Simulizi : Mimi Kabla Yako
Sehemu Ya Pili (2)
Aliingiwa na wasiwasi huku akiamini bwana Otieno angemuua mwanaye, alikuwa amemgundua mtu huyo kwani aliwahi kumfanyia kitendo kisicho cha kibinadamu. Alichanganyikiwa zaidi alipoiona picha ya David jambo lililomfanya aiangalie picha hiyo kila wakati. Hakuamini hata kidogo kama mtoto huyo aliyempiga na risasi mbili kwa mkono wake kisha kwenda kumtupa ndani ya ziwa Victoria, alikuwa hai. Kuna wakati akiwa katika ofisi yake hiyo alihisi labda alikuwa anaota.
Todzo hakuelewa jambo lililokuwa linaendelea zaidi ya kuomba apewe fedha zake. BwanaAbraham hakutaka kijana huyo ajue jambo ambalo alilihitaji lifanyike usiku wa siku hiyo hivyo akimwondoa shaka alimwamuru muhasibu wa kampuni yake amwandikie hundi ya milioni ishirini kijana huyo. Akiwa na furaha baada ya kuandikiwa hundi hiyo, Todzo aliondoka akiwa amepewa onyo kuwa asimwambie mtu juu ya taarifa aliyokuwa ameitoa. Lengo kubwa la bwana Abraham lilikuwa ni kuhakikisha usiku wa siku hiyo anafanikisha zoezi la kumuua David na bwana Otieno Ndakufurila. Baada ya kuondoka kwa Todzo, bwanaAbraham alipiga simu kwa kiongozi wa kundi la Eastern Black Killers aliyejulikana kwa jina la Mswadzu. Alimweleza kiongozi wa kundi hilo nia yake ya kuhakikisha bwana Otieno Ndakufulira na David wanauawa siku hiyo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walielewana vizuri na kiongozi wa kundi hilo lililokuwapo eneo la Mbarara, kilomita chache kutoka eneo la Beshenyi ambako bwana Otieno, David na mwanaye walikuwapo. Baada ya makubaliano hayo ikiwa ni pamoja na malipo, majira hayo ya saa moja bwanaAbraham alipewa jukumu moja. Alielezwa atume picha za watu hao watatu kwa njia ya mtandao, walihitaji kumjua mwanaye ambaye hakupaswa kuuawa na zaidi Otieno Ndakufurila na David waliopaswa kuuawa. Bila kupoteza muda akiwa na haraka huku akihitaji kuona watu hao wanauawa. BwanaAbraham aliongoza kwenye gari lake na kulitoa kwa kasi katika ofisi zake kiwandani hapo. Alikuwa amebeba picha pia alizopewa na Todzo. Lengo lake lilikuwa kuelekea nyumbani kwake ili kukamilisha zoezi hilo la kutuma picha hizo. Hilo liliwezekana kwa vile alikuwa na chumba chake cha kusomea ambacho kilikuwa na kompyuta na kila aina ya kifaa cha kuafanikisha zoezi hilo huku akiwa ameunganisha mtandao pia. Baada ya dakika arobaini na tano aliegesha gari lake mbele ya nyumba yake kabla ya kuanza kutembea kwa kasi akielekea ndani. Mkewe alikuwa sebuleni huku akiwa na mawazo na zaidi akiwa hajui jambo lolote juu ya hatma ya mwanaye.
BwanaAbraham alimsalimia mkewe huku akionekana mwenye haraka aliongoza hadi katika chumba chake cha kujisomea. Bila kupoteza muda alizichukua picha alizokuwa nazo na kuzihamishia chapa zake katika kompyuta aliyokuwa nayo. Alitumia picha tatu tofauti, moja ikiwa ya David, nyingine ya bwana Otieno Ndakufurila lakini pia ikiwapo ya mwanaye Sabinus. Picha hizo alizoandika maelezo chini yake alizituma kwenye anuani ya barua pepe ya kiongozi wa kundi la Eastern Black Killers bwana Mswadzu. Alifanikisha zoezi hilo kwa haraka huku lengo haswa likiwa ni kuhakikisha bwana Otieno na David wanauawa. Alitabasamu kidogo akiamini alikuwa amemaliza kazi, alichukua simu yake na kumpigia kiongozi wa kundi hilo akiwa na nia ya kumwambia tayari alikuwa amezituma picha hizo.
“I need to see the dead body of respective guys but still don’t hurt anyway my son” (“nahitaji kuona maiti za watu husika lakini pia msimuumize mwanangu”) Alisikika bwanaAbraham mara baada ya simu yake kupokelewa na kutoa taarifa juu ya picha alizokuwa ametuma.
“Ok! The deal begins, I`m going to switch off my phone then it will be in air after this simple massacre” (“Sawa! Kazi inaanza, nazima simu yangu na itakuwa hewani mara baada ya mauaji haya rahisi”) Alisikika upande wa pili wa simu bwana Mswadzu kabla ya kukata simu.
BwanaAbraham alionesha furaha juu ya kila jambo lililokuwa likiendelea, alizima komputa yake kabla ya kuanza kutembea akielekea sebuleni kwake akiwa na furaha kiasi tofauti na alivyokuwa awali. Jambo hilo lilimfanya mkewe amuulize furaha aliyokuwa nayo ilitokana na nini. Bwana Abraham hakuongea kitu zaidi ya kumpa mkewe picha zote alizokuwa amepewa na bwana Todzo. Mkewe akiwa amechanganyikiwa alihitaji maelezo juu ya picha hizo za watu ambao wote aliwafahamu akiwapo mwanaye. BwanaAbraham bila kuficha alimweleza kila jambo mkewe mpaka wakati huo ambao tayari alikuwa ametuma picha za watu hao katika kundi la Eastern Black Killers ili bwana Otieno Ndakufurila na David wauawe. Mkewe alikuwa amepata mshtuko huku akishangaa kuona David alikuwa hai ilhali aliamini mtoto huyo alitupwa katika ziwa Victoria akiwa ameuawa na mumewe. Alipoitazama picha ya Otieno Ndakufurila, moyo wake ulishtuka huku akikumbuka mambo kadhaa yaliyokuwa yamejili juu ya mtu huyo. Mkewe pia akiwa amempuuzia Otieno na David alikuwa na shauku ya kutaka kuuona ujumbe ulioambatana na picha hizo ambao tayari ulikuwa umetumwa kwa wauaji hao ili wafanye kazi yao.
Bwana Abraham akiwa na furaha kidogo alianza kuongoza katika chumba chake cha kusomea ambako mara baada ya kufika hakupoteza muda, kwani aliiwasha kumputa aliyokuwa ameitumia. Baada ya zoezi hilo alifungua anuani yake ya barua pepe kabla ya kuelekea katika eneo la ujumbe uliokuwa umetumwa. Huko ndiko walikohisi kufa, kwani ni kweli ujumbe huo ulikuwa umetumwa huku picha mbili chini yake zikiwa zimeaandikwa “kill him” (“muueni”) na moja ikiwa imeandikwa “Don’t kill him”(“msimuue”). Jambo lililowachaganya ni picha ya David ambayo chini yake iliandikwa “msimuue” badala ya ile ya Sabinus. Jambo hilo alikuwa amelifanya Bwana Abraham kutokana na haraka alizokuwa nazo wakati akituma picha hizo. Alikuwa amewahurusu watu hao wamuue bwana Otieno Ndakufurila na mwanaye Sabinus. Akiwa amechanganyikiwa alichukua simu yake na kujaribu kumpigia kiongozi wa kundi la Eastern Black Killers bwana Mswadzu ili amwambie wamuue David badala ya Sabinus. Alichanganyikiwa zaidi baada ya kugundua simu ya kiongozi huyo ilikuwa haipatikani kama alivyosema kuwa angeizima kwa ajili ya shughuli ya kuua.
BwanaAbraham na mkewe wakiwa wamechanganyikiwa walibaki wakizunguka zunguka ndani ya nyumba yao wakiwa hawana jambo la kufanya. Bwana Abraham hakuwa na namba nyingine ya simu ya watu wa kundi hilo zaidi ya ile ya Mswadzu. Akiwa hayuko sawa aliirudia komputa yake na kutuma ujumbe mfupi tena kwenye anuani ya kundi hilo. Alikaa kwa muda wa nusu saa akisubiri lakini hakukuwa na majibu yoyote yaliyorudishwa. Jambo hilo ndilo lilimfanya aamini tayari watu wa kundi hilo walikuwa wameenda kufanya kazi yao ya kuua. Wakati huo mkewe alikuwa ameishiwa nguvu akiwa amejilaza sakafuni katika sebule ya nyumba yao hiyo. Baada ya masaa kama matatu huku akiwa kama amenyeshewa na mvua kutokana na jasho lililomtoka kama maji, alipata wazo. Aliwaza kupigia simu kituo cha polisi ili kuwaeleza kama kulikuwa na wahalifu waliotaka kufanya mauaji katika kijiji hicho cha wavuvi wa eneo la Bushenyi.
Bwana Abraham alizidi kuchanganyikiwa baada ya simu hiyo aliyoipiga kuita kwa muda mrefu pasipo kupokelewa. Akiwa hana mwelekeo simu yake ilipokelewa baada ya dakika arobaini na tano. Askari aliokuwa anaongea nao walikuwa wa jiji hilo la Entebbe, bila kupoteza muda aliwaeleza kuwa alikuwa amepata taarifa juu ya watu waliotaka kufanya mauaji katika kijiji cha wavuvi eneo la Bushenyi. Askari walimwelewa baada ya maelezo marefu ila walimwambia kuwa walihitaji kuongea na askari wa eneo la Mbarara ambao walikuwa karibu na eneo la tukio. Bwana Abraham aliwaelewa na hivyo alitulia ili kusubiri taarifa ambayo angepewa kutoka kwa askari hao. Baada ya saa moja walimpigia simu na kumwambia kuwa bado walikuwa wakiendelea na jitihada za kuwataarifu askari wa eneo la Mbarara, hiyo yote ilitokana na mfumo mbovu wa mawasiliano uliokuwepo wakati huo. Jambo hilo lilimfanya bwanaAbraham achanganyikiwe kabisa kwani masaa mengi yalikuwa yamepita na hivyo alianza kuamini uwezekano wa mwanaye kuuawa. Aliishia kujilaza sakafuni akiwa hana nguvu kama mkewe huku moyoni akiwa ameanza kuamini mwanaye angeuawa.
* * * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mswadzu alikuwa kiongozi hatari akiwa na mafunzo ya kutosha ya kijeshi. Kutokana na ujira mdogo wa mshahara kutoka serikalini aliamua kuachana na kazi ya jeshi na kwenda kuanzisha kundi lake la shughuli haramu. Jambo hilo lilifanikisha majaribio ya mauaji hata ujambazi kutokana na ujuzi aliokuwa nao akiwa na vijana wake wa Eastern Black Killers. Mara baada ya kupokea kazi aliyoiona ndogo kutoka kwa mtu tajiri bwanaAbraham, alielekea mpaka kwenye anuani yake ya barua pepe kabla ya kuchapicha picha alizotumiwa kwa kuzihamishia katika karatasi. Majira ya saa tatu usiku magari mawili ya kundi lake hilo yalikuwa katika kasi yakielekea katika kijiji cha Bushenyi. Alikuwa ameongozana na vijana wake watano huku akiwa ameweka muda wa masaa matatu wa kukamilisha zoezi hilo. Njiani alikuwa akiangalia picha ambazo moja wapo iliandikwa chini yake mtoto husika asiuawe. Picha aliyoamini ilikuwa ya mtoto wa bwanaAbraham. Yeye na kundi lake akili zao hazikuwa sawa wakati huo na ilikuwa rahisi kwao kumuua mtu yeyote ambaye angekuwa hana hatia, kwani walikuwa tayari wametumia dawa za kulevya. Walitawaliwa na mtazamo wa kuua tu huku wakiwaza kuendelea na zoezi la ujambazi mara baada ya kazi hiyo waliyoiona ndogo.
Majira ya saa sita usiku magari yao yaliwasili katika kijiji hicho cha Bushenyi huku eneo hilo likiwa tulivu. Kelele kidogo zilikuwa zikisikika katika eneo la mbali kidogo ambako kulikuwa na watu waliokuwa wakiendelea kunywa pombe za kienyeji. Wakati wakiendelea kutafakari nini cha kufanya huku magari yao yakiwa yamezimwa taa katika eneo hilo lililokuwa na giza kiasi. Walimshuhudia mlevi mmoja akiwa anayumbayumba akielekea katika eneo walilokuwapo. Mswadzu alichukua bastola moja kutoka kwa kijana wake na kujiweka sawa kumkabili mlevi huyo. Hatimaye alivyokaribia alimvamia na kumpiga kabali shingoni huku akiwa amemwelekezea bastola yake kwenye paji lake la uso. Mlevi huyo hakushtuka zaidi ya kuanza kutukana akiwa haelewi jambo lililoendelea. Kijana mmoja wa Mswadzu aliwasha tochi waliyokuwa nayo na kufanya eneo hilo lionekane vizuri huku wakimshtua mlevi huyo.
“We don’t want to kill you, but just take us to Otieno Ndakufurila`s house” (“hatuhitaji kukuua, lakini tupeleke katika nyumba ya Otieno Ndakufurila”) alisikika Mswadzu akimweleza mlevi huyo ambaye fahamu zilimrudia ghafla mara baada ya kuona eneo hilo halikuwa na usalama hata kidogo. Watu hao walikuwa na bunduki huku mmoja wao akionekana ameshika magunia mawili.
Bila kupoteza muda, mlevi huyo alianza kuwapeleka kwenye nyumba ya bwana Otieno huku nyuma yake akiwa ameonyeshewa bunduki za aina tofauti zilizoshikwa na vijana wa Mswadzu. Akitembea kwa kuyumba yumba alikuwa akitetemeka pia haja ndogo ilikuwa imeshapenya na kufanya suruali yake ionekane imeloa. Wakiwa katika umakini wa kutosha walipita katika nyumba nyingi za watu masikini wa eneo hilo kabla ya kuifikia nyumba waliyoelezwa kuwa ilikuwa ya Otieno Ndakufurila. Walimweleza yule mlevi waliyekuwa naye akae chini asubirie kuhurusiwa, jambo ambalo alililtekeleza. Wakati huo kulikuwa na tochi nyingine zilizokuwa zimewashwa, vijana wawili wa Mswadzu waliurukia kwa mateke mlango wa nyumba hiyo na baada ya muda mfupi ulifunguka. Bwana Otieno Ndakufurila alikuwa wa kwanza kutoka katika nyumba hiyo akiwa haelewi jambo lililokuwa linaendelea. Alikuwa amevaa bukta moja iliyokuwa chafu huku pia ikiwa imechanika chanika. Sehemu nyingine ya mwili wake ilikuwa wazi huku akiwa na makovu kama vile alikuwa ameungua na moto.
Mara baada ya kutoka alionesha mshtuko huku akiwa amegundua jambo ambalo lingeendelea wakati huo lingekuwa kuuawa. Vijana wa bwana Mswadzu walimvamia na kumpiga mateke mfululizo kabla ya kumwelekeza akae eneo la pembeni kidogo na yule mlevi. “Hey! You the Bastard, where’s Sabinus and David?....” (“wewe mwanaharamu, wako wapi Sabinus na David?”) alisikika Mswadzu akimuuliza Otieno aliyekuwa analia na kutetemeka. Mswadzu akiwa na hasira alirudia tena swali hilo ambalo halikujibiwa kwa mara ya pili na Otieno. Aliwaeleza vijana wake wamshushie kipigo bwana Otieno, jambo lililoanza kuchukua nafasi. Walianza kumpiga kila sehemu ya mwili wake na baada ya sekunde kadhaa alikuwa akitokwa na damu sehemu tofauti za mwili wake. Ghafla walishtushwa na kelele za David na Sabinus waliotoka ndani wakilia huku wakiwaomba vijana hao waache zoezi hilo la kumpiga bwana Otieno.
Mswadzu aliwaeleza vijana wake wamfunge na kamba David miguu na mikono, jambo lililotekelezwa na mtoto huyo aliwekwa sehemu ya peke yake. Sabinus aliwekwa sehemu moja na bwana Otieno Ndakufurila huku wote wakionekana wakitetemeka kupindukia. Mswadzu alicheka kidogo kabla ya kuchukua bunduki aina ya AK 47 kutoka kwa kijana wake. Aliikoki vizuri bunduki hiyo na kuielekeza kwenye paji la uso wa bwana Otieno Ndakufurila, kelele za David zilisikika akipinga jambo lililotaka kuendelea ila alishindwa kutoka eneo alilokuwapo kwa vile alifungwa kamba. Sabinus alikuwa kama ameishiwa nguvu kwani alikuwa ametoa macho, hali hiyo ilikuwa hivyo pia kwa mlevi aliyekuwa kando kidogo. Bila huruma Mswadzu alimmiminia risasi tatu bwana Otieno kwenye paji lake la uso na kumfanya Sabinus azimie muda huo huo akiwa haamini. Kijana mlevi akiwa hofu pia tayari alipata hisia za kuuawa kama jambo ambalo lilikuwa limemtokea Otieno, hivyo alionekana akiwa hajatulia. David aliongeza kelele za kulia baada ya tukio hilo lakini Mswadzu na vijana wake walimpuuzia huku wakionekana kama hawana mpango naye. Mswadzu aliwaamuru vijana wake wamuweke kwenye gunia bwana Otieno jambo lililotekelezwa haraka.
Mswadzu alimgeukia Sabinus na kumpiga risasi tatu za kifuani, na yeye pia aliamriwa awekwe kwenye gunia baada ya zoezi hilo akiwa ameshafariki. Wakati huu David alikuwa halii kwani naye pia aliishiwa nguvu baada ya kuona kifo cha binamu yake huyo na mwishoe alizimia. Vijana wa Mswadzu walianza kumuweka Sabinus kwenye gunia pia. Wakati zoezi hilo likiendelea, kijana mlevi alikurupuka na kuanza kukimbia akiamini angefuata. Akiwa mita kadhaa toka eneo hilo alipigwa na Mswadzu risasi moja mgongoni iliyompelekea aishie kuanguka chini. Kwa kasi ya ajabu vijana wa hao wa Eastern Black Killers walianza kuyaburuza chini magunia hayo yaliyokuwa yameloa damu. Mmoja wao alikuwa amembeba David huku kiongozi wao akiwa wa kwanza wakielekea katika eneo walilokuwa wameegesha magari yao.
Kulikuwa na kelele za watu wakipiga yowe baada ya kusikia milio ya risasi lakini Mswadzu aliendelea kupiga risasi hewani jambo lililowafanya watulie katika makazi yao. Baada ya dakika tano walikuwa wameyafikia magari yao, huku mwili wa Otieno ukiwekwa kwenye moja ya gari ilhali wa Sabinus ukiwekwa kwenye gari jingine pia. David alipakizwa eneo la mbele la gari mojawapo huku wakiwa wanampepelea ili azinduke. Magari hayo yaliondolewa kwa kasi eneo hilo, safari ikiwa imeanza wakiwa wanaelekea Mbarara ambako yalikuwapo makao ya kundi lao. Baada ya kuendesha magari yao kwa kasi kwa umbali wa kilomita kama ishirini na tano walikutana na magari matatu ya polisi ambayo yalikuwa yakiendeshwa kwa kasi kuelekea eneo la Bushenyi walikokuwa wametokea. Hawakujali jambo hilo huku wakiamini uwezekano wa kutolewa taarifa juu ya mauaji waliyokuwa wameyafanya.
Majira ya saa tisa usiku magari yao yalikuwa yakiegeshwa katika katika msitu mdogo ambako kulikuwa na makao makuu ya kundi lao. Eneo hilo lilikuwa mbali kidogo kutoka kwenye makazi ya watu wa jimbo hilo la Mbarara. Wakati huo Mswadzu alikuwa akiwaza pesa tu, ni muda ambao hata David tayari alikuwa amezinduka akiwa hana nguvu na mtulivu, walikuwa wamemfungua kamba walizomfunga. Mswadzu alihitaji safari kuelekea jijini Entebbe ianze usiku huo ili siku hiyo hiyo waweze kuchukua malipo yao nyakati za mchana. Hivyo alihitaji mwili wa bwana Otieno na Sabinus uhamishiwe kwenye majeneza ili wasafirishwe kama maiti zilizokuwa zikielekea katika jiji hilo. Hakupata taabu kwani vijana wake wengine alishawapatia kazi ya kuandaa majeneza hayo. Miiliya Otieno na Sabinus ilihamishiwa katika majeneza hayo yaliyokuwapo. Baada ya zoezi hilo, liliandaliwa gari jingine aina ya Land Cruiser ambalo majeneza hayo yalipakizwa. Mswadzu akiwa na vijana wake wawili walianza safari nyingine na gari hilo wakiwa wameongozana pia na David. Baada ya nusu saa, gari lao lilikuwa katika kasi likiiacha ardhi ya sehemu hiyo ya Mbarara. Muda wote David alikuwa kama hana akili nzuri kwani alikuwa kimya akiamini angeuawa pia ndani muda mfupi uliokuwa umesalia. Jambo lililokuwa gumu kwake kulielewa lilihusiana na kuuawa kwa Sabinus. Akiwa anaamini kila jambo lililoendelea lilikuwa chini ya baba yake mkubwa bwana Abraham, alimchukia mtu huyo huku akiamni kuwa hana huruma hata kidogo kwani ndiye aliyewahurusu watu hao kuua. Kichwani aliona ni bora afariki kwani watu alioamini walikuwa ndio ndugu zake kwa wakati huo wote walikuwa wamefariki.
* * * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Abraham na mkewe walikuwa wamechanganyikiwa kwa kiasi kikubwa huku wakiamini kuwa tayari mwanao alikuwa ameuawa. Hiyo yote ilifuata baada ya taarifa walizopata toka kituo cha polisi zilizoeleza kuwa askari wa Mbarara walichelewa kufika eneo la tukio na kukuta wahusika wakiwa wameshauawa na miili yao haikuwapo eneo la tukio. Jambo hilo ndilo lilimfanya aamini kuwa tayari mwanaye alikuwa ameuawa. Alikuwa chumbani kwake akiwa na mkewe huku wote wakilia, hakuwa na hamu hata ya kujaribu kumpigia simu Mswadzu kwani aliamini mtu huyo angemkamilishia machungu juu ya taarifa ya kifo cha mwanaye. Jambo hilo ndilo lilimfanya aamue kuzima simu yake muda wote wa siku hiyo huku mlinzi wa nyumbani kwake akiwa amepewa agizo la kutomhurusu mtu yeyote kuingia.
Muda wote mkewe alikuwa akimlaumu mumewe juu ya zoezi aliloamini lilikuwa la kipuuzi kwani alifanya uzembe wa kuhurusu mwanao auawe badala ya kuuawa kwa David. Majira ya saa nane mchana ni wakati ambao bwana Abraham alipata ujasiri kidogo akiwa anaamini kama mwanaye ameuawa hakuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kuyakubali matokeo. Wakati huu alitaka kuhakikisha kama kweli hisia zake juu ya kifo cha mwanaye zilikuwa ni za kweli. Aliamua kuwasha simu yake akiwa na lengo la kumpigia Mswadzu ili amuulize juu ya jambo lililokuwa linaendelea mpaka wakati huo. Sekunde kadhaa baada ya kuiwasha simu yake, alishtuka kidogo baada ya simu hiyo kuanza kuita, alipoangalia jina la mpigaji aligundua alikuwa Mswadzu.
Alibakia akiiangalia simu yake huku akiogopa kupokea, iliita mpaka mwisho lakini hakuthubutu kuipokea. Mswadzu alipiga kwa mara ya pili na hapo ndipo bwana Abraham alijikaza na kuipokea, baada ya salamu Mswadzu alimtaka waonane haraka katika ofisi zake zilizokuwa katika kiwanda cha nguo cha bwana Abraham. Baada ya maelezo hayo Mswadzu alikata simu, bwana Abraham alijaribu kumpigia akihitaji kujua juu ya watu aliowaua lakini simu yake pia ilikuwa haipatikani ghafla. Jambo hilo lilimpa hisia bwanaAbraham za kuamini mtu huyo alikuwa ameshazima simu. Akiwa amechanganyikiwa juu ya imani aliyokuwa nayo kuwa mwanaye alikuwa ameuawa, alitoka nyumbani kwake akikimbia akiwa na ufunguo wa gari na kuelekea katika gari lake aina ya Mercedez Benz. Aliingia kwenye gari hilo kabla ya kuliwasha na kuliondoa kwa kasi eneo hilo la nyumbani kwake.
Mkewe alimshuhudia bwanaAbraham akitoka kwa kukimbia nyumbani kwao hapo, hakuna alilolifanya zaidi ya kuendelea kulia akilitaja jina la mwanaye Sabinus akiamini tayari alikuwa ameuawa. Bwana Abraham aliendesha gari kwa kasi na baada ya dakika kadhaa alikuwa amefika katika eneo la kiwanda chake. Bila kupoteza muda aliongoza mpaka eneo la mapokezi ambako alienda kumkuta bwana Mswadzu, kiongozi wa kundi la Estearn Black Killers aliyekuwa akimfahamu.
“Where are they? Aah! Had you killed my son? Tell me Mr!” (“Wako wapi? Aaah! Ulimuua mwanangu? Niambie”) Alilalama bwana Abraham katika eneo hilo la mapokezi lililokuwa na wafanyakazi wake kadhaa. “Calm down Mr. Abraham this isn’t right place to talk, he’s alive and everything is perfect”(“tulia bwana Abraham hii siyo sehemu muafaka ya kuongea, ni mzima na kila kitu kiko sawa”) Alimjibu Mswadzu huku akisimama kumfuata. Bwana Abraham alishtuka kidogo baada ya kugundua kuwa eneo hilo lilikuwa na wafanyakazi wake kadhaa. Alimwambia Mswadzu amfuate, huku akitokwa jasho alitembea haraka akiongoza kuelekea katika ofisi yake. Baada ya sekunde kadhaa walikuwa katika ofisi hiyo. Mswadzu hakuhitaji mazungumzo ya aina yeyote zaidi pesa alizokuwa ameahidiwa kupewa. Alimweleza bwana Abraham akamilishe malipo yake kabisa ili mambo mengine yaweze kuchukua nafasi ikiwa ni pamoja na kupelekwa eneo ambalo alikuwa amewahifadhi watu alioelezwa awaue pamoja na mwanaye bwana Abraham akiwa hai. Baada ya kubishana kwa muda mfupi bwana Abraham aliamua kukubaliana na ombi hilo, alimuita muhasibu mkuu wa kiwanda chake na kumweleza amwandikie Mswadzu hundi ya milioni ishirini na tano za Uganda kama walivyoahidiana.
Muhasibu huyo hakupoteza muda zaidi ya kuandika hundi hiyo aliyokabidhiwa Mswadzu. Muda wote wakati zoezi hilo likiendelea bwanaAbraham alikuwa akitokwa na jasho, lakini pia alikuwa akitetemeka huku akiwa hatulii katika ofisi yake hiyo. Baada ya kukabidhiwa hundi hiyo Mswadzu alimweleza bwana Abraham amfuate. Waliongoza mpaka nje katika eneo la maegesho ya magari na kupanda katika gari la bwana Abraham kabla ya kuondolewa kwa kasi kwa gari hilo. Kulikuwa na utulivu wa kutosha ndani ya gari hilo huku bwanaAbraham aliyekuwa kwenye uskani akisikiliza maelezo ya Mswadzu. Alikuwa akiendesha gari hilo huku akiwa na hali ya hofu iliyoonekana wazi. Mswadzu hakutaka kuongea jambo zaidi na bwana Abraham huku kichwani akiwa ametawaliwa na fikra za kuamini alikuwa ameifanya kazi ya mteja wake huyo ipasavyo.
Baada ya saa moja la kuwapo barabarani kwa kasi ya ajabu bila kufika sehemu husika bwana Abraham akiwa na hasira aliuliza eneo walilokuwa wakielekea. Mswadzu alimtoa hofu huku akimwambia kuwa walikuwa wamekaribia sehemu husika waliyokuwa wakielekea. Baada ya dakika kadhaa walikuwa katika eneo la mashamba ya miwa yaliyokuwapo katika eneo la Kamengo lililopo Kusini - Magharibi mwa jiji la Entebbe. Wakati huo ilikuwa yapata saa kumi na moja na nusu jioni, bila kupoteza muda bwana Abraham alisimamisha gari kama alivyokuwa ameelezwa. Eneo hilo lilikuwa na giza kidogo kutokana na miwa iliyokuwa imestawi vizuri ikiwa imepandwa kila upande wa barabara hiyo lakini pia eneo hilo lilikuwa tulivu na hakukuwa na dalili za kuwapo kwa mtu yeyote. Kulikuwa na sauti za ndege waliokuwa katika mashamba hayo, bwanaAbraham alibaki kimya huku akiwa haelewi jambo ambalo lingefuata. Mswadzu alichukua simu yake na alionekana kama alimpigia mtu, baada ya sekunde kadhaa alionekana akiongea na kijana wake akimweleza afike eneo walilokuwapo na bwana Abraham.
Walibaki kimya huku wakitazamana lakini bwanaAbraham akiwa na hofu kupindukia, baada ya dakika kadhaa lilifika gari moja aina ya Land Cruiser ambalo liliegeshwa pembeni kidogo na eneo walilokuwapo. Walishuka vijana wawili wa kundi la Eastern Black Killers na kwenda kusimama mbele yao, Mswadzu aliwaoneshea ishara ambayo waliielewa. Waliongoza mpaka upande wa nyuma wa gari hilo na kuanza kutoa majeneza, Walitoa jeneza la kwanza kabla ya kuanza kuliburuza mpaka eneo walilokuwa wamesimama bwana Abraham na Mswadzu. Walielekea upande wa nyuma wa gari hilo kwa mara ya pili na wakati huu walirudi wakiburuza jeneza la mtu aliyeonekana alikuwa mtoto. Bwana Abraham hofu iliongezeka na alianza kuishiwa nguvu kadri sekunde zilivyoendelea, Mswadzu alimkonyeza kijana wake akiashiria afungue jeneza lililoonekana ni la mtu mzima. Kijana mmoja alilisogelea na kufungua jeneza hilo, bwana Abraham alishtuka kidogo aliposhuhudia mwili wa Otieno Ndakufurila akiwa amefariki huku mwili huo ukitoa harufu. Kijana wa Mswadzu alilifunga jeneza hilo na mfuniko wake. Akaanza kulisogelea jeneza la mtu aliyeonekana kuwa ni mtoto, kadri alivyozidi kulisogelea, bwana Abraham alikuwa akitetemeka kupindukia huku akiwa amelitolea macho.Kichwani bado alikuwa anaamini kuwa huenda mwanaye alikuwa hai. Kijana huyo alilifunua jeneza hilo na mwili wa Sabinus ulionekana, hapo ndipo bwana Abraham aliishiwa nguvu na kuanguka chini, baada ya sekunde kadhaa alikuwa amepoteza fahamu.
Ndani ya jeneza alikuwapo mwanaye Sabinus akiwa amefariki ambaye pia mwili wake ulikuwa ukitoa harufu. Mswadzu na vijana wake hawakuelewa jambo lililokuwa linaendelea. “Where’s that little child” (“yuko wapi yule mtoto”) Alisikika Mswadzu akimuulizia David aliyeamini alikuwa mtoto wa bwana Abraham.
“He’s inside the car, I think he’s sick because he hasn’t eaten since yesterday” (“yupo ndani ya gari, nadhani anaumwa kwa sababu hajala toka jana”) Alijibu kijana mmoja.
“Take him out!... immediately”(“mtoeni nje… haraka”) Alipaza sauti Mswadzu na ndani ya sekunde kadhaa David alitolewa nje akiwa ameishiwa nguvu. Aliburuzwa na vijana hao wawili wa Eastern Black Killers waliomshika mabega mpaka eneo alilosimama Mswadzu.
Walikuwa wameingiwa na hisia wakiamini kuwa inawezekana walikuwa wamemuua mtoto ambaye hakupaswa kuuawa. Hivyo walianza kumuuliza David jinsi alivyohusiana na Bwana Abraham. Lengo lao hilo halikufanikiwa hata kidogo kwani David hakuwajibu na alionekana kama mtu aliyekata tamaa akiwa tayari kwa kifo. Mawazo yake yalitawaliwa na hisia akiamini kuwa duniani hakuwa na ndugu zaidi ya Otieno Ndakufurila na Sabinus ambao tayari walikuwa wamefariki. Aliona ni bora auawe ili ajumuike nao baada ya kupata karaha za muda mrefu zilizosababishwa na baba yake mkubwa, bwanaAbraham. Zikiwa zimepia dakika kama tano tangu azimie bwanaAbraham huku David akiwa hawapi ushirikiano wa maswali yao, walishtushwa na mngurumo wa magari yaliyoonekana yalikuwa mbali sana lakini yalielekea eneo walilokuwapo. Mswadzu aliwakonyeza vijana wake na walitoka wakikimbia na kuelekea katika gari lao aina ya Land Cruiser, mara baada ya kuingia kwao liliwashwa na kuondolewa kwa kasi eneo hilo. Hawakuwa na hofu huku wakiamini walikuwa wametekeleza kazi yao kama walivyokuwa wameelezwa.
David alikuwa mtulivu kwa muda huku akiwa amekata tamaa kabisa, ghafla alipata msukumo wa haraka akilini na moyoni mwake pia. Kuna kitu kilimsukuma na kumpa imani kuwa wakati huo ndio ulikuwa muda muafaka wa kumuua bwana Abraham. Msukumo huo ulimpa imani ya ghafla ya kuamini bwana Abraham alipaswa auawe kama alivyowatuma watu waliomuua Sabinus na Otieno zaidi familia yake. Mambo hayo yaliyomjia kwa haraka kichwani mwake, alikumbuka jinsi alivyonusurika kufariki katika ziwa Victoria baada ya kupigwa risasi na na kutupwa kwenye maji ya ziwa hilo kabla ya kuokolewa na marehemu Otieno Ndakufurila. David alisimama huku mkono mwake wa kulia ukishika bega lake la kushoto katika eneo lililokuwa na kovu la risasi na hapo hasira zilizidi zaidi huku aliwaza kuua. Aliamini jambo hilo lilikuwa linawezekana kwani wauaji waliokuwa wameondoka aliwasikia wakisema bwanaAbraham alikuwa amezimia.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alikimbia haraka na kulifuata gari la bwanaAbraham aina ya Mecedez Benz lililokuwapo eneo hilo. Alielekea eneo la uskani wa gari hilo kisha alifungua buti baada ya kufanya hivyo kwa kasi alielekea eneo la nyuma la gari hilo. Bila kupoteza muda aliifungua buti ya gari hilo kabla ya kuliona boksi la vifaa vya gari, lengo lake lilikuwa kupata kifaa chenye ncha kali ili amchome nacho bwana Abraham. Hakufanikiwa kukiona kifaa chenye ncha kali zaidi ya spana moja ya matairi ya gari hilo iliyokuwa na muundo wa msalaba. Aliamua kuichukua spana hiyo kabla ya kuanza kuelekea eneo alilokuwapo bwanaAbraham. Wakati akielekea eneo hilo alisikia mngurumo wa magari yaliyoonekana kuwa karibu kabisa na eneo hilo, hakujali hata kidogo. Alimsogelea bwanaAbraham na bila huruma aliinyanyua spana hiyo kabla ya kumpiga nayo kwa nguvu kichwani. Hasira ndizo ziliongezeka akiwa hana huruma kabisa, aliinyanyua kwa mara ya pili spana hiyo na kumpiga tena bwanaAbraham, wakati huu ncha moja ya spana hiyo ilizama katika jicho la kushoto la tajiri huyo na kufanya damu ianze kumtoka kama maji.
David alianza kuin`gan`ganiza spana hiyo itoke katika jicho hilo ili aendelee kumpiga lakini haikutoka. Ilikuwa imeingia sawasawa katika jicho hilo na kuliharibu kabisa. Damu iliyoruka kutoka kwenye jicho hilo ilianza kumfikia David katika nguo alizokuwa amezivaa, hakujali na alikuwa akiizungusha spana hiyo kila upande ili itoke bila mafanikio. Kwa mbali bwanaAbraham alionekana kama alitupatupa mikono kutokana na maumivu aliyoyapata, ghafla magari mawili ya mizigo yalionekana yakijongea eneo hilo. David alishtuka na kuyashuhudia magari hayo, alipandwa na hasira akiamini zoezi lake lilikuwa limeingia dosari. Alisogea kando kidogo tayari kwa kukimbia, lakini kabla hajafanya hivyo aliwaza jambo, alirudi eneo alilokuwapo bwanaAbraham kwa kasi aliishishindilia ile spana ndani ya jicho la tajiri huyo akitumia unyayo wa mguu wake wa kulia. Baada ya kufanya hivyo alitoka akikimbia na kuingia katika mashamba hayo ya miwa yaliyokuwapo eneo hilo.
Alikimbia kwa kasi huku akiamini watu hao wangedhania ni yeye aliyehusika na taswira nzima iliyokuwapo eneo la tukio. Moyoni alikuwa na amani kidogo ya kumpiga bwana Abraham huku akimini jambo moja la kumpofoa jicho la kushoto tajiri huyo. Bado alikuwa na hasira dhidi ya kifo cha familia yake, binamu yake Sabinus na zaidi mtu aliyeokoa maisha yake aliyemtegemea kama baba na mama yake bwana Otieno Ndakufurila. Akiwa amekimbia kwa muda wa dakika kama kumi alitulia kidogo kwenye mashamba hayo ya miwa huku akiwa na hofu, siyo hofu ya kukamatwa bali pia hofu ya nyoka ambao aliwahi kuelezwa na marehemu baba yake kuwa walikuwa wengi kwenye mashamba hayo ya miwa. Akiwa anahema kwa taabu alisikia vishindo vya watu wakikimbia kuelekea eneo alilokuwapo ambao walionekana walikuwa wakisukuma miwa kila upande ili kupata njia kama alivyokuwa anafanya.
Hakupoteza muda kwani alielewa kuwa walikuwa wakimfuata yeye alianza kukimbia tena kwa kasi akielekea mbele katika shamba hilo la miwa lililokuwa kama msitu. Alikimbia kwa muda wa zaidi ya dakika ishirini pasipo kusikiliza kama watu waliomfukuzia walikuwa wakimfuata. Mwishoe akiwa amechoka sana alijitupa katikati ya shamba hilo la miwa huku akiwa tayari kwa lolote ambalo lingeweza kutokea. Wakati huo katika shamba hilo kulikuwa na giza kama usiku huku majira hayo yakiwa kama saa moja kasoro ya usiku. David alibaki ametulia huku akisikiliza uwezekano wa watu waliokuwa wakimfukuzia kufika eneo alilokuwapo. Alitulia kwa muda wa dakika kama ishirini katika eneo hilo huku akiwa hajasikia mtu yeyote akimfuata. Ghafla alisikia vishindo vya watu wakijongea eneo alilokuwapo, alitaka kukimbia ila alitulia baada ya kuamini kuwa angewajulisha kama alikuwa karibu pia.
Watu hao walitembea na kwenda kusimama karibu yake kwa umbali kama wa mita tano, hakuwaona kwani wakati huo ilikuwa giza kupindukia, alisikia wakiongea huku wakionekana kushindwa kuendelea na kazi hiyo kutokana na giza.
“Lets go back to the police station, there we will provide all information about this killer” (“tuelekee kituo cha polisi huko tutatoa taarifa muhimu juu ya muuaji huyu”) Alisikika mmoja wao taarifa iliyompa faraja David aliyewasikia wakiongea.
Alibaki ametulia akisikia vishindo vyao wakiondoka, ghafla alishtushwa na kitu kilichomgonga kwenye mguu wake wa kushoto kama vile sindano. Alitaka kupiga kelele kwa maumivu hayo lakini alijikaza kwa vile watu waliokuwa wakimtafuta hawakuwambali sana. Alihisi maumivu kadri sekunde zilivyozidi kwenda jambo hilo lilimfanya aelekeze mkono wake kwenye mguu huo wa kushoto. Kabla hajashika eneo husika alishtushwa na kitu kilaini alichokigusa, alipokipapasa vizuri aligundua alikuwa nyoka aliyeanza kutoweka eneo hilo alilokuwapo. David alibaki mtulivu huku akitetemeka kupindukia lakini hofu yake ikiwa zaidi juu ya kupiga kelele na kugundulika. Nyoka huyo alijiburuza juu ya mguu wake huku akionekana kama alikuwa akielekea sehemu. Hatimaye hakupata hisia za nyoka huyo mguuni mwake. Alinyanyuka haraka na kufungua kamba ya kiatu kimoja kabla ya kuifunga kamba hiyo upande wa juu na eneo alilokuwa amegongwa na nyoka huyo. Akitumia nguvu zake zote aliikaza kamba hiyo huku akiwa anaelewa madhara ya sumu hiyo kama alivyowahi kufundishwa na walimu wake ambayo haipaswi kusambaa mwilini.
Baada ya zoezi hilo hakusikia tena kelele za vishindo vya watu waliokuwa wakimtafuta na tayari mguu wake ulianza kuvimba eneo la chini alilofunga ili sumu hiyo isipite. Hakuwa na amani na eneo hilo hivyo alianza kunyanyuka taratibu akiwa na lengo la kuondoka eneo hilo. Wakati akianza kutembea kwa taabu kuondoka, alishtuka na kujitupa upande wa mbele wa eneo hilo baada ya mguu wake wa kulia kuzama kwenye shimo aliloamini lilikuwa la nyoka. Alisimama tena kwa mara ya pili huku akianza kutembea kwa taabu zaidi akitetemeka.
Baada ya dakika kadhaa alishtushwa na barabara iliyokuwa karibu na upande huo aliokuwa akiukimbilia wakati akifukuzwa. Wakati huu alikuwa amechoka sana na alihisi tayari sumu ilikuwa imeanza kufanya kazi. Mguu wake wa kushoto ulikuwa umevimba sana, akiwa hana nguvu aliwaza kujitahidi kufika katika barabara hiyo na kujilaza huku akiamini angepatikana mtu wa kumsaidia. Alijitahidi kutembea na baada ya dakika kadhaa alikuwa amejilaza barabarani akiwa hana matumaini. Alikuwa hana nguvu hata kuweza kunyanyua hata mkono huku akiwa na maumivu makali ya mguu, baada ya sekunde kadhaa alipoteza fahamu.
Baada ya nusu saa lilionekana gari moja dogo la kutembelea lililoandikwa Kamengo Sugar Cane Plantation Co. Ltd ambalo lilikuwa likitumia njia hiyo aliyokuwa amjilaza David. Hatimaye gari hilo lilijongea na kuegeshwa kando yake kidogo. Alishuka mzungu mmoja kwenye gari hilo aliyeonekana akiongea peke yake. Mara baada ya kumsogelea David na kumchunguza akiwa na tochi yake mkononi, aligundua jambo kabla ya kumbeba na kumpakia kwenye gari lake kisha aliliwasha na kuliondoa kwa kasi eneo hilo.
* * * *
Wafanyakazi wa magari ya kubeba miwa wa kampuni ya Kamengo Sugar Cane Co. Ltd ndio walikuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio lililokuwapo na miili ya watu wawili waliouawa pamoja na mtu waliyemtambua kama tajiri mkubwa nchini Uganda. Alikuwa bwanaAbraham aliyekuwa hana fahamu na zaidi alikuwa na spana ya gari iliyoshindiliwa sawasawa katika jicho lake la kushoto huku damu nyingi ikimtoka. Vijana hao sita waliokuwa watatu kila gari la kampuni hiyo iliyokuwa inahusika na miwa walishtushwa na mtoto mdogo waliyeamini alihusika na mauaji hayo ambaye alikimbia na kuzamia katika mashamba hayo ya miwa. Jambo walilofanya ni kumweleza dereva mmoja kati ya wawili waliokuwapo ampeleke bwana Abraham katika hospitali kuu ya jiji la Entebbe. Walimweleza pia atoe taarifa kituo cha polisi juu ya kila jambo lililokuwapo eneo hilo. Bila kupoteza muda dereva huyo aliwasha gari la bwanaAbraham lililokuwapo eneo hilo huku likiwa limeachwa funguo zake katika eneo la uskani.Aliligeuza gari hilo kabla ya kuondoka na bwana Abraham ambaye walimtoa spana jichoni.
Kijana mwingine kati ya hao sita alibakia eneo hilo akiwa na maiti lakini pia alikuwa akilinda magari ya kampuni hiyo. Vijana wengine waliingia wakikimbia kwa kasi katika shamba hilo la miwa wakiwa wa imani ya kumkamata mtoto waliyeamini alikuwa muuaji. Wakiwa na hofu pia juu ya mtoto huyo walikuwa wakitembea pamoja katika jitihida hizo za kumtafuta huku wakiwa na zana tofauti mikononi mwao. Mpaka majira ya saa moja jioni walikuwa wameshindwa kufanikisha lengo lao hivyo wakaamua kurudi eneo la tukio hilo. Walipofika katika eneo hilo tayari kulikuwa na askari kadhaa waliokuwa wakichukua maelezo kutoka kwa kijana mwenzao, nao waliungana naye kuelezea kila jambo walilokuwa wameliona.
Walitoa maelezo yao wakiamini mtoto aliyekuwapo eneo hilo kama alikuwa siyo muuaji basi alikuwa anahusiana kwa kiasi kikubwa na wauaji. Baada ya maelezo hayo ya awali askari waliondoka na maiti hizo mbili huku wakiahidi kuendelea na upelelezi zaidi na walitegemea kupata maelezo kutoka kwa bwanaAbraham aliyekuwa hospitali wakati huo. Utata ulioanza kuonekana dhahiri ulihusiana na uchunguzi waliobaini kuwa watu hao walikuwa wameuawa siku mbili au moja iliyokuwa imepita.
Majira ya saa nne usiku bwana Abraham alirudiwa na fahamu lakini jambo lililomshtua ni maumivu aliyokuwa akiyapata katika upande wa jicho lake la kushoto na kichwa kwa ujumla. Alishtushwa pia na rafiki zake kadhaa waliokuwa wakimwangalia kwa huruma waliokuwa kando ya kitanda alichokuwa amelazwa. Akiwa bado hajaongea kitu alielekeza mkono wake haraka katika jicho lake la kushoto na kugundua lilikuwa limefungwa na pamba za hospitali. Akiwa hajatulia vizuri huku rafiki zake wakiwa wamemsogelea na kuanza kumfariji, alikumbuka mwili wa mwanaye akiwa ameuawa aliouona mara ya mwisho katika jeneza. Kumbukumbu hizo zilimfanya aanze kulia kwa sauti kama mtoto mdogo, alikuwa akikumbuka mambo mengi mfululizo yaliyoashiria ugumu wa kumpata mtoto mwingine na mke wake.
Jambo hilo lilimfanya alie huku akijibamiza huku na huko, rafiki zake walimtuliza na mwishoe alitulia baada ya muda mrefu wa kulia. Madaktari kadhaa waliokuwa wakimhudumia walifika katika kitanda alichokuwa amelala na waliwaeleza rafiki zake waondoke wakidai walihitaji kuongea na bwanaAbraham. Alibakia kimya huku akipata maumivu makali sana katika jicho lake la kushoto ambalo hakujua lilikuwa limepatwa na tatizo gani, lakini pia hakujua madaktari walitaka kuongea naye juu ya jambo gani? Daktari mmoja aliyejitambulisha kwa jina la William akiwa ndiye daktari mkuu wa macho alianza kwa kumpa pole bwanaAbraham kwa tatizo alilokuwa amelipata. Baada ya maelezo hayo ya awali alimweleza kuwa hawakuwa na uwezo wa kuokoa jicho lake hilo la kushoto hivyo walikuwa wakimsubiri azinduke ili ikiwezekana awaruhusu wamweke jicho la bandia. Bwana Abraham alilia kwa uchungu huku akishika eneo la jicho lake hilo la kushoto, alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Hasira zake ziliongezeka huku akiwaza kumuua mtu aliyehusika kupotezea kiungo chake hicho muhimu.
Wakati huo hasira zake alikuwa amezielekeza kwa kiongozi wa kundi la Eastern Black Killers, bwana Mswadzu aliyeamini alihusika na tukio hilo. Akiwa pia haelewi hatma ya David kwa wakati huo, alipanga kuhakikisha mtoto huyo anafariki ndani siku chache baada ya kupona kwake. Alipanga kuhakikisha Mswadzu anamuua pia kwani aliumia sana juu ya mtu huyo aliyemuua mtoto wake pekee ingawaje yeye ndiye alikosea kutoa maelezo. Baada ya siku nne alikuwa amewekwa jicho la bandia akiwa anaona kwa jicho moja tu la kulia. Siku hii ndiyo aliyoenda kujumuika na familia yake pamoja na mkewe aliyekuwa kama mwehu katika zoezi zima la kumzika mwanao pekee Sabinus. Mbali na maumivu aliyokuwa nayo Bwana Abraham alijikaza na kushiriki katika siku hiyo iliyokuwa ngumu kwake. Wakati huo alipata taarifa za kuwa Otieno Ndakufurila alikuwa amezikwa na jeshi la polisi baada ya kukosa mtu ambaye alikuwa ndugu yake na kuweza kuuchukua mwili wake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mazishi hayo ya mwanaye, bwanaAbraham akiwa na majonzi nyumbani kwake huku akiendelea na matibabu alipata taarifa iliyomshtua kuwa mtu aliyeharibu kiungo chake muhimu alikuwa David. Taarifa hiyo aliipata toka kwa kijana mmoja wa kampuni ya Kamengo Sugar Cane Plantation Co. Ltd aliyekuwa miongoni mwa vijana waliomwona David akihangaika kuitoa spana ya gari katika jicho la bwanaAbraham. Hasira alizozipata hazikuelezeka huku akiwa ametoa taarifa kwa jeshi la polisi kuwa David, ambaye alidai kuto mfahamu jina alikuwa miongoni mwa vijana wa kundi la Eastern Black Killers. Lengo lake kubwa alihitaji jeshi la polisi limrahisishie kazi ya kumkamata Mswadzu na kundi lake zaidi David akiwa na lengo la kuwaua.
Hakukuwa na mazungumzo yeyote yaliyokuwa yakiendelea kati ya bwanaAbraham na mkewe aliyemchukia mumewe huyo ghafla. Hakushangaa jambo hilo huku kichwani akiwaza mambo mengi ambayo hayakuwa na jibu kuhusu suala la mtoto. Hiyo ilitokana na suala zima la uzazi lililohusiana na mkewe kwani hakuwa na uwezo wa kuzaa tena, yaani alikuwa mgumba. Miaka kadhaa iliyokuwa imepita mwanamke, huyo mara baada ya kumzaa marehemu Sabinus alipata matatizo makubwa ya kiuzazi jambo lililopelekea daktari aliyehusika naye ashauri mwanamke huyo afunge kabisa kizazi ili kuokoa maisha yake. Jambo hilo halikupingwa na bwanaAbraham kutokana na upendo aliokuwa nao kwa mkewe na zaidi kwa mwanao. Hivyo mkewe alikuwa amefungwa kizazi, miaka zaidi ya kumi iliyokuwa imepita na suala la mtoto mwingine lilikuwa limepotea kabisa vichwani mwao. Siku zote Sabinus alikuwa kiunganishi cha familia hiyo lakini ghafla alipotea na jambo hilo lilimchanganya zaidi mkewe Abraham akiamini mwisho wake wa kuwapo katika ndoa hiyo ulikuwa umefika.
* * * *
David alishtuka majira ya saa tatu asubuhi akiwa hospitali huku pembeni wakiwa wamekaa wauguzi kadhaa. Wakati huo hakusikia maumivu yeyote zaidi ya eneo alilogongwa na nyoka ambalo kwa mbali alihisi maumivu. Baada ya sekunde kadhaa aliwauliza wauguzi hao juu ya mtu aliyemfikisha hospitalini hapo kwani mara ya mwisho alikumbuka alikuwa akijikongoja kujongea katika barabara iliyokuwa kando ya mashamba ya miwa. Swali hilo lililoeleweka alijibiwa na muuguzi mmoja kuwa kuna mzungu mmoja wa kampuni ya Kamengo Sugar Cane Plantation Co.Ltd ndiye aliyekuwa amemfikisha eneo hilo. Alielezwa kuwa mtu huyo ndiye ambaye alikuwa ameshamlipia fedha za matibabu huku akiwa ametoa ahadi ya kufika siku hiyo ili kwenda kumjulia hali na zaidi alihitaji ukweli juu ya matatizo aliyokuwa ameyapata.
David aliyaelewa maelezo hayo lakini kichwani aliwaza kukimbia eneo hilo la hospitali ndogo iliyokuwapo Kamengo ambayo ilitumiwa zaidi na wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakati huo alikuwa bado akifikiria jinsi ambavyo angekimbia kwa vile wauguzi hao walikuwa karibu naye muda wote. Alikuwa anaamini kuwa wauguzi hao walikuwa wamepewa fedha za kutosha jambo lililowafanya wawe karibu naye huku wakionyesha kumjali. Majira ya saa nne asubuhi alifurahi kuletewa kifungua kinywa huku ikiwapo na mikate ya kutosha. Hiyo yote ilitokana na njaa aliyokuwa nayo, alikuwa hajala kwa siku nzima iliyokuwa imepita jambo lililopelekea hata tumbo lake kutetemeka.
Kichwani aliwaza kutoroka mara baada ya kupata kifungua kinywa, hata wakati wa kutekeleza zoezi hilo la kupata kifungua kinywa alikuwa makini huku akizungusha macho yake kila upande. Baada ya dakika kadhaa alimaliza zoezi hilo akiwa anawaza jinsi ya kutoroka mara simu ya muuguzi mmoja iliita kisha akaipokea na alisikia jinsi maongezi hayo yalivyoendelea yaliyowataka wauguzi hao wasimhurusu David kuondoka. Jambo hili lilimpa hisia kuwa tayari mambo yalikuwa mabaya, alihisi uwezekano wa taarifa zake kumfikia bwanaAbraham na zaidi askari. Aliwaomba wauguzi wake hao aelekee chooni, hawakubishia ombi hilo huku wakimwambia mzungu aliyemfikisha hospitali hapo alikuwa njiani kuelekea eneo hilo. Alionyeshwa upande uliokuwa na vyoo vya wagonjwa wa kiume. David alianza kutembea huku akiwaza kukimbia muda huo katika Hospitali hiyo. Baada ya sekunde kadhaa alikuwapo eneo la chooni huku akizungusha macho huku na kule akiwaza jinsi atakavyoweza kutoroka. Akiwa katika mawazo hayo huku akizunguka alifanikiwa kuuona mlango uliokuwa ukitenganisha vyoo vya kike na vya kiume ambao ulikuwa wazi. Bila kupoteeza muda alipita upande huo wa pili wa vyoo vya kike kabla ya kuwashtua watu kadhaa waliokuwa wakijisaidia. Wengine walishindwa kujizuia kwani walimtukana huku wakiwa na jazba na kumwona alikuwa hana heshima. David hakujali hilo akiwa na umakini mkubwa alifanikiwa kutoka upande wa pili wa wodi la wanawake na kwa haraka alianza kutembea kuelekea eneo la nje la hospitali hiyo. Wakati akijaribu kutoka alishtuka baada ya kuliona gari la polisi likiegeshwa katika eneo la mbele la hospitali hiyo. Aliwashuhudia kwa umbali askari watatu wakishuka katika gari hilo wakiwa wameongoza na mzungu mmoja. Tayari alielewa kuwa mambo yalikuwa yameharibika.
Aliwasubiria watu hao waliotembea na kuzamia upande uliokuwa wa wodi la wanaume, hapo ndipo alipotoka akikimbia kuiacha hospitali hiyo. Wakati akikimbia alikuwa na hofu ya kuitwa jambo lililomfanya akimbie kwa kasi pasipo kugeuka nyuma. Baada ya dakika tano alikuwa mbali na eneo la hospitali hiyo huku akianza kuingia katika mitaa ya watu walioishi karibu na hospitali hiyo. Moyoni bado alikuwa na ujasiri na kuamini huo ulikuwa mwanzo wa mapambano. Jambo lililomuudhi ni suala zima la kushindwa kwake kumuua bwana Abraham kutokana na watu waliotokea wakiwa na magari. Akiwa anaamini alikuwa amelipoteza jicho moja la baba yake huyo mkubwa bado alikuwa na imani juu ya uwezo wake wa kumuua mtu huyo aliyeipoteza familia yake zaidi Otieno Ndakufurila aliyekuwa mlezi wake. Aliumia pia juu ya kifo cha Sabinus aliyekuwa binamu yake lakini hasira ziliongezeka kila alipokumbuka kuwa bwanaAbraham alihusika na kifo hicho cha mwanaye. Wakati huo alianza kuingiwa na hisia akiamni huenda watu waliotumwa kumuua walikosea na kumuua Sabinus. Hilo aliliamini ghafla kutokana na upendo alioufahamu wa bwana Abraham na Mkewe kwa mwanao Sabinus.
Mzungu aliyekuwa miongoni mwa mameneja wa Kamengo Sugar Cane Plantation Co. Ltdakiwa na askari waligundua baada ya muda mfupi kuwa mtoto waliyemfuata hospitalini hapo alikuwa amekimbia. Jambo hilo liliwaongezea hisia wakiamini mambo waliyokuwa wameelezwa kuwa mtoto huyo alikuwa miongoni mwa watu wa kundi la Eastern Black Killers. Walihakikisha hilo kwa vile pia mtoto huyo walielezwa kuwa alikuwa amempofoa jicho tajiri mkubwa nchini Uganda bwana Abraham baada ya kumpiga na spana ya matairi ya gari. Hawakuwa na jambo la ziada zaidi ya kuondoka huku askari wakiwa wamepanga kuendelea na msako dhidi ya mtoto huyo.
* * * *
Todzo akiwa mpiga picha ambaye aliwapiga picha bwana Otieno Ndakufurila, Sabinus pamoja na David na kuzipeleka picha hizo kwa bwanaAbraham. Alikuwa na furaha kupindukia baada ya kupewa fedha zake milioni ishirini za Uganda. Furaha aliyokuwa nayo ilihusiana na suala zima la kuamini kuwa alikuwa miongoni mwa matajiri. Alichokifanya alielekea katika jimbo la Mbarara na kununua nyumba ya kawaida iliyokuwa na vyumba vitatu na mara baada ya zoezi hilo alinunua gari dogo aina ya Suzuki la kutembelea. Wakati huo hakumfikiria tena bwanaAbraham wala bwana Otieno na watoto wawili aliowapiga picha. Hakufikiria madhara yeyote ambayo yaliweza kutokea kutokana na picha alizokuwa amewapiga kina Otieno na kwenda kuzikabidhi kwa bwana Abraham kabla ya kupewa fedha hizo zilizobadilisha maisha yake.
Baada ya wiki moja ya kufurahia mafanikio yake hayo, alisafiri na rafiki yake aliyekuwa akimfundisha kuendesha gari na wakielekea Bushenyi katika kijiji cha wavuvi alikoishi katika maisha yake yote ya awali. Lengo haswa lilikuwa kwenda kuonesha mafanikio aliyokuwa ameyapata kwa wakati huo. Alipofika huko alienda kupata mshtuko baada ya kuelezwa juu ya mauaji ya kutisha yaliyofanyika usiku wa siku aliyopokea malipo ya kupeleka picha kwa bwanaAbraham. Mauaji hayo yaliyokuwa dhidi ya familia ya bwana Otieno na mwanakijiji mmoja yalimpa hisia tofauti kwani alikumbuka mara ya mwisho alielezwa na bwanaAbraham kuwa asimweleze mtu juu ya picha alizokuwa amezipeleka. Uchungu waliokuwa nao watu juu ya mauaji hayo ulimwingia hata yeye na alijikuta akitaka kuujua ukweli wa jambo hilo zaidi. Hisia zake zilianza kumfikiria vibaya bwanaAbraham kwani awali wakati akipeleka picha hizo aliamini mtu huyo alikuwa akimtafuta mwanaye lakini suala la mauaji wakati huu lilimtisha.
Aliamua kumpigia simu bwana Abraham na kumuuliza juu ya mauaji hayo yaliyokuwa yametokea. Tajiri huyo alisita kuelezea jambo hilo kabla ya kumtaka Todzo amfuate katika ofisi zake zilizokuwapo jijini Entebbe baada ya siku mbili. Todzo alimwelewa kabla ya kuwaita wanakijiji kadhaa na kuwaeleza kuwa angeutafuta ukweli wa vifo vya watu wa familia hiyo ya bwana Otieno. Wanakijiji hao walimwamini kutokana na maendeleo aliyokuwa nayo wakati huo lakini hakuthubutu kuongelea jinsi alivyoziuza picha alizopiga kwa bwanaAbraham ambazo zilibadili maisha yake. Hatimaye Todzo aliondoka na kurudi eneo la Mbarara huku kichwani akiwaza kutimiza ahadi ya kukutana na bwanaAbraham. Akilini alijihisi alihusika na mauaji hayo jambo lililopelekea nafsi yake kumsuta na kuhitaji kuujua ukweli wa vifo vya familia ya Otieno Ndakufurila.
Bwana Abraham akili yake ilikuwa haijatulia huku akiwaza kuua tu, mtu aliyewaza kuanza kumuua alikuwa bwana Mswadzu kwani aliamini hawezi kuishi bila kuitoa roho ya mtu huyo. Ingawaje yeye ndiye aliyetoa maelezo kwa makosa na kupelekea mtu huyo amuue mwanaye lakini wakati huu aliwaza kumpoteza pia. Alipanga kuanza na Mswadzu kisha aendelee kumfuatilia David kwa vile mtoto huyo hakujua eneo alilokuwapo na zaidi aliamini kuwa alihitaji maandalizi ya kutosha juu yake. Aliamua kumpigia simu na kumpongeza Mswadzu kwa kazi aliyoifanya na alimwomba afike jijini Entebbe akiwa amemuahidi kumpa kazi nyingine. Mswadzu alikubaliana na maelezo ya bwana Abraham na aliahidi kufika jijini Entebbe siku husika waliyoelewana.
Tayari bwanaAbraham alikuwa na furaha moyoni mwake akiamini mwanzo wa malengo yake ulikuwa umeanza kuchukua nafasi. Wakati akiendelea na maandalizi ya kuhakikisha anamuua Mswadzu alipata kikwazo kidogo, kwani alipigiwa simu na mpiga picha bwana Todzo. Kijana huyo alionekana akifanya udadisi juu ya kifo cha bwana Otieno na mwanaye Sabinus. Bwana Abraham aliingiwa na hasira juu ya kijana huyo ambaye picha zake hazikutoa matunda yoyote zaidi ya kusababisha kifo cha mwananye. Aliwaza kumjumuisha kijana huyo katika mauaji aliyopanga kumfanyia Mswadzu. Hivyo alimpa ahadi ya kufika jijini Entebbe siku moja na Mswadzu ili awaue wote. Alikuwa akihofia pia uwezekano wa kijana huyo kutoa siri katika jeshi la polisi juu ya mambo machache aliyokuwa anayafahamu kuhusiana na picha na zaidi mauaji yaliyokuwa yametokea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bwana Abraham ambaye muda wote alikuwa haongei na mkewe aliendeleza tabia yake ya ulevi huku akilala katika mahoteli tofauti na wakati mwingine alikuwa akilala ofisini kwake. Tayari alikuwa ameingiwa na hisia za kuachana na mkewe kwa vile alijielewa kwamba alikuwa mwanaume kamili aliyeweza kumpata mtoto kwa mwanamke mwingine. Alikuwa ameandaa kundi lake la mauaji dhidi ya Mswadzu na Todzo ambayo alipanga yaende kufanyika katika eneo la ziwa Kyoga. Hatimaye siku husika aliyopanga kufanikisha mauaji hayo dhidi ya watu hao ilifika. Mswadzu ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika katika ofisi ya bwanaAbraham majira ya saa kumi jioni. Mara baada ya kuingia katika ofisi ya tajiri huyo alimwona bwana Abraham akiendelea kunywa pombe ofisini kama hana akili nzuri. Alikuwa amevaa miwani ambayo haikuhurusu Mswadzu kuona macho ya bwanaAbraham, alifanya hivyo ili asigundulike kama alikuwa na jicho moja la kulia lililofanya kazi huku akiwa na jicho bandia la kushoto.Kabla ya kuanza kwa maongezi bwanaAbraham alimuuliza Mswadzu aina ya pombe aliyohitaji.
Mswadzu ambaye pia alikuwa mlevi alimjibu bwana Abraham ambaye alichukua simu yake na kuonekana akimpigia mtu ili alete bia aina ya Bell iliyokuwa maarufu nchini Uganda ambayo Mswadzu alieleza kuwa aliihitaji. Baada ya dakika moja aliingia dada mmoja na bia hizo za kopo zaidi ya tano, alimfungulia Mswadzu moja wapo na alianza kunywa. Walianza maongezi yao pia huku wote wakinywa pombe ya aina moja, wakati huo bwanaAbraham hakumweleza kazi ambayo alimwitia ili ampatie. Alikuwa akimpongeza Mswadzu kwa kazi aliyokuwa ameifanya na walikuwa katika maongezi ya kawaida huku moyoni akimchukia mtu huyu kupindukia. Baada ya dakika kumi wakati Mswadzu akiwa ameanza kunywa kopo la pili la bia hiyo, macho yake yalionekana dhahiri yalikuwa mazito kama vile mtu aliyehitaji kulala wakati huo. Hali hiyo iliendelea kadri dakika zilivyozidi kwenda, alijitahidi kujizuia asilale lakini ilishindikana, kwa mbali bwanaAbraham alionekana akitabasamu baada ya kuelewa zoezi lake alilofanya lilianza kufanya kazi.
Baada ya dakika kadhaa Mswadzu alianguka na kulala kabisa sakafuni katika ofisi hiyo. Bwana Abraham akiwa anatabasamu aliwaapigia simu vijana wake akiwataka wafika katika ofisi hiyo. Baada ya mfupi waliingia vijana wanne waliokuwa na misuli na vifua vipana, wakiwa warefu lakini pia walikuwa weusi sana. Walipoingia hawakuongea jambo zaidi ya kumchukua Mswadzu na kumweka kwenye gunia walilokuwa nalo. Walimbeba kwa pamoja na kuanza kutembea wakielekea nje na nyuma yao aliwafuata bwana Abraham ambaye alikuwa bado hajalewa. Waliongoza mpaka nje na kumpakiza Mswadzu kwenye buti la gari moja kati ya magari mawili aina ya Land Cruiser yaliyokuwapo. Eneo hilo la nje pia kulikuwa na vijana wengine wanne wa bwanaAbraham ambao walikuwa kimya wakimsikiliza bosi wao.
“We’re waiting for Todzo, the cameraman, after that only killing will take place” (“tunamsubiri Todzo, mpiga picha baada ya hapo ni mauaji tu yatachukua nafasi”) alisikika bwanaAbraham, wakati huo alikuwa na msokoto wa bangi aliokuwa akiuvuta huku akiwa amezungukwa na vijana wake. Alikuwa ni mtu ambaye hakuwa na upendo hata kidogo wakati huo huku akiwaza kuua tu. Hakuwa na hofu juu ya ujio wa Todzo kwani tayari alikuwa amemtaarifu kwamba alikuwapo jijini Entebbe. Bwana Abraham aliwaamuru vijana wake waingie kwenye gari na wajiandae kwa ajili ya safari hiyo ya mauaji aliyopanga yakafanyike katika ziwa Kyoga. Baada ya nusu saa, gari moja dogo la kutembelea aina ya Suzuki liliwasili katika eneo hilo la kiwanda hicho cha nguo cha bwanaAbraham. Gari hilo liliongoza mpaka eneo la maegesho, Todzo alishuka na kuanza kutembea haraka akielekea eneo lamapokezi., bwana Abraham hakumuelewa mtu aliyefika wakati huo, jambo lililomfanya awe mtulivu. Kiunoni kwake alikuwa ameweka bastola iliyokuwa na risasi za kutosha akiwa tayari kwa mauaji. Ghafla simu yake ya mkononi iliita na alipoiangalia aligundua kuwa ilikuwa imepigwa na mfanyakazi wake wa eneo la mapokezi. Baada ya sekunde kadhaa za kuongea na mfanyakazi wake huyo aligundua mtu aliyekuwa amefika na gari hilo aina ya Suzuki alikuwa ni Todzo.
Alitoa maagizo kuwa kijana huyo aelekezwe eneo ambalo alikuwapo ili amfuate.
Bwana Abraham, kwa utulivu wa kutosha aliitoa bastola yake huku akiifunika na leso kabla ya kuishika mkononi pasipo kugundulika. Kulikuwa na pilika pilika za wafanyakazi wake kiwandani hapo lakini wengi wao hawakuwa na mazoea ya kutomsogelea kwani walimtambua kama mtu mkali. Katika eneo la maegesho alilokuwapo kulikuwa na utulivu wa kutosha na tayari aliwaeleza vijana wake wajiandae kwa kazi. Hatimaye baada ya muda mfupi alimwona Todzo kwa mbali akielekea eneo alilokuwapo, alijiweka sawa tayari kwa kumkabili. Kijana huyo alimfikia na alianza kunyoosha mkono wake wa kulia ili wasalimiane, bwana Abraham pia alinyoosha mkono wake wa kulia uliokuwa na Bastola aliyofunika na Leso.
Alinyoosha bastola hiyo moja kwa moja tumboni kwa Todzo tofauti na kijana huyo alivyotegemea kuwa wangesalimiana. BwanaAbraham aliitoa leso iliyofunika Bastola hiyo kabla ya kumsihi Todzo kuwa mtulivu. Kijana huyo aliyeanza kutetemeka kupindukia ghafla, alitii amri hiyo. Alielekezwa aingie katika moja ya gari anina ya Land Cruiser katiya magari mawili yaliyokuwapo ambayo vioo vyake havikuhurusu mtu wa nje kuona ndani. Wakati akiusogelea mlango mmoja wa gari hilo alishtushwa kuona ukifunguliwa na mtu aliyekuwapo ndani.Todzo hakupoteza muda, aliingia katika gari hilo kabla ya kuamriwa akae katikati vijana wawili wa bwanaAbraham katika siti za nyuma za gari hilo. Huku akiwa na hofu aliamini kuwa mwisho wa maisha yake ulikuwa umefika hiyo ilitokana na hali halisi aliyoiona ndani ya gari hilo. Vijana wanne waliokuwapo walikuwa wakivuta bangi zaidi maumbile yao yalionekana ya kimazoezi huku wakiwa weusi na sura zilizoonesha kukosa huruma. Akiwa hajatulia vizuri kijana mmoja kati ya hao wawili aliokaa nao aliiweka bastola yake kwenye mbavu za Todzo huku akimwambia asitikisike hata kidogo.
Bwana Abraham mara baada ya kuhakikisha Todzo ameingia kwenye gari moja wapo, aliongoza kwenye gari jingine kabla ya kuingia na kuwaamuru vijana wake waondoe magari hayo eneo hilo. Magari hayo yaliondolewa kwa kasi, kabla ya kutoka kwenye geti kuu la kiwanda hicho. Baada ya nusu saa walikuwa wameshika barabara iliyoelekea katika jiji la Kampala, huko walitarajia kushika barabara nyingine ambayo ingewawezesha kufika katika ziwa la Kyoga lililokuwapo kaskazini mwa jiji hilo. Lengo lao lilikuwa ni kufika katika ziwa hilo nyakati za usiku ili wafanikishe mauaji hayo. Walipanga kufanya mauaji hayo eneo la mbali na jiji la Entebbe ili wasiweze kugundulika kama walikuwa wakihusika. Moyoni bwanaAbraham alikuwa na amani kidogo huku akiamini zoezi hilo lingefanikiwa zaidi alimfikiria David, mtoto aliyekuwa kikwazo kwake kwa muda mrefu.
Majira ya saa tisa usiku, magari yao baada ya kuwapo katika safari ndefu yalikuwa yakiegeshwa katika eneo la wazi lililokuwa kando na ziwa Kyoga. Eneo hilo lilikuwa na giza, huku likiwa halina makazi ya watu. Bila kupoteza muda vijana wa bwanaAbraham walimshusha Mswadzu kutoka kwenye buti ya gari alilokuwapo. Walimtoa kwenye gunia na kumweka chini ikiwa umbali wa mita kadhaa toka kwenye maji ya ziwa hilo. Wakati huo Todzo aliyekuwa amenyoosha mikono huku akiwa anatetemeka alielewa wazi mwisho wake ulikuwa umefika. Alikuwa mtulivu akisubiri kuuawa kwani alijaribu kuomba msamaha katika muda wote wa safari lakini hakuweza kufanikiwa kupata msaada huo. Akiwa bado hajatulia alipigwa teke la kifuani na kijana mmoja wa bwana Abraham lililompelekea aishie kuanguka eneo alilokuwapo Mswadzu ambaye bado hakuwa na fahamu.
Bwana Abraham aliwaoneshea ishara vijana wake watatu ambayo waliielewa kabla ya kuonekana wakiingia kwenye magari waliyofika nayo. Walitoka na bunduki tatu kila mmoja yake zililizokuwa aina ya AK 47. Huku wakitabasamu walionekana wakiunganisha bunduki hizo, baada ya dakika moja walikuwa wamemaliza zoezi hilo. Jambo lililofuta waliweka risasi za kutosha na kusimama kwa pamoja wakiwa wamefuatana ilhali bunduki zao zikiwa zimeelekezwa kwa Todzo na Mswadzu. Walikuwa tayari kufanikisha mauaji dhidi ya watu hao lakini walisubiria amri ya mwisho kutoka kwa bwana Abraham. Todzo aliyekuwa na fahamu alilia kwa uchungu akiomba msamaha lakini hakujibiwa kitu. Kulikuwa na utulivu wa sekunde kadhaa kabla ya bwana Abraham kuonyesha ishara iliyowahurusu vijana wake kuua.
Bila huruma vijana wake walimimini risasi kama hawana akili nzuri, mlio wa risasi uliosikika eneo hilo ulikuwa kama kuna vita. Todzo alipiga kelele kwa maumivu huku akijizungusha chini katika eneo hilo lakini kelele hizo hazikusitisha jambo la vijana hao kutekeleza kazi yao. Mswadzu naye kwa umbali alionekana akirusha mikono na miguu kutokana na karaha ya risasi hizo. Hatimaye zoezi hilo lilikamilika, vijana wa bwanaAbraham bila kupoteza muda waliisogelea miili hiyo na kuivutia kwa kasi katika upande wa maji ya ziwa hilo. Waliivuta miili hiyo mpaka maji yalipoanza kuwa katika usawa wa viuno vyao hapo walilidhika kwani tayari miili hiyo ilikuwa ikielea majini.
Walirudi wakikimbia kwenye magari yao kabla ya kuingia na kuyaondoa kwa kasi eneo hilo la tukio walilofanya mauaji hayo. Baada ya dakika kadhaa walikuwa wakiendelea kuliacha eneo hilo ziwa Kyoga huku bwana Abraham akiwa na furaha kidogo, alianza kukumbuka jinsi walivyofanikisha zoezi hilo kirahisi. Walifanikiwa kumnasa Mswadzu kirahisi ikiwa ni baada ya kumwekea dawa ya usingizi wa muda mrefu katika bia ya Bell ambayo aliihitaji. Dawa hiyo waliyoitumia ilikuwa ikiitwa Ambien (Zolpidem) ambayo ilikuwa na uwezo wa kumfanya mtu kulala kwa muda mrefu. Dawa hiyo ndiyo iliyopelekea Mswadzu afariki akiwa usingizini. Mafunzo ya kijeshi na ujanja wote aliokuwa nao hakuweza kuutumia baada ya kuwekewa dawa hiyo katika bia aliyokunywa.
BwanaAbraham kwa wakati huu alikuwa ametawaliwa na mambo matatu ambayo bado yalikuwa yakimuumiza kichwa. Jambo la kwanza alihitaji kuandaa mauaji dhidi ya David ambaye hakufahamu eneo alilokuwapo. Pia alihitaji kuwa na mtoto suala lililopelekea aanze kumkumbuka mwanamke aliyetembea naye miaka miwili iliyokuwa imepita ambaye alimweleza kuwa alikuwa na mtoto wake lakini alimkataa mtoto huyo. Jambo lililoanza kumwingia akilini pia lilihusiana na mkewe, aliwaza kuachana na mwanamke huyo. Kwa vile alielewa hakuwa na uwezo wa kumpa mtoto baada ya kufungwa kizazi ilhali yeye akiwa na uwezo wa kumwoa mwanamke mwingine na kumpata mtoto. Aliwaza pia jambo lililokuwa gumu, alihitaji kumuua pia mwanamke huyo kwa vile alikuwa na siri zake nyingi toka mwanzo mpaka wakati huo. Aliamini asipofanya zoezi hilo lazima mwanamke huyo angezitoa siri zake zote, ikiwamo ya mauaji aliyoyafanya dhidi ya familia ya mdogo wake bwana Jahnson ili kuupata utajiri aliokuwa nao wakati huo.
* * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ikiwa yapata saa kumi na moja jioni David alionekana akitembea na kundi la watoto wa mitaani wa eneo la Kiriri. Eneo hilo lilikuwa umbali wa kilometa zaidi ya ishirini likiwa Kaskazini-Magharibi toka eneo la hospitali aliyokuwa amekimbia. Alikuwa amefika eneo hilo kwa kutembea kwa miguu ikiwa ni baada ya kukutana na mtoto mwenzie wa mitaani aliyeitwa James ambaye alikubali kumsaidia kuukwepa mkono wa bwanaAbraham lakini naye alikuwa mgeni katika eneo hilo la Kiriri. Umbali wa Kamengo mpaka Kiriri ulikuwa mrefu sana kwake jambo lililopelekea miguu imuume sana siku mbili za mwanzo mara baada ya kufika eneo la Kiriri. Alikuwa katika mavazi duni sana ya nguo zilizokuwa zimechanika chanika sana wakati rafiki yake James naye akiwa hivyo.
Muda wote walikuwa wakitembea na watoto wa mitaani wa eneo hilo lengo haswa likiwa ni kuyafahamu maisha ambayo watoto hao walikuwa wakiishi katika eneo hilo. Ingwawaje watoto wenzao hao hawakutaka kutembea nao lakini walijitahidi kadri walivyoweza kuwa karibu nao. Baada ya wiki mbili tayari walikuwa wenyeji wakiwa wanaelewa jinsi ya kuishi katika eneo hilo. Pia walikuwa wamepata sehemu ya kulala ambayo watoto wa mitaani wa eneo hilo walikuwa wakilala. Malazi yao yalikuwa katika eneo la gereji moja iliyokuwa na majengo chakavu ambayo kwa wakati huo ilikuwa haitumiki. Pia ilikuwa na magari kadhaa mabovu yaliyokuwa juu ya mawe ambayo hayakuwa na dalili zozote za kutolewa eneo hilo. Walielezwa na watoto wa mitaani wenzao walioishi eneo hilo kuwa walianza kupata hifadhi katika majengo hayo ikiwa ni baada ya ajali ya moto iliyoipata gereji hiyo kutokana na hitilafu ya umeme. Walielezwa toka wakati huo wa ajali hiyo hakuna jitihada zozote zilizofanywa na waamiliki za kuitengeneza gereji hiyo jambo lililopelekea watoto hao wajihifadhi.
David na James walikuwa marafiki wakubwa jambo lililowafanywa watembee pamoja kila siku wakiwa katika eneo hilo la Kiriri. Jambo hilolilifuata baada ya kuyafahamu vizuri maeneo ya sehemu hiyo. Kazi yao kubwa waliyoifanya ilikuwa ni kubeba mizigo ya watu sehemu tofauti za eneo hilo. Mara nyingi walikuwa wakipatikana katika soko kuu la Kiriri ambako walifanikiwa kupata fedha zilizowakimu kwa chakula mara baada ya kubeba mizigo. David alimpenda sana rafiki yake James kutokana na tabia ya uwazi aliyojijengea, tayari alikuwa amemtambua mtoto mwenzie huyo kama alikuwa raia wa Kenya. Wazazi wake walihamia nchini Uganda miaka zaidi ya kumi iliyokuwa imepita wakati huo James akiwa na umri wa miaka minne.
Baba yake James alikuwa mtaalam wa kilimo aliyehitimu shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha kilimo na tekinolojia cha Jomo Kenyata kilichopo nchini Kenya. Mara baada ya masomo yake alimuoa mama yake James ambaye alihitimu pia katika chuo hicho. Wazazi wake waliishi nchini Kenya katika maisha ya ndoa kwa miaka mitano huku wakiwa wananfanya kazi. Kutokana na ujuzi wa masuala ya kilimo aliokuwa nao baba yake James, kampuni ya Kamengo Sugar Cane Plantation Co.Ltd ilimfuata nchini Kenya ikiwa na lengo la kutaka kumuajiri. Baada ya maridhiano hayo, James akiwa na miaka minne wakati huo,walihamia nchini Uganda na wazazi wake walianza kazi katika kampuni hiyo husika.
Huko ndiko ambako siku zote James akiwa na David alikuwa akimlaumu baba yake kwani alianza mahusiano na wanawake tofauti zaidi ya mkewe. Baada ya miaka miwili wazazi wake walikuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. James alimweleza David kuwa alibahatika kumpata mdogo wake wa kike lakini kutokana na kuambukizwa pia virusi hivyo mdogo wake huyo alifariki akiwa na miezi mitatu. Hatimaye mwaka wa tatu wa kuwapo nchini Uganda ndio ambao rasmi wazazi wake walianza kuumwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi walivyokuwa navyo. Maisha yalibadilika ndani ya muda mfupi kwani kutokana na kuumwa kwa muda mrefu wazazi wake walisimamishwa kazi. Baba yake aliamua kuuza nyumba waliyokuwa nayo katika eneo la Kamengo akiwa na lengo la kutafuta dawa za kuwaponya ugonjwa huo lakini haikuwezekana.
Hatimaye ulifika muda ambao wazazi wake walifariki kwa wakati tofauti huku wakiwa hawaja mwachia hata kitu kimoja. Wakati huo James alikuwa darasa la kwanza akiwa na miaka saba. Marafiki wa baba yake walijitahidi kumlipia ada katika shule ya bweni aliyokuwa akisoma katika eneo la Kamengo kwa miaka miwili. Akiwa ni mwanafunzi ambaye muda wake wa likizo alikuwa akiiishi shule, marafiki hao wa baba yake walishindwa kumlipia ada ya shule akiwa darasa la nne jambo lililopelekea afukuzwe shule na kuishia kuwa mtoto wa mitaani mpaka wakati huo.
Historia hiyo fupi ya James ilikuwa ikimpa nguvu David siku zote akiamini akiwa na rafiki yake huyo mpya kila jambo lingewezekana. Wakati huo James alikuwa na umri wa miaka kumi na nne ilhali David akiwa na miaka kumi na mbili na tayari walikuwa wameweka malengo yao kadhaa. Walihitaji kwa kiasi kikubwa kurudi tena shule kwa vile waliamini jambo hilo lingewezekana na mwishoe wangetimiza ndoto zao. Mbali na mipango hiyo moyoni David alikuwa bado ana hasira dhidi ya baba yake mkubwa bwana Abraham. Mara kadhaa wakati alipomkumbuka alijikuta akipandwa na hasira dhidi yake na kujiapiza kuwa ni lazima angelipa kisasi siku moja.
Kwa muda wa mwezi mmoja David alianza kubadilika akiwa na mwonekano tofauti na ule wa awali. Kifua chake kilikuwa kimemjaa kama vile alikuwa mtu wa mazoezi hiyo yote ilitokana na kazi nzito za kubeba mizigo walizofanya. Wakati akiwa anaendelea kuzoea harakati zao hizo za maisha, mwenzie James alikuwa ameashazoea. Kila siku walikuwa na mazoea ya kukutana na watu tofauti huku wakijaribu kuwaomba msaada, lengo haswa likiwa ni kurudi shule. Hawakufanikiwa kupata msaada wowote katika harakati zao hizo lakini hawakukata tamaa. Wakati huo hawakuwa na shaka juu ya chakula kwani jinsi walivyojituma katika kufanya kazi katika eneo hilo la Kiriri ndivyo walivyoweza kujikimu katika hitaji hilo. Maisha yao yalikuwa katika misingi ya tabia njema, tofauti na watoto wengi wa mitaani ambao walikuwa wezi. Bado walikuwa wakiishi katika gereji waliyofikia ambako walipata gari moja aina ya Isuzu lililokuwa juu ya magogo katika eneo hilo la gereji. Gari hilo la mizigo lililokuwa na mabati chakavu sana halikuwa na bodi lake la nyuma huku likiwa limetolewa vitu vingi.
Siku moja majira ya saa kumi jioni wakati James na David wakiwa bado katika harakati zao za kujitafutia riziki. Lilifika gari moja kubwa la mizigo ambalo lilikuwa limeandikwa Abraham Textile Industry. Gari hilo lilikuwa limetokea barabara ya Kamengo, mara baada ya kuliona James alimshtua David aliyekuwa akisinzia katika eneo la mti mmoja waliokuwa wamepumzika. Walianza kulifuatilia kwa nyuma gari hilo huku wakikimbia na hatimaye liliishia kuegeshwa katika eneo la maduka ya nguo yaliyokuwapo eneo hilo la Kiriri. Walikuwa wakiamini kuwa wangepata nafasi ya kushushwa mzigo katika gari hilo, wauza maduka wa eneo hilo walijongea kwenye eneo la mbele la gari hilo huku wakionekana kama walikuwa wakilipia bidhaa walizozihitaji. Baada ya muda mfupi David na James walipata kibarua cha kushusha mzigo toka kwenye gari hilo na kupeleka katika maduka matatu tofatuti ya wamiliki hao.
Walianza kazi hiyo huku wakisaidiana na vijana wengine kadhaa. Walikuwa na furaha baada ya kuamini siku hiyo tayari ilikuwa imepata ukombozi kwani fedha walizotarajia kuzipata waliamini zingewatosha kwa chakula siku hiyo. Wakati David akiendelea kushusha mzigo huo wa Khanga pamoja na mashuka alikuwa haelewi bidhaa hizo zilikuwa za kampuni gani. Huku akiendelea kufanya kazi hiyo kwa kujituma alianza kukumbuka kiwanda cha marehemu baba yake kilichoitwa Johnson Textile Industry ambacho kilikuwa kikizalisha bidhaa kama hizo walizokuwa wakishusha. Baada ya dakika kadhaa walifanikiwa kumaliza kushusha mzigo huo kwa mmiliki wa duka la kwanza wakiwa wanapeleka mzigo huo katika stoo zao. Hatimaye walikamilisha kwa mmiliki wa pili na walianza kupeleka mzigo huo kwenye duka la mmiliki wa tatu. David wakati akitoka katika stoo ya mmiliki wa duka hilo alishtuka kidogo baada ya kuona eneo la mbele la kioo cha gari hilo aina ya Scania walilokuwa wakishusha mzigo huo. Lilikuwa limeandikwa Abraham Textile Industry jambo lililomfanya aendelee kushusha mzigo katika gari hilo huku akihusianisha jina hilo na la baba yake mkubwa bwana Abraham.
Alianza kufikiria mambo mengi jambo lililomfanya hata ufanisi wake katika kazi hiyo upungue. Wakati wakiwa wanarudi kutoka kwenye stoo ya mmiliki wa duka hilo ili wachukue mzigo kwa mara ya mwisho. Ghafla David alishtushwa na sauti ya mwanamke aliyemwita toka katika eneo la mbele la gari hilo, alitulia kidogo akiwa amesimama na James wakiwa na lengo la kumwona mtu huyo aliyemwita David. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio akianza kuhisi uwezekano wa jina la baba yake mkubwa bwana Abraham aliloliona katika gari hilo lilihusiana na fikra zake. Walishuhudia mlango ukifunguliwa kabla ya mwanamke aliyemtambua vizuri kushuka katika gari hilo. David alijihisi miguu ikimwishia nguvu huku akibaki anamwangalia mwanamke huyo, alikuwa mke wa bwana Abraham. Walibaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa huku David akigundua mambo mengi toka kwa mwanamke huyo, kiafya alikuwa amekonda sana tofauti na alivyomfahamu. Pia alikuwa na makovu usoni na sehemu tofauti za mwili wake, wakiwa bado wanatazamana mwanamke huyo alianza kulia kwa uchungu huku akilitaja jina la David.
Hatimaye alianza kumsogelea akiwa na lengo la kumkumbatia, ghafla David alipata nguvu miguuni mwake kabla ya kuondoka akikimbia kwa kasi na kuwaacha eneo hilo.
“David don’t run son, I need to help you” (“David usikimbie mwanangu, nahitaji kukusaidia”) Alipaza sauti hiyo mke wa bwana Abraham huku akiirudia mara mbili akimwita David lakini hakuthubutu kurudi eneo hilo. James naye alianza kujisogeza pembeni taratibu baada ya kuona maandishi ya mbele ya gari hilo kisha akakumbuka maelezo ya David na mwishoe alipata picha. Baada ya kusogea umbali wa mita kama nne naye alitoka akikimbia akimwacha mkewe bwana Abraham akimlilia David.
Mke wa bwana Abraham alionesha uchungu dhahiri na zaidi nia ya kumpata David, hata watu waliokuwapo eneo hilo waligundua kuwa mama huyo hakuwa na nia mbaya juu ya mtoto huyo. Walisubiri kwa nusu saa wakiamini huenda David angerudi akiwa na rafiki yake lakini haikuwa hivyo jambo lililopelekea mkewe Abraham awaruhusu vijana wake waliondoe gari eneo hilo na safari ilianza wakielekea jijini Entebbe. Mke huyo wa tajiri mkubwa nchini Uganda ambaye watu kadhaa walishangaa kumwona akizunguka katika gari hilo ya mumewe hakuondoka bure. Alimwachia mmiliki mmoja wa duka ambalo waliuza bidhaa hizo kiasi cha laki tano za Uganda akiwa amemweleza fedha hizo apewe David lakini pia aliacha namba yake ya simu akiwaambia kuwa mtoto huyo amtafute.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kukimbia David aliongoza mpaka katika eneo la gereji ambalo walikuwa wakilala na rafiki yake wa karibu James. Akili yake ilikuwa haijatulia huku akiwaza kukimbia eneo hilo la Kiriri ili kuokoa maisha yake. Hakuwa na amani na mama yake mkubwa huyo hata kidogo akiamini taarifa juu yake zingemfikia adui yake mkubwa bwana Abraham. Baada ya kuwapo katika gari hilo bovu aina ya Isuzu kwa muda wa dakika kadhaa, James naye alifika na alianza kumtuliza rafiki yake huyo. Alikuwa na mtazamo tofauti akiamini huenda mke wa bwana Abraham hakuwa na nia mbaya. Hata hivyo kuna wakati alihisi unyenyekevu wa mwanamke huo huenda ilikuwa njia ya kuhitaji kufanikisha kumkamata David.
James hakuwa tayari kukubaliana na wazo la kuhama eneo hilo walilokuwa wakiishi kama watoto wa mitaani huku akimhakikishia David kuwa angemlinda. Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu kwao kwani walilala njaa na zaidi walikuwa wakijitathimini jinsi walivyokuwa maskini. Walizungumza kwa muda mrefu kabla ya kupitiwa na usingizi majira ya saa nane usiku. Walilala wakiwa hawana hatma ya maisha yao ambayo siku zote walitafuta pesa ya kujikimu siku husika pekee. Asubuhi ya siku iliyofuata waliamka majira ya saa kumi na moja asubuhi, hiyo yote ilitokana na njaa iliyokuwa ikiwauma kupindukia. Waliongoza mpaka eneo la soko kuu la Kiriri na huko walienda kuongea na mama ntilie waliokuwa wakiuza chakula karibu na soko hilo. Mama mmoja aliwapa masharti ya kuwapa chakula iwapo wangemsaidia kufanya usafi eneo alilokuwa akifanyia biashara. Jambo hilo lilikuwa jepesi kwao kwani walipiga deki na kufanya usafi eneo lililozunguka biashara ya mama huyo. Majira ya saa kumi na mbili na nusu walikuwa wamemaliza kazi hiyo. Mama huyo aliwapa chai ambayo alikuwa akiiandalia nyumbani kwake na baada kifungua kinywa hicho walijiona wako safi. Walimshukuru sana mama huyo kabla ya kuanza mizunguko yao ya kujitafutia riziki.
Siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwao kwani hawakupata kazi ya kufanya kama ilivyokuwa kawaida. Wakati wakiendelea kutafuta kazi pia walikuwa wakiongea na watu tofauti ambao walikuwa wakiwaomba msaada wa kuwasaidia kimaisha na zaidi kurudi shule. Siku zote watu wengi hawakuwasikiliza huku wakiamini walikuwa wakorofi. Waliendelea kuhangaika kutafuta kazi bila mafanikio, majira ya saa tisa mchana tayari hitaji la chakula lilianza kusumbua vichwa vyao. Walikuwa wamekaa chini ya mti mmoja wakitafakari jinsi ambavyo siku hiyo ingeenda. Wakati wakiwa bado kwenye dimbwi la simanzi hiyo nzito, walilishuhudia gari moja la kifahari lililokuwa na muundo kama wa Hummer likiegeshwa katika mgahawa mmoja wa kifahari uliokuwa mbele yao.
David na James walinyanyua vichwa vyao huku wakiungana na watu wengine waliokuwapo eneo hilo, lengo haswa likiwa kutaka kumshuhudia mtu ambaye angeshuka katika gari hilo. Wakiwa wametoa macho alishuka mwanaume mmoja mwafrika aliyekuwa amejazia sana kifua ambaye aliongoza mpaka katika mlango wa mbele wa kushoto wa gari hilo na kuufungua. Baada ya sekunde kadhaa msichana mmoja aliyekuwa mzungu ambaye kwa wastani angekadiliwa kuwa na miaka ishirini na tatu alishuka katika gari hilo. Walibaki wakiwa wamemtolea macho msichana huyo ambaye pia alikuwa mrembo sana huku akiwa mrefu. Alifuatiwa na dereva wa gari hilo aliyekuwa mwafrika, mrembo huyo alianza kuongozwa na waafrika hao walioonekana kuwa wenyeji wake na waliingia katika mgahawa huo wa kifahari.
Mara baada ya watu hao kuzamia katika mgahawa huo James na David walitazamana. Wote walionekana kama vile walihitaji kufanya jambo. David ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoa wazo akihitaji waonane na mrembo huyo wa kizungu ili wamwombe msaada. James hakupinga jambo hilo kwani hata yeye wazo lake lilikuwa ni kuhitaji kujaribu kuonana na mrembo huyo. “May be she’s our savior from Lord, let’s try James” (“labda ni mkombozi wetu toka kwa Mungu, tujaribu James”) Alisikika David akiongea huku akinyanyuka eneo walilokuwapo kabla ya kufuatiwa na James. Walikuwa katika mavazi duni ya nguo zilizokuwa chafu na zilizochanika sehemu tofauti lakini walijipa tumaini. Taratibu walianza kutembea wakijongea katika mgahawa husika uliokuwa mita kadhaa toka eneo walilokuwapo.
Vichwani walielewa kuwa lazima wangezuiwa kuonana na mrembo huyo wa kizungu lakini walijipa matumaini. Hatimaye waliufikia mlango wa mgahawa huo kabla ya kuufungua na kuanza kuingia taratibu. Wakiwa bado hawajaingia sawasawa mhudumu mmoja wa mgahawa huo aliwaona kabla ya kuwahi eneo walilokuwapo na kuwazuia. David na James kwa utulivu walijieleza kuwa waliitwa na mzungu ambaye alikuwa ameingia katika mgahawa huo. Mhudumu huyo alijitahidi kuwazuia lakini hakufanikiwa kwani walikuwa wabishi na James alianza kulia kama mtoto mdogo. Jambo hilo lilimfanya mhudumu huyo aamue kuwahurusu kuingia katika mgahawa huo baada ya kuona watoto hao walikuwa kero kwa wateja wao. Baada ya kuingia David akifuatwa na James aliongoza akielekea katika meza aliyokuwapo msichana yule mzungu waliyekuwa na nia ya kuonana naye.
Kabla hawajamfikia mrembo huyo, mtu ambaye waliamini alikuwa akimlinda msichana huyo ambaye walimwona toka awali aliwazuia wasimsogelee msichana huyo.
“Hey! What do you want from my boss, aah! Nobody is allowed to get closer to her”(“Hey! Nini mnataka kutoka kwa bosi wangu, Aah! Hakuna mtu anayehurusiwa kuwa karibu yake”) Alilalama baunsa huyo huku akiwasukuma kina David ilhali wakipiga kelele za kuomba msaada wa kuonana na msichana huyo. Tayari walianza kuhisi kushindwa kwao kufanikisha zoezi hilo huku wakiishia kuanguka chini baada ya kusukumwa kwa nguvu na baunsa huyo. “No! Jimmy don’t hurt them, just relax and….. I need to talk with them” (“hapana Jimmy usiwaumize, tulia na….. nahitaji kuongea nao”) Alisikika mrembo huyo kwa sauti nyororo iliyowapa ahuweni kina David. Walisimama haraka na kwenda kujumuika katika meza ya msichana huyo.
Baada ya kujitambulisha kwao, waliagiziwa chakula na msichana huyo aliyeonekanakuwa na huruma. Tayari walikuwa wametambua kwamba alikuwa mrembo wa jimbo la Carifonia la nchini Marekani ambaye alikuwa katika ziara yake ya kiutalii nchini humo Uganda. Bila kupoteza muda David na James walianza kwa kujieleza matatizo yao kwa ufupi kabla ya kuomba msaada kwa mrembo huyo. Alionekana akitokwa na machozi baada ya kusimuliwa visa hivyo juu ya maisha yao. Alibaki ametulia kwa muda mrefu bila kuwajibu huku akionekana kama alitafakari jambo. Hatimaye alinyanyua kichwa na kukubali kuwasaidia jambo lililokuwa la furaha kwao kupindukia.
Aliwaeleza kuwa msaada ambao angewasaidia ungefahamika kuanzia siku iliyofuata huku akiwataka wakutane eneo hilo majira ya saa nane mchana siku iliyofuata. Wakati huo, mrembo huyo aliyejitambulisha kwa jina la Natalie Brown alikuwa akielekea katika eneo la Kamengo. Hivyo siku iliyofuata akiwa anarudi toka huko aliwaeleza kuwa angeangalia jinsi ambavyo angeweza kuwasaidia. Hatimaye msichana huyo aliondoka akiwa amewaacha na furaha huku wakiamini ndoto zao zilikuwa zikielekea kukamilika ndani ya muda mfupi. Hawakuwa na shaka kwa wakati huo kwani walielezwa watumie chakula chochote walichokihitaji katika mgahawa huo mpaka siku hiyo iliyofuata.
Majira ya saa moja nusu usiku baada ya kula chakula katika mgahawa huo walikuwa wakielekea katika eneo lililokuwa na malazi yao huku wakiwa wametawaliwa na furaha. Walikuwa wakiwaza mambo mengi, kubwa likiwa hisia zao za kurudi tena shule. James alipitiliza katika hisia zake kwani aliamini kuwa huenda wangesafiri na mrembo huyo kuelekea nchini Marekani. Baada ya nusu saa walikuwa wamefika katika eneo la gereji lililotumika kwa ajili ya malazi yao na tayari walikuwa katika gari lao walilolala siku zote. Bado walikuwa wakimzungumzia Natalie Brown waliyeamini angebadili taswira ya maisha yao. Wakati huo kulikuwa na kelele za watoto wa mitaani waliokuwa katika chanzo cha moto uliokuwa ukikokwa kila siku katika eneo hilo. Wenzao hao walikuwa na mazoea ya kukesha na kusimuliana mambo kadhaa yaliyojili kutwa nzima mpaka majira ya saa saba usiku.
Hawakuwa na mazoea ya kujumuika na wenzao ambao walikuwa wakifanya matukio haramu tofauti na ilivyokuwa kwao. Majira ya saa tatu usiku wakiwa wameanza kupata usingizi katika maboksi waliyolala walishtushwa na mlio wa risasi zilizosikika nje ya eneo hilo. Zaidi kulikuwa na mwanga mkali uliomulika kila upande wa eneo hilo huku vipaza sauti vikisikika. Baada ya kuamka kwao na kutulia kidogo waligundua uwepo wa polisi eneo hilo jambo lililowafanya waanze kuamini ndoto zao zilikuwa zimefikia mwisho. Askari hao kupitia vipaza sauti walisikika wakiwaeleza watu wote waliokuwa eneo hilo watoke nje kwa usalama wao. David alinyanyuka kidogo na kuchungulia eneo la nje kabla ya kuwashuhudia askari wengi waliokuwapo eneo hilo huku wenzao wengi wakiwa tayari wametii amri.
James alikuwa akitetemeka huku machozi yakimtoka akiamini ndoto zao zilikuwa zimeshapotea. Wakati wakiwa bado hawajaamua jambo la kufanya lilitolewa onyo la mwisho wakielezwa watu wote watoke katika magari hayo chakavu yaliyokuwapo. Bado walibaki wakitetemeka huku wakiwa hawako tayari kujitokeza. Baada ya onyo hilo la mwisho askari walianza kufanya msako eneo hilo wakikagua gari moja mpaka jingine. Hofu yao wakati huo iliongezeka na walijilaumu kwa nini hawakutoka. Hatimaye askari hao waliwakamata kiurahisi kabla ya kuwapiga sawasawa jambo lililopelekea wote wazimie. Walishtuka siku iliyofuata wakiwa ndani ya selo ya polisi huku wakiwa na kundi kubwa la wenzao walioishi katika eneo la gereji. Walikuwa na majereha kadhaa waliyoyapata baada ya kupigwa na askari, zaidi David ambaye paji lake la uso lilikuwa limevimba.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawakujua jambo ambalo lingeendelea huku wakiwa wameelezwa kuwa walikamatwa kutokana na kuongezeka kwa matukio ya uhalifu yaliyokuwa yakisababishwa na wao. Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo moyoni walivyoumia wakimini wangeukosa msaada wa Natalie Brown aliyeahidi kuwasaidia. David ndiye aliyekata tamaa kabisa kwani alimini lazima angekamatwa katika kituo hicho cha polisi wakati wa kutoka. Jambo hilo ndilo lililomfanya aachane na hisia zake za kuweza kusaidiwa na Natalie. Majira ya saa saba mchana walifika askari saba katika selo hiyo iliyokuwa na mateso makali. Kwani kulikuwa na watu wengi na zaidi maji ya barafu yaliyokuwa yamemwagwa sakafuni. Askari hao hawakupoteza muda, walianza zoezi lao la kuwatoa watoto hao wa mitaani kwa adhabu ya viboko sita huku wakiwa wameaswa kutorudi tena eneo walilokuwa wakiishi awali. Watoto hao walitii amri hiyo na zoezi hilo lilianza kuchukua nafasi, wengi wao walikuwa wamechoshwa na mateso ya eneo hilo huku wakiwa na majeraha kadhaa waliyoyapata wakati wakikamatwa.Zoezi hilo lilichukua nafasi ndani ya muda wa nusu saa huku James na David wakiwa wamekumbatiana, walikuwa wakilia. Hiyo yote ilitokana na hofu waliyokuwa nayo ya kutenganishwa na askari hao. James aliitwa baada ya wenzao wote kutoka. Alitekeleza amri hiyo huku akiwa bado anaendelea kulia na hatimaye alipigwa viboko, baada ya dakika mbili alikuwa nje akimsubiri David atoke baada ya adhabu yake pia. Alimsubiri kwa dakika kumi lakini haikuwa hivyo, David hakutoka katika kituo hicho cha polisi. Tayari ilikuwa yapata saa nane kasoro ishirini, wakiwa wamebakiwa na dakika chache walizopaswa wakutane na Natalie Brown, Mmarekani waliyeamini angebadili mtazamo wa maisha yao.
Hatimaye wakati akiwa anafikiria juu ya jambo la kufanya alilishuhudia gari la askari likiegeshwa mbele ya kituo hicho. Baada ya dakika kadhaa alimwona rafiki yake huyo akitolewa katika kituo hicho cha polisi huku akiwa amefungwa pingu. David alikuwa akilia huku akimsisitiza James aondoke eneo hilo. Tayari alionekana akiwa amekata tamaa juu ya kila jambo, alionyesha dhahiri utayari wake wa kupelekwa mikononi mwa bwanaAbraham na mwishoe kuuawa. Ndoto zake za kulipa kisasi zilipotea ndani ya muda mfupi na tayari alikuwa katika mkono wa sheria. Baada ya kupakizwa katika gari hilo askari wanne walipanda pia kabla ya kuliondoa kwa kasi eneo hilo wakiwa na mhalifu huyo, mtoto ambaye jeshi la polisi liliamini alikuwa ni mfuasi wa kundi la Eastern Black Killers.
James hakuwa na jambo la kufanya huku akilia aliona jambo pekee lililokuwa limesalia nikutimiza ahadi waliyopewa na Natalie Brown. Huku akikimbia aliongoza mpaka katika Mgahawa husika ambako alienda kumwona mzungu huyo akiwasubiri. Hakuficha jambo kwani alimweleza kila kitu juu ya kukamatwa kwao na mwishoe jeshi la polisi kuendeleza msimamo wake wa kumshikilia David. Mrembo huyo aliumia sana juu ya tukio hilo huku akiwa tayari ameutambua ukweli wa maisha ya watoto hao. Akiwa na James siku iliyofuata walijaribu kutafuta uwezekano wa kumpata David lakini haikuwezekana kwani alikuwa akishikiliwa na jeshi la polisi la jijini Entebbe kama walivyoelezwa. Walijitahidi kujaribu kumtoa katika mkono wa sheria mtoto huyo lakini haikuwezekana.
Baada ya wiki mbili James akiwa na Mmarekani huyo, Natalie Brown walikuwa katika ndege ya shirika la British Airways. Walikuwa safarini wakielekea nchini Marekani baada ya tararibu zote zilizomhusu James kukamilika. Aliondoka nchini humo kama mtoto yatima aliyepatiwa msaada na mrembo huyo ya jimbo la Carifonia nchini Marekani. Mrembo huyo alitarajiwa kushiriki katika kinyan`ganyiro cha mashindano ya urembo ya nchi hiyo kwa mwaka huo akiliwakilisha jimbo lake la Carifonia. Wakati safari ikiendelea James alijawa na maswali mengi juu ya uhai wa David! Hakujua hatma ya rafiki yake huyo huku akiamini kuwa huenda alikuwa ameshauawa na bwanaAbraham! Akiwa katika wimbi la mawazo hayo mazito, alijipa imani akiamini pia labda rafiki yake huyo alikuwa hai kwa uweza wa mwenyezi Mungu kwani bado alikuwa na kazi ya kulipa kisasi kwa mwanaharamu bwanaAbraham aliyeipoteza familia yake...!
SEHEMU YA PILI
Miezi kadhaa Iliyopita.
Jinsi alivyokuwa mtu yeyote angeweza kumtambua kuwa hakuwa mtu mwema, sura yake ilikuwa imekunyamana kama mtu mwenye hasira muda wote. Alionekana akiwa amevaa miwani ambayo haikuruhusu mtu kumwona jicho lake bovu la kushoto kwani aliona kwa kutumia jicho la kulia tu! Moyoni hakuwa na huruma hata kidogo huku akiwa na hulka ya kufanya mauaji kwa mtu yeyote ambaye angemkosea. Jambo lililomfanya awe hivyo lilimhusu mtoto David, alikuwa amefanya majaribio mengi ya kumuua mtoto huyo lakini alishindwa. Jambo lililomuuma zaidi lilihusiana na mtoto wake pekee, Sabinus aliyempoteza katika harakati za kumuua David. Alichanganyikiwa zaidi kila alipokuwa akikumbuka kuwa mkewe hakuwa na uwezo wa kupata ujauzito tena kutokana na matatizo ya uzazi aliyoyapata miaka kadhaa iliyopita na hivyo kupelekea afungwe uzazi. Alifungwa uzazi wake wakati tayari wakiwa na mtoto mmoja, Sabinus ambaye alikuwa amefariki.
Aliyekuwa kwenye dimbwi la mawazo haya hakuwa mwingine bali ni bwana Abraham. Mtu aliyekosa huruma ambaye alifanikisha mauaji dhidi ya mdogo wake Johnson miaka kadhaa iliyokuwa imepita kutokana na tamaa ya mali za mdogo wake huyo. Majira hayo ya saa nne asubuhi akiwa mtulivu alikuwa ofisini kwake akiwaza jambo la kufanya. Mwishoe alipata jibu na kuamua kuchukua jukumu lililokuwa gumu kuliamua siku zote. Aliwaza kumuua mkewe kwa vile hakuwa na uwezo wa kuzaa tena na hivyo kumkosesha raha ya kuwa na mtoto. Aliwaza kufanya hivyo kutokana na siri zake nzito za mauaji ambazo hakuna mtu aliyezitambua zaidi ya mkewe. Aliamini kama angemwacha mwanamke huyo pasipo kumuua basi siri zake zote zingelifikia jeshi la polisi kirahisi.
Jambo jingine lililomwingia kichwani pia aliwaza kumtafuta mwanamke aliyewahi kumpatia ujauzito miaka kadhaa iliyokuwa imepita kabla ya kuukana ujauzito wa mwanamke huyo. Hakumsahau David, mtoto wa mdogo wake marehemu Johnson ambaye alikuwa bado anasumbua kichwa chake. Alipanga kuhakikisha anafanikisha mauaji haraka iwezekanavyo ili amiliki kwa amani utajiri aliourithi kutoka kwa mdogo wake. Bwana Abraham hakupoteza muda, majira ya saa tano asubuhi aliondoka na gari lake katika ofisi za kiwanda chake cha Abraham Textile Indusrty kilichokuwapo katika jiji la Entebbe, nchini Uganda. Aliwaza kwenda kumtafuta mwanamke aliyempa ujauzito na mwishoe kumkataa. Akiwa ndani ya gari lake aina ya Range Rover, alitumia nusu saa akiwa barabarani kabla ya kuifikia hoteli ya Entebbe View ambayo mwanamke huyo, Aminata aliyekuwa akimtafuta alikuwa akifanyia kazi.
Hakupata taabu kutokana na umaarufu aliokuwa nao nchini Uganda wa kumiliki viwanda tofauti, alipokelewa vizuri na kuongozwa mpaka katika ofisi ya kiongozi wa hoteli hiyo. Mara baada ya kuingia katika ofisi hiyo alianza kwa kumuulizia Aminata ambaye awali aliwahi kuwa mhudumu wa hoteli hiyo miaka kadhaa iliyokuwa imepita. Hakuficha jambo kwani alijieleza kuwa aliwahi kumpa ujauzito mhudumu huyo.
Baada ya maelezo yake hayo, kiongozi wa hoteli hiyo alitoa ushirikiano wa kumhurusu mfanyakazi wake mmoja ili ampeleke kwa Aminata ambaye alimtaja kuwa alijulikana kama mama Gray kwa wakati huo. Jina hilo lilifuata baada ya kujifungua mtoto wa kiume lakini pia alikuwa ameacha kazi katika hoteli hiyo mwaka mmoja uliokuwa umepita. Hatimaye bwana Abraham aliondoka hotelini hapo akiwa na mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo aliyeelezwa ampeleke eneo aliloishi Aminata. Moyoni alikuwa na furaha huku akiwa na shauku ya kumwona mtoto wake. Jambo lililomfurahisha zaidi lilitokana na taarifa za awali alizopewa kuwa Aminata alijifungua mtoto wa kiume aliyeitwa Gray. Baada ya nusu saa gari lake lilikuwa likiegeshwa mbele ya nyumba moja ya kupanga iliyokuwa katika eneo la watu masikini la jiji hilo la Entebbe. Bwana Abraham alishuka kwenye gari lake akifuatiwa na msichana aliyeongozana naye. Akiwa anaangalia huku huko alishtushwa na mtoto mmoja aliyekuwa akicheza katika eneo la mbele la nyumba hiyo. Alikuwa mtoto wa wastani wa miaka mitatu huku akiwa amevaa bukta ndogo iliyotoboka ovyo ilhali akiwa hajavaa nguo nyingine zaidi. Alikuwa mchafu huku akiwa amekonda sana hali iliyoashiria kuwa alikosa malezi bora. Mtoto huyo alimshtua bwana Abraham kwa vile alikuwa amefanana kwa kiasi kikubwa na Sabinus, mwanaye aliyekuwa ameshafariki. Akiwa bado hajaongea jambo msichana aliyekuwa ameongozana naye alisikika akiongea. “That’s your child Mr. and you don’t have to argue because you two have cloned” (“yule ni mtoto wako na hustahili kubishia kwa vile mmefanana”).
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment