butiliasi akaachana na swala la kutaka kumuua mfuasi wake kwa gobole. Akili yake ikamuhama. Alijihisi sasa zama zake za kukamatwa zinaenda ukingoni. Wafuasi wake mmoja baada ya mwingine waliaanza kukimbilia ndani ya lori. Butiliasi naye alitamani sana akimbilie ndani ya lori lakini tayari lile gari lilikuwa limeshafika karibu yake. Likasimama!
***********
“ Nimesema jisalimishe mwenyewe pumbavu” Aliongea mmoja wa watu waliokuwa wamevalia sare za kiaskari. Muda wote Levina alikuwa hajitambui. Kojo zito lilikuwa limeshachukuwa sura mpya ndani ya nguo yake ya ndani mpaka ya nje. Mchirizi wa kojo la moto moto ndio ulichochea zaidi hofu kwa Levina. Akili yake ilishakata tamaa kwa kuwa mikononi mwa watu asiowafahamu.
“Jamani polisi kwani nimefanya kosa gani mimi” Levina alizidi kugumia.
“ Twende uko, pumbavu”
Yule askari aliyevalia sare za kipolisi alikuwa mkali sana. Alimvuta Levina kutoka katika banda la kuhifadhia mbwa. Alimchukuwa mkono wake na kumvuta kwa nguvu zote. Levina hakuwa na msaada tena wowote wala kujua nini kinaendelea. Magongo yake yaliokuwa yakimsaidia kukokota mguu mmoja aliokuwa amebaki nao hayakusadia tena. Alijikuta akiburutwa mpaka eneo la nje kabisa. Yule askari bado alizidi kuwa mkali pale Levina alipoleta ubishi. Levina alizidi sana kulia. Alikata tama!
Askari yule hakuwa na hata chembe ya huruma. Alizidi kumburuta Levina kutoka naye mpaka nje ya geti.
Levina alilia sana mpaka kukaukwa na sauti. Macho yake yalikosa kabisa ushirikiano.Vumbi la chini alipokuwa akiburutwa lilisalimiana na pua na hata macho yake. Alijihisi kama amemwagiwa pilipili usoni. Alipikicha sana macho kwa mkono wake mmoja. Macho yake yakapata upenyo. Yakapenyeza! Aliweza kuuona mwili wa Gervas ukiwa chini. Ulikuwa umetapakaa damu nguo zote. Gervas alikuwa tayari ameteketezwa kwa risasi na hao hao watu waliokuwa wamevalia nguo za kiaskari.
“ Gervassssss” Levina alipiga wangwi kwa nguvu zote.
Haikusaidia kitu zaidi ya yule askari kumburuta hivyo hivyo levina akiwa na mguu mmoja na kumpakiza ndani ya gari lao la kipolisi. Kitendo cha Levina kuingia tu kwenyelile gari ya kipolisi ghafla alishangaa macho yake kukutana na kundi la wenzake wakiwa wamefungwa kamba mikononi mwao. Kamba mikononi na miguuni. Walionekana kulia kwa Vikwifukwifu. Levina alishindwa kujizuia. Alijikuta akidondoka mpaka chini nakuzimia.
******
Mwendo wa masaa kumi Levina alikuwa bado amezimia. Maumivu makali maeneo ya mguu wake mmoja ulipokuwa umekatwa ndiyo yaliomchochea kushtuka.. Giza lilikuwa limeshatanda sana na manyunyu yalikuwa yakiashiria kuna mvua nje. Levina hakuweza kumtambua mtu yeyote mule ndani ya lile gari kutokana na kutanda giza pana ndani yake. Harufu za damu na vumbi vumbi ndizo alizihisi puani mwake. Levina alishangaa mikono yake kuwa huru. Haikuwa imefungwa kwa kamba. Taratibu alichukuwa mkono wake mmoja nakuanza kupapasa maeneo ya pembeni yake. Kila alipokuwa akipapasa alijikuta kugusana na miili ya watu. Aliendelea kupapasa zaidi. Miguno ya watu ndiye iliojibu kichwa cha Levina kuwa wako hai. Akiwa bado katika kuangaza uku na kule mara alishangaa tochi ndogo kuwashwa ndani ya lile gari. Levina alishtuka! Hofu! Jasho likamjia ghafla na macho kuyatoa.
“Ipo amuka bebe bhana nani vile, mutu ya dar?” Aliongea kwa mashauzi yuke askari.
“ Nyie kina nani, na mnatupeleka wapi?” Levina akajibu kwa ukali.
“Sisi? Sisi hapana kosa, kama mutu kuwa na makosa siyo sisi” Alijitetea.
Kichwa cha Levina hakikuwa sambamba kabisa na masikio. Sauti aliweza kuitambua ni kati ya watu watokao nchini Congo lakini hakulijua lolote iweje wamchukuwe tena kwa kumtesa kiasi kile. Pili iweje wameingia nchini tena wakiwa na sare za mapolisi wa kitanzania. Na tatu yeye na wenzake wanapelekwa wapi na kufanyeje?
“ Nawauliza nyie kina nani?” Levina aliendelea kuhoji kwa ukali.
Yule askari hakuwa na msalia mtume hata kidogo. Ndani ya muda mfupi alikuwa ameshachoshwa na maswali ya Levina. Alichukuwa kitako cha gobole lake na kumpiga Levina maeneo ya usoni.
“Subiri ufike ndio utajua waenda wapi, mbuzi wee tena yule mwenye mukia murefu!”
Ilimladhimu Levina kuendelea kukaa kimya asijue muafaka wake. Aliyasikilizia maumivu ya kile kitako cha gobole kimya kimya usoni mwake. Akatulia kwa muda! Taaratibu Mawazo yalianza kumjenga tena katika himaya ya kichwa chake. Mawazo juu ya maisha yake. Aliwakumbuka sana Jamila na Gervas. Kamwe hakuamini kama kuna siku atakuja kuwapoteza maishani sana sana Gervas. Alihisi kama ni ndoto kwa yeye kushuhudia Gervas akiuliwa mbele ya macho yake. Machozi yalianza kuchukua nafasi yake.
“Noo Noo Gervas usife, muacheni jamani muacheniiiiii”
Levina alikuwa kama nusu chizi nusu timamu. Alijikuta akitoa makelele mengi sana mule ndani ya lile gari. Askari yule yule aliyempiga mara ya kwanza alichukuwa tena ubavu wa gobole lake na kumpiga nalo Levina lakini bado Levina alikuwa mbishi. Alimkanyaga kwa mateke eneo la mguuni kwa Levina ambapo palikuwa pamekatwa, bado ndio kwanza alikuwa akizidisha kelele kwa Levina. Gari lote na njia yote Levina alikuwa amezua tafrani kwa vurugu zake. Aliwasumbua sana.
“Gervas wangu mumuue nyinyi na mimi mnanipeleka sipajui, bora mniue tu, niueni?”
“Weye mutoto ya bongo nasemaje?”
“Niueni, si mnaitaka roho yangu? Ichukueni sasa?”
Ndani ya masaa takribani matatu ndipo Levina alitulia tena baada ya yule askari mwingine mmoja kutoa sindano katika sare yake ya kiaskari na kumchoma nayo Levina. Usingizi wa haja ukampitia Levina. Akaacha kelele.
Safari ilizidi kusonga na sasa lile gari lilikuwa likikatiza njia panda ya himo kuelekea kambi ya Tarakea huku malengo yao makubwa yakiwa ni kuibukia Kisoro wakipitia njia ya Kabale. Kitendo cha kuingia tu kambi ya Tarakea, askari wa zamu wa mpakani wakasimamisha lile gari. Wakatoa tochi na kuanza kumulika kuanzia mbele kwa dereva.
“Nyie mapolisi wa Tanzania?” Aliuliza mmoja wa askari wa Tarakea.
“Ndio”
“Vitambulisho vyenu viko wapi kuonesha kuwa ni askari? Na mnaelekea wapi usiku huu?”
Yule askari wa Tarakea alikuwa amechezwa na machale. Kabla hajamaliza kuuliza tu alishangaa mtu kutoka ndani ya ile gari nakumuwahi sindano ya shingoni. Hajakaa sawa yule askari aliyekuwa akibishana na Levina mara kwa mara akalikoki gobole lake nakusambaratisha lile eneo la kambi ya Tarakea. Wakafanikiwa! kilichofuata waligongeana mikoni ishara ya kupongezana kisha wakanyoosha silaha zao juu na kuendelea na safari yao.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haikuwachukuwa muda mrefu sana matone ya mvua yakachukuwa nafasi yake tena. Mvua ikaanza kunyesha na kwa safari hii ilikuwa ni mvua haswa. Dereva akaliwasha gari lao mwanga mkali kuweza kuona mbele. Waliendelea kusonga taratibu kuhofia kuyumba ama kuteleza kwa gari yao kutokana na lami kuwa mtelezo sana.
“ Don, Don, luku, luku Yule si bosi”
Askari mmoja wapo alikuwa tayari ameona kitu mbele ya macho yake. Lori kubwa kiasi lilikuwa limepoteza uelekeo. Lilikuwa limegota pembeni na baadhi ya watu kushuka wakiwa na silaha.
“Is it Butiliasi? Our Boss?” (Yule ni Butiliasi? Bosi wetu?) Aliongea yule askari kwa kustaajabu.
“ Yeah, but tulipanga tuwakute tulipowaacha Bunagana, why?” Alilalama.
Walisogea mpaka eneo la karibu kisha wakaendelea kuwasha taa zaidi nakulisimamisha gari lao. Walistaajabu wenzao wakikimbilia nyuma ya lori na hata Butiliasi mwenyewe kunyosha mikono juu kuonesha ishara ya kujisalimisha. Wale askari wakashuka ndani ya lile gari lao. Wakasogea mpaka eneo alipo Butiliasi.
“Our boss?”
Butiliasi alistuka. Akatoa kicheko cha kujiachia.
“Osward, Osward? Wajua bhana nyie muko zoea mitani mingi!”
Butiliasi alijichekesha baada ya kugundua kuwa walikuwa ni wafuasi wake aliokuwa amewatuma waende tanga na Dar es salaam kuchukuwa mateka wengine kisirisiri.
“ Hii gari ya mupolisi na hizo minguo iko pata wapi Osward” Butiliasi alihoji.
Osward alijichekea kimoyomoyo kisha akamtazama mwenzake aliyekuwa naye amefoji nguo za kiaskari wakitanzania. Wakapeana mikono.
“Siye toto janja ya mubongo” Wakamjibu Butiliasi.
**************
“Ahhhaaa haaa haaaa” Butiliasi aliachia cheko cha dharau.
“Sasa mie bamutu mubishi huwa sipendelei, mukaza ya dereva nimefirigisa, kwisha”
“Buti? Namuchinjia baharini?” Alihoji muasi mwenzake.
Butiliasi akaitikia kwa kichwa na kilichofuata nikuhakikisha wamelitoa lile lori nje ya barabara. Hawakuwa na kamba hivyo walichokifanya waliwafungua wale mateka wao kamba kisha waliunga unga na kupata kamba nzito ambayo waliitumia katika kufunga lile lori na upande mwingine kufunga katika gari yao ile ndogo ya polisi ambayo walikuja nao kutoka Tanzania.
Ndani ya dakika ishirini kazi kubwa ilikuwa imeshakamilika ambapo lile lori kubwa lilikuwa tayari ilimeshatoka pembezoni mwa barabara. Lilikuwa katika lami likisukumwa na gari ndogo ya polilsi kutoka Tanzania aina ya one ten. Butiliasi na wafuasi wale aliokuwa amewatuma Tanzania walikuwa wamekaa katika one tena tena siti za mbele huku wale waasi wengine wakiwa sambamba katika lori la nyuma kwa ajili ya kuwachunga mateka wao wasije kutoroka. Safari yao ikaanza kwa kugeuka nakuelekea Nairobi uku malengo yao ni kurudi katika kambi yao ya Uganda,bunagana.
Zile sindano za usingizi alizokuwa amechomwa Levina sasa zilikuwa zimeshakwisha muda wake. Levina alianza kwa kutoa jicho moja uku sura yake akiikunja kunja mithili ya mtu aliyetoka kulala akiamka na uchovu. Alijihisi kichwa chake kizito sana. Mwanga mkubwa wa ndani ya lile lori uliashiria kabisa kumaanisha kuwa kumeshapambazuka.
“Hapa ni wapi?” Alihoji Levina kwa sauti ya ukali.
“Wee mutoto ya bongo umeanza ennh” Alijibu muasi.
Macho yalizidi kumtoka Levina. Fahamu za haraka zilishindwa kumrejea katika kichwa chake. Alibaki akishikwa na butwaa asijue nini kinaendelea. Alijitahidi sana kuvuta kumbukumbu kuwepo eneo lile lakini bado alishindwa kujua. Alijikagua mwili wake kuanzia mikononi mpaka mguu wake mmoja aliokuwa amebaki nao lakini bado hakuweza kuambulia kufahamu chochote. Akageuza kichwa chake na kuwatazama wale mateka wenzake, mateka tofauti wakike kwa waume napo hakujua kitu.
“Gervas wangu yupo wapi??” Aliropoka Levina.
Yule muasi na mateka karibia wote walijikuta wakitoa macho na mshangao kwa Levina. Levina ambaye dhahiri alionesha kuchanganyikiwa kwa kitu. Alijitahidi nakusimama mule ndani ya lori kwa kutumia mguu mmoja aliokuwa amebaki nao baada ya ule wa kwanza kukatwa kwenye ajali kipindi cha nyuma.
“Hivi wewe mutoto ya bongo upewe mukitu gani utulie, musindano haukutoshi siyo?”
“Namtaka Gervas wangu, na mnanipeleka wapi? Nawauliza mnanipeleka wapi..
Kabla Levina hajamalizia kuongea alishangaa kuwashwa kibao na yule muasi.Aliyumba yumba na mguu mmoja kisha alidondoka mpaka chini. Maumivu ya kupigwa kibao ukichanganyia na maumivu ya mguu wake yalihamsha hisia tofauti kwa Levina. Hasira kali zilimtawala. Hasira zile za kipindi cha nyuma. Kamwe Levina hakupenda kuonewa ama kunyanyasika. Alijikuta akishikilia lile gobole la muasi kwa nguvu zote. Yule muasi naye hakutaka kuzidiwa nguvu na mwanamke. Alijikuta akisumbuana na Levina mguu mmoja. Yule muasi hakuwa na mwenzake wa kumsaidia zaidi ya kuwekwa peke yake nyuma na mateka huku waasi wenzake wote wakiwa katia one ten wakiwalinda mateka wengine. Alijitahidi kusumbuana na Levina lakini Levina alimzidi nguvu japokuwa alikuwa na mguu mmoja. Levina alikuwa na unjanja sana pindi ashindanapo na mwanaume. Alichofikiria na moyo wake kilikuwa sahihi sana kumnyong’onyesha yule muasi. Mikono yake miwili aliyokua amebakiwa nayo aliitumia vilivyo kuisogeza mpaka katika sehemu za siri za yule muasi. La haula! Levina alifanikiwa kuzifikia. Akazinyongorota mithili ya bangi linavyosokotwa. Yule muasi akaliachia lile gobole lake lidondoke mpaka chini. Alijihami kwa kushikilia maumbile yake ya sehemu za siri lakini Levina alishikilia zaidi. Makelele ya mateka yalianza kuchochea hisia tofauti ndani ya lile lori. Kwa upande wa yule muasi alijiona kudharirika wakati kwa upande wa Levina alijiona shujaa kupitiliza.
“Shujaaa, shujaaa shujaaa….!!” Mateka wote walishangilia kwa pamoja.
Levina aliachia mkono mmmoja uendelee kumshika yule muasi eneo la sehemu nyeti wakati ule mkono mwingine aliuhamishia mpaka chini na kuchukua gobole. Kilichofuata Levina alichukuwa lile gobole nakulielekeza eneo la sehemu za siri za yule muasi. Yule muasi alijisalimisha kwa kunyoosha mikono yake juu nakufanya umati wa mateka kuendelea kupiga kelele. Kelele za kumsifia Levina. Roho ya huruma ikaanza kumtawala Levina baada ya yule muasi kuvujwa na jasho mwili mzima. Suruali yake ilikuwa imejawa na mkojo ambapo ulikuwa ukimtiririka mpaka chini.
“Shiiiiiiiii” Levina aliwanyamazisha wale mateka kwa ishara ya mdomo.
Mateka wote walibaki kimya wakimtazama Levina. Alichokifanya Levina aligeuka nyuma nakuangalia lango la kutokea ambapo lile lori lilikuwa halipo spidi sana kutokana na kusukumwa na gari ya mbele yao. kisha akamgeukia yule muasi.
“Ninachokitaka ujirushe mwenyewe utoke ndani ya lori hili”
“Mimi, hapana mamaa ya mubongo, hii kitu haifai, mubayaa!” Alijitetea mfuasi.
“Nahesabu mpaka tatu usipojirusha nakupasua sasa hivi” Levina alimfokea.
Yule muasi aliogopa kifo cha kupigwa na gobole. Hakuwa tena na ujanja zaidi ya kuelekea mpaka katika mlango wa lori na kujitupa nje. Alibiringita kwenye lami mara nyingi sana uku lile lori likiendelea kwa mwendo. Muda wote Levina alikuwa akimnyooshea ishara ya kumlenga endapo atarudi kudandia lile lori. Na hapo ukawa mwisho wa yule muasi.
“Oyeeeeeee” Levina alinyoosha gobole lake juu kushangilia ushindi na wale mateka wengine.
Walijihisi wamekuwa huru baada ya kumtupa yule mfuasi mmoja.
“Bado ile ya kule” Aliropoka mateka mmoja wapo akimwambia Levina.
Kabla hajamalizia tu mara wakashtuka kusimama kwa lori lao. Hofu ikazidi kutanda. Mateka wote macho wakayalekezea kwa kwa Levina maana tayari walimuona kama ndio mkombozi wao. Mkombozi baada ya kumuondoa yule mfuasi aliyekuwa akiwasimamia. Kimya kikatawala ghafla na sauti kwa mbaali walianza kuzisikia. Sauti ile ilizidi kuwa kubwa kuonesha ishara kuwa mtu wale wamefika karibu. Alichokifanya Levina aliwaoneshea ishara ya mkono wale mateka kuwa watulie kisha alifungua mlango wa kutokea nakajificha nyuma ya mlangoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bana jese, Jese?” aliongea mmoja wa wafuasi aliyekuwa amekaa kwenye gari la mbele na Butiliasi.
Aliingia moja kwa moja mpaka kwenye lile lori akiwa na hasira huku akimwita mwenzake walikuwa wametoka naye Tanzania kuchukuwa mateka. Kitendo cha yule mfuasi kuingia tu ndani ya lile lori.
“Jese, Jese” Aliendelea kuita yule mfuasi. Hakuweza kumuona huyo mfuasi mwenzake zaidi ya wale mateka kumtizama kwa macho ya huruma. Alichokifanya yule muasi alitoa sauti kali.
“Butiiii, butiiiiii!!” Aliita yule mfuasi akimaanisha anamuita kiongozi wake Butiliasi.
Levina taratibu alitoka nyuma ya mlango wa lile lori na hapo hapo aliinua lile gobole lake nakumnyooshea yule mfuasi. Yule mfuasi alibaki hajielewi.
“Ole wako ukipiga makelele nakupasua hapa hapa?” Aliongea Levina kwa sauti ya kibabe huku akiwa amesimama kwa kutumia mguu mmmoja. Yule mfuasi alikuwa mtii baada ya kugusishwa gobole maeneo ya kichwani mwake. Aliinamisha kichwa chini na mikono yake yote miwili aliielekeza juu kuashiria kuwa amesaliti amri. Levina hakutaka kuchelewesha muda hata kidogo alichokifanya.
“Haya toka, toka ongoza nje mwenyewe, na nyie wengine wote nifuateni” Aliamrisha Levina.
Wale mateka wote wakatoka ndani ya lile lori. Levina alikuwa mstari wa mbele huku akiwa amemshikia gobole eneo la kichwaani yule mfuasi na kushuka naye mpaka chini. Kitendo cha kushuka naye tu mara wafuasi wengine watatu wakiongozwa na Butiliasi wakawa wameshafika.
“Na nyie chini, chini nimesema?” Aliongea Levina kwa kujiamini. Wale wafuasi walitaka kuleta ubishi lakini Levina alizidisha ukali na kuamua kumuua yule mfuasi mbele ya macho yao. Yule mfuasi akadondoka mpaka chini na kutapatapa akimaanisha anakata roho kisha kimya kikatawala. ndipo Butiliasi na Wenzake ikabidi watii amri ya Levina kuchuchumaa mpaka chini.
“Hapa ni wapi? Nani anapajua hapa??” Levina aliongea kwa ukali uku akiwaangalia wale wafuasi pamoja na baadhi ya mateka wale.
“ Eneo lote hili linaitwa Kakamega na hapo mbele kuna msitu mkubwa sana unaitwa msitu wa Kakamega” Aliongea mmoja ya mateka kwa kutetemeka.
Levina aliweka huruma yake pembeni kwa muda na alichoikifanya. Aliwageukia wale mateka.
“haya watano watoke hapo na kufungua kamba ya hilo hapo lori haraka haraka sana” Aliamrisha Levina akiwaambia wale mateka.
Ndani ya muda mfupi wale mateka walikuwa tayari wameshafungua kamba kutoka katika lile lori. Walikua tayari wameshamfikishia Levina.
“Haraka haraka nataka muwafunge hawa waasi na ole wake muasi yeyote alete ubishi namtoa utumbo hapa hapa” Aliongea Levina kwa sauti ya kibabe.
Wale mateka walifanya hivyo tena ndani ya muda mfupi na walipomaliza Levina aliwasihi waelekee katika gari lile ndogo (One ten) na walipofika waliwapakiza wale waasi na wale mateka waliobaki waliobaki walibanana ndani ya gari ndogo. Levina na wale waasi waliokuwa wamefungwa kamba walikaa mbele kabisa na Levina. Levina alichukuwa gobole lake na kuliweka pembeni. Alishika ufunguo wa gari uliokuwa umening’inia katika msteringi na kuliwasha gari. Gari likagoma kuwaka, alijaribu mara tatu nne lakini gari ilibaki hivyo hivyo. Eneo la kuonesha kipimo cha mafuta lilionesha alama nyekundu likimaanisha gari halina mafuta.
“Shiiit!!!” Levina alipiga msteringi kwa hasira.
Muda wote Butiliasi alikuwa pembeni ya Levina akicheka kwa dharau uku mikono yake iliyokuwa imefungwa kamba nene ikiwa inataka kudumbukia katika mfuko wa suruali yake. Aliilazimisha kuingiza mfukoni pasipo Levina kujua chochote. Ndani ya muda mchache Butiliasi alifanikiwa kuvuta kiberiti cha gesi cha kuwashia sigara. Akacheka tena kwa dharau.
******************************
Butiliasi alizidisha kucheka hali iliyomfanya Levina amgeukie kumuangalia kwa hasira. Kwa Vikwifukwifu!
“Kinachokuchekesha nini sasa..?” Levina alimkoromea Butiliasi kwa ukali.
Butiliasi hakumjibu Levina chochote zaidi ya kuongeza tena kile kicheko mara mbili yake. Alijua wazi ni kwanini ameamua kutoa kicheko. Zile kamba ambazo mateka walikuwa wamemfunga zilikuwa zikiteketea taratibu nyuma ya mikono ya Butiliasi. Ziliteketea kwa kuchoma na kiberiti cha gesi kinachotumika kuwashia sigara kimya kimya pasipo moshi kutoka. Levina hakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nyuma ya mikono ya Butiliasi.Hata harufu ya moshi hakuweza kuisikia kutokana na Butiliasi kuchoma taratibu kwa kuzima na kuwasha. Levina aliamini kabisa Butiliasi hawezi kutoka pale kwa jinsi alivyokuwa amefungwa na kamba nzito, alijua wazi tayari wako katika himaya yake yeye Butiliasi na waasi wenzake.
“Kaa kimya, kimyaaaaaa!!” Levina alitoa sauti kali baada ya kuchoshwa na vicheko vya Butiliasi kupitiliza.
Butiliasi alijifanya bado amefungwa mikono yake kumbe ilikuwa tayari imefunguka. Imefunguka kwa kuunguzwa kidogo na kiberiti cha gesi. Aliitoa mkono wake mmoja taratibu na kisha kuanza kuupenyeza nyuma nyuma uku akilitafuta lile gobole ambalo Levina alikuwa amelihifadhi pembeni yake. Butiliasi alifanikiwa kulivuta lile gobole. Butiliasi alionesha tabasamu kidogo kisha akalikoki lile gobole nakumnyooshea Levina.
“Wee mutoto, wewe Sali sala zako za mwisho” Aliongea Butiliasi kwa sauti ya kibabe.
Levina alikuwa haelewi wala kuamini chochote. Alijihisi kama ni ndoto ama uchawi kutoka kwa Butiliasi. Aliinamisha kichwa chake na macho yakatizama upande wa chini ya butililiasi nakushuhudia kiberiti cha gesi cha kuwashia sigara sambamba na kambakamba zilizokuwa zimeteketea kidogo. Macho yalizidi kumtoka Levina akiendelea kumuangalia Butiliasi. Butiliasi mishipa ya hasira ilimpanda kichwani mwake.
“Haya haraka mufungue Osward na mikel, haraka?” Butiliasi alitoa amri kwa Levina.
Levina hakuwa na ujanja tena. Alijikuta akitoa mikono yake nakuwafungua wale waasi kamba mikononi. Alipomaliza tu kuwatoa kamba mikononi, mmoja wa mateka alitoka nyuma na kuja mpaka eneo la mbele, mateka kutoka Uganda ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Levina amepanda gari mbele na wale mateka. Aliyekuwa bega kwa bega na Levina katika kumbeba bega moja kutokana na matatizo ya Levina ya mguu mmoja. Mateka ambaye alijitolea kuwa karibu na mateka wengine huku jukumu kubwa akimwachia Levina la kuendesha gari kutokana na na yeye mwenyewe kutokujua kuendesha gari. Mateka huyo sasa alikuwa ameshafika eneo la mbele ya one ten kwa ushujaa. Alikuwa amekuja kumuhimiza Levina waondoke wanachelewa.
“Mbona hatuendi vipi nini tatizo?” Aliuliza yule mateka.
Butiliasi alihamisha lile gobole kutoka usoni mwa Levina na kuhamishia mpaka usoni mwa yule mateka. Macho yalibaki nakuwa na sintofahamu kwa yule mateka. Butiliasi akafyatua liloe gobole nakumteketeza na papo hapo ukawa mwisho wa yule mateka. Alidondoka mpaka chini na kufariki.
“Bado wewe?” Butiliasi alimwambia Levina.
Butiliasi alimsukuma Levina mpaka nje. Osward na mwenzake walishuka na kilichofuata ni kumpiga mateke Levina mithili ya wacheza mpira wakiwa uwanjani. Walimpiga mateke huku na kule wakisaidiana na Butiliasi. Wale mateka wenzake na Levina waliokuwa nyuma ya ile one tena kamwe hawakuthubutu kutoka nje. Waliogopa sana kitendo cha mwenzao Levina kuwa vile. Levina ambaye walidhani huenda ndiye mkombozi wao na sasa alikuwa amegeuzwa kuwa mpira tena mpira ule wanaocheza kina Messi na Ronaldo. Levina hakuweza kabisa kutoa sauti zaidi ya kubingirita mwenyewe chini. Alibingirita mara nyingi sana kiasi cha kuhisi maumivu katika ule mguu wake mmoja. Maumivu makali lakini Butiliasi na waasi wenzake hawakujua kama maeneo hayo yanamuumiza Levina na hata wangejua wasingeacha. Walimtesa sana Levina pale chini hali iliyosababisha Levina kuchubuka karibia maeneo yote ya usoni na mikononi. Wale mateka ambao walikuwa bado wakichungulia nyuma ya ile gari walishindwa kujizuia kuna wenguine walijikuta wakitoa machozi ya huruma na Wengine kutamani kuelekea kumuokoa lakini wakikumbuka kwa jinsi Butiliasi alivyokuwa mkali, alivyokuwa mnyanyasaji na mbabe toka wapo bunagana,Uganda. Waliogopa!
Baada ya mateso kwa Levina ya muda mrefu, Levina alipoteza fahamu, alipoteza kwa ajili ya mapigo aliyokuwa ameyapata na maumivu ya ndani kwa ndani. Butiliasi alitoka katika lile eneo nakuelekea nyuma ya lile gari lao, eneo ambalo mateka walikuwapo wamejikunyata kwa woga wa kutoka wakiogopa huenda na wenyewe wakafyatuliwa kama mwenzao ama kupigwa mateke kama Levina endapo wakiamua kutoka hata nje ya lile gari.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Shuka wote, mutu yote shuka muchini mara moja” Aliamrisha Butiliasi.
Mateka wote walishuka kwa fujo zote. Walishuka kwa woga nakujipanga mstari mmoja kama alivyokuwa akiwafanyia Butiliasi pindi wakiwa kambi yao ya waasi kule Bunagana,Uganda.
“Hii menzetu bhana, inajifanya mujanja, ila siye ni mujanja zaidi yake! Na ole wake mutu nyingine ije itoke na kufanya hivi, nitaifirigisa, nitaimaliza!” Alisema Butiliasi kwa ukali akiwaambia wale mateka wengine waliokuwa wamebaki akiwaoneshea Levina aliyekuwapo amepoteza fahamu mbele yao.
“Nataka mutu nne hapa mbele yangu haraka sana” Butiliasi alitoa amri kwa ukali.
Wale mateka walisakiziana kila mmoja alibaki akimwangalia mwenzake, dhahiri walijua kifo ndiyo kinafuatia baada ya kumzimisha Levina kwa mkumopiga mateke. Waliogopa kutoka ghata mmoja.
“Narudia tena mutu tatau hapa mbele?” Butiliasi alionesha sura ya ukali.
Bado wale mateka walikuwa wakiogopa kwenda mbele. Osward na muasi mwenzake waliamua kuwachukuwa watu wanne wanaotaka wenyewe kinguvu na kumsogezea Butiliasi.
“Nyie mutu, huyu ipo nazimia bana, bebeni begani wote nne. Na nyie wengine, musafari yetu umeanza, tutapita hili pori la Kakamega, gari imegoma tupilia kule mafuta iko kwishaa, Osward?” Aliongea Butiliasi na kisha kumuita Osward.
“Osward hakikisha huu musafara wewe iko kaa nyuma na ingia mbele ya hilo mlori kuna migiobole mingine. Na kama mutu iko mubishi fyatulia ikafie mbele”
Osward alifanya kama alivyokuwa ameagizwa na Butiliasi. Ndani ya muda mfupi alikuwa tayari ameenda ndani ya lile lori eneo la mbele na kurudi na gobole mbili akampa moja muasi mwenzake,Mikel kisha Osward alirudi tena katika lori. Alichukuwa madumu mawili ya lita ishirini ishirini yaliokuwa na maji ya kunywa ambayo walikuwa wakiyatumia mateka toka wapo Banagana,Uganda. Maji ambayo walikuwa wakiyageuza kama chakula chao walipokuwa wakiishiwa na mikate. Osward akawakabidhi mateka wawili yale madumu ya maji kisha walianza safari uku wakiwa nyuma kabisa na Butiliasi akiongoza msafara kwa mbele. Levina alikuwa amebebwa juu juu na wale mateka wenzake wanne. Alikuwa amepoteza fahamu kutokana na kipigo kutoka kwa Butiliasi na waasi wenzake.
Safari ya kukatisha msitu wa Kakamega ilikuwa ipo katikati. Hali ya hewa ya ubaridi ilikaza kabisa miguu ya wale mateka. Walitamani kusimama kwani na njaa ilikuwa imeshawatawala baada ya kukaa kwa muda karibia siku moja na nusu bila kupata mikate walioizoea zaidi ya kuishia kunywa maji kupitia madumu makubwa waliokuwa nayo toka wametoka kambi ya waasi Bunagana,Uganda.
******
Msitu wa Kakamega, Msitu ambao ni maarufu sana nchini Nairobi. Idadi ya watu chini ya mia moja inafanya msitu wa Kakamega kuonekana mtulivu muda wote kana kwamba hakuna watu waishio. Jamii ya watu wanaoishi katika msitu huu wengi wao wana asili ya kimasai. Chakula chao kikubwa ni nyama za wanyama pori na maji wanayotumia yanatokana na ukungu ambao unazalisha umande. Asubuhi wanawake kwa waume hujificha maeneo mbali mbali katika msitu wa Kakamega katika kuyakinga maji ambayo yanapatikana kwenye majani mapana. Inasadikiwa kuwa msitu huu hapo mwanzo walikuwa wakiishi wazee waliokuwa na nywele ndefu kutokea masikioni mpaka chini. Wazee waliokuwa hawajui kuongea zaidi ya kuwasiliana kwa vitendo. Na katikati ya msitu huu pamezungukwa na jiwe kubwa ambalo wana Kakamega hulitumia kufanya ibada zao na hata kutoa kafara mbali mbali. Kamwe sura ngeni wana Kakamega walikuwa hawaziruhusu katika himaya yao. Miaka ya karibuni wanakijiji wa Kakamega walishawahi kuwaua Raia wa Marekani ambao walikuja kufanya upelelezi juu ya msitu huo. Waliwachakaza vibaya mno na maiti zao wakapeleka kama sadaka yao katika jiwe kuu la kwao. Inakadiliwa kuwa Aguati Thorong’ong’o ni mmoja ya wazee wa zamani mwenye umri mkubwa ambaye yupo mpaka sasa ndani ya msitu huo. Alijitahidi sana kujifunza lugha akiwa mkubwani na kujua.Wana Kakamega waliamua kumpa uongozi wa juu kutokana na historia ya hapo na pia uzoefu wa Aguati wa kujua msitu huo na hata madhara yake. Aguati alijaliwa kipaji cha hali ya juu cha kuweza kutambua adui katika himaya yao. Alikuwa anamachale ya kuhisi tukio litakalokuja liwe jema ama baya. Aguati alitumika sana hata kuwatahadharisha wana Kakamega pale wanyama wakali na wenye kudhuru walipokuwa wakisogelea maeneo yale.
Na sasa Aguati alikuwa hoi kitandani akiugulia maumivu ya uzee wake wa muda mrefu. Uzee haukumfanya asahau matukio ya hatari na yenye kudhuru.
“Anyango yoo!” Aliita Aguati akimwita mtoto wake.
“Aaaaan!!” Aliitikia Anyango.
“Ring iluong jotelo” (Kimbia ukawaite)
Aguati Alikuwa akihema juu juu. Alikuwa kama mtu aliyeona tukio litakalokuja kichwani mwake. Mwili wake haukuwa katika hali ya kawaida. Alimwamuru mtoto wake Onyango aende akawaite wanaume karibia wote wa Kakamega waje awape taarifa. Anyango alifanya hivyo kama desturi ya Kakamega. Alichukua pembe la ndovu lililokuwa limewekewa nailoni kwa ajili ya kutoa sauti nyembamba na nzito kwa muda mmoja. Anyango akalipiga lile pembe la ndovu kwa sauti ya juu na ndogo kidogo ishara kuwa wanaoitwa ni wanaume tupu. Wana Kakamega wakakusanyika haraka kwa mzee Aguati Thorong’ong’o.
“dhi uru e thim ung’ii jomabiro gi silaha mager,(Nendeni porini muangalie hao wanaokuja na silaha kali), Aliongea Aguati akiwaambia vijana wake wa Kakamega.
“ fanyeni mjifiche na mhakikisheni hawajafika eneo hili hapa. Wawekeni hatiani ni wabaya sana. Wapo wamembeba msichana mmoja juu na watatu wakiwa wameshikilia bunduki na wengine madumu makubwa!” Alimaliza kusema Aguati.
Wale wanaume wa Kakamega wote wakajikusanya na kisha kutawanyika msituni uku kila mmoja akiwa ameshikilia mishale yenye sumu kali na usoni mwao wakiwa wamejipaka matope mazito.
************
Butiliasi na waasi wenzake bado waliokuwa wakikatiza katika msitu mkubwa wa Kakamega pasipokuwa na hofu yeyote. Makelele ya wadudu na ndege hayakuwa yakiwaogopesha sana. Sauti mbili mbili zilizokuwa zikitoka kila pande zilizidi kuhamasisha safari ya waasi pamoja na wale mateka waendelee kutembea kwa kasi bila kuchoka. Kuna kipindi wale mateka waliokuwa wamembeba Levina walichoka. Walimshusha na kupewa mateka wengine wambebe. Levina alikuwa bado si mtu wa kujielewa. Fahamu hazikuweza kumrudia mapema kutokana na kipigo alichokuwa amekipata kutoka kwa Butiliasi na waasi wenzake. Mateka walikuwa wamechoka zaidi kutokana na kutozoea mikiki mikiki ya hapa na pale. Kuna waliokuwa wakitamani kupumzika lakini kila wakimkumbuka kiongozi wao Butiliasi aliyekuwa mstari wa mbele waliogopa sana. Waliamini kabisa endapo wakijifanya wabishi watatolewa utumbo. Msafara wao uliendelea kuwa wa kimya kimya kwa muda mrefu sana. Ghafla Butiliasi alisimama. Wafuasi na mateka wote walisimama pia wakimwangalia.
“Osward? Osward” Aliita Butiliasi.
“Yes Boss!” Aliitikia Osward.
“Hapa itabidi tupumzike mudogo. Tupumzike!” Aliamuru Butiliasi.
Nyuso zao walionesha wote kuchoka. Msemo wa kupumzika kutoka kinywani kwa Butiliasi ulileta afadhali ndani ya miili ya wale waasi na hata mateka. Walimshusha Levina chini na madumu yao ya maji. Kila mmoja alijiwahi kukinga mkono ili anywe yale maji. Kiu kilikuwa kimeyateketeza makoromeo yao na kupausha midomo. Waasi wakiongozwa na Butiliasi nao wakaweka magobole yao chini nakunywa maji.Wakiwa bado katika kujipatia maji mara ghafla walishangaa kuzungukwa na umati wa watu waliokuwa wamevalia nguo za watu waishio katika msitu. Nguo zenye asili ya ngozi ya wanyama. Walikuwa zaidi ya arobaini huku mikononi mwao wakiwa wameshikilia mishale. Waliwazingira wakina Butiliasi haraka haraka nakuyawahi yale magobole kwa kuyachukuwa kutoka pale chini. Butiliasi alibaki kutoa macho kwa sintofahamu. Aliona kama miujiza.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Lala, lala dhie muberema!” (Lala nyie wapumbavu).Aliongea mmoja kati ya wale wanakijiji.
Kikosi chote cha Butiliasi kikawa hakina tena ujanja zaidi ya kutii amri mbele ya mishale mikali waliokuwa wamenyooshewa kutoka kwa wale wanaume wa Kakamega. Haraka haraka wale wanaume walijigawa, wengine walikimbilia kwenye miti nakukata kamba kamba na baadhi yao walikuwa wakiendelea kuwanyooshea mishale wakina Butiliasi na wenzakke. Baada ya muda Butiliasi na wenzake wote walikuwa chini ya himaya nyingine. Himaya ya wanakijiji wa Kakamega. Walikuwa wakiwaongoza kwa kucheka vicheko vya furaha mdomoni na mioyoni mwao. Walikenua meno njia nzima huku mikono yao ikiwa imekaza kwa kuendelea kuwanyooshea mishale wakina Butiliasi. Furaha yao kubwa ni kupata idadi ya watu wengi ambao wanakijiji wa Kakamega waliona kuwa mungu wao atafurahia sana kutokana na kuwa walikuwa wakipeleka kafara ya mtu mmoja kwa mwezi. Sasa walikuwa wakielekea katika katika jiwe lao kuu la kutolea kafara. Halikuwa mita nyingi kutoka katika eneo ambalo waliwakamata kina Butiliasi. Walisimama kwa muda kisha walianza kubishana wao kwa wao wana Kakamega.
“Kwanini tusimpeleke kwa Aguati, Aguati baba yetu kwanza?” Walianza kubishana wale wana Kakamega.
Walikuwa wakibishana kwanza kiongozi wao Aguati thorong’ong’o aweze kuwaona wale waliowateka ndipo wawapeleke Katika jiwe lao kuu la kutolea kafara.
“Hapana hii wapo wengi sana, ni hatari unaona bunduki zao zilivyokuwa kali?” Aliongea Otieno. Mmoja kati ya wana Kakamega huku akionesha zile bunduki na madumu ya maji waliyokuwa wamewapora wakina Butiliasi. Butiliasi alikuwa na hasira sana alijiona siyo shujaa kutokana na kuwa chini ya ulinzi haswa na watu waliokuwa wamebeba mishale tu wakati wao walikuwa wanamagobole na endapo wasingekunywa maji wangeweza kuwamaliza. Akili yake ilimfanya kujiona mtupu na mtoto mdogo sana mbele ya wanakijiji wa Kakamega. Akili yake ilikuwa ikimchemka sana jinsi ya kujinasua pale. Alitamani sana zile gobole zao walizokuwa wamewakabidhi wale wana Kakamega kiurahisi. Mawazo yake wyaklikuwa mengi sana mpaka alifikiria kile kiberiti cha gesi ambacho alikitumia kipindi kile yupo chini ya ulinzi wa Levina. Alijutia baada ya kujifungua kipindi kile alikitupa kile kiberiti mule mule ndani ya ile gari. Hakuwa tena na ujanja wa kujifungua wala kujinasua kamba za miti alizofungwa kwa nyuma na lile kundi la wanaume wa Kakamega. Alishusha pumzi uku akiwatokea macho ya hasira wale wana Kakamega ambao bado walikuwa wakijibishana juu ya wao wapelekwe wapi.
Levina bado alikuwa hana kumbukumbu zozote. Kipigo alichokuwa amekipata kutoka kwa Butiliasi na waasi wenzake kilikuwa ni kipigo kitakatifu. Alipoteza fahamu haswa pasipo kupatiwa huduma ya kwanza wala huduma yeyote. Njia nzima waliokuwa wamembeba mateka, Levina alikuwa akivujwa na damu kutoka puani. Kuna wakati damu zilitokea maeneo ya mdomoni lakini hakuna aliyekuwa akijua wala kujali zaidi ya Butiliasi na waasi wenzake kuendelea na safari mpaka pale walipokamatwa na wana Kakamega. Na sasa Butiliasi macho yake alikua akiyalekeza chini kumuangalia Levina. Levina ambaye kwa mara nyingine alikuwa amenusurika kufungwa kamba za miti mikononi na wanaume wa Kakamega kutokana na kupoteza fahamu. Walijua dhahiri hawezi kutoroka kutokana na kupoteza fahamu na hata hivyo wana kaka mega waliona kumfunga kamba mtu aliyekuwa nusu mfu ni bora wambebe hivyo hivyo na kwenda kumtupa katika jiwe lao la kutolea kafara.
“Zoisa, Zoisa ndio tuende” Aliongea Otieno mmoja kati ya wana Kakamega waliokuwa wakiendelea kubishana kuhusiana na ule umati wa mateka na waasi waupeleke kwa kiongozi wao Aguati ama moja kwa moja wanapotolea kafara. Baada ya mabishano ya wenyewe kwa wenyewe na kuafikiana sasa walikuwa wameanza ile safari yao ya kuelekea katika jiwe la kutolea kafara. Walianza kupandisha kimlima kidogo. Sauti za wanyama wakali zilianza kuzidi eneo lote. Wote walikaa kimya wakitazamana. Upande wa wanaume wa Kakamega walikuwa wakijua kabisa kuwa mungu wao amehisi kuna kafara inakuja hivyo ni ishara yake lakini kwa upoande wa kina Butiliasi hakukuwa hata na mmoja aliyekuwa akiijua historia ya hapo wala hilo eneo husika la kutolea kafara. Kimya cha muda mrefu kilitawala na baada ya hapo popo wale wa usiku walianza kutawala karibia eneo lote la ule msitu.Walikuwa ni popo wengi sana waliokuwa wakizingira kiasi kwamba eneo lote likawa giza tena giza nene wakati ilikuwa ni asubuhi kuelekea mchana.
“Watatu watatu mbele kwenye lile jiwe?” Aliamrisha Otieno,kiongozi wa muda wakina Kakamega.
Alikuwa akiwaambia wale watu waanze kujigawa kwa kwenda kupeleka kafara. Awamu ya kwanza wanaume wa Kakamega walimchukuwa Osward na mateka watatu pamoja na yale magobole yao waliyowakamata nakupandisha nao mpaka eneo la juu kabisa kwenye hilo jiwe ambapo kati kati ya hilo jiwe kuna pango kubwa sana lililojawa giza nene. Wale wanaume baada ya kuwafikisha waliwasukuma wale mateka na Osward wote na kilichofuata ni sauti za mwangi za kulia kuonesha kuwa wamezama parefu sana. Baada ya hapo wale wanakijiji wa kakamega walipiga makofi sambamba na kunyoosha mishale yao juu kwa furaha zote.
“Wengine watatu?” Aliongea Otieno.
Waliwachukuwa tena mateka watatu na muasi mmoja pamoja na madumu yale ya maji uku wakimwacha Butiliasi na Levina kwanza. Walipandisha nao mpaka juu na kufanya kama walivyokuwa wamefanya awali. Waliwatupa na kupiga tena makofi sambamba na mishale yao kuonesha juu. Waliendelea na zoezi hilo mpaka wakabaki wawili wa mwisho ambapo alikuwa amebaki Butiliasi, na Levina. Waliwachukuwa hivyo hivyo na kumbeba Levina juu juu huku Butiliasi akiwa anasukumwa na kamba ziko mikononi mwake. Butiliasi alijitahidi kuwa mbishi lakini alikutana na wabishi zaidi yake. Aliendelea kupanda kulekea kwenye jiwe kiubishi uku akigeuka nyuma. Asingeweza kufanya lolote Butiliasi kutokana na umati mkubwa wa wana Kakamega uliokuwa ukimtazama na kuhakikisha anadumbukia katika jiwe la kutolea kafara. Jiwe alipokuwa akiishi mungu wao. Kitendo cha wanakijiji wa Kakamega kuwafikisha Levina na Butiliasi mpaka juu na kutaka kuwaachia tu, mara ghafla Levina fahamu zikamrudi. Akashtuka! Akaruka katika mikono ya wale wanaume wa Kakamega. Akabiringita mpaka chini kabisa kutoka kwenye kile kimlima kidogo kilichokuwa na jiwe lao ka kafara. Levina aliumia sana kwa kubingirita mpaka chini kabisa ambapo alikutana na ule umati wa wanakijiji wa Kakamega umemzunguka. Umemzunguka kwa hasira ya kujirusha nje ya jiwe. Jiwe aliokuwa akiishi mungu wao. Waliona sadaka ile inataka kuingia doa. Kitendo cha wale wanakijiji wa Kakamega kumshangaa Levina, hapo hapo Butiliasi akatumia akili zake za kuzaliwa. Aliwasukuma wale watu waliokuwa naye juu wakimsindikiza. Aliwasukumiza kwenye jiwe la kutolea kafara wakamezwa wote. Wana Kakamega hawakulitambua mara moja kwani akili yao yote na macho ilikuwa katika kumzingira na kumuangalia Levina aliyekuwa amebiringita vibaya mpaka chini kabisa. Baada ya kumshika Levina pale chini macho yao sasa yalihamia juu yakaangaza na kumuona Butiliasi akiwa akiwa peke yake akihangaika kufungua kamba kwa kutumia lile jiwe la kutolea kafara. Alikuwa ameliinamia kwa mikono yake akisugua mikono yake iweze kujinasua.
“Ochieng yupo wapi na wengine?” Aliuliza Owino baada ya kumuona Butiliasi peke yake juu pasipo ulinzi wowote.
“Nilisikia kelele tu nikajua yule pale ametupwa, atakuwa ameshaenda kwa mungu wetu.” Aliongea mmoja wa wana akkakamega. Wanakijiji wote wakachukua mishale yao pembeni ya viuno vyao na kunyooshea juu alipokuwa Butiliasi uku wakitaka kuifyatua.
**********************
Butiliasi alikuwa tayari ameweza kufanikiwa kutoa ile kamba aliyekuwa amefungwa mikononi. Kamba iliyokuwa ya asili ya miti ya misituni. Mapigo ya moyo ya Butiliasi yalizidi kumwenda kasi. Kasi mithili ya yule mkimbiaji namba moja duniani Usain Bolt. Hakujua nini afanye baada ya wanakijiji wa Kakamega wote kumnyooshea mikuki yenye sumu kali wakitaka kummaliza kabisa.
“Shuka, Shuka mwenyewe?” Alitamka Otieno, kiongozi wa muda wa Kakamega. Alikuwa akimtaka Butiliasi aweza kushuka pale mwenyewe kabla hawajaamua kumfyatua. Ile asili ya utukutu ya Butiliasi bado ilikuwa imeganda katika ngozi yake.Alizidi kuwa mbishi. Hakutaka kuyasikiliza yale maneno japokuwa alikuwa akinyooshewa mishale mingi na wana Kakamega.
“Tuna hesabu mpaka tatu usiposhuka?” Aliongeza Otieno.
Bado Butiliasi alikuwa kimya akiwatizama kwa chini. Hasira kali zilizidi kumjaa kutokana na waasi wenzake wa M23 wote kumezwa na Shimo la kutolea kafara, shimo ambalo wanakijiji wa Kakamega siku zote waliamini kuwa mungu wao anaishi uko. Anaishi kwa kula nyama za watu.
“Moja…” Otieno alianza kuhesabu.
“Mbili….” Bado aliendelea kuhesabu.
Butiliasi alikunja sura yake na kuusogeza mkono wake puani kupyenga kamasi zilizokuwa zikiomba njia katika pua yake. Kamasi ambazo zilimisi kusalimiana na mkono japo mmoja wa Butiliasi.Kabla Otieno hajamalizia kuhesabu. Butiliasi alinyoosha mikono yake juu nakujifanya kama akitaka kujirusha katika shimo. Wanakijiji wa Kakamega wote walibaki kimya wakishangaa kitakachoendelea. Waliamini dhahiri kuwa Butiliasi kakubaliana na amri ya kiongozi wao,Otieno. Amri ya Butiliasi kujitupa mwenyewe katika shimo pale juu ya jiwe la kutolea kafara. Kimya cha muda kilitanda na baada ya muda. Otieno aliwafanyia ishara wenzake wote kuwa wampandie Butiliasi uko uko juu.
Walishusha mikuki yao chini wote kisha wakaanza kupiga makelele uku wakipanda juu ya kimlima alipokuwamo Butiliasi. Butiliasi alibaki akitetemeka mwenyewe akiwaangalia. Walimfikia nakumzoa kisha Otieno alimshika mikono yake. Butiliasi alijifanya mbishi wa kuzaliwa. Alimchukuwa Otieno bila kujali ule umati umemzingira pale juu na kumtupa mpaka ndani ya shimo lao la kutolea kafara kisha Butiliasi alinyoosha mikono juu kuashiria ushindi.
“Oyeeee!!”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wanakijiji wa Kakamega walibaki na butwaa.Hawakuamini! Kamwe kwao haijawahi kutokea kiongozi akadumbukizwa katika shimo la kutolea kafara. Walibaki wakiangaliana kisha macho yao waliyageuza na kumwangalia Butiliasi. Bandidu! Bandidu haswaa!
Hasira kali kutoka kwa wana Kakamega ziliwafanya wamshike nakumsukuma Butiliasi mpaka chini kabisa alipokuwamo Levina. Butiliasi alibiringita mithili ya tairi la gari pindi likiachiwa kwenye kamteremko. Alishtukia amegota chini kabisa kwenye mwili wa Levina. Wakatazamana! Levina hasira kali na Butiliasi hasira kali. Wanakijiji wa Kakamega wakanyoosha mikono yao juu na mishale kuonesha ushindi. Walishuka kwa fujo mpaka chini kabisa kisha walichukua miti mikubwa nakuwafunga Levina na Butiliasi mithili ya mgonjwa mahututi akiwa kwenye machela. Maumivu makali ya ndani kwa ndani yalimuumiza sana Levina na hata Butiliasi naye alikuwa akiugulia maumivu hayo hayo makali. Wanakakamega hawakutaka tena wawatupe katika shimo la kafara kutokana na kujifanya wabishi. Pili Walichukizwa sana na kitendo cha kiongozi wao wa muda,Otieno kusumkumwa na Butiliasi. Waliamini hata mungu wao anaweza kuchukizwa kwa kitendo cha kumpokea kiongozi ambaye alikuwa akiwasaidia japokuwa kwa muda pindi wakienda kujinusuru kwa kitu. Majonzi! Njia nzima wanakijiji wa Kakamega walikuwa wakilia kwa vikwifukwifu. Iliwauma sana kuondokewa na Otieno wao.
Baada ya mwendo kidogo waliingia katika himaya yao. Himaya ambayo ilikuwa ikisimamiwa kwa muda mrefu na Aguati mwana wa thorong’ong’o ambaye kwa muda huu naye alikuwa hoi kitandani kutokana na uzee kuchukuwa nafasi yake. Alikuwa hajiwezi hata kuinuka wala kutembea. Wanakakamega waliwashusha Chini Butiliasi na Levina. Waliwashusha kwenye uzio wao wa kutolea adhabu pindi mwana Kakamega alipokuwa akikosea. Waliwaning’iniza vilivyo uku macho na vifua vyao vikielekea chini kutazamana na ardhi ya Kakamega. Hawakumuonea huruma Levina hata mara moja japokuwa alikuwa na mguu mmoja. Ndio kwanza walimfunga kamba zao eneo la kuanzia kiunoni mpaka kwenye mti mkubwa. Maumivu makali yaliendelea kuzitesa nyoyo zao. Si Levina wala Butiliasi wote walikuwa wakiendelea kuumia sana. Jua kali likaanza kuwaumiza.
Walipomaliza kuwafunga waliwasha na taa zao pembezoni kuzunguka lile eneo kwani na giza nalo lilikuwa tayari limeshatoka na baada ya hapo wana Kakamega wote wakaelekea eneo lao la vikao. Eneo ambalo kuna nyumba ya makuti na huwa ni maalumu kwa kukutana wakiume kwa wakike wote endapo mwenzao atafariki. Walienda kumjadili Otieno wao aliyetupwa katika jiwe la kafara huku wakiwaacha wenzao wane wawalinde Butiliasi na Levina. Njaa na kiu kwa pamoja vikayatesa sana matumbo ya Levina na Butiliasi. Kuna wakati jasho liliwatiririka sana. Kuna wakati Levina alitokwa sana na damu maeneo ya puani. Na hata mguu ule uliokuwa umekatwa uliendelea kumvimba eneo la mapajani nakumuuma sana.
“Naombeni maji, maji!!” Alitamka Levina kwa sauti ya juu.
Waangalizi wanne waliokuwepo wakiwasimamia Levina na Butiliasi. Walishangaa sauti ya Levina. Wakamsogelea kwa karibu.
“Wasemaje?” Walimuuliza Levina.
“Nasikia kiu,nasikia njaa, mwili hauna nguvu naumia,naumia mimi!!” Levina aliwalalamikia.
Wale wanaume hawakutaka kufanya chochote. Walichokifanya ni kujigawa. Wawili walienda mpaka kwa Aguati kwanza wapewe ruhusa kama wanaweza kuwapa chochote. Walipofika kwa Aguati. Aguati alikuwa kapitiwa na usingizi lakini hisia zote na akili zilikuwa zikifanya kazi vilivyo.
“Busebo?” Aliita Aguati uku macho yake akiwa ameyafumba. Alimwita mmoja kati ya wale waliokuwa wamemfuata.
“Naam Aguati!” Aliitika Busebo.
“Yule mwanamke mliomfunga, hana hatia. Mnamtesa bure. Yeye ametokea Tanzania na alitekwa na wenzake ambao mliwatupa kwa baba yetu shimoni. Muende mkamfungue na mhakikishe mnampa huduma zote yeye ni kama ndugu yetu. Hana matatizo na sisi ila yule mwingine sio mtu mwema. Ameua wengi sana wasiokuwa na hatia.” Aliendelea kuongea Aguati kwa sauti ya chini chini.
Busebo alimtonya mwenzake baada ya Aguati kuongea maneno yale. Yaliwaingia akilini sana. Yaliwagusa sana kutokana na Levina kumshirikisha kwenye kundi moja la kina Butiliasi. Walienda moja kwa moja mpaka nje ili kushirikiana na wenzao wawili waliowaacha wamfungue Levina. Lakini kitendo cha kufika pale walishangaa kukuta Si Levina wala Butiliasi wote wakiwa hawapo pale na wale wenzao wawili waliokuwa wamewaacha chini walikuwa tayari wameshafariki. Walijitahidi kuangalia pembeni. Walichomoa moja kati ya mitaa yao ya mikonge, mitaa ile mikubwa mithili ya mwenge nakuangaza chini. Walifanikiwa kuona damu damu nyingi zikitiririka kwa kufuata njia. Wakaanza kuzifuatilia.
*******
Butiliasi alikuwa amewatuma waasi wenzake wanne kipindi kile kwenda nchini Tanzania wakitokea kwenye kambi yao waliokuwa wameiweka,Bunagana,Uganda. Waasi wawili walielekea Tanzania Osward na Jesse ambao walifanikiwa kuingia Tanga nakupora gari ya polisi ambapo waliwachukuwa mateka wachache kisha wakaelekea mpaka Dar es salaam na kufanikiwa kuwapata mateka wachache akiwamo Levina. Walifanikiwa kurudi salama usiku na kumkuta Butiliasi akiwa njiani amekwama baada ya Lori lao lililojaa mateka kupoteza uelekeo. Osward na Jesse walimsaidia kiongozi wao Butiliasi kutoa lile lori na kisha walilifunga kamba na kuendelea na safari.
Waasi wengine wawili Osusu na Papii wao waliingia katika jiji la Arusha. Waliingia kimya kimya nakufanikiwa kuliteka gari binafsi likiwa limebeba familia ya wanaume wane pamoja na mwanamke aliyekuwa na mtoto mdogo sana mwenye miaka miwili. Waliwateka na kurudi nao mpakani ambapo walipita njia ile ile ya Tarakea. Na walipofika mpakani walikuta hali si shwari. Mapolisi wa kitanzania walikuwa wamezingira wakifanya ukaguzi wa gari moja baada ya jingine. Osusu, muasi aliyeshindikana na kiumbo,kinguvu na hata kiakili kamwe hakukubali kushindwa kukamatwa. Alichokifanya aliiwasha gari yake na kutoka spidi ya ajabu. Mapolisi wa kitanzania nao hawakuwa nyuma. Walikimbizana naye njia nzima kwa muda mrefu hadi wale mapolisi wa kitanzania walikata tama na kusimamisha gari lao nakugeuza mpakani. Osusu na wale mateka walipofika mbele kabisa yule mwanamke aliyekuwa na mtoto alikuwa tayari ameshapoteza fahamu. Alichokifanya Osusu ni kufungua gari na kumtupa nje kabisa. Mumewe akishirikiana na familia yake nao walianza kuleta kizaazaa ndani ya gari baada ya mkewe kutupwa. Akashindana nao nguvu uku gari likiwa katika mwendo kasi. Papii ndiye aliwanyamazisha baada ya kuinua gobole lake nakumuelekezea yule mwanaume. Wote wakabaki kimya kama wamenyeshewa na mvua. Osusu alislismamisha gari na kilichofuata ni kumtupa yule mwanaume kisha waliendelea na safari. Safari ambayo Osusu alimkabidhi Papii ambebe yule mtoto na baada ya mwendo kidogo gari yao ilianza kusumbua. Tatizo! Mlio wa ajabu wa injini ulikuwa ukiunguruma. Walisimamisha lile gari na kufungua upande wa mbele. Gari ilikuwa imechemka vilivyo, moshi mkali ulitoka ulioambatana na fukuto zito. Wakaangalia na upande wa mafuta. Hakukuwa na mafuta na hata oili nayo ilikuwa imewaishia. Hawakuwa na jinsi tena zaidi ya kuliacha lile gari. Giza nalo lilikuwa likitaka kuchukua nafasi yake na kutaka kufunika eneo lile.Walianza kutembea wakiamini gari lolote litakalojipendekeza lazima waliteke. Baada ya mwendo mrefu kidogo uku Papii akiwa amembeba yule mtoto mdogo pembeni upande wa kushoto na mkono mwingine akiwa na gobole mara wakakatuna na lori lao pamoja na gari ya polisi ya kitanzania. Waliinyemelea taratibu. Na walipofikia walikuta miili ya wenzao wawili ikiwa chini. Na mateka wengine wakiwa wameshafariki.Walisikitika sana. Wakiwa bado wamezubaa walishangaa sauti za watu zikitoka nyuma ya lile lori. Sauti mbili zilizoonesha kuita kwa kuchoka. Osusu hakuwa muoga. Aliingia mpaka nyuma ya lile lori nakukuta likiwa limefungwa na komeo. Alilifungua uku gobole lake akiwa amelielekeza eneo la ndani. Hakuweza kumuona yeyote kutokana na giza lile change kutanda.
“Nani ipo humu, mutu ya wapi?” Aliita Osusu kwa sauti ya juu.
“Sisi, Tuokoeni jamani. Tunakufa!” Waliitika wale watu.
Osusu alinyemelea kufuata sauti ilipokuwa ikitoka mpaka alipokaribia lile eneo na alipofika aligusana na turubai. Alihisi ndipo ile sauti ilipokuwa ikiptoka. Akalifunua turubai kwa nguvu. Kilichofuata ni mihemo ya watu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sisi ingi mateka kutoka Bunagana,Uganda. Tulitekwa na kikundi cha M23. Tunawaomba sana msaada wenu” Wale watu walijitetea.
“Muko mungapi?” Alisema Osusu
“Tupo wanaume watatu tulifunikwa na turubai wenzetu walipotoka nakuondoka na waasi. Waliamua kutuficha ili baadaye tuje tuwaokoe” Aliongea mmoja kati ya wale mateka akiamini kuwa wapo mikono salama.
“Inuka, wote inuka tutoke muchini kwanza” Osusu Aliwaambia wale watu.
Wale mateka walijua usalama wao ndio huo. Walishuka wakiwa na furaha ya hali ya juu. Walipofika chini kabisa mmoja wa wale mateka aliongea.
“Tumeshashuka tunaelekea wapi” Aliuzia kwa furaha akiamini wako huru.
“Huku, haraka pumbavu nyie?” Osusu aliwageuka.
Osusu aliingia ndani ya ile gari ndogo ya polisi nakutaka kuiwasha lakini hata mlio wa kuwaka haukutokea zaidi ya eneo la mafuta kuonesha kuwa yameisha. Wakaona ni bora waingie msituni na wale mateka wao. Osusu akiwa nyuma na Papii akiwa upande wa mbele akiongoza msafara uku wale mateka wote wakiume wakiwa katikati na mmoja wao akiwa amepewa ambebe yule mtoto mdogo na kutembea kwa kukimbia kwa kukatiza msitu wa Kakamega.
Mwendo wa nusu saa uliwafanya Osusu ahisi kitu mbele yao. Moto mkubwa na taa zilizokuwa zipo mithili ya mwenge kwa mbali ndizo ziliwavuta. Osusu alimgeukia Papii kwa furaha nakumnyooshea eneo lile uku kichwani mwake akiamini kabisa itakuwa sehemu yao ya kupumzika kwa muda. Walianza kusonga taratibu na walipofika hatua kadhaa walianza kuhisi kuna watu wamejificha. Wakabadili muondoko nakusogea kwa kunyatanyata. Mtoto waliokuwa naye akatoa sauti ya kulia kwa sauti ya juu uku akikohoa. Yule mtoto alikuwa amezingirwa na nyoka katika mwili wake. Yule mateka aliyekuwa amembeba yule mtoto alimrusha kwa woga yule mtoto mpaka chini akadondoka. Osusu alikasirika sana kitendo cha mateka yule kumdondosha mtoto mpaka chini. Alimfuata yule mateka bila kuhofia eneo walipo. Alimtandika vibao vya haja. Chali! Yule mateka naye akadondoka mpaka chini. Osusu alimfuata yule mtoto ambapo yule nyoka alikuwa ameshaondoka katika mwili wake na kumpatia mateka mwigine ambebe. Waliendelea kunyata mpaka wakafikia karibu na lile eneo lililokuwa likiwaka taa.
“Buti, Buti?” Alistaajabu Osusu baada ya kumuona kiongozi wao waliomuamini siku zote akiwa ametundikwa juu juu. Taratibu Osusu aliwaoneshea ishara wenzake kuwa wamsubiri kwanza. Akakitumia kisu chake kukirusha mpaka kwa yule mwana Kakamega aliyekuwa akiwalinda kina Butiliasi. Kisu kikampata usoni akadondoka akifurukuta. Akafa! Mwana Kakamega mwenzake aliyebaki akashangaa. Azidi kushangaa uku na kule asielewe kitu. Kitendo cha kutaka kupiga makelele tu.Osusu akawa ameshachukuwa kisu kingine na kumrushia.Kikampata shingoni. Na yeye akadondoka hapo hapo. Akafa!. Osusu akamwambia mwenzake abaki kwanza. Akaenda kumfungua kwanza bosi wake Butiliasi kisha akataka kuondoka naye.
“No, no Osusu, fungua na hii ni mutu muzuri sana. Tumeteseka nayo! Fungua na yeye”
Alisemaa Butiliasi akimwambia Osusu amfungue Levina.
Alimfungua na kumchukua Levina ambapo alikuwa na mguu mmoja. Osusu alijitahidi kumbeba upande upande begani nakutokomea pamoja na wale mateka wengine kusikijulikana uku Butiliasi akikabidhiwa gobole na Osusu kuongoza msafara.
***********
Giza lilizidi kuwa totoro. Sauti za milio ya ajabu ya popo na wanyama kama fisi zilizidi kutanda eneo zima. Eneo lote la msitu wa Kakamega lilikuwa limemezwa kwa giza nene.Hali ya ubaridi kwa mbali ikaanza kuchukuwa sura mpya. Si Osusu,Papii wala Butiliasi hata mateka waliokuwa na hata tochi. Levina pamoja na mateka wengine waliona dunia chungu. Levina yeye alikuwa amechoka kupitiliza. Alihisi mwili wake haufai kufananishwa na mwili wa binadamu yoyote kutokana na mateso aliyopitia na maumivu yaliojikusanya mpaka kufikia hapo. Njia nzima alikuwa akining’inizwa begani na Osusu uku Papii akiwa bega kwa bega kwa kuwalinda mateka waliokuwa wamefungwa kamba mikononi mwao kwa kuwanyooshea gobole. Baada ya kutembea mwendo wa mbali kiasi njia nzima giza wasijue uelekeo. Mara ghafla mbalamwenzi nayo ilianza kuchukua nafasi yake na kutanda eneo lote. Kukawa na mwanga kiasi. Wakaweza kuonana na kutambuana uku wakiendelea na safari yao.
“Nimechoka sasa, nimechoka nataka kupumzika” Alisema Levina kwa sauti ya ukali.
“Umechoka, Wewe ndiye namubeba Osusu au yeye iko mubeba wewe?” Alisema Butiliasi kwa sauti ya ukali uku akimsogelea Levina karibu.
“Nasikia njaa sijala hii siku ya pili, hata maji nayo imekuwa shida, nasikia kiu. Bora nife tu, niueni nife tu kuliko kuendelea kuteseka na kosa langu silijui” Levina aliendelea kusema kwa ukali wenye kutia huruma. Alilalama sana hali iliyosababisha Butiliasi kuanza kuwa na huruma. Huruma ambayo maishani mwake Butiliasi hakuwahi kuwa nayo hata chembe. Alifikiria sana kuanzia walipotekwa wote msituni na wanakijiji wa Kakamega. Alikumbuka Levina alipopata mateso ya kubiringita kama yeye kutoka kwenye kimlima kule kwenye jiwe la kutolea kafara. Butiliasi akajihisi kama ni mkosaji namba moja kwa Levina.
“Osusu? Unamumaji ya akiba? mupe mumaji inywe, mupee!” Aliongea Butiliasi akimwambia Osusu. Osusu alikuwa akihifadhi maji yake kwenye kibegi chake alichokuwa akikibebelea mgongoni njia nzima. Alikivua na kuchomoa kidumu cha lita tano kilichokuwa kina maji mengi. Kisha alitoa na vipande viwili vya mikate mikavu. Mikate ambayo ilikuwa imegandamana kwa ubaridi. Ilikuwa ni mikate ile migumu sana hata kwa kuitafuna. Levina alipewa ile mikate na maji. Alifakamia utadhani alikuwa na mwaka hajakiona chakula. Ile njaa iliyokuwa ikisugua tumbo lake nakuwa gumu sasa likaanza kuachia. Levina alianza kujihisi uhafadhali. Nguvu zilianza kumrejea taratibu. Tabasamu pana alilitoa Butiliasi baada ya kuona Levina akimalizia kula ile mikate na kushushia na maji. Hata njaa na kiu ambavyo navyo vilikuwa vikisumbua tumbo la Butiliasi alijiona kama ameshashiba. Osusu akainama chini kwa nia ya kumbeba Levina begani kwa upande ili waendelee na safari. Safari ya kutoka katika msitu wa Kakamega. Kitendo cha kutaka tu kumuweka Levina begani. Sauti ya yule mtoto ikaanza kutoka, Yule mtoto waliokuwa naye kina Osusu kutokea Arusha walipokwenda kuteka mateka. Mtoto ambaye alipewa ndugu yake kumshika. Ndugu yule wa kiume ambaye peke yake kati ya wale mateka hakuwa amefungwa kamba mikononi. Kumbe yule ndugu alikuwa ameshachomwa na mshale wanye sumu kali mgongoni mwake. Alidondoka chini na mtoto. Osusus alijitahidi kumuwahi yule mtoto aliyekuwa bado akiendelea kulia kwa sauti ya juu. Hawakujua mshale ule umepigwa na nani. Waliangaliana wenyewe kwa wenyewe. Butiliasi akalikoki gobole lake na kutaka kulipiga upande ule ulipotokea mshale lakini alisita na kushusha gobole lake chini. Hasira kali ziliendelea kumshika uku akihema kwa juu juu kwani alitokea sana kuwachukia wanakijiji wa Kakamega kwa jinsi walivyomfanya hapo awali.
“Osusu? Papii? Mukazi sasa umeanza. Wametuchokoza na sisi tuna majibu yetu, iko taka muvurugu hii watu ya uku?” Aliongea Butiliasi kwa sauti ya ukali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Mupe hiyo toto huyo mudada imbembeleze na itakuwa naye siku zote kuanzia sasa, Lete mupanga?” Aliendelea Butiliasi uku akiomba panga. Kila mmoja alibaki kumtazama Butiliasi asielewe anataka kufanya nini pale. Osusu alimwelewa vilivyo bosi wake kamwe hakupenda masihara wala kuchokozwa katika kundi lao na watu wengine. Alimpatia panga kutoka katika kibegi chake. Butiliasi akalivua shati lake nakuelekea mpaka pembeni ya kichaka na kisha kuanza kukata majani ambapo alitoka na mti mkubwa kiasi. Mti ambao ulikuwa umekaa kwa juu mithili ya kipago tena kile cha mananati. Kwa mbele ulikuwa mpanti ule wa kusongea ugali. Aliukata na kuuchonga vizuri kwa kutoa majani kisha akampatia Levina.
“Hii iko kusaidia wewe kutembea, ipo kama mufimbo ya chuma ile ya hospitali ya wagonjwa” Aliongea Butiliasi akimpatia Levina fimbo ya kujishikiza upande mmoja aliokuwa hana mguu. Levina aligeuka na kuwa mama wa muda uku Osusu akimwachia kibegi chake kilichokuwa kimejaa mikate pamoja na dumu la maji dogo. Waasi wote walichukuana na mateka waliokuwa wamewafunga kamba mikononi mwao nakurudi katika himaya ya kile kijiji cha Kakamega. Hasira kali kutoka kawa Butiliasi akiongozwa na muasi mwenzake Osusu walianza kutafuta njia ya kuelekea kambi ya Kakamega. Magobole yao yalikuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna kitakachokatiza mbele yao. Kwa upande wa nyuma Papii alikuwa akiwanyooshea gobole wale mateka wasije wakatoroka.Hawakujali cha mishale wala mikuki yenye sumu wanayotumia wana Kakamega katika kujilinda na adui.Akili yao ilikuwa ni moja tu ya kwenda kusambaratisha kijiji chote. Baada ya mwendo kidogo.
“Simameni hapo hapo, simama?” Sauti kutoka kwa wanakakamega zilitikisa masikio ya Butiliasi na wenzake. Walikuwa ni wakina Kakamega wakiwazunguka kama walivyofanya awali walivyowateka walipokuwa wamezubaa katika kujipatia maji. Na sasa walikuwa wamewazingira na kutaka kuwafanya kama awali. Butiliasi machale yalimzidi sana. Hisia kali zilikuwa mwilini mwake. Alikuwa ameshajitolea kwa kufa safari hii. Aliyazungusha macho yake na kuhesabu kimya kimya umati ule uliokuwa umewazunguka. Umati wa wana Kakamega zaidi ya sitini. Kakamega waliokuwa na hasira mara mbili ya kwanza kuuliwa kwa Otieno wao na ya pili kuwaua tena kina Kakamega wenzao wa nne na ya tatu kutoroka kutoka katika himaya yao. Waliona ni dhihaka sana kwao. Hawakutaka kusikia neno lolote la kujitetea kutoka kwa Butiliasi ama wenzake wote.
“Aguati, Aguati, Aguati Aguati” Walinyoosha mikono juu kuonesha ushindi uku wakilitaja jina la Aguati yule kiongozi wao wa muda mrefu aliyekuwa akiishi nao kama kiongozi. Kitendo cha kunyoosha mikono juu wale kina Kakamega ndicho kiliwapa nafasi Butiliasi na waasi wenzake kufanya watakavyo. Waliyanyoosha magobole yao nakuanza kuwamiminia mmoja baada ya mwingine uku wakikoki haraka haraka na kufyatua mara nyingi watakavyo. Wale wana Kakamega baadhi yao walikuwa waoga sana. Waliona mlio tofauti ukitoka kwa Butiliasi kupitia gobole lake. Katu hawakulijua gobole linatoa sauti ya aina gani. Kuna waliokimbia mbio na kuacha mishale yao na wengine walikimbilia machakani na kujificha uku wakitolea macho gobole linavyowapiga wenzao na kudondoka papo hapo. Butiliasi akajiona shujaa. Shujaa wa kukimbiwa na hata kuwauwa baadhi yao. Risasi za gobole zilikuwa zimeshamuishia kabisa lakini ni Osusu pekee aliyekuwa amebakia na mashine gani begani mwake kwani alikuwa na silaha za aina mbili. Aliivua ile mashine gani na kumkabidhi Butiliasi. Butiliasi kwa kupenda sifa, kwa hasira akazimwaga kama njugu kuzunguka kichaka chote na kilichofuata ni sauti za watu wakilia kwa kuweweseka na kufa.
Butiliasi akawafanyia ishara ya mkono wenzake kuwa wamfuate. Wakaanza kumfuata kuelekea eneo ambalo kwa mbele yake waliona taa za mienge. Kila mmoja alilikumbuka eneo hilo. Eneo ambalo ndio kambi kuu ya kina Kakamega. Eneo kamwe Butiliasi asingeweza kulishahau katika kichwa chake. Eneo ambalo yeye na Levina walipata mateso makali kwa kufungwa kamba wakining’inizwa. Walipolifikia lile eneo Butiliasi alianza kukisambaratisha kijumba kimoja baada ya kingine. Wakina mama waliokuwa wakiandaa chakula na wengine wakiwa wameshalala walijikuta wakidondoka na kufariki papo hapo kutokana na risasi kali kuwaingia. Butiliasi alizidi kujiona shujaa. Alihakikisha vijumba karibia vyote amevidumbukiza risasi. Sasa ikawa zamu ya kuingia katika nyumba ambayo alihisi ni ya kiongozi mkuu. Alikumbuka mara ya mwisho walipokuwa wametekwa na kufungwa kuna baadhi ya kina Kakamega walikuwa wakiongelea kuhusu kuingia uko na kupata ushauri. Butiliasi akausukuma mlango kwa kutumia miguu yake.
“Mutu yeyote ijisalimishe haraka kabla sijaimaliza?” Butiliasi aliongea kwa mkwara. Kimya kikaendelea kutanda. Hatua moja baada ya nyingine. Uku bunduki yake iliyokuwa bado imesheeheni rundo la risasi kiunoni mwake ikiwa imeeelekezwa mbele. Walikutana na kitanda kizuri ambacho ndani yake hakikuwa na mtu yeyote. Butiliasi kwa kupenda sifa nacho kitanda akakipiga risasi kadhaa. Sauti ya kizee kwa mbali ikaanza kusikika. Sauti ambayo kamwe hakuwahi kuisikia hapo nyuma. Sauti ambayo inamikwaruzo mikwaruzo ndani yake.
“Unataka nini? Wana wangu umewaua karibia wote. Na hata mdogo wangu Otieno ulimtupa katika shimo la baba yetu. Ndio ulivyopenda?” ile sauti iliongea.
“Wewe ni munani na ipo wapi, jisalimishe haraka?” Alisema Butiliasi kwa ukali.
“ Naitwa Aguati mwana wa thorong’ong’o na unataka kuniona?” Aguati alisema.
“Sio kukuona, iko taka mudamu yako, iko taka kuteketeza mutu wewe” Aliendelea Butiliasi.
Kabla hajakaa vizuri Butiliasi na waasi wenzake walishangaa kupigwa makofi na mtu wasiyemuona. Na baada ya hapo walishangaa vyungu kuwapitia vichwani mwao wakayumba yumba wakitaka kudondoka kabla hawajakaa sawa walishangaa mitama ya ajabui wakipigwa miguuni mwao. Butiliasi chini, Osusu na Papii nao chini, Mateka wale waliokuwa nao wamefungwa kamba mikononi nao chini kabisa. Butiliasi akataka kuinuka akaambulia tena teke la tumbo. Akajikuta bunduki yake ikielea juu juu.
“Naitwa Aguati, bado manataka kunijua?” Aliongea Aguati.
“Ndio nataka kukuteketeza” Alijibu Butilkiasi kwa utata.
Walishangaa sasa fimbo zikiwatandika pasipo kumuona anayewatandika. Walitandikwa haswaa na baada ya kila mmoja kutandikwa karibia mwili mzima bila kujali wengine walikuwa ni mateka. Ile bunduki iliyokuwa ikielea ikaanza kutoa risasi kutokea upande wa nje uku ikitaka kuwafuata. Ikaganda! Zile gobole mbili walizokuwa wamebaki nazo Papii na Osusu nazo wakajikuta zikiporwa haraka haraka uku wakishangaa nazo zikielekea juu kama ilivyo kwa bunduki ya Butiliasi. Baada ya hapo wakajikuta watupu, Uchi kama walivyozaliwa.
“Bado mnataka kunijua” Aguati aliwauliza tena.
***************
Baridi kali lilikuwa likiendelea kuusumbua mwili wa Levina. Yale maumivu ya kipindi kile bado yalikuwa yakiendelea kumnyanyasa taratibu. Ukungu uliochanganyikana na giza jepesi uliteka eneo lote alipokuwamo Levina. Yule mtoto aliyeachiwa alikuwa akimsumbua sana Levina kwa kulia kwa sauti ya juu muda wote. Hakuwa akilia kwa maumivu bali yule mtoto alikuwa akilia kwa kukosa maziwa ya mama yake aliyokuwa ameyazoea toka amezaliwa. Maziwa ambayo asingeweza kuyapata tena. Maziwa ambayo Levina aligundua hilo tatizo. Alijitahidi kukamua ya kwake lakini haikusaidia chochote kwani maziwa yake hayakuweza kutoa chochote zaidi ya maji maji ya uchungu kwa mbali. Levina alijua sana kuwa mtoto anasikia njaa, tena alijua kuwa njaa ya mtoto ni mara kumi ya mtu mzima. Njaa mbayo ilitikisa tumbo laini la mtoto. Levina alihaha kumtafutia chakula. Alijitahidi japo kufungua kwenye lile begi na kutoa ile mikate,Akampatia! lakini haikusaidia kitu. Alitumia akili ya kuzaliwa ya kuchukua ile mikate na kuchanganya na maji katika kiganja cha mikono yake na kusaga kwa kutumia maji maji mpaka vikalainika na kuwa kama uji wa ulezi. Kwa mbali mtoto alianza kupokea mdomoni mwake. Mtoto alianza kufakamia taratibu mpaka akazoea. Levina hakuchoka kufanya hivyo hivyo mara nyingi atakavyo ili mtoto yule aweze kushiba. Mtoto tumbo likamjaa. Akashiba ndii!!
Maswali mengi yakakizingira kichawa cha Levina hakujua chanzo cha mtoto yule. Alijua tu mtoto yule ametekwa lakini hakujua ametekwa wapi kama ni Kenya ama Uganda au Tanzania. Alimuonea huruma mama yake na mtoto japo hakumjua. Akili yake ilijijenga kwa Hasira alizokuwa nazo Osusu na Papiii lazima mama wa yule mtoto atakuwa ni maiti uko alipo.
“Nitamlea mpaka mwisho wa maisha yangu” Alijisemea kimoyo moyo Levina uku akiwa amemshikilia yule mtoto ambaye kwa muda huu usingizi ulikuwa umeshamchukuwa kwa kushiba kile chakula alichokuwa amemlisha Levina. Levina alitoa vitu vyote ndani ya lile begi la Osusu na kumdumbukiza mtoto yule. Kisha alinyanyuka kwa kutumia gongo ambalo alitengenezewa na Butiliasi. Gongo la kutembelea vizuri kwakuwa alikuwa na mguu mmoja. Alimbeba yule mtoto bengani akiwa ndani ya lile begi nakuanza safari yake uku mkono mmoja akiwa ameshikilia kidumu cha maji nakutokomea zake kusikojulikana.
************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment