Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

MIMI KABLA YAKO - 5

 





    Simulizi : Mimi Kabla Yako

    Sehemu Ya Tano (5)



    Hatimaye walifika katika chumba husika kabla ya daktari huyu kukifungua na mwishoe waliingia, walimwona mkewe mkubwa Abraham akiwa amekaa katika kitanda chake. Alitabasamu sana baada ya kuwaona, labda zaidi kwa kumwona dakrari wake bwana Rashid. “Welcome doctor how’s your day?” (“karibu daktari, siku yako inaendaje?”) Alisikika mwanamke huyo ambaye alionekana kama siyo mwehu, alikuwa msafi na usoni hakuashiria kama alikuwa bado na ulemavu wa akili.

    “Okay, Okay I’m fine friend, but…. This police officer need to ask you some questions, is that right with you?” ( Sawa, sawa, mimi ni mzima rafiki lakini …. Huyu askari anahitaji kukuuliza maswali kadhaa, unatatizo na jambo hilo” Alisikika daktari Rashid aliyekuwa hajiamini akimweleza mke mkubwa wa bwana Abraham ambaye alivuta pumzi ndefu kabla ya kutikisa kichwa akikubali lakini ghafla alionekana akiwa mnyonge. “Thanks doctor, you can go now I need some minutes with her” (“Ahsante daktari, unaweza kwenda sasa, nahitaji dakika kadhaa”) Alisikika kijana wa bwana Leo kwa sauti yake nzito, zaidi ya hilo alikuwa amejengeka vizuri mwili wake jambo lililoashiria kuwa huenda hakuwa mtu wa mchezo. “Okay, okay” (“sawa, sawa”) Alisikika daktari Rashid huku akinyoosha mikono tayari kwa kuondoka aliongoza mpaka mlangoni akiwa na lengo la kutoka lakini ghafla aligeuka na kuonekana kama alihitaji kumwambia jambo askari, jambo ambalo hakulitimiza kwani alibaki kinywa wazi kwa sekunde kadhaa akishangaa. Alikuwa ameuona mchoro ( tattoo) ya nyoka katika shingo ya askari huyo ambaye wakati huo alikuwa akifunua faili lake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa miaka mingi alikuwa akielewa kuwa askari yeyote hahurusiwi kuwa na mchoro (tattoo) katika mwili wake lakini hii ya kijana huyu ilimchanganya zaidi. Alitoka haraka akiwa na wazo la kwenda kumpigia simu James ambaye alikuwa mhusika mkuu wa mgojwa huyo na alitaka kujua kama alikuwa akijua juu ya ujio wa askari yeyote katika hospitali yao kwa lengo la kumhoji mke mkubwa wa Abraham. Daktari Rashid alionekana akikimbia kuelekea kwenye eneo la lifti ili aelekee ghorofa ya kumi kulikokuwa na ofisi yake na huko ndiko alikuwa na namba ya simu ya James aliyoihifadhi kwenye simu yake. Hatimaye alionekana akiendelea kusubiria lifti eneo husika.

    Mara baada ya kuondoka kwa daktari Rashid, kijana wa bwana Leo aliyekuwa kwenye mwonekano wake wa kiaskari alitembea na kwenda kukaa kando ya mke mkubwa wa bwana Abraham ambaye mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana. “Okay, Mom here we go….” (“sawa mama, tunaanza…”) aliongea huku akifungua faili lake kama vile alikuwa tayari kwa kufanya mahojiano. Kabla hajaendelea na zoezi lolote, mara simu ya askari huyo iliita na alionekana kuchukizwa nayo, alitembea haraka kando karibu na mlango kabla ya kuipokea na kuanza kuongea kwa sauti ya chini, “hey Mr. Leo what’s up?... Let me finish this, …aah! Give me some time, …ooh! Yes we shall get that money” (“Hey bwana Leo kuna nini? …. Niache nimalize hili … aah! Nipe muda kidogo … ooh! Ndiyo tutazipata zile hela”) Aliongea kwa sauti ya chini ambayo mke mkubwa wa bwana Abraham aliisikia, hofu ilimtanda zaidi baada ya kuuona mchoro (tattoo) shingoni mwa askari huyo, aliisogelea haraka Maka-peni iliyokuwa mezani kwake na kuificha. Hatimaye kijana wa bwana Leo alimaliza kuongea na simu alianza kutembea kurudi katika kitanda cha mke mkubwa wa bwana Abraham, mwanamke ambaye alisikika akiongea kabla ya kijana huyo kufika kitandani hapo. “hey please, for few second can I go to toilet?” (“ hey tafadhari, kwa sekunde kadhaa naweza kwenda chooni?”) Alisikika mama huyo akimwambia kijana huyo ambaye alionekana kughadhabika sana. Kijana huyo hakumjibu zaidi ya kutikisa kichwa akikubali ombi hilo, Mkewe mkubwa bwana Abraham alitembea haraka kuelekea chooni katika choo kilichokuwa karibu na chumba hicho kilichojitosheleza kwa kila kitu. Hatimaye aliingia katika choo hicho, kijana wa bwana Leo alitembea na mwishoe aliishia kutaa kitandani huku akionekana kuwa na hasira.

    Baada ya dakika moja mke mkubwa wa bwana Abraham alitoka katika choo hicho huku akitabasamu, alikuwa hajashika kitu pia, wakati huo alikuwa na amani, alitembea na kisha aliishia kukaa mbele ya kijana wa bwana Leo. Kijana huyo alianza kumuuliza maswali tofauti ambayo alijibiwa kwa ufasaha na mwanamke huyo aliyeonekana kuwa na furaha. Ghafla kijana huyo alimrukia mwanamke huyo na kumkaba shingoni kwa nguvu huku akiwa amemlaza kitandani. Jambo lililomshangaza mwanamke huyo hakuhangaika kujitoa wala kupiga kelele, bila kupoteza muda kijana huyo alilitoa bomba lake aliloweka dawa awali lililokuwa kwenye mfuko wa sare zake, alilielekeza bomba hilo shingoni mwa mwanamke huyo kisha alimchoma kwenye mshipa mmoja wapo na mwishoe aliisukuma dawa iliyokuwa kwenye bomba hilo. Mwanamke huyo bado hakumsumbua, alikuwa mtulivu na wakati huo iliposukumwa dawa hiyo alionekana kupata maumivu fulani kwani alianza kuitupa tupa mikono na miguu yake, kijana huyo aliendelea kumshikilia kwa dakika tatu kabla ya kumwachia. Wakati huo mwanamke huyo alikuwa ametulia huku akiwa ametoa macho, hakuwa na nguvu tena. Kijana wa bwana Leo alichukua bomba lake la sindano na kulirudisha kwenye shati lake la sare hiyo kama awali. Alimlaza vizuri mwanamke huyo kitandani na kisha alimfunika na shuka lililokuwapo. Alibeba faili lake na kuanza kutembea, akiwa tayari kwa kuondoka, aliufuata mlango na kuufungua kisha alitoka na kuufunga, aliendelea kutembea akiondoka.

    * * *

    Mara baada ya kuondoka daktari Rashid akielekea ofisini kwake, alifika huko na kufanikiwa kumpigia simu James lakini tatizo lilikuwa moja kijana huyo alikuwa hapokei simu, alirudia zaidi ya mara kumi lakini haikupokelewa. Alijaribu kutafuta namba za simu za mahakama kuu ya kitongoji cha Des Moines kwa msaada wa mtandao lakini hakufanikiwa pia, jambo lilikuwa likimwingia moyoni mwake akiwaza kama alikuwa amechelewa sana kumwokoa mwanamke huyo, hisia zake zilikuwa zimetanda zikiamini mauaji tu. Aliwaza kwenda tena katika chumba cha mgonjwa wake ili akahakikishe kama alikuwa hai, alifikiria kuingia katika chumba hicho hata kama mahojiano yangekuwa bado yakiendelea.

    Baada ya kuwapo kwenye lifti kwa sekunde kadhaa hatimaye alitoka katika ghorofa ya pili na alianza kutembea kwa haraka akielekea chumba nambari thelathini na tano, alikuwa akitokwa na jasho kupindukia ingawaje hali ya hewa ilikuwa ni baridi. Wakati akiwa kwenye kordo akielekea huko alishtushwa kumwona kijana wa bwana Leo akitembea huku akitabasamu akiwa amevaa sare zake za askari wa Sheriff kama kawaida. “Hey, I told you that she knows something and now we have enough evidence” (“hey, nilikwambia anajua kitu na sasa tuna vielelezo vya kutosha”) Alisikika kijana wa bwana Leo akimwambia daktari Rashid. Kwa jinsi alivyokuwa akijiamini alipoteza hata hisia alizokuwa nazo daktari huyo, kidogo alianza kumwamini japo hakumwamini kabisa.

    Kijana huyo alimwomba daktari huyo amtoe, hakupinga kwa vile kijana huyo alionekana kujali sana jambo hilo na alikuwa akiendelea kumweleza mambo ya uongo aliyodai alielezwa na mke mkubwa wa bwana Abraham. Walitembea mpaka katika mlango mkuu wa kutokea katika hospitali hiyo, eneo ambalo daktari Rashid aliamua kuishia, ni wakati ambao alianza kurudi ndani na kijana wa bwana Leo alitembea haraka akielekea eneo la maegesho.

    Bila kupoteza muda aliingia kwenye gari lililokuwa na mwonekano wa gari za askari wa Sherrif huku akitabasamu alimuashiria jambo Aminata ambaye alionekana akitabasamu pia. Kijana huyo aliliwashwa gari hilo kabla ya kuongoza barabara kuu na huko alianza kuliendesha kwa kasi akiwa ameshika barabara iliyoelekea katika kitongoji cha Des Moines wakiuacha mji huo mdogo wa Urbandale. Aliliendesha gari hilo kwa nusu saa kabla ya kulisimamisha na kumweleza Aminata ashuke na atafute usafiri mwingine kwa usalama wao zaidi, kijana huyo alimweleza pia ahakikishe anakamilisha malipo ya mauaji hayo ndani ya siku tano, malipo aliyopaswa kuyafanya kwa Mr. Leo aliyekuwa bosi wa kijana huyo na mmiliki wa klabu ya Cowboys Night Club. Aminata hakubisha, alishuka kwenye gari hilo kabla ya kumshuhudia kijana huyo akiliondoa kwa kasi akimwacha. Bila kuchelewa Aminata naye alikodi teski ambayo alihitaji impeleke nyumbani kwake katika mji mdogo wa Saylor. Ikawa hivyo aliondoka eneo hilo na gari akiwa na furaha kidogo huku akiwa amemweleza dereva wa gari hilo amuwahishe nyumbani kwake.

    * * *

    Daktari Rashid alikuwa amechanganyikiwa kupindukia baada ya kugundua mke mkubwa wa bwana Abraham ameuawa na kijana ambaye aliamini hakuwa askari pia, alijilaumu na kulia kwa uchungu akijihisi kuhusika na kifo. Wakati huo alikuwa anazunguka zunguka katika hospitali hiyo ya St. Joseph Lunacy Hospital, taarifa hizo za kuuawa kwa mwanamke huyo zilikuwa zimeshamfikia James na David walioahidi kufika hospitali hapo haraka iwezekanavyo. Askari wa mji huo wa Urbandale walikuwa wamepewa taarifa na waliahidi kufika eneo la hopsitali hiyo baada ya muda mfupi. Ikawa hivyo, baada ya nusu saa askari wa mji huo walifika katika hospitali hiyo, mara baada ya kuuangalia vizuri mwili huo waliwahurusu madaktari waendelee na uchunguzi zaidi kwa mwanamke huyo.

    Hatimaye mwili wa mke mkubwa wa bwana Abraham ulichukuliwa na kupelekwa maabara ambako madaktari walianza kuuchunguza ili kujua sababu kubwa iliyopelekea kifo cha mwanamke huyo. Wakati madaktari wakiendelea na uchunguzi wao zaidi ni wakati ambao askari walikuwa wakichukuwa maelezo kutoka kwa daktari Rashid na mwanamke ambaye alikuwa eneo la mapokezi. James, David na Jacqueline walifika eneo la hospitali hiyo wakati zoezi hilo la kuhojiwa kwa daktari na mwanamke wa mapokezi likiendelea. Wote walionekana kuchanganyikiwa na zaidi David aliyeanza kupoteza matumaini kabisa, hakuwa na shahidi mwingine zaidi ambaye angeweza kumsaidia katika kesi yake dhidi ya bwana Abraham. Ushirikiano aliokuwa akiupata kutoka kwa wakuu wa polisi wa nchini Uganda ulikuwa mdogo na wakati huo aliamini angeshidwa kuwa na shahidi katika kesi hiyo iliyopaswa kusikilizwa tena baada ya siku saba zilizosalia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya saa moja madaktari wa hospitali hiyo walikuja na majibu yao mbele ya askari wa mji huo na kina David pia, uchunguzi wao ulionyesha marehemu alikuwa amechomwa na bomba sindano eneo la shingoni na walimini bomba hilo lilimwingizia sumu hatari aina ya Strychnine iliyomuua mwanamke huyo. Sumu hiyo ya Strychnine inauwezo wa kumuua binadamu ndani dakika nane mpaka kumi na ni sumu ambayo ilielezwa kuwa ni vigumu kwa mtu kupona hata madaktari wakimuwahi ikiwa imeshamwingia. Swali lililofuata lilihusiana na juu ya mtu aliyemuua na ni kwa nini alimuua? David alijibu swali hilo huku akieleza imani yake kuwa mwanamke huyo alikuwa ameuawa kwa amri ya mkewe mdogo wa bwana Abraham, Aminata huku akiamini alifanya hivyo ili kupoteza ushahidi uliopaswa utolewe katika kesi ya mume wake.

    Askari waliona mawazo hayo yalikuwa ya msingi sana, waliamua kupiga simu katika kituo cha polisi cha mji wa Saylor ambao mwanamke huyo, Aminata alikuwa akiishi. Waliwaagiza askari wa kituo hicho waende haraka sana nyumbani kwa mama huyo ili wakafanye mahojiano naye juu ya mauaji hayo yaliyokuwa yametokea. Askari wa kituo hicho waliahidi kutoa ushirikiano katika zoezi hilo, kwani waliwajibu askari wenzao kuwa wangeenda katika nyumba ya mwanamke huyo ndani ya nusu saa.



    Baada ya saa moja askari wa kituo cha Saylor walipiga simu wakieleza kukamilisha mahojiano yao na mwanamke huyo, Aminata ambaye alikana kuhusika na mauaji hayo lakini zaidi walikuwa wakiamini kwamba alikuwa ameeleza jambo la ukweli, hawakuhisi mwanamke huyo alikuwa akihusika na mauaji hayo. Wakati huo James na wenzie walionekana kuchanganyikiwa zaidi juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea, mambo yalionekana kuwa magumu kadri dakika zilivyozidi kwenda. Hawakuwa na jinsi zaidi ya kufikiria kufanya mazishi ya mwanamke huyo siku iliyofuata ili waanze kuangalia ustaarabu mwingine. Ikawa hivyo, siku iliyofuata mwanamke huyo aliyekuwa mke mkubwa wa bwana Abraham alizikwa katika makaburi ya mji huo wa Urbandale. Mazishi yake yalifanikishwa na askari wa mji huo pamoja na James, Jacqueline na David ambao walikuwa kama ndugu pekee waliohudhuria mazishi hayo.

    Siku hii pia kijana aliyehusika na mauaji ya mwanamke huyo alianza kutafutwa katika mji huo. Hawakuwa na picha halisi ya kijana huyo lakini walitumia chache walizozipata kupitia kamera za ulinzi za hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital. Waligundua kuwa kijana huyo alikuwa makini na kazi yake hiyo kwa vile picha zote hazikumwonyesha sura yake vizuri, alikuwa akiinamisha kichwa chake wakati akitembea katika hospitali hiyo na jambo hilo lilianza kuonekana kuwa tatizo katika zoezi la kumtafuta kijana huyo.

    Wakati msako dhidi ya kijana huyo ukiendelea David, Jacqueline na James walirudi katika hoteli yao ya Des Moines Motel wakiwa wamechanganyikiwa sana, ni wakati ambao walitumia muda mwingi kupiga simu nchini Uganda wakiomba msaada kwa askari wa jeshi hilo, msaada ambao haukupatikana. Walizidi kuchanganyikiwa zaidi kwa vile hawakupata taarifa yeyote ya kukamatwa kwa kijana ambaye alikuwa amefanikisha mauaji dhidi ya mke mkubwa wa bwana Abraham, kijana ambaye waliamini angeeleza mtu ambaye alikuwa amemtuma kufanikisha mauaji hayo. Bado walikuwa wakiamini kuwa Aminata alikuwa akihusika na mauaji hayo lakini hawakuwa na ushahidi wa jinsi gani alihusika. Walibaki watulivu huku wakitegemea msaada kutoka kwa jeshi la polisi la nchini Uganda ambalo bado halikuonyesha ushirikiano wa kutosha.

    * * *

    Aminata alikuwa nyumbani kwake muda wote huku akiwa na imani kuwa kufanya jambo hilo kungeweza kumuepusha kuhusishwa na mauaji ya mke mkubwa wa bwana Abraham. Moyoni alikuwa na furaha kwani alihakikisha kifo cha mwanamke huyo kilichotangazwa na televisheni tofauti za jimbo hilo, wakati huo alikuwa akiwaza kwenda kumfikishia ujumbe huo mume wake ili kumpunguzia hofu akiwa katika kituo cha polisi cha Altoona. Tayari alikuwa amempata wakili wa kesi hiyo ambaye kwa wakati huo alikuwa amevutiwa na mazingira ya kesi na aliamini wangeweza kushinda kesi hiyo. Ingawaje aliumia kidogo kwa kujihusisha katika mauaji kwa mara ya kwanza lakini alipuuzia jambo hilo kwa vile kwake mke mkubwa wa bwana Abraham hakuwa na mchango na jambo alilolithamini ni uwepo wa mume wake nyumbani kwao siku zote.

    Hatimaye ilifika siku ya Ijumaa, siku ambayo zilikuwa zimepita siku tano toka mauaji dhidi ya mkewe Abraham yafanyike. Siku hii ndiyo alifikiria kwenda kumtembelea mume wake na pia aliwaza kwenda katika klabu ya Cowboys Night Club ili kulipa malipo ya mauaji dhidi ya mke mkubwa wa bwana Abraham.

    Majira ya saa nne asubuhi alikuwa barabarani akiliendesha gari lake la ghari aina ya Rolls-Royce Phantom kwa kasi akiwa ameshika barabara iliyoelekea mji wa Altoona huku akikiacha kitongoji hicho cha Des Moines. Kichwani alikuwa akiwaza kwenda kutoa taarifa ya kifo cha mke mkubwa wa bwana Abraham taarifa aliyoamini ilikuwa njema. Baada ya saa moja alikuwa katika kituo kikuu cha polisi cha mji wa Altoona ambacho mumewe alikuwa akishikiliwa. Askari walimpeleka mpaka kwenye chumba cha wageni na alikaa upande wa pili wa kijumba kimoja wapo huku akitenganishwa na dirisha ambalo lilikuwa na uzio wa chuma na kioo kizito. Alibaki ametulia huku akiwa mnyonge kiasi, alikuwa ameishika simu ya mezani ya eneo hilo akiwa tayari kwa kuongea na mume wake bwana Abraham.

    Baada ya dakika nne mumewe huyo alitolewa kutoka kwenye chumba chake na kufikishwa upande wa pili tayari kwa maongezi na mkewe. Ndani ya muda mfupi alionekana kupungua sana mwili wake na zaidi alikuwa mnyonge. Nyuma yake alionekana askari mmoja aliyejengeka mwili akiwa amesimama. Alichukua simu ya mezani kabla ya kusikika akimuuliza swali mkewe. “hey, how things?” (“hey, mambo yanaendeleaje?”) Aliongea bwana Abraham kwa mara ya kwanza akimuuliza. “ AAP…, so how do they treat you?”( “AAP…., kwani wanakuhudumiaje?”) Alisikika mkewe akijibu, jibu lililomfanya mumewe atabasamu aligundua jambo tayari. “AAP,….oops! you might be kidding me? They treat me good” (“AAP … oops! utakuwa unanidanganya, wananihudumia vizuri”) Alisikia bwana Abraham.

    “Why? I can’t lie to you” (“ Kwa nini? siwezi kukudanganya”) Alimjibu mkewe na maongezi yao mengine yaliendelea huku bwana Abraham akionekana kusawazika makunyanzi yake ya usoni na unyonge ulipungua. Baada ya dakika kumi mkewe Aminata aliondoka kituoni hapo huku akiwa na furaha baada ya kuamini kuwa alishamfikishia ujumbe mume wake na furaha yake iliongezeka zaidi kwani aliamini alikuwa amempunguza mawazo. Alikuwa amefikisha taarifa ya kifo hicho kwa staili yake. AAP kilikuwa ni kifupisho ambacho bwana Abraham alipenda kukitumia na vijana wake ili kuficha siri zao mara baada ya kazi kadhaa kufanyika. Aminata alifahamu pia maana ya herufi hizo zilizomaananisha “All As Planned” (“Kila jambo kama lilivyopagwa”).

    Tayari alielewa kwamba mume wake alilitambua jibu alilomwambia kwa vile mara ya mwisho alipewa kazi ya kuhakikisha anamuua mke mkubwa wa bwana Abraham.

    Wakati huo alikuwa akiliendesha gari lake kwa kasi akirudi katika kitongoji cha Des Moines, alikuwa akiwaza kwenda kumwona bwana Leo na kumkamilishia malipo yake baada ya kijana wake kufanikisha mauaji dhidi ya mke mkubwa wa bwana Abraham. Baada ya saa moja alikuwa akiegesha gari lake katika eneo la maegesho la benki ya Atlantic Stewardship Bank, mara baada ya kuegesha gari hilo alishuka haraka na kuanza kutembea akielekea ndani ya benki hiyo na mwishoe aliingia. Bila shaka alikuwa akienda kuchukua fedha kwa ajili ya malipo ya bwana Leo.

    Baada ya dakika kumi alitoka katika benki hiyo akiwa ameshika vizuri mkoba wake, aliongoza mpaka kwenye gari lake kabla ya kuingia na kuliondoa kwa kasi eneo hilo la benki. Wakati huo alikuwa akiliendesha kwa kasi akielekea katika klabu ya Cowboys Night Club iliyomilikiwa na bwana Leo, klabu iliyokuwapo nje kidogo ya kitongoji hicho cha Des Moines. Dakika ishirini na tano baadaye alikuwa akiegesha gari hilo nje ya klabu hiyo. Hakupoteza muda alitembea haraka akielekea eneo la ndani. Hakusumbuliwa na mhudumu aliyekuwapo eneo la kaunta ambaye alimwongoza kuelekea eneo ambalo bwana Leo alikuwapo akipanga mikakati yake siku zote, eneo lililokuwa chini ya klabu yake hiyo ya pombe. Mwishoe Aminata aliingia katika chumba kilichovutia cha bwana Leo ambacho muda wote alikuwa akihudumiwa na warembo kadhaa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara baada ya mhudumu aliyemsindikiza Aminata kurudi kaunta, bwana Leo aliwakonyeza warembo walikuwa wakimhudumia waliokuwapo katika chumba hicho kikubwa ambao waliondoka na kuelekea katika chumba kingine kama ilivyokuwa kawaida yao. Wakati huo bwana Leo alikuwa akivuta msokoto ambao Aminata aliamini ulikuwa ni wa bangi kama alivyomwona akivuta mara ya mwisho pia, hakujali juu ya jambo hilo alitoa fedha zote alizozichukua kwa ajili ya malipo kwa bwana Leo na kuziweka mezani. Bwana Leo alizichukua fedha hizo na kuanza kuzihesabu taratibu, baada ya dakika tatu alimaliza kabla ya kunyanyuka akiwa amekasirika, kuna jambo lilionekana kuto kuwa sawa hata Aminata alianza kuogopa.

    “Hey mom, stop playing with me, I told you to bring forty eight thousands dollar, how much is this?” (“Hey mama, usinichezee, nilikwambia uniletee dola elfu arobaini na nane, hizi ni shilingi ngapi?”) Alisikika bwana Leo baada ya kuwa kimya kwa sekunde kadhaa akimwangalia Aminata. “Oops! Sorry Mr. Leo, I heard like you needed forty five thousands, don’t worry money is not a problem, I will bring here ten thousands dollar by tomorrow, I hope you will be happy” (“Oops! Samahani bwana Leo, nilikusikia kama ulihitaji dola elfu arobaini na tano, usijari fedha siyo tatizo, nitakuleteta kesho dola elfu kumi, nadhani utafurahi”) Alisikika akiongea Aminata na kumfanya bwana Leo atabasamu kidogo kwani alikuwa akimdai mwanamke huyo dola elfu tatu tu. “…And make sure you do that..” (“… Na uhakikishe unafanya hivyo…”) Alimalizia tabasamu lake kwa kuongea hayo bwana Leo. Mwishoe Aminata aliondoka katika klabu hiyo ya bwana Leo akiwa amemwahidi kurudi siku iliyofuata iliyokuwa ya Jumamosi na Jumatatu ya juma lililofuata kesi ya bwana Abraham ilitarajiwa kusikilizwa kwa mara nyingine.

    * * *

    David, Jacqueline na James walionekana kuchanganyikiwa kadri siku zilivyozidi kusogea ili kesi ya bwana Abraham isomwe tena. Tayari wakati huo ikiwa ni siku ya Ijumaa walikuwa wamebakiwa na siku tatu ili kesi hiyo isomwe tena siku ya Jumatatu. Hawakujua jambo la kufanya kwa vile walikuwa wamekosa kabisa ushirikiano kutoka kwa jeshi la polisi nchini Uganda. Walibaki watulivu huku wakimwomba mwenyezi Mungu awasaidie katika zoezi hilo zito lililokuwa mbele yao, walihitaji haki itendeke. Wakati wakiwa bado hawajafikiria jambo la kufanya kwa wakati huo David alitoa wazo, aliwaambia waende katika hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital. Alihitaji wakakikague chumba cha mke mkubwa wa bwana Abraham aliyekuwa marehemu kwa wakati huo. Awali wenzie walipinga zoezi hilo, lakini kwa vile hawakuwa na jambo walilokuwa wakilifanya walikubali kutembelea katika hospitali hiyo.

    Majira ya saa tano asubuhi walikuwa kwenye gari la James aina ya Ferarri lililokuwa likiendeshwa kwa kasi kiasi kuelekea katika hospitali St. Joseph Lunacy Hospital iliyokuwa katika mji wa Urbandale. Baada ya saa moja walikuwa wamefanikiwa kufika katika hospitali hiyo, gari lao lilionekana likiegeshwa katika eneo la maegesho. Mara baada ya kuegeshwa, walishuka na walianza kutembea taratibu wakielekea katika hospitali hiyo huku wakiwa wanyonge. Mara baada ya kufika katika eneo la mapokezi waliomba kukutana na daktari Rashid. Mwanamke aliyekuwa eneo hilo alimpigia simu daktari huyo ambaye aliahidi kuwafuata. Baada ya dakika kadhaa daktari huyo alifika na kusalimiana nao, ni wakati ambao David alimwomba daktari huyo awahurusu kwenda kukiangalia chumba alichokuwa akikaa mke mkubwa wa bwana Abraham aliyekuwa ameshafariki.

    Daktari huyo hakuwa na pingamizi na alianza kutembea akiwaongoza katika chumba hicho ambacho hakikuwa na mgonjwa mwingine kwa wakati huo. Baada ya dakika kumi walikuwa katika chumba hicho wakikichunguza, David ndiye aliyeonekana akikagua zaidi kila eneo la chumba hicho. Hali ilikuwa tofauti kwa daktari Rashid, Jacqueline na James ambao muda wote walikuwa wamesimama huku wakiamini kuwa chumba hicho hakikuwa na kitu. Baada ya dakika mbili David naye aliacha zoezi hilo huku akiwa amekata tamaa. Alikaa kwenye kitanda kilichokuwapo huku akionekana kuchoka, James na wenzie bado walikuwa wamesimama. Utulivu ndiyo ulikuwa umetawala kwani hakuna mtu aliyekuwa akiongea, wakati huo ulikuwa mgumu kwao.

    ‘Hey sir, can I use that toilet?” (“Hey, naweza kutumia choo kile?”) Alisikika Jacqueline kwa sauti ya chini akimweleza daktari Rashid ilhali akionyesha choo hicho. “Why not? You can use it” (“Kwa nini usitumie? Unaweza kukitumia”) Alimjibu daktari Rashid kwa sauti ya chini pia.

    Jacqueline alitembea taratibu kabla ya kuingia katika choo hicho, mara baada ya kuingia aliiona maka-peni ikiwa imetupwa katika tundu la choo hicho huku ikielea, jambo hilo lilimkatisha tamaa za kutimiza haja zake, alibaki amesimama huku akizungusha macho yake huku na huko kabla ya kuyaona maandishi madogo yaliyoandikwa ukutani. Kwa haraka aliamini maandishi hayo yalikuwa yameandikwa na maka-peni aliyoiona. Aliusogelea taratibu ukuta huo kabla ya kuanza kuona kilichoandikwa ukutani hapo, aliyasoma maandishi hayo yaliyokuwa yameandikwa hivi.



     ‘ Dear David … Joseph Kanyenzi ( Killa Jose ). Please forgive me’ (‘Kwako David …. Joseph Kanyenzi (Killa Jose). Tafadhari nisamehe.’) Alimaliza kusoma ujumbe huo Jacqueline, ujumbe ambao ulionekana kama uliandikwa haraka.

    “Hey, guys there’s something here” ( “Jamani kuna kitu hapa”) Alisikika Jacqueline ambaye aliwafanya wenzie wote waingie katika choo hicho haraka, David alikuwa wa kwanza kwenda kuusoma ujumbe uliokuwa umeandikwa ukutani kwa furaha alisikika, “now, this is the answer…” (“sasa, hili ndiyo jibu”).

    Daktari Rashid alikuwa akiiangalia maka-peni ambayo siku zote ilikuwa katika chumba cha mke mkubwa wa Abraham, alikumbuka hata siku aliyouawa mwanamke huyo aliiona maka-peni hiyo. Hisia zake zilianza kumwingia akiamini mwanamke huyo aliandika ujumbe huo kabla ya kuuawa kwa vile maandishi yake yalionekana kama yaliandikwa kwa haraka sana. James bado hakuwa na furaha sana, bado hakuelewa jina hilo lililoandikwa ukutani lilikuwa likimaananisha nini. David alihisi mtu aliyekuwa ameandikwa ukutani hapo alikuwa ni raia wa Uganda na kwa vyovyote vile aliamini kwamba aliandikwa ili awasaidie katika ushahidi wa kesi yao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kupoteza muda waliamua kupiga simu katika kituo kikuu cha polisi cha jiji la Entebbe ambako walikuwa wakipiga kwa wiki kadhaa mpaka wakati huo, mara baada ya simu yao kupokelewa waliomba msaada wakutafutwa kwa bwana Joseph Kanyenzi au Killa Jose. Lilipotajwa jina la Killa Jose, mkuu wa kituo aliwakatisha maelezo yao kwa kuwaeleza kuwa kijana huyo alikuwa ni mhalifu sugu aliyesumbua nchini humo miaka kadhaa iliyokuwa imepita.

    Wakati huo Killa Jose alikuwa jela akitumikia kifungo cha miaka kumi huku akiwa amebakiwa na mwaka mmoja ili atoke, kifungo hicho kilifuata baada ya kukamatwa na hatia ya kujaribu kufanya mauaji dhidi ya tajiri mmoja miaka kumi iliyokuwa imepita. Taarifa hiyo ilikuwa njema kwa David na wenzie ambao walifurahi ghafla, waliomba wapewe nafasi ya kuongea na mfungwa huyo. Mkuu huyo wa kituo aliwaahidi kuongea na mkuu wa gereza kuu la Ndolwa alikofungwa mhalifu huyo ili waweze kuongea naye. David, Jacqueline na James wakiwa na furaha waliondoka katika hospitali hiyo ya St. Joseph Lunacy Hospital na kuelekea katika hoteli yao waliyokuwa wakiishi ya Des Moines Motel iliyokuwapo katikati ya kitongoji hicho. Baada ya saa mbili waliweza kuunganishwa na mhalifu huyo Joseph Kanyenzi maarufu kama Killa Jose ambaye aliwapa ushirikiano wa kutosha.

    “I hate Mr. Abraham; he used me wrong, he’s a reason why I’m in Jail. He assigned me to murder his fellow businessman, the trial that brought me in Jail” (“Namchukia sana bwana Abraham, alinitumia vibaya, yeye ni sababu ya mimi kuwa jela, alinipa kazi ya kumuua mfanyabiashara mwenzie, jaribio lililonileta jela”) Alisikika Killa Jose. Aliendelea kulalamikia pia kitendo cha tajiri huyo kutomtembelea hata siku moja akiwa jela ilhali alikuwa amemsaidia katika kazi zake nyingi na zaidi alikuwa akijua siri zake pia. Walipomuuliza juu ya mke mkubwa wa bwana Abraham, Killa Jose aliwaeleza kuwa aliwahi kupewa kazi ya kumuua mama huyo lakini alimnusuru katika kifo hicho baada ya kutengeneza mazingira yaliyowafanya vijana wenzie na bwana Abraham waamini kuwa mwanamke huyo alikuwa amefariki. Mwishoni walimuuliza kama angeweza kutoa ushahidi juu ya kesi iliyokuwa ikimkabili bwana Abraham, Killa Jose alikubali kuwasaidia katika zoezi hilo.

    Wakiwa na furaha, David na James walianza kuwasiliana na wakuu wa jeshi la polisi na magereza wa nchini Uganda, walikuwa wakiomba msaada wa kusafirishwa kwa mfungwa Killa Jose aliyekuwapo katika gereza la Ndolwa. Zoezi hilo halikuwa gumu sana kwani waliombwa watume fedha za kutosha kwa ajili ya safari ya kila Jose na askari ambaye angeongozana naye katika safari hiyo, fedha hizo zilikuwa zinapaswa kuwa za kwenda na kurudi nchini Marekani pamoja na gharama za malazi. Jambo hilo halikuwa gumu kwani ndani ya masaa sita James alikuwa ametuma dola elfu hamsini kwa wakuu wa jeshi la polisi wa nchi hiyo akiwa na lengo kuu la kuona Killa Jose anasafirishwa mpaka Marekani. Hakujari kabisa juu ya fedha alizokuwa amezituma, alihitaji kumshuhudia shahidi huyo akifika nchini Marekani kumsaidia rafiki yake David. Furaha yao iliongezeka zaidi baada ya kugundua kuwa Killa Jose alikuwa ni miongoni mwa vijana waliomsindikiza bwana Abraham katika fukwe za ziwa Victoria siku aliyo dhamiria kumuua David kwa kumpiga risasi mbili na hatimaye kutupwa kwa David katika ziwa hilo kabla ya kuokolewa na Otieno Ndakufulika.

    Hatimaye safari ya Killa Jose kuelekea nchini Marekani kutoa ushahidi katika kesi dhidi ya bwana Abraham ilikamilika, mhalifu huyo alikuwa akitarajiwa kusafiri siku ya Jumanne ya tarehe ishirini na moja ya mwezi huo wa Februari. Alikuwa chini ya mwanajeshi aliyefahamika kwa jina la Moses Mgallah, kijana aliyekamilisha mafunzo yake ya kijeshi nchini Cuba. Alikuwa akiaminika sana na kwa kufanya hivyo waliamini wangepunguza gharama za kumsafirishwa Killa Jose chini ya askari wawili kwani mhalifu huyo alikuwa mtu hatari pia. Taarifa hizo za kufurahisha kwa David na wenzie walizipata siku ya Jumapili na walikuwa wakiwaza kumwomba jaji wa kesi hiyo aisogeze mbele kwa vile ilisomwa tena siku iliyofuata, siku ya Jumatatu.

    Hawakuwa na hofu juu ya jambo hilo kwa vile walihakikishiwa pia na mawakili kadhaa kuwa ombi lao lazima lingesikilizwa. Siku iliyofuata majira ya saa mbili asubuhi walionekana wakiwa wanaelekea katika eneo la maegesho ya magari. Jacqueline alikuwa amependeza na gauni lake ilhali David na James walikuwa wamevaa suti nyeusi zilizowapendeza pia. Mara baada ya kuingia kwenye gari la James aina ya Ferarri kijana huyo aliliondoa kwa kasi kiasi, safari ikiwa imeanza wakielekea katika mahakama kuu ya kitongoji hicho cha Des Moines ili kusikiliza kesi ya bwana Abraham iliyotarajiwa kusomwa tena kwa mara ya pili.

    * * *

    Aminata akiwa mke mdogo wa Abraham mara baada ya kuondoka katika klabu ya bwana Leo ya Cowboys Night Club alikuwa na furaha sana. Hakujali hata kiasi kidogo cha dola elfu kumi alichokuwa amemwahidi bwana Leo, zilikuwa ni fedha chahe ukilinganisha na uwezo wake. Aliamini angeweza kumpa hata zaidi ya fedha hizo alizozihitaji. Siku iliyofuata ya Jumamosi alikuwa bize akiongea na wakili aliyekuwa na jukumu la kumtetea mumewe. Alitumia muda wa siku nzima kumwelezea wakili huyo kila kitu alichotakiwa kumweleza kwa vile wakili huyo alihitaji kujua mambo mengi. Wakili wa kesi hiyo aliyaelewa mambo yote yaliyojiri kipindi cha nyuma, bado alikuwa na uhakika wa kuweza kumsaidia bwana Abraham kama asingepatikana shahidi mwingine wa uhakika kama ilivyokuwa kwa mke mkubwa wa bwana Abraham aliyekuwa marehemu wakati huo.

    Siku iliyofuata Aminata aliimaliza akiwa nyumbani kwake na mwanaye mdogo Anita, alikuwa akiifikiria kesi ya mume wake hata malipo aliyopaswa ayafanywe kwa bwana Leo alianza kusahau. Wakati huo alikuwa akiiwazia kesi hiyo iliyotarajiwa kusikilizwa kwa mara nyingine siku iliyofuata. Hatimaye siku hiyo ya Jumatatu ilifika, majira ya saa mbili asubuhi, Aminata alionekana akitoka nyumbani kwake akiwa amependeza ilhali akiwa amebeba mkoba wake mdogo, aliongoza mpaka katika eneo la maegesho la nyumba yao na mwishoe aliingia katika moja ya gari la kifahari aina ya Mercedez Benz lililokuwa toleo jipya kwa wakati huo. Aliliendesha kwa kasi kiasi akiondoka nyumbani kwake hapo, nyumba iliyokuwapo katika mji wa Saylor. Alihitaji kufika haraka katika mahakama kuu ya kitongoji cha Des Moines ili kusikiliza kesi ya mume wake iliyotarajiwa kusikilizwa siku hiyo kwa mara ya pili, alikuwa akiamini kuwa huo ungekuwa mwanzo wa ushindi wa familia yake.

    Baada ya saa moja na robo, gari lake lilionekana likiegeshwa katika eneo la maegesho ya magari katika mahakama kuu ya Des Moines. Ni wakati ambao Aminata alimtafuta wakili wa mume wake aliyekuwa ameshafika mahakamani hapo. Baada ya dakika kadhaa walionekana wakiongea jambo na wakili huyo. Alikuwa ameliona gari la James lakini hakujua eneo ambalo kijana huyo pamoja na David walikuwapo. Alikuwa akiwachukia sana na kuna wakati alitamani kama aandae zoezi la kumuua David lakini kwa wakati huo zoezi hilo lilikuwa gumu kwa vile kijana huyo alikuwa akilindwa na fedha ya rafiki yake James sawasawa.

    Hatimaye ilipotimia saa nne kasoro asubuhi walianza kujongea katika chumba husika kilichopaswa kutumika kusikilizwa kesi ya mume wake. Huko kulikuwa na watu wengi waliokuwa wameshafika, wakiwapo James, Jacqueline na David, zaidi ya hao walijitokeza watu kadhaa waliokuwa wakitokea Afrika Mashariki ambao waliishi nchini humo. Utulivu ndiyo uliokuwa umetawala na ilipofika saa nne kamili bwana Abraham alifikishwa kizimbani tayari kwa kesi yake kuanza. Wakili wake alikuwa amesogea mbele na alikuwa tayari kwa kumtetea mteja wake. Jaji wa kesi hiyo aliisoma kwa mara nyingine kabla ya kuwaita watu wa upande wa ushahidi kutoa utetezi wao. James alisimama na kuelezea tukio lililokuwa limetokea juma lililopita, tukio lililokuwa la kuuawa kwa mke mkubwa wa bwana Abraham ambaye alikuwa shahidi mkubwa. Alielezea juhudi za jeshi la polisi zilizoendelea za kumtafuta mhusika wa mauaji hayo. Jaji wa kesi hiyo alishtuka kidogo na kwa jinsi alivyokuwa, alionekana kama aligundua jambo.

    James hakuishia hapo alianza kueleza juu ya shahidi wao mwingine ambaye alitarajiwa kufika nchini Marekani siku iliyofuata. “….yeah we have another witness from Uganda who’s Joseph Kanyenzi, he will be coming in America by tomorrow, this time we shall make sure no one touches our informant” (“…ndiyo tuna shahidi mwingine kutoka Uganda anayeitwa Joseph Kanyenzi, atakuwa akija Marekani kesho, wakati huu tutahakikisha hakuna mtu anayemgusa shahidi wetu”) Alisika James akiendelea na maelezo yake mbele ya jaji, wakati huo maelezo yake yalimshtua sana bwana Abraham ambaye kila mtu aliweza kumwona mahakamani hapo akishtuka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    . Jasho lilianza kumtiririka kama vile alikuwa amenyeshewa na mvua hata jaji wa kesi hiyo aliligundua hilo. Hakuwa bwana Abraham peke yake hata mkewe Aminata alishtuka pia kwani alimtambua vizuri Joseph Kanyenzi maarufu kama Killa Jose. Alitambua mtu huyo alikuwapo jela nchini Uganda baada ya kukamatwa wakati akiwa katika jaribio la kumuua tajiri mmoja aliyekuwa mpinzani wa mumewe na zaidi alitumwa na bwana Abraham. Jambo lililomchanganya zaidi Aminata lilihusiana na ukweli kwamba Killa Jose alikuwa akijua mambo mengi kuliko hata mkewe mkubwa bwana Abraham aliyekuwa marehemu kwa wakati huo. Huku akitokwa na jasho pia alihisi kuchanganyikiwa kadri James alivyoendelea kujieleza. Hata wakili wa bwana Abraham aliamini kuna jambo halikuwa sawa tayari. James alimaliza kwa kuomba hekima za jaji wa kesi hiyo zitumike ili kesi hiyo isikilizwe tena baada ya siku mbili wakati shahidi huyo wa kesi hiyo akiwa amefika katika jimbo hilo.

    Jaji wa kesi hiyo aliyeonekana kuwa na hamu ya kuujua ukweli pia alisika “nothing can proceed now until our witness steps in our court and tell us what he knows about Mr. Abraham” (“Hakuna jambo litakaloendelea kwa sasa mpaka shahidi wetu afike mahakamani na kutuambia anachokijua kuhusu bwana Abraham”) Alisikika jaji huyo kabla ya kugonga nyundo akiwa ametangaza kesi hiyo isikilizwe tena siku ya Alhamisi. Aminata alikuwa mtu wa kwanza kutoka mahakamani hapo akiwa na hasira, alikuwa ameushika ufunguo wa gari lake mkononi, wakili wa bwana Abraham alimfuata haraka nje. Mwanamke huyo alikuwa amechanganyikiwa kiasi kwamba alisahau hata mkoba wake aliofika nao mahakamani hapo. Mara baada ya kutoka nje hakujali sauti ya wakili aliyekuwa akimwita, aliongoza mpaka kwenye eneo la maegesho kabla ya kuingia kwenye gari lake na kuliwasha, aliliondoa kwa kasi sana eneo hilo akiwa na hasira.

    Wakati huo watu waliofika mahakamani hapo walianza kuondoka taratibu, huku James, Jacqueline na David wakionekana wanakumbatiana, walikuwa na furaha na walielewa kila jambo lilikuwa likienda kama lilivyopagwa. Bwana Abraham naye alikuwa ameshaondolewa mahakamani hapo. Wakiwa wa mwisho James na wenzie walianza kutoka pia mahakamani hapo lakini David aligundua kitu, hakuwaambia wenzie. Aliuona mkoba alioamini ulikuwa wa Aminata kwa vile ulikuwa karibu na eneo alilokuwa amekaa, alitembea haraka kuufuata. Mwishoe aliuchukuwa na alianza kutembea akiwafuata James na Jacqueline na mwishoe walikuwa nje. James alimshauri David aurudishe mkoba huo mahakamani ili mwanamke huyo aufuate, lakini David alikuwa anasita, hakuwa tayari kufanya jambo hilo. Jacqueline naye aliungana na James akimwomba David aurudishe mkoba huo lakini bado kijana huyo alikuwa akisitasita.

    Walibaki wamesimama eneo hilo la nje kwa dakika kadhaa wakishauriana huku James akiamini wangetafuta matatizo kwa kuondoka na mkoba huo. David alikuwa na lengo la kwenda kuuchunguza mkoba huo na pia simu ya mwanamke huyo kama ilikuwepo, aliamini asingekosa kitu cha kuwasaidia. Wenzie hawakukubaliana na mawazo hayo. Wakati wakiendelea na mabishano mara simu ya Aminata ilianza kuita toka kwenye mkoba huo, David aliufungua haraka na kuitoa simu hiyo. Alipoiangalia aligundua mpigaji alikuwa anaitwa Mr. Leo, alitaka kuipokea simu hiyo lakini aliwaza jambo, aliamua kumpa simu hiyo Jacqueline na alimweleza aipokee, David alisogeza sikio lake akitaka kusikia mazungumzo ambayo yangefuta. “hey mom, where you at?” (“hey mama, uko wapi?”) Ilisikika sauti ya bwana Leo kutoka upande wa pili wa simu, alionekana kama alikuwa na jazba.

    “Home… what’s up Mr. Leo?” (“nyumbani…. Kwani kuna nini bwana Leo?”) Alisikika akiuliza Jacqueline. “Hey, listen to kill someone isn’t easy task, I give you three hours to pay the remained cash, failure to that, I will plan what to do” (“ hey, sikiliza kuua mtu siyo kazi rahisi, nakupa saa tatu ulipe fedha iliyobakia, ukishidwa, nitajua la kufanya”) Alisikika kijana huyo aliyeongea na Jacqueline kabla ya kukata simu akiwa na jazba. David pia alikuwa amesikia kila jambo. Wote walivuta pumzi wakiwa wameujua ukweli mwingine pia, baada ya James kuelezwa jambo lililokuwa limetokea walitambua zoezi lililopaswa kuchukua nafasi wakati huo. David aliutupa mkoba wa mwanamke huyo chini na walitoka wakikimbia wakielekea kwenye gari la James walilofika nalo awali, walikuwa wamebeka simu pekee ya Aminata. Mara baada ya kuingia kwenye gari hilo aina ya Ferrari, James aliliondoa kwa kasi na safari ilianza wakielekea katika kituo cha polisi kikuu cha kitongoji hicho cha Des Moines. Baada ya dakika ishirini gari hilo la James liliegeshwa katika kituo hicho, David na wenzie walishuka haraka na kuongoza ndani ya kituo hicho. Walitumia muda wa nusu saa kuwaeleza askari juu ya kila jambo lililokuwa limetokea juu ya kifo cha mke mkubwa wa bwana Abraham na jinsi walivyoweza kumpata mtu waliyeamini alikuwa ni muuaji wa mwanamke huyo.

    Askari wa kitongoji hicho waliwasiliana na wenzao pia wa kituo cha polisi cha Urbandale ambao waliwasisitizia kuwa kila jambo waliloelezwa lilikuwa sahihi. Askari aliyekuwa akifanya upelelezi wa kesi ya mauaji hayo aliyekuwa katika kituo hicho cha Urbandale aliwaahidi kujumuika nao baada ya saa kadhaa. Kwa wakati huo walikuwa na uhakika na kila jambo kuwa mtu aliyepiga simu iliyopokelewa na Jacqueline ambaye walimtambua kama bwana Leo ndiye alihusika na mauaji ya mke mkubwa wa bwana Abraham. Jambo lililofuata, walihitaji kujua eneo ambalo bwana Leo alikuwepo. Halikuwa zoezi zito kwa vile teknolojia yao ilikuwa imekuwa, askari waliohusika na masuala ya taarifa za kiteknolojia waliingia katika mtandao maalum wa kiupelelezi na walitafuta eneo ambalo bwana Leo alipiga simu yake kwa mara ya mwisho, simu iliyopokelewa na Jacqueline. Baada ya dakika tano waligundua simu hiyo ilipigwa kutoka katika klabu ya Cowboys Night Club. Ili kuhakikisha kama bwana Leo bado alikuwepo katika klabu hiyo, walimwambia Jacqueline amweleze kwa ujumbe mfupi wa maneno wa simu kuwa alikuwa akienda katika eneo la klabu hiyo ya bwana Leo kumalizia malipo yake.

    Jacqueline hakuchelewa, alielekea katika eneo la ujumbe mfupi wa maneno na kuandika, “I’m coming” (“nakuja”). Kisha aliutuma ujumbe huo kwa bwana Leo, baada ya sekunde nne kompyuta za askari hao zilizofuatilia ujumbe huo, zilionyesha kuwa ujumbe huo ulikuwa umepokelewa katika jengo la Cowboys Night Club. Dakika moja baadaye bwana Leo alijibu ujumbe huo mfupi wa simu na ulisomeka “I’m waiting” (“nakusubiria”). Kila kitu kilikuwa kwenye mstari mpaka wakati huo. Mkuu wa kituo hicho kikuu cha kitongoji cha Des Moines alitoa magari sita na askari thelathini, askari wa watano wakiwa na gari moja walipaswa waondoke na gari hilo muda huo ili kwenda kumkamata Aminata ambaye tayari kwa asilimia tisini alikuwa akihusishwa na mauaji ya mke mkubwa wa bwana Abraham. Askari hao waliondoka wakielekea mji mdogo wa Saylor ambao Aminata alikuwa akiishi. James, David na Jacqueline walibakia kituoni hapo wakiwa na furaha.

    Askari wengine pia wakiwa na silaha nzito waliondoka wakielekea nje kidogo ya kitongoji hicho kulikokuwa na klabu ya bwana Leo ya Cowboys Night Club. Ulikuwa ni mwendo wa dakika ishirini au thelathini kwa kutumia gari. Kwa jinsi walivyokuwa wakikimbiza magari yao iliwachukua dakika kumi na tano kufika katika eneo la klabu ya bwana Leo, magari yao yakikimbizwa yaliegeshwa haraka huku yakiacha vumbi eneo hilo. Wakati magari mengine yakiwa hayajaegeshwa vizuri, askari wote walionekana wakiwa wamesharuka huku wakielekea kwa kasi ndani ya klabu hiyo. Askari wote ishirini na tano waliingia katika klabu hiyo, mhudumu aliyekuwapo kaunta aliwaongoza mpaka eneo alilokuwapo bwana Leo ambaye hakuwa na ujanja. Mageti yote ya eneo hilo yalivunjwa na risasi za askari hao walioonekana kuwa na uchu na wahalifu. Walimkamata kirahisi bwana Leo na vijana wake wawili ambao walikuwa wakiendelea kutumia dawa za kulevya.

    Ingawawalikuwa na silaha pia lakini bwana Leo na vijana wake walitulia baada ya kugundua kuwa askari hao walikuwa wengi sana, waliwaona kupitia kamera zilizotegwa kila sehemu katika jengo hilo. Baada ya dakika tano zoezi la kukamatwa kwa bwana Leo na vijana wake lilikamilika kirahisi na wakati huo wahalifu hao waliokuwa hawajaelezwa kitu walianza kupelekwa katika kituo cha polisi cha Des Moines. Askari walikuwa wamebeba vithibitisho vya dawa za kulevya walizoziona wakitumia wahalifu hao pamoja na baadhi ya silaha walizokuwa nazo. Bwana Leo alionekana kuchanganyikiwa ghafla, alikuwa akijihusisha na shughuli zake haramu kwa miaka kadhaa lakini hakuwahi kukamatwa kirahisi kama ilivyokuwa imetokea wakati huo, alihisi kuna mtu alikuwa amemchongea kwa askari hao. Hisia zake zilianza kuwa juu ya Aminata ambaye alikuwa amewasiliana naye mara ya mwisho kabla ya kukamatwa kwao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya nusu saa, walikuwa katika kituo cha polisi cha Des Moines, mbali na vijana wawili ambao makosa yao ya haraka yalikuwa ni utumiaji wa dawa za kulevya na kumiliki silaha kinyume cha sheria, bwana Leo alikuwa akituhumiwa kwa kosa la kumuua mke mkubwa wa bwana Abraham, kosa ambalo alilikana. Kijana huyo mzungu alikuwa ameshachanganyikiwa na alielewa kila jambo lilikuwa limesababishwa na Aminata. Alikuwa akiamini mwanamke huyo alitumwa ili kumwingiza katika mtego huo. Baada ya saa moja Aminata alifikishwa kituoni hapo huku akilia kwa uchungu, tayari alikuwa ameshachanganyikiwa zaidi juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea. Mwanamke huyo alijumuishwa na bwana Leo, hofu aliyokuwa nayo ilimfanya akubali kushiriki katika mauaji dhidi ya mke mkubwa wa bwana Abraham. Alikuwa kama mwehu kwa wakati huo huku akiamini mwisho wake na mumewe pia ulikuwa umeshafika.

    Akiwa kituoni hapo alimwonyesha kijana mmoja kati ya wawili waliokamatwa wakiwa na bwana Leo kuwa ndiye aliyemuua mke mkubwa wa bwana Abraham. Bwana Leo bado aliendelea kukana kuhusika na mauaji hayo hata Aminata alionekana akiogopa kumtaja kijana huyo. Kwa haraka kosa la bwana Leo na kijana wake mwingine likawa ni utumiaji wa dawa za kulevya na kumiliki silaha kinyume cha sheria lakini bado askari waliendelea kuwahoji huku wakiamini kuwa bwana Leo ndiye aliyepanga mpango mzima wa mauaji yaliyokuwa yametokea. Baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa, askari walilidhika na kesi yao ilitarajiwa kufunguliwa siku iliyofuata. Wakati huo Jacqueline, James na David walikuwa wameondoka na kuelekea katika hoteli ya Des Moines Motel, walikuwa na furaha wakiamini kila jambo lilikuwa limeshafika mwisho wakati huo.



    * * *

    Siku iliyofuata kesi ya Aminata, bwana Leo pamoja na vijana wake wawili ilifunguliwa katika mahakama kuu ya jitongoji hicho cha Des Moines. Wakati jalada hilo likifunguliwa wakili wa bwana Abraham alikuwapo mahakamani na aliweza kusikia kila jambo lililokuwa likiendelea. Aligundua mwisho mbaya wa kesi ya bwana Abraham na hakuona haja ya kuendelea kupoteza muda wake kumtetea mhalifu huyo. Kwa wakati huo hakuweza kuongea tena na Aminata kwa vile alikuwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa kituo cha polisi cha kitongoji hicho. Aliamua kokodi gari mchana wa siku hiyo na kuelekea katika kituo cha polisi cha Altoona. Lengo lilikuwa ni kwenda kumweleza bwana Abraham kuwa hakuweza kuendelea na zoezi la kumtetea katika kesi yake.

    Baada ya nusu saa wakili huyo alikuwa akitembea taratibu akielekea katika chumba cha wageni wa kituo hicho cha polisi cha Altoona, huko aliomba kuongea na bwana Abraham aliyetolewa tayari kwa kuongea na wakili huyo baada ya dakika kadhaa. Wakati huo bwana Abraham alikuwa amedhoofu kiafya na kwa haraka mtu angeweza kuhisi alikuwa kituoni hapo kwa miezi kadhaa. Bwana Abraham hakuonyesha ushirikiano wa kuongea na wakili huyo huku akiwa kimya alionekana kama mtu aliyekata tamaa. Wakili alimweleza juu ya kusudio lake la kuachana na kesi hiyo, bwana Abraham alikuwa ametulia huku machozi yakimtoka, alionekana kama alikuwa akijutia jambo. Alibakia kuwa kimya kabla ya kushtuka baada ya kuambiwa na wakili huyo kuwa mke wake, Aminata alikuwa chini ya ulinzi kwa kosa la mauaji ya mke wake mkubwa.

    Wakati huo bwana Abraham aliiacha simu yake na kuondoka eneo hilo walilokuwa wakiongea, alipoteza tumaini kabisa baada ya kujitambua kuwa kesi nyingine ya mauaji dhidi ya mke wake mkubwa ingemwangukia kwa vile walifanya hivyo wakati wakijaribu kupoteza ushahidi wa kesi yake.

    Akiongozwa na askari aliyekuwa na bunduki mkononi, bwana Abraham alitembea taratibu akielekea katika chumba chake. Baada ya dakika moja alifika katika chumba hicho na aliingia, aliongoza mpaka katika kitanda chake na kujilaza. Alikuwa akitokwa na machozi, kumbukumbu za mambo mengi zilianza kumjia. Alianza kukumbuka watu rukuki aliowaua katika maisha yake. Kwa muda wa saa tatu mfululizo hakumaliza maovu mengi aliyokuwa ameyapitia katika maisha yake. Alimkumbuka hata mwanaye Sabinus aliyeuawa kwa amri yake kimakosa. Siku hiyo moyoni mwake alijihisi mkosaji na alistahili kuhukumiwa.

    Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu sana katika maisha yake yote, aliota ndoto nyingi tofauti za watu wote aliokuwa amewaua waliozidi kumi na tano. Watu hao walimjia wakiwa na mavazi meupe ndotoni huku wakimuuliza kwa nini aliwaua. Roho ya mauti ilimwingia bwana Abraham, na yeye alikuwa tayari kwa kufa. Hakuona raha ya kuwa katika chumba hicho cha polisi huku wafu wakimuulizakila dakika iliyoenda, kwa nini aliwaua? Usiku wa siku hiyo aliwasumbua askari wa kituo hicho waliofika kumwangalia katika chumba alicholala kila baada ya saa kwa vile alikuwa akipiga kelele kila wakati akidai aliwaona watu waliovaa nguo nyeupe kwenye chumba chake. Hakulala kabisa siku hiyo kwani kila aliposinzia ndipo ndoto hizo mbaya aliziota.

    Siku iliyofuata alikuwa mwingi wa mawazo na hakutaka kula kabisa, alikuwa akiziwazia picha tofauti za marehemu waliomjia ndotoni akiwapo mwanaye Sabinus. “Dad why you killed me” (“baba kwa nini uliniua?”) Ilikuwa sentensi ya mwanaye huyo aliyoikumbuka kila wakati kutoka ndotoni, bwana Abraham alikuwa amekata tamaa na alijutia kila baya alilokuwa amelifanya maishani mwake. Alitamani siku ya kesi ifike na ikiwezekana ahukumiwe kunyongwa kwa vile alikuwa amechoka kuishi na alihisi alistahili adhabu hiyo. Usiku wa siku hiyo ya Jumatano kuamkia Alhamisi mambo yaliendelea kama usiku uliopita. Watu aliowaua waliendelea kumsumbua ndotoni na wakati huu walikuwa wakimlalamikia kwa mambo mengi maovu aliyoyafanya. Bwana Abraham hakupata hata repe la usingizi, kwani alihangaika usiku kucha, wakati huo hali ilibadilika hata akiwa macho kuna wakati alihisi wafu hao walikuwa wamekaa pembeni yake. Muda wote alikuwa akipiga kelele akiwataja majina na kuwaomba msamaha. Kuna wakati askari walikaa nje ya chumba chake kilichokuwa na geti lililotengenezwa kwa nondo ambalo lilihurusu wao kuona ndani. Walishangaa kumwona mwanaume huyo akiwa amepiga magoti akiomba msamaha kwa watu ambao hata wao hawakuwaona. Walianza kuamini kuwa bwana Abraham alikuwa akinyemelewa na ulemavu wa akili.

    Siku iliyofuata ya Alhamisi aliamka akiwa amechoka sana, siyo tu kwa kupiga kelele za kuomba msamaha usiku mzima lakini pia alikuwa amechoka kuendelea kuishi. Hakuona sababu ya kwenda mahakamani siku hiyo na kusomewa adhabu ya kifo ambayo ingeweza kuchukua nafasi hata baada ya miezi mitatu. Mateso aliyokuwa akiyapata wakati wa usiku yalimchoshana alitamani kuyakwepa haraka sana. Roho ya mauti ilikuwa imemkaa kichwani na moyoni mwake pia. Alikuwa akiwaza kufa tu kwa wakati huo dunia ilikuwa imemchosha sana. Majira hayo ya saa moja asubuhi alikuwa akiwaangalia askari waliokuwa wakipita mara kadhaa nje ya chumba chake huku wakiwa wamebeba bunduki, alitamani kama watambue kuwa alitaka kupigwa na risasi mpaka kufa. Uovu wake ulikuwa umempeleka mbali na alimini hangeweza kusamehewa mbele ya mwenyezi Mungu kwa mauaji yote aliyokuwa ameyafanya, aliwaza kufa tu!

    Majira ya saa mbili asubuhi, askari mmoja mzungu alionekana akifungua geti la chumba cha bwana Abraham akiwa tayari kwa kuanza safari ya kumpeleka katika mahakama kuu ya kitongoji hicho cha Des Moines ambako kesi ya bwana Abraham ilipaswa kusikilizwa kwa mara ya nyingine. Askari huyo alikuwa amebeba bunduki yake begani na wakati akiendelea kufungua geti hilo bwana Abraham alionekana akiiangalia kwa umakini silaha hiyo, aliwaza kufanya jambo, aliamini jibu la swali lake lilikuwa limepatikana. Mara baada ya mlango huo kufunguliwa askari huyo alimwonyeshea silaha yake na kumuamuru atoke. Bwana Abraham alitembea taratibu kabla ya kutoka. Askari huyo alimweleza atembee kuelekea nje tayari kwa kuondoka kituoni hapo, bwana Abraham alitembea kidogo kabla ya kusikika. “Hey, please I need to go to the toilet” ( “hey, tafadhari nahitaji kwenda chooni”) Alisikika bwana Abraham baada ya kutembea kwa hatua tatu.

    Askari huyo alimwangalia kwa sekunde kadhaa kabla ya kumkubalia kwa kutikisa kichwa, bwana Abraham aligeuka na kuanza kutembea akielekea eneo la chooni katika kituo cha polisi hicho, nyuma yake alifuatwa na askari huyo ambaye alikuwa bado amemwelekezea bunduki yake bwana Abraham. Walipita mbele ya vyumba vingine ambavyo kulikuwa na watuhumiwa wengine ambao wengi wao walikuwa bado wamelala, wakati wakitembea bwana Abraham aligeuka mara kadhaa akimchunguza askari huyo. Alikuwa akimwangalia jinsi alivyokuwa ameishika bunduki yake hiyo aina ya AK 47. Baada ya dakika moja walikuwa wakiingia katika vyoo vya watuhumiwa wa kituo hicho, ndani ya chumba hicho kikubwa cha mariwato kulikuwa na bafu kadhaa pia mbali na vyoo vilivyokuwapo. Bwana Abraham alitembea taratibu wakati ambao askari aliyekuwa ameongozana naye akiwa nyuma yake, karibu kidogo. Hatimaye wote waliingia katika chumba hicho ni wakati ambao bwana Abraham alivuta pumzi ndefu, alikuwa tayari kwa kufanya jambo. Alimwona vizuri askari nyuma yake akiwa ameshika bunduki yake kizembe.

    Kwa kasi ya ajabu bwana Abraham aligeuka na kuivuta kwa nguvu bunduki ya askari huyo, ambayo alimnyang’anya sawasawa, askari huyo akiwa na jabza alimsogelea kwa kasi bwana Abraham akiwa na lengo la kumpiga ngumi kwa vile tundu la bunduki lilikuwa nyuma ya bwana Abraham na aliamini hangeweza kupigwa risasi. Bwana Abraham aliyepata nguvu za ghafla aliikwepa ngumi ya askari huyo ambaye aliyumba baada ya kumkosa. Ni wakati ambao bwana Abraham hakuchelewa kwani alimpiga kwa nguvu kichwani askari huyo na kitako cha bunduki hiyo, na kipigo hicho kilimpeleka mpaka chini askari huyo ambaye alipigwa tena na bwana Abraham akiwa chini na mwishoe alizimia.

    Bwana Abraham alipumua kidogo wakati damu ikianza kumtoka askari huyo aliyekuwa chini, aliikoki bunduki yake tayari kwa kujiua, alishusha chini bunduki hiyo huku akiwa ameelekeza tundu lake chini ya kidevu chake, alionekana akitabasamu kwa sekunde kadhaa huku akiwa anaiangalia kamera mojawapo iliyokuwa chooni hapo, tayari alitambua kwamba askari wengi walikuwa wakielekea eneo hilo baada ya kumwona alichokuwa akifanya. Hilo ndilo lilifuata akiwa bado anatabasamu alisikia makanyagio ya askari wakikimbia kuelekea eneo hilo, alivuta pumzi kabla kufyatua risasi. Mlio wa sauti kubwa ndiyo uliosikika kwa wakati huo. Risasi hiyo ilipenya chini ya kidevu chake kabla ya kutoa tundu utosini kwake, safari ya bwana Abraham ilikuwa imefika mwisho.

    Aliiachia bunduki yake aliyokuwa ameishika na taratibu alionekana akianguka chini, alianguka akiwa amepiga magoti kabla ya kuanguka sakafuni kabisa akiwa amelalia tumbo. Damu ilikuwa ikimtoka kwa kasi ikisambaa eneo hilo na tayari askari wa kituo hicho walikuwa wameingia chooni hapo. Wachache wao walimwangalia mwenzao aliyekuwa amezimia na walimwondoa haraka eneo hilo kumwahisha hopsitali. Askari wengine walibaki wamesimama wakimwangalia bwana Abraham ambaye roho ya mauti ilikuwa imefanikiwa kuchukua uhai wake.

    * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mhalifu Joseph Kanyenzi maarufu kama Killa Jose, akiwa mfungwa wa gereza la Ndolwa nchini Uganda, alikuwa amewasili nchini Marekani akiwa chini ya ulinzi mkali wa mwanajeshi Moses Mgallah. Mara baada ya kufikia katika jimbo la Washington DC siku ya Jumanne, mhalifu huyo na mwanajeshi aliyemuongoza walilala katika jimbo hilo, huku ulinzi ukiwa umeongezeka kwa vile James alilipia gharama za kumlinda bwana Joseph Kanyenzi katika kampuni maarufu ya ulinzi iliyofahamika kwa jina la American Ultimate Security (AUS) kampuni iliyoshirikiana na Mosses kumlinda Killa Jose. Ulinzi huo ulitokana na agizo la mkuu wa gereza la Ndolwa ambaye alihitaji mfugwa huyo arudi kumaliza kifungo chake. Mbali na suala hilo la kimsingi, David na James hawakuwa tayari kumpoteza shahidi huyo kwa mara ya pili.

    Siku iliyofuata Killa Jose akiwa chini ya ulinzi huo mkali alianza safari kuelekea katika jimbo la Iowa, kwake alijisikia faraja kwani katika maisha yake hakufikiria hata siku moja kama angeweza kuitembelea nchi hiyo ya Marekani. Alijisikia faraja sana, baada ya saa mbili ndege hiyo ya shirika la Daily Washington Flight ilikuwa ikiburuza matairi yake katika uwanja wa ndege wa Des Moines International Airport. Uwanjani hapo walikuwepo askari wengine wa kampuni hiyo ya ulinzi ya American Ultimate Security (AUS) walioandaa magari yao mawili tayari kwa kumpokea Killa Jose. Uwanjani hapo pia alikuwepo James, Jacqueline na David ambao walikuwa na furaha muda wote wakiamini wangeshinda kesi yao siku iliyofuata. Mara baada ya Killa Jose kutoka katika eneo la mapokezi akiwa chini ya ulinzi wa Mosses na askari kadhaa, aliongoza katika eneo walilokuwa wakina David na kusalimiana nao, walionekana wakimshangaa kidogo. Akiwa amefungwa pingu, alikuwa mtu wa makamo aliyeenda hewani huku akiwa na kifua kipana, kwa haraka mtu angeweza kujua kwamba alikuwa mtu hatari sana kwa vile alionekana akiwa na makovu mengi, kwa jinsi alivyoongea, sauti yake ilionyesha kama alikuwa na huruma kidogo.



    Killa Jose aliongozwa mpaka kwenye gari husika na safari ilianza wakielekea katika hoteli ya Des Moines Motel ambako mfungwa huyo alikuwa ametafutiwa hifadhi, alionekana akiwa na furaha. Baada ya nusu saa walikuwa katika hoteli hiyo, walitumia muda mrefu siku hiyo kuongea na Killa Jose aliyeyafahamu mambo mengi ya bwana Abraham. Waliyajua mengi pia ambayo walikuwa hawayafahamu. Mpaka usiku wa siku hiyo walikuwa na uhakika wa kushinda kesi yao kwa msaada wa Killa Jose. Siku iliyofuata ya Alhamisi kama ilivyotarajiwa walindoka katika hoteli hiyo majira ya saa mbili asubuhi huku wakiwa na ulinzi mkali kama kawaida, iliwachukua muda wa nusu saa kufika katika mahakama kuu ya kitongoji hicho cha Des Moines. Walikuwa wamefika mahakamani hapo saa moja na nusu kabla.

    Hatimaye ilipotimia saa nne kamili asubuhi walikuwa wameshajongea katika chumba husika tayari kwa kusikiliza kesi ya bwana Abraham. Watu hawakuwa wengi siku hiyo na hali ilibadilika kwani siku zote kila ilipofika wakati huo mshtakiwa, bwana Abraham alikuwa akifikishwa kizimbani lakini siku ya leo hakufikishwa, walibaki wametulia wakiwa hawajui jambo lililokuwa linaendelea. Hatimaye hakimu aliingia katika chumba hicho kwa kuchelewa pia. Alibaki ametulia kwa sekunde kadhaa kabla ya kutangaza kifo cha bwana Abraham, alieleza kuwa tajiri huyo alijiua asubuhi ya siku hiyo baada ya kumnyang’anya bunduki askari aliyekuwa akimtoa katika chumba chake ili afikishwe mahakamani hapo kuhudhuria kesi hiyo. Jaji alieleza imani yake ya kuamini kwamba bwana Abraham alikuwa na hatia lakini alihitaji muda wa dakika kadhaa wa kuongea na shahidi toka Uganda na alieleza kuwa angetoa maamuzi ya mwisho ya mahakama baada ya siku mbili.

    Watu wengi walishtuka kusikia kifo cha bwana Abraham mahakamani hapo lakini hali ilikuwa tofauti kwa James na David ambao hawakuonyesha hisia zozote lakini waliamini ushindi walishaupata. Killa Jose alipelekwa mpaka katika ofisi ya jaji huyo na huku alitoa maelezo yake ya dakika arobaini na tano kwa jaji huyo kabla ya kuhurusiwa. Aliondoka mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi kama kawaida na alirudishwa katika hoteli ya Des Moines Motel na huko taratibu za kurudishwa nchini Uganda zilitarajia kuanza siku iliyofuata.

    Hatimaye siku hiyo ilifika na Killa Jose aliondoka katika jimbo hilo la Iowa akielekea katika jimbo la Washington Dc tayari kwa safari ya kurudi nchini Uganda. Ni siku ambayo mhalifu huyo alitokwa na machozi, alipenda kuwapo katika nchi hiyo hata akiwa chini ya ulinzi huo mkali. James alimpa kiasi cha dola elfu thelathini zilizokuwa sawa na milioni thelathini na saba kijana Mosses Mgallah ambaye alikuwa mwanajeshi aliyefanikisha zoezi la kufikishwa kwa Killa Jose nchini humo. David alimpa Killa Jose namba yake ya simu na alimweleza kuwa ampigie kama angebadilika na kuwa mtu mwema mara baada ya kumaliza kifungo chake cha mwaka mmoja jela. David alimwahidi kumsaidia kama angekuwa raia mwema. Killa Jose alishukuru sana na muda wote akiwa kwenye ndege alikuwa akiiangalia namba hiyo, walipofika Washington DC alikuwa ameshaikalili, safari yao ya kurudi Uganda iliendelea siku hiyo hiyo kwani waliondoka nchini Marekani kwa ndege ya shirika la British Airways.

    Siku hiyo ndiyo ambayo bwana Abraham alizikwa pia huku mazishi yake yakiongozwa na David. Bwana Abraham alizikwa katika makaburi ya mji wa Urbandale. Kaburi lake lilikuwa mbele ya lile la mkewe mkubwa ambaye aliuawa akiwa katika hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital. Mazishi ya bwana Abraham yalihuzuliwa na Gray Abraham ambaye alikuwa na wiki kadhaa tu akiwa mfugwa wa gereza la Spring Hill, alionekana kubadilika kwa kiasi kikubwa na aliyalaani makosa yake na zaidi ya baba yake ambayo awali hakuwahi kuyafahamu. Mama yake Gray, Aminata naye alikuwepo eneo hilo la mazishi na wote walikuwa chini ya ulinzi mkali. Anita akiwa mtoto mdogo wa bwana Abraham na Aminata, alionekana akiwa na uso mkavu na hakulia hata kidogo, alikuwa amebebwa na Jacqueline huku akiwa amemng’ang’ania kifuani kama mama yake, hakutaka kumsikia mama yake aliyekuwa akilia na kujutia makosa yao. David aliwaonea huruma lakini hakuwa na jinsi, alikuwa amevaa suti nyeusi huku akiwa mtulivu muda wote, akishirikiana na rafiki yake James, walihakikisha shughuli hiyo inamalizika kama ilivyopagwa.

    Baada ya mazishi hayo, wakati Gray Abraham na mama yake Aminata wakitakiwa kuondoka eneo hilo na askari, walijikuta kwa pamoja wakimkimbilia David kabla ya kwenda kumpigia magoti wakimwomba msamaha. David aliwanyanyua na kuwaeleza kuwa amewasamehe, hakuwa na kinyongo nao. Gray aliondoka makabuRini hapo na gari la gereza la Spring Hill akiwa na amani kidogo, hakuamini kama alikuwa amesamehewa kwani hata makosa ya baba yake aliona yanamhusu, alijiuliza juu ya upendo wa David ambao ulikuwa wa tofauti kwa vile aliamini haikuwa rahisi kwa mtu mwingine kuongoza shughuli ya mazishi ya bwana Abraham huku akiwa adui wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aminata naye aliondoka makaburini hapo akiwa na amani kidogo ingawaje alitambua hukumu ambayo ingempata kuwa haingekuwa nyepesi. Siku iliyofuata mahakama kuu ya kitongoji cha Des Moines ilitangaza kuwa mali zote za bwana Abraham nchini humo na nchini Uganda zilikuwa mali halali za kijana David Johnson. Huku mali hizo zikielezwa kwamba awali zilikuwa mali halali za marehemu Johnson aliyefariki katika ajali ya moto akiwa na familia yake baada ya kuuawa na bwana Abraham. Bwana Johnson ndiye aliyekuwa baba yake David ambaye kwa sasa alikuwa mrithi halali wa mali hizo. Furaha ya David na James pamoja na Jacqueline ilikamilika. Kwani kila kitu cha bwana Abraham kilikabidhiwa kwa David.

    David akishauriwa na James pamoja na mshauri wake mkuu aliyemwajiri aliamua kuuza kila mali ya bwana Abraham iliyokuwapo nchini humo. Aliiacha nyumba iliyokuwapo nchini Uganda pamoja na kiwanda cha nguo ambacho alikibadilisha jina na kukiita Johnson & Son Textile Industry, lilikuwa ni jina lile lile la kiwanda hicho lililo tumika awali, wakati huo aliongezea “son” akimaananisha Johnson na mwanaye. David aliamua kuuza kila mali ya bwana Abraham akifuta kumbukumbu ya uovu katika miaka ishirini iliyokuwa imepita wakati bwana Abraham akimiliki mali za baba yake. Wakati huo alianzisha kampuni kubwa ya usafirishaji nchini Marekani iliyoitwa Johnson & Son Transportation Company iliyohusika na usafirishaji wa majini na nchi kavu. Aliamua kuwekeza katika biashara hiyo zaidi kwani alinunua magari ya mizigo zaidi ya mia nne na meli nne zilizokuwa zikisafirisha mizigo majini kwenda nchi tofauti. Magari yake ya mizigo yalikuwa yakifanya kazi sehemu tofauti nchini humo. Mkewe Jacqueline alikuwa amemwanzishia kampuni ndogo iliyo jishughulisha na nguo za watoto nchini humo na maisha yaliendelea vizuri.

    Wakati huo Aminata alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukubali kuhusika na kifo cha mke mkubwa wa bwana Abraham. Kijana wa bwana Leo aliyemuua mwanamke huyo alifahamika mahakamani kwa jina la Terrence naye alihukumiwa kifungo cha maisha. Bwana Leo na kijana wake mwingine walihukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano kwa kujihusisha na uhalifu tofauti katika jimbo hilo la Iowa.

    Ilikuwa ni ratiba ya kila juma ya David ambaye aliwatembelea Gray na Aminata katika magereza yao kila siku ya Ijumaa. Aminata alikuwa amefungwa katika gereza kuu la Des Moines, mama huyo na mwanaye walifarijika sana kutembelewa na David mbali na uovu wa hali ya juu waliokuwa wamemtendea.

    * * *

    Baada ya mwaka mmoja mafanikio ya David yaliendelea kuonekana zaidi kwa vile alikuwa akishauriwa na James pamoja na washauri wake kadhaa wa kiuchumi. Tayari alikuwa na meli zaidi ya kumi na tano na magari rukuki ya mizigo nchini humo, hakuwa na hofu ya maisha hata kidogo. Ni wakati ambao David alipigiwa simu siku moja na bwana Joseph Kanyenzi maarufu kama Killa Jose ambaye alimhakikishia kuwa alishaachana na uhalifu. David hakuwa na tatizo kwani alimsaidia Killa Jose, alimtumia fedha kiasi cha dola elfu hamsini zilizokuwa zaidi ya milioni sabini na tano za kitanzania ambazo alimshauri aanzishe biashara. Ilikuwa furaha kwake alipopigiwa simu na bwana Joseph Kanyenzi tena akielezwa kuwa biashara yake iliendelea vizuri nchini Uganda.

    Jacqueline alitarajiwa kuleta neema katika familia ya David kwani alikuwa na ujauzito, na huyo alitarajiwa kuwa mtoto wao wa pili baada ya Anita, mtoto wa bwana Abraham aliyewatambua kama wazazi wake. Aliwaita kama baba na mama wakati wote na walimzoea kama mwanao. Miezi mitatu baadaye Jacqueline alijifungua mtoto wa kike waliyemwita jina la Suzzane, jina lililokuwa la mama yake mzazi David aliyekuwa marehemu. Wakati huo Gray Abraham alitoka jela pia na kuungana na familia ya David huku akiwa na hana matatizo nao, alikuwa amejifunza mengi na alijutia makosa yake.

    Tofauti na imani ya Gray ya kuanza kuhangaika kutafuta maisha, alishtuka baada ya kugundua David alikuwa amemjengea nyumba katika jimbo la Michigan ambalo hata yeye alikuwa akiishi, nyumba hiyo ilikuwa imeshajengwa miezi kadhaa iliyopita. Zaidi ya jambo hilo alikuwa amemwanzishia duka kubwa la vifaa vya umeme katika jiji hilo lililotumia jina la Gray Abraham na jambo alilopaswa kufanya lilikuwa ni kuendeleza mali hizo alizopewa na binamu yake. Gray alifurahi sana na alijifunza kuwa na upendo kama huo wa David ambao hakuutegemea.

    Jacqueline na David hatimaye walifunga harusi katika jimbo la Michigan miezi kadhaa baadaye, harusi iliyohudhuliwa na James aliyeongozana na mke wake wakati huo, Zena. Mrembo wa siku nyingi, wakati huo akiwa mama, Natalie Brown pamoja na mumewe walihudhuria pia. Wazazi wa Jacqueline walikuwapo pia huku wakiwa wameambatana na ndugu zao kadhaa kutoka Tanzania. Akiwa amevaa suti nadhifu, Joseph Kanyenzi alikuwa mmoja wa watu waliohudhulia kutoka Uganda, hakutaka kuitwa Killa Jose tena, alikuwa na furaha kushiriki katika harusi ya mtu aliyebadili maisha yake.

    Gray naye hakuwa nyuma akiwa na mchumba wake alihudhulia harusi hiyo iliyofana. David alifurahia kila jambo kwa vile siku zote alihitaji kufunga harusi wakati akiwa katika kilele cha mafanikio. Hakuwaza mafanikio yake pekee kwani alijali mafanikio ya ndugu zake na watu aliowapenda pia na aliamini alifanikisha jambo hilo kwa aslimia tisini. Jioni ya siku hiyo wageni wengi walionekana wakiendelea kusherekea katika ukumbi wa hoteli iliyofahamika kwa jina la Fantastic Moments Hotel. Muziki wa taratibu ulikuwa ukipigwa lakini ghafla muziki huo ulizimwa na taa zilielekezwa eneo la jukwaa ambalo David na Jacqueline walikuwa wamesimama huku wakiwa wamevaa mavazi ya kupendeza, David alikuwa ameshika kipaza sauti na pembeni yake mkewe alikuwa amesimama akiwa amemkumbatia kiubavu. Mbele yao kulikuwa na meza ndogo yenye vinywaji laini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yeah! Of course, I’m pretty sure about all of us, we are having a good time of our life; we have to believe always that everything we have is for God’s sake, so we better share what we have with those who haven’t, we better love each other and recall this word of God, LOVE, cheers guys”

    (“ndiyo, nina uhakika wote hapa tunafurahia wakati mwingine wa maisha yetu, inatupasa tuamini wakati wote kwamba kila kitu tulicho nacho ni kwa rehema za mwenyezi Mungu, kwa hiyo inatupasa tugawane tulivyonavyo na wasionavyo, inatupasa tupendane na kulikumbuka neno hili la mwenyezi Mungu, UPENDO”) Alimaliza kuongea David ambaye alipokea glasi yenye kinywaji laini toka kwa mkewe ambaye aligongesha naye glasi hiyo kabla kunywa kinywaji hicho. Jambo hilo liliendelea pia ukumbi mzima kwa waalikwa wote waliofika katika harusi hiyo iliyofana. David na Jacqueline tayari walikuwa mke na mume na maisha mazuri yalitarajia kuendelea baina yao.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog