Search This Blog

Wednesday, 1 June 2022

MOYO WA KUPENDA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : IBRAHIM GAMA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Moyo Wa Kupenda

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Ilikuwa ni siku ya jumapili tulivu, katika majira ya magharibi iliwakutanisha watu mbalimbali katika fukwe ya pwani ya Coco kwenye mji wa Dar es salaam, wilaya ya Kinondoni.

    Watu walikuwa wengi waliokuwa wakipunga hewa. Wengine wakiogelea na kucheza katika maji chumvi ya bahari. Watu wengine wakiuza na kununua bidhaa mbalimbali. Wapo waliokuwa wanakula na wapo watu waliokuwa wamekaa ndani ya magari yao, wakifanya maongezi na wenza wao. Wengine walikuwa wakila vitale vya mnazi, wapo waliokuwa wakinywa maji ya madafu, Ili mradi kila mtu alikuwa katika pilika pilika zake akifurahia maisha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati baadhi ya watu wengi waliokuwa katika fukwe ile wakifurahia maisha, hali ilikuwa tete na tofauti kabisa katika upande mwengine wa fukwe ile. Kwani alikuwapo mwanaume ambae hakuwa na raha kabisa ya maisha, wala hakutaka kuishi tena katika dunia ya maisha haya, alikuwa ametawaliwa na huzuni kubwa na majonzi yasiyosemeka.

    Hakika dunia haikuwa na maana kwake tena, kila kitu alikiona ni bure tu, bure kabisa. Moyo wake na fikira zake zilimpeleka mahala pale katika fukwe ile kwa azma moja tu. Nayo nikuitoa roho yake uhai wake. Alikuwa anadhani kujiuwa ndiyo suluhisho pekee la kuondokana na madhila yaliyomsibu katika moyo wake.

    Mfukoni mwake katika suruali aliyovaa, alikuwa na kitu ambacho kilimbadilishia muelekeo wa maisha yake, muelekeo wa maisha ya ndoa na mwanamke mrembo kuliko mwanamke yeyote aliepata kuwa nae. Mwanamke aliekuwa na damu ya nguo, mwenye kuvaa nguo yoyote akapendeza, mwanamke mwenye kutembea kwa matao, mwanamke mwenye sura jamali, mwanamke mwenye matiti madogo ya duara, yaliyopambwa na chuchu nene, mwanamke mwenye rangi ya asili ya weupe. Mwanamke mwenye shepu inayomtamanisha kila mwanamme kummiliki. Mwanamke mwenye macho makubwa na mazuri utayotaka uyatazame saa zote, mwanamke aliempenda kuliko kitu chochote duniani. Mwanamke aliemvisha pete ya uchumba miezi miwili tu nyuma.

    Sasa akiwa amebakiza mwezi mmoja kabla hajafunga nae ndoa, ndipo yalipompata masahibu makubwa sana maishani mwake na kuondosha kabisa matumaini ya kuishi.

    Mwanaume Yule aliekuwa katika pande nyingine ya fukwe ile alikuwa amekaa juu ya jiwe la mwamba wa bahari, mikono yake ikiwa mashavuni mwake, machozi yakimtiririka moyo ukimuuma kwa huzuni na simanzi.

    Alikuwa akiyatazama yale maji ya bahari yaliojaa muda ule, mawazo mengi mabaya yalipita kichwani mwake. Alikuwa anafikiri kujitosa kwenye maji mengi ili aitoe roho yake, pia alikuwa na mawazo ya kujipiga kichwa chake katika mawe yale makubwa aliyokuwa amekaa, ilimradi alikuwa anakitafuta kifo ambacho kingemuua haraka sana. Hakuwa na hamu ya kuendelea kupumua katika ardhi hii ya Mungu, bali alitawaliwa na ghamu kubwa.

    Alikuwa anayakhiyari mauti kuliko kuwa hai, hakuwa na raha moyoni mwake, hakuipenda tena dunia kwani dunia ilishamtenga na kitu akipendacho, lakini pia maisha yake yalishaingia dosari kubwa sana. Amekipoteza kitulizo cha moyo wake. Akaamua kukisaliti kidole na jiwe, liwalo kwake naliwe. Moyo wa kupenda umemfikisha katika sintofahamu kubwa.

    Mwanaume yule alikaa pale juu ya jiwe akiwa peke yake, mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio, mafua mepesi yalimchuruzika puani mwake, akatowa kitambaa cha kufutia jasho akawa anafuta machozi pamoja na mafua yaliyokuwa yameshika kasi sasa.

    “kwa nini mimi lakini Mungu wangu? Kosa langu ni kupenda? Utulivu wangu kujilinda kwangu, vyote vimekuwa kazi bure, hapana mimi sipo tayari kuendelea kuishi juu ya mgongo wa dunia hii basi nasema basi, dunia kwa nini unanifanya hivi lakini aaaagh?!”

    Ilikuwa ni sauti yenye huzuni na yakukata tamaa sana ya mwanaume aitwae Ramadhani, lakini mwenyewe alipendelea sana kuitwa kwa kukatishwa jina lake na kuitwa Rama.

    Rama alikuwa akisema maneno yale huku akilia pale juu ya jiwe. Uchungu aliokuwa nao aliwachukia wanawake, aliilaumu nafsi yake kwa kupenda kwa asilimia zote.

    Hatimae aliingiza mkono wake mfukoni akatowa bahasha nyeupe iliyokuwa imeshachanwa. Akaitazama bahasha ile machozi yakazidi kumtoka, hatimae akaifungua na kuisoma tena.

    Safari hii akiisoma akiwa pale ufukweni juu ya jiwe la mwamba, baada ya awali kuifungua na kuisoma zaidi ya mara tatu akiwa nyumbani kwake. Ulikuwa ni waraka mfupi uliokuwa umeandikwa katika mtindo wa shairi, lenye beti nane. Waraka ule aliukuta nyumbani kwake akirejea kutoka kazini kwake.

    Waraka ule ulikuwa ukitoka kwa mtu aliekuwa akimpenda kuliko kitu chochote hapa duniani. Uliandikwa na mtu aliemvesha pete ya uchumba miezi miwili iliyopita. Hatimae leo mchumba yule anamtowa machozi, anamuumiza moyo wake na kuiona dunia kwake haina maana tena bila ya kuwa na ampendae. Hakika alipagawa sana kila kitu kwake kilisimama, yote kwa sababu ya Rebeca John Makuka, mtoto wa kitanga aliechanganya kabila baba yake akiwa ni Mduruma, na mama yake akiwa ni Mdigo. Mwanamke aliekaa jikoni kumpikia chakula ambacho hajawahi kuipata ladha yake kwa mpishi mwengine tangu ajue kula, mwanamke bingwa katika bahari ya mapenzi, mwenye miguno na vilio vya mahaba, vinavyomfanya hata khanithi kupata nguvu na kusimamisha uume wake.

    Rama aliusoma waraka ule kwa kilio cha kwikwi kwani ulikuwa unasomeka hivi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa muhibu wangu Rama, honey wangu mtukuka

    Moyo wangu waniuma, tena ninasikitika

    Niliyowatenda uma, na wewe yamekufika.



    Ulinipenda kwa dhati, kwa hilo sina mashaka

    Ukafikia wakati, kunioa ukataka

    Ila si yako bahati, Nimekwisha athirika



    Nafsi inanisuta, mimi haya kutamka

    Nilio wauwa sita, kwa Ukimwi hatotoka

    Yule alonikamata, Rama nitakukumbuka



    Takukumbuka kwa mengi, sijawahi kukuchoka

    Walokupenda ni wengi, lakini hukuwataka

    Vijana kwa mashangingi, na waliotakasika



    Najua jinsi gani, dear utavyoteseka

    Lakini tufanye nini, maji yameshamwagika

    Nakuomba samahani, ewe wangu muhibaka



    Nitazidi kukupenda, kwa miaka na miaka

    Popote nitapokwenda, siachi kukumbuka

    Dokta wangu wa kidonda, tiba zilizonyooka



    Ishi kwa matumaini, dunia ishatutoka

    Rudi hima kwa manani, radhi zake kuzitaka

    Hakika kwa Rahmani, hakuna kitoshindika



    Akupendae maisha, Rebeka John Makuka

    P,o box merudisha, nchini ninaondoka

    Pendo kwako halijesha, milele takukumbuka.



    Rama alimaliza kuusoma waraka ule, akakunja ngumi kwa hasira machozi yakamzidi uwezo, macho yake yakawa hayaoni sawasawa kwa kujaa machozi, Alijizoazoa na kutaka kutimiza dhamira yake, ambayo nafsi yake ilimuongoza kwa dhati kabisa kujiuwa na kuiacha dunia.

    Kwa macho yenye machozi, alisimama wima akaanza huhesabu moja, mbili, ta..! hakumaliza neno tu, alisikia sauti ikimwita nyuma yake. “Kakaa, kakaaa, kakaaaaa!”

    Rama aligeuka nyuma kuangalia mtu aliekuwa akimwita kwa fujo, akamuona dada mmoja wa makamo nae machozi yakiwa yanamtiririka mashavuni mwake.

    Rama alipigwa na butwaa kwamba nini kinachomliza dada Yule, akakosa jibu akaamua kuendelea na dhamira yake, lakini kabla hajajitosa katika maji yaleyaliyokuwa yamejaa pomoni, alimuona dada yule akilia na kumsihi asifanye lile jambo alilokuwa anataka kulifanya.

    Dada Yule alimwambia “Hapana usifanye hivyo, matatizo hayakimbiwi matatizo yanakabiliwa na kuyashinda. Usijaribu kufanya hivyo kwani unaweza kuongeza tatizo lengine badala ya kulimaliza!”

    Rama akiwa amesimama pale juu ya jiwe, aligeuza uso wake akamtizama yule dada kwani maneno yale yalimuingia akilini mwake, yakamchoma hadi kwenye moyo wake. Akawa anapata tabu kutaka kumjua dada yule, na amejuwaje kama yeye anataka kujiuwa? Lakini pia uso wa yule dada bado ulikuwa ukitiririsha machozi na kushuka mashavuni mwake.

    Rama alishangaa sana dada yule analia kwa ajili yake kwa tendo alilotaka kulifanya au analizwa na yake? Jibu la maswali yale hakulipata ilibidi alirudi akae kitako, akaketi pale pale juu ya jiwe, akajiinamia kwa huzuni asiwe na lakufanya kwa wakati ule akampa mgongo yule dada.

    Yule dada alipanda pale juu ya jiwe akawa amekaa mbele ya Rama wakawa wanatazamana uso kwa uso.

    “Samahani najuwa huna dhamira njema! Nipo hapa muda mrefu, nakuona upo hapa peke yako tena ukiwa huna furaha, tofauti na wenzako wanavyoyaponda maisha. Tena bila shaka itakuwa huna sababu nzito za kufanya dhamira mbaya kama sababu ambazo mie ninazo! Lakini hata mie mwanzo nilitaka kufanya hivyo kama wewe ulivyotaka na nilikuja hapa kwa ajili ya azma hiyo! Lakini nilipokuja hapa nikaona hiyo siyo njia muwafaka, yakutatuwa tatizo langu hivyo nimeahirisha jambo hilo kwa muda, nakuomba na wewe uahirishe dhamira yako kwanza!.”

    Yule dada macho yake yalikuwa yamevimba na mekundu bila shaka atakuwa amelia kwa muda mrefu sana, alimwambia Rama maneno yale huku akimtazama usoni.

    Rama nae alimtazama kwa makini dada yule huku akiwa anafuta machozi machoni mwake, lakini kila alipokuwa akivuta kumbukumbu ya yule dada kama aliwahi kumuona sehemu, lakini sura ile ilkuwa ni ngeni kabisa machoni mwake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yule dada alikuwa mrembo sana, kiasi ukimuweka yeye na Rebeca John Makuka, mchumba wa Rama, unaweza kuwatofautisha kwa urefu na ufupi tu, lakini karibu vitu vingi walishabihiana.

    “Kaka yangu nyie wanaume hamna maana kabisa katika dunia hii, nimetokea kuwachukia maishani mwangu, yaani nawaona ni wauwaji wakubwa nyie tena ni watu wabaya sana!”

    Yule dada alimwambia Rama maneno yale, ambayo yalimuumiza moyo wake na yalizidi kumshangaza sana. Yalimshangaza kwa kuwa yeye ameumizwa na mwanamke na amefikia hatua ya kujiuwa ili aondoke kabisa katika mgongo wa dunia hii, kwa sababu ya mwanamke sasa anatokea mwanamke kisha anamwambia kuwa wanaume anawachukia na siyo watu wazuri.

    Rama akili yake iligoma kufanya kazi itakiwavyo, hivyo akabaki amemtumbulia macho tu Yule dada huku akimshangaa. Hakuwa na lakusema kwa wakati ule, alijionea kivuzovuzo tu.

    Yule dada alimtazama Rama kwa makini, kisha akamwambia kwa sauti kavu na ya chini. “Hivi kwa nini nyie wanaume mnakuwa makatili namna hii?!”

    Rama alimtazama yule dada kama akili zake zipo sawasawa, hakika akaziona dalili zote za kuwa ametimia akili zake.

    “Kwa nini nyie wanawake mnakuwa makatili namna hii?!”

    Sasa ikawa zamu ya Rama kumuuliza yule dada, aliekuwa bado hana furaha katika moyo wake, lakini akiwa hakubaliani na uamuzi wa kujiuwa, yeye wala mtu mwengine yoyote yule awae.

    “Yaani mimi nakuuliza swali badala yakunijibu swali, wewe unanigeuzia swali tena? Hivi unajuwa kama hapa nilipo, nimefikishwa na mwanaume kama wewe baada ya kunitenda, hadi naiona dunia hii siyo nzuri kwangu nakufikia kuwachukia nyie wanaume wote mliozaliwa na mwanamke mwenzangu?!”

    Yule dada alimwambia Rama yale maneno huku uso wake ukionesha kukata tamaa. Lakini pia bado hali ya huzuni ikionekana dhahiri shahiri usoni mwake.

    Rama alimjibu Yule dada kwa sauti iliyokuwa inakwaruza.

    “Hapa nataka kujiuwa ni kwa sababu ya mwanamke kama wewe, ameniumiza amenibadilishia maisha yangu, amenifanya nisitamani kuishi tena katika dunia hii, yaani bora nife uchungu huu utakuwa haupo, kuliko kuishi nikiwa na maumivu makubwa namna hii, hakika alieumba mapenzi alikusudia mapenzi yaje kutupa raha walakini leo nayachukia mapenzi sana, kwani mie moyo wa kupenda umenipelekea hadi mapenzi yamenipa karaha na jeraha kubwa.”



    Yule dada alimtazama Rama kwa makini, akagundua maneno anayosema alikuwa akimaanisha ukweli ndani yake. Yaani kwa mapenzi ndiyo hasa yaliyotaka kuchukua uhai wa maisha yake. Dada yule aliinamisha kichwa chini, wakawa kimya kila mtu akiwa kwenye tafakuri nzito za mambo yaliyowasibu.

    Mara wakasikia sauti ikiwaambia, “Heei nyie hamuoni muda huu umekwenda kwa nini mnajificha huku, au mnataka kugeuza Guest hapa eee, haya shuka chini haraka sana kuja hapa!”

    Sauti ile ilikuwa ni ya askari polisi aliekuwa amevaa nguo za kiraia, mikononi mwake ameshika kifaa cha mawasiliano, ‘Radio call’ akiwa yupo na askari mwenzake aliekuwa amevaa sare za jeshi la polisi akiwa na bunduki mikononi mwake akiwa ameikoki na kuwaelekezea pale walipokuwa Rama na Yule dada ambae hajamfahamu jina lake, wala mahali anapoishi.

    Rama na Yule dada walishuka kutoka katika lile jiwe, wakawafata wale askari hiyo ikiwa inakwenda majira ya saa moja usiku.

    “Hivi nyie hamjuwi kama kukaa huku mwiso ni saa kumi na mbili? Sasa hivi ni saa ngapi na nyie bado mpo huku?”

    Yule askari aliekuwa amevaa kiraia aliwasaili Rama na yule dada, huku akiwaonesha saa yake waitazame. Rama na yule dada wao wakakaa kimya hawakusema neno. Yule askari baada yakuona hajibiwi, akamuuliza yule mwanamke.

    “Wewe unaitwa nani na huyu ni nani wako?”

    Yule dada alimtazama yule askari kwa jicho kali akamjibu.

    “Mimi naitwa Faudhia Mnyone, na huyu bwana wala simfahamu!”

    Wale askari walitazamana kama watu waliokuwa hawajaelewa lile jibu.

    Rama aligeuka kumtazama yule dada aliemtambua kwa jina lake baada ya kujitambulisha, halafu akainamisha kichwa chake chini.

    Yule dada akamwambia yule askari huku akimtazama.

    “Hatuwezi kufanya Guest mahala hapa wakati uwezo wa kwenda Lodge hata hotel ninao. Kwa taarifa yako jinsi nilivyovurugwa sina hamu kabisa ya kufanya hilo tendo mie! Na hapa hakuna kibao kinachoonesha muda wa mwisho wa watu kukaa huku ni saa ngapi, bora wewe umesema kwamba muda umekwisha basi tunakwenda zetu, kwani imekuwa kesi?!”

    Yule dada baada yakusema maneno yale alianza kuondoka eneo lile huku akiwa amekasirika sana.

    Yule askari akamzuwia kuondoka kisha akawaambia.

    “Wee dada unajibu kijeuri eee? Haya kaeni chini sasa yaani mnavunja sheria halafu unaleta kujua yaani unaongea sana siyo?”

    Rama alijaribu kuwanasihi wale askari waliokuwa mbogo, lakini hakufanikiwa kwani yule dada kwenye mafuta ya petrol yeye akawasha moto.

    “Sikai chini mimi niueni tu, kwanza sina faida ya kuishi katika dunia hii mimi, nyie wote ndiyo wale wale tu ni wanaume, sijuwi kwa nini mungu aliwaumba viumbe nyie?! Nyie mnataka rushwa na mie siwapi nipelekeni popote mnapotaka.”

    Wale askari walimtazama yule dada aliekuwa amesema maneno yale huku akiondoka zake, katika eneo lile kwa mwendo wa pole.

    Kazi ilibaki wa Rama kwani alitumia mbinu za kila aina ili kuwapoza wale wanausalama waliokuwa wamefura kwa hasira.

    Hatimae kwa tabu sana Rama alifanikiwa kuwashawishi na kuwalegeza askari wale kwa sauti ya chini na ya kubembeleza wakaachiwa.

    “Viongozi huyo ni mke wangu mie, na amenifumania na mwanamke mwengine, hivi hapa tulikuja kuyaweka sawa tu matatizo yetu. Japo yeye amenikana kuwa hanifahamu, hivi ni kweli kwa namna mlivyotukuta tulivyokaa ni watu tusiyofahamiana?! Yule amechanganyikiwa tu, hivyo nawaomba samahani sana viongiozi kwani mke wangu tangu anifumanie amewachukia wanaume wote”

    Wale askari walikubaliana na Rama kuwa Yule mwanamke amechanganyikiwa, kwani katika hali ya kawaida mara nyingi baadhi ya wanawake wamekuwa ni waoga sana kwa askari polisi, lakini mwanamke yule kwa vile alivyokuwa tofauti pamoja na maneno ya fedhuli aliyokuwa akiyatamka, wakaona kweli alikuwa amepagawa. Hivyo wakaachiliwa wende zao.

    Rama alipiga hatua kumfata Faudhia hadi akamfikia kisha akamsemesha kwa upole.

    “Faudhia nyumbani wapi unapoishi na ningependa kusikia matatizo yako, ambayo umesema ni makubwa kuliko yangu ili ikiwezekana tuweze kushauriana namna ya kuyatatuwa”

    Rama alisema maneno yale huku akiwa karibu na Faudhia Mnyone aliekuwa amepiga hatua hadi katika maegesho ya magari yaliokuwa pale Coco Beach.

    “Kaka yangu sidhani kama nitaweza kukusaidia kwani, tayari hapa akili yangu ishakuwa mbaya sana, hapa ninafikiri niliwashe hili gari kisha niende kasi nikajipigize mahali ambapo najuwa sitakuwa majeruhi ila ni marehemu kamili.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Rama alimshangaa yule mwanamke, na akaitazama ile gari ambayo sasa Faudhia Mnyone alikuwa ameiegemea. Ilikuwa ni Toyota Halier muundo mpya, ilikuwa imewekwa Rimu sport ikiwa na matairi mapana yaliyotokeza zaidi pembeni, Rimu zake zikiwa na mng’ao wa rangi ya fedha.

    “Sasa Faudhia ulinikataza mimi nisichukue maamuzi niliyokuwa nimeyakusudia, halafu wewe unataka ukajiuwe huoni mie ulinikatili? Kwa nini usingeniacha nikajiulia mbali, badala yake umenikatishia kifo kisha hutaki kunipa ushirikiano?!”

    Rama alikuwa akimwambia Faudhia Mnyone huku akimtazama usoni moja kwa moja, ndipo alipoyaona macho ya Faudhia Mnyone yakiwa yanamwaga machozi.

    Kadiri macho ya Faudhia yalivyokuwa yanamwaga machozi, ndivyo uzuri wake ulivyozidi kuonekana wazi mbele ya Rama. Hakika Faudhia alikuwa ni mwanamke mwenye sifa zote za kuitwa mrembo.

    Pale alipokuwa alikuwa amevaa suruali kipande iliyoishia magotini, suruali ile ilikuwa ni ya kitambaa cha Lineni, juu alivalia shati la Lineni lililokuwa la rangi ya kijivu kama rangi ya ile pensi aliyovaa. Kichwani mwake alikuwa amekata nywele zake, miguu yake mipana ilikuwa imevaliwa vikuku vya shanga kila mguu, pia ilikuwa imevaa viatu vyepesi vya ‘simple’ vya rangi ya kijivu, akawa amelinganisha rangi za viatu vyake sawasawa na rangi ya nguo zake alizovaa.

    Alikuwa ananukia marashi mazuri mwilini mwake, masikioni mwake amevaa hereni pana za ringi za dhahabu zijulikanazo kama rusha roho, vidole vyake vipana vya mikono vimepambwa na pete za thamani, mkono wake umeveshwa saa nyembamba yenye rangi ya dhahabu, shingoni mwake amevaa cheni nene mithili ya mnyororo mpana iliyombana kidogo shingoni mwake, ikiwa ni dhahabu halisi, machoni mwake hakupaka kitu chochote, lakini uso wake ulikuwa kama vile uliopakwa fondeshna na angel face, hakika mwili wake uliojazia kwa mpango, ulimgawa ukawa unamuonesha kiuno chake, makalio yaliyotokeza, kifua chake kilichokuwa sawa na mwili wake, meno yake meupe alipokuwa akizungumza ungependa aendelee kusema tena na tena kwa namna yalivyojipanga vyema kinywani mwake.

    Rama alitingisha kichwa kwa masikitiko kuwa kama huyu dada hivi alivyo ndiyo ametoka ili akajidhuru, je akiwa anatoka matembezini au katika shughuli na maharusi huwa anakuwaje?!

    Rama alitaka kufahamu matatizo yaliyomsibu mrembo yule hata akawachukia wanaume wote duniani, ndiyo maana alikuwa akimnyenganyenga ili aweze kufahamu mambo yaliyomsibu, ilihali matatizo yake akiyapa likizo kwa muda.

    Rama alimlinganisha Faudhia Mnyone alivyo, na aliekuwa mchumba wake Rebeka binti John Makuka, aliona Rebeka alimzidi urefu kidogo Faudhia kwani Rebeka alikuwa akimpita kimo yeye ila Faudhia Mnyone walikuwa vimo vyao vinalingana.

    “Naweza kukwambia kilichonisibu lakini sihitaji kusaidiwa tafadhali, kama utakuwa tayari kufata sharti hilo nitakwambia lakini kama utataka kunisaidia basi tafadhali shika njia yako na mimi nishike yangu”

    Faudhia mnyone alimwambia Rama huku sasa machozi yakiwa yamemfika mashavuni mwake. Uso wa Faudhia ulibadilika kwa kulia ukawa mwekundu mara dufu ya ulivyo, tendo ambalo lilimfanya azidi kupendeza.

    “Sawa nimesikia Faudhia, ila naomba kama utaniruhusu basi siyo tuongelee hapa tena, ila tutafute sehemu tukaelezane matatizo yetu, kwani muda wa kukaa mahala hapa umekwisha tusijekutafuta matatizo na askari bure”

    “Wale wanakataza kule siyo huku, huku watu wanakaa hata hadi saa tano za usiku, mie nyumbani kwangu sipahitaji hata kupaona, kwani kila nikitazama picha za mume wangu, na huyo mwanaharamu moyo wangu unaniuma sana, yaani wanaume nyie?! Kila nikifikiria namna tulivyokuwa tukiishi na mume wangu, ninaumia sana kwani hapa nilikuja tangu asubuhi majira ya saa tano, sijala kitu na sijisikii njaa, nyumbani kwangu sijarudi tangu nilipotoka asubuhi na sitaki kurudi, nitabaki humu kwenye gari hadi mauti yatakaponikuta.”

    Faudhia Mnyone alitamka maneno yale huku akiingia katika gari yake. Rama nae kitendo bila kuchelewa, akaingia ndani ya gari ile upande wa abiria.

    Faudhia alimtazama Rama kwa muda kisha akainamisha kichwa chake katika usukani wa gari yake, akalalia ule mzunguko wa usukani kwa paji lake la uso.

    “Ninahitaji kujuwa Faudhia madhila yaliyokusibu, hivyo tafadhali naomba unielezee kwani sina amani katika nafsi yangu”

    Rama alimwambia Faudhia mnyone akiwa ndani ya gari huku akiwa amemgeukia akimtazama kwa utulivu mkubwa.

    Faudhia hakumjibu kitu aliwasha gari na kuiondosha taratibu huku akiwa hana amani kabisa, aliiendesha gari ile huku akiwa hajuwi wapi anapoelekea.

    Rama akamuuliza. “Faudhia tunakwenda wapi sasa?”

    Faudhia huku akiwa anatazama mbele akamjibu Rama “Wala sijuwi mie naona nafata barabara tu”

    Rama akamwambia “Tafadhali naomba egesha gari pembeni Faudhia”

    Faudhia alitii amri akasimamisha gari na kumgeukia Rama akasema. “Umeshafika kwako?” Lakini Rama hakushuka badala yake alimwambia.

    “Naomba tutafute sehemu tukae tuzungumze kuliko kuzunguka tu kwani tunaweza kupata ajali ikatufanya tuwe walemavu wa maisha, wakati sie tunahitaji kuwa maiti kabisa!”

    Faudhia alimsikiliza akamuuliza. “Unataka tukakae wapi?”

    Rama akamjibu “Twende Magomeni pale kwa magoma moto”

    Faudhia aliendesha gari kuelekea Magomeni mataa katika hoteli ya Travel tine au kwa Magoma moto, akaiingiza gari ndani akaiegesha katika maegesho lakini hakushuka chini, akiwa mle ndani ya gari alifikiri hili na lile hatimae akaanza kumuhadithia Rama madhila yaliyomsibu.



    *******

    “Naitwa Faudhia Baddy Mnyone, naishi Mikocheni, nina miaka thelathini nafanyakazi ya kuuza vifaa vya urembo katika duka langu lililopo Kariakoo katika jengo la Swahili Plazza ghorofa ya kwanza. Niliolewa miaka mitatu iliyopita nikiwa na miaka ishirini na saba, Mume wangu anafanya kazi Hazina, nilikuwa ninampenda sana, lakini hii leo ninamchukia kupita maelezo.Ninamchukia kupita kiumbe chochote duniani”

    Faudhia alipofika hapo alinyamaza kusema akakilaza kichwa chake katikati ya usukani wa gari lake, na mara honi ikabonyezwa ikapiga kelele mfululizo, hadi pale alipokiinuwa kichwa chake honi ile ilisimama kulia.

    Faudhia hakujali kabisa kama alibonyeza honi ya gari ikaleta usumbufu kwa watu kadhaa waliokuwa wakistarehe wakipata burudani za vinywaji. Lakini pia wakisubiri muziki wa Taarabu kutoka kwa Band ya Jahazi Modern Taarabu waliokuwa watumbuize muda mfupi ujao katika ukumbi ule, kama ilivyokuwa ada yao kwa kila siku za Jumapili.

    Wale watu waliokuwa wakipata kilevi katika kaunta ile ya chini nao walimuona mpigaji wa honi ile alikuwa amelewa pombe.

    Lakini Faudhia alikuwa amelewa mapenzi yake yaliyovurugwa. Katu siku ile hakuweka hata funda moja la pombe kinywani mwake, ingawa alikuwa ni mnywaji mzuri tu wa Khamru.

    “Hebu niambie kwani amekufanya nini hasa hadi ukaamua umchukie kiasi hicho?” Rama alimuuliza Faudhia huku akiwa na wahaka mkubwa wa kutaka kujuwa jambo lile.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Katika miaka mitatu ya ndoa yetu, hatukujaaliwa kupata mtoto, na kila nikipima vipimo vinaonesha mie sina tatizo lolote. Mume wangu alipopima takribani mara tatu katika hospitali tofauti ilionekana ana tatizo la mbegu zake za kiume kukosa nguvu za kuchavusha yai la mwanamke. Lakini hadi leo hii, hataki kukubaliana na vipimo kwa madai kwamba kabla ya kunioa mimi alishatia mimba mwanamke, na akazaa nae mtoto mmoja wa kiume, tena akadai wanashabihiana sana na yeye. Sasa akaniambia kuwa tutaishi hivihivi hadi Mungu atakapoamua kutupa kudura zake, kumbe alikuwa ananicheza shere tu.”

    Faudhia alisimama kuzungumza akafuta machozi usoni mwake kwa kitambaa safi cheupe, kisha akaendelea.

    “Leo nikiwa dukani asubuhi, shoga yangu Isabela George yeye yupo facebook akaniambia niingie Facebook katika akaunti ya mume wangu nione vimbwanga. Hakika nilipoingia niliona vimbwanga na sikutaka kuamini macho yangu kabisa juu ya kitu nilichokiona, nikaamua palepale ofisini kwangu, kwa kuwa ninayo compyuta na printa, pamoja na mashine ya kutoa photocopy niprinti zile picha za mume wangu na mwanamke mwengine ambae simfahamu wakifunga ndoa bomani hapa hapa Dar es salaam. Wakati tangu juzi mume wangu hayupo nyumbani amenambia anasafiri kwenda kikazi Africa ya kusini, kumbe amekwenda kuoa!”

    Faudhia alikuwa akizungumza kwa uchungu kabisa na hasira zikionekana wazi katika uso wake.

    “Yaani amekwenda kuowa kwa sababu apate mtoto au ndiyo pesa zimemzuzuwa? Na huyo mwanamke aliemuowa yeye analinganaje kwa jinsi wewe hivi ulivyo! Ama kweli penye miti hakuna wajenzi dah!”

    Rama aliweka kando machungu yake kwa muda akamuuliza Faudhia huku akitikisa kichwa kumsikitikia mume wa Faudhia kupoteza almasi kwa goroli.

    ”Kwa kusema kweli huyo mwanamke maashaallah ni mzuri ila kinachoniuma mimi huyo bwana lazima atakuwa amekwenda kuoa kwa ajili ya kupata mtoto tu, kwani kwa mume wangu nimejitahidi sana kumridhisha kwa kila hali ila yeye amenisaliti, huo ndiyo ugomvi wangu kwani mimi sina tatizo la uzazi japo watoto nawatamani sana lakini mume wangu ndiyo alikuwa tatizo, sasa mie ningefanyaje ili nizae kwani sikuwa tayari hata siku moja kumsaliti, tangu nimeolewa sijawahi kutoka nje ya ndoa yangu. Iweje leo nahukumiwa kwa kosa lisilo langu? Kisha wamerusha picha zao katika mitandao ya kijamii ili nione na kunirusha roho mimi, hakika roho yangu imeumia sana. Kwa hakika wamefanikiwa kuirusha tena siyo kuirusha tu ila wameiweka juu ikining’inia.”

    Faudhia alisema maneno yale huku akitiririsha machozi kemkem mashavuni mwake.

    “Naweza kuziona hizo picha?!”

    Rama alimuuliza Faudhia akiwa na shauku ya kumfahamu mume wake, mwenye kuacha mke mrembo kama Faudhia, lakini pia akitaka kumfahamu huyo mwanamke mwenye sifa ya kuitwa mzuri hata Faudhia akawekwa kando.

    Faudhia alifungua droo ya gari yake akatowa bahasha kubwa ya khaki, akamkabidhi Rama mikononi mwake na yeye akatulia kimya akitazama mbele ya kioo.

    Rama kwa wahaka mkubwa aliifunguwa ile bahasha kwa pupa, akakutana na picha zaidi ya nane. Zikiwa katika mikao tofauti tofauti.

    Rama macho yake pale yalipokuwa yaliziona zile picha, lakini hakuyaamini kwa picha alizokutana nazo. Akanyoosha mkono juu ya kipaa cha gari ile akawasha taa ya ndani, mwanga mkubwa ulionekana ndani ya gari ile na kuweza kukiona chochote mle ndani kwa ufasaha zaidi.

    Rama macho yake, yaliganda kumtizama yule mwanamke aliekuwa akionekana katika picha ile, moyo wake ukaongezeka mapigo yake, alitaka kusema neno lakini mdomo wake haukufunguka, ila machozi yalifanikiwa kupenya katika makazi yake na kudondokea ile picha iliyokuwa mikononi mwake, yakaanguka na kuirowanisha picha ile kwa upande wa yule mwanamke.

    Faudhia aligeuza shingo yake macho yake yakamtizama Rama aliekuwa anahema kwa kuzitafuta pumzi, mara aliyaona machozi ya Rama yakitoka na kuirowesha picha ile akashangaa sana. Alipotaka kumsemesha, alimuona Rama akipoteza nguvu kwa kulegea mwili wake na hatimae akamuangukia na kumuegemea Faudhia pale alipokaa huku akitowa kauli nyembamba kwa huzuni.

    “Rebeka mpenzi umeuumiza moyo wangu umenidanganya mpenzi kumbe umekwenda kuolewa?!”

    Faudhia alimshika Rama huku akipigwa na mshangao, kwani aliyasikia maneno ya Rama kwa usahihi. lakini alipojaribu kumsemesha alikuwa amechelewa Rama alipoteza nguvu, pumzi zikasimama kimya kikatawala.

    Faudhia alimtikisa kwa nguvu huku akiita kwa nguvu “Kaka, kakaa, kakaaaaa” Lakini alikuwa akiongea peke yake sauti yake haikupata mtu wa kuipatiliza. Ilikuwa kama mtu aliekuwa akisomea maiti akaondoka na ujaka wake. Alizikusanya zile picha akaziweka katika bahasha yake na kuziweka mahali zilipokuwa awali.

    Na kwa kuwa gari ile ilikuwa imepandishwa vioo vyake juu kiyoyozi kikitowa huduma ya hewa safi isiyo ya joto, iliifanya sauti ya Faudhia ipotelee mle mle ndani ya gari ile haikuweza kutoka nje.

    Pamoja na baridi kali la kiyoyozi cha gari ile, lakini mwili wa Rama ulivuja jasho jingi sana kama mtu aliekuwa ametembea katika joto kali kwa mwendo wa miguu.

    Mlinzi wa hoteli ile alivutwa na kelele za honi zilizokuwa zimelia kwa mfululizo, akaelekea upande ule uliokuwa umelia honi ile, akaiona gari ndogo ikiwa imewasha taa ya ndani, hivyo aliweza kuona kwa vizuri kila kitu kilichokuwa kikiendelea ndani ya gari ile.

    Mlinzi yule alipiga hatua zaidi hadi pale katika gari ile, akamuona mwanamke akimtikisa mwanaume aliekuwa amemuegemea akiwa hatikisiki wala hatowi ushirikiano wowote, yule mlinzi akashawishika kugonga mlango wa gari ile upande wa dereva, lakini mwanamke aliekuwa mle ndani hakufunguwa mlango lakini badala yake alikuwa akiendelea kumsukasuka yule mwanaume aliekuwa amelala mle ndani.

    Yule mlinzi alipoona hapewi ushirikiano akatowa simu yake na kupiga kituo cha polisi Magomeni usalama, kilichokuwa jirani na pale, akatowa taarifa ya hali anayoiona machoni mwake, na hatuwa alizochukuwa lakini mtu aliekuwamo ndani ya gari hiyo hampi ushirikiano, hivyo akahitaji msaada kutoka polisi, akahitaji nguvu zaidi kwani yeye hawezi kuvunja mlango au kioo cha gari ile itakuwa ni kinyume na utaratibu wa kazi yake.

    Faudhia Baddy Mnyone, hakuwa na habari kabisa kuhusu mlinzi alekuwa akigonga mlango wa gari yake, kwani akili zake zilikuwa zishachanganyikiwa kwa tendo la yule kaka ambae hamtambui jina lake wala mahali anapoishi, akiwa amezirai ndani ya gari yake, tena amezirai baada ya kuoneshwa picha, ambazo kabla hajazirai ametamka kuwa mke wa mume wake, yeye ni mchumba wake.

    Faudhia ndipo alipotanabahi kuwa ndiyo maana huyu bwana alimkuta kule ufukweni akitaka kujiuwa, kumbe mwanamke aliemuumiza ndiye hasimu wake, ndiye mke mwenzie. Hakika alitaka afahamu zaidi na zaidi juu ya huyo mwanamke lakini nani atakaempa ukweli kama sie yule kaka aliekuwa nae pale.

    Wazo la haraka lilimjia ampekue mifukoni mwake ili kama anaweza kupata japo kitambulisho chochote kile, ili aweze kumtambua jina lake na namba yake ya simu tu. Wazo lile aliliafiki akaanza kumpekuwa katika mifuko yake ya suruwali, akaanza na mfuko wa mbele kulia mfuko ule aliutowa wote nje lakini haukuwa na kitu.

    Akaupekuwa mfuko wa mbele wa upande wa kushoto nao pia alitoka kapa kwani haukuwa na kitu vilevile. Faudhia huku akianza kukata tamaa alitumia nguvu za ziada akafanikiwa kumlaza ubavu yule kaka na kuingiza mkono wake katika mfuko wa suruali wa nyuma, mkono wake ulikamata kitu.

    Aliutowa mkono wake kwa wahaka mkubwa akatoka na bahasha iliyofunguliwa, aliitazama kwa haraka akaichukuwa na kuiweka pembeni juu ya ‘dash boad’ akaendelea kumpekuwa tena katika mfuko wa shati lakini hakufanikiwa kupata kitu chochote zaidi ya ile bahasha iliyokuwa imefunguliwa.

    Faudhia akaifungua ile bahasha na kuanza kuisoma kwa fadhaa.

    Kwa muhibu wangu Rama, honey wangu mtukuka

    Moyo wangu waniuma, tena ninasikitika

    Niliyowatenda uma, na wewe yamekufika.



    Ulinipenda kwa dhati, kwa hilo sina mashaka

    Ukafikia wakati, kunioa ukataka

    Ila si yako bahati, Nimekwisha athirika



    Nafsi inanisuta, mimi haya kutamka

    Nilio wauwa sita, kwa Ukimwi hatotoka

    Yule alonikamata, Rama nitakukumbuka

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Takukumbuka kwa mengi, sijawahi kukuchoka

    Walokupenda ni wengi, lakini hukuwataka

    Vijana kwa mashangingi, na waliotakasika



    Najua jinsi gani, dear utavyoteseka

    Lakini tufanye nini, maji yameshamwagika

    Nakuomba samahani, ewe wangu muhibaka



    Nitazidi kukupenda, kwa miaka na miaka

    Popote nitapokwenda, siachi kukumbuka

    Dokta wangu wa kidonda, tiba zilizonyooka



    Ishi kwa matumaini, dunia ishatutoka

    Rudi hima kwa manani, radhi zake kuzitaka

    Hakika kwa Rahmani, hakuna kitoshindika



    Akupendae maisha, Rebeka John Makuka

    P,o box merudisha, nchini ninaondoka

    Pendo kwako halijesha, milele takukumbuka.

    Faudhia nguvu zilimwisha aliishiwa pozi kabisa mawazo yake yote yalimsikitikia mumewe kwa kuvamia vizuri asivyovijuwa kwa undani. Akawaza kuwa hivi sasa watakuwa wapo katika fungate na bila shaka tendo la ndoa ndilo litakuwa limechukuwa nafasi kubwa sana.

    Akawaza kuwa mtu na mkewe hawavai mpira hasa kama mwanamke halei mwana ndiyo kabisa, ukizingatia na mke wenyewe ni mpya kwani siku zote kipya kinyemi ingawa kidonda. Faudhia moyo wake mapigo yake yakaanza kupiga taratibu yakipoteza na kutoka katika hali yake ya kawaida, alikosa nguvu kabisa hata yakuinuwa kidole, aliuona ugonjwa wa Ukimwi tayari umebisha hodi kwa mumewe.

    Aliwaza mumewe kuwa katika taswira ya furaha tele kupata mke mrembo lakini bila kufahamu kuwa ameingia katika mtandao, ameingia katika namba nane ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ukimwi, kwamba anafurahia kuuliwa na maradhi ambayo hadi leo hii, bado serikali inasema dawa za kutibu ugonjwa huo hakuna, hata hizo dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo, siku za hivi karibuni serikali imekili kuwa wajanja na watu wenye tamaa wanazichakachua.

    Macho yake aliyahisi mazito, kichwa kilimuuma sana kwa kuelemewa na lindi la mawazo hatimae bila kujitambuwa akaanguka akiuangukia mwili wa Rama, akiwa na ule waraka mkononi mwake nae akapoteza fahamu.

    Yule mlinzi alimuona yule dada mle ndani ya gari akimpekuwa mwanaume aliekuwa hatikisiki, akahisi kuwa mwanamke aliekuwa ndani ya gari ile ni mwizi anamuibia mwanaume aliekuwa nae ndani ya gari akiwa amelewa.

    Hivyo akatowa simu yake kwa mara nyingine akapiga Polisi zuia uhalifu usitokee akisisitiza kitendo anachokiona, akapewa jibu upande wa pili kuwa askari wenye silaha wapo njiani wanaelekea hapo, hivyo wahakikishe hatoroki huyo mtuhumiwa, simu ilikatwa na yule mlinzi akawa amepatwa na kihoro akiwaona askari wanachelewa kufika katika eneo la tukio.

    Mara simu ya yule mlinzi ikaita na yeye akaipokea.

    “Wana usalama hapa upo sehemu gani, sie tumeshaingia ndani getini?”



    Mlinzi akawaelekeza askari wale sehemu alipo, na katika sekunde kadhaa askari wale walifika katika eneo la tukio, na mara moja wakaanza kushughulika.

    Askari polisi watatu waliizunguka gari ile macho yao yakitazama ndani ya gari ile wakawaona watu wawili wakiwa wamelaliana mwanaume akiwa chini na mwanamke akilala juu yake.

    Taa ya ndani ya gari ile ilikuwa bado inawaka, na mashine ya gari ile ilikuwa bado ikiunguruma, dereva wa gari ile automatic aliweka gia katika sehemu ya P, ikiashiria Parking hivyo haikuweza kuiruhusu gari ile kutembea hata kama ingesukumwa. Milango ya gari ilikuwa imelokiwa loki zikiwa zipo chini kabisa zimejifunga. Kwani gari ile iktembea kwa mwendo wa kasi wa kilometa 30 kwa saa, loki zake hujifunga zenyewe.

    Askari wale walijaribu kuifunguwa milango ile lakini walishindwa, walipojaribu kugonga kwa nguvu hawakupata jibu kwani wale watu mle ndani ya gari walikuwa hawana fahamu kabisa na kitu kinachoendelea katika dunia hii.

    Sauti kubwa ya kugonga gari ile ya wale askari, iliwavuta watu waliokuwa wanakunywa pale uwani katika Hoteli ile ambapo ndipo bendi zinapotumbuiza pamoja na mapaparazi wa magazeti pendwa na wale wa luninga waliokuwa wamekwenda kutafuta habari katika onesho la Bendi ya Jahazi.

    Mapaparazi wale walivutika na kitendo kile cha maaskari kuwamo ndani ya hoteli ile wakiwa na silaha, na kugonga kwa nguvu katika gari ile. Hivyo kwa tukio lile hawakusubiri kualikwa bali wakajisogeza na kuingia kazini bila kufanya ajizi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Picha mnato zilipigwa pamoja na picha za video kwa ajili ya luninga. Katika muda wa dakika zipatazo kumi tu watu walikuwa kijiji wamejaa kuizunguka gari ile. Kila mtu alikuwa akisema lake, wapo waliokuwa wakisema wale wamelewa chakari wamelala, wapo waliosema wale wamekufa, pia wapo waliosema kuwa wale wamejiuwa ili mradi kila mwenye lake alisema na watu wakamsikiliza.

    Yule mlinzi wa hoteli ile alikuwa yupo katika wakati mgumu sana, kwani waandishi habari walikuwa wakimuhoji maswali kwa dafaa. Kabla swali hili hajamaliza kujibu, alitupiwa swali lingine na muandishi mwingine basi ilikuwa maswali juu ya swali.

    Askari wale waliwarudisha watu nyuma ili wasiisogelee ile gari, na kiongozi wa polisi wale aliekuwa na cheo cha Sajenti katika mabega yake, akamuamuru askari wa chini yake avunje kioo cha gari ile ili wafunguwe loki za gari ile na kufunguwa mlango kwani kulikuwa hakuna njia nyingine mbadala yakuufanya mlango ule ufunguke.

    Constebo wa polisi (PC) alitumia kitako cha bunduki aliyokuwa ameibeba mikononi mwake, bunguki aina ya G3 alipiga pigo moja takatifu kioo cha upande wa kulia kwa dereva kikakubali pigo lile kikamwaga chenga nyingi za vioo vilivyowaangukia Rama na Faudhia waliolaliana ndani ya gari ile, na vioo vingine vikamwagika chini nje ya gari.

    Waandishi habari walipoona yule askari PC anajiandaa kuvunja kioo cha gari ile, wakamuhama yule mlinzi wakawa wapo sambamba na tukio la kuvunjwa kioo, hakika wale mapaparazi walijiona ni watu wenye bahati kubwa kwa siku ile kuamua kwenda katika hoteli ile kusaka habari, kwani walipata habari hasa tena habari sahihi za wao wenyewe kushuhudia zisizokuwa na mashaka, ubishi wala kupandishiwa kitu ili kupendezesha habari ile.

    Askari kiongozi wa askari wale, aliingiza mkono wake ndani ya gari ile akatowa loki na kufanikiwa kufunguwa mlango wa gari ile. Akapanda ndani ya gari ile, akamshika shati Faudhia aliekuwa amelala juu ya mwili wa Rama, akamtikisa taratibu akikusudia kumuamsha, Ila Faudhia hakuamka. Alipouachia mwili wa Faudhia ukaanguka mzimamzima kichwa chake kikining’inia katika miguu ya Rama, shati lake likapanda juu kifuani mwake na kitovu chake cheupe kilichoingia ndani, kikawa kinaonekana kwa sehemu kubwa kama siyo chote.

    Mkononi mwake Faudhia alikuwa bado ameikamatia karatasi iliyompelekea kuchukuwa fahamu zake. Yule askari Sajenti aliichukuwa karatasi ile mkononi mwa Faudhia, akaitazama kwa muda, kisha akaiweka mfukoni mwake.

    Akapeleka kichwa chake kifuani kwa Faudhia, akaweka sikio lake kifuani upande wa kushoto kwa Faudhia kusikiliza kama anapumua, sikio lake likagusa katika chuchu pana zenye joto jingi sikioni mwake, moyo wa Sajenti ukapiga kwa kasi kwa sekunde kadhaa, ukipoteza kabisa muelekeo. Aliusikia moyo wa mwanamke yule ukipumua kwa tabu sana katika pigo moja moja. Aliondoa sikio lake pale sikioni, akali tupia macho titi lile lenye kuvuta mithili ya sumaku kwa taka za chuma. Akayashusha macho yake pale katika kitovu cha Faudhia, suruali yake ikaanza kumbana maeneo ya kati ya mwili wake, akalazimisha kuyaondosha mawazo mabaya moyoni mwake akarejea kazini. Ama kweli moyo wa kupenda ameumbiwa binaadamu.

    Akaweka sikio lake katika kifua cha Rama kuusikiliza moyo wake kama unapumua, akausikia ukipumua na kupiga kwa tabu sana.

    Akawanusa midomo yao kama wanaharufu ya pombe au sumu au kemikali yoyote, lakini hakupata harufu alioitarajia kuinusa, watu wale hawakuwa wananuka pombe wala chochote katika vinywa vyao.

    Sajenti akageuza uso wake na kuwatazama wenzake kisha akawaambia.

    “Hawa hawajalewa kabisa, bila shaka watakuwa wamefikwa na jambo zito, haraka tuwawahishe hospitali kwa uchunguzi zaidi kwani mapigo yao ya moyo kwa mbali sana yanafanya kazi, yamaanisha wapo hai hawa.”

    Wale askari wakasaluti kuonesha kukubali maagizo ya kiongozi wao, kisha wakafungua milango ya gari ile ya nyuma ambayo loki zake zilishafunguliwa na kiongozi wao pale alipotumia Loki kuu kutoa loki ya mlango wa mbele wa kwa dereva ambayo iliruhusu kufunguka loki za milango yote.

    Wakapanda wao pamoja na yule mlinzi wa hoteli aliekuwapo pale muda wote. Askari wale wawili walikaa madirishani na mlinzi aliwekwa kati, katika kiti cha nyuma cha gari ile. Rama na Faudhia waliachwa katika kiti cha mbele upande wa kushoto wakiwa bado wamelaliana. Sajenti alikaa katika usukani wa gari akaiendesha gari ile hadi kituo cha Polisi Magomeni Usalama.

    Waandishi habari waliisindikiza kwa picha gari ile, na wale wapiga picha za video walidiriki kuikimbiza gari ile hadi ilipotoka nje getini, yote nikatika kukamilisha habari ziwe nzuri.

    Baada ya kufika kituo cha Polisi yule mlinzi akaachwa pale kutowa maelezo yake kwa kadiri alichokiona. Rama na Faudhia walishushwa wakapakiwa nyuma katika gari ya Polisi Land Cruser Pickup yenye namba za PT.

    Ile gari ya Faudhia ikawekwa chini ya uangalizi wa Polisi, Rama na Faudhia haraka wakawahishwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

    Yule mlinzi wa Hoteli ya Traveltine katika kutowa maelezo yake, alieleza kila kitu alichokiona kuanzia honi iliyokuwa imeita kwa fujo, hadi yeye ikambidi akakague eneo lile kwa usalama zaidi, kwani honi ile hata baada ya kulia kwa fujo hakukua na gari iliyotoka katika maegesho iliyolilia honi ile, ndiyo maana ikampasa aende kukagua kwa nini honi ile ililizwa vile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaendelea kueleza kuwa alipofika pale, alishuhudia kupitia mwanga wa taa ya gari ile, mwanamke akiwa mzima akimsukasuka mwanamme alieuwa amemlalia, pia alimuona akimpekuwa kutaka kumuibia ndivyo alivyohisi yeye, na hata bahasha aliyoitowa ndani ya mfuko wa nyuma wa suruali ya mwanamme na hata alipoisoma alikuwa akimtizama, ila alipatwa na mshangao alipomuona akimlalia yule mwanaume. Alipogonga mlango ili ajue kama wapo sawa, hakuitikiwa kabisa na hata walipokuja wana usalama bado walikuwa katika hali ile ile, huo ukawa ndiyo mwisho wa maelezo yake..

    Baada ya kutoa maelezo yale mwisho alisaini maelezo yake akaruhusiwa kurudi katika lindo lake baada yakuandika mawasiliano yake, akaelezwa kuwa akihitajika kutoa ushahidi ataitwa.

    Askati aliekuwa akimchukulia maelezo yale yule mlinzi, alikwenda katika gari ya Faudhia akaanza kuipekua gari ile kwa makini sana. Alipofungua droo la gari ile, alikutana na bahasha ya Khaki, pamoja na kadi halisi ya gari, na leseni halisi ya udereva daraja D’ ya mwanamke. Alivichukuwa vitu vile akaendelea kupekuwa gari ile hadi nyuma ya buti, lakini hakuweza kupata vitu vilivyokuwa tofauti na vile alivyovipata ndani ya gari. Akafunga Buti la gari ile akarudi ofisini kwake ili kuanza kukusanya ushahidi wa jambo lile. Hiyo ikiwa ni majira ya saa mbili za isha, mara waandishi habari wakatia timu Polisi kupata habari zaidi.





    2

    Katika chumba kikubwa tulivu, kilichosheheni samani za gharama kubwa chenye mwanga wa kutosha, kilichokuwa kikizizima baridi la kiyoyozi, meza za vioo zilizokuwa na mauwa ya thamani kubwa zilikipendezesha chumba kile. Na meza ya mpingo iliyonakshiwa kwa usanifu mkubwa, ilitapakaa chupa tupu za bia, na sahani tupu za udongo zilizokuwa na mabaki ya mifupa ya kuku na viazi.

    Jokofu dogo lililojaa vinywaji lilikuwa halisikiki kama limewashwa ingawa lilikuwa likifanya kazi sawasawa. Luninga kubwa ya Bapa (FLAT SCREEN) iliyowekwa ukutani iliyokuwa imewashwa ikiwa katika stesheni ya taifa ya TBC 1. Usiku ule wa saa tano kasoro dakika kadhaa, ilikuwa katika kipindi kilichokuwa hewani cha muziki mchanganyiko, muziki uliokuwa ukiwaburudisha wanandoa waliokuwa katika fungate.

    Chumba kile kilitawaliwa na utulivu mkubwa, kimya kilitawala sana sehemu ile. Wapenzi wawili waliopendana kwa muda mfupi, hatimae wamefunga pingu za maisha na kuwa ni mume na mke.

    Mwanaume alikuwa akifurahia mapenzi motomoto ya mkewe, na mwanamke alikuwa akitowa huduma kwa mumewe kwa moyo mkunjufu.

    Mwanamke alikimudu kitanda sana, kiasi mume aliona hakufanya makosa kabisa kumuowa yeye, bwana alipelekwa puta kitandani, alikimbizwa mchakamchaka, alipigishwa jalamba, ilimradi fungate ile ilikuwa hakuna kulala.

    “Rebeka mpenzi unamapenzi matamu sana, unajuwa kukatika, unajuwa kunichombeza kwa mahaba. Mke wangu Faudhia niliekaa nae kwa miaka mitatu, umemfunika vibaya sana kwa siku moja tu umemuacha mbali sana. Hivi ulikuwa wapi siku zote mpenzi wangu?!”

    “Mpenzi Faridi hata mie naburudika sana tena nimefurahi sana, kuolewa na wewe kwani unanipa burudani hadi sitaki umalize, yaani unanimalizaje?!”

    “Usijali mpenzi kama nilivyokuahidi nitakununulia nyumba, pia uwe na biashara yako mwenyewe, kwani mie mke wangu mkubwa ni mtata sana, mwanamke hazai anajaza choo tu, mie kila siku nataka mtoto yeye kuzaa hazai sasa wa nini mwanamke wa namna hiyo kama naishi na shoga!”

    “Ila nakuomba uniahidi jambo moja mume wangu, ikiwa nitakuzalia mtoto, bi mkubwa umuwache kwani ataniendea mbio, kwa wivu wa kuzaa kwangu asije akanitia Nzi wa kijani bure, akanihusudi mwana wa mwenziwe. Atuwache watu tuliojaaliwa uzazi tuzae mtu unakaa nae kwa miaka mitatu kuzaa hazai, basi hata kuharibu mimba tu pia hajawahi? Hebu mpe talaka bwana tujinafasi sie, unamng’ang’ania kwani umezaliwa nae?.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mke wangu shaka ondoa kwani hadi sasa bila shaka atakuwa habari imeshamfikia huko alipo, kwani picha za harusi yetu, tayari nishazisambaza katika mitandao ya kijamii, ili aone ashikwe na uchungu aondoke, hivyo usiwe na wasiwasi hana muda mrefu ataondoka tu. Hapa tukimaliza saba yetu unaingia katika nyumba yako, kwani nishawapa kazi madalali wakutafutie nyumba nzuri, hivyo hilo niachie mie kwani pesa kwangu siyo tatizo, tatizo langu ni mtoto tu”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog