Search This Blog

Sunday, 19 June 2022

MIMI KABLA YAKO - 4

 





    Simulizi : Mimi Kabla Yako

    Sehemu Ya Nne (4)



    Muuguzi huyo aliamua kumshika bega David ambaye alishtuka kabla ya kusikika “Amekufa!... amekufa…” Alipomwangalia muuguzi na kumgundua alisikika akiongea kwa mara nyingine tena. “Niambie dada yangu kama ameshakufa, niambie, mbona sijamwona?”

    “Hajafariki kaka, Jacqueline ni mzima na alizinduka muda mfupi toka uondoke” alijibu muuguzi huyo.

    David alipata ahueni moyoni mwake na aliamua kukaa vizuri katika kitanda alichokuwapo ili asikie eneo ambalo Jacqueline alikuwa ameelekea “Ni mzima ila ameondoka na baba yake majira ya saa kumi usiku…” Aliongea muuguzi huyo kauli iliyoonekana kumchanganya David tena ghafla. Maswali mfululizo yalifuata akitaka kujua eneo ambalo Jacqueline alikuwa ameelekea kabla ya kugundua kuwa alikuwa ameelekea jijini Dar es salaam. Alielezwa kuwa msichana huyo alizimia wakati akimsubiria baba yake ambaye walikuwa wote safarini kuelekea jijini Dar es salaam. Hivyo walikuwa wameendelea na safari hiyo wakitumia gari binafsi baada ya hali ya kiafya ya msichana huyo kuwa nzuri kidogo zaidi walikuwa na daktari waliyesafiri naye. Hatimaye muuguzi huyo alimaliza maelezo yote juu ya Jacqueline kabla ya kumpa David karatasi iliyoviringishwa na fedha ambayo msichana huyo aliomba David apewe.

    David aliifungua karatasi hiyo kwa haraka akiwa na shauku nayo, mara baada ya kuifungua aliziona noti za elfu kumi, ambazo zilikuwa kumi zikiwa zimeviringishwa. Alipoiangalia karatasi hiyo aligundua ilikuwa imeandikwa na aliamua kuanza kuisoma.

    ‘Nashukuru kwa msaada wako David, nilihitaji tuonane nikushukuru ila imeshindikana. Nina matatizo ya kuumwa kichwa kwa miaka mitatu sasa toka nipate ajali ya gari. Sina mengi zaidi ya kukutakia kazi njema. says Jacqueline’. Alimaliza kuusoma ujumbe huo David kabla ya kusikika akiuliza “Hajaacha namba ya simu?”. Muuguzi alitikisa kichwa akiashiria kuwa Jacqueline hakuacha namba ya simu. Alipoziangalia fedha zilizokuwa zimeviringishwa aligundua zilikuwa laki moja lakini haziku maananisha kitu kwake zaidi ya hulka yake ya kuhitaji kumwona Jacqueline. David aliagana na muuguzi huyo ambaye kabla walikuwa wakionana mara kadhaa na alimfahamu jina. Kichwa chake kilikuwa hakijatulia huku akionekana akimwaza Jacqueline muda wote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alielekea katika duka la Sabinus store lililokuwapo Njombe mjini karibu na soko kuu, eneo lililokuwa la kazi. Siku hiyo mbali ya kufanya kazi kama ilivyokuwa kawaida yake, alikuwa akimfikiria Jacqueline kupindukia. Kuna wakati alikuwa akiwaza kuondoka Njombe ili aelekee jijini Dar es salaam na lengo kubwa likiwa kwenda kumtafuta Jacqueline. Jambo lililokuwa gumu lilihusiana na mahali ambako angempata mrembo huyo. Aliamua kutulia huku akiendelea na kazi lakini kichwani alikuwa na mipango tofauti, kubwa likiwa la kuhakikisha anampata Jacqueline. Wakati huo kichwa chake kilitawaliwa na msichana huyo zaidi tofauti na awali ambapo alikuwa akiwaza jinsi ya kufanya malipizi ya kifo dhidi ya bwana Abraham. Kuna wakati pia alikuwa akimkumbuka James, rafiki yake wa miaka zaidi ya kumi na tatu iliyokuwa imepita. Alikuwa akikumbuka jinsi alivyoukosa msaada kutoka kwa Natalie Brown, mrembo wa jiji la Carifonia aliyeahidi kuwasaidia kabla ya yeye kukamatwa na polisi. Alikuwa akihisi kuwa James alikuwa nchini Marekani baada ya kupata msaada kutoka kwa Natalie Brown. Hakuwa na jambo la kufanya kwa wakati huo aliokuwa na mawazo sana.

    Baada ya siku mbili akiwa anaendelea na shughuli zake katika duka la Sabinus store, alimshuhudia muuguzi aliyemwachia jukumu la kumwangalia Jacqueline siku tatu zilizokuwa zimepita akifika katika duka lao. Wakati huo alikuwa akipima waya wa umeme kwa ajili ya mteja, aliacha shughuli hiyo na kumweleza kijana mwenzie aifanye. Alisogea upande mwingine akiwa na lengo la kumpokea muuguzi huyo aliyefika kama mteja. Hatimaye muuguzi huyo alifika kabla ya kusalimiana kwao, David alikuwa kimya huku akihisi kuwa huenda Jacqueline alikuwa amerudi tena hospitalini. “David, si ulikuwa unahitaji namba ya simu ya yule msichana” Alisikika yule muuguzi baada ya mazungumzo ya muda mfupi. “Ndiyo! Dada yangu….. unayo?” Alijibu David ambaye ghafla alionekana akiwa amemtolea macho. “Hapana, sina ila kuna karatasi hii niliiona katika kitanda chake ina namba ya simu ya mtu” Alimjibu muuguzi huyo huku akimkabidhi David karatasi hiyo ndogo.

    Bila kupoteza muda David aliipokea kabla ya kuiona karatasi hiyo ikiwa imeandikwa Mary John ikifuatiwa na namba ya simu iliyokuwa ya mtandao wa Vodacom. Tatizo aliloligundua katika namba hiyo ya simu, ilikuwa haina namba moja ya mwisho kati ya tarakimu sita za namba hiyo mbali na zile za mwanzoni. Hiyo yote ilitokana na kuchanika kwa karatasi hiyo huku ikiwa imetoka na namba ya mwisho.

    David alimshukuru sana muuguzi huyo kwa msaada wa kumpelekea namba hiyo huku akiwa tayari amepata wazo juu ya jambo la kufanya. Hatimaye muuguzi huyo aliondoka akimwacha David akifikiria. Tayari alikuwa ameingiwa na hisia akiamini jina la msichana aliyekuwa katika namba ya simu hiyo alikuwa mdogo wake Jacqueline au dada yake. Hiyo yote ilitokana na majina yao kufanana kwani hata jina la mzazi wa Jacqueline lilikuwa ni John. Baada ya kufikiria kwa muda mfupi alipata jibu, aliwaza kupiga namba hiyo ya simu akimalizia na namba tofauti za mwisho. Aliwaza kuanza na sifuri mpaka namba tisa katika kumalizia namba ambayo haikuwapo na aliamini lazima angempata Mary katika moja ya namba ambazo angezitumia.

    Jambo hilo ndilo alilolifanya, akianza na sifuri. Alifanya zoezi hilo kwa muda mfupi na alifikia namba saba pasipo mafanikio lakini namba nane na ile ya tisa zote zilionekana zilikuwa na watu waliozitumia lakini zilikuwa hazipatikani. Jambo hilo ndilo lililomfanya David azipige namba hizo kila baada ya muda mfupi lakini hazikupatikana.

    Siku iliyofuata wakati wa asubuhi namba iliyokuwa ikiishia na tisa ilifanikiwa kuita na kupokelewa, alijitambulisha kama daktari wa Jacqueline aliyehusika na matatizo ya kichwa. Mtu aliyeipokea alijitambulisha kwa jina la Mary, akiwa dada yake Jacqueline na aliahidi kumtumia namba ya Jacqueline baada ya muda mfupi.

    Hiyo yote ilifuata baada ya maelezo mafupi ya David aliyedai kuwa alitaka kumpa maelezo Jacqueline jinsi ya kujiepusha na maumivu ya kichwa yaliyokuwa yakimpata. Katika mazungumzo hayo pia David aliweza kugundua kuwa Jacqueline alikuwa mwanafuzi kwani alielezwa kuwa alikuwa shuleni wakati huo. Baada ya dakika tano simu ya David ilionyesha kulikuwa na ujumbe mfupi wa maneno uliokuwa umeingia, alipouangalia aligundua ilikuwa namba ya simu ya Jacqueline aliyokuwa ameiomba. Namba hiyo ilimfanya apige kelele akiwa na furaha baada ya kuipata kwani ilikuwa ndiyo dira juu ya kila jambo kwake.

    Siku hiyo jioni alimpigia simu msichana huyo na kujitambulisha kuwa yeye ndiye aliyemsaidia baada ya kuanguka akiwa amepoteza fahamu mjini Njombe. Jacqueline alifurahi kuwasiliana na David zaidi alimwomba msamaha huku akimweleza kuwa alisahau kumwandikia namba yake ya simu siku aliyoondoka Njombe. Huo ulikuwa mwanzo wa mawasiliano baina yao na tayari David alimtambua zaidi msichana huyo aliyekuwa anasoma katika shule ya kimataifa ya St. Mary ya jijini Dar es salaam akiwa kidato cha sita. Wakati huo wa mwezi wa kumi alikuwa amebakiwa na miezi minne ili amalize elimu yake ya sekondari.

    Katika mazungumzo yao waliyokuwa wakiyafanya, David alibaini mambo mengi kutoka kwa Jacqueline, mojawapo aligundua alikuwa mkarimu. Ilikuwa haipiti siku bila David kumpigia simu msichana huyo kwani kwa kufanya hivyo alikuwa akipata amani ya moyo na kujihisi alikuwa ametimiza ndoto za kuwa na mrembo huyo katika maisha yake. Jacqueline naye alikuwa hampatii picha David zaidi ya sauti yake aliyokuwa akiitumia kujenga taswira ya jinsi kijana huyo alivyo. Jambo hilo lilikuwa gumu na hakuweza kutambua David alikuwa kijana wa aina gani! Mbali na tabia yake ya kumjali ikiwa ni pamoja na kumpigia simu kila siku.

    Kadri mazungumzo yao kwa njia ya simu yalivyozidi kuendelea Jacqueline alianza kuhisi jambo likimwingia moyoni mwake. Alikuwa akifanya kosa ambalo alijiapiza kutolifanya katika maisha yake. Siku zote alikuwa hayupo tayari kumpenda mtu asiyemfahamu tena kupitia mazungumzo ya simu lakini wakati huu alihisi jambo hilo lingetokea. Kwa vile alishindwa kuvumilia juu ya jambo hilo alimwomba David atafute uwezekano ili waweze kukutana. Alihitaji kumfahamu kijana huyo ambaye upendo aliokuwa akijaribu kuupinga kila mara uliongezeka zaidi kutokana na vile alivyomsaidia akiwa mjini Njombe baada ya kupoteza fahamu.

    David akiwa na furaha aliamini mwanzo wa imani iliyokuwa moyoni mwake ulikuwa umeanza. Wakati huo alikuwa akiwaza kuondoka mjini Njombe ili aelekee jijini Dar es salaam na lengo kubwa lilikuwa pia kuanza mwanzo wa safari ya kulipiza kisasi dhidi ya baba yake mkubwa, bwana Abraham. Hakuwa tayari kuendelea kutaabika huku akiwa na mali nyingi alizoachiwa na marehemu baba yake. Aliamua kumweleza mmiliki wa duka la Sabinus store juu ya lengo lake hilo. Mmiliki huyo hakuwa na kinyongo juu ya ombi la kuacha kazi alilolitoa David. Baada ya wiki mbili alimkamilishia malipo yake ya miezi nane aliyokuwa akifanya kazi. Alipewa kiasi cha shilingi milioni moja kama malipo yake kutokana na makubaliano yaliyokuwapo awali. Siku ya Jumamosi ya tarehe mosi, mwezi Novemba alikuwa kwenye gari akisafiri kutoka Njombe, moyoni alikuwa akiamini angekutana na Jacqueline ndani ya siku kadhaa zilizofuata.

    Alifika jijini Dar es salaam majira ya saa kumi na mbili jioni kabla ya kuelekea kulala katika nyumba moja ya kulala wageni iliyokuwapo maeneo ya Manzese. Baada ya wiki moja David alikuwa tayari amepata chumba alichopanga maeneo ya Mbagala na fedha zote alizokuwa nazo alitumia kununua kitanda pamoja na vitu kadhaa. Wakati huo alikuwa amebakiwa na kiasi kidogo cha fedha alizopanga kuzitumia kwa siku kadhaa huku akifikiria shughuli ya kufanya. Jambo lililomkaa kichwani lilihusiana na msichana Jacqueline, hivyo aliamua kumpigia simu akiwa na lengo la kukutana naye. Msichana huyo hakupinga ombi hilo huku akionyesha shauku kubwa ya kukutana na David.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku ya Jumapili kama walivyokuwa wameahidiana, David alikuwa akimsubiria msichana huyo katika mgahawa mmoja uliokuwapo maeneo ya Ubungo. Akili yake ilikuwa imetawaliwa na sura ya msichana huyo ambaye alimwona kwa mara ya kwanza mjini Njombe.

    Majira ya saa sita mchana wakati akiendelea kunywa kinywaji chake laini alimshuhudia msichana mrembo akifika katika mgahawa huo. Mbali na moyo wake kulipuka kwa furaha lakini msichana huyo hakumchanganya kwani hakuwa mwingine zaidi ya Jacqueline. David alibaki ametulia katika meza aliyokuwa amekaa, alimshuhudia msichana huyo akiangalia huku na huko kama vile alikuwa akimtafuta mtu. Aliendelea kumwangalia Jacqueline ambaye mara kadhaa alimwangalia David ambaye alionekana kama hamtambui. Hatimaye msichana huyo alichukua simu yake na kuonekana akimpigia mtu. Baada ya sekunde kadhaa simu ya David ilianza kuita kwa sauti ambayo hata Jacqueline aliisikia.

    “Haa! Kumbe wewe ndiyo David nilikuwa nahisi hivyo” Alisikika Jacqueline akimwambia David kabla ya kijana huyo kuonekana anasimama. Alijongea kwa msichana huyo na walikumbatiana. “Mimi ndiye David..... Nilishakutambua ila nilitaka usumbuke kidogo” Alisikika David mara baada ya kukumbatina na msichana huyo. Wote walielekea katika meza aliyokuwa amekaa David ambaye alimwagizia kinywaji laini msichana huyo pia.

    Walifurahia kukutana kwao huku kila mmoja akivutiwa na mwenzie. Wakati huo Jacqueline alikamilisha wazo lililokuwa kichwani mwake, alikuwa tayari kuwa na David katika maisha yake kutokana na utanashati aliokuwa nao kijana huyo. Mbali na ukweli aliokwisha kuaambiwa na kijana huyo ambaye hakufanikiwa kumaliza hata shule ya msingi lakini alikubaliana na wazo lililokuwa kichwani mwake. Siku hiyo ilikuwa ya furaha kwao kwani walifahamiana zaidi.

    Baada ya wiki mbili David alikuwa akifanya kazi ya ulinzi katika kampuni ya ulinzi iliyokuwapo jijini. Alikuwa amefanikiwa kupita katika usaili wa kampuni hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa aliokuwa nao. Hiyo yote ilitokana mafunzo ya kijeshi aliyokwisha yapata miaka kadhaa iliyokuwa imepita wakati akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mbali na kazi hiyo aliyokuwa ameipata, tayari alikuwa na uhusiano na Jacqueline huku wakiwa na ahadi walizopeana katika maisha yao ya baadaye. David alikuwa amemsimulia msichana huyo kwa ufupi juu ya maisha yake na hakumalizia kisa chake baada ya kuona Jacqueline akiumia kusikika maisha hayo. Wakiwa katika mwanzo wa uhusiano wao David aligundua mambo kadhaa kutoka kwa Jacqueline, alikuwa akisumbuliwa sana na wanaume na mara kadhaa alikuwa akiwajibu vibaya walivyokuwa wakimpigia simu. Msichana huyo alimwondoa hofu David huku akimwambia kuwa angehakikisha anajilinda ili siku moja watimize ndoto zao.

    * * *

    Bwana Abraham alikuwa na mafanikio makubwa katika biashara zake nchini Uganda na sehemu nyingine tofauti za bara la Afrika. Taabu za maisha kwake zilikuwa zimepotea zaidi alikuwa akifurahia maisha na mke wake Aminata aliyekuwa mama wa watoto wawili kwa wakati huo. Mbali na Gray walikuwa wamebahatika kumpata mtoto mwingine wa kike aliyekuwa akiitwa Anita aliyekuwa na umri wa miaka mitatu. Wakati huo Gray aliyekuwa na umri wa miaka kumi na nane alikuwa akisoma kidato cha sita katika shule ya kimataifa ya St. Mary ya jijini Dar es salaam, nchini Tanzania. Bwana Abraham hakuwa na hofu juu ya jambo lolote na alikuwa akiamini David alikuwa ameshakufa kama ilivyokuwa kwa mkewe mkubwa ambaye aliwatuma vijana wake walioongozwa na Killa Jose wamuue pia miaka kadhaa iliyokuwa imepita.



    Alikuwa akiamini David aliuawa na wauaji waliowakata vichwa askari wa jeshi la polisi ambao walipata ajali na David ambaye hakupatikana eneo la tukio. Mafanikio aliyoyapata ndio yaliyomfanya ahame nchini Uganda na kuelekea nchini Marekani katika jiji la Iowa.

    Alienda kuanza maisha na familia yake katika jiji hilo huku mwanao Gray akiwa anatarajiwa kuungana nao mara baada ya masomo yake ya sekondari, elimu aliyokuwa akisoma nchini Tanzania. Alikuwa na furaha katika kila hatua yake ya maisha huku akiwa na upendo kwa familia yake. Wakati huo alikuwa amepunguza ukatili aliokuwa akiufanya miaka kadhaa iliyokuwa imepita zaidi alikuwa akifurahia maisha yake. Katika jiji la Iowa alianzisha pia biashara kwa kupitia maduka kadhaa aliyoyafungua. Alikuwa akiishi katika nyumba ya kifahari jambo lililomfanya asahau hata mwanzo wa mali hizo alizokuwa akizifurahia katika maisha yake.

    Gray Abraham kama alivyofahamika katika shule ya kimataifa ya St. Mary alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha sita ambaye hakuna mwanafunzi ambaye hakumtambua. Hiyo yote ilitokana na uwezo wake kifedha. Halikuwa jambo la kushangaza kwa kijana huyo kuonekana akizunguka na magari ya kifahari jijini Dar es salaam. Mara nyingi wakati shule yao ilipofunga alikuwa akitumia muda wake wa likizo kufurahia maisha akiwa katika hoteli za kifahari huku baba yake akimtumia fedha za matumizi. Hakuwa na hofu juu ya maisha kwani alikuwa akitegemea kurithi utajiri wa baba yake aliyekuwa kila kitu kwake. Huku akiwa na maendeleo mabovu kitaaluma hakujali jambo hilo ambalo hata baba yake alilitambua, yeye alikuwa akipenda starehe zaidi.

    Katika maisha yake hayo ya ujana mbali ya wasichana kadhaa aliokuwa nao ambao walikuwapo nchini Uganda kuna jambo lilikuwa tofauti kwake katika mahusiano. Alikuwa amekutana na msichana katika shule aliyokuwa akisoma ambaye alikuwa tofauti na wasichana wengi aliowahi kukutana nao. Jambo hilo ndilo lilimfanya awe mtulivu akiwa Tanzania kwani alikuwa akitumia muda mwingi kumfuatilia msichana huyo ambaye hakuwahi kumpa nafasi. Jacqueline John ndiye alikuwa msichana pekee aliyeisumbua akili ya Gray na kumfanya amuwazie kila siku. Jambo lililokuwa likimpa hamasa ya kumpata msichana huyo haraka lilitokana na muda wa kuwapo shuleni hapo kwa vile walibakiwa na miezi mitatu ili wamalize kidato cha sita. Hakuwahi kupata jibu lolote zuri toka kwa Jacqueline zaidi ya kuwa rafiki yake wa kawaida. Siku zote alijiapiza kuhakikisha hamkosi msichana huyo akiwa shuleni hapo, alipanga kumpata kwa gharama yeyote.

    Suala la kumkosa msichana huyo lilimuumiza sana kichwa na alikuwa akiwaza kutafuta ufumbuzi juu ya jambo hilo. Kwani mara baada ya masomo yake alikuwa akitarajia kuelekea nchini Uganda kabla ya kuelekea nchini Marekani katika jimbo la Iowa ili kuungana na familia yake. Wazo lililokuwa limemkaa kichwani, aliwaza endapo Jacqueline angemkubali alihitaji wakasome wote masomo ya elimu ya juu nchini Marekani. Kutokana na uwezo wa kifedha wa baba yake alikuwa akiamini kwamba hakuna jambo ambalo lingeshindikana.

    Baada ya kuona bado Jacqueline hakubali kuwa na uhusiano naye aliwaza kufanya jambo. Aliamua kuanza kumfuatilia msichana huyo kila sehemu aliyokuwa anaeenda. Lengo lake kuu lilikuwa ni kuhakikisha anamfahamu mtu ambaye alikuwa na uhusiano na msichana huyo. Kwa kufanya hivyo aliamini angeweza kupata sehemu ya kuanzia ili kumpata msichana huyo kwa vile siku zote alikuwa akiamini msichana huyo alikuwa na mahusiano na mtu. Jitihada zake za kumfuatilia Jacqueline alikuwa akizifanya akishirikiana na rafiki zake kadhaa. Moyoni Gray alikuwa mtu ambaye hakuwa na huruma hata kidogo na tabia yake hiyo ilikuwa ikiendana kwa kiasi kikubwa na ile ya baba yake bwana Abraham.

    Mwezi Januari tarehe kumi, siku ya Jumamosi wakiwa wamebakiwa na siku kadhaa waanze mtihani wa kumaliza kidato cha sita, Gray alionekana maeneo ya Kariakoo akimfuatilia Jacqueline. Huku akiwa anatembea kwa tahadhari alimfuatilia msichana huyo aliyeenda kuishia kwenye benki ya taifa ya biashara. Alisimama kwa mbali huku akimwona Jacqueline anamwonyeshea ishara mtu aliyekuwa ndani ya benki hiyo. Gray alitulia na baada ya dakika kadhaa alimshuhudia kijana mmoja akitoka katika benki hiyo akiwa amevaa mavazi ya kampuni ya ulinzi. Kijana huyo alionekana akiwa katika furaha kama ilivyokuwa kwa Jacqueline, alimfuata msichana huyo kabla ya kuwaona wakikumbatiana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gray aliumia kushuhudia tukio hilo huku akiwa amegundua kuwa Jacqueline alikuwa na uhusiano na mlinzi huyo wa benki. Alitulia huku akiwaona wakizungumza na baada ya dakika kadhaa waliagana kabla ya Jacqueline kuanza kuondoka. Alisubiria kwa muda huku akimshuhudia msichana huyo akiondoka ilhali mlinzi huyo naye akiingia katika benki hiyo. Mara baada ya Jacqueline kuzamia, Gray alianza kutembea akielekea katika benki hiyo. Lengo lake lilikuwa ni kutaka kumfahamu vizuri kijana ambaye alionekana kuwa na uhusiano na Jacqueline. Sura yake ilikuwa imebadilika huku moyoni akiumia kwa kumkosa Jacqueline ambaye alionekana kumpenda mlinzi huyo ambaye alimwona hakuwa na mtazamo wowote katika maisha. Kichwani aliingiwa na wazo la kuhakikisha anampata Jacqueline kwa gharama yeyote.

    Hakumhofia hata kidogo mlinzi huyo wa benki kwani alikuwa akiamini ilipo pesa hakuna jambo lililokuwa linashindikana. Mara baada ya kuingia katika benki hiyo alichukua karatasi zitumikazo kwa malipo na alionekana akiijaza moja wapo. Wakati akiendelea na zoezi hilo alikuwa akimwangalia mara kadhaa mlinzi huyo ambaye alikuwa karibu naye. Baada ya kuijaza karatasi hiyo alitulia kabla ya kumkazia macho kijana huyo, kwa haraka aligundua alikuwa mkakamavu kutokana na alivyojengeka mwili wake kwa mazoezi. Wakati akiendelea kumtathimini vizuri mlinzi huyo aligeuka na waligongana macho yao. Mlinzi huyo alishtuka na kuanza kumwangalia Gray kwa umakini huku akionekana kama alikuwa amegundua kitu.

    Baada ya sekunde kadhaa mlinzi huyo alimfuata Gray kabla ya kusikika akimuuliza swali. “Samahani unaitwa nani? Kuna mtu nakufananisha naye!” “Aah! Mimi naitwa Gray kwani vipi?” alimjibu huku akiwa na hofu kidogo. “Aah! Umefanana sana na binamu yangu mmoja ambaye kwa sasa ni marehemu” Alisikika mlinzi huyo ambaye alianza kugeuza kichwa chake taratibu. Wakati huo Gray alikuwa amegundua kuwa mlinzi huyo alikuwa akiitwa David Johnson kama lebo ya shati lake ilivyokuwa imeandikwa. Gray alianza kuondoka taratibu eneo hilo la benki huku David akionekana kumwangalia sana, alikuwa ameishika karatasi aliyoijaza kwa ajili ya kuweka fedha ambayo aliondoka nayo.

    Wakati huo David alikuwa katika zamu yake kwenye benki hiyo ya taifa ya biashara kama alivyokuwa amepangwa na kampuni yake ya ulinzi. Alikuwa ameshtushwa na kijana ambaye alimwona dakika kadhaa zilizokuwa zimepita kwani alikuwa anafanana sana na binamu yake Sabinus, aliyefariki miaka kadhaa iliyokuwa imepita. David bado alikuwa akiishi Mbagala huku kazi hiyo ya ulinzi aliyokuwa akiifanya ikimsaidia kujikimu na mahitaji yake kadhaa. Kichwani alikuwa ametawaliwa na mpango juu ya jinsi ya kuondoka nchini Tanzania ili aelekee Uganda kwani alihitaji kupata haki yake ya mali za marehemu baba yake.

    Alikuwa akionekana na furaha ambayo siku zote ilitokana na uhusiano wake na Jacqueline aliyekuwa mfariji wake juu ya kila jambo. Wakati huo alikuwa akiwasiliana naye kwa njia ya simu tu kwani msichana huyo alikuwa amebakiwa na siku chache ili aingie kwenye mtihani wake wa mwisho.

    Mwezi Februari tarehe ishirini, Jacqueline alimaliza mtihani wake wa mwisho na mara baada ya kuondoka shule aliongoza kwa David akiwa na lengo la kusherekea naye mafanikio aliyokuwa ameyapata. Siku hiyo David alikuwa amejiandaa kwani alikuwa na pesa za kutosha ili kufurahia mafanikio ya msichana huyo wa ndoto zake.

    Mara baada ya kukutana walielekea katika hoteli moja iliyopo maeneo ya Kunduchi. Wakati huo msichana huyo alikuwa akihisi kichwa chake kikimuuma kwa mbali kama ilivyokuwa kawaida yake juu ya tatizo hilo. Hakutaka kumweleza David juu ya jambo hilo na zaidi hakuwa tayari kuikatisha furaha ya siku hiyo ambayo walikuwa wakiisubiria kwa hamu. Alikuwa akielewa maumivu hayo yalikuwa yameongezwa na zoezi la kusoma kwa muda mrefu wakati wakiwa katika mitihani yao. Walitumia usafiri wa teksi ya kukodi kufika katika hoteli hiyo. Walianza kunywa vinywaji laini huku wakionekana wakiwa na furaha ya kuwa pamoja. Baada ya nusu saa wakati zoezi hilo likiendelea David aligundua kitu kutoka kwa Jacqueline. Alikuwa akishika kichwa chake kama vile kilikuwa kinamuuma sana, jambo hilo lilimkumbusha siku ya kwanza alipokutana na msichana huyo mjini Njombe. Alikumbuka jinsi alipomwona akishika kichwa kabla ya kupoteza fahamu, alimsogelea na kuonekana akimuulizia Jacqueline juu ya hali yake lakini ghafla alikuwa akimjibu kwa taabu sana. Alipokigusa kichwa cha msichana huyo aligundua kilikuwa kimepata joto kupindukia.

    Jambo hilo lilimpa hofu David ambaye wakati huo msichana huyo alikuwa haongei kabisa huku macho yake yakiwa yamemtoka. Aliondoka eneo hilo akikimbia huku akiwa na lengo la kukodi teksi ili imwahishe msichana huyo hospitali. Hakutumia muda mrefu kulipata gari hilo kutokana na kelele alizokuwa akizitoa alipofika katika eneo la maegesho ya teksi hizo. Akiwa na dereva teksi pamoja na wapita njia waliosikia akilalamika juu ya tatizo la Jacqueline waliongoza mpaka eneo alilokuwa amemwacha msichana huyo. Walipofika waligundua Jacqueline alikuwa amepoteza fahamu huku akiwa amelalia meza waliyokuwa wakiitumia.

    Bila kupoteza muda walisaidiana kumbeba kabla ya kuishia kumpakia msichana huyo katika teksi hiyo ambayo David alikuwa ameikodi. Baada zoezi hilo aliingia kwenye gari hilo ambalo liliondolewa kwa kasi wakiwa na lengo la kumwahisha Jacqueline hospitali. David alikuwa amemkumbatia msichana huyo huku akitokwa na machozi pasipo kujitambua. Siku zote alikuwa akihofia uhai wa msichana huyo ambaye aliamini alikuwa wa ndoto zake. Majira ya saa kumi kamili teksi hiyo ilikuwa ikifika eneo la hospitali ya serikali iliyopo Mwananyamala ambako Jacqueline alipokelewa na taratibu za kimatibabu zilianza kuchukua nafasi.

    David alisubiri kwa muda mrefu nje ya chumba maalum ambacho Jacqueline alikuwa akifanyiwa matibabu pasipo majibu yeyote. Ilipotimia saa moja usiku aliamua kumfuata muuguzi mmoja huku akiwa na hasira baada ya kuona anaambiwa asubiri kila mara wakati matibabu dhidi ya Jacqueline yakiendelea. Alimfuata muuguzi huyo baada ya kuona hapewi maelezo yeyote juu ya maendeleo ya msichana huyo. Hasira zake kwa muuguzi huyo bado hazikuzaa matunda kwani aliambiwa aendelee kusubiri. Majira ya saa tano usiku walinzi waliokuwa wakizunguka eneo hilo la hospitali walimtaka aondoke. Alielezwa pia na muuguzi mmoja kuwa taratibu zote za kimatibabu dhidi ya Jacqueline zilikuwa zikiendelea. Muuguzi huyo alimwambia David kuwa bado masaa kadhaa yalikuwa yakihitajika ili kukamilisha matibabu dhidi ya Jacqueline. Hatimaye David aliamua kuondoka hospitalini hapo akiwa na lengo la kurudi siku iliyofuata asubuhi. Alitoa nje kabla ya kuanza kuelekea katika kituo cha mabasi akiwa na matarajio ya kuelekea Mbagala alikokuwa akiishi.

    Kichwani alikuwa ametawaliwa na mawazo juu ya Jacqueline na hakujua hatma ya mrembo huyo. Hata alipofika Mbagala majira ya saa saba usiku hakuwa na amani kwani usiku mzima hakulala hata kidogo huku akiwa na mawazo sana. Ilipotimia saa kumi na moja na nusu alifajiri alianza kujiandaa akiwa na lengo la kwenda katika hospitali aliyomwacha Jacqueline iliyopo maeneo ya Mwananyamala. Baada ya zoezi hilo alielekea katika kituo cha mabasi kabla ya kupata gari na kuanza safari ya kuelekea hospitali. Kichwani bado alikuwa akiwaza mambo mengi pasipo kupata jibu huku akimkumbuka bwana Abraham, mtu ambaye alimchukia sana katika maisha yake.

    Saa moja na robo alikuwa akifika katika hospitali husika ambayo alimwacha Jacqueline. Bila kupoteza muda aliongoza eneo la mapokezi kabla ya kwenda kueleza shida yake ya kutaka kumwona Jacqueline. Jambo lililomshangaza lilihusiana na mshtuko ambao aliuonyesha muuguzi aliyekuwapo katika eneo hilo la mapokezi. “Umesema huyo msichana ni mchumba wako?” Alisikika akiuliza muuguzi huyo baada ya kuwa amemuuliza kwa zaidi ya mara tatu. “Nimesema huyo ni mchumba wangu…. Mbona hunielewi nesi? Naomba unielekeze eneo alipo” alijibu David kwa ukali ikiwa ni mara ya tatu baada ya kuona haelewani na muuguzi huyo.

    “Ok! Nifuate ili uonane na daktari mwenyewe, suala hili sihusiki nalo” Alisikika muuguzi huyo ambaye alianza kufuatwa na David aliyeonyesha hofu ghafla ilhali ukali aliokuwa nao ukiwa umepotea.

    Waliongoza mpaka katika chumba ambacho nje yake kilikuwa kimeandikwa Daktari Mkuu na mara baada ya kuingia katika chumba hicho Daid alimshuhudia daktari mmoja akiwa amekalia kiti alichokuwa akizunguka nacho kila upande katika eneo alilokuwapo. Muuguzi aliyekuwa naye alimtambulisha David kwa daktari huyo ambaye alishtuka kidogo kabla ya kumuoneshea ishara muuguzi huyo aondoke katika ofisi hiyo. Jambo hilo lilichukua nafasi kwani muuguzi huyo alionekana akiondoka katika ofisi hiyo wakati ambao David aliyetawaliwa na uoga wa ghafla aliambiwa akae katika kiti kilichokuwapo.

    Alimkazia macho daktari huyo aliyekuwa amekaa naye huku akisubiri jambo ambalo angeambiwa, katika chumba chao utulivu ulitawala wakati ambao daktari huyo alikuwa akimwangalia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Kijana pole sana kama ni kweli Jacqueline alikuwa mchumba wako” Alisikika daktari huyo baada ya ukimya wa muda mfupi. David alimtolea macho huku akiwa ametulia lakini mapigo yake ya moyo yakiwa yanamwenda mbio. “Aah! Pole sana kwa sababu hivi tunavyoongea Jacqueline hatuko naye tena duniani” Aliongeza daktari huyo kabla ya kuendelea. “Ilikuwa muda mfupi tu toka uondoke jana usiku, majira ya saa sita kasoro tulishindwa kuokoa maisha ya mchumba wako ingawaje tulijitahidi kwa uwezo wetu wote na hivi ninavyoongea mwili wake umeshachukuliwa na familia yake, nadhani utasafirishwa kwenda kwao mkoani Dodoma kwa mazishi” Alimaliza Daktari huyo ambaye aliongea katika sauti ya taratibu iliyokuwa imejaa upole na huzuni juu ya tatizo hilo alilolipata David.

    David aliishiwa pumzi na kuhisi kama kuna kitu kilikuwa kimemkaa shingoni, aliburuzika taratibu toka katika kiti alichokuwa amekaa kabla ya kupiga magoti na mwishoe aliinamisha kichwa chake pia kama alikuwa msikitini. Alitulia kwa muda wa dakika kumi huku akiwa hasikilizi mambo kadhaa yaliyokuwa yakielezwa na daktari huyo aliyekuwa akimshauri. Baada ya muda huo aliinua kichwa chake huku usoni akionekana kama alikuwa amebadilika ghafla kwani alikuwa mweupe kupindukia. Mashavu yake yalikuwa na majimaji ya machozi baada ya kulia huku akiwa hajitambui.

    Alinyanyuka katika eneo hilo alilokuwapo na kuanza kuondoka taratibu huku akiwa hajaaga pia, jambo hilo lilikuwa limemchanganya kwa kiasi kikubwa hata daktari aliyekuwa akimwita alikuwa hamsikii.Alitoka eneo hilo la hospitali kabla ya kutokomea mitaani huku akionekana kama vile akikuwa amechanganyikiwa.

    Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili David alikuwa ndani ya chumba chake alichokuwa amepanga maeneo ya Mbagala huku akiwa anashinda na kulala katika chumba hicho. Chakula chake kikubwa kilikuwa mikate aliyoinunua pamoja na maji. Hakuwa na chakula kingine zaidi ya hivyo huku akiwa ametawaliwa kwa kiasi kikubwa na mawazo juu ya hatma ya maisha yake yaliyokuwa yamepoteza mwelekeo kabisa. Kwa muda mrefu akiwa katika chumba hicho alikuwa akimkumbuka sana Jacqueline na zaidi wazazi wake waliopoteza maisha miaka mingi iliyokuwa imepita. Kwa kiasi kikubwa alikuwa amechanganyikiwa na alishindwa kuhudhuria msiba wa msichana huyo kwa vile hakujua eneo ambalo alikuwa akiishi. Mbali na jambo hilo aliamini angeumia zaidi kama angehudhuria mazishi ya msichana huyo. Alijaribu kumpigia simu dada yake Jacqueline aliyeitwa Mary John lakini alikuwa hapatikani kama ilivyokuwa kwa namba ya Jacqueline ambaye hakuwapo tena duniani.

    Hatimaye baada ya kuona dalili mbaya za hatma maisha yake aliamua kuelekea katika ofisi ya kampuni yake ya ulinzi iliyokuwapo maeneo ya Posta. Lengo lake kubwa lilikuwa kwenda kuomba msamaha kwa viongozi wa kampuni hiyo ya ulinzi ambayo alikuwa akifanyia kazi kwa sababu hakwenda kazini kwa muda wa wiki mbili. Alipofika huko mambo yalikuwa magumu kwake kwani viongozi wa kampuni hiyo walikuwa wamemtoa katika orodha yao ya wafanyakazi wao. Kitu pekee alichokipata ilikuwa ni barua ya kufukuzwa kazi na kampuni hiyo. David alizidi kuchanganyikiwa kutokana na uamuzi huo uliofikiwa na kampuni hiyo iliyokuwa ikimwamini kikazi. Mbali na lengo lake la kuomba msamaha David alikuwa katika mwonekano wa ovyo ambao ilikuwa vigumu kwa mtu kumwajiri. Alikuwa amevaa suruali chafu ambayo ilikuwa sawa na shati lake lililokuwa hivyo pia. Wakati mwingine alikuwa akitokwa na kamasi pasipo kujitambua jambo ambalo mtu yeyote ambaye angemwona angegundua kuwa hakuwa sawa au alikuwa na matatizo ya kisaikolojia.

    Hatimaye David aliondoka na kurudi maeneo ya Mbagala katika chumba alichokuwa amepanga huku akiwa katika hali ileile ya kuchanganyikiwa. Baada ya wiki mbili za ugumu wa maisha aliamua kuanza kuuza maji ya kunywa eneo la Magomeni. Alifanya kazi hiyo katika foleni ya magari yaliyokuwapo eneo hilo mara kadhaa. Hakuna jambo alilokuwa akilifikiria kwani kila alilowaza lilikuwa gumu. Alikuwa akiwaza kurudi nchini Uganda ili kwenda kudai haki ya urithi wake kutoka kwa bwana Abraham lakini alipowaza suala la nauli alikuwa akikata tamaa kabisa. Biashara yake hiyo ya maji ilikuwa ikimsaidia kwa chakula tu na hakuna jambo alilonufaika kutokana na fedha alizokuwa akizipata.

    * * * *

    Gray Abraham kama lilivyokuwa jina lake alikuwa ni kijana ambaye kwa kiasi kikubwa aliendana na tabia za baba yake bwana Abraham. Kwake mambo ya visasi pamoja na uonevu yalikuwa ni ya kawaida sana. Hilo ndilo lililokuwapo wakati huo ikiwa ni baada ya kumaliza masomo ya sekondari katika shule ya kimataifa ya St.Mary.Alikuwa amemfanyia tukio kubwa ambalo kwa David halingeweza kufutika katika kumbukumbu za maisha yake kama angeligundua siku moja. Wakati huo alikuwapo jijini Entebbe na Jacqueline ambaye walikuwa na uhusiano huku wakiwa na ahadi ya kufunga harusi katika siku za usoni baada ya masomo yao ya chuo. Alikuwa amefanya tukio kubwa lililofanikisha furaha yake ya kumpata msichana huyo aliyekuwa akimuumiza moyo wake kwa muda mrefu.

    Wakati huo walikuwapo jijini humo kwa wiki kadhaa, Gray alikuwa akifanya taratibu za hati za kusafiria ili msichana huyo pamoja na yeye waelekee katika jiji la Iowa nchini Marekani kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu. Yote hayo yalikuwa yametokea baada ya kufanikisha tukio la kuthibitisha vifo vya watu wawili tofauti. Alikuwa amefanikiwa kutoa taarifa kwa David kuwa Jacqueline alikuwa amekufa lakini alifanikiwa pia kumdanganya msichana huyo kuwa David alikuwa amefariki. Aliyafanikisha hayo baada ya kushirikiana na watu kadhaa waliomfanikishia zoezi hilo.

    Miezi kadhaa iliyokuwa imepita baada ya kuonana na David kwa mara ya kwanza katika benki aliyokuwa akifanya kazi ya ulinzi, alimwajiri mtu aliyekuwa akimfuatilia kijana huyo kila sehemu aliyokuwa anaenda ikiwa ni pamoja na mienendo yake na Jacqueline. Hata baada ya kumaliza mitihani yake zoezi hilo lilikuwa likiendela kabla ya kufanikiwa kwake kutoa taarifa potofu zilizo wahusu watu hao wawili. Siku ambayo Jacqueline alizimia kwa mara ya mwisho kutokana na maumivu ya kichwa, alikuwa akiwafuatilia David na msichana huyo waliokuwapo maeneo ya Kunduchi. Akiendelea kuwafuatilia, alikuwa katika teksi moja ya kukodi iliyokuwa eneo la maegesho huku akiwa nyuma ya kila mwenendo wa watu hao waliokuwa wapenzi. Wakati akiwa anaendelea na zoezi hilo la kuwafuatilia, aligundua kuwa Jacqueline alikuwa amepoteza fahamu.

    Alimshuhudia David akihangaika kutafuta gari na mwishoe alipata teksi ya kukodi, akisaidiana na watu kadhaa walimpakia kwenye gari msichana huyo na safari ilianza wakielekea hospitali. Bila kuchelewa Gray alimwamuru dereva aliyekuwa naye alifuatilie gari hilo na jambo hilo lilichukua nafasi. Waliwafuata mpaka walipoishia katika hospitali moja ya serikali iliopo maeneo ya Mwananyamara. Akiwa kwenye gari aliwaona wauguzi wakisaidiana na David kumchukua msichana huyo kisha walianza kuingia naye ndani ya Hospitali hiyo. Wakati huo Gray aliona ulikuwa muafaka kutimiza lengo lake. Huku akijificha kwa kofia alishuka kwenye gari hilo na kumfuata muuguzi mmoja aliyekuwa akiingia hospitalini hapo.

    Baada ya kumsimamisha muuguzi huyo alimwomba namba ya simu ya daktari mkuu wa hospitali hiyo. Jambo hilo halikuwa gumu kwani aliipata namba hiyo. Bila kupoteza muda alirudi tena katika gari alilofika nalo kisha alimpigia simu daktari mkuu wa hospitali hiyo. Alimwomba atoke nje katika eneo hilo walilokuwapo, daktari huyo hakubisha na baada ya dakika tano alitoka na kuongoza kwenye gari alilokuwapo Gray. Alitii wito huo kwa sababu pia alielezwa kulikuwa na kazi ya fedha za kutosha.Alimwomba daktari huyo waende katika baa moja iliyokuwapo karibu na hospitali hiyo kwa ajili ya maongezi mafupi. Jambo hilo lilichukua nafasi na baada ya dakika kumi walikuwa katika maongezi yao.

    Gray alikuwa akimtaka daktari huyo atoe taarifa potofu kwa David, kijana aliyempeleka mgonjwa wake dakika kadhaa zilizokuwa zimepita katika hospitali yao. Alitaka daktari huyo aeleze kuwa msichana huyo alikuwa amekufa. Jambo hilo lilichukua muda kabla ya kueleweka kwa daktari huyo aliyehitaji kiasi cha milioni sita za kitanzania ili kufanikisha zoezi hilo. Jambo hilo halikuwa gumu kwa Gray ambaye hakukosa pesa kutoka kwa baba yake aliyekuwa tajiri mkubwa nchini Uganda na wakati huo akiwa na biashara zake pia nchini Marekani. Baada ya makubaliano hayo, Gray alihitaji msaada juu ya jambo jingine lililokuwa la muhimu sana kwake alihitaji pia kumchukua Jacqueline aelekee naye nchini Uganda kama mgonjwa aliyekuwa akienda kutibiwa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daktari huyo alilikubali ombi hilo lililokuwa dogo pia kwani aliahidi kumchoma sindano za usingizi Jacqueline mara baada ya kuzinduka ili asafiri kama mgonjwa katika safari iliyopangwa kufanyika siku iliyofuata. Mara baada ya makubaliano hayo Gray alitoa milioni mbili kama malipo ya awali kati ya milioni sita alizopaswa kulipa. Daktari huyo akiwa na furaha aliondoka na kuahidi kuwa kila jambo lingekuwa sawa. Baada ya zoezi hilo Gray alichukua simu yake na kumpigia afisa mmoja wa uwanja wa ndege ambaye alikuwa akifahamiana naye. Alihitaji aandae tiketi mbili huku nyingine akieleza ilikuwa ya mgonjwa ambaye alipaswa kusafiri naye siku iliyofuata na zaidi alihitaji msaada juu ya ukweli kwamba Jacqueline hakuwa na hati ya kusafiria nje ya nchi. Aliahidiwa kusaidiwa jambo hilo na alijisikia furaha kwa jitihada hizo alizokuwa amefanya.

    Alimwamuru dereva teksi aondoe gari katika eneo hilo walilokuwapo mara baada ya kurejea katika gari. Wakati huo alikuwa akitaka waelekee katika ofisi za kampuni iliyokuwa imemwajiri David iliyokuwapo maeneo ya Posta huko alitaka pia kufanya jambo. Baada ya dakika arobaini na tano alikuwapo katika ofisi hizo na aliomba kuonana na kiongozi mkuu wa kampuni hiyo ya ulinzi. Hakupata taabu kwani aliongozwa na msichana aliyekuwapo mapokezi mpaka katika ofisi ya kiongozi huyo. Mara baada ya kuingia katika ofisi hiyo Gray alianza maongezi na kiongizi huyo. Alikuwa akihitaji amsaidie jambo dogo lilokuwa muhimu sana kwake. Alihitaji kiongozi huyo atoe taarifa potofu kuhusu David kwa mtu mmoja tu. Alihitaji kiongozi huyo amweleze Jacqueline kuwa David aliuawa na majambazi wakati akiwa kazini katika benki aliyokuwa akifanyia kazi maeneo ya Kariakoo, majambazi walifanya jaribio la kuiba katika benki hiyo. Taarifa hizo alimweleza kiongozi huyo kuwa zilipaswa kutolewa baada ya siku kadhaa endapo angehitajika kufanya hivyo. Jambo hilo lilikuwa gumu kuingia akilini mwa kiongozi huyo ila alipoelezwa kuhusu milioni tatu za kitanzania aligundua lilikuwa rahisi ghafla. Alikubali kumsaidia kutoa taarifa hizo batili kwa msichana huyo ambaye Gray aliahidi kumpeleka eneo hilo siku yeyote kuanzia siku hiyo.

    Hatimaye jambo hilo lilifanikiwa kwa aslimia zote baada ya Gray kumpatia kiongozi huyo kiasi cha milioni moja na nusu huku akiwa amepanga kumalizia fedha ambazo zilisalia siku ya tukio husika. Baada ya majadiliano hayo Gray aliondoka huku akionekana kuwa mtu mwenye tabasamu muda wote. Aliamini mipango yake ingefanya kazi kama alivyokuwa amepanga. Bado alikuwa akiwaza jambo jingine kubwa zaidi alilowaza lichukue nafasi pia. Hatimaye alipanda kwenye gari alilofika nalo eneo hilo alilokuwa amekodi kabla ya kuelekea katika hoteli aliyokuwa amepanga. Huko alikuwa akiwasiliana na daktari aliyempa jukumu ya kumpotosha David, daktari ambaye aliyemweleza juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Akiwa katika hoteli hiyo pia alielezwa kuwa kila kitu juu ya safari yake na Jacqueline kilikuwa sawa, safari iliyotarajiwa kuanza siku iliyofuata majira ya saa moja asubuhi. Hayo yote alielezwa na afisa aliyempa jukumu la kuandaa safari hiyo.

    Wakati huo ikiwa majira ya saa nne usiku Gray alielezwa kuwa David bado alikuwepo hospitali, baada ya saa moja alipewa taarifa nyingine kuwa kijana huyo aliondolewa na walinzi wa hospitali huku wakiwambia afike siku iliyofuata. Jambo hilo lilikuwa la furaha kwa Gray ambaye pia ilipotimia saa sita usiku alipigiwa simu na daktari na kupewa tarifa za kuzinduka kwa Jacqueline. Msichana huyo alichomwa sindano za usingizi mara baada ya kuzinduka na hakupata muda wa kukumbuka hata jambo. Gray siku iliyofuata majira ya saa kumi na moja asubuhi akiwa na gari alilokodi alifika katika hospitali husika iliyokuwapo Mwananyamara na kumchukua Jacqueline ambaye bado alikuwa usingizini. Aliongozana na dakatari pamoja na wauguzi kadhaa na walimfikisha msichana huyo uwanja wa ndege akiwa kama mgonjwa aliyesafirishwa kwenda nje ya nchi. Hilo lilifanikiwa na majira ya saa moja asubuhi Gray alikuwa ndani ya ndege ya shirika la Uganda Airline na Jacqueline ambaye alikuwa amelala mpaka wakati huo. Moyoni alikuwa na furaha juu ya kila hatua ya mambo aliyokuwa akiyafanya. Tayari alikuwa amemlipa Daktari aliyempa kazi ya kuhakikisha anamwambia David kuwa Jacqueline alikuwa amekufa.

    Hakuwa na hofu huku akiwa na mpango wa kumpeleka Jacqueline katika kampuni ya ulinzi aliyokuwa akifanyia kazi David ili naye apewe taarifa ya uongo ya kifo cha mchumba wake huyo. Kukamilisha zoezi hilo ipasavyo alikuwa amemwachia kiasi cha milioni moja rafiki yake mmoja aliyemsindikiza uwanja wa ndege. Alimwomba rafiki yake huyo ahakikishe anaandaa kaburi hewa maeneo ya Mbagala ambalo hangezikwa mtu lakini kibao cha kaburi hilo alihitaji kiandikwe David Johnson. Baada ya saa kadhaa Jacqueline alikuwa chini ya uangalizi mkali wa madakari waliohusika na vichwa katika hospitali kuu ya jiji la Entebbe. Wakati huo Gray alikuwa na amani zaidi baada ya kupigiwa simu na kuelezwa kuwa David alikuwa amepewa taarifa za uongo zilizohusu kifo cha Jacqueline.





    Madaktari waliokuwa wakimtibu msichana huyo katika hospitali hiyo walimhakikishia Gray kuwa wangemaliza tatizo la maumivu ya kichwa alilokuwa akisumbuliwa Jacqueline. Zoezi la matibabu yake liliambatana na upasuaji mdogo wa kichwa eneo la nyuma kwa vile kulikuwa na uvimbe uliokuwa unachangia kupoteza fahamu kwa msichana huyo.

    Baada ya siku mbili Jacqueline alizinduka akiwa katika eneo ambalo hakulitarajia, alikuwa katika chumba maalum alicholazwa. Chumba hicho kilikuwa na maua mbalimbali yaliyoashiria upendo pamoja na kumpa pole. Jambo hilo lilimshtua sana na alihisi kuwa mambo hayo yalifanywa na David akishirikiana na wazazi wake. Hakuna mtu aliyekuwepo katika chumba hicho jambo lilompa maswali zaidi. Alipojishika kichwani aligundua kulikuwa na pamba zilizozunguka eneo hilo. Wakati huo alijisikia mwepesi na hakuwa na maumivu ya kichwa hata kidogo. Baada ya dakika kadhaa akiwa anatafakari juu ya kila jambo lililokuwa eneo hilo aligundua mlango ulikuwa ukifunguliwa. Alikaa vizuri akiwa na hamu kubwa ya kumwona mtu ambaye angeingia. Alishtuka mara baada ya mtu huyo kuingia kwani hakumtarajia hata kidogo. Alikuwa Gray ambaye mkononi alikuwa na maua kadhaa yaliyoashira upendo. Alijongea eneo la kitandani alilokuwapo kisha alimkabidhi maua hayo. Jacqueline aliyapokea huku akiwa haelewi jambo lililokuwa likiendelea.

    “Pole sana Jacqueline kwa ufupi ni kwamba sasa hatuko Tanzania tupo Uganda” Ilikuwa sentensi ya kwanza ya Gray ambayo ilimshtua sana Jacqueline. Gray alianza kuelezea jinsi msichana huyo alivyofika nchini humo huku jambo kubwa akimdanganya kuwa alikuwa amezidiwa sana na matibabu yake yalishindwa kufanyika nchini Tanzania. Aliendelea kumweleza kuwa alijitolea kumpeleka nchini humo baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya zaidi. Mbali na jambo hilo alidai Jacqueline alikuwa hana msaada baada ya kuachwa peke yake katika hopsitali aliyofikia iliyokuwapo maeneo ya Mwananyamara. Jambo lililomshtua sana Jacqueline alielezwa kuwa wazazi wake hawakuwa na taarifa zake lakini alichanganyikiwa zaidi alipoambiwa kulikuwa na tukio baya lililompata David.

    Alikosa amani ghafla hasa alipoaambiwa kuwa kulikuwa na jambo baya lililompata mchumba wake. Hakuambiwa jambo hilo na Gray aliyeahidi kumwambia mara baada ya kupona kwake kabisa. Zoezi lililochukua nafasi wakati huo, Jacqueline alitoa namba ya simu ya baba yake ambaye alipigiwa simu akiwa nchini Tanzania na kuelezwa kuwa mwanaye alikuwa nchini humo Uganda. Taarifa hizo ziliishtua sana familia ya msichana huyo iliyokuwa ikimtafuta. Wazazi wake waliandaa safari ya kuelekea nchini Uganda waliyopanga kusafiri baada ya siku tano. Bwana John akiwa ndiye baba yake Jacqueline alishtushwa na taarifa walizopewa na mke wake juu ya mwanao. Zaidi walionesha furaha juu ya Gray kwa msaada alioutoa katika kuokoa maisha ya mwanao. Baada ya siku tano walisafiri kuelekea jijini Entebbe nchini Uganda. Wakati huo walielezwa kuwa mwanao alikuwa amehurusiwa kutoka hospitali na alikuwa katika nyumba ya mwenyeji wao Gray. Mara baada ya kushuka katika ndege kwenye uwanja wa ndege wa jiji hilo walichukuliwa na gari dogo wakiwa na dereva aliyetumwa kuwachukuwa. Akili zao zilikuwa zimetawaliwa na shauku kubwa ya kutambua maendeleo ya kiafya ya mwanao na zaidi walihitaji kumshukuru kijana aliyeokoa maisha ya mwanao.

    Majira ya saa kumi na moja jioni walikuwa wakiingia katika nyumba ya kifahari iliyokuwapo katika eneo la matajiri wa jiji hilo. Wakati huyo bwana John na mkewe walikuwa watulivu wakiwa hawaelewi jambo lolote kuhusiana na nyumba hiyo zaidi utajiri wa magari yaliyokuwapo yameegeshwa eneo la nje ya nyumba hiyo. Mara baada ya kushuka kwao walilakiwa na mwanao Jacqueline ambaye alitoka ndani ya nyumba hiyo huku akionekana akiwa mzima wa afya kabisa. Nyuma yake alifuatwa na Gray ambaye naye pia aliwasogelea wazazi hao kabla ya kuwasalimia. Baada ya salamu waliingia ndani ya nyumba hiyo ya kifahari ambayo hawakuwahi kuioa katika maisha yao mbali na uwezo wa kifedha walikuwa nao kidogo wakiwa nchini Tanzania.

    Jambo lililowashangaza nyumba hiyo alikuwa akiishi kijana aliyemsaidia Jacqueline aliyejitambulisha kwa jina la Gray peke yake. Hakuwapo mtu mwingine zaidi ya watumishi wa ndani ambao hawakulala katika nyumba hiyo pamoja na walinzi waliokuwapo eneo la geti kuu muda wote. Baada ya muda mfupi waligundua kuwa mzazi wa Gray aliyeitwa Abraham alikuwapo nchini Marekani akiendeleza biashara zake akiwa na familia pia. Gray aliwaelekeza kila jambo lililohusu uwepo wa Jacqueline nchini humo Uganda kwa matibabu. Hawakuwa na kitu chochote walichompa Gray zaidi ya kumshukuru kwa msaada wake. Bwana John na mkewe hawakuelewa uhusiano uliokuwapo baina ya Jacqueline na Gray, hiyo yote ilitokana na upendo waliooneshwa na mwenyeji wao.

    Majira ya saa nne usiku wazazi hao walielekea kulala wakiwa wamemwacha mwanao pamoja na Gray ambao bado walikuwa wakiongea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naomba uniambie tatizo lililompata David, maana nimeshapona tayari na nahitaji kujua” Alisikika Jacqueline akimwambia Gray, muda mfupi baada ya wazazi wake kwenda kulala. Mpaka wakati huo hakuwa na amani huku akiwa na hofu juu ya usalama wa mchumba wake. Gray alivuta pumzi kidogo kabla ya kutulia akionekana kama hakuwa tayari kumjibu ombi hilo. Jacqueline aliendelea kulalamika mwishoe alikatishwa na Gray ambaye alikubali kumwambia baada ya muda huku akionekana kujali jambo alilotaka kulizungumza.

    “Jacqueline pole sana lakini kila jambo nitakalo lizungumza naomba unielewe, ukweli ni kwamba David aliuawa na majambazi katika tukio la uvamizi lililotokea katika benki aliyokuwa akifanya kazi” Alisikika Gray akimwambia mrembo huyo ambaye ghafla alimtolea macho kutokana na taarifa hiyo aliyopewa. Hakuamini hata kidogo kwamba mtu ambaye alikuwa mchumba wake hakuwa hai wakati huo. Akiwa katika hali hiyohiyo aliishia kuanguka chini akiwa amepoteza fahamu. Gray akiwa na mshtuko kidogo hakuwa na hofu juu ya jambo hilo kwani alionekana akiichukua simu yake. Alimpigia simu daktari ambaye alikuwa ameongea naye aliyeishi karibu na nyumbani kwao. Alimuandaa daktari huyo kwani alikuwa akiamini uwezekano wa kupoteza fahamu kwa Jacqueline kama ilivyokuwa imetokea.

    Baada ya dakika kumi daktari huyo alifika katika nyumba hiyo kabla ya kuanza kumtibu msichana huyo aliyezinduka baada ya dakika kadhaa huku akiwa mtulivu. Alikuwa ametulia ilhali akitokwa na machozi juu ya taarifa ya kufariki kwa David. Siku iliyofuata alikuwa katika hali hiyohiyo jambo lililowapa hofu wazazi wake pia. Gray alichukua jukumu la kuwaeleza juu ya kila jambo lililokuwa linaendelea ikiwa ni pamoja na taarifa yake potofu akidai David alikuwa amefariki. Wazazi wake wakishirikiana na Gray walisaidiana kumtuliza Jacqueline wakiwa na lengo la kumbadili mtazamo na zaidi akubaliane na kila jambo lililotokea lakini hawakufanikiwa. Wakati huo bwana John akiwa na mkewe waligundua kuwa mwanao hakuwa na uhusiano wowote na Gray.

    Baada ya wiki moja walikuwa safarini wakitumia ndege ya shirika la Uganda Airlines wakirudi nchini. Bado Jacqueline alikuwa mnyonge huku akiwa haamini kama mchumba wake alikuwa amefariki. Katika safari yao hiyo walikuwa wamesindikizwa na Gray ambaye lengo lake kubwa lilikuwa ni kumpeleka Jacqueline katika ofisi ya kampuni ya ulinzi iliyokuwapo maeneo ya Posta jijini Dar es salaam. Huko aliamini angeenda kukamilisha adhma yake ya udanganyifu juu ya kifo cha David. Alipolikumbuka kaburi bandia ambalo alihakikishiwa kuwa lilikuwa tayari maeneo ya Mbagala, alijikuta akitabasamu muda wote. Hakuwa na hofu huku akiamini kuwa alibakiwa na siku kadhaa ili aanze uhusiano wake mpya na mtu aliyekuwa akimpenda toka siku nyingi.

    Tayari alikuwa anawaza kuifuata familia yake nchini Marekani katika jimbo la Iowa na huko alipanga kwenda na msichana huyo aliyempenda, Jacqueline. Mipango yake ilienda kama alivyokuwa ameipanga kwani msichana huyo alikamilishiwa taarifa hizo za kifo cha David na kiongozi wa kampuni ya ulinzi ambayo David alikuwa akifanyia kazi. Jacqueline alielezwa kuwa David alipigwa risasi wakati akiwa katika benki aliyokuwa akifanyia kazi maeneo ya Kariakoo. Mara baada ya taarifa hizo Jacqueline aliongozwa mpaka maeneo ya Mbagala ambako Gray na rafiki yake walienda kumwonyesha kaburi la kijana huyo lililoandikwa David Johnson katika kibao chake. Waliweka mataji na maua tofauti juu ya kaburi hilo. Wakati huo aliamini kila jambo alilokuwa ameelezwa na hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo. Gray alijumuika na familia ya msichana huyo iliyokuwa ikiishi maeneo ya Masaki kwa muda wa wiki moja. Siku moja kabla ya kuondoka kwake kurudi nchini Uganda, Gray aliomba kufanya kikao pamoja na familia hiyo. Alitumia nafasi hiyo kumweleza bwana John na mkewe pamoja na Jacqueline aliyehudhira kikao hicho juu ya lengo alilokuwa nalo la kutaka kuoa katika familia hiyo. Alikuwa akimhitaji Jacqueline na bila kuficha alieleza kila jambo ikiwa ni pamoja na kipindi cha miaka kadhaa aliyotumia kumfuatilia msichana huyo.

    Wakati huo alieleza adhma yake ya kutaka kusafiri na Jacqueline kuelekea nchini Marekani katika jimbo la Iowa ambako baba yake bwana Abraham alikuwapo. Wazazi wa Jacqueline hawakuwa na kinyongo hata kidogo juu ya Gray, hilo lilifuata baada ya kufurahia msaada alioutoa kijana huyo ikiwa ni pamoja na ahadi aliyoahidi kumsomesha pia mwanao nchini Marekani. Mambo yalikuwa tofauti kwa Jacqueline ambaye hakuwa tayari hata kidogo kuolewa na Gray. Jambo pekee alilolijibu, alidai alihitaji kuwa mpweke baada ya kufiwa na mwanaume aliyeamini alikuwa wa ndoto zake siku zote. Wazazi wake walijaribu kumbadili msimamo wake lakini hawakufanikiwa jambo hilo waliloshirikiana na ndugu zao kadhaa.

    Hatimaye Gray aliamua kuondoka nchini Tanzania akielekea nchini Uganda. Alikuwa ameacha ombi moja kwa Jacqueline na familia yake. Alihitaji msichana huyo amfuate nchini Uganda tayari kwa safari ikiwa angebadili mtazamo wake ndani ya wiki mbili. Wazazi wa Jacqueline waliendeleza ushawishi kwa mtoto wao ili aolewe na Gray. Kila siku iliyoenda walikuwa wakiwaita watu tofauti ili wawasaidie kumbadili msimamo mwanao lakini haikuwa hivyo. Jacqueline hakubadilika alionekana akiwa na msimamo juu ya maamuzi yake. Baada ya wiki moja msimamo wake ulibadilika na ghafla, alionekana kukubaliana na ombi la Gray ambaye alikuwa mtanashati pia. Jambo hilo lilikuwa la faraja kwa familia yake iliyoamini ingeongeza utajiri kupitia ndoa ambayo ingefungwa kati ya Gray na Jacqueline. Akiwa na furaha bwana John alimpigia simu Gray na kumweleza juu ya taarifa za Jacqueline kukubali kuolewa naye. Taarifa ambazo zilionekana kuwa za neema sana kwa Gray.

    Hatimaye baada ya siku tatu msichana huyo alikuwa ndani ya ndege akiwa safarini kuelekea jijini Entebbe nchini Uganda. Alikuwa tayari kuolewa na Gray baada ya David kufariki kama alivyoamini. Mara baada ya kufika katika jiji hilo alipokelewa na mchumba wake mpya kabla ya kuelekea nyumbani kwao. Siku iliyofuata Gray alikuwa akishughulikia safari ya kuelekea nchini Marekani. Alikuwa na furaha juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea huku akiwa ameingiwa na jambo jipya moyoni mwake. Aliwaza kumshawishi baba yake ili afunge harusi na msichana huyo haraka iwezekanavyo. Alikuwa akihisi uwezekano wa David kugundua kuwa mrembo huyo alikuwa hai. Baada ya wiki moja walifanikisha lengo lao na walikuwa safarini wakielekea nchini Marekani ndani ya ndege ya shirika la British Airways.

    * * * *

    Mambo yalizidi kuwa magumu kwa David ambaye hakujua hatma ya maisha yake ilhali akiwa na kidonda moyoni mwake. Bado alikuwa akiumia mara kadhaa juu ya kifo cha Jacqueline. Thamani yake haikuwapo kama awali kwani muda wote alikuwa mchafu na mtu yeyote angegundua kwamba hakuwa sawa. Wakati huo alikuwa akiendelea na kazi yake ya kuuza maji aliyokuwa akiifanya maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam, majira ya jioni alikuwa akirudi Mbagala ambako alikuwa amepanga chumba. Alikuwa hajui hatma ya maisha yake kwa vile hakuwa na msaada ya wowote.



    Baada ya miezi miwili alipata matatizo ya kifua yaliyopelekea aachane na kazi ya kuuza maji. Kwa siku kadhaa alikuwa maeneo aliyopanga huku chakula chake kikiwa mikate na maji. Alikula chakula hicho mara mbili kwa siku kutokana na kiasi kidogo cha fedha alichokuwa nacho.

    Siku moja wakati akiwa amejipumzisha nje ya chumba chake katika nyumba aliyokuwa amepanga alisikia kelele za mtu aliyekuwa akipita eneo hilo. Alijiweka sawa akiwa na lengo la kumsikiliza mtu huyo akiamini alikuwa mlevi kutokana na kelele alizozitoa

    “…. Mimi ni muuaji tena muuaji wa kutisha na rudia tena… Muuaji wa kutisha” Alisikia kelele hizo David kabla ya kujiweka sawa ili asikilize. Aliendelea kuisikia sauti hiyo ya kike na alihisi mtu huyo alikuwa mwehu au alikuwa amelewa.

    “Mimi siyo Mtanzania huku nilikimbilia tu, hiyo yote ni kwa sababu mume wangu alitaka kuniua nchini Uganda…. Nikiwa huko nilishirikiana na mume wangu kumuua mdogo wake bwana Johnson ambaye tulimtegea bomu nyumbani kwake…” Maelezo hayo yalimshtua zaidi David ambaye alianza kutembea haraka kablaya kutoka akikimbia akielekea eneo alilosikia sauti hiyo. “ Tulijaribu kumuua David, mtoto wa bwana Johnson tukishirikiana na mume wangu ili turithi utajiri wake lakini tulishidwa, maovu yangu ni mengi kwani nilimsaliti mchumba wangu miaka mingi iliyopita bwana Otieno Ndakufurila ambaye pia tulimumwagia tindikali tukishirikiana na mume wangu” David alikuwa ameshatoka huku akiwa anamwangalia mama yake mkubwa kama alivyomtambua. Alikuwa mwehu huku akiwa katika mavazi ya ajabu kupindukia, hakuwa mwingine bali mke mkubwa wa bwana Abraham. Akiwa na hasira, David alitulia ili aendelee kusikiliza maelezo yaliyotoa siri za mwanamke huyo na mumewe.

    “Hatukuishia hapo tulihusika na mauaji ya Otieno pamoja na Sabinus ambaye wauaji walikosea na kumuua mwanangu huyo…. Walipaswa wamuue David” Alibaki akimwangalia mwanamke huyo na mwishoe alipandwa na hasira zaidi juu yake. Alimvamia na kuanza kumpiga kwa ngumi na mateke mfululizo. Hasira zilimpanda huku akikumbuka kifo cha familia yake pamoja na ndugu zake wa karibu akiwapo Sabinus pamoja na bwana Otieno Ndakufurila.

    Watu kadhaa waliomshuhudia akifanya tukio hilo lisilo la kibinadamu walimuwahi na kumzuia kumpiga mwanamke huyo.Baada ya dakika kadhaa akiwa ametulia pasipo kueleza chanzo cha kumpiga mwehu huyo aliamua kuondoka na kurudi nyumbani kwake. Alitulia kwa masaa kadhaa na kugundua kuwa hakuwa na sababu ya kumnyanyasa mwanamke huyo ambaye adhabu ya matendo yake alikuwa ameshaanza kuipata. Jambo lililochangia maamuzi yake hayo lilihusiana na jinsi alivyomsikia mwanamke huyo aliyekuwa ameachana na mume wake, bwana Abraham. Zaidi alishtushwa na maelezo ya kuwa baba yake huyo mkubwa alitaka kumuua. David alijaribu kumpeleleza mwanamke huyo kabla ya kuelezwa kuwa alikuwapo nchini Tanzania kwa muda wa miaka kadhaa akiwa mwehu hivyo hivyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    David alijijengea tabia ya kumfuatilia na mwishoe alipata kisa kingine baada ya kugundua kuwa mwanamke huyo alinusurika kuuawa baada ya kupata msaada kutoka kwa mhalifu Killa Jose aliyeamriwa kumuua na mume wake. Baada ya siku kadhaa akiwa amepona alirudi tena maeneo ya Magomeni na kuendelea na shughuli yake ya kuuza maji. Wakati huo biashara yake ilikuwa ngumu sana na alimfanya akate tamaa ya kuendelea na mihangaiko ya maisha yake. Walikuwapo askari wa jiji ambao walikuwa wakizuia biashara ndogondogo zilizokuwa zikifanyika maeneo tofauti ya jiji. Jambo hilo lilisababisha akamatwe na askari hao mara kadhaa na usalama wake ulikuwa ni kuwapa fedha zote alizokuwa nazo.

    David alichanganyikiwa zaidi kila alipokumbuka kuwa ilimpasa arudi nchini Uganda kulipa kisasi kwa baba yake mkubwa ambaye wakati huo alikuwa amekamisha hisia zake baada ya kugundua kuwa ndiye aliyekuwa muuaji wa familia yake. Kila mara alipomfikiria baba yake huyo alipandwa na hasira ambazo zilitokana pia na ugumu wa maisha aliyokuwa nayo akiwa analala bila kula mara kadhaa. Siku moja nyakati za mchana alikuwapo maeneo ya Magomeni akiendelea na shughuli yake ya kuuza maji. Akiwa sambamba na wenzie waliokuwa wakiuza maji, kichwani alikuwa na mawazo tele. Alikuwa akiwaza juu ya mambo kadhaa aliyopitia katika maisha yake na wakati huo jinsi alivyokuwa hata watu kadhaa waliokuwa kwenye magari walimwita wakihitaji maji pasipo mafanikio, alikuwa kwenye mwingi wa mawazo.

    Akiwa katika dimbwi la mawazo hayo walionekana askari wa jiji wakijongea katika eneo hilo alilokuwa na wenzie waliouza vitu tofauti. Wenzie walifanikiwa kuwaona askari hao kabla ya kuanza kukimbia. Wakati zoezi hilo likiendelea mmoja wao alimwita David ambaye alikuwa bado katika dimbwi la mawazo na hakutii hatari aliyoelezwa na mwenzie kwa vile akili yake ilikuwa mbali kimawazo. Hatimaye askari hao waliokuwa wakiwafukuzia walifika eneo hilo kabla ya kumkamata David na kumvutia kando kidogo ya barabara walianza kumpiga kwa mateke pamoja na virungu kila sehemu ya mwili wake. Alijaribu kujitoa katika karaha hiyo lakini hakufanikiwa kutokana na idadi ya askari hao waliokuwa watano. Aliamua kujikinga kichwa chake kwa mikono ilhali askari hao wakiwa bado wanaendelea kumpiga, alilia kwa uchungu lakini hawakujali zaidi ya kuendeleza zoezi lao.

    Baada ya dakika kadhaa alipoteza fahamu huku akiwa amezungukwa na kiasi kikubwa cha damu, alikuwa amesukumwa na askari hao katika mfereji uliokuwa kando ya barabara hiyo. Askari hao walikuwa wameondoka na maji aliyokuwa akiyauza pamoja na fedha zote alizokuwa nazo. Wakati huo kwa uoga wauzaji maji na wenzie kadhaa walionekana wakijongea katika eneo hilo la mfereji kwa tahadhari kubwa. Mara baada ya kumfikia walimwagia maji baada ya kugundua kuwa alikuwa amezimia. Baada ya dakika kadhaa David alirudiwa na fahamu lakini alikuwa akilia kwa uchungu juu ya kila jambo lililokuwa limetokea baada ya kupigwa. Sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa na majeraha ambayo yalimkatisha tamaa kwa vile hakuwa na fedha hata kidogo.

    Wenzake hao walimsaidia kumpeleka katika chumba alichokuwa amepanga maeneo ya Mbagala. Hawakuwa na fedha za kumpeleka hospitali na David aliwaomba wamrudishe Mbagala alikokuwa akiishi. Akiwa katika chumba chake muda wote, alikuwa akiishi kwa msaada alioupata toka kwa wapangaji wenzie ambao pia walimnunulia dawa kadhaa ili atumie katika majeraha aliyokuwa nayo. Alikuwa amekata tamaa na muda wote alikuwa akisikiliza redio yake ndogo ambayo ndiyo ilikuwa kama mtu wake wa karibu. Ndoto za kutafuta fedha ili arudi nchini Uganda zilikuwa zimepotea na alikuwa akiumia kila siku alipokifikiria kifo cha mchumba wake Jacqueline. Siku moja wakati akiendelea kusikiliza redio ya shirika la utangazaji la Tanzania, alisikia tangazo aliloamini lingebadili maisha yake na mwishoe kwenda kulipiza kisasi kwa bwana Abraham. Tangazo hilo lilimfanya aanze kukimbia nje ya nyumba hiyo aliyopanga akiwa na gongo lililomsaidia mguu wake wa kushoto uliokuwa mbovu baada ya kupigwa na askari. Unyonge aliokuwa nao ulipotea huku akionekana akiwa amepata uhakika wa maisha yake ghafla. Jambo hilo liliwashangaza wapangaji wenzie kwani kwa muda wa miezi kadhaa hawakufanikiwa kumwona David akiwa na furaha aliyokuwa nayo. Wakati huo alikuwa akiwaomba wapangaji wenzie simu, alionekana kama alikuwa akihitaji kufanya jambo.

    * * * *

    James Natalie Brown halikuwa jina geni kwa raia wa Marekani hususani wale ambao walikuwa wafuatiliaji wa riwaya katika magazeti mbalimbali ya nchini humo. Alikuwa mtunzi mahiri wa riwaya katika vitabu pia ambavyo vilikuwa vikiuza nakala nyingi nchini humo. Umaarufu wake uliendana na mafanikio kwani alikuwa na kampuni kadhaa ikiwapo iliyojishughulisha na uandaaji wa filamu pamoja na ile iliyohusika na uchapishaji wa vitabu. Historia ya James ilikuwa kivutio pia nchini humo ambayo aliiandikia kitabu kilichoitwa `Sometimes Life` kilichouza nakala nyingi pia nchini humo. Alikuwa na asili ya kiafrika akitokea nchini Uganda, miaka kadhaa iliyopita, alikuwa mtoto wa mitaani katika eneo la Kiriri nchini Uganda. Mafanikio yake yalitokana na msaada mkubwa alioupata kutoka kwa Natalie Brown aliyekuwa mrembo wa jimbo la Carifonia miaka kadhaa iliyokuwa imepita pia.

    Kutokana na msaada huo wa kusomeshwa mpaka kufikia mafanikio aliyokuwa nayo, aliamua atumie jina la James Natalie Brown akimshukuru mrembo huyo ambaye wakati huo alikuwa ameolewa nchini humo. Jambo ambalo James alikuwa halisahau siku zote, alikuwa akimkumbuka David ambaye walikuwa wote enzi za utoto wao katika eneo la Kiriri wakiwa watoto wa mitaani. Hakumsahau jinsi mwenzie huyo alivyokamatwa na askari wakati ambao alipaswa asaidiwe pia na Natalie Brown. Mpaka wakati huo hakujua kama David alikuwa hai au la! Alikuwa na shauku juu ya rafiki yake huyo kwa vile aliyajua maisha yake ya awali akiwa amenyan`ganywa mali na baba yake mkubwa bwana Abraham. Kuhakikisha upendo wake kwa David pamoja na bara la Afrika James aliwaza kufanya jambo. Alipanga kutumia muda wake wa mapumziko ya mwisho wa mwaka akiwa nchini Uganda na huko alihitaji kutunga riwaya inayohusu mambo tofauti yanayotokea Afrika na alitarajia kuiita riwaya hiyo kwa jina la ‘Afrikanaz’. Mbali na riwaya hiyo ambayo mauzo yake alihitaji yatumike kusaidia Afrika ambako aliamini ndiyo kwao, alihitaji pia kumtafuta David ili amsaidie kama alikuwa bado hai. Hilo ndilo alilolifanya, mwishoni mwa mwaka alisafiri mpaka nchini Uganda na kufikia katika jiji la Entebbe. Baada ya mapumziko ya wiki moja alianza kuandika riwaya yake ya `Afrikanaz`ambayo alitumia mazingira ya Afrika Mashariki, mbali na zoezi hilo alilokuwa akilifanya alitoa matangazo ya kumtafuta David katika vituo tofauti vya redio na televisheni. Alikuwa akiamini kama David alikuwa hai nchini humo angempata, zoezi hilo lilichukua hatua katika vituo vya habari kwa muda wa wiki moja pasipo mafanikio.

    Mshauri wake wa karibu aliyekuwa naye pamoja na wengine kadhaa waliokuwapo nchini Marekani walimshauri ajaribu matangazo hayo katika nchi nyingine pia mbali na Uganda. James alitekeleza ushauri huo kwani alilipia matangazo hayo ambayo ujumbe wake ulikuwa ni kumtafuta David Johnson. Matangazo hayo yaliwakilishwa katika vituo vyote vya habari nchini Kenya pamoja na Tanzania lakini pia yalipelekwa Burundi na Rwanda. Kuhakikisha David anapatikana, James alilipia matangazo hayo mpaka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mawazo ya James yalifanikiwa kwani baada ya wiki mbili alipigiwa simu na David aliyemwambia alikuwapo nchini Tanzania. Akiwa na furaha ilhali haamini kama kweli David alikuwa hai, alisafiri kutoka Uganda kuja nchini Tanzania kwa lengo moja la kumsaidia David. Ndoto zake zilitimia kwani alifanikiwa kumwona David ingawaje alilkuwa katika hali mbaya sana kiafya na kimaisha kwa ujumla. Akiwa na uchungu alikuwa na wazo moja tu la kumsaidia rafiki yake huyo wa miaka mingi iliyokuwa imepita. Alihitaji kuhakikisha anaupata utajiri wake ulionyan`ganywa na baba yake mkubwa bwana Abraham.

    Aliamini kila jambo lilikuwa likiwezekana kutokana uwezo mkubwa wa kifedha aliokuwa nao. Akiwa nchini Tanzania alifanikiwa kumwona pia mkewe bwana Abraham ambaye alikuwa mwehu, hakuwa na muda wa kupoteza kwani alianza kutafuta hati ya kusafiria ya David na baada ya wiki moja waliipata kabla ya kusafiri kuelekea nchini Uganda. Huko wakati James akiendelea na uandishi wa riwaya yake ya `Afrikanaz`, David alikuwa akimpeleleza bwana Abraham kabla ya kugundua kuwa alihamia nchini Marekani. Alitoa taarifa hizo kwa rafiki yake James ambaye alihitaji wasafiri wote kuelekea nchini Marekani na lengo lilikuwa moja tu, kwenda kuufuata utajiri wa David. Wakati wakiwa katika maadalizi safari hiyo James aliwaza jambo na kuona lingekuwa la msingi sana. Alihitaji mkewe bwana Abraham ambaye alikuwa mwehu apelekwe nchini Marekani pia. Aliamini mwanamke huyo angetoa mchango katika kuzipata mali za David. Kukamilisha jambo hilo aliwatafuta watu aliowatuma nchini Tanzania kumchukua mwanamke huyo aliyekuwa mwehu, zoezi ambalo hilo lilichukua nafasi.





    Hatimaye safari yao ilikamilika na siku ya Januari pili walikuwapo ndani ya ndege ya shirika la British Airways wakielekea nchini Marekani. Furaha ya James iliongezeka zaidi baada ya kuambiwa na vijana wake kuwa mkewe bwana Abraham aliyekuwa mwehu tayari alikuwa chini yao na walitarajia kusafiri siku iliyofuata kuelekea nchini Marekani pia wakitokea Tanzania. Muda wote David akiwa katika ndege hiyo alikuwa na furaha huku akihisi mwanzo wa maisha mazuri ulikuwa umekaribia. Alikuwa ameshapata matibabu huku akiwa katika mwonekano wake wa kuvutia mbali na makovu ya majereha kadhaa yaliyoonekana sehemu tofauti za mwili wake. Alikuwa amevaa suti yenye rangi nyeusi iliyokuwa ya ghali na alionekana akianza kusahau karaha alizozipata akiwa Magomeni kama muuza maji pamoja na makazi yake duni aliyokuwa akiishi maeneo ya Mbagala.

    * * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gray alikuwapo katika jimbo la Iowa nchini Marekani na Jacqueline, walikuwa katika maandalizi ya harusi yao waliyopanga kuifunga katika jimbo hilo. Maandalizi hayo yalifuata baada ya ombi la Gray kwa baba yake akiwa na hofu ya kumkosa msichana huyo katika maisha yake. Harusi hiyo ilipangwa kufungwa katika kitongoji cha Des Moines kilichopo kusini mwa jimbo hilo. Harusi yao ilikuwa imebakiwa na wiki tatu huku baba yake akiwa na furaha juu ya hatua hiyo aliyoifikia mwanaye Gray. Bwana Abraham bado alikuwa mvaaji wa miwani ambayo ilizuia watu kuona jicho lake la kushoto lililokuwa bovu zaidi hakuwa na hofu hata kidogo. Alikuwa akiamini kuwa David alishakufa miaka mingi iliyokuwa imepita na alipanga kumfanyia mtoto wake harusi ya kifahari kutokana na uwezo wa kifedha aliokuwa nao wa kufanya jambo lolote. Akiwa hana furaha, Jacqueline moyoni alikuwa akiumia juu ya uamuzi wake ambao kwa kiasi kikubwa ulisababishwa na wazazi wake. Hakuwa na jambo la kufanya zaidi ya kukubali kuolewa na Gray ambaye alimvutia lakini haikuwa kama alivyovutiwa na kumpenda David awali, mwanaume aliyemuwaza kila siku.

    Wakati maandalizi yao yakiendelea, James na David nao walikuwepo katika jimbo la Iowa wakifuatilia nyendo zao. Ni wakati ambao David alipata mshtuko wa moyo ambao aliamini hakuwahi kuupata katika maisha yake, aligundua mrembo na mwanamke wa ndoto zake alikuwa hai. Hakuwa mwingine bali ni Jacqueline, alitaka amfuate mwanamke huyo lakini alizuiwa na James aliyeandaa kila jambo la kuhakikisha mali za David zinapatikana. Wakati huo mkewe bwana Abraham wa miaka kadhaa iliyokuwa imepita, aliyekuwa mwehu alikuwa katika hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital iliyokuwa maalum kwa walemavu wa akili katika mji wa Urbandale wa jimbo hilo la Iowa. Mji ambao haukuwa mbali na kitongoji cha Des Moines ambacho Gray na Jacqueline walitarajia kufunga harusi. James alipanga zoezi zima juu ya kuzipata mali za David na wakati huo tayari askari wa jimbo hilo la Iowa walikuwa wamepewa kisa kizima cha maisha ya David na waliahidi kutoa msaada kwa kijana huyo.

    David alikuwa amegundua mchezo aliofanyiwa na Gray ambaye alikumbuka kuwa aliwahi kukutana naye nchini Tanzania katika benki ya kibiashara iliyokuwapo maeneo ya Kariakoo. Kwa uelevu wake aligundua kuwa kijana huyo aliandaa zoezi zima la kutoa taarifa za uongo juu ya kifo cha Jacqueline na aliamini alifanya hivyo kwa mchumba wake pia. Aliamini lazima kijana huyo alimweleza Jacqueline kuwa hata yeye David alikuwa amekufa. Wakati huo James alipanga ukweli juu ya kila jambo ufahamike katika siku ya harusi ya Gray na Jacqueline na askari walikubali kutoa msaada katika zoezi hilo. Mpango huo wa James ulionekana kuwa kama tukio la filamu au tukio la aina ya riwaya nyingi alizokuwa ameandika. Hatimaye zilibakia siku tatu ili harusi kati ya Gray na Jacqueline ifungwe.

    Wakati huo Gray alikuwa katika hoteli ya kifahari ya Iowa City Hotel iliyokuwapo karibu na kitongoji cha Des Moines akisubiri harusi yake. Jacqueline naye alikuwapo katika hoteli mojaya kitongoji cha Indianola akisubiri harusi hiyo pia. Hoteli hizo walizokuwapo tayari zilikuwa zimetambulika kwa James na David waliokuwa wakiwafuatilia kwa kila jambo walilokuwa wakilifanya.

    Hatimaye siku ya harusi ilifika ikiwa ni Jumamosi ya kwanza ya mwezi Febeuari, majira ya saa tatu asubuhi magari saba ya polisi yalionekana yakiwa nje ya hoteli ya Iowa City Hotel. Ndani ya gari moja la polisi alikuwapo David aliyekuwa amevaa suti nadhifu kama vile alikuwa akienda kufunga harusi siku hiyo. Pembeni yake alikuwa amekaa James aliyekuwa ametulia pasipo hofu akiwa na mavazi kama ya David. Gari moja wapo pia alikuwepo mkewe mkubwa wabwana Abraham aliyekuwa mwehu huku akionekana kuchekacheka muda wote.

    Wakati huo ulikuwa ni mwanzo wa kuzifuatilia mali za David kwa muuaji, bwana Abraham na walitarajia kuona tajiri huyo akifikishwa kizimbani kujibu mashtaka yake. Hatimaye yalionekana magari manne ya kifahari yakiingia katika hoteli hiyo ili kumchukua Gray kuelekea katika kanisa la kikistro lililokuwapo katika kitongoji cha Des Moines tayari kwa misa ya harusi. David akiwa na askari hao pamoja na James walitulia katika magari yao pasipo kufanya jambo lolote. Baada ya dakika kumi magari hayo yalianza kutoka katika hoteli hiyo ikiwa ni baada ya kumchukua Gray aliyekuwa bwana harusi.

    Magari hayo wakati yakiendelea kujongea katika geti kuu ili kuelekea katika kanisa husika kwa ajili ya harusi hiyo, askari hao walishuka kwenye magari kabla ya kuyazuia magari hayo ya msafara wa harusi. Askari hao walimuamuru Gray ashuke na mpambe wake kwenye gari walilokuwapo, jambo walilolitekeleza na mara baada ya kushuka Gray alifungwa pingu na askari hao. Alionekana kama amechanganyikiwa ghafla kutokana na tukio hilo huku akianza kutokwa na machozi. Wakati akiwa katika mshtuko huo wa majonzi alilishuhudia gari jingine la polisi likifunguliwa mlango kabla ya kushuka kwa David akiwa na mpambe wake James. Wakiwa wanatabasamu waliongoza mpaka katika gari aliloshushwa Gray na mpambe wake kabla ya kuingia. Wakati huo Gray aliishiwa nguvu kabisa kabla ya kuanguka chini huku akiwa ametoa macho, alikuwa haamini kila jambo lililokuwa likiendelea. Askari walimvuta wakimburuza kabla ya kumpakia katika gari moja la polisi lililoondoka naye kuelekea kituo cha polisi.

    Kiongozi aliyekuwa akiwaongoza askari hao aliamuru magari hayo ya harusi yawashwe na safari ianze kuelekea katika kanisa husika la kitongoji hicho cha Des Moines ambako harusi ya Gray ilipaswa ifugwe. Baada ya kutangulia kwa magari hayo ya harusi yalifuata magari sita ya polisi mbali na lile lililokuwa limempeleka Gray kituo cha polisi. Mpambe wa Gray aliyekuwa raia wa Marekani, alibaki katika geti la hoteli hiyo akishangaa shangaa. Hakuelewa jambo lililokuwa likiendelea. Baada ya dakika arobaini na tano walifika katika kanisa moja la kikistro lililopo katika kitongoji hicho cha Des Moines ambako tayari watu walikuwa wamefurika, bibi harusi pia alikuwa ameshafika huku akisubiliwa bwana harusi. Askari wawili wawili wakitembea ndiyo walioongoza msafara huo lengo lao lilikuwa kumficha David na James waliokuwa wakifuata nyuma. Walitangulia askari zaidi ya kumi na nne wakiwa wawili wawili ilhali wakiwa na bunduki zao mabegani jambo lililotoa picha tofauti ya harusi hiyo ambayo haikuwahi kutokea katika kanisa hilo. Mwishoni alifuata David akiwa na James na nyuma yao kabisa alikuwepo mkewe bwana Abraham wa miaka mingi iliyopita aliyekuwa mwehu, alikuwa ameshikwa mkono na askari mmoja huku akiendelea kucheka cheka.

    Jacqueline akiwa mbele ya kanisa pamoja na wazazi wake sambamba na bwana Abraham na mkewe mdogo, Aminata walishtushwa na sura ya harusi hiyo na walibaki wametoa macho ili kushuhudia jambo ambalo lingetokea. Askari walipofika eneo la mbele la kanisa hilo walitembea kueleka upande wa kushoto ilhali wengine walitembea kuekea upande wa kulia. Hatimaye ulifika wakati uliokuwa wa maajabu kwani sura za David na James zilionekana vizuri mbele yao. Jacqueline alionekana akiwa kama hajielewi vizuri, ghafla alipata nguvu za miguuni kabla ya kukimbia kwa kasi na kumvamia David aliyemkumbatia kwa nguvu. Walibaki wamekumbatiana huku Jacqueline akiwa amemtolea macho David kabla ya kupoteza fahamu akiwa mikononi mwa David. Askari kadhaa walimchukua Jacqueline kutoka mikononi mwa David na kuanza kuelekea nje ya eneo hilo la kanisa. Watu wote walikuwa wamesimama huku wakiwa hawajui jambo lililokuwa likiendelea.

    Bwana Abraham aliyesimama pembeni ya mkewe mdogo, Aminata, alikuwa amezilazimisha kope zake hata za jicho lake bovu akiwa haamini kuwa mtu aliyekuwa mbele yake ni David. Alikuwa akitetemeka kupindukia kwani alikuwa ameigundua sura ya David vizuri na zaidi sura ya mkewe mkubwa aliyeamini alikuwa amekufa. Mkewe huyo mkubwa wakati huo alikuwa akiwaangalia askari waliokuwa wakitoka na Jacqueline na alionekana akichekacheka kama kawaida yake. Wazazi wa Jacqueline pia walikuwa wametoa macho wakiwa hawaelewi jambo lolote lililokuwa likiendelea. Kanisa lilikuwa na utulivu huku watu wakitazamana zaidi David aliyemkazia macho baba yake mkubwa bwana Abraham!





    Utulivu ndiyo uliokuwa umetawala ndani ya kanisa lililokuwa likitarajiwa kufungwa harusi ya Gray na msichana mrembo Jacqueline. Taswira ya harusi hiyo ilikuwa imebadilika kwa muda wa dakika kadhaa baada ya askari zaidi ya kumi na nane kuingia kanisani wakiwa na bunduki zao mikononi, zaidi bwana harusi mtarajiwa hakuwapo kanisani hapo zaidi ya vijana wawili waliofika ambao hawakutambulika na idadi kubwa ya watu waliotarajia kushiriki ibada hiyo. Mwanamke mmoja mwehu aliyekuwapo kanisani hapo aliwachanganya zaidi watu waliojumuika katika misa hiyo akiwamo mchungaji aliyesimama madhabahuni ambaye alikuwa tayari kwa kuongoza misa.

    Kwa mtu ambaye aliweza kuwasogelea kwa ukaribu vijana wawili watanashati ambao walifika kama bwana harusi na mpambe wake angeweza kuwatambua majina yao. Suti zao zilikuwa na lebo ya majina yao kwenye mfuko wa koti la suti, mmoja wao suti yake iliandikwa James na mwingine ilisomeka kama David, kijana ambaye alikuwa amemtolea macho mwanaume aliyekuwa akitetemeka kupindukia mbele yao, ambaye pia alikuwa amevaa miwani iliyozuia mtu kuona jicho lake bovu. Mwanaume huyo ambaye si mwingine zaidi ya bwana Abraham alikuwa amesimama karibu na mkewe mdogo, Aminata.

    Mwanamke aliyeonekana kuwa mwehu hakuwa mwingine zaidi ya mkewe mkubwa wa bwana Abraham wa miaka kadhaa iliyopita aliyekuwa mwehu. Alikuwa akizungusha macho yake kila upande wa kanisa hilo kabla ya kuvunja ukimya mara baada ya kumwona bwana Abraham. Alimnyooshea kidole kwa haraka kabla ya kusikika kwa sauti, “Catch him! He’s a killer…, dangerous killer, catch him!” (“Mkamateni! Ni muuaji…. Muuaji hatari, mkamateni”) Alisikika mkewe mkubwa wa Abraham huku akiirudia sentensi hiyo. Alionekana akijificha mgongoni mwa askari mmoja wapo, akiashiria kumwogopa bwana Abraham. Watu waliokuwapo kanisani hapo walipatwa na mshangao juu ya kelele za mwanamke huyo na zaidi bwana Abraham alionekana kuchanganyikiwa ghafla. Kiongozi wa askari hao alimsogelea bwana Abraham ambaye jicho lake la kulia lilikuwa likitokwa na machozi kabla ya kusikika. “Is that true you’re the killer?” (“Ni kweli wewe ni muuaji?”) Aliuliza askari swali ambalo ilichukua sekunde kadhaa kabla ya bwana Abraham kukubali kwa kutikisa kichwa, alionekaa kama alikuwa amekumbuka mambo mengi kichwani mwake kwa muda mfupi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alivuta pumzi ndefu kabla ya kusikika, “No, I am not a killer, this woman might be crazy” (“Hapana, mimi siyo muuaji, huyu mwanamke atakuwa mwehu”). Askari hao walionekana wakitazamana kabla ya mmoja wao kusikika. “Okay whatever, I know in America you’re innocent until proved guilty, so from now onward you will be under arrested for the murder case of Johnson’s family and several other people, you will prove your sinless in a court” (“Sawa na ninajua kuwa nchini Marekani huna hatia mpaka hapo utakapo thibitika kuwa mtuhumiwa, kwa hali hiyo kuanzia sasa uko chini ya ulinzi kwa shtaka la mauaji ya familia ya Johnson na watu wengine rukuki, utathibitisha kama huna hatia mahakamani”)

    Askari huyo alionekana akiwakonyeza wenzie ambao bila kuchelewa walimfunga pingu bwana Abraham kabla ya kuanza kuondoka naye eneo hilo la kanisani. Watu waliokuwapo kanisani walionekana kuchanganyikiwa zaidi juu ya tukio hilo. Baada ya askari hao kuongoza nje na mtuhumiwa bwana Abraham, James, David wakiwa na mkewe mkubwa bwana Abraham walifuata, mwanamke huyo alikuwa akiendelea kucheka cheka. Mkewe mdogo bwana Abraham aliishiwa nguvu na kujikuta akikaa chini huku akilia, mama na baba yake Jacqueline waliokuwa mbele kanisani hapo walionekana wakimtuliza.

    Mara baada ya kutoka nje bwana Abraham alipakizwa kwenye gari akiwa chini ya ulinzi mkali na safari ilianza kuelekea katika kituo cha polisi kilichopo katika mji wa Altoona pembeni kidogo ya kitongoji hicho cha Des Moines ambako pia Gray alikuwa amepelekwa. Kabla ya askari hao kuondoka wakiwa na mtuhumiwa huyo walionekana wakiongea jambo na David aliyekuwa na James. Hatimaye askari hao waliondoka wakiwa na mtuhumiwa huyo.

    Wakati huo kulikuwa na magari mawili ya kifahari ya James yaliyofika kanisani hapo, hawakutumia magari waliyofika nayo awali wakitokea katika hoteli ya Iowa city hotel, James alionekana akiongea na vijana wake ambao walimwongoza mkewe mkubwa wa bwana Abraham ambaye aliingia ndani ya gari mojawapo aina ya Ferrari na safari ilianza wakiwa wameelezwa wampeleke mwanamke huyo katika hospitali ya walemavu wa akili ya St. Joseph Lunacy Hospital iliyokuwapo katika mji wa Urbandale ambayo alifikia toka awali akitokea Tanzania. James na David pia waliingia kwenye gari jingine aina ya Ferrari na walionekana wakiwa na nyuso za furaha, hawakujali umati wa watu wengi uliokuwapo nje ya kanisa hilo, umati uliokuwa wa raia wengi watokao Afrika Mashariki walijitokeza kusindikiza harusi hiyo iliyokuwa imeota mbawa.

    Gari lao liliwashwa na dereva wake James na safari ilianza kuelekea katika hoteli ya Des Moines Motel ambayo walikuwapo kwa wiki kadhaa, wakati huo David alirudiwa na kumbukumbu za kumwona Jacqueline akiwa hai kwa macho yake, tabasamu pana lilionekana usoni mwake. Alionekana akiwa tayari kwa kumwambia James jambo lakini simu ya rafiki yake huyo iliita na alishindwa kuongea jambo hilo. James aliipokea. “Yeah! …. Of course, my brother would like to see her …. Is she at Central Hospital of Des Moines?… Okay we drive back” (“Ndio …. Kaka yangu angependa kumwona … yupo katika hospitali ya Central Hospital of Des Moines?... sawa tunarudi”) Alisikika akiongea James na mmoja wa askari ambaye aliondoka na Jacqueline kanisani, ambaye alimweleza hospitali ambayo mrembo huyo alikuwapo.

    James alimweleza dereva wa gari hilo aligeuze na safari ianze kuelekea katika hospitali ya Central Hospital of Des Moines ambayo haikuwa mbali na eneo walilokuwapo. David alielezwa pia jambo lililofuata lilikuwa ni kwenda kumwona Jacqueline. Alitabasamu kupindukia na alielezea hisia zake za furaha aliyokuwa nayo na zaidi msaada ya hali na mali aliokuwa amepewa na rafiki yake huyo James. Wakati huo David alikuwa akitamani wafike haraka katika hospitali hiyo ili aweze kukamilisha furaha yake. Baada ya nusu saa walikuwa wamefika katika hospitali hiyo ya Central Hospital of Des Moines, bila kuchelewa waliongozwa na muuguzi mmoja kuelekea katika chumba maalum ambacho Jacqueline alikuwa amelazwa na wakati huo hali yake walielezwa ilikuwa shwari.

    Walitembea kwa haraka kuelekea katika chumba hicho kilichokuwapo katika ghorofa ya kwanza ya hospitali hiyo hatimaye waliingia katika chumba hicho. Walimwona Jacqueline akiwa amekaa katika kitanda chake huku akiwa na furaha. Jacqueline alitabasamu zaidi alipomwona David aliyeongozana na James, alishuka haraka kutoka kwenye kitanda chake na kwenda kumkumbatia kwa nguvu David, walibaki wamekumbatiana kwa dakika moja kabla ya kuachana, wote walikuwa wakitokwa na machozi ya furaha pasipo kujitambua. Huo ndio ulikuwa wakati ambao David alimtambulisha Jacqueline kwa rafiki yake wa siku nyingi James Natalie Brown.

    Furaha ilitawala kati yao na walionekana wakiongea mambo mengi yaliojiri baina yao, baada ya nusu saa Jacqueline alikuwa ameutambua ukweli wa mchezo waliokuwa wamefanyiwa na Gray Abraham, binamu yake David ambaye alikuwa akimpenda Jacqueline pia. Kwa muda mfupi aliyajua mengi na mengine ambayo hakuyatambua awali, hata bwana Abraham aliyekuwa akiamini kuwa ni mtu mwema alimchukia pia ghafla. Baada ya saa tatu waliruhusiwa kuondoka na Jacqueline ambaye hakuwa tayari kulala katika hospitali hiyo. Safari yao ilianza wakielekea katika hoteli ya Des Moines Motel. Iliwachukua saa mbili kuwapo barabarani na mwishoe walifika katika hoteli hiyo ya kifahari, James aliongoza mpaka kwenye chumba chake. David naye aliongoza na Jacqueline katika chumba chake pia kati ya viwili vilivyokuwa vimeongozana. Ni wakati ambao David na Jacqueline waliongea mengi na walifahamiana zaidi, ni wakati uliokuwa wa kumbukumbu zaidi katika maisha yao. Mpaka siku mpya ya Jumapili ya kwanza ya mwezi huo wa Februari inafika, hakukuwa na jambo lililokuwa jipya sana baina yao.

    Jumapili hii ni siku ambayo Jacqueline na David wakiwa na James waliungana pamoja na kwenda kushiriki misa katika kanisa moja la kikistro katika jimbo hilo. Jioni yake ilikuwa nzuri zaidi kwani mrembo Zena Msumi akitokea jimbo la New York akiwa mwanamitindo maarufu kiasi chake, aliungana nao. Mrembo huyo aliyekuwa na asili ya Tanzania alikuwapo nchini Marekani kwa miaka kadhaa. Huyu ndiye mrembo aliyemvutia zaidi James na kuahidi kumuoa siku moja. Kulikuwa na utani baina yake James na marafiki zake kadhaa ambao siku zote walikuwa wakiamini alimpenda mrembo huyo kwa vile alikuwa na asili ya Afrika Mashariki, alikataa juu ya jambo hilo lakini kwa kiasi kikubwa huo ndiyo ulikuwa ukweli. James alijisikia vizuri zaidi kuwa na Zena, mwanamke wa ndoto zake. Warifurahi pamoja usiku huo huku wakiongelea mambo tofauti tofauti, maisha yalionekana kuwa sawa kwao wote wakati huo.

    Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ambayo kesi za Gray na ya baba yake bwana Abraham zilitarajiwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza. Kesiya Gray haikuwa ngumu, ilitarajiwa kutolewa hukumu siku hiyo hiyo kwa vile kulikuwa na kila uwezekano wa kesi hiyo kuweza kukamilika. Kesi ya bwana Abraham haikuwa na uwezekano huo kwa vile ilihitaji upelelezi wa kutosha kabla ya kufikia maamuzi yake. Ni kesi iliyohitaji ushahidi wa kutosha na ushirikiano wa jeshi la polisi la nchini Marekani na lile la Uganda ili kukamilika kwa vile bwana Abraham alishakuwa raia halali wa Marekani. Kama hatia ingethibitika juu yake, bila shaka shtaka la kifo lingeweza kuwa juu yake kwa vile hakukuwa na mabadiliko katika sheria ya nchi hiyo juu ya muuaji, sheria iliyokuwa ikipingwa na wanaharakati kadhaa wa haki za binadamu.

    Mara baada ya kuamka kwa James na David wakiwa na wachumba wao safari ya kwanza ilikuwa ni kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Des Moines International Airport uliokuwapo katika kitongoji hicho. Huko walikuwa wakimsindikiza Zena aliyekuwa akitakiwa kurudi jijini New York ili kuendelea na shughuli zake za uanamitindo. Mrembo huyo alikuwa na furaha baada ya kuwa mchumba wake na gwiji wa uandishi wa riwaya nchini humo kijana James kwa saa kadhaa. Hatimaye walifika katika uwanja huo wa ndege wa kimataifa na Zena aliondoka kama ilivyokuwa imepangwa. Safari ilianza tena, kwa sasa walikuwa wakielekea katika mahakama kuu ya kitongoji hicho cha Des Moines ambako muda wa saa mbili ulikuwa umesalia ili kesi ya Gray ianze kusikilizwa, hawakuwa na shaka kwani mahakama hiyo haikuwa mbali na uwanja huo wa ndege, ikawa hivyo.

    Baada ya saa mbili walikuwapo mahakamani hapo katika chumba husika ambacho kesi ya Gray ilitarajiwa kusikilizwa. Ndani ya chumba hicho walionekana wazazi wa Jacqueline wakiwa watulivu lakini pia alionekana mkewe mdogo bwana Abraham, Aminata aliyekuwa amechukia muda wote. Mbali na watu hao pia walikuwapo watu kadhaa waliokuwa na asili ya Afrika bila shaka walikuwa waafrika waishio nchini humo. Hatimaye Gray alipandishwa kizimbani huku akionekana kuwa mnyonge sana, tayari mama yake alikuwa amemwajiri wakili ambaye alipaswa kumtetea katika kesi hiyo. Ni wakati ambao mama yake Gray, Aminata alionekana akifuta machozi yaliyomtoka pasipo kujitambua. Shtaka la Gray lilikuwa fupi tu, alishtakiwa kwa kosa la kutoa maelezo ya vifo vya watu wawili tofauti ambao ni David na Jacqueline na hatimaye kutaka kufunga ndoa na Jacqueline ambaye alimdanganya kuwa David amekufa, kesi iliyotafsiriwa kama ya kunyang’anya mke mtarajiwa wa mtu. Akiwakilishwa na wakili wake, Gray alikubaliana na mashtaka hayo huku wakili wake akiomba msaada wa mteja wake kusamehewa kwa kosa hilo lililoelezwa kuwa ni la kwanza kwake. Wakili alielezea umuhimu wa kijana huyo ambaye alikuwa akitegemewa na mama yake kwa wakati huo baada ya baba yake pia kuwa mikononi mwa polisi kwa shtaka la mauaji.

    Tofauti na imani za watu hao wachache waliokuwapo mahakamani hapo walioamini hukumu ndogo ingetolewa na hakimu mwanamke aliyeonekana kutojipenda¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬ kwa kuwa rafu rafu, mwanamke huyo alimhukumu Gray kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela, hakuruhusu kiasi chochote cha faini kulipwa badala ya kifungo hicho zaidi aligonga nyundo kuashiria kesi hiyo ilikuwa imekamilishwa. Askari walimfuata kizimbani Gray ambaye alikuwa akilia pia wakati huo na kuanza kumtoa mahakamani hapo kabla ya kuongozwa mpaka katika basi la gereza la Spring Hill, gereza lililokuwapo kusini mwa jimbo hilo la Iowa. Mkewe mdogo wa bwana Abraham, alionekana akiwa amechanganyikiwa zaidi juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea. Hatimaye Gray akiwa na wafungwa wengine waliondoka mahakamani hapo na basi hilo na safari ilianza wakielekea katika gereza hilo la Spring Hill.

    Baada ya saa moja wakati wakiwa wanasubiria kesi ya bwana Abraham, Jacqueline alionekana akiwa mnyonge kiasi huku akiwa amesimama kando ya David aliyemkumbatia, wazazi wake walikuwa karibu pia huku wakiwa wameutambua kiasi ukweli wa kila jambo lililokuwa limetokea. James alionekana akiwa na furaha juu ya kila hatua iliyokuwa ikiendelea na akili yake ilikuwa imetawaliwa na shauku ya kusikia hukumu ya kifo dhidi ya bwana Abraham, kila alipokumbuka maisha magumu aliyoishi na rafiki yake David katika eneo la Kiriri nchini Uganda, alijikuta akitokwa na machozi peke yake. Wakati huo Aminata, mkewe mdogo bwana Abraham alikuwa ametulia huku akiwa amepandikizwa hasira kichwani mwake, alikuwa akimchukia sana David, Jacqueline zaidi James aliyetambua alisababisha kila jambo lililokuwa likitokea.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya dakika kadhaa, vijana wa James walifika na mke mkubwa wa bwana Abraham ambaye hakuwa akicheka cheka sana kama kawaida yake, kesi ya bwana Abraham ilitarajiwa kusomwa baada ya dakika kadhaa zilizokuwa zimesalia. Hatimaye muda husika ulifika, walijongea katika chumba husika kilichopaswa kutumika kusikilizwa kesi hiyo. Wakati huo idadi ya watu iliongezeka wengi wao wakiwa ni wale walioshuhudia harusi ikivunjika baada ya askari kuikatisha kanisani. James na David walionekana kushtushwa na hali ya mkewe mkubwa wa bwana Abraham aliyekuwa mtulivu tofauti na awali, alikuwa akicheka cheka lakini haikuwa kama awali. James aliamua kumuuliza kwa kumnong’oneza daktari aliyeongozana na mwanamke huyo hospitali hapo juu ya utulivu wa mwanamke huyo. Alijibiwa na daktari huyo kuwa mwanamke huyo alikuwa na mabadiliko baada ya kupata matibabu ya awali na walihisi huenda angepona akiwa katika hospitali yao ya St. Joseph Lunacy Hospital. Jambo hilo lilimpa sababu James ya kutabasamu zaidi.

    Hatimaye bwana Abraham aliyeonekana mnyonge alifikishwa kizimbani ili kusomewa mashtaka yake, wakati huo mkewe mkubwa alimwona lakini alibaki kimya huku akiwa amemtolea macho. Kama ilivyotarajiwa bwana Abraham alisomewa mashtaka ya mauaji dhidi ya familia ya Johnson na wafanyakazi wake wawili, mwanaye Sabinus, Otieno na iliaminika kwamba alikuwa ameua watu wengi zaidi ya hao. Kama ilivyotarajiwa bwana Abraham alikana mashtaka aliyosomewa. Mpaka wakati huo mkewe mdogo, Aminata hakuweza kupata wakili wa kesi ya mumewe kwa vile mawakili wengi walikuwa wakiamini kushinda kesi hiyo kwa bwana Abraham ilikuwa ni ndoto. Ni wakati ambao ulikuwa wa tofauti kwani mkewe mkubwa wa bwana Abraham alionekana akitokwa na machozi juu ya tamko la kukana mashtaka aliyosomewa bwana Abraham. Upande wa ushahidi uliambiwa utoe utetezi wake na James alikuwa mtu wa kwanza kuelezea kila jambo alilokuwa akilifahamu kutoka kwa David katika kipindi cha miaka mingi iliyokuwa imepita, alielezea jinsi alivyomfahamu bwana Abraham na kisa chake na David. Kijana David aliyeonekana akiwa na uchungu ndiye alikuwa wa pili kutoa ushahidi wake huku akionesha kovu la risasi lililokuwa katika bega lake la kushoto alilolipata kwa kupigwa na bwana Abraham miaka kadhaa iliyokwisha pita. David alijitahidi kuelezea kila jambo alilolifahamu kwa uchungu yakiwapo mauaji dhidi ya bwana Otieno Ndakufurila na binamu yake Sabinus.

    Jaji wa kesi hiyo alionekana akiwa amemtolea macho David aliyeongea kwa uchungu juu ya visa vya maisha yake vilivyotokana na hila alizodai zilifanywa na bwana Abraham. Baada ya ushahidi wa David, shaidi wa tatu ambaye hakuwa mwingine zaidi ya mke mkubwa wa bwana Abraham alisimama na kutembea akielekea mbele ya chumba hicho cha mahakama kabla ya kuapa na kisha kuanza kutoa ushahidi wake. Lilikuwa ni jambo lililowashangaza zaidi David na wenzie

    “… It’s true, we killed them, that Mr. Abraham was my husband and we cooperated to kill Mr. Johnson and his family, not only them! we killed several other people, am I lying Mr. Abraham?” (“… Ni kweli, tuliwauwa, yule bwana Abraham alikuwa mume wangu na tulishirikiana kumuua bwana Johnson na familia yake, siyo hao tu! Tuliwawaua watu wengine wengi, nadanganya Abraham?”) Alisikika mke mkubwa wa bwana Abraham mara baada ya kuanza kutoa utetezi wake, jambo aliloliongea lilimfanya bwana Abraham aone haya, aliinamisha kichwa chake. Jaji naye alibaki mdomo wazi huku akitambua kuwa shahidi huyo mwanamke naye alikuwa mtuhumiwa.

    “We are guilty Mr. Abraham am I lying?” (“Tunahatia bwana Abraham, nadanganya?”) Wakati huo mkewe huyo alikuwa akiongea kuku akitembea kuelekea eneo alilokuwa amesimama bwana Abraham jambo lililokuwa kinyume cha sheria, aliendelea kuirudia sentensi yake ili bwana Abraham akubali, jaji alionekana akitikisa kichwa kabla ya kugonga na nyundo kwenye meza yake.

    “Hey Mom, please get back to your place, hey!” ( “Hey mama, tafadhari rudi kwenye nafasi yako, hey!”) Alisikika jaji huyo lakini mke mkubwa wa bwana Abraham alionekana kutosikiliza, jaji huyo aliwaonyeshea ishara askari waliokuwepo ambao walimkamata mama huyo kabla hajamfikia bwana Abraham, walianza kumvuta wakimtoa nje ya mahakama hiyo huku akiwa analia.

    Jaji alitaka kujua hali ya kiafya ya mama huyo kabla ya kuelezwa kwamba hakuwa na akili vizuri lakini alikuwa akipona kwa wakati huo, mwishoe alisikika. “Okay, she needs to get cured before she gets back in the court again and face her case as well, they’re killer, she has said. There’s something I have recognized as well…” (“sawa, anahitaji matibabu kabla ya kurudi tena mahakamani kukabiliana na kesi yake pia, ni wauaji, amesema. Kuna jambo nimeligundua pia…”). Jaji wa kesi hiyo aliiahirisha mpaka baada ya wiki mbili akiwa anaamini mke mkubwa wa bwana Abraham angekuwa amepona kabisa na kwenda kutoa ushahidi wake mahakamani hapo lakini pia kujibu kesi yake ya mauaji. Jaji alihurusu watetezi zaidi siku ya kesi hiyo iliyopaswa kusikilizwa tena tarehe ishirini ya mwezi huo wa Februari.

    Hatimaye bwana Abraham aliondoka akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari wa kituo cha polisi cha Altoona. Mke mkubwa wa bwana Abraham pia aliondoka na vijana wa James na safari ilianza akirudishwa katika hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital iliyokuwapo katika kitongoji cha Urbandale. Wazazi wa Jacqueline waliondoka na James, David pamoja na mwanao huyo. Walikuwa wameshautambua ukweli wa kila jambo, tayari walizielewa hila za bwana Abraham na mambo mazito aliyokwisha mtendea David. Mke mdogo wa bwana Abraham, Aminata aliondoka pia akiwa amechanganyikiwa tayari aliona kesi hiyo ilikuwa ikielekea kuwa na mwisho mbaya kama ilivyokuwa imetokea kwa mwanaye, Gray. Alihisi kuchanganyikiwa kwa vile hakuwa tayari kumwona bwana Abraham akihukumiwa kunyogwa mpaka kufa au kifungo cha maisha zaidi alitambua utajiri wote waliokuwa nao ungenyang’anywa na kuelekezwa kwa David, kijana aliyekuwa mrithi halali wa mali za marehemu baba yake. Wakati huo Aminata aliwaza kufanya jambo, hakuwa tayari kushuhudia mkosi huo ukiendelea kuiangamiza familia yake. “I am going to do something, I’m not a looser” (“Nitafanya jambo, mimi siyo wa kushidwa”) Alisikia akiongea peke yake wakati dereva wa gari lake akiendelea kuliendesha kurudi nyumbani kwake.

    * * *

    Mke mdogo wa bwana Abraham, Aminata alifika mapema siku iliyofuata ya Jumanne katika kituo cha polisi cha Altoona ambako mume wake alikuwa akishikiliwa. Bila kupoteza muda aliwaomba askari wa kituo hicho nafasi ya kuongea na mume wake, jambo ambalo alikubaliwa. Baada ya dakika kadhaa alikuwa katika chumba cha wageni ambao walikuwa wakiwatembelea watuhumia wa kituo hicho cha polisi. Akiwa mtulivu katika dirisha ambalo lilitenganishwa na uzio wa chuma na kioo kizito, ilikuwa vigumu kumsikia mtu wa upande wa pili akiongea pasipo kutumia simu maalum iliyotumika. Aminata alikuwa amekaa kwenye kiti huku akiwa ameshika mkonga wa simu ya mezani akiwa tayari kwa kuongea na bwana Abraham ambaye alikuwa hajafika bado, kichwani alikuwa akiwaza kufanya jambo ambalo bado hakulitambua. Alikuwa akiwaza kumwokoa mume wake katika mkono huo wa sheria kabla ya kufikiria jambo la kufanya dhidi ya mwanaye Gray aliyekuwapo tayari katika gereza la Spring Hill.

    Baada ya muda kidogo bwana Abraham alifika na kukaa upande wa pili, alionekana akiwa amenyong’onyea lakini nyuma yake alikuwa amesimama askari aliyekuwa tayari kufuatilia kila jambo ambalo lingeendelea. "Toina nsonga ya kunoonya nze soka ote olii omukazi nga tanaba kuona kugeenda mukooti” (“huna sababu ya kunifuata mimi, hakikisha unamuua yule mwanamke kabla hajapona na kutoa ushahidi mahakamani”) Alisikika bwana Abraham akiongea kwa lugha ya kiganda iliyomchanganya askari ambaye alikuwa nyuma yake ambaye hakuelewa kitu. “hey guys, speak English, don’t use anonymous language here” ( “Nyinyi, tumieni kiingereza na siyo lugha isiyofahamika hapa” ) Alisikika askari huyo huku akiligongagonga bega la bwana Abraham.

    Aminata hakumsikia askari huyo kwa vile alikuwa hatumii simu lakini dhahiri alimwona usoni kuwa askari huyo alikuwa ameghadhabika. Alitikisa kichwa akiashiria amemwelewa askari huyo, lakini kichwani alikuwa ametambua jambo kubwa sana. Ndiyo, mke mkubwa wa bwana Abraham alipaswa kuuawa ili kesi hiyo ikose nguvu wakati wa kutoa ushahidi kwani mwanamke huyo ndiye alikuwa shahidi mkubwa wa kesi hiyo. Aminata na bwana Abraham waliendelea kuongea kwa kiingereza mpaka walipokamilisha maongezi yao.

    Mara baada ya kutoka kituoni hapo Aminata alielewa kazi aliyopaswa kuifanya na aliamini ilikuwa ni ndogo, aliitambua hospitali ambayo mke mkubwa wa bwana Abraham alikuwa akitibiwa, hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital iliyokuwapo katika mji wa Urbandale. Wakati huo alikuwa akiliendesha gari lake la ghari aina ya Rolls-Royce Phantom kwa kasi, alikuwa akielewa sehemu ya kwenda kuanzia ili kufanikisha mauaji yaliyokuwa mbele yake. Baada ya dakika arobaini na tano alikuwa akiliegesha gari lake mbele ya klabu ambayo mbele yake lilionekana bango kubwa lililoandikwa Cowboys Night Club, ilikuwa ni klabu ambayo alikuwa akijumuika na mume wake mara kadhaa kila mwisho wa wiki. Mbali na shughuli zake mbalimbali alitambua kuwa klabu hiyo ya pombe ilikuwa inajishughurisha na kazi nyingine za uuzazi wa dawa za kulevya na ujambazi, klabu hiyo ilikuwa nje kidogo ya kitongoji cha Des Moines.

    Aliyatambua hayo kupitia kwa mume wake bwana Abraham aliyewahi kumweleza miezi kadhaa iliyokuwa imepita. Mara baada ya kushuka kwenye gari lake hilo la kifahari, Aminata alionekana akitembea haraka kuelekea kwenye klabu hiyo mwishoe aliingia katika klabu hiyo iliyokuwa tulivu muda huo wa asubuhi. Wafanyakazi kadhaa walionekana wakifanya usafi, wachache wao walikuwa wakimwangalia wakati akitembea kuelekea katika eneo la kaunta. “Can I see your boss?, Mr. Leo…..” (“Naweza kumwona bosi wako? Bwana Leo…”) Alisikika Aminata mara baada ya kusalimiana na mhudumu aliyekuwa eneo hilo. Mhudumu huyo wa kike aliyekuwapo kaunta alionekana akimchunguza kwa umakini Aminata huku akiwa hamjibu, ni dhahiri aliamini kuwa Aminata hakustahili kuonana na bwana Leo. Mhudumu huyo alibinua mdomo wake kwa dharau kabla ya kuchukua simu yake mezani na kuonekana akiandika namba kadhaa, alibaki ametulia akisikiliza upande wa pili.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hey there’s a mom here, she wants to see you, can I allow her?” (“ Kuna mama hapa anataka kuonana na wewe nimuhurusu?”) Alisikika mhudumu huyo mara baada ya simu yake kupokelewa. “Who’s she? Tell her to face our security camera” (“Ni nani huyo? Mwambie aiangalie kamera yetu”) Alisikika bwana Leo upande wa pili. Mhudumu huyo alionekana akimwelekeza Aminata aitazame kamera yao iliyokuwa imefungwa eneo la juu la kaunta hiyo huku ikizunguka, kwa wakati huo ilikuwa imezungushwa na kuelekezwa eneo la kaunta. Aminata aliiangalia kamera hiyo kabla ya kuonekana akipunga mkono wake.

    “Hey, I know her, Abraham’s wife, let her in” (“namfahamu, mke wa Abraham, mhurusu aje”) Alisikika upande wa pili bwana Leo, mhudumu huyo alikata simu kabla ya kumwangalia Aminata kwa sekunde kadhaa, kisha alitoka kaunta na kumwambia amfuate. Walitembea wakiifuata kordo moja kabla ya kuliona geti kubwa lililokuwa limefugwa na makufuli makubwa matatu, eneo hilo lilikuwa na giza kiasi hali iliyoanza kumtisha Aminata. Mhudumu huyo alilifungua geti hilo, walitembea kidogo kabla ya kuanza kushuka ngazi wakielekea eneo la chini la klabu hiyo. Aminata alishangaa kwani hakuhisi kama kulikuwa na uwezekano wa kuwa na vyumba chini ya jengo hilo. Baada ya dakika moja walikuwa katika geti jingine ambalo mhudumu huyo alikuwa akilifungua pia, mara baada ya kulifungua, ulionekana mlango mwingine wa kitasa ambao nao ulifunguliwa kabla ya mandhari nzuri kuonekana ndani ya chumba kizuri kilichokuwapo. Mhudumu huyo alimnyoshea mkono Aminata ikiwa ishara ya kumhurusu aingie na alifanya hivyo. Mhudumu huyo alianza kufunga geti alilofungua akiwa tayari kwa kurudi kaunta.





    Mara baada ya kuingia katika chumba hicho Aminata aliwaona warembo kadhaa walioonekana kutoa huduma mbalimbali kwa bwana Leo aliyekuwa amekaa kwenye sofa moja na kunyoosha miguu yake aliyoiweka kwenye meza ndogo iliyokuwapo. Vinywaji vikali vilionekana mezani na wakati huo alikuwa akivuta msokoto mkubwa ambao Aminata aliamini ulikuwa ni wa bangi. Bwana Leo aliwakonyeza warembo waliokuwa wakimhudumia ambao waliondoka na kuingia katika chumba kingine.

    Bwana Leo alianza kwa kusalimiana na Aminata na alionekana kufahamiana sana na bwana Abraham aliyemtaja kama rafiki yake. “ So…., now you need me to help you in your husband case, I can’t help that, Its too complicated” ( “Kwa hiyo, unataka nikusaidie katika kesi ya mume wako, siwezi kukusaidia, ni ngumu sana”) Alisikika bwana Leo mara baada ya kuongea mambo kadhaa. Aminata alivuta pumzi na kukanusha mawazo hayo ya bwana Leo, bila kuchelewa alimweleza ombi lake la kutaka kushuhudia mke mkubwa wa bwana Abraham akiuawa akiwa katika hospitali ya walemavu wa akili ya St. Joseph Lunacy Hospital ili mwanamke huyo asiwe hai siku ya kesi ya mumewe.

    Bwana Leo ambaye alikuwa ni mzungu huku akiwa na umbo dogo alitabasamu kwani alitambua kazi hiyo ilikuwa ndogo sana kwa vijana wake waliokuwa wakitimiza kazi walizopewa. Alikubaliana na Aminata kukamilisha mauaji hayo na alihitaji dola elfu arobaini na nane zilizokuwa sawa na milioni hamsini na saba za kitanzania kwa wakati huo. Aminata alifurahi kuona zoezi hilo likielekea kukamilika kirahisi tu tofauti na alivyo tegemea, kiasi cha pesa alichoambiwa hakikuwa kikubwa kwake, jambo kubwa alilolihitaji lilikuwa ni kushuhudia mke mkubwa wa bwana Abraham akiuuawa. Bwana Leo alimwahidi Aminata kuwa angemtuma kijana wake baada ya siku tano ili ampeleke katika hospitali hiyo na mauaji hayo yaweze kuchukua nafasi. Zoezi hilo lilitarajiwa kuchelewa kwa siku hizo kwa vile bwana Leo alieleza kuwa vijana wake wengi walikuwa na kazi walizopewa kwa wakati huo. Aminata alikuwa na amani na hakujali kuchelewa kwa zoezi hilo, jambo kubwa lilikuwa ni kushuhudia mauaji yakichukua nafasi. Aliondoka katika klabu hiyo ya Cowboys Night Club huku akiliendesha gari lake kwa furaha bado alikuwa akihisi mumewe angeshinda kesi, hakufikiria hata kidogo juu ya adhabu yeyote ambayo ingeweza kumpata baada ya kesi yake, bado aliamini ilipokuwapo fedha kila jambo liliwezekana.

    * * *

    Wazazi wa Jacqueline walikuwa wameondoka katika jimbo la Iowa huku wakiwa wameelekea katika jimbo la Michigan walikotarajiwa kuanza safari yao ya kurudi Tanzania lakini wakielekea Uingereza kwanza. Walikuwa wameondoka huku wakiwa wamemtakia kila la heri mwanao Jacqueline na David katika kesi dhidi ya Abraham iliyokuwa ikiendelea. Wakati huo walikuwa wakilijua kila jambo na walitamani kila kitu kiishe vizuri ili Jacqueline na David waweze kuishi maisha ya amani na upendo. Wakati huo David muda wote alikuwa akiutumia kuongea na wakuu wa jeshi la polisi wa nchini Uganda haswa wale wa jimbo la Entebbe ambao alihitaji msaada wa ushahidi wao siku ya kesi ya bwana Abraham, alijaribu kuwakumbusha kila jambo aliloweza kulikumbuka lakini bado matukio ya mauaji aliyokuwa akiyaelezea yalionekana kupotezwa kumbukumbu zake. Mambo yalionekana kuwa magumu kutokana na hali halisi ya nchi nyingi za kiafrika zisizotunza vizuri kumbukumbu za matukio tofauti.

    David hakukata tamaa kutokana msaada usioridhisha alioupata kutoka katika jeshi hilo bado aliamini ukweli lazima ungepatikana. Aliendelea kufanya kila jambo aliloona lingefaa huku akifarijiwa na mchumba wake Jacqueline, jambo lililomsumbua lilihusiana na wakuu wengi wa jeshi waliohisi alikuwa akiwadanganya. James hakuwa mbali alikuwa akimshauri mambo kadhaa wakiwa katika hoteli waliyokuwapo ya Des Moines Motel. James aliyekuwa akiandika riwaya yake ya Afrikanaz hakuwa na hofu kabisa bado imani yake kubwa ilikuwa kwa mke mkubwa wa bwana Abraham ambaye walimtembelea kila siku hospitali. Jambo lililowafurahisha, mama huyo alikuwa akiendelea kupona kadri siku zilivyozidi kusogea hata tabia yake ya kucheka cheka ilikuwa imepungua sana. Daktari maalum aliyemtibu mama huyo alikuwa akiamini angeweza kupona ndani ya wiki moja kabla ya siku ya kesi, na ndiye aliyeonekana kuwa shahidi mkubwa wa kesi hiyo.

    * * *

    Siku ya Jumamosi ya juma la pili la mwezi Februari, majira ya asubuhi Aminata alikuwa ndani ya nyumba yake ya kifahari akiwa na mwanaye mdogo wa kike, Anita, mtoto wa miaka mitatu ambaye bado alikuwa haelewi vizuri jambo lililokuwa likiendelea dhidi ya baba yake na kaka yake Gray, muda wote alikuwa chini ya uangalizi mzuri wa wafanyakazi wengi walioajiliwa katika nyumba ya bwana Abraham iliyokuwapo katika mji mdogo wa Saylor, ukiwa umbali wa kilometa thelathini kutoka katika kitongoji cha Des Moines. Wakati huo Aminata alikuwa akimsubiria kijana wa bwana Leo ambaye alikuwa ametumwa nyumbani kwake. Ilikuwa ni siku ambayo mauaji dhidi ya mke mkubwa wa Abraham yalitarajiwa kuchukua nafasi. Baada ya saa moja kijana huyo alifika nyumbani kwake hapo huku akiwa anaendesha teski ndogo ya polisi. Aminata alishtuka akihisi jambo baya lilikuwa limetokea kwa vile gari hilo lilionekana kama la polisi dhahiri. Alitoka haraka akiwa amebeba mkoba wake baada ya kumuaga mwanaye Anita ambaye pia hakuwa na mapenzi sana na wazazi wake ambao walikuwa bize muda wote. Aliwapenda zaidi wafanyakazi wa nyumba waliokuwa wakimlea kwani wakati wote alikuwa nao na kuna wakati alitamani kuondoka nao kwa vile walikuwa hawalali katika nyumba hiyo.

    Mara baada ya kutoka alikutana na kijana mwafrika aliyekuwa amevaasare za askari wa kikosi cha Sheriff. Hawakuongea mambo mengi na askari huyo, hatimaye Aminata aliyekuwa na furaha aliingia katika gari hilo na safari ilianza wakielekea katika hospitali ya St. Joseph Lunacy Hospital iliyokuwapo katika mji cha Urbandale. Ulikuwa ni mwendo wa saa mbili ili kufika katika hospitali hiyo toka katika mji huo wa Saylor.

    Kijana aliyetarajiwa kwenda kufanikisha zoezi hilo la mauaji hakuwa muongeaji sana, muda wote akiliendesha gari hilo kwa kasi alikuwa mtulivu na hakutaka kujitambulisha jina lake kwa Aminata aliyeomba kumfahamu. Alionekana kama kijana aliyekuwa makini na kazi aliyokuwa akiifanya kwani hakuwa amebeba kitu chochote hata Aminata alipojaribu kuangalia huku na huko aligundua kulikuwa na faili tu la askari huyo bandia. Baada ya saa mbili gari lao liliegeshwa mbele ya hopsitali kubwa ya walemavu wa akili ya St. Joseph Lunacy Hospital. Wakiwa wametulia eneo hilo la maegesho, kijana huyo aliomba jina la mke mkubwa wa bwana Abraham na Aminata alionekana akiliandika kwenye kikaratasi. Ili kukamilisha vizuri zoezi hilo, alitoa picha pia kwenye mkoba wake na kumkabidhi kijana huyo ambaye alifungua boksi dogo lililokuwa mbele ya gari hilo na kutoa bomba la sindano na dawa moja wapo iliyokuwa kwenye kichupa kidogo. Kijana huyo alikitikisa vizuri kichupa hicho kabla ya kuchoma bomba la sindano kwenye eneo lake la juu na kuanza kuifyonza dawa hiyo. Mara baada ya kuifyonza aliliweka vizuri bomba hilo la sindano likiwa na dawa hiyo ndani ya mfuko wa sare yake hiyo ya askari wa Sheriff. Kichupa kidogo chenye dawa alikirudisha kwenye boksi dogo alikokichukua.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “So sit in the back seats of this car, I will be back after quarter an hour” (“Ukae kwenye siti za nyuma za gari hili, nitarudi baada ya robo saa”) Alisikika kijana huyo kabla ya kuchukua faili lake na kufungua mlango akiondoka eneo hilo la maegesho, alikuwa akitembea kuelekea katika mlango mkuu wa kuingilia katika hospitali hiyo.

    Aminata alifuata maelekezo bila kupoteza muda alipita eneo la katikati la gari hilo na alikaa katika siti za nyuma za gari hilo, alivuta pumzi ndefu kabla ya kutabasamu akiamini kila jambo ligekuwa sawa baada ya robo saa. Wakati huo alilisogelea boksi dogo lililokuwa na kichupa ambacho kijana wa bwana Leo alikuwa amechukua dawa kwenye bomba la sindano. Alilifungua boksi hilo dogo na kukitoa kichupa kichobakiwa na dawa yake kidogo, alikisoma kikaratasi kilichokuwa kimebandikwa kwenye kichupa hicho kilichoandikwa Strychnine. Aminata aliamini bila shaka jina hilo liliwakilisha sumu harari iliyokuwa ndani yake. Aminata alikirudisha kichupa hicho kwenye boksi husika kabla ya kubaki ametulia akiamini furaha yake ingekamilika baada ya muda mfupi.

    Mara baada ya kuondoka eneo la maegesho kijana wa bwana Leo alitembea na kuongoza mpaka eneo la mapokezi ambako alimweleza mwanamke aliyekuwapo eneo hilo kuwa alihitaji kufanya mahojiano na mgonjwa ambaye alimpa jina lake. Mwanamke huyo aliyekuwa eneo hilo la mapokezi alionekana akilitafuta jina la mgonjwa huyo kwenye kompyuta yake kabla ya kumjibu kijana huyo aliyeamini alikuwa ni askari. Alimwambia kuwa mgonjwa aliyemhitaji alikuwa katika chumba namba thelathini na tano lakini mtu yeyote aliyehitaji kuonana na mgonjwa huyo ilikuwa ni lazima amwone daktari wake. Kijana wa bwana Leo aliyetulia na kuonekana kama askari nadhifu katika utendaji wake kazi alitulia wakati mwanamke huyo wa mapokezi alipoonekana akibonyeza namba kadhaa kwenye simu yake ya mezani na mwishoe alimsikia akiongea na mtu aliyemweleza alikuwa na mgeni wake eneo hilo la mapokezi. Muda wote kijana huyo akiwa amesimama alikuwa ameinamisha kichwa chake, alifanya hivyo akificha sura yake mbele ya kamera ya ulinzi iliyokuwapo eneo hilo. Ujanja wake huo haukugundulika na mwanamke aliyekuwa eneo hilo la mapokezi.

    Baada ya dakika nne daktari mmoja aliyevaa koti lililoandikwa daktari Rashid alifika eneo hilo la mapokezi kabla ya kuonyeshwa mgeni wake, kijana aliyekuwa amevalia sare za askari wa Sheriff. “I had no information about your coming, I wasn’t informed earlier” (“Sikuwa na taarifa juu ya ujio wako, sikujulishwa”) Alisikika daktari huyo baada ya mazungumzo na kijana huyo kwa dakika kadhaa huku akiwa ameoneshwa kitambulisho chake pia.

    “Yeah!, sure sir but its urgent case, they have sent me to make interrogation with her for few minutes, she knows something and we all know that”) (“Ni kweli, lakini ni jambo la haraka, wamenituma nifanye mahojiano naye kwa dakika kadhaa, anajua kitu na wote tunalitambua hilo”) Alisikika kijana wa bwana Leo akijibu kwa ufasaha. Daktari Rashid hakuwa na la kubisha, hakuhisi kama askari huyo angekuwa mtu mbaya, alimweleza kijana huyo amfuate. Waliongoza mpaka eneo la lifti kabla ya kuelekea katika ghorofa ya pili kulikokuwapo na chumba nambari thelathini na tano. Hatimaye walikuwa katika eneo hilo wakitembea kuelekea kwenye chumba husikahuku kijana huyo askari akiwa amelishika vizuri faili lake mkononi alitembea akificha sura yake kama awali kuzikwepa kamera zilizokuwapo eneo hilo. Daktari Rashid alikuwa ametangulia lakini kwa wakati huohakuwa sawa kwani kadri walivyozidi kujongea kwenye chumba husika mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio kupindukia. Hakujua ni kwa nini lakini hisia za tukio baya kutokea zilianza kumwingia, aliwaza kufanya jambo.

    Hatimaye walifika katika chumba husika kabla ya daktari huyu kukifungua na mwishoe waliingia, walimwona mkewe mkubwa Abraham akiwa amekaa katika kitanda chake. Alitabasamu sana baada ya kuwaona, labda zaidi kwa kumwona dakrari wake bwana Rashid. “Welcome doctor how’s your day?” (“karibu daktari, siku yako inaendaje?”) Alisikika mwanamke huyo ambaye alionekana kama siyo mwehu, alikuwa msafi na usoni hakuashiria kama alikuwa bado na ulemavu wa akili.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog