Simulizi : Niache Na Moyo Wangu
Sehemu Ya Tatu (3)
Ilipoishia…
“Mamaaaa!!! Baaa baaaaa!” Sauti ile iliendelea kuita na sasa hivi ilikuwa imewasogelea kwa ukaribu. Alikuwa ni Stan akiwa na Sara amemshika mkono kwa kumuongoza.
Songa nayo sasa…
Mwili wake ulikuwa ukisisimka mara kwa mara kwa kuwaona wale vichaa mbele ya macho yake. Aliamini kabisa hata kama ni vichaa lakini watabaki kuwa wazazi wake waliomzaa. Aliahidiana na moyo wake kwa haraka zaidi kuwa ni lazima atumie njia zozote kuwaweka sawa, kuwaweka pamoja na kuwajali kama wazazi. Hakujali umri wake ni mdogo, la hasha! hata makazi anayoishi hakujua ataishije.
Muda wote Stan alikuwa na rafiki yake wa karibu,rafiki ambaye ni kipofu pia naye amepitia katika mateso na manyanyaso kama yake,Sara. Waliwasogelea wale vichaa na kusimama mbele yao. Ujasiri!! Stan alichukua mkono wake na kumshika yule mwanamke chizi.
“Mamaaa? Kwa nini mlinitoroka?” Stan alilalama.
Yule mama chizi akakaa kimya kwa muda kisha akaachia bonge la cheko akishika mdomo wake kwa mkono mmoja na kumfanya yule chizi wa kiume kumshika bega Stan naye akicheka kwa dharau.
“Dogo? inamaana mimi ni baba yako?”
“Ndio wewe ni baba yangu na huyu ni mama yangu. Kwanini mlinitoroka nikiwa mdogo sana?” Stan aligomba kwa kujiamini. Akili yake ilishamleta kuwa anaoongea nao si machizi bali ni watu wa kawaida. Stan aligomba sana uku machozi yakimlenga lenga. Umati wa wafanyabiashara sokoni wale waliokuwa wamewatimua vichaa hao walikuwa wakijisogeza taratibu katika eneo lile. Stan alizidisha kufoka kwa sauti ya juu uku wale machizi wakinyamaza kwa muda kwa kumuangalia kisha wakicheka wenyewe kwa wenyewe kwa kugongeana mikono.
“Mume wangu?” Aliita chizi yule wa kike.
“Enhh mke wangu!!” Aliitika mwenzake.
“Kumbe tuna mtoto mkubwa hivi tena mzuriii?, haya unaitwa nani mwanangu?” Aliuliza yule chizi kwa kukejeli.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hasira kali zilikuwa zimeshampanda Stan. Hasira za kutorokwa kwa wazazi wake toka akiwa mdogo sana. Wazazi ambao kwa sasa hawana muelekeo na kuwa machizi. Simile!! Stan alishindwa kabisa kuendelea kuona wakikejeli wale vichaa ingawa yeye ni mtoto wao. Aliamini maneno ya yule mzee kwa asilimia zote kuwa ni wazazi wake.
Kwa kujiamini Stan aliachia mkono wake aliokuwa ameshikana na mama yake,mama yule chizi nakumtandika nao kibao cha haja! Paaa!!!
Umati wote ukalipukwa kwa furaha. Macho ya Stan akayageuza uku na kule kushangaa wale watu waliokuwa wakishangilia kwa furaha. Akili yake ikalifananisha lile tukio na tukio lile la kuchota maji alivyomfanyizia yule baba yake na Sara na umati kumzunguka kwa makelele.
Lile kofi likamwingia vilivyo yule chizi wa kike. Chizi wa kiume akaumia sana kwa lile kofi kupigwa mwenzake akamshikilia mkono Stan kwa nguvu zote.
“Nitakuuua? nitakumaliza?” Aliongea yule chizi wa kiume.
Akamuachia mkono Stan. Mkono wa Stan ukabakiwa na ganzi. Ukawa ukitetemeka wenyewe kwa wenyewe.
“Stan? Stan?” Aliita Sara.
Alikuwa haelewi chochote kinachoendelea kutokana na upofu wa macho aliokuwa nao. Aliweza kuzisikia tu sauti za watu na sauti ya kile kibao alichopigwa yule chizi wa kike. Muda wote alikuwa akasimama wima pembeni ya Stan akisuburi Stan amalizane nao waondoke.
“Sara, Hapa leo lazima niondoke na baba na mama” Aliongea Stan kwa kuhema.
“Haya wachuk…
Kabla Sara hajamalizia kuongea tu. Sauti kali ilisikika upande wa pili.
“Stannn Stannn”
Wote Stan,wale machizi na hata ule umati ukageuza vichwa vyao kuisikiliza ile sauti inapotokea. Alikuwa ni baba Devotha akija mbio. Alikuwa kama mtu aliyekuwa na kitu mdomoni akishindwa kuongea na kuishia kuita jina. Hakuwa na nguvu za kutembea haraka haraka kutokana na kuonekana akihema sana na kujikongoja kwa taratibu akinyoosha mkono mmoja juu kuonesha ishara ya Stan asogee. Stan hakuweza kuelewa ishara hiyo kwa mara moja. Alishamchukia baba Devotha toka moyoni mwake. Alimchukia kwanza kwa tabia alizomlelea za kikatili mpaka amekuwa japokuwa alimsomesha pili alimchukia kwa kitendo cha kumficha baba na mama yake mzazi walipo nakuishia kumdanganya kuwa walishazamaga na meli na pia aliamchukia sana kwa kitendo chake cha kutembea na mke wa yule mzee ambaye alikuwa rafiki yake sana na kumpa mimba hivyo kupoteza uelekeo wa familia ya yule mzee. Sasa matukio yote yakaulipua moyo wa Stan upya. Moyo ukalipukwa!!. Ukamtuma moja kwa moja ahamie mpaka katika upande wa mfuko wa suruali yake. Akachomoa ile bastola. Maishani mwake Stan hakuwahi hata kuishika wala kuitumia ile bastola. Aliikoki kwa kutaka kumtetekeza kabisa baba Devotha ambaye alikuwa ameshasogea maeneo ya karibu yake. Umati wote ukashika mikono vichwani na wengine midomoni. Hakukuwa hata na mmoja wa kwenda kumuokoa baba Devotha kutokana na wote kuogopa bastola aliyoishika Satn. Stan alikuwa ameshadhamiria. Dhamiria haswaa kuaa!!. Wale chizi na wenzake wakabaki wakicheka wenyewe pembeni ya Stan. Jasho kali likamtiririka Stan katika paji la uso wake. Mishipa ya hasira ikawa ikipishana uku meno yake akiyasaga! akaivuta ile bastola nakutaka kuifyatua kwa kutetemeka. Akaifyatua!!
Risasi ile ikashindwa kumpata baba Devotha kutokana na Stan kutetemeka sana mikono. Alikosea kupiga kwenye uelekeo unaotakiwa nakujikuta akiiachia maeneo ya juu kabisa mbali na baba Devotha alipo.
“Usisogee. Nitakuua., Simama hapo hapo?” Stan aliongea kwa hasira.
Safari hii aliikoki tena vizuri nakumnyooshea kabisa maeneo ya karibu na uso wake. Umati wote ukaendelea kukaa kimya. Sara bado hakuweza kujua kinachoendelea pale kutokana na upofu aliokuwa nao. Zile kelele za watu za kupiga makelele na kunyamaza ghafla hakuzielewa zilikuwa zikimaanisha nini. Alihisi huenda Stan wake akipigana na wale baba na mama yake vichaa.
“Niambie hawa ni wazazi wangu? na kwanini ulinificha wewe baba?” Aliongea Stan.
“Niue tu. Niue Stan lakini amini kuwa hao sio baba na mama yako? sio hao Stan!! twende nikakoeneshe baba na mama yako walipo? shusha hiyo bastola mwanangu Stan nikakuoneshe!”
“Mimi sio mtoto wako tena?” Stan aliongea kwa hasira.
Akaishusha ile bastola chini nakuing’ang’ania mkononi vilivyo kisha akamshikilia Sara mkono mwingine.
“Sara twende . Si umemsikia huyu baba yangu akisema kuwa hawa sio wazazi wangu?. Na ole wake anidanganye kwa mara ya pili. Haki ya mama naua. Lazima nimuue. Twende uko?” Aliongea Stan.
Tayari Stan alikuwa kama aliyelishwa damu ya mbwa mwitu au nyati kabisa. Hakuwa na hata chembe kidogo ya kusema kuwa baba Devotha amemlea mpaka kufika hapo. Ndio kwanza aliinua tena ile bastola nakumnyooshea bastola baba Devotha nakumuongoza uku mkono mmoja akimshika Sara na kuongoza kwa kumfuata baba Devotha anapoelekea. Wale vichaa walibaki sokoni pale pale wakiyakodoa macho wasielewe kinachoendelea. Hawakuweza kuongozana na Stan kwa sababu ya uchizi waliokuwa nao. Hawakuwelewa kabisa nini kinaendelea kati yao kutokana na ukichaa waliokuwa nao. Wafanyabiashara karibu wote walirudi kuendelea na biashara zao na wale machizi walivamia jalala la pembeni na kujipatia mabaki ya matunda matunda yaliokuwa yametupwa sokoni. Matunda yaliooza ama kuharibika.
“Hatufiki tu? Twende?” Aliamrisha Stan.
“Ni kwangu mwanangu tunaenda kwani umepasahau?” Aliongea baba Devotha.
“Kwako ni kwako mi hiyo hainihusu? ninachotaka niwaone baba na mama yangu na tena wakiwa hai ole wako unidanganye tena?” Stan aliongea kwa kujiamini kutokana na kuwepo kwa ile bastola mkononi mwake. Njia nzima watu walikuwa wakimshangaa Stan kumvaa baba yake waliomzoea. Nguo zake zilizojaa damu damu zimliogopesha karibu kila mtu mtaa mzima na kuogopa hata kuwafuatilia kwa nyuma. Ndani ya dakika kadha wakawa wameshafika nyumbani kwa baba Devotha. Nyumba aliyolelewa Stan mpaka kukua kwake.
“Devotha? Devotha?” aliita baba Devotha.
Devotha hakuwepo. Waliusukuma mlango nakuingia wote. Moja kwa moja baba Devotha akawaingiza Stan na Sara katika chumba chake. Chumba ambacho ndani yake kuna chumba kingine ambapo Stan hakuwahi kukiona hicho chumba cha pili toka amekuwa kutokana na kuzibwa na kabati la kuhifadhia nguo. Aliposogeza tu kabati moshi mkali ukaanza kutoka kwa kuwafuata. Chafya zikamuanza Sara na kisha zikafuatia kwa Stan mfululizo. Baba Devotha akabaki kimya akimtazama Stan usoni. Stan na Sara wakakooa sana.
“Unanidanganya siyo? mama na baba yangu wako wapi?” Stan aliongea kwa sauti ya juu na ya ukali.
“Wapo subiri watatokea sasa hivi?”
Ndani ya muda mfupi hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kuongezeka ule moshi na chafya mfululizo. Safari hii Stan hakuwa na simile hata kidogo. Akainyanyua ile bastola yake kwa lengo la kutaka kumfyatua baba Devotha, kitendo cha kutaka kufyatua risasi tu zikagoma. Zilikuwa zimeshakwisha katika ile bastola.
“Anhaa haaa haaa” Baba Devotha akacheka kwa sauti.
“Shut up! (Kaa kimya)” Stan aliongea kwa kujiamini.
“Na lazima leo nikurudishe kwa wazazi wako. Umenishinda. Unataka kuniua? mimi? mimi baba Devotha?” Alilalama baba Devotha.
Baada ya ule moshi kutoka kwa muda mrefu sana ukimuingia puani Sara na Stan. Sara alianza kuweweseka na Stan vivyo hivyo.Baba Devotha akawachukuwa nakuwaweka mikononi mwake. Akawarusha upande ule ulipokuwa ukitoka moshi kisha akafunga kile chumba kwa kurudishia kabati lake la kuhifadhia nguo. Kimya!!
“Wasalimie sana wazazi wako pumbavu” Aliongea baba Devotha kwa majigambo uku akielekea joikoni. Alichukuwa kijiko na kutoa unga unga uliokuwa katika pindo la suruali yake. Akachanganya hapo hapo kijiko kikafuka moshi wenye harufu ya kuvutia. Akaanza kujifukizia mwilini kwa hisia.
“Nisameheni, msimuue mteseni tu waungwana!!”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
Rundo la mapolisi wakiongozwa na mkuu wa polisi kanda, Rafaeli walikuwa wameshafika tukio la mauaji ya mfanyabiashara maarufu lililotokea usiku. Ilikuwa ni asubuhi sana baada ya kupewa taarifa juu ya mauaji yaliokuwa yametokea usiku. Kulikuwa na madaktari bingwa wa kukusanya vipande vipande vya alama sambamba na kupiga mahesabu ya vipimo mbali mbali vya tukio lilivyotokea. Waliingia mpaka ndani ya gari nakuchukua alama za damu damu zilizokuwa zimetanda katika siti za gari la mfanyabiashara maarufu.
“Mpaka sasa hamjampata mtu au kusikia yoyote aliyehusika na tukio hili?” Aliongea Rafael, kamanda mkuu wa msafara baada ya kuufunua mwili wa mfanyabiashara maarufu aliyekuwa tayari marehemu.
“Hapana bwana Afande ila kuna mwili wa mama mmoja umekutwa umekufa uko pale tumeufunika toka jana usiku” Alijibu mmoja wa polisi aliyekuwa doria toka usiku.
Wale mapolisi walisogea na madakatari wao napo wakachukuwa vipimo vyote na alama za majeraha kisha walirudishia kwa kuufunika ule mwili. Wakiwa katika kutaka kuondoka afande mmoja aliyekuwa doria toka usiku aliwasimamisha.
“Mkuu? mkuu kuna jambo tumesahau kukwambia?” Aliropoka yule polisi.
“Jambo gani?” Rafael aliuliza kwa mshangao.
“Jana usiku kuna vijana wawili mmoja ni msichana aliyekuwa kipofu na mwingine ni wa kiume alikuwa amechafuka damu damu lakini…
Kabla yule polisi hajamaliza kujieleza alishangaa kupigwa kofi kali kutoka kwa kamanda mkuu,Rafael.
“Yupo wapi sasa? unaniletea maelezo baadala uniambie mmemkamata au yupo hatiani kituo gani, pumbavuuu?? yupo wapi na hizo damu damu amezitoa wapi?” Aliongea Rafel kwa ukali.
“Mkuu, yule kijana tutampata tu kwani Afande Julias anamj…
“Kabla tena hajamaliza kuongea aliongezwa kibao cha nguvu.
Namtaka huyo kijana na huyo binti mikononi mwangu sasa hivi na hili lifanyike ndani ya nusu saa siondoki nataka majibu haraka iwezekanavyo na huyo kijana atatusaidia katika kujibu kesi hii ya mauaji.
*********
Kamanda wa polisi,Rafaeli alikuwa bado ana hasira kubwa sana kutokana na mauaji yaliokuwa yamefanyika pale tena ni hatua chache na kituo cha polisi. Mauaji ya mfanyabiashara maarufu anayejulikana sana katika maeneo mbali mbali ya jiji na hata mtaani hapo mbezi. Maaskari takribani wanne waliingia ndani ya gari ndogo ya polisi ile waliokuwa wakiitumia katika kufanya doria kipindi cha usiku. walikuwa na lengo moja tu. Lengo la kumtia hatiani kijana ambaye alionekanika usiku akiwa na damu damu katika nguo zake,kijana ambaye ni askari mmoja tu kati ya wale wanne aliyekuwa akimjua kwa sura kutokana na kuwekwa lokapu kwa muda mfupi.
“Stan, yes anaitwa Stan” Aliongea askari mmoja kimoyo moyo.
Njia nzima alikuwa wa kutafuta jina la Stan kichwani mwake. Alimkumbuka sana na yule mama msamaria mwema aliyekuwa amekuja kumtoa pamoja na yule binti kipofu waliokuwa wameongozana naye.
“Katiza embu mtaa huu” Aliamrisha yule askari.
Bado waliendelea kuchanja mitaa pasipo kujua wapi watampata kijana huyo. Hawakuwa na muelekeo maaulum. Kuna wakati walijikuta wakirudia mitaa ile ile.
“Bosi ametuambia ndani ya nusu saa lakini sijui kama itawezekana aisee” Aliongea mmoja wa maaskari.
“Ndio tukazane tuhakikishe tumempata. Mimi najua kile ni kijana kidogo sana na huenda hakikai hata mbali na mitaa hii”
Baada ya mwendo mrefu wa hapa na pale hatimaye walianza kuuliza mtaa mmoja baada ya mwingine wakiulizia jina la Stan.
“Anaitwa Stan, jana usiku alionekanika na binti mmoja hivi kipofu” Aliongea Askari akimuuliza mpita njia.
“Anhh unamzungumzia Stan wa baba Devotha?”
“Embu tuambie yupo wapi na hapo kwa baba Devotha ndio wapi?”
“Stan ameonekanika leo soko kuu la mbezi akifanya mtiti. Siku hizi amekuwa mbogo kweli mna haki ya kumtafuta dahh. Sijui atakuwa amewehuka Stan kwani alikuwa sokoni akizungukwa na umati wa watu akidai machizi wa kule sokoni ndio wazazi wake, mie sina mbavu duhh” Alimalizia yule kijana kwa utani.
Maaskari hawakuwa na haja ya kusikiliza tena stori zaidi ya kuongoza mpaka soko kuu kumtafuta Stan. Walijipanga haswa kana kwamba waliokuwa wakimtafuta ni kipande cha mtu kumbe ni kijana mdogo sana wa miaka kumi na saba. Ndani ya dakika kadha wakawa wameshafika katika eneo la la soko kuu. Breki ya kwanza waliingia uku na kule kumsaka alipo. Kila mtu alikuwa akiwatolea maaskari. Kuna baadhi ya vichwa vya wafanyabiashara vilikuwa tayari kufanya kazi na kuelewa nini kinaendelea baada ya muda mfupi uliopita Stan kurusha risasi juu.
“Tunamtafuta kijana mdogo mdogo nguo zake zina damudamu mmemuona wapi?” Aliongea Askari akimuuliza mmoja wa wafanyabiashara.
“Anhh yule alikuwepo muda si mrefu ameondoka na baba mmoja uku kamshikia bastola wameelekea upande ulee”
“Kwa wapi na huyo baba aliyeondoka naye mnamfahamu?”
“Hapana ila baadhi ya watu walikuwa wakimfahamu huyo mzee na kumuita baba Devotha sijui. Na walikuwa wakisema kuwa ni mtoto wake kabisa kwa jinsi alivyokuja kuja”
Yule askari hakutaka tena maelezo zaidi ya kuwachukuwa wenzake na kuingia katika gari.Walikuwa wakifukuzana na muda waliokuwa wamepewa na kiongozi wao wa kazi. Kamanda mkuu wa kikosi,Rafaeli. Waliona endapo muda waliopewa ungepitiliza yangeweza kuwa mengine weza wakatimuliwa kazi kwa uzembe au kupewa adhabu yoyote. Waliliwasha gari kwa kasi ya ajabu na zoezi la kuelekea kupatafuta nyumbani kwa baba Devotha ikaanza rasmi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haikuwachukuwa muda sana kutokea pale sokoni. Walizunguka na gari mwendo mchache sana uku wakiulizia nyumbani kwa baba Devotha, nyumbani kwa kijana mmoja mtukutu aliyoonekanika na binti kipofu kwani ndani ya muda mfupi Stan alikuwa ameshajizolea umaarufu mkubwa sana mtaani. Umaarufu kwa kupigana na mfanyabiashara maarufu mtaani na hata maeneo mbali mbali ya jiji. Pili kumng’ang’ania binti kipofu kuwa naye karibu na kumtetea kwa kila jambo. na kuwa miongoni mwa kijana wadogo sana kuingia lokupu ya kituo chao cha polisi cha mtaani na nne kuwang’ang’ania machizi nakudai ni wazazi wake uku akitishia kumuua na bastola baba yake wakufikia baba Devotha.
Mapolisi walipata maelekezo yote juu ya nyumbani kwa baba Devotha baada ya kuuliza kidogo tu. Baada ya kutaja jina la Stan kwa mara nyingine. Walipoifikia nyumba ya baba Devotha walishuka na kuizingira mtu yoyote asiweze kutoroka. walifungua milango yote iliyokuwa wazi. Waliingia vyumbani bila majibu yoyote.
“Stan, Stan??” aliita mmoja wa wale maaskari kwa sauti ya juu.
“Baba Devotha? Baba Devotha?” Aliita tena lakini kimya kingi kiliendelea kutanda katika eneo lile. Wale mapolisi walianza kuonesha kukata tamaa. Walitaka kuondoka lakini ni mmmoja kati ya maaskari wale alikuwa tayari amekiona kitu baada ya kuingia jikoni. Alikuwa amekiona kitu kama hirizi kikiwa kimejikusanya juu ya meza ya jikoni.
“Hawa watu wa humu ni wachawi nini?” Aliongea yule askari uku akikigeuza geuza kile kitu kilichofanana na hirizi kwa kutumia mdomo wa bunduki yake.
Kile kitu kama hirizi kikawa kimefungua sura mpya ndani ya ile nyumba ya baba Devotha. Wakaanza kukagua uku na kule. Wakafunua makabati moja baada ya lingine. Taharuki!!
“Tokaa, toka mwenyewee?? Pumbavu sana weweee?” Aliongea askari mmojawapo baada ya kuinama chini kidogo na kukutana uso kwa uso na sura ya mtu. Alikuwa ni baba Devotha akiwa amejikunyata katikati ya makabati yale ya jikoni kwa kuogopa mapolisi. Yule askari kwa hasira alizokuwa nazo alijikuta akimpiga teke la uso baba Devotha ndani ya kabati. Baba Devotha hakuwa na jinsi zaidi ya kutoka uku mikono yake miwili akiwa ameinyoosha juu juu kusalimu amri.
“Mtoto wako yupo wapi tunamtaka? si nakuuliza wewe?” Aliongea yule askari kwa sauti ya ukali.
“Mwanangu Devotha? Devotha hayupo kaenda kuchota maji?” Alijitetea baba Devotha. Kamwe aliapa na moyo wake asiwaambie mapolisi juu ya Stan alipo. Alijua tu wanayemtafuta ni mtoto wake wa kufikia Stan. Aliona endapo atasema alipo Stan basi siri yake yote ya kuwa mchawi itafichuka. Na pia aliamini kabisa kuwa Stan na Sara aliowaficha ndani ya chumba chake cha kichawi watakuwa wameshachukuliwa na wachawi wenzake na kufanyiwa anavyotaka.
“Narudia tena kwa mara ya mwisho la sivyo nakulipua hapa hapa, Mtoto wako Stan yupo wapi?” Aliongea yule askari kwa hasira na kumtishia baba Devotha ili tu ataje alipo Stan.
“Nilimwacha Sokoni kwakweli sijui hata yupo wapi kwa sasa?” Aliendelea kujitetea baba Devotha akinyanyua mikono juu kujizuia sura asipigwe.
“Afande Marwa? hiri riadhabu rake rinaishia hapa hapa jikoni ritatuambia ukweri kabisa riripo ristani”
Yule askari alichukuwa kiberiti pale jikoni nakumvua shati baba Devotha na kisha kulichoma lote. Walipomaliza kulichoma shati la baba Devotha kabla ule moto ulioshika shati hujaisha wakatishia kumchoma nao ili tu ataje Stan alipo.
“Ritaje ristani ripo wapi wewee rimzee, tunakuteketeza hivyooo, shauri rako!!” Yule askari alizidi kumtisha baba Devotha. Ndio kwanza kama unamtisha kuku aondoke kwa kumwagia punje za mchele. Baba Devotha aliona ni bora akafa anajiona na siyo kutaja Stan alipo. Aliona atakuwa amewakosea sana wachawi wenzake na utakuwa mwisho wa maisha yake endapo itajulikana na mapolisi maficho yake ndani ya kile chumba, nyuma ya kabati lake.
“Niueni tu lakini ninachojua Stan yupo sokoni” Aliendelea kulia kwa kujitetea baba Devotha.
“Afande, hapa atatupotezea muda twende naye kwa mkuu tukamwambie kuwa huyu anajua Stan alipo tuone mkuu wetu atafanyaje”
Wale maaskari waliupinguza kasi ya kuwaka ule moto uliokuwa umetanda ndani ya shati la baba Devotha pale jikoni nakuacha likitoa moshi. Wakamsukuma kwa kumburuta baba Devotha uku wakimpiga mateke mithili ya mpira wa miguu mpaka karibu na gari lao. Wakampakiza na kurudi nao eneo husika pale walipomuacha kamanda wao mkuu,Rafaeli.
*********
Jua la asubuhi lilikuwa limeshaanza kukolea kuashiria imefika muda wa saa tano kuelekea mchana wa saa sita.Watu wengi waliokuwa bado wakielekea makazini iliwabidi kusimamisha safari zao kila walipofikia nyumba ya kina Devotha. Kulikuwa na sintofahamu baada ya maaskari wale kuondoka. Ule moto waliokuwa wakimtishia kumuunguza baba Debotha nakuzimwa kubaki moshi hakukuwa u mezimwa vizuri. Ulisababisha nyumba kuanza kuungua taratibu. Devotha mtoto pekee wa baba Devotha alikuwa katika kutafuta maji ya kupikia. Alikuwa amerejea nyumbani na kukutana watu wengi wakiwa wanashangaa kulipuka kwa nyumba upande mmoja wa eneo la jikoni. Ni wasamaria wachache tu waliokuwa na moyo wa kuuzima ule moto kwa kutumia mchanga na hii yote ni kutokana na uhaba wa maji katika maeneo waliokuwa wakiishi,mbezi luis.
“Baba? Baba maama yangu weee baba yangu weee” Aliongea Devotha kwa kuchanganyikiwa uku akiirusha ile ndoo ya maji kichwani na kumwagika mpaka chini. Alikuwa kama nusu rasi nusu majinuni kwa jinsi alivyokuwa akishuhudia. Aliwaza mengi sana kichwani ndani ya muda mfupi. Siri kubwa aliyokuwa ameitunza yeye na baba yake alihisi huenda imeharibika. Siri ya kuwa na chumba maalumu cha wachawi ndani bila mtu yoyote kujua. Alihisi huenda wachawi wale waliokuwa wakiwasaidia kutoka katika kile chumba wamekasirika. Kwa hasira na haraka haraka alizokuwa nazo Devotha aliutoa mkono wake nakuupitisha mpaka kwenye pindo la nguo yake ya ndani. Akakutana na hirizi kubwa aliyokuwa ametengenezewa na baba yake toka akiwa mdogo. Ile hirizi akaivuta nakuitoa kisha akaiweka mdomoni mwake. Akaibumba!! Baada ya hapo akapata nguvu za ajabu, akakimbia moja kwa moja mpaka ndani. Moto ulikuwa mkubwa sana lakini kwa Devotha hakuweza kuungua hata kidogo. Ule umati wote ukabaki ukishika vichwa na midomo usielewe muujiza unaotendeka kwa Devotha kupishana na moto mkali. Devotha aliingia moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha baba yake kilichokuwa kikianza kutoa moshi kuashiria moto uko karibu kuanza katika chumba hicho.
“Baba? Baba uko wapi?” Aliita Devotha akiliangalia kabati lilikokuwa limezuia kile chumba. Kimya kingi kiliendelea kutanda katika eneo lile. Nguvu za ajabu alizokuwa nazo Devotha aliweza kulisogeza lile kabati kubwa la nguo pembeni. Chumba kile chote kisichokuwa hata na mlango kikatoa harufu kali sana iliyoambatana na moshi.
“Baba, baba?” Aliita Devotha kwa huruma.
Baada ya Devotha kuita kwa muda bila majibu yoyote akataka kuingia ndani ya kile chumba. Kitendo cha kutaka kuingiza mguu wake mmoja tu akasikia kishindo kuashiria kuna watu ama mtu mkubwa anataka kutoka katika kile chumba.
“Baaa baaaaa?? Baaa baaaa?” Aliita devotha mithili ya teja ama mtoto mchanga uku udenda ukimchirizika.
Kile kishindo kiliendelea kusogea na baada ya muda aliweza kukutana na sura ya Stan ikiwa inatoka. Alikuwa ni Stan huyu huyu aliyokuwa amemzoea. Alikuwa ametoka ndani ya chumba na mikono yake miwili akimbeba Sara aliyekuwa amelegea mwili mzima. Stan alionesha kuwa na hasira kali sana usoni mwake.
“Mmemuua Sara wangu siyo? Your next?” Aliongea Stan akimshusha Sara chini. Kitendo cha kumaliza tu kumshusha Sara chini pale pale Devotha akatema lile lihirizi aliokuwa ameliweka mdomoni kiupande. Lilikuwa limeshamzidia mdomoni kwa kulihifadhi. Pale pale na Devotha akadondoka na kupoteza fahamu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
Stan alionekana kama kuchanganyikiwa kwa kuwa na sintofahamu. Wasichana wawili walikuwa mbele yake,Sara na Devotha na tena wote wakiwa katika kupoteza fahamu. Alilivua shati lake bila kujali lile joto kali lililoanza kutamba katika kile chumba.Joto lililotokana na moto mkali uliokuwa ukiwaka nyumba yote ya baba Devotha. Stan alianza kwa kumpepea Sara wake. Alikuwa akimpepea kidogo kisha anainamisha kichwa chake mpaka kifuani mwa Sara kwa kusikilizia mapigo ya moyo ya Sara kama yakidunda ama la! Alifanya hivyo mara nyingi zaidi lakini jibu lilliendelea kubaki pale pale. Mapigo ya moyo ya Sara yalikuwa yakienda taratibu sana. Hakuwa Sara wa kawaida kwa jinsi alivyokuwa aikihema.
“Sara? Saraaaa?” Aliita Stan kwa ukali.
Bado kimya kilizidi kuwa kingi. Joto lile lililokuwa limezidi katika kile chumba lilisababisha Stan kulowa mwili mzima vivyo hivyo na Sara na Devotha. Hawakuwa wamelowa kwa maji bali jasho na fukuto zito la ndani ndilo lililochochea zaidi. Stan hakujua atatokaje mule ndani. Alilitupa lile shati lake pembeni kisha akamnyanyua Sara nakumning’ing’iniza begani kwake kisha akataka kuondoka. Kitendo cha Stan kunyanyua tu mguu hapo hapo na Devotha naye akawa ameshashtuka. Alikuwa ameshafungua jicho moja toka kipindi Stan akihangaika kumpepea Sara. Hakuwa Devotha wa kawaida kama alivyozoeleka. Alikuwa ameshauvaa ule uchawi kutokana na ile hirizi aliyokuwa ameibumba hapo awali. Kwa nguvu za kichawi alizokuwa nazo aliweza kuzinduka na kuukamata mguu wa Stan na kumzuia asitembee. Stan hakulijua hilo. Kila akiinua mguu wake alihisi mzito wenye kuzuiliwa.
“Niache? Niache uko?” Alilalamika Stan baada ya kugundua mguuni mwake ameshikwa na Devotha.
“Sikuachi Stan. Stan baba yangu umempeleka wapi? Na kwanini unamtesa baba yangu?” Alilalamika Devotha.
Stan alitumia nguvu za miguu kumpiga teke Devotha amuachie lakini ndio kwanza alikuwa kama amechokoza nyuki. Devotha alizidisha zile nguvu na safari hii aliung’ang’ania mguu wa Stan kwa kuuchezesha na kusababisha Stan kuzidiwa nguvu na kudondoka mpaka chini na Sara. Kwa kutambaa!! Vidole vya Devotha vikaongezeka kucha. Akatumia makucha yake kukwaruza chini nakusogea maeneo alipokuwepo Stan na Sara. Yale makucha yakajiongeza urefu zaidi na zaidi akamchoma nayo Sara.
“Devothaaa, Devothaaaa” Alilalamika Stan kwa sauti ya ukali.
Ndio kwanza kwa Devotha kama mbuzi akipigiwa gitaa vile. Aliuinua tena mkono wake nakumtoboa toboa Sara hadi maeneo ya usoni mwake. Ule uso wa upofu aliokuwa nao Sara ukageuka na kuwa bahari ya damu. Sara alitobolewa ovyo ovyo maeneo ya machoni alipokuwa amefanyiwa operesheni na kutolewa macho yote mawili. Eneo hiloo likageuka na kutoa damu nyingi sana.
“Stan naumia. Stan kwanini unanifanyia hivi?” Alilalamika Sara kwa kushtuka toka alipozimia. Alihisi huenda Stan ndio anayemfanyia yale yote.
“Stan ni bora unichome na huu moto ninaohisi kuliko kunitoboa eneo la macho yangu. Eneo nililofanyiwa operesheni naumia sana Stan” Bado Sara aliendelea kulalamika.
Maneno yale yalimuingia sana Stan. Stan aliyekuwa amelegea kwa muda baada ya kudondoshwa na Devotha kwa nguvu za kishirikina mpaka chini. Stan aliokuwa hajiwezi hata kuinuka wala kufanya lolote zaidi ya kumuangalia Sara wake akiteketea kwa makucha marefu kutoka mikononi mwa Devotha.
“Devotha? Devothaa” Stan alibaki kulalamika tu mwenyewe chini.
Baada ya Devotha kumchoma choma sana Sara kwa kutumia makucha mwili mzima. Sara alionekana kama kuishiwa nguvu na kuzimia pale pale alipo. Alionekana kama ni mtu aliyepoteza tena ufahamu au maisha kabisa baada ya mwili wake kukutana na kucha za kimaajabu, kucha za kichawi kutoka katika mikono ya Devotha. Pale pale Devotha naye akainama nakulala kabisa. Alikuwa pia nguvu zimempotea kabisa. Nguvu za kichawi za muda mfupi.
Moto sasa ukawa umewasili bila ya kupiga hodi katika kile chumba alichokuwepo Sara,Devotha na Stan. Moto mkali uliokuwa ukiiteketeza nyumba maeneo ya jikoni. Stan nguvu zile zilizompotea zikamrejea upya baada ya Devotha kuishiwa. Alijikuta akiweza kuinuka kwa kutumia miguu yake. Akasimama, Dede!! Hasira kali zilimganda, alikunja ndita ya muda nakusogea kwa pembeni yake alipokuwa amelala Sara. Akaupitisha mdomo wake mpaka karibia na masikio ya Sara. Akanena!!
“Sara nisamehe sikuwa mimi?”
Kisha Stan akambeba Sara begani kama awali lakini baada ya kutaka kutoka kupambana na ule moto aweze kufika nje. Akili ikamrudisha, akageuka kwa nyuma na kumuangalia Devotha.
“Haiwezekani mpaka nimshudie akifa” Aliongea Stan akiwa bado katika hasira.
Alimshusha Sara kwa mara ya pili nakumfuata Devotha pale chini. Devotha aliyokuwa hata hajitambui kutokana na kuishiwa zile nguvu za kichawi alizokuwa nazo ndani ya muda mfupi. Alipomfikia Devotha alimchukuwa kwa nguvu nakumsogezea katika moto mkali upande wa pili uliokuwa ukizidi kupamba moto. Kitendo cha kumaliza kumtupa Devotha tu mara alishangaa ndani ya kile chumba wakiingia watu wengi wengine wakiuzima ule moto na wengine wakionekana ni mapolisi wakiingia huku wakiongozana na baba Devotha aliokuwa nyang’anyang’a kwa kipigo. Nguo zake zilikuwa hazitamaniki kwa kulowa damu.
“Stan mwenyewe huyo hapo”
*******
Kamanda mkuu wa kikosi Rafaeli, muda wote alikuwa katika kuwasubiri mapolisi waliokuwa bega kwa bega kumtafuta kijana mdogo anayejulikana kwa jina moja la Stan. Kijana anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mfanyabiashara maarufu jijini na haswa maeneo ya mbezi luis. Kijana ambaye ilikuwa ikisemekana kuwapo maeneo ya sokoni lakini napo haikuwa hivyo alidaiwa kuwa aliondoka hapo sokoni nakuelekea na baba yake wa kufikia anayejulikana kwa jina la baba Devotha. Mapolisi walifanikiwa kumpata baba Devotha ila waliamini endapo wangemkamata baba Devotha ingekuwa rahisi kumpata Stan. Walimchukuwa baba Devotha na kumpeleka eneo walipokuwa wamemuacha kamanda wao mkuu wa kikosi,Rafaeli. Kitendo cha baba Devotha kufikishwa tu mbele ya Rafaeli akiwa amefungwa pingu mikononi. Rafaeli hakuwa na chakuuliza zaidi ya kumuwahi kwa makofi pamoja na mateke mfululizo.
“Pumbavu sana umetusumbua sana” Aliongea kamanda Rafaeli kwa ukali.
Rafaeli alijua huenda ni Stan huyo ndio aliokuwa akiwasumbua. Alimpiga ovyo ovyo mwili wote kwa fujo.
“Kwanini umeuwa? Kwanini?” Rafael aliendelea kumuadhibu baba Devotha.
“Mkuu?” Afande mmoja aliita upande wa pili.
“Na wewe nii?” Aliongea Rafaeli.
“Mkuu huyo ni baba yake na sio Stan tuliokuwa tukimtafuta?”
“Mnasemaje?”
“Stan mpaka sasa hatujampata na hajulikani aliko, ila tukiwa na huyo baba yake atatueleza jinsi ya kumpata?”
Hasira kali zikamganda kamanda Rafaeli. Hasira za kumuadhibu mtu ambaye siyo mwenyewe.
“Niliwaambia mumlete huyu au Stan?”
Kamanda Rafaeli alizidi kuwa mbogo zaidi. Alimsogelea yule afande kwa pembeni nakutaka kumpiga. Akasita!! akamrudia baba Devotha.
“Tunamtaka Stan ndani ya dakika kumi tuwe tumempata, sawa?” Aliongea kamanda Rafael.
Baba Devotha alikuwa mbishi sana. Hakujibu chochote zaidi ya kutunisha domo kwa hasira na kuzira. Kamanda Rafaeli hakuacha kumpiga, alinyanyua mguu wake nakumpiga baba devotha katikati ya mapaja yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Stan yupo wapi?”
“Sijui jamani nilimuacha sokoni”
Kamanda Rafaeli akaona haitoshi akaingia katika gari yake mbele. Akatoka na praizi ile ya kubania vitu vya chuma. Akamtanua nayo mdomo kinguvu baba Devotha na kung’ang’ania jino moja akitishia kulitoa.
“Nakuuliza Stan yupo wapi?”
“yupo sokoni nilipomuacha”
“Hapana sokoni walituambia yupo naye” Aliropoka afande mwingine pembeni.
Kamanda Rafael hakutaka mchezo kabisa. Safari hii akalivunja jino moja la mbele la baba Devotha. Damu zikaanza kusalimiana na mdomo. Zikamvuja!!
“Stan yupo wapi?” Rafael aliuliza tena.
Safari hii alilishikilia jino la pembeni kabisa ya mdomo. Jino ambalo huwa ni refu katika majino ya pembeni ya mdomo wa binadamu.
“Ngoja!!, ngoja afande nikuambie!!” Aliongea baba Devotha.
Ndio kwanza kamanda Rafael masikio yake yalikuwa kama yamepigwa pamba. Alimvuta jino baba Devotha kwa nguvu. Jino likalegea nakutaka kutoka. Akaliacha nakuamia jino la mbele bila kuhofia damu damu nyingi zilizokuwa zikiomba njia kutoka katika mdomo wa baba Devotha.
“Stan, Stan yupo wapi?”
“Yupo? Yupo? Twendeni nikawaoneshe?” Aliongea baba Devotha akilia kama mtoto.
Kibano kilikuwa cha haja. Aliona kama ukibogoyo ukiomba njia katika mdomo wake mbele ya kamanda Rafaeli. Kamwe hakutaka uchungu wote uendelee kutendeka katika mdomo wake. Alichokifanya alisema ukweli juu alipo Stan. Kuwa yupo kwake amemfungia. Kamanda mkuu Rafaeli akiongozwa na maaskari karibia wote walienda mpaka nyumbani kwa baba Devotha na walipofika kwa nje tu walishangaa kukutana na rundo la wananchi wakihangaika kuuzima moto uliokuwa umetanda ndani ya nyumba.
“Devotha yupo ndani baba muwahi?” aliongea mmoja kati ya wale wasamaria wema waliokuwa wakijitahidi kupambana na moto mkali uliokuwa umeshika nyumba haswa. Moto ambao uliwazidia nguvu wote. Moto ambao sasa ulikuwa mbele ya macho ya Sura za mapolisi wakiongozwa na kamanda wa kikosi,Rafaeli.
“Tuingie, wengine chukuwa maji katika ndoo hizo hapo pembeni na wengine chukuwa mchanga.” Aliamrisha kamanda Rafaeli.
Wale mapolisi wakafanya hivyo. Wakaweza kuuthibiti upande mmoja wa moto. wakaingia wakimtanguliza baba Devotha mbele. Wakatafuta chumba kimoja baada ya kingine. Walipofika chumba cha baba Devotha tu walishuhudia Stan akimtupia Devotha katika moto kwa lengo la kumteketeza. Hasira zilizoambatana na kwikwi zikamganda baba Devotha. Akawaoneshea mapolisi kuwa Stan waliokuwa wakimtafuta yupo mbele yao.
**********
“Sio mimi!! Hapana sijaua mimi!!” Aliongea Stan kwa kutetemeka.
Alikuwa hajitambui baada ya kushuhudia rundo la mapolisi likiwa ndani ya kile chumba cha baba Devotha. Walikuwa wamemzunguka duara. Sara alikuwa bado yupo chini hoi mwili wote ukilowa damu na amepoteza fahamu wakati Stan alikuwa akimmalizia Devotha kumtupia sehemu kulipokuwa na moto mwingi kwa kumsukumiza kwa mateke.
“Stan? Stan” Aliita kamanda wa kikosi,Rafaeli.
“Naam!!”
“Afande, mfungeni pingu haraka?” Aliamrisha Rafaeli.
Pale pale wale mapolisi hawakutaka tena kumchelewesha Stan. Walimfunga pingu Stan. Wakamchukuwa Sara na Devotha waliokuwa hawajitambui nakuwabeba juu juu mpaka nje ambapo waliwapakiza katika gari la polisi nakuelekea nao kituoni ndipo waelekee hospitali kuwatibia.
“Mnanipeleka wapi? Nawauliza wapi?” Stan alihoji kwa ukali.
“Tulia mpumbavu mkubwa wee!! ulichokifanya hukijui?”
“Sina makosa mie, nipeni Sara wangu, niacheni huru na Sara wangu”
Yale makelele yaliwachosha mapolisi sana. Walishindwa kuvumilia malalamiko ya Stan. Afande mmoja alioonesha kuchukizwa sana alitoa mdomo wa bunduki na kumpiga nao Stan kichwani. Stan akaa kimya kwa muda.
Haikuwachukua muda sana kuingia katika kituo kikubwa cha polisi.Walitia timu!! Hakikuwa kile kituo ambacho Stan aliwekwa kwa mara ya mwisho bali kwa amri za kamanda wa kikosi,Rafaeli iliwabidi kumpeleka Stan na baba Devotha kuwafungulia kesi katika kituo kikubwa cha polisi. Kutokana na ukubwa wa kesi.
“Haya shuka shuka haraka washusheni hao” Aliamrisha Rafaeli baada ya kushuka kwa upande wa mbele wa gari.
“Hao waliopoteza fahamu waacheni humo humo ndani ya gari tukitoka hapa tunaelekea hospitali kwa ajili ya matibabu yao waandikieni pf3 haraka” Aliendelea kuamrisha kamanda wa kikosi,Rafaeli.
“Hapana siwezi shuka nikamwacha Sara wangu. Kama mnaniua niueni tu? niueni nasema nipigeni risasi nife najiona na siyo kumuacha Sara wangu hapa!!” Aliongea Stan kwa kujiamini uku machozi yakiomba njia katika paji la uso wake.
“Shuka?” Aliongea afande mmoja uku akimpiga kwa mateke Stan ashuke.
“Nimesema niueni, niacheni na moyo wangu jamani hamsikiii. Niacheni na Sara wangu! kama mnataka kunifunga nifungeni na Sara wangu” Alilalamika Stan.
Mapolisi hawakuwa na tena mswalie mtume. Walimburuta kwa nguvu zote Stan aliyekuwa king’ang’anizi ndani ya lile gari. Stan aliokuwa akitaka ashuke na Sara wake. Sara yule binti kipofu. Aliona wazi endapo atamuacha Sara mbali naye akija kushtuka atateswa sana na mapolisi au jaamii kwa ujumla. Moyo wa Stan ulibaki bado kwa Sara.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Afande, namuomba Sara!! nishusheni na Sara wangu jamani!! watamuonea, jamii inamtenga? jamii inamnyanyasa, jamii inamtenda kila kukicha kipenzi cha Mungu. Sara hapendwi!! Mimi pekee ndio wakutibu matatizo yake!!” Stan aliongea uku bado akiendelea kulia.
Uchungu mkali ulimzidia Stan. Uchungu dhidi ya kushuhudia Sara akibakishwa kwenye gari na yeye kushuka. Ile ahadi aliyokuwa amempa Sara ndio ilimuuma sana moyoni mpaka rohoni. Ahadi ya kuwa na yeye karibu kwa matatizo yote. Ahadi ya kuhakikisha Sara anaishi bila manyanyaso ndio ilimuuma sana. Stan alitamani kujitoa zile pingu mkononi lakini haikuwezekana kutokana na zile pingu kutengenezwa kwa kutumia chuma kigumu. Alibaki akishuka uku shingo yake akiigeuza upande wa nyuma kumuangalia Sara wake. Sara aliokuwa amelala pasipo kuongea neno lolote kutokana na kupoteza fahamu.
Kamanda wa kikosi,Rafaeli akiongozwa na mapolisi mbali mbali walikuwa naye katika kushirikiana juu ya kesi iliyokuwa imeripotiwa pale kituoni. Juu ya kesi tata iliotokea usiku katika maeneo ya mbezi luis. Kesi ya mfanyabiashara maarufu. Kesi ambayo mapolisi walifanikiwa kumpata Stan na baba Devotha kwa ajili ya kuujua ukweli wa kesi ile.
“Wavueni mikanda na wasachini kisha waingie kwa uku nyuma” Aliamrisha Rafaeli baada ya kuifikia kaunta ya opilsi.
Ni mama mmoja tu aliokuwa akionesha kulia mpaka kukata tamaa katika kituo cha polisi. Mama ambaye alikuwa na mwenzake akimfuta machozi. Haikujulikana mapema mama huyo anapotokea au yupo pale kwa madhumuni yapi kutokana na kufika pale muda mfupi kabla wakina Stan hawajafika lakini kitendo cha Stan na baba Devotha kuwasili pale kilichukuwa sura mpya kwa yule mama. Alilia kwa sauti ya juu na kufanya kila polisi kumshangaa kwa kile kilio alichokuwa amekiangua. Kilikuwa ni kilio kile cha kukwaruza, kilio cha kukata tamaa ya kitu.
“Kwanini mmemuua jamani, kwanini” Alilalama yule mama.
Mapolisi walijitahidi kushrikiana na yule mama wa pembeni katika kumnyamazisha yule mama lakini ndio kwanza kama walikuwa wakichochea kuni kavu katika moto ulioshika sufuria.
“Niacheni, niacheeeeee, uwiiiiii mume wangu weweeeee!!” yule mama aliendelea kulia.
Wale mapolisi wote wakamgeuzia macho baba Devotha. Wote akilini walijua moja kwa moja atakuwa ni mume wake. Yule mama akatoka mbio pale uku akilia moja kwa moja mpaka kwenye gari la polisi kwa upande wa nyuma. Akaangalia upande wa nyuma. Macho yake yakagongana na miili ya mabinti wawili, Devotha na Sara.
“Uwiiiii mwanangu wewe, mwanangu nini kimekupata?” Aliendelea kulalamika yule mama kwa kulia.
Pale pale mapolisi wakaliondoa lile gari haraka na kuelekea hospitali kwenda kuwapelekea Sara na Devotha waliopoteza fahamu wote.
Safari hii alikaa chini kabisa nakuanza kutapata tapa kwa kukata tamaa ya kuishi. Mishipa ya pembeni mwa shingo yake ikiwa imemtoka haswa. Akapooza sauti!! Mapolisi walimfuata mpaka karibu yake nakumshika kwa utaratibu lakini yule mama alifurukuta na kuanza kulia upya. Mayowe!!
“Mlivyomfanya mume wangu inatosha, na hata mlichomfanya mwanangu inatosha jamani. nitaishi na nani tena, nitaishi wapi mimi, nitaishi vipi mimi?” Alio ngea yule mama kwa kigugumizi na hasira kali.
Wale mapolisi walimsogeza kwa kumlazimisha uku akilalamika mpaka karibu na kaunta ya polisi., Wakamtuliza, Akasizi!!
Walichukuwa maelezo ya kwanza kwa upande wa baba Devotha kuhusiana na familia yake na pili kuhusiana na tukio la kuhusika kumuua mfanyabiashara maarufu. Katika maelezo ya baba Devotha alikana katu katu kuhusika na hata usiku huo alijiteteta kwa kusema kuwa alikuwa na marafiki zake katika mgahawa wa kahawa na akataja mashahidi aliokuwa nao. Mapolisi waliyachukuwa maelezo yote kisha wakamweka lokapu baba Devotha na baada ya hapo wakaanza kuchukua maelezo ya Stan.
Stan hakuwa na cha kujitetea sana zaidi ya kusema alikuwa amewekwa ndani na mfanyabiashara huyo ambaye ni marehemu mchana wake na baada ya hapo alikuja kutolewa na mama msamaria mwema usiku kwa kuwekewa dhamana ya pesa na huyo mama ambaye kwa sasa ni marehemu na baada ya hapo walitoka kituoni ilikuwa giza sana na walipoteana njia na huyo mama. Kitendo cha kupoteana kwa muda njiani Stan alikiri kutokuelewa kilichomkuta huyo mama kutokana na kusikia mlio wa risasi ukitokea ndani ya gari la marehemu huyo mfanyabiashara maarufu na alimwacha Sara na kwenda kuangalia nini kimetokea.Alikutana na huyo mama ameshafariki. Damu nyingi zilizokuwa zikimtoka yule mama kifuani, damu zilizoonesha za kupitiwa na risasi nyingi zikamuingia ndani ya shati la Stan na ndio alizokuwa nazo. Baada ya kumuacha yule mama kuelekea eneo la tukio alishangaa kumkuta yule baba wa Sara akiwa marehemu.
Baada ya kuchukuwa maelezo ya haraka kwa Stan na baba Devotha waliamuru wawekwe lokapu uku. Wakamgeukia yule mama.
“Haya wee mama tukusaidie nini?” Aliongea yule kamanda mkuu wa kikosi,Rafaeli.
“Mimi ni mke wa marehemu mfanyabiashara na yule aliokuwepo katika gari ni mwanangu kabisa tuliokuwa tukiishi naye siku zote anaitwa Sara. Ni kipofu wa macho, haoni siku zote na alipotea ghafla kwenye mazingira ya kutatanisha nashangaa kumkuta akiwa na damu nyingi, amefanyaje?” Alihoji yule mama.
“Tumemkuta akiwa ndani ya nyumba ya yule mzee pamoja na yule mwenzake na huyo hapo kijana tuliotoka kuchukuwa maelezo yake. Si umemsikia akisema kuwa alikuwa naye?”
“Hapana afande huyo ni mwannagu, huyo kijana atakuwa anajua kila kitu hata kuhusu huyo mwanangu” Alianza kulalamika yule mama.
“Hapana afande, huyo ,mama mie simfahamu. na kwanza Sara aliniambia kuwa alikuwa akinyanyaswa sana na wazazi wake…
Kabla Stan hajamalizia kuongea chochote pale pale kamanda mkuu wa kikosi akahisi kitu. Akamsimamisha Stan. Stan aliokuwa bado na pingu mikononi.
“Inuka, inuka nimesema” Aliamrisha kamanda Rafaeli.
Stan aliinuka kwa kusitasita.
“Umesema wazazi wake walikuwa wakimnyanyasa sana huyo binti?”
“Ndio alivyoniambia Sara”
“Kwahiyo walivyokuwa wakimnyanyasa wee ukamchukuwa Sara?”
“Ndio afande niliona bora niwe naye karibu..
Afande akamzaba tena kibao Stan cha haja!
“Unauwezo wa kukaa na binti mdogo vile, unaweza kumuhudumia wewe? haya wazazi wake walikuwa wanamnyanyasa ukafanyanyaje ndio ukamuua baba yake si ndio?”
“Hapana afande sikumuua mimi..
Kabla Stan hajajibu tena akaongezwa kibao.
“ Si umesema katika maelezo yako ulioandika hapa uliwekwa lokapu mara ya kwanza na baba yake na huyo Sara?”
“Ndio afande”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sasa si ulikuwa ukimchukia na aliligundua hilo na ndio maana alikuweka ndani kwa ajili ya binti yake au?”
“Ndio”
“Haya basi wee ndio uliomuua hakuna tena haja ya kuzungushana hapa wakati inaeleweka moja kwa moja na maelezo yako yamejitosheleza”
“Hapana afande, sijaua mimi, sijaua kabisaaa!!”
“Umeua si maelezo yapo na umeyasema mwenyewe kuwa uliwekwa ndani na baba yake na Sara? sasa utaisaidia polisi kwa mauaji hayo na lazima uozee ndani ikibainika ni kweli umeua, Nitasimamia mpaka hatua ya mwisho, Pumbavu wee!!”
************
Jua kali liliendelea kutawala katika jiji la Dar es salaam. Jua lililosababisha kuwepo kwa joto kali ambapo kila mpita njia alikuwa hakosi kuwapo na kitambaa cha kufuta jasho mkononi ama mfukoni. Gari ndogo ya polisi aina ya ‘Land Rover’ ilikuwa ikiingia maeneo ya kituo kidogo cha kutolea afya cha masista maeneo ya mbezi Luis. Mapolisi walionekana kutokwa kwa jasho jingi sana maeneo ya usoni mwao kutokana na joto lile kali. Walikuwa wamesimama nyuma ya gari uku kwa upande wa chini yao kukiwa na mabinti wawili waliokuwa wamepoteza fahamu. Sara na Devotha. Hawakuwa wakijielewa karibu njia nzima toka wametoka katika kituo kikubwa cha polisi. Baada ya mwendo mrefu kidogo ni Sara pekee aliyeanza kuonesha utofauti baada tu ya kufikishwa na kushushwa katika kituo kidogo cha afya cha masista. Manesi walikuwa shapu kwa kuleta vitanda vya kubebea wagonjwa mahututi.
“Hawajielewi hawa wote wabebeni vizuri” Aliongea polisi mmoja baada ya kufika.
Kwa kusaidiana na manesi wa zamu waliwashusha Sara na Devotha kisha waliwapakiza katika vitanda maalumu vya kubebea wagonjwa. Walikuwa haraka sana katika kuwapatia huduma ya kuwapakiza kisha kuwakimbiza wodini.
“Wapelekeni chumba cha wagonjwa mahtuti kulee” Aliongea daktari.
Ndani ya muda mfupi walikuwa wameshawekwa pamoja katika chumba cha wagonjwa mahtuti.
“Pf3 zipo wapi za hawa wagonjwa?” Daktari aliomba kibali kutoka polisi.
“Hii hapa ya yule pale na hii nyingine ya huyu hapa!!” Aliongea polisi.
“Nahitaji manesi watatu tu na wengine kaendeleeni na kazi” Aliongea daktari.
Wale mapolisi walitoka nje na kumuacha daktari akiwa na wale manesi tayari kwa kuwaangalia wale wagonjwa. Alishika vifaa vyake vya kuvaa mikononi. Ni Sara peke yake alionesha bado kama kushtuka kidogo. Pua zake zilikuwa mapema katika kunusa nusa hapa na pale. Alikuwa ameshazinduka kutoka katika ufahamu. Hakuweza kutoa macho na kugundua yupo maeneo gani kutokana na upofu aliokuwa nao. Upofu wa kutokuwa na jicho hata moja.
“Hapa ni wapi?” Aliongea Sara kwa sauti kubwa.
“Tulia binti hapa upo sehemu nzuri tu!” Daktari alimpa maneno mazuri.
“Stan wangu yupo wapi? Stan yupo wapi?” Alilalama Sara.
Sara alisumbuana na daktari pamoja na wale manesi katika kumshika ndani ya muda mfupi toka waingie. Upofu aliokuwa nao Sara ulisababisha kutokujua maeneo alipo. Akili yake yote ilimleta huenda yupo chini ya himaya ya baba Devotha. Hakuweza kujua vizuri zaidi ya yale maumivu aliyokuwa akichomwa chomwa ovyo na Devotha kwa kutumia makucha. Makucha marefu ya kichawi. Maumivu yalimzidia kadri Sara alivyokuwa akikunja sura yake kwa ukali.
“Namtaka Stan? Staaaaaaannn!!!” Sara alilia akimtaja Stan.
Daktari yule hakuwa na jinsi zaidi ya kuwasihi wale manesi wamshike vizuri kisha akaivuta sindano yake na kuichomeka katika kichupa cha dawa ambapo alivuta dawa na kumchoma nayo Sara. Ilikuwa ni sindano ya usingizi. Sara alitapatapa!! Nguvu za ajabu zilimtawala ghafla nakujikuta akiwasukuma wale manesi karibia wote. Chalii!!
Akapapasa upande wa mezani nakuibuka na kifaa kimojawapo cha kufanyia operesheni. Kilikuwa ni kifaa cha chumachuma kwa mbele kimechongoka. Alikivuta nakumchoma. Hapo hapo nesi mmoja aliyekuwa amemsogelea karibu yake. Aliambulia kile chuma shingoni mwake.
“Kwanini mnataka mumtese Stan wangu?. Kawakosea nini?” Aliendelea kulalamaika Sara.
“Binti Stan sisi hatumjui na hapa ni hospitali umeletwa ukiwa hujitambui. Tulia basi tukutibu. Uso wako wote unadamu damu. Tulia basi ufutwe tukutibie” Aliongea daktari kwa kutetemeka akimbembeleza Sara.
Sara hakuwa na nguvu za kuweza kujibu tena. Ile sindano aliokuwa amechomwa ilikuwa tayari imeshasambaa katika mwili wake. Ilijipenyeza vya kutosha kiasi cha kumkosesha nguvu tena Sara za kutapatapa walakupiga makelele. Usingizi ulikuwa ukimlenga lenga kwa kuzubaa. Yule nesi mmoja ambaye alikuwa ameshughulikiwa na Sara kwa muda mfupi alikuwa hajiwezi. Walimuunganisha kitandani wakawa watatu nakuanza kuwatibia wote. Walianza kumfuta futa zile damu karibia zote mwilini mwa Sara. Matobo tobo na mikwaruzo ya kucha yalikuwa yameuchakaza uso wa Sara vilivyo. Uso uliokuwa na mishono miwili mikubwa maeneo ya machoni kutokana na kutolewa macho kipindi cha nyuma. Ile mishono ilikuwa imetawaliwa na kucha kucha. Kucha ndefu za kichawi kutoka kwa Devotha masaa kadhaa yaliopita.
Ndani ya muda mfupi Daktari alikuwa ameweza kumsafisha vizuri Sara uso wote na baadhi ya maeneo ya mwilini yaliokuwa yameathirika na makucha marefu.
Sehemu zilizokuwa zimeathirika sana aliziwekea dawa nyingi sambamba na pamba pamba. Hakuwa Sara yule tena kutokana na mwili wake mpaka uso kutawaliwa na pamba pamba. Alikuwa hajielewi kwa kuchomwa ile sindano ya usingizi.
“Muwekeni pale pembeni!!, mleteni huyo mwingine!” Aliamrisha dokta.
Alikuwa ni Devotha. Devotha yule aliyebadilika ghafla katika chumba chao na kutokwa na makucha marefu kiasi cha kufanikiwa kumdhuru Sara karibia uso wote. Devotha ambaye na yeye alikuwa amepoteza ufahamu. Hakuweza kujitambua hata yupo maeneo gani.
Daktari alichukuwa vipimo vyake vya kuangalia mapigo ya moyo nakumpima. Hakuweza kugundua mapema kutokana na Devotha kutokutoa pumzi yoyote. Ikambidi daktari ainamishe kichwa chake mpaka katika kifua cha Devotha kuhakikisha mapigo ya moyo kama yanaenda sawa. Kizungumkuti!! Yalikuwa yakidunda kwa shida sana. Yalikuwa si mapigo ya moyo ya binadamu wa kawaida kutokana na kudunda kwa shida tena yakidunda yalikuwa yakidunda haswa.
“Hapa kuna shida! Huyu mgonjwa anamatatizo makubwa sana!” Aliongea daktari kwa kuonesha kutoa macho kidogo.
Ubaridi wa kile chumba cha wagonjwa mahututi uliweza kumshtua Devotha kutoka katika hali ya kutokuwa na ufahamu. Kwa nguvu zile zile alizokuwa nazo kwa mara ya mwisho, zile nguvu za kichawi zikamrejea upya Devotha.
“Mnataka kunifanya nini?” Sauti mbili mbili za kike na za kiume mfululizo zilikuwa zikitoka mdomoni mwa Devotha.
“Binti embu tulia hapa upo hospitali” Daktari aliongea.
“Nimefanyaje mpaka mnilete uku, nimewakosea nini au mnataka na nyinyi niwa…
Kabla Devotha hajamalizia kuongea chochote tayari yule daktari alikuwa amefanya kama alivyomfanyia Sara. Sindano yake mkononi tayari ilikuwa imeshakubaliana na kichupa cha dawa na kuwa kitu kimoja na kuisababisha ile sindano kujawa na dawa ya kutosha. Kwa haraka haraka yule daktari alikuwa ameshaichukuwa ile sindano na kumshika shingoni Devotha akitaka kumchoma. Kitendo cha daktari kuinua tu juu ile sindano hapo hapo alijikuta kuzidiwa nguvu na Devotha. Devotha aliyekuwa na nguvu za kichawi. Alimzuia yule daktari kwa kumshika mkono wake uliokuwa na sindano kwa nguvu zote. Wale manesi wakataka kuingilia kati kwa kumshika kwa nguvu Devotha lakini hawakuweza kuambulia kitu chochote zaidi ya kurushwa kila mmoja.
“Kawaiteni wale polisi?” Aliamrisha daktari kwa kigugumizi akikohoa.
Devotha hakulijali hilo ndio kwanza aliwasogelea wale manesi waliokuwa wameambiwa wakawaite mapolisi. Wale manesi walikuwa waoga sana. Kila Devotha alipokuwa akipiga hatua ndivyo na wale manesi wakiongozwa na daktari wao walikuwa wakijitanua kwa kujisogeza kwa uoga sehemu moja wote. Devotha alimsogelea Sara nakumbeba uku akishuhudiwa na wale manesi pamoja na daktari wao. Akafungua nguo yake ya ndani nakuchomoa hirizi moja kati ya mbili alizokuwanazo katika pindo la nguo yake ya ndani. Akaibumba mdomoni na moja akamlisha Sara aliyekuwa amepoteza fahamu halafu akamfunika mdomo. Kwa nguvu za kichawi Devotha alimbeba Sara kwa mbele mpaka katika kona ya kile chumba cha wagonjwa mahtuti nakuyeyuka uku wakiwaacha Dakari na wale manesi wakihaha kwa kusikilizia maumivu na mishtuko ya mioyo yao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***********
Si baba Devotha wala Stan aliyekuwa na hasira zaidi ya kuwekwa selo katika kituo cha polisi. Wote moyoni mwao walijiona hawana makosa yoyote kuwepo pale ila ukweli kamili ulibaki moyoni mwa Stan. Stan alikuwa akijua wazi mauaji yamesababishwa na nani kutokana na mara ya mwisho kukabidhiwa bastola na yule mama msamaria mwema. Maswali mengi sana yalitawala kichwa chake. Alishajiona ni mkosaji mbele ya jamii hata baba yake wa kufikia hakutaka kumuangalia usoni kabisa zaidi ya kuumia ndani kwa ndani.
Walikuwa wamewekwa selo ya chumba kimoja na walikuwa wawili tu ndani ya chumba kimoja.
“Stan mwanangu?” Aliongea baba Devotha kwa sauti ya upole.
Stan hakuwa na cha kumjibu zaidi ya kushikwa na kwikwi na wala haikuwa kwikwi ya maji bali ilikuwa ni kwikwi ya hasira kali. Alijua wazi kuwa baba yake huyo wa kufikia ni mchawi kupindukia kutokana kwanza na kuwaficha katika chumba cha wachawi na pili kumshuhudia mtoto wake kabisa,Devotha akipata nguvu za kichawi katika kutapika hirizi kubwa kutoka mdomoni kisha kupata nguvu za ajabu katika mikono kwa kuchomoa makucha marefu ambayo yalimdhuru vibaya sana Sara.
“Hapana mie siyo mtoto wako kabisa!! tena sitaki hata kukusikia ukisema mwanangu futa kauli yako wee mzee” Aliongea Stan kwa hasira.
“Utabaki kuwa mwanangu tu kutokana na kukulea ukiwa mdogo kukusomesha mpaka kukufikisha hapo ulipo. Na nitaendelea kukuita mwanangu na nitakukukanya pale unapokosea. Mwanangu mimi naumia sana na yote umesababisha wewe mwenyewe kumbuka nyumba yangu imeshatekea kwa moto sababu ni wewe na kipofu mwenzako kile kitoto..
Kabla baba Devotha hajamalizia kulalamika alishangaa kupigwa kibao cha haja kutoka kwa Stan. Kamwe maishani Stan hakuwahi kumfokea baba yake wa kufikia wala kumtishia kwa kumpiga lakini kwa hasira kali alizokuwa nazo alijikuta akimpiga baba yake huyo bonge la kibao.
“Kwa hapo umenidharau sana na hata msichana ambaye ni mpofu tena siyo wakupenda ni matatizo ya kibanadamu unambagua na kumdharau, wee mzee fala kabisa..”Stan alimalizia kwa kutukana akiwa bado katika hasira kali.
“Stan mwanangu?” Aliita baba Devotha.
“Nimeshakwambia mie sio mtoto wako, katoto kako kachawi kapo uko kamepelekwa sijui hospitali” Aljibu Stan kwa kejeli.
“Ikifika usiku Stan utaniita tu baba. Utaniamkia kabisa na tutafanya mambo mengi na kukupeleka kwa wazazi wako kamili walipo. Nimeshindwa Stan mie sikupenda ila wazazi wako ndio waliyataka yote haya mimi kuwa hivi ngoja itimie usiku nikurudishe tu.” Alimaliza kuongea baba Devotha kwa kulalamika uku akitoa machozi na kichwa akikiinamisha chini.
*************
“Wee mzee, wewee na uchawi wako huo hapa humpati mtu?” Stan aliongea kwa kujiamini.
“Ndio nakwambia na usije kuniomba msamaha kwani hakutakuwa na hukumu ya msamaha mbele ya wazazi wako. Nimefanya utu kwa muda mrefu sana. Nimekulea lakini matunda yake ninachokipata sasa hivi naletwa polisi kwa ajili yako. Unanitishia maisha mimi baba mlezi wako? na mpaka kuungua kwa nyumba yangu chanzo ni wewe pumbavu” Baba Devotha aliongea kwa hasira.
Maneno yale ndio kwanza yalikuwa yakiingia masikioni mwa Stan nakuranda randa kisha yanarudi yalipotoka. Stan alishakuwa kama kalishwa sumu kali ya nyoka. Alishaapa hatokuja kumsamehe baba Devotha kwa vyovyote vile. Aliona ni bora wakafungwa naye tu kuliko kuishi naye huru kwenye adhabu zisizo na mpango.
Muda ulizidi kuyoyoma,mchana hatimaye giza likawadia. Giza lile la mbalamwezi.
Hakukuwa na hata ndugu yoyote aliyokuja kutoa dhamana au kujua kesi ya baba Devotha na Stan inaendeleaje. Stan alikaa na baba Devotha selo moja pamoja na baadhi ya watuhumiwa lakini ukaribu wa mashaka ndio uliowavuta pamoja. Ukaribu ule wa chura na mtoto wake wakiwa majini lakini wakiona mdudu yoyote anamuwahi. Ukaribu wa kuchukiana kwa kurushiana maneno ya ajabu na kutishiana ndio uliokuwa ukiendelea baina ya Stan an baba Devotha.
Watuhumiwa wengine walibaki kimya wakifuatilia kinachoendelea kati ya Stan na baba yake wakufikia,baba Devotha. Walikuwa katika kufuatilia tamthiliya kali ambayo kila mmoja alitamani kujua kitakachotokea usiku. Hakukuwa na makelele ya juu bali ni vicheko vya chini chini pasipo kulipia kiingilio. Vicheko vile viliwafanya hata polisi waliokuwa kaunta kuu ya kituo kutokujua kinachoendelea ndani ya selo.
“Haya giza ndio hilo limaeshaingia fanya sasa unavyotaka kufanya? fanya?” Aliongea Stan akimwambia baba Devotha. Alikuwa bado katika hasira ya hali ya juu.
“Stan, Stan utateketea sasa hivi?” Aliongea kwa ukali baba Devotha.
“Ndio nataka kuteketea lakini lazima niteketee na wewe?”
“Mimi?”
“Ndio lazima niteketee na wewe baba Devotha kubwa la wachawi wa chinichini”
“mimi mchawi siyo haya subiri nikutengeneze” Alimaliza kuongea baba Devotha.
Aliinama chini akapiga chafya ya nguvu. Alipiga mara tatu mfululizo lakini chafya ya tatu haikuwa ile chafya ya kawaida. Haikuwa chafya kama ya awali. Ilikuwa ni mchafya wa haja!! Mchafya ambao ulitoka na kitu kama hirizi ndogo ndogo iliokuwa na rangi nyeupe na nyeusi mithili ya mnyama,Pundamilia.
Ile hirizi ikatambaa chini wale watuhumiwa karibia wote wakajisogeza ukutani wakiikwepa ile hirizi ndogo. Ikametameta!!
Woga!! makelele ya chini kwa chini yakaanza kuchukuwa nafasi miongoni mwa watuhumiwa. Stan akajihisi kama kutaka kulegea mwili. Akajipa moyo konde. Ujasiri!! hofu ikampotea ghafla. Akasogea taratibu mpaka katika lile eneo ilipokuwa ile hirizi. Akataka kuishika lakini kabla hajaishika geti la selo likafunguliwa. Polisi mmoja aliokuwa na tochi kubwa akaangaza.
“Stan, Stan yupo wapi namhitaji haraka!” Afande aliita.
“Naam!”
“Toka njoo mara moja?” Aliongea yule afande.
*********
Jua la muda mrefu lilipoza kwa mara moja. hakuna aliyetaka kuamini wala kupindisha macho yake pembeni. Wote walikuwa katika kufuatilia tukio la mbele yao. Tukio ambalo nyumba iliokuwa ikitekea ilizima ghafla na mvua kunyesha eneo moja tu lililozungukwa na nyumba hiyo.
“Si nilisema mimi, niliwaambia huyu mzee ni mchawi mkabisha. Oneni maajabu ya dunia sasa kama nyumba haijajirudishia ilivyokuwa yenyewe!!” Aliongea mmoja wa watu waliokuwa wakitolea macho nyumba ya baba Devotha ikiungua.
“Hakuna!! hali ya kawaida tu hiyo. Wasomi wenzetu wanajua kila kitu kuhusu hali za hewa kama hizi”
“Wasomi? Msomi gani anayetambua kuwa nyumba inanyesha sehemu moja, wapi pameandikwa? hata vitabu vya dini hakuna sehemu iliyoandikwa hivyo. Au na wewe mchawi mwenzake nini?” Aliongea kwa kutania.
Waliendelea kuongea mashuhuda, kila mmoja akiongea lake. Wale waliokuwa wakikazana kuizima nyumba kwa maji kidogo pamoja na mchanga waliacha mara moja baada ya ile mvua ya ajabu kunyesha maeneo yale. Watu walizidi kuongezeka zaidi kuangalia maajabu.
“Mwenyewe yupo wapi?” Aliongea mzee mmoja alioonekana kutetemeka.
“Nani?”
“Mhusika wa hii nyumba baba Devotha yupo wapi?”
“Alikuja hapa akiwa na mapolisi wamemfunga pingu kwa nyuma wakaingia mpaka ndani na kutoka na watoto wake, Stan na Devotha na binti mmoja hivi”
“Wameelekea wapi?”
“Dahh kwakweli wala sifahamu lakini lazima watakuwa wameelekea polisi tu kwani walipanda gari la polisi chini ya ulinzi mkali na kuondoka nao”
Yule mzee alikuwa akitetemeka mwili wote. Alipiga kichwa chake kwa hasira kisha akanyanyua mguu wake wa kushoto nakupiga teke hewani.
“AAaaahh!!! Kwanini niliwaruhusu waondoke asubuhi yote ile?” Aliongea yule mzee kwa sauti ya chini chini na ya hasira.
Alikuwa ni yule mzee aliokuwa na Stan na Sara usiku wote. Yule mzee aliyempokea Sara na Stan usiku na kuwapatia chakula cha usiku. Mzee ambaye alikuwaga rafiki mkubwa wa baba Devotha na wakaachana urafiki wao wa damu kutokana na baba Devotha kutembea na mkewe. Mzee ambaye anaijua siri ya Stan na wazazi halisi wa Stan. Ndio yule mzee aliyemwambia Stan kuwa wazazi wake wanapatikana sokoni na tena ni vichaa wasiojielewa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sasa alikuwa amechanganyikiwa kwa alivyosikia Stan yupo mikononi mwa polisi wakiwa wote na baba Devotha na Sara yule binti kipofu. Roho yake ikamuuma sana kwa kutunza siri kwa muda mrefu. Ilimuuma kwa kutokumwambia ukweli Stan usiku ule ule juu ya baba Devotha na uchawi aliokuwa amekabidhiwa na kina Kakamega. Uchawi ambao kama baba Devotha angejivua hapo hapo angefariki. Siri hiyo alikuwa nayo mzee huyo pekee na hii ilikuwepo kabla hawajaacha urafiki wao wa karibu. Kabla hajatendwa na kuchukuliwa mke na baba Devotha.
“Hapa! hapa!, hapa!, hapa! ngoja!, ngoja!” Aliongea mwenyewe.
Alikuwa ameshaikoki akili yake sahawia. Wazo lake lilikuwa sahihi. Wazo la kwenda moja kwa moja moja kwa mchungaji maarufu kibaha. Yule mchungaji aliyomuombea Stan kipindi akiwa mdogo sana na kumtoa mashetani ya Kakamega. Mchungaji ambaye kwa mikono yake miwili aliweza kumbatiza Stan na kuanzia hapo aliweza kumbadilisha Stan na kuwa binadamu wa kawaida mwenye kufuata maadili yote.Mchungaji John.
Yule mzee aliingia kwenye daladala moja kwa moja akitokea mbezi mpaka Kibaha kwa mchungaji John. Lengo likiwa ni kwenda kumpa taarifa ikiwezekana amchukue moja kwa moja nakuelekea kituo alicho Stan na baba Devotha.
Kichwani mwake aliamini kabisa Stan asingeweza kuwa kitu kimoja na baba Devotha. Alilijua kabisa ni lazima Stan atakuwa ameshaharibu mambo kwa kujua kuwa baba Devotha alikuwa akimdanganya kuhusu wazazi wake halisi.Akili yake ikaganda wa tukio la uchawi wa baba Devotha na uko walipo huenda baba Devotha akatoboa ukweli na Wanakakamega wakamchukuwa Stan.
Siti ya kwenye dala dala aliiona chungu yule Mzee. Alikuwa akisimama na kukaa mara kwa mara bila kujielewa.
Ndani ya muda mfupi alikuwa ameshafika kibaha. Ilikuwa imeshatimu saa 03:16 alasiri. Alikuwa ameshafika nje ya geti la mchungaji John. Akabonyeza kitufe cha kengele. Kengele ikaita na punde akaja kufunguliwa.
“Shikamoo!” Aliongea binti mmoja aliokuja kufungua geti.
“Marhaba, mchungaji nimemkuta?”
“Hapana, ameelekea kwenye maombi kanisani kwake palee!!”
Hakutaka kusubiri yule mzee moja kwa moja hadi kanisani kwa mchungaji John. Ndio kwanza mchungaji alikuwa ameanza maombi. Ikambidi yule mzee asubiri nje mpaka maombi yatakapomalizika. Baada ya lisaa moja na nusu maombi yakawa yameshakwisha. Yule mzee akajionesha kanisani. Mchungaji akatoka nakumfuata.
“Za masiku baba mchungaji?”
“Salama tu za nyumbani? kwema huko?”
“Kwema tu lakini sio sana mchungaji?”
“Kunani tena? matatizo? naona jasho na hali yako si ya kawaida unahema sana vipi nini kimekusibu tena?”
“Unakumbuka yule kijana wetu tuliomuokota katika gari na baba Devotha miaka zaidi ya kumi na tano iliopita? yule hadi ukambatiza hapa kipindi tunaishi maeneo ya palee?”
“Namkumbuka sana yule kijana siwezi kumsahau maishani mwangu, Vipi kafanyaje tena?”
“Mchungaji kama unavyojua yule baba yake aliokuwa aking’ang’ania kuishi naye alikuja kuwa mchawi kupindukia. Mchawi wa kuwanga. Mchawi wa kuwageuza watu misukule kiasi cha kuchukiwa na kutengwa mtaa mzima kwa kumuogopa. Hapa alikorofishana na yule mtoto wake na ninavyokuambia lazima atamfanya vibaya nasikia wamepelekwa wote polisi”
“Polisi kisa nini ndio uchawi?”
“Hapana baba mchungaji, Yule kijana wake alikuja kwangu jana usiku sana akiwa hajielewi. Alilala kwangu tukaongea mengi sana uku akilalamika kuhusu anavyoishi na baba yake huyo, Nilimuonea huruma sana mpaka ilinibidi nimwambie ukweli juu ya wazazi wake halisi yule kijana kuwa ni wale vichaa tuliowaombea sana kipindi kile toka tuwapate kwenye gari lakini mashetani yao yalikuwa makali tukashindwa na kuwaacha. Kijana akaondoka akiwa na hasira sana. Sasa muda huu nimefika kwako nimeambiwa kijana yupo na mapolisi wameondolewa hapo kwao na wapo kituoni we unadhani uko watakuwa salama na huyo baba Devotha aliogeuka kuwa mchawi”
“Inawezekana lakini inahitaji nguvu ya bwana wetu Yesu kristo katika kumlinda na kumuongoza kijana na pia kumuondoa uchafu huyo baba Devotha”
“Nakuomba sana mchungaji twende japo ukamtie nguvu kijana nasikia wapo kituoni twende sasa tusilale leo itupite” Alimalizia yule mzee.
Mchungaji John hakuwa na jinsi zaidi ya kuelekea kwenye madhabahu yake nakuchukuwa kikopo kilichokuwa na maji ya uzima. Maji ya Baraka. Akachukua na biblia ndogo kisha akamchukuwa yule mzee nakuingia katika gari lake mwenyewe na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza rasmi.
Mwendo haukuwa mkubwa sana walifikia kituo cha polisi. Hakikuwa kituo alichokuwepo Stan na baba Devotha bali kilikuwa ni kile kituo cha awali alichokuwa amewekwa Stan.
“Huyo kijana hayupo hapa na jalada lake lilifutwa na likafunguliwa upya. Yupo kituo kikubwa cha polisi kimara mwisho kwa kesi kubwa sana.
Safari iliendelea kwa mchungaji John na yule mzee. Foleni ya hapa na pale ilizidi kuupeleka muda. Wakajikuta wakiingia kituo kikubwa cha polisi muda wa usiku kidogo. Usiku wa saa moja moja kwani na kagiza kalikuwa kameshachukuwa nafasi yake. Wakafika kituo kikubwa cha polisi kimara mwisho. Kulikuwa na mapolisi wachache waliokuwa doria. Yule mzee alikuwa ni mtu wa kwanza kushuka katika gari nakuwafuata mapolisi. Akawaomba sana juu ya mchungaji amfanyie tu Stan maombi na kumkabidhi biblia ndogo.Iliwachukuwa muda mrefu sana yule mzee kuweza kuwashawishi mapolisi kutokana na kesi iliokuwa ikimkabili Stan. Wakasanda!!
“Tupe pesa kidogo kama ni hivyo” Aliongea polisi mmoja.
“Shilingi ngapi sasa” Aliongea yule mzee.
“Si unatuona tupo wangapi? kila mmoja ela ya chakula usiku, elfu 50 inatosha”
“Dahh, punguzeni jamani kumbuka tupo kwa ajili ya maombi tu na sio kitu kingine”
“Elfu 30 lete fasta”
“Sikia, hapa hata mchungaji yule pale hajui kama natoa pesa yoyote. Na hapa mfukoni nina elfu 20 tu. Chukueni bwana nioneeni huruma nataka mwanangu awe katika imani ya bwana Yesu Kristu katika kesi yake hii. Mungu amuongoze amsimamie na amlinde kwa kesi anayokabiliwa nayo” Aliongea yule mzee bila hata kujua kesi rasmi iliokuwa ikimkabili Stan.
Tamaa!! Yule polisi aliichukuwa ile pesa kichini chini akaiweka mfukoni kisha akamwambia yule mzee amuite mchungaji pembeni yake. Wakaingia hadi meza kuu ya polisi. Stan akaenda kuitwa na polisi mmoja akiwa ameshika tochi kubwa mkononi mwake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment